Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAIFA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA JIJINI MWANZA

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally alipowasili kwa ajili ya Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana kuelekea ukumbini na Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally tayari kwa Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wajumbe kabla ya kuanza Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiongoza Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani na Rais Wa Zannzibar na Baraza la Mapinduzi Dkt. Ally mohamed Shein pamoja na Makamu wa Rais  Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Jijini Mwanza leo Desemba 11, 2019.


RATIBA YA MAZISHI YA NDUGU YETU JOHNSON MASABALA MJINI BUKOBA

VOA SWAHILI: Duniani Leo December 10th, 2019

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI, LEO

UJENZI BANDARI YA LUSHAMBA WATUMIA SH.BILIONI 1.265, HUDUMA KUANZA RASMI MWEZI HUU...WANANCHI WAISHUKURU TPA, SERIKALI KWA KUWAJALI

$
0
0
 Gati ya Bandari ya Lushamba iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza ikiwa imekamilika baada ya Mamlaka ya Usimamizi ya Bandari nchini(TPA) kutumia Sh.bilioni 1.265 kuboresha miundombinu ya bandari hiyo ili kutoa huduma kwa wananchi wanaozunguka Visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria.
 Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Kanyara Benjamin Nhungwizi akielezea faida ambazo wananchi wanaozunguka Ziwa Victoria watazipata baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya Bandari ya Lushamba iliyopo katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Mchindiuza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu katika Bandari ya Lushamba na inatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mwezi huu.Waandishi hao wapo kwenye kutembelea miradi ya TPA katika Ziwa Victoria.
 Baadhi ya waendesha  mitumbwi katika Bandari ya Lushamba wakiwa katika maandalizi ya kuanza safari ya kutoka bandarini hapo kuelekea moja ya visiwa vilivyomo katika Ziwa Victoria
 Mmoja ya wakazi wa kijiji cha Kanyara akiwa katika mtumbwi wake katika bandari ya Lushamba wilayani Sengerema ambapo ametumia nafasi hiyo kuiopongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu ya bandari hiyo
  Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Mchindiuza(kushoto) akiwa na baadhi ya waandishi akiangalia namna ambavyo kamera aina ya Droon ikichukua picha za bandari ya Lushamba.
 Moja ya jengo la bandari ya Lushamba likionekana kwa mbali baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya bandari hiyo



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Sengerema

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) katika Visiwa vya Ziwa Victroria imesema kuwa ujenzi wa miundombinu katika bandari ya Lushamba katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema ambao umetumia Sh.bilioni 1.265 umekamilika na hivyo huduma rasmi katika bandari hiyo unatarajia kuanza mwezi huu.

Kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa bandari la Lushamba usalama wa abiria na mzigo yao hakuwa salama kwani walikuwa wakilazimika kabla kuingia kwenye chombo kuanza kupita kwenye maji hali iliyokuwa changamoto hasa kwa wagonjwa ambao hawakuwa na uwezo kabisa wa kupita ndani ya maji.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Mchindiuza wakati akizungumza na waandishi wa habari waliopo katika ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya uboreshaji wa miundombinu katika Ziwa hilo ikiwa ni mkakati wa TPA kuhakikisha inaboresha miundombinu ya bandari.

Amefafanua kuwa banari ya Lushamba inapatikana katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Segerema na kwamba wao kama mamlaka ya bandari wamewekeza kwa kujenga mundombinu kama inavyonekana. "Mradi huu wa ujenzi wa gati la Lushamba rasmi ulianza mwaka 2105 lakini wakati tukiwa tunaendelea na ujenzi wa upande wa gati kuna changamoto za mgogoro wa ardhi uliibuka na baada ya kuumaliza, tukaendelea na ujenzi mwaka 2018 na sasa umekamilika.

"Mradi huu kwa ujumla wake umehusisha ujenzi wa gati, jengo la abiria, jengo la kuhifadhia mizigo pamoja na eneo la vyoo na sehemu ya ulinzi. Jumla mradi hu umegharimu Sh.bilioni 1.265 kama. Matarajio ya mradi huu utaweza kutoa huduma katika visiwa zaidi ya sita ambavyo vinazunguka eneo hili la Lushamba,"amesema Mchindiuza na kuongeza visiwa hivyo vinategemea kupata huduma katika bandari hiyo ya Lushamba.

Amesema kama ambavyo ameeleza awali katika Ziwa Victoria kuna vsiwa vingi ambavyo vimejengewa miundombinu na ndani ya hivyo vsiwa kuna watu wanaishi ambao wanategemea kila kitu kisafirishwe hadi kuwafikia kwa kutegemea miundombinu hiyo ya bandari.

"Kabla ya ujenzi wa bandari hii watu moja kwa moja walikuwa wakipanda kwenye vyombo kwa kupita kwenye maji lakini pia kulikuwa na wagonjwa ambao walikuwa wanashindwa kupanda kwenye hivyo yombo vya maji.Baada ya ujenzi huu wananchi wanafurahia na wanasema sasa angalu wanao taasisi na Serikali kwa ujumla inawajali.

"Matarajio yetu ndani ya mwezi huu Bandari ya Lushamba itaanza kutoa huduma rasmi kwa kuhudumia wananchi wanaozungika visiwa vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria kwa kuanzia na kuishia hapa. Vyombo ambavyo mnaviona vimezagaa hapa kisiwani, vyote vitaanzia safari hapa kwenye gati la Lushamba , ikiwa pamoja na abiria kukata tiketi kwa ajili ya safari pamoja na kusafirisha bidhaa zao,"amesema na kuongeza ni matarajio yao kuona shehena kubwa iliyokuwa ikipita maeneo hayo sasa shehena zaidi za mizigo pamoja na abiria watapita katika bandari hiyo.

Akieleza zaidi kuhusu hali ya mazingira kabla ya ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo, Mchindiuza amesema kuwa kabla ya ujenzi wa gati hilo wananchi walikuwa wakishuka moja kwa moja kwenye maji, walikuwa wakishuhudia baadhi ya wananchi wakiangukia ndani ya maji kwa kushindwa kupanda ngazi lakini sasa mambo ni tofauti. "Kwa ujumla hali haikuwa nzuri kuumfanya mwananchi aingie kwenye chombo lakini kwa kujenga gati hili tumewasaidia kiusalama. Chombo kitapaki pembeni, abiria au mizigo itapakiwa vizuri na kisha safari kuanza".

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kanyara Benjamin Nhungwizi amesema kuwa anaishukuru Serikali kuu kwa kuliona eneo lao hilo la kwa kuweka vizuri miundombinu ya bandari na anaamini uwepo wa bandari hiyo unamanufaa makubwa kwa wananchi.

