Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

Ndege ya Tanzania yashikiliwa Canada, Serikali yaelezea masikitiko yake

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa,  ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ( ATCL), Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni,  inashikiliwa nchini Canada na kesi ipo mahakamani.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Mabalozi mbalimbali, Waziri Kabudi amesema kuwa, ndege hiyo inashikiliwa baada ya kufunguliwa kwa kesi mpya, kesi ambayo imefunguliwa na  Mkulima aliyeshindwa Kesi aliyoifungua nchini Afrika Kusini.

Profesa Kabudi ameongeza kuwa,  Serikali imekasirishwa na vitendo vya  ndege zake  kushikiliwa nchini Canada, na kwamba tayari amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Canada hapa nchini kumueleza kuhusu jambo hilo.

Waziri Kabudi pia ametumia hafla hiyo kuwataka Mabalozi hao wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mataifa mbalimbali, kwenda kusimamia vizuri matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali, kwa kuwa kumekua na matumizi mabaya ya fedha  kwenye Ofisi za Ubalozi.

Ametolea mfano Ubalozi wa Tanzania huko Addis Ababa - Ethiopia  ambapo kumekua na ubadhirifu mkubwa na fedha na kuongeza kuwa kwa sasa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) inaendelea na uchunguzi.

Katika hafla hiyo, Rais John Magufuli amewaapisha Mabalozi Watano ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

GSM WAFUNGUA DUKA JINGINE LA SAMANI ZA NDANI MIKOCHENI, WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA

$
0
0
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Duka jipya la GSM HOME lililopo Mikocheni A Barabara ya Mwai Kibaki jijini, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Silent Ocean ,Salaa Mohamed amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika duka jipya na la aina yake la GSM Home ili kujipatia samani (fenicha) bora kabisa za kiwango cha kimataifa zinazoendana na kipato chao.
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo Novemba 22, mwaka huu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka hilo lililopo Mikocheni A barabara ya Mwai Kibaki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya GSM pamoja na wadau wengineo.

Kwa mantiki hii, napenda niwapongeze kwa ajili ya kuendelea kuwa wabunifu na kuja na wazo la kuanzisha duka hili kubwa la samani ambalo linasaidia watu pamoja na taasisi kupata samani zenye ubora hapa nchini.
“Napenda kuwahimiza Watanzania kufika katika duka hili jipya na la aina yake ili kuweza kujipatia samani bora na ambazo zitaendana na kipato chao. Napenda niwapongeze GSM kwa kuendelea kuwa wabunifu na kuja na wazo la kuanzisha duka hili kubwa la samani ambalo linasaidia watu pamoja na taasisi kupata samani zenye ubora hapa nchini,” alisema Mohamed.

Alisema kutokana na uwepo wa makampuni ya GSM, maelfu ya Watanzania wameweza kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na hivyo kujipatia kipato kinachowasaidia kuendesha maisha yao.

“Makampuni ya GSM yamekuwa mdau muhimu na mwenye mchango mkubwa kwa nchi yetu na pia tunatarajia mchango wenu kuongezeka zaidi hasa katika utekelezaji wa lengo la kitaifa la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda pamoja na uchumi wa kati kufikia mwaka 2025,” alisema.

Aliongeza: “Napenda kuwahakishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, itaendelea kutengeneza mazingira mazuri na rafiki ya ufanyaji biashara ili kampuni kama GSM ziendelee kukua. Serikali imedhamiria kutekeleza mapendekezo yaliyopo kwenye waraka wa Blueprint yanayolenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili nchi yetu iweze kufika kwenye uchumi wa kati.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa GSM Group, Fatma Abdallah, lengo la kuzindua duka hilo ni kuziba pengo lililopo sokoni katika usambazaji wa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, lakini pia kuwasogezea wananchi huduma zao.
“Duka hili jipya linatarajiwa kuhudumia na kukata kiu kwa watanzania wote kwani mahitaji haya ni muhimu sana katika jamii yetu, hususan fenicha za majumbani na maofisini zinazopatikana hapa GSM HOME kwa ubora wa kimataifa.

Alizitaja bidhaa zinazopatikana katika duka lao hilo kuwa ni ‘shelving’, sofa, kabati za ukutani, meza za kahawa, meza za chakula, vitanda na fenicha za chumba cha kulala, makabati ya nguo na nyinginezo za kupendezesha ofisi na nyumba.

“Napenda kuwahabarisha Watanzania kuwa fenicha zetu ni bora na za kisasa zikiwa zimetengenezwa kwa umakini wa hali ya juu na kufanyiwa tathmini ya kubaini ubora wake wa kimataifa,” alisema.

Alisema mbali ya fenicha, wanauza vyombo vya aina zote vya jikoni, bafuni na chooni vya chapa (brand) kutoka Italia pamoja na vifaa vya umeme.

Sambamba na uzinduzi huo, Fatma alisema kutakuwa na ofa na promosheni nyingi, ikiwemo punguzo la asilimia 10% kwa mwezi huu mzima wa Novemba kwa mteja atakayenunua mzigo wa thamani kuanzia sh 200,000.








RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WATANO IKULU CHAMWINO JIJINI DODOMA.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Maj. Jenerali Anselm Shigongo Bahati kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Mohamed Abdallah Mtonga kuwa Balozi waTanzania Nchini Abu dhabi (UAE) , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijiniDodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Burundi , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Jestas Abouk Nyamanga kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Ali Jabir Mwadini kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Saud Arabia , Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba23, 2019.
Mabalozi wapya watia sahihi hati za kiapo cha Maadili kwa
Watumishi wa Umma kilichoongozwa na kamshna wa Tume ya Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli . Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi wa John Kijazi, Waziri wa Mamboya nje Profesa Palamagamba Kabudi ,Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Waziriwa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi wakwanza kushoto pamoja na Mabalozi wapya mara baada ya tukio la uapisho Ikulu chamwino jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwagawia Vitafunwa wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho ya Mabalozi iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Mabalozi wapya wakila kiapo cha Maadili kwa Watumishi wa Umma
kilichoongozwa na kamshna wa Tume ya Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli . Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwapisha Mabalozi watano walioapishwa kuiwakilisha Tanzania katika Nchi za Burundi, Abu Dhabi (UAE) ,Ubelgiji, Misri pamoja na Saud Arabia katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Novemba 23, 2019.

