Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 3276 | 3277 | (Page 3278) | 3279 | 3280 | .... | 3352 | newer

  0 0

  Na Ahmed Mahmoud, Arusha

  Wanasayansi Afrika wametakiwa kufanya tafiti zenye kuleta mslahi ya nchi katika uchumi wa kati na zenye kujibu changamoto za wananchi katika mali ghafi na rasilimali vitu ili bara la Afrika liweze kusonga mbele kimaendeleo kuliko hivi sasa kwa kuwa bara hili ni masikini pamoja na kuwa na mali ghafi na rasilimali nyingi kila kona.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo na Ufundi,William Ole Naasha wakati akifungua Kongamano la Jumuiya ya Wanasayansi watafiti wa mali ghafi na rasilimali vitu Afrika lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Cha Nelson Mendela kilichopo Mkoani Arusha na kushirikisha wanasayansi kadhaa duniani.

  Naasha amesema Bara la Afrika ndio linaloongoza kwa kuwa na mali ghafi na rasilimali nyingi lakini ndio bara pekee masikini duaniani hivyo ni wajibu wa wanasayansi kufanya utafiti wa mali ghafi na rasilimali vitu ili wananchi wa bara hilo waweze kunufaika rasilimali zilizowazunguka.

  Alisema na kuwataka wanasayansi kufanya tafiti zenye kujibu changamoto zinazowazunguka wananchi na kupata majibu sahihi ili bara la Afrika liweze kuendelea na kutoka katika umasikini wa kupindukia uliopo sasa.

  Waziri amesema kwa hapa nchini wanasayansi wanahitajika sana kwa sasa katika sera ya serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Magufuli ya Uchumi wa Viwanda na Uchumi wa Kati ili waweze kufanya tafiti mbalimbali za mali ghafi na rasilimali vitu na kutoa majibu sahihi za kuondoa changamaoto za wananchi.

  Alisema wanasayansi wenyewe wa hapa nchini ndio wanaoweza kufanya tafiti za mali ghafi na rasilimali na sio kungojea wanasayansi kutoka nchini.

  ‘’Tufanye tafiti zinazotatua changamoto ndani ya nchi ili tutokea katika dimbwi la umasikini kwani Bara la Afrika ni tajili lakini tunashindwa kutumia ipasavyo mali ghafi na rasilimali watu zilizopo’’alisema

  Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Prf Emmanuel luoga alisema kuwa kongamano kama hilo linasaidia katika kuleta elimu mpya katika masuala ya kitafiti kwani wanasayansi waliobobea kutoka katika kila pembe ya dunia wamewasili katika kongamano hilo kujadili mambo mbalimbali ya kitafiti katika Bara ya Afrika.

  Prf Luoga alisema baada ya kongamano hilo wanasayansi wa Afrika wanaweza kupata kitu kipya zaidi katika shughuli za kitafiti lengo ni kutaka mali ghafi na rasilimali iliyopo katika Bara la Afrika kunufaisha wananchi wake.

  Amesema wanasayansi waliobobea kutoka katika nchi zilizoendelea duniani wamekuja katika kongamano hilo lengo ni kutaka kuwapiga msasa wanasayansi wa Afrika kufanya tafiti zenye kujibu changamoto kwa wananchi na zenye manufaa kwa kwa jamii na sio vinginevyo.

  Naye Rais wa Jumuiya hiyo,Prf Hulda Swai amesema kuwa jumuiya hiyo ina zaidi ya miaka 21 na kila baada ya miaka miwili wanasayansi wa jumuiya hiyo hukutana na kila mmoja hutakiwa kuja na suluhisho la tafiti alilofanya kwa maslahi ya wananchi wa Bara la Afrika.

  Prf Swai amesema Bara la Afrika ni bara lenye utajili mkubwa wa mali ghafi na rasilimali vitu na kutoa mfano wa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo{DRC} lakini wananchi wake ni masikini wa kupindukia hivyo ni wajibu wa wanasayansi kufanya tafiti za kina na kuja na majibu yenye kuleta suluhisho kwa jamii kunufaika na mali ghafi na rasilimali vitu.

  0 0

   
   The Chargé d’Affaires of the United States Embassy in Tanzania, Dr. Inmi Patterson, and Katavi Regional Commissioner, Mr. Juma Homera, cut a ribbon at Mpanda hospital laboratory as part of the 20th anniversary of the Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) in Tanzania recently. Chargé Patterson dedicated the new U.S. government-funded hospital laboratory that will strengthen the diagnostic capacity of the Katavi Region’s health system.  As a member of the United States’ President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), Walter Reed administers comprehensive HIV prevention, care and treatment programming in health care settings throughout the Southern Highlands, as well as to hospitals and clinics operated by the Tanzanian People’s Defense Forces.  WRAIR provides life-saving HIV treatment to more than 235,000 Tanzanians, in addition to contributing to medical research on HIV, Ebola, Malaria, Influenza and Tuberculosis to improve and save Tanzanian lives.
   The Chargé d’Affaires of the United States Embassy in Tanzania, Dr. Inmi Patterson, and Katavi Regional Commissioner, Mr. Juma Homera, shake hands after unveiling of the plaque at Mpanda hospital laboratory as part of the 20th anniversary of the Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) in Tanzania recently. Chargé Patterson dedicated the new U.S. government-funded hospital laboratory that will strengthen the diagnostic capacity of the Katavi Region’s health system.  As a member of the United States’ President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), Walter Reed administers comprehensive HIV prevention, care and treatment programming in health care settings throughout the Southern Highlands, as well as to hospitals and clinics operated by the Tanzanian People’s Defense Forces.  WRAIR provides life-saving HIV treatment to more than 235,000 Tanzanians, in addition to contributing to medical research on HIV, Ebola, Malaria, Influenza and Tuberculosis to improve and save Tanzanian lives.
   The Chargé d’Affaires of the United States Embassy in Tanzania, Dr. Inmi Patterson, and Katavi Regional Commissioner, Mr. Juma Homera, smile and enjoy traditional dance after ribbon cutting and unveiling of the plaque at Mpanda hospital laboratory as part of the 20th anniversary of the Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) in Tanzania recently. Chargé Patterson dedicated the new U.S. government-funded hospital laboratory that will strengthen the diagnostic capacity of the Katavi Region’s health system.  As a member of the United States’ President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), Walter Reed administers comprehensive HIV prevention, care and treatment programming in health care settings throughout the Southern Highlands, as well as to hospitals and clinics operated by the Tanzanian People’s Defense Forces.  WRAIR provides life-saving HIV treatment to more than 235,000 Tanzanians, in addition to contributing to medical research on HIV, Ebola, Malaria, Influenza and Tuberculosis to improve and save Tanzanian lives.
   The Chargé d’Affaires of the United States Embassy in Tanzania, Dr. Inmi Patterson, and Katavi Regional Commissioner, Mr. Juma Homera, pose for a photo in front of the RC’s office after ribbon cutting and unveiling of the plaque at Mpanda hospital laboratory as part of the 20th anniversary of the Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) in Tanzania recently.