"Kwanza biashara zitaongezeka kwasababu kutakuwa na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ambao wanaoingia kuchukua biashara na wanaotoka kuchkua biashara, kwa hiyo watafaidika.Tukiangalia biashara zinazotoka visiwani sana ni samaki , zinatoka visiwani kwenda maeneo ya mbali na pia biashara zinazotoka viwasiwani kwenda visiwani ni pamoja na viwanyaji kama bia na bidhaa nyingine ambazo zinahitajika kwa binadamu,"amesema.

Ametaja baadhi ya visiwa ambavyo vitanufaika na kukamilika kwa miundombinu ya bandari ya Lushamba ni Kasarazi , Gembare, visiwa jirani vya kijiji cha Soswa, Namango, Chembaya, Chemagati na Zikagura .Pia kuna Kisiwa cha Maiosme ambacho nacho kipi kata jirani ya kata yao na kwamba kabla ya miundombinu kukamilika biashara hazikuwa nzuri kwani hakukua na muingiliano mkubwa watu lakini sasa biashara zimechangamka.

MUFTI MKUU TANZANIA APIGA MARUFUKU MZIKI MOTO KTK MAHARUSI AU SHEREHE YOYOTE YA KIISLAM

SIMBA SC CLUB YAMTANGAZA KOCHA WAKE MPYA

$
0
0
Na Yassir Simba, Michuzi Tv

Mabingwa watetezi wa Tanzania bara Simba Sports Klabu imemtangaza Sven Vanderbroeck raia wa Ubeligiji kuwa kocha wake mkuu akichukua nafasi ya mbelegiji aliyetimuliwa hivi karibuni.

Vanderbroeck amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Zambia pia alishinda ubingwa wa Afrika( AFCON) akiwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon mwaka 2017.Kocha huyo atakuwa akisaidiwa na  Selemani Matola aliyetambulishwa jana.

 

Katika Kipindi cha Miaka 4 Tumeshuhudia Uwajibikaji- Waziri Mkuchika

$
0
0

Na. Immaculate Makilika -MAELEZO

Serikali ya Awamu ya Tano yafanikiwa kuleta mabadiliko ya kiutendaji yaliyosaidia kuongeza ufanisi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza leo jijini Dodoma, kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binandamu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, George Mkuchika alisema “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, inasimamia kikamilifu maadili katika utumishi wa umma, na katika kipindi cha miaka minne tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika utumishi wa umma.”

 Aliongeza “kiwango cha uadilifu katika utumishi wa umma kimeongezeka kwa kiasi kukubwa. Hivyo, ninapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza watumishi wote ambao wameitikia wito wa Serikali wa kuzingatia maadili katika utumishi wa umma”

Waziri Mkuchika, alibainisha juhudi mbalimbali ambazo Serikali imezichukua katika kuhakikisha utumishi wa umma unazingatia maadili, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mbalimbali zinazosimamia wa utendaji katika Utumishi wa Umma kama vile Sheria Na. 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, na miongozo mingine ya kiutumishi ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara.

Adha, jitihada nyingine za Serikali ni maboresho katika programu mbalimbali, pamoja na kuimarisha uadilifu katika sekta ya umma, kwa kutekeleza Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpangokazi wake, ambapo taasisi zote za umma zinapaswa kuwa na Kamati za Kusimamia Uadilifu.

Vilevile, Waziri Mkuchika amewataka viongozi wote katika utumishi wa umma kusimamia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi ili kutekeleza azma ya Serikali ya kuboresha utumishi wa umma kuwawezesha wananchi kupatiwa huduma bora na bila usumbufu wa aina yoyote. 

Ambapo, alisisitiza kuwa  Rais Magufuli, amekuwa kila mara akionesha kutokuvumilia watendaji wabovu  Serikalini, na  wananchi wameonyesha kufurahishwa na juhudi na msimamo wa Rais pamoja na Serikali yake katika kusimamia maadili katika utumishi wa umma. Umakini na uharaka wa Serikali katika kuchukua hatua dhidi wa watumishi wasiozingatia maadili sio tu umeongeza ufanisi kazini bali pia umeongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa, alisema kuwa watumishi wa umma wanatakiwa kukemea mambo mabaya na kuwa mfano bora kwa wengine.

Naye, Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Harold Nsekela, aliipongeza Serikali kwa kufanya maadhimisho ya maadili na haki za binaadamu nchini kwa vile yanatoa fursa kwa vongozi na watumishi wa umma kujitathimini.

“Naishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuheshimu mikataba ya Kimataifa na kuiridhia, kwani maadhimisho haya ni muhimu yanatoa fursa ya kujitathimini kama taifa limefanya jitihada za kutosha za kupambana na rushwa, kuzingatia misingi ya utawala bora, maadili na haki za binaadamu”.

Kongamano la Maadhimisho Siku ya Maadili na Haki za Binandamu, limefikia  kilele leo,likiwa na kauli mbiu inayosema maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha Utawala bora na Haki za binadamu, limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa utumishi wa umma pamoja na watumishi wa umma.


HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI IMEZIDI KUHIMLIKA

$
0
0


 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme Tanzania(TANESCO) na mwenyekiti wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa Tanesco, Dkt Tito Esau Mwinuka  akifafanua jambo katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika Mkoani Morogoro leo disemba 11,2019.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Morogoro leo disemba 11,2019.
……………………….
Na Farida Saidy Morogoro 

Hali ya upatikanaji wa umeme nchini imezidi kuhimlika ambapo kwa sasa mfumo wa gridi ya taifa una wastani wa zaidi ya megawati 200 kwa siku wakati mahitaji ya juu ya umeme yamapanda kufikia megewati 1120 mpaka kufikia Novemba 2019.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO na mwenyekiti wa baraza kuu, Dkt Tito Esau Mwinuka  katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa Tanesco leo disemba 11,2019.Mkoani Morogoro ambapo amesema kuwa hali ya utendaji na kasi ya utoaji huduma ndani ya shirika imezidi kuboreka ikiringanisha na hapo awari.  

Katika hatua nyingine Dkt Mwinuka  amesema kuwa mradi wa power reliability enhancement program( POREP )Utasaidia kuhakikisha miundombinu ya usambazaji umeme inafanyiwa matengenezo,na kuondoa kero ya kukatika katika kwa umeme,hivyo utasaidia kuokoa mapato ya yanayopotea kutokana na kukatika mara kwa mara kwa umeme.

