Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

PINDA, LOWASSA, SUMAYE, MALECELA WATOA YA MOYONI KUHUSU UONGOZI WA RAIS MAGUFULI

$
0
0

Said Mwishehe-Michuzi TV-Mwanza

MAWAZIRI wakuu wa wastaafu kwa nyakat tofauti katika Serikali za Awamu zilizopita wamepata nafasi ya kutoa salamu za sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa nchi yetu ambapo kwa sehemu kubwa wamehimiza umoja, amani na mshikamano kwa Watanzania.

Rais Magufuli wakati akizungumza na wananchi katika sherehe hizo ambazo zimefanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wastaafu kutoa neno lolote katika sherehe hizo.

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinga alikuwa wa kwanza kupata nafasi ya kuzungmza ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Watanzania wote kutokana na kusherehekea miaka hiyo 58 ya Uhuru.Pia alitoa shukrani zake kwa Rais Magufuli.

"Ninamshuru Rais kwa kunipa nafasi, tukuahidi tutaendelea kukuunga mkono kwa kazi ambazo unafanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.Niwaombe Watanzania tushikiriene kulinda amani na utulivu wa Taifa letu kama msingi muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu,” amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa yeye amesema amani ni jambo muhimu katika nchi yetu na kwamba anakumbuka hotuba ya Rais Magufuli ya kuhamsisha Watanzania kutunza amani.

"Mwalimu Nyerere aliwahi kutuambia enzi za uhai wake kuwa akija mtu mtu jeuri na fedhuri na kisha akauliza Watanzania mna nini , mjibuni tuna amani. Hivyo msingi huo wa kwamba tuna amani ndio unaomuwezesha Rais wetu Magufuli kufanya kzi zake, anafanya kazi nzuri sana.

"Kama akiachiwa akapiga miaka yake 10 nchi hii itabadilika, itakuwa nchi kubwa na yenye maendeleo makubwa sana.Nawaomba tumuunge mkono, tumsaidie nchi yetu iende mbele, "amesema Lowassa huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumwabia hongera.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Frederick Sumaye amewapongeza Watanzania na wakati huo huo amempongeza Rais Maguful kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kujenga uchumi wa nchi yetu.

Sumaye amesema kuwa uhuru wa kisiasa ambao leo Watanzania wanasherehekea iwe chachu sasa ya kwenda katika uhuru wa kiuchumi na anaamini kwa kazi inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, nchi itapiga hatua.

"Bado tuna tatizo la utegemezi lakini naamini kwa kazi inayofanywa na Serikali hii ya Awamu ya Tano na zingine zote za nyuma tutakuwa sawa kiuchumi,"amesema.

Waziri Mkuu mstaafu John Malecela amempongeza Rais Magufuli na kwamba kazi ya kuleta maendeleo ambayo anaifanya inaonekana kwa vitendo na watu wakitaka ushahidi waende Dodoma wataona jinsi ilivyobadilika na kwamba Serikali inafanya maendeleo kwa kasi kubwa.

"Kwangu mimi ni Mkoa wa Dodoma, ningependa nieleze watu wa Dodoma tunao ushahidi kwa vitendo kuhusu maendeleo ambayo yanafanywa na Serikali yetu chini ya Serikali ya Awamu ya Tano,"amesema Malecela.
 Waziri Mkuu Mstaafu Mhe,Edward Lowassa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehezilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  

RAIS MAGUFULI ATATANGAZA KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5, 533...ATAJA SABABU ZA KUSAMEHE

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza

RAIS DK. John Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 5, 533 ambao walikuwa wamefungwa hela kwa makosa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuonesha furaha yake ya kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa nchi yetu.

Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambazo ndiko zimefanyika sherehe za Uhuru kitaifa, Rais Magufugli alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa siku za karibuni alipaa nafasi ya kutembelea gereza la Butimba mkoani Mwanza na kushuhudia idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu, hali ambay o kama binadamu ilimuumiza sana.

“Baadhi yenu mtakumbuka miezi michache iliyopita nilitembelea baadhi ya magereza likiwemo gereza ma Butimba, nilishuhudia kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wafungwa na kwa taarifa niliyopewa hali kama hiyo haiko kwenye gereza hilo tu bali ni kwa magereza yote nchini na mpaka leo tuna wafungwa 17,547 na mahabusu 18,256, hivyo kwa pamoja wanakuwa 35,803 hii ni idadi kubwa,"amesema Rais Magufuli.

Amesema kuwa kwa kuwa hata Mungu anasehe ambao wamemkosea, hivyo naye kwa mujibu wa Katiba ya nchi anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafunwa ambao wametiwa hatiani, hivyo leo Desemba 9 anatoa msamaha kwa wafungwa 5533 na kwamba watolewe gerezani kuanzia kesho.

Amefafanua wafungwa ambao amawasemehe ni wale ambao wamefungwa kati ya kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja na wengine ambao wamekutana na msamaha wa Rais ni wafungwa ambao wamefungwa miaka mingi na tayari wameshatumikia sehemu kubwa ya kifungo chao.

"Tunafahamu kuna baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo kama kuiba kuku, kumtukana rafiki yake, kujibizana na mpenzi wake au mshikaji wake na wengine kwa kukosa mawakili wa kuwatetea katika kesi zao lakini wengine kwa kushindwa kulipa fani na kuna wengine wamefungwa kwa kuonewa.

“Kama binadamu hali niliyojionea pale Butimba ilinihuzunisha na kunisikitisha sana ilikuwa hali mbaya, hivyo kwa kutambua kuwa hakuna mwanadamu aliyemkamilifu na wote hapa tumeshatubu na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na kwa kutambua wafungwa wengi wanajutia makosa yao na hawako tayari kuyarudia.

"Ninapenda nitumie nafasi hii kwa mujibu wa madaraka niliyopewa ya kusamehe au kufuta adhamu ya mtu aliyetiwa hatiani na mahakama nimeguswa na nimeamua kusamehe jumla ya wafungwa 5,533,” amesema Rais Magufuli.

Aidha ameagiza wafungwa hao ambao amewapa msamaha waondolewe mara moja kuanzia kesho a hatarajii kusikia au kuona wanafanyiwa mizengwe na kwamba orodha ya wafungwa aliwaowasemehe yote anayo na atakabidhi kwa Kamishan Jenerali wa Magereza.
 