PICHA NA IKULU


Rais Magufuli aagiza kusimamishwa kazi kwa RPC, RCO na Meneja TRA Shinyanga na kesho kupokea gawio la Serikali Chamwino

SERIKALI YAMPA SIKU 14 MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MAGU

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akimsikiliza Msimamizi wa ujenzi wa mradi wa maji mji wa Magu, Mhandisi Wilbert Bujiku akielezea hatua zilizofikiwa za ujenzi wake.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akitoa maelekezo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji Magu. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventura Kiswaga na kulia ni Msimamizi wa ujenzi wa mradi, Mhandisi Wilbert Bujiku.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventura Kiswaga wakari wa ziara ya kukaga ujenzi wa mradi wa maji wa Mji wa Magu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akitoa maelekezo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji Magu.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na ujumbe aliyoambatana nao wakimsikiliza msimamizi wa mradi, Mhandisi Wilbert Bujiku (hayupo pichani) akiuelezea mradi.
Eneo la chanzo cha maji cha mradi wa Mji wa Magu ambapo kuna mitambo ya kuvutia maji yanayotoka ziwani.

**********************************

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa muda wa siku 14 kwa Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji Mji wa Magu.

Ametoa agizo hilo Novemba 22, 2019 alipofanya ziara kwenye mradi huo Wilayani Magu, Mkoani Mwanza ili kujionea hatua ya ujenzi iliyofikiwa sambamba na kuzungumza na Mkandarasi.

Mara baada ya kutembelea eneo la chanzo cha maji na kituo cha tiba ya maji cha mradi, Mhandisi Sanga alibainisha kuwa ameridhishwa na ujenzi wa mradi na kwamba tayari wananchi wameanza kupata huduma ya maji lakini yapo maeneo machache ambayo bado hayajakamilika inavyopasa na hivyo kumtaka Mkandarasi kuhakikisha anayakamilisha kwa muda aliyopangiwa.

“Mradi unaridhisha umejengwa vizuri ila tu shida ninayoiona hapa kuna maeneo machache bado hayajakamilishwa vizuri ambayo kitaalam tunaita ‘snags’ kama kuna pipe imechomoka, koki, kurudishia rangi, na vingine vidogo vidogo. Maelekezo yangu ni kwamba ndani ya wiki mbili kuanzia leo maeneo haya yakamilike,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Aliongeza kuwa Mkandarasi amekwishafanya kazi kubwa na kwamba hizo chache zilizobaki ahakikishe anazikamilisha haraka na kwamba baada ya siku hizo 14 awe amekabidhi mradi kwa Mamlaka ya Maji Mji wa Magu na awe ameondoka kwenye eneo la mradi ili kuondokana na gharama mbalimbali za usimamizi wake.

“Hata kama hatumlipi mkandarasi kwa hizi kazi zilizobakia lakini gharama bado zitakuwepo tu ikiwa ni pamoja na kulipa watendaji wetu ambao ni wasimamizi wa mradi fedha za kujikimu na gharama zingine zikiwemo za usafiri wa kuja kukagua kazi mara kwa mara na hivyo kutumia mafuta,” alisema Mhandisi Sanga.

Aliongeza kuwa fedha za ujenzi wa mradi ni za wananchi kwani zilitolewa na wadau wa maendeleo ambao aliwataja kuwa ni Benki ya Maendeleo ya Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kama mkopo wa masharti nafuu ambao Serikali inapaswa kulipa.

Alitahadharisha kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli haipo tayari kushuhudia matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi na kwamba haitowavumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi kote nchini bila sababu za msingi.

“Namshukuru sana Mhe. Rais ambaye kimsingi ndio mtoaji wa fedha, tunasema fedha imetolewa na wafadhili lakini ni mkopo wa masharti nafuu na hivyo zitalipwa kwa kodi za wananchi, kwa hiyo tutahakikisha hata shilingi ya mwisho inatumika vizuri na hatuwezi kumtazama Mkandarasi afanye anavyojisikia yeye wakati wa kukamilisha mradi,” alisema Mhandisi Sanga.

Akizungumzia maeneo ambayo hayajafikiwa na mradi na uhitaji upo, Mhandisi Sanga alielekeza Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Magu (MAUWASA) pamoja na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wayafanyie kazi na kwamba kwa maeneo yatakayokuwa nje ya uwezo wao wayawasilishe wizarani ili wananchi wote waliokusudiwa waweze kunufaika na mradi huo. 

Aidha, alishukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Wilaya ya Magu kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Magu, kwa ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa mradi na kwa uhamasishaji walioufanya kwa wananchi waliokuwa wakidai fidia.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventura Kiswaga aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa wa maji ambao aliuelezea kuwa ni mwarobaini wa kero ya muda mrefu ya upatikanajni wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wake.

Naye msimamizi wa mradi kutoka MWAUWASA, Mhandisi Wilbert Bujiku aliahidi kusimamia vyema utekelezaji wa maelekezo ya Naibu Katibu Mkuu na kwa wakati kama ilivyoelekezwa.

Aidha, akiwasilisha taarifa ya mradi kwa ujumla, Mhandisi Bujiku alisema mradi utanufaisha zaidi ya wananchi 120,000 na kwamba hadi hivi sasa jumla ya kaya 4,911 tayari zimeunganishwa na wanapata huduma ya maji na kwamba vituo 21 vya kuchotea maji pia vimejengwa maeneo mbalimbali kulingana na idadi ya wakazi wa maeneo husika.

Aliongeza kuwa mradi umehusisha ujenzi wa tenki la lita milioni mbili za maji, ulazaji wa bomba kuu kutoka ziwani hadi kwenye tenki umbali wa kilomita 10.9 na bomba za usambazaji kwa wananchi umbali wa kilomita 67 na kwamba umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 16.

