Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

WAKALA WA BENKI YA NMB WAPIGWA MSASA

$
0
0

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB - Filbert Mponzi akimkabidhi Khalifa Kimaro-mmoja wa mawakala cheti cha ushiriki mafunzo ya uwakala.
Mmoja wa mawakala akiuliza swali kwa watoa mada
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd akimkabidhi Betty  Rutihanda-mmoja wa mawakala cheti cha ushiriki mafunzo ya uwakala.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawakala – James Manyama akitoa mada 

**********************************

MAWAKALA wa Benki ya NMB Halimashauri za Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam wamepigwa msasa katika Semina ya kuwajengea uwezo na kuboresha huduma inayomfikia mteja wa NMB katika maeneo yao pamoja na kujilinda na uhalifu na utakatishaji fedha.

Katika semina iliendeshwa hivi karibuni katika maeneo ya Sinza na Ilala jijini Dar es Salaam,Mawakala wa Benki ya NMB walipata fursa ya kupewa elimu juu ya kumpatia mteja huduma bora, kuuliza maswali na elimu juu ya kujikinga na vitendo vya kihalifu ikiwemo kupitisha fedha chafu, ambapo ni kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza katika Semina hiyo Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd, alisema NMB Wakala ni njia inayomfikishia huduma mteja kwa urahisi zaidi na kwa wakati.

“Kwa nini tunawatumia mawakala, tumeona kwamba ni njia moja wapo inayoweza kutufanya tuwafikie wateja wetu ambao ni watanzania zaidi ya Milioni 60, hatuwezi kufika kila eneo huwa kidogo kuna ugumu wake lakini kupitia mawakala tunaweza kuwapata kila eneo wenye uwezo wa kuwahudumia wateja wetu kama vile ambavyo tumekusudia.

“Mteja wetu anaweza kutoa pesa, kuweka pesa, ataweza kulipia miamala mbali mbali, kama kulipia malipo ya maji, umeme, malipo ya serikali na ada za shule, tunasisitiza kwamba wateja wetu waendelee kutuamini kupitia mawakala wetu ambao wanaendelea kutoa huduma.

“Tumekuwa na semina mbali mbali, tukiwa tunaendelea kuwajengea uwezo mawakala ili waendelee kutoa huduma zetu kwa ukaribu Zaidi. Muhimu ni muongozo wetu kila mwaka tunataka tuwasikilize changamoto juu ya huduma zetu, tuwaulize maswali watuulize maswali wote kwa pamoja tuweze kuhakikisha huyu mtanzania anapata huduma zetu kokote kule anakopatikana kwa ufanisi mkubwa.

Badru alisema, sio kwa Dar es Salaam tu, bali wameendesha semina kama kwa zaidi ya maeneo 40 nchi nzima. Semina hizi zimeleta mafanikio makubwa sana, hasa kwa kuokoa muda wa mteja, kupata huduma ya uhakika na kwa urahisi.

“Sisi kwetu wateja ni wafalme na ndio maana tunaendelea kuwa na huduma za mbadala kama, wakala, masine za ATM, na NMB Mkononi ili kuweza kumfikia mteja wetu kiurahisi zaidi.”alisema Badru.

Naye Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawakala – James Manyama, alisema lengo la kukutana na Mawakala ni kuwapa muelekeo wa wapi Benki inaelekea kwa  wakati na kuwapa mafunzo jinsi ya kujilinda na utakatishaji fedha pamoja na kuingiza fedha katika mikono ya gaidi.

“Kama Mawakala, tunawapa wajibu wa kutunza amana za wateja, kutunza usiri wa wateja, mawakala wetu wamethibitisha ubora wa huduma zetu na wameahidi kwenda kutoa huduma bora kwa wateja wetu” alisema Manyama.

Kwa upande wa Mawakala waliohudhuria semina hiyo walitoa kongole zao kwa NMB kwa jinsi ambavyo inawajali kwa kuwapaa elimu na fursa ya kutoa changamoto zao ili kuweza kuboresha huduma zao.

“Nafurahi sana kuwa karibu na NMB, nafurahia kuwepo katika hii semina, NMB wanatoa huduma nzuri, pia wako karibu na sisi mawakala wao, kila wakala anafanya kazi kwa ukaribu sana na tawi lake la NMB linalomhudumia, nashauri Watanzania wenzagu kuchangamkia fursa ya Uwakala wa NMB maana inalipa” Tedy Michael – Wakala NMB Makumbusho.

“Tunashukuru kwa semina hii ambayo imetupa elimu juu ya nini cha kufanya kwa wateja wetu, tumepata mbinu mbadala ya kutoa huduma bora kwa wananchi na tunawaahidi benki yetu pendwa ya NMB kuwa tutafanya kazi kwa weledi na kuhakisha wateja wanafurahia huduma zetu.” Alisema Khanifa Kimaro – Wakala NMB Kimara.

NAIBU WAZIRI MABULA AMVAA DED ULANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro Mathayo Masele wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Malinyi unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Kulia) akielekea kukagua ofisi za Ardhi za halmashauri ya wilaya ya Ulanga wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ulanga Juma Kapilima.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpa maelekezo Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Ulanga Luis Ndumbaro wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya.

****************************


Na Munir Shemweta, WANMM ULANGA


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kumpatia maelezo kuhusiana na uamuzi wake wa kuondoa kasma ya ardhi na mipango miji kwenye bajeti ya mapato ya ndani baada ya sekta hiyo kuhamishiwa Wizarani.

Uamuzi huo wa Dkt Mabula unafuatia kuelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya kuwa moja ya changamoto inayoikabili sekta ya ardhi kwenye wilaya yake ni ukosefu wa fedha za uendeshaji wa ofisi uliosababishwa na halmashauri kuondoa kasma ya ardhi na mipangomiji baada ya sekta hiyo kuhamia wizara ya ardhi jambo alilolieleza limesababisha utekelezaji majukumu ya kila siku kuwa magumu.

Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika wilaya hiyo mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alimtaka Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga Juma Kapilima kumpa taarifa ya maandishi kuhusiana na suala hilo kwa kuwa Waraka uliotolewa kuhusiana na suala hilo unaeleza wazi kilichohamishiwa wizarani ni Mamlaka ya Nidhamu na Ajira pekee.

‘’Hii ni serikali moja, ofisi ya Mkurugenzi ni Mamlaka ya upangaji, nataka maelezo ya msingi maana waraka unajieleza na ulienda kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya na hata mishahara ya watumishi wa sekta ya ardhi bado inalipwa na TAMISEMI’’ alisema Dkt Mabula,

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Ulanga, mbali na changamoto ya ukosefu wa fedha katika sekta ya ardhi, wilaya yake inakabiliwa pia na uchache wa watumishi hususan katika fani za Mipango Miji, Uthamini, Uchoraji Ramani na Watunza Kumbukumbu alioueleza kuwa unasababisha shughuli zilizopangwa kutofanyika kwa ufanisi.

Aidha. Naibu Waziri Mabula alionesha kutoridhishwa na kasi ya zoezi la urasimishaji na upimaji viwanja kwenye wilaya ya Ulanga na kueleza kuwa halmashauri hiyo inatakiwa kuongeza kasi katika mazoezi hayo mawili ili kuwa na mji uliopangika na kuepuka ujenzi holela.

