Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Wasimamizi wa Uchaguzi wa vituo vya kupiga kura waaswa kuwa waadilifu

$
0
0
Msimamizi wa  Uchaguzi Wilaya ya Tandahimba Ahmada Suleiman amewaomba wasimamizi katika vituo vya kupiga kura kuwa waadilifu sambamba na kuwahi katika maeneo yao ya vituo siku ya uchaguzi jpili

Akizungumza kwenye semina  na wasimamizi wa vituo wa Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji mwaka 2019, alisema kuwa wafanye kazi hiyo katika weledi na uaminifu ili zoezi liishe katika amani na utulivu

" Sisi ni miongoni mwa Wilaya ambazo tunafanya uchaguzi hivyo ninyi wasimamizi hakikisheni  wananchi wanatimiza haki yao bila vikwazo vyovyote visivyo vya lazima," alisema Ahmada

Naye mwezeshaji George Kashura aliwaeleza kuwa wanatakiwa kufuata taratibu za kufungua kituo na kufunga "Mkifika kwenye vituo vyenu hakikisheni mnaweka  vifaa vyenu sawa ili muweze kwenda na muda unatakiwa," alisema Kashura.

Uchaguzi katika Wilaya ya Tandahimba unatarajiwa kufanyika jpili katika Kata ya Tandahimba na Kata ya Nanhnyanga.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tandahimba akizungumza na wasimamizi wa vituo vya kumpigia kura.

 Baadhi ya wasimamizi wa vituo vya kumpigia kura
 Mmoja Kati ya wasimamizi wa kituo akionyesha jinsi ya kufunga sanduku la kura
 Mwezeshaji George Kashura akiwapa maelekezo wasimamizi wa vituo


Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Awataka Watumishi Rukwa kupambana na Udumavu

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Rukwa (hawapo pichani)
Wakuu wa taasisi mbalimbali zinazohudumu katika mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani)
Wakuu wa Idara na vitengo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakimsikiliza kwa makini Wazriri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa pongezi zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (aliyepo kushoto kwake) muda mfupi kabla ya kumkaribisha kuwasalimu watumishi wa mkoa wa Rukwa.

…………………

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mizengo Pinda amewasisitiza watumishi mkoani Rukwa kuhakikisha kila mmoja katika nafasi yake anafanya kazi kwa uadilifu na kueleza kuwa utendaji kazi wa aina hiyo ndio njia pekee ya kupeleka maendeleo ya mkoa mbele na hatimae kuutoa mkoa katika umasikini.

Amesema kuwa amesikitishwa na taarifa iliyolewa hivi karibuni kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2018 ambapo mkoa wa rukwa umeonekana kushika mkia kwa kuwa na asilimia 45 ya umasikini nchini kwa mahitaji ya msingi huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na asilimia 8 ya kiwango hicho huku mkoa wa Katavi uliozaliwa kutoka mkoa wa rukwa ukiwa na asilimia 29

Pia ameshtushwa kuwa mkoa wa Rukwa ambao ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini kuwa na kiwango kikubwa cha udumavu pamoja na kuongoza kuwa na kiwango kikubwa cha umasikini wa chakula kwa asilimia 19 wakati Katavi ukiwa na asilimia 9.

“Tukikaa sisi kama wataalamu, najua baadhi ya wilaya wameshapata maafisa lishe, tutawatengenezea mfumo tuwaonganishe na majukumu ya zahanati na vituo vya afya na hospitali zetu za wilaya, mama anapokuwa ametunga mimba lazima aambiwe aende kliniki, lakini kliniki si kupima tu uzito nakadhalika, hapana, kubwa ni kuona kwamba huyu mama mzazi anapata lishe stahiki?” Alihoji.

Amesema kuwa fikra zilizopo katika makabila yaliyopo mkoa wa Rukwa na Katavi wanaamini kuwa kula mboga za majani ni umasikini wa kutupwa kwahiyo kama mkoa una kazi kubwa ya kubadili fikra za watu hao na kuonyesha umuhimu wa kula mboga za majani.

Ameyasema hayo katika salamu zake kwa watumishi wa mkoa wa Rukwa hivi karibuni ambapo kikao hicho kiliwajumuisha wakuu wa taasisi, idara, wakala za serikali pamoja na watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mh. Joachim Wangabo.

Wakati akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Joachim Wangabo alimpongeza Mh. Pinda kwa kuhakikisha anasogeza huduma muhimu kwa wananchi kwa kuugawa mkoa wa Rukwa na kuzaliwa Mkoa wa Katavi ambapo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Katavi wanafaidika na maendeleo yanayopatikana kutokana na uwepo wa huduma muhimu za kijamii katika halmashauri tano za mkoa huo.

“ Wilaya ya Mpanda ilikuwa inapakana na Kaliua, Uvinza na inapakana na Sikonge Mkoa wa Tabora, Sasa fikiria huyo RC aliyekuwa anatoka Sumbawanga kwenda mpaka huko, huenda ukakaa miaka mitano usifike maeneo mingine, ilikuwa ni shida kweli na miundombinu yake ilikuwa ni matatizo makubwa sana kwahiyo kuugawa huu mkoa wa Rukwa kuwa mikoa miwili umetoa unafuu mkubwa sana wa kimaendeleo” Alisema.

Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 kwa kumega sehemu ya Mikoa ya Tabora na Mbeya. Mkoa una eneo la kilomita za mraba 27,765, kati ya hizo Kilomita za mraba 22,844 (82.3%) ni za nchi kavu na Kilomita za mraba 4,921 (17.7%) ni za maji. Mkoa una jumla ya Wilaya tatu (3), zenye Halmashauri nne (4), Tarafa 16, Kata 97, Vijiji 339, Vitongoji 1,825, Mitaa 167 na Kaya 199,766. Mwaka 2010 mkoa uligawanywa na kuzaliwa mkoa wa Katavi.

Taasisi za Nunuzi Wasisitizwa Kuandaa Mpango wa Ununuzi Ili Mahitaji Yapatikane kwa Wakati

$
0
0

Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa seina hiyo eneo la Mtumba katika Mji wa Serikali leo jijini Dodoma mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe hao juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake za mwaka 2013 ili wawe na usimamizi sahihi wa mikataba yenye kuleta tija na thamani bora ya fedha za Serikali.(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)

……………………

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Wataalamu wa Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) wamesitiza Taasisi za Nunuzi kuandaa vizuri mpango wa ununuzi na kusimamia utekelezaji wake ili mahitaji husika yaweze kununuliwa na kupatikana kwa wakati. 

Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo eneo la Mtumba katika Mji wa Serikali jijini Dodoma, Mwezeshaji wa mafunzo ambaye pia ni Afisa Ununuzi wa Umma kutoka (PPRA) Frank Yesaya amesema nia ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe hao juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake ili wawe na usimamizi sahihi wa mikataba yenye kuleta tija na thamani bora ya fedha za Serikali.