WAZIRI MHAGAMA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA UKIMWI IPOGOLO

$
0
0
Msimamizi Mkuu wa huduma za matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) Dkt. Onesmo Ng’ande akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya utoaji wa huduma za UKIMWI alipotembelea na kuweka jiwe la msingi ujenzi huo katika Kituo cha Afya cha Ipogolo Iringa.
Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela akitoa salamu wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimjulia hali Mzee Marko Mveyange aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Ipogolo kwa ajili ya matibabu.
Mwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Mhe.Omari Badwel (Mb) wa Bahi akitoa salamu za kamati hiyo wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipokea maelezo kutoka kwa Dkt. James Mfuse anayesimamia Maabara ya Kituo cha afya cha Ipogolo kuhusu ujenzi wa Jengo la Kituo cha utoaji wa huduma za UKIMWI alipotembelea kuweka jiwe la msingi Novemba 22, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wananchi wa Ipogolo walioshiriki wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha utoaji wa huduma za UKIMWI linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya cha Ipogolo mkoani Iringa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumza wananchi wa Ipogolo (hawapo pichani) walioshiriki wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha utoaji wa huduma za UKIMWI linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya cha Ipogolo mkoani Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa taarifa hali ya UKIMWI katika mkoa huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Ally Hapi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembea mkoani hapo.


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasele akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla hiyo.

************************************

MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Ipogolo Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya mradi wa uboreshaji wa vituo 20 vitakavyotoa huduma za UKIMWI kwa wasafirishaji wa masafa marefu.

Hafla hiyo iliyofanyika tarehe 22 Novemba, 2019 katika Kata ya Ruaha Kijiji cha Ipogolo mkaoni Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya ,Omari Badweli (Mb) wa Bahi, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Hamad Ahamad Njovu na wawakilishi kutoka , Ofisi ya Rais -TAMISEMI , Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,TANROADS pamoja na watendaji kutoka Halmashauri.

Kabla ya kuweka Jiwe la Msingi, Waziri Mhagama alipongeza juhudi za Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi za uratibu na utekelezaji wa masuala ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuhakikisha ujenzi wa vituo 20 unaanza katika maeneo yenye vichocheo vya maambukizi ikiwemo barabara zinazotumiwa na wasafirishaji wa masafa marefu.

“Uboreshaji wa majengo ya Kituo cha Afya cha Ipogolo kwa niaba ya maboresho kama haya kwenye vituo 20 vilivyoko kando kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam hadi mipaka ya Kasumulu (Tanzania/Malawi) na Tunduma (Tanzania/Zambia) ili kutoa huduma za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa ufanisi kwa wasafirishaji wa masafa marefu pamoja na jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo utasaidia kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuzingatia mchango utakaotokana na ujenzi wa vituo hivi”.

Waziri alieleza, ujenzi huo unaotekelezwa kupitia programu ya sattf barabara kuu ya Dar es salaam hadi mipaka ya Tunduma/Nakonde (Zambia) na Kasumulu/Songwe(Malawi) kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya kwa wananchi wa Tanzania na kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) pamoja na marekebisho yake. Uboreshaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ni moja ya utekelezaji wa haki za binadamu katika kupata huduma za afya na haki ya kuishi.

Aidha alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi hususani wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU) wanapata haki ya matibabu ya VVU na magonjwa nyemelezi, haki ya kutokubaguliwa na haki za kushirikishwa. WAVIU nao pia wana wajibu wa kulinda wengine wasipate maambukizi ya VVU.

Kwa kuzingatia Sheria ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (Kuzuia na Kudhibiti) Na. 28 ya mwaka 2008 na Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 zote zinatoa wajibu kwa kila mtu kulinda na kutetea haki za WAVIU.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwa niaba ya Mkoa wa mkoa huo Mhe.Ally Hapi alieleza kuwa, ujenzi wa vituo hivyo utasaidia kupunguza maambukizi na kuongeza tija katika huduma zitakazotolewa kupitia vituo hivyo.

“Ujenzi wa kituo hiki uwe chachu ya kuendelea kutumia huduma za Ukimwi ikiwemo matumizi sahihi ya dawa za kufubaza virusi ili kuendelea kuwa na afya njema na kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo nchini’”alisema Kasesela

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela alieleza kuwa, jamii haina budi kuendeea kuunga mkono jitihada hizo na kuhakikisha tatizo la unyanyapaa linatokomezwa kabisa na kuendelea kuishi kwa upendo, usawa na amani.

“Uzinduzi wa leo umeonesha upendo na kujali masuala ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI hiyo niwaombe viongozi wa dini kuungana na jitihada za mapambano haya kwa kuzitumia nafasi zenu kukemea masuala ya unyanyapaa kwa watu wanaosihi na maambukizi.

“Viongozi wa dini tuendelee kuliangalia hili kwa kukemea masuala ya unyanyapaa kwa malengo ya kuifikia 909090 na ikumbukwe hakuna sababu ya kufanya hivyo kwa kuzingatia usemi usemao asohili analile,”alisisitiza Leticia.

SIMBA SC YAINYUKA RUVU SHOOTING KIBABE 3-0 YAJIKITA KILELENI VPL

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono baada ya kuwafunga maafande wa Ruvu Shooting goli 3-0.

Mchezo huo umepigwa leo kwenyw Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kwa Ruvu Shooting kuwakaribisha wanamsimbazi hao mechi iliyochezwa majira ya saa 10 alasiri.

Leo, Miraji Athuman ameendela kuwa nyota wa mchezo baada ya kufanikiwa kufunga goli 2 ndani ya mechi hiyo iliyomalizika kwa ushindi wa 3-0.

