Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Rushwa ya ngono inaondoa utu wa mwanamke-wadau

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

 WADAU wa kutetea ukatili wa kijinsia wamesema kuwa rushwa ya ngono  kwa wanawake waliofanyiwa lazima wapaze sauti zao ili kukomesha tabia hiyo katika kujenga utu kwa mwanamke.

Wakizungumza katika kongamano  la maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia wamesema kuwa wanawake wanaofanyiwa ukatili wa rushwa ya ngono wamekuwa wakibaki na maumivu huku wengine wakiendelea kuumizwa na rushwa hiyo.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao ni Chama cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA) , Mfuko wa Uhifadhi wa Wanawake , Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (Takukuru)pamoja na Jeshi  la Polisi.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Wanawake Mary Rusimbe amesema rushwa ya ngono inarudisha nyuma maendeleo ya wanawake kutokana na baadhi ya wanaume kuhitaji rushwa ya ngono ili kuwawezesha.

Amesema wameanzisha mtandao wa pamoja wa kupaza sauti za  kupinga rushwa za ngono katika jamii ikiwa ni Wanawake kuzungumza mara anapoona ili kufanikisha jambo lake lazima atoe rushwa hiyo basi atoe taarifa katika vyombo husika kwa ajili ya kukomesha.

Amesema kuwa rushwa iko katika hata shule za msingi ,Sekondari ambapo hao wanafanyiwa na kisha wanakaa kimya hali ambayo inawafanya kubaki na majeraha.Rusimbe amesema kuwa kujenga tabia ya jamii kuacha kufumbia macho suala la rushwa ya ngono.

 Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 ya  kupinga ukatili wa kijinsia ni Kataa Rushwa ya Ngono ,Jenga Kizazi chenye usawa.

Mkurugenzi huyo amesema baadhi yao wanatumia madaraka vibaya sehemu mbalimbali kwa wanawake na wanaume kuwapandisha vyeo watu kwa ajili ya rushwa hali ambayo inaondoa utu wa kupanda kwa vyeo hivyo.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada Pamela O' Donnell amesema kuwa rushwa ya ngono ipo duniani kote hivyo mapambano hayo ni ya dunia nzima katika kupaza sauti.

Nae Mwakilishi wa Shirika wa Kimataifa linaloshughukia wanawake  Agnes Hanti amesema kuwa mapambano yaendelee katika kujenga utu wa watu katika kuondokana na rushwa  ya ngono.Mwnyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Rehema Ludanga amesema kuwa kwa wafanyakazi wanaofanyiwa kutoa taarifa na hatua zikachukuliwa.
 Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Christina Onyango  akizungumza kuhusiana namna jeshi la polisi linavyokabiliana na rushwa ya ngono
 Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa linaloshughukia wanawake Agnes Hanti akitoa namna Shirika hilo linavyoshirikiana n wadau katika kupinga ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono wakifatilia mada katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam.

DC MKINGA AWATAKA WENYEVITI WAPYA KUACHA KUJISHUGHULISHA NA BIASHARA MAGENDO

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yonna Mark akizungumza wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari kulia ni Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole
Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark akifuatiliwa na Afisa Mfawidhi Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria 
Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani akizungumza kulia ni Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo 
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo 
Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria akieleza jambo katika mkutano huo
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo

MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yona Mark amewaonya wenyeviti wapya wa vijiji na vitongoji wilayani humo kuacha kujshughulisha na biashara za magendo badala yake wawe ndio walinzi wa kuwafichua wahusika ili kukomesha vitendo hivyo.

Mark aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari.

Alisema kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi ya Kenya hivyo ikiwemo ukanda wa bahari na nchi kavu hivyo upo uwezekano wa vitendo vya namna hivyo kufanya huku akiwataka viongozi hao kuvikemea na kutokuviruhusu kwenye maeneo yao.

“Ndugu zangu wevyeviti wa vijiji na vitongoji acheni kushirikia kwenye vitendo vya biashara za magendo kwani kufanya hivyo tunaikosesha serikali mapato yake ambayo yangesaidia kuchochea shughuli za kimaendeleo lakini pia niwaambie kwamba tutakaobaini tutashughulikiwa kwa mujibu wa sheria”Alisema Mkuu huyo wa wilaya

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wataendelea kushirikiana na TRA kufanya operesheni za kupambana na vitendo vya biashara haramu za magendo ili kuvikomesha kabisa kwani kutoka Tanga mpaka mpakani eneo la Horohoro wana kilomita 70 za maji hivyo kupambana na hilo wataanzisha bandari ndogo eneo la moa wilayani Mkinga.

Alisema kwamba wanaanzisha ili kuiwezesha serikali kupata kodi huku akieleza wanatarajia kulifanya hilo miezi michache ijayo watakuwa wamekwisha kufungua huku akiwataka wafanyabiashara hao kutumia njia halali za kupisha bidhaa zao badala ya zile za panya.

,dc akizungumzia mashine za EFD alisema zinawasaidia wafanyabiashara kutokana na kwamba zinaweka mahesabu yao vizuri kutokana na kwamba kila kinachouxwa kinaonekana.hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kutangaza biashara zao ili ziweze kutambulika na hatimaye kuweza kupata wateja na hatimaye kuwza kuingiza kipato.ulipaji wa kodi

Awali akizungumza Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar alisema kwamba hivi sasa walipa kodi wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo kwa vitendo na kuonekana maendeleo mbalimbali ikiwemo madawa, elimu bure na miradi mbalimbali inatekelezwa kupitia kodi hizo.

Naye kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Duga (CCM) Ally Ally amesema umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi ni mkubwa kutokana na kwamba maendeleo yanayopatikana yanatokana na uwepo wa ulipaji wa kodi hizo.

“Mimi kama diwani wa Kata ya Duga nitaendelea kuhakikisha ninahamasisha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa lengo la kusaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo “Alisema

Hata hivyo pia Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari ili kuwasaidia ukuaji wa maendeleo.

“Kwani wafanyabiashara kulipa kodi ndio Taifa linaendelea lakini pia kuchochea ukuaji wa maendeleo lakini pia hakikisheni mnatoa risiti wakati mnapouza bidhaa zenu “Alisema

ZAIDI YA WAKULIMA 500,000 WAMEJENGEWA UWEZO CHINI YA MFUMO SHIRIKISHI WA UDHIBITI UBORA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali wakati wa hafla ya uzinduzi wa kongamano la kitaifa la kilimo-hai la siku mbili linalofanyika Jijini Dodoma tarehe 26 Novemba 2019. 
Sehemu ya washiriki wa kongamano la kitaifa la kilimo-hai la siku mbili linalofanyika Jijini Dodoma tarehe 26 Novemba 2019 wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano la kitaifa la kilimo-hai la siku mbili linalofanyika Jijini Dodoma tarehe 26 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias canal, Wizara ya Kilimo)
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji  akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kongamano la kitaifa la kilimo-hai la siku mbili linalofanyika Jijini Dodoma tarehe 26 Novemba 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Nchi mbalimbali Duniani zinajadili na kuweka mikakati ya kuendeleza kilimo-hai. Mwaka 2010, Umoja wa Afrika kupitia Marais wake, ulipitisha Azimio la mpango na mkakati wa kilimo-hai kuelekea ajenda yake ya miaka 50 ijayo (Agenda 2063), na kuzitaka nchi zote kuchukua hatua kutekeleza azimio hilo.


