Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

HAFLA YA UTOAJI TUZO ZA MASOMO KWA WANAFUNZI BORA CHUO KIKUU ARDHI 2019 YAFANA

0
0

Mkurugenzi wa Kampuni S-M Cathan, Turyahikayo Mugisha akimkabidhi akimkabidhi mwanafunzi bora wa Mwaka katika masomo yote Hellen Shita Cheti cha utambuzi na hundi ya fedha wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao. Wanaoshuhudia (wa nne kushoto) ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga (wa pili kushoto), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Carolyne (kulia) na baadhi ya wanataaluma wa chuo. (Imeandaliwa na Robert Okanda)

SEHEMU ya wanafunzi wa chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kuzawadiwa baada ya kufanya vizuri katika masomo yao.

SEHEMU ya wanafunzi wa chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kuzawadiwa baada ya kufanya vizuri katika masomo yao.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa akimkabidhi mmoja wa wanafunzi cheti cha kumtambua kwa kufanya vizuri kwenye masomo yake wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Carolyne Nombo (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Shahada za uzamivu, tafiti na Machapisho- Dkt. Yasin Senkondo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa akimkabidhi Maryhappines Kamazima cheti cha utambuzi kwa kuibuka mwanafunzi bora wa Mwaka wa pili katika fani ya Utawala wa maji na Usafirishaji, iliyodhaminiwa na Chama cha Uhandisi wa Mazingira (TAEES) wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Carolyne Nombo (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Shahada za uzamivu na Machapisho wa ARU, Dkt. Yasin Senkondo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa akimkabidhi mwanafunzi bora wa Mwaka katika masomo yote Doreen Tiibuza mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa shahada ya ubunifu wa mandhari ya ndani wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa ARU –Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga na Naibu Makamu Mkuu wa ARU-Mipango Fedha na Utawala, Profesa Carolyne Nombo.

SEHEMU ya wazazi, wageni na wanafunzi wa chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kuzawadiwa baada ya kufanya vizuri katika masomo yao.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa akimkabidhi mmoja wa wanafunzi cheti cha kumtambua kwa kufanya vizuri kwenye masomo yake wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Carolyne Nombo (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Shahada za uzamivu na Machapisho- Dkt. Yasin Senkondo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa (wa kumi na mbili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa hafla hiyo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na wadhamini tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao.

BENKI YA CRDB YA CRDB YAZINDUA MKOPO YA ‘BOOM ADVANCE’ KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

0
0
 Benki ya CRDB imezindua mikopo maalum kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ijulikanayo kama “Boom Advance”, uzinduzi huo umefanyika katika tamasha la michezo la ‘CRDB Bank – TOT Bonanza’ na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili alisema huduma ya Boom Advance imelenga katika kuwasiaidia wanafunzi kutatua changamoto ya kifedha pindi wawapo vyuoni. “Kwa muda mrefu tumekuwa tukiangalia ni kwa namna gani tunaweza kuipatia suluhisho changamoto hii ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa inachangia kuathiri masomo ya wanafunzi,” alisema Adili.

Adili alisema mkopo huo wa Boom Advance unatolewa kidijitali kupitia huduma yetu ya SimBanking App, ambapo ni njia rahisi itakayowawezesha wanafunzi kufurahia huduma hiyo wakiwa chuoni bila kutembelea benki jambo ambalo lingeweza kuingiliana na muda wa masomo. “Tumefanya hivi tukifahamu kuwa wanafunzi wengi wa vyuo wapo katika kizazi cha kidijitali,” aliongezea Adili.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ijulikanayo kama 'Boom Advance' uliofanyika wakati wa tamasha la michezo la CRDB TOT Bonanza wikiendi hii.
Ili kupata huduma ya Boom Adavance mwananfunzi anatakiwa kuwa mnufaika wa mkopo kutoka Bodi ya Mikopo HESLB na kusajiliwa katika mfumo wa Benki wa utoaji mikopo kidijitali “Digital Disbursment System”.

Akiongelea baadhi ya sifa na faida za Boom Advance Adili alisema mkopo huo wa Boom Advance unamuwezesha mwanafunzi anaweza kukopa kuanzia TZS 40,000 hadi TZS 120,000 bila riba huku muda wa kurejesha mkopo ukiwa hadi siku 45 tokea kuchukua mkopo, ambapo alisema muda huo umezingatia mpaka mwanafunzi atakapo pata mkopo mwengine kutoka HELSB.
Msheheraji katika uzinduzi wa huduma ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ijulikanayo kama 'Boom Advance', Meena Ally akipata maoni ya mmoja wa wanufaika wa mkopo huo ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Mbaraka Mohammed uliofanyika wakati wa tamasha la michezo la CRDB TOT Bonanza wikiendi hii. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Bidhaa wa Benki ya CRDB, Edwin Kasali. 
Adili alisema katika mkopo huo wa Boom Advance malipo yanafanyika moja kwa moja baada ya mkopo kuingia kwenye akaunti ya mwananfunzi, lakini pia mwanafunzi anaweza kufanya malipo (yote/sehemu) mwenyewe bila kusubiri hela ya mkopo kutoka HELSB kuingia.

Alizungumza kwaniaba ya wanafunzi wa vyuo vikuu mwanafunzi wa Chuo cha Kodi, Catherine Constatine ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma hiyo ya Boom Advance huku akisema itakwenda kuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi hususan katika kipindi ambacho wanakuwa wakisubiri mkopo kutoka HELLSB au pindi wanapoishiwa fedha.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ijulikanayo kama 'Boom Advance' uliofanyika wakati wa tamasha la michezo la CRDB TOT Bonanza wikiendi hii.
Hivi karibuni Benki ya CRDB pia ilifanya maboresho katika Akaunti ya ya wanafunzi ya scholar ambapo hivi sasa akaunti hiyo haina makato ya aina yoyote, mwanafunzi pia anaunganishwa na mifumo ya kidijitali itakayomuwezesha kupata huduma za benki popote pale alipo ikiwamo TemboCard, SimBanking, Internet banking na CRDB Wakala.

Tamasha hilo pia liliambatana na michezo mbalimbali ambapo timu za mpira wa miguu na kikapu za Benki ya CRDB na timu za vyuo vikuu ziliumana vikali.

MIAKA 58 YA UHURU

MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AHUDHURISHA MAHAFALI YA 13 YA CHUO HICHO DAR.

0
0

Mkuu wa Chuo kikuu Ardhi (ARU) Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya akiongoza andamano la wana taaluma katika mahafali ya kumi na tatu ya chuo hicho kwa minajili ya kutunukisha digrii na Stashahada za chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es Salaam Disemba 7 2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa (kulia) na Naibu Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Juma Muhumbi. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo. 

SEHEMU ya wahitimu wakifuatilia matukio ya mahafali yao yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (ARU). 

Juu na chini; baadhi ya wahitimu wakifuatilia matukio ya mahafali yao yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (ARU). 

SEHEMU ya wahitimu wakifuatilia matukio ya mahafali yao yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (ARU)

Furaha ya mafanikio; Baadhi ya wahitimu wakijipiga picha y 'selfie' wakati wa kufungwa kwa mahafali yao yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (ARU).
Mkuu wa Chuo kikuu Ardhi (ARU) Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya (kushoto) akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa.

Mkuu wa Chuo kikuu Ardhi (ARU) Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanataaluma baada ya kuhitimisha mahafali hayo. 

BENKI YA DTB-TANZANIA, LIONS CLUB WAENDESHA KLINIKI YA VIPIMO NA TIBA KWA WANANCHI WA MBAGALA MBANDE, JIJINI DAR

0
0
Mkurugenzi wa Benki ya DTB-Tanzania, Viju Cherian (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki hiyo, Madhava Murthy (kushoto) wakimwangalia Ayasa Mohamed aliyefika kupata matibabu katika kituo cha matibabu ya bure iliyoandaliwa na Klabu ya Lions kwa udhamini wa benki ya DTB-Tanzania ukiwa ni upimaji wa Macho na Sukari kwa Mwananchi wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam, Desemba 8, 2019. Picha na Othman Michuzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DTB-Tanzania, Viju Cherian akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki hiyo, Madhava Murthy, wakikagua kliniki ya utoaji huduma ya afya kwa Wananchi wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam. Zoezi hili liliendeshwa Klabu ya Lions kwa udhamini wa Benki ya DTB-Tanzania, Desemba 8, 2019.
Meya wa Temeka, Mstahiki Abdallah Chaurembo akipatiwa vipimo wakati alipotembelea kliniki ya vipimo kwa Wananchi wa wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam. huduma hizo zilikuwa zilitolewa na Klabu la Lions kwa udhamini wa Benki ya DTB-Tanzania Desemba 8, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa benki ya DTB-Tanzania, Madhava Murthy.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DTB-Tanzania, Viju Cherian akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki hiyo, Madhava Murthy, wakikagua kliniki ya utoaji huduma ya afya kwa Wananchi wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam. Zoezi hili liliendeshwa Klabu ya Lions kwa udhamini wa Benki ya DTB-Tanzania, Desemba 8, 2019.
Daktari wa Macho, Ladislaus Ndimila akimuelekeza jambo mmoja wa wanafunzi wenye tatizo la uoni hafifu waliofika kwenye klinini ya utoaji huduma ya afya kwa Wananchi wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam, iliyofanyika Shule ya Msingi Mbande,  Desemba 8, 2019. Zoezi hili liliendeshwa Klabu ya Lions kwa udhamini wa Benki ya DTB-Tanzania
Afisa Mawasiliano wa Benki ya DTB-Tanzania, Hadijah Natalia Tuwano akipokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wananchi waliofika
kwenye klinini ya utoaji huduma ya afya kwa Wananchi wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam, iliyofanyika Shule ya Msingi Mbande,  Desemba 8, 2019. Zoezi hili liliendeshwa Klabu ya Lions kwa udhamini wa Benki ya DTB-Tanzania
Afisa wa Benki ya DTB-Tanzania, Peter Boaz akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye klinini ya utoaji huduma ya afya kwa Wananchi wa eneo la Mbagala Mbande, jijini Dar es salaam, iliyofanyika Shule ya Msingi Mbande,  Desemba 8, 2019. Zoezi hili liliendeshwa Klabu ya Lions kwa udhamini wa Benki ya DTB-Tanzania.
Huduma ya Dawa ikiendelea kutolewa.

K-Finance yawaomba Watanzania kukopa kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Devotha Minzi(katikati), akiwapa Maelekezo Mwenyekiti wa tume ya Ushidani ,Prof.Humphrey Mushi(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa tume ya ushidani, John Mduma wakati wa maonyesho ya kusherekea Siku ya Ushindani duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Judith Minzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Devotha Minzi(katikati),akimpa maelekezo mteja(kulia) aliyetembelea banda hilo wakati wa Maonyesho ya siku ya ushindani Duniani yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa K-FINANCE Judith Minzi.
Afisa Mikopo wa Kampuni ya K-FINANCE,inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na wateja binafsi Bernadetha Martini akimuelekeza jambo Mteja aliyetembelea bandao hilo wakati wa Maonyesho ya Siku ya ushindani wa kibiashara duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam .

 Kampuni ya K-Finance ambayo hutoa huduma za kifedha na mafunzo ya kibiashara kwa wajasiriamali na kwa watu binafsi, imetoa wito kwa wafanyabiashara hapa nchini kujengea utamaduni wa kukopa na kupata ushauri wa kibiashara kwa ajili ya kukuza mitaji yao.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Judith Minzi wakati ya Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

‘K-Finance ilianzishwa kwa lengo maalumu la kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo ili kufanikisha matarajio yao kwa ukuaji wa biashara zao na hivyo basi, kukuza na kuchangia uchumi wa nchi. Ukuaji wa biashara sio tu kwa manufaa au kwa faida ya wajasiriamali wenye biashara hizo lakini pia kuna manufaa kwa uchumi kwa ujumla’ Minzi alisema.

Aliongeza kuwa huduma zitolewazo ni pamoja na mkopo wa muda mfupi kwa kiasi cha fedha kinachoanzia na shilingi milioni 1 hadi millioni 50 kwa ajili ya mahitaji binafsi na ya wajasiriamali wenye biashara zinazoendeshwa na zilizosajiliwa kwa taratibu za kisheria ambazo zinahitaji mkopo ili kuendeleza bishara hizo ikiwemo kulipia sehemu za uwekezaji mfano ardhi, fedha kwa ajili ya tenda, pamoja na fedha za kufanyia oda mbalimbali bila kusahau mikopo ya watumishi walioajiriwa katika sekta binafsi kuwapatia fedha za kujikimu, kulipia ada ya shule na kulipa bili mbalimbali. Mikopo inatolewa ndani ya masaa 48 baada ya makubaliano kukamilika na malipo ya mkopo ni kwa muda wa mwezi mmoja(1) mpaka miezi kumi na mbili(12).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi wa K-FINANCE Devotha Minzi alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo kumeleta matokeo chanya kwa jamii kwa kutoa huduma za kifedha kwa watu wenye kipato cha chini na cha kati kwa kuwapa mikopo inayowafaa kutokana na mahitaji yao na kuwasaidia kukua kiuchumi na kuwakomboa pindi wanapokuwa na hali ngumu.

K-Finance, imekuwa moja kati ya kampuni kubwa zinazotoa mikopo midogomidogo jijini, na inazidi kuwa kwa kasi mwaka hadi mwaka, alisema mwenyekiti huyo wa bodi huku akiongeza kuwa kampuni hiyo inatarajiwa kuandaa semina kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kibiashara Januari 18 mwakani pale Hekima Garden kwa lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali katika kukuza biashara zao na kusihi wote kuhudhuria tukio hilo la kipekee

Benki ya Barclays yatwaa ushindi Tuzzo za NBAA

0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya mshindi wa tatu katika kitengo cha mabenki makubwa ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na  Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ya Benki yaa Barclays Tanzania, Bernard Tesha katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Kulia ni Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Fedha wa benki hiyo, Muhsin Kaye na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. Isaya Jairo. 
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Barclays Tanzania, Bernard Tesha (kulia), na Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Fedha wa benki hiyo, Muhsin Kaye, wakionyesha tuzo ya mshindi wa tatu katika kitengo cha mabenki makubwa ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na  Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) iliyoshinda benki hiyo mara baada ya kukaabidhiwa jijini Dar es Salaam h kwa Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ya Benki yaa Barclays Tanzania, Bernard Tesha katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Benki ya DCB yaibuka kidedea tuzo za NBAA

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza katika kitengo cha mabenki madogo na ya kati ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia kabisa ni Mkaguzi wa Hesabu za Ndani wa DCB, Samwel Stephano.
Mkaguzi wa Hesabu za Ndani wa Benki ya Biashara ya DCB, Samwel Stephano (kulia) akionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza katika kitengo cha mabenki madogo na ya kati ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) mara baada ya kukabiodhiwa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa DCB, Nelson Swai.

Wanafunzi 81 St. Anne Marie wachaguliwa shule za vipaji maalum

0
0
WANAFUNZI 81 waliomaliza darasa la saba katika shule ya St. Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara wamechaguliwa kujiunga na shule za serikali za wanafunzi wenye vipaji maalum.

Akizungumza na Michuzi media, Mkuu wa shule hiyo, Gradius Ndyetabula amesema jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu walikuwa 99 amapo katika matokeao yao anafunzi wote 99 wa shule hiyo walifaulu kwa wastani wa daraja A na shule hiyo kushika nafasi ya kwanza katika Wilaya ya Ubungo, ya kwanza Mkoa wa Dar es Saam na ya 13 kitaifa.

Amesema shule hiyo pia kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana wanafunzi wote walifaulu kwa wastani wa alama A na shule ikashika nafasi ya kwanza wilaya ya Ubungo, nafasi ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya sita kitaifa.

Amesema siri ya mafanikio hayo ni maandalizi mazuri ya wanafunzi hao hivyo kuchaguliwa kwao kwenda kwenye shule za vipaji maalum si jambo la kubahatisha.

“Shule hii inautajiri wa miundombinu ambao unatokana na uzoefu wa muda mrefu kwani shule hii imetimiza miaka 20 tangu ianze kutoa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa, kutokana na mafanikio haya tunawaomba wazazi waendelee kutuamini na kutuletea watoto na mwezi huu wa Desemba tunaendelea kupokea wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo,” alisema

Ndyetabula amesema kwa upande wa sekondari shule ya St Anne Marie Academy matokeo yamekuwa mazuri kwani matokeo ya kitaifa kidato cha nne 2018, wanafunzi 28 walipata DIV One, wanafunzi 58 DIV II na wanafunzi 48 DIV III na hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la nne wala 0.

"Kwenye matokeo ya kidato cha sita 2019 wanafunzi 19 walipata DIV one, wanafunzi 47 DIV II, wanafunzi 21 DIV III na kwamba hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la nne wala 0 kwenye matokeo hayo...,

“Namshukuru mwalimu mkuu na timu yake kwa umahiri walioonyesha kuwaandaa vijana hawa, miundombinu bora yote ipo kuanzia maabara, maktaba, maji na umeme wa uhakika maana maji hata yakikatika tunaakiba ya mwezi mzima, umeme vile vile hatuna shida hapa ni kusoma tu ” amesema Mkurugenzi wa shule hizo, Dk. Jasson Rweikiza

“Tunawashukuru wazazi kwa kutuamini na tunawaomba muendelee kutuamini kwa kutupa watoto wenu tumekuwa tukiendelea kuboresha mazingira ya kujisomea mwaka hadi mwaka,” alisema
Mkuu wa Taaluma Msaidizi wa St Anne Marie Academy, Kasenga James (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo, Gradius Ndyetabula baada ya wanafunzi 81 wa shule hiyo waliomaliza darasa la saba kuchaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum hivi karibuni.