Aliongeza kwa kusema, katika zoezi la urasimishaji linaloendelea nchini halmashauri ya Ulanga inatakiwa kukaa na wananchi pamoja na makapuni ya urasimishaji ili kukubaliana gharama za urasimishaji na kusisitiza kiwango cha shilingi 150,000 kilichowekwa na Wizara kinaweza kupungua ili kuwafanya wananchi wengi kushiriki,

‘’Kuna halmashauri zimekubaliana na makampuni ya urasimishaji ambapo gharama zimepungua hadi kufikia 60,000 hivyo ninyi hapa msing’ang’anie kiwango cha 150,000 maana kinaweza kupungua kulingana na ugumu wa kazi na idadi ya watu waliojitokeza kurasimishwa’’. Alisema Dkt Mabula

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametembelea wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro na kuitaka wilaya hiyo kuongeza kasi ya upimaji, upangaji na umilikishaji ardhi na kuzingatia kupanga mji wa kiserikali utakaojumuisha taasisi zote za umma.

Aidha, Dkt Mabula alikagua ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya Malinyi pamoja na nyumba ya Mkuu wa wilaya unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo alionesha kufurahishwa na kasi ya ujenzi wa majengo hayo mawili yanayotarajiwa kukabidhiwa rasmi mwanzoni mwa mwaka ujao 2020.

MIAKA KUMI YA KAKANGAGA SHULE YA BAKWATA INAYOPOKEA WAKIRISTO.

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Shule ya Kiislamu ya KAKANGAGA MUSLIM SECONDARY SCHOOOL iliyopo Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, imetimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake, ikiwa tayari imekwisha hitimisha Vidato vya Nne mara nane toka Mwaka 2009.

Shule hiyo inayomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Kwa miaka mitano sasa imekuwa chini ya usimamizi madhubuti wa Uongozi wa Katoro Islamic Seminary, ambao pia ni wasimamizi wa Kahama Islamic, hali ambayo imechangia Mafanikio makubwa kwa Muda Mfupi toka ilipokabidhiwa, ukilinganisha na awali wakati ilipokuwa ikiendeshwa na BAKWATA.

Akitaja baadhi ya mafanikio hayo katika Taarifa fupi ya Shule hiyo kwenye mahafali ya kuwaaga Kidato cha NNE mwaka huu, yaliyofanyika Shuleni Mwishoni mwa wiki, Makamu wa Shule Ustadhi Fuadi Iddi amesema kuwa Shule imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka, kupitia jitihada zinazofanywa na Uongozi wa Shule, walimu pamoja na wanafunzi, Kwa kuwapatia mazoezi ya kutosha, kutunza nidhamu ya Wanafunzi Kwa kuchukua hatua stahiki pale yanapotokea makosa, huku akiongeza kuwa kwa Kidato cha Nne wanaohitimu Mwaka huu, matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa, Shule ilipata Division one (10), D.II (35), D.III (21), D.IV (2), Zero (0). na shule ilishika nafasi 3/22 Kiwilaya na 13/171 Kimkoa.

Katika kuweka kando dhana ya Udini, Lilian Adriani, Kiiza Tugara, na Miriam Oscar ni miongoni mwa wahitimu wa Kidato cha Nne 2019 Kakangaga, mbali na mambo mengine wanaeleza wazi kuwa Mavazi ya Kujistiri, Taaluma na Maadili mema ndio sababu pekee zilizowashawishi kutoka shule zao za awali na kuhamia Kakangaga, hivyo na kuwepo kwao katika shule ya Kiislamu ilihali wao ni wakiristo, wamejifunza mambo mengi, yakiwemo Upendo, ushirikiano, na Umoja bila kubaguana.

 Pichani ni Wahitimu wa Kidato cha Nne Kakangaga Muslim Seminary, licha ya kuwa shule ni ya Kiislamu kimaadili lakini wao ni wakristo, kutoka kushoto ni Lilian Adrian, Kiiza Tugara na Miriam Oscar kama walivyokutwa na kamera yetu.
Pichani ni Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Kakangaga wakionekana na nyuso katika mahafali yao yaaliyofanyika Jumamosi hii shuleni Kakangaga Mkoani Kigoma.
 Pichani Baadhi ya Viongozi wa Dini kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Viongozi wa BAKWATA wamiliki wa Shule ya Kakangaga Muslim wakiwa meza Kuu katika mahafali ya kuhitimisha Kidato cha Nne kwa Mwaka wa Nane toka kuanzishwa shule hiyo.
 Pichani ni Mhitimu wa Kidato cha Nne Kakangaga Samir Haruna, ambae amekuwa Imam wa Shule toka Kidato cha Kwanza, akisoma Qur-an miongoni mwa Juzuu alizohifadhi, wakati wa mahafali yao ya kuhitimu Jumamosi hii.
 Pichani ni Mkuu wa Shule Kakangaga Muslim  Ustadh Abdul-Jalil Siraji Mustapha moja kati ya zao la Katoro Islamic Seminary, akitoa Salaam zake kwa Wazazi, walezi, na wanafunzi(hawapo pichani) wakati wa mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne 2019.

WAZIRI BITEKO ACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA IMALANGUZU

$
0
0


**************************************

Na Tito Mselem, Bukombe

Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa mifuko 100 ya saruji pamoja na mbao zenye htamani ya Shilingi milioni 4.2 ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Imalanguzu Wilayani Bukombe Mkoani Geita. 

Waziri Biteko ametoa mchango huo ili kutatua changamoto ya huduma za afya katika Kijiji cha Imalanguzu Wilayani Bukombe ambapo huduma hizo zimekuwa kikwazo kwa wakazi wa Kijiji wa Kijiji hicho kwa muda mrefu. 

Waziri Biteko ametatua changamoto hiyo alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi na kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji hicho na kubaini mapungufu makubwa katika sekta ya afya Wilayani humo.

Aidha, Waziri Biteko, amewapongeza Walimu wote wa Wilaya ya Bukombe kwa ushindi mkubwa walioupata baada ya Wilaya hiyo kuongoza katika ufaulu wa darasa la saba kimkoa na kushika nafasi ya 27 kitaifa kati ya shule 188. Wakati huo huo, Waziri Biteko, ametoa rai kwa wananchi wa Imalanguzu kuhakisha wanapeleka watoto wao shule kwani ndiyo urithi pekee ambao unaweza kumuachia mtoto na baadae ukamsadia.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatoa kila mwezi zaidi ya shilingi bilioni 27 ili watoto wetu wasome bule na nchi hii inahitaji wasomi wengi ili walisaidi taifa hili, nitashangaa sana nikisikia mzazi hajampeleka mtoto wake shule,” alisema Biteko.

Pamoja na hayo, Waziri Biteko amewaasa wanafunzi wote Wilayani humo kutekeleze wajibu wao wa kusoma kwa bidii na mara baada ya kumaliza elimu zao na kupata kazi wasiwasahau wazazi wao waliowapeleka shule badala yake waachane na zana ya kuwatelekeza wazazi wao ili wahudumiwe na TASAF.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko, amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa hatua za kukuza uchumi wa nchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya madini, viwanda, afya na kilimo. 

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa maendeleo aliyoyaleta, amejenga Reli ya kisasa, amenunu ndege zakutosha na ameanzisha miradi mikubwa mingi ambayo nimafanikio makubwa katika taifa letu, tumuunge mkono Rais wetu,”.