"Idadi hii ya wafungwa ambao nimetoa msamaha ni kubwa sana na huenda watu wakashangaa lakini ninayo madaraka ya kisheria ya kutoa msamaha."amesema Rais Magufuli huku akiutaja Mkoa wa Kagera kuwa ndio wenye idadi kubwa ya wafungwa waliosamehewa ukifuatiwa na Mkoa wa Morogoro,Dodoma na Dar es Salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea moja ya Gereza jijini Mwanza na kushuhudia mlundikano mkubwa wa wafungwa

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AWAHIMIZA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI, MSHIKAMANO

$
0
0
RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano huku akielezea furaha aliyonayo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli wa kuleta maendeleo nchini.

Mzee Mwinyi ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati wa Sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo zimefanyika Uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuria na viongozi wa kada mbalimbali na mamia ya wananchi.

Amesema kuwa umoja wetu ni vema Watanzania wakaendelea amani , mshikamano na usalama na kwamba amani linahitaji watu wengi kuliko wanaohitajika kwenye kufanya maovu.

"Katika kulinda amani tunahitajika kuwa wengi lakini kufanya maovu hakuhitaji watu wengi na hao wanaofanya maovu kama wapo basi waache kwani maovu hayana maana,"amesema Mzee Mwinyi.

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Urusi yafungiwa miaka minne kushiriki michuano mikubwa duniani, ikiwemo Olimpiki ya mwaka 2020 na kombe la dunia mwaka 2022

$
0
0
Urusi imefungiwa kwa miaka minne kushiriki michezo yoyote mikubwa ya kimataifa na wakala wa kupambana na dawa za kusisimua misuli (Wada).

Inamaanisha kuwa bendera ya Urusi haitapepea wala wimbo wao wa taifa wa nchi yao hautapigwa kwenye michuano kama ya Olimpiki ya mwaka 2020 na michuano ya kandanda ya kombe la dunia ya mwaka 2022 nchini Qatar.

Lakini kwa wanamichezo ambao watathibitisha kutotumia dawa hizi wataruhusiwa kushiriki lakini kwa kigezo cha kutoiwakilisha Urusi.

Kamati kuu ya Wada imefanya maamuzi haya katika mkutano wake mjini Lausanne, Switzerland.

Hatua hii inakuja baada ya wakala wa kupambana na dawa za kusisimua misuli nchini Urusi (Rusada) kutajwa kutotii na kuziharibu sampuli za wanamichezo wa Urusi Januari 2019.

Hata hivyo ilitakiwa kusiwasilisha sampuli hizo kwa Wada baada ya tuhuma zilizopelekea kufungiwa kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2018.

Wada inasema Rusada ina siku 21 kukata rufaa. Kama haitofanya hivyo pendekezo hilo litafikishwa katika mahakama kuu ya michezo (Cas).

Makamu Rais wa Wada Linda Helleland amesema zuio hili ''halitoshi''

''Binafsi nilitaka kuwepo vikwazo ambavyo vitakua vikali zaidi,'' alisema.''Tunapaswa kuwasafisha wanamichezo ambao hawahusiki na vikwazo hivi kwa kadri tuwezavyo''
 

Rwanda yazindua kampeni ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi vya Ebola

$
0
0
Rwanda imezindua kampeni yake ya kwanza ya kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola. Zaidi ya watu elfu mbili na mia mbili wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo tangu mwezi Agosti mwaka jana.

Waziri wa afya wa Rwanda, Diane Gashumba, alisema watu laki mbili wanatarajiwa kupata chanjo hiyo katika maeneo yanayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kipaumbele kitapewa wafanyikazi wa afya, maafisa wa uhamiaji, polisi na wale wanaojihusisha na biashara ya mipakani.

Ni kwa nini Rwanda iliamua kutoa chanjo hiyo ilhali haijakabiliwa na ugonjwa wa Ebola?

Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola ilizinduliwa jana katika mji wa Rubavu kaskazini magharibi mwa Rwanda , mji unaopakana na mji wa Goma nchini DRC. kampeni hii itakuwa ikiendelea hata katika mji wa Rusizi kusini magharibi mwa Rwanda,mji unaopakana na mji wa Bukavu pia nchini Congo.

Rwanda haijakabiliwa na ugonjwa wa Ebola,lakini miji yake ya Rubavu na Rusizi inafanya biashara kubwa na nchi ya Congo,na ni miji yenye uingiliano mkubwa wa wananchi kutoka nchini mbili.
 

Wakala wa Vipimo (WMA) wabaini matumizi sahihi ya mizani maeneo mengi jijini Dar es Salaam

$
0
0
Na Grace Gurisha

MENEJA wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Kinondoni, Charles Mavunde amesema maeneo mengi ya Mkoa wa Dar es Salaam wamekuta matumizi ya mizani yapo sahihi ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Mavunde amesema hayo leo, Desemba 9,2019  wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika mabucha ya nyama   yaliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujilidhisha kama vipimo vipo sahihi kwa mujibu wa sheria ya vipimo sura ya 340 , mapitio ya mwaka 2002 na kanuni zake.

Alisema wamepita kwenye mabucha mengi kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na pia kila bucha wamebandika tangazo kuangalia vigezo muhimu ambavyo mtumiaji wa vipimo na mnunuzi anatakiwa kuvifuata.

Mavunde alisema kwa ujumla maeneo mengi waliyopita matumizi yapo sahihi na wafanyabiashara wanafuata sheria na wananchi wamehamasika na wamefahamu kwamba ni vitu gani ambavyo wanazingatia katika manunuzi ya nyama.

"Leo tumefanya ziara ya kushtukiza katika mabucha ya Mwenge  kuangalia kama matumizi ya mizani yanafuata sheria za vipimo, kama tunavyofahamu kila baada ya miezi 12 inatakiwa kuhakikisha,

" Kwa ujumla tumekuta matumizi ya mizani yanafuata sheria za vipimo, tumekuta mabucha mawili yanatumia mizani miwili miwili ila mmoja ndiyo haujahakikiwa, watu hawa wamejaziwa fomu nakuchukuliwa hatua kadri sheria ya vipimo inavyoeleza,"alisema Mavunde

Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mkoa wa Ilala, Saad Haruna alisema kama muuzaji wa atakuwa amesababisha kwa makusudi yeye mwenyewe kuutengua mzani ili usiweze kufanya kazi vizuri,atakuchukuliwa hatua za kisheria.
"Hatua za kisheria kwa wakala wa vipimo zipo za aina mbili faini au kwenda mahakamani na gauni inaanzia Sh.100,000 hadi Sh. Milioni 20. Kwa hawa watu wa mabucha adhabu yao inaanzia sh 100,000 hadi Sh 500,000," alisema.
Afisa Vipimo namba Moja kutoka Wakala wa Vipimo nchini, Bw.Mohammed akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi ya kifaa cha kupimia vipimo vya kuuzia nyama, mara baada ya Kufanya ukaguzi wa Kustukiza katika mabucha ya Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 09, 2019.