SHEREHE ZA UHURU ZAWAKUTANISHA TENA FREEMAN MBOWE, SUMAYE NA LOWASSA

0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu-Mwanza

WAMEKUTANA katika Sherehe za uhuru za miaka 58 za uhuru! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kukutana na aliyekuwa Mgombea urais wa Chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Edward Lowassa. Mbali ya kukutana na Lowassa, Mbowe pia amekutana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye ambaye naye siku za karibuni ametangaza kujindoa ndani ya chama hicho.

Kupitia sherehe hizo za Uhuru viongozi hao wamekutana ana kwa ana ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba ambako ndiko zimefanyika sherehe hizo zikiongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

Iko hivi Mbowe aliingia uwanjani hapo akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ambao kila mmoja alikuwa amevalia suti nadhifu na mashati meupe ndani.Safarii hii hawakuwa wamevalia sare zao za kombati.

Katika uwanja huo uwanja hakukuwa na wanachama wa Chadema waliovaa sare za chama hicho.Miaka ya nyuma ilizoeleka kwenye sherehe za kitaifa wana-Chadema kuvalia sare zao lakini safarii hiii wameamua kuweka kando. Wakati wa wana CCM baadhi yao wao walionekana wakiwa na mavazi yao maalumu yenye chama za rangi za chama hicho za kijani na njano.

Hata hivyo Mbowe na Nyalandu baada ya kuingia katika uwanja huo mapema asubuhi waliingia kwa kupita katika lango la viongozi wa kitaifa na kupokelewa kwa heshima zote kama ilivyofanyika kwa viongozi wengine.

Walipopokelewa walioneshwa eneo maalumu ambalo lilitengwa kwa ajili ya wageni wa kitaifa kuungana na viongozi wengine ambao tayari walikuwa wamefika eneo hilo la uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa kukumbusha tu Mbowe na Chama chake cha Chadema walikuwa wamesusia sherehe hizo kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2015 baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani.

Hata hivyo wakati Mbowe anazungumza mbele ya Rais Dk.Magufuli alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa ameamua kushiriki kwenye sherehe hizo yeye na Chama chake kama inshara ya kurejesha umoja , upendo na msikamano kwa Watanzania.

Ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Rais Magufuli kuhakikisha anarejesha utengamano wa maeleno na maridhiano huku pia akiomba uhuru wa demokrasia.

MNYIKA, LEMA NDANI YA MAGANDWA,CCM KIJANI NA NJANO YAO WAKATI WA SHEREHE ZA UHURU

0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza

MBUNGE wa Kibamba jijini Dar es Salaam John Mnyika pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakiwa wameongozana na Meya wa Ubungo Boniface Jacob wametinga uwanja wa CCM Kirumba Mjini Mwanza katika Sherehe ya miaka 58 ya Uhuru wakiwa wamevaa sare zao za magwanda huku wana CCM wakiwa na sare zao za kijani na njano.

Wabunge hao kama ambavyo ilivyo kwa viongozi wengine wa kisiasa walioshiriki sherehe hizo walipata nafasi ya kukaa jukwaa kuu kushuhudia kila kinachoendelea uwanjani hapo.Viongozi wa Chadema kwa muda mrefu walikuwa wamesusia kushiriki sherehe hizo lakini safari hii wameona isiwe tabu. Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana naye alikuwa miongoni mwa walioshiriki.

Wakati huo huo mbali ya wabunge hao, pamoja na wabunge wengine lukuki wa CCM walioshiriki katika sherehe hiyo, idadi kubwa ya wananchi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani nao wamejitokeza kwa wingi,Idadi ya watu ilikuwa kubwa kiasi cha Rais Dk.John Magufuli kueleza watu waliojitokeza ni wengi sana na haijapata kutokea kuona kuna viongozi wa kada zote na kwa awamu tofauti.

Ukweli ni kwamba hamasa ya wananchi wa Mwanza kushiriki kwenye sherehe hizo ni kubwa na mapema kabisa ilionekana namna ambavyo makundi ya watu yalivyokuwa yakipita mtaani kuelekea CCM Kirumba.

Katika kuhakikisha watu wanapata nafasi ya kuingia uwanjani mapema, milango ilikuwa imefunguliwa saa 10 alfajiri na hivyo kutoa nafasi kwa kila aliyekwenda kutotumia muda mwingi kupanga foleni ya kuingia uwanjani hapo.

Ilpofika saa moja asubuhi karibu majukwaa yote ya uwanjani hapo yalikuwa yamejaa na wakati huo huo watu wakiendelea kuingia kwa kupanga foleni.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa idadi kubwa ya watu kujitokeza uwanjani hapo ni mapenzi ya Watanzania kwa Serikali na Taifa lao.
MBUNGE wa Kibamba jijini Dar es Salaam John Mnyika

TPA WATAJA MAMBO MATANO WANAYOJIVUNIA MIAKA MINNE YA RAIS MAGUFULI

0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu -Mwanzania

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) umeamua kutaja mambo matano muhimu ambayo kwa sasa wanajivunia nayo katika utendaji wao wa kazi katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani.

Akizungumza jijini Mwanza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema jambo la kwanza ambalo wanajivunia nalo ni kukua kwa uwezo wa bandari zilizopo Bahari Kuu na Maziwa Makuu yote nchini.

“Katika kupima uwezo wa bandari ni pamoja na kuangalia tani za shehena ambazo tunazihudumia ukilinganisha na wengine au ukijilinganisha na kipindi kilichopita.

"Hili swali la nini tunajivunia, kwanza tunamshukuru Rais Dk.John Magufuli ambaye kwa nia yake ya dhati amedhamiria kufufua na kuimarisha bandari kama sehemu muhimu kwa uchumi wa nchi. Ni swali la kawaida katika misingi ya menejimenti , sababu unajivunia nini maana yake ni matokeo ya kufanikisha utekelezaji kwa kile ulichopanga.

"Kama ukilima shamba unatarajia kuvuna na utakuwa na malengo ya magunia kiasi gani au tani ngapi kwa heka, sasa ukizipata zile ndiyo unasema najivunia kwa kupata kile nilichoanga au zaidi,"amesema.
Amesema TPA imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine ili kufufua meli na miudombinu ya bandari nchini na kazi hiyo imekuwa ikifanyika kwa mafaniko makubwa.

“Kwetu sisi tukiona kuna meli nyingi tunapata usingizi lakini meli zikikosekana hata usingizi hauji kabisa na unaamka usiku kuanza kuuliza kwa mameneja , maana yake kila mahali kukiwa hivyo, Bandari ya Dar es Salaam imeongeza meli.

"Tunazihasebu meli kwa wingi wake na ukubwa wake kwa maana ya uwezo, unaiangalia Tanga, Mtwara, meli zinavyoongezeka, ndivyo usingizi unavyopatikana, meli zikipungua ndivyo unaihirisha kulala na kuangalia unazitafutaje, hivyo tunajivunia ongezeko la meli,"amesema Mhandisi Kakoko.

Ameongeza kuwa wakati wanaanza kazi kwa maana ya menejiment na bodi mwaka 2016 , meli zilikuwa chache sana na hiyo ilianza mwaka 2014/2015.Ndio ambacho mzigo wa shehena ilipungua, hivyo hicho ni kipimo cha kwanza.

“Nchi zote tulishusha mzigo na ndio kipindi tulipingwa na hao mnaosema wanasambaza propaganda kuwa Bandari ya Dar es Salaam imechoka na haina tofauti na bibi kizee ambaye hata akipaka wanja hauwezi kutoka.

"Ni kipindi ambacho wengi wenu mlipiga picha magofu ya bandari ambayo yalikuwa yamebomolewa kwa ajili ya kujenga miundombinu,"amesema Mhandisi Kakoko na kuongeza hivyo wanajivunia hatua waliyofikia na mpango uliopo ni kuongeza shehena ambapo haipungui tani milioni moja kwa mwaka.

Na kwamba awali walikuwa wanahudumia tani milioni 14.7 kwa mwaka lakini kutokana na kuimarishwa kwa huduma bandarini wakafanikiwa kufikia tani milioni 17.8 na sasa wanazungumzia tani milioni 18.1.

Pia anasema wanajivunia kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kwani kwa sasa mapato yamepanda ikilinganisha na huko nyuma ambapo kwenye upande wa shehena walikuwa na ongezeko la asilimia 6 hadi 7 na sasa wamekwenda asilimia tisa hadi 11 mwaka.

“Kwenye fedha tunakipimo hicho hicho, tumekuwa na fedha ingawa sina tamkwimu hapa,lakini tulikuwa tunakusanya Sh.bilioni 300 na imekuwa ikipanda mwezi hadi mwezi. Tulitoka Sh.bilioni 300, tukaenda Shilingi bilioni 320, baadae Sh.bilioni 360,"amesema.

Ameongeza kuwa hivyo wamekuwa na ongezeko kati ya Sh. bilioni 10 kila mwaka hadi Sh.bilioni 20 na kusisitiza kuwa wakati menejmenti na bodi walipokuwa wanaingia walikuwa wanafikisha Sh. bilioni 608 , lakini sasa wamepanda na kufikia Sh.bilioni 940 na mkakati wao ni kufikia makusanyo ya Sh.trilioni 1.4.

Wakati jambo jingine ambalo wanajivunia kayika kupindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwa na uwezo wa kutoa gawio la Sh. bilioni 480 na kwamba hivi sasa wamekuwa wakipata inayozidi Sh.bilioni 240.

“Hivyo kigezo cha pili ni mapato kwa njia ya fedha ambayo unaweza kuyaona yana uwiano na shehena tunayoihudumia , tunataka kujihakikishia kuendelea , tumejilinganisha na wenzetu market share yetu kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ni asilimia 26 wakati bandari ziko nyingi tu tena kubwa ,unaweza kusema ziko bandari kama sita au saba. Tukiziunga bandari zote hizo sisi bado tunaongoza kwa asilimia hizo.

“Kwa hiyo ni zaidi ya robo kwa mfano sasa hivi kuna tani zaidi ya milioni 60 hadi milioni 70 ambazo ziko kwenye bara hili (Afrika)ambazo zinaingia na kutoka , sisi kama tunahiyo basi tuna Market Share kubwa. Tunamshukuru Rais, kwani tunapozungumzia viwanda vya ndani kwetu ni faida
“Miradi inayoendelea nchini kwetu inatuinua sana , kwa mfano mradi wa reli kuna vyuma ambavyo vinaingia nchini, na kupitia vyuma hivyo na mitambo mingine tunapata fedha, hata mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere nako tutapata fedha kupitia mradi huo kwani malighafi za ujenzi zitapita kwenye bandari yetu,” alisema.

Pia Mhandisi Kakoko amesema wanajivunia vigezo vya uzalishaji , kwa maana ya muda unaotumika katika kutoa huduma kuanzia malori yanapoingia , yanavyopakia shehena, muda gani wa kupakua na kupakia mizigo ya shehena.

"Muda gani meli inakaa kwenye gati. Tangu unapofunga kamba ya kwanza , unaanza kuhudumia meli hadi inapofungua kamba ya mwisho inapoanza kuondoka , kwasababu meli kwa kawaida inafungwa na kamba nne au tano
“Sasa tunaanza kuhesabu tangu ilipofungwa kamba ya kwanza maana ile ni huduma , ukichelewa kufunga kamba ni kupoteza muda, kama muda kupakia na kushusha shehena inahesabiwa.

"Hivyo kufungua kamba ya mwisho na meli kuanza kutembea ile ni muhimu sana , inatakiwa muda uwe mdogo hata kama mzigo ni mkubwa, kwani inapima uwezo wako wa kutoa huduma, hivyo katika eneo hilo tumefanikiwa,” amesema.

Wakati huo huo amesema uhusiano mzuri kati yao na wadau wengine ni jambo muhimu kwao na hilo wanajivunia nalo sana kwa sasa."Mahusiano mazuri na wadau wengine kwetu ni muhimu na hayawezi hayapimiki kwa tani,"amesema.

Alisema suala la uhusiano mwema kwa jamii kupitia biashara hurudisha wateja, kwani hakuna mteja anayekubali kuleta vitu vyake mahali penye kelele au katika eneo ambalo muda wowote inaweza kutokea vita na mzigo ukapotea.

Pia amesema amani iliyopo nchini ni jambo la aseti ambayo watalaamu hawajaweza kubainisha thamani ya amani ni shilingi trilioni ngapi lakini hiyo kwa Tanzania imekuwa fursa nyingi ya bandari zake kuwa sehemu salama ukilinganisha na nchi nyingine
 Ukarabati wa MV. Victoria ukiendelea katika Ziwa  Victoria ukiwa ni mkakati wa kuimarisha huduma ya usafiri wa meli katika ziwa hilo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini Mhandisi Deusdedit Kakoko akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Mwanza

MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI ATAJA MKAKATI KUKOMESHA BANDARI BUBU ZOTE 601 ZILIZOPO

0
0
*Asema wanaomiliki bandari zao binafsi nao lazima watambuliwe kisheria
 
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu -Mwanza

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema pamoja na mikakati inayoendelea kuimarisha sekta ya bandari, moja ya changamoto iliyopo ni wingi wa utitiri wa bandari bubu ambapo kwa sasa zimefikia 601 huku akitaja hatua za kuhakikisha bandari hizo zote zinakuwa sio bubu tena kwa kuchkua hatua kwa mujibu wa sheria.

Amesisitiza TPA imeiona changamoto hiyo, hivyo imedhamiria kuwa muda sio mrefu lazima ziwe zimepatiwa majibu yake ili nazo zianze kuingiza mapato kwa Serikali kutokana na huduma zinazoendelea kwenye bandari hizo kokote ziliko iwe katika maziwa makuu au bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza , Mhandisi Kakoko ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio lukuki yaliyopatikana ndani ya Mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.
Ambapo amesema licha kuwa na mafanikio makubwa ambayo wanajivunia, bado ni wajibu wao kuendelea kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto ikiwemo hiyo ya uwepo wa bandari bubu.

"Awali kulikuwa na bandari bubu 437 lakini baada ya muda kidogo tukabaini zimeongezeka tena hadi kufikia bandari bubu 601.Hivyo mkakati wetu ni kuhakikisha hakuna bandari bubu hata moja ndani ya nchi yetu, na huo ububu hautakuwepo bali ziwe na ndimi ya kutoa fedha.

"Kuwa na bandari bubu ni ngumu kujua kitu gani kinasafirishwa kupitia bandari hizo , hivyo kiusalama nayo sio jambo nzuri, lazima tufahamu kila kinachoingia na kutoka ndani ya bahari zetu.Tutaweka utaratibu maalumu wa kuzitambua bandari zote bubu na kimsingi tayari tunazifahamu na muda mchache ujao zote zitakuwa zinatambuliwa na TPA.

Amesisitiza katika kuhakikisha bandari bubu zote zinatambuliwa na TPA, pia watatumia utaratibu wa kushirikisha viongozi wa maeneo husika ambao nao watakuwa sehemu ya wadau muhimu,"amesema Mhandisi Kakoko.

Amesema kuwa kama uwepo wa bandari bubu unatokana na gharama kubwa katika bandari zilizopo, hilo ni jambo ambalo linazungumzika kwani TPA haipo kwa ajili ya kutaka faida kubwa zaidi ya kutoa huduma kwa gharama nafuu.

"Ukweli tumejipanga kuzidhibiti zote, kama kuna sababu ya kuwepo kwa bandari hizo tutata kufahamu na kutafuta jibu la pamoja.Kama kwenye bandari zetu gharama ni kubwa, ni jambo ambalo linazungumzika, tuko tayari kupunguza na hatimaye sote tuwe tunatumia bandari zinazotambuliwa na TPA.

"Tunatambua pia kuna baadhi ya watu binafsi wanamiliki bandari zao na kuendelea na shughuli za utoaji wa huduma kwa wananchi.Nako tumeanza mazungumzo na baadhi yao ili hatimaye nao tujue wanachokifanya na huduma ambazo wanazitoa na hapo tutapa kodi yetu na hivyo Serikali kuingiza fedha.Hatuna nia mbaya na wanaomiliki bandari lakini lazima tuwatambue na tuepeane maelekezo ya nini ambacho tunataka kuona kinaendelea kwenye bandari hizo,"amesema Mhandisi Kakoko.

Kuhusu mikakati iliyopo katika kuboresha miundombinu katika bandari za maziwa makuu zikiwemo bandari za Ziwa Victoria, Mhandisi Kakoko amesema TPA kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Kampuni ya Huduma za Meli na TRC wameendelea na mkakati wa kuboresha bandari hizo.
"Katika Ziwa Victoria mikoa yote ambayo ziwa hili limepita, kuna bandari na zile ambazo zilikuwa zimeanza kulega lega na kuchoka kimiundombinu,sasa matengenezo yanafanyika , Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kujenga miundombinu ya bandari hizo na hakika mambo yanakwenda vizuri,"amesema Mhandisi Kakoko.

Hata hivyo amesema kwa kutambua umuhimu wa bandari kama kichocheo muhimu cha maendeleo ya wananchi wa kanda ya Ziwa, TPA imeweka mkakati wa kuhakikisha kila mkoa uliopo kwenye ziwa hilo au kila wilaya kunakuwa na bandari.

"Kila Mkoa utakuwa ba bandari kubwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi, na hivyo hivyo kwa kila wilaya nako kutakuwa na bandari na huo ni mkakati ambao tutaunza awamu ya pili ya malengo yetu."
Akizungumzia bandari ambazo kwa kanda ya Ziwa ni maalum kwa ajili ya kusafirisha mizigo ,ameitaja bandari ya Kemondo, Bandari ya Mwanza Kaskazini na Bandari ya Musoma ambazo hizo zilikuwa na mfumo wa reli ambazo zinakwenda moja kwa moja kwenye meli kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji mzigo, hivyo mojawapo ya kazi inayoendelea sasa ni kufufua miundombinu katika bandari hizo na kazi inakwenda vizuri.

