Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

MCHAKATO WA KUTAFUTA MISS UTALII KIKANDA KUANZA DESEMBA,2019

$
0
0

 Baadhi ya Walimbwende wa 2013 na 2014 walioshiriki katika Shindano waliohudhulia semina ya waandano la Miss Utalii.
 Rais wa shindano miss Utalii, Gideon Chipungahelo akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari, katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa utalii tukitaka mabadiliko katika urembo ni lazima kufanya mambo mazuri zaidi ya urembo na kuwawezesha washiriki kuwa na maarifa mengi ya masuala ya Utalii.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Shindano la kutafuta mlimwende katika utalii (Miss Tourism), katika Hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.

 Afisa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bona Masenge akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa vyomo vya haari jijini Dar es Salaam katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Sanaa za Maonesho, Wilium Chitanda akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini kwaajili ya kuandika habari za Miss Utalii kwa uelewa zaidi. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.
 Rais wa shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania(TAFCA), Adrian Nyangamawe akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika habari za mlimbwende wa Utalii (Miss Tourism) katika semina iliyofanyika hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.



 Baadhi ya Walimbwende wa 2013 na 2014 walioshiriki katika Shindano waliohudhulia semina ya waandano la Miss Utalii.

Moja ya watoa Mada katika Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari.

MCHAKATO wa usaili wa kumtafuta mlimbwende wa urembo katika utalii (Miss Tourism) kuanza Desemba, 2019.

Akizungumza na wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam, Afisa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bona Masenge, amesema kuwa shindano la Mlimbwende katika utalii litaambatana na kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.

 Bona amesema kuwa BASATA imewaamini waandaaji wa Shindano la Miss utalii kwani kunavigezo mbalimbali ambavyo wamekidhi vya kikanuni, kisheria na kwaajili ya kuandaa shindano hilo.

"Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) linahusika na mashindano haya kwa ukaribu ili kuhakikisha waandaaji wa mashindano haya wanakidhi vigezo na kufata taratibu na sheria zilizowekwa na Baraza".
 Amesema Bona

Bona amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa Utalii limeweza kuwapa ajira za kudumu vijana kwa kuinua vipaji vya  vijana wengi na kukuza utalii hapa nchini.

"Mashindano ya mlimbwende wa Utalii yameweza kuinua vipaji kwa washiriki na baadhi wameweza kupata ajira za kudumu na yameweza kukuza utalii kitaifa na kimataifa".

Kwa upande wake Rais wa shindano la miss Utalii, Gideon Chipungahelo amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa utalii tukitaka mabadiliko katika urembo ni lazima kufanya mambo mazuri zaidi ya urembo na kuwawezesha washiriki kuwa na maarifa mengi ya masuala ya Utalii.
Amesema watakaohitaji kushiriki Mahindano hayo wakae mkao wa kula kwani tunata yanayotakiwa ni Mapinduzi Makuwa katika tasnia nchini.

"Miss yourism Tanzania (Mlimbwende wa utalii Tanzania) historia yake kabla na baada ya uhuru shindano la kwanza la kupata mshindi wa dunia katika ulimbwende wa Utalii. 
Amesema Chipunagahelo.

Hata hivyo mchakato huo wa kutafuta Mlimbwende katika utalii utachukua zaidi ya Miezi sita ili kuwapa muda majaji kufanya kazi ya kutafuta Mrembo anayekidhi vigezo vyote na atakayetuwakilisha duniani na kutuletea taji la dunia hapa nchini.

WAKAZI WA SHELUI, WAMLILIA MAGUFULI, AWAHIDI KUTOA MILIONI 250

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaahidi wananchi wa tarafa cha Shelui Mkoani Singida kuchangia Milioni 250 kwaajili ya kujenga Kituo cha Afya katika tarafa hicho.

Ameyasema hayo baada ya mwananchi wa Maeneo ya Shelui, Aidani Shabani kutoa kero ya kutokukamilika kwa kituo cha Afya cha Shelui kutokukamilika kwa miaka 15 sasa, kilichopo Mkoani Singida

"Lakini hapa kwetu shelui tunatatizo moja Mheshimiwa Rais, Tatizo Kubwa tulilonalo la kituo cha Afya kwenye Tarafa yatu ya Shalui, Hatuna Kituo cha Afya, kituo cha Afya tulichonacho kimeanza kujengwa sasahivi ni miaka 15, na wananchi tulichangia, alikuja kipindi anamalizia Mheshimiwa Rais Jakaya akaja akasimama pale, Akasema "Mimi kama Rais wenu Yuko wapi mwenyekiti? " Akaja mwenyekiti akasema; "Nakupongeza Sana Mwenyekiti" na Kile kituo cha Afya nitachangia  akasema atachangia milioni 200 ",". Amesema shabani.

Hata hivyo Shabani amesema kuwa tangu tumeanza harakati ni miaka 15 kile kituo cha afya kipo vilevile kwani kila ajali zikitokea watu wanapoteza maisha  kwasababu wanapelekwa katika hospitali ya wilaya Kihomboi mbali na lami, hivyo inakuwa shida kuwafikisha majeruhi.

"Tunakuomba Mheshimiwa kizingatie kile kituo cha Afya na ujue tatizo ni nini?, kama michango inatoka kwanini hakikamiliki? utusimamie baba kituo cha afya kikamilike".

Hivyo rais Dkt. Magufuli katika kumjibu mwananchi huyo alitaka kumtambua katibu tarafa , mtendaji wa kata na mkuu wa mkua kwaajili kujua ratiba ya kituo cha afya cha Shelui.

Baada ya kupata maelezo kutoka kwa viongozi hao, Rais Dkt. Magufuli, amesema kuwa akawashukuru wananchi hao kwa maendeleo ya eneo hilo.

"Ahadi hii ilitolewa na Rais mpendwa kikwete nataka kiwadhibitishie sasa, hizo milioni 200 nitazitoa na ziongezeke na (Madawa) dawa yaanze kupatikana vizuri. Nataka niwaahidi ndugu zangu msema kweli ni mpenzi wa Mungu huu ni mwezi wa ngapi?.... mwezi wa 11(Novemba),Mnipe mwenzi mmoja  mwezi wa 12 (Desemba), kujiandaa kwa sababu kunasherehe  nyingi watu mnasheherekea mwaka mpya!,  mwezi wa kwanza  milioni mia 200 zitakuwa hapa zinaendeleza  msichange tena kwaajili ya kituo cha afya.

Kwahiyo Mkuu wa Wilaya  usiwachangishe wananchi wa hapa kwa sababu ya kituo cha afya, tutakijenga tukimalizie, kama ambavyo rais wa awamu ya nne alivyoahidi, aliahidi,  mimi nitatekeleza kama kijana wake, ninajua ninyi ni hamuwezi kusema uwongo, si ndio ndugu zangu?".

Katika suala la Kituoa cha Afya Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa "Hili la afya la hospitali, lazima kiwe kituo kikubwa  cha afya, hizo milioni 200, tena nitaongeza na mimi nichangiepo kidogo zitakuwa milioni 250".

Rais, Dk. Magufuli amesema tatizo la maeneo ya kuegesha magari anawaachia halmashauri ya wilaya, pamoja na DC na watendaji wa eneo hilo, ili waamue wanataka kujenga maegesho ya magari wapi.

Rais Dkt. Magufuli alisimama barabara kwaajili ya kuwasikiliza wananchi waliokuwa wamekusanyika alipokuwa wakielekea Kahama mkoani shinyanga.

DKT.BASHIRU ASHIRIKI MAULID YA TUMBATU ZANZIBAR.

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally, akisindikizwa na wenyeji wake wakiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe.Haji Omar Kheri baada ya ufunguzi wa Maulid ya kuadhimisha Sherehe ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Kisiwani Tumbatu.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally,akiwa katika Boti maalum na Viongozi mbali mbali wa CCM wakielekea Kisiwani Tumbatu Zanzibar kwa ajili ya ufunguzi wa Maulid ya kuadhimisha Sherehe ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W),ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoanza jana Unguja.
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabhi , akisoma dua katika Maulid ya kuadhimisha Sherehe ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Kisiwani Tumbatu.


NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa,amesema Viongozi na Waumini wa Dini mbali mbali wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Nasaha hiyo ameitoa katika Maulid ya kuadhimisha sherehe ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) huko katika Msikiti wa Gomani kisiwani Tumbatu,Maulid hayo ambayo ni makubwa katika kisiwa hicho yaliyofanyika Novemba 26 ya mwaka 2019 sawa na mwezi 28 mfungo sita 1441 Hijjiria. 

Dkt.Bashiru alieleza kuwa japokuwa Serikali haina dini haiimanishi dini haina mchango katika maendeleo ya nchi,na kinyume chake taasisi hizo za kiimani zina mchango mkubwa katika maendeleo unaotakiwa kulindwa na kuenziwa kwa gharama yoyote.

Alisema kinachozuiwa ni tabia za kuendekeza imani kali za kidini zinazosababisha madhara ya kuchonganisha,kubaguana na kufarakanisha jamii na kusababisha machafuko na migogoro ya kuharibu Amani ya nchi.

“Miiko ya muumini yeyote ndio Miiko ya raia mwema yoyote,Masharti ya dini yoyote ndio masharti ya Serikali yoyote yenye ustawi wa maendeleo.

Tuna kila sababu ya kulinda tunu hii ya Amani na Utulivu wa nchi ambayo msingi wake ni uwezo wa uhuru wa kuabudu bila mipaka, na kila Mwananchi kuheshimu dini ya mwenzake.’,alisema Dkt.Bashiru.

Aliwakumbusha Waumini wa dini hiyo kila wanapokutana wakumbushane historia ya uhuru wa Dini uliopo hivi sasa nchini.Aliongeza kuwa Amani na Utulivu wa nchi havikupatikana hivi hivi bali bali umetokana na juhudi za Serikali zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar, zilizofanya kazi ya ziada ya uwepo wa misingi hiyo.

Alisema viongozi wa dini wanaoelekea katika uzeeni na wale waliofariki wanatakiwa kila Maulid kukumbukwa mchango wao walioutoa katika huduma za kiimani kwani wao ni alama tosha ya kupanda mbegu bora ya kiimani kwa watoto na vijana wa kiislamu.

Pia Katibu Mkuu huyo Dkt.Bashiru, akitoa nasaha zake, alisema daima Waumini wa dini hiyo wathamini na kuenzi juhudi za Waasisi Taifa ambao ni Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Karume na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwani ndio waliopigania uwepo wa haki ya uhuru wa kuabudu.

Katika maelezo yake Dkt.Bashiru, aliwataka Vijana wa Tumbatu kulinda Historia iliyotukuka ya Maulid hayo ya kiimani na kijamii ili yaendelee kufanyika kwa ufanisi kwa kila mwaka.

Kupitia maulid hayo Dkt.Bashiru,aliwasihi Wazazi,Walezi na Viongozi mbali mbali wa Dini na Serikali kuwa karibu zaidi na Walimu wa Madrasa kwa kuwatimizia mahitaji yao ya msingi ili wanaendee kufundisha watoto kwa bidii kwani wengi wanajitolea.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu, Mhe.Haji Omar Kheri aliwashukuru Wageni waalikwa kwa kuthamini hafla hiyo ya Maulid kwani ushiriki wao ni sehemu ya Umoja na Mshikamano wa Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini.

Mhe.Haji,alisema msikiti huo wa Gomani yanapofanyika maulid una historia kubwa ya harakati za Ukombozi na Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964, kwani Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Karume aliwasihi kufika katika Msikiti huo katika harakati za kufanya Mapinduzi ya kuondosha dhiki na dhuruma kwa Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar.

Mapema Maelfu ya Waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kwa ujumla walijitokeza katika bandari ya Tumbatu, kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally aliyekuwa mgeni rasmi, ambaye yupo nchini kwa ajili ya siku ya ziara ya siku tisa (9) ya kikazi ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Kampeni ya ujenzi Wa vyumba vya madarasa Arumeru yafanikiwa kwa asilimia 100

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Kampeni ya ujenzi Wa vyumba vya madara mapya 107 ilioanzishwa na Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  imekamilika na kupita malengo kwani wilaya hiyo imeweza kujenga vyumba vya  madarasa 149.

Akizungumzia  kampeni hiyo  Mkuu huyo Wa wilaya  alisema kuwa kampeni hiyo ilianza Mara baada ya kuingia tu wilayani humo ambapo alikuta wilaya hiyo   ikikabiliwa na tatizo LA uhaba Wa  vyumba vya  madarasa.

"Nikizungumzia sekta ya Elimu katika wilaya ya  Arumeru kama mtakumbuka nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Tarehe 28/08/2019 Wilaya yenye Halmashauri mbili za Arusha Dc, na Meru Dc zenye jumla ya tarafa 6 na kata 53 Zenye Majimbo mawili ya Arumeru Mashariki na Magharibi   Moja kati ya kazi niliyoanza nayo ni kuanzisha kampeni ya ujenzi wa madarasa 107 mapya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi ujenzi ambao unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 2  na sasa tumeweza kujenga vyumba vya madarasa 149 badala ya 107" Alisema Muro

Alibainisha kubwa Katika Halmashauri ya Meru Vyumba 35 vya madarasa ya shule za msingi na Sekondari yamekamilika na Vyumba 42 vya madarasa ya sekondari na msingi vipo kwenye hatua za mwisho kukamilika
Aliongeza kuwa mejiongeza kwa kujenga Mejengo ya utawala 2 hatua ya ukamilishaji, pamoja na Maabara 2 za science hatua ya uzekaji 
Pamoja na  kukamilisha ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la wadhibiti ubora wa Elimu .

Alisema kuwa hadi sasa imefikisha mwaka mmoja  ambapo
katika Halmashauri ya Meru wameshajenga vyumba na majengo 82 

Alibainisha katika Halmashauri ya Arusha Madarasa yaliyokamilika 34 ambapo alisema  yameanza kutumiwa kwa ajili ya sekondari na msingi na yaliyo katika hatua ya mwisho ni madarasa 73 kwa ajili ta shule za msingi na sekondari, katika Halmashauri ya Arusha jumla ya Madarasa 107 yanajengwa katika kampeni hiyo

Aidha alibainisha kuwa Kampeni  ya madarasa hayo mpaka sasa imewapa fursa ya kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 149 kutoka malengo ya kujenga vyumba 107, hivyo tumevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 100%

"Tumeweza kuongeza uandikishwaji
Wilaya imefanikiwa kuongeza idadi ya wananfunzi wanaojiunga na elimu ya msingi, sasa katika wilaya ya Arumeru wananfunzi wote wanaopaswa kuanza elimu ya msingi wanaandikishwa kwa asilimia mia 

Alisema madara haya yameaidia kwani hadi sasa Wilaya imeendelea kuongoza kwa kuwa wilaya ya kwanza kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi wa sekondari kidato cha sita (form six), na wako kwenye kumi bora kwa ufaulu kidato cha nne (form four)

"Naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutusaidia fedha kwa ajili ya utoaji wa elimu Bure jambo ambalo limetusaidia kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa, pili Niwashukuru sana wakurugenzi wa Halmashauri za Meru Emanuel Mkongo na kwa upande Wa  Arusha Dc  Advera Nbabagoye na mtangulizi wake Mhe Dkt. Charles wilson Mahera , pi waheshimiwa madiwani kwa kuridhia utoaji wa vifaa na fedha kidogo " alisema muro

Aliwashukuru pia  ubalozi wa japani ambao umewasaidia zaidi ya milioni 100, pamoja na  wadau wote  wa maendeleo , viongozi wa dini na wananchi ambao wamesimama na sisi katika kipindi hiki cha kuweka msingi wa Maendeleo ya elimu katika wilaya ya Arumeru.
 Mkuu Wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro akikagua moja ya darasa

WADAU ZAIDI YA 300 WA KILIMO HAI WAPATA MATUMAINI MAKUBWA BAADA YA WIZARA YA KILIMO KUAHIDI KUSHIRIKI KIKAMILIFU...WATOA USHUHUDA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

WADAU wa kilimo hai zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania wamekutana Jiini Dodoma katika Kongamano la Kimataifa la kilimo hai huku wengi wao wakiwa na matumaini makubwa ya kuendelezwa kwa kilimo hicho baada ya Serikali kupitia Waziri wa Kilimo na  Chakula Japhet Hasunga kuelezea namna ambavyo Wizara hiyo itatoa kipaumbele kikubwa.

Wakizungumza leo katika Kongamano hilo la Kimataifa la Kilimo Hai , linaloendelea Mjini Dodoma, wadau hao wameiambia Michuzi Media Group kuwa wamefurahishwa na kauli ya Serikali iliyotolewa na Waziri Hasunga na kwamba wanaamini sasa kilimo hicho nitapata msukumo mkubwa nchini Tanzania.

Jana  wakati Waziri Hasunga anafungua kongamano hilo,amewaambia wadau wa kilimo hicho kuwa Serikali itaweka mkazo katika kuhakikisha Watanzania wanajihusisha nacho na katika sheria ya kilimo itakayokuja kilimo hicho kitakuwa na nguvu kisheria.

Mdau wa Kilimo Hai ambaye pia ni moja ya wajumbe wa Taasisi ya Kuelendeleza Kilimo Hai Tanzania(TOAM) Janeth Maro amesena  hakika wamefurahi kusikia sauti ya Serikali katika kushirikiana na wadau hao kukiendeleza kikamilifu na hiyo ni hatua kubwa yenye kuashiria kilimo hai kinakwenda mbele zaidi ya kilimo sasa.

Mkulima wa Kilimo Hai kutoka mkoani Morogoro Pendo Ndemo amesema ukweli uliopo kilimo hicho kinafaida kubwa ya kiuchumi na kiafya na kusisitiza kuwa wanaojihusisha na kilimo hai wengi wamefanya maendeleo makubwa.

 Ambapo amesema pia anajishughulisha na ugugaji na sasa anafuga kiasili  baada ya kupata elimu inayohusu kilimo hai."Nikuwa nafuga kiasili ,ninao ng'ombe wachache lakini wenye tija.Nimefanya maendeleo makubwa."

Wakati huo huo mkulima mwingine wa kilimo hai kutoka Masasi aliyejitambulisha kwa jina la Kuruthumu amesema amekuwa akijihusisha na kilimo hicho kwa miaka saba na kwamba amepiga hatua kubwa kimaendeleo na amekuwa akilima mazao mchanganyiko.

Kwa upande wake Mariam Kasambara amesema kwamba anajihusisha na kilimo hicho tangu mwaka 2012 huko mkoani Morogoro amesema kabla ya kuanza kilimo hai alikuwa mtumiaji mkubwa wa kilimo kinachotumia kemikali lakini baada alipata ushauri na kuanza kilimo hicho.

"Kilimo hai kwa kweli kwangu mimi nakiona kinafaa kwa mkakati hizo tulizonazo ni vema tukajikita katika kilimo hai .Magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa mangi yanachangiwa na ulaji mkubwa wa vyakula ambavyo vinatokana kemikali ambazo nyingi ziko kwenye mbolea, dawa za kuondoa wadudu.Njia pekee ya kuondoka na magonjwa ni kujikita katika kilimo hai,"amesema Paulini.

 Katika kongamano hilo pamoja na wakulima kutoa ushahidi  mzuri kuhusu kilimo hicho wamesisitiza ni vema Serikali ikaendelea kushirikiana na wadau wa kilimo hicho kutatua changamoto zilizopo kwenye kilimo hicho.Hata hivyo Waziri wa Hasunga aliahidi kutatua changamoto hasa kwa kutambua vyakula vya kilimo hai ni salama zaidi.

Naye Albert Katagwira anayejihusisha na kilimo cha kahawa kinachotumia kilimo hai amesema anazo heka 150  za zao hilo na kwamba zao la kahawa ni la kimkakati na changamoto kubwa ilikuwa soko.

Hivyo baada ya kuona changamoto hizo aliamua kujikita katika kilimo hai na kwamba ametenga heka 50 na kuna tofauti kubwa hasa ya bei."Kahawa ninayo Lima mimi natumia kilimo hai, angalau nauza  vizuri kuliko wenzangu wanaolima kahawa kwa kilimo cha kisiasa,"amesema.

Amesema kutokana na kujikita na kilimo hicho msimu wa kilimo uliopita amechaguliwa kuwa mkulima Bora wa mwaka wa  kilimo cha kahawa na shamba lake la kahawa inatumika kama shamba darasa na kuna vyuo vingi wanafunzi wake wanakwenda kujifunza .Amesema hata mbolea anayotumia ni ya mabaki ya majani ya kahawa na mbolea ya samadi. 

Hata hivyo wadau wengine wamesema bado kuna changamoto ya kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu kilimo hai na kwamba kuna watu wanatamani kujua kwa kina  kuhusu kilimo hicho

Wakati Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ametumia nafasi hiyo kueleza kuna kila sababu ya kujengewa hoja zinazoshawishi kilimo hicho."Ninachokiona hapa wote tunaweza kujihusisha na kilimo hai lakini kuna mahali hatujaelewana jinsi ya kwenda pamoja kufikia kilimo hai."
Mbunge wa jumbo la  Chemba Juma Nkamia akichangia wakati wa kongamano la Kimataifa la Kilimo hai ambapo wadau zaidi ya 300 wakutana Mjini Dodoma kujadili mikakati ya kukiendeleza kilimo hicho.
Baadhi ya wadau wa kilimo hai wakifuatilia majadiliano ya kilimo hai yanayoendelea jijini Dodoma.

BASATA WAMPA BARAKA ZOTE MISS UNIVERSE KWENDA KUWAKILISHA NCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limemkabidhi bendera mwakilishi wa mashindano ya Ulimbwende ya dunia ya  Miss Universe 2019 yanayotarajia kufanyika Jiji la Atlanta nchini Marekani.

Mashindano hayo yatafanyika Desemba 08 mwaka huu, na kwa Tanzania yatawakilishwa na Shubila Stanton Kaigarula (23) Miss Universe Tanzania ambaye anasafiri leo Novemba 27 kwenda kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya ulimbwende ya Miss Universe nchini Marekani. 

Katibu Mtendaji  Godfrey Mngereza amekabidhi bendera kwa mrembo huyo na ameitumia nafasi hii kuwaasa Wasanii wengine nchini wajijengee tabia ya kuaga ili kupata baraka za Serikali.

 Amesema, pindi wanapohitajika kusafiri kwenda kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano mbalimbali ni muhimu serikali kufahamu na hilo linajenga taswira nzuri kwa taifa.
 Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza akikabidhi bendera kwa Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya ulimbwende Miss Universe 2019 yanayotarajia kufanyika Jiji la Atlanta Nchini Marekani Desemba 12 mwaka huu

TAWI LA YANGA MAFINGA WAKABIDHI TANKI NA PAMPU ZA MAJI KWA SHULE YA SEKONDARI IYONGOLE

$
0
0
Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi amewapongeza Wanachama wa Yanga Tawi la Mafinga, maarufu kama Vanyalutogo kwa juhudi za kutatua changamoto katika jamii.

Chumi amesema kitendo walichokifanya ni uwanamichezo uliotukuka  ambapo kwanza walianza na tanki la.maji na sasa wameleta pampu za kuvutia maji.

“Hongereni sana Yanga Mafinga, huu ni uwanamichezo uliotukuka, kwanza mlianza na Tanki la maji, lakini tena mkajiongeza mumekabidhi na pump.  Huu ni uzalendo wa kimichezo.”amesema Chumi.

 Tawi hilo la Mafinga limetoa msaada wa Tanki la Maji na Mashine ya kuvuta maji (Water Pump) kwa Shule ya Sekondari ya Iyongole.

Wanachama hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao tawi Gift Mwachang'a wamwtoa vifaa hivyo kwa wanafunzi ili kiutatua changamoto ya maji kwenye shule hiyo.

 “Vifaa hivi vyote vimetolewa na Wanayanga wenyewe, hii ni Timu ya Wananchi na tunawafikia Wananchi kwa namna mbalimbali,” Mwachang’a.
 

NEEMA ZANZIBAR, SMZ YAPATA GAWIO LA BILIONI 25

$
0
0


Na Iddi Haji, Maelezo, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepata faida zaidi ya shilingi bilioni 25 ikiwa ni malipo ya huduma za matumizi ya mkonga wa taifa, Serikali mtandao Visiwani Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Mkonga wa Mawasiliano Zanzibar, Mhandisi Shukuru Awadhi Suleiman amesema kwamba fedha hizo zimelipwa kutoka katika makapuni ambayo yanatumia huduma zao.

“Tumepata fedha hizo ambazo kutoka Kampuni ya simu ya ZANTEL ikiwa ni malipo kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2024” Alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema kwamba Serikali mtandao imekuwa na faida kubwa kwa wananchi ambapo sasa huduma za afya, kodi na elimu zimekuwa zikitolewa kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

Amesema katika sekta ya afya, kumekuwa na mafanikio makubwa katika huduma, vituo vya afya 24 Unguja na Pemba vimeunganishwa katia mfumo wa Serikali mtandao.

“Leo hii mgonjwa anaweza kufanyiwa vipimo kama vya X-ray katika hospitali ya Kivunge Mkoa Kaskazini Unguja na, vipimo vile vitasomwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja bila ya mgonjwa au daktari kulazimika kusafiri” Alisema Mkurugenzi Mhandisi Shukuru.

Mkuruhenzi huyo amesema kwa kutumia huduma za Serikali Mtandao, huduma za vyeti vya kuzaliwa imekuwa rahisi kwa sasa kwani wananchi wanapata vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya zao.

“Sasa hivi Wakala wa Usajili na Matukio ya Kijamii Zanzibar wanatumia huduma hizi, watu wanapata vyeti vyao vya kuzaliwa katika Wilaya zao, wanaomba huko na taarifa zao zinatumwa Makao Makuu na kufanyiwa kazi” Alisema Mkurugenzi Shukuru.

Mbali ya sekta hizo, pia Kampuni ya Uunganganishaji Maudhui ya ZMUX inatumia mkonga wa taifa katika kurusha matangazo ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Akizungumzia sekta ya kodi, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kwamba Bodi ya Mapato Zanzibar ni moja ya watumiaji wakubwa wa huduma za Serikali mtandao ambapo sasa huduma za kodi zimeunganishwa katika mtandao mmoja.

Amesema tayari wamepokea maombi ya makampuni ya simu, TTCL, na kampuni ya Comnet kutaka kutumia huduma za mkonga wa taifa.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Dkt Mzee Suleiman amesema kumekuwa na mafanikio katika matumizi ya TEHAMA hasa baada ya kukamilika kwa mkonga wa taifa.

Dkt Mzee amesema mwaka 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein alitoa agizo la kuhakikisha Zanzibar inaongeza kasi ya matumizi ya TEHAMA katika shughuli mbalimbali.

Mkurugenzi huyo amesema kuna vituo 10 vya kuwafundisha wananchi matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ambapo mafunzo hayo yanatolewa bure kwa wananchi.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA SHELUI, IGUNGA NA NZEGA MKOANI TABORA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waNzega mjini (hawaonekani pichani) Mkoani Tabora wakati akielekeaIsaka mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waIgunga mkoani Tabora wakati akielekea Nzega.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waShelui mkoani Singida wakati akielekea Igunga mkoani Tabora.
Wananchi wa Shelui wakishangilia mara baada ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli kusimama katika eneo hilo. PICHA NA IKULU

Watumishi wa TAA wasisitizwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania  Mhandisi Julius Ndyamukama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanya kazi akifafanua jambo wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha , kulia kwake ni Katibu wa Baraza hilo Bi, Naomi Semadio.
Wajumbe Wengine  wa Mkutano wa 24  wa Baraza Kuu  la Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini taarifa mbalimbali wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Wajumbe wa Mkutano wa 24  wa Baraza Kuu  la Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini taarifa mbalimbali wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha hapo .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania  Mhandisi Julius Ndyamukama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanya kazi alipokuwa akimkaribisha  mgeni rasmi wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Bw, Grayson Mwaigombe akifunga Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Arusha aliyenyoosha mkono Mhandisi Elipid Tesha akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza kuu la Wafanyakazi walipotembelea miradi inayoendelea katika Kiwanja hicho..

Watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania wamesisitizwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa umma mahala pa kazi kwa kufuata taratibu na kanuni za uendeshaji wa kazi za Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi) Bw, Grayson Mwaigombe  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leornard Chamuriho alipokuwa akifunga Mkutano wa 24 wa Baraza kuu la Wafanyakazi Jijini Arusha.
“Umetolewa mfano  na Mwenyekiti wa Baraza  eneo la uendeshaji katika Kiwanja cha Ndege cha  kimataifa cha Julius Nyerere kwa mujibu wa sheria za maadili na sheria za fedha za Umma kama Watumishi tunaohudumia Mamlaka hatupaswi kujiingiza katika shuguli za kibiashara za Mamlaka husika kwani sheria za maadili ya umma zinatoa muongozo wa katazo wa kushiriki shuguli za biashara za Taasisi yako” alisema.
Aidha Mwaigombe aliendelea kusema tathmini mbalimbali kutoka kwa Idara na Vitengo mbalimbali na yale yote yaliyotolewa kama mchango na taarifa, Menejimenti ya Mamlaka iangalie namna ya kuyafanyia kazi na kuboresha ili kufikia kikao kingine kuwe na taarifa zinazoridhisha kutokana na yale yaliojadiliwa.
Akizungumzia kuhusu afya Bwana Mwaigombe alisema elimu iliyotolewa ya ugonjwa wa Homa ya ini ikalete chachu kwa wajumbe wa Baraza hilo ili kuweza kupima  afya zao  huku menejimenti ikiangalia namna ya kulifanyia kazi kwa kuweza kuwasaidia Watumishi wote kuweza kupima na kupata chanjo kwani limekuwa ni gonjwa linalopoteza nguvu kazi katika kulijenga Taifa kwa ujumla.
Awali akizungumzia kuhusu uadilifu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano huo  Mhandisi  Julius ndyamukama alisema ni lazima Watumishi wote wajitathmini haswa katika eneo la kuwa miongoni mwa watu wenye mikataba ya biashara ndani ya Taasisi kwani ni kinyume na taratibu za maadili ya utumishi wa umma huku akiwashauri wanaofanya hivyo kujitathmini.
Pia Mhandisi Ndyamukama alisisitiza kuwa ni  kosa kutuma taarifa za Taasisi  kiholela  na  zisizo rasmi kwenye makundi sogozi (Social Media)  na vyombo vya habari ikiwa sio msemaji wa Taasisi  hivyo Watumishi wanapaswa kuliangalia hilo kwa umakini kwani hata sheria ya mwaka 2015  ya makosa ya mtandao hairuhusu kufanya hivyo.
Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa  Baraza pia wameweza kutembelea Kiwanja cha ndege cha Arusha kujionea miradi mitatu ambayo inafanywa na kiwanja hicho ikiwemo la utengenezaji wa eneo jipya la maegesho ya magari  lenye ukubwa wa mita za mraba 13,296  kwa kiwango cha lami ambalo litakuwa na uwezo wa  kupaki magari 250 , eneo la “parallel tax way” lenye urefu wa  mita 500  ambalo litasaidia ndege kuelekea  katika eneo la maegesho ya ndege  na barabara mbadala ya njia ya magari.
 Akizungumza Meneja wa Kiwanja hicho cha Ndege Mhandisi Elipid Tesha  alisema  baada mara baada ya kukamilika kwa miradi hiyo mradi utakaofuata baada ya taratibu za zabuni kukamilika ni  kuongeza eneo  la mita 200 la  barabara ya kuruka na kutua ndege  ili kuwezesha ndege aina za Bombardier Dash 8 Q- 400 kuweza kutua katika Kiwanja hicho pamoja na eneo la kugeuzia ndege.
Mkutano huo wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi umefanyika kwa siku mbili  katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha ukijumuisha Wajumbe Kutoka Kanda mbalimbali pamoja na menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na kufungwa rasmi katika siku ya jana.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DK.PHILIP MPANGO ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI UTOAJI TUZO KWA WALIOPATA ALAMA ZA JUU MAFUNZO YA MASOKO YA MITAJI NA DHAMANA

$
0
0

Na Ripota Wetu, Michuzi Globu ya jamii

WAZIRI wa Fedha na mipango Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu 20 kati ya 16623 waliopata alama za juu katika mafunzo ya kukidhi vigezo vya kimataifa vya masoko ya mitaji na dhamana.

Atolewaji wa tuzo hizo unatarajia kufanyika kesho Novemba 28 ,2019 katika Ukumbi wa Benki  kuu jijini Dar es Salaam .

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya mosoko ya mitaji na dhamana (SMCA) Nicodemus Mkama .amefafanua kuwa mamlaka  hiyo ambayo itatoa tuzo hizo kesho pamoja na mambo mengine  inawajibu wa kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji ambayo ni sehemu  ya mfumo wa sekta ya Fedha unaowezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu au Fedha za muda mrefu kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Mamlaka hiyo ina majukumu makubwa mawili ambayo yanawezesha kuendelea na kusimamia ili kuhakikisha kwamba yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria katika kutimiza wajibu wa kuendeleza mamlaka hiyo imetekeleza mambo majumumu makubwa  mawili.

"Moja tuliendesha shindano la wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini ambapo tulitarajia kuwa nawashiriki wapatao 7000 lakini tumeweza kupata washiriki 16623 hivyo tumevuka lengo na kuweza kupata mafanikio asilimia 233.

"Haya ni mafanikio makubwa sana katika shindano hili, na hii imetokana na matumizi ya simu ambayo tuliweza kutumia teknolojia ambayo tulifanya utafiti tuliona nyezo inayotumiwa na wanafunzi wengi  vyuoni na katika taasisi za elimu  juu nchini hivyo shindano hili limepata mafanikuo makubwa na kesho tutatoa tuzo.kwamba kwa waliopata alama za." Amesema Mkama

Amesema katika Utoaji huo wa tuzo mshindi wa kwanza atapata Fedha tasilim shilingi milioni 1.8 na mshindi wa pili atapata shilingi 1.4 ambapo mshindi wa tatu atapata laki 8 ,na mshindi wa nne  shilingi 4 na washindi wengine 20 waliopata alama za juu watapata laki 2.5.vilevile watatakiwa kuziwekeza katika hisa ambazo za Kampuni zilizoorodheshwa katika soko la hisa Dar es Salaam.

Amesema vilevile  kutakuwa na hafla za kuwatunuku watendaji katika masoko ya mitaji ambao wanakidhi  viwango vya kimataifa kwa ajili ya kujiendesha katika masoko yeyote ulimwenguni.

Pia amesema kampuni zilizowezesha kununua na kuuza hisa kwenye soko la hisa ambao wanaita na kwamba ili uweze kupata leseni kutoka katika mamlaka moja wapo moja ya kigezo ni kuhakikisha kwamba unapata mafunzo ambayo yanakidhi vigezo vya kimataifa na hiyo ni katika kutekeleza itifaki ya soko la Jumuiya ya Afrika mashariki ambapo taasisi katika usimamizi wa masoko  ya mitaji katika ukanda Afrika Mashariki wamekubaliana kwamba wanatakiwa kuweza kukidhi viwango na vigenzo vya kimataifa.

Amesema mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana ili weza kuingia makubaliano ya ushirikiano na moja  taasisi ya kimataifa ya nchini uingereza ili kuweza kushirikiana  kutoa mafunzo hayo hivyo waliweza kutoa mafunzo kwa shiriki ambao sasa wanakidhi vigezo vya kimataifa.
  Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya mosoko ya mitaji na dhamana (SMCA) Nicodemus Mkama akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu mamlaka hiyo kutoa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu 20 kati ya 16623 waliopata alama za juu katika mafunzo ya kukidhi vigezo vya kimataifa vya masoko ya mitaji na dhamana,ambapo ameeleza kuwa  katika tukio hilo Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Fedha na Mipangap Dkt Philip Mpango.
Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya mosoko ya mitaji na dhamana (SMCA) Nicodemus Mkama akitoa ufafanuzi zaidi mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar namna mamlaka hiyo  ilivyojipanga kutoa tuzo hizona kuongeza kuwa Mamlka hiyo inawajibu wa kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji ambayo ni sehemu  ya mfumo wa sekta ya Fedha unaowezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu au Fedha za muda mrefu kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

WALIMU 4,046 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WAFUKUZWA KAZI

$
0
0
KATIKA Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Winifrida Rutaindurwa amesema jumla ya walimu 4,046 wa shule za msingi na sekondari wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo utoro kazini, kukiuka maadili na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi.

Rutaindurwa ameyasema hayo katika mkutano wa siku mbili uliolenga kuwajengea uwezo Makatibu Wasaidizi wa TSC kutoka Wilaya zote Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, jijini Dodoma.

Katika Maelezo ya kumkaribisha Naibu Waziri (Elimu) wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara, Rutaindurwa alisema kuwa tangu TSC ianze kufanya kazi mwezi Julai, 2016 walimu 7,123 walifunguliwa mashauri ya kinidhamu baada ya kukiuka maadili ya kiutumishi.

“Mheshimiwa Naibu Waziri katika makosa yaliyotendwa kwa kipindi cha miaka mitatu, makosa 5,447 yalikuwa ya utoro kazini, makosa 1,290 kukiuka maadili, makosa 162 uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi na makosa mengine kwa ujumla wake yalikuwa 224”, alieleza Rutaindurwa.

Alifafanua kuwa TSC imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kiutumishi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Walimu ambapo walimu 4,046 walifukuzwa kazi, walimu 930 walipewa onyo/karipio, walimu 284 walipunguziwa mshahara, walimu 244 walisimamishiwa nyongeza ya mshahara, walimu 237 walishushwa cheo na walimu 14 walipewa adhabu ya kufidia hasara. 

Alieleza kuwa walimu wengi walikutwa na makosa ya utoro wakati wa zoezi la uhakiki wa watumishi kwa kuwa waliondoka kwenye vituo vyao vya kazi bila kufuata taratibu na kuruhusiwa na waajiri wao, hivyo walichukuliwa hatua za kinidhamu. 

“Wengi wa walimu waliotiwa hatiani kwa makosa ya utoro, walikuwa wameenda masomoni bila kupata ruhusa kutoka kwa waajiri wao na zoezi la uhakiki wa watumishi lilipofanyia ndipo ikagundulika kuwa ni watoro na mchakato wa kuwachukulia hatua za nidhamu ukaanza,” alisema. 

Akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Naibu Waziri anayeshughulikia elimu katika ofisi hiyo, Mhe. Mwita Waitara alieleza kuwa TSC bado ina kazi ya kufanya ili kuhakikisha walimu wanakuwa na uelewa wa kutosha juu ya taratibu za kiutumishi ili wajiepushe na makosa ya kinidhamu. 

Aliweka bayana kuwa Serikali haijivunii kuwafukuza kazi walimu wake iliyowaajiri yenyewe ikizingatiwa kuwa bado kuna changamoto ya upungufu wa walimu katika maeneo mbalimbali nchini. 

“Kwa kweli tunasikitika kuwa idadi ya walimu waliofukuzwa kazi ni kubwa, lakini ni lazima watumishi wa umma muelewe kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli haina huruma kabisa na watumishi wazembe wasiozingatia Maadili na Miiko ya kazi yao”, alisema Waitara.

Pamoja na hayo, Mhe. Waitara alieleza kuwa walimu wamekuwa na kero na malalamiko mbalimbali yanayosababishwa na kutowajibika kikamilifu kwa baadhi ya watendaji wa wanaoshughulikia masuala yao.

Alieleza baadhi ya kero hizo kuwa ni kucheleweshwa kwa malipo ya kusafirisha mizigo kwa walimu waliostaafu, walimu waliostahili kupandishwa madaraja kutopandishwa kwa wakati, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kukataa kupitisha barua za walimu wanaoomba kuhama kutoka Wilaya moja kwenda nyingine na walimu kutotendewa haki katika mashauri ya nidhamu. 

Kutokana na changamoto hizo, Naibu Waziri alipiga marufuku tabia ya baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ya kuzuia kupitisha barua za walimu wanaoomba uhamisho na kueleza kuwa wao sio wenye mamlaka ya kutoa uamuzi wa ombi la mwalimu anayetaka kuhamia wilaya nyingine. 

“Ni marufuku kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzuia kupitisha barua za walimu wanaoomba uhamisho. Wao wanapaswa kupitisha, kuweka maoni yao na kuruhusu maombi hayo yaende kwa mhusika aliyeandikiwa. Mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa ombi la uhamisho wa mwalimu ni Katibu Mkuu, TAMISEMI,” alisisitiza Mhe. Waitara.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri aliiagiza TSC kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa orodha ya walimu waliostahili kupandishwa madaraja lakini hawakupandishwa na kuiwasilisha TAMISEMI ili taratibu nyingine ziweze kufanyika.
Naibu Waziri (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kazi wa Makatibu wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu wa Wilaya, Tanzania Bara. Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo jijini Dodoma, Novemba 26 na 27, 2019.

RAIS WA ZANZIBAR AIZINDUA BOTI MPYA YA KAMPUNI YA AZAM MARINE YA KILIMANJARO VII

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuizindua Boti Mpya ya Kisasa ya Kilimanjaro VII, ya Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Makampuni ya Kilimanjaro Fast Ferreis na Azam Marine Ndg. Said Salim Bakhressa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar.Mhe. Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa wakishuhudia uzinduzi huo wa Boti hiyo uliofanyika katika eneo la Hoteli Verde Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Boti ya Kisasa ya Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries, uliofanyika katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar, (kulia kwa Rais ) Mwenyekiti wa Makamupuni ya Kilimanjaro Fast Ferries na Azam Marine.Ndg.Said Salim Bakhressa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein,na(kushoto kwa Rais ) Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar.Mhe.Balozi.Mohamed Ramia Abdiwawa na Mwenyekiti wa Makampuni ya Kilimanjaro Fast Ferries na Azam Marine.Ndg.Said  Salim Bakhressa. wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya  Azam Marine.Ndg.Abubakar Aziz Silim, akitowa maelezo ya Boti hiyo baada ya hafla ya Uzinduzi huo uliokanyika katika eneo la Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Nahodha wa Boti ya Kilimanjaro VII.Ndg.John Mkwiche, akiwa katika chumba cha kuongozea boti  wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi huo uliofanyika leo 27-11-2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar.Mhe Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kulia kwa Rais) wakiwa katika chumba cha kuongozea boti hiyo ya Kilimanjaro VII,  baada ya uzinduzi wake uliofanyika leo,27-11-2019, na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza, Mwenyekiti wa Makampuni ya Kilimanjaro Fast Ferries na Azam Marine.Ndg. Said Salim Bakhressa wakiwa katika chumba cha kuongozea boti hiyo ya Kilimanjaro VII baada ya kuizindua leo katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
BAADHI ya Wageni Waalikwa wakihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Boti ya Kisasa ya Kilimanjaro VII, uliofanyika leo katika viwanja vya ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia hafla hiyo (hayupo pichani)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya Kilinjaro Fast Ferries na Azm Marine. Ndg. Said Salim Bakheressa, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar akihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Boti ya Kilimanjaro VII, uliofanyika leo 27-11-2019.
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries Ndg, Abubakari Aziz Salim, akitowa maelezo ya kitaalam ya Boti ya Kisasa ya Kilimanjaro VII, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Boti hiyo uliofanyika katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)    

CHALINZE WAASWA KUIAMINI CCM KWA KUIPA USHINDI 2020-ZIKATIMU

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WANANCHI wa Halmashauri ya Chalinze ,mkoani Pwani wameaswa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiweze kupete kwenye uchaguzi mkuu ujao 2020 ,kutokana na utekelezaji madhubuti wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake ,Dkt.John Magufuli kupunguza changamoto katika sekta mbalimbali .

Akielezea namna utekelezaji wa ilani ya CCM ilivyogusa nafsi ya jamii katika halmashauri hiyo, baada ya kikao cha baraza la madiwani ,Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu, alieleza ,maeneo yote ya jimbo hilo yamepita bila kupigwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji na vijiji hivyo anasema dalili ya mvua mawingu anaimani CCM itashinda kwa kishindo 2020.
 Zikatimu alisema, ndani ya miaka 57 jimbo hilo lilikuwa na nishati ya umeme katika vijiji nane pekee ambapo tangu kuingia madarakani Rais Magufuli zaidi ya vijiji 40 vina umeme na vingine vikiendelea kufikishiwa umeme kupitia mradi wa REA ,Peri-Urban na ujazilizi.

Alibainisha, vijiji 20 ndivyo vilivyokuwa na maji ambapo kwa sasa jumla ya vijiji 67 vinapata maji na mradi wa maji CHALIWASA unaendelea hivyo kufikia mwaka ujao tatizo la maji litabaki historia.

Mwenyekiti huyo alielezea kwamba, zahanati 39 zilikuwepo na toka 2015 hadi sasa 43 zinajengwa na kati ya hizo nne zimekamilika,mbili zinatoa huduma na nyingine zipo katika mbalimbali za ujenzi.
Aidha, katika kipindi cha July -Septemba mwaka huu jumla ya sh.milioni 416 zilitengwa kwa ajili ya mfuko wa vijana,wanawake na wenye ulemavu .

"Wapinzani wanaona aibu, hawana jipya ,kwani Rais Magifuli kurejesha heshima ya chama,ni mafanikio makubwa yametokana na utekelezaji wa ilani na hakuna ubishi kwa hili"alifafanua Zikatimu.

Hata hivyo ,akizungumzia changamoto na mafanikio ya sekta ya elimu,Zikatimu alisema halmashauri hiyo imetenga sh.milioni 360 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na imetenga sh.milioni 579 kuzielekeza shule za sekondari kujenga madarasa.

"Sh.milioni 115 tumezipeleka Chahua kujenga shule mpya ya sekondari ambazo zitasaidia kujenga madarasa sita,milioni 110 Lupungwi kata ya Mandera kujenga madarasa matano na matundu ya vyoo,Pera milioni 40 kuongeza vyumba vy madarasa na milioni 60 kujenga maabara, na Kiwangwa imepelekwa milioni 40"

Diwani wa kata ya Kimange,Hussein Hading'oka alisema shule ya sekondari ya Kimange inakabiliwa na upungufu wa madarasa na bwalo la kulia chakula wanafunzi kwani kwa sasa hamna hali inayosababisha kula chakula chini ya miti.

Nae diwani kata ya Kibindu ,Ramadhani Mkufya alisema, katika kata hiyo shule ya sekondari ina upungufu wa madarasa manne.

Alieleza, upungufu huo unasababisha msongamano madarasani ,kwani wanafunzi wengine hukaa 150-200 katika darasa moja.

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA) YATOA GAWIO LA BILIONI 29 KWA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE

$
0
0
TMDA inaendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa gawio kwa Serikali kwa kila mwaka ambapo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali iliyopo madarakani, Mamlaka hiyo imefikisha jumla ya bilioni 29.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa kutoa gawio la TMDA kwa mwaka 2018/19 baada ya kumkabidhi Rais Magufuli mfano wa hundi yenye thamani ya bilioni 12.475 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino tarehe 24 Novemba, 2019; Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA, Mhe. Balozi Dkt. Ben Moses alisema, “Kazi ya Bodi yangu ni kuhakikisha tunaisimamia ipasavyo Mamlaka hii ili iweze kutimiza majukumu yake ya msingi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutekeleza maelekezo ya Serikali kwa maendeleo ya nchi yetu, na kwa kweli Menejimenti na watumishi wa Taasisi hii wamekuwa wakifanya kazi kwa kujituma na kuweza kufikia mafanikio haya na tutahakikisha yanakuwa endelevu.”
Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Danstan Hipolite alisema, “TMDA itaendelea kusimamia ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii, lakini pia itaendelea kusimamia vema rasilimali za Serikali ilizo nazo ili kuwa na tija na kuchangia katika pato la Taifa kama ambavyo Serikali imekuwa ikielekeza.”
TMDA ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo kabla ya tarehe 01 Julai, 2019 ilijulikana kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambapo jina hilo lilibadilika baada ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 kufanya marekebisho katika Sheria Mama ya taasisi hiyo kwa kuhamisha majukumu ya udhibiti wa bidhaa za vyakula na vipodozi kwenda katika Shirika la Viwango Tanzania.

WATAKA USHIRIKISHWAJI KATIKA MIPANGO MIJI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji Profesa Wilbert Kombe amesema tofauti kubwa kati ya mipango ya kiuchumi na ile ya maendeleo ya ardhi ndiyo chanzo kikubwa cha kutokuwepo miji iliyopangika na kutaka kuwepo ushirikishwaji ili kuwa na miji iliyopangika.

Profesa Kombe alisema hayo leo tarehe 27 Novemba 2019 katika mahojiano maalum wakati wa kikao cha siku tatu cha Wataalamu wa Mipango kinachoendelea jijini Dodoma.

Alisema, kwa sasa mipango, sera na utekelezaji kuhusiana na masuala ya mipango miji vipo lakini tatizo kubwa ni tofauti katika mipango ya kiuchumi na maendeleo kwenye sekta ya ardhi kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji ambayo iko chini ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema kuwa, tatizo lingine linalochangia suala hilo ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusiana na manufaa wanayoweza kuyapata katika ardhi iliyopangwa

‘’Mtu ukipanga ardhi yako unaongeza thamani hata kabla haijaongezewa huduma nyingine kama vile maji na umeme ndyo maana kuna tofauti kubwa kati ya anayeuza ardhi iliyopangwa na yule ambaye haijapangwa’’ alisema Profesa Kombe.

Alihimiza uwepo wa ushirikiano baina ya Serikali na sekta nyingine katika masuala mbalimbali yanayohusu upangaji miji ili kuepuka kuwa na maeneo yasiyopangwa ambayo mwisho wa siku ni kuwa na makazi holela.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa alisema, Mkutano wa wataalamu wa mipango miji unaoendelea unawakutanisha wataalaumu wote wa mipango miji kutoka serikalini na sekta binafsi ukiwa na lengo la kuboresha mipango miji nchini na kubainisha kuwa msisitizo mkubwa ni ushirikishwaji kwenye mipango ya matumizi ya ardhi.

Kwa mujibu wa Mtutwa, Ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika mipango miji ya maeneo mbalimbali nchini siyo tu utarahisisha masuala ya upangaji miji bali utaepusha hasara kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed aliiomba serikali kuipa kipaumbele mipango ya maendeleo ya ardhi kwa kuwa ardhi ndiyo kila kitu hususan katika masuala yanayohusu shughuli za binadamu.

Dkt Mohameda alisema, tatizo kubwa kwa wananchi wengi ni kutegemea matokeo ya haraka kwenye sekta hiyo wakati suala hilo linaweza kuhitaji mipango ya muda mrefu hasa katika masuala ya Mipango Kabambe.
  Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa (Kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Imaculata Senje na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara Hamdoun Masoor wakiwa katika Mkutano wa Wataalamu wa Mipango Miji Nchini unaoendeleo jijini Dodoma leo tarehe 27 Novemba 2019.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji Profesa Wilbert Kombe (Kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Vicent Shaidi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam Dkt Dawah Magembe wakiwa katika Mkutano wa Siku tatu wa Wataalamu wa Mipango Miji unaofanyia jijini Dodoma leo 27 Novemba 2019.
 Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano wa Wataalamu wa Mipango Miji unaoendelea jijini Dodoma leo 27 Novemba 2019.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdoun Mansoor akiwasilisha mada katika mkutano wa Wataalamu wa Mipango miji unaoendelea jijini Dodoma leo tarehe 27 Novemba 2019.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA ISAKA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
 
 
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nzega mjini Mkoani Tabora wakati akielekea Isaka mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Isaka Mkoani Shinyanga wakati akielekea Kahama. PICHA NA IKULU

Rais Dkt. Magufuli akizungumza na Wananchi wa Kahama

$
0
0
 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kahama mkoani Shinyanga.
 Wananchi wa Kahama wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika Wilaya hiyo wakati akitokea Mkoani Dodoma.

TB KUWAKUTANISHA WABUNGE, VIONGOZI WA DINI MWANZA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
KAMATI ya Wabunge wanaojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi imesema changamoto ya inayowakabili watu wanaougua ugonjwa huo lakini hawafikiwi na huduma za tiba imeishawishi kukutana na viongozi wa dini zote nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo wabunge walio kwenye mapambano ya TB Oscar Mukasa amesema  jijini Mwanza alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano utakaowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali nchini ili kusaidia kusambaza elimu kwenye jamii.

Mkutano huo utakaofanyika Ijumaa jijini Mwanza, mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenister Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Seleman Jafo watashiriki.

Alisema idadi ya watu nchini, wanaougua ugonjwa wa TB nchini ni kubwa huku changamoto yao kubwa ikiwa ni kutofikiwa na huduma za tiba.

“Ugonjwa wa TB ni tatizo kubwa la kiafya duniani,na hapa nchini watu zaidi ya 60,000 wanaougua hawafikiwi na huduma za tiba, hivyo kama hawapati matibabu jambo ambalo ni hatari kwa kuwa mtu mmoja anaweza kuambukiza watu 20,”alisema

Mukasa alisema wameamua kushirikisha viongozi wa dini kueneza elimu kuoitia nyumba za na endapo zitatumika vizuri zitasaidia kufikisha ujumbe na kuleta ufahamu kwa jamii juu ya tatizo na watakuwa wameunganisha nguvu pamoja na serikali yao.

“Kazi ya Bunge ni kuleta ushawishi, kuleta ustashi wa kisiasa na kuisimamia serikali na hivyo kutumia nyumba za ibada ni mkakati wa kuongeza elimu kwa jamii katika vita ya kupambana na TB kuhakikisha jamii haiathiriwi ,kwa sababu kabla ya kutumia dawa watajua unavyoambukiza,unatibiwaje lakini bila elimu itakuwa kazi bure,”alisema Mukasa.

Alieleza kuwa ushawishi huo wa viongozi wa dini utaifanya serikali kuendelea kuongeza nguvu kwenye vita hiyo kwa kuwa hayatengenishwi na mifumo ya dini na wakiamua wanaweza kufikia maeneo mengi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema maambukizi ya TB yako juu kwani takwimu za 2018 zinaonyesha wagonjwa wa TB 4,640 sawa na asilimia 6 wanatoka mkoani humu.

“Jambo hili ni kubwa lakini linazungumzwa juu juu, hivyo wataalamu wabobezi watatusaidia kupata elimu na taarifa sahihi kwenye mkutano huo wa wadau ili kupambana na tatizo hilo kwa umahiri na ufanisi mkubwa,”alisema Mongela.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa wadau ili kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Kifua kikuu (TB),utakaofanyika Ijumaa jijini humu.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Oscar Mukasa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mkutano wao na viongozi wa dini ambapo mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge Job Ndugai.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) Oscar Mukasa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mjumbe wa kamati ya wabunge walio kwenye mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na na Ukimwi akielezea mikakati ya kamati hiyo ili katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo nchini ambapo Ijumaa wiki watakuna na viongozi wa dini zote nchini na Spika wa Bunge Job Ndugai atakuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.Picha zote na Baltazar Mashaka

BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA YALETA NEEMA KWA WAFANYABISHARA WA TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa mkutano kati ya Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) na Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi na Mshauri wa Masuala ya Mikakati wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Bi. Catherine Kimaryo akizungumza na Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi ulioandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), (hawapo pichani), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka, (wa pili kushoto) na Ujumbe kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), ukiongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Fedha Bw. Lloyd Muposhi (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamaoja na Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi, mkutano huo umefanyika Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wasafirishaji wa mazao ya biashara nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mazungumzo yalikuwa yakiendelea kati yao na Uongozi wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), walipokutana kwa ajili ya kuboresha biashara kati yao uliondaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Josephine Majura-Wizara ya Fedha)

************************************

Na Josephine Majura, Dar es Salaam

Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), imeahidi neema kwa Wafanyabiashara nchini kwa kuwapatia mikopo nafuu itakayowawezesha kusafirisha na kuuza bidhaa za kilimo nje ya nchi

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Bw. Lloyd Muposhi, wakati ujumbe wa Benki hiyo uliopo nchini kwa ziara ya kikazi, ulipokutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa mazao hayo nje ya nchi ikiwemo nafaka, chai, kahawa na katani.

Bw. Muposhi, ameeleza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalikua mazuri yenye kujenga ambapo kwa mwaka ujao wa fedha ameahidi benki hiyo itawawezesha wafanyabishara ama sekta binafsi kimtaji ili waweze kukuza mitaji yao na kufanya biashara ya ushindani na yenye tija.

Kwa upande wake Mkurenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka ameishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuratibu mkutano huo na kuwakutanisha Wafanyabiashara na Uongozi wa Benki ya Biashara na Maendeleo ambapo wamepata muda wakubadilishana uzoefu na kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto mbalimbali zinazokabili usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uzoefu wa kufanya biashara pamoja na ukosefu wa mitaji.

Bw. Edwin alisema changamoto kubwa iliyopo kwa Wafanyabiashara wa ndani ni ukosefu wa mitaji kwa kuwa ni gharama kubwa kusafirisha bidhaa kwenda nje ya nchi hivyo iwapo TDB wataanza kutoa ufadhili kwa Wafanyabiashara wa Tanzania watakuwa wamewasaidia sana kuondokana na tatizo hilo.

Naye mmoja wa Wafanyabiashara walioshiriki katika mkutano huo Mkurugenzi wa ALASKATANZANIA, Bi. Jennifer Bash ameipongeza Serikali kwa kuandaa mkutano huo kwani umetoa fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya Wafanyabiashara hao na uongozi wa benki hiyo.

Alieleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili Wafanyabiashara wengi ni uhaba wa fedha na mitaji hivyo mkutano huo umetoa mwanga kwao kwa kuwa wamezungumza mambo mengi ambayo iwapo yatatekelezwa yatapunguza ombwe lililopo la ufanisi wa biashara kwa wafanyabiashara wengi.

Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam ambapo ulihusisha Uongozi kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images