Pia, Waziri Biteko, amewasisitiza wananchi Wilayani Bukombe kuhakikisha wanafanya kazi ili waibadirishe Wilaya ya Bukombe iwe Bukombe mpya na yenye mafanikio, wasikubali kudanganywa kwamba maendeleo yataletwa na Serikali badala yake wafanye kazi wakishirikiana na Serikali ndiyo maendeleo yakuja.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bukombe Rozaria Masokola, amempongeza Waziri Biteko kwa msaada alioutoa katika kuhakikisha changamoto ya kituo cha afya katika Kijiji cha Imalanguzu inakuwa historia.

Benki ya Exim Yazidi kujitanua zaidi, Yaingia Ethiopia.

$
0
0
Benki ya Exim Tanzania imezidi kujitanua zaidi nje ya mipaka ya Tanzania kwa kufungua kituo cha huduma za benki hiyo (Commercial Representative Office ) katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse wakati akifungua rasmi tawi jipya la benki ya Exim Tanzania lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam ikiwa ni baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania. Katika uzinduzi huo, Dk Kibesse alimuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Kufuatia hatua hiyo Benki hiyo inakuwa taasisi ya kwanza ya kifedha nchini Tanzania kuendesha shughuli zake kwenye mtandao wa mataifa matano  ikiwemo  Ethiopia ambayo inatajwa kuwa ndio nchi ya pili kwa ukubwa wa idadi  ya watu barani Afrika.Mataifa mengine ambayo benki hiyo inaendesha huduma zake ni pamoja Uganda, Comoros na Djibouti.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es salaam mapema leo ilisema kwamba benki hiyo imepata leseni ya kufungua na kuwa na Ofisi ya Mwakilishi wake nchini Ethiopia kupitia tawi lake la nchini Djibouti na imepanga kuanza kazi kutoa huduma zake nchini humo hivi karibuni.
"Tunatarajia kwamba huduma zetu zitaanza  kutolewa kikamilifu mapema mwezi Disemba, 2019 kupitia Ofisi ya Mwakilishi wetu kibiashara  iliyopo katika Jengo la Zouleka LKG, ghorofa ya 2, Sub City Bole, 2160 / B. Addis Ababa. '' alisema Bw Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo kupitia taarifa hiyo.
Alisema upanuzi huo  wa Ethiopia unakuja kama sehemu ya mikakati wa upanuzi wa benki hiyo kwa ujumla katika kutimiza matarajio yake ya kuwa Benki ya Pan African. Aidha ufunguzi wa ofisi hiyo  ya uwakilishi utakuza mipango ya kimkakati katika kuongeza ushirikiano na nchi mbambali  za Afrika na inatoa jukwaa muhimu kwa Benki hiyo kuuza huduma zake za kipekee kwa biashara za nje.
"Hii ni hatua muhimu kwa Benki ya Exim ikiwa kama kikundi.'' Alisema Matundu  huku akibainisha kuwa ukuaji thabiti wa uchumi nchini Ethiopia ambao umechochewa na uwekezaji mkubwa wa umma na ongezeko la wateja ndio sababu nchi hiyo imekuwa kivutio kwa taasisi za kifedha kuwekeza katika taifa hilo.
Alisema kuwa Benki hiyo pia inakusudia kusaidia ufanyaji wa biashara baina ya Tanzania  na Ethiopia,  kusoma soko na fursa za uwekezaji zilizopo huku ikishiriki katika kuendesha ukuaji wa uchumi baina ya nchi hizo mbili.
Aliongeza kuwa Ethiopia imerekodi viwango vya juu zaidi vya ukuaji wa uchumi ulimwenguni kote katika miaka michache iliyopita na imeorodheshwa  miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi barani Afrika kulingana na takwimu zaShirika la Fedha Duniani (IMF).
"Tunatazamia fursa zaidi za ukuaji kupitia soko la Ethiopia, haswa kwa kuzingatia mageuzi yaliyofanyika hivi karibuni nchini humo. Tunaamini kwamba kuna fursa nyingi za ukuaji wa uchumi nchini Ethiopia, na Benki ya Exim kama kikundi tunataka kuwezesha hili. "Alisema.
Aidha ukuaji huo wa Benki ya Exim umeonesha kuivutia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambapo hivi karibuni, akifungua rasmi tawi jipya la benki hiyo lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam ikiwa ni baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse aliipongeza benki hiyo huku akiahidi kuipa ushirikiano zaidi katika kufanikisha adhma yake ya kufungua matawi zaidi nje ya nchi.
“Ni fahari kwetu kuona benki ya kizalendo inafanya mambo makubwa kama haya. Mmekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mabenki hapa nchini jinsi inavyojizatiti kujiimarisha ndani na nje ya mipaka ya nchi.Hatua hii ni sawa na kuitikia kilio cha wadau wa huduma za kifedha hapa nchini  wanaohitaji huduma zinazokidhi mahitaji yao pia huduma zinazolingana na zile za kimataifa na kwenye mazingira yaliyobereshwa.’’ Alisema Kibesse.

Mtanzania Ateuliwa Nafasi Nyeti Umoja Wa Mataifa.

$
0
0

Mtanzania, Elizabeth Maruma Mrema, ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Sekretarieti inayosimamia Mkataba wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa tofauti za kibiolojia (CBD) yenye makao yake makuu Monteal, Canada kuanzia Disemba 1, mwaka huu.

Uteuzi huo umefanywa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw António Guterres kufuatia kujiuzulu kwa Bi Cristiana Pasca Palmer,raia wa Romania kutokana na sababu za kiafya.

Kulingana na taarifa iliyotumwa kwenye wavuti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira (UNEP), uteuzi huo unatajwa kuwa unaongeza matumaini katika uhifadhi wa masuala ya bayonuai ya kibaiolojia, matumizi endelevu ya baiolojia hizo, na ugawaji wa faida zitokanazo na rasilimali za kijenitiki kwa kuzingatia usawa na haki.

Kabla ya kuteuliwa kwake, Bi Mrema alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Makao makuu ya UNEP jijini Nairobi, Kenya ambapo amefanya kazi kwa zaidi ya miongo miwili.

Majukumu yake katika Idara ya Sheria ya UNEP ni pamoja na uratibu wa ujenzi wa uwezo, maendeleo, utekelezaji na pia kufuatilia utekelezaji wa sheria za mazingira na mikutano ya kimataifa ya mazingira. Pia aliongoza masuala yanayohusiana na utawala wa kimataifa wa mazingira.

Bi Mrema ni Mwanasheria kitaaluma na Mwanadiplomasia akiwa na Shahada ya Sheria (LLB) (Hons) kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, Shahada ya Uzamili (LLM) kutoka Chuo Kikuu cha Dalhousie, Canada na Stashahada ya Juu katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa na diplomasia (Summa Cum Laude) kutoka Kituo cha Mahusiano ya Kigeni na Diplomasia jijini Dar-es-salaam.

Aidha, Bi Mrema amechapisha nakala kadhaa zinazohusiana na sheria za kimataifa za mazingira, ufuatiliaji na utekelezaji wa mikataba na maendeleo ikiwemo makubaliano kadhaa ya mazungumzo kuhusu hali mazingira ya kimataifa pamoja na miongozo inayotumika sasa na UNEP katika mipango yake ya kujengeana uwezo.