Amesema kwa kutumia usafiri wa meli na reli, gharama za usafirishaji ziko chini ikilinganishwa na kusafirisha mizigo kwa njia usafiri wa malori hasa kwa kuzingatia kusafirisha kwa barabara inapofika kuanzia kilometa 500 gharama inakuwa kubwa lakini wa kutumia reli na baadae meli unasafirisha mzigo mkubwa lakini kwa gharama nafuu.

Wakati huo huo, Mhandisi Kakoko amesema kauli ya Rais ya kutaka kurudishwa kwa Shirika la Meli ya Taifa, wao wameipokea kwa mikono miwili na ilikuwa ni kilio chao cha muda mrefu, hatimaye kimesikika kwani wanaamini shirika hilo litakaporejea idadi ya meli zitaongezeka na wao bandari wanachotamani kuona ni uwepo wa meli nyingi nchini.

Ametoa mfano nchi ya Ethiopia ndio yenye meli nyingi kwa kuwa na meli 96 lakini hawana ukanda wa bahari, wakati Tanzania yenye kilometa zaidi ya 1, 440 za bahari kuna meli 14 tu na kati ya hizo nne ndio zinatoa huduma.Hivyo lazima kuwepo na meli za kutosha na hasa kwa kutambua Tanzania inaweza kutumia eneo la maji tu kujiendesha kiuchumi.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini Mhandisi Deusdedit Kakoko akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mambo ambayo mamlaka hiyo inajivunia katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli
wananchi wakiendelea na shughuli zao katika Bandari ya Musoma mkoani Mara ambapo kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ni kwamba bandari hiyo ni miongoni mwa bandari zilizopo katika Ziwa Victoria ambazo zipo katika mkakati wa kuboreshwa kiundombinu

RAIS MAGUFULI AANIKA MAFANIKIO MIAKA 58 YA UHURU

0
0

*Aelezea hatua kwa hatua namna Watanzania wanavyoshiriki kuleta maendeleo ya nchi yetu

*Ahimiza umuhimu wa kuendelea kulinda amani, umoja, upendo na mshikamano

Na Said Mwishehe-Michuzi Globu ya jamii-Mwanza

RAIS Dk.John Magufuli amewaongoza maelfu ya Watanzania katika kusherehekea sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika ambazo zimefanyika katika Jiji la Mwanza ambapo pia viongozi karibu wote wa Serikali na vyama vikuu vya siasa wamehudhuria.

Wingi wa watu katika sherehe hizo umesababisha baadhi ya wananchi kwenda kukaangalia sherehe hizo katika Uwanja wa Furahisha baada ya uwanja wa CCM Kirumba kujaa na kukosekana nafasi kabisa ya watu kukaa.

Rais Magufuli wakati anazungumza na Watanzania walioko uwanja wa CCM Kirumba leo jijini Mwanza ameelezea furaha aliyonayo katika kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wetu ambapo kuna hatua kubwa ya maendeleo ambayo imefanyika kwa nyakati tofauti kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa Awamu ya Tano ambayo nayo inaendeleza pale ambapo watangulizi wengine wameishia.

Hata hivyo amesema kuwa sababu za kufanyika Mwanza kwa sherehe hizo ni kuondoa mazoea ambayo yameoeeleka kuwa kuna mikoa fulani ndiko ambako zifanyikie. Pia amesema kuwa ifahamike sherehe za Uhuru hazikufanyika kwa miaka miwili, mwaka 2015 na mwaka 2018.

"Fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe katika miaka hiyo zilikwenda kutumika kufaya maendeleo ya Watanzania.Tunafahamu sherehe hizo huambatana na fursa mbalimbali, kuchochea maendeleo ya mkoa huo na leo hii pamoja na mambo mengine tunajivunia amani iliyopo nchini kwetu tangu tumepata uhuru, tumeendeelea kulinda umoja na mshikamano.

"Hii ni siku muhimu kwa Watanzania wote lakini nikiri Mwanza mmefunika , mmejitokeza kwa wingi sana katika sherehe hizi ukingalisha na maeneo mengine.Hongereni sana, nimeambiwa uwanja umejaa, kule nje kumejaa, Uwanja wa Furahisha umejaa, hii haijawahi kutokea. Siku kama ya leo Desemba 9, mwaka 1961 Tanganyika ilipata Uhuru wake kutoka kwa wakoloni,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa uhuru huo ulitokana na jitihada za Watanganyika wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele na shupavu katika kusimamia misingi ya kuwaunganisha Watanganyika na hatimaye kupata uhuru.

Ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa wazee wetu 17 ambao Julai 7 mwaka 1954 walishiriki kikao cha kwanza baada ya TANU ambayo ilifanikisha kupatikana kwa Uhuru wetu. "Hawa wazee wanastahili pongezi kutokana mchango ambao wameutoa kwa Taifa letu."

Pia amewapongeza viongozi waliopita pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio ambayo nchi yetu imepata tangu kupata Uhuru wake mwaka 1961.Pamoja na mafanikio amesema kujenga nchi nako kuna changamoto zake, hivyo ni vema wananchi wote wakaendelea kushirikiana kuhakikiha nchi inasonga mbele kimaendeleo.

"Hivyo jukumu la kizazi cha sasa ni kuendeleza pale walipoishia watangulizi. Kinachofurahisha zaidi nchi yetu amani imeendelea kuimarika, nchi yetu imekuwa yenye umoja na mshikamano, namshhukuru Rais Shein (Dk. Ali) ambaye tunashirikiana kulinda Muungano wetu kikamilifu,"amesema.

Ameongeza Uhuru ambao tuliupata mwaka 1961 ni hatua za mwanzo za kujikomboa kisiasa lakini sasa ni wakati wa kuendelea kuweka mipango kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi. Kujenga nchi si lelemama, ni kazi ngumu na tumevuka milima na mabonde, hivyo leo hii ni fursa ya kufanya tathmini kuhusu wapi tumefikia, katika ujenzi wa taifa letu.

"Na katika hilo napenda kutumia fursa hii kuzipongeza awamu zote ambazo zimetangulia kwani zimefanya kazi kubwa ya kujenga nchi yetu.

"Kila awamu imefanikiwa kufanisha majukumu yake kuanzia Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Awamu ya Pili ya Mzee Mwinyi (Ali Hassan), Awamu ya Tatu Mzee Mkapa (Benjamin) pamoja na Awamu ya Nne ya Mzee Kikwete (Jakaya)".

Ametaja baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana ni kuendelea kudumishwa kwa amani nchini. Amani iliyopo imesababisha nchi kusifika ndani na nje ya Bara la Afrika.

Rais Magufuli amesema kuwa mafanikio mengine ni katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua maendeleo ambayo yamefanyika nchini.

"Nitoe mifano michache wakati tunapata Uhuru baada ya kutawaliwa na wakoloni kwa takribani miaka 76 nchi yetu ilikuwa na barabara za lami zinazounganisha mkoa na mkoa, wilaya na wilaya zilikuwa kilometa 360 tu. Kipande cha barabara ya Dar e s Salaam hadi Morogoro pamoja na kipande cha Tanga-Korogwe na Arusha- Moshi.

"Kwa sasa tuna barabara za lami kilometa 12,679.55, wakati kilometa nyingine zaidi ya 2400 zinaendelea kujengwa kwa kiwangon cha lami huku pia kilometa 7,087 zipo kwenye hatua mbalimbali za maandalizi kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami,"amesema.

Pia amesema madaraja ambayo yamejengwa nchini madogo ni zaidi ya 8,000, ya kati zaidi ya 79 na madaraja makubwa 17 na mengine yapo kwenye hatua mbalimbali ikiwamo daraja ya Busisi ambalo ujenzi wake umezinduliwa kwa kuwekwa jiwe la msingi na daraja la Salender jijini Dar es Salaam.

Katika huduma za afya, Rais Magufuli amesema kwa nchi ilipokuwa inapata uhuru kulikuwa na vituo vya kutolea huduma za afya 1,095, yaani hospitali 98, vituo vya afya 22 na zahanati 975, lakini sasa idadi imeongezeka kwa kiwango kikubwa. "Kuna vituo vya afya 7,293, hospitali 178, na zahabati 6,285."

Kuhusu shule alisema mwaka 1961 kulikuwa na shule za msingi 3,100 na sasaa kuna shule za msingi 17,379, wakati shule za sekondari zilikuwa 41, leo hii kuna sekondari 4,817, Chuo Kikuu, kilikuwa kimoja na sasa kuna vyuo vikuu 48.

Amesema hiyo ni mifano michache kati ya mingi kutokana na maendeleo ambayo yamefanyika nchini kwetu ambapo alitumia nafasi hiyo kuelezea kuongeza kwa watumishi wa umma wa kada mbalimbali ikiwemo kada ya madaktari waliosajiliwa ukilinganisha na huko nyuma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza.

MLIMBWENDE KUTOKA AFRIKA KUSINI AWABWAGA 87 MASHINDANO MISS UNIVERSE

0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MREMBO kutoka Afrika Kusini Zozibini Tunzi (26) amejinyakulia taji la Miss Universe kwa mwaka 2019 akizibwaga nchi 87 zilizoshiriki mashindano yaliyofanyika huko Atlanta nchini Marekani.

Zozibini amevalishwa taji hilo usiku ya jumapili ya Desemba 08 baada ya kupitia katika raundi zote huku akijibu vyema  maswali yaliyohusu jamii ikiwemo ni kueleza kwanini awe chaguo katika mashindano hayo

Moja ya maswali ambayo Zozibini alijibu baada ya kuulizwa kwanini awe chaguo la kuwa Miss Universe alisema kuwa;

"Nimekua katika dunia ambayo mwanamke kama mimi mwenye ngozi na nywele za aina yangu haijawahi kuzingatiwa kuwa ni mwanamke mzuri, ninafikiri ni wakati wa kuacha hili leo, ninataka watoto wangu wanitizame  na kuona sura zao zikiakisi yangu" ameeleza mlimbwende huyo.

Washindi waliofuatia ni mrembo kutoka Mexico (Miss Mexico) na mrembo kutoka Puerto Rico.

Sophia Aragon ambaye ni Miss Mexico ameeleza kuwa urembo unaweza kutumika kwa namna mbalimbali ambazo zinalenga kusaidia jamii.

Mshindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 Catriona Gray kutoka Ufilipino ameeleza kuwa mabadiliko yameendelea kufanyika katika mashindano hayo na yana mwelekeo mzuri.

Katika madhindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara 68 sasa Tanzania iliwakilishwa na Shubila Shanton Kaigarula (23).

Wameondoka Majenerali wa Sekta Binafsi Tanzania

0
0
Na Paul R.K Mashauri

Elvis Tables Musiba, Sir. Andy Chande, Dr. Reginald A. Mengi, Ruge Mutahaba na Ali Mfuruki.

Miaka michache iliyopita tulimpoteza Elvis Tables Musiba aliyekuwa Mwenyekiti wa TPSF (Tanzania Private Sector Foundation). Mwaka jana tukampoteza Sir. Andy Chande aliyekuwa kiongozi wa sekta binafsi toka enzi za ukoloni.

 Mwaka huu tumewapoteza wafanyabiashara 3 wakubwa ambao walikuwa viongozi na watu muhimu sana kwa sekta binafsi Tanzania. Dr. Reginald Abraham Mengi aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI (Confederation of Tanzania Industries) na TPSF, Ruge Mutahaba aliyekuwa mjumbe wa MOAT (Media Owners Association of Tanzania) na mjumbe wa TRA Stakeholders Forum na jana tumempoteza Mr. Ali Mfuruki aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table.

Vijana wengi wamewaona na kuwasikia hawa watu "the generals" lakini wengi hawajui historia ya sekta binafsi Tanzania na mchango wao katika kuifikisha sekta binafsi hapo ilipo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoeleza japo kwa kifupi mchango wao kwa sababu kwa namna moja au nyingine wote hawa kuanzia Sir. Andy Chande, Elvis Tables Musiba, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mr. Ali Mfuruki na Ruge Mutahaba nimefanya nao kazi za sekta binafsi kwa karibu sana.

Sir. Andy Chande nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa "boards" mbalimbali za taasisi kama MOI, IMTU, TRL nk. Na pia alikuwa mshauri katika "board" ya kampuni yangu mwenyewe. Ni bahati mbaya sana kwamba mwezi moja kabla ya kifo chake, mimi na Sir. Andy Chande tulipanga kukutana ili mimi Paul Mashauri nimfanyie "interview" ya namna sekta binafsi ya nchi hii ilivyokuwa kabla na baada ya uhuru. "Interview" ile ilikuwa itumike kama kipindi cha TV ili wengi zaidi wanufaike na uzoefu aliokuwa nao. Bahati mbaya Sir. Andy Chande alifariki kabla hatujakamilisha jambo hilo jema.

Elvis Tables Musiba nilifanya naye kazi akiwa Mwenyekiti wa TPSF na mimi nikiwa mjumbe wa kamati mbalimbali za sekta binafsi Tanzania. Tulisaidiana kuchangisha fedha"fundraising" kwa shughuli mbalimbali za kitaifa, na alitumia wakati huo kunisimulia mambo mengi sana.

Mr. Ali Mfuruki nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa CEO Round Table na mlezi wa TRBN (Tanzania Responsible Business Network) chini ya UN Business Compact na mimi nikiwa ni mjumbe wa "secretariat" ya TRBN.

Dr. Reginald Abraham Mengi nilifanya naye kazi yeye akiwa ni Mwenyekiti wa CTI na mimi nikiwa ni mjumbe wa kamati ya SME ya CTI. Na Ruge Mutahaba nilifanya naye kazi wote tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum.

Mara nyingi wote hawa walitumia muda wao mwingi kunisimulia vitu vingi sana wao wakiwa wakubwa kwangu kiumri na mimi nikiwa mdogo sana kwao. Wakati huo nilikuwa sijui kwanini wananiambia mambo yote hayo ya sekta binafsi kwa sababu kwanza nilikuwa mdogo sana na pili sikuwa na nafasi wala heshima kubwa kama walizokuwa nazo wao lakini jana baada ya kupata taarifa za kifo cha Mr. Ali Mfuruki nikagundua pengine walitaka siku moja niyasimulie hayo ili kizazi cha leo kipate kuelewa.

Wafanyabishara vijana, viongozi vijana katika serikali na wajasiriamali vijana wanaochipukia, lazima waelezwe kwamba historia ya sekta binafsi Tanzania haiwezi kuelezwa pasipo majina ya hawa wote niliowataja hapo juu. Lakini pia wapo wengine ambao wameshatutoka na wengine ambao bado wapo hai. Pia sitatenda haki nisipowataja japo baadhi yao. Hao ni pamoja na marehemu Mzee Mwakitwange, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mwapachu, Elvis Tables Musiba, Mzee Iddi Simba na wengine ambao sikupata kuwafahamu. Hawa walikuwa waanzilishi wa TCCIA mwishoni mwa miaka ya 80 kabla ya baadhi yao kuondoka TCCIA na kuanzisha CTI. Kwanini waliondoka na TCCIA kuanzisha CTI? Hiyo ni mada nyingine ambayo inahitaji makala tofauti na hii.

Ukiondoa Mzee Mwakitwange ambaye alitangulia mbele za haki zamani kidogo, wengine wote akiwemo Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mapachu na Mzee Iddi Simba nimepata kufanya nao kazi na kupata simulizi zao. Mzee Anorld Kileo ambaye alikuwa ni CEO wa TBL kwa muda mrefu sana na kiongozi wa TPSF yeye aliniita ofisini kwake na kunikalisha chini kwa masaa zaidi ya 3 akinieleza sekta binafsi ilipotoka na namna walivyopambana kuifikisha hapo ilipo. Ukurasa huu hautoshi kuandika historia yote ya ujasiriamali Tanzania ambayo vijana wengi wangependa kuijua lakini Dr. Juma Mwapachu aliandika kitabu chenye historia hii vizuri sana. Mimi nitagusia yale niliyoelezwa na hawa "generals" wa sekta binafsi Tanzania kwa kifupi sana.

1.Sir. Andy Chande, Mwanzilishi, Chande Mills

Sir Andy Chande alinieleza kwamba baada ya Uhuru wa nchi hii, Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere alitaka kumteua kwenye baraza la mawaziri. Lakini akamwambia Mwalimu Nyerere, naomba uniache kwenye sekta binafsi. Mwalimu Nyerere aliheshimu mawazo ya Sir. Andy Chande. Lakini Mwalimu Nyerere akaamua kumteua Sir. Andy Chande kuwa mjumbe wa kamati ya uchumi na maendeleo mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru. Kwa vijana wasiomfahamu Sir. Andy Chande huyu ndiye aliyekuwa mfanyabiashara wa kitanzania mwenye nguvu kubwa za kiuchumi wakati wa ukoloni na hata baada ya kupata uhuru. Aliendesha biashara ya kifamilia iliyoitwa Chande Mills ambayo baadaye ilitaifishwa na serikali mwaka 1967 wakati wa "Nationalization" na kuwa NMC (National Milling Corporation) kiwanda ambacho baadaye kilikuja kununuliwa na Bakhresa.

Sir. Andy Chande ndiye aliyekuwa mtanzania mwenye asili ya kiasia kuanza kutoa misaada kwa watu (philanthropism) kuanzia wakati wa uhuru mpaka alipofariki dunia miaka michache iliyopita. Kilichonishangaza kuhusu Sir. Andy Chande ni kwamba hata baada ya serikali kutaifisha biashara yake, bado aliendelea kutumia mtandao wake wa watu "network" akili na maarifa yake kuitumikia nchi. Sir. Andy Chande ananisimulia anasema, baada ya serikali kutaifisha biashara yake, Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu, akamuuliza; Rafiki yangu Chande; unataka kwenda wapi baada ya serikali kuchukua biashara yako kwa manufaa ya umma?