Aidha makusanyo ya fedha za ndani yamepanda ukilinganisha na hapo awari ambapo kwa mwezi oktomba 2019 shilingi  bilioni 160.4 zimekusanywa huku oktoba 2018 shilingi bilioni 155.9 zilikusanywa,hata hivyo shirika linadaiwa shilingi bilioni 952 ambapo lipo katika mikakati ya kuweza kulipa deni hilo.

Kwa upande wake Mhe Mwalimu Mohamed Utaly Mkuu wa Wilaya ya Mvomero ambaye pia amemwakirisha Mkuu wa Mkoa wa Mrogoro Mhe Loata Sanare akifungua mkutano huo amelipongeza shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa kazi kubwa inayoifanya ya kusambaza na kuunganisha umeme kwa  wananchi wa mijini na vijijini.

 Hata hivyo amelitaka shirika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kukatika kwa umeme mara kwa mra,ambpo amesema kukatika kwa umeme kunasababisha hasara kubwa kwa watanzania hususani wenyevinda na vikubwa vidogo .

Mkutano huo unaketi mkoani morogoro kwa siku tatu ambapo umefunguliwa na mkuu wa wilaya ya mvomero ambaye amemwakilisha mkuu wa Mkoa Wa Morogoro Mhe Loata Sanare na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo,Paul Sangeza Mwenyekiti wa TUICO, Mhandisi Elangwa Mgeni Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco ya kujenga na kurekebisha miundombinu ya umeme (ETDCO).

Wengine ni Shairu Idrissa mwakirishi wa Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco inayoshughurika na utafiti wa uzarishaji umeme kutumia joto ardhi (TGDC)mhandisi yusuphy kitivo kaimu meneja mkuu wa kampuni tanzu ya tanesco inayoshughurika  na utengenezaji wa nguzo za zege (TCPM)

MKURUGENZI MKUU TANTRADE AWATAKA WADAU WA ALIZETI MKOANI SINGIDA KUPANGA MIKAKATI YA PAMOJA KUONGEZA UZALISHAJI ALIZETI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka amewataka Wadau wa Alizeti wa Mkoa wa Singida kupanga mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa Alizeti ili kutosheleza mahitaji makubwa ya viwanda vya kusindika alizeti ambavyo vinashindwa kuzalisha mafuta kwa mwaka mzima kutokana na kukosekana kwa malighafi.

Bw. Rutageruka ametoa wito huo wakati akiongea na Wasindikaji, wakulima wa alizeti na watendaji wa Serikali wakati wa Mkutano na Wadau wa alizeti wa Mkoa wa Singida uliofanyika leo tarehe 11.12.2019 katika Ukumbi wa VETA.

Mkutano huo umeandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Singida pamoja na Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Singida ( SISUPA) na kushirikisha Wadau wapatao 110 kutoka Mkoa wa Singida.

MAHAKAMA YAWAHUKUMU MIAKA MIWILI JELA MALINZI NA MWESIGWA AU FAINI SH. 500,000

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani au faini ya shilingi laki tano kwa aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini (TFF) Jamal Malinzi kwa shtaka ya kughushi nyaraka za muhtasari wa kikao cha kamati tendaji ya TFF huku aliyekuwa katibu Mtendaji   Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa akikutwa na mashtaka 2 ikiwemo  kughushi nyaraka za muhtasari wa kikao cha kamati tendaji ya TFF na shitaka la kutengeneza nyaraka za uongo ambapo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani au kulipa faini ya shilingi milioni moja.

Akisoma hukumu hiyo kwa masaa matano Hakimu Mkazi Maira Kasonde amesema kuwa washtakiwa wote walikutwa na mashtaka 30 na mahakama imeona hawana kesi ya kujibu katika mashtaka 10 yakiwemo matumizi mabaya ya ofisi, kughushi nyaraka, kujipatia Fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa Fedha.

Amesema kuwa katika mashtaka ya kujipatia Fedha kwa njia ya udanganyifu yaliyokuwa yanamkabili Malinzi upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha hilo kwa kushindwa kuleta ripoti za Ukaguzi zilizoonesha kuwa fedha zilizopokelewa zilikuwa halali au vinginevyo.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Kasonde amesema kuwa mashtaka hayo hayajathibitishwa kwa kuwa fedha alizopokea Malinzi ambazo ni dola za kimarekani 173,335 na shilingi 39,100,000 ni marejesho ya mkopo aliyoikopesha TFF.

Amesema ushahidi hautoshelezi kueleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walitumia vibaya madaraka yao kwa kuwa hakuna faida waliyoipata na fedha zilizopokelewa zilikuwa ni marejesho ya mkopo.

Pia mahakama hiyo imewaachia huru aliyekuwa mhasibu wa Shirikisho la mpira nchini (TFF)  Nsiande Mwanga na karani wa Shirikisho hilo Frola Lauya.

Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi Simon Wankyo aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu Kali wa washtakiwa wawili ambao ni aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini  (TFF) Jamal Malinzi na aliyekuwa katibu mtendaji wa shirikisho hilo Celestine Mwesigwa.

Wakili wa utetezi Nehemia Nkonko aliiomba Mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu  kwa kuwa wamekaa gerezani kwa miaka miwili na nusu, pia washtakiwa hao hawajawahi kukutwa na shtaka lolote hivyo adhabu itakayotolewa izingatie kuwa washtakiwa walitenda hivyo kwa kuiokoa TFF na sio kwa kujinufaisha wao wenyewe.

Nkonko alisema kuwa mshtakiwa Malinzi  amekuwa akisumbuliwa na tatizo la presha na umri wake wake  kwa sasa ni miaka 60, na kwa upande wa mshtakiwa wa pili Celestine Mwesigwa ana mama wa miaka 89 ambaye ni mgonjwa na watoto wadogo ambao wanamtegemea hivyo mahakama iwapatie unafuu wa adhabu.

  Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi pamoja na katibu Mtendaji  wa  Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa wakiwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya hukumu yao kutolewa ya kwenda jela miaka miwili ama kulipa faini ya shilingi laki 500,000/=.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi pamoja na katibu Mtendaji  wa  Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa wakiwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jioni ya leo walipokuwa wakisubiri kusomewa hukumu.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi pamoja na aliyekuwa karani wa Shirikisho hilo Frola Lauya wakiwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jioni ya leo walipokuwa wakisubiri kusomewa hukumu.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv).

