Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WATANZANIA KUNUFAIKA NA VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYA ITAKAYOZINDULIWA KESHO, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kesho Novemba 28, 2019 unatarajia kuzindua rasmi vifurushi vya bima ya afya ili kuwapa fursa wananchi wengi kujiunga na kunufaika na huduma za bima hiyo kulingana na mahitaji yao na kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya vifurushiaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema, vifurushi hivyo vinatoa fursa kwa mtu mmoja mmoja, familia au makundi mbali mbali ya wananchi kujiunga na huduma hizo.

"Mpango huu wa vifurushi utawezesha wananchi wengi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha na hivyo kukabiliana na gharama za matibabu ambazo garama yake imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na ambazo wakati mwingine kushindwa kuzimudu kwa wakati", amesema Konga.

Amesema, mpango huo wa Vifurushi vya bima ya afya unatoa uwanja mpana wa wananchi kujiunga na bima ya afya kwa kujipimia kulingana na mahitaji ya huduma, ukubwa wa familia na umri. Vifurushi hivi vimegawanywa katika makundi matatu yanayojulikana kama Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya.

"Kuanza kwa mpango huu kumekuja baada ya kuona uhitaji uliopa katika umma wa kuwa na uwigo mpana wa wananchi kujiunga na Mfuko huu. Hitaji la huduma hizi limedhihirika wazi baada ya kufanya majaribio ya mpango huu(Pilot test) mwezi Septemba mwaka huu kwa muda wa wiki tatu ambapo mwitikio ulikuwa mkubwa kutoka kwa wananchi. Tathmini ya majaribio hayo ilitoa nafasi ya kufanya maboresho mbalimbali ya mpango huu na sasa uko tayari kwa ajili ya kuletwa kwa wananchi," amesema 

Amesema viwango vya uchangiaji wa vifurushi hivi vinaanzia 192,000 kumezingatia hali halisi ya makundi yote na kutawezesha Watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko na kuwa na uhakika wa kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua hivyo kuondokana na changamoto za kukosa matibabu.

Aidha, uanzishwaji wa mpango wa vifurushi unawawezesha wananchi wengi zaidi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha. 

Hivyo, kutokana na maboresho haya, amesema wananchi wana fursa ya kukabiliana na gharama za matibabu ambazo zimekua zikiongezeka siku hadi siku na wakati mwingine kushindwa kuzimudu na kuangukia katika janga la umaskini au kifo.

"Kuanza kwa mpango huu ambao viwango vyake vya uchangiaji vinaanzia 192,000 kumezingatia hali halisi ya makundi yote na kutawezesha Watanzania wengi zaidi kujiunga na kuwa na uhakika wa kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua hivyo kuondokana na changamoto za kukosa matibabu," amesema

Aidha, uanzishwaji wa mpango wa vifurushi unawawezesha wananchi wengi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha. Hivyo, kutokana na maboresho haya, wananchi wana fursa ya kukabiliana na gharama za matibabu ambazo zimekua zikiongezeka siku hadi siku na wakati mwingine kushindwa kuzimudu na kuangukia katika janga la umaskini au kifo.

Amesema, vifurushi hivi vitasaidia wananchi wenye kujali afya zao na kuwa na uhakika wa kupata huduma mwaka mzima ambapo mwanachama atapatiwa kadi ya matibabu ya Mfuko ambayo ataitumia kupata huduma katika vituo zaidi ya 7,500 vilivyosajiliwa na mfuko nchini.

"Wanachama wa vifurushi hivi watanufaika na huduma za matibabu kuanzia ngazi ya zahanati hadi Hospitali ya Rufaa ya Taifa katika vituo zaidi ya 7,500 Tanzania nzima ikiwa ni vya Serikali, Binafsi na vya Madhehebu ya Dini. Aidha, mwanachama atakwenda ngazi ya Hospitali ya Kanda ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Taifa kwa utaratibu wa rufaa," amesema.

Amesema vifurushi vyote vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya vimezingatia upana wa huduma kwa mwananchi ikiwa ni kuanzia gharama za kumwona daktari, vipimo, dawa, kulanza, upasuaji mkubwa na mdogo, matibabu ya kinywa na meno na mengineyo. Ukubwa wa kitita cha mafao utazingatia aina ya kufurushi ambacho mtu atachagua..
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Bw. Bernard Konga akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika hilo zilizopo jengo la Ushirika jijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza uzinduzi wa vifurushi vipya vya bima ya afya vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya vitakavyozinduliwa kesho kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Kulia ni Baraka Maduhu Meneja Takwimu na Utafiti (NHIF) na katikati ni Bi. Angella Mziray Meneja uhusiano wa (NHIF)
 Meneja uhusiano wa (NHIF) Bi. Angella Mziray akizungumza jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ,kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Bw. Bernard Konga akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo mbaimbali wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mara baada ya mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.


TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA JPC NA NAMIBIA

Wadau wa Michezo wakutana kujadili mpango mkakati wa kuendeleza michezo nchini.

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
(katikati) akisisitiza jambo kwa wadau wa michezo wakati wakati wa kikao cha wadau hao kutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Leodger Tenga na kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa baraza hilo Bi. Neema Msitha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
(mwenye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa michezo wakati wa kikao cha wadau hao kutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuf Singo (kushoto) akitoa neno la
shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. HarrisonMwakyembe (kulia) wakati wa kikao cha wadau wa michezo kutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Leodger Tenga .





Mdau wa michezo Bw. Henry Tandau akifafanua jambo kwa wadau wa michezo  wakati wa kikao cha wadau hao kutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha akitoa mada wakati wa kikao cha wadau wa michezo kutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wadau wa michezo wakiwa katika majadiliano wakati wa kikao cha wadau haokutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wadau wa michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha wadau hao kutoa maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya michezo nchini mapema hii leo Novemba 27, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, CONSTANTINE KANYASU ARIDHISHWA NA UTAYARI WASANII KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari akiwaelezea mikakati ya jinsi Wizara ya Maliasili na utalii,ilivyojipanga kushirikiana na wasanii katika kutangaza vuvitio vya utalii katika mkutano uliofanyika jana jioni JIjini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja ya baadhi ya Miss Tourism Tanzania waliokuwa washindi wa mashindano katika miaka minne iliyopita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Afisa wa Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAW) Mary Kagasheki aliyewasilisha mada ya Utalii katika mkutano uliowakutanisha wasanii mbalimbli nchini katika maandalizi ya awali ya kumtafuta miss Tourism Tanzania.
( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

**************************************


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewapongeza Wasanii kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kunadi vivutio vya Utalii.

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewahakikishia Wasanii hao kuwa yeye pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangala wapo tayari muda wote kutoa ushirikiano kwa Msanii yeyote atakayetaka kufanya kazi na Wizara hiyo.

Akizungumza na wasanii mbalimbali pamoja na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana usiku, Mhe.Kanyasu amesema kazi ya sanaa nchini inakua kwa kasi sana, Hivyo wasanii hawawezi kuachwa nyuma katika kutangaza na kuhamasisha Utalii

Katika Mkutano huo uliwakutanisha Wasanii mbalimbali wakiwemo wa wasanii filamu,vichekesho, uchongaji pamoja Washindi wa Miss Utaliu wa miaka minne iliyopita. Mhe.Kanyasu amesema Sanaa ni kichochea cha utalii.

Amesema ushirikiano huo wa Wasanii ni hatua muhimu kwa katika kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 ni kufikisha idadi ya watalii mbili na nusu.