Mchezo huo ulioanza kwa kila upande kumsoma mpinzani wake, ilichukua dakika 40 kwa Miraji kufumga goli la kwanza akimalizia pasi ya Kapombe, goli  lililodumu mpaka muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili Simba , Simba waliendelea kutafuta goli na kulisakama lango la Wapinzani wao, na katika dakika ya 47  Simba wanapata goli la  pili kupitia kwa  mbrazil Tairone Santos aliyemalizia kona ya Francis Kahata.

Miraji anaiandikia Simba goli la tatu na la ushindi  akimalizia pasi ya Kahata dakika ya 75.

Ruvu Shooting ilipambana kutafuta bao la kufutia machozi na ilifanya jaribio matata kupitia kwa Abdlhaman Mussa dakika ya 80 na haikuzaa matunda.

Simba inabaki kilelelni ikiwa na pointi zake 25 na inaishusha Kagera Sugar yenye alama 23 hadi nafasi ya pili kwa sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.


WABUNGE NA WAJUMBE WA SHIRIKISHO LA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Walemavu, Mhe. Stellah Ikupa (Mb), (katikati) akizungumza wakati Wabunge na Wajumbe kutoka Shirikisho la Watu wenye Mahitaji Maalum walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Watu wenye Mahitaji Maalum Mhe. Riziki Lulida (Mb), (wa pili kushoto) akizungumza wakati yeye pamoja na ujumbe wake walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro.
Katibu wa Shirikisho la Watu wenye Mahitaji Maalum Mhe. Amina Mollel (Mb), (kushoto) akizungumza wakati yeye pamoja na wajumbe wenzake walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro.
Mhifadhi Mambo kale katika Hifadhi ya Ngorongoro, Bw. Godfery Ollemoita, (kulia) akiwaelezea Wabunge na Wajumbe kutoka Shirikisho la Watu wenye Mahitaji Maalum Udongo unaohama wakati walipotembelea hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Walemavu, Mhe. Stellah Ikupa (Mb), (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Kamishina wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Fredy Manango (kushoto kwake), Wabunge na Wajumbe kutoka Shirikisho la Watu wenye Mahitaji Maalum walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro.
Kamishina wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Fredy Manango (kulia) akizungumza na Wabunge na Wajumbe kutoka Shirikisho la Watu wenye Mahitaji Maalum wakati walipotembelea mamlaka hiyo.

Wagombea 1,851 wa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoani Rukwa.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakimsikiliza Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali za mitaa manispaa ya Sumbawanga Andre Zumba (kushoto) wakati akiwaonesha mfano wa karatasi ya kupigia kura siku ya tarehe 24.11.2019.

Wagombea wa vyama vya upinzani wapatao 1,851 kushiriki katika nafasi mbalimbali za uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini tarehe 24.11.2019 ili kuwapata wawakilishi katika ngazi ya kijiji, mtaa, kitongoji pamoja na wajumbe mchanganyiko na wajumbe wa viti maalum katika ngazi hizo.

Taarifa kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa inasema kuwa wagombea hao hawatakuwa na uwezo wa kuweka mawakala kisheria kwasababu mawakala hao wanatakiwa kuwa na kiapo cha kisheria pamoja na utambulisho kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi na kuongeza kuwa ni isipokuwa mgombea mwenyewe ndiye anaweza kuwa wakala.

Aidha, ametahadharisha kuwa endao kutatokea vurugu katika maeneo ambayo kwasababu nembo ya chama cha upinzani imetumika wakati mgombea amejitoa ambapo yawezekana alijitoa kwa kuchelewa au aliamua kutosumbuka kujitoa,Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zitaimarisha ulinzi katika maeneo ya kupiga kura.

Idadi ya wagombea wa vyama vya upinzani waliobakia Mkoani Rukwa baada ya mwisho wa tarehe ya kujitoa 16.11.2019 saa 10 jioni ni katika vijiji 67 (19.7%), Vitongoji 348 (19.1)%, mitaa 9 (5.4%), wajumbe mchanganyiko 876 (11.8%) na wajumbe wa viti maalumu 551 (19.1%). Mkoa una jumla ya vijiji 339, vitongoji 1,817, mitaa165. Wajumbe mchanganyiko 7,420 na wajumbe wa viti maalum 2,875.

RC MAKONDA AWAAPISHA WAJUMBE WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA KINONDONI NA TEMEKE

$
0
0
NA K-VIS BLOG

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, leo Novemba 23, 2019 amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni na Temeke.

Kwa upande wa Wilaya ya Kionondoni, walioapishwa ni pamoja na Bw. Derek Murusuri, Balozi Celestine Christopher Liundi na Mama Merina Mlunde. 

Aidha Mheshimiwa Makonda pia aliwaapisha wajumbe wengine wane wa Wilaya ya Temeke. Akitoa nasaha zake baada ya zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda aliwataka Wajumbe hao kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro na sio kuichochea. 

Aliwataka Wajumbe hao kutumia mbinu zote kutatua migogoro ya ardhi ili mashauri yasiwe yanachukua muda mrefu. "Muwe msaada kwa watu wote na hasa wanyonge, wajane na yatima ili wapate haki yap," alisisitiza. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia), akimuapisha Bw. Derek Murusuri kuwa Mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni. 
Mhe. Makonda akimkabidhi kitendea kazi Bw. Murusuri mara baada ya kumuapisha. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul makonda (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Abubakar Kunenge (wapili kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe hao baada ya kuwaapisha.

