Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

0
0


Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru amewaongoza wadau wa haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huku akivitaka vyombo vya usimamizi wa sheria kuzingatia usawa na haki dhidi ya kesi zinazohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kilele cha Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Kauli Mbiu ya “Kizazi chenye Usawa : Simama Dhidi ya Ubakaji” kimefanyika leo Desemba 10,2019 katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack. 
 
Akizungumza, Otaru alisema ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni vyema vyombo vya usimamizi wa sheria ikijumuisha jeshi la polisi na mahakama kuzingatia haki na usawa katika maamuzi ya kesi zinazokiuka haki za Wanawake na Watoto Otaru alitumia fursa hiyo pia kuitaka jamii kuachana na mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili huku akitaka kuwepo kwa nguvu ya pamoja kupinga ndoa za utotoni zinazosababisha watoto kutopata haki ya elimu. 
 
"Bado kuna changamoto ya uwepo na mila na desturi ya ndoa za utotoni pamoja na kukosekana na usawa wa umiliki mali. Ni wakati sasa jamii kuachana na mila potofu zinazochochea ndoa za utotoni pamoja na imani za kishirikina zinazokandamiza ustawi wa wanawake na watoto",alisema Otaru. Alisema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kuzingatia haki za wanawake na watoto kwa kuwafichua wahalifu wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake pamoja na kuwashirikisha wanawake katika ngazi ya familia na ngazi mbalimbali za uongozi.

Otaru alisema mkoa wa Shinyanga unaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akibainisha kuwa tayari mkoa umefanikiwa kuunda kamati 7 za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ngazi ya mkoa na wilaya pamoja na kamati 130 ngazi ya kata ambapo kati ya kamati 130, 51 zimepewa mafunzo na zimeanza kutekeleza majukumu yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la The Voice of Marginalized Society (TVMC),Mussa Jonas Ngangala alisema shirika lake limekuwa mdau mkubwa katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na tayari limeanzisha kamati 11 za MTAKUWWA ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.

“TVMC inaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha tunamkomboa mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili,tunahamasisha jamii iwe na umoja ili kusaidia wananchi kuondokana na ukatili wa kijinsia”,alisema Ngangala.

"Tunaadhimisha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa, uzoefu kujenga uwezo wa pamoja. Katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia tunawaomba wadau kuunganisha nguvu na kubuni mikakati ya kijamii ambayo italeta suluhisho la kudumu” aliongeza Ngangala.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack ambapo alisema zinahitajika nguvu za pamoja ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mkurugenzi wa Shirika la The Voice of Marginalized Society (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.



Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,Mfinanga John akitoa taarifa ya jeshi la polisi kuhusu kesi za ukatili wa kijinsia wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.



Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Maafisa wa polisi Dawati la jinsia na watoto mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Mkurugenzi wa Huheso Foundation Juma Mwesigwa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Wadau wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.



Wanafunzi wakitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Kundi la Ngoma za Asili maarufu Mabulo ya Jeshi linaloongozwa na Msanii Wanzingiza likitoa burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Meza kuu wakifuatilia burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.

Burudani ya Ngoma ya Ununguli kutoka Bugimbagu ikiendelea.

Msanii Wanzigiza kutoka Isela halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiimba wimbo maalumu wa kupinga ukatili wa kijinsia.
Wanafunzi wakiwa kwenye maaandamano kuelekea katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga ambapo kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

NYUMBA ZA WAGENI ZACHANGIA KUONGEZEKA KWA MFUMUKO WA BEI

0
0
Charles James, Michuzi TV

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioisha mwezi Novemba mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioisha mwezi Oktoba.

Hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuepo kwa mwaka ulioisha mwezi uliopita.

Akizungumza na wandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja ambapo amesema ongezeko la mfumuko wa bei limesababishwa na mahitaji makubwa ya bidhaa pamoja na usafirishaji.

Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioisha kumechangiwa na ongezeko la bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoisha Novemba mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba mwaka jana.

" Bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi huu kulinganisha na mwaka jana ni pamoja na Mchele kwa asilimia 6.6, Unga wa Muhogo asilimia 7.8, Nyama asilimia 2.6, Mafuta ya Kupikia asilimia 7.2, Maharage asilimia 8.6, Mbogamboga asilimia 6.0 na Mihogo kwa asilimia 5.8," Amesema Minja.

Amesema kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi huu kulinganisha na Novemba 2018 ni pamoja na mavazi asilimia 2.7, Mkaa asilimia 4.4, Samani asilimia 3.1, Huduma ya Malazi kwenye nyumba za wageni asilimia 5.0 na mazulia kwa asilimia 6.3.

Pia mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.1 kwa mwaka ulioisha Oktoba 2019.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Bi Ruth Minja akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo.

SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZA DINI ZA KIELIMU KUITUMIA VYEMA TUME YA CSSC

0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI] Dkt.George Jidamva,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoriki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC]  uliofanyika leo jijini Dodoma.


Na.Charles James,Michuzi TV

kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala kutoka Tamisemi Dkt. George Jidamva ametoa Rai kwa Taasisi za dini za Elimu hapa nchini kuhakikisha  zinaitumia vyema Tume(cssc), ili liwe Daraja imara la kuwasilisha hoja serikalini.

Dkt.Jidamva ameyasema hayo  leo jijini Dodoma alipomuwakilisha Naibu katibu mkuu Elimu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Bw.Gerald  Mweli, amesema Tume ya kikristo ya huduma za jamii[CSSC] imekuwa na Mchango mkubwa katika  jamii hivyo ni vyema ikaungwa mkono kwa jitihada zote  za kusimamia ubora wa elimu nchini kwa makanisa

“Ni jambo jema kwamba wazazi wengi wanafurahishwa  na juhudi za Makanisa katika utoaji wa elimu nchini,ni imani yangu mtaendelea kutoa elimu iliyobora  na Maadili mema  kwa kufuata taratibu,sera,sheria na miongozo iliyopo hivyo tume ya CSSC imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi, na nitoe rai tu kwa Taasisi za Makanisa kuitumia vyema ili liwe daraja imara  la kuwasilisha hoja kwa serikali”amesema.