Akizungumzia mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nne tangu yalipoanzishwa, Mhe.Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Mashindano hayo kwa kubuni vipengele viwili vya kuwatafuta Walimbwende yaani Mlimbwende Utalii wa Tanzania pamoja na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa. ( Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism International )

Amesema ubunifu huo utasaidia kunadi vivutio vya utalii kitaifa kwa kumtumia Mlimbwende wa Utalii wa Tanzania huku vivutio hivyo vya Utalii vitadiwa Kimataifa na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yana sura mpya kwa kuzingatia muono wa Kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mashindano hayo, Gideon Chipungahelo amesema vigezo vya kuwapata Washindi hao mbali ya Ulimbwende watakaokuwa nao watazingatia uelewa walionao katika kuvijua vivutio vya Utalii vilivyopo nchini

” Tunamtaka Mlimbwende atakayekuwa balozi wa Utalii na Mwenyekiti ushawishi wa kuwafanya watu wengine wahamasike kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.” alisisitiza Mratibu huyo..

Akizungumzia maandalizi ya Maonesho hayo, Chipungahelo amesema yataanza mwezi Disemba na kumalizika mwezi Machi mwakani ambapo yatafanyikia jijini Dar es Salaam .

Aidha, Mratibu huyo, Chipungahello amesema kwa upande wa Mashindano ya Utalii wa Kimataifa, nchi 56 zimeonesha utayari wa kushiriki katika Mashindano hayo.

Naye, Mwakilishi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA,) Anna Masenge amesema Mashindano hayo yatazingatia maadili ya Mtanzani na kamwe hayatakuwa kichocheo cha kuharibu utamaduni huo kwa vile Waandaji hao watazingatia kanuni na miongozo iliyotolewa na BASATA 

Kufuatia hali hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika kinyang’iro hicho huku akiwatoa hofu wazazi kuwa Mashindano hayo sio uhuni kama wengi wanavyoyachukulia.

MIAKA MINNE YA MAFANIKIO MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo, akisisitiza jambo kwa A Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), Kuhusu Mafanikio ya Ofisi hiyo, ikiwemo ununuzi wa vifaa vya TZS Bilioni 6.5 na Ujenzi wa Maabara za kanda, Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza naWaandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ikiwemo ununuzi wa vifaa vya TZS Bilioni 6.5 na Ujenzi wa Maabara za kanda kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

IGP SIRRO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MADAWATI YA KIJINSIA KURIPOTI UKATILI

$
0
0


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro 


SERENGETI, MARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuacha  kujihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili jambo linalopelekea vitendovya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua Ofisi za dawati la jinsia na watotoMugumu wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo wananchi wametakiwakwenda kuripoti matukio ya ukatili hili hatua ziweze kuchukuliwa.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwaonya wananchi kuacha mara moja vitendo
vya kihalifu hususani wizi wa mifugo.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utu wa Mtoto (CDF) bwana Koshuma Mtengete amesema kuwa, ni vyema jamii ikaendelea kuelimika kwa kutoa taarifa za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ikiwa ni sambamba na kutokufumbia macho vitendo hivyo.

Kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya
Serengeti ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Nurdin Babu amesema kuwa,
wilaya yake imeendelea kutoa elimu kwa kuwaelimisha wananchi hususan
kwenye masuala ya kiusalama ikiwemo kuachana na mila kandamizi na
zilizokwisha kupitwa na wakati.

BAADHI YA WAKAZI MTAMBANI WAMLILIA LUKUVI,NDIKILO NA KAWAWA KUPEWA HAKI YAO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, Bagamoyo

Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Mtambani Kimarang'ombe Kata ya Nianjema Bagamoyo mkoani Pwani, wanaodai kutapeliwa ardhi yao ya hekari 34 ,wamemtaka Waziri wa ardhi William Lukuvi ,serikali ya mkoa na wilaya kuwasaidia kurejeshewa eneo lililovamiwa ili waishi kwa amani.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao na Waandishi wa habari katika eneo hilo Fatuma Ramadhani, Hussein Temo, Isdory Mwepong'we na Makolega Turuka, walielezea masikitiko yao ya kutakiwa kuondoka katika eneo waliloishi miaka 40 sasa.

Fatuma alisema ,walifika kwenye eneo hilo mwaka 1974 wakianza kulima, kabla ya Mkuu wa wilaya miaka hiyo Shaaban Kandoro kufika katika eneo hilo, akimtaka mmiliki na kukuta pori kubwa.

"Alipofika alituuliza mmiliki, na alitoa miezi mitatu kwa viongozi wamtafute mmiliki, kama hajajitokeza eneo hilo ataligawa kwa wananchi waliokuwepo, huku akiwataka viongozi wa kijiji wakati huo na kata kumfatuta," alisema Fatuma.

Nae Hussein Temo alieleza baada ya muda aliouweka Mkuu huyo wa wilaya wakati huo kumalizika pasipo kupatikana mmiliki, akaamua kuwagawia eka mojamoja kila mtu akaanza kuyaendeleza kwa kilimo, huku wengine wakijenga nyumba za muda.

"Tulishangazwa ulipofika mwaka 2010 kuwaona watu wakiwa na darubini wanapima maeneo hayo pasipokujulishwa, tuliitana na kukubaliana kwenda kwa viongozi wa Kijiji, ambapo Mwenyekiti akatuambia hata yeye hana taarifa ya zoezi hilo," alisema Temo.

Kwa upande wake Makolega Turuka alihoji uhalali wa Omary Sud ambaye kwa sasa ni marehemu, ambaye ni mkazi wa Bagamoyo alikuwa wapi kwa zaidi ya miaka 40, na kusema kuna mchezo mchafu wa kutaka kuwaondoa wananchi hao kisha wapige bei.

"Kesi ilifunguliwa mahakamani na kufikia 2010 Sud alikiri eneo hilo si lake ,na kesi ilifutwa kisha kusema walionunua kupitia yeye warudishe fedha ama kuwalipa fidia wazee hao"

Akizungumzia sakata hilo,ofisa ardhi wilayani hapa Wendeline Izana alisema kuwa, taarifa hizo alipatiwa na Ofisa Mtendaji Kata kwamba eneo hilo ni la Omari Sud.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Yussuph Mgala alisema kwamba analitambua eneo hilo miaka mingi kabla hajashika wadhifa huo, na kwamba linamilikiwa na Sud kabla ya kuwapatia wananchi hao walime mazao ya muda mfupi, na kwamba 2010 alifika kwa ajili ya kupima viwanja.

Mtendaji Kata wa Nianjema Sezary Madasha alifafanua, anatambua eneo hilo ni la Sud, hivyo aliwashauri wananchi hao wakafungue mashitaka katika mahakama ambayo ndio yenye maamuzi kisheria.

Rais Magufuli Mgeni Rasmi Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru Jijini Mwanza

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wahabari kuhusu maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania leo Novemba 27, 2019 Jijini Mwanza, maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo kwa mara ya kwanza.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa mkoa waMwanza Mhe. John Mongella na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo Novemba 27, 2019 Jijini Mwanza, maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo kwa mara ya kwanza.
************************************

Na Mwandishi Wetu- Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri zinazotarajiwa kufanyika Kitaifa mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongella amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika Disemba 9, 2019 kwa mara ya kwanza katika mkoa huo katika uwanja wa CCM Kirumba.

Kauli mbiu ya sherehe hizo ni “ Miaka 58 ya Uhuru na miaka57 ya Jamhuri:Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni Msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa Letu,” Alisistiza Mhe. Mongella.

Akifafanua amesema kuwa Shughuli zitakazofanyika wakati wa madhimisho hayo ni pamoja na gwaride maalum, burudani kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya,ngoma za asili kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara.

Aidha Mhe. Mongella amesema kuwa kutakuwa na shughuli mbalimbali kuelekeamaadhimisho hayo ikiwemo Mashindano ya ngonjera, Maigizo,Kwaya,Mashairi,Mashindano ya mbio za mitumbwi,Bonanza la michezo, mchezo wa bao, na mechi ya mpira wa miguu.