Katika kufikia azimio hili la Umoja wa Afrika, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau imefanikiwa kuwa na Sera ya Kilimo iliyohusisha kilimo-hai kwa upana wake na uwekezaji kwenye viwanda vinavyo chakata mazao ya kilimo-hai.


Hii inaenda sambamba na jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli ya kutaka Tanzania ifikie uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sera ya viwanda. Ambapo kumeanzishwa dawati la kilimo-hai katika idaya ya Maendeleo ya Mazao ili  kufikia idadi ya wakulima  na wafugaji 149,000 waliothibitishwa na kuingia katika fursa ya masoko ya bidhaa za kilimo-hai kimataifa, wanaozalisha kwenye eneo la hekta takribani 278,000.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 26 Novemba 2019 wakati akifungua kongamano la kitaifa la kilimo-hai la siku mbili linalofanyika Jijini Dodoma na kuongeza kuwa zaidi ya wakulima 500,000 wamejengewa uwezo chini ya mfumo shirikishi wa udhibiti ubora (participatory guarantee system - PGS) kwa ajili ya soko la ndani na la Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Ameongeza kuwa kilimo-hai Duniani katika mataifa mbalimbali kinakua kwa kasi kubwa. Inakadiriwa kuwa soko la bidhaa na mazao ya kilimo-hai duniani ni wastani wa Euro 89 bilioni ambapo hiyo ni fursa kubwa kwa kwa Tanzania kwani ni nchi ya tatu kati ya tano barani Afrika zinazoongoza kwa kuwa na eneo na idadi kubwa zaidi zilizo thibitishwa katika mfumo huo wa kilimo-hai, ikiongozwa na Uganda na Ethiopia na kufuatiwa na Kenya na Jamhuri ya Kidemokrsi ya Kongo (DRC).


Waziri Hasunga amesema kuwa kufuatia kupitishwa kwa mtaala mpya unaojumuisha stadi na programu za kilimo-hai katika vyuo vya mafunzo ya kilimo na vyuo vikuu kikiwemo SUA, inatarajiwa idadi hiyo ikiongezeka mara dufu. Vyama vikuu vya ushirika – KCU, KNCU na KDCU pamoja na makampuni kama Biore, Biosustain, Biolands na OLAM  wamewezesha nchi yetu kufikia mafanikio hayo.


Pia, ametoa mwito kwa wadau wa kilimo-hai nchini kufanya kazi kwa karibu na Wizara na Taasisi zake na Serikali yote kwa ujumla ili kwa pamoja kuwezesha upatikanaji wa uhakika wa chakula na lishe na masoko utakao boresha maisha ya watanzania walio wengi kwenye sekta ya kilimo.


Amesema kuwa baadhi ya changamoto katika kuendeleza kilimo-hai nchini ni pamoja na uhakiki (certification) wa mazao hayo kuwa ya kilimo hai, fedha kwa ajili ya uwekezaji katika kilimohai kibiashara, kutoyafikia masoko maalumu (niche market) hususani katika nchi za Ulaya kutokana na kutokidhi vigezo vya masoko hayo na tishio la mabadiliko ya tabianchi ambayo ni fursa katika kuendelea kilimohai nchini.


Waziri Hasunga amewahakikishia wadau wote waliohudhuria katika mkutano huo kuwa Wizara ya kilimo itaendelea kushirikiana nao kwa karibu hivyo wasisite kuwasilisha mapendekezo yao wakati wowote ili Serikali iyashughulikie kwa maslahi ya kuendeleza kilimo-hai nchini.


Kadhalika, amewasihi wadau wote kupitia kongamano hilo, kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili kuweza kuongeza uzalishaji kupitia kilimo-hai.


MWISHO

DC IKUNGI ATAKA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MAJEMBE AUCTION MART AKAMATWE

$
0
0
Albeto Mweta mkazi wa Kijiji cha Ighaka wilayani Ikungi mkoani Singida, akionesha mabaki ya nyumba yake inayodaiwa kubomolewa na Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart bila ya kufuata taratibu na kuiacha familia yake ya watu 15 kukosa mahali pa kuishi.
Hamisi Said Mdimu akizungumzia jinsi alivyopata eneo hilo linalo lalamikiwa.
Wananchi wakiwa nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi walipofika kuelezea jinsi wanavyofahamu historia ya eneo lenye mgogoro.
Mzee Seleman Mhandi akizungumzia historia ya eneo lenye mgogoro.
Albeto Mweta, akizungumzia jinsi alivyo bomolewa nyumba yake.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo amemuagiza mkuu wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) kumkamata Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart kwa kukiuka taratibu kwa kubomoa nyumba ya Albeto Mweta mkazi wa Kijiji cha Ighaka wilayani humo na kusababisha familiya yake kukosa mahali pa kuishi.

Katika hatua nyingine Mpogolo amemtaka mkazi mwingine wa kijiji hicho Hamisi Said kufika ofisini kwake mapema wiki hii akiwa na barua yenye uthibitisho wa kisheria uliompa mamlaka ya kusimamia kesi iliyompa ushindi na kuweza kuwapeleka maofisa wa Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart kwenda kubomoa nyumba hiyo kwa kumsainisha Mwalimu Halima Nguya ili asimamie zoeli hilo badala ya Afisa Mtendaji.

DC Mpogolo aliongeza kuwa maofisa wa kampuni hiyo walifika katika Wilaya ya Ikungi kuja kubomoa nyumba hiyo wakitokea wilaya nyingine ya Singida mjini pasipo kuripoti ofisi yoyote ya serikali au kwa OCD ili wajue na kujiridhisha kama zoezi hilo lilikuwa likifanyika kihalali au laa.

Mpogolo alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki wakati akisikiliza maelezo ya pande mbili kati ya Hamisi Said na Albeto Mweta ambao walikuwa na kesi ya kugombea shamba la ekari moja ambalo kila mtu akidai ni lake.

Hata hivyo kumekuwa na sintofahamu katika maamuzi ya mahakama kitengo cha ardhi mkoani hapa kumpa ushindi Hamisi Said wakati shamba hilo likidaiwa kuwa lilikuwa la mkwe wake Hassani Mwinyimvua ambaye kwa sasa ni marehemu.

Imeelezwa kuwa Hassani Mwinyimvua ana watoto wakubwa waliosoma na wananafasi kubwa za kazi serikalini alishindwaje kuwapa kazi ya kufuatilia shamba hilo badala yake ampe mkwe wake Hamisi Said.

Hamisi Said akizungumzia tukio hilo alisema eneo hilo lilikuwa na mkwe wake Hassan Mwinyimvua ambaye alimchagua kulifuatilia kama msimamizi na kuwa lilikuwa la urithi wa baba yake.

Mzee Seleman Mhandi ( 85) ambaye anajua historia ya maeneo hayo anasema hata wao hawajui jinsi Hassan Mwinyimvua alivvyopata eneo hilo lililopo ndani ya maeneo ya ukoo wa akina Mweta.

Albeto Mweta ambaye ni mlalamikaji wa kubomolewa nyumba yake anasema eneo hilo ni la urithi na alikabidhiwa na baba yake Colman Mweta tangu mwaka 1984.

