Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 325 | 326 | (Page 327) | 328 | 329 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt.Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima 
  Picha na Freddy Maro wa Ikulu.

  0 0

  KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),Bwana Jumane Sagini akiongea na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kusainiwa mkataba wa kusimamia mradi wa mabasi yaendayo haraka kati ya Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) na Kampuni ya Uholanzi ya REBEL Group jijini Dar es Salaam jana. Wengine kulia ni Kaimu Afisa Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo na Mshauri wa Masuala ya Fedha wa REBEL Group, Bw.Jeroen Kok (kushoto).
  Kaimu Afisa Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo(kulia) akibadilishana nyaraka za makubaliano na Mshauri wa Masuala ya Fedha wa REBEL Group, Bw.Jeroen Kok (kushoto) muda mfupi baada ya kusaini mkataba jijini Dar Es Salaam jana anayeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),Bwana Jumanne Sagini.


  0 0


  0 0

  Na Francis Godwin, Iringa 
   BASI mmoja limenusurika kuwaka moto na daladala moja imeteketea yote kwa moto leo wakati wanafunzi wa masomo ya welding  katika gereji moja eneo la uwanja wa Samora mjini Iringa wakijifunza kuunga ngao ya daladala hiyo yenye namba za usajili T189 AWN . 
   Tukio hilo limetokea leo majira ya 8.15  mchana wakati vijana wawili wanaojifunza kuunga wakiendelea na mafunzo ya kuunga ngao ya daladala hilo. 
   Akizungumzia ajali hiyo mmoja kati ya wafanyakazi wa gereji hiyo Filibert Mwihava alisema kuwa chanzo cha daladala hilo kuwaka moto ni vijana wawili ambao wanajifunza ufundi wa kuunga vyuma katika eneo hilo kufanya kazi hiyo bila kuzingatia kanuni ya kazi hiyo. 
  Alisema vijana hao walikuwa wakiunga ngao ya nyuma ya daladala hilo jirani na tenki la mafuta na kutokana na cheche zilizokuwa zikitoka zilisababisha moto kulipuka.
   Hata hivyo alisema lichaya kuwa na kifaa cha kuzimia moto bado walishindwa kukitumia kifaa hicho kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya kukitumia. Mwihava alisema kutokana na moto huo kushika daladala hilo linalofanya safari zake kati ya Tumaini na Zizi la Ng'ombe mjini Iringa hakuna mtu aliyedhurika zaidi ya basi lenye namba za usajili T 457 AMQ ambalo limetekea upande wa mbele kabla ya kuokolewa . 
   Pia alishukuru kikosi cha zimamoto na uokoaji mjini Iringa ambao walifika kwa wakati na kufanikiwa kuzima moto huo ambao ungeweza kusababisha madhara makubwa katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na ofisi maduka ya watu waliojenga kuzunguka uwanja wa Samora kuteketea.. 
   Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kiongozi wa askari wa zimamoto ambao walifika eneo hilo John Zacharia alisema kuwa kuwa chanzo cha moto huo ni uzembe wa ofisi hiyo. 
  Alisema hata kifaa cha zimamoto walichokuwa nacho kilikuwa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika muda mrefu, wakati  kifaa cha kuzimia moto kilichokuwemo katika daladala hilo ni  kidogo zaidi na maalum kwa gari dogo ambacho pia kilikuwa hakifanyi kazi. 
   Zacharia aliwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuzingatia sheria za zimamoto ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto badala ya kudanganya na kuona kama wanaonewa pale wanapolazimishwa kuwa na vifaa hivyo.
  Wananchi Iringa  mjini  wakilitazama daladala  lililowaka  moto wakati likiwa kwa mafundi welding  likichomelewa leo eneo la uwanja wa  samora
  Daladala  likiwaka  moto  huku kikosi cha zimamoto na uokoaji  wakizima moto huo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   4 Rooms (including 1 Master bedroom)
  2 Toilets
  1 Bathroom
  1 Kitchen
  1 Sitting room
  1 Dinning room
  1 Garage (car park)
  Area: 1/2 acre
  Located at Mbezi Msakuzi, Dar es salaam, 
  just 5km from Morogoro Road.
  Contact: 0717 589 011  0 0

  Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi Methusela Msebula kilichotokea juzi (Januari 13 mwaka huu) katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

  Mwamuzi Msebula ambaye alikuwa mwamuzi daraja la kwanza (class one) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, maradhi ambayo yalimsababisha kuwa nje ya uchezeshaji mechi za mpira wa miguu kwa karibu misimu miwili.

  Msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani, Msebula alitoa mchango mkubwa katika fani ya uamuzi nchini, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima. Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo (Januari 15 mwaka huu) nyumbani kwao Kanyigo, Bukoba mkoani Kagera.

  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Msebula, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

  Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

  Boniface Wambura Mgoyo
  Ofisa Habari na Mawasiliano
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi

  Kamishna wa Polisi Jamii Nchini, (CP) Mussa Alli Mussa, amewataka maofisa wa Polisi pamoja na askari kote nchini, kuhakikisha wanafanya kazi zao katika misingi ya uwazi na usasa, dhana itakayosaidia uenezi wa Polisi jamii/ulinzi shirikishi katika kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu.

  Kauli hiyo ameitoa jana wakati alipokutana na baadhi ya watendaji wa Jeshi la Polisi katika wilaya ya kipolisi ya Ilala, katika kikao cha pamoja kuhusiana na utendaji wa Polisi katika dhana ya Polisi jamii na namna ambavyo Jeshi hilo linavyoweza kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa pamoja na kushirikiana na wananchi na jinsi wanavyoshirikishwa.

  Kamishna Mussa, aliongeza kuwa, tangu kuanzishwa kwa Polisi jamii/ulinzi shirikishi, mafanikio makubwa yameweza kufikiwa kwani mpaka sasa makundi kadhaa ya uhalifu yameweza kugundulika na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuangamizwa ikiwa pamoja na  wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria, alisema.

  Hata hivyo, Kamishna Mussa, aliwataka wananchi  kuwathamini na kuwapa ushirikiano maofisa wa Polisi/Polisi Kata pamoja na vikundi vya Ulinzi Shirikishi hatua ambayo itasaidia  kukabiliana na matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali na kuifanya jamii kuishi kwa amani pasipo kuwepo kwa matukio hatarishi.

  Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Lazaro Mambosasa, alisema kuwa,  Jeshi l Polisi limejipanga katika kukabiliana na aina zote za uhalifu na kwamba alitamuonea ama kumdhurumu mtu yeyote katika kusimamia na kulinda usalama wa raia na mali zao.

  Mambosasa, ameongeza kuwa, kila askari katika nafasi yake anawajibu wa kuhakikisha kuwa, jamii inaondokana na uhalifu pamoja na matishiona huku akiwataka maofisa na askari kuwa na utayari katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia dhana ya Polisi Jamii/Ulinzi shirikishi, alisema.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa shirikisho la waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam,waliomtembelea ofisini kwake leo.Mh. Lowassa alikutana na viongozi hao kupanga utaratibu wa kufanya harambee ya kuchangia saccos ya shirikisho hilo.Mwezi Disemba mwaka jana,Mh Lowassa alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la bodaboda kwenye viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam ambapo aliahidi kukutana na uongozi huo kwa ajili ya kuandaa harambee ya kuwasaidia kumiliki pikipiki waendesha bodaboda wa Dar es salaam.

  0 0

  EAC Secretary General Amb Dr Richard Sezibera with EAC Deputy Secretary General incharge of Planning and Infrastructure Dr Enos Bukuku at the EAC-IMF Workshop on Fiscal Mgt of Oil and Natuarl Gas in EA.
  Group Photo EAC-IMF Workshop on Fiscal Mgt of Oil and Natuarl Gas in EA. 

  A three-day workshop on Fiscal Management of oil  and Natural Gas in East African organized by the East African Community together with the International Monetary Fund  (IMF) opened today at Mount Meru Hotel, in Arusha,Tanzania.

  The 15-17 January workshop is designed to discuss key issues that EAC governments face in managing the fiscal impacts of oil and gas development and emphasize how the issues and policy choices are interlinked. These relate to design of the fiscal regime (tax and non-tax instrument) and revenue collection; options for the macro-fiscal policy framework and fiscal anchor as well as institutional reforms to integrate natural resources revenues into the budget and credible medium-term frameworks.