Shughuli za kikanda zitakazofanyika ni pamoja Kongamano la Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu litakalofanyika tarehe 6, Disemba, 2019 Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza.

Alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hizo nipamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dkt. Ali Mohamed Shein.

Viongozi wastaafu wakiwemo Marais, Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu ni miongoni mwa waalikwa wa sherehe hizo,Aidha , Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini ni miongoni mwa waalikwa wa sherehe hizo.

Juma la kilele cha maadhimisho hayo litakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika kikanda kuanzia Disemba 2, 2019 hadi tarehe 8 Disemba, 2019 kwenye mikoa ya Kagera, Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.

SIMBACHAWENE AZITAKA HALMASHAURI KUTOA ELIMU YA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akifungua Mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na utayari wa nchi katika kukabiliana na changamoto hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) Audax Rukonge akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Mratibu wa kitaifa wa TCSAA Shakwaanande Natai, Mjumbe wa Bodi ya ANSAF Joseph Kavishe na Mshauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Lucy Ssendi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo.
Mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na utayari wa nchi katika kukabiliana na changamoto hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) ukiendelea.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia matukio.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati akifungua mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisalimiana na mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (kushoto) akilakiwa na mwenyeji mwenyeji wake Mkurugenzi wa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) Audax Rukonge wakati akiwasili ukumbi wa mkutano.

………………..

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa halmashauri zote kuwa na mipango kabambe inayotekelezeka kwa ajili ya kuhakikisha elimu ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi inawafikia wakulima katika maeneo yao.

Pia amezitaka kuwajengea uwezo maafisa ugani kutekeleza jukumu hili muhimu pamoja na kuboresha mawasiliano na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na kuboresha ufikishaji wa taarifa hizi kwa wakulima na maelekezo ya nini wafanye kulingana na hali ya wakati husika. 

Simbachawene ametoa wito huo leo Novemba 27, jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na utayari wa nchi katika kukabiliana na changamoto hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF).

Alisema mabadiliko ya tabianchi ni tishio duniani huku Tanzania ikiathiriwa na mabadiliko ya misimu na mtawanyiko mbovu wa mvua, ukame na mafuriko ya mara kwa mara, ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa yasiyosikia dawa ya mimea na wanyama, ambavyo vimesababisha wakulima wengi kutopata mavuno ya kutosha na yaliyotarajiwa.

Aliongeza kuwa wanawake na vijana wameonekana kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kutokana na ukosefu wa nyenzo za kisasa za kilimo, elimu, kipato kidogo na kushindwa kumiliki ardhi ingawa ndio wenye kufanya kazi kubwa ya uzalishaji.

“Tunaona uharibifu wa vyanzo vya maji husababisha mama zetu na mabinti zetu kutembea umbali mrefu kusaka maji, hii inaweka usalama wao katika mazingira hatarishi na kaya zinapokosa chakula cha kutosha kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, wanawake na watoto ndio waathirika wakuu,” alisema.

Aidha waziri huyo aliwataka wadau wa maendeleo kuhakikisha mbinu zinazotumika katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinakuwa shirikishi na zinazingatia ushiriki thabiti wa wanawake na vijana. 

Alitaka pia kuwepo na mikakati kabambe ya kulikwamua kundi hilo na changamoto hii kama vile uchimbaji wa visima katika maeneo ambayo kwa kiasi kikubwa vyanzo vya maji vimekauka kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

“Niwashukuru na kuwapongeza ndugu zetu wa ANSAF kwa kutuleta pamoja ili tujifunze na kushauriana namna bora ya kusaidia jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Nizidi kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono juhudi hizi kwa kupeleka miradi ya kilimo stahimilivu kwa mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima, ili kuunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha tunafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

KONGAMANO LA KILIMO HAI LAELEZWA MADHARA YANAYOPATIKANA KATIKA MBEGU ZILIZOBADILISHWA VINASABA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

BAADHI ya wataalamu wa kilimo hai wametumia Kongamano la Kimataifa la kilimo hai wamezungumzia madhara ya kutumia mbegu zilizobadilishwa vinasaba yakiwemo ya kijamii na kichumi.

Akizungumza leo Novemba 27 mwaka 2019 Mjini Dodoma katika Kongamano la Kimataifa la Kilimo hai , wakati anawasilisha mada iliyohusu mbegu za GMO, Malmo Paul 

ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa baadhi ya madhara yanayopatikana katika mbegu zilizobadilishwa vinasaba kwa upande wa kijamii ni kwamba umiliki  wa mbegu hizo kwa asilimia 95 zinamilikiwa na kampuni moja,hivyo wakulima hawaruhusiwi  kutunza hivyo wanatakiwa kununua mbegu hizo kila wanaohitaji.

Amesema katika uchumi, ripoti ya utafiti uliofanyika USA inaonesha mbegu za zilizobadilishwa vinasaba(GMO) hazimnumfaishi mkulima kiuchumi kwa hiyo unakuta mkulima anakuta hasara kwani mazao ya mbegu zilizobadilishwa vinasba mazao yake hayana uzao mkubwa ikilinganishwa na mazao yanayopatikana katika kilimo hai.

Amesema kiafya ,imeelezwa kuwa usambazaji wa ugonjwa kwa njia ya hewa na wadudu wanavyofanya uchavushaji  ni mkubwa na hivyo kusababisha ugonjwa wa kansa na kutoa mfano katika nchini ya India kumekuwepo na matumizi ya kemikali na hivyo kusababisha madhara makubwa kiafya. 

Akifafanua zaidi Paul amesema kuwa kiwanda cha Textile Exchange wao katika kilimo cha pamba wanazuia  matumizi ya GMO isiendelee, hivyo watu waendelee na matumzi ya kilimo hai ambacho kina soko la uhakika."Ukuaji wa uzalishaji wa pamba ya ya kawaida Tanzania ni nchi ya tatu lakini kwa uzalishaji wa pamba ya Organic Tanzania ni ya kwanza.

Amesema pamba ya Organic inaweza kufanyika kwenye eneo kubwa na katika eneo dogo pia na hivyo kusababisha  uzalishaji kuwa mkubwa.

Wakati wa majadiliano hayo pia imeelezwa kuwa nchini Tanzania kunajitihada ambazo inafanyika kuhakikisha mbegu za kilimo hai zinaendelea kutunzwa na kuna aina za vinasaba 7000 ambazo.mbegu zake zimehifadhiwa.Huku wadau wa kongamano hilo wakieleza kuna haja ya nchi kutoruhsu uingizwaji wa mbegu zilizobadilishwa vinasaba.

Wametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu pia wa jamii katika ngazi ya familia kujihusisha  na kilimo hai na kutumia mazao yatokanayo na kilimo hicho. 
Wadau wa kilimo hai wakiwa katika Kongamano la Kimataifa linaoendela Mjini Dodoma wakifuatilia majadiliano yanayohusu kilimo hicho ambapo pia wamepata  nafasi ya kuelezwa madhara ya mbegu za GMO

MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA YAJIVUNIA MAFANIKIO LUKUKI MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO,WATOA PONGEZI RAIS MAGUFULI

$
0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) imeeleza kwa kina mafanikio ambayo wamepata katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano onayoongoozwa na Rais Dk.John Magufuli.

Mbali ya kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka minne, TanTrade imesema niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo wanampongeza  Rais wa Dk.John Magufuli kwa kutimiza miaka minne madarakani na kwa kuongoza nchi yetu kwa umahari ili kufikia katika uchumi wa kati na wa viwanda. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Movemba 27,mwaka 2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa Khamis amesema kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana ambayo Watanzania wana kila sababu ya kufahamu ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza TanTrade ni Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania  ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 4 ya mwaka 2009 na kuanza shughuli zake rasmi Septemba, 2010 na moja ya jukumu lake ni kukuza na kuendeleza biashara ya ndani na nje ya nchi ili kuimarisha biashara yenye tija katika maendeleo ya kiuchumi.