Afisa wa Kampuni ya Udalali ya Majembe Aution Mart kutoka Dodoma aliyesimamia zoezi la kubomoa nyumba hiyo, Edwin Binamu alisema zoezi hilo walilifanya kisheria baada ya mahakama kutoa hukumu na kuwa walimsainisha Mwalimu Halima Nguya kwa kuwa alikuwa akikaimu nafasi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho ambaye kwa wakati huo alikuwa yupo likizo ya uzazi.

MAHAKAMA YA MWANZO MTAE MBIONI KUFUNGULIWA

$
0
0
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Mruma Mruma (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Mkadiliaji Majenzi (QS) Yassin Khatib kutoka Mamlaka ya Majengo Tanzania(TBA) (wa pili kulia) akifuatiwa na Bw. Gaston Dindili , ambaye ni Fundi wa kampuni ya M/S Kiko Investment Ltd. Kushoto kwake ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Lushoto Mhe. Japhet Manyama akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Lushoto,Bw. Emmanuel Safari
Muonekano wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo ya Mtae.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Mruma akisaini kitabu cha wageni katika Mahakama ya Mwanzo Mtae, kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mtae Bw. Miraji Bakari Msagati.
………………

Na Amina Ahamad- Tanga

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Mhe. Amiri Mruma amesema Mahakama ya Mwanzo Mtae itafunguliwa haraka iwezekanvyo ili kuweza kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa huduma hiyo katika eneo hilo.

Hayo yalisemwa na Mhe. Mruma wakati alipofanya ziara ya kikazi Novemba 25, mwaka huu kwenye mahakama hiyo ili kukagua ujenzi wa mahakama hiyo,utendaji kazi wa Mahakama ya Wilaya Lushoto, Mahakama ya Mwanzo Mnazi na Mlalo na shughuli za gereza la .la kilimo la Mng’aro.

Katika ziara hiyo Mhe. Jaji Mruma alitembelea na kufanya ukaguzi katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto ambapo alikagua usimikaji wa miundombinu ya huduma ya intaneti kupitia mkongo wa Taifa, usajili wa mashauri kwenye mfumo wakuratibu na kusajili mashauri kwa njia ya kielektroniki (JSDS 2) na ulipaji wa tozo na ada za kimahakama kupitia mfumo wa malipo wa Serikali (GePG).

Mhe. Jaji Mruma aliridhishwa na utendaji wa Mahakama ya Wilaya ya Lushoto chini ya Mhe. Japhet Manyama Hakimu Mkazi Mfawidhi ambapo alitoa pongezi.

Akiwa wilayani humo, Mhe. Jaji Mruma alipata fursa ya kukagua mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mtae ulioanza tarehe 29 Desemba 2018.

Kwa mujibu wa tathmini ya mshauri elekezi, (QS) Yassin Khatibu alisema mradi huo umekamilika kwa asilimia tisini na tano (95) % ambapo tayari mfumo wa umeme umeshasimikwa na huduma ya maji safi imekamilika na maji yanapatikana kwa wingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtae, Fredson Masuke ambaye alimweleza Jaji Mruma kuwa kuwepo wa matukio mengi ya kihalifu yanayoripotiwa kituoni hapo, hali inayosababisha uhitaji mkubwa wa huduma za Mahakama.

Jaji Mruma aliahidi kufunguliwa mapema kwa Mahakama hiyo ili kesi zianze kusikilizwa na kutolewa maamuzi kwa misingi ya kisheria.

Hivyo itasaidia kupunguza matukio ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi, pale wasiporidhishwa na maamuzi ya baraza la kata na wengine kukata tamaa kupekeka kesi zao Mahakama ya Mwanzo Mnazi, Mlalo au Dochi kwa kukosa fedha za kusafiria zaidi ya kilometa 60.

MAAJABU YA NISHATI JADIDIFU KUBAINIKA DAR

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo, Mhandisi Prosper Magali.

*Vyuo kampuni lukuki ‘mguu sawa’ kwa maonesho
ZAIDI ya kampuni 20 za nishati jadidifu, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, wabunifu na vyuo mbalimbali zitashiriki maonesho ya Siku ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu Tanzania yanayoanza Ijumaa hii jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo, Mhandisi Prosper Magali, amesema maonesho hayo yatahusisha elimu, teknolojia, vifaa na huduma za nishati itokanayo na jua (solar power), upepo, na biomass.

Mhandisi Magali amezitaja baadhi ya kampuni na taasisi zilizothibitisha kushiriki maonesho hayo kuwa ni pamoja na Tirdo, Brac, Solar Sister, Ewura, Ubalozi wa Uholanzi, Carmatec,  Baraka Solar Specialist, Davis & Shirtlif, Chloride Solar, Energy Plus, Wraptec, Snv, Tarea na Ensol Tanzania Limited.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu: “NISHATI JADIDIFU KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA 2025,” yatafunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene Ijumaa Novemba 29, 2019 na kufungwa siku inayofauata (Jumamosi Novemba 30 mwaka huu) na Waziri wa Nishati, Dk Kalemani atakayemwakilisha Waziri Mkuu.

“Kimsingi, maonesho hayo yatakayofanyika Ijumaa Novemba 29 na Jumamosi Novemba 30, mwaka huu katika Viwanja ya Mnazimmoja hapa Dar es Salaam,” alisema.

Akaongeza: “Wadau na watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kushuhudia teknolojia ya renewable energy (nishati jadidifu) kwa kuwa licha ya mambo mengi mazuri yatakayofanyika na kuoneshwa, hakuna kiingilio”.

Mintarafu lengo la maonesho hayo, Magali amesema ni kuionesha jamii namna Nishati Jadidifu inavyoweza kuchangia maendeleo ya Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo Mwaka 2025.

Ofisa wa Menejimenti ya Rasilimali wa TAREA, Cecilia Richard amesema jijini Dar es Salaam kuwa, katika maonesho hayo wataalamu mbalimbali na wadau wa nishati jadidifu watatoa elimu kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo nishati hiyo.

“Ni nafasi pia watu waje wajue hata namna ya kubaini huduma au bidhaa feki za nishati jadidifu ili wasiangukie mikononi mwa wafanyabiashara wasio waaminifu,” alisema Cecilia.
Akaongeza: “… Tunataka tutoke kwenye zama za nishati kama za umeme kutumika kuwashia taa na kupikia pekee, sasa twende katika zama za kutumia umeme nyumbani kwa uzalishaji wa kuongeza kipato”.

Uchunguzi umebaini kuwa, maonesho hayo yanayoandaliwa na TAREA kwa ufadhili wa taasisi za Ubalozi wa Uholanzi, Energy Plus, Brac, Chloride Solar, Solar Sister na Ewura hufanyika kila mwaka.
 TAREA ni jumuiya yenye wanachama zaidi ya 796.

MAHAKAMA YA WATOTO DAR YAMALIZA MASHAURI KWA ASILIMIA 98

$
0
0
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto,iliyopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Mhe. Elizabeth Missana,(kulia) akizungumzia kuhusu mahakama hiyo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania waliopishwa hivi karibuni.

……………………

Na Magreth Kinabo-Mahakama

Mahakama ya Watoto, iliyopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kumaliza mashauri 438 katika kipindi cha Januari 2019 hadi Novemba 22, mwaka huu sawa asilimia 98.