Sir. Andy Chande akamuambia Mwalimu Nyerere; "sina pa kwenda". Mwalimu akamuambia "sasa kuanzia leo, wewe ndio utakuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hii mpya inayomilikiwa na wananchi wote wa Tanzania. Sir. Andy Chande akajibu " sawa Mh. Rais". Na ikawa hivyo. Ingekuwa sisi vijana wa leo, rafiki yako ndiyo kiongozi wa nchi au DC au Mkuu wa mkoa au Waziri, anakufahamisha maamuzi ya serikali, tungeleta urafiki na mambo binafsi kwenye mambo ya nchi. Lakini Sir. Andy Chande alikuwa anajua kutofautisha ni wakati gani Nyerere, "rafiki" yake anaongea na ni wakati gani Nyerere, "Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu" anaongea. Alikuwa anajua mipaka yake.

Kutokana na uwezo wa Sir. Andy Chande, Mwalimu Nyerere alimpa uenyekiti wa "boards" nyingi sana ikiwa ni pamoja na TRL, ATC nk. Pia alikuwa Mwenyekiti wa "board" ya Kioo Ltd, Shaaban Robert Secondary School, IST, Barclays bank, Taasisi ya walemavu buguruni nk. Siwezi kuzimaliza zote ni nyingi mno.

Nilikuwa nyumbani kwake Upanga alipokuwa akisimulia haya. Nikamuuliza sasa uliwezaje kukubali kuwa Mwenyekiti wa "board" ya kampuni ambayo umeihangaikia miaka mingi na sasa si yako tena. Akasema mke wangu alinitia sana moyo. Lakini pili kwenye biashara usiweke mambo moyoni. Ukiweka mambo moyoni utakufa. Moyoni nikajisemea; Huyu kampuni yake aliyoisotea miaka mingi imechukuliwa. Tena siyo kampuni yenye mapato ya shilingi milioni 10 au bilioni moja. Unazungumzia mabilioni ya shilingi. Lakini bado maisha yakaendelea. Wewe umepoteza mteja mmoja unataka kufunga biashara. Kwanini? Hayo ni masomo ambayo nataka vijana wengi wayashike, kwamba;

I.Mke au mume wako ana mchango mkubwa sana katika maisha yako ya uongozi, biashara au ujasiriamali. Unapooa au kuolewa lazima uangalie mtu ambaye atakutia moyo wakati ukipitia changamoto za maisha kama ilivyokuwa kwa Sir. Andy Chande. Sio mke au mume ambaye atakukimbia ukifilisika au ukifilisiwa au ukishushwa cheo au ukifukuzwa kazi.

Wakati Sir. Andy Chande akiniambia haya, mke wake alikuwa ni mgonjwa na alikuwa anapata matibabu nchini Uingereza. Pamoja na umri wao mkubwa walipendana sana na kutiana moyo. Na mara nyingi nilipowatembelea niliona Sir. Andy Chande akimhudumia mke wake kwa hali na mali. Kipindi hicho pia Sir. Andy Chande naye hali yake ya kiafya haikuwa nzuri lakini hakuacha kufanya kazi. Alikuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali ya Uingereza na Canada. Sir. Andy Chande alikuwa rafiki mkubwa wa familia ya Malkia wa Uingereza-Qeen Elizabeth, Waziri mkuu wa Canada, na Marais wastaafu akiwemo Mh. Rais Ali Hassan Mwinyi, Mh. Rais Benjamin Mkapa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
II.Somo la pili ni kwamba ukiwa mfanyabiashara au mjasiriamali, usiweke mambo moyoni, utakufa. Sir Andy Chande na Mwalimu Nyerere walikuwa ni marafiki wakubwa. Lakini maamuzi ya kutaifisha biashara ya Sir. Andy Chande hayakufanywa na mwalimu kama "mtu binafsi" ingawa yeye alikuwa ni mkuu wa nchi. Yalifanywa na serikali. Iwe yalikuwa ni maamuzi mazuri au mabaya, Sir. Andy Chande aliyapokea na kuyaunga mkono. Urafiki wao uliendelea na yeye aliendelea na maisha kama vile hakuna lililotokea.

Leo ukimkopa rafiki yako hela akakuambia hana hela za kukusaidia au hawezi kukupa ana mipango na hela alizonazo, una "mdelete" mpaka kwenye simu yako, "unamblock" facebook, "unamunfollow twitter, instagram na youtube". Ukimpigia simu rafiki yako asipopokea mara 2 au mara 3, unatuma ujumbe mfupi; "acha ujinga pokea simu" hata hujui kama yuko hospitali-ICU kalazwa au bafuni anaoga.
Uko wapi ujasiri wa akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha leo? Iko wapi nidhamu ya akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha wakati huu? Sir. Andy Chande ananiambia wakati akiwa na Chande Mills, mama Maria Nyerere alikuwa akienda kiwandani kuchukua mabaki ya mahindi kwa sababu alikuwa anafuga. Akasema mama Maria alikuwa hataki akifika kiwandani apewe "priority" wengine wasubiri. Alikuwa anapanga foleni kama wanawake wengine. Hata yeye alipojaribu kumshawishi ahudumiwe kwanza alikataa. Vijana wa leo ambao ni viongozi jifunzeni kitu hapa kutoka kwa mama Maria Nyerere. Wake au waume zenu wajishushe. Wasitake kupewa "priority" kwa sababu tu ni wake au waume wa viongozi. Akienda benki au saloon, mwambie na yeye apange foleni kama wengine. Ndio watu wakubwa "great people" wanavyoishi. Hawana makuu ingawa ni wakuu.

2.Elvis Tables Musiba, Mwenyekiti wa zamani, TPSF

Nikiwa mtoto mdogo nilikuwa nasoma vitabu vya Elvis Tables Musiba. Moja kati ya vitabu ambavyo sitopata kuvisahau ni kitabu kinachoitwa NJAMA. Kitabu kile cha kipelelezi kilikuwa kina "character" anaitwa Willy Gamba. Ulikuwa ukisoma vitabu vya Elvis Tables Musiba ni kama unaangalia sinema ya Rambo. Nakumbuka nilipokinunua kitabu kile sikulala usingizi mpaka nilipokimaliza. Willy Gamba alikuwa mtu hatari sana ndani ya ile simulizi. Na Elvis Tables Musiba alikwa ni gwiji na mwandishi mkubwa na mzuri sana. Kila ninapokutana na rafiki yangu Eric James Shigongo ambaye pia ni mwandishi wa vitabu namkumbuka Elvis Tables Musiba. Siku moja nitamuuliza Eric James Shigongo alipata wapi hamasa ya kuandika vitabu. Inawezekana alisoma pia vitabu vya Elvis Tables Musiba.

Nilipokutana na Elvis Tables Musiba nilishangaa kugundua kuwa alikuwa ana kipaji kingine cha biashara na uongozi. Wakati tunachangisha fedha kwa ajili ya kongamano moja katika sekta ya utalii, aliniita ofisini kwake Mirambo House karibu na ofisi za benki ya dunia. Tulikuwa tunahitaji kuchangisha kama shilingi milioni 100. Elvis Tables Musiba akamuomba katibu muhtasi wake amletee simu. Sikuelewa simu ya nini kwenye kuchangisha fedha. Nilitegemea tungeshirikiana kuandika barua na "proposals" za kuchangisha fedha. Lakini haikuwa hivyo. Simu ilipoletwa akaanza kazi. Alikuwa anatuuliza mnataka kampuni gani ituchangie fedha. Kwa hiyo kazi yetu ikawa ni kutaja majina ya makampuni na yeye anapiga simu. Nilishangaa kuona Elvis Tables Musiba hahitaji tumpe namba za simu. Alinyanyua simu na kupiga kila tulipotaja kampuni. Na alipopiga hakuongea na katibu muhtasi au mkurugenzi wa fedha. Aliongea na CEO, Director General au Mwenyekiti wa "board". Namba alizipata wapi? sijui. Lakini ndani ya saa moja tulikuwa na shilingi milioni 60.

Nikagundiua huyu si mtu wa mchezo. Ana "connections" za ajabu. Nikamuuliza hebu niambie haya mambo unayafanyafanyaje mbona kwangu mageni? Akasema "reciprocate". Hili ni neno la kiingereza linalomaanisha "rudisha wema'. Elvis Tables Musiba aliwasaidia wengi kufika pale walipo ikiwa ni pamoja na CEOs. Kumbuka amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za kampuni nyingi. Wengi wa hawa CEOs ameshiriki kuwafanyia usahili kwa wao kuwa pale. Ndio maana haikumchukua muda kupata milioni 60. Alikuwa akiongea na watu ambao ni sehemu ya mchango wake katika maisha ya mafanikio yao. Hii ikanifanya nimdadisi zaidi. Nikamuuliza wewe ulianzaje biashara?

Akasema mtaji wangu wa biashara ulitokana na kuuza vitabu. Vitabu kama NJAMA ndivyo vilivyonitoa. Lakini nilipoanza biashara haikuwa rahisi. Mimi nilikuwa mtanzania wa kwanza "mswahili" kumiliki "Bureau De Change"-anasema Elvis Tables Musiba. Lakini siku moja nikiwa Musoma, nikasikia kwenye redio kwamba biashara yangu iko mikononi mwa serikali. Kidogo nipate kichaa. Lakini sikukata tamaa nikaanza upya. Akasema nyie vijana wa siku hizi mnalalamika mazingira magumu ya biashara. Nawashangaa sana. Tuulize sisi. Haikuwa rahisi kama mnavyofikiria. Kutoka kwa Elvis Tables Musiba nikajifunza yafuatayo;

I.Biashara ni mahusiano na watu. Elvis Tables Musiba kutumia saa moja kupata milioni 60 sio mchezo. Aliwekeza kwa watu. Leo hii kutafuta Tsh. 10,000/= ya luku ukikwama usiku wa manane na hauna salio kwenye simu ni shughuli pevu. Unaweza ukapiga namba zote kwenye simu yako usipate hata shilingi moja. Lakini Elvis Tables Musiba alitumia saa moja tu kupata shilingi milioni 60. Ina maana kila dakila alipata shilingi milioni 1.

II.Kipaji chako ndio mtaji wako. Badala ya kulalamika huna mtaji, angalia una kipaji gani? Elvis Tables Musiba alikuwa na kipaji cha kuandika hadithi. Ndicho kilichompa mtaji wa kuanzisha biashara. Eric James Shigongo aliwahi kuniambia pia, kwamba kipaji chake cha kuandika hadithi ndicho kilichomsaidia kuanzisha kampuni ya magazeti pendwa na kudumu mpaka leo (Global Publishers). Mifano ni mingi. Bila mpira Mbwana Samata angekuwa wapi? Bila mpira George Weah angekuwa Rais wa Liberia? badala ya kulalamika anza na kipaji chako? Mimi nilianza kwa kuandaa makongamano. Unaweza ukawa unaandaa harusi vizuri kila mtu anashangaa. Lakini bado unafikiri hicho siyo kipaji. Unafikiri kipaji ni "kuimba" tu! Mwenzako makongamano yalinipeleka mpaka Ikulu, yakanipa na mtaji wa kuanza.

III.Usikate tamaa. Elvis Tables Musiba anasema amefilisika mara nyingi katika maisha yake lakini alipambana akarudi tena kwenye mstari. Hakujinyonga. Baadhi ya biashara zake zilikwama. Lakini hakukata tamaa wala hakujenga chuki na watu. Kifupi, hakutafuta mchawi. Alianza upya na kusonga mbele. Alishirikiana na watu katika sekta binafsi na serikalini. Hiyo ndiyo roho ya "ujasiri wa mali" au "spirit" ya ujasiriamali au "entrepreneurship". Ni mlolongo wa kushindwa na kushinda, kushindwa na kushinda mpaka kieleweke.

3.Dr. Reginald Abraham Mengi, Mwenyekiti Mwanzilishi wa IPP Group na Mwenyekiti wa zamani wa CTI na TPSF

Dr. Reginald Abraham Mengi alinishirikisha mwanzoni kabisa wakati akianza kuandika kitabu chake cha "I Can, I Must, I Will". Nakumbuka alinipigia simu akasema njoo ofisini. Akaniambia nataka uwe sehemu ya team itakayonisaidia kukamilisha hili zoezi. Akaniomba nimtafutie vijana wengine wa kushirikliana na Prof. Msamali Nangoli, mwanazuoni wa Uganda aliyekuwa akiishi nchini Kenya, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho "No More Lies About Africa". Prof. Msalami Nangoli alikuwa rafiki mkubwa wa Nelson Mandela, mpigania Uhuru na Rais wa kwanza wa serikali ya kidemokrasia nchini Afrika ya kusini. Akiwa gerezani, Nelson Mandela alikuwa akisoma makala za Prof. Msamali Nangoli, makala ambazo zilipitishwa gerezani kiujanja kama kifungashio cha chapati. Kumbuka akiwa gerezani, Mandela hakuruhusiwa kusoma hata magazeti.

Ili kukamilisha zoezi la kuandika kitabu cha Dr. Reginald Abraham Mengi chini ya uongozi wa Prof. Msamali Nangoli, nilipewa "tapes" za hotuba za Dr. Reginald Abraham Mengi nyingi sana (mabox kwa mabox) ili nizipitie. Pia tuliwahoji watu wengi waliofanya kazi na Dr. Reginald Abraham Mengi. Bahati mbaya sana katikati ya safari ya kumsaidia Dr. Reginald Abraham Mengi kuandika kitabu chake, Prof. Msamali Nangoli akafariki dunia na Dr. Reginald Abraham Mengi akasitisha zoezi kwa muda. Baadaye akapata namna nyingine ya kumalizia kitabu chake kizuri.

Tulipokuwa na Prof. Msamali Nangoli tulimshawishi sana Dr. Reginald Abraham Mengi kubadilisha "title" au jina la kitabu lakini alikataa. Sisi tulipendekeza kitabu chake kiitwe; Dr. Reginald Abraham Mengi-How I became Rich; Financially, Morally, Materially. Lakini hakutaka hata kutusikiliza. Baadaye nilikuja kugundua tulikuwa tunakosea sana kumshawishi abadilishe jina la kitabu cha "I Must, I Can, I Will". Kwanini?

Kwa sababu siku moja nikiwa nyumbani kwake Kinondoni, nilimuuliza. Kwanini "I Must, I Can, I will"?. Akasema kwa sababu maisha ya biashara yana changamoto sana. Akaniuliza Paul, kwani unafikiri changamoto za biashara Tanzania ni zipi. Moyoni nikasema sasa Dr. ananiuliza swali gani "simple" namna hii. Au anataka kupima uwezo wangu wa kufikiri? Nikamwambia kubwa ni 3. Kwanza Mitaji au "Capital", Pili Masoko au "Markets", Tatu Rasilimali Watu au "Human resource". Akasema umekosa. Akasema kwanza Roho Mbaya, Pili Chuki, Tatu Wivu. Nilichoka kichwa. Akasema ili ufanikiwe lazima ukabiliane na hizi changamoto 3 nilizokutajia kisha uunganishe na hizo za mitaji, masoko na rasilimali watu. Ndio maana ya "I Must, I Can, I Will". Lazima udhamirie kutoka moyoni kupambana na changamoto.

Dr. Reginald Abraham Mengi akasema tulipotoka ni mbali kuliko tulipo. Akasema nakumbuka wakati nimeanzisha biashara ya maji ya kunywa, nilienda kwenye maonyesho ya sabasaba kuonyesha biashara mpya ya maji. Akasema watu waliokuwa wakipita kwenye banda langu walikuwa wananishangaa sana. Wanasema "huyu mchaga anapenda sana hela". Mpaka anatuuzia maji? Kweli leo hii nchi hii tumefikia hatua ya kuuziana maji? Dr. Reginald Abraham Mengi akasema kwa hiyo unaweza ukaona "Kilimanjato Pure Drinking Water" imeshamiri ukafikiri ni lelemama. Haikuwa rahisi. Bora hawa ambao wanaanza kuuza maji leo. Sisi tulioanza tulipata shida. Kwa sababu hakuna aliyezoea kuuziwa maji. Lakini Paul ukweli ni kwamba huwezi kushindana na mtu aliyeanza. Aliyekutangulia amekutangulia tu!

Dr. Reginald Abraham Mengi akaendelea kusema zaidi ya hapo kujenga sekta binafsi haikuwa rahisi. Kumbuka historia ya nchi hii toka kipindi cha wakoloni. Toka enzi hizo biashara zilikuwa kwa matabaka. Wa kwanza pale juu ni wazungu, wa pili waarabu na wa tatu wahindi. Sisi wazawa wa "kiswahili" tulikuwa hatufikiriwi kabisa kuwa "matajiri". Kuna wakati nilinunua Mercedez Benz lakini nilikuwa naogopa kuliendesha. Kwa sababu mifumo ya kiuchumi ilikwishakamatwa na matabaka mengine. Kwahiyo unavyoona sekta binafsi imefika hapa ni mapambano kwelikweli. Mswahili kumiliki kiwanda miaka ya sabini na themanini na Mswahili kuwa kiongozi wa sekta binafsi ambayo haina waswahili wengi ulikuwa ni mtihani ambao ilibidi kuushinda. Haikuwa kazi rahisi. Mimi Paul Mashauri nimeona na kusimuliwa mengi pengine nahitaji kitabu kizima kuzungumza ya Dr. Reginald Abraham Mengi. Lakini kuna mafundisho machache nataka niyataje hapa;

I.Biashara si lelemama. Changamoto ni nyingi kuliko fursa. Lazima ubadilishe hizo changamoto ziwe fursa ili fursa ziwe nyingi kuliko changamoto. Hii haiwezekani pasipo kuwa na moyo mgumu "a iron heart". Kama unataka uache kazi uanze biashara ukifikiri ni mteremko jifikirie tena na tena na tena. Nakumbuka wakati nimemualika Dr. Reginald Abraham Mengi kuongea na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alirudia hilo. Akasema; "safari ya mafanikio ni kama pambano la ngumi. Kuna makonde ya kuyakwepa, kuna makonde ya kuyazuia ambayo yakikupata yanasambaratisha uso wako au kukuua kabisa lakini kuna wakati ambao lazima ujibu mapigo ili ushinde pambano. Mh. Jokate Mwegelo, DC, Kisarawe, kipindi hicho akiwa chuoni, alikuwa "Moderator" katika tukio hilo. Anaweza akayakumbuka maneno haya.