  0 0


  0 0

   Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo amemkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakala ya vitabu vya hotuba zake alizozitoa kwa nyakati tofauti wakati wa uongozi wake wa miaka kumi.Pichani Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akikabidhi Rais Kikwete vitabu hivyo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.VitABU hivyo vimechapishwa na kampuni ya Mkuki na Nyota chini ya Mkurugenzi wake Bwana Walter Bgoya Picha na Freddy Maro.

  0 0
 • 01/15/14--12:59: mbwa wa polisi....

 • 0 0

  NA RAMADHANI ALI- MAELEZO ZANZIBAR 
  Wizara ya Afya ya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa makubaliano wa kuanzishwa kwa majaribio kutolewa huduma za maradhi ya afya ya akili katika Hospitali ya Makunduchi iliyoko Mkoa wa kusini Unguja. Uwamuzi wa kuifanya Hospitali ya Makunduchi kuanzisha huduma hiyo inatokana na mapendekezo ya Wizara ya Afya ya mwaka 2008 na taarifa ya Afya ya akili Zanzibar ya Jumuia ya Ulaya. 
  Wadau watatu wanashirikiana katika mpango huo ambao ni Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha Norway, Hospitali ya Afya ya akili ya Kidongochekundu na Mradi wa kuimarisha Afya Zanzibar. Katika sherehe za utiaji saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Wizara iliwakilishwa na Katibu Mkuu Dk. Mohammed Jiddawi, Chuo Kikuu cha Haukeland kiliwakilishwa na Dk. Ingavr Bjelland, Dk. Peter McGovern alitia saini kwa upande wa Mradi wa kuimarisha Afya kijiji cha Makunduchi na Dk. Khamis Othman alitia saini kwa upande Hospitali ya Kidongo Chekundu. 
  Wadau hao watatu watashirikiana katika kuimarisha kujenga uwezo huduma za maradhi ya Afya ya akili kwa visiwa vya Unguja na Pemba, kuanzisha mtaala wa kufundisha masomo ya afya ya akili wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) na kuunga mkono maendeleo ya mafunzo yanayotolewa kwa wauguzi wa Hospitali ya Makunduchi na Hospitali ya Kidongo chekundu. 
  Katika hatua za awali zitakazoanzia mwaka huu, kliniki ya afya ya magonjwa ya akili ya Hospitali ya Mkunduchi itasimamiwa kwa kiasi kikubwa na Hospitali ya Kidongo chekundu na mafunzo yatatolewa katika mwaka wa kwanza wa kuanzishwa huduma katika Hospitali hiyo. Hatua ya pili ya mpango huo itakayoanza mwezi Januari mwakani ambapo kliniki hiyo itakuwa imeimarika na Hospitali mama ya Kidongo chekundu kuridhika na hatua iliyofikia, Hospitali hiyo itaruhusiwa kujiendesha yenyewe katika masuala mbali mbali ya uongozi na tiba. 
  Kwa mujibu wa makubaliano hayo Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland itasimamia na kuimarisha mitaala ya elimu ya magonjwa ya Afya ya akili kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi ikiwemo kusimamia mafunzo hayo. 
  Wadau wote kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha huduma za magonjwa ya afya ya akili katika kliniki ya Makunduchi kwa mujibu wa misingi ya Shirika la Afya Duniani. Hospitali ya Makunduchi itakuwa ni ya pili kutoa huduma za magonjwa ya Afya ya akili kwa kisiwa cha Unguja na kwa Kisiwa cha Pemba huduma hiyo bado inaendelea kutolewa katika Hospitali ya Chake Chake tu.
    Dk. Ingvar  Bjelland kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland  nchini Norway akitoa maelezo jinsi  Hospitali hiyo itakavyotoa huduma ya magonjwa ya Afya ya akili Zanzibar katika sherehe za kutiliana saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jiddawi  na Dk. Peter McGovern  wakitia saini makubaliano ya kuanzisha huduma za Aya ya magonjwa ya akili katika Hospitali ya Makunduchi. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya akishuhudia utiaji saini  katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Dk. Ingvar  Bjelland kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland  nchini Norway na Daktari bingwa wa magonjwa ya akili wa Hospitali ya Kidongo chekundu wakitia saini makubaliano ya kuanzishwa huduma za magonjwa ya Afya ya akili katika Hospitali ya Makunduchi Kusini Unguja.

