Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 326 | 327 | (Page 328) | 329 | 330 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Rais wa Chama cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) Injinia Peter Chisawillo akizindua rasmi utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS Mobile System) kuhusu madhara yatokanayo na urejeshwaji wa ada za biashara kila mwaka kwa lengo la kuishawishi serikali kuweka sera, sheria na taratibu rafiki kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini leo jijini Dar es salaam.
  =======  ======  =========
  TCCIA YAZINDUA UTAFITI KUKUSANYA MAONI YA WAFANYABIASHARA KUHUSU ATHARI ZA UREJESHWAJI WA ADA YA LESENI ZA BIASHARA.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  16/5/2014, Dar es salaam.

  Chama cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua rasmi utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS Mobile System) kuhusu madhara yatokanayo na urejeshwaji wa ada za biashara kila mwaka kwa lengo la kuishawishi serikali kuweka sera, sheria na taratibu rafiki kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini.

  Akizungumzia utafiti huo leo jijini Dar es salaam Rais wa cha hicho Injinia Peter Chisawillo amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 serikali ilitangaza urejeshwaji wa ada ya leseni za biashara nchi nzima na kuongeza kuwa utaratibu huo unaomlazimu mfanyabiashara kukata leseni na kuilipia kila mwaka unakwenda kinyume na sheria ya leseni ya mwaka 1972.

  Amesema kuwa sheria hiyo na hasa marekebisho yake ya mwaka 2004  yaliwezesha leseni za biashara kutolewa bure na mara moja tu kwa kipindi cha maisha yote ya biashara jambo ambalo linakiukwa.

  “Tayari kuna malalamiko mengi kwa jumuiya ya wafanyabiashara yanayotufikia kutoka kuanzia ngazi za wilaya na mikoa juu ya urejeshwaji wa ada hiyo, sekta binafsi inailalamikia serikali kwa kutoishirikisha katika urejeshaji wa utaratibu huu ambao unaiathiri sekta hii moja kwa moja” amesema Injinia Chisawillo.

  Ameeleza kuwa sekta binafsi inaamini kuwa serikali imeamua kuongeza mapato bila kuzingatia nia ya urasimishaji wa sekta isiyo rasmi kwa lengo la kuharakisha uchumi kwa ujumla na kuongeza kuwa hakuna mwongozo maalum uliotolewa na serikali kuelekeza namna maombi ya leseni yatakavyoshughulikiwa.

  Amesema sekta binafsi inaamini kuwa ili kuondoa urasimu na usumbufu kwa wafanyabiashara pindi wanapoomba leseni kila mwaka , serikali itumie kumbukumbu zilezile kila mwaka bila kulazimu mfanyabiashara  kufuata mlolongo wa taratibu za kuomba leseni kila mwaka kwa lengo la kuokoa muda na kupunguza kupanda kwa gharama za uendeshaji wa biashara.

  Aidha Injinia Chisawillo amesema kuwa utafiti huo unaofanywa na TCCIA) utafanyika kwa muda wa wiki 4 ukiwahusisha wanachama wote  takribani 22,000 (Elfu Ishirini na mbili) na wale wasio wanachama na unafadhiriwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la BEST –AC ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu zao kwenda namba 15539  na kutoa maoni kuhusu urejeshwaji wa ada hiyo

  0 0

   Mtoto mkubwa wa Marehemu JAji George Bakari Liundi, ndg. Taji Liundi na Mkewe wakiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Baba yao,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo kwenye Makaburi ya Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. 
   Mke wa Marehemu Jaji George Bakari Liundi akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mumewe wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo kwenye Makaburi ya Chang'ombe jijini Dar leo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  The East African Legislative Assembly (EALA) resumes business next week in Kampala, Uganda where it shall be holding its first Plenary this year. The Plenary which takes place from Monday, January 20th, 2014 to Thursday, January 30th, 2014 is the Fourth Meeting of the Second Session of the Third Assembly.

  The President of the Republic of Uganda, H.E Yoweri Museveni is expected to address a Special Sitting on Tuesday, January 21st, 2014.