Wakati majukumu ya msingi ya Mamlaka hiyo ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ya kilimo, madini, vivutio vya asili, bidhaa zinazozalishwa viwandani na huduma mbalimbali zinazotolewa kibiashara. Kwa upande wa Sekta ya Kilimo, baadhi ya mazao hayo (agricultural produces or commodities) ni mahindi, kahawa, korosho, pamba, pareto, mchele, kokoa, na mazao mengine ya kimkakati. 
Amesema kwa upande wa sekta ya viwanda, ni bidhaa yoyote ya kiwandani (manufactured products) ambayo ina mahitaji ya soko la ndani na lile la nje ya nchi.  Kwa upande wa sekta ya huduma (trade in services) ni huduma zote zinazotolewa kibiashara- jukumu letu ni kutangaza huduma hizo katika masoko ya ndani na nje nchi. 

"TanTrade pia imekuwa ikiratibu utafutaji wa masoko ya mazao mengine (Nontraditional Products) yakiwemo ya asali, bidhaa za viungo (spices), mafuta ya kula na mihogo.Jukumu kubwa ambalo limekuwa likitekelezwa ni kusimamia mnyororo mzima wa thamani kuanzia kwenye hatua ,"amesema Latifa Khamis.

Kuhusu mafanikio ya TanTrade...amesema ni pamoja na taarifa za upatakinaji wa masoko ndani na nje ya nchi ambapo ameeleza mamlaka imekuwa na jukumu la utoaji taarifa za upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi, mathalan kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 jumla ya Kampuni 31,891 zilipatiwa taarifa mbalimbali za kibiashara kuhusu bei na masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi. 
Amesema kati yao wafanyabiashara 405 waliweza kuunganishwa na masoko na kuuza tani 102,000 za mahindi, tani 2,000 za karanga, tani 5,000 za soya, tani 50 za ufuta, tani 7 za majani ya papai, kilogramu 200 za unga wa ubuyu, tani 2 za iliki, tani 5,000 za muhogo na tani 3.2 za tangawizi ya unga.

"Miongoni mwa bidhaa zilizoonesha uhitaji mkubwa katika masoko ya nje ni pamoja na matunda, samaki na mazao ya bahari (mwani), jamii ya mikunde, asali, kahawa, chai, korosho, viungo na vyakula.  Maulizo hayo yalitoka katika nchi za India, Nchi za ukanda wa SADC, China, Japan, nchi jirani za Afrika Mashariki (EAC), Falme za Kiarabu, Misri, Marekani, Vietnam na Ulaya.

"Mbali na kusambaza taarifa za uhitaji wa bidhaa mbalimbali TanTrade kwa kushirikiana na Wanunuzi kutoka nchi mbalimbali iliratibu semina za kutangaza fursa za biashara katika nchi zao ikiwa ni muendelezo wa kimkakati wa kupenya katika masoko yao. Semina mbalimbali ziliratibiwa ambapo wafanyabiashara na wadau 425 walishiriki ili kutambua fursa za masoko ya nje na taratibu za kuyafikia masoko katika nchi za Uswidi, Ufaransa, Ukraine, China na Rwanda,"amesema Khamis.


Ameongeza kuwa kuwa kuhusu ukuzaji na Uendelezaji wa Masoko ya Nje ya Nchi TanTrade imeendelea kukuza na kuendeleza bidhaa za kutafuta masoko kupitia Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF). TanTrade imeendelea kuratibu Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) kwa lengo la kutoa fursa za kutangaza bidhaa zilizoongezwa thamani na upatikanaji wa teknolojia ili kupanua wigo wa masoko ya nje ya nchi.

Pia upatikanaji wa teknolojia husaidia kutatua changamoto za uzalishaji hafifu wa bidhaa za kilimo, uchenjuaji wa madini n.k. Kila mwaka wastani wa kampuni 3,000 kutoka nchini na kampuni zaidi ya 500 kutoka zaidi ya nchi 35 hushiriki Maonesho hayo. Ambapo amesema mwenendo wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa miaka minne ni kama ifuatavyo  mwaka 2016 jumla ya washiriki 2,573,    Mwaka 2017 jumla ya washiriki 2,610, Mwaka 2018 jumla ya washiriki 3,605 na mwaka 2019 jumla ya washiriki 3,860 .

Amesema maonesho haya yamekuwa na matokeo chanya, mathlani kwa mwaka 2019 mafanikio yaliyopatikana kutokana na uratibu huo ni  kwamba Kampuni 437 zilipata oda ya kufanya biashara (Business deals) zenye thamani ya Sh. 7.93 bilioni. Mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya wastani wa Sh. 209,450,000. Ajira za muda mfupi zipatazo 14,912 zilipatikana katika kazi mbalimbali za Maonesho kama vile ujenzi, ulinzi na usalama. Kuvutia watembeleaji wapatao 260,037 kutoka ndani na nje ya nchi.

Pia upatikanaji wa mapato ya Serikali kutokana na Kodi mbalimbali ikiwemo VAT, Ushuru wa Forodha na Kodi ya uingizaji bidhaa (Import Duty), fursa za kibiashara kwa watoa huduma mbalimbali hasa wajasiliamali wadogo wadogo  na kuongeza kila mwaka TanTrade inaratibu ushiriki wa kampuni za Tanzania katika Maonesho nje nchi hususan zile tulizo na utengamano nazo kama vile EAC, SADC ambapo wastani wa kampuni 200 hushiriki.

"Lengo la ushiriki wa makampuni ya Kitanzania kuhamasishwa kushiriki ni fursa ya kutambulisha bidhaa zao kwenye nchi hizo na kuingia mikataba ya kibiashara ili kupata masoko endelevu,"amesema.

Akizungumzia  Ukuzaji na Uendelezaji wa Masoko ya Ndani amesema TanTrade katika kutekeleza adhima ya Tanzania ya Viwanda ilianzisha Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika kila mwaka Mwezi Desemba yaliyoanza mwaka 2007 katika uwanja wa Mwl J.K.Nyerere   Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.

Amefafanua wastani wa makampuni 497 hushiriki kila mwaka ili kuunga mkono kauli mbiu hiyo. Mafanikio kwa wazalishaji wa bidhaa nchini wanapata fursa ya kutambulisha bidhaa zao pamoja na kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Tanzania kwa Watanzania. Kupitia Maonesho hayo wazalishaji mbalimbali wa mazao ya kilimo wameunganishwa na wenye viwanda kwa lengo la kuuza malighafi na hivyo kuwezesha kuwa na soko lenye uhakika.

Pia TanTrade kwa kushirikiana na taasisi inayosimamia wadau wa Mbogamboga na matunda (TAHA) kwa kushirikiana na Shirika la Biashara la Kimataifa (ITC) iliandaa mradi wenye lengo la kuboresha masoko ili kuongeza mauzo ya nje (MARKUP) kwa wazalishaji wa parachichi nchini. Mradi huo ulilenga kuwasaidia wazalishaji wa parachichi ili kufaidika na fursa ya upatikanaji wa mitaji ya biashara, mafunzo ya namna ya kufikia soko la nje pamoja na kuwa sehemu ya ushiriki wa maonesho mbalimbali yatakayoenda sambamba na mikutano ya kibiashara (B2B).