   The Chargé d’Affaires of the United States Embassy in Tanzania, Dr. Inmi Patterson, and Katavi Regional Commissioner, Mr. Juma Homera, pose for a group photo with WRAIR staffs, U.S. and Tanzanian government officials after ribbon cutting and unveiling of the plaque at Mpanda hospital laboratory as part of the 20th anniversary of the Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) in Tanzania recently.

  0 0

  Mkuu  wa Wilaya ya Kinondoni  Daniel Chongolo amesema kuwa katika kuhakikisha tunakuza uchumi wa Viwanda, Wilaya hiyo imeandaa maonesho ya wajasiriamali  wa bidhaa zangozi yatakayofanyika Disemba 12 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Packers.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Chongolo amesema kuwa maonesho hayo ambayo yata ambatana na uuzwaji wa bidhaa hizo yatafanyika ikiwa ni katika mkakati wa kutangaza na kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini.

  Amesema kuwa lengo la maonesho hayo ni kutangaza uwezo wa wadau wa ngozi, kuelimisha jamii kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa hizo zenye ubora zinazozalishwa hapa nchini sambamba na kuongeza soko la ajira kwa vijana.

  Amefafanua kuwa katika maonesho hayo yatahusisha wajasiriamali kutoka Wilaya ya Kinondoni pamoja na Halmashauri nyingine zilizo alikwa ikiwemo Ilala, Temeke, Ubungo pamoja na Kigamboni.

  Chongolo amefafanua kuwa kupitia sensa ya mwaka 2012, Manispaa ya Kinondoni inajumla ya wakazi zaid ya milioni 1.3, ambapo idadi hiyo inategemea kupata bidhaa za ngozi, ikiwemo Viatu, Mikanda, Mabegi na pochi zinazo tokana na bidhaa za ngozi.
  Chongolo ameeleza kuwa hali hiyo imekuwa tofauti kutokana na watu hao kutumia bidhaa zinazozalishwa kutoka nje ya nchi na hivyo kuwasihi wannachi kupenda kutumia bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini.

   “Tanzania ni miongoni mwa nchi kubwa barani Afrika zinazo zalisha ngozi kwa kiasi kikubwa , lakini pia Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu Afrika zenye mifugo mingi  , Tanzania ni Nchi  pia ambazo zinatumia bidhaa hizo kwa wingi, mfano rekodi inaonyesha kuwa  jumla ya viatu zaidi ya milioni 53  zinaingia na kutumika kila mwaka” ameeleza  Chongolo.

  Rais wetu mpendwa, Dk. John Magufuli kila siku amekuwa akisisitiza kujenga viwanda ili kufikia uchumi wa kati, na sisi wasaidizi wake tunaliangalia hilo kwa kulifanyia kazi, ndio mana tumeona tuwaweke pamoja wajasiriamali wa bidhaa za ngozi, na hatutaishia hapa tunampango mwakani tuyafikishe mbali zaidi” amesema Chongolo.

  Serikali ya Viwanda, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa pamoja na kwamba Tanzania inazalisha ngozi nyingi lakini ipo changamoto kubwa inayotokana na malighafi hizo kusafirishwa nje ya nchi jambo ambalo amesema limesababisha kuwepo kwa uhaba wa ngozi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa hizo.

   Hata hivyo Mhe. Chongolo amesema kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ni Kinondoni yetu, Viwanda vyetu, Tanzania yetu ambapo kupitia maonesho hayo itakuwa ni fursa kwa vijana wengi kujiajiri , kuongeza pamoja na kukuza viwanda vya ndani vya ngozi na hivyo kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa hizo.

   Pix. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akisisitiza jambo wakati akiongea na Wanahabari kuhusiana na maandalizi ya maonesho ya bidhaa za ngozi yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers kuanzia tarehe 12 Disemba 2019.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akiongea na Waandishi wa Habari katika maandalizi ya maonesho ya bidhaa za ngozi yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers ikihusisha Wafanyabiashara wa bidhaa hizo zaidi ya 100.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia soda, inayozalishwa katika kiwanda cha Nyanza Bottling, kilichopo jijini Mwanza, kabla ya kuzindua upanuzi wa kiwanda hicho, Desemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua upanuzi wa kiwanda cha Nyanza Bottling, kilichopo jijini Mwanza, Desemba 10, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifungua upanuzi wa kiwanda cha Nyanza Bottling, kilichopo jijini Mwanza, Desemba 10, 2019.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua mitambo ya kuzalisha soda, katika kiwanda cha Nyanza Bottling, kilichopo jijini Mwanza, baada ya kufungua rasmi upanuzi wa kiwanda hicho, Desemba 10, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua ghala la kuhifadhia soda, katiak kiwanda cha Nyanza Bottling, kilichopo jijini Mwanza, baada ya kufungua rasmi upanuzi wa kiwanda hicho, Desemba 10, 2019.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia mashine ya kuzalisha mvuke unaotumika katika uzalishaji, kwenye kiwanda cha Nyanza Bottling, kilichopo jijini Mwanza, baada ya kufungua rasmi upanuzi wa kiwanda hicho, Desemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikagua moja ya bomba lililopo kwenye mradi wa maji wa Muze group uliopo Sumbawanga Vijijini.
   Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa maji wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi wa maji wa Muze group uliopo Sumbawanga Vijijini, awali mradi huu ulikuwa ujengwe na Mkandarasi kwa Bilioni 5.9 lakini kwa kutumia wataalamu wa ndani (Force account) utajengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 3.1. Mradi unakwenda vizuri na vijiji viwili kati ya vijiji 10 vitaanza kupata maji mwezi huu.
   Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akielekea kukagua mradi wa maji wa Muze group uliopo Sumbawanga Vijijini, awali mradi huu ulikuwa ujengwe na Mkandarasi kwa Bilioni 5.9 lakini kwa kutumia wataalamu wa ndani (Force account) utajengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 3.1. Mradi unakwenda vizuri na vijiji viwili kati ya vijiji 10 vitaanza kupata maji mwezi huu.
   Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akipata maelezoya mradi wa maji kutoka kwa wataalam wa mradi wa maji wa Muze group uliopo Sumbawanga Vijijini, awali mradi huu ulikuwa ujengwe na Mkandarasi kwa Bilioni 5.9 lakini kwa kutumia wataalamu wa ndani (Force account) utajengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 3.1. Mradi unakwenda vizuri na vijiji viwili kati ya vijiji 10 vitaanza kupata maji mwezi huu.