:MLIOPITA BILA KUPIGWA MKAWATETEE WANYONGE,MSIWE MABWENYENYE-POLE POLE

$
0
0

Na Woinde Shizza michuzi Tv ,Arusha 


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha  Mapinduzi,  Hamphrey Polepole amewataka viongozi wa  CCM waliopita bila kupigwa na wale watakao chaguliwa kesho katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaofanyika nchi nzima kuhakikisha wanafanya kazi ya kutumikia wananchi kwa weledi na kujali wanyonge ,kutatua kero zao pamoja na kuwatambua wanyonge ,na sio kuanza kujisikia na kubweteka

Pole Pole ameyasema hayo leo katika kata ya Sombetini wakati akifunga kampeni za kuwanadi wagombea wanaogombania uongozi wa  nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali ya mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho November 24 nchini,   ambapo alifafanua kuwa kila atakae fanya kazi akatambue kuwa yeye ni mtumishi, isije ikatokea mmoja wao akaja akawa bwenyenye ,mangi meza mabega juu kama dereva wa trekta, badala yake wakawatumikie watanzania kama vile Rais Magufuli anavyofanya kazi ya kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Alibainisha kuwa wao kama CCM wanataka kuandika historia mpya  katika nchi ya Tanzania ,kwani Rais Magufuli alipopewa dhamana ya uongozi alijitoa kwelikweli kuwa sadaka kwa ajili ya kuwatumikia watanzania  na akawatumikia vyema na ndio maana katika kipindi cha miaka minne ameweza kuwaletea wananchi maendeleo makubwa ambayo kwa kipindi cha  nyuma hayakuwepo.

"katika kipindi hiki cha miaka minne Rais Magufuli ametekeleza vyema Ilani ya chama cha Mapinduzi,amefanikiwa kuleta mradi wa maji wa bilioni 520 ,Elimu bure,mahospitalini dawa zipo   ,barabara za lami kila mahali hivyo kwakweli ni mtu anaefanya kazi kwa vitendo na sio muongeaji kama hao wengine wasiofanya maendeleo ,wamekuwa wakipinga serikali kila kitu hata kama inafanya vyema ,wao kitu ambacho hawapingi ni kupokea posho tu bungeni ambazo zinatolewa na Serikali ya CCM"alisema Polepole

Katika hitimisho hilo la kampeni katibu huyo wa itikadi na uenezi wa CCM aliwapokeaa baadhi ya wanachama wa chama cha CHADEMA,akiwemo aliyekuwa meya wa jiji la Arusha Kalisty Lazaro pamoja na mwenyekiti wa baraza la madiwani la halmashauri ya Arusha .

Akiongea mara baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi Aliyekuwa meya wa jiji la Arusha Kalisty Lazaro alisema kuwa ameamua kumuunga Rais magufuli mkono kwa kuhamia chama cha mapinduzi ili aweze kufanga kuchapa kazi ipasavyo 

Alisema kuwa ameshidwa kukaa katika chama ambacho kinafanya kazi ya kupinga serikali katika kila jambo,hatakama ikifanya vyema Yenyewe imekuwa ikipinga huku akibainisha kuwa yeye alivyokuwa meya alishirikiana na serikali na ndio maana ameweza kutekeleza miradi mbalimbali ya jiji la Arusha.

Naomba umpelekee Rais magufuli salam kuwa nimeona nimuunge mkono ,na kwakweli katika kipindi changu cha umeya wa jiji la Arusha nilishirikiana na serikali ikiwemo mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya ,mkurugenzi na ndio maana hata jiji letu likaweza kufika hapa lilipo nadiriki kusema pamoja nilikuwa chadema ila nilikuwa natekeleza ilani ya CCM "alisema Kalist

Akiongea katika mkutano huo katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Musa Matoroka  aliwataka wananchi wa jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi kesho kupiga kura na kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika ngazi ya serikali za mitaa  kwa amani na upendo 
Aliyekuwa Meya wa jiji la Arusha kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ),Kalist Lazaro akiwapungia wananchi  na wanachama wa CCM mara baada ya kutambulishwa rasmi kuhamia chama hicho katika mkutano wa kufunga kampeni za Serikali za mitaa uliofanyika katika kata ya Sombetini,jijini humo leo.Pichani kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha  Mapinduzi,  Hamphrey Polepole 




.

THBUB yaombwa kufundisha elimu ya utawala bora nchini Kenya

$
0
0
Kamishna Rose Macharia (katikati) akiwatambulisha kwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kulia) maafisa alioongozana nao katika ziara aliyoifanya kwenye ofisi za tume Novemba 22, 2019. Aliyepeana mkono na Mwenyekiti ni Patrick Owinu. Wa pili kutoka kushoto anayetizama ni Kairishi Marimba na aliye nyuma ya Mwenyekiti ni Waziri Kipacha kutoka Sekretarieti ya Maadili nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea na wageni wake kutoka Kenya waliotembelea ofisi za tume kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya utawala bora na maadili ya viongozi.
Kamishna wa tume, Dkt. Fatma Halfan akisisitiza jambo katika kikao kifupi kilichaofanyika Dodoma baina ya tume na ujumbe kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na rushwa nchini Kenya Novemba 22,2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu.



Na Mbaraka Kambona 

Kamishna wa Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa nchini Kenya, Rose Macharia ameikaribisha Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora (THBUB) kushirikiana nao kufundisha elimu ya maadili ya viongozi katika chuo chao cha taifa cha maadili ili kukuza na kuimarisha utawala bora katika nchi hizo. 

Macharia alitoa kauli hiyo katika ziara fupi aliyoifanya katika ofizi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo Dodoma Novemba 22, 2019. 

Akiongea katika kikao baina yake na Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, Macharia alisema kuwa wametembelea tume kwa sababu wanatambua kuwa hiyo ni taasisi kongwe katika masuala ya usuluhishi na usimamizi wa utawala bora na ndio taasisi ya kwanza barani Afrika iliyoanzishwa na Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kazi hiyo. 

Macharia alieleza kuwa kwa kutambua uimara na ukongwe wa tume katika masuala ya utawala bora ndio maana wameona ni vyema kuja kujifunza na kutafuta namna nzuri ya kushirikiana katika kujenga maadili ya viongozi na utawala unaofaa kwenye jamii zao. 

“masuala ya maadili ya uongozi kwetu yalianzishwa mwaka 2011 kwa sheria ya maadili na mapambano dhidi ya rushwa, hivyo taasisi yetu bado ni changa, tumekuja kujifunza kutoka kwenu ili tuweze kushirikiana kwa njia tofauti kuhakikisha nchi zetu zinakuwa na utawala unaofaa”,alisema Macharia 

Macharia aliendelea kusema kuwa katika chuo chao wanafundisha masuala ya maadili ya uongozi, hivyo anawakaribisha tume kwenda kushirikiana nao katika chuo hicho kufundisha kwani lengo la chuo hicho ni kukuza maadili ya viongozi. 