  The Assembly which shall be presided over by the Speaker, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa expects to debate on the following Bills and deliberations:

  EAC Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2012
  EAC Integration (Education) Bill, 2014
  EAC Supplementary Appropriation Bill, 2014
  receive and consider reports from various Committees of the Assembly
  consider Motions and Questions brought before the House.

  EALA is also expected during the period to receive and meet different stakeholders as part of its representative activities.

  The East African Legislative Assembly is the Legislative Organ of the East African Community. Its Membership consists of a total of 52, of whom 45 are elected Members (9 from each Partner State) and seven ex-officio members (the Ministers responsible for EAC Affairs from the Partner States, the Secretary General of the Community and the Counsel to the Community).

  The East African Legislative Assembly has legislative functions as well as oversight of all East African Community matters.  The enactment of legislation of the Community is effected by means of Bills passed by the Assembly and assented to by the Heads of State, and every Bill that has been duly passed and assented to become an Act of the Community and takes precedent over similar legislations in the Partner States.

  EALA has recently launched its second Strategic Plan (2013-2018). The formulation of the Strategic Plan was an all-inclusive process involving the EALA Commission, Members, staff and other stakeholders.

  The Strategic Plan has six main strategic issues:
  1.    EALA’s main Administrative Autonomy, Capacity and Efficiency
  2.    Negotiations for the EAC Pillars of integration
  3.    EALA’s Corporate image, institutional status, growth and development
  4.    Capacity building in regional Parliamentary Practices
  5.    Effective, sustainable and Results-oriented communication and sensitization on
         EAC integration
  6.    Robust and effective Monitoring and Evaluation.

  0 0

  Shkamoo Ankal. 
  Hongera sana kwa kutusuza nyoyo na blogu jamii. Ankal. Kuna mtu aliniagiza simu mbili za Blackberry toka Marekani, ambazo baada ya kununua akaniambia nimpe kwanza alafu atanilipa baadae. Nimekataa kumpa na sasa nauza hizi simu ambazo ni mpya na original toka Marekani. Naomba mwenye interest ani contact. Hizi simu ziko kwenye orginal box zake nilinunua toka Blackberry $699. Sitaki faida, nataka tu hela zangu. Mwenye kuzihitaji tuwasiliane kwa email hii  
  mbezi1980@yahoo.com


  0 0

  Tamasha la filamu la Nchi za Jahazi - ZIFF linatangaza kuwa tarehe za kufunga kupokea filamu zitazoshindana katika kinyanganyiro cha ZIFF2014 ni tarehe 31 January, 2014, hii ikiwemo pia filamu za Kiswahili (Bongo Movies)
  Mashindano yamo katika nyanja tofauti pamoja na:

  1. Filamu Bora ya Tamasha (Golden Dhow)
  2. Filamu ya pili kwa ubora (Silver Dhow)
  3. Documentary Bora (Golden Dhow)
  4. Documentary ya Pili kwa ubora (Silver Dhow)
  5. Filamu Fupi Bora (East Africa Talent Award)
  6. SIGNIS Award (Best documentary)
  7. Verona Award (Best African Feature film)
  8. Sembene Ousmane Award (Best Development film $5000)
  ZUKU Awards
  1. Best Swahili Film (Tsh 1 mil)
  2. Best Swahili Film Actor (Tsh 500,000)
  3. Best Swahili Film Actress(Tsh 500,000)
  4. Best Camera
  5. Best Sound
  Haya shime tujitowe kimasomaso mwaka huu watanzania turudishe heshima yetu afrika mashariki.
  Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na filamu iliyoshinda kimataifa:
  FESPACO  - Arusi ya Mariamu, 1985- (Tuzo 12 kimataifa)