Aidha ,ametumia Fursa hiyo kuipongeza TUME ya kikristo ya huduma za jamii( CSSC ) kwa kuanzisha   Huduma ya udhibiti ubora  ,uhakiki wa Takwimu na Mitihani ya pamoja  kwa Madarasa ya Mitihani kitaifa  huku akiasa kuweka Mazingira Mazuri ya Ushirikiano   kwa ngazi ya kata na Halmashauri.

Hata hivyo ameshauri ombi la asilimia moja ya gharama za uendeshaji wa shule [WCF] kufanana na ya serikali ya asilimia 0.5 iletwa kwa maandishi yenye ufafanuzi na Tume kwa hatua zaidi.

Mkurugenzi wa Elimu wa Tume Kikristo  ya Huduma za jamii[CSSC]Mwalimu Petro Masatu Pamba amesema ufaulu kwa shule za makanisa umekuwa chachu nchini ambapo mwaka 2013 hadi 2018  matokeo ya kidato cha nne kwa shule zilizo na wanafunzi zaidi ya 40 ,shule 100 bora  ,kanisa limekuwa  na ufaulu wa wastani wa asilimia 70%.

Pia amesema Makanisa yameendelea kuboresha ufundishaji wa Masomo ya sayansi kwa kutumia TEHAMA.

“shule 42 mpaka sasa zinatumia mfumo huu kwa uratibu wa PLATFORM ya Tume Walimu,wanafunzi na Menejimenti ya Shule kuboresha umahiri kwa wanafunzi  na matumizi ya utawala”amesema.

Akitoa neno la Shukrani, Padri kutoka jimbo katoriki la Moshi mkoani Kilimanjaro ,Padri.William  Ruwahi’ch ameipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini .

”Tunashukuru sana kwa serikali kwa kuendelea kuthamini mchango wa  shule za kanisa ,tunaahidi kuhakikisha tunatoa elimu bora”amesema.

Aidha,amesema kuna changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na leseni ya Biashara kwani taasisi za kanisa zinatoa huduma na si za kibiashara.

EAST AFRICAN LEGISLATIVE ASSEMBLY: 10TH IPG KICKS OFF IN KAMPALA, EAC SELECT SIDE LOSE IN SOCCER CURTAIN RAISER, RECOVER IN NETBALL

0
0
East African Legislative Assembly, Kampala, Uganda: December 10th 2019: 
The 10th edition of the EAC Inter-Parliamentary Games (IPG) kicked off yesterday in Kampala, Uganda. To commence the twelve-day extravaganza was a football curtain raiser pitting an EAC Select Side featuring legislators from the Partner States’ Parliaments and the management of the East African Water and Sports Cultural Organization (EAWASSCA) in a thrilling encounter at the St Mary’s Kitende Stadium, Kampala.    

The water body pipped the EAC legislators 2-1. In netball, the EALA legislators beat the water body managers 22-16. In the second curtain raiser soccer match involving staff members, EALA drew 1-1 with Parliament of Uganda, while the EALA netball team similarly drew 22-22 with EAWASSCA netball team.

Attention shifts this morning to the MTN arena in Lugogo where netball action kicks off with Parliament of Uganda facing off with Parliament of Burundi in the first match before Parliament of Kenya takes on Parliament of Tanzania in the second match of the day.

In Men’s volleyball, Parliament of Uganda will face stiff opposition from Parliament of Burundi in the first match, before Parliament of Kenya locks horns with Parliament of Tanzania in the second match of the day at the same venue.  The Volleyball women matches will take the same script with Parliament of Uganda playing Parliament of Burundi before Parliament of Kenya faces EALA in the next match.

In football, EALA will take on Parliament of Kenya at the KCCA Grounds in a match to be preceded by another thriller involving four-time Champions, Parliament of Uganda, who take on Parliament of Burundi.   

Earlier on yesterday, the Speaker of the Parliament of Uganda, Rt Hon Rebecca Kadaga, officiated at the Pre-Tournament Conference calling on legislators to use the opportunity to nurture networking and bonding among the legislators.

In her remarks, Rt Hon Kadaga underscored the need for ensuring parliamentary diplomacy, saying various activities were necessary to ensure the people of East Africa move together in integration process. “We are here to learn from each other, appreciate each other in order to strengthen the integration process.  I thank you for the honour of giving Parliament of Uganda to host the 10th Inter-Parliamentary Games”, Rt. Hon Kadaga said.  

“When we established the Community in 1999, we declared it people-centred. I am happy that the people are moving together in that direction”, Rt Hon Kadaga said.Hon Mary Mugyenyi representing the EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin, called for the spirit of collegiality to prevail as the games take place.

“Through a networking event of this nature, the spirit of harmony, friendship and camaraderie must be extended at all times and all differences resolved amicably”,she said. 

As we mark the decade of sporting activities, we should not just reflect on the past achievements, but rather herald on what the future portends. Integration is progressive and therefore, we should chart the path as defined in our integration agenda”, Hon Mugyenyi added.

The legislator reiterated the importance of making the integration pillars work. She said the tenets of the Common Market Protocol were yet to be fully harnessed and exploited.
“Free movement and a free market should just not be a mirage – but a reality”, she said.

“We should exploit the opportunities offered by sports and culture as anchored under Article 119 of the Treaty for the Establishment of the EAC if we are to continue to drive the agenda and to find solutions to the myriad of challenges that sometimes/often come in the way of integration”, she added.

EALA Member, Hon Rose Akol presented a paper on the milestones of the EAC themed: EAC@20: Deepening Integration, Widening Co-operation while former EALA Member, Hon Bernard Mulengani presented a paper on Discipline and Etiquette.

The IPG which was mooted 10 years ago has over the years realized several successes.  Fundamentally, Parliamentary games are a key aspect of building relations between the EALA and the National Legislatures in the EAC region. The games play a fundamental part in enabling EALA’s interaction with Members of the National Legislatures in the Partner States as envisaged in Article 49 (2a) of the Treaty for the Establishment of EAC.