“Lengo la chuo chetu ni kukuza maadili ya viongozi ili kuwa na utawala unaofaa, siku zote tunasema ni vyema kuzuia kuliko kusubiri jambo liharibike ndio muanze kulirekebisha”, alisisitiza Macharia 

Naye, Jaji Mwaimu akiongea katika kikao hicho kifupi alisema kuwa ni kweli tume ni taasisi kongwe sana katika masuala ya utawala bora ambayo ilianzishwa mwaka 1965 na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati huo ikiitwa tume ya kudumu ya uchunguzi kwa lengo maalumu la kusimamia maadili ya viongozi mpaka ilipobadilishwa kikatiba mwaka 2001 kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 

“Jambo hilo mlilolifanya la kuwa na chuo cha maadili ni maamuzi mazuri, na hivyo sisi sote kwa pamoja tuna mahala pa kujifunza pia kutoka kwenu”, alisema Mwaimu 

“Japo sisi tume hatufanyii kazi moja kwa moja masuala ya maadili ya viongozi lakini tumekuwa na ushirikiano mzuri sana na Sekretarieti ya maadili ya viongozi na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (PCCB), na mara zote wananchi wanapoleta malalamiko yanayohusu maadili ya viongozi au masuala yanayohusiana na rushwa tumekuwa tukiyaelekeza huko kwani wao ndio taasisi zilizoundwa kusimamia masuala hayo” Jaji Mwaimu alimueleza Kamishna Macharia 

Akiongea awali, Jaji Mwaimu alimueleza Kamishna huyo kuwa tume ni Idara huru ya serikali iliyoanzishwa kikatiba na kupewa jukumu la kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za binadamu na kusimamia misingi ya utawala bora. 

“Mimi na wenzangu tuliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hii tutajitahidi kuhakikisha tunafanya kazi zetu kwa weledi mkubwa tukizingatia sheria na taratibu zilizowekwa na nchi”,alieleza Jaji Mwaimu 

Naye, Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dkt. Fatma Halfan alisema katika kikao hicho kuwa suala la ushirikiano ni jambo muhimu, hivyo waendelee kushirikiana, na kuhusu suala la kwenda kufundisha katika chuo hicho cha maadili nchini Kenya ni jambo linalowezekana na wako tayari kushirikiana nao katika kufanikisha hilo. 

Aidha, Dkt. Fatma alimueleza Kamishna Macharia kuwa tume ni taasisi ya muungano hivyo wakipata nafasi wasisite kwenda Zanzibar pia ili kujifunza zaidi. 

Katika ziara yake hiyo, Kamishna Macharia aliambatana na maafisa kutoka tume hiyo ya Kenya ambao ni Kairishi Marimba, Patrick Owinu na Stella Mbele. 

Wengine ni Viongozi waandamizi kutoka Sekretarieti ya Maadili nchini ambao ni Waziri Kipacha na Jasmin Bakari. 

YAELEZWA BADO JAMII INAUELEWA MDOGO KUHUSU MASUALA YA MABADILIKO YA TABIANCHI, WADAU WAKUTANA KUWEKA MIKAKATI KUKABILI MABADILIKO HAYO

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

IMEELEZWA kuwa bado kuna uelewa mdogo kwa jamii kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi na kutojua namna gani wanaweza kuyakabili mabadiliko hayo kwa kipindi hiki dunia inapokabiliana nayo.

Akizungumza Dar es Salaam jana ,Mratibu wa Jukwaa la Elimu la Azaki zinazojishughulisha na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na nishati jadidifu, Baraka Machumu amefafanua kwa kipindi cha sasa jamii inapaswa kujua hatua za kuchukua dhidi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema asasi ya kiraia zinazohusiana na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi zinauweza wa pamoja wa kusaidia jamii katika kuwapa elimu ya namna gani wanaweza kupambana na mabadiliko hayo.

Machumu amesema asilimia kubwa ya jamii inajua mabadiliko ya tabianchi ni kunyesha kwa mvua kubwa na kuwepo na mafuriko na sio kujua kwa upana wake hata juu ya utumiaji wa nishati jadidifu.

“Wadau wote kwa pamoja ni vema kushirikiana na kujifunza kwa upana juu ya mabadiliko ya tabianchi na kujua ni namna gani yanaweza yakakabiliwa kwasasa hususani kuhimiza jamii kupanda miti,kutumia nishati mbadala na uhifadhiji wa taka ngumu katika sehemu maalum,”amesisitiza.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mradi wa Uwajibikaji katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi (CATI)unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kutoka Jukwaa la Mabadiliko Tabianchi(FORUMCC),Jacquiline ,Masswo amesema jukwaa hilo linatoa fursa kwa Azaki zilizoshiriki katika mafunzo hayo kujua namna gani watakavyowajibika katika elimu juu ya mabadiliko ya tabianchi nakujua njia za kukabiliana na mabadiliko hayo kwa kutumia nishati jadidifu.

“ Ujumbe wa ForumCC wa taasisi hizi ni kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika udhibiti wa taka ngumu hivyo ni fursa kwa azaki hizi kukutana mara kwa mara kujifunza katika nyenzo mbalimbali na kupeleka kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi, na kupata elimu juu ya uwajibikaji na kuzifanya taasisi hizo kuimarika katika sera na mikakati katika kuwahudumia wananchi,”amesisitiza.

Wakati huo huo Mratibu wa Mradi wa masuala ya nishati jadidifu unaofadhiliwa na Shirika la Hivos kutoka ForumCC ,Euphrasia Shayo,ameeleza takribani taasisi 31 zimeshiriki Jukwaa hilo katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya mabadiliko ya tabianchi,Utunzaji wa Taka ngumu pamoja na suala la uwajibikaji.