WANANCHI WANAOTUMIA BANDARI YA MAGARINI WILAYANI MULEBA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUAMUA KUBORESHA MIUNDOMBINU

$
0
0
 Baadhi ya abiria wakipakia mizigo katika boti za abiria katika Bandari ya Magarini wilayani Muleba mkoani Kagera.Bandari hiyo imeboreshwa kwa kujengwa kwa miundombinu yake ikiwemo majengo ya ofisi, vyoo na gati kwa ajili ya meli na boti kuegesha bandarini hapo.

 Baadhi ya abiria wakiingia ndani ya boti ya abiria kabla ya kuanza kwa safari kutoka Bandari ya Magarini kuelekea katika visiwa vingine vilivyomo katika Ziwa Victoria.

 Abiria wakiwa wamekaa ndani ya boti kwa ajili ya kuanza safari katika bandari ya Magarini.

 Mmoja wa wakazi wa Muleba akiwa katika bandari ya Magarini (aliyenyoosha vidole) akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliofika bandarini hapo kuangalia uboreshwaji wa miundombinu katka bandari hiyo.

 moja wa wananchi akielekea kupanda boti ya abiria katika bandari ya Magarini wilayani Muleba mkoani Kagera.
Boti ya abiria ikiwa imeegesha ikisubiri kuanza kupakia abiria katika Bandari ya Magarini wilayani Muleba mkoani Kagera.



Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Muleba

WANANCHI wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera na hasa wanaoutumia usafiri wa meli na boti za abiria kufanya safari zao mbalimbali katika Visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria wameipongeza Serikali Kuu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kwa hatua yake ya kuboresha miundombinu ya Bandari ya Magarini ambayo sasa imekamilika.

Wakizungumza na Michuzi Globu ya Jamii pamoja na Michuzi TV, wananchi hao wamesema kuwa hakika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli kupitia TPA umeonesha namna ambavyo umedhamiria kuboresha maisha ya watu kwa kuhakikisha huduma muhimu zinapewa kipaumebele na kwamba wao miundombinu ya bandari katika Ziwa Victoria ni muhimu kwani ndio njia rahisi ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Akizungumza leo kuhusu bandari ya Magarini, Mkazi wa eneo hilo Paul Stephen amesema kuwa wanathamini kazi inayofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika kuboresha miundombinu ya bandari hiyo ambayo kabla ya uboreshwaji wa miundombinu wananchi walikuwa wanapata huduma ya usafiri wa boti za abiria katika mazingira magumu.

"Tunatoa shukrani kwa Serikali pamoja na Mamlaka ya Bandari kwa hatua hii iliyochukua ya kuboresha majengo , gati na ofisi za Bandari ya Magarini ambayo kwetu ni muhimu katika shughuli za kiuchumi.Tunaitegemea sana kwani ndio ambayo tunaitumia tunapotaka kufanya safari zetu za kila siku.Kwa uboreshaji wa miundombinu ambao umefanyika, tutaona manufaa yake na itakuwa chachu ya maendeleo kwetu,"amesema Stephen.

Wakazi wengine wa eneo hilo wametoa ombi kuhusu kuangaliwa upya kwa ushuru ambapo walisema wanalipa Sh.600 wakati katika maeneo mengine bei ya ushuru kwa kila abiria ni Sh.200 au Sh.400.Hivyo ni matarajio yao Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari itasikia kilio chao kwa kushusha gharama za ushuru.

Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika Bandari za Ziwa Victoria Morric Mchindiuza amesema kuwa amesikia maombi ya wananchi hao kuhusu bei ya ushuru.Amesema kuwa katika bandari zote nchini gharama ya ushuru kwa kila abiria ni Sh.600 na kinachotokea kuna bandari bubu ambazo zenyewe zinatoza bei ya Sh.200 hadi Sh.400.

"Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, tunao utaratibu ambao unatambulika kisheria kuhusu ushuru na tozo nyingine.Hili la ushuru wa abiria bandari zote nchini bei yake ni moja na hivyo kinachosemwa na wananchi ni ushauri ambao tumeuchukua na tutaufanyia kazi.Hata hivyo kama ambavyo tumekuwa tukielekeza kila siku bandari bubu zinakwenda mwishoni , hivyo bei ya ushuru itabaki ile inayotambuliwa na TPA,"amesema Mchindiuza wakati anafafanua kuhusu gharama za ushuru bandarini.

Kuhusu bandari hiyo ya Magarini amesema kuwa kwa sasa ujenzi wa miundombinu umekamilika kwa asilimia kubwa na kilichobaki ni kuanza kutumika rasmi kwa majengo ya bandari hizo ingawa kwa upande wa gati imeanza kutumika.

"Tumejipanga kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya bandari zetu za Ziwa Victoria na ndio maana kila mahali ambapo tunakwenda utakuta aidha ujenzi umekamilika au unaendelea na mkakati wetu ni kuhakikisha usafiri wa meli unakuwa wa uhakika ili wananchi sasa waweze kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine,"amesema Meneja huyo.

TCRA YAONYA MAKAMPUNI YA SIMU KUUZA LAINI ZA SIMU BILA KUSAJILIWA

$
0
0
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Imelda Salumu akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji  wa usajili wa laini za simu kwa njia ya vidole Babati mkoani Manyara.
 Elizabeth Kitundu Mkuu wa Wilaya ya Babati akizungumza katika mkutano huo na wananchi waliojitokeza kwaajili ya kusajili laini zao za simu pamoja na kufuata namba zao za NIDA ,Kulia kwake ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA)Mhandisi Imelda Salum.
Mgeni rasmi Elizabeth Kitundu Mkuu wa Wilaya ya Babati akiwa na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA)Mhandisi Imelda Salumu pamoja na wadau wa mawasiliano kutoka makampuni ya simu mara baada ya kutoa elimu kwa wananchi na kuwaeleza umuhimu wa kusajili laini zao za simu.
Emmanuel joshua-Afisa NIDA mkoa Manyara akizungumza katika mkutano huo wilaya ya Babati.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Babati wakiwa katika foleni kwenye Banda la NiDA wilayani Babati Mkoani Manyara.



Na.Vero Ignatus,Manyara

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)imeonya makampuni ya simu kuuza laini za simu bila kusajiliwa ikiwa ni mkakati wa serikali kuzuia matumizi ya laini za simu yanayokiuka maadili na sheria za nchi.


Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Imelda Salum   amesema kuwa malengo ya Serikali kusajili laini za simu ni kuhakikisha usalama wa raia unaoweza kufanyika kupitia mitandao ya simu na pale mwanamchi anapotumia huduma za mawasiliano.

Mkuu huyo wa kanda  amesema kuwa mwananchi akisajili laini yake ya simu kutumia alama za vidole na kwakutumia namba za NIDA ni rahisi serikali kuwatambua watu ambao  wanatumia huduma hiyo kinyume na taratibu na sheria zilivyowekwa .