Frank ameongeza kuwa ni muhimu uwepo ushirikiano kati ya vyombo vinavyohusika na kufanya maamuzi na kutekeleza shughuli mbalimbali katika mchakato wa ununuzi wa umma.

Vyombo hivyo ni pamoja na mamlaka ya kuidhinisha bajeti, bodi ya zabuni, kitengo cha ununuzi, idara tumizi, Kamati ya tathmini ya zabuni, timu ya majadiliano pamoja na kamati ya ukaguzi.

“Ni muhimu kushirikiana, kila mmoja atimize wajibu na majukumu yake bila kuingiliana hatua inayopelekea mchakato wa ununuzi kuwa wa tijakatika ofisi husika.” alisema Frank.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ununuzi na Ugavi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Cecilia Kasonga amesema mafunzo yanasaidia kuwaimarisha katika kutekeleza majukumu yao ambapo ni vema mafunzo yatolewe mara kwa mara ili kurahisisha kazi na kuwapa fursa wajumbe wa bodi kujua taratibu za ununuzi wa umma hatua itakayosaidia kutoa maamuzi sahihi

KUNDI LA PILI KOZI YA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA MAGEREZA WAHITIMU MAFUNZO YA UONGOZI CHUO KPF – MKOANI MOROGORO

$
0
0
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama (kushoto) akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(kundi la pili) ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo.
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakila kiapo cha utii kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akikagua Gadi ya heshima iliyoandaliwa na kundi la pili la Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza lililofanyika Novemba 22, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akiwa katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka kundi la pili la Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
Kundi la pili la Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika Sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Novemba 22, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu(kundi la pili) wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
Maofisa Wahitimu(kundi la pili) wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu(kundi la pili) wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza waliosimama mstari wa nyuma. Mafunzo hayo yamefungwa leo Novemba 22, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).

TCDC SACCOS YAJIVUNIA MAFANIKIO

$
0
0
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC SACCOS) kimepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ambapo akiba za chama zimeongezeka kufikia Shilingi 97,933,820.00 kutoka Shilingi 39,827,800.00  mwaka 2017 kilipoanzishwa rasmi, sawa na ongezeko la Shilingi 58,106,020.00.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa chama hicho, Aron Ibrahim amesema Hisa za lazima zimefikia Shilingi 25,765,000.00 na chama kimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi 153,850,000.00.

Aidha, katika kipindi hicho, jumla ya kiasi cha Shilingi 114,118,411.00 kimesharejeshwa chamani na faida ya shilingi 16,779,250.00 imepatikana. Vile vile, jumla ya mikopo iliyopo kwa wanachama ni shilingi 137,283,945.00 hadi Oktoba 2019.

Katika mkutano huo Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCDC SACCOS walipokea Taarifa ya Kamati ya Usimamizi kwa kipindi cha mwezi Januari 2019 hadi Septemba 2019 iliyosomwa na mwenyekiti wa Kamati, Boniphace Moshi ambapo alisema hali halisi ya hisa na mtaji wa chama kwa pamoja umefikia  Shilingi 119,466,070.00.

Vilevile Wajumbe wa mkutano mkuu wa TCDC SACCOS walipokea Taarifa Huru ya Mkaguzi wa nje ya mwaka wa fedha ulioishia 2018 kwa Wanachama kuhusu Taarifa ya Wakaguzi na Taarifa ya za TCDC SACCOS kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 31 Desemba, 2018. Taarifa hiyo ya ukaguzi uliofanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) ilionyesha kuwa chama kwa mwaka 2018 kimepata Hati yenye Mashaka.

Mkaguzi Dorah Meta  kutoka COASCO amesema baadhi ya mapungufu yaliyobainika mwaka uliotangulia yamefanyiwa kazi na amewapongeza viongozi wa TCDC kwa kuhakikisha kuwa dosari zilizobainika wakati wa ukaguzi uliotangulia zimeondolewa.

Katika mkutano huo, viongozi wapya wa TCDC SACCOS walichaguliwa baada ya waliokuwepo kumaliza kipindi chao cha miaka mitatu (3). Waliochaguliwa ni Aron Ibrahim aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti,  wajumbe wapya wa Bodi waliochaguliwa ni Boniphace Moshi, Ndinagwe Mwambola, Petronila Shirima, Ally Ndenya, Biyaga Nzohumba na Baraka Lukio; na Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi ni Jackson Mushumba, Josephat Simkoko na Consolata Kiluma.
Mwenyekiti wa TCDC SACCOS, Aron Ibrahim akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma
 Makamu Mwenyekiti wa TCDC SACCOS, Boniphace Moshi akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu  wa TCDC SACCOS wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma
 Viongozi wapya wa TCDC SACCOS waliochaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa TCDC SACCOS uliofanyika leo tarehe 22/11/2019 Jijini Dodoma

SIMBACHAWENE, KALEMANI KUPAMBA MAONESHO YA KITAIFA YA NISHATI JADIDIFU

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa TAREA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo, Mhandisi Prosper Magali.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, watapamba maonesho ya Siku ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu Tanzania yanayoanza Ijumaa Novemba 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi umebaini kuwa, maonesho hayo yanaandaliwa na Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) kwa ufadhili wa taasisi za Kingdom of The Netherland, Energy Plus, Brac, Chloride Solar, Solar Sister na Ewura. TAREA ni jumuiya yenye wanachama zaidi ya 796.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa TAREA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo, Mhandisi Prosper Magali alisema maonesho hayo yatafanyika Ijumaa Novemba 29 na Jumamosi Novemba 30, mwaka huu katika Viwanja ya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.

“Maonesho yatafunguliwa Ijumaa na Waziri mwenye dhamana ya Mazingira, George Simbachawene na kufungwa Jumamosi na Waziri wa Nishati, Dk Kalemani atakayemwakilisha Waziri Mkuu,” alisema Magali na kuongeza: “Wadau na watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kushuhudia teknolojia ya renewable energy (nishati jadidifu) kwa kuwa licha ya mambo mengi mazuri yatakayofanyika na kuoneshwa, hakuna kiingilio.”

Aidha, Mhandisi Magali alisema lengo la Maonesho hayo yenye kaulimbi isemayo: “NISHATI JADIDIFU KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA,” ni kuionesha jamii namna Nishati Jadidifu inavyoweza kuchangia maendeleo ya Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo Mwaka 2025.

“Maonesho yatahusisha Teknolojia ya Nishati Jadidifu, Kutembelea Maeneo Yanayotumia Nishati Jadidifu kuona teknolojia hii inavyofanya kazi, pamoja na warsha na majadiliano ya kitaalamu,” alisema.

KUHUSU PICHA, TAARIFA NA MAELEZO ZAIDI, bonyeza hapa; https://sites.google.com/site/tareatzevents/red2019

Rotana yazindua hoteli ya hadhi ya nyota tano Johari Rotana jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Mwonekano wa Jengo la katika jengo la MNF  ambamo kuna hoteli ya Johari Rotana

 Baadhi ya picha za vitu na samani zinazopatikana katika hoteli ya yota tano Johari Rotana inapatikana katika jengo la MNF katikati ya jiji la Dar es Salaam ikiwa na vyumba vikubwa 253, vyumba vya kifahari na makazi.
Baadhi ya Misosi inayopatikana katika Hoteli Mpya ya Johari Rotana.