Alisema jukwaa hilo linatoa fursa kwa taasisi hizo kushirikiana katika kujengeana uwezo katika masuala mbalimbali yanayohusu mabadiliko ya tabianchi. Ameongeza Azaki hizo zimekutana kwenye majadiliano hayo kupitia ufadhili wa Shirika la HIVOS ambalo nalo limeshiriki kuyafanikisha na kwamba HIVOS limejikita katika kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu kama sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Pamoja na mambo mengine amesema wadau waliokutana kwenye Jukwaa hilo, ni sehemu ya mikakati ya kuhaakikisha jamii ya Watanzania wanakuwa na uelewa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu ambayo ina umuhimu mkubwa katika mazingira ya sasa.

Article 0

RADI YAUWA MMOJA ARUMERU NA KUJERUHI WATANO

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha 

Mtoto mmoja aliejulikana kwa jina la Mejoole Melau Loitale (14) amefariki dunia na wengine wa tano kujeruliwa mara baada ya Radi kubwa ilioambatana na mvua kubwa ilionyesha katika kata ya Sambaya wilayani Arumeru.

Akiongelea tukio hilo mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa tukio hilo lilitokea November 23 majira ya jioni ambapo zilitokea mvua kubwa ambazo ziliambatana na Radi ilipiga na kusababisha madhara ya watu sita, akiwemo mtoto ambaye alifariki wakati wa jitihada za kumkimbiza hospital zikifanyika .

Aidha alibainisha kuwa majeruhi mmoja amelazwa katika hospitali ya Seliani Ngaramtoni ambae ametambuliwa kwa jina la Melau likindasaru loita ( 35 )anaendelea vizuri huku majeruhi wengine wanne wameruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na kutopata madhara makubwa.

Muro alitoa Rai kwa wananchi wote wa Arumeru kuendelea kuchukua tahadhari wakati wa kipindi hiki cha mvua kikiendelea kwa kuhakikisha hawakai chini ya miti, au kwenye nguzo za nyaya za umeme.

Alitumia muda huo kutoa pole na rambirambi kwa familia ya Marehemu na kuendelea kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurejea katika shughuli zao za kawaida za kijamii. 

Aliongeza kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama , kwa kushirikiana na vikosi vya zimamoto na uokoaji viko katika hali ya tahadhari na utayari mkubwa wa kukabiliana na majanga yeyote yatakayo weza kutokea hivyo aliwataka wananchi kukaa na amani kwani Serikali ipo kwa ajili yao .


CCM Tabora Yajitamba Katika Uchaguzi Wa Serikali Za mitaa

$
0
0


Na, Editha Edward -Tabora

Wagombea wote wa chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mkoani Tabora wamepita kwa asilimia 95 bila ya kukosa wapinzani kutokana na vyama vingine kutoweka na Wagombea wengine kujitoa 

Hayo yamebainishwa na katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Solomoni Kasaba alipokuwa akizungumza na blog hii ofsini kwake

Amesema kuwa hata kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji mkoani hapo asilimia 95 ya Wagombea wote wa CCM wameshapita bila kupingwa asilimia 5 tu ndio watakaofanyiwa uchaguzi 

Katika hatua nyingine amefafanua kuwa kati ya vijiji 715 vya Mkoa mzima CCM imekosa wapinzani katika vijiji 675 hivyo Wagombea wake watapita bila kupingwa, huo ukiwa Ni ushindi wa asilimia 94.7 na uchaguzi utafanyika katika vijiji 38 tu sawa na asilimia 5.3

Aidha amebainisha kuwa kati ya mitaa 148 ya Mkoa mzima Wagombea 140 wa CCM wamepita bila kupingwa huo ukiwa Ni ushindi wa asilimia 94.5 hivyo uchaguzi utafanyika katika mitaa 8 tu ambayo Ni sawa na asilimia 5.5

Katika upande wa Vitongoji Solomoni Amesema kati ya vitongoji 3619 vya Mkoa mzima Ni vitongoji 3397 wamepita bila kupingwa hivyo uchaguzi utafanyika katika vitongoji 228 tu sawa na asilimia 6

Aidha  ametaja vyama vitakavyochuana na CCM kuwania nafasi hizo kwa baadhi ya maeneo kuwa ni NRA,  CCK, CHADEMA, CUF, Democratic Part, Demokrasia Makini, NCCR Mageuzi  na ADA TADEA. 
Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Solomoni Kasaba.

Biteko aunga mkono juhudi za wananchi jimboni Bukombe

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ameendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika jimbo hilo ambapo Novemba 23, 2019 ametoa ahadi ya mbao 700 zenye thamani ya shilingi milioni 4.2 kwa ajili ya upauaji wa Zahanati ya Kijiji cha Imalanguza.

Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara huku pia akitoa ahadi nyingine ya mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Imalanguza.
Na George Binagi-GB Pazzo, Geita

 Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano huo.
 Wakazi wa Kata ya Bukombe wakimsikiliza mbunge Doto Biteko kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguza.
 Mwonekano wa Zahanati ya Imalanguza ambayo pia mbunge Doto Biteko amekabidhi mabati 250 kwa ajili ya upauaji.
Diwani wa Kata ya Bukombe, Rozalia Masokola akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MISA YA JUMAPILI PAROKIA YA MT.MARIA IMACULATA CHAMWINO JIJINI DODOMA

$
0
0
 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka takati wa misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 24, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya  misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 24, 2019.Picha na IKULU. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki kaaika misa ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Maria Imaculata Chamwino Ikulu kijijini Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 24, 2019. Hui ni mara ya Kwanza kwa
Rais na Familia yake kushioriki katika misa katika parokia hii toka ahamkie rasmi Dodoma

WAKALA WA BENKI YA NMB WAPIGWA MSASA

$
0
0
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB – Filbert Mponzi akimkabidhi msimamizi wa Rede’s Investment Traders – mmoja wa mawakala cheti cha ushiriki mafunzo ya uwakala.
Mmoja wa mawakala akiuliza swali kwa watoa mada
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd akimkabidhi Agatha Makungu – mmoja wa mawakala cheti cha ushiriki mafunzo ya uwakala.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawakala – James Manyama akitoa mada 

**********************************

MAWAKALA wa Benki ya NMB Halimashauri za Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam wamepigwa msasa katika Semina ya kuwajengea uwezo na kuboresha huduma inayomfikia mteja wa NMB katika maeneo yao pamoja na kujilinda na uhalifu na utakatishaji fedha.