  0 0  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk. Mshindo Msola amewaahidi wanachama wa timu hiyo kuwa mpaka kufika Mei mwakani watakuwa wameingia katika mfumo wa uwekezaji kwa njia ya hisa.

  Kauli hiyo imekuja baada ya maswali mengi kutoka kwa Wanachama wa Klabu hiyo kutokana na klabu kuwa na malimbikizi makubwa ya madeni na kufikia wachezaji kuandika barua za kuachana na timu hiyo.

  Dk. Msola amesema hiyo ilikuwa ni ahadi ya pili kwenye kampeni yake na mchakato wake unaendelea hivyo hadi kufikia mwezi Juni itakuwa imekamilika.

  Msola ameongeza kuwa katika mchakato huo watawa washirikisha Wanachama katika kila hatua ili maamuzi yawe ya watu wote.

  "Mchakato ukienda sawa mpaka Juni mwakani tutakuwa tumeingia kwenye mfumo wa kisasa wa uendeshaji wa klabu kwa uwekezaji wa hisa. Hii ni ahadi yangu kwa Wanachama wa Yanga," amesema Dk.Msola.

  Akizungumzia suala la madeni ya mishahara kwa wachezaji, Msola amesema Madeni waliyoyakuta toka mwezi wa 5 walivyoingia ni pamoja na deni la serikali(TRA,Ardhi)  mil 800, fedha za usajili za wachezaji  kwa miaka miwili nyuma mil 250.

  Amesema, madai ya makocha waliokowepo akiwepo Hans Van De Pluijm ni Milion  100, deni la golikipa Rostand mil 60, Donald Ngoma,Obrey Chirwa zaidi ya mil 100.

  Mapato ya Yanga toka wameingia kutoka kwa wadhamini ni Bilioni 2.2 wakati matumizi ni bil 4 na  mishahara imekwama kwa sababu ya michezo ya CAF ilianza mapema kuliko ilivyotegemewa kwa hiyo ikaharibu bajeti.

  Yanga imekuwa inasuasua katika kulipa mishahara kwa wachezaji na kupelekea kuwa na migomo ya mara kwa mara kaa wachezaji.

  0 0

   Bi Godfrida Mwashitete  mkazi wa Kijiji cha Ikumbilo Ileje akiwa njiani kurukdi kwake baada ya kupata msamaha wa Mhe.Rais 2019.
   Baada ya kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais katika gereza la Ileje raia hawa wakijiandaa kurudi makwao ili kuungannana familia zao.
   Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndg.Joseph Mkude aliyevaa suti ya bluu na tai nyekundunda akizungumza na waliopata msamaha wa Rais akisisitiza maagizo ya r
  Waliokuwa wafungwa katika Gereza la Ileje wakisubiri kurusiwa kurudi kwao baada ya kupata msamaha wa Rais 2019.

  Na:Daniel Mwambene Ileje

  Wafungwa 15 Wilayani Ileje mkoani Songwe wamenufaika na msamaha wa Rais alioutoa wakati wa sherehe za Uhuru 2019 huku Mkuu wa Wilaya akiwataka kuzingatia maagizo ya Mhe.Rais Magufuli.

  Ikiwa ni asubuhi tulivu iliyojaa mawingu yanayodondosha matone madogomadogo jumla ya wafungwa 15 wakiwemo wanaume 14 na mwanamke mmoja wamejikuta wakiachiwa huru mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo akiwa na Kamati ya Ulinzi pamoja na vyombo vya habari.

  Tukio hilo lililofanyika ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuwachia wafungwa waliokuwa na sifa ili kurudi uraiani kuunganana na jama zao.

  “Msiende kuwa wanyonge kwasababu mmetoka gerezani,nendeni mkapambane na maisha na kuhakikisha kuwa mnainua hali zenu na kuwa mfano wa kuigwa na jamii”alisisitiza Ndg.Joseph Mkude Mkuu wa Wilaya ya Ileje.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hiz wakiwa njiani kuelekea makwao baadhi yao waliipongeza serikali kwa kufanya hivyo wakiahidi kwenda kuwa raia wema.

  Godfrida Mwashitete mwanamke pekee aliyeachiwa siku hiyo alisema kuwa,katika maisha haitakiwi kurahisisha mambo kwa kuvunja sheria hali aliyoielezea kuwa mkono wake ukikupitia unaweza kufungwa na kujikuta unaachana na maisha ya uhuru.

  Aliongeza kuwa anamshukuru Rais na watendaji wake wote waliofanikisha yeye kuachiwa ili akaungane na familia yake aliyoachana nayo kwa takribani mwaka mzima.
  Shida Mbughi alifurahia kuachiwa akimpongeza Mhe.Rais kwakuwa hakutegemea kuwa msamaha kama huo ungemwangukia yeye pia akisema anaenda kuwa raia mwema.  0 0

  Jumla ya Wafungwa 293 kutoka magereza Ya Ukonga, Keko,Segerea na Wazo Hill  jijini Dar es salaam leo wameachiwa huru kwa Msamaha wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alietoa Msamaha kwa Wafungwa 5,533 waliokuwa wakitumikia kifungo kwenye magereza mbalimbali Nchi nzima.

  Wafungwa hao wameachiliwa huru leo Mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Abubakar Kunenge, Kamanda Wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam ambapo Kwa pamoja wamewataka walioachiliwa huru kwa msamaha wa Rais kuhakikisha hawarudii kufanya makosa.

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Kamishina Msaidizi wa Magereza Julius Mtambala amesema kati ya Wafungwa hao 293 walioachiliwa huru 130 wanatoka Gereza la Ukonga,54 Gereza la Keko, 74 Gereza la Segerea na 35 wanatoka Gereza la Wazo hill.