Amesema kuwa mwananchi anaposajili laini yake ya simu kwa alama ya vidole na namba ya NIDA kuisaidia serikali kuwa na takwimu sahihi za watumiaji wa mawasiliano kwaajili ya mipango mbali mbali ya Serikali.

"Kuna watu wanatumia laini ishirini thelathini lakini ni laini ambazo huwezi kuzijua zinamilikiwa na nani anaweza akazitumia vibaya kuwaibia watu,kuwatapeli , kutukana wengine ,kutumia kugha za kuudhi kwenye mitandao" Alisema Mhandishi Imelda

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu ametoa wito kupitia uhamasishaji wa kusajili laini za simu wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya usajili kabla ya muda uliowekwa kufikia mwisho.

"Kifungu cha kumi cha kanuni cha kukinda watumiaji cha mwaka 2018 zinamtaka mtu yeyote anayeuza au anayetoa laini yeyote ya simu aisajili kwanza kabla haijatumika"alisema Dc Babati.

Amesema zoezi hilo linaloendeshwa na TCRA la kusajili lipo kwenye masuala ya kisheria na haitakiwi  na hairuhusiwi mtu kutumia laini ya simu bila kuisajili.

Amesema kuwa TCRA kwa kushirikiana na wadau na kamati zilizoundwa ilizindua rasmi zoezi la usajili wa laini za simu kwa wa alama za vidole kwa nchi nzima ambapo usajili huo unaendelea katika maduka yote ya watoa huduma za mawasiliano pamoja na mawakala wenye vitambulisho maalum

Mhe. Kitundu amesema kuwa usajili wa majaribio ulizinduliwa rasmi machi 2018 kwenye mikoa sita ikiwemo mkoa Magharibi Zanzibar,Dar es salaam, Iringa,Singida ,Pwani na Tanga ambapo ulionyesha mafanikio makubwa. 

Aidha amesema kuwa hadi sasa jumla ya laini za simu zilizosajiliwa hadi kufikia 22 Novemba 2019 jumla ya laini milioni 16.9 zimesajiliwa sawa na asilimia 38% ya laini zote za simu zinazotumika.

Mhe.Kitundu amesema Laini zote za simu zinazotumika zinakadiriwa kuwa zaidi ya  milioni 45 hivyo bado idadi ya waliosajili ipo chini na inaonyesha kuwa wananchi wengi haqajasajili laini zao za simu.

Serikali kupitia TCRA inarndelea kutoa elimu kwa umma juu ya usajili wa laini za simu kwa alama ya vidole na kuwahimiza watumiaji wote wa huduna za mawasiliano na kuhakikisha kuwa wanasajili laini zao kwa mujibu wa sheria za nchi.

Naye Afisa kutoka Mamlaka ya vitambulisho ya Taifa NIDA Emmanuel Joshua amesema jukumu lao kuu ni kuweza kutoa utambulisho pamoja na kutoa vitambulisho vya Taifa,ambapo wanafanya  majukumu hayo sambamba,kwani kitambulisho ndicho ambacho kinatangulia ambapo kitambulisho ni matokeo ya juhudi ya kutengeneza mfumo wa utambulisho  

Amesema kwa kushirikiana  na Mamlaka ya Mawasiliano wamekuwa wakifanya juhudi hizo kuhakikisha kuwa zoezi la usajili wa laini za simu linafanikiwa na wananchi wote wanasajili kwa kutumia alama za vidole.

Amesema kwa upande wa wilaya ya babati zoezi hilo linaendelea vizuri kwani matarajiao yalikuwa ni kusajili laini 253025 ambapo hadi sasa wameweza kusajili watu kwa asilimia 94%ya watu waliolenga kuwasajili hivyo wananchi wameitikia wito kwa wingi.

Amewataka wananchi kuweza kufuatilia namba zao za usajili kwani zoezi la kuwasajili wanachama wanachama wapya bado linaendelea,amewataka kwenda kuangalia namba namba zao katika ofisi za watendaji kwa wale ambao watakuwa wamepata changamoto waweze kufika ofisi za NIDA Manyara ili waweze kupatiwa huduma.