Kabla ya kujiunga na Kitengo cha Sheria cha UNEP mnamo Juni 2014, Bi Mrema alikuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira, anayesimamia uratibu, shughuli na utoaji wa programu kuanzia mwaka 2012 na kwa mwaka mmoja, pia aliwahi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo.

Mnamo mwaka 2004 alipewa tuzo ya Meneja wa UNEP bora zaidi wa mwaka kuwahi kutokea, aliyotambulika kama Tuzo ya Wafanyikazi ya UNEP Baobab kwa utendaji bora na kujitolea kufikia malengo ya UNEP.

Mnamo mwaka wa 2009 aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa UNEP/ Sekretarieti ya Mkataba juu ya Uhifadhi wa wanyamapori wanaohama (CMS)

Kabla ya kujiunga na UNEP, Bi Mrema alifanya kazi na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania na hadi anaondoka alikuwa Mshauri Mwandamizi wa Sheria.

Katika kipindi cha uhudumu wake kwenye Wizara hiyo Bi Mrema, pia alikuwa Mhadhiri wa Sheria ya Umma ya Kimataifa na Diplomasia ya Mkutano katika Kituo cha Uhusiano wa nje na diplomasia cha Tanzania.
 
 Bi. Elizabeth Maruma Mrema  

PSPTB YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WA ZANZIBAR

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman akizungumza na wahitimu wa mafunzo yaliyokuwa yanaendeshwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB) kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa fedha na utawala wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB) Paul Bilabaye na kushoto ni Mratibu wa Miradi Zanzibar(ISPGGIII) Khalifan Ali Said.
Mkurugenzi wa fedha na utawala wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB) Paul Bilabaye akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugeniz wa Maendeleo  ya Taaluma ya Bodi hiyo wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa na PSPTB kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.Katikati ni  Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman  na kulia ni Mratibu wa Miradi Zanzibar(ISPGGIII) Khalifan Ali Said.
 Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB), Amos Mang'ombe akitoa ufafanuzi kwa ufupi kwa mgeni rasmi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman  kuhusu mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwa maofisa wa ununuzi wa Zanzibar yaliyofanyika  kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mjenga uwezo na Huduma za Ushauri wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Haitham Said Hassan akizungumzia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na  Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB) kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalamu wa ununuzi kutoka Zanzibar wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman alipokuwa anafunga mafunzo kwa wataalam hao yaliyofanyika kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma - PSPTB, Shamim Mdee(kushoto),  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi ( PSPTB) Sophia Kiyeyeu(katikati) na Afisa mkuu wa Teknolojia ya habari na mawasiliano wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB), Grace Msele(kulia) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman alipokuwa anafunga mafunzo kwa wataalam hao yaliyofanyika kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman akiwakabidhi vyeti baadhi ya wataalam wa Ununuzi kutoka Zanzibar wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar(ZPPDA) Othman Juma Othman akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini Tanzania(PSPTB) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 14 katika ukumbi wa TaGLA jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja 

Benki ya NMB yakabidhi gawio la Shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio la Shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurungezi wa Benki ya NMB - Margaret Ikongo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB - Ruth Zaipuna (kulia) katika hafla ya upokeaji wa gawio na michango kwa Serikali iliofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma mapema leo. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango – Dkt. Philip Mpango na Spika wa Bunge la Tanzania -Job Ndugai.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani a Dkt John Pombe Magufuli,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea gawio na michango kutoka katika Taasisi, Makampuni na Mashirika ya Umma hafla,hiyo imefanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo.

Tandahimba yafanya uchaguzi kwa amani

$
0
0
Wananchi wa Tandahimba leo wamepiga kura kuchagua kiongozi wa Kitongoji na wajumbe mchanganyiko katika Khali ya utulivu na amani

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tandahimba Ahmada Suleiman  amesema wanachi wamejitokeza katika kata zote mbili ambapo uchaguzi umefanyika

"Katika vituo vyote ambavyo nimetembelea wananchi wamejitokeza kushiriki kupiga kura,na zoezi Hilo limefanyika kwa amani na utulivu Hadi Sasa," alisema Suleiman.
 Afisa Mtendaji wa kata ya Nanhyanga Zamaradi  akitimiza haki yake
 Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tandahimba Ahmada Suleiman
 Wananchi wa Kijiji Cha Mlingano kata ya Nanhyanga wakisubiri kupiga kura
 Wananchi wa Kijiji chaDodoma kata ya Nanhyanga wakisubiri kupiga kura
Wananchi wa kiwanjani kata ya Tandahimba wakisubiri kupiga kura

RAIS DKT. MAGUFULI AIMWAGIA SIFA DAWASA KWA KUTOA GAWIO KWA SERIKALI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (katikati) akipokea gawio lenye thamani ya Bilioni 1.3 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili kulia)  akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akishudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto). Picha zote na Othman Michuzi, Dodoma.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli ameipongeza Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kuweza kuwasilisha gawio la Bilioni 1.3

Dkt Magufuli amepokea jumla ya Trilioni 1.05 kutoka taasisi, mashirika na makampuni, hafla iliyofanyika leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

Hayo ameyasema leo wakati wa hafla ya kupokea kwa michango, gawio na  ziada kutoka kwa Tasisis, mashirika na makampuni yenye umiliki wa serikali au hisa.

Akitoa pongezi hizo, Magufuli amesema yapo mashirika na taasisi mbalimbali hazijapelekea gawio ila anampongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kwa kufanikisha mamlaka hiyo kutoa gawio.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja, katika hafla ya kukabidhi Gawio kwa Serikali, iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma leo. 

"Jenerali Mwamunyange emeleta gawio, ametoka katika ukuu wa majeshi nimempeleka katika maji (Dawasa) na amefanya vizuri , hongera sana", amesema Magufuli.

Amesema, kutokana na hilo anaamini kuwa wenyeviti wa bodi wakiwa Wanajeshi basi mashirika yataenda vizuri katika uendeshaji na kila mwaka gawio litakuwa kinazidi.

"Kuna jumla ya mashirika, taasisi na makampuni karibu 266 lakini ukiangalia walioleta ni 79, yapo mengine 187 hayajaleta nakuagiza Waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango awatumie barua nawapa siku 60 walete gawio au wakishindwa tuyataifishe," amesema.
Aidha, amesema ndani ya miaka mitano kuanzia 2014-15 mashirikia yaliyotoa gawio yalikuwa ni 24 walikabidhi jumla ya Bilioni 130, kwa mwaka 2015-16 yalikuwa ni 25 yakikabidhi bilion 249, mwaka 2016-17 yakipanda hadi 38  wakitoa gawio la bilioni 677 na kwa mwaka 2017-18 yakiwa 40 wakikabidhi bilioni 842. Pia kwa mwaka wa 2018-19 mashirika na taasisi zilipanda hadi kufikia 79 wakitoa jumla ya Trilioni  1.05.

Dawasa wamekuwa moja kati ya taasisi na mashirika ya Serikali 79 yaliyotoa gawio la Bilion 1.3 kwa serikali.

Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa mamlaka kutoa gawio kwa serikali na kwa mwaka huu wamekabidhi bilioni 1.3 kwa mwaka 2018-19.