  0 0

  Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (wa pili kulia) akibadilishana nyaraka na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude, baada ya kuingia makubalianao ya mpango wa pamoja wa kutoa huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi, katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji - TTCL, Mruta Hamis. Picha zote na Othman Michuzi.
  Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akishuhudia uzinduzi wa huduma ya kuhamisha fedha kati ya SimBanking na T-Pesa uliofanywa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude
  Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (aliyesimama) akizungumza jambo wakati akiongoza hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na wa TTCL wakifatilia hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 

  Na Ripota Wetu.

  Benki ya CRDB na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo wamezindua mpango wa pamoja kupitia huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema mpango huo unalenga katika kuwarahisishia wateja kuhamisha fedha kutoka akaunti za CRDB kwenda T-Pesa, kuhamisha fedha kutoka T-Pesa kwenda akaunti yoyote ya CRDB pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia Simbanking.

  “Lengo letu ni kuwapa wateja wetu uzoefu bora zaidi pindi watumiapo huduma ya SimBanking. Tunataka kuona mteja akiingia kwenye SimBanking USSD kwa kupiga *150*03# au SimBanking App aweze kumaliza mahitaji yake yote ya kifedha ‘One Stop Shop’ ikiwamo miamala ya T-Pesa,” alisema Raballa.

  Raballa alisema ushirikiano huo na TTCL utataidia kusogeza huduma kwa watanzania wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini. Takwimu zinaonyesha ni asilimia 60 ya watanzania ndio wameunganishwa na mfumo wa kifedha kupitia simu za mkononi, wakati ni asilimia 17 tu ya watanzania ndio wanaotumia huduma za kibenki.
  “Benki ya CRDB inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Watanzania wengi wanapata huduma za kifedha, hatua ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wetu wa taifa letu. Tunafurahi kushirikiana na TTCL katika kufanikisha azma hii "aliongezea Raballa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa T-Pesa, Lulu Mkude, alisema ushirikiano huo ni mafanikio makubwa kwa TTCL, kwani utawawezesha maelfu ya watanzania wote wa mijini na vijijini kupata huduma za kifedha za kwa urahisi.

  Lulu alisema TTCL kuunganishwa kwa huduma ya T-Pesa na SimBanking kutawasiaidia wateja wa Benki ya CRDB kuweka pesa kwa urahisi kwenye akaunti zao kupitia T-Pesa lakini pia kuongeza salio au kuwatumia ndugu jamaa na marafiki fedha kwenye akaunti zao za T-Pesa.

  ''Kufurahia huduma mteja atatakiwa kuingia katika menu ya T-Pesa kwa kupiga *150*71#, na kisha kuchagua huduma ya SimBanking,” alisema Lulu Mkude, huku akisisitiza kwamba hivi sasa TTCL imejipanga vilivyo kusogeza mawakala wake wa T-Pesa karibu zaidi na wananchi hususani vijijini ambapo kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha


  0 0

  Baadhi ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli wakiagana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kulia) Desemba 10, 2019 mara baada ya kuachiwa kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
  Sehemu ya Wafungwa 136 kutoka  mkoa wa Simiyu  waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  wakiwa tayari kuondoka katika Gereza la Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada  ya kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
  Sehemu ya Wafungwa 136 kutoka  mkoa wa Simiyu  waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  wakishuka kwenye magari yaliyowasafirisha kutoka magereza mbalimbali mkoani Simiyu kuwaleta Gereza la Bariadi, Desemba 10, 2019  kwa ajili ya kuruhusiwa kurejea majumbani kwao kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Desemba 10, 2019  mara baada ya kuwaachia  wafungwa 136 kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.

  Bw. Buluba George miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa msamaha huo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019
  Baadhi ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli wakiagana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kushoto) Desemba 10, 2019   mara baada ya kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
  Bw. Musa Lazaro miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa msamahahuo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019 
  Baadhi ya wafungwa wakitoka katika gereza la Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada ya kuachiwa huru kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza. PICHA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA SIMIYU  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
  WATU wanne wanaotuhumiwa kuwateka nyara watoto wawili na kudai fedha kiasi cha sh. milioni mbili wamekamatwa na polisi baada ya kutuma ujumbe wa vitisho kwenye simu ya mama wa watoto hao ambao ni wa familia moja.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa (pichani) alisema kuwa watu hao walikamatwa baada ya kutumiwa kiasi cha fedha.

  Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi huko Bwilingu wilaya ya kipolisi Chalinze watoto wawili mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (8) na mwingine wa kiume (5) ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Bwilingu.

  "Tulipata taarifa kupotea kwa watoto hao tarehe 5 Desemba na tulianza kufuatilia kwa mitandao ya simu iliyoonekana kutuma ujumbe kwa mama wa watoto hao Claudia Fute simu hiyo yenye namba 0715 648672 iliyosajiliwa kwa jina la Subira Kasenga," alisema Nyigesa.

  Alisema kuwa simu hii ilituma jumbe nyingi za vitisho kwa mama mzazi na kutaka atumiwe fedha haraka kiasi hicho vinginevyo angewadhuru watoto hao na kuwafanya lolote hata kuondoa uhai wao.

  "Kwa kutumia namba hiyo pia tulibaini namba nyingine ya Farida Gabriel iliyokuwa ikisisitiza mtekaji aendelee kushikilia watoto kea sababu pesa itatumwa tu na kumsisitizia Kasenga kuwa akomae kwani mama wa watoto anatafuta fedha atume," alisema Nyigesa.

  Aidha alisema kuwa katika kuhakikisha wanafanikisha katika kufanikisha kukamatwa wahusika walituma kiasi cha shilingi 400,000 kwa mtuhumiwa na ndipo wakati akitoa alikamatwa na polisi.

  "Watuhumiwa waliokamatwa ni Husna Hussein Mwinyigoha (18) ambaye ndiye aliyeteka watoto akitumia jina la Subira pia namba yake nyingine ni 0693838511 na 0719648672 iliyosajiliwa kwa jina la Subira Kasenga,Farida Gabriel (34) mwenye namba ya simu 0716461161 na 0784641456, Said Thomas mwenye namba 0692986611 na Miraji Mrisho Mbega," alisema Nyigesa. 

  Alibainisha  watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika ili wajibu tuhuma zinazowakabili za utekaji watoto hao wadogo.