Mawakala wa Vipimo Tanzania wakiwa katika Bucha za Nyama maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua mizani kama ina viwango ambavyo vinatakiwa.

JOWUTA NI CHOMBO SAHIHI KWA WAFANYAKAZI WA VYOMBO VYA HABARI-MSUYA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Elias Msuya akizungumza na waandishi wa haari wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea waandishi wa habari kuandika habari za jinsia na usawa jijini Dar es Salaam leo.
 Mkufunzi, Simbarashe Msasanuri, akitoa mada katika Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za jinsia na Usawa jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) jijini Dar es Salaam leo.

CHAMA cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) ndio chombo Sahihi kwa waandishi wa habari hasa wanawake ambacho kipo kwaajili ya kutetea haki zote mahala pakazi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari (JOWUTA), Elias Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari hasa wanawake wa jijini Dar es Salaam kuandika habari za jinsia na usawa amesema kuwa waandishi wa habari wote wakiungana wanakuwa na sauti ya pamoja katika kutatua changamoto inapomkkabiri mwandishi wa habari ambaye atakuwa amejiunga na chama cha JOWUTA.

Msuya amesema kuwa Chama cha JOWUTA kimesajiliwa kwaajili ya kuwaunganisha waandishi wa habari na kuwa na lengo moja katika kuhabarisha umma.

"Waandishi wengi wakiwa katika vyombo vya habari hufanyiwa unyanyasaji, hawana mahala pa kusemea sasa  JOWUTA ndio chombo sahihi kwaajili ya kutatua changamoto zinazowakumba waandishi wa habari wakiwa kwenye vyombo vyao".

Msuya amewaasa waandishi na wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika vyombo vya habari wajiunge na chama hicho kwani gharama za kujiunga ni ndogo ili kuwe na uwezekano wa kutetewa na chama litokeapo tatizo.

 Kwa Upande wake Mwezeshaji wa masuala ya kijinsia, Simbarashe Msasanuri amesema kuwa ili kutatua changamoto za waandishi wa habari ni lazima waandishi wenyewe wavunje ukimya na kuandika vitendo vya unyanyasaji wowote unaotokea katika vyombo vyao.

Hata hivyo amesema kuwa pia mfumo dume katika vyombo vya habari lazima uondoke kwa waandishi wa habari wanawake kujituma na kuwania nafasi za uongozi zilizopo katika vyomo vya habari wanavyoviandikia.

Msasanuri amefafanua kuwa waandishi wa habarinwaachane na hali ya kuridhika pale walipo na waongeze juhudi ya kuweza kuendelea mbele.

"Muungane waandishi wa habari wanawake  katika chama cha JOWUTA ili muwenze kuwa kitu kimoja na changamoto zitatatuliwa ".

Hata hivyo JOWUTA ni chama amacho kimesajiliwa mwaka jana na mpaka sasa kinawanachama 130, chama hicho ni chama cha wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika vyombo vya habari na sio waandishi tuu.

TWENDEZETU MAKETE SAFARI IMENOGA

$
0
0
CHAMA CHA MAENDELEO MAKETE (MDA)
KAMATI YA MICHEZO NA UTAMADUNI
MAKETE TOUR DECEMBER 2019

MDA-MAKETE TOUR DEC. 2019
Hatimaye ile safari kubwa ya kurudi nyumbani (Makete) Msimu wa sikukuu (December) 2019 imewadia.
Unakaribishwa sana kuungana na Wanamakete wenzako kurudi nyumbani na kwenda kufanya Utalii,Matembezi na kusanyiko la pamoja.


1. TAREHE YA SAFARI
Safari itaanzia Dsm kwenda Makete kwa Usafiri wa Basi Tar 22/12/2019 na tutakuwa Makete hadi tar 27/12/2019 baada ya hapo utaruhusiwa kuondoka au kubaki na kuendelea na majukumu yako binafsi.

2. MATUKIO
 -Tar 22/12/2019 itakuwa siku ya Safari, wakati wa safari tutawachukua wote njiani( Barabara ya Dsm kwenda Njombe) ambao watakuwa wamejiorodhesha kusafiri na wamelipia
- Tar 23/12/2019 tutakuwa na ziara ya kutembelea (Hospital ya Bulongwa, Hospital ya Makete (W), Hospital ya Ikonda.Tunaweza fika Madihani na Utengule pia.
-Tar 24/12/2019 tunatembelea Matamba na Kitulo.
-Tar 25/12/2019 watu wataruhusiwa kwenda kushiri Christmass na ndugu zao.
-Tar 26/12/2019 tutakuwa na Kusanyiko la pamoja.

-Tar 27/12/2019 tutaruhusu watu kuanza kurejea Mikoani.

3. USAFIRI
-Tutatumia basi (Upoma Basi yatakuwepo) kutoa Dsm hadi Makete kwa wale watakaolipia.Tumeshazungumza naye.

-Watu wa Mbeya Tumeshapata COSTA safii za Kuwabeba kwa watakao lipia.

-Mizunguko ya Ndani tutatumia Usafiri wa palepale Wilayani (Costa).

4. NAULI
-Kutoka Dsm hadi Makete Tsh. 45,000 hivyo kwenda na kurudi ni Tsh. 90,000

-Mizunguko ya ndani utachangia nauli kiasi Tsh. 20,000

5. MALAZI
-Kwa ambao wanandugu karibu na Makete Mjini mtaruhusiwa kulala Makwenu.
-Kwa wale ambao ndugu wapo mbali sana watahigaji pa kulala (Hotel zipo tutafanya booking na utajilipia kama ni Single au Double ).