KATIKA jitihada za kuongeza uwepo wake katika sekta ya utalii inayokuwa kwa kasi barani Afrika, Rotana ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza katika uendeshaji wa hoteli barani Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya na Uturuki, imetangaza leo ufunguzi rasmi wa hoteli ya hadhi ya nyota tano ya Johari Rotana ndani ya jiji la Dar es Salaam. Hoteli hiyo ndiyo imefungua mlango kwa kampuni hiyo katika soko la Afrika Mashariki.

Hoteli hiyo yenye mandhari ya kuvutia inapatikana kwa urahisi kabisa ndani ya jengo la MNF lililopo katikati ya jiji. Pamoja na kuwa na vyumba vya kukodi vipatavyo 60 vyenye samani ndani yake, Johari Rotana ina vyumba 253 vyenye ukubwa wa kutosha ikiwemo vyumba 193 vya kifahari. Kupitia vyumba vya hoteli hiyo vilivyopo kuanzia ghorofa ya 13 kwenda juu, mkaaji anaweza kuona na kufurahia mandhari ya kuvutia ya bandari na jiji la Dar es Salaam.

Akizungumzia ufunguzi huo, Guy Hutchinson, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Rotana alisema: "Kama sehemu ya mkakati wetu wa muda mrefu, Afrika inaendelea kuwa soko muhimu sana
kwa Rotana. Kupitia ufunguzi wa hoteli hii ya Johari Rotana, kampuni yetu imetimiza hatua muhimu katika safari yetu. 

"Tumeweka viwango vipya katika usanifu majengo, muundo, teknolojia, na ubora wa huduma. Tunategemea hoteli hii ya Johari Rotana ambayo ni ya kwanza kwetu katika kanda ya Afrika Mashariki italeta ladha ya kipekee katika sekta. Tuna uhakika kwamba kuwepo kwa huduma mbali mbali za kukidhi mahitaji ya wateja ikiwemo vyumba vyenye ukubwa wa kutosha, vyakula na vinywaji vya aina mbalimbali, huduma za kisasa za mikutano ikiwa ni pamoja na kuwa na ukumbi mkubwa zaidi nchini wa kufanyia mikutano na sherehe – tumejiweka katika nafasi nzuri sana ya ushindani katika soko".

Hata hivyo Mwenyekiti wa kampuni miliki CRJE Ltd (Afrika Mashariki) Hu Bo, alisema: "Tuna miaka 50 ya utendaji bora nchini Tanzania, na tunafurahi sana kufungua hoteli hii ya kisasa zaidi ya Johari Rotana. Tunajivunia kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha miundombinu katika sekta hii na kutangaza vivutio maarufu vya watalii vya nchini ikiwemo jiji la biashara la Dar es salaam.

"Johari Rotana ni hoteli ya tisa ya kiwango cha nyota 5 ambayo tumejenga nchini Tanzania. Kwa uzoefu wetu mkubwa katika biashara ya ujenzi wa hoteli na katika soko hili linalobadilika, tunaelewa vizuri mahitaji ya wateja, na kwa hakika Johari Rotana itakidhi mahitaji haya".

"Ningependa kuwashukuru washirika wetu kutoka bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), kitengo cha uwekezaji cha Benki ya Dunia, kama mashirika makuu katika mradi huu, pamoja na kampuni ya Rotana, ambayo tumeshirikiana nayo kusimamia jengo hili. Tuna uhakika kuwa hoteli yetu mpya itakidhi mahitaji ya soko yanayokua na itatoa huduma ya kipekee kwa wageni na wakazi wa jijini Dar es salaam".

Johari Rotana ina migahawa minne maridadi itakayo toa huduma ya vyakula vya aina tofauti ikiwemo Kibo Lobby Lounge, mgahawa wa siku nzima wa Zafarani, mgahawa wenye vyakula asili vya Kichina Noble House na mgahawa uliochangamka na wenye burudani wa Hamilton Gastropub.

Vivutio vingine vya hoteli hii ni pamoja na ukumbi mkubwa wa mikutano nchini Tanzania, bwalo la hoteli kubwa zaidi Tanzania lenye ukubwa wa mita za miraba 900 na paa lenye urefu wa mita 6.5 ambalo pia linaweza kugawanywa katika kumbi ndogo tatu. Hoteli hii pia ina kumbi zingine
sita za mikutano, kituo cha huduma za biashara, ofisi zenye hadhi ya juu, na eneo la maegesho ya magari kwa ndani, na hivyo kuifanya hoteli hii kuwa ni sehemu hakika kwa wageni wa kibiashara na mapumziko.

Wageni wanaokaa Johari Rotana pia watapata fursa ya kuchagua huduma mbali mbali za mazoezi na tiba za mwili, pamoja na bwawa la kuogelea la nje, vifaa vya mazoezi ikiwemo ulingo wa ndondi, na huduma nyingine mbalimbali za kiustawi wa mwili.

WAZIRI HASUNGA APIGILIA MSUMARI, SERIKALI HAITOPANGA BEI ELEKEZI YA MAHINDI NA MCHELE

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akichimba mashimo kwa ajili ya kupanda mahindi wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa pamoja na wakulima wakisafisha shamba kwa ajili ya kupanda mahindi wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa shambani wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiondoka shambani akiwa pamoja na wakulima mara baada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Novemba 2019 amezindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 ambapo amewataka wakulima kote nchini kulima mazao ya chakula na biashara kwani serikali inaendelea kuimarisha masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Katika uzinduzi huo wa msimu wa kilimo uliofanyika katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe amewahakikishia wakulima kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeanzisha kitengo cha masoko chini ya wizara ya Kilimo ambacho moja ya kipimo chake kiutendaji ni kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ndani na nje ya nchi.

Alisema serikali imeweka msisitizo katika kuimarisha mazao mbalimbali ya chakula, biashara pamoja na mazao ya mbogamboga na matunda hivyo wakulima hawapaswi kuwa na wasiwasi na masoko ya mazao yao kwani yataendelea kuimarika maradufu.

Mhe Hasunga ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha kuwa inasimamia utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanauza mbolea kwa bei elekezi ili kuwanufaisha wakulima kwani mbolea ni miongoni mwa Pembejeo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wakulima wanalima mazao yenye tija.

Alisema kuwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza mbolea zaidi ya bei elekezi anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni ya kufanya biashara hiyo.

Kuhusu Mbegu za mazao, Mhe Hasunga ameitaka Taasisi ya Udhibiti wa mbegu nchini (TOSCI) kuhakikisha kuwa mbegu zinazopelekwa kwa wakulima nchini zinakuwa katika ubora unaostahili huku akiagiza wauzaji wa mbegu feki kuchukuliwa hatua.