II.Usiogope kuanzisha njia pasipo na njia. Usiogope kuwa wa kwanza kufanya jambo ambalo wengine wanasita kufanya. Maana yake ni kwamba "be the pioneer". Dunia tunayoishi iko hapa ilipo sababu ya "pioneers". Christopher Columbus angeogopa kusafiri kutoka Spain pengine America (New Land) ingechelewa sana kutambulika katika uso wa dunia. Hata wewe usiwe mtu wa kusubiri wenzako waanze. "Legends" sio wale wanao "copy na kupaste" Legends ni waanzilishi. Kuanza sio lazima iwe ni kwenye biashara. Hata kwenye familia yako unaweza ukawa wa kwanza kuwa "mbunge".

4.Mr. Ali Mfuruki, Aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table

TRBN (Tanzania Responsible Business Network) ilipoanza niliombwa na Partner wa KPMG Ketan Patel pamoja na Partner wa Deloitte Joe Eshun niwe "Moderator" katika sherehe za uzinduzi wa TRBN pale Serena Hotel. Tulikuwa na CEOs zaidi ya 300. Mgeni rasmi alikuwa ni Mr. Ali Mfuruki, Mwenyekiti wa CEO Round Table. Baada ya ufunguzi nilikuwa na muda wa kutosha wa kuongea na Mr. Ali Mfuruki. Jambo moja Mr. Ali Mfuruki aliniambia ambalo sitolisahau ni kwamba lazima uwe na msimamo na lazima ukubali kupoteza baadhi ya vitu ikiwa ni pamoja na fedha kusimamia unayoyaamini. Akaniambia nyie vijana sasa hivi ndio mmekuwa mameneja kwenye makampuni na viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali. Sasa wakati mwingine unakutana na kijana kwenye kampuni ambaye amepewa mamlaka, kijana ambaye unaweza kumzaa anataka akuzungushe, akunyanyase ili umpigie magoti. Mimi siwezi. Bora nikose hela kuliko kushusha heshima yangu.

Wapo vijana ambao wanamsikia Mr. Ali Mfuruki leo hii lakini hawajakutana na Mr. Ali Mfuruki na kuzungumza naye ana kwa ana. Sijui umesikia nini juu yake lakini Mr. Ali Mfuruki alikuwa na msimamo wa kipekee. Alikuwa anafikiria vizuri sana sio katika biashara zake tu hata kwa nchi. Ndio maana kifo chake kimetushtua kama Taifa. Unaweza ukawa unafikiria vizuri lakini kwa mambo yako binafsi na familia yako. Hilo ni jambo zuri na ndiyo jambo la pili baada ya kumfikiria Mungu. Lakini unapojiongeza na kufikiria Taifa na watu wengine ndani ya Taifa unakuwa wa tofauti zaidi. Ndivyo alivyokuwa Mr. Ali Mfuruki. 

Kuna siku nilikutana naye nikamuuliza Mr. Ali Mfuruki lini unaandika kitabu? Akaniambia nimeanza kuandika. Siku niliposikia ametoa kitabu, nikawahi bookshop Mlimani City kununua. Lakini baada ya kusoma kile kitabu nikagundua nilichofikiria kuwa kitakuwepo kwenye kitabu sicho. Mr. Ali Mfuruki hakuwa ameandika kitabu kuhusu yeye na mke wake na watoto wake. Alikuwa ameandika kitabu kuhusu uchumi wa viwanda. Huyo ndio Mr. Ali Mfuruki. Ndiyo sababu alidumu kama Mwenyekiti wa CEO Round Table kwa miaka mingi. Sio kwamba alipenda kuhodhi madaraka. Alikuwa ana uwezo kichwani. Na vyeo vingi alikuwa anakataa. Na pale alipokubali alijitoa kwa dhati. Amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za Mwananchi Communications Ltd, amekuwa kwenye "board" ya Geita Gold Miming (GGM), Mwenyekiti wa "board" ya Vodacom nk. Waulize waliofanya kazi naye. Kile kilikuwa kichwa kingine.

Wakati fulani nilialikwa katika uzinduzi wa "Private Equity Fund" moja pale Golden Tulip Hotel. Alikuwepo Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waheshimiwa mawaziri na wafanya biashara. Mr. Ali Mfuruki alikuwa miongoni mwa waalikwa pia. Siku ile Mr. Ali Mfuruki aliongea kitu kikubwa sana. Akasema, wakati Marekani inataka kwenda mwezini miaka ya 60. Rais wa nchi hiyo J.F. Keneddy alitangaza kwamba Mmarekani yoyote atakayekuja na wazo au "idea" au "ubunifu" au "teknolojia" ambayo itaisaidia Taifa la Marekani kufika mwezini au kufika hatua moja mbele katika ndoto ya nchi kwenda mwezini, serikali ya Marekani italipa fedha kununua hilo wazo au huo ubunifu. Mr. Ali Mfuruki akasema; ili sisi kama Taifa tuweze kwenda mbele lazima kuwe na mbinu za kujenga "uhitaji" au "demand" ya ugunduzi na ubunifu "Creativity and innovation" . Akasema "kufikiria" ni kazi. Kugundua kitu ni gharama. Lazima ufanye "research" au "utafiti". Tukitaka watu wetu wawe wabunifu lazima tutengeneze mbinu za kumfikirisha mtu akijua kabisa kuwa nguvu zake hazitoenda bure.

Mr. Ali Mfuruki alikuwa haongei "nadharia". Sijawahi kumsikia akiongea "pumba". Kwa historia yake yeye ni mhandisi au "engineer" kwa lugha ya kiingereza. Mr. Ali Mfuruki Alipotoka nchini Ujerumani aliposomea, kuja nyumbani Tanzania kufanya biashara, aliona kuna fursa, kuna "demand" au "uhitaji" wa bidhaa za teknolojia hasa kompyuta. Kipindi hiki nchi ilikuwa imefunguka na serikali pamoja na makampuni binafsi yalikuwa yanabadilisha teknolojia kutoka katika mfumo wa kizamani wa "fax" na "typewriters" kuja kwenye matumizi ya kompyuta. Ndivyo kampuni yake ya Infotech Technologies Ilivyoanza. Huwezi kuzungumzia Teknolojia Tanzania pasipo kumzungumzia Mr. Ali Mfuruki ingawa amekuwa na biashara nyingi zaidi ya hiyo. Yeye ni baba katika eneo hili la TEHAMA hapa Tanzania pamoja na kwamba unapozungumzia ujio wa WoolWorth unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki na hata unapozungumzia ujio wa Zuku unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki. Nini cha kujifunza hapa;

I.Tunaishi katika dunia ya ubepari au "capitalism". Dunia ya "ubepari" na dunia ya ujamaa au "socialism" ni dunia 2 tofauti. Katika dunia ya ubepari mtu anaweza akakudhalilisha kwa sababu amekupa fursa. Mtu anaweza akataka umuabudu na umpigie magoti kwa sababu anakupa biashara. Mtu anaweza akakuvunjia heshima mbela ya mke na watoto wako kwa sababu bila yeye huwezi kupata mshahara. Haya ndiyo mambo ambayo Mr. Ali Mfuruki aliniambia hayataki. Akasema bora niwe "broke" au "masikini" kuliko kudhaliliswa. Alikuwa na msimamo.

II.Vijana wengi wanatamani kuheshimiwa kama Mr. Ali Mfuruki. Lakini hawajui kuwa heshima haiji kwenye kikombe cha chai. Inajengwa kwa jasho kubwa. Mimi Paul Mashauri ambaye nimekaa na hawa watu najua. Mimi Paul Mashauri ambaye nimetumika sana kwenye sekta binafsi nijaua. Ni kazi ngumu na inataka moyo. Kumbuka Mr. Ali Mfuruki ni mfanyabiashara. Ana biashara zinazomuangalia yeye. Na bado aangalie ya nchi. Sio jambo dogo. Kumbuka akifanya hivyo waziri ni sawa kwa sababu mwisho wa mwezi analipwa mshahara. Ni sehemu ya "job description". Lakini unapokuwa Mwenyekiti wa hizi taasisi za sekta binafsi unatumia akili zako na nguzu zako kama msaada na mchango kwa Taifa. Ingawa sina uhakika kama ukifilisika unapewa tena mtaji na Taifa. Ndio maana nasema inataka moyo. Ni vijana wangapi wako tayari kufanya hivyo? Kuacha biashara yako na watoto wako kuhangaikia ya wengine?

III.Mr. Ali Mfuruki alikuwa anafikiri vizuri "thinker" kwa sababu alikuwa anatumia muda mrefu sana kukutana na watu wa haiba tofauti, kusoma, kusafiri kupata "exposure" nk. Hakuna mtu alikuwa anamlipia tiketi ya ndege kusafiri. Alikuwa anajilipia mwenyewe. Leo unataka kuwa kama Mr. Ali Mfuruki unashinda instagram unasoma udaku. Hautaki kwenda kwenye kongamano lolote zaidi ya matamasha ya muziki na comedy. Kila tasnia ina utamaduni wake. Ukitaka kuketi katikati ya wakuu lazima ufikirie kama wakuu. Mr. Ali Mfuruki aliitwa na wakuu, alikaa meza moja na wakuu akiwemo Barack Obama, Rais Mstaafu wa Marekani sio kwa sababu alikuwa "handsome" mwenye "six packs" tumboni kuliko watanzania wote. La hasha! Alikuwa na madini adimu kichwani.

5.Ruge Mutahaba, Aliyekuwa Mkurugenzi au "Director" wa programs, Clouds Media Group

Niliposikia amefariki, nilisikitika sana. Kwa sababu miezi michache iliyopita kabla ya taarifa hizo nilimpigia simu. Nikamwambia kaka Ruge kuna kongamano la vijana na wazazi tunaandaa naomba uje uzungumze hasa na vijana. Akajibu akasema "count me in". Lakini miezi kadhaa nyuma, Ruge mwenyewe alinipigia simu. Akasema Paul wewe na mimi kama "speakers" lazima tufanye mambo ya kusaidia nchi. Akaniambia hebu andika "andiko" au "proposal" ya kusaidia Taifa letu kwa kutumia "speakers" kuhamasisha fikra mbadala hasa katika mambo ya msingi ya kitaifa. Nilikesha usiku ule nikaandika ile "proposal" na nikamtumia Ruge kwa email. Ile "propoal" niliipa jina la "Speakers Without Boarders".

Wengi walimfahamu Ruge Mutahaba kwenye "media" na "muziki" lakini Ruge Mutahaba alikuwa ni zaidi ya media na muziki. Ndio sababu alipofariki hata Rais wa nchi alitoa neno. Uwezo wa Ruge Mutahaba ulikuwa hauna shaka. Ubishi wake kwa kile alichokiamini ulikuwa si wa kitoto. Na utayari wake kujitoa kwa ajili ya wengine hauelezeki. Siweki chumvi na mimi sio mnafiki wala sisemi haya yote kwa sababu hayupo tena duniani. Niliyasema haya hata alipokuwa hai. Niliyasema ya Mr. Ali Mfuruki wiki iliyopita ambayo ni wiki moja kabla hajafariki. Sio wote wana moyo wa kusema nani aliwasaidia katika maisha yao lakini mimi nasema kwa sababu duniani hakuna mtu anayetoka bila msaada wa mtu mwingine. Hakuna kitu kama "self-made". Kusaidiwa sio lazima iwe pesa .Hata mwalimu wa shule ya msingi alikusaidia kujua kusoma na kuandika. Leo unasemaje kuwa wewe ni "self-made millionaire"? Humkumbuki hata mkeo au mumeo aliyekutia moyo ulipokata tamaa?

Ruge Mutahaba alinisaidia sana mimi na vijana wengine wengi. Yeye ndiye aliyenitambulisha kwa Azim Jamal aliye kuja kuwa rafiki yangu mkubwa katika "motivational speaking". Huyu ni mnenaji au "speaker", mwandishi wa vitabu au "author", mtaalam wa menejimenti au "consultant" na mfanyabiashara aliyebobea. Azim Jamal amefanya kazi na kuandika vitabu pamoja na wataalam na wanenaji "speakers" wakubwa duniani kama Brian Tracy. Kumlipa Azim Jamal kuzungumza kwenye tukio lako sio chini ya dola za Kimarekani milioni 10 au fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 20 ndani ya siku moja. Lakini kwa sababu ya urafiki na heshima ya Ruge Mutahaba, Azim Jamal alikuja kuzungumza kwenye tukio nililoandaa bila kulipwa hata shilingi moja. Baada ya hapo tulifanya kazi nyingi sana na Azim Jamal.
Pili wakati tunaanzisha gazeti la Familia, yeye ndiye aliyenipa matangazo ya bure. Alisema wewe unafanya kazi kubwa sana kuhamasisha vijana. Hakuna anayekulipa kwa kujitolea kwako. Malipo yako yatakuwa matangazo nitakayokupa Clouds FM. Kwa moyo ulionao ukitoka wewe, wengi zaidi watatoka. Ruge Mutahaba alilipa gharama ya kazi yangu kwa vijana. Si hayo tu, yeye pamoja na Joseph Kusaga ndio walionipa studio za Clouds TV kutengeneza sinema yangu iitwayo "Maisha Ni Siasa". Angalia sinema hii yote Youtube. Sio mimi tu, wako wengi aliowasaidia. Hata serikali inatambua nini Ruge Mutahaba alifanya katika nchi hii. Uzoefu wangu wa Ruge Mutahaba tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum ulinidhihirishia uwezo wake wa kuangalia mambo kwa jicho la tatu. Ndio sababu alikuwa mbunifu sana. Kila tulipokuwa na kikao, Ruge Mutahaba hakuwa wa kwanza kuongea. Lakini alipopata nafasi ya kuongea, aliipindua pindua mada na wote tukaiona hoja husika kwa namna ambayo hatukuiona hapo kabla.

Kila nikimkumbuka Ruge Mutahaba nakumbuka mmoja kati ya vijana ambao walijiongeza. Ungeniuliza ni akina nani wanafanya sana kazi bila kuchoka ningekuambia ni Ruge Mutahaba. Binafsi sijui alikuwa anapumzika saa ngapi. Unakutana na kijana anasema anataka kuwa kama Ruge Mutahaba na bado analala saa 2 usiku na anaamka saa 2 asubuhi. Unataka kuwa kama Ruge yupi? Sijaona mimi mtu anafanya vitu vikubwa vya kitaifa na analala usingizi wa pono. Uliza wasaidizi wa Rais kama wanalala? Kama unajua huwezi kufanya kazi kwa bidii kubali kuwa wa kawaida. Usifikiri nazungumzia "utajiri". Hilo ni suala lingine. Unaweza usiwe tajiri lakini bado ukawa si wa kawaida. Akina Dr. Martin Luther King Jr. na Nelson Mandela hawakuwa matajiri lakini pia hawakuwa wa kawaida. Lazima utofautishe kati ya kuwa "rich" au "tajiri" na kuwa "great". Hapa sizungumzii utajiri nazungumzia "greatness". Hata mwizi anaweka kuwa "tajiri" lakini inahitaji "akili nzuri", "kujitoa kwa wengine" na "kujituma" ili uwe "great" Vitu vinavyobadilisha jamii havihitaji mtu mzembe. Kama kusoma tu hii makala mpaka hapa umeshachoka unatamani iishe utaweza kuwa kama Ruge Mutahaba? Kuna mambo ya msingi ya kujifunza kutoka kwa Ruge Mutahaba;

I.Ubishi. Hakuna kitu kinakuja kirahisi. Mafanikio sio muujiza, yanafanyiwa kazi. Usifikiri Ruge Mutahaba alifika pale alipofika sababu ya "Clouds" kama media. Hatukatai ukweli kwamba alikuwa ni mmoja wa watu walioijenga Clouds Media Group. Kwanza, ulikuwa ukisikia Clouds FM iko hewani, sura mbili zinakuja kichwani kwako; Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Hata isingekuwa "media" Ruge Mutahaba angefanya vitu vikubwa tu kwa sababu alikuwa ni "mbishi" asiyekubali kushindwa. Miaka 3 iliyopita nilimualika Ruge Mutahaba katika kongamano la Vijana lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) pale Serena Hotel. Kongamano lilikuwa chini ya mradi wa kutoa mitaji kwa mawazo bora ya biashara kwa vijana "Ajira Yangu" Project ambayo niliisimamia.

II.Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Ruge Mutahaba akasema "ukija kwangu na wazo au "idea" yako nakurudisha mara 3 au mara 4. Sio kwa sababu wazo lako ni baya. Nataka nione kama kweli wewe ni mbishi na uko tayari kupambana mpaka wazo lako lipate maisha. Vijana wa leo hawako hivyo. Wanataka mambo ya chapchap kama mabando ya internet. Hawana uthubutu. Wanaamini kwenye michongo na kushikwa mkono. Wanakata tamaa mapema. Hata wakija kwako uwe "mentor" wao wanakuja "kifursa zaidi". Wanataka uwe "mentor" wao na hapohapo uwape "hela". Hiyo sio "mentorship" hiyo ni "sponsorship". Sasa hatujui unataka nini? Unataka "mentorship" au "sponsorship"?Hawajui kuwa hata akina Ruge Mutahaba walipitia vikwazo lakini walikuwa wabishi.