  0 0

  Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru amewaongoza wadau wa haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huku akivitaka vyombo vya usimamizi wa sheria kuzingatia usawa na haki dhidi ya kesi zinazohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  Kilele cha Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Kauli Mbiu ya “Kizazi chenye Usawa : Simama Dhidi ya Ubakaji” kimefanyika leo Desemba 10,2019 katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack. Akizungumza, Otaru alisema ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni vyema vyombo vya usimamizi wa sheria ikijumuisha jeshi la polisi na mahakama kuzingatia haki na usawa katika maamuzi ya kesi zinazokiuka haki za Wanawake na Watoto Otaru alitumia fursa hiyo pia kuitaka jamii kuachana na mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili huku akitaka kuwepo kwa nguvu ya pamoja kupinga ndoa za utotoni zinazosababisha watoto kutopata haki ya elimu. "Bado kuna changamoto ya uwepo na mila na desturi ya ndoa za utotoni pamoja na kukosekana na usawa wa umiliki mali. Ni wakati sasa jamii kuachana na mila potofu zinazochochea ndoa za utotoni pamoja na imani za kishirikina zinazokandamiza ustawi wa wanawake na watoto",alisema Otaru. Alisema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kuzingatia haki za wanawake na watoto kwa kuwafichua wahalifu wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake pamoja na kuwashirikisha wanawake katika ngazi ya familia na ngazi mbalimbali za uongozi.
  Otaru alisema mkoa wa Shinyanga unaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akibainisha kuwa tayari mkoa umefanikiwa kuunda kamati 7 za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ngazi ya mkoa na wilaya pamoja na kamati 130 ngazi ya kata ambapo kati ya kamati 130, 51 zimepewa mafunzo na zimeanza kutekeleza majukumu yake.


  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la The Voice of Marginalized Society (TVMC),Mussa Jonas Ngangala alisema shirika lake limekuwa mdau mkubwa katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na tayari limeanzisha kamati 11 za MTAKUWWA ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga. 


  “TVMC inaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha tunamkomboa mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili,tunahamasisha jamii iwe na umoja ili kusaidia wananchi kuondokana na ukatili wa kijinsia”,alisema Ngangala. 


  "Tunaadhimisha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa, uzoefu kujenga uwezo wa pamoja. Katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia tunawaomba wadau kuunganisha nguvu na kubuni mikakati ya kijamii ambayo italeta suluhisho la kudumu” aliongeza Ngangala.


  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
  Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019 - 
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
  Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack ambapo alisema zinahitajika nguvu za pamoja ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
  Mkurugenzi wa Shirika la The Voice of Marginalized Society (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,Mfinanga John akitoa taarifa ya jeshi la polisi kuhusu kesi za ukatili wa kijinsia wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Maafisa wa polisi Dawati la jinsia na watoto mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Mkurugenzi wa Huheso Foundation Juma Mwesigwa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Wadau wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Wanafunzi wakitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Kundi la Ngoma za Asili  maarufu Mabulo ya Jeshi linaloongozwa na Msanii Wanzingiza likitoa burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Meza kuu wakifuatilia burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Burudani ya Ngoma ya Ununguli kutoka Bugimbagu ikiendelea.


  Msanii Wanzigiza kutoka Isela halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiimba wimbo maalumu wa kupinga ukatili wa kijinsia.

  Wanafunzi wakiwa kwenye maaandamano kuelekea katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga ambapo kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

  0 0

  Na Editha Edward, Michuzi TV, Tabora 

  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewasisitiza wafungwa Walionufaika na Msamaha wa Rais ya jamhuri ya muungano wa Tanzania alioutoa hapo jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru kuwa wautumie Msamaha wa Rais kwa kutenda mema katika jamii wanazoenda kujumuika nazo kwani walipokuwa katika magereza hayo walijifunza mafunzo mbalimbali ikiwemo useremala ujenzi uashi kilimo poa walijifunza heshima na maadili hivyo ni vyema kuutumia vizuri Msamaha hyo

  Mkuu wa gereza la uyui Omary Tensen amesema wafungwa hao Walionufaika kwa Msamaha wa Rais hapo jana kwa pamoja amewataka kuhakikisha hawarudi kufanya makosa hivyo wautumie fursa Hiyo kufanya kazi kwa bidii katika jamii zao ili kujikimu kiuchumi

  Sonda Deus ambae ni miongoni mwa wanufaika wa Msamaha wa Rais amesema anamshukuru mhe, Rais Magufuli kwa kuwakumbuka walioko magerezani na anafurahi kuachiwa huru na  kwenda kuungana na familia yake. 
  Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akizungumza leo na wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru.

   Mkuu wa gereza la uyui Omary Tensen akizungumza na wafungwa Walionufaika na Msamaha wa Rais

  Baadhi ya wafungwa Walionufaika na Msamaha wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wakiwa nje ya gereza tayari kwenda makwao

  Gereza kuu la Uyui la Mkoani Tabora


  0 0


  "

  0 0

  Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza akitoa maelezo kwa Bi.Graceous Gallet Afisa Mlinzi wa Walaji kutoka Tume ya Ushindani (FCC) wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye maonesho ya nne ya Bidhaa za Viwanda yaliyomalizika na kufungwa jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jiji Dar es salaam
  Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza akitoa maelezo kwa Bi.Graceous Gallet Afisa Mlinzi wa Walaji kutoka Tume ya Ushindani (FCC) na wenzake wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye maonesho ya nne ya Bidhaa za Viwanda yaliyomalizika na kufungwa jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jiji Dar es salaam

  Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza akitoa maelezo kwa Bi.Graceous Gallet Afisa Mlinzi wa Walaji kutoka Tume ya Ushindani (FCC) wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye maonesho ya nne ya Bidhaa za Viwanda yaliyomalizika na kufungwa jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jiji Dar es salaam

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu akielekeza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita uliofikia 86%. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.

  Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu, akiwa na Mhandisi kutoka Wizara ya Afya Eng. Mbuya, pamoja na Mhandisi kutoka TBA Eng. Glady Jefta wakikagua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) wakati wa ziara ya Waziri kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.  Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel pamoja na Mhandisi kutoka TBA Glady Jefta wakati wa ziara ya Waziri Ummy kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

  Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita uliofikia asilimia 86% kukamilika, unaotaraji kuanza kutoa huduma machi 31 mwakani.