  Ikashinda tena FESPACO - Mama Tumaini (1987) Tuzo ya Unicef)
  Kenya na Uganda wakati huo bado wamelala!!
  ZIFF 2014 -Tarehe 14-22 June- ZANZIBAR.
   Tembelea www.ziff.or.tz kwa maelezo zaidi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kiteto baada ya kuwasili wilayani humo Januari 16, 2014 kufuatilia suala la mauaji ya wakulima.
  Eneo la Mtanzania wilayani Kiteto ambalo ni moja kati ya maeneo ya makazi yaliyovamiwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji ambapo watu watatu waliuawa na nyumba kuchomwa moto. Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitembelea eneo hilo Januari 16, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanakijiji wa Mtanzania Januari 16, 2013 wakati alipokwenda kuwapa pole kufuatia uvamizi waliofanyiwa na watu wanaosadikiwa kuwa wafugaji ambao waliua watu watatu na kuchoma nyumba . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.
  Baadhi ya wananchi wa Kiteto wakimsikiliza Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na kuchoma moto nyumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akiteta jambo na Mkurugezi wa Kampuni ya Weli Media nchini David Lee wa kwanza kulia, ugeni huo ulimtembelea Mheshimiwa Waziri kuomba eneo kwa ajili ya kufanyia Tamasha litakaloshirikisha wasanii kutoka China na Tanzania.Katikati ni Bwana Juma Mabakila Mkurugenzi wa Kampuni ya Optima Aviation Security Limited
  Mkurugezi wa Kampuni ya Weli Media nchini David Lee wa kwanza kulia akiongea na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara ambapo ugeni huo ulimuomba Mheshimiwa Waziri eneo kwa ajili ya kufanyia Tamasha litakaloshirikisha wasanii kutoka China na Tanzania Katikati ni Bwana Juma Mabakila Mkurugenzi wa Kampuni ya Optima Aviation Security Limited (Picha zote na Benjamin Sawe wa WHVUM).

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kuwajuilia hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman, pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya waliolazwa katika hospitali hiyo. 
  Viongozi  hao wamelazwa katika hospitali hiyo wakisumbuliwa na matatizo ya moyo. Wakizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais, wamesema wanaendelea vizuri na kwamba afya zao zinaendelea kuimarika siku hadi siku, tofauti na walipofikishwa hospitalini hapo. 
  Waziri Haroun anatarajiwa kupelekwa nchi Afrika ya Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewaombea viongozi hao wapone haraka ili waendelee na majukumu ya kulitumikia taifa.
    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimuombea dua  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman, alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Picha na Salmin Said, OMKR


  0 0

  MKURUGENZI wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba  (pichani) ameshinda kesi ya kukutwa na simu gerezani iliyokuwa inamkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 
  Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia mahakama kuhusu tuhuma hiyo. 
  Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuanzia saa 3:30 mpaka 4:20 asubuhi. Kusoma sakata hilo lote tembelea kwa Mjengwa BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Boniface Kanemba akifungua semina hiyo.
  Wadau.
  Mshiriki wa semina hiyo akiuliza swali.
  Washiriki wa semina.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Ofisa wa PPF akitoa mada.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Serikali Mtandao ambaye pia ni Makamu wa Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Dk. Jabir Bakari Kuwe (kulia), akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau, kuhusu usalama wa fedha kwenye mitandao ya simu pamoja na mkutano mkuu wa taasisi hiyo uliofanyika Dar es Salaam.
  Washiriki wa mkuitano huo.
  Dk. Carina Wangwe akitoa mada.
  Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Boniface Kanemba (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau, kuhusu usalama wa fedha kwenye mitandao ya simu pamoja na mkutano m.kuu wa taasisi hiyo uliofanyika Dar es Salaam.
   Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akitoa mada.
  Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Boniface Kanemba akizungumza na waandishi wa habari.
  --------------------------------
  WANANCHI wametakiwa kuepuka kugawa taarifa zao muhimu kuhusiana na mawasiliano yao ya simu pamoja na taarifa muhimu za kibenki.

  Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia ongezeko la wizi wa fedha katika akaunti za benki na simu za mkononi unaofanywa na matapeli hapa nchini.

  Rais wa Taasisi inayojishugulisha na Ukaguzi wa Mitandao ya ISACA Tanzania , Boniface Kanemba alisema kuwa matapeli hao wanaweza kutumia nambari za simu za mkononi na akaunti ya benki kujua namba za siri za kuchukulia fedha.

  Alisema kuwa ili kuepuka wizi wa aina hiyo ni vema wananchi wakachukua tahadhari dhidi ya utoaji wa taarifa kwa kuwa inakuw ani vigumu kuwakamata pindi wakishafanya uhalifu huo.