Hayo yalisema na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Elizabeth Missana, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Novemba, 27 mwaka huu, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Alisema yaliyofunguliwa mwaka 2018 ni 406 na mwaka 2019 Januari 2019 hadi Novemba 22, mwaka huu yalifunguliwa mashauri 390.

Alisema idadi hiyo ya kesi hizo iliongezeka imekuwa ikiongezeka katika kipindi cha mwaka huu kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda la kuwataka wanawake waliozaa watoto na kutekelezwa na wanaume waliowapa ujauzito kujitokeza hadharani ili waweze kusaidiwa.

Aliongeza kuwa idadi kubwa ya mashauri iliongezeka katika kipindi cha miezi ya tisa .10 na 11, ambapo mashauri mengi ni ya madai.

Mhe. Missana alisema mpaka sasa Mahaakama hiyo ina mashauri yaliyobaki ni 151, kati ya hayo 28 ni ya mlundikano na 12 ni yale ambayo hawana mamlaka ya kuyasikiliza, lakini mashauri 14 wana mamlaka nayo ila sababu mbili zinasubiri majibu ya vipimo vya vinasaba (DNA).

Mashauri mengine 12 yamechelewa kwa sababu mashahidi wanafika mahakamani kwa kusuasua.

‘Tumefanikiwa kumaliza mashauri haya kwa sababu tulifanya vikao na wadauwa ustawi wa jamii na kuwaomba wananchi watusaidia watusaidie kuhudhuria katika mashauri hayo,’ alisema.

Katika Mahakama hiyo, mashauri yaliyobaki mwaka 2017ni 139 na yaliyoamuliwa mwaka 2018 ni 339 na yaliyobakia mwaka 2018 ni 199. Mwaka 2019 mahakama hiyo iliingia na mashauri 199.

VIONGOZI WA USHIRIKA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUONGEZA USHIRIKIANO

$
0
0
 Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika (Uhamasishaji), Charles Malunde (kushoto) akiongea kwenye Kikao kati ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara (TCDC), Dkt. Benson Ndiege na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David Simba, kilichofanyika Jijini Dodoma leo Jumanne, Novemba 27.
 Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara (TCDC), Dkt. Benson Ndiege (katikati) akiongea kwenye Kikao kati yake na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David Simba, kilichofanyika Jijini Dodoma leo Jumanne, Novemba 27, 2019.
 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David akiongea kwenye Kikao kati yake na Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, kilichofanyika Jijini Dodoma leo Jumanne, Novemba 27, 2019.   
 pamoja ya viongozi wa Sekta ya Ushirika kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zazibar  mara baada ya Kikao kati ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara (TCDC), Dkt. Benson Ndiege na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David Simba, kilichofanyika Jijini Dodoma leo Jumanne, Novemba 27.

VIONGOZI katika Sekta ya Ushirika kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zazibar wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika sekta hii ili kuweza kubadilishana uzoefu wa namna bora ya jinsi ya kusimamia na kuimarisha vyama vya ushirika hapa nchini.
Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa kikao kati ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara (TCDC), Dkt. Benson Ndiege na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David Simba, kilichofanyika Jijini Dodoma leo Jumanne, Novemba 27, 2019.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David Simba ambaye ameambatana na Viongozi wa Taasisi ya fedha ya Ushirika Zanzibar Faraja Union Limited (Financial Access Reliability by Joint Action – FARAJA) yupo katika ziara Tanzania Bara kutembelea na kujionea mafanikio yaliyopatikana katika baadhi ya vyama vya ushirika vinavyofanya vizuri katika mikoa ya Dar Es Salaam, Dodoma  na Iringa.
Akiongea katika kikao hicho, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara (TCDC), Dkt. Benson Ndiege amewapongeza viongozi kutoka Zanzibar kwa uamuzi wao wa kufanya ziara ya kujifunza na kupata uzoefu kutoka Tanzania Bara kwenye vyama vya ushirika vinavyofanya vizuri ili waweze pamaoja na mambo mengine kuiendesha kwa mafanikio Taasisi ya FARAJA.
“Vyama vya Ushirika ni taasisi nzuri na zina manufaa makubwa kwa Wanaushirika, tatizo ni baadhi ya viongozi wanaoviendesha na kuvisimamia vyama vya ushirika kutokuwa waaminifu na waadilifu, hivyo lazima viongozi wa Ushirika tuweke mfumo mzuri wa kusimamia vyama hivi,” amesema Dkt. Ndiege. 
Dkt. Ndiege amewataka viongozi wa ushirika kutoka Zanzibar kujifunza na kujielimisha kutokana na mafanikio na changamoto watakazojionea kwenye uendeshaji wa vyama vya ushirika watakavyovitembelea hapa nchini ikiwa ni pamoja na Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (TFC) na Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SCCULT).
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar, Khamis David Simba, amesema kuwa lengo la ziara yao kama viongozi wa Serikali wanaosimamia Sekta ya Ushirika Zanzibar na viongozi wa Taasisi ya FARAJA limeleta matumaini makubwa kutimia kwa kuwa wameweza kubadilshana mawazo na uzoefu na viongozi wenzao wa Tanzania Bara kwenye uendeshaji na usimamizi  wa Vyama vya Ushirika.
“Tumejifunza mengi na tumepata darasa zuri, kwa kubadilishana mawazo na kubaini baadhi ya sababu zinazotufanya tusiweze kupata mafanikio makubwa katika uendeshaji na usimamizi wa Vyama vya Ushirika katika maeneo yetu,” amesema Khamis David Simba, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Zanzibar.
FARAJA ni taasisi ya fedha inayoundwa na Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), Vyama vya Uzalishaji na Vikundi vya Wajasiliamali vilivyosajiliwa rasmi kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya Zanzibar. Taasisi hii inaendeshwa kwa kufuata misingi na kanuni za ushirika na Inafanya kazi Zanzibar (Unguja na Pemba).

PROFESA KABUDI ATIKISA KENYA

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, CONSTANTINE KANYASU ARIDHISHWA NA UTAYARI WASANII KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari akiwaelezea mikakati ya jinsi Wizara ya Maliasili na utalii,ilivyojipanga kushirikiana na wasanii katika kutangaza vuvitio vya utalii katika mkutano uliofanyika jana jioni JIjini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja ya baadhi ya Miss Tourism Tanzania waliokuwa washindi wa mashindano katika miaka minne iliyopita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Afisa wa Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAW) Mary Kagasheki aliyewasilisha mada ya Utalii katika mkutano uliowakutanisha wasanii mbalimbli nchini katika maandalizi ya awali ya kumtafuta miss Tourism Tanzania.
( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

**************************************


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewapongeza Wasanii kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kunadi vivutio vya Utalii.

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewahakikishia Wasanii hao kuwa yeye pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangala wapo tayari muda wote kutoa ushirikiano kwa Msanii yeyote atakayetaka kufanya kazi na Wizara hiyo.