  Na.Rayson Mwaisemba, WAMJW- GEITA

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la huduma za mama wajawazito na Watoto Mkoani Geita.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita ambayo imefika zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi

  “Habari njema kwa Wananchi, Serikali kupitia Wizara ya Afya tuna Bilioni 1.9 kwa ajili ya kujenga jengo la akina mama wajawazito pamoja na Watoto wachanga, tunakamilisha taratibu tayari kuanza ujenzi huo” alisema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy aliendelea kusema, Hospitali hiyo inajengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la upasuaji (thieta), jengo la mionzi (radiolojia), huku akisisitiza kuwa majengo hayo ya wodi yaliyokamilika yataanza kutoa huduma ili kuendelea kuwasaidia wananchi.

  Waziri Ummy amesema, Serikali tayari imepeleka Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa kituo cha Afya vya Katoro, ikiwa ni azma ya Serikali ya kuboresha huduma za Afya katika ngazi ya chini, ili kuzipunguzia mzigo Hospitali za Rufaa za Wilaya na Mikoa.

  “Tulianza kujenga vituo vya Afya zaidi ya 352 katika Halmashauri mbali mbali, muelekeo tunazungumzia huduma za Afya kwa wote, kupitia kuwekeza katika vituo vya Afya na Zahanati, ndio maana wiki iliyopita tulileta Milioni 800 kwa ajili ya kuongeza majengo katika kituo cha Afya Katoro na Buseresere” amesema Waziri Ummy

  Licha ya kuridhishwa na ujenzi huo, Waziri Ummy amemuagiza Mkandarasi kutoka TBA kuhakikisha unamaliza unakamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo mapema, huku akisisitiza ifikapo mwaka kesho Mwezi Machi 31, Hospitali hiyo ianze kutoa huduma za Afya kwa Wananchi.

  “Mipango ya Serikali, tunategemea ifikapo tarehe 31 Machi, nikija hapa anikabidhi Hospitali, sitokuja kukagua Hospitali, mimi nitatimiza wajibu wangu wa kutafuta fedha, nataka ifikapo tarehe hiyo tuanze kutoa huduma kwa Wananchi ” amesema.

  Aidha, Waziri Ummy, amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Geita kuwa ,Serikali imejipanga kuhusu Watumishi wataohudumu katika Hospitali hiyo, huku akiwatoa wasi wasi kuhusu upatikanaji wa vifaa vya kutolea huduma katika Hospitali hiyo.

  Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Geita.

  “Naomba niendelee kumshukuru Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutenga fedha katika Mkoa wetu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wanyonge, huu ni Mkoa mpya una watu wengi, na una changamoto nyingi, lakini changamoto zote Wizara imezichukua na kutekeleza” alisema

  0 0

  Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara Johansen Kahatano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA)akizungumza na Mabalozi wa Usalama barabarani RSA pamoja wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (PSCSO)wakiwa katika  stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam zowezi la Abiria Paza sauti katika.
  Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama barabarani John Seka akiteta jambo na Mkurugenzi wa udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA) Jahansen Kahatano katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Ubungo.
  Mkurugenzi wa udhibiti wa  Usafiri wa Barabara  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Jahansen Kahatano katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Ubungo.Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA,pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (PACSO)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
  Mkurugenzi wa Tafiti za kisheria  RSA Augustus Fungo akieleza wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso) kuja Tanzania bara kujifunza namna RSA inavyoendesha shughuli zao za usalama barabarani na namna ilivyofanikiwa kiutendaji
  Nuru Hatibu Hussein mkaguzi wa wamagari stendi kuu ya Mabus Ubungo akiwa anatoa ufafanuzi kuhusiana na majukumu yao ya kila siku katika stendi hiyo kabla na magari kuanza safari kuelekea mikoani.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Pemba Association for Civil Society Organization (PACSO )akizungumza mara baada ya zoezi la abiria paza sauti lililoendeshwa na Mabalozi wa usalama barabarani stendi kuu ya mabasi Ubungo na kuwashirikisha wageni kutoka Pemba.
  Majira Kafumu Mweyekiti wa umoja wa madereva wa mabasi makubwa nchini Tanzania UWAMATA akizungumza na mabalozi wa usalama barabarani pamoja na wageni kutoka PACSO
  Wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa RSA Taifa John Seka ,aliyepo kulia kwake ni Elias Xavier ambaye ni Mshauri Muelekezi kutoka Asasi ya Foundation for Civil Society( FCS)Kushoto kwake ni Katibu Umoja wa madereva wa mabasi makubwa Tanzania,wa pili kutoka kushoto ni mmoja kati ya wageni kutoka Pemba waliokuja kupata uzoefu namna RSA inavyoendesha sughuli zake.
  Picha baadhi ya wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)wakiwa katika  stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam zowezi la Abiria Paza sauti katika
  Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
  Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
  Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
  Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam.  Na.Vero Ignatus 

  Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)wameendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kutoa elimu kwa abiria kutoa taarifa pale wanapoona ukiukwaji na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani 


  Elimu hiyo inamsaidia abiria kutambua kuwa anatakiwa kuripoti vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama wake ,wa chombo pamoja na usalama wa anachosafiria,mwendokasi,ulevi wa dereva,upitaji wa hatari wa magari mengine bila kufuata sheria na alama za barabarani ,dereva kuzungumza na simu akiwa anaendesha,pamoja na kuripoti lugha chafu na uhasama kwa abiria 

  Akizungumza Mkurugenzi wa Udhibiti wa usafiri wa Barabara wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini(LATRA) Johansen Kahatano amesema utaratibu wa kufuatilia mwendokasi wa mabasi ya abiria haujasitishwa upo na unaendelea kutumika na wanaendelea kuwafuatilia wahusika na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

  Amesema kuwa kwa kushirikiana na Asasi za kiraia ambazo zinashughulika na masuala ya usalama barabarani ikiwemo RSA, zimekuwa msaada wa mkubwa kwani zimekuwa zikitoa elimu kwa abiria kufahamu wajibu wao wa msingi wawapo ndani ya chombo cha usafiri,katika kuripoti vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama wa gari na abiria kwa ujumla.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tafiti za kisheria  RSA Augustus Fungo amesema kuwa wa wageni hao walikuja Tanzania bara kujifunza namna RSA inavyoendesha shughuli zao za usalama barabarani na namna ilivyofanikiwa kiutendaji.

  Fungo amesema RSA ilipokea jumla ya wageni 21 kutoka Pemba kutoka kwenye muunganiko wa Asasi 93 ambapo zinaunda  PACSO ambapo zimekuja Asasi 14 kwaajili ya kubadilishana ujuzi hususani katika maswala ya mitandao.