RAIS DK.MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH.BILIONI 11 KWA MWAKA 2018 KUTOKA PUMA ENERGY TANZANIA

$
0
0
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imetangaza gawio la Sh.bilioni 22 kwa wanahisa wake kwa mwaka 2019 ambapo leo Novemba 24 imekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Dk.John Magufuli Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Taarifa ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari imefafanua kwa kina kuwa kampuni inamilikiwa kwa pamoja na serikali (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50. 

Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Imeelezwa kuwa majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.

Taarifa hiyo imesema kufikia mwisho wa mwaka ulioishia Desemba 31 2018 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi bilioni 25. Kampuni iliwekeza takribani shilingi bilioni 16 kwa mwaka 2018 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo ukamilishwaji wa mfumo wa kujazia mafuta katika jengo namba Tatu (Termina 3) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar e salaam.

Pia ununuzi wa vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

"Wakurugenzi wa kampuni wamependekeza gawio la Sh.bilioni 22 bolioni kwa mwaka ulioishia Disemba 2018. Hivyo Kila mwanahisa atapata shilingi 11 bilioni. (2017 gawio lilikuwa 18 bilioni, 2016 gawio lilikua 14 bilioni na 2015 gawio lilikua 9 bilioni.) 

"Kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 57 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2016 na kwa asilimia 22 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2017. 

"Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,"imesema taarifa hiyo

Dominic Dhanah, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Limited amesema kuwa ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2018 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato. Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko. 

Pia ameongeza kuwa taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12% mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017

Dhanah pia amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt John Pombe Magufuli na Serikali yake katika mikakati yake ya kukusanya kodi, kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani na kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2019/20. 

Amesema kuwa mikakati hiyo imewezesha PumaEnergy Tanzania kupata kazi ya kuuza mafuta katika mradi wa reli ya kati “standa gauge”, mradi wa bwawa la umeme la Mwl. Nyerere kule Rufiji, Daraja jipya la Salender na miradi mingine mingi ya kimkakati.

" Miradi hii mikubwa inatoa fursa kwa wawekezaji mbali mbali kufanya biashara na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi. Puma itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa Puma Energy utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio yenye thamani ya Bilioni 11 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dkt Selemani Majige (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Ofisa Mawasiliano na Mwanasheria wa Kampuni hiyo Goodluck Shirima (kulia). Gawio hilo limekabidhiwa leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Selemani Majige(wa kwanza kulia) akiwa na wageni wengine waalikwa wakati wa tukio la kampuni,mashirika na Taasisi zikabidhi gawio kwa Serikali ambapo Rais Magufuli amepokea gawio leo Novemba 24,2019 Ikulu Chamwino jijini Dodoma
Godluck Shirima kutoka Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania(wa kwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa ghafla ya Taasisi, Mashirika na Kampuni kukabidhi gawio kwa Serikali,ambapo Kampuni ya Puma amekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Magufuli leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma
 Rais Dk.John Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi,Mashirika na Kampuni baada ya tukio la kukabidhiwa kwa gawio iliyofanyika leo Novemba 24 Ikulu Mjini Dodoma

Waziri Mkuu Afunga Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya gazeti, kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, Yussuf Khamis, wakati akitembelea mabanda, kwenye Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaliyofungwa rasmi Novemba 24, 2019. Kutoka kushoto ni Maafisa Biashara na Matangazo, Rahma Juma,Khalid Hussein na Khadija Khamis.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Afisa Manunuzi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar, Shinuna Ismail, wakati akitembelea mabanda, kwenye Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaliyofungwa rasmi Novemba 24, 2019. Kutoka kushoto ni Maafisa Biashara na Matangazo, Rahma Juma,Khalid Hussein na Khadija Khamis.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika mwani, wakati akifafanuliwa jambo na Naibu Mkurugenzi Mkuu TAN TRADE, Latifa Khamis, kwenye Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaliyofungwa rasmi Novemba 24, 2019, kwenye viwanja vya Fumba Zanzibar.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi, kwenye Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliyoyafungwa rasmi Novemba 24, 2019
Wananchi waliofika Mwenyekiti ufungaji wa Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia, kwenye Maonesho hayo, Novemba 24, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Wajasiriamali Jumuiya Afrika Mashariki, Josephat Royemam, kwenye Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliyoyafungwa rasmi Novemba 24, 2019. Kutoka Kushoto ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Balozi Amina Salum Ally na Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar, Shadya Mohamed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume, wakati akiwasili Mwenyekiti Viwanja vya Fumba, kufunga Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, Novemba 24, 2019.

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 60 KWA MASHIRIKA 187 AMBAYO HAYAJATOA GAWIO YAHAKIKISHE YANATOA, WAKURUGENZI, WENYEVITI WA BODI WAKALIA KUTI KAVU...

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio yenye thamani ya Bilioni 169 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prof. Ignatus Rubalatuka (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Deusdedit Kakoko Goodluck Shirima (kulia). Gawio hilo limekabidhiwa leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango. Picha zote na Othman Michuzi, Dodoma.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii - Dodoma

RAIS Dk. John Magufuli ametoa siku 60 kwa wakurugenzi na wenyeviti wa bodi za Mashirika, Taasisi na Kampuni za umma 187  kuhakikisa wanatoa gawio kwa Serikali, kinyume na hapo waondoke wenyewe katika nafasi zao kabla ya kuwachukulia hatua.

Amesisitiza ili kuhakikisha kampuni, mashirika na taasisi zinatoa gawio umefika wakati wa kuingia nao mikataba wote ambao wanapewa majukumu ya kusimamia kampuni hizo ili wakishindwa kuleta faida washitakiwe na ikiwezekana wafungwe kabisa, kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakidekezwa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 24, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma baada ya kupokea gawio kutoka kwa mashirika, kampuni ya taasisi ambapo amesisitiza wote ambao hawajatoa gawio wahakikishe wanatoa ndani ya siku 60 ambazo ni sawa na miezi miwili kuanzia leo na watakaoshindwa watakuwa wamejifukuza kazi wenyewe.

"Serikali hadi sasa imewekeza mtaji wa Sh.Trilioni 59.6 kwa mashirika na taasisi 266 lakini pamoja na uwekezaji mkubwa kuna changamoto ya usimamizi na utendaji mbovu kwenye mashirika ambayo serikali ina hisa mapato yanayopatikana ni kidogo, Mfano mwaka 2014/15 Serikali ilikusanya Sh.bilioni 130 kutoka mashirika 24, 2015/16 zilikusanywa Sh.Bilioni 249.3 kutoka taasisi na mashirika 25,"amesema .

Hivyo Rais Magufuli amesema kutokana na hali hiyo Serikali ilianza kuchukua hatua mbalimbali ambazo zimeongeza ukusanyaji ambapo mwaka 2016/17 zilikusanywa Sh.Bilioni 677 kutoka taasisi 38,na mwaka  2017/18 zilikusanywa Sh.Bilioni 842.13 kutoka mashirika na taasisi 40, mwaka 2018/19 Sh.Trilioni 1.05 kutoka taasisi na mashirika 79.