“Vilevile naagiza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuhakikisha kuwa wanazalisha mbegu za kutosha na kuzifikisha kwa wakulima kwa wakati ili katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 kuwa na uzalishaji mkubwa na tija kwa wakulima” Alisema.Kwa upande wa Viuatilifu, Waziri Hasunga ameiagiza Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu ukanda wa Kitropiki (TPRI) kuhakikisha wanafanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini na kuondoa viuatilifu feki vyote sokoni.

Ameongeza kuwa TFRA inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kote nchini kuhusu matumizi sahihi ya Viuatilifu ili kuondoa dhana ya wakulima kuwa na malalamiko mengi kuhusu viuatilifu.

Aidha, Mhe Hasunga amesisitiza kuwa serikali inayoongozwa na Dkt Magufuli haitawapangia bei ya mazao yao wakulima hususani mazao makuu ya chakula na biashara kwani wakulima wanapokuwa wanalima mazao yao hakuna watu wanaowasaidia hivyo wakati wa kuuza pia wanapaswa kuamua bei kulingana na soko.

Mhe Hasunga pia amewataka wakulima kujihusisha zaidi na kilimo kinachozingatia hifadhi ya udongo (Climate Smart Agriculture) kwa kuchimba mashimo na kupanda mbegu kuliko kilimo kinachoharibu udongo kilichozoeleka.

YANGA SC YAENDELEZA UBABE,YAIKUNA JKT 3-2

$
0
0
YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia jioni ya leo kuichapa JKT Tanzania 3-2 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa sita na kujiinua kutoka nafasi ya 15 hadi ya 12 sasa ikilingana kila kitu na Azam FC iliyopo nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi saba.

Yanga ilifanikiwa kupata goli  lake la kwanza dakika ya 11kupitia kwa Patrick Sibomana akimalizia krosi ya Deus Kaseke kufuatia shambulizi lilioanzishwa na beki Ally Abdulkarim Mtoni ‘Sonso’. 

Dakika mbili baadae Adam Adam akaisawazishia JKT Tanzania akimalizia pasi ya Mwinyi Kazimoto na matokeo kuwa 1-2.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda misimu miwili mfululizo iliyopita, Juma Balinya akaifungia Yanga goli  la pili dakika ya 22 akimalizia pasi ya beki wa kulia Juma Abdul.

Mshambuliaji mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga akaifungia Yanga goli  la tatu dakika ya 35 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Damas Makwaya kumchezea rafu Kaseke nje kidogo ya boksi.

Mshambuliaji Daniel Lyanga akategua mtego wa kuotea wa mabeki wa Yanga kuifungia JKT Tanzania nao la pili dakika ya 45 na ushei akimalizia pasi ya beki Adeyum Saleh Ahmed.

Kipindi cha pili Yanga walicheza kwa kujizuia kuruhusu goli lingine huku wakishambulia kwa tahadhari na wakafanikiwa kuvuna ushindi wa pili mfululizo chini ya kocha mpya na wa muda, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mkongo, Mwinyi Zahera aliyefukuzwa mwanzoni mwa mwezi.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Farouk Shikaro, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Papy Kabamba Tshishimbi, David Kaseke, Mapinduzi Balama/Mohamed Issa ‘Banka’ dk50, David Molinga/Abdulaziz Makame dk61, Juma Balinya na Patrick Sibomana/Mrisho Ngassa dk77.

JKT Tanzania;  Abdulrahman Mohamed, Michael Aidan, Adeyoum Ahmed, Frank Nchimbi, Damas Makwaya, Jabr Aziz, Mwinyi Kazimoto, Rchard Maranya/Hafidh Mussa dk64, Daniel Lyanga, Adam Adam/Anuary Kilemile dk83 na Edward Songo/Mohamed Rashid dk72.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Alliance imeifunga KMC 2-1 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza,m mabao yake yakifungwa na Geofrey Luseke dakika ya 15 na David Richard dakika ya 30. Luseke tena akajifunga dakika ya 77 kuwapatia bao la kufutia machozi KMC.

Namungo FC wakapoteza mechi ya kwanza nyumbani msimu huu wakichapwa 3-1 na Coasta Union Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Coastal yalifungwa na Mtenje Albano dakika ya 15, Deogratius Anthony dakika ya 76 na Paul Bukaba aliyejifunga dakika ya 90 na ushei huku la Namungo likifungwa na Reliants Lusajo dakika ya 16.

Kagera Sugar ikaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, magoli yake yakifungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 10 na Nassoro Kapama dakika ya 64, huku Paul Nonga akiwafungia wageni kutoka Iringa dakika ya 85.
Ndanda FC ikapokea kipigo cha 2-0 kutoka kwa Polisi Tanzania ambayo magoli  yamefungwa na Andrew Chamungu dakika ya 11 na Idd Mobby dakika ya 83.

Na goli la  dakika ya 83 la Samson Mbangula likainusuru Tanzania Prisons kupoteza mechi nyumbani ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC iliyotangulia kwa goli la Raphael Aroba dakika ya 70 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC
 JKT Tanzania

RAIS DKT MAGUFULI AKABIDHI JENGO LA WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI KWA JESHI LA POLISI, KUWA MAKAO MAKUU YAKE

$
0
0
Jengo ambalo Rais Dkt John Pombe Magufuli amelikabidhi Jeshi la
Polisi kufanya Makao Mkuu yake jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22,2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95,hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola alipowasili Tayari kukabidhi kwa Jeshi la Polisi jengo kwa jail ya Makao make yake jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22, 2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95, hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi fungi za jengo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro wakati akikabidhi jengo hilo kuwa Makao makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22, 2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95, hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikilkiza Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro alipokuwa akishukuru kwa kukabidhiwa jengo hilo litakalokuwa Makao makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22, 2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95, hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akishukuru kwa kuwakabidhi jengo la Makao makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22, 2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95, hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kukabidhi jengo kwa adili ya Makao makao Makuu ya Jeshi la polisi jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22, 2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95, hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa wakandarasi wa jengo ambalo amelikabidhi kuwa Makao makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22,2019. Awali jengo ambalo Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95, hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro pamoja na viongozi waandamizi wa Kesho la polisi baada ya kukabidhi jengo hilo ambalo litakuwa Makao makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22,2019. Awali jengo hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamanda wa Polisi wa Dodoma Giles Muroto baada ya kukabidhi jengo la Makao makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma Leo Ijumaa November 22, 2019. Awali jengo hilo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Maji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi picha za jengo ambalo amelitoa kuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro wakati wa sherehe fui ya uwekaji jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Polisi eneo la Nzuguni leo Ijumaa Novemba 22, 2019

PICHA NA IKULU

Agizo la Rais Magufuli Latekelezwa kwa Asilimia 100 Sumbawanga

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (katikati waliokaa) Katika Picha ya pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga pamoja na viongozi wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa pongezi zake kwa Madiwani na Watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika baraza la madiwani lililofanyika katika mji wa Laela.
Madiwani wa kwanza kushiriki katika baraza la madiwani la kwanza kufanyika katika mji wa Laela ambapo ndio makao makuu mapya ya halmashauri ya Wilaya hiyo.