Katika semina iliendeshwa hivi karibuni katika maeneo ya Sinza na Ilala jijini Dar es Salaam,Mawakala wa Benki ya NMB walipata fursa ya kupewa elimu juu ya kumpatia mteja huduma bora, kuuliza maswali na elimu juu ya kujikinga na vitendo vya kihalifu ikiwemo kupitisha fedha chafu, ambapo ni kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza katika Semina hiyo Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd, alisema NMB Wakala ni njia inayomfikishia huduma mteja kwa urahisi zaidi na kwa wakati.

“Kwa nini tunawatumia mawakala, tumeona kwamba ni njia moja wapo inayoweza kutufanya tuwafikie wateja wetu ambao ni watanzania zaidi ya Milioni 60, hatuwezi kufika kila eneo huwa kidogo kuna ugumu wake lakini kupitia mawakala tunaweza kuwapata kila eneo wenye uwezo wa kuwahudumia wateja wetu kama vile ambavyo tumekusudia.

“Mteja wetu anaweza kutoa pesa, kuweka pesa, ataweza kulipia miamala mbali mbali, kama kulipia malipo ya maji, umeme, malipo ya serikali na ada za shule, tunasisitiza kwamba wateja wetu waendelee kutuamini kupitia mawakala wetu ambao wanaendelea kutoa huduma.

“Tumekuwa na semina mbali mbali, tukiwa tunaendelea kuwajengea uwezo mawakala ili waendelee kutoa huduma zetu kwa ukaribu Zaidi. Muhimu ni muongozo wetu kila mwaka tunataka tuwasikilize changamoto juu ya huduma zetu, tuwaulize maswali watuulize maswali wote kwa pamoja tuweze kuhakikisha huyu mtanzania anapata huduma zetu kokote kule anakopatikana kwa ufanisi mkubwa.

Badru alisema, sio kwa Dar es Salaam tu, bali wameendesha semina kama kwa zaidi ya maeneo 40 nchi nzima. Semina hizi zimeleta mafanikio makubwa sana, hasa kwa kuokoa muda wa mteja, kupata huduma ya uhakika na kwa urahisi.

“Sisi kwetu wateja ni wafalme na ndio maana tunaendelea kuwa na huduma za mbadala kama, wakala, masine za ATM, na NMB Mkononi ili kuweza kumfikia mteja wetu kiurahisi zaidi.”alisema Badru.

Naye Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawakala – James Manyama, alisema lengo la kukutana na Mawakala ni kuwapa muelekeo wa wapi Benki inaelekea kwa wakati na kuwapa mafunzo jinsi ya kujilinda na utakatishaji fedha pamoja na kuingiza fedha katika mikono ya gaidi.

“Kama Mawakala, tunawapa wajibu wa kutunza amana za wateja, kutunza usiri wa wateja, mawakala wetu wamethibitisha ubora wa huduma zetu na wameahidi kwenda kutoa huduma bora kwa wateja wetu” alisema Manyama.

Kwa upande wa Mawakala waliohudhuria semina hiyo walitoa kongole zao kwa NMB kwa jinsi ambavyo inawajali kwa kuwapaa elimu na fursa ya kutoa changamoto zao ili kuweza kuboresha huduma zao.

“Nafurahi sana kuwa karibu na NMB, nafurahia kuwepo katika hii semina, NMB wanatoa huduma nzuri, pia wako karibu na sisi mawakala wao, kila wakala anafanya kazi kwa ukaribu sana na tawi lake la NMB linalomhudumia, nashauri Watanzania wenzagu kuchangamkia fursa ya Uwakala wa NMB maana inalipa” Tedy Michael – Wakala NMB Makumbusho.

“Tunashukuru kwa semina hii ambayo imetupa elimu juu ya nini cha kufanya kwa wateja wetu, tumepata mbinu mbadala ya kutoa huduma bora kwa wananchi na tunawaahidi benki yetu pendwa ya NMB kuwa tutafanya kazi kwa weledi na kuhakisha wateja wanafurahia huduma zetu.” Alisema Khanifa Kimaro – Wakala NMB Kimara.

SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA 55 YA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI MWIKA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza mwanafunzi wa mwaka wa pili Shahada ya Utawala na Wanyamapori, Ndg. Boaz Loya aliemuelezea kuhusu tabia za ndege mbalimbali alipokuwa akikagua maonesho yaliyoandaliwa na Chuo hicho leo Mkoani Kilimanjaro. Wa pili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt.Khamis Kigwangala.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wahitimu wa Chuo cha usimamizi wa wanyamapori mwika wakati wa mahafali ya 55 ya chuo hicho leo Mkoani Kilimanjaro
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangala wakati alipowasili kama mgeni rasmi katika mahafali ya 55 ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mwika leo Mkoani Kilimanjaro.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mwika kama mgeni rasmi katika mahafali ya 55 ya Chuo hicho leo Mkoani Kilimanjaro.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na viongozi mbalimbali wa serikali, watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mwika na wageni waalikwa wakati alipowasili kama mgeni rasmi katika mahafali ya 55 ya Chuo hicho leo Mkoani Kilimanjaro.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Dkt. Anna Mghwira alipomtembelea leo Ofisini kwake Mkoani Kilimanjaro.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa kumi kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Chuo cha usimamizi wa wanyamapori mwika katika mahafali ya 55 ya chuo hicho yaliyofanyika leo chuoni hapo Mkoani Kilimanjaro.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images