6. CHAKULA
-MDA itakuhudumia siku ya Kusanyiko tu.
-Siku zingine zote kila mtu atajitegemea chakula.

7. KUSANYIKO TAR 26/12/2019
-Kusanyiko tutafanyia Madihani Villa (Tayari tumeshapewa Ukumbi).
-Kusanyiko litahusisha viongozi wa MDA na Wilaya na wageni mbalimbali waalikwa wakiungana na wote waliosafiri.
-Tutakuwa na Chakula cha Pamoja
-Tutakuwa na Burudani, Nyimbo za asili.
-Tutakuwa na elimu kuhusu, mila, chakula na tamaduni za Wanamakete.
-Tutakuwa na Kufahamiana 
-Mwisho neno kutoka Viongozi wa MDA na Wilaya kuhusu maendeleo ya wilaya yetu.

8. WAHUSIKA WA MAKETE TOUR
-Mwanamakete yeyote yule aliyeko tayari awe Mwanachama wa MDA au sio Mwanachama wa MDA utaruhusiwa kusafiri.

9. MWISHO
Kwa kujiorodhesha kusafiri,kulipia, tunaomba uwasiliane na namba hizi
+255746-234567 WhatsApp
+255756-998888 Calls

ASANTE
Kwa niaba ya Kamati ya Michezo na Utamaduni
FESTO RICHARD TUNTEMEKE SANGA
Mwenyekiti

BRELA YATOA ELIMU YA USAJIRI NA URASIMISHAJI WA BIASHARA KWA UMMA

$
0
0
Maonyesho ya Nne ya bidhaa za viwandani yamefikia tamati leo tarehe 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Mwl. J.K Nyerere (Sabasaba). Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka amesema Maonyesho hayo yamekuwa chachu ya maendeleo katika kufikia uchumi wa kati wa maendeleo ya Viwanda huku akiwataka wadau wote wa Viwanda na Biashara Kupanua wigo wa Biashara kwa Maendeleo ya Nchi yetu.

Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka (Kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Tantrade Bwana Edwin Rutageruka.
Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka amekabidhi cheti cha ushiriki kwa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kupokelewa na Bi Robertha Makinda, Afisa Habari na Mawasiliano BRELA.
Wafanyakazi wa BRELA wakiwa kwenye banda la Maonyesho ya Bidhaa za Viwanda katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere ( Sabasaba) kutoka kulia ni Hilary Mwenda Afisa Tehama, Robertha Makinda Afisa Habari na Mawasiliano,Yusuph Nakapala Afisa Leseni, Ruth Mmbaga Afisa Mwandamizi Msaidizi wa Usajili na Hellen Mhina Msaidizi wa Usajili Mkuu.
Wateja mbalimbali waliotembelea banda la BRELA na kupatiwa Elimu ya kurasimisha biashara zao.

Wakala wa Vipimo Waadhimisha Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, kwa Kufanya Ukaguzi wa Kustukiza

$
0
0
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke, Bw.Krishna Mahamba,
akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kutumia mizani iliyosawa kwa wauzaji wa mabucha , mara baada ya Kufanyaukaguzi wa Kustukiza katika mabuchani yaliyoko Mwenge Jijini Dar es Salaammapema leo Desemba 09, 2019.
Mmoja ya Wauzaji wa mabucha yaliyoko Mwenge Jijini Dar es Salaam, Petro
Makole, akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu
umuhimu wa kutumia mizani iliyosawa kwa wauzaji wa mabucha , mara baada ya Kufanyiwa ukaguzi wa Kustukiza buchani kwake Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 09, 2019. Afisa Vipimo namba Moja kutoka Wakala wa Vipimo nchini, Bw.Mohammed
akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi yakifaa cha kupimia vipimo vya kuuzia nyama, mara baada ya Kufanya ukaguzi waKustukiza katika mabucha ya Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba09, 2019.



*************************************

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Wakala wa Vipomo Nchini (WMA) imesema kuwa itaendelea kulinda maslahi yawatumiaji na afanyabiashara kupata stahiki sahihi katika manunuzi na uuzaji wabidhaa zao kwa kutumia vipimo vinavyoendana na thamani ya pesa inayolipwa na mteja.

Akizunngumza Jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kustukiza kwa Wafanyabiashara wa Mabucha, Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke, Krishna Mahamba amesema kuwa dhumuni la ziara hiyo ni kuangalia kama vipimo vinazingatiwa na wauzaji ili kuleta usawa kwa wateja na wauzaji hao.

“Katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, Wakala wa Vipimo leotumeamu kufanya zoezi hili ambalo linafanyika Nchi nzima ili kulinda haki zabiashara kwa wateja na wauzaji kwenye mabucha haya, kwani mara nyingi katika siku za sikukuu kama hizi wauzaji huwa wanachezea vipimo”, Krishna Mahamba Kaimu Meneje (WMA) Mkoa wa Temeke.

Alieleza kuwa wafanyabiashara wa mabucha wanapaswa kutumia mizani
iliyopimwa ili kumuwezesha mpata huduma katika mabucha yao kupata bidhaa kulingana na thamani ya pesa yake na kuweza kuleta usawa pande zote mbiliyaani mteja na muuzaji.

Naye Kaimu Meneje Wakala wa Vipimo Mkoa wa Kinondoni, Charles Mavundealisema kuwa leo wakala wa vipimo imefanya zoezi hilo ili kuangalia kamawafanyabiashara wa Mabucha wanazingatia Sheria ya Vipimo nchini Sura namba340 ambayo inamtaka mfanyabiashara kutumia vipimo sahihi kulingana na bei ya bidhaa yake aliyoipanga kwa wanunuzi.

Mavunde alito wito kwa watanzania kuwa wanapokuwa wanaadhimisha sikukuukama ilivyokuwa leo miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika wawe makini nawafanyabiashara katika sehemu zote za biashara kuanzia kwenye mabucha, sokoni na kwenye vituo vya mafuta kwa kuwa siku hizo wafanyabiashara huchezea vipimo na kutoa bidhaa kwa kuwapunja wateja wao.

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano kutoka (WMA), Irene John alisema kuwawakala wa vipimo hawajalala katika siku za sikukuu, wataendelea kufanya ziara za kustukiza kwenye sehemu mbalimbali za biashara ikiwemo kwenye mabucha,sokoni na Vituo vya mafuta ili kuleta usawa kati ya Muuzaji na Mteja kupata stahiki zao kulingana na thamani ya pesa inayolipwa.