Amefafanua ni vema tukajiuliza katika  mashirika hayo 266 yaliyochangia 79 na Serikali imeweka mtaji wa Sh.Trilioni 59.6, yanabaki mashirika 187 ambayo hayana habari ya kuchangia wakati yana bodi, na bodi zina wenyeviti ambao wanalipana posho kila wanapokaa, wakurugenzi wanapanga semina, mikutano, wanasafiri, wanastarehe, wana magari na serikali imeweka pale fedha zake.

"Kuna  mashirika ambayo mishahara yake inalipwa na Serikali na wengine wamepewa nyumba. Unaweza kujiuliza katika situation ya namna hiyo ungekuwa wewe ndo Rais ungefanyaje?Tena unaweza kukuta wengine wapo hotelini wanaangalia TV, fedha ambazo Serikali imewekeza katika mtaji huo ni za watanzania,"amesema.

Amesema waliopewa jukumu la kusimamia mashirika , kampuni na taasisi hizo kila siku wanafanya biashara lakini wakizungumza wanasema wanapata hasara lakini magari wanayo, mikutano wanafanya, wanakwenda katika starehe mbalimbali lakini gawio wameacha zinatolewa na kampuni 79.

Hivyo amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango kuwaandikia barua wanaosimamia mashirika hao ya kuwataka ndani ya siku hizo 60 wawe wametoa gawio kwa Serikali na kwamba muda wa kubembelezana umekwisha.

Amefafanua kuwa kama mwenyekiti ameteuliwa na yeye ni vema siku hiyo ikifika akajiondoa mwenyewe kwani hatakuwa mwenyekiti tena na kama ameteuliwa na mwingine pia wajiondoe wenyewe."Kama ni Mkurugenzi naye ajihesabu hayupo, wapo wanaolipwa mishahara Sh.Milioni 15 kwa mwezi, halafu hakuna gawio hata senti tano why?hufai kuwepo,"amesema.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemwambia Dk.Mpango awaandike barua wale wote wasiokuwepo kwenye orodha ya mashirika 79 yaliyotoa gawio na orodha yao anayo. "Sasa hawa wengine wenye vibuli hivi ni wanani?Katibu Mkuu na Msajili baada ya siku 60 ambaye hataleta gawio lolote ajihesabu hayupo."

Hata hivyo amesema haijalishi Serikali ina hisa kiasi gani hata kama ni asilimia tano wanapaswa kutoa gawio na kwamba hakuna sababu ya kufanya biashara ya hovyo."Nchi za Scandinavia zinajiendesha kwasababu ya magawio zina watu waaminifu, hapa kwetu tunakila kitu bado tunashindwa kujisamamia na kwenda kuomba ufadhili kwa nchi hizo,"amesema.


MSAJILI HAZINA AELEZA WALIVYOFANIKIWA KUONGEZA KIWANGO CHA MAKUSANYO YA MAPATI YASIYO YA KODI

$
0
0
Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka akitoa hotuba yake katika hafla ya kupokea Gawio la Serikali iliyofanyika, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma leo. Picha na Othman Michuzi.

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii 

MSAJILI wa Hazina Athumani Mbuttuka amesema kwa sasa wanajivunia kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka katika kampuni, taasisi, na mashirika ya umma yanayotokana na gawio, michango ya asilimia 15, na mapato ya Taasisi na Mashirika ya Umma, marejesho ya mtaji uliozidi, na ziada ya mwisho wa mwaka.

Mafanikio hayo yametokana na utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa mwaka 2018 wakati wa mashirika, taasisi na kampuni mbalimbali zikitoa gawio kwa Serikali. 
Mbuttuka amesema hayo leo Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma wakati wa Taasisi, Mashirika na Kampuni mbalimbali zikabidhi gawio kwa Serikali ambapo hundi hizo zimepokelewa na Rais Dk.Magufuli.

Amefafanua kuwa hundi ambazo zimepokelewa zinajumuisha Mapato ya Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 31 mwaka 2019 na kwamba katika kipindi cha miaka mitano, makusanyo ya mapato kutokana na uwekezaji kwenye mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa yameongezeka  kufikia Sh.trilioni 1.05 mwaka 2018/19 kutoka Sh.bilioni 161.04 mwaka 2014/15, ikiwa ni ongezeko la asilimia 552.
Ameongeza katika makusanyo hayo, Sh. bilioni 683.23 ya makusanyo yote kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2019 yalipitia katika Akaunti ya Msajili wa Hazina na Sh.bilioni 370.59 ziliwasilishwa moja kwa moja kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kutoka Michango ya Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bodi ya Michezo ya Kubashiri, Mamlaka ya Anga Tanzania; na Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Petroli Tanzania.

Amesema kuwa mapato hayo yanatokana na gawio, michango ya asilimia 15 na huduma za jamii. ongezeko hili la mapato limechangiwa na maelekezo yako thabiti kwa Mashirika na Taasisi za Umma katika kuimarisha makusanyo na kupunguza matumizi yasiyo na tija; ukusanyaji wa maduhuli kwa mfumo wa kieletroniki [GePG],
Aidha, Udhibiti wa Matumizi; na kuongeza usimamizi wa Mashirika ya Umma na Makampuni yanayomilikiwa kwa hisa chache na Serikali. Masuala mengine ni ufuatiliaji wa kina na mapitio ya mikataba ya wanahisa, mikataba ya kimenejimenti na mikataba ya misaada ya utaalamu katika makampuni yanayomilikiwa kwa hisa chache na Serikali.

Pia, ufuatiliaji wa matumizi kwa Mashirika na Taasisi za Umma, mapitio ya sera za gawio, kutoa miongozo kwa bodi za wakurugenzi, kupitia mipango-mkakati na mipango ya biashara, na kuingia mikataba ya utendaji na Bodi za Wakurugenzi za Mashirika ya Umma.

Amesema kuwa ulipaji wa gawio umeimarika zaidi kwenye mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa zaidi ya asilimia 50 ambapo rejesho la mtaji limeendelea kukua kutoka asilimia 1.5 mwaka 2014/15 hadi asilimia 7.21 mwaka 2018/19 ikilinganishwa na kampuni zinazomiliki hisa chini ya asilimia 50, ambapo rejesho la mtaji limeongezeka kutoka asilimia 5.3 mwaka 2014/15 hadi asilimia 6.64 mwaka 2018/19. Hali hii inaonesha ufanisi katika Mashirika ya Umma una imarika.

"Idadi ya Kampuni na Mashirika yanayotoa gawio na kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali ni ndogo ikilinganishwa na idadi iliyopo na ukubwa wa sekta. Kampuni na Mashirika 40 kati ya 81 yaliyopaswa kutoa gawio yameshindwa kutokana na kujiendesha kwa hasara au kuwa na mtaji mdogo,"amesema.

Amebainisha kazi ya kurekebisha Mashirika na Makampuni wanayoyasimamia inaendelea. Hadi kufikia mwezi Juni 2019, mashirika 15 yaliunganishwa na kuwa mashirika 6 na shirika moja lilitenganishwa na kuwa mashirika mawili.
Ameongeza lengo kubwa la kuunganisha au kutenganisha mashirika hayo ni kuipunguzia Serikali gharama na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Wakati huo huo, amesema kwamba Ofisi ya Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na ESRF inaendelea kufanya tathmini ya kina kwa mashirika yote ya biashara kwa lengo la kubaini hatua stahiki za kuchukua ili kuboresha utendaji wake kwa ujumla.