…………….

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewapongeza madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kuweza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa tarehe 6, Oktoba 2019 alipokuwa katika ziara yake ya siku 3 ambapo aliiagiza halmashauri hiyo kuhamia Laela pamoja na halmashauri nyingine nchini kuhamia katika maeneo yao ya kiutawala.

Amesema kuwa ni watumishi 16 tu kati ya watumishi 165 wa makao makuu ya halmashauri wanaotumia mifumo ya watumishi (LAWSON), mfumo wa mapato LGRCIS), Mfumo wa malipo wa EPICOR, TASAF na Kitengo cha Uchaguzi ndio waliobaki mjini wakisubiri miundombinu hiyo kukamilika katika makao mapya ya halmashauri hiyo katika Mamlaka ya mji mdogo wa Laela.

“Nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kushirikiana na Wadau wengine (Mfano TTCL) ahakikishe anaunganisha Makao Makuu Mapya ya Halmashauri Laela kwenye Mkongo wa Taifa. Hii itawezesha Mifumo mingine inayotumia Mtandao wa mawasiliano kuweza kufanya kazi kutokea hapa hapa Laela. Ninamuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha Watumishi ambao bado hawajahamia Laela wawe wamehamia ifikapo tarehe 1 Januari, 2020.” Alisema.

Aidha, ameitaka menejimenti ya halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wadau kufanya tathmini juu ya kuwafikia wananchi waliopo mbali na Laela kama vile kutoka katika vijiji vya mfinga, Mwadui, Kalumbaleza wanaokwenda kupata huduma Laela ambao wanatoka umbali wa zaidi ya kilometa 150.

Ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani la kwanza kufanyika katika makao makuu hayo mapya ya halmashauri hiyo tarehe 21.11.2019, kikao kilichohudhuriwa na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri.

Awali akitoa taarifa ya maandalizi ya kuhamia katika makao hayo mapya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule alisema kuwa kitengo cha uchaguzi kimebaki mjini kutokana na kukosekana kwa eneo kubwa la kuhifadhia vifaa vya uchaguzi lakini mara tu uchaguzi utakapopita kitengo hicho kitahamia katika mji wa Laela.

“Kwahiyo Wakimaliza uchaguzi wakiandaa ile taarifa tutahakikisha nao wanahamia haa Laela, Watu wa Fedha na watu wa Utumishi wanawasiliana na watu wa TTCL ili mokongo ule wa taifa uweze kupatikana hapa Laela na zile huduma zao ziweze kuhamia hapa Laela, kwa ujumla shughuli zinaenda vizuri na wananchi wanaendelea kuhudumiwa vizuri hapa Laela,” Alisema.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Apolinari Macheta alisema kuwa watumishi wa halmashauri hiyo walikuwa wakishiriki usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika eneo ambalo halikuwa la kwao na pia walikuwa wakichangia maendeleo katika maeneo ambao sio ya kwao.

“Tulichelewa sana na ni maamuzi ambayo yangefanyika hata huko nyuma tungeweza kuwa parefu zaidi lakini tunakushukuru sana kwa namna mji wetu wa Laela ulivyo hautofautiani na mji wa sumbawanga na hata kama ni changamoto ni za kawaida haziwezi kufanana na za wengine kwakweli tunaonekana tuko mjini.” Alisema.

Wakati akitoa neno la Shukurani mbunge wa jimbo la Kwela Mh. Ignus Malocha alisema kuwa yeye ndio wa kwanza kutangulia kwani ofisi yake ilikuwa ya kwanza kabla ya Mkurugenzi kuhamia katika mji huo baada ya wiki mbili tu tangu Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa agizo hilo, hivyo alimshukuru mkuu wa mkoa kwa kusimamia zoezi hilo la utekelezaji wa agizo la Rais.

KAMPUNI YA BUSINET AFRICA YADHAMIRIA KUENDELEZA ZAO LA ALIZETI MKOANI SINGIDA

$
0
0


Meneja wa Mradi wa Kampuni ya BusinetAfrika Irene Njovu, akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida jana, katika kikao cha wadau wa zao la alizeti kilichofanywa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Kikao kikiendelea .
Meneja wa Mradi wa Kampuni ya BusinetAfrika Irene Njovu, Irene Njovu, akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.


Na Waandishi Wetu, Singida

KAMPUNI ya BusinetAfrica imedhamiria kuwasaidia Wakulima Mkoani Singida namna ya Kutengeneza maandiko ili waweze kupata mikopo kwenye Mabenki itakayowasaidia katika shughuli za kilimo. 

Kampuni hiyo imewakutanisha pamoja viongozi wa vyama vya ushirika kutoka kila wilaya za mkoa huo, wakulima wa zao la alizeti na wasindikaji wa zao hilo kwa lengo la kuwaunganisha na taasisi za Kifedha ili waweze kufanya kazi kwa pamoja. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kikao hicho Meneja wa Mradi wa Kampuni hiyo, Irene Njovu alisema kampuni hiyo imekuja na mradi wa kuwasaidia wakulima wa zao la alizeti kupata mikopo kwa kuwaunganisha na Benki ya Kilimo na Maendeleo Tanzania (TADB) kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa ili waweze kupata mikopo. 

"Tumekuja na mradi wa kuendeleza zao la Alizeti Mkoa wa Singida na tumeamua kuwaunganisha wakulima na taasisi za kifedha hususani benki yao ili waweze kupata mikopo katika msimu huu wa kilimo". alisema Njovu. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika 'SIFACU' Mkoa wa Singida, Yahaya Hamis alisema kutokana na wakulima wengi pamoja na Viongozi wa vyama vya ushirika kutokujua kuandika maandiko ili kupata mikopo, kwa kupitia mradi huo watakuwa na ufahamu na kuanza kuandika maandiko yatakayosaidia kupata mbegu bora na kuongezeka uzalishaji wa zao hilo. 

Hata hivyo wakulima wameshukuru kwa hatua hiyo lakini hofu yao wameona mradi huo umechelewa, hivyo wameomba taasisi za kifedha hususani Benki ya Kilimo na Maendeleo Tanzania (TADB) ambayo ndio wameunganishwa nayo kutoa mikopo mapema ili waweze kupata mbegu bora kwa wakati kabla msimu haujaisha, huku wasindikaji wakiwa na matumaini ya kupata malighafi ya kutosha baada ya mradi huo kuwafikia.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 23.2019

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Ndg. Mathias Kabunduguru alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Ndg. Mathias Kabunduguru alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Ndg. Mathias Kabunduguru alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Ndg. Mathias Kabunduguru alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Ndg. Mathias Kabunduguru alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

ANTONIO CONTE AWAFUNDISHA WACHEZAJI WAKE KUJAMIANA

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Inter Milan ya Italia ina lengo lakumaliza Ligi (Serie A) ikiwa katika nafasi ya kwanza, katika kuhakikisha timu hiyo inashika usukani hadi mwisho wa msimu huu, Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Antonio Conte amewapa somo Wachezaji wake namna yakufanya mapenzi katika kipindi cha Ligi ili kuwa na kiwango bora wawapo uwanjani. 