“Katika Maadhimisho haya ya Miaka 58 Uhuru Tanganyika hatujalala tumefanyazoezi la ukaguzi wa kustukiza kwenye mabucha hapa Mwenge Jijini Dar es Salaam na zoezi hili linafanyioka nchi nzima, na lengo kuu ni kulinda stahiki za wateja na wauzaji ili kila mtu akitoa pesa ya lita moja apate lita moja, akitoa pesa ya kilo moja vilevile apate kilo moja”, Irene John Meneja Mwasiliano (WMA).

RAIS MAGUFULI ATANGAZA KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5, 533...ATAJA SABABU ZA KUSAMEHE

$
0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza

RAIS DK. John Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 5, 533 ambao walikuwa wamefungwa hela kwa makosa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuonesha furaha yake ya kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa nchi yetu.

Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambazo ndiko zimefanyika sherehe za Uhuru kitaifa, Rais Magufugli alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa siku za karibuni alipaa nafasi ya kutembelea gereza la Butimba mkoani Mwanza na kushuhudia idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu, hali ambay o kama binadamu ilimuumiza sana.

“Baadhi yenu mtakumbuka miezi michache iliyopita nilitembelea baadhi ya magereza likiwemo gereza ma Butimba, nilishuhudia kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wafungwa na kwa taarifa niliyopewa hali kama hiyo haiko kwenye gereza hilo tu bali ni kwa magereza yote nchini na mpaka leo tuna wafungwa 17,547 na mahabusu 18,256, hivyo kwa pamoja wanakuwa 35,803 hii ni idadi kubwa,"amesema Rais Magufuli.

Amesema kuwa kwa kuwa hata Mungu anasehe ambao wamemkosea, hivyo naye kwa mujibu wa Katiba ya nchi anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafunwa ambao wametiwa hatiani, hivyo leo Desemba 9 anatoa msamaha kwa wafungwa 5533 na kwamba watolewe gerezani kuanzia kesho.

Amefafanua wafungwa ambao amawasemehe ni wale ambao wamefungwa kati ya kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja na wengine ambao wamekutana na msamaha wa Rais ni wafungwa ambao wamefungwa miaka mingi na tayari wameshatumikia sehemu kubwa ya kifungo chao.

"Tunafahamu kuna baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo kama kuiba kuku, kumtukana rafiki yake, kujibizana na mpenzi wake au mshikaji wake na wengine kwa kukosa mawakili wa kuwatetea katika kesi zao lakini wengine kwa kushindwa kulipa fani na kuna wengine wamefungwa kwa kuonewa.

“Kama binadamu hali niliyojionea pale Butimba ilinihuzunisha na kunisikitisha sana ilikuwa hali mbaya, hivyo kwa kutambua kuwa hakuna mwanadamu aliyemkamilifu na wote hapa tumeshatubu na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na kwa kutambua wafungwa wengi wanajutia makosa yao na hawako tayari kuyarudia.

"Ninapenda nitumie nafasi hii kwa mujibu wa madaraka niliyopewa ya kusamehe au kufuta adhamu ya mtu aliyetiwa hatiani na mahakama nimeguswa na nimeamua kusamehe jumla ya wafungwa 5,533,” amesema Rais Magufuli.

Aidha ameagiza wafungwa hao ambao amewapa msamaha waondolewe mara moja kuanzia kesho a hatarajii kusikia au kuona wanafanyiwa mizengwe na kwamba orodha ya wafungwa aliwaowasemehe yote anayo na atakabidhi kwa Kamishan Jenerali wa Magereza.
"Idadi hii ya wafungwa ambao nimetoa msamaha ni kubwa sana na huenda watu wakashangaa lakini ninayo madaraka ya kisheria ya kutoa msamaha."amesema Rais Magufuli huku akiutaja Mkoa wa Kagera kuwa ndio wenye idadi kubwa ya wafungwa waliosamehewa ukifuatiwa na Mkoa wa Morogoro,Dodoma na Dar es Salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea moja ya Gereza jijini Mwanza na kushuhudia mlundikano mkubwa wa wafungwa

TEKNOLOJIA YA LAMI YA KITANZANIA BADO HAIJAPANGIWA MATUMIZI

$
0
0
Moja ya barabara ambayo bado haijazibwa viraka.
Mchoro kwaajili ya maandalizi ya kuziba sehemu ya barabara iliyoharibika
Muonekano wa barabara iliyozibwa kwa kutumia lami ya baridi  baada ya kuzibwa viraka maeneo yaliyoharibika.

Na Irene Mwidima, Globu ya jamii
TANGU kuzinduliwa kwa teknolojia mpya ya uzalishaji wa lami hapa nchini Oktoba, 2014 bado kumekuwa na changamoto ya kutokupangiwa matumizi ya kujenga barabara na Serikali.

Hayo yamesemwa na Meneja masoko wa kampuni ya Starpeco LimitedJones Mkoka wakati akizungumza na michuzi blog leo katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Makoka amesema teknolojia hiyo ni rahisi kwani huchnganywa na maji ya baridi na kufanya kazi kama lami inayochemshwa

"Ujenzi wa barabara zote upo chini ya TANROAD na TARURA,  na wao ndio hutoa tenda za ukandarasi wa barabara, huwa wanatoa aina na viwango vinavyotakiwa na mradi husika,  lami yetu bado haijaanza kuruhusiwa kwenye ujenzi wa barabara". Amesema Mkoka

Licha Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kushirikiana na chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii bado wabunifu wa lami hiyo hawajapata tenda ya kutengeneza hata barabara moja.

Licha ya kuwa na chngamoto hiyo kampuni ya kampuni ya Starpeco Limited imeweza kuuweka viraka katika barabara ya Changanyikeni na barabara ya uvumbuzi zilizopo chuo kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na kumwaga lami mpya katika baraara ya Kileleni yenye urefu wa Kilomita 120.

Aidha amesema kuwa baada ya kuona changamoto hiyo wakona wajitokeze mbele waweze kueleza jinsi inavyoweza kutumika kwa urahisi lami hiyo ya baridi kutengenezea barabara.

"kwahiyo baada ya kuona changamoto hiyo tukaona ni bora tujitokeze mbele tuweze kueleza jinsi inavyoweza kutumika,  na tunashukuru wazo letu liliweza kupokelewa na kazi tumeanza,  tumeweza kuirekebisha barabara ya Kileleni, lakini pia tuliweza kuziba viraka vya barabara ya Uvumbuzi kutoka kutoka maeneo ya Utawala mpaka chuo cha COET".