The tournament disciplines include football (St Mary’s Kitende and KCCA Grounds), walk-race, netball (MTN Arena Lugogo), golf (Kigo Serena Golf Course), athletics (Namboole Stadium), tug-of-war (Namboole) and volleyball (MTN Arena Lugogo). Athletics will feature races in 100 meters, 200 meters, 400 metres, 800 and 1500 metres respectively for men and women. The 4x 400m relay and the 4x 100m races are also on the cards.

The Games themed: “The EAC: One Spirit; One Destiny: Strengthening Integration through 10 Years of Inter-Parliamentary Games” brings together EALA and the National Legislatures.

EAC  Select Side featuring legislators from the Partner States’ Parliaments and the management of the East African Water and Sports Cultural Organization (EAWASSCA) in a thrilling encounter at the St Mary’s Kitende Stadium, Kampala. 
 EALA netball team drew 22-22 with EAWASSCA netball team. 
Ibrahim Jamal intercepts a pass during the match. EALA drew 1-1 with Parliament of Uganda
EALA legislators beat the water body managers 22-16

MAZISHI YA MFANYABIASHARA ALI ABDUL MUFURUKI MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

KWANINI Infinix S5 NI SIMU SAHIHI KWAKO?

0
0
KILA mmoja anapenda kuwa na simu kali na ya kijanja. Kwa kutambua hilo tunakuletea Infinix S5, simu yenye ubora wa karne ya 21, ambayo imeingia sokonI rasmi Oktoba 2019. Kuifahamu zaidi, ambatana na mimi tukiichambua simu hii:

Muundo wake
Infinix S5 imekuja na teknolojia ya kisasa kwenye kioo ambapo kamera yake ipo pembeni (hole-punch diplay) na hivyo kukifanya kioo cha simu kuonekana kwa ukubwa wake, tofauti na matoleo ya simu yaliyopita. Kioo cha simu kina ukubwa wa inchi 6.6 (uwiano wa 20:9), ambapo sasa utaweza kujinafasi zaidi unapoitumia.

Umbo la simu hii ni la plastiki na linapatikana katika rangi mbalimbali (Quetzal Cyan, Violent na Nebula Black). Ina sensa ya alama za vidole kwa nyuma ambayo inashikika kwa urahisi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa taarifa zako.

Upande wa kushoto wa simu kuna sehemu mbili za kuweka laini (Nano-SIM cards), na sehemu ya kuweka memory vard (microSD) ya ukubwa hadi 256GB.

Vitufe vya kuongeza na kupunguza sauti vipo upande mwingine. Upande wa chini wa simu kuna tundu la spika (ear/headphones) na sehemu ya kuchomeka USB na chaja.

Boksi la simu linakuja na ‘cover’ la simu, ‘screen protector’ USB cable, kipini cha kutolea laini na chaja.

Muundo wa Ndani
S5 ina RAM 4GB ukubwa wa kuhifadhi taarifa 64GB. Mambo mengine ni pamoja na Bluetooth 5, dual-band Wi-Fi, Rediao, USB-OTG na GPS. Mfumo endeshi (OS) wa simu hii ni Android 9 Pie na unaboresheka zaidi kwenda matoleo mengine.

Mbali na kuwa na Play Store, sehemu ya kupakua programu mbalimbali kama simu nyingine zilivyonayo, S5 imejumuisha pia Palm Store na AHA Games, ambapo unaweza kupakua programu na michezo mbalimbali.

Ukiwa unacheza game unaweza kuiweka simu yako kuzuia simu jumbe zisiingie au mtu asikupigie (DnD) ili kutokukusumbua, lakini unaweza kuziacha kama itakavyokupendeza wewe. Eneo la kitufe cha nyumbani (home button) unaweza kuweka muundo unaoutaka wewe kwani kuna chaguzi mbalimbali.

Katika simu hii kuna kitu kinaitwa ‘Intelligent voice broadcast’ ambacho kinakutajia jina la programu iliyoleta taarifa kwenye simu yako, au jina la mtu anayekupigia simu.

Uwezo wake na Uimara wa Betri
Simu hii ina uzito wa gramu 178, ikimaanisha unaweza kuitumia kwa mkono mmoja bila kuchoka, na pia wembamba wake ni milimita 7.9.

Utendaji wake ni bora na inaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja bila kupata moto, kukwama au kuzima. Spika za simu zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na hivyo kukufanya ufurahie unapozitumia kusikiliza muziki.

Sensa ya alama ya vidole inafanya kazi kwa haraka zaidi kufungua simu, lakini mbali na hilo, simu hii inaweza kutambua sura yako, hivyo ukaitumia kama njia ya kufungulia simu (face recognition).

Betri yake (4000mAh) hitoki, inaweza kutumika kwa saa 13 na dakika 24 mfululizo bila kuchajiwa, lakini matumizi ya kawaida ina uweza wa kukaa hadi saa 36.

Kamera
Infinix S5 ina jumla ya kamera tano, ambapo kamera nne zipo nyuma ya simu, na moja ipo mbele.

Kamera kuu ya nyuma ya S5 ina ukubwa wa 16 megapixels (na aperture f/1.8 pamoja na PDAF). Mbali na hiyo kuna kamera yenye 5 megapixels ambayo inatumika kupiga picha za karibu. Pia kuna kamera nyingine yenye 2 megapixels ambayo inatumika kama sense kwa ajili ya picha (portrait mode), na kamera ya nne ni sensa kwa ajili ya mwanga (low light sensor).

Mbele ya Infinix S5 kuna kamera kwa ajili ya selfie yenye ukubwa wa megapixels 32, ambayo itakuwezesha kupata picha zenye ubora mkubwa. Hata hivyo unaweza kupunguza ukubwa huo hadi 16 megapixels ili kukuwezesha kupata picha isiyo na ukubwa (MBs nyingi) lakini yenye ubora.

Kiwango cha juu cha ubora wa video ni 1080p. Programu ya kamera (camera app) ina mfumo kukuwezesha kupiga picha bora kwa kutumia AI beauty system, ambapo mbali na hiyo kuna mifumo ya AR Stickers na Panorama, yote kwa ajili ya picha. 

GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA NA YUNA WAADHIMISHA KILELE CHA KAMPENI YA SIKU 16 YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

0
0

Katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Haki za Binadamu duniani, leo Shirika la Global Peace Tanzania ikishirikiana na Washiriki wao Youth of United Nations (Yuna) Tanzania wameendesha Mjadala juu ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia, mjadala ulijikita zaidi katika kujadili haki za Watu wenye ulemavu Tanzania.

Sherehe hizi zilifanyikia katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki Dar Es Salaam, Tanzania Mgeni rasmi alikuwa Bi Ummy Nderiananga Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu Tanzania SHIVYAWATA)

Mgeni rasmi Bi Ummy Nderiananga Mwenyekiti wa Chama cha walemavu Tanzania, akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu .Mgeni maalumu Ndugu Stella Swaumu Vuzo, Afisa habari Umoja wa Mataifa akielezea kwa kirefu historia ya siku ya haki za binadamu na umuhimu wa kuadhimisha siku hii maalumu.

Washiriki walipata nafasi ya kujadili kwa undani juu ya Haki za Binadamu, hususani haki za watu wenye ulemavu, aidha washiriki wamesisitizia uwepo wa mazingira rafiki ya kuwahudumia watu wenye ulemavu wanaopitia masuala ya ukatili wa kijinsia

Leo tumeadhimisha kilele cha Siku ya Haki za Binadamu, lakini harakati hizi bado zinaendelea, ni za kila siku mpaka pale Ukatili wa kijinsia utakapo tokomezwa.

#16DaysofActivism#HumanRightsDay#LeavingNoOneBehind#OrangeTheWorld#Tanzania #GlobalPeace #UN

KINONDONI YA ANDAA MAONESHO YA BIDHAA ZA NGOZI VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS JIJINI DAR

0
0
MKUU  wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amesema kuwa katika kuhakikisha tunakuza uchumi wa Viwanda, Wilaya hiyo imeandaa maonesho ya wajasiriamali wa bidhaa zangozi yatakayofanyika Disemba 12 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Packers.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Chongolo amesema kuwa maonesho hayo ambayo yata ambatana na uuzwaji wa bidhaa hizo yatafanyika ikiwa ni katika mkakati wa kutangaza na kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini.

Amesema kuwa lengo la maonesho hayo ni kutangaza uwezo wa wadau wa ngozi, kuelimisha jamii kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa hizo zenye ubora zinazozalishwa hapa nchini sambamba na kuongeza soko la ajira kwa vijana.

Amefafanua kuwa katika maonesho hayo yatahusisha wajasiriamali kutoka Wilaya ya Kinondoni pamoja na Halmashauri nyingine zilizo alikwa ikiwemo Ilala, Temeke, Ubungo pamoja na Kigamboni.

Mhe. Chongolo amefafanua kuwa kupitia sensa ya mwaka 2012, Manispaa ya Kinondoni inajumla ya wakazi zaid ya milioni 1.3, ambapo idadi hiyo inategemea kupata bidhaa za ngozi, ikiwemo Viatu, Mikanda, Mabegi na pochi zinazo tokana na bidhaa za ngozi.

Mhe. Chongolo ameeleza kuwa hali hiyo imekuwa tofauti kutokana na watu hao kutumia bidhaa zinazozalishwa kutoka nje ya nchi na hivyo kuwasihi wannachi kupenda kutumia bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi kubwa barani Afrika zinazo zalisha ngozi kwa kiasi kikubwa , lakini pia Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu Afrika zenye mifugo mingi , Tanzania ni Nchi pia ambazo zinatumia bidhaa hizo kwa wingi, mfano rekodi inaonyesha kuwa jumla ya viatu zaidi ya milioni 53 zinaingia na kutumika kila mwaka” ameeleza Mhe. Chongolo.

Rais wetu mpendwa, Dk. John Magufuli kila siku amekuwa akisisitiza kujenga viwanda ili kufikia uchumi wa kati, na sisi wasaidizi wake tunaliangalia hilo kwa kulifanyia kazi, ndio mana tumeona tuwaweke pamoja wajasiriamali wa bidhaa za ngozi, na hatutaishia hapa tunampango mwakani tuyafikishe mbali zaidi” amesema Mhe. Chongolo.

Serikali ya Viwanda, Chongolo amefafanua kuwa pamoja na kwamba Tanzania inazalisha ngozi nyingi lakini ipo changamoto kubwa inayotokana na malighafi hizo kusafirishwa nje ya nchi jambo ambalo amesema limesababisha kuwepo kwa uhaba wa ngozi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa hizo.

Hata hivyo, Chongolo amesema kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ni Kinondoni yetu, Viwanda vyetu, Tanzania yetu ambapo kupitia maonesho hayo itakuwa ni fursa kwa vijana wengi kujiajiri , kuongeza pamoja na kukuza viwanda vya ndani vya ngozi na hivyo kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa hizo.

Imetolewa leo Disemba 10
na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni.

In Loving Memory of our Beloved Ms. Badriya Ramadhani Haji Nee ’Kiondo' : 25th January 1958 – 11th December 2017.

0
0

We miss you

Our hearts continue to ache with sadness, and

many tears still flow.

What it meant to lose you, no one will ever know.

We still hold you close within our hearts,

And there you will remain.

To walk with us throughout our lives, until we meet again.

Deeply remembered by your Husband Frank  Kiondo, Sons Eddie and Ibrahim Frank and in law Perla, granddaughter’s , Anjelina ,Aisha and Amaris  Ibrahim, your mother Bi Fatma, mother in  laws Anna and Agatha, brother and sister in laws, your brother Yusuf, Haji, Abdillah and their wifes, daughters  Mariam and Badriya Iddi, collegues, cousins, nieces, relatives, friends, and our good neighbors.

(Kisomo) that will be held on 12nd December 2019 at Madrass Fasbir Sabran Jamiaah , Tumbatu, Uvivini,  Zanzibar after Alasir prayer 4.30 p.m.

Inna lillah Wainnalillah Rajuin

Wabillah Tawfiq

DIT YAANDAA MAONESHO MAALUM YA TEKNOLOJIA MBALIMBALI ZA TEHAMA

0
0

KATIKA shamra shamra za maafali ya 13 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambayo yatafanyika Disemba 12 mwaka huu, wamendaa maonyesho maalumu ya teknolojia mbalimbali za TEHAMA ambapo pamoja na mambo mengine huduma mbalimbali kwa wananchi zitatolewa ikiwa ni pamoja na kutengenezewa simu pamoja na kompyuta zao.