  0 0

  Funga mwaka ya Flora Mbasha mkoani 
  Tanga siku ya mkesha wa mwaka mpya

  0 0

  Faustine Ruta, Bukoba
  Alhamisi ya leo Daraja la Mto Kanoni linalounganisha Manispaa ya Bukoba na Wilaya nyingine na pia likitumika kama njia kuu ya kwenda Nchi jirani limezinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIAN MASSAWE. 

  Daraja hili lilikuwa kwenye ukarabati takriabni miezi nane sasa ambapo watumiaji wa vyombo vya moto walikuwa wakilazimika kupitia kwenye Barabara ya muda ya Nyakanyasi, Migera au Kashura kuingia katika Manispaa ya Bukoba.
  Limekamilika sasa. Pongezi kwa Tanroads Kagera na karibu Bukoba.


  0 0

   Mbunge wa Viti maalum Jimbo la Iringa akizungumza na wananchi hawapo pichani kuelezea kazi alizofanya katika jimbo la Iringa katika mkutano uliofanyika katika kiwanja cha Mwembetogwa.
   Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa ccm katika kiwanja cha mwembetogwa
  Baadhi ya wanachama vijana wa chadema waliorudisha kadi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ccm wilaya katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)
  =========  ========  ===========
  MBUNGE LITA KABATI AELEZA ALIYOYAFANYA HADI SASA KATIKA UBUNGE

  Na Denis Mlowe,Iringa
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rita Kabati ameeleza kazi mbali mbali alizozifanya katika jimbo la Iringa mjini ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi kilichoko jirani na chuo Kikuu cha Iringa(Tumaini).

  Kabati alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kuwa ataendelea kutatua  kero za wananchi wa Iringa mjini kila anapopata nafasi za kuwahudumia wananchi hao.

  Alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika utendaji na kuwa siku zote atawapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini na kuwa kuwa siku zote kwake atahakikisha anatenda zaidi na amekuwa akijenga hoja za kusaidia Jimbo la Iringa mjini na sio kutoa kejeli kwa serikali akiwa mbungeni .
  Akielezea mambo ambayo amepata kutekeleza alisema ni pamoja na kusaidia sekta ya elimu vitabu na kompyuta pamoja na kusaidia vikundi vya vikoba katika jimbo hilo la Iringa mjini kusaidia vijana katika harakati za kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha mashindano ya Kabati Star Search.

  Kwa upande wake katibu wa CCM Iringa mjini Hassan Mtenga alisema yeye alikuwa jimbo la Freeman Mbowe ambae sasa anatangaza kutogombea jimbo la Hai.

  Alisema zama za ubunge wa Mchungaji Peter Msigwa katika jimbo la Iringa mjini umekwisha na sasa atake ataondoka na asipotaka ataondoka.

  "Mwambieni mbunge Msigwa wakati  wa kuwadanganya wananchi umekwisha  na lazima sasa awaeleze wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  wapi  anapelekea fedha za mfuko wa  jimbo ambazo  zinatolewa kila mwezi na Rais Jakaya  Kikwete"

  Hata  hivyo alimuagiza meya  kupambana ili  fedha  kiasi cha Tsh milioni 15  zinazotolewa na rais Kikwete kuona zinafanya kazi gani katika ofisi ya mbunge  pia kutembelea  Hospital  na vituo vya afya  ili  kuona changamoto mbali mbali ndani ya wiki tatu kupeleka majibu katika ofisi yake.

  Aidha aliwataja  vijana  kuleta maendeleo  ya mji wa Iringa na sio vijana  wa kutumiwa kuvuruga maendeleo ya mji wa Iringa.

  " Nawaombeni  wananchi  kuwa tayari  tumemshika pua mbunge Msigwa na naomba  wananchi tusaidiane kumnywesha panado na ninamuomba  Msigwa fedha za kiinua mgogo  zake asije  tena katika jimbo la Iringa mjini atumie  kwa kazi nyingine  ....tumeanza mkakati  huu kwa ajili ya kumng’oa Msigwa

  0 0

  Tungependa kukukaribisha kwenye huduma yetu ya Usafiri jijini kwa kutumia mabasi maalumu kwa sababu kuu tatu au zaidi.