Akizungumza na wasanii mbalimbali pamoja na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana usiku, Mhe.Kanyasu amesema kazi ya sanaa nchini inakua kwa kasi sana, Hivyo wasanii hawawezi kuachwa nyuma katika kutangaza na kuhamasisha Utalii

Katika Mkutano huo uliwakutanisha Wasanii mbalimbali wakiwemo wa wasanii filamu,vichekesho, uchongaji pamoja Washindi wa Miss Utaliu wa miaka minne iliyopita. Mhe.Kanyasu amesema Sanaa ni kichochea cha utalii.

Amesema ushirikiano huo wa Wasanii ni hatua muhimu kwa katika kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 ni kufikisha idadi ya watalii mbili na nusu.

Akizungumzia mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nne tangu yalipoanzishwa, Mhe.Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Mashindano hayo kwa kubuni vipengele viwili vya kuwatafuta Walimbwende yaani Mlimbwende Utalii wa Tanzania pamoja na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa. ( Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism International )

Amesema ubunifu huo utasaidia kunadi vivutio vya utalii kitaifa kwa kumtumia Mlimbwende wa Utalii wa Tanzania huku vivutio hivyo vya Utalii vitadiwa Kimataifa na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yana sura mpya kwa kuzingatia muono wa Kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mashindano hayo, Gideon Chipungahelo amesema vigezo vya kuwapata Washindi hao mbali ya Ulimbwende watakaokuwa nao watazingatia uelewa walionao katika kuvijua vivutio vya Utalii vilivyopo nchini

” Tunamtaka Mlimbwende atakayekuwa balozi wa Utalii na Mwenyekiti ushawishi wa kuwafanya watu wengine wahamasike kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.” alisisitiza Mratibu huyo..

Akizungumzia maandalizi ya Maonesho hayo, Chipungahelo amesema yataanza mwezi Disemba na kumalizika mwezi Machi mwakani ambapo yatafanyikia jijini Dar es Salaam .

Aidha, Mratibu huyo, Chipungahello amesema kwa upande wa Mashindano ya Utalii wa Kimataifa, nchi 56 zimeonesha utayari wa kushiriki katika Mashindano hayo.

Naye, Mwakilishi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA,) Anna Masenge amesema Mashindano hayo yatazingatia maadili ya Mtanzani na kamwe hayatakuwa kichocheo cha kuharibu utamaduni huo kwa vile Waandaji hao watazingatia kanuni na miongozo iliyotolewa na BASATA 

Kufuatia hali hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika kinyang’iro hicho huku akiwatoa hofu wazazi kuwa Mashindano hayo sio uhuni kama wengi wanavyoyachukulia.

Naibu Waziri Shonza: Wafundisheni Vijana Mila na Desturi za Makabila

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM,Mbulu
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa wadau mbalimbali katika jamii kujitokeza kuandaa matamasha ya kufundisha vijana katika kuhusu maadili, mila na desturi nzuri.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Wilayani Mbulu alipokuwa akifunga Tamasha la Nne la Utamaduni na Michezo la Jamii ya Wairaiq lilolenga kutoa piga vita mila potofu na kutoa kuwafundisha vijana wa jamii hiyo maadili,mila na desturi za jamii hiyo ili waweze kuzitunza na kuzienzi .
Akiendelea kuzungumza katika tamasha hilo Naibu Waziri huyo aliendelea kutoa wito kwa vijana wa jamii hiyo  kuhakikisha wanazingatia malengo ya tamasha hilo ikiwepo kuzingatia suala la uwajibikaji na kuchapa kazi na pia kuacha masuala ya ulevi.
“Kila jamii katika taifa letu ikijipanga kufanya tamasha kama hili la utamaduni kwa vijana hakika tutajenga taifa bora lenye nidhamu,uwajibikaji na wachapakazi na hii itasadia sana kupunguza wahalifu katika jamii yetu,”amesema Mhe.Shonza.
Pamoja na hayo Naibu Waziri huyo mwenye dhamamana ya utamaduni na michezo alitoa pongezi kwa uongozi wa Kanisa Katoliki Wilaya ya Mbulu kwa kuandaa tamasha hilo lenye tija kwa vijana ambao ndiyo taifa la kesho pamoja na Redio Habari Njema inayosimamiwa na kanisa hilo kwa kuelimisha umma kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo mila na desturi.
Kwa upande wa Mhasham Askofu Mkuu Jimbo la Kanisa Katoliki Mbulu Anthony Lagweni Gaspar ambaye ndiyo kiongozi mkuu aliyoratibu tamasha hilo alitoa ombi kwa serikali  kwa kuomba kuanzishwe kituo cha kutunzia kumbukumbu za kimila na kuhifadhi zana mbalimbali za jadi ikiwemo vifaa vya muziki wa asili kama marimba.
“Kuwepo kwa kituo kinachoelezea historia,utamaduni,mila na desturi za watu wa jamii ya kiiraiq katika wilaya hii ya mbulu kutasaidia kuongeza mapato kupitia watalii na kutangaza asili jamii hii pamoja na umahiri watu wake katika mchezo wa riadha,’’alisema Mhasham Askofu Gaspar.
Halikadhalika Askofu huyo aliendelea kusema kuwa kupitia tamasha hili tunapenda kukemea fikra za vijana za kuto wajibika na badala yake kusubiri kurithishwa mali za wazazi tunataka vijana waache uvivu na zaidi wajitume kutafuta mali zao wenyewe badala ya kutegemea mali za wazazi.
Naye Mbunge Mbulu Vijijini Bw.Flatei Massay alishukuru uongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa juhudi kubwa wanayofanya ya kusimamia masuala ya Michezo na Utamaduni kwa sasa.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akicheza ngoma  ya asili na vijana wa jamii ya Kiiraiqw waliyoshiriki shindano la Mr.Mayo na Miss Imbori ambao wanahistoria katika jamii hiyo katika masuala ya mila na desturi leo katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Wilayani Mbulu wakati wa sherehe za kufunga Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo la jamii hiyo lililoandaliwa na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu.
 
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwataka vijana wa jamii ya kiiraiqw kuzingatia yote waliyofundishwa katika Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo la jamii ya Wairaqw,alipokuwa akifunga tamasha hilo leo lililofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere,Wilayani Mbulu.
 Askofu Mhasham Askofu Anthony Lagweni Gaspar akitoa ombi kwa serikali la kujengwa kituo cha kiutamaduni kitakachohifadhi Historia, Mila na Desturi za Wairaiqw kwa ajili ya utalii  wakati kufunga Tamasha la Nne la Utamaduni na Michezo la jamii hiyo leo lilofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere, (wapili kushoto)Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza na wakwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.
 Washindi wa Shindano la Miss Imbori na Mr.Mayo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuwa washindi katika Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo liloandaliwa na Kanisa Katoliki Jimbo la  Mbulu wakati wa sherehe za kufunga tamasha hilo lilofanyika katika Uwanja wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.
 Msanii muziki wa asili Bw.Maganga Singida akitoa burudani kwa kupiga Marimba wakati wa sherehe za kufunga Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo la jamii ya Wairaiqw lililofanyika leo katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Wilayani Mbulu.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watano kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Mhasham Baba Askofu Anthony Lagweni Gaspar (wanne kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya Wilaya ya Mbulu leo katika uwanja wa Kanisa la Katoliki Jimbo la Mbulu (wasita kulia) ni Mkuu wa Wilaya Bw.Chelestino Mofuga.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimkabidhi zawadi Miss Imbori ()  wa Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo kwa jamii ya Wairaiqw ambaye jina lake halikufahamika kwa haraka leo katika sherehe za kufunga tamasha hilo lilofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Wilayani Mbulu.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimkabidhi zawadi mshindi namba moja wa kike katika mashindano ya ridhaa ya Tamasha la Utamaduni na Michezo katika sherehe za kufunga tamasha hilo lilokuwa likifanyika leo katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Wilayani Mbulu.