WAZIRI JAFO AAGIZA HALMASHAURI NCHINI KUIGA UFANISI WA MIRADI YA WILAYA YA IKUNGI

$
0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI)  Mhe. Suleiman Jafo akizungumza na Mtaalamu wa Maabara Bi. Happyness Nyaruke wakati alipotembelea kituo cha Afya Sokoine Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI)  Mhe. Suleiman Jafo, akikagua Kituo cha Afya Sokoine Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi (wa nne kulia) akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI)  Mhe. Suleiman Jafo. 
 Muonekano wa majengo ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI)  Mhe. Suleiman Jafo, akipata maelezo ya  ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Edward Mpogolo akizungumza na watumishi waliohudhuria kwa ajili ya kumsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jaffo wakati wa ziara yake katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jafo juu ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wakati alipotembelea ofisini hapo.
 Muonekano wa majengo ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  Mhe. Juma Ali Mwangi akizungumza.
 Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu, Singida
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jafo amempongeza hadharani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya eneo hilo kwa gharama ndogo sana ikilinganishwa na uhalisia.
Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake kupitia mfumo wa ‘force account’, wameweza kutumia kiasi cha sh. 420 milioni pekee kujenga ukumbi wa mikutano wa kisasa na wenye viwango, na 200 kujenga jengo kubwa la ofisi, huku akisisitiza kwa kuzitaka halmashauri ambazo bado hazijaanza ujenzi wa majengo ya ofisi na kumbi za kisasa za mikutano kuja kujifunza Ikungi.
Waziri Jafo akiwa kwenye ziara ya kawaida mkoani Singida, na kupata fursa ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya, na miradi mingine ya halamshauri akitokea Jijini Mwanza, alisema katika uongozi wake amepita kwenye halmashauri nyingi lakini hajawahi kukutana na jengo la ukumbi mzuri na wa kisasa kama huo wa halmahauri ya Ikungi.
“Mkurugenzi kilichonifurahisha ni namna mlivyozingatia thamani ya pesa (value for money) na ubora, nilisema nataka ofisi ya TAMISEMI ifanye mabadiliko na mapinduzi ya kiutendaji, tulikotoka huko nyuma hatukuwa na sifa nzuri, lakini leo hii kila mahali ukitazama ikiwemo hapa Ikungi huwezi kuamini,” alisema
Alizitaka halmashauri za Kondoa na Iramba kwa kuanzia kuja kujifunza kupitia wenzao hao wa Ikungi, ambao idadi ya majengo yao yote yamegharimu sh 1.5 bilioni pekee “nataka wengine wakitaka kujenga ofisi waje kujifunza hapa, iwe duplicate kwa wengine kuja kucopy na kupaste,” alisema Jafo
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo alisema kiasi hicho cha pesa sh 1.5 bilioni kilitolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa halmashauri hiyo kwenye eneo la utawala bora.
Alisema kati ya pesa hizo sh 1.3 milioni zimetumika kujenga ofisi, nyumba ya DC, na Hospitali ya wilaya, huku Serikali ikiwa tayari imewatengea fedha nyingine zaidi ya sh. milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa vituo vya afya vya Sepuka, Ihanja na Iyumbu.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi, Justice Kijazi, alisema tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo mwaka 2013, watumishi wa eneo hilo wamekuwa wakipanga na kukodi majengo ya watu binafsi kwa mikutano mbalimbali, ikiwemo kutumia hadi nyumba za wageni kwa shughuli za ofisi.
….alisisitiza kuwa jengo la ukumbi huo mpya na wa kisasa mbali ya kutumika kwa shughuli mbalimbali za mikutano ya kikazi, lakini pia litatumika kama kitega uchumi cha kuingizia halmashauri hiyo mapato, huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Ali Mwangi, akimuomba Waziri Jaffo kusaidia mchakato wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya kwa ustawi wa afya ya wakazi wa eneo hilo.
Hata hivyo, pamoja na kufurahishwa na Ikungi lakini hakufurahishwa na utendaji na usimamizi wa miradi ya vituo 2 vya afya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Iramba, ambavyo kwa mda mrefu ujenzi wake umekuwa ni wa kusuasua.
“RAS (Katibu Tawala wa mkoa) mwambie RC (Mkuu wa Mkoa) nimesikitishwa sana na watu wa Iramba, pale kuna uzembe wa hali ya juu unaofanywa na DC na DED, haiwezekani fedha zimekwenda lakini bado matatizo ya kutokamilika kwa vituo hivyo viwili vya ‘ndago’ na kinampanda yakiendelea,” alisema Jafo
na kuongeza; “Natoa siku 4 leo jumanne (jana) nataka ninapoondoka hapa kufikia ijumaa nipate maelezo ya DC na Mkurugenzi wake kwanini wasiwajibishwe,” alisema.

BANDARI YA NYAMIREMBE WILAYANNI CHATO KUFUNGUA MILANGO USAFIRISHAJI MIZIGO NA ABIRIA, KUIMARISHA SHUGHULI ZA UTALII

$
0
0
 Uzio wa Bandari ya Nyamirembe ukiwa umeshakamilika kama sehemu ya kuimarisha usalama bandarini hapo baada ya ujenzi wa miundombinu yake kukamilika.
 Baadhi ya nyumba za zamani ambazo zilikuwa zinatumiwa na watumishi wa Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita.
 aadhi ya mafundi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa kuhusu ujenzi wa bandari ya Nyamirembe kutoka kwa Meneja wa TPA Bandari za Ziwa Victoria Morric Mchindiuza (PICHA ZOTE NA SAIDI MWISHEHE-CHATO)
 Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa gati lililojengwa katika bandari ya Nyamirembe wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) kuboresha miundombinu ya ya bandari za Viwa Victoria
 Muonekano wa gati ya Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 awamu ya kwanza na mkakati wa Mamlaka ya Bandari ni kuanza ujenzi wa awamu ya pili ya gati hiyo ili kuosogeza kwenye kina kirefu cha maji kwa ajili ya meli kubwa kuweza kushusha na kupakia abiria pampoja na mizigo.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa gati ya Bandari ya Nyamirembe ambayo tayari imekamilika kwa awamu ya kwanza.
 Sehemu ya muonekano wa gati ya Bandari ya Nyamirembe baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.
 Mhandisi Anderson Robert Ndogae akizungumza waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa gati ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita.
 Moja ya jengo la Bandari ya Nyamirembe likiwa limekamilika ikiwa ni mkakati wa ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo kwa ajili ya kuboresha usafiri wa meli Ziwa Victoria.

Said Mwishehe Michuzi Globu ya jamii -Chato

IMEELEZWA kwamba hatua ya Mamlaka ya Usimami Iwa Bandari Tanzania (TPA), kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita, sasa kutafungua milango ya usafirishaji wa mzigo na shughuli za utalii nchini. 

Pia imeelezwa bandari hiyo itakapokamilika itakuwa ni uwezo wa kusafirisha mizigo katika nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuanzia Machi mwaka 2020 baada ya kukamilika kwa meli zinazoendelea kujengwa na nyingine kufanyiwa matengeneza makubwa katika Ziwa Victoria. 

Hayo yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machindiuza alipokuwa akielezea hatua za ujenzi wa bandari hiyo ambapo tayari baadhi ya majengo yamekamilika huku awamu ya kwanza ya gati nayo ikiwa imeshamilika licha ya kuwepo kwa awamu ya pili ya ujenzi wa gati hiyo ili kuosegeza kwenye kina kirefu cha maji kwa ajili ya meli kubwa kuweza kushusha na kupakia mizigio na abiria.

Amefafanua kuwa Bandari ya Nyamirembe ni mlago muhimu kwa uchumi wa Ziwa Victoria kwani kwa muda mrefu ilikuwa na manufaa kwa wananchi na wasafirishaji wa mizigo na kuchochea maendeleo huku akisisitiza kuwa bandari hiyo ni muhimu kwa TPA na wananchhi kwa ujumla hasa.

"Historia ya Bandari ya Nyamirembe ni kwamba ilianza kufanyakazi mwaka 1960 na tangu wakati huo ilikuwa chini ya Shirika la Reli Tanzania(TRC).Hata hivyo kutokana na mabadiliko ilipofika mwaka 1997 ilikabidhiwa kwa Kampuni ya Huduma za  Meli na tangu wakati huo zipo meli zilikuwa zikifika hapa na kutia nanga na ambayo ilikuwa na uwezo wa kuibeba abiria 593 na kuibeba tani 350,"amesema.

Ameongeza kuwa na meli hiyo ilikuwa ikibeba mazao mbalimbali yakiwamo ya pamba, mchele na kwamba  ilikuwa kama daladala katika maeneo yote muhimu ilikuwa inasimama kuchukua abiria na mizigo. "Na sasa TPA kutokana na umuhimu wake tuliwekeza na kuiuhisha kwa kuanza ukarabati wake kwa gharama za za Shilingi bilioni 4.128 kwa kuhusisha ujenzi wa gati,mnara wa meli na  jengo la abiria.