III.Uwezo wa kufanya lolote unalolitaka. Nilisema hapo mwanzo kwamba wengi wanamjua Ruge Mutahaba kwa sababu ya "media", "muziki" na "matamasha". Ruge Mutahaba alikuwa zaidi ya hapo. Ruge Mutahaba alikuwa pia anandaa sinema. Nikiwa chuo kikuu Ruge Mutahaba alirekodi sinema inaitwa "Kelele". Yeye mwenyewe binafsi alikuwa nyuma ya kamera kuhakikisha sinema inarekodiwa vizuri. Ingawa sikumbuki kama aliwahi kuitoa ile sinema lakini nilichojifunza ni kwamba alijua anaweza kufanya kitu zaidi ya kimoja. Kuna mikakati mingi sana na miradi mikubwa ya kitaifa mbayo Ruge Mutahaba alikuwa nyuma yake ingawa hakuonekana mstari wa mbele. Huyo ndiyo Ruge Mutahaba niliyemfahamu mimi. 

Leo hii unatamani siku moja upewe heshima aliyopewa Ruge Mutahaba lakini hujiulizi nini kitu cha tofauti unafanya? Zaidi ya kutoka bwenini, kwenda darasani kisha kwenda bwaloni kula ubwabwa nini kingine unafanya? Zaidi ya kutoka kazini na kwenda baa au kwenye harusi kula pilau, nini kingine unafanya?Unawezaje kuwa kama Ruge au zaidi ya Ruge kwa maisha ya pembe tatu?Unawezaje kufikia ndoto zako kwa maisha ya pembe tatu? Hata kama umeajiriwa. Usiku unafanya nini?

Tanzania imepoteza watu muhimu sana katika muda mfupi sana. Niliyoyataja hapa kwa hawa "generals" ni machache sana ukilinganisha na niliyoyafahamu na nisiyoyafahamu. Hawa watu walitumia vyema uwepo wao hapa duniani na uwepo wao katika hii nchi kuleta utofauti. Ni "generals" walioondoka lakini nchi bado ipo. Pamoja na utofauti wao, hawa wote wanasifa zinazofanana. Pamoja na mapungufu yao wote hawa wana faida zinazofanana.

1. Waliwekeza katika maarifa
 2. Waliwekeza katika watu 3. Walitumia karama, vipaji na elimu zao kuleta utofauti na kulitumikia Taifa 4. Hawakuwa wepesi kukata tamaa hata walipopitia magumu katika ngazi za familia zao, maisha yao binafsi, biashara zao na kazi za kitaifa 5. Wameacha alama katika nchi hii, alama ambayo itaendelea kuishi ingawa wao hatunao tena. Amani ya bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nao, familia zao, ndugu zao, marafiki zao na watanzania wote kwa ujumla.  

Makala hii imeandikwa na Paul R.K Mashauri@hakimiliki 2019. Hairuhusiwi kuchapisha Makala hii au sehemu ya Makala hii pasipo idhini ya mwandishi. Wasiliana na mwandishi kupitia ceo@masterclassworldwide.co.tz

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 58 YA UHURU NA 57 YA JAMHURI UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri leo Jumatatu December 9, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli akipokea heshima baada ya kuwasili katika Uwanja wa CCMKirumba jijini Mwanza kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 yaJamhuri leo Jumatatu December 9, 2019.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati waSherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri zilizoongozwa na RaisDkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu December 9, 2019.
Kikosi cha Makomando wa JWTZ wakioneshaumahiri wao wa kufanya zoezi la uokozi katika mfano wa Tukio laUtekaji.
Kikundi cha Sungusungu cha kutoka Kwimbamkoani Mwanza kikitumbuiza katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru waTanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza.
Baadhi ya Mawaziri wakiimba na kucheza wimbo wa Harmonize wakati wa sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba jijjini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri leo
Jumatatu December 9, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza. 
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe
zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

Wameondoka Majenerali wa Sekta Binafsi Tanzania

0
0
Na Paul R.K Mashauri

 Pichani juu kushoto ni Elvis Tables Musiba, Ali Mufuruki na pichani chini kulia ni Sir. Andy Chande, Ruge Mutahaba pamoja na Dkt. Reginald Mengi enzi za uhai wao.

Miaka michache iliyopita tulimpoteza Elvis Tables Musiba aliyekuwa Mwenyekiti wa TPSF (Tanzania Private Sector Foundation). Mwaka jana tukampoteza Sir. Andy Chande aliyekuwa kiongozi wa sekta binafsi toka enzi za ukoloni. Mwaka huu tumewapoteza wafanyabiashara 3 wakubwa ambao walikuwa viongozi na watu muhimu sana kwa sekta binafsi Tanzania. Dr. Reginald Abraham Mengi aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI (Confederation of Tanzania Industries) na TPSF, Ruge Mutahaba aliyekuwa mjumbe wa MOAT (Media Owners Association of Tanzania) na mjumbe wa TRA Stakeholders Forum na jana tumempoteza Mr. Ali Mfuruki aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table.

Vijana wengi wamewaona na kuwasikia hawa watu "the generals" lakini wengi hawajui historia ya sekta binafsi Tanzania na mchango wao katika kuifikisha sekta binafsi hapo ilipo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoeleza japo kwa kifupi mchango wao kwa sababu kwa namna moja au nyingine wote hawa kuanzia Sir. Andy Chande, Elvis Tables Musiba, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mr. Ali Mfuruki na Ruge Mutahaba nimefanya nao kazi za sekta binafsi kwa karibu sana.

Sir. Andy Chande nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa "boards" mbalimbali za taasisi kama MOI, IMTU, TRL nk. Na pia alikuwa mshauri katika "board" ya kampuni yangu mwenyewe. Ni bahati mbaya sana kwamba mwezi moja kabla ya kifo chake, mimi na Sir. Andy Chande tulipanga kukutana ili mimi Paul Mashauri nimfanyie "interview" ya namna sekta binafsi ya nchi hii ilivyokuwa kabla na baada ya uhuru. "Interview" ile ilikuwa itumike kama kipindi cha TV ili wengi zaidi wanufaike na uzoefu aliokuwa nao. Bahati mbaya Sir. Andy Chande alifariki kabla hatujakamilisha jambo hilo jema.

Elvis Tables Musiba nilifanya naye kazi akiwa Mwenyekiti wa TPSF na mimi nikiwa mjumbe wa kamati mbalimbali za sekta binafsi Tanzania. Tulisaidiana kuchangisha fedha"fundraising" kwa shughuli mbalimbali za kitaifa, na alitumia wakati huo kunisimulia mambo mengi sana.

Mr. Ali Mfuruki nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa CEO Round Table na mlezi wa TRBN (Tanzania Responsible Business Network) chini ya UN Business Compact na mimi nikiwa ni mjumbe wa "secretariat" ya TRBN.

Dr. Reginald Abraham Mengi nilifanya naye kazi yeye akiwa ni Mwenyekiti wa CTI na mimi nikiwa ni mjumbe wa kamati ya SME ya CTI. Na Ruge Mutahaba nilifanya naye kazi wote tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum.

Mara nyingi wote hawa walitumia muda wao mwingi kunisimulia vitu vingi sana wao wakiwa wakubwa kwangu kiumri na mimi nikiwa mdogo sana kwao. Wakati huo nilikuwa sijui kwanini wananiambia mambo yote hayo ya sekta binafsi kwa sababu kwanza nilikuwa mdogo sana na pili sikuwa na nafasi wala heshima kubwa kama walizokuwa nazo wao lakini jana baada ya kupata taarifa za kifo cha Mr. Ali Mfuruki nikagundua pengine walitaka siku moja niyasimulie hayo ili kizazi cha leo kipate kuelewa.

Wafanyabishara vijana, viongozi vijana katika serikali na wajasiriamali vijana wanaochipukia, lazima waelezwe kwamba historia ya sekta binafsi Tanzania haiwezi kuelezwa pasipo majina ya hawa wote niliowataja hapo juu. Lakini pia wapo wengine ambao wameshatutoka na wengine ambao bado wapo hai. Pia sitatenda haki nisipowataja japo baadhi yao. Hao ni pamoja na marehemu Mzee Mwakitwange, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mwapachu, Elvis Tables Musiba, Mzee Iddi Simba na wengine ambao sikupata kuwafahamu. Hawa walikuwa waanzilishi wa TCCIA mwishoni mwa miaka ya 80 kabla ya baadhi yao kuondoka TCCIA na kuanzisha CTI. Kwanini waliondoka na TCCIA kuanzisha CTI? Hiyo ni mada nyingine ambayo inahitaji makala tofauti na hii.

Ukiondoa Mzee Mwakitwange ambaye alitangulia mbele za haki zamani kidogo, wengine wote akiwemo Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mapachu na Mzee Iddi Simba nimepata kufanya nao kazi na kupata simulizi zao. Mzee Anorld Kileo ambaye alikuwa ni CEO wa TBL kwa muda mrefu sana na kiongozi wa TPSF yeye aliniita ofisini kwake na kunikalisha chini kwa masaa zaidi ya 3 akinieleza sekta binafsi ilipotoka na namna walivyopambana kuifikisha hapo ilipo. Ukurasa huu hautoshi kuandika historia yote ya ujasiriamali Tanzania ambayo vijana wengi wangependa kuijua lakini Dr. Juma Mwapachu aliandika kitabu chenye historia hii vizuri sana. Mimi nitagusia yale niliyoelezwa na hawa "generals" wa sekta binafsi Tanzania kwa kifupi sana.

1.     Sir. Andy Chande, Mwanzilishi, Chande Mills

Sir Andy Chande alinieleza kwamba baada ya Uhuru wa nchi hii, Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere alitaka kumteua kwenye baraza la mawaziri. Lakini akamwambia Mwalimu Nyerere, naomba uniache kwenye sekta binafsi. Mwalimu Nyerere aliheshimu mawazo ya Sir. Andy Chande. Lakini Mwalimu Nyerere akaamua kumteua Sir. Andy Chande kuwa mjumbe wa kamati ya uchumi na maendeleo mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru. Kwa vijana wasiomfahamu Sir. Andy Chande huyu ndiye aliyekuwa mfanyabiashara wa kitanzania mwenye nguvu kubwa za kiuchumi wakati wa ukoloni na hata baada ya kupata uhuru. Aliendesha biashara ya kifamilia iliyoitwa Chande Mills ambayo baadaye ilitaifishwa na serikali mwaka 1967 wakati wa "Nationalization" na kuwa NMC (National Milling Corporation) kiwanda ambacho baadaye kilikuja kununuliwa na Bakhresa.

Sir. Andy Chande ndiye aliyekuwa mtanzania mwenye asili ya kiasia kuanza kutoa misaada kwa watu (philanthropism) kuanzia wakati wa uhuru mpaka alipofariki dunia miaka michache iliyopita. Kilichonishangaza kuhusu Sir. Andy Chande ni kwamba hata baada ya serikali kutaifisha biashara yake, bado aliendelea kutumia mtandao wake wa watu "network" akili na maarifa yake kuitumikia nchi. Sir. Andy Chande ananisimulia anasema, baada ya serikali kutaifisha biashara yake, Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu, akamuuliza; Rafiki yangu Chande; unataka kwenda wapi baada ya serikali kuchukua biashara yako kwa manufaa ya umma?

Sir. Andy Chande akamuambia Mwalimu Nyerere; "sina pa kwenda". Mwalimu akamuambia "sasa kuanzia leo, wewe ndio utakuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hii mpya inayomilikiwa na wananchi wote wa Tanzania. Sir. Andy Chande akajibu " sawa Mh. Rais". Na ikawa hivyo. Ingekuwa sisi vijana wa leo, rafiki yako ndiyo kiongozi wa nchi au DC au Mkuu wa mkoa au Waziri, anakufahamisha maamuzi ya serikali, tungeleta urafiki na mambo binafsi kwenye mambo ya nchi. Lakini Sir. Andy Chande alikuwa anajua kutofautisha ni wakati gani Nyerere, "rafiki" yake anaongea na ni wakati gani Nyerere, "Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu" anaongea. Alikuwa anajua mipaka yake.

Kutokana na uwezo wa Sir. Andy Chande, Mwalimu Nyerere alimpa uenyekiti wa "boards" nyingi sana ikiwa ni pamoja na TRL, ATC nk. Pia alikuwa Mwenyekiti wa "board" ya Kioo Ltd, Shaaban Robert Secondary School, IST, Barclays bank, Taasisi ya walemavu buguruni nk. Siwezi kuzimaliza zote ni nyingi mno.

Nilikuwa nyumbani kwake Upanga alipokuwa akisimulia haya. Nikamuuliza sasa uliwezaje kukubali kuwa Mwenyekiti wa "board" ya kampuni ambayo umeihangaikia miaka mingi na sasa si yako tena. Akasema mke wangu alinitia sana moyo. Lakini pili kwenye biashara usiweke mambo moyoni. Ukiweka mambo moyoni utakufa. Moyoni nikajisemea; Huyu kampuni yake aliyoisotea miaka mingi imechukuliwa. Tena siyo kampuni yenye mapato ya shilingi milioni 10 au bilioni moja. Unazungumzia mabilioni ya shilingi. Lakini bado maisha yakaendelea. Wewe umepoteza mteja mmoja unataka kufunga biashara. Kwanini? Hayo ni masomo ambayo nataka vijana wengi wayashike, kwamba;

      I.          Mke au mume wako ana mchango mkubwa sana katika maisha yako ya uongozi, biashara au ujasiriamali. Unapooa au kuolewa lazima uangalie mtu ambaye atakutia moyo wakati ukipitia changamoto za maisha kama ilivyokuwa kwa Sir. Andy Chande. Sio mke au mume ambaye atakukimbia ukifilisika au ukifilisiwa au ukishushwa cheo au ukifukuzwa kazi.

Wakati Sir. Andy Chande akiniambia haya, mke wake alikuwa ni mgonjwa na alikuwa anapata matibabu nchini Uingereza. Pamoja na umri wao mkubwa walipendana sana na kutiana moyo. Na mara nyingi nilipowatembelea niliona Sir. Andy Chande akimhudumia mke wake kwa hali na mali. Kipindi hicho pia Sir. Andy Chande naye hali yake ya kiafya haikuwa nzuri lakini hakuacha kufanya kazi. Alikuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali ya Uingereza na Canada. Sir. Andy Chande alikuwa rafiki mkubwa wa familia ya Malkia wa Uingereza-Qeen Elizabeth, Waziri mkuu wa Canada, na Marais wastaafu akiwemo Mh. Rais Ali Hassan Mwinyi, Mh. Rais Benjamin Mkapa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

    II.          Somo la pili ni kwamba ukiwa mfanyabiashara au mjasiriamali, usiweke mambo moyoni, utakufa. Sir Andy Chande na Mwalimu Nyerere walikuwa ni marafiki wakubwa. Lakini maamuzi ya kutaifisha biashara ya Sir. Andy Chande hayakufanywa na mwalimu kama "mtu binafsi" ingawa yeye alikuwa ni mkuu wa nchi. Yalifanywa na serikali. Iwe yalikuwa ni maamuzi mazuri au mabaya, Sir. Andy Chande aliyapokea na kuyaunga mkono. Urafiki wao uliendelea na yeye aliendelea na maisha kama vile hakuna lililotokea.

Leo ukimkopa rafiki yako hela akakuambia hana hela za kukusaidia au hawezi kukupa ana mipango na hela alizonazo, una "mdelete" mpaka kwenye simu yako, "unamblock" facebook, "unamunfollow twitter, instagram na youtube". Ukimpigia simu rafiki yako asipopokea mara 2 au mara 3, unatuma ujumbe mfupi; "acha ujinga pokea simu" hata hujui kama yuko hospitali-ICU kalazwa au bafuni anaoga.
Uko wapi ujasiri wa akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha leo? Iko wapi nidhamu ya akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha wakati huu? Sir. Andy Chande ananiambia wakati akiwa na Chande Mills, mama Maria Nyerere alikuwa akienda kiwandani kuchukua mabaki ya mahindi kwa sababu alikuwa anafuga. Akasema mama Maria alikuwa hataki akifika kiwandani apewe "priority" wengine wasubiri. Alikuwa anapanga foleni kama wanawake wengine. Hata yeye alipojaribu kumshawishi ahudumiwe kwanza alikataa. Vijana wa leo ambao ni viongozi jifunzeni kitu hapa kutoka kwa mama Maria Nyerere. Wake au waume zenu wajishushe. Wasitake kupewa "priority" kwa sababu tu ni wake au waume wa viongozi. Akienda benki au saloon, mwambie na yeye apange foleni kama wengine. Ndio watu wakubwa "great people" wanavyoishi. Hawana makuu ingawa ni wakuu.

2.     Elvis Tables Musiba, Mwenyekiti wa zamani, TPSF

Nikiwa mtoto mdogo nilikuwa nasoma vitabu vya Elvis Tables Musiba. Moja kati ya vitabu ambavyo sitopata kuvisahau ni kitabu kinachoitwa NJAMA. Kitabu kile cha kipelelezi kilikuwa kina "character" anaitwa Willy Gamba. Ulikuwa ukisoma vitabu vya Elvis Tables Musiba ni kama unaangalia sinema ya Rambo. Nakumbuka nilipokinunua kitabu kile sikulala usingizi mpaka nilipokimaliza. Willy Gamba alikuwa mtu hatari sana ndani ya ile simulizi. Na Elvis Tables Musiba alikwa ni gwiji na mwandishi mkubwa na mzuri sana. Kila ninapokutana na rafiki yangu Eric James Shigongo ambaye pia ni mwandishi wa vitabu namkumbuka Elvis Tables Musiba. Siku moja nitamuuliza Eric James Shigongo alipata wapi hamasa ya kuandika vitabu. Inawezekana alisoma pia vitabu vya Elvis Tables Musiba.