  1. Tunaamini wafanyakazi wanaotumia muda mrefu njiani kwa kutafuta usafiri, au kwa kukwama kwenye foleni wakati wakielekea makazini, huwa wanafika wamechoka tayari na hivyo kupelekea kuwa na umakini wa kiwango cha chini pamoja na kupunguza uzalishaji.

  2. Kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakati ukiendesha gari, inaaminika kuwa ni mazingira yanayosababisha kiwango cha juu sana cha msongo, na ni sababu ya watu wengi kutokuwa na furaha kwa muda mwingi wawapo makazini.

  3.Gharama za kuendesha gari kwa siku moja kwenye jiji la Dar es Salaam, kwenda kazini na kurudi zinakisiwa kuwa zaidi ya Tsh. 30,000/= kwa gari ya kawaida yenye viti vitano. Hii inamaana kuwa kwa kila kiti kimoja cha gari lako, kinakugharimu Tsh. 6000/=. Endapo unatumia kiti kimoja tu cha gari lako, inamaanisha unapoteza Tsh. 24,000/= kwa kila siku unapotumia gari lako kwenda kazini, kwa siku 20 za kazi ni sawa na Tsh. 480,000/= na ni zaidi ya Tsh. 5,760,000/= kwa mwaka zinazopotea kwa wewe kuendelea kutumia gari lako binafsi kwenda kazini na kurudi.

  Kampuni ya City Ridez Travels & Tours ingependa kukuletea suluhisho la matatizo haya kwa ujumla wake. Lengo letu ni kupunguza idadi ya magari binafsi yanayotembea muda wa kwenda na kurudi kazini kwa kukuletea usafiri maalumu, wenye starehe, wakutegemewa na kwa gharama nafuu.

  Hapa City Ridez Travels & Tours tunahusika na usafiri maalumu wa mabasi, kwa minajili ya kutoa njia mbadala ya kusafiri ukiwa ndani jiji. Kimsingi tukizingatia zaidi kwenye Ubora, Uaminifu na Usalama.HABARI ZADI BOFYA HAPA.  0 0

   Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, George Liundi wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho

   Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi, wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

   Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakitafakari msiba huo wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Picha na OMR.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Winch Energy Tanzania akiwasilisha mada mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (aliyekaa upande wa kulia) kwenye ukumbi ulioko kwenye ofisi  za Wizara ya Nishati na Madini. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kampuni ya Winch Energy Tanzania kutambulisha majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme wa nishati ya jua.
  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter  Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.


  0 0

  Baadhi ya dawa zinazodaiwa ni feki


  TANGU kuanzishwa kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza, kumekuwa na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wakulima wanaingia kwenye kilimo cha kisasa.

  Juhudi hizo zimetiliwa nguvu zaidi katika kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo ili kuwafanya wakulima kuzitumia na kuimarisha kilimo chao.
  Baadhi ya dawa zinazodaiwa kuwa feki

  Pamoja na juhudiz hizo za serikali, bado kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wakulima juu ya pembejeo hizo za kilimo, ambapo zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuharibu mazao.

  Kwa mfano, mboleo ya Minjingu imekuwa ikilalamikiwa na wakulima kwa kile kinachoelezwa kukausha mazao yao na kutokuwa na virutubisho vya msingi kwa ajili ya ukuaji wa mazao.

  Katika kuonyesha kuwa kuna matatizo ya msingi katika kupatikana kwa dawa na mbolea kwa ajili ya mazao ya wakulima, kelele nyingi zimekuwa zikisikika pia bungeni kulalamikia mbolea na dawa feki.  Katika Bunge lililopita baadhi ya wabunge waliitaka serikali kushughulikia malalamiko ya wakulima kutokana na mbolea na dawa zinazosambazwa na mawakala kutokuwa na ubora.

  Wabunge hao walieleza kuwa pamoja na serikali kuhamasisha wakulima kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza lakini kumekuwa na tatizo la mbolea na dawa hizo kutokidhi viwango na matokeo yake kuua mazao.  Katika kujibu malalamiko ya wabunge, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwahi kueleza kuwa serikali inafanyia kazi malalamiko ya dawa na mbolea ya Minjingu.

older | 1 | .... | 325 | 326 | (Page 327) | 328 | 329 | .... | 3348 | newer