Mchiundaza amesema kuwa bandari hiyo sasa itakwenda kuchochea utalii na hiyo inatoka na uwepo wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato, Rubondo ambapo pia shughuli za utalii zitaongezeka.

 "Tuna matarajio makubwa ya kuongezeka kwa watalii ambao watakuja kwenye hifadhi yetu mpya ya Burigi -Chato, hivyo kwetu sisi TPA ni fursa nyingine ya kibiashara kwani wengi watapenda kutumia usafiri wa meli kuja huku na kwa kukumbusha tu kusafiri kwa meli nako ni sehemu ya utalii na wengi watapenda."
Mwisho
 

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO DISEMBA 12,2019

WAKUU WAWILAYA ZOTE ZA MKOA WA ARUSHA KUSANYENI DATA ZA WAZAZI WASIOWEZA KUTIMIZA WAJIBU-GAMBO

$
0
0

Na Woinde Shizza, Arusha

Mkuu wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wakuu Wa wilaya zote za mkoa Wa Arusha kukusanya data za wazazi ambao wameshidwa kutimiza wajibu wao Wa kuwasomesha pamoja na kuwahudumia watoto wao ambao wapo chini ya miaka 18.

Aidha pia aliwataka wapeleke taarifa zote za matukio ya ambayo yameripotiwa kwenye wilaya zao yanaohusiana na ukatili Wa kijinsia klikiwemo idadi ya mashauri yaliopelekwa mahakamani , mangapi hayajapelekwa mahakamani ,na sababu ya kutopeleka ninini kama kunavikwazo waviainishe ili viweze kufanyiwa Kazi haraka iwezekanavyo.

Aliyasema hayo Jana kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Wa kijinsia kwa mkoa Wa Arusha yaliongozwa na maandamano ya jeshi LA Polisi na kuhitimishwa katika hospital ya rufaa ya mkoa Wa Arusha (mount Meru) ambayo yamebeba kauli mbiu ya "Kizazi chenye usawa simama dhidi ya ubakaji".

" tutachukuwa taarifa zote tutakazo zibaini na tutachunguza kama changamoto zipo katika mahakamani zetu , Polisi , au kwa wataalamu wetu Wa afya ambao wanatakiwa kutoa taarifa rasmi ya ripoti ya kitaalamu yakuthibitisha kama kweli kuna MTU amefanyiwa ukatili Wa kijinsia ili iwe kama ushaidi Wa kumpeleka muhalifu mahakamani tukiwa na ushaidi Wa kutosha na tunasema Leo sisi kama mkoa Wa Arusha tumeanza Kazi ya kuwasaka na kuwachukulia watu wale wote wanaofanya matukio ukatili Wa kijinsia"alisema Gambo

Alibainisha kuwa taarifa inaonyesha kadri Siku sinavyoenda matukio ya ukatili Wa kijinsia yanapungua lakini taarifa,mwitikio na twasira inaonyesha matukio ya ukatili Wa kijinsia yapo ,na hii inatokana uwezekano Wa baadhi ya matukio kutoripotiwa katika sehemu husika au baadhi ya wananchi wamekata tamaa baada ya kuona matukio wanayoripoti hayafiki katika hatua ambayo waowanategemea.

Kwa upande wake kamanda Wa Polisi mkoa Wa Arusha Jonathan Shana alisema wao kama kama jeshi LA Polisi wameshaanza Kazi rasmi ya kuwathibiti watu wanaofanya matendo ya ukatili Wa kijinsia nawanaanza rasmi kuwasaka popote pale walipo na watawachukulia hatua Kali za kisheria hivyo aliwasihi wananchi watii sheria bila shuruti , na kuwaambia kuwa mapambano ya kupinga ukatili Wa kijinsia ni wakila mtu awe mwanaume au mwanamke.

Nae mganga mfawithi Wa hospital ya rufaa ya mount Meru Shafii Msechu alisema kuwa kwa mwaka huu wamepokea waanga Waliofanyiwa ukatili Wa kijinsia 333 waliopelekwa mahakamani 10 kesi zilizopelekwa mahakamani zikiwa ni tisa na wanahakisha wahalifu wanachukuliwa hatua ,alisema wananchi wamekuwa hajitokezi kutoa taarifa za namna wanavyofanyiwa ukatili huo wengi wao wakiwa wanaogopa kuonekana kitu ambacho kinawanyima haki yao.

Nae kamishina msaidizi Wa Polisi ambae pia ni Mwenyekiti Wa mtandao Wa Polisi wanawake mkoa Wa Arusha (TPF-NET) Mary Kipesha alisema kuwa matukio ya ukatili Wa kijinsia yamepungua sana kwa mwaka huu tofauti na mwaka Jana ambapo Kwa kipindi cha mwaka 2018 kesi za ukatili Wa kijinsia ziliripotiwa 161 huku mwaka huu 2019 January hadi December zikiwa zimeripotiwa kesi 89 ambapo kunaupungufu Wa asilimia 32.5%.

Kwa upande Wa kesi za kulawiti mwaka Jana 2018 zilikuwa 62 huku mwaka huu 2019 kwa kipindi cha January adi December zikiwa na kesi 52 ambapo kunaupungufu Wa asilimia 7.9% na hii inaonyesha wamepata mafanikio makubwa mno ya kupunguza uhalifu Wa unyanyasaji Wa kijinsia , hivyo katika kuakikisha swala hili linaisha wataendelea kutoa Elimu kwa wanafunzi Wa mashuleni, vyuoni pamoja na wananchi kwa ujumla .


Mkuu Wa mkoa Wa Arusha akiongea katika kilele cha siku 16 cha maadhimisho ya wiki ya upingaji wa ukatili wa kijinsia kwa watoto
kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akiongea wakati kilele cha siku 16 za maadhimisho kupinga vita ukatili Wa kijinsia kwa watoto

Kamishina msaidizi wa Polisi ambae pia ni Mwenyekiti Wa mtandao Wa Polisi wanawake mkoa Wa Arusha (TPF-NET) Mary Kipesha akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.


Askari wa jeshi lA Polisi mkoa wa Arusha wakiwa katika maandamano


Mkuu wa. Mkoa Wa Arusha wakiwa ananyakua nyakua na askari Polisi Wa mkoa Wa Arusha Mara baada ya maandamano kuwasili ndani ya hospital ya rufaa ya Mount Meru

Wafanyakazi wa SBL wajumuika pamoja kusherehekea kuaga mwaka 2019

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika viwanda vya Moshi, Dar es Salaam na Mwanza, jana walijumuika pamoja kusherehekea msimu wa sikukuu kwa kuaga mwaka 2019 na kuukaribisa mwaka 2020.