Mhadhili Msaidizi wa DIT, Daudi Mboma anasema Taasisi hiyo imeandaa maonyesho maalum ya Tehama ambayo yapo chini ya mradi wa Escrip unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Amesema mradi huo utaanzishwa katika Kampasi ya Dar es Salaam ambapo wataanzisha kituo cha ICT ambayo itakuwa ya kikanda itakayojikita hasa katika usalama wa mitandao.

"Tumeandaa baadhi za wabunifu wanafunzi hapa kwenye Taasisi na wengine ambao wameanzia hapa kwetu na sasa wanajitegemea wamefanikiwa kuanzisha kampuni zao, watakua hapa kuanzia leo hadi siku ya mahafali wakitoa huduma ya kutengeneza kompyuta na simu bure," anasema Mboma.

Karuma Nicholas ni Mwanafunzi aliyesoma katika Taasisi hiyo na ni mmiliki wa kampuni ya Testlimit, anasema elimu inayotolewa DIT ni ya kipekee kwani wanafundisha zaidi kwa vitendo Jambo lililomuwezesha kufanya kazi nyingi za TEHAMA.

Wananchi wanaalikwa katika viwanja vya Taasisi hiyo kutembelea maonesho hayo kujifunza pamoja na kupata huduma bure ya kutengenezewa simu pamoja na komputa zao.



MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA) YATEMBELEA GEREZA LA SEGEREA,YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adam Fimbo ametembelea gereza la Segerea na kutoa msaada wa Katoni 45 za taulo za kike, Katoni 10 za pampas na dawa mbalimbali kwa  wafungwa na mahabusu wa gereza hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TMDA), Bw. Adam Fimbo akimkabidhi Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura msaada wa katoni 45 za taulo za kike, katoni 10 za Pampas na dawa mbalimbali kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la hilo leo jijini Dar es salaam Kulia ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea na Kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula.
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo mara baada ya kukabidhiwa msaada wa katoni 45 za taulo za kike, katoni 10 za Pampas na dawa mbalimbali kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la hilo leo jijini Dar es salaam katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea na Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya msaada huo Kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula na kushoto ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura pamoja na Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula wakijadiliana jambo mara baada ya kukabidhiana nyaraka zenye orodha ya dawa na vifaa vilivyotolewa kama msaada kwa zahanati hiyo katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza.
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akitoa shukurani zake kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo mara baada ya kukabidhiwa msaada huo kushoto ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza na katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akipokea zawadi ya mkoba kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Wanawake Segerea Afande Teopista Gauza wakati alipotembelea gereza hilo na kukabidhi msaada wa dawa na vifaa mbalimbali, Anayeshuhudia tukio hilo ni George Wambura Mkuu wa Gereza la Segerea.
Msaada wa vifaa mbalimbali pamoja na dawa uliokabidhiwa kwa George Wambura Mkuu wa Gereza la Segerea na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akitoa maelezo kwa kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo wakati alipotembelea zahanati ya gereza hilo na kutoa msaada wa dawa na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wafungwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akizungumza jambo na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakati alipotembelea zahanati hiyo na kujionea huduma mbalimbali za kitabibu zinavyofanyika.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akiongozwa na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura na Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula wakati akitembelea na kujionea huduma zinavyotolewa katika zahanati hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akiongozwa na Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakiwasili katika zahanati hiyo.

Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa -Mkuu wa Wilaya Mmanda.

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Mtwara

 Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa kwani vitambulisho vya Taifa vinavyotumika katika usajili wa laini hizo ndio baadae watanzania tutatumbuliwa kwa kuwa na vitambulisho vya mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya uu Mtwara Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa Uhamasishaji wa Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Mmanda amesema changamoto kwa baadhi ya Wananchi wa Mtwara kupata vitambulisho ni kutokana na wanatoka nchi jirani ya Msumbiji hivyo lazima wafuate taratibu za Uhamiaji.

Amesema kuwa kila mtu ahakikishe anapata kitambulisho cha taifa ili aweze kusajili laini yake kwa alama za vidole kwani namba zitafungwa Desemba 31 na ambao hawatafanya namba hizo zisizosajiliwa zitafungwa na kugaiwa kwa watu wengine.

Amesema kuwa taarifa zilizosambaa katika mtandao ya kijamii kuwa zoezi la kuzima laini simu Desemba 31 kuwa limeongezwa ni kuzipuuza na kwamba zoezi liko palepale.

Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki Wananchi waache kununua simu Mkononi kwani kuna watu wanaweza kufanya uhalifu na mwisho wa siku mtu akaingia katika matatizo.

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko Amesema zoezi la usajili kwa Mkoa wa Mtwara lipo kwa Wilaya zote na kutaka Wananchi wajitokeze kupata kusajili laini za simu .

Amesema zoezi la kuzima simu liko palepale hivyo watu waache kupotosha zoezi hilo.Eseko Amesema kanda ya Mashariki wamezindua Uhamasishaji kumekuwa na matokeo makubwa kwa Wananchi kuhamasika katika kujisajili.

Afisa Usajili wa Mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Gide Magila amesema changamoto wanayokutana nayo ni watu kusajili majina mara Mbili na wakati mwingine kusahau kumbukumbu walivyosajili.
 Foleni ya Wananchi wakiwa katika ufatliaji wa namba za vitambulisho vya Taifa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa alama  vidole katika uwanja wa Sabasaba mjini Mtwara. 

 Wananchi wakiwa katika foleni ya kuangalia namba za vitambulisho vya Taifa katika mfumo wa NIDA
 Afisa Msajili wa Mkoa wa Mtwara  wa Mamlaka ya a Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Gide Magila  akitoa changamoto wanazokutana na Wananchi wakati usajili na uangaliaji majina katika mfumo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akizungumza na Wananchi wakati wa Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mkoa wa Mtwara.
 Mabanda ya watoa huduma za simu kwa ajili ya kusajili laini za simu za  Wananchi kwa alama za vidole.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza namna kanda ya TCRA inavyohamasisha Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ATAKA TAFITI ZINAZOFANYWA ZIJIBU CHANGAMOTO ZILIZOPO KWENYE JAMII

0
0
Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema tafiti zinazofanyika nchini zinatakiwa kujibu changamoto zinazoikabili jamii ya watanzania na Afrika kwa ujumla.

Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Arusha
akifungua Mkutano wa kumi wa Kimataifa wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi Afrika (AMRS- 2019) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Kiongozi huyo amesema Tanzania imejikita katika ujenzi wa uchumi wa  kati kupitia  viwanda hivyo ni lazima tafiti zinazofanyika zijikite kwenye maeneo ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili zitumike kuimarisha utengenezaji bidhaa na huduma zinazoendana na azma hiyo.

“Ni nani anaamua nini kifanyiwe tafiti, je tafiti hizo ni za kuwafaidisha waliopo nje ya nchi au watanzania? ni lazima tujikite kwenye tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto zilizopo katika mataifa yetu na hivyo sisi wenyewe  tuwe waanzilishi wa ajenda ya utafiti kulingana na mahitaji,” alisema Naibu Wazirii Ole Nasha

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi ambae pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Hulda Swai amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utaainisha na kujadili maeneo ya vipaumbele vya tafiti ambavyo vitatumiwa na Vyuo Vikuu pamoja na Taasisi za kitafiti.

Akizungumza katika Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ametoa changamoto kwa wajumbe wa AMRS kuja na suluhisho la namna bora ya kutumia  vizuri utajiri wa malighafi zilipopo Afrika  kwa ajili ya maendeleoya Bara la Afrika.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Prof Emmanuel Luoga amesema kufanyika kwa mkutano huo katika chuo cha NM-AIST ni moja ya mambo muhimu katika kukuza uwezo wa Chuo kufanya tafiti zinazokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa.

“Wote mnafahamu kuwa Chuo hiki kina hadhi ya Kimataifa, kwa hiyo wanapokuja wageni wa aina hii kupitia majadiliano yao wanasaidia kuongeza ujuzi mpya katika masuala ya tafiti ikiwa ni pamoja na kukuza mashirikiano baina ya Taasisi hizi,” alisema Prof. Luoga

Mkutano wa Kimataifa wa Jumuiya ya Afrika ya Watafiti katika Malighafi unafanyika kwa siku nne Jijini Arusha kuanzia Desemba 10, 2019 ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini tangu ilipoanzishwa mwaka 2000, na unakutanisha zaidi ya watafiti 300 kutoka nchi 36 ulimwenguni.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kumi wa Kimataifa wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi jijini Arusha
 Rais wa Jumuiya ya Watafiti katika malighafi   Afrika Prof. Hulda Swai akielezea wajibu, malengo, mafanikio na matarajio ya Jumuiya hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kumi wa jumuiya hiyo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa kumi wa Kimataifa wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Mhe. William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Prof. Emmanuel Luoga akielezea kuhusu malengo na shughuli zinazotekelezwa na Chuo hicho wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kumi wa Jumuiya ya watafiti katika Malighafi  unaoendelea chuo hapo.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wakiwa na wadau mbalimbali wa tafiti. Mstari wa mbele  kushoto kwake ni Rais wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi na kulia kwake ni Naibu Katihu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi  na Teknolojia Prof. James Mdoe akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha NM-AIST Prof. Emmanuel Luoga.

WATU WANNE WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUWATEKA WATOTO WAWILI CHALINZE-WANKYO

0
0

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

WATU wanne wanaotuhumiwa kuwateka nyara watoto wawili na kudai fedha kiasi cha sh. milioni mbili wamekamatwa na polisi baada ya kutuma ujumbe wa vitisho kwenye simu ya mama wa watoto hao ambao ni wafamilia moja.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa alisema kuwa watu hao walikamatwa baada ya kutumiwa kiasi cha fedha.

Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi huko Bwilingu wilaya ya kipolisi Chalinze watoto wawili mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (8) na mwingine wa kiume (5) ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Bwilingu.

“Tulipata taarifa kupotea kwa watoto hao tarehe 5 Desemba na tulianza kufuatilia kwa mitandao ya simu iliyoonekana kutuma ujumbe kwa mama wa watoto hao Claudia Fute simu hiyo yenye namba 0715 648672 iliyosajiliwa kwa jina la Subira Kasenga,” alisema Nyigesa.

Alisema kuwa simu hii ilituma jumbe nyingi za vitisho kwa mama mzazi na kutaka atumiwe fedha haraka kiasi hicho vinginevyo angewadhuru watoto hao na kuwafanya lolote hata kuondoa uhai wao.

“Kwa kutumia namba hiyo pia tulibaini namba nyingine ya Farida Gabriel iliyokuwa ikisisitiza mtekaji aendelee kushikilia watoto kea sababu pesa itatumwa tu na kumsisitizia Kasenga kuwa akomae kwani mama wa watoto anatafuta fedha atume,” alisema Nyigesa.

Aidha alisema kuwa katika kuhakikisha wanafanikisha katika kufanikisha kukamatwa wahusika walituma kiasi cha shilingi 400,000 kwa mtuhumiwa na ndipo wakati akitoa alikamatwa na polisi.

“Watuhumiwa waliokamatwa ni Husna Hussein Mwinyigoha (18) ambaye ndiye aliyeteka watoto akitumia jina la Subira pia namba yake nyingine ni 0693838511 na 0719648672 iliyosajiliwa kwa jina la Subira Kasenga,Farida Gabriel (34) mwenye namba ya simu 0716461161 na 0784641456, Said Thomas mwenye namba 0692986611 na Miraji Mrisho Mbega,” alisema Nyigesa.

Alibainisha watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika ili wajibu tuhuma zinazowakabili za utekaji watoto hao wadogo.

WANA JUKWAA LA CHALINZE WATOA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI 120

0
0





NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

WANA-Jukwaa la Chalinze

Tunayoitaka linaloundwa na wapenda maendeleo wa Chalinze Bagamoyo Pwani,wamemkabidhi mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete risiti ya sh. milioni 1.8 kwa ajili ya mifuko 120 ya saruji kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimu,katika shule ya msingi Kibiki.