Pia amesema Wizara ya Fedha na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) zinaratibu zoezi la uhakiki wa mali za umma nchi nzima ambapo mpaka kufikia Juni 30, 2019 idadi ya mali 531 zilikuwa zimetambuliwa na kurejeshwa kwenye mikoa 10 iliyopitiwa.

Amesema kati ya mali zilizorejeshwa kuna majengo (337), viwanja (140), mashamba (10), maghala (41) na mali zingine (3). Aidha, katika mali zilizobainika kuna kampuni mbili Songwe Water Company Limited na Liquid Storage Company Ltd ambazo Serikali inamiliki kwa asilimia 100 na 40 mtawalia na zoezi hili bado linaendelea.
Vilevile, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2019 OMH ilikuwa imerejesha viwanda 31 vilivyothibitika kutofanya kazi na taratibu za kisheria zinaendelea katika hatua mbalimbali.

Amesema wazi kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina inakabiliwa na changamoto ambazo zikipata ufumbuzi inaweza kuboresha zaidi ukusanyaji wa mapato. Kuhusu changamoto amesema kuwa mojawapo ni mfumo hafifu wa TEHAMA wa utoaji taarifa na ufuatiliaji, changamoto za Sheria ya Msajili wa Hazina, ongezeko la mahitaji ya watumishi wenye utaalamu na uzoefu wa kazi, na kukosekana kwa Mfuko wa Fedha za Uwekezaji.

BENKI YA CRDB YAKABIDHI GAWIO LA SHILINGI BILIONI 7.2 KWA RAIS DKT. MAGUFULI

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio kwa Serikali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. Wengine pichani ni Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa fedha Dkt. Philip Mpango.

Na Kilo Mgaya, Dodoma.

Benki ya CRDB imekabidhi gawio la shilingi bilioni 7.2 kwa Serikali baada ya kupata matokeo mazuri ya kifedha katika mwaka wa fedha unaoishia Desemba 2018. Gawio hilo limekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea gawio na michango kwa Serikali iliyofanyika Ikulu, Chamwino Dodoma, Rais Magufuli amepongeza mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa na manufaa kwa Watanzania kupitia gawio linalotokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali.
"Taasisi nyengine zijifunze kutoka kwenu, tunahitaji kuona Watanzania wananufaika na uwekezaji wao kwani fedha hizi ndio tunakwenda kujenga reli, barara pamoja na ujenzi wa hospitali na vituo vya afya, nawapongeza sana," alisema Rais Magufuli.

Wachambuzi wa masuala ya fedha wanatazamia Benki ya CRDB kutoa gawio kubwa zaidi mwakani kwa Wanahisa wake ikiwamo Serikali baada ya kupata matokeo mazuri zaidi mwaka huu 2019 ambapo katika matokeo ya fedha ya nusu ya tatu ya mwaka benki hiyo iliripoti faida ya jumla ya shilingi bilioni 92.16 ukilinganisha na shilingi bilioni 52.25 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema matokeo mazuri ya kifedha ambayo benki hiyo imeyapata mwaka huu yanatokana na maboresho na uwekezaji katika mifumo ya kidijitali uliolenga kuongeza urahisi kwa wateja kupata huduma popote walipo jambo lililosaidia kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja.

"Tumehakikisha tunaboresha njia zetu mbadala za utoaji huduma kama SimBanking, SimAccount, Internet Banking, CRDB Wakala, Mashine za manunuzi (PoS), pamoja na kuunganisha mifumo yetu na mfumo wa malipo wa Serikali GePG, hii imerahisisha wateja kujihudumia wenyewe kwa kufanya miamala pale walipo," alisema Nsekela.

Nsekela alisema huduma hizo za kidijitali za Benki ya CRDB zimesaidia sana kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki nchini hususani vijijini. “Sasa hivi tuna CRDB Wakala zaidi ya 15,000 ambao wamesambaa nchi nzima,” aliongezea Nsekela.

Serikali imewekeza ndani ya Benki ya CRDB kupitia mfuko wa ushirikiano na Serikali ya Denmark (DANIDA), Mifuko ya uhifadhi wa jamii ya PSSSF, NSSF, ZSSF na GEPF, Mfuko wa Bima ya afya (NHIF), Mfuko wa Maendeleo wa Lindi, Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakifurahi jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako, wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakifurahi jambo na Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akizungumza na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichele, wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange, wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay. 
Afisa Mkuu Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshakanabo akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa, wakati  wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. 



SEKTA ISIYO RASMI KUONGEZEWA TIJA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali zote mbili (Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) zinatambua mchango wa sekta isiyo rasmi, hivyo zimekuwa zikifanya juhudi mbalimbali kuendeleza na kuongeza tija katika sekta hiyo. 

Amesema katika kuhakikisha sekta hiyo inaendelea, Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara kwa wajasiriamali wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuendelea kuwapatia vyeti vya uasili ambavyo vimetoa unafuu mkubwa wa kodi na tozo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 24, 2019)wakati akifunga Maonesho ya Wajasiriamali wa Tanzania kusherehekea miaka 20 ya uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Fumba, Zanzibar.

Amesema wanapohitimisha maonesho hayo sambamba na kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatakiwa wajitathmini kuona kama wametimiza malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo. 

“Vilevile, tuendeleze ujirani mwema, kupanua na kuimarisha ushirikiano wa watu wa Afrika Mashariki ili kuharakisha ukuaji wa kiuchumi sanjari na kuboresha maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki kiuchumi, kisiasa na kijamii.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuzungumzia kuhusu vikwazo visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha wajasiriamali kufanya biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo amesema vimeendelea kutatuliwa kupitia majadiliano baina ya Tanzania na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo kwa lengo la kuvipunguza na kuviondoa kabisa.

Waziri Mkuu amesema kupitia majadiliano hayo, Serikali imefanikiwa kuratibu zoezi la uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyo vya kiforodha 15kati ya 24vilivyoripotiwamwaka 2019 navikwazo tisa vilivyobakiahatua ya kuvipatia ufumbuzi inaendelea.

Hata hivyo,Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutekeleza mkakati wa kutoa elimu kwa umma ili kuhakikisha wajasiriamali wanachangamkia fursa za kibiashara zitokanazo na Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Waziri Mkuu amesema mkakati huo unahusisha zoezi la kufanya utafiti wa uelewa wa Watanzania kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki na matokeo ya utafiti huo yatatumika katika kutoa elimu kwa umma kulingana na mahitaji.

Katika kutatua changamoto ya mitaji kwa wajasiriamali, Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 ya kuweka mfumo wa kuvitambua, kuvisajili na kuviwezesha vikundi vyenye mwelekeo wa ushirika na ujasiriamali. 

Amesema miongoni mwa hatua zinazochukuliwa ni kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa taasisi za fedha na mifuko mbalimbali ya umma na binafsi kutoa mikopo kwa wajasiliamali kwa riba nafuu na ikiwezekana isiyo na riba.

“Katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Juni, 2019 mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 42.06 kwa vikundi11,487 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ilitolewa. Vilevile, mikopo hiyo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri imeendelea kuzingatia uwiano wa asilimia nne kwa vikundi vya wanawake, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu.” 