  Akizumzia juu ya safari yao Mkururugenzi Mtendaji wa PACSO Mohamed Najim amesema wamejifunza mambo mengi haswa namna Taasisi ya RSA inavyofanya kazi kwa kwakujitolea na mooyo wa kufanya kazi kwa pamoja na utendaji kazi.

  Amesema wameshangazwa na utendaji kazi wa Askari namna wanavyokagua magari kabla hayajaanza safari jambo ambalo Zanzibar ni  nadra sambamba na abiria wanavyopewa uhuru wa kujieleza tofauti na Zanzibar wanaangalia zaidi wamiliki.

  ''Tukifika Zanzibar tunaenda kukaa na  kufanya mkutano na Chama cha Usafirishaji cha Pemba (PESTA)ili tuweze kuwashirikisha yale tuliyojifunza Tz bara kwajili ya mabadiliko''

  Kwa upande wake mkaguzi wa magari stendi kuu ya ubungo Nuru Hatibu Hussein amesema kuwa kazi yao kubwa ni kukagua magari kabla ya kuanza safari kuangalia mifumo yake injini,mwendo,gari litakalikutwa na linahitilafu wanaliweka pembeni kwaajili ya matengenezo,gari ambalo linahitilafu kubwa halitaruhusiwa kuendelea na safari badala yake wanawapa muda kisheria kwa masaa manne kurekebisha dosari zilizopo ikishindikana wanabadilisha gari au kurudisha nauli za abiria.

  Aidha amesema zipo changamoto kubwa wanazokabiliana nazo haswa wakati wa kukagua magari hayo kwani hakuna sehemu muhimu iliyotengwa kwaajili ya kukagulia magari hao ,bali inawaazimu kulala chini ya gari ili waweze kulikagua huku dereva akiwa ndani jambo ambalo wakati mwingine ni hatarishi kwa maisha yao.  

  Zoezi hilo la abiria paza sauti lilifanyika mwishoni mwa juma na kushirikisha Taasisi ya RSA,Asasi za Kiraia kutoka Pemba (PACSO)Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani pamoja na LATRA

  Sheria ya usalama barabarani ya mwaka sura ya 168 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 inamtaka kila mtumiaji wa barabara kufahamu sheria na kuelewa namna matumizi bora ya barabara kwa nia ya kuepuka kuvunja sheria pamoja na kuepuka ajali kutokana na matumizi mabaya ya barabara

  0 0


  Charles James, Michuzi TV

  PAUL Labile Pogba. Ni fundi haswa uwanjani, ni mchezaji ambaye kila Timu na kocha yeyote angetamani ammiliki kama mchezaji wake.

  Atakupa ubora mkubwa uwanjani, atakuza biashara ya Jezi zako na kuongeza idadi ya mashabiki.

  Ni sahihi kusema Pogba ni miongoni mwa wachezaji wenye mvuto wa kibiashara hivi sasa na ni miongoni mwa mastaa wa soka wenye nyota Kali pia.

  Kama hufahamu kinachoendelea hivi sasa kuhusu Labile Pogba wacha nikujuze kwamba mwamba amekataa ofa mpya iliyowekwa mezani na Manchester United.

  Mwanzoni ilionekana hafurahishwi na mbinu za kocha Jose Mourinho, alivyotimuliwa na kuletwa Ole Gunnar bado Pogba ameendelea kuonesha msimamo wake wa kutaka kusepa.

  Tatizo ni nini? Pesa? Hapana. Uhakika wa namba? Hapana. Pogba uhakika wa kucheza upo tena mkubwa tu. Nini tatizo? Hii ndio hoja ya msingi.

  Kabla ya mitikisiko ya Pogba kutaka kuondoka Golikipa wa Manchester United, David de Gea nae alitikisa kiberiti cha kutaka kuondoka kwa muda mrefu.

  De Gea hakua anahitaji mshahara mkubwa kama United walivyodhani, na yeye alichoshwa na maisha ya Old Trafford. Alihitaji changamoto mpya.

  Na hata sasa licha ya kusaini mkataba mnono bado anataka kuondoka hafurahii tena maisha ya United. Amechoka.

  Kwahiyo kinachofanywa na Pogba hivi sasa ni muendelezo wa kile ambacho kilianzishwa na De Gea.

  Bahati mbaya mashabiki na Uongozi wa United hawataki kuukubali ukweli kwamba mastaa wa timu Hiyo wamechoka kuendelea kuwepo hapo walipo.

  Gwiji la fasihi duniani, Chinua Achebe amewahi kusema, " Ukitaka kujua mvua imekunyeeshea kiasi gani basi ni lazima ukumbuke tone la kwanza lilikudondokea wapi,"

  United wanapaswa kukumbuka tone la kwanza liliwadondokea wapi. Maana hakuna kinachowatesa kama kuona wachezaji wakiwa hawana furaha na maisha ya Klabu yao.

  Duniani kama utataja Klabu za ndoto za wachezaji wengi basi ni Real Madrid, Manchester United na Barcelona.

  Leo inakuaje hawa akina Pogba wairingie Klabu yenye mataji mengi Uingereza? De Gea anaanzaje kuwadengulia mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya England?

  Timu yenye thamani kubwa England inaanzaje kuangaika kubembeleza wachezaji wawili watatu kusaini? Ni lazima tukubaliane kwamba lipo tatizo sehemu.

  Turudi katika msemo wa Chinua: Tone la kwanza la mvua lilianza kuwadondokea United mchana ule wa Mei 8, 2013.

  Hapa ndipo matatizo yote yalipoanzia, ubabe wao ulitia nanga hapa, hizi jeuri zote zimesababishwa na kuondoka kwa Kocha Alex Ferguson.

  Baada ya Ferguson kustaafu United walishindwa kuishi bila mzee huyu, wangeishije bila kocha aliyewapa mataji zaidi ya 30 katika kipindi cha miaka 27? Hakika ni ngumu.

  Na kosa lao ni kukataa kujenga upya timu, ukiangalia aina ya wachezaji ambao Fergie alikua nao sio 'quality' ya wachezaji wanaotakiwa hivi sasa kwenye soka la ushindani.

  Ferguson alikua na kikosi chake cha kawaida sana. Valencia, Ashley Young, Phil Jones, Smalling hii ndo ilikua aina ya wachezaji wake ambao leo kesho mashabiki wa United wanawaona mitumba ila walibeba ubingwa na Babu.

  Kubadilisha makocha mara kwa mara kumewaathiri pia, toka aondoke Fergie wameajiri makocha wanne tofauti.