Kupitia Jarida la L'Equipe Kocha huyo amenukuliwa akisema “Katika msimu, mahusiano hayatakiwi kufanywa kwa muda mrefu, lazima ufanye mapenzi kidogo ikiwezekana pale ukiwa na mpenzi wako”

Conte anataka kushika usukani wa Serie A akiwa na Inter Milan wenye alama 31 mpaka sasa akiwa na michezo 12 akiachwa alama moja na Juventus wenye alama 32 katika msimamo wa Ligi hiyo.

Somo lakujamiana kwa Wanamichezo wengi duniani, Je? ni funzo kwa Wachezaji wa Inter Milan – mnamo 2010 katika Michuano ya Kombe la Dunia, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Fabio Capello aliwaambia Nyota wake kutofanya mapenzi na Wake zao, Rafiki zao wa Kike ili kuwa nguvu na kulinda viwango vyao uwanjani. Lakini Uingereza ilitupwa nje ya Michuano hiyo mapema baada ya hatua ya Makundi ya Michuano hiyo mikubwa Ulimwenguni.

Kwa Aliyekuwa Bondia wa Uzito wa Juu, Mike Tyson mnamo mwaka 2017 alieleza alijizuia kujamiana kipindi cha miaka mitano ili kuwa na Kiwango Bora licha yakueleza alikuwa hafahamu chochote kuhusu suala hilo.

Aliyekuwa Bondia mahiri katika historia ya Ngumi, Muhammad Ali, imeelezwa kuwa aliwahi kusema kipindi anajiandaa kupambana Pigano kubwa huwa anajizuia kujamiana kwa wiki sita.
Kocha Mkuu wa Inter Milan, Antonio Conte

RAS TANGA ATAKA WANANCHI KUNUFAIKA NA UWEPO WA MISITU

$
0
0

Na Mwandishi Wetu,Tanga 

KATIBU Tawala (RAS) wa mkoa wa Tanga, Zena Saidi amesema ili kupunguza upotevu na  uharibifu wa  rasilimali misitu ni lazima jamii inayozungukwa na misitu iweze kunufaika kiuchumi, kijamii na maendeleo.

Said aliyasema hayo jijini hapa wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari  kuhusu Program ya Kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC).

Alisema mafunzo hayo ya mradi wa FORVAC kwa waandishi wa habari ni muhimu katika kuhakikisha jamii inapata ufahamu kuhusu faida ya rasilimali misitu.

Katibu misitu inaweza kuwa endelevu iwapo dhana nzima ya Usimamizi Shirikishi wa   Misitu (USM) inaonekana katika matokeo chanya.

Alisema misitu inaweza kutumiwa bila kuharibika kwa kuhamasisha kilimo rafiki na misitu kama kilimo cha iliki, pilipili mannga, kufuga nyuki na shughuli nyingine rafiki.

"Misitu ikitunzwa kwa mfumo shirikishi itaweza kuwa na matokeo chanya. Ila hilo litawezekana iwapo waandishi wa habari watashirikiana na kada zote kuelimisha," alisema.

Katibu tawala huyo alisema elimu ya USM inapaswa kusambazwa nchi nzima na waandishi wa habari ndio chanzo muhimu.Said alisema mkoa wa Tanga utunzaji wa mazingira upo vizuri hali ambayo inasadie upatikanaji wa maji kuwa wa uhakika.

Alisema wapo baadhi ya watu walitaka kuharibu msitu wa Amani Muheza lakini kwa sasa wamewadhibiti huku wakihamasisha upandaji wa miti ili misitu iwe endelelevu.Katibu tawala aliwataka watekelezaji wa miradi kutumia lugha rahisi wanapoelezea miradi hiyo ili kurahisisha ujumbe unaofikia waandishi.

Alisema takwimu zinaonesha kwa mwaka Tanzania inapoteza hekta zaidi ya 469,000 huvyo ni vema zikawepo jitihada za utunzaji wa misitu.Mratibu wa Program wa FORVAC, Emmanuel Msofe alisema wamelazimika kutoa mafunzo kwa vyombo vya habari ili waweze kuulewa mradi na kuelimisha jamii.

Msofe alisema program hiyo inatelelezwa katika wilaya 10 za Handeni, Kilindi, Mpwapwa, Liwale, Ruangwa, Nachingwea, Mbinga, Namtumbo, Songea na Nyasa.

"Nikiwaona nyie wanahabari nawaona Watanzania milioni 53 kwani madhumuni ya program ni kuona jamii inanufaika na kupata taarifa," alisema.Alisema program hiyo inagusa uchumi, jamii na maendeleo kupitia rasilimali misitu bila kusababisha uharibifu.

"Tunaongeza thamani ya mazao ya misitu, kujengea uwezo wadau kwa maana teknolojia na ujuzi, ugani, taarifa, sheria, Sera na miongozo mbalimbali," alisema.

Kwa upande wake Mratibu wa Program Kanda ya Tanga, Petro Masolwe alisema mradi huo ulionza mwaka 2018 umeweza kuongeza mnyororo wa thamani katika maeneo yenye mradi.

Masolwa alisema baadhi ya nchi duniani ikiwe Finland zimeendelea kupitia misitu hivyo Tanzania inapaswa kutumia rasilimali hiyo kuchochea maendeleo.

"Pamoja na kupigania program hiyo waandishi wanapaswa kuandika kuhusu kampeni ya upandaji miti nchini kote. Tutaweza kupunguza uharibifu NA uootevu wa misitu," alisema.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Zena Said akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimisha wananchi faida za utunzaji wa misitu.

 Katibu Tawala (RAS) wa mkoa wa Tanga, Zena Said akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu Program ya Kuendeleza Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Misitu (FORVAC) yaliyofanyika mkoani hapo jana.Kulia ni Mratibu wa Program ya FORVAC, Emmanuel Msofe

TAARIFA KWA UMMA: HIFADHI TATU MPYA ZATANGAZWA RASMI, UTEUZI WA BODI YA TAFORI

ELIMU YA KODI YATAKIWA KUTOLEWA ZAIDI KWA WANANCHI

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHANGAMOTO ya kutoa na kudai/kutoa risiti mara baada ya kununua au kuuza bidhaa imeelezwa kuendelea katika baadhi ya maeneo huku ikishauriwa elimu zaidi kuhusiana na umuhimu wa elimu ya Kodi kuendelea kutolewa  kwa wananchi kote nchini ili kuwawezesha kutambua umuhimu wa kulipa Kodi hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 12 ya Chuo Cha Kodi (ITA) Naibu Gavana wa Benki kuu Julian Raphael  Banzi amesema bado Kuna uhitaji wa kutoa elimu ya kodi kwa kwa wananchi na chuo hicho kina wajibu na kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini ( TRA) katika kuhakikisha  wanawashawishi na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa kulipa Kodi.