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inahamasisha uundwaji wa vikundi vya wajasiriamali, kusimamia utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi hivyo sambamba na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali na wawekezaji wengine kufanya shughuli zao bila bughudha.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeanzisha mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa lengo la kutoa mitaji na huduma nyingine za kifedha zenye masharti nafuu kwa wananchi wa Unguja na Pemba. Mfuko huu umelenga wananchi wenye kipato kidogo ili waweze kuzalisha mali kwa kujiajiri na kupunguza umaskini.

Amesema hadi kufikia Juni 2019 kupitia mfuko huo mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 3.5 ilikuwa imetolewa na kuzifikia jumla ya Shehia 346. “Mfuko huu kupitia mradi wa mbogamboga na matunda umetoa mikopo 263 kwa wakulima wa mbogamboga na matunda 384 wa Pemba yenye thamani ya sh. milioni 60.6 na wakulima 384 wa Unguja yenye thamani ya sh. milioni 151.3.

Amesema Serikali imeendelea kufanya maonesho mbalimbali ya Wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Maonesho hayo yametoa fursa kwa wajasiriamali kupata ujuzi, taarifa za masoko, teknolojia, mbinu na taratibu mbalimbali za kufanya biashara ili kukuza shughuli zao. 

Maonesho hayo yamewapatia wajasiriamali uthubutu wa kushiriki wao binafsi katika maonesho mengine kwenye nchi za Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Sudan Kusini, Msumbiji na Marekani. Pia wameweza kufanya ziara katika nchi ya China ambako walijifunza na kununua mashine za kisasa kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa bidhaa zao ili ziweze kushindana katika soko la ndani na nje.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika mwani, wakati akifafanuliwa jambo na Naibu Mkurugenzi Mkuu TAN TRADE, Latifa Khamis, kwenye Maonesho ya Wajasiriamali, katika Kusherehekea Miaka 20 ya Uanzishwaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaliyofungwa rasmi Novemba 24, 2019, kwenye viwanja vya Fumba Zanzibar.

Uchaguzi wa serikali za mitaa wafanyika kwa amani Morogoro

$
0
0

Na, farida Saidy, Morogoro
Zoezi la kupiga kura kuchagua wenyeviti wa Vijiji, Mitaa, na Vitongoji limefanyika kwa Amani Mkoani Morogoro ambapo Halmashauri sita kati ya tisa zimeshiriki katika zoezi hilo lililofanyika Nchini kote Novemba 24, 2019 huku zaidi ya wakazi laki moja Mkoani humo wakitajwa kushiriki zoezi hilo.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoani Morogoro Jacob Kayange wakati akitoa taarifa za awali kuhusu mwenendo wa zoezi hilo Mkoani humo.

Kayange amebainisha kuwa Halmashauri zilizoshiriki katika zoezi hilo ni pamoja na Halmashauri ya Mji Ifakara, Kilombero, Ulanga, Morogoro, Kilosa na Manispaa ya Morogoro huku Halmashauri ya wilaya Gairo, Mvomero na Malinyi hazikushiriki uchaguzi huo kwa sababu ya wagombea wake kupita bila kupingwa baada wagombea wengine kukosa sifa za kushiriki uchaguzi huo.

“Mkoa wetu wa Morogoro ni miongoni mwa Mikoa inayoshiriki zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa linalofanyika leo Novemba 24 mwaka huu, na katika Mkoa wetu Halmashauri sita kati ya tisa ndizo zitakazoshiriki katika zoezi la kupiga kura na Halmashauri tatu hazitoshiriki …..”, alisema Kayange.

Kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro pamoja na vituo vingi kukutwa havina wapiga kura kwa madai kuwa wagombea katika maeneo hayo wamepita bila kupingwa bado maeneo hayo ya kupigia kura vilionekana kuwa katika hali ya Amani na Utulivu.

Mitaa iliyotembelewa wakati wa zoezi la kupiga kura ni pamoja na kata ya Mbuyuni katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambayo ina Mitaa sita, ambapo mitaa mitano kati ya hiyo wagombea wake wa Kutoka Chama cha Mapinduzi CCM walipita bila kupingwa huku Mtaa mmoja wa Magulumbasi kuripotiwa kuwa na mpinzania kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichukua fomu lakini alikosa sifa baada ya kujaza fomu hiyo.

Issa Juma ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Mgonahanzeru chini ya mgombea Kerene Jackson Huzi amesema ana imani kwamba mgombea wao anafaa kutetea kiti hicho kwa kuwa amekuwa karibu katika kusaidia kero mbalimbali za wananchi katika kipindi chote alichokuwa madarakani.

Naye mgombea Nafasi ya Uenyekiti wa mtaa wa Mgonahanzeru Kerene Jackson Huzi ambaye amepita bila kupingwa amewasihi wagombea wenzake waliopita bila kupingwa kujitahidi kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.

Kwa mujibu wa Mratibu wa zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro Bw. Jacob Kayange , jumla ya Watu waliojiandikisha kupiga kura katika Mkoa huo ni 1,101,588 sawa na asilimia 79 ya wakazi wake. Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa na wasimamizi wa Uchaguzi huo baadae hii leo.

EAC LAUNCHES CITIZENS’ ENGAGEMENT CAMPAIGN AS PART OF ITS 20TH ANNIVERSARY CELEBRATIONS

$
0
0
 The East African Community has launched a Citizens Engagement Campaign as part of its 20th Anniversary celebrations.

The campaign dubbed as ‘The EAC I Deserve’ seeks to reach more than 10 million East Africans over the next one year.

The campaign will, among other things, include social media interfaces and a regional Youth Videos and Animations Competition involving all the six EAC Partner States. A total prize of US$25,000 awaits the innovative 30 youthful winners in the competition.

Launching the campaign at the EAC Headquarters, EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko said that the whole idea behind the maiden video and animations drive was to enable the youth in the region to capture real stories about the benefits the Community has had on citizens’ lives, narrate the challenges citizens are facing that can be jointly addressed and to gauge the citizens’ aspirations of the EAC they want.

“Demographics dictate that the youth must actively engage in the integration process, for the bloc is yours and the EAC Vision 2050 is your future. Much as the youth account for over 65% of East Africa’s total population, capturing and incorporating your dreams and aspirations in the integration agenda through video and animations is imperative,” said Amb. Mfumukeko.

The SG said that the campaign also intends to encourage constructive and innovative coverage of the EAC integration process in the print, electronic and online media to provide ordinary East Africans, potential investors and tourists with insights on the existence of the bloc and opportunities in store for them.

“The objective is to motivate individual journalists and their media houses to take up regional issues as their key area of interest and as their specialised writing genre,” said the SG.

The SG outlined the many achievements of the Community since its establishment 20 years ago notably the various policy initiatives, new infrastructure, regional industrialisation, healthcare approaches, increased intra-EAC trade, and the Common Higher Education area.

He, however, observed that the region still needs to do more in all sectors to realise the many and varied aspirations of its 170 million citizens.

“As we celebrate what we have achieved so far, we wish to hear stories from every East African on the impact the EAC has made to his or her life and the future he or she wants the region to be. We at the EAC Secretariat are keen on capturing dreams and aspirations of every citizen of the region during and after this celebration through the Citizen’s Engagement Campaign we are launching today.

“This campaign will enable you citizens, particularly the online community, to use the digital space as your platform for engaging us at the EAC Secretariat, Partner States, the East African Legislative Assembly, the East African Court of