  Mbaya zaidi wanawapa tageti ya ubingwa kila kocha anaekuja wakidhani ni rahisi. Soka limebadilika wanapaswa kuwekeza upya kwenye mfumo wa uendeshaji ili kurudisha mafanikio yaliyopotea.

  Wakiendelea kuamini wao ni Timu kubwa watabaki kumaliza msimu bila taji na wachezaji mastaa wataondoka maana hakuna mchezaji asietaka kutwaa ubingwa.

  Pogba anasisitiza kuondoka kwa sababu anaanza mwaka wa tano sasa na haoni dalili za kubeba ubingwa wa Ligi Kuu wala taji la Ulaya.

  Mipango chini ya kocha Ole Gunnar haimuoneshi mafanikio mbele. Anaitizama United kama Timu ya kawaida mbele ya Liverpool na Manchester City msimu ujao.

  Kwanini aendelee kubaki sehemu isiyo na mvuto na mataji? Kwanini asiende Madrid au kurudi Juventus akabebe mataji.

  TUFIKIE MWISHO

  Manchester United ni Klabu kubwa, wanahitaji kuyarudisha mafanikio yao ili kuvutia nyota wengi kujiunga nao.

  Kipindi cha Ferguson walifanikiwa kwa sababu ya ushawishi aliokua nao kocha mwenyewe na 'status' ya Klabu ilijieleza.

  Leo hii ni mwaka wa sita hawajabeba Kombe la Ligi Kuu, wanapita taratibu katika njia ambayo Liverpool wameteseka nayo kwa miaka 29 sasa bila EPL.

  Njia pekee ya kurudisha mafanikio katika Dunia ya sasa siyo kuwekeza pesa nyingi. Inawabidi wajitoe mhanga na kukubali kuanza upya.

  Wakidhani wana pesa na ukubwa wa Timu yao wakaendelea kusajili wachezaji wenye majina makubwa wakitegemea watapata mataji basi ndivyo watakavyozidi kulichimba kaburi lao wenyewe.

  Wakubali kuanza moja. Watafute Kocha ambaye anaweza kujenga Timu kutokea chini, wamvumilie bila kumpa presha ndani ya miaka mitatu minne watarudisha ubabe wao.

  Wanaweza kutetereka kibiashara lakini Hiyo ndio njia pekee ya kurudisha umwamba wao kwenye Ligi Kuu na UEFA, tofauti na hapo akina Pogba wataendelea kuwaringia sana tu.

  Liverpool walianza hivyo hivyo ikawachukua miaka 29 kuanza kurudisha makali yao. Arsenal huu ni mwaka wa 16 hawajui ladha ya EPL.

  Ukienda Italia, AC Milan toka wanyeeshewe na mvua wameshindwa kukumbuka tone la kwanza liliwadondokea wapi.

  Kuendelea kuamini mafanikio yao yataletwa na Ole Gunnar ni kujitekenya na kujicheka wenyewe. Kuzidi kuwa na Ed Wood kama Mkurugenzi wa Michezo ni tatizo lingine lenye uhusiano na kirusi. Period!

  0683 015145

  0 0


  Wafungwa waliopatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania wakiondoka katika gereza la Mbozi; Jumla ya waafungwa 96 Mkoani Songwe wamepata msamaha wa Rais Magufuli.

   Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akiwa katika gereza la Mbozi ambapo wafungwa 96 Mkoani Songwe wamepatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania
  Wafungwa waliopatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania wakiwa nje ya gereza la Mbozi kwa ajili ya kuondoka, Jumla ya wafungwa 96 Mkoani Songwe wamepata msamaha wa Rais Magufuli.

  ………………
  Wafungwa 96 Mkoani Songwe wamekuwa miongoni mwa wafungwa Zaidi ya 5000 waliopatiwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufuatia maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika jana jijini Mwanza.
  Mapema leo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amefika katika gereza la Mbozi ambapo wafungwa 45 wanapatiwa msamaha wa Rais huku wafungwa wengine wakiwa katika Magereza ya Wilaya za Ileje na Songwe ambapo amezungumza na wafungwa hao kabla hawapewa ruhusa ya kuondoka gerezani hapo.
  “Nimeingia gerezani na kukuta wafungwa waliopata msamaha wa Rais Magufuli wakiwa na furaha na wamempongeza sana Rais wetu, lakini pia wafungwa waliobaki wamefurahia uamuzi wa Rais Magufuli wa kutoa msamaha kwani na wao wana tumaini la kupatiwa msamaha siku za baadae.”, amesema Brig. Jen. Mwangela.
  Brig. Jen. Mwangela ameongeza kuwa wafungwa waliobaki wamempa changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matatizo ya uhaba wa maji na ucheleweshaji wa nakala za hukumu mambo ambayo ameahidi kuyashughulikia haraka iwezekanavyo.
  Kamishna Msaidizi wa Magereza Laizack Mfaume Mwaseba amesema amekuwa akipokea malalamiko ya ucheleweshaji wa nakala za hukumu kutoka kwa wafungwa na amekuwa akiwasiliana na mahakimu ili waweze kuzitoa nakala hizo kwakuwa ucheleweshaji huo unawanyima haki wafungwa ya kukata rufaa.
  Ameongeza kuwa pamoja na changamoto ya maji katika gereza hilo kuna changamaoto za uhaba wa vitendea kazi na sare kwa wafungwa mambo ambayo tayari wamesha yawasilisha kwa kamishana Mkuu wa Magereza kwa ajili ya utatuzi.
  Mmoja wa wafungwa wa gereza la Mbozi Victoria Adam amemshukuru Rais Magufuli kwa msamaha alio mpatia na kumuombea kwa Mungu aendelee kumlinda huku akieleza kuwa amejifunza mambo mengi alipokuwa gerezani na sasa anaenda kuwa raia mwema.
  Naye Fred Andrea Daud ambaye amepata msamaha wa Rais Maguufuli amesema bahati aliyoipata ya Msamaha ataitumia vizuri kwa kufanya kazi halali kwakuwa Vijana wengi wamekuwa wakichagua kazi ambazo zinawaingiza katika matatizo
  Ameongeza kuwa magereza ni sehemu ya urekebishaji na yeye amerekebika hivyo anawashauri vijana wote wafanye kazi halali ambazo hazitawaletea matataizo kwakuwa kazi halali zipo nyingi.

older | 1 | .... | 3276 | 3277 | (Page 3278) | 3279 | 3280 | .... | 3352 | newer