NCAA yaahidi kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii ndani ya Hifadhi

$
0
0
Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeahidi kuendelea kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii katika sekta za afya, elimu, maji na Mifugo kwa wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo.

Ahadi hiyo imetolewa na Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi wakati wa ziara yake ya kutembelea maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Hifadhi hiyo ikiwa ni adhma ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi hao kama sehemu ya hifadhi wananufaika na mapato yatokanayo na Utalii kwa kusaidia ujenzi wa miradi ya kijamii hususan elimu, afya, maji na huduma za Mifugo.

Dkt. Manongi ameeleza kuwa kupitia mpango wa kusaidia huduma za maendeleo kwa wakazi wanaoshi ndani ya Hifadhi hiyo , NCAA imesaidia Ujenzi wa Shule za Msingi zaidi ya 22, shule mbili za Sekondari, zahanati katika vijiji mbalimbali, miradi ya maji pamoja na chanjo za mifugo.

“Wakazi mnaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ni sehemu ya wadau wa uhifadhi, kwa kutambua umuhimu huo Serikali yenu kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itaendelea kutenga fedha katika mapato yake ya kila mwaka ili kusaidia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa kuwekeza katika elimu ya watoto wetu na kuwajengea mabweni ili kwa kuweka mazingira rafiki ya kusoma kutokana na jiografia ya maeneo ya wafugaji” ameeleza Dkt Manongi.

Ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha 2019/2020 pamoja na miradi mingine iliyopangwa kutekelezwa tayari Mamlaka hiyo imepanga kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 10 mwezi Desemba, 2019 kama sehemu ya kusaidia ujenzi wa darasa na ununuzi wa madawati 50 katika shule ya msingi Olpiro iliyoko kata ya Eyasi ili kuwasaidia watoto wa jamii ya Wadatoga kusoma katika mazingira bora na kuhakikisha kuwa utaratibu wa utoaji wa  huduma ya chakula kwa watoto wa shule hiyo unaendelea.


Kamishna Manongi amebainisha kuwa mpango wa muda mrefu wa Mamlaka hiyo ni kujenga Mabweni hasa kwa shule ambazo watoto wanatembea umbali mrefu ili kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kusoma kwa kukaa shuleni na kuepuka kutembea umbali mrefu kila siku.
 Kamishina wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt Freddy Manongi (kushoto) akiongozana na watendaji mbalimbali wa Tarafa ya Ngorongoro na kata ya Eyasi wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Mamlaka hiyo.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Eyasi iliyoko ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wakimsikiliza Dkt Manongi.
Dkt Freddy Manongi akiongea na watendaji pamoja na wananchi wa kata ya Eyasi kuhusu miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mahakama ya Wilaya ya Ilala kumaliza mashauri 150 kati ya 194 ya mlundikano ifikapo Desemba 30, mwaka huu

$
0
0

Na Magreth Kinabo- Mahakama
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, iliyopo Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, imepanga kumaliza mashauri 150 kati ya 194 ya mlundikano ifikapo Desemba 30, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo leo, Mhe. Martha Mpaze Novemba 27, mwaka huu, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, jijini Dar es Salaam.

Ambapo alisema mashauri hayo yaliyozidi umri wa miezi 12 ni ya madai na jinai, hivyo ambayo wana mamlaka nayo ni 150, na yasio na mamlaka nayo ni 44 kwa kuwa ni ya mauaji yanahitaji kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Aliongeza kwamba mashauri hayo 150 kila hakimu atasikiliza mashauri nane kwa kuwa hivi wana idadi ya mahakimu 18.

Mpaze alitaja sababu za mashauri hayo kuzidi umri ni baadhi ya mashahidi kutofika mahakamani kwa wakati na kuwepo kwa waendesha mashtaka wachache.

Aidha Mhe. Mpaze alifafanua kuwa Mahakama hiyo kwa mwaka inasajili mashauri 3,335.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2018, Mahakama hiyo ilisajili mashauri 3,038 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba, ambapo mashauri 2,624 yalimalizika, wakati katika kipindi hicho pia mwaka 2019 mashauri 2,812 yalisajiliwa na yaliyomalizika ni 2,973.mashauri. Mashauri yaliyobakia kwa mwaka 2018 ni 1,491na mwaka 2019 ni 1,456. Mahakama hiyo ilizinduliwa rasmi Februari 6, mwaka 2019
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala , Mhe. Martha Mpaze (aliyevaa blauzi ya bluu) akizungumza jambo kuhusu mahakama hiyo na majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania waliapishwa hivi karibuni.
Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

WANAFUNZI 237 WAPATA MAFUNZO YA BTEC KUTOKA MTANDAO WA KUSIMAMIA HAKI ZA MTOTO WA KIKE CAMA

$
0
0
 Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,Naomi Swai akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mkutano mkuu wa mwaka wa kumi na tatu wa CAMA AGM uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi Centre Marantha.

Na, Irene Mwidima, Globu ya Jamii
DSJ
MTANDAO wa Kupambana na Kusimamia  haki  za msingi za mtoto wa Kike CAMA AGM wamefanya mkutano Mkuu wa  kumi na tatu wa kufunga mwaka na Kukabidhi vyeti kwa wanafunzi  237 waliohitimu mafunzo ya  BTEC.

 Mkutano huo umefanyika leo Jijini  Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi  Afisa Mwandamizi Wa Elimu ya Sayansi na Teknolojia Naomi Swai akimwakilisha Kamishna wa Elimu Dr Lyabwene Mutahaba,

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwenyekiti wa CAMA Taifa Tanzania Mwanahamisi Boraafya amesema CAMA imeanzishwa mwaka 2006 ikiwa na matumaini ya kumsaidia binti au mtoto wa kike na kusimamia haki zao za msingi na  Ikiwa imeanzishwa ndani ya mkoa mmoja ambao ni Iringa.

Amesema, baadae walizidi kutanua wigo na  kwenda mikoa mingine mpaka kufika mikoa tisa ambayo ni Iringa, Dar-es-salaam, Tanga, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Pwani na Singida.

"Wakati tunaanzisha mtandao huu ulilenga zaidi katika kumsaidia binti au mtoto wa kike ikiwemo ma  kumsimamia haki zake za msingi na kuepukana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, pia kuwapa mafunzo mbalimbali yatakayowainua kiuchumi," amesema Mwanahamisi.

Afisa Mwandamizi Naomi amesema  serikali ya awamu ya tano  inalenga kujenga uchumi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na Ili kutimiza malengo hayo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndiyo yenye dhamana ya kusimamia utoaji elimu, ujuzi, maarifa na stadi zitakazowawezesha vijana wetu kutoa mchango unaotakiwa katika ujenzi wa uchumi wetu.

Naomi amesema, wamejipanga kusimamia vyema elimu na mafunzo yanayotolewa ili kuhakikisha yanakuwa bora na yanatoa mchango wenye tija katika ujenzi wa uchumi wa nchi.