"TanTrade ilifanikiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa soko la vitunguu maji ambapo, iliratibu mkutano wa umoja wa wafanyabiashara wa vitunguu maji soko la Mwanakwerekwe Zanzibar ili kuwaunganisha na wazalishaji hao na masoko yenye tija.TanTrade imefanikiwa kuratibu uanzishwaji wa vyama vya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini. Lengo la kuanzisha vyama hivyo ni kuwatambua ili kuweza kwa pamoja kuongeza nguvu ya kupenya kimasoko na pia kuwasaidia katika kutatua changamoto za kimasoko. Vyama hivyo vilivyoratibiwa uanzishwaji ni Wazalishaji wa bidhaa za ngozi (TALEPA), Wazalishaji wa Viungo vya Chakula (TASPA) na Wazalishaji wa bidhaa za mihogo (TACCAPA) ,"ameongeza.

Ametaja mambo mengine yaliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne ni utoaji wa mafunzo kwa wazalishaji wa bidhaa za kilimo.TanTrade ilitoa mafunzo kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchi ikiwa ni malengo ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vinavyokidhi mahitaji ya masoko, kutambua na kushauri mbinu bora za kutatua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya kibiashara katika mnyororo wa thamani. 

Amesema mafunzo hayo huwa shirikishi na taasisi zingine za kimkakati. Mafunzo yametolewa ni kwa wazalishaji wa bidhaa za Mafuta katika zao la Alizeti kwa mkoa wa Lindi, Zao la Mwani, Kahawa kwa Zanzibar, Zao la Muhogo. 

Kuhusu kuimarisha biashara za mipakani amesema TanTrade kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara inatekeleza mipango mbalimbali yenye lengo la kuwasaidia wafanyabiashara kukidhi vigezo vya kibiashara, kujenga mazingira rafiki ya biashara na kurahisisha bidhaa kuvuka mipaka kupelekwa nchi jirani. 

Utekelezaji huo ni pamoja na uimarishwaji wa Kamati za Pamoja Mipakani (JBC) na kutoa mafunzo juu ya sheria na taratibu za kufanya biashara mipakani. Jumla ya kamati saba za pamoja (Joint Border Committees) zimeundwa katika mipaka ya Tunduma, Kasumuru, Mutukula, Rusumo, Kabanga, Sirari na Namanga. 

"TanTrade inaendelea kuzisimamia kamati hizo ili kuhakikisha zinafanya kazi na kufikia malengo tarajiwa ikiwa ni pamoja na kuratibu uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru.  TanTrade inaendelea kushirikiana na kamati hizo ili kuweza kuwa na taarifa sahihi za upatikanaji wa biashara katika mipaka ya nchini. Taarifa hizo ni kigezo muhimu katika kuhamasisha biashara za mipakani na kutoa ushauri mahususi wa kisera,"amesema Khamis.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa Khamis akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 27,2019 kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli.

Jumuiya ya Afrika Mashariki yasaini mkataba wa EURO milioni 10 na umoja wa nchi za Ulaya.

$
0
0
Aliyepo kulia ni Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki,Liberat Mfumukeko akisaini mkataba wa EURO milioni 10 na Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania.Manfredo Fanti (aliyepo kushoto)kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi hizo.



Jumuiya ya Afrika Mashariki imesaini mkataba wa EURO milioni 10 na umoja wa nchi za Ulaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi uanachama wa jumuiya hiyo.

Mkataba huo umesainiwa mapema leo katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo na Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Liberat Mfumukeko na Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya Tanzania ,Manfredo Fanti.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo ,Katibu mkuu wa EAC ,amesema kuwa, fedha hizo zimetolewa na jumuiya ya umoja huo ili kuziwezesha nchi wanachama kukabiliana na changamoto ya usalama ambayo imekuwa na kikwazo kikubwa Cha maendeleo katika nchi hizo.

Ameshukuru jumuiya hiyo kwa msaada huo ambao umekuja muda muafaka na kuongeza kuwa, jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana kwa ukaribu Sana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo ,Mfumukeko amesema kuwa,jumuiya hiyo ya nchi za Ulaya wamekuwa washirikiana kwa muda mrefu na jumuiya hiyo ambapo katika kipindi cha miaka mitano wamekwisha kutoa kiasi Cha EURO milioni 85 .

Kwa upande wake ,Balozi wa jumuiya ya umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Manfredo Fanti amesema kuwa, wataendelea kusaidia jumuiya hiyo katika maswala mbalimbali ya maendeleo .

“tumekuwa tukisaidia jumuiya ya Afrika Mashariki katika miradi mbalimbali tangu mwaka 2007 ambayo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.”amesema Balozi huyo.

Wananchi washauriwa kuvifanyia tathimini ya kina Vyama vya Siasa nchini

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Bashiru Ally,akiweka jiwe la msingi katika Tawi la CCM Bandamaji Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akiwahutubia Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa,Wilaya, Mabaraza ya jumuiya za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ziara zake za kuimarisha Chama Zanzibar.

************************************


NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.


WANANCHI wameshauriwa kuvifanyia tathimini ya kina Vyama vya Siasa nchini vyenye usajili na vinavyopokea na ruzuku kisha kuchagua Chama chenye sifa na vigezo vya kuongoza nchi.

Wito huo ameutoa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Bashiru wakati akizungumza na Wana CCM na Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema Watanzania wanahitaji chama chenye nguvu, kitakachosimamia rasilimali za nchi,kitakacholinda mipaka ya nchi,kitakacholinda Mapinduzi,Muungano na Uhuru kama kinavyofanya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema Vyama vya upinzani vya Tanzania sio madhubuti na havina uwezo wa kushindana na CCM kwani havipo karibu na wananchi vimekuwa vikiibuka wakati wa uchaguzi bila kuwa na sera wala muelekeo wa kiushindani katika medali za kisiasa.

Alisema CCM imejipambanua katika kuwahudumia wananchi kama kilivyoahidi katika kampeni zake zilizopita.

Katika maelezo yake Kkatibu mkuu alisema chama hicho kimetengeneza fomu milioni moja kwa ajili ya uchaguzi wa ndani kuwashindanisha wana ccm kwa uchaguzi wa ndani ya chama kwa lengo la kupata wagombe bora na wenye sifa, upinzani waseme wao wamepitia mchakato upi kuwapata wagombea wao waonadai wameenguliwa kwa kuonewa..

Alisema chama cha mapinduzi CCM ndio chama pekee Nchini Tanzania chenye kufuata na kutoa demokrasia kuliko vyama vyengine vyote vya upinzani.

Alisema kwa msingi huo ndio maana chama hicho kinaendela kukubalika zaidi Tanzania katika kila kona.

Alisema ifike wakati lazima wananchi watambue hakuna chama kingine zaidi ya CCM kitakachoendeleza na kusimamia misingi imara ya kulinda mapinduzi sambamba na kulinda Muungano.

Aidha katibu mkuu aliweka wazi kwamba tafsiri ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unatoa picha kuwa chama hicho kitashinda kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

KIPYENGA CHA KUJAZA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA CHAFUNGWA LEO

$
0
0



Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mchakato wa uchaguzi mdogo kujaza nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Mapiduzi CCM mkoa wa Arusha ambayo hadi sasa inashikiliwa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Lotha Sanare umefungwa leo ambapo zaidi ya wagombea 40 wamejitokeza kuomba nafasi hiyo.

Uchaguzi huo unakuja baada ya Nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na mwenyekiti aliyekuwepo Loatha Sanare kuchaguliwa kuwa mkuu wa mkoa wa morogoro mapema mwezi wa kumi mwaka huu

Mchakato huo ambao ulianza November 25 umevuta hisia za waombaji wa nfasi hiyo ambao wameonyesha hamasa kubwa wakati wa kuchukuwa na kurudisha fomu licha ya uongozi wa mkoa wa chama hicho kutotaja majna hadi sasa.

Licha ya kuwepo uchaguzi huo mdogo hadi wagombea wanarudisha fomu zao za kuomba nafasi hiyo chama hicho kimekuwa kwenye usiri mkubwa tokea siku ya mwanzo ya kutoa fomu hadi leo siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo mara baada ya kurudisha fomu mmoja ya wagombea wa nafasi hiyo Charles Panga ambaye ndiye mgombea kijana zaidi kati ya waliogombea nafasi hiyo alisema kuwa umri sio tatizo la uongozi bali mawazo ya kiuongozi na utendaji ndio silaha kubwa kwa mwanasiasa.

Alisema kuwa amejipanga pindi atakapopitishwa kwenye uchaguzi huo kuhakikisha chama hicho kinaisimamia serikali kutekeleza ilani ya chama hicho 2020 na kuwa daraja la wananchama wapya kuweza kuongoza kwa vitendo na kuacha siasa za kizamani za makundi ndani ya chama hicho

“Nitakuwa sehemu ya kukipigania chama changu na wakati wote nitakuwa tayari kupokea maelekezo ya kufikia sehemu ya kuendelea chama change kushika dola na kushinda chaguzi mbalimbali”alisema Panga.

Alisema kuwa chama hicho pindi akipata ridha hiyo atasaidiana na viongozi kuhakikisha kuwa wananchi na wanyonge kero zao zinashughulikiwa kwa kuwa chama ndio mtetezi wa wananchi hao naye kuwa sehemu ya kuwasaidia wananchi kufikia malengo hayo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo au mwishoni mwa wiki ambapo hadi sasa wananchama wa chama hicho wapo mkao wa kula kuhakikisha wanampata mwenyekiti wao wa mkoa katika uchaguzi huo.

Duru za kisiasa mkoani hapa zimejikita kwa wagombea kuhakikisha wanapata mwenyekiti sahihi wa kuvaa viatu vya Loatha Sanare ambaye utendaji wake ulimfanya mwenyekiti wa chama hicho Taifa na Rais Dkt.John Magufuli kumchagua kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kuchukuwa nafasi ya Dkt. Kabwe Stephen na hivyo kuvutia wagombea zaidi ya 40 hadi dirisha lilipoungwa saa kumi jioni November 27

SERIKALI WEKENI MAZINGIRA RAFIKI KWA WALEMAVU MASHULENI MOLLEL

$
0
0

Na Ahmed Mahmoud Arusha

MBUNGE viti maalum mkoa wa Arusha, Amina Mollel, ameiomba serikali kuboresha miundo mbinu kwenye shule za msingi na sekondari ili kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye ulemavu wa viungo waweze kupata maeneo salama ya kujisaidia kuliko hali ilivyo sasa.

Mbunge huyo ametoa kilio hicho Novemba 27 kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa,RCC, alipokuwa akichangia hoja ya Idara ya afya iliyowasilishwa na mganga mkuu wa mkoa, Dakta Wedson Sichelwe, iliyokuwa ikielezea hali ya patikanaji wa dawa mkoani humo.

Mbunge, huyo alisema miundo mbinu iliyopo kwenye shule hizo sio rafiki kwa wenye ulemavu ,ambapo kwenye ziara yake aliyoifanya shule mbalimbali mkoani humo ameshuhudia walemavu wakitaabika kwenda kwenye vyoo .

Alisema hali hiyo inauma kwa kuwa walemavu wanataabika hivyo kutokana na serikali kutekeleza mpango wa chakula bure unatakiwa uende sambamba na uboreshaji wa miundo mbinu rafiki kwa walemavu .

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga, ameiomba serikali kuhakikisha dawa zinawafikia wananchi na kuwaondolea usumbufu wa kupata dawa mara baada vipimo vya magonjwa.

Alisema taarifa ya upatikanaji iliyotolewa na mganga mkuu hailingani na hali halisi ilivyo vijijini ingawa serikali inatoa fedha za dawa na halmashauri zinalipa wazabuni.ambao wamekuwa hawafikishi huduma hizo kwa wananchhi.

Alisema kuna baadhi ya wazabuni hawana uwezo hivyo waangaliwe upya utendaji wao kwa kuwa wanasababisha usumbufu kwa wananchi kwa sababu hawana uwezo na kusababisha mlundikano wa wananchi kusafiri umbali mrefu kusaka dawa.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Longido, Toba Nguvilo, alisema katika kata za Kitumbeine na Girarungwe, wilayani Longido, Zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na Kanisa la KKKT kadi za bima ya afya iliyoboreshwa hazipokelewi.

Alisema wananchi wenye kadi za bima iliyoboreshwa wamekuwa wakishindwa kupata huduma ya tiba kutokana na kadi hizo kutokupokelewa wala kukubalika na hivyo kujikuta wakikosa huduma za matibabu.

Kwa upande wake mchungaji Simon Dereva wa KKKT kwa niaba ya askofu Simoni Masangwa, alisema watalishughulikia tatizo ili kadi hizo ziweze kupokelewa na wananchi wapate huduma huduma za matibabu kwa kuwa serikali imeonyesha ushirikiano wa hali ya juu.

Awali akiwakilisha taarifa yake mganga mkuu wa mkoa,Dakta Wedson Sichelwe, alisema kiwango cha upatikanaji wa dawa katika mkoa huo ni asilimia 99% na kuwaondoa hofu wajumbe na wananchi kuwa suala la dawa katika mkoa sio changamoto kama ilivyokuwa siku za nyuma

Wakati huo huo imeelezwa kuwa mkoa wa Arusha una upungufu wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari 262 ,ambapo wilaya ya Meru inaongoza kwa kuwa na upungufu wa vyumba 66 huku wilayua ya Longido ikiwa na upungufu wa vyumba vine tu.

Katibu tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, ameyasema hayo alipokuwa akiwakilisha taarifa ya utekelezaji war obo ya pili ya mwaka ya kamati ya ushauri mkoa ya mwaka 2018/19.

Alisema mkoa katika kutekeleza maazimio ya kikao kilichopita cha mwezi Marchi mwaka huu mkoa unaanza mkakati wa kujenga vyumba hivyo vya madarasa kwa shule za sekondari ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi watakaojiunga na kidatoo cha kwanza mwakani.

Kuhusu afya ,alisema Kwitega,amesema kuwa mkoa unaendelea na ujenzi wa hospital za wilaya za Longido, Karatu Ngorongoro na halmashauri ya Jiji la Arusha ,ambapo ujenzi wake upo kwenye kiwango kizuri.

Alisema kikao kilichopita msisitizo ulikuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo Sekretari ya mkoa na mamlaka za serikali za mitaa mwaka 2018/19 mkoa uliidhinishiwa shilingi ,67,570,830,394.10 kwa ajili ya miradi.

Watafiti nchini wametakiwa kuhakikisha Tafiti wanazofanya zinasaidia kutengeneza Sera

$
0
0
Naibu waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe.
Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua Mkutano wa mwaka na kongamano la
Kisayansi la chama chaMadaktari wa mifugo Tanzania (TVA).
Zingine zote ni picha za washiriki wa mkutano wakifuatilia mada na hotuba za
ufunguzi wa mkutano huo mapema leo.
Prof. Robinson Mdegela ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo SUA akiwasilisha mada juu ya dhana ya afya moja kabla ya kuanza
kwa mkutano huo.
Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael
Chibunda na Mweyekiti wa Kikao hicho akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo kwenye ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali
Matamwe Said akitoa neno kabla ya Kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya Mhe.
Dkt. Faustine Ndugulile kufungua mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA) Prof. Dominic
Kambarage akieleza malengo ya Mkutano huo wa Kisayansi mbele ya Mgeni
Rasmi.


***************************************

Na: Calvin Edward Gwabara


Watafiti nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa tafiti wanazofanya zinasaidia katika kutengeneza sera au kuziboresha ili kutoa mchango wa moja kwa moja kwa jamii na taifa badala ya kuishia kwenye makabati na machapisho ya kimataifa.

Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua Mkutano wa mwaka nakongamano la Kisayansi la chama chaMadaktari wa mifugo Tanzania (TVA)uliokutanisha wadau wote wa Afya moja kutoka wizara,Taasisi za elimu yajuu,Taasisi za utafiti,Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania uliofanyika kwene ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.

Dkt.Ndugulile amesema Kuna tafiti nyini zinafanywa nchini lakini zinaishia kwenye machapisho ya kimataifa lakini ifike wakati matokeo mazuri ya kazi nzuri za utafiti zinazofanywa wa watafiti nchini ziweze kuisaidia serikali kutunga sera nzuri ambazo zitatengeneza miongozo mizuri ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

”Niwapongeze sana TVA kwa kufanya mkutano huu mkubwa wa kwanza nchini unaowakutanisha wadau wengi wa dhana ya afya moja kutoka sekta mbalimbali na ni matumaini yangu na ya serikali kuwa kwa mjumuiko huu mkubwa wa watafiti mtakuja na mapendekezo mazuri ambayo yataisaidia serikali kufanya maamuzi sahihi kwenye kutelekeza dhana hii ya afya moja” Aliema Dkt.Ngugulile.

Naibu huyo wa Wizara ya afya amesema ulinzi wa afya ya Binadamu,mimea nawanyama unahitaji ushirikiano wa wadau wote na kwamba Serikali tayariilishaanza kutekeleza mpango huu kwa kuanzisha dawati la afya moja kwenyeofisi ya waziri mkuu ambalo linasaidia kuratibu utekelezaji wa dhana hii ambayo sasa ndio ajenda ya dunia kwa umuhimu wake.

”Niwaombe elimu hii ambayo mnaitoa katika ngazi ya kitaifa ifike hadi kwenye ngazi za serikali za mitaa kwa kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika ngazi hiyo kwenye sekata mbalimbali ili nao wapate uelewa ili iwe rahisi kwenye utekelezaji wa mpango mkakati huu wa kidunia ambao kitaifa uliziduliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mwaka 2015” Alisisitiza Naibu waziri wa Afya Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile.

Mhe. Ndugulile ametaka kuwepo kwa takwimu za kina kuhusu masuala ya Afya moja hapa nchini kutokana na kuwepo kwa wadau mbalimbali wanaofanya kazi hiyo ili takwimu hizo zisaidie serikali kwenye kufanya maamuzi ya vipaumbele katika kuwekeza fedha zake maana bila hivyo ni ngumu kuishawishi serikali kufanya maamuzi.

Akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua Mkutano huo
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Matamwe Said amesema umuhimu wa Dhana ya afya moja kwa taifa ndiyo imeifanya serikali kuona umuhimu wa kuanzisha dawati kwenye ofisi ya waziri mkuu ambalo limeleta mafanikio makubwa katika mkakati huu ambao ndio ajenda ya dunia kwa sasa.

Amesema kuwa Mabadilio ya tabia nchi yanapelekea kuwepo kwa magonjwa kwa mimea,Wanyama na Binadamu ambayo sasa yanahatarisha afya hivyo ni muhimu wadau wote kwa pamoja wakaweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na dawati ili kuboresha afya za binadamu.Kanali Said amesema Mkutano huu ulioandaliwa na TVA na kuratibwa na ofisi ya
Waziri Mkuu ni mwanzo wa mikutano mingi ambayo itafuata ya kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja kwa sekta zote ili kutimiza mpango wa dhana ya Afya moja nchini.

Nae kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA) Prof. Dominic Kambarage amesema kwa mara ya kwanza TVA imefanya kongamano la aina hiyo la kisayansi ambalo limelenga kwenye mada moja ya dhana ya afya moja na kuwakutanisha wadau wote katika ngazi zote.

Amesema linapotokea tatizo la ugonjwa wa mifugo wanaofanya kazi hiyo ni
madaktari wa mifugo lakini kwa kuwepo kwa magonjwa sita makubwa
yanayoambukizwa kati ya binadamu na wanyama kuna kila sababu ya kuwepo kwa ushrikino wa pamoja maana matatizo hayo yanagusa wataalamu wa aina tofauti tofauti katika kuyatatua.

” Zaidi ya asilimia 70 ya magonjwa ya Binadamu vyanzo vyake ni kutoka kwa Wanyama na wanyama na serikali inatumia fedha nyingi kwenye kutibu ugonjwa unapotokea hivyo ni wakati sasa umefika wataalamu wakaanza kushirikiana ili kukinga wanyama na adhari zinazoweza kutokea kwa bidamu kama ilivyo kwa magonjwa kichaa cha mbwa” Alisema Prof. Kambarage.


Prof. Kambarage ametoa wito kwa jamii kuacha kulala ndani na mifugo yao ili kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa hayo yasiyo na lazima lakini pia kuipatia kinga mifugo yao pale inapotakiwa kwa wakati.

NSSF, NHC, WHC KAMILISHENI MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI -MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati alipotembelea mradi wa nyumba za NHC, zilizopo Mtoni Kijichi katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi wa NSSF, Balozi Alli Siwa, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasalimia Watoto wa Chekechea wa Shule ya Kids Paradise, iliyopo ndani ya Mradi wa Nyumba za NHC, Mtoni Kijichi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

****************************************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za Umma katika wilaya Kigamboni jijini Dar es salaam zinapaswa kukamilika haraka ili ziuzwe ua kupangishwa kama ilivyokusudiwa.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 27, 2019) baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za NSSF, NHC na Watumishi Housing iliyopo katika wilaya ya Kigamboni.

Waziri Mkuu amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi jijini Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba nyingi nzuri zimejengwa na zinahitahi umaliziaji mdogo tu ili ziweze kukalika.

Hivyo, Waziri Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na uwekaji wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka katika nyumba zake 161 zilizoko Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko Dungu ili ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea kwa nyumba hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.

Ili kufanikisha jambo hilo Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali atathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.

Pia, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo.

Mheshimiwa Majaliwa pia ameitaka Menejimenti ya NSSF kufikiria namna ya kuzungumza na viongozi wa vyuo mabalimbali kama vile Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mwalimu Nyerere ili wanafunzi wa vyuo hivyo wapatiwe fursa ya kupanga katika nyumba hizo kwa bei watakazomudu.

Pia Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam ukishirikiana na SUMATRA kuanzisha njia za mabasi ya daladala zitakazoanzia au kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua nyumba hizo kupata usafiri wa umma. 

Vilevile, Waziri Mkuu ameuagiaza uongozi huo kuhakikisha kwamba eneo la Mtoni Kijichi zilipojengwa nyumba za NSSF na NHC linapata huduma za Shule, Kituo cha Afya na Kituo cha Polisi kwani litakuwa na wakazi wengi .

Ili kuongeza thamani ya nyumba hizo na kuvutia wapangaji na wanunuzi, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Menejimenti ya NSSF kuboresha barabara kwenye mitaa yote zilipojengwa nyumba hizo kwa kushirikiana na TARURA.

“Nashauri ziwekwe taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi ili kupendezesha eneo na kuwafanya wananchi wahamasike kununua na kuishi katika nyumba hizi” amesema Majaliwa.

Akiwa kwenye Mradi wa Nyumba za NHC Mtoni Kijichi, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea Shule ya Awali ya Kids Paradise na kufurahishwa na utaratibu mzuri wa shirika hilo wa kukumbuka kujenga jengo zuri la Shule hiyo na kulipangisha ili kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi katika nyumba hizo wanapata fursa ya kusoma elimu ya awali.

Akizungumza baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC Mwongozo, Mheshimiwa Majaliwa ameutaka uongozi wa NHC kuwa karibu na wateja wanaopanga au kununua nyumba zao. “ Shughulikieni malalamiko yote yanayotolewa na wateja wenu ili wajenge imani kwenu, Alisisitiza Majaliwa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama alisema wizara yake imeyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kwamba watafanya kila njia ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, william Lukuvi alimwambia Waziri Mkuu kuwa amekwishatoa maagizo kwa NHC ijenge uzio japo wa waya na wapande michongoma ili kuweka ulizi kwenye eneo la nyumba zao za Dungu.

Mheshimiwa Lukuvi alisema amewapa NHC miezi mitatu ili wafanye marekebisho katika nyumba ambazo zimelalamikiwa na wateja kuwa zina kasoro ili kujenga imani kwa wateja wao.

Mapemba Mkadiriaji Majengo wa NSSF, Abon Mhando ambaye pia ni Kaimu Meneja wa Miradi wa NSSF alimwambia Waziri Mkuu kuwa Mradi wa ujenzi wa nyumba wa Tuangoma una jumla ya nyumba 161 na kati ya hizo nyumba 76 zimekamilika. Aliwataja wakandarasi wanaojenga mradi huo kuwa ni Kampuni za CASCO, Advent na NANDRA.

Alisema Mradi wa Dungu una jumla ya nyumba 439 na kati ya hizo nyumba 95 zimekamilika na jumla ya makampuni 13 yameshiriki katika ujenzi wa mrdi huo.

Kuhsu mradi wa Mtooni Kijichi Mhando alisema mradi huo una jumla ya nyumba 820 na kati ya hizo nyumba 417 zimekamilika.

Rais Magufuli apiga marufuku Halmashauri kukopa benki

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Novemba, 2019 amepiga marufuku halmashauri zote za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya hapa nchini kukopa fedha za kutekeleza miradi kutoka benki, na badala yake ameagiza miradi hiyo itekelezwe kwa kutumia fedha za bajeti na mapato ya ndani ya halmashauri hizo.


Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati akiwasalimu wananchi wa Ushirombo katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Chato Mkoani Geita.


Kabla ya kuwasalimu wananchi hao, Mhe. Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Kahama Mkoani Shinyanga ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji huo Bw. Anderson David Msumba amemueleza kuwa halmashauri hiyo imekopa shilingi Bilioni 8 kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi.


Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi huyo kuachana na mkopo huo na amepiga marufuku halmashauri zote nchini kwenda kukopa benki fedha za kutekeleza miradi, na kwa ambazo zimeshakopa kurejesha fedha hizo vinginevyo Wakurugenzi wa halmashauri hizo wataondolewa katika nyadhifa hizo.


Amefafanua kuwa mamlaka ya kukopa fedha za miradi ya Serikali yapo mikononi mwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na sio kila halmashauri kukopa inavyotaka tena kwa riba kubwa kwa kuwa mwishowe Watanzania wote ndio watakaowajibika kuilipa kupitia hazina.


Akiwa katika safari hiyo Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Igunga, Nzega, Tabora pamoja na maeneo yote yaliyopangwa kupitiwa na mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuwa matatizo ya maji yanayowakabili wananchi hao yatakwisha baada ya mradi huo kukamilika.


Mhe. Rais Magufuli amesema mradi huo ambao utagharimu shilingi Bilioni 620 hadi kukamilika upo katika hatua za ujenzi na mara maji yatakapofikishwa katika maeneo hayo Serikali itahakikisha yanasambazwa kwa wananchi.


Kabla ya kufika Igunga, Nzega na Tabora, Mhe. Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Shelui Mkoani Singida ambapo amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo kutoa shilingi Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Shelui ifikapo Januari 2020, baada ya wananchi hao kuomba wasaidiwe kujengewa Kituo cha Afya kama walivyoahidiwa miaka ya nyuma.


Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa maeneo hayo pamoja na maeneo mengine ya Isaka, Kahama, Masumbwe, Uyovu Runzewe na Bwanga kwa mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na amewahimiza kuendelea kuchapa kazi za uzalishaji mali hasa wakati huu ambapo mvua zinanyesha ili kujihakikishia chakula na kipato zaidi kutokana na kilimo.


Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imechukua hatua mbalimbali za kupigania maslahi ya Watanzania ikiwemo sekta ya madini ambapo pamoja na kuwatetea wachimbaji wadogo imetunga sheria ya kuhakikisha nchi inanufaika na rasilimali hiyo, na katika hilo ameipongeza kampuni ya dhahabu ya Barrick kwa kukubaliana na Serikali kuunda kampuni ya pamoja iitwayo Twiga ambapo Serikali itakuwa inapata faida kwa asilimia 50 na kampuni ya Barrick itapata asilimia 50.


Akiwa Kahama, Mhe. Rais Magufuli amewasikiliza akina Mama watatu waliokuwa wakidai kudhurumiwa haki zao ambapo ameagiza Askari Polisi (Koplo Pascal Edward) anayedaiwa kusababisha kifo cha Mme wa Evanis Raymond Mzare baada ya kumgonga na gari, kusimamishwa kazi mara moja na hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi yake kutokana na kudaiwa kufanya njama za kuharibu kesi inayomkabili.


Pia amemuagiza Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga ACP -Sofia Jongo kumkamata mtu aitwaye Daudi anayedaiwa kumpiga hadi kumvunja mkono Mama aitwaye Maria Mavita wakati akifanya kazi zake za kuponda kokoto na amemuagiza Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Bw. Clement Mkusa kufuatilia kesi ya Mama aitwaye Joyce Lenard anayedai hati ya nyumba yake imeghushiwa na kuna njama zinafanyika kumpora nyumba hiyo.


Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

27 Novemba, 2019


Viongozi wa Dini kushiriki mapambano dhidi ya Kifua Kikuu

$
0
0
 Viongozi wa dini mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kukutana jijini Mwanza ili kwa pamoja kusaini maazimio ya kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa Kifua Kikuu (TB) kupitia nyumba zao za ibada.

Mwenyekiti wa kambi rasmi ya wabunge wanaopambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, Oscar Mkasa (kuli) ameyasema hayo Novemba 27, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza kuhusiana na shughuli hiyo.


Mkasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Madawa ya Kulenya amesema shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika Ijumaa Novemba 29, 2019 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.


Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) amebariki shughuli hiyo akisema itasaidia kutoa elimu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao takribani asilimia sita ya wagonjwa wote nchini wanatoka mkoani humo.

Na George Bingai-GB Pazzo, Mwanza
Tazama Video hapa chini

WAZIRI KABUDI ALIVYOWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS MAGUFULI KWA RAIS WA KENYA

$
0
0
Mjumbe maalum na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amewasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Uhuru Kenyatta juu ya masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Nchi hizo mbili na Kimataifa.

Katika Ujumbe huo Tanzania imesema itaiunga mkono Kenya katika nafasi ya Kiti na Mjumbe asiyewakudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2021/2022.

Mara baada ya kukabidhi na kueleza ujumbe wa Rais Dkt Magufuli kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepata fursa ya kushiriki katika uzinduzi wa ripoti ya Mpango wa kujenga umoja na mshikamano baina ya wakenya ujulikanao kama Building Bridge Initiative,ambapo amewataka wakenya kushikamana na kuziba mianya ya siasa za kikabila ili kuwa na Taifa moja kwa ajili ya maendeleo.

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema Taifa hilo kwa miaka mingi limekuwa likiendeshwa wa siasa za kikabila jambo ambalo amesema halileti afya kwa ustawi wa Kenya kutokana na kuwa kila baada ya uchaguzi Taifa hilo huanza kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi badala ya kuzingatia masuala ya maendeleo.

Rais Kenyatta amewataka wanasiasa wenzake kuacha siasa zinazochochea mgawanyiko na kuwataka kutumia fursa iliyojitokeza kupitia Building Bridge initiative kutoa maoni ya namna bora ya kufanya siasa za kistaarabu zisizochochea uhasama.

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images