Aidha amesema kuwa Serikali inatekeleza mpango wa miaka mitano 2016/2017 na 2020/2021 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu na utekelezaji huo unaenda sambamba  na uthabiti na makusanyo ya kodi.

"Tunatambua kuwa Chuo Cha Kodi kina fursa ya kipekee nchini na hasa kwa kutoa mafunzo ya forodha na Kodi yenye uhalisia wa kiutendaji hivyo basi, Chuo hiki kina wajibu wa kuhakikisha kwamba kinatoa wataalamu walio mahiri katika masuala ya forodha na Kodi ili kuisaidia Serikali kutekeleza vipaumbele vya bajeti na hatimaye kufanikisha dhima ya kujenga uchumi wa viwanda" ameeleza.

Pia amewashauri wataalamu wa Chuo hicho kuendelea kujiimarisha zaidi katika utafiti wa masuala mbalimbali ya Kodi hasa katika sekta maalumu na zinazoibuka ikiwemo gesi, mafuta, kilimo na madini ili kuweza kuongeza makusanyo yatakayosaidia pia kuimarisha miundombinu ya Chuo hicho.

Kwa upande wake Kamishina wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Dkt.Edwin Mhede amewashauri wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi kufanya kazi kwa bidii na kuepukana na rushwa Jambo ambalo limekuwa likikwamisha shughuli nyingi za maendeleo na amekipongeza Chuo hicho kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi ili kuwajengea uwezo zaidi kiutendaji.

Mhede amesema kuwa Serikali kupitia TRA wataendelea kushirikiana na chuo hicho ili kiweze kuendelea kuwa kitovu Cha Kodi katika ukanda wa Afrika Mashariki na amewashauri wahitimu hao kutumia maarifa waliyoyapata katika kuleta tija kwa jamii na taifa me ujumla pamoja kuwa mabalozi bora wa kutoa elimu ya kodi popote watakapokwenda.

Mkuu wa Chuo hicho Profesa. Isaya Jairo amesema wanafunzi wapatao 417 wamehitimu  na kutunukiwa shahada mbalimbali katika ngazi  ya cheti, astashahada na shahada mbalimbali na kusema kuwa wameendelea kukarabati miundombinu kwa kutumia Fedha za ndani na ameishukuru Serikali kupitia  TRA kwa kuendelea kuhakikisha kila mipango ya kutoa wamahiri bora  inakamilika.

Amesema kuwa katika miaka 12 ya Chuo hicho wanajivunia zaidi katika utoaji wa mafunzo ya forodha na Kodi wakiwa ni  Chuo pekee nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini licha ya kuwa na changamoto ya rasilimali fedha.

Prof. Jairo amewashauri wahitimu kutumia mafunzo waliyoyapata kuleta tija kwa Jamii na kuwa wazalendo katika kulitumikia  taifa hasa kwa wakati huu ambao nchi imejikita katika kujenga uchumi wa kati na viwanda.
 Kamishina wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Dkt. Edwin Mhede akizungumza katika mahafali ya kumi na mbili ya Chuo Cha Kodi (ITA) ambapo alieleza kuwa Serikali kupitia Mamlaka hiyo itaendelea kufanya kushirikiana na chuo hicho ili kuweza kutoa wataalamu mahiri wenye kuleta matokeo chanya kwa jamii, leo jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Astashahada ya uzamili ya masuala ya Kodi wakivaa kofia baada ya kutunukiwa shahada hiyo na Naibu Gavana wa benki kuu Julian Raphael Banzi ambaye aliwashauri kutumia maarifa waliyoyapata katika kuleta mabadiliko katika jamii na kuwa mabalozi bora, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali waliohudhurishwa katika mahafali ya kumi na mbili ya Chuo hicho.

TCRA YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI ILBORU

$
0
0

 Mkuu wa kanda ya Kaskazini Imelda Salum akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilboru iliyopo Mkoani Arusha leo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza na wageni waalikwa na wanafunzi katika shuke ya Sekondari Ilboru katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa vya Tehama vilivyotolewa na TCRA.
Mkurugenzi mtendaji wa Ausha DC Alvera Ndabagoye akizungumza katika hafla hiyo Wakikadidhiana karatasi za  Makabidhiano ya vifaa kati ya Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Mhandisi Imelda Salum pamoja na Mkuu wa Shule ya Ilboru Dennis Otieno yakiendelea
Uwekaji sa saini katika karatasi za makabidhiano kati ya Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Mhandisi Imelda Salum pamoja na Mkuu wa Shule ya Ilboru Dennis Otieno yakiendelea .
Wakibadilishana karatasi za makabidhiano kati ya Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Mhandisi Imelda Salum pamoja na Mkuu wa Shule ya Ilboru Dennis Otieno yakiendelea ,Wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega na Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha 
 Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo katika ukumbibwa shule hiyo
Mkuu wa Shule ya sekondari ya ILBORU Dennis Otieno akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na TCRA.

Na.Vero Ignatus,Arusha 

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) imekabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Ilboru iliyopo mkoani Arusha ambapo kigezo kikubwa ni ufaulu na kushika nafasi ya juu katika ngazi ya Taifa. 

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Mkuu wa kanda ya Kaskazini Mhandisi  Imelda Salum ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa TCRA Nchini Mhandisi James Kilaba amesema kuwa Mamlaka hiyo ina jukumu la kuhakikisha kuwa mawasiliano yanawafikia wananchi wale waliopo mjini na wale waliopo nje ya mji bila kusahau makundi yenye mahitaji maalumu.

''TCRA imeweka imeweka katika mpango mkakati wake utaratibu wa kusaidia utoaji wa vifaa vya vifaa vya Tehama kwa wenye mahitaji makundi maalumu kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vinavyopangwa katika kila mwaka wa utekelezaji''alisema Mkuu wa Kanda.

Amesema lengo kuu la kutoa vifaa kwa wanafunzi ili waweze kutumia huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,katika kusaidia kupata mahitaji yao ya kimasomo, kama vile vitabu kwenye mtandao na rejea mbalimbali,sambamba na kutoa chachu katika kufikisha,kurahisisha upatikanaji kwa waalimu na wanafunzi,kuandaa masomo,kuwawezesha kuweka habari za shule kwenye mtandao.

Ametoa wito kwa uongozi wa shule hiyo kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vya TEHAMA vinatumika katika matumizi salama ya mtandao ili yaweze kuleta tija kama ilivyokusudiwa,kwani vikitumika vibaya ni hasara.

''Naomba niweke msisitizo kwenye suala zima la matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na matumizi sahihi salama ya mtandao,kwani mtandao ukitumika vizuri ni jambo zuri na lenye manufaa sana,lakini ikitumika vibaya ni hasara''Alisema Mhandisi Imelda.

Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameishukuru TCRA kwa kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo Maalumu ya ILBORU,ambapo ametoa wito kwa walimu na wanafunzi kujitahidi kutumia vifaa hivyo kwa makusudi maalum yaliyokusudiwa huku akiwataka kuvitunza vifaa hivyo ili vidumu.

Kwitega mesema kuwa Mkoa wa Arusha umejipanga kuboresha ufaulu katika shule zake na kuhakikisha kuwa ufaulu unakuwa nzuri kuanzia ngazi ya Kata hadi Kitaifa ili kuleta sifa njema.  

Pia amewaagiza Tehama ngazi ya mkoa kutoa sapoti ya kiufundi kwaajili ya kusaidia vifaa hivyo viendelee kufanya kazi kwa manufaa ya Elimu.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya seondari ya Ilboru Dennis Otieno ameishukuru TCRA kwa kuwapatia vifaa hivyo vya TEHAMA na ameahidi kuwa watavitumia kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa huku akisema vitawasaidia kutuma matokeo ya wanafunzi kwa wazazi,sambamba na wanafunzi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kujisomea na kufahamu mambo mbalimbali bila kuvunja sheria ya mtandao.

''Hapa shuleni tunao wanafunzi ambao ni watundu sana katika mambo ya mtandao,kunammoja aligundua kifaa cha kutambua kama mwanafunzi anayo simu shuleni na mwingine aligundua kifaa cha kutambua kama mwanafunzi anaumwa ambapo taarifa zinatumwa mapema kwa mzazi,hivyo kwetu sisi kupata vifaa hivi ni faraja sana.''Alisema mkuu wa shule

Katika mwaka wa fedha 2018/2019, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imeshatoa vifaa kwa shule tano nchini kwa kuzingatia vigezo vya ufaulu,matokeo ya mtihani wa Taifa mwaka 2015,ambapo shule ya Ilboru ni miongoni mwa shule hizo zilizofanya vizuri kitaifa na hivyo kuweza kukidhi mahitaji ya kupewa vifaa vya TEHAMA.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Computer,UPS,Printer,utengenezaji wa tovuti za shule pamoja na kuunganisha kwenye mtandao ambapo vifaa hivyo viliwasilishwa na kufungwa shuleni hapo mnamo mwezi Agosti mwaka huu

WANAFUNZI WAANAOSOMEA KICHINA WATUNUKIWA TUZO BORA, MAFANIKIO

$
0
0





 Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa kutoa tuzo kwa wanafunzi ambao wanasoma Lugha ya Kichina pamoja na kozi ya Kichina hapa nchini.Hafla fupi ya kutoa tuzo hizo imefanyika katika ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Wiiliam Ole Nasha akizungumza wakati wa kutoa tuzo kwa wanafunzi wanaosoma Kichina hapa nchini pamoja na kozi za kichina. Tuzo hizo zimetolewa jijini Dar es Salaa katika Ubalozi wa china hapa nchini.
 Mmoja ya wanafunzi walioshindana katika shindano la ubunifu lililofanyika nchini China na kuiuka kidedea katika kuendeleza Teknolojia ya ulishaji wa Samaki, Amos Benjamini akizungumza wakati wa kupewa tuzo kwa wanafunzi wanaosoma Somo la kichina na Kozi ya kichinz
 Mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Gloria Gabriel akizungumza lugha tatu tofauti ili kuwapa uelewa baadhi ya wachina na watanzania waliofika katika hafla fupi ya kuwapa tuzo wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya kichina hapa nchuni.
 Baadhi ya washiriki.
 Wageni Waalikwa.
 Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Wiiliam Ole Nasha  akitoa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaofanya vizuri katika masomo ya kichina hapa nchini.

 Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akitoa tunzo kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini kwa kufanya vizuri katika masomo ya kichina, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa China.
 Picha ya Pamoja.
Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke akiteta jambo na Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Ole nasha wakati wa utoaji tuzo kwa wanafunzi wanaosoma kichina na kozi za kichina waliopata tuzo bora na tuzo za h

KATIKA kuendeleza ushirikiano wa seikali ya china na Tanzania nchinya china imekuwa miongoni mwa nchi inayotoa ufadhili kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa  Tanzania wanaoomba ufadhili wa kusomea kozi mbalimbali nchini china. 

Akizungumza na wakati wa kutoa tuzo ya Balozi , Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke kwa wanafunzi wanaosoma  Lugha ya kichina hapa nchini katika vyuo mbalimbali, amesema kuwa ushirikiano baina ya China na Tanzania unazidi kuimarika zaidi hasa wanafunzi wa Tanzania wanapojifunza Lugha ya Kichina.

"Kwa mwaka huu Serikali ya China limetoa nafasi 302 za ufadhili kwa wanafunzi wanaojifunza kozi mbalimbali nchini". Amesema Wang Ke.

Amesema kuwa Serikali ya China imekuwa nchi inayotoa idadi kubwa zaidi ya nafasi za Ufadhili kwa wanafunzi wa Tanzania.

"Mpaka sasa wanafunzi 1900 wamepata ufadhili wa serikali ya China na kwenda kusoma nchini China miongoni mwao wamehitimu nchini china na wamerudi Tanzania kwaajili ya ujenzi wa sekta mbalimbali hapa nchini". Amesema Wang Ke.

Hata hivyo mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa China Amos Benjamini alishiriki katika kambi ya ugunduzi kwa vijana duniani(UNLEASH) yaliyofanyika  Shenzhen aliibuka kidedea kwa kubuni teknolojia ya kulisha Samaki.

Katika tuzo hizo wanafunzi 20 wamepata tunzo bora na wengine 60 wamepata tuzo ya Mafanikio, wanafunzi hao ni kutoka  vyuo mbalimbali.

Hata hivyo Naibu waziri wa Elimu na Teknolojia, Ole Nasha amesema kuwa ushirikiano wa China na Tanzania haujaanza sasa ushirikiano huu ni wa mda mrefu hasa  ukiona Reli ya TAZARA unaweza ukajua ni wa muda gani.

 "Kumekuwa na vijana wengi sana ambao wanasoma kwenye vyuo mbalimbali kwa msaada wa serikali ya nchini china kwahiyo China imekuwa sehemu ya wanafunzi wa kitanzania kwenda kujipatia mafunzo mbalimbali". 

Nasha amebainisha kuwa kwa kwa miaka mitatu  kunawanafunzi zaidi 200 wameenda kusoma kwa msaada wa china.

Nasha amesema kuwa ni fursa kwa wanafunzi wa Tanzania kujua Lugha ya kichina ili waweze kufundisha wanafunzi wengine hapa nchini.

Miongoni mwa waliopata tuzo bora na tuzo za mafanikio wamesema kuwa Lugha ya kichina kwa sasa ipo sokoni kwa mtanzania kujua Lugha mbalkmbali duniani zitamsaidia kupata Ajira hata kwenye makampuni ambayo yanatoa ajira kwa kuzingatia kigezo cha kujua Lugha yao.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images