"Napenda kuupongeza mtandao wa CAMA kwa kuhamasishwa ushiriki wa jamii katika kuboresha miundombinu ya kufundisha na kujifunza shuleni ikiwemo utoaji wa chakula, vifaa vya shule kwa wanafunzi, kuboresha miundombinu kama madawati, vitanda, ukarabati wa mabweni ya wasichana na nyumba za walimu, hii imechangia kuongeza uelewa kwa jamii katika utekelezaji wa waraka wa elimu bila malipo",amesema Naomi

Pia ameongeza, "Niwapongeze pia kwa kuanzisha elimu ya stadi za maisha katika shule za sekondari. Elimu hii imewezesha wanafunzi kujitambua, kuboresha ustawi wao na kufahamu vipawa vya ndani walivyonavyo, kuboresha mahudhurio na kupunguza utoro mashuleni"

"Napenda kuwapongeza wahitimu 237 wa BTEC nitakaowapatia vyeti vyao siku ya leo. Kwa kweli nimefurahi kuona vijana wana ari ya kujiendeleza ili kujiongezea ujuzi na maarifa na baada ya kuwagawia vyeti mkutano huu utakuwa umefungwa rasmi", amesema Naomi 

Mtandao wa CAMA umekuwa na utaratibu wa kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa vijana na hususani wakiwalenga watoto wa kike ili waweze kujikimu kimaisha na kuachana na masuala ua unyanyasaji wa kijinsia.
 Upendo Essau kutoka Mwanza mfadhiliwa wa CAMFED akipokea cheti cha kutambua uwezo wake katika fani mbalimbali kutoka kwa Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,Naomi Swai leo katika ukumbi wa Msimbazi Centre Marantha jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu 237 wa BTEC wakimsiliza kwa makini Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,Naomi Swai.
 Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,Naomi Swai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa BTEC leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv).

TIMU YA KILOMBERO SOKA NET ACADEMY KUFUANA NA MPWAPWA MJI NOVEMBA 30,2019

$
0
0

Na Farida Saidy, Globu ya Jamii

TIMU ya Kilombero Soka Net academy ya Ifakara mkoani Morogoro imekamilisha maandalizi yake ya michuano ya Azam Federation inavyoendelea hivi Sasa , na inatarajiwa kuondoka kesho Ijumaa kuelekea Mkoani Dodoma.

Timu ya Kilombero, itasafiri hadi mji wa  mpwapwa ili kupambana na Timu ya Mpwapwa mji mechi itakayochezwa siku ya Jumamosi  November 30 katika Uwanja wa Mji Mpwapwa uliopo wilayani humo.

Mwenyekiti wa Kilombero Soka Net Academy  Mohamedi Kambi akizungumza na Michuzi Blog, amesema kuwa maandalizi yote yamekamili na wapo tayari kupambana na Mpwapwa Mji kwani kikosi chao kimejiandaa kwa ajili ya kupata ushindi.



Ameongeza amesema kuwa Mwalimu amewandaa vyema wachezaje wake kucheza mchezo huo wa ugenini na amewahakikishia wana Kilombero kuwa watarudi na ushidi mnono kutoka kwa wana Mpwapwa hiyo sikU hivyo wasiwe na shaka kabisa.

Katika hatua nyingine amewaomba watanzania hususani Wanamorogoro kwa ujumla kuichangia timu hiyo kwani ni mara ya kwanza inacheza michuano hiyo na inavijana chipukizi wanaohitaji kuendelezwa kwenye timu hiyo.

Kampeni ya TCRA ya Mnada kwa Mnada yawafikia wakazi wa Makambako katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

$
0
0
 Wananchi wakiwa katika mstari kupata namba ya kitambulisho cha Taifa ili aweze kusajili laini za simu kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Idara ya Maji ya Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe.


 Foleni ya Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako na viungo vyake wakiwa katika mistari ya kupata namba za vitambulisho vya Taifa.
 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John akizungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Idara ya Maji ya Mji huo.
 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John akizungumza na Wananchi wa Makambako wakati wa usajili wa laini za simu kwa alama.
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akizungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa Uhamasishaji wa Wananchi kujisajili laini za simu kwa alama za vidole.

WAKAZI wa Makambako mkoani Njombe na viunga vyake  wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya  Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima

 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini  wa TCRA  Asajile John   amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mji Mdogo wa Makambako kufika katika Viwanja vya idara ya maji kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA.

 Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ili kila mwananchi aweze kuwa na namba ya vya Taifa au kuwa na kitambulisho kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.

John  amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja huduma za mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.

Hata hivyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa
 kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana  makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.

Amesema  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo lilipotolewa.

"TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema.John

Ameongeza kuwa  Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini.

Kwa upande wa Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi  kuangalia namba  vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

IRADA STYLE KUONESHA UBUNIFU WAKE NDANI YA RED RIBBON FASHION JUMAMOSI HII

$
0
0

Mbunifu wa mavazi ya Stara,   Irada Mahadhi MtongaNa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya Red Ribbon Fashion Gala 2019 yatakayofanyika Novemba 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo  yameandaliwa na Ujuzi Initiatives chini ya Designer Nguli Khadija Mwanamboka ambapo itafanyika Novemba 30 mwaka huu ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.

Wabunfiu mbalimbali 12 wakubwa kutoka  nchini wanaungana kwa pamoja  kupambana na maambukizi ya Ukimwi kwa kutumia Ubunifu wao wa Mavazi

Mbunifu wa mavazi ya Stara,   Irada Mahadhi Mtonga " Irada Style" amesema kuwa kwa mwaka huu Jukwaa la Fashion show hawatapanda wanamitindo pekee bali litakuwa na mchanganyiko wa watu mashuhuri mbalimbali watakaovalia mavazi ya wabunifu hawa kama kuonesha ushirikiano wao wa mapambano dhidi ya Ukimwi

Amesema, maonesho ya mwaka huu yatahudhuriwa na watu mashuhuri na kwa upande wake amejipanga kuonesha ubunifu wake mpya wa mavazi yake ambayo yamekuwa yanapendwa sana na wakina dada na mama.

Irada amesema pia hawataangalia wabunifu wakubwa tu, hata wazoefu, wachanga na wale wanaoanza wataonesha mavazi yao ikiwa ni jitihada za kupambana kwa pamoja katika kutokomeza maambukizi ya Ukiwmi kwa kutumia ubunifu

Wabunifu wengine watakaoshiriki kwa mwaka huu ni Martin Kadinda,
Jamila. Asya Hamsin, Malika. Khadija Mwanamboka, Jojo the African, Kulwa Mkwandule, Katty Collection, Zamda, Abdul Mwene, Melanin, Lucky na Bijoux na wengineo.

Watu wamshuhuri watakohudhuria ni pamoja na Lady Jaydee, Angela Bondo, wabuidu Ally Remtullah na Mustafa Hassanali huku kiingilio kikiwa ni  120,000  kwa viti vya VIP na kawaida ikiwa  35,000.