“SBL imeajiri takribani wafanyakazi 800 kupitia ajira za moja kwa moja kwenye viwanda vyake huku ikitengeneza ajira zisizo za moja kwa moja kwa maelfu ya Watanzania, alisema mkurugenzi wa Mahusiano kwa Ummawa kampuni hiyo John Wanyancha kwenye maadhimisho ya sherehe hizo katika kiwanda cha Mwanza.

“Katika maadhimisho ya leo, wafanyakazi wetu wanaburudika kwa kupata chakula na vinywaji pamoja na burudani za kwaya kutoka makanisa yaliyo jirani na viwanda vyetu vitatu. Pia wanapata nafasi ya kusikiliza hotuba za kutia moyo na kujenga kutoka kwa menejimenti ya kampuni.

Malengo yetu yanaendelea kubaki kuwa mwajiri bora. Tutaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kuwa tunaamini ni jambo la msingi katika kuwapa motisha na hivyo kufanya kazi kwa bidi zaidi,” aliongeza Wanyancha

SBL ni mzalishaji wa Serengeti Premium Lager, bia inayotengenezwa na kimea kwa asilimia 100 na pia SBL ni msambazaji wa pombe kali zenye viwango vya kimataifa ambazo ni pamoja na Johnnie Walker, Ciroc, Smirnoff vodka, White Horse, J&B na nyinginezo.

Kwa upande mwingine, Serengeti Premium Lager ni mdhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars huku Serengeti Lite ikiwa mdhamini wa ligi ya soka ya wanawake. Ukiachana na michezo, SBL inafadhili miradi mbali mbali inayolenga kusaidia jamii katika maeneo mbali mbali nchini kwenye maeneo kama upatikanaji wa maji safi na salama, unywaji wa kistarabu pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zenye kipato duni sana.

Kwa mujibu wa Wanyancha, kampuni ya SBL inawasaidia wakulima wazawa wanaolima mazao yanayotumiwa na viwanda vyake kwenye uzalishaji wa bia kama shayiri, mahindi na uwele. Kupitia mpango wa kusaidia wakulima, wakulima wanapata mbegu bora pasipo malipo, ushauri wa kitaalamu wa bure kutoka kwa maofisa ughani na pia huunganishwa na taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo inayposaidia kuongeza uzalishaji wao.

Mwaka 2018, SBL ilinunua tani za ujazo 17,000 za nafaka kutoka kwa wakulima wazawa ambazo ni sawa na asilimia 70 ya jumla ya mahitaji yake kwa mwaka. Nafaka hizi hununuliwa kutoka kwa mtandao wa wakulima 40 walio chini ya mpango wa kampuni hiyo na pia yapo malengo ya kuongeza idadi.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Serengeti wa kiwanda cha Mwanza, wakifurahia kujumuika pamoja katika sherehe za kuaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2020 zilizofanywa na kampuni hiyo jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Bia ya Serengeti, John Wanyancha,akizungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Mwanza kwa utendaji wao.

SERIKALI HAITOPANGA BEI ELEKEZI KWENYE MAZAO–WAZIRI HASUNGA Inbox x

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya wakulima wa korosho Mkoani Lindi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akisisitiza jambo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi tarehe 11 Disemba 2019 wakati alipowasili mkoani humo akiwa katika ziara ya siku mbili kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Lindi

Serikali imesema kuwa haitopanga bei elekezi kwenye mazao mbalimbali ya kilimo kuanzia msimu ujao wa kilimo wa mwaka 2019/2020 badala yake itaacha soko liamue.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 11 Disemba 2019 wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.

Waziri Hasunga amesema kuwa katika kipindi kirefu serikali imekuwa ikijihusisha kupanga bei elekezi ya mazao jambo ambalo huchochea sintofahamu kwa wakulima wakati bei ya mazao katika soko la Dunia inaposhuka.

Amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa inasimamia kwa weledi sekta ya kilimo ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na uhalali katika biashara ya mazao ya wakulima kwa kuangalia mwenendo wa soko la Dunia, uwezo wa wanunuzi na kiasi kitakacholipwa kwa wakulima.

“Tumepanga bei huko kwenye Pamba tumekoswakoswa, Tukapanga kwenye kahawa mambo mabaya, kwenye tumbaku mambo mabaya, tumesema wakulima wenyewe wanapolima ndio wapange bei” Alisema Mhe Hasunga

Katika upande mwingine Waziri Hasunga amesema kuwa serikasli kupitia wizara ya Kilimo inajipanga kuhakikisha kuwa inawasimamia maafisa ugani kwa weledi mkubwa ili waweze kuwasaidia wakulima ili kuwa na uzalishaji wenye tija.

Amesema kuwa wizara imekusudia kuweka utaratibu utakaowawezesha maafisa ugani hao kuwa na fomu maalumu zitakazopima utendaji kazi wao.

Mhe Hasunga amesema kuwa ofisi za maafisa ugani ni mashambani hivyo ni lazima wapimwe ufanisi wao wa kazi kwa kwenda mashambani na jinsi walivyowasaidia wakulima.

Kwa upande mwingine waziri Hasunga amezitaja taasisi za fedha kutofanya vizuri katika kuwasaidia wakulima ili kupata mikopo yenye riba nafuu jambo litakalowanufaisha na kuongeza uwezekano wa kuwa na zana bora za kilimo kadhalika pembejeo bora.

Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amebaini baadhi ya wakulima waliouza korosho zao kwa serikali katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 kutolipwa fedha zao jambo ambalo limemshangaza Kwakuwa serikali ilishatoa fedha zote kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao.

KATIBU MKUU MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisaini kitabu cha Wageni alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Chen Xiaoding (kulia) jijini Beijing, China Desemba 11, 2019. Dkt. Mnyepe yupo nchini humo kushiriki Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa Nchi zinazoendelea.

Dkt. Mnyepe amemuhakikishia Mhe. Chen kuwa, Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na China kupitia Jukwa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (Forum on China-Africa Cooperation - FOCAC). Aidha, kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa, mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanakuwa na tija kwa chi zinazoendelea hususan nchi za Afrika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Chen Xiaoding wakiwa katika picha ya pamoja jijini Beijing, China.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Chen Xiaoding walipokutana kwa mazungumzo jijini Beijing, China Desemba 11, 2019
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images