Kiwanda cha lami baridi inayochanganywa na maji kipo Kipawa jijini Dar es salaam na kilianzishwa mwaka 2014,  na faida kubwa ya hii lami inaruhu ujenzi wa barabara bila kuchemaha lami,  kama ijulikanavyo lami zingine za kawaida ni lazima zichemshwe kwa ajili ya kuchanganywa na kokoto.

Benki ya NMB yatwaa Tuzo ya NBAA kwa mwaka mwingine mfululizo.

$
0
0
BENKI ya NMB imetwaa tuzo maalum kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) kama Benki bora ya Taarifa za Kifedha zilizokaguliwa na kutambuliwa kimataifa kwa mwaka 2018,ilikoshinda benki kadhaa nchini.

Benki hiyo imetambuliwa kwa kufikia kiwango bora katika utayarishaji wa taarifa zake za kifedha, kulingana na mahitaji ya taarifa (viwango vya kuripoti za kitaifa na kimataifa).

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo kwa NMB, ni ushindi wa mara ya pili mfululizo, ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo NBAA ilisema taarifa za mahesabu za NMB zimeendelea kuwa bora kila mwaka, ubora uliowasukuma majaji kuwapa tuzo hiyo kwa mara nyingine.

Akizungumzia vigezo vilivyotumika kupata washindi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mr.Pius Maneno, amesema walipatikana kwa kuangalia washiriki waliovuka asilimia 75 ya vigezo vilivyowekwa.

Naye Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Mr. Benedicto Baragomwa, amesema wao kama wataalam wa masuala ya fedha, wanatambua umuhimu wa kuandaa vitabu vya mahesabu vya Benki kwa njia na mifumo inayozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

“Ushindi huu unadhihirisha namna ambavyo tumejikita katika kudumisha uadilifu wa hali ya juu kwenye uwasilishaji wa taarifa zetu za kifedha za mwaka,” alisema Baragomwa baada ya kupokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani.

Baragomwa alibainisha kuwa, wawezeshaji wa benki hiyo wameandaliwa katika misingi inayofuata na kuheshimu viwango vya kimataifa vinavyotambuliwa na IFRS, pamoja na mahitaji ya ndani.

Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imetoa shukrani kwa wafanyakazi na kujivunia mfumo bora wa Uongozi na utendaji hasa kitengo cha fedha. "Tuzo hii imepatikana nyuma ya mfumo uliopo wa utawala bora na michakato ya udhibiti ambayo inakuza uwazi wa taarifa za kifedha, uwajibikaji,ueledi na kiwango cha juu cha uadilifu wa takwimu. Hongera kwa kila mtu, haswa timu ya kifedha kwa kuongoza maandalizi ya Taarifa ya Fedha ya Benki ya NMB.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani, akimkabidhi Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, Tuzo ya Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2019, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA). Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, akionesha Tuzo aliyoipokea ya Benki ya NMB kuwa Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2018, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa utoaji tuzo.

LIVE | SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ALI MUFURUKI UKUMBI WA JNICC

IBADA YA SHUKURANI YA MAMA JONEL MATURE MAWALA, RIVERDALE, MARYLAND

$
0
0

Wnafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja katika ibada ya shukurani ya mama Jonel Mature Mawala iliyofanyika siku ya Jumampili Dec 8, 2019, Riverdale, Maryland
 Mussa Shedasfa mmoja wa marafiki wa Dennis Makundi (mtoto wa marehemu) hayupo pichani akiongea machahe.
Leaha Nyaki akiongea kwenye ibada hiyo ya shukurani.
Bishop Maturlu (koti jeusi) akijumuika katika chakula cha pamoja na familia.
 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakifuatillia ibada hiyo.
Ndugu, jamaa na marafikia wakijumuika katika chakula cha pamoja.
 Ndugu, jamaa na marafiki wakijumuika katika chakula cha pamoja.
 Chakula kikiendelea.
Wanafamilia wakiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wakati wa chakula cha pamoja.

MAHAFALI YA 30 YA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

$
0
0



Bi. Pili Said Kassimu ambaye ni mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Stashahada akipokea cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa akitoa hotuba wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambapo aliwataka wahitimu wakawe raia wema na kuitumia elimu waliyoipata ipasavyo kwa ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. George D. Yambesi akitoa neno kwa wahitimu pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kutoa hotuba yake.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa (katikati) akiwa katika Meza Kuu na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bagamoyo pamoja na viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni bagamoyo (TaSUBa). 

Wahitimu wakisikiliza hotuba kwa umakini kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye alikua ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa (hayupo pichani).

Mhitimu wa ngazi ya Stashahada Bw. David Nashoni akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake mbele ya mgeni rasmi ambaye alikua ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa.

 

Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikitoa burudani wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi hiyo.

IPACE YAWAPIGA MSASA WENYEVITI NA MABALOZI WAPYA WA SERIKALI ZA MITAA JUU YA UKATILI

$
0
0

FREDY MGUNDA, IRINGA.
Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuheshimu haki zote za mtoto ili kuepukana na ukatilii unaendelea kwa watoto kwa kuwalea katika malezi mazuri yenye faida katika maisha ya baadae.

Hayo yamezungumzwa na afisa wa dawati la jinsia na watoto Elizabert Swai wakati wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi na wanahabari kwa uratibu wa shirika lisilo kuwa la kiserikali linalo jihusisha na masuala ya usaidizi wa kisheria katika manispaa ya Iringa (IPACE).

Swai alisema kuwa wenye viti, wapya waliopishwa hivi karibuni wametakiwa kuzifikisha tuhuma zozote za ukatili wa kijinsia katika dawati la jinsia la jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Alisema kwamba matukio ya ukatili wa jinsia yamekuwa yakiongezeka na watu wa Kwanza kukutana nayo ni wenyeviti wa mtaa hivyo ni muhimu kufikisha hatua za mbele,watoto wengi wamekuwa wakibakwa au kunyanyaswa kijinsia.

Aidha Swai ametoa wito kwa watu wanaokumbana na matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji kujitokeza katika kituo cha polisi ndani ya masaa 72 ili kuweza kufanya upelelezi na kutibiwa kama umeambukizwa magonjwa ya zinaha au ukimwi.

Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa shirika lisilo kuwa la kiserikali linalo jihusisha na masuala ya usaidizi wa kisheria katika manispaa ya Iringa (IPACE) Isaac Kikoti alisema kuwa katika siku 16 wamefanikiwa kutoa msaada wa kisheria kwa wahanga mbalimbali katika jamii ya watu waishio katika manispaa ya Iringa ,na walio nje ya manispaa na wametatua migogoro ya ardhi,ndoa ,mirathi ,matunzo ya watoto na ukatili wa kijinsia

“Ndoa na ardhi kesi hizi zimekuwa nyingi katika jamii zimechukua nafasi kubwa katika jamii ya wananchi wa manispaa ya Iringa na tumefanikiwa kuwasaidia kwa kuwaandikisha wateja wetu katika vitu vya ushauri kama Mahakamani,Polisi,Ustawi wa jamii na Dawati la jinsia manispaa ya Iringa” alisema Kikoti.

Alisema kuwa wamefanya utafiti kwa wanao tendewa vitendo vya ukatili kwa kuangalia maendeleo yao baada ya mashauri yao kutatuliwa na kugundua wana endelea vizuri na wamegundua kuwa elimu iliyotolewa kwa wananchi wanatoa ushirikiano kwa kutoa taarifa.

“vitendo vya ukatili vime pungua katika jamii kwa asilimia kubwa baada ya watu kupata ushauri kutoka kwa PARALEGAL na jamii imenufaika baada ya elimu wameweza kujua haki zao za msingi na kuondokana na mila na desturi potofu lakini wanakuwa wazi kupeleka mashauri katika vyombo vya sheria”alisema Kikoti

Lakini pia Kikoti alizitaja changamoto ambazo wamekuwa wanakabiliana nazo ni kutokuwa na usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ili kuifikia jamii kwa ufasaha ,Jamii kutotoa ushirikiano pale ambapo vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinatokea,Mabadiliko ya sheria mpya ya msaada wa kisheria,pindi ambapo kila msaidizi wa kisheria anapaswa kulipa ada Tsh 30,000 kwa mwaka na Taasisi kuto kuwa na mradi wa kujiwezesha.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye semina hiyo mwenyekiti wa kuwasimamia watetezi wa kisheria Tanzania Bara Eliah Kasanga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeanzisha baraza watetezi wa kisheria kwa lengo la kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kiuchumi ili nao waweze kupata haki zao.

“Ukifika mahakamani mtafute anayesimamia utetezi wa kisheria utapata msaada wa kisheria,maana ya mheshimiwa Rais ni kwamba mtu asifungwe kwa sababu hana uwezo ila ufungwe kwa sababu unakosa nah ii sheria ipowazi inapswa kusambazwa kwa wenyeviti wote mkoani hapa ili kwasaidia wananchi kupata haki zao” alisema Kasanga

Na afisa utamaduni wa manispaa ya Iringa Merysina Ngowi alisema kuwa watoto wanaofanyiwa ukatilii wamekuwa wanaathirika kisaikolojia kutokana na matendo yanakuwa yamewakumba.

Alisema kuwa watoto wakifanyiwa ukatili wanapata madhara makubwa katika maisha yao hivyo wananchi wanatakiwa kuheshimu haki za watoto.

Mwenyekiti wa shirika lisilo kuwa la kiserikali linalo jihusisha na masuala ya usaidizi wa kisheria katika manispaa ya Iringa (IPACE) Isaac Kikoti akiongea wakati wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi na wanahabari kuhusiana na ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya washiriki wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi,wadau mbalimbali na baadhi ya wanahabari.

SANNA MARIN AWA WAZIRI MKUU KIJANA ZAIDI DUNIANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa Usafirishaji wa nchi ya Finland, Sanna Marin ameapishwa leo na kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 34 tu. Hii inamfanya kuwa Waziri mkuu kijana zaidi kwa sasa ulimwenguni. Jumapili wiki iliyopita alishinda kura za wabunge wa chama cha Social Democrat baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Antti Rinne kujiuzulu Jumanne wiki iliyopita baada ya tuhuma kwamba alishindwa kudhibiti mgomo ulioanzishwa na wafanyakazi wa Posta na Muungano wa chama cha Kati (Centre Party) kudai hauna imani naye tena.

Waziri Mkuu mchaguliwa, Sanna Marin ameeleza kuwa na kazi kubwa ya kujenga imani. Alipohojiwa na shirika la habari la Reuters alisema;

 “Sikupata kufikiria katika umri huu au jinsia yangu, ninafikiria tu juu ya sababu zilizonipelekea kuwa kwenye siasa na mambo yaliyowajengea imani wapiga kura kwangu” ameeleza.

Marin alianza kupanda katika uongozi mara baada ya kuongoza Mamlaka ya Mji wa Viwanda wa Tampere, akiwa na umri  wa miaka 27 tu.

Chama cha Social Democrats ni kikubwa zaidi kwenye muungano unaoongoza serikali ya Finland. Marin alipata umaarufu mkubwa baada ya kumshinda kiongozi mkuu wa Muungano huo Bungeni Antti Lindtman.

Marin sio kiongozi pekee mkubwa ulimwenguni mwenye umri kati ya miaka 30, wengine ni Kiongozi wa Ukraine, Oleksiy Honcharuk( Miaka 35) na Waziri Mkuu wa Nchi ya New Zealand, Jacinda Ardern mwenye miaka 39.

Vyama vikuu katika Bunge la Finland vinaongozwa na wanawake, wanne kati yao ni kati ya miaka 30. Li Andersson (32) anaongoza Left Alliance; Maria Ohisalo (34) anayekiongoza chama cha Umoja wa Kijani,  Chama cha Kati (Centre Party) kinaongozwa na  Katri Kulmuni(32); na Bi. Anna-Maja Henriksson ambaye ana miaka  55, akiongoza Chama cha  Swedish People's Party of Finland.