Nilipokutana na Elvis Tables Musiba nilishangaa kugundua kuwa alikuwa ana kipaji kingine cha biashara na uongozi. Wakati tunachangisha fedha kwa ajili ya kongamano moja katika sekta ya utalii, aliniita ofisini kwake Mirambo House karibu na ofisi za benki ya dunia. Tulikuwa tunahitaji kuchangisha kama shilingi milioni 100. Elvis Tables Musiba akamuomba katibu muhtasi wake amletee simu. Sikuelewa simu ya nini kwenye kuchangisha fedha. Nilitegemea tungeshirikiana kuandika barua na "proposals" za kuchangisha fedha. Lakini haikuwa hivyo. Simu ilipoletwa akaanza kazi. Alikuwa anatuuliza mnataka kampuni gani ituchangie fedha. Kwa hiyo kazi yetu ikawa ni kutaja majina ya makampuni na yeye anapiga simu. Nilishangaa kuona Elvis Tables Musiba hahitaji tumpe namba za simu. Alinyanyua simu na kupiga kila tulipotaja kampuni. Na alipopiga hakuongea na katibu muhtasi au mkurugenzi wa fedha. Aliongea na CEO, Director General au Mwenyekiti wa "board". Namba alizipata wapi? sijui. Lakini ndani ya saa moja tulikuwa na shilingi milioni 60.

Nikagundiua huyu si mtu wa mchezo. Ana "connections" za ajabu. Nikamuuliza hebu niambie haya mambo unayafanyafanyaje mbona kwangu mageni? Akasema "reciprocate". Hili ni neno la kiingereza linalomaanisha "rudisha wema'. Elvis Tables Musiba aliwasaidia wengi kufika pale walipo ikiwa ni pamoja na CEOs. Kumbuka amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za kampuni nyingi. Wengi wa hawa CEOs ameshiriki kuwafanyia usahili kwa wao kuwa pale. Ndio maana haikumchukua muda kupata milioni 60. Alikuwa akiongea na watu ambao ni sehemu ya mchango wake katika maisha ya mafanikio yao. Hii ikanifanya nimdadisi zaidi. Nikamuuliza wewe ulianzaje biashara?

Akasema mtaji wangu wa biashara ulitokana na kuuza vitabu. Vitabu kama NJAMA ndivyo vilivyonitoa. Lakini nilipoanza biashara haikuwa rahisi. Mimi nilikuwa mtanzania wa kwanza "mswahili" kumiliki "Bureau De Change"-anasema Elvis Tables Musiba. Lakini siku moja nikiwa Musoma, nikasikia kwenye redio kwamba biashara yangu iko mikononi mwa serikali. Kidogo nipate kichaa. Lakini sikukata tamaa nikaanza upya. Akasema nyie vijana wa siku hizi mnalalamika mazingira magumu ya biashara. Nawashangaa sana. Tuulize sisi. Haikuwa rahisi kama mnavyofikiria. Kutoka kwa Elvis Tables Musiba nikajifunza yafuatayo;

      I.          Biashara ni mahusiano na watu. Elvis Tables Musiba kutumia saa moja kupata milioni 60 sio mchezo. Aliwekeza kwa watu. Leo hii kutafuta Tsh. 10,000/= ya luku ukikwama usiku wa manane na hauna salio kwenye simu ni shughuli pevu. Unaweza ukapiga namba zote kwenye simu yako usipate hata shilingi moja. Lakini Elvis Tables Musiba alitumia saa moja tu kupata shilingi milioni 60. Ina maana kila dakila alipata shilingi milioni 1.

    II.          Kipaji chako ndio mtaji wako. Badala ya kulalamika huna mtaji, angalia una kipaji gani? Elvis Tables Musiba alikuwa na kipaji cha kuandika hadithi. Ndicho kilichompa mtaji wa kuanzisha biashara. Eric James Shigongo aliwahi kuniambia pia, kwamba kipaji chake cha kuandika hadithi ndicho kilichomsaidia kuanzisha kampuni ya magazeti pendwa na kudumu mpaka leo (Global Publishers). Mifano ni mingi. Bila mpira Mbwana Samata angekuwa wapi? Bila mpira George Weah angekuwa Rais wa Liberia? badala ya kulalamika anza na kipaji chako? Mimi nilianza kwa kuandaa makongamano. Unaweza ukawa unaandaa harusi vizuri kila mtu anashangaa. Lakini bado unafikiri hicho siyo kipaji. Unafikiri kipaji ni "kuimba" tu! Mwenzako makongamano yalinipeleka mpaka Ikulu, yakanipa na mtaji wa kuanza.

  III.          Usikate tamaa. Elvis Tables Musiba anasema amefilisika mara nyingi katika maisha yake lakini alipambana akarudi tena kwenye mstari. Hakujinyonga. Baadhi ya biashara zake zilikwama. Lakini hakukata tamaa wala hakujenga chuki na watu. Kifupi, hakutafuta mchawi. Alianza upya na kusonga mbele. Alishirikiana na watu katika sekta binafsi na serikalini. Hiyo ndiyo roho ya "ujasiri wa mali" au "spirit" ya ujasiriamali au "entrepreneurship". Ni mlolongo wa kushindwa na kushinda, kushindwa na kushinda mpaka kieleweke.

3.     Dr. Reginald Abraham Mengi, Mwenyekiti Mwanzilishi wa IPP Group na Mwenyekiti wa zamani wa CTI na TPSF

Dr. Reginald Abraham Mengi alinishirikisha mwanzoni kabisa wakati akianza kuandika kitabu chake cha "I Can, I Must, I Will". Nakumbuka alinipigia simu akasema njoo ofisini. Akaniambia nataka uwe sehemu ya team itakayonisaidia kukamilisha hili zoezi. Akaniomba nimtafutie vijana wengine wa kushirikliana na Prof. Msamali Nangoli, mwanazuoni wa Uganda aliyekuwa akiishi nchini Kenya, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho "No More Lies About Africa". Prof. Msalami Nangoli alikuwa rafiki mkubwa wa Nelson Mandela, mpigania Uhuru na Rais wa kwanza wa serikali ya kidemokrasia nchini Afrika ya kusini. Akiwa gerezani, Nelson Mandela alikuwa akisoma makala za Prof. Msamali Nangoli, makala ambazo zilipitishwa gerezani kiujanja kama kifungashio cha chapati. Kumbuka akiwa gerezani, Mandela hakuruhusiwa kusoma hata magazeti.

Ili kukamilisha zoezi la kuandika kitabu cha Dr. Reginald Abraham Mengi chini ya uongozi wa Prof. Msamali Nangoli, nilipewa "tapes" za hotuba za Dr. Reginald Abraham Mengi nyingi sana (mabox kwa mabox) ili nizipitie. Pia tuliwahoji watu wengi waliofanya kazi na Dr. Reginald Abraham Mengi. Bahati mbaya sana katikati ya safari ya kumsaidia Dr. Reginald Abraham Mengi kuandika kitabu chake, Prof. Msamali Nangoli akafariki dunia na Dr. Reginald Abraham Mengi akasitisha zoezi kwa muda. Baadaye akapata namna nyingine ya kumalizia kitabu chake kizuri.

Tulipokuwa na Prof. Msamali Nangoli tulimshawishi sana Dr. Reginald Abraham Mengi kubadilisha "title" au jina la kitabu lakini alikataa. Sisi tulipendekeza kitabu chake kiitwe; Dr. Reginald Abraham Mengi-How I became Rich; Financially, Morally, Materially. Lakini hakutaka hata kutusikiliza. Baadaye nilikuja kugundua tulikuwa tunakosea sana kumshawishi abadilishe jina la kitabu cha "I Must, I Can, I Will". Kwanini?

Kwa sababu siku moja nikiwa nyumbani kwake Kinondoni, nilimuuliza. Kwanini "I Must, I Can, I will"?. Akasema kwa sababu maisha ya biashara yana changamoto sana. Akaniuliza Paul, kwani unafikiri changamoto za biashara Tanzania ni zipi. Moyoni nikasema sasa Dr. ananiuliza swali gani "simple" namna hii. Au anataka kupima uwezo wangu wa kufikiri? Nikamwambia kubwa ni 3. Kwanza Mitaji au "Capital", Pili Masoko au "Markets", Tatu Rasilimali Watu au "Human resource". Akasema umekosa. Akasema kwanza Roho Mbaya, Pili Chuki, Tatu Wivu. Nilichoka kichwa. Akasema ili ufanikiwe lazima ukabiliane na hizi changamoto 3 nilizokutajia kisha uunganishe na hizo za mitaji, masoko na rasilimali watu. Ndio maana ya "I Must, I Can, I Will". Lazima udhamirie kutoka moyoni kupambana na changamoto.

Dr. Reginald Abraham Mengi akasema tulipotoka ni mbali kuliko tulipo. Akasema nakumbuka wakati nimeanzisha biashara ya maji ya kunywa, nilienda kwenye maonyesho ya sabasaba kuonyesha biashara mpya ya maji. Akasema watu waliokuwa wakipita kwenye banda langu walikuwa wananishangaa sana. Wanasema "huyu mchaga anapenda sana hela". Mpaka anatuuzia maji? Kweli leo hii nchi hii tumefikia hatua ya kuuziana maji? Dr. Reginald Abraham Mengi akasema kwa hiyo unaweza ukaona "Kilimanjato Pure Drinking Water" imeshamiri ukafikiri ni lelemama. Haikuwa rahisi. Bora hawa ambao wanaanza kuuza maji leo. Sisi tulioanza tulipata shida. Kwa sababu hakuna aliyezoea kuuziwa maji. Lakini Paul ukweli ni kwamba huwezi kushindana na mtu aliyeanza. Aliyekutangulia amekutangulia tu!

Dr. Reginald Abraham Mengi akaendelea kusema zaidi ya hapo kujenga sekta binafsi haikuwa rahisi. Kumbuka historia ya nchi hii toka kipindi cha wakoloni. Toka enzi hizo biashara zilikuwa kwa matabaka. Wa kwanza pale juu ni wazungu, wa pili waarabu na wa tatu wahindi. Sisi wazawa wa "kiswahili" tulikuwa hatufikiriwi kabisa kuwa "matajiri". Kuna wakati nilinunua Mercedez Benz lakini nilikuwa naogopa kuliendesha. Kwa sababu mifumo ya kiuchumi ilikwishakamatwa na matabaka mengine. Kwahiyo unavyoona sekta binafsi imefika hapa ni mapambano kwelikweli. Mswahili kumiliki kiwanda miaka ya sabini na themanini na Mswahili kuwa kiongozi wa sekta binafsi ambayo haina waswahili wengi ulikuwa ni mtihani ambao ilibidi kuushinda. Haikuwa kazi rahisi. Mimi Paul Mashauri nimeona na kusimuliwa mengi pengine nahitaji kitabu kizima kuzungumza ya Dr. Reginald Abraham Mengi. Lakini kuna mafundisho machache nataka niyataje hapa;

      I.          Biashara si lelemama. Changamoto ni nyingi kuliko fursa. Lazima ubadilishe hizo changamoto ziwe fursa ili fursa ziwe nyingi kuliko changamoto. Hii haiwezekani pasipo kuwa na moyo mgumu "a iron heart". Kama unataka uache kazi uanze biashara ukifikiri ni mteremko jifikirie tena na tena na tena. Nakumbuka wakati nimemualika Dr. Reginald Abraham Mengi kuongea na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alirudia hilo. Akasema; "safari ya mafanikio ni kama pambano la ngumi. Kuna makonde ya kuyakwepa, kuna makonde ya kuyazuia ambayo yakikupata yanasambaratisha uso wako au kukuua kabisa lakini kuna wakati ambao lazima ujibu mapigo ili ushinde pambano. Mh. Jokate Mwegelo, DC, Kisarawe, kipindi hicho akiwa chuoni, alikuwa "Moderator" katika tukio hilo. Anaweza akayakumbuka maneno haya.

    II.          Usiogope kuanzisha njia pasipo na njia. Usiogope kuwa wa kwanza kufanya jambo ambalo wengine wanasita kufanya. Maana yake ni kwamba "be the pioneer". Dunia tunayoishi iko hapa ilipo sababu ya "pioneers". Christopher Columbus angeogopa kusafiri kutoka Spain pengine America (New Land) ingechelewa sana kutambulika katika uso wa dunia. Hata wewe usiwe mtu wa kusubiri wenzako waanze. "Legends" sio wale wanao "copy na kupaste" Legends ni waanzilishi. Kuanza sio lazima iwe ni kwenye biashara. Hata kwenye familia yako unaweza ukawa wa kwanza kuwa "mbunge".

4.     Mr. Ali Mfuruki, Aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table

TRBN (Tanzania Responsible Business Network) ilipoanza niliombwa na Partner wa KPMG Ketan Patel pamoja na Partner wa Deloitte Joe Eshun niwe "Moderator" katika sherehe za uzinduzi wa TRBN pale Serena Hotel. Tulikuwa na CEOs zaidi ya 300. Mgeni rasmi alikuwa ni Mr. Ali Mfuruki, Mwenyekiti wa CEO Round Table. Baada ya ufunguzi nilikuwa na muda wa kutosha wa kuongea na Mr. Ali Mfuruki. Jambo moja Mr. Ali Mfuruki aliniambia ambalo sitolisahau ni kwamba lazima uwe na msimamo na lazima ukubali kupoteza baadhi ya vitu ikiwa ni pamoja na fedha kusimamia unayoyaamini. Akaniambia nyie vijana sasa hivi ndio mmekuwa mameneja kwenye makampuni na viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali. Sasa wakati mwingine unakutana na kijana kwenye kampuni ambaye amepewa mamlaka, kijana ambaye unaweza kumzaa anataka akuzungushe, akunyanyase ili umpigie magoti. Mimi siwezi. Bora nikose hela kuliko kushusha heshima yangu.

Wapo vijana ambao wanamsikia Mr. Ali Mfuruki leo hii lakini hawajakutana na Mr. Ali Mfuruki na kuzungumza naye ana kwa ana. Sijui umesikia nini juu yake lakini Mr. Ali Mfuruki alikuwa na msimamo wa kipekee. Alikuwa anafikiria vizuri sana sio katika biashara zake tu hata kwa nchi. Ndio maana kifo chake kimetushtua kama Taifa. Unaweza ukawa unafikiria vizuri lakini kwa mambo yako binafsi na familia yako. Hilo ni jambo zuri na ndiyo jambo la pili baada ya kumfikiria Mungu. Lakini unapojiongeza na kufikiria Taifa na watu wengine ndani ya Taifa unakuwa wa tofauti zaidi. Ndivyo alivyokuwa Mr. Ali Mfuruki.

Kuna siku nilikutana naye nikamuuliza Mr. Ali Mfuruki lini unaandika kitabu? Akaniambia nimeanza kuandika. Siku niliposikia ametoa kitabu, nikawahi bookshop Mlimani City kununua. Lakini baada ya kusoma kile kitabu nikagundua nilichofikiria kuwa kitakuwepo kwenye kitabu sicho. Mr. Ali Mfuruki hakuwa ameandika kitabu kuhusu yeye na mke wake na watoto wake. Alikuwa ameandika kitabu kuhusu uchumi wa viwanda. Huyo ndio Mr. Ali Mfuruki. Ndiyo sababu alidumu kama Mwenyekiti wa CEO Round Table kwa miaka mingi. Sio kwamba alipenda kuhodhi madaraka. Alikuwa ana uwezo kichwani. Na vyeo vingi alikuwa anakataa. Na pale alipokubali alijitoa kwa dhati. Amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za Mwananchi Communications Ltd, amekuwa kwenye "board" ya Geita Gold Miming (GGM), Mwenyekiti wa "board" ya Vodacom nk. Waulize waliofanya kazi naye. Kile kilikuwa kichwa kingine.

Wakati fulani nilialikwa katika uzinduzi wa "Private Equity Fund" moja pale Golden Tulip Hotel. Alikuwepo Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waheshimiwa mawaziri na wafanya biashara. Mr. Ali Mfuruki alikuwa miongoni mwa waalikwa pia. Siku ile Mr. Ali Mfuruki aliongea kitu kikubwa sana. Akasema, wakati Marekani inataka kwenda mwezini miaka ya 60. Rais wa nchi hiyo J.F. Keneddy alitangaza kwamba Mmarekani yoyote atakayekuja na wazo au "idea" au "ubunifu" au "teknolojia" ambayo itaisaidia Taifa la Marekani kufika mwezini au kufika hatua moja mbele katika ndoto ya nchi kwenda mwezini, serikali ya Marekani italipa fedha kununua hilo wazo au huo ubunifu. Mr. Ali Mfuruki akasema; ili sisi kama Taifa tuweze kwenda mbele lazima kuwe na mbinu za kujenga "uhitaji" au "demand" ya ugunduzi na ubunifu "Creativity and innovation" . Akasema "kufikiria" ni kazi. Kugundua kitu ni gharama. Lazima ufanye "research" au "utafiti". Tukitaka watu wetu wawe wabunifu lazima tutengeneze mbinu za kumfikirisha mtu akijua kabisa kuwa nguvu zake hazitoenda bure.