  Alisema kuwa matapeli wa aina hiyo walikuwa zaidi katika Kenya na lakini kwa sasa inaonekana wamevamia zaidi hapa nchini na kutumia ujuzi huo.

  Alisema kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki peke yake kiasi cha zaidi ya trilioni 80 zimeibwa kwa njia ya utapeli.

  Aliongeza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo tayari taasisi yake inaendelea na utoaji wa semina mbalimbali kwa wadau wa teknolojia ya mawasiliano na watu wa usalama kwa ujumla.

  "Najau wizi wa aina hii ulikuwa zaidi katika nchi za Ulaya na Afrika Magharibi na ukanda huu wa Afrika ya Mashariki ulikuwa zaidi Kenya lakini kwa sasa hawa matapeli wamevamia ukanda huu wa Afrika Mashariki na hali inazidi kuwa mbaya"alisema Kanemba.

  Taasisi hiyo ya ISACA ilianza kazi hapa nchini mwaka 2003 na imekuwa ikifanya ukaguzi wa usalama wa fedha na matukio mengine muhimu kwa njia ya mtandao.

  0 0

  Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  (kushoto) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema
  Mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  akihutubia leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema
  Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  (kushoto) akiendelea kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema

  Kwa picha na habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Sudan Mhe. Omar Al-Bashir, akiangalia Hati za utambulisho mara tu baada ya kuzipokea kutoka kwa Balozi  Dkt. Batilda Salha Buriani katika Ikulu ya Khartoum.
   Mhe. Rais Omar Al-Bashir akipeana mkono na Mhe. Balozi Batilda muda mfupi kabla ya kupokea rasmi Hati za utambulisho kutoka kwa Mhe. Balozi  kwenye ofisi za Ikulu ya Sudan
   Mhe. Balozi akimtambulisha  ndg. Nicholaus J. Mwakasege, afisa wa ubalozi wa Tanzania Nairobi kwa Mhe. Rais Omar Al-Bushir
   Mhe. Omar Al- Bashir akifanya Mazungumzo na Mhe. Balozi Batilda kwenye Ikulu ya Rais wa Sudan
  Kushoto ni Balozi Abdelbagi H. Kabeir, Mkuu wa Idara ya Afrika, Sudan pamoja na Mhe.Kamal Ismail Saeed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan wakiwa kwenye mazungumzo ya pamoja kati ya Mhe, Rais Omar Al-Bashir na Mhe. Balozi Batilda

   Mhe. Balozi Batilda akikagua Gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake kwenye  viwanja vya Ikulu ya Sudan
  Mhe. Balozi Batilda akiwa amesimama na Maofisa wa serikali ya Sudan wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Sudan zikiimbwa na bendi maalum kwenye viwanja vya Ikulu, Sudan.

  Mhe. Balozi Batilda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Tanzania walioko SUdan.

  0 0


  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA
  KANDA YA KASKAZINI

  (Tanga, Kilimanjaro, Arusha & Manyara)

  TAARIFA KWA UMMA

  WAGOMBEA WA UDIWANI - KANDA YA KASKAZINI

  Tarehe 15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini.

  Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.

  Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:

  JINA LA MGOMBEA
  KATA
  JIMBO
  MKOA
  BI. MWANAISHA MOHAMED OMARI
  KIOMONI
  TANGA DC
  TANGA
  BW. KAGOMA FRANK HENRY
  KIBORLONI
  MOSHI MJINI
  KILIMANJARO
  BW. ALLY BANANGA
  SOMBETINI
  ARUSHA MJINI
  ARUSHA
  BW. CHARLES SAMWEL MGATA
  PARTIMBO
  KITETO
  MANYARA
  BW. SANING’O KONE
  LOLERA
  KITETO
  MANYARA

  Katika uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao kwa kuzingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za wananchi zilizoletwa na CCM kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.

   Aidha chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe 15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya. Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.

  Hivi sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka. Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo halitaisha kirahisi hivi hivi.

  Niwaombe wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu tuunganishe nguvu zetu kwa sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na rasilimali zetu, ili tuwashughulikie CCM ambao wamekuwa wakiendelea kuwatesa Watanzania kwa sera zao mbovu na uongozi wa kihuni ambao haujali kabisa maisha ya Watanzania.