Akimkabidhi risiti hiyo ,mwenyekiti wa Jukwaa Alhaj Hamisi Nassoro, alisema mchango huo ni wa wana-Jukwaa hilo.

Alisema, Jukwaa linaundwa na wadau wa maendeleo, na kwamba wamedhamilia kupambana na changamoto za kielimu.
Aidha Nassoro aliomba fedha za maendeleo na wananchi zitumike kwa maslahi ya jamii.

“Hapa ni mwanzo wa shughuli zetu za kuipeleka mbele Chalinze yetu, lakini katika hili wana-Jukwaa tunaomba tupatiwe taarifa za kina, za uwepo wa tetesi za matumizi mabaya ya zaidi ya shilingi milioni miamoja, zinazotajwa kutumika pasipokufuatwa kwa utaratibu,” alisema Alhaj Nassoro.

Ridhiwani aliwashukuru wana-Jukwaa na kuwaomba wanajukwaa kulitumia kwa kuchochea maendeleo na sio kuwa sehemu ya kuleta migongano kwa wana-Chalinze. 

“Katika Jukwaa kuna baadhi ya mijadala mingine haileti tija, utaona mtu unatuma jambo ambalo wazi linalenga kuchafuana kisiasa, hili jambo sio zuri mimi niko tayari hata kukaa na sturi hapa mbele nikawapa ruksa ha kuuliza maswali yenu yote, kisha nikayajibu,” alisema Ridhiwani.
Kwa upande wake diwani Lufunga alisema kuwa katika kuunga mkono uboreshaji elimu katani humo, halmashauri ya Chalinze na Mbunge huyo wameshaipatia fedha za kujenga vyumba vya madarasa katika shule zilizomo katani humo, pia amewashukuru wana-Jukwaa kwa moyo huo.

Nae mmoja wa wajumbe Omary Mtiga alisema kuwa wao katika Kata ya Kibindu walikuwa na Jukwaa kama hilo walilolipatia jina la Kibindu Tunayoitaka, ambalo limeleta mafanikio makubwa katika uboreshaji wa shule katani humo.  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Magreth Kileo anawashukuru wadau hao kwa kuguswa na mahitaji ya shule hiyo, na kwamba msaada huo utapunguza adha ya upungufu wa vyumba

Miradi ya JUMEME yaziondoa gizani kaya 5,000 Ukerewe

0
0
 Baadhi ya mafundi mitambo wa kampuni ya JUMEME, wakifunga mitambo ya umeme jua katika moja ya miradi ya kampuni hiyo huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza.
 Moja ya mitambo ya kuzalisha umeme jua kutoka kampuni ya JUMEME iliyopo katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. 

ZAIDI ya kaya 5,000 katika kisiwa cha Ukara kilichopo wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, zimenufaika na umeme jua unaozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya usambazaji umeme vijijini (JUMEME).

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Profesa Costa Mahalu katika hotuba yake kwa maofisa kutoka Umoja wa Ulaya na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), waliotembelea miradi ya umeme jua iliyopo wilaya hapo.

Profesa Mahalu alisema kaya hizo zimenufaika kutokana na awamu ya kwanza ya mradi wa usambazaji umeme katika kisiwa hicho cha Ukara.
“Awamu ya kwanza ya iliyopewa jina la "Uzalishaji umeme wa katika kukuza uchumi wa Tanzania’ imeonesha utofauti kutokana na faida za kiuchumi na kijamii zilizopatikana.

“Kwa sababu mbali na kaya 5,000 kunufaika pia, wafanyabiashara wadogo na viwandani pia wameunganishwa. Lakini taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii kama vile maji vijijini na hospitali zimeunganishwa,” alisema.

Alisema huduma za JUMEME zimevifikia vijiji 20 kwenye visiwa 10 tofauti, na kuchochea uchumi wa eneo hilo jambo lililosaidia kuibua fursa nyingi za ajira.

"Malengo ya muda mrefu kwa JUMEME ni kuendelea  kushirikiana na wazalishaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwa waajiriwa wa eneo husika," alisema Prof. Mahalu ambaye pia ni Makamu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT).

Aidha, alisema kampuni hiyo imekuwa ikizingatia utoaji wa fursa za ajira kwa watanzania ili kuisaidia Serikali kukabiliana na uhaba wa ajira kwa vijana nchini.

"Kila mmoja wa wafanyakazi wanaofanya kazi ya uhandisi katika miradi 12 ya JUMEME, ni Mtanzania. Kati ya watu 25 wanaounda timu ya kudumu ya JUMEME wenyeji ni 22, ambao hupewa upendeleo wa wazi linapokuja suala la kufanya kazi.

“Kwa kuzingatia mafanikio ya awamu hii ya kwanza, tunatumaini kuwa na uwezo wa kutoa fursa zaidi za kazi kwa vijana wetu kwa kuendelea nao katika awamu ya pili, ya tatu na kuendelea zaidi katika miradi ya JUMEME. " alisema.

Alisema ili kuongeza uweledi na ufanisi wa waajiriwa wazalendo, kampuni hiyo inaendelea kutoa mafunzo yanayowajengea uwezo wahandisi wa ndani na vijana wataalamu kwa madhumuni ya kuendesha gridi ndogo ndogo zinazoendelea kujengwa hapa nchini.

Pia alisema lengo la JUMEME ni kutoa umeme wa uhakika na wa bei nafuu kwa wakazi husika hususani maeneo ambayo umeme gridi ya Taifa haiwezi kufika.

“Lengo letu ni kufunga mifumo 300 ya uzalisha umeme utakaoweza kuingizwa kwenye ya gridi ya Taifa na kusaidia watu zaidi ya 1,000,000 ifikapo mwaka 2023 katika vijiji mbalimbali nchini Tanzania.

Aliongeza kampuni hiyo ya JUMEME ilioundwa mwaka 2014  chini ya mradi wa "Micropower Economy roll out in Tanzania" na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), inalenga kukuza, kujenga, na kuendesha gridi ndogo za umeme jua katika vijijini mbalimbali  nchini.