Mr. Ali Mfuruki alikuwa haongei "nadharia". Sijawahi kumsikia akiongea "pumba". Kwa historia yake yeye ni mhandisi au "engineer" kwa lugha ya kiingereza. Mr. Ali Mfuruki Alipotoka nchini Ujerumani aliposomea, kuja nyumbani Tanzania kufanya biashara, aliona kuna fursa, kuna "demand" au "uhitaji" wa bidhaa za teknolojia hasa kompyuta. Kipindi hiki nchi ilikuwa imefunguka na serikali pamoja na makampuni binafsi yalikuwa yanabadilisha teknolojia kutoka katika mfumo wa kizamani wa "fax" na "typewriters" kuja kwenye matumizi ya kompyuta. Ndivyo kampuni yake ya Infotech Technologies Ilivyoanza. Huwezi kuzungumzia Teknolojia Tanzania pasipo kumzungumzia Mr. Ali Mfuruki ingawa amekuwa na biashara nyingi zaidi ya hiyo. Yeye ni baba katika eneo hili la TEHAMA hapa Tanzania pamoja na kwamba unapozungumzia ujio wa WoolWorth unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki na hata unapozungumzia ujio wa Zuku unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki. Nini cha kujifunza hapa;

      I.          Tunaishi katika dunia ya ubepari au "capitalism". Dunia ya "ubepari" na dunia ya ujamaa au "socialism" ni dunia 2 tofauti. Katika dunia ya ubepari mtu anaweza akakudhalilisha kwa sababu amekupa fursa. Mtu anaweza akataka umuabudu na umpigie magoti kwa sababu anakupa biashara. Mtu anaweza akakuvunjia heshima mbela ya mke na watoto wako kwa sababu bila yeye huwezi kupata mshahara. Haya ndiyo mambo ambayo Mr. Ali Mfuruki aliniambia hayataki. Akasema bora niwe "broke" au "masikini" kuliko kudhaliliswa. Alikuwa na msimamo.

    II.          Vijana wengi wanatamani kuheshimiwa kama Mr. Ali Mfuruki. Lakini hawajui kuwa heshima haiji kwenye kikombe cha chai. Inajengwa kwa jasho kubwa. Mimi Paul Mashauri ambaye nimekaa na hawa watu najua. Mimi Paul Mashauri ambaye nimetumika sana kwenye sekta binafsi nijaua. Ni kazi ngumu na inataka moyo. Kumbuka Mr. Ali Mfuruki ni mfanyabiashara. Ana biashara zinazomuangalia yeye. Na bado aangalie ya nchi. Sio jambo dogo. Kumbuka akifanya hivyo waziri ni sawa kwa sababu mwisho wa mwezi analipwa mshahara. Ni sehemu ya "job description". Lakini unapokuwa Mwenyekiti wa hizi taasisi za sekta binafsi unatumia akili zako na nguzu zako kama msaada na mchango kwa Taifa. Ingawa sina uhakika kama ukifilisika unapewa tena mtaji na Taifa. Ndio maana nasema inataka moyo. Ni vijana wangapi wako tayari kufanya hivyo? Kuacha biashara yako na watoto wako kuhangaikia ya wengine?

  III.          Mr. Ali Mfuruki alikuwa anafikiri vizuri "thinker" kwa sababu alikuwa anatumia muda mrefu sana kukutana na watu wa haiba tofauti, kusoma, kusafiri kupata "exposure" nk. Hakuna mtu alikuwa anamlipia tiketi ya ndege kusafiri. Alikuwa anajilipia mwenyewe. Leo unataka kuwa kama Mr. Ali Mfuruki unashinda instagram unasoma udaku. Hautaki kwenda kwenye kongamano lolote zaidi ya matamasha ya muziki na comedy. Kila tasnia ina utamaduni wake. Ukitaka kuketi katikati ya wakuu lazima ufikirie kama wakuu. Mr. Ali Mfuruki aliitwa na wakuu, alikaa meza moja na wakuu akiwemo Barack Obama, Rais Mstaafu wa Marekani sio kwa sababu alikuwa "handsome" mwenye "six packs" tumboni kuliko watanzania wote. La hasha! Alikuwa na madini adimu kichwani.

5.     Ruge Mutahaba, Aliyekuwa Mkurugenzi au "Director" wa programs, Clouds Media Group

Niliposikia amefariki, nilisikitika sana. Kwa sababu miezi michache iliyopita kabla ya taarifa hizo nilimpigia simu. Nikamwambia kaka Ruge kuna kongamano la vijana na wazazi tunaandaa naomba uje uzungumze hasa na vijana. Akajibu akasema "count me in". Lakini miezi kadhaa nyuma, Ruge mwenyewe alinipigia simu. Akasema Paul wewe na mimi kama "speakers" lazima tufanye mambo ya kusaidia nchi. Akaniambia hebu andika "andiko" au "proposal" ya kusaidia Taifa letu kwa kutumia "speakers" kuhamasisha fikra mbadala hasa katika mambo ya msingi ya kitaifa. Nilikesha usiku ule nikaandika ile "proposal" na nikamtumia Ruge kwa email. Ile "propoal" niliipa jina la "Speakers Without Boarders".

Wengi walimfahamu Ruge Mutahaba kwenye "media" na "muziki" lakini Ruge Mutahaba alikuwa ni zaidi ya media na muziki. Ndio sababu alipofariki hata Rais wa nchi alitoa neno. Uwezo wa Ruge Mutahaba ulikuwa hauna shaka. Ubishi wake kwa kile alichokiamini ulikuwa si wa kitoto. Na utayari wake kujitoa kwa ajili ya wengine hauelezeki. Siweki chumvi na mimi sio mnafiki wala sisemi haya yote kwa sababu hayupo tena duniani. Niliyasema haya hata alipokuwa hai. 

Niliyasema ya Mr. Ali Mfuruki wiki iliyopita ambayo ni wiki moja kabla hajafariki. Sio wote wana moyo wa kusema nani aliwasaidia katika maisha yao lakini mimi nasema kwa sababu duniani hakuna mtu anayetoka bila msaada wa mtu mwingine. Hakuna kitu kama "self-made". Kusaidiwa sio lazima iwe pesa .Hata mwalimu wa shule ya msingi alikusaidia kujua kusoma na kuandika. Leo unasemaje kuwa wewe ni "self-made millionaire"? Humkumbuki hata mkeo au mumeo aliyekutia moyo ulipokata tamaa?

Ruge Mutahaba alinisaidia sana mimi na vijana wengine wengi. Yeye ndiye aliyenitambulisha kwa Azim Jamal aliye kuja kuwa rafiki yangu mkubwa katika "motivational speaking". Huyu ni mnenaji au "speaker", mwandishi wa vitabu au "author", mtaalam wa menejimenti au "consultant" na mfanyabiashara aliyebobea. Azim Jamal amefanya kazi na kuandika vitabu pamoja na wataalam na wanenaji "speakers" wakubwa duniani kama Brian Tracy. 

Kumlipa Azim Jamal kuzungumza kwenye tukio lako sio chini ya dola za Kimarekani milioni 10 au fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 20 ndani ya siku moja. Lakini kwa sababu ya urafiki na heshima ya Ruge Mutahaba, Azim Jamal alikuja kuzungumza kwenye tukio nililoandaa bila kulipwa hata shilingi moja. Baada ya hapo tulifanya kazi nyingi sana na Azim Jamal.

Pili wakati tunaanzisha gazeti la Familia, yeye ndiye aliyenipa matangazo ya bure. Alisema wewe unafanya kazi kubwa sana kuhamasisha vijana. Hakuna anayekulipa kwa kujitolea kwako. Malipo yako yatakuwa matangazo nitakayokupa Clouds FM. Kwa moyo ulionao ukitoka wewe, wengi zaidi watatoka. Ruge Mutahaba alilipa gharama ya kazi yangu kwa vijana. Si hayo tu, yeye pamoja na Joseph Kusaga ndio walionipa studio za Clouds TV kutengeneza sinema yangu iitwayo "Maisha Ni Siasa". 

Angalia sinema hii yote Youtube. Sio mimi tu, wako wengi aliowasaidia. Hata serikali inatambua nini Ruge Mutahaba alifanya katika nchi hii. Uzoefu wangu wa Ruge Mutahaba tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum ulinidhihirishia uwezo wake wa kuangalia mambo kwa jicho la tatu. Ndio sababu alikuwa mbunifu sana. Kila tulipokuwa na kikao, Ruge Mutahaba hakuwa wa kwanza kuongea. Lakini alipopata nafasi ya kuongea, aliipindua pindua mada na wote tukaiona hoja husika kwa namna ambayo hatukuiona hapo kabla.

Kila nikimkumbuka Ruge Mutahaba nakumbuka mmoja kati ya vijana ambao walijiongeza. Ungeniuliza ni akina nani wanafanya sana kazi bila kuchoka ningekuambia ni Ruge Mutahaba. Binafsi sijui alikuwa anapumzika saa ngapi. Unakutana na kijana anasema anataka kuwa kama Ruge Mutahaba na bado analala saa 2 usiku na anaamka saa 2 asubuhi. Unataka kuwa kama Ruge yupi? Sijaona mimi mtu anafanya vitu vikubwa vya kitaifa na analala usingizi wa pono. Uliza wasaidizi wa Rais kama wanalala? Kama unajua huwezi kufanya kazi kwa bidii kubali kuwa wa kawaida. Usifikiri nazungumzia "utajiri". Hilo ni suala lingine.

 Unaweza usiwe tajiri lakini bado ukawa si wa kawaida. Akina Dr. Martin Luther King Jr. na Nelson Mandela hawakuwa matajiri lakini pia hawakuwa wa kawaida. Lazima utofautishe kati ya kuwa "rich" au "tajiri" na kuwa "great". Hapa sizungumzii utajiri nazungumzia "greatness". Hata mwizi anaweka kuwa "tajiri" lakini inahitaji "akili nzuri", "kujitoa kwa wengine" na "kujituma" ili uwe "great" Vitu vinavyobadilisha jamii havihitaji mtu mzembe. Kama kusoma tu hii makala mpaka hapa umeshachoka unatamani iishe utaweza kuwa kama Ruge Mutahaba? Kuna mambo ya msingi ya kujifunza kutoka kwa Ruge Mutahaba;

      I.          Ubishi. Hakuna kitu kinakuja kirahisi. Mafanikio sio muujiza, yanafanyiwa kazi. Usifikiri Ruge Mutahaba alifika pale alipofika sababu ya "Clouds" kama media. Hatukatai ukweli kwamba alikuwa ni mmoja wa watu walioijenga Clouds Media Group. Kwanza, ulikuwa ukisikia Clouds FM iko hewani, sura mbili zinakuja kichwani kwako; Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Hata isingekuwa "media" Ruge Mutahaba angefanya vitu vikubwa tu kwa sababu alikuwa ni "mbishi" asiyekubali kushindwa. Miaka 3 iliyopita nilimualika Ruge Mutahaba katika kongamano la Vijana lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) pale Serena Hotel. Kongamano lilikuwa chini ya mradi wa kutoa mitaji kwa mawazo bora ya biashara kwa vijana "Ajira Yangu" Project ambayo niliisimamia.

    II.          Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Ruge Mutahaba akasema "ukija kwangu na wazo au "idea" yako nakurudisha mara 3 au mara 4. Sio kwa sababu wazo lako ni baya. Nataka nione kama kweli wewe ni mbishi na uko tayari kupambana mpaka wazo lako lipate maisha. Vijana wa leo hawako hivyo. Wanataka mambo ya chapchap kama mabando ya internet. Hawana uthubutu. Wanaamini kwenye michongo na kushikwa mkono. Wanakata tamaa mapema. Hata wakija kwako uwe "mentor" wao wanakuja "kifursa zaidi". Wanataka uwe "mentor" wao na hapohapo uwape "hela". Hiyo sio "mentorship" hiyo ni "sponsorship". Sasa hatujui unataka nini? Unataka "mentorship" au "sponsorship"?Hawajui kuwa hata akina Ruge Mutahaba walipitia vikwazo lakini walikuwa wabishi.

  III.          Uwezo wa kufanya lolote unalolitaka. Nilisema hapo mwanzo kwamba wengi wanamjua Ruge Mutahaba kwa sababu ya "media", "muziki" na "matamasha". Ruge Mutahaba alikuwa zaidi ya hapo. Ruge Mutahaba alikuwa pia anandaa sinema. Nikiwa chuo kikuu Ruge Mutahaba alirekodi sinema inaitwa "Kelele". Yeye mwenyewe binafsi alikuwa nyuma ya kamera kuhakikisha sinema inarekodiwa vizuri. Ingawa sikumbuki kama aliwahi kuitoa ile sinema lakini nilichojifunza ni kwamba alijua anaweza kufanya kitu zaidi ya kimoja.

 Kuna mikakati mingi sana na miradi mikubwa ya kitaifa mbayo Ruge Mutahaba alikuwa nyuma yake ingawa hakuonekana mstari wa mbele. Huyo ndiyo Ruge Mutahaba niliyemfahamu mimi. Leo hii unatamani siku moja upewe heshima aliyopewa Ruge Mutahaba lakini hujiulizi nini kitu cha tofauti unafanya? Zaidi ya kutoka bwenini, kwenda darasani kisha kwenda bwaloni kula ubwabwa nini kingine unafanya? Zaidi ya kutoka kazini na kwenda baa au kwenye harusi kula pilau, nini kingine unafanya?Unawezaje kuwa kama Ruge au zaidi ya Ruge kwa maisha ya pembe tatu?Unawezaje kufikia ndoto zako kwa maisha ya pembe tatu? Hata kama umeajiriwa. Usiku unafanya nini?

Tanzania imepoteza watu muhimu sana katika muda mfupi sana. Niliyoyataja hapa kwa hawa "generals" ni machache sana ukilinganisha na niliyoyafahamu na nisiyoyafahamu. Hawa watu walitumia vyema uwepo wao hapa duniani na uwepo wao katika hii nchi kuleta utofauti. Ni "generals" walioondoka lakini nchi bado ipo. Pamoja na utofauti wao, hawa wote wanasifa zinazofanana. Pamoja na mapungufu yao wote hawa wana faida zinazofanana.

1. Waliwekeza katika maarifa 2. Waliwekeza katika watu 3. Walitumia karama, vipaji na elimu zao kuleta utofauti na kulitumikia Taifa 4. Hawakuwa wepesi kukata tamaa hata walipopitia magumu katika ngazi za familia zao, maisha yao binafsi, biashara zao na kazi za kitaifa 5. Wameacha alama katika nchi hii, alama ambayo itaendelea kuishi ingawa wao hatunao tena. Amani ya bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nao, familia zao, ndugu zao, marafiki zao na watanzania wote kwa ujumla.  
Makala hii imeandikwa na Paul R.K Mashauri@hakimiliki 2019. Hairuhusiwi kuchapisha Makala hii au sehemu ya Makala hii pasipo idhini ya mwandishi. Wasiliana na mwandishi kupitia ceo@masterclassworldwide.co.tz

TANESCO ARUSHA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RC GAMBO

0
0
Picha ya viongozi wa mitaa kata ya  Olasiti na wataalam wakiwa katika wakiwa katika mtaa wa Oleresho pamoja na maafisa kutoka Tanesco ambapo walipitia kuhakiki kaya zisizokuwa na umeme. 
Na Vero Ignatus,Arusha.
Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo  kwa 
Shirika la umeme Tanesco limeanza kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambalo aliwataka kuwaunganishia umeme kaya zaidi ya 200 zilizopo katika kata ya Olasiti ,baada ya Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo ikiongozwa na Diwani na Afisa Tarafa ya Elerai  pamoja na Wataalamu wa Tanesco kufanya ziara ya kupima maeneo na kufanya zoezi la kubaini kaya hizo ili kuziunganishia na umeme.
Alex Martinni diwani wa  wa Kata ya Olasiti  alisema watahakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa ambapo wamewatembeza wataalamu kutoka Tanseco ili waweze kujionea  kaya hizo zilizoko katika mtaa wa Oleresho na Kimindoros ambazo licha ya kuwa ndani ya jiji la Arusha hazina huduma ya umeme.
Martin  ameipongeza serikali kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wananchi na kuagiza wananchi hao waunganishe na huduma ya umeme ambayo ni kichocheo cha maendeleo kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi amesema kuwa wataalamu hao wameanza kupima maeneo na hatua inayofuata ni kuweka nguzo na kusogeza umeme  tayari kwa ajili ya kuwaunganishia wananchi.
Cholobi amesema kuwa kufika kwa Wataalamu hao wa Tanesco ni  utekelezaji wa Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipofanya ziara yake katika kata hiyo na kusikiliza kero za wananchi ambapo aliwataka Tanesco kufika katika kata hiyo na kuwauganisha wananchi na huduma ya umeme.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Oleresho Elia Kayan  amesema kuwa wanatarajia kaya nyingi zitanufaika na huduma ya umeme licha ya kukaa muda mrefu bila kupata huduma ya umeme.
Amesema kuwa serikali imetoa agizo hilo kutokana na kutambua changamoto za wananchi hao hivyo wananchi wapo tayari kushirikiana na Wataalamu katika kutekeleza agizo hilo.
''Tumeanza kuwahamasisha wananchi kuandaa nyumba zao na kuweka mifumo ya kuingiza umeme ili umeme huo ukifika karibu na makazi yao kusiwe na vikwazo vyovyote" Alisema Mwenyekiti huyo

Mtaalamu kutoka Tanesco Idara ya Upimaji aliyejitambulisha kwa jina la Elia amesema kuwa tayari wamejionea hali halisi na kuwataka Wenyeviti wa mtaa kufanya vikao na kukubaliana njia ambazo umeme utapita ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima katika utekelezaji wa agizo hilo.

HARMONIZE NA VIKUNDI VYA UTAMADUNI VYANOGESHA SHEREHE ZA MIAKA 58 YA UHURU NA 57 YA JAMHURI JIJINI MWANZA

0
0

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara akicheza ngoma na
wacheza ngoma ya Litungu ya kabila la Wakurya waliokuwa wakitumbuiza
kunogesha Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza leo Desemba 9, 2019.
Msanii Rajabu Abduli maarufu kama “Harmonize” akitumbuiza
katika kunogesha Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Desemba 9, 2019.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Latest Images