WAFUNGWA 79 WA GEREZA KUU BUTIMBA WALIONUFAIKA NA MSAMAHA WA RAIS WAACHILIWA LEO JIJINI MWANZA

$
0
0
 Baadhi ya wafungwa wakiume wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na Msamaha wa Rais wakitoka katika lango la Gereza Kuu Butimba tayari kwenda kuungana na familia zao. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo wa kihistoria.
 Wafungwa wa kike Gereza Kuu Butimba – Sehemu ya Wanawake wakitoka gerezani baada ya Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo na wameahidi kutokurejea katika uhalifu.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike akitoa taarifa fupi ya zoezi zima la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais katika mikoa mbalimbali nchini mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari jijini Mwanza leo Desemba 10, 2019.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo akizungumza na Wafungwa wa Gereza Kuu Butimba kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais leo Desemba 10, 2019. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike.
 Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mwanza pamoja na Kamishna  Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike wakishuhudia wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais katika Gereza Kuu Butimba wakipewa mali zao na nauli ya kwenda kuungana na familia zao leo Desemba 10, 2019 kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa husika wa msamaha huo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(vazi la kitenge) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa mwanza alipowasili gereza Butimba kushuhudia zoezi la uachiliaji wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais.
Mfungwa mnufaika wa Msamaha wa Rais, William Dingu akizungumza na Wanahabari(hawapo pichani) baada ya kuachiliwa huru leo. Mfungwa huyo amemshukru Rais kwa msamha huo, aidha,  amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kumwezesha ujuzi wa wa fani ya ujenzi ambao ameupatia gerezani kupitia programu ya Urekebishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Mgalu : REAIII ni “BABA LAO” TANESCO na REA, msiache Kijiji hatutarudi nyuma

$
0
0
Na Zuena Msuya ,Pwani
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) kuhakikisha hawaruki kijiji katika REA Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaoanza mapema mwezi Januari 2020 kwa kuwa awamu hii ni ya mwisho kuunganisha Vijiji.
Mgalu alisema hayo, Desemba 8, 2019 wakati akiwasha umeme katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mgalu alifafanua kuwa katika utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili ni wa mwisho katika kusambaza umeme vijijini, miradi itakayofuata ni kusambaza umeme katika Vitongoji, hivyo REA na TANESCO wahakikishe wanashirikisha Serikali za Mitaa ili kuorodhesha vijiji vyote kwa umakini na usahihi ili viweze kupatiwa umeme ifikapo  Mwezi, June 2021.
Alieleza kuwa huenda Tanzania inaongoza  kwa kuwa ya nchi ya kwanza kwa  nchi za Afrika Mashariki katika kusambaza umeme vijijini, ambapo  mpaka sasa ina vijiji 8115, vilivyounganishwa na umeme kati ya vijiji  12,000,  vijiji 4000 vilivyosalia  kazi ya kusambaza umeme na kuwaungaishia wateja inaendelea ili kufikia  Mwezi Juni 2020 vijiji 10336 viwe  vimeunganishiwa umeme na kubakiwa na  vijiji  1,200 ambavyo hivi vitaendelea kuunganishiwa  umeme  hadi kufia mwezi June 2021, vijiji vyote nchini vitakuwa vimeunganishwa na umeme.
“TANESCO na REA, hakikisheni hamuachi kijiji, hii ni awamu ya mwisho kwa mradi wa REA mzunguko wa tatu, “Hii ndiyo Baba lao”, hatutarudi nyuma tena kuunganisha vijijini, miradi itakayokuja sasa itakuwa ni maalum kwa ajili ya vitongoji, hivyo basi mshirikishe serikali za mitaa kuhakikisha hakuna kinachoachwa nyuma na bei ya kuunganishiwa umeme ni shilingi 27,000, na ni marufuku kuwauzia wateja Nguzo wala LUKU”  alisisitiza Mgalu.
Aidha aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi ya REA, kwa kukubali na kuridhia maombi ya nyongeza ya Kaya  5000, ambazo zilizomba kuunganishiwa umeme na zoezi hilo likafanyika kwa Mkoa wa pwani,hivyo alitaka utaratibu huo uendelee kwa maeneo mengine nchini  kwa kuwa miradi hiyo imetumia gharama kubwa katika kuitekeleza na lengo ni kuwafikia wananchi wote.
Sambasamba na hilo aliitaka TANESCO kuangalia namna bora nzuri ya kuwawezesha wateja kulipia gharama za kuunganisha umeme katika majumba yao, ikiwezekana kuwakopesha na baadaye walipie kupitia LUKU au Ankara zao au kuwawekea utaratibu wa kulipia kidogo kidogo ili kila mmoja aweze kuunganishwa na umeme.
Aliwaeleza kuwa TANESCO wasikatae fedha pale mteja anapotaka kulipa kwa awamu, isipokuwa waweke utaratibu mzuri wa walipo hayo kwa lengo la kumsadia mteja yule ambaye hawezi kuzilipa zote kwa mara moja ili aunganishiwe umeme.
Alirudia kusema utaratibu wa bei ya shilingi elfu 27,000 uliotolewa na Rais kwa miradi ya TANESCO inalenga wateja walio vijijini ambapo kuna miradi ya REA,lakini agizo hilo haliwahusu wateja waliopo kwenye Manispaa na Majiji katika miradi ya TANESCO inayoendela kutekelezwa  kwa sababu TANESCO inatakiwa ijiendesha kutokana na mapato yake.
Hata hivyo alisema kuwa  kwa sasa serikali inapokea maoni yanayotaka gharama ya shilingi 27,000 iwe nchi nzima, maoni hayo yatafanyiwa utafiti kwa kina na kuona namna bora ya kupunguza bei ya kuwaunganishia umeme wateja  waliopo katika  Manispaa na Miji ili kila mmoja aweze kupata huduma hiyo kwa gharama anayoweza kuimudu.
 Katika hatua nyingine, Mgalu alitumia fursa hiyo kugawa mifuko 50 ya saruji isaidie ujenzi wa shule za msingi katika kijiji hicho ikiwa kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mifuko hiyo ya saruji aliikabidhi kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Ki
jiji cha Migude Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na baadaye kutembelea shule zenye uhitaji mkubwa  vifaa na miundombinu.

 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wakazi wa Kijijizi cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(kushoto) akimtwika ndoo ya maji mmoja wa akina Mama wa Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, katoka katika kisima cha maji kinachotumia umeme wa REA baada ya Naibu Waziri kuwasha umeme katika kijiji hicho.
 Mbunge wa Bagamoyo. Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( pili kushoto) akikata utepe kuashiria kuwasha umeme katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho.
 Moja ya kisima cha maji kilichounganishwa na umeme wa mradi wa REA katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwasha umeme katika kijiji hicho.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( pili kushoto) akitoa zawadi ya mifuko ya saruji kwa viongozi wa serikali za mitaa kusaidia ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji hicho na sehemu ya kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images