TAA yasaidia kutokomeza mimba za Utotoni mkoani Tabora

0
0



Mbunge wa Viti Maalum wa Jimbo la Tabora, Mhe. Munde Tambwe (wenye gauni la kijani na njano) hivi karibuni akiwa na Kaimu Meneja Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Rose Comino (wa tatu kushoto) akimwakilisha, Mhandisi Julius Ndyamukama kukabidhi saruji tani 12.5 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike wa Kata mbalimbali za Tabora.
Kaimu Meneja Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Rose Comino (wa pili kushoto) hivi karibuni akimwakilisha, Mhandisi  Julius Ndyamukama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge Viti Maalum (CCM), Mhe. Munde Tambwe (wa tatu kushoto) mara baada ya kukabidhi msaada wa saruji tani 12.5, kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa kike wa shule za sekondari. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaTabora, Joseph Kashushura (kushoto) na Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndegecha Tabora (wapili kulia).
Moja wa Shule ya sekondari ya Kata ya Itonjanda ya Manispaa ya Tabora, ambayo itajengwa bweni la watoto wa kike ili kuondoa mimba za utotoni. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) hivi karibuni imetoa msaada wa saruji tani 12.5 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo.
***************************************


MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imeungana na Mbunge wa Viti Maalum na Wakazi wa Mkoa wa Tabora kusaidia jitihada zao za kutokomeza mimba za utotoni kwa kutoa msaada wa tani 12.5 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike wa shule za sekondari.

Akikabidhi saruji hiyo hivi karibuni katika Kata ya Itonjanda, Manispaa ya Tabora, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Julius Ndyamukama, ambayo ni sawa na mifuko 250 ya saruji, Kaimu Meneja wa Biashara wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Rose Comino, amesema TAA, ipo bega kwa bega katika suala zima la kusaidia jamii katika masuala mbalimbali likiwemo la Elimu, ambapo watoto wote ni sawa na wanastahili kupata elimu na sio kukatizwa masomo kutokana na vikwazo mbalimbali zikiwemo mimba za utotoni.

Rose amesema Wananchi wa Tabora waungane kwa pamoja kuunga mkono jitihada za Mhe. Mbunge Viti Maalum Munde Tambwe la ujenzi wa mabweni kwa ajili ya watoto wa kike wa shule za sekondari, ambao wanatembea umbali mrefu kwenda shule, ambapo sasa watokomeza mimba za utotoni na kushirikiana kuwabaini wale wote wenye kutenda matendo hayo maovu.

“Kwa pamoja tuoneshe jitihada za dhati kwa kuhakikisha watoto wetu wanakuwa sehemu salama mabwenini, ninauhakika wa asilimia 100 kwa 100 tutapata watoto wengi wa kike watakaomaliza shule na kufanya vizuri katika masomo yao,” amesema Rose.
Amesema TAA ni miongoni mwa taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na.30 ya mwaka 1997 na kupewa dhamana na Serikali ya kuvisimamia na kuviendesha jumla ya viwanja 58, imekuwa ikitekeleza sera yake ya kurudisha kwa Jamii katika masuala mbalimbali yakiwemo ya elimu.

Rose amesema viwanja vya ndege vinatoa fursa mbalimbali za kibiashara zikiwemo za kuendesha migahawa, hoteli, maduka ya bidhaa mbalimbali, usafirishaji wa mizigo ikiwemo mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Pia viwanja vya ndege vimekuwa ni miongoni mwa eneo linalozalisha ajira rasmi na zisizo rasmi, ambazo zinahusisha mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yenye kutoa huduma katika maeneo ya viwanja vya ndege.

Naye Mhe. Tambwe ameushukuru uongozi mzima wa TAA kwa kusaidia jitihada hizo, ambazo anauhakika kwa lengo alilojiwekea ataweza kusaidia ujenzi wa mabweni mengi katika kila kata ya Mkoa wa Tabora.

“Naomba ndugu zangu tuunge jitihada hizi nilizoanzisha, na pia kuungana na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kutoa elimu bure, mimi nimezaliwa hapa Tabora na nimeona jinsi gani mabinti zetu wanavyotembea umbali mrefu kwenda na kurudi shule jambo ambalo linachangia kupata vishawishi njiani na kujikuta wanapata mimba za utotoni.” Amesema Mhe. Tambwe.

Hatahivyo, amesema mifuko 100 kati ya hiyo 250 itapelekwa kwenye Kata ya Itonjanda, ili ujenzi uanze mara moja, na 150 iliyosalia itapelekwa kwenye shule nyingine.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itonjanda ameshukuru msaada huu uliotolewa na TAA kwani watoto wamekuwa wakitembea umbali wa Kilometa 10 kwenda shule, na wamekuwa wakiathirika kutokana na kupata mimba.

“Tumuunge mkono Rais wetu kwani Tanzania bila elimu haitaienda tuunge jitihada hizi kwani watoto wanakuwa wananawiri sana wanapoingia shule za sekondari, kwani wamekuwa wakipewa fedha ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikiwaponza na kujikuta wanapata ujauzito.” Amesema.

IGP SIRRO AKIWA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA MKOA WA SIMIYU

0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, ACP William Mkonda na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani humo wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Dodoma. Picha na Jeshi la Polisi.

BANDARI LUSHAMBA KUMEKUCHA...SIKIA ANACHOKISEMA MENEJA WA TPA ZIWA VICTORIA

KATIBU MKUU DKT. MNYEPE ASHIRIKI MKUTANO WA HAKI ZA BINADAMU BEIJING, CHINA

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe yuko nchini China kushiriki Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea  unaofanyika jijini Beijing. 

 Mkutano huu uliondaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China kwa kushirikiana na Ofisi ya Habari ya Baraza la Taifa la nchini humo, umelenga kuzikutanisha  nchi zinazoendelea kwa lengo la kubadilishana taarifa na kujadili kwa pamoja masuala ya Haki za Binadamu.

Dkt. Mnyepe  ambaye pia aliwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano huo, amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zingine duniani katika kulinda na kutetea Haki za Binadamu sambamba na kuendelea kuheshimu, na kufuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutokuingilia masuala ya ndani ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing, China.
Sehemu ya hadhira iliyojitokeza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea wakifuatilia hotuba iliyokuwa ukitolewa na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing, China.  
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images