  Imetolewa leo tarehe 16 Januari 2014.
  Amani Golugwa
  Katibu wa Kanda ya Kaskazini
  +255 754 912 914 au 0784 343 275
  golugwa@gmail.com

  0 0

  Kundi la wafanyabiashara 15 kutoka Oman limewasili jijini Dar es Salaam ambapo inatarajiwa kuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal nyumbani kwake, Oysterbay baada ya Uzinduzi wa Baraza la Biashara baina ya Tanzania na Oman. 
   Wafanyabiashara hao ambao wanakuja nchini baada ya kuvutiwa na fursa zilizopo nchini ambazo zilielezwa vema na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa ziarani nchini humo aiwa na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini. 
   Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuwasili kwa ujumbe huo, mwenyekiti wa Baraza la Biashara nchini, Evarist Maembe alisema uzinduzi wa baraza hilo utaimarisha biashara baina ya nchi zote mbili na pia kuwaunganisha na Chama cha Wafanyabiashara wa nchi za Ghuba (Gulf Chamber). Alisema ugeni huo ambao pia utafanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda utakuwepo nchini kwa siku kadhaa ambapo ytatembelea Zanzibar na Bagamoyo na kufanya majadiliano ya kibiashara na wadau wa sekta hiyo nchini. 
   “Tutajadili jinsi ya kubadilishana watalaam wa fani mbalimbali za kilimo na kuangalia mahitaji ya wenzetu hao ambao kimsingi wangependa kuagiza vyakula kutoka nchini ambao ni karibu badala ya kufanya hivyo Israel ambako pia ni mbali kulinganisha na Afrika. 
   Maembe alisema hadi kufikia hatua hiyo ni kutokana na ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Oman ambayo iliwasisimua wafanyabiashara wa nchini humo ambao waliona kuna haja ya kuwa na mtandao wa ushirikiano na Tanzania ambako raia hao wa Oman wana uhusiano nako. 
   “Walivutiwa na ukweli kuwa tunaunganishwa na historia kwani wao wanaamini kuwa uku Tanzania hasa Zanzibar wana ndugu na jamaa zao ambao wapo huko na kikubwa zaidi ni kuwa kuna mwingilino wa tamaduni baina yetu na wao” Maembe alisema. 
   Alibainisha kuwa Oman wanatamani vitu vingi kutoka huku ikiwa ni pamoja na mbogamboga kama bamia, nyanya chungu na mazao mengine ambayo kwao hakuna lakini nchini yanapatikana na kikubwa zaidi wanayafahamu kutokana na mwingiliano wa kiutamaduni uliopo.
   Wafanyabiashara wa Oman wakiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe.  Ali Ahmed Saleh (wa tano kushoto) na mwenyekiti wa baraza la biashara Evarist Membe (wa tatu kushoto).
   Baozi wa Oman nchini, Mhe. Ali Ahmed Saleh (kulia) na mwenyekiti wa baraza la biashara, Evarist  Membe wakitoa maelekezo kwa wageni wao kabl;a ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere.
  Mwenyekiti wa Baraza la Biashara nchini, Everist Membe akiwapokea wafanyabiashara kutoka Oman 

  0 0


   Mgombea Uwakilishi Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki kwa Chama cha Wananchi CUF Bwa. Abdulmalik Haji Jecha 
  Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akimkabidhi Fomu za kugombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Bwa Abdulmalik Haji Jeche. fomu yake ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo alipofika Ofisi za Tume Maisara Zanzibar.

  0 0


   Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar  kupitia Chama cha CHADEMA Bwa. Hashim Juma Issa
  Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akitowa maelezo kwa Mgombea wa CHADEMA Bwa Hashim, alipofika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya MjiniMagharibi Maisara kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo lillilokuwa Wazi baada ya Mwakilishi wake kuvuliwa Uwanachama na Chama chake Mhe, Mansoor Yussuf Himid, mwaka jana 
   Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akimkabidhi Fomu Mgombea wa Uwakilishi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
   Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Hashim Juma Issa akisaini baada ya kupokea fomu hizo kutoka kwa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki

  0 0

  Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Suluhu Ali Rashid, akitowa maelezo kwa mgombea wa CCM alipofika kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi katika Ofisi za Tume Maisara. 
  MGOMBEA nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi mdogo wa  Jimbo la Kiembesamaki Bw. Mahmoud Thabit Kombo, akikabidhiwa Fomu ya kugombea nafasi hiyo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Suluhu Ali Rashid, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara

                        MGOMBEA nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi mdogo wa  Jimbo la Kiembesamaki Bw. Mahmoud Thabit Kombo akionesha fomu zake baada ya kukabidhiwa na Afisi wa Tume ya Uchaguzi

  0 0

  Habari za mchana ndugu wanahabari, 
  Tumewaita ili kutoa taarifa kwa wananchi juu ya tukio ambalo limetokea ndani ya Mkoa wetu ambalo kwa kiasi kikubwa linataka ufafanuzi kutokana na jinsi linavyozungumzwa huko nje. 
   Siku ya tarehe 13/01/2014 majira saa 9:55 jioni hapo Rahaleo kwa Mchina Tambi palitokea tukio la unyangani wa kutumia silaha. 
  Tukio hili lilitokea wakati Bw: SAID SEIF SALAMI 34, Riami wa RAHALEO ambaye ni MFANYA BIASHARA wa vyakula anayefanyia biashara yake Kibanda Maiti na anaishi mtaa wa RAHALEO alipofanyiwa unyanganyi huo. 
   Mfanya biashara huyu alifunga biashara yake majira ya saa 9:45 jioni ya siku hiyo ya tarehe 13/01/2014 na kuchukua pesa za mauzo ya kutwa jumla ya T.sh 11,500,000/= ambazo alizifunga katika bahasha /mfuko wa kaki na kuondoka nazo kuelekea nyumbani kwa kutumia gari yake no. Z. 128 EW NISSAN Rangi ya silver. 
  Alipofika maeneo ya Raha Leo Kwa Mchina Tambi ndipo gari moja yenye no. Z.866 EX aina ya SCUDO ilipomzinga kwa mbele na ghafla aliona watu watatu wametokezea wakiwa na silaha mbili, moja ikiwa ni bastola na nyengine ni SMG. 
  Watu hao walimlazimisha kwa usalama wake awape ule mfuko wenye pesa. Kwa kuhofia usalama wake alitoa pesa zote jumla ya T.SH 11,500,000/= Majambazi hao baada ya kitendo hicho cha kuchukua hizo pesa walikimbilia kwenye gari yao. 
  Kitendo hicho kilifanyika mbele ya watu ambao walianza kupiga kelele za mwizi!, mwizi!, mwizi!, kelele ambazo zilimfanya dereva wa gari ya majambazi kuondosha gari na kuwaacha wenzao watatu chini. Wakati huo wananchi walipiga simu Polisi huku juhudi za ukamataji zikiendelea. 
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam akionesha bastola iliyotumia katika uhalifu wa kumpora fedha mfanyabiashara katika maeneo ya rahaleo Zanzibar ikiwa na risasi zake kamili, ilihusika katika tukio hilo.
   Kamanda Mkadam akionesha moja ya Silaha aina ya SMG ambayo ilikuwa haina magazine waliokuwa wakiitumia watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Raha Leo na kuitupa katika eneo la msikiti wa Muembe Shauri wakati wakikimbia.
  Silaha zilizokamatwa na watuhumiwa wa ujambazi huo
  Kamanda Mkadam akiwaonesha waandishi moja ya silaha aina ya Gobole,waliofanikiwa Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa wakati akijiandaa kwenda kufanya uhalifu maeneo ya mtoni.  
  Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam, kuhusiana na uhalifu uliofanyika mwanzo mwa wiki hii katika maeneo ya Rahaleo na kumpora fedha shilingi milioni kumi na moja katika tukio hilo na polisi kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, kwa ushirikiano wa Wananchi wa kwahani. Picha na Othman Mapara

  0 0
 • 01/17/14--00:15: Article 24


older | 1 | .... | 326 | 327 | (Page 328) | 329 | 330 | .... | 3348 | newer