Jaji Mwaimu akutana na Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi Zanzibar

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Mheshimiwa Assaa Ahmad Rashid akiongea katika kikao kifupi baina yake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipokutana mapema leo Novemba 28, 2019 katika hoteli ya Madina Al Bahr iliyopo Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na Wa kwanza kulia ni Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo, Paul.
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Mheshimiwa Assaa Ahmad Rashid akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipokutana mapema leo Novemba 28, 2019 katika hoteli ya Madina Al Bahr iliyopo Visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Mheshimiwa Assaa Ahmad Rashid akiongozana kuelekea katika chumba cha mkutano na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu Novemba 28, 2019 katika hoteli ya Madina Al Bahr iliyopo Visiwani Zanzibar.
Picha ya pamoja.


Na Mbaraka Kambona,


Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ameitaja tasnia ya habari kuwa ndio wadau wakubwa wa haki za binadamu nchini.


Jaji Mwaimu alitoa kauli hiyo Novemba 28, 2019 katika mkutano uliofanyika Visiwani Zanzibar wa  kuwajengea uelewa wa pamoja  Makamishna wa tume walioteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli.


Jaji Mwaimu alieleza katika mkutano huo kuwa katika kutekeleza jukumu walilopewa la kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za binadamu chini wanawategemea sana vyombo vya habari kuelimisha jamii kuhusu haki zao.

“Vyombo vya habari ni wadau wetu wakubwa sana, wao ndio waelimishaji, wao ndio wamekuwa wakati wote wakiibua matukio mbalimbali ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa lengo la kuujulisha au kuelimisha umma”,alisema Jaji Mwaimu


“Nyie ndio mtakaoitangaza tume, kwa msingi huo, niseme kuwa tutaendelea kuwashirikisha katika yale yote tutakayokuwa tunayafanya ili kupitia nyinyi wananchi watafahamu kuhusu tume inachokifanya”,aliongeza

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa tume haiwezi kufanya kazi peke yake bila kushirikiana na wadau wengine kama vyombo vya habari, Idara nyingine za serikali, Asasi za Kiraia  na taasisi za kimataifa.


“Ni lazima tujenge mahusiano mazuri ya kazi baina yetu, hatuwezi kufanya kazi peke yetu, ni muhimu kufanya kazi na idara mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo”, alisisitiza  


Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Assaa Ahmad Rashid, ambaye ndiye aliyefungua mkutano huo kama mgeni rasmi, alimueleza Jaji Mwaimu kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa, kwa kuwa haki za binadamu ndio msingi katika nchi yetu, wameaminiwa hivyo hawana budi kulitekeleza jukumu hilo kwa ufanisi mkubwa ili kuwasaidia wananchi.


“Jukumu mlilopewa Serikali ni kubwa, sisi tunawaahidi kuwa tutaendelea kutoa ushirikiano katika kuifanya tume iweze kutekeleza majukumu yake vizuri”, alisema Rashid


Rashid aliendelea kusema kuwa Kuteuliwa kwa viongozi hao kunatoa fursa kamili na ya  wazi kwa mwananchi kupeleka lalamiko lake, na kwamba serikali imejenga mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa wadau wote hususani  Asasi za Kiraia, na wakati wote serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote ikiwemo za kimataifa ili kuhakikisha yale malengo yaliyowekwa yanafikiwa.


“Tunatambua kuwa katika kutekeleza majukumu yenu kuna changamoto mnazo kutana nazo, ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi kuhusu haki zao,lakini muendelee kueneza elimu hiyo kwa kushirikiana na taasisi zingine”,aliongeza Rashid. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Atembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia nyanya zilizopandwa katika kitalu nyumba, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Aulath Mustafa, wakati akiangalia nyanya zilizopandwa katika kitalu nyumba, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye maabara ya Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia bwawa la samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanasayansi wa Maabara, katika Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, Dkt. Shadrack Ulomi (kushoto), wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi, katika Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Walimu pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mwanafunzi anayesomea Udaktari wa Falsafa (PHD), Redempta Kajungilo, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva , wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekeza jambo, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa chakula samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

WAZIRI MKUU: NCHI YETU INAHITAJI WATAALAMU WA SEKTA YA UVUVI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji kupata watendaji wa sekta ya uvuvi kuanzia ngazi ya vitongoji kwani kuna vijiji vina mito, maziwa na baadhi vimepakana na bahari na hivyo kutoa fursa za uvuvi.

“Nchi yetu inahitaji kupata watendaji kuanzia ngazi ya vitongoji kwani vipo vijiji vyenye fursa za uvuvi hivyo vinahitaji maofisa ugani ili waweze kufanya kazi vijijini na katika vitongoji, lengo likiwa ni kuwasaidia wavuvi wadogowadogo wajue namna bora ya kuvua na kuhifadhi samaki,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli leo jioni (Alhamisi, Novemba 28, 2019), wakati akizungungumza na wahadhiri na wanafunzi mara baada ya ziara yake ya kutembelea Kampasi ya Kunduchi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema hivi sasa Serikali inaandaa mazingira mazuri ya kuendesha sekta ya uvuvi kwa kupata watalaamu wa ngazi mbalimbali watakaoisimamia sekta hiyo.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambayo imejikita katika ujenzi wa uchumi wa viwanda inasisitiza uwepo wa vyuo vya ngazi mbalimbali ili tuweze kupata watalaamu wa kuendesha viwanda vinavyojengwa nchini,” amesema.

Amesema Serikali inawatambua na inawahitaji sana wasomi wanaopata taaluma zao katika vyuo mbalimbali hapa nchini ikiwemo kampasi ya Kunduchi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambayo kwa sasa inatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vitendo ya shahada ya awali, kufundishia na kufanya utafiti kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili pamoja na wafanyakazi watafiti.

Waziri Mkuu amesema angependa kuona watafiti na watalaam wanapewa fursa ya kuongoza na kusimamia maeneo mbalimbali yanayohusiana na utafiti walioufanya ili kupata matokeo sahihi na chanya ya utafiti wao. 

Amesisitiza kuwa Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo thabiti ambayo amemkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bw. Luhaga Mpina ambaye ameyafanyia kazi na yameleta mafanikio makubwa katika sekta ya uvuvi nchini.

“Hatua ya kwanza ya kuboresha sekta ya uvuvi ilikuwa ni kuwaondoa watumishi wabovu na wasio waamifu na nafasi zao kuwapa watumishi wazuri, wenye taaluma ya uvuvi, waaminifu na wanaojali zaidi maslahi ya Taifa, kazi ambayo imefanywa na Waziri na watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,” amesema.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi ,Vijana na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema Serikali inaitegemea sana Kampasi ya Kunduchi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa vile watalaam wanaopata taaluma zao katika kampasi hiyo wanahitajika sana katika maendeleo ya uvuvi nchini.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kujenga uchumi wa viwanda ambavyo vitatumia malighafi inayopatikana nchini ikizalishwa na Watanzania wenyewe na bidhaa zake kuuzwa ndani na nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia Watanzania kuwa hivi sasa idadi ya samaki na mapato ya Serikali yanayotokana na uvuvi yameongezeka.

Amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kazi ya usimamizi wa na udhibiti wa uvuvi nchini, mauzo ya bidhaa za uvuvi nje ya nchi yalikuwa ni sh. bilioni 371 kwa mwaka na hivi sasa Serikali inajipatia sh. biloni 691 kwa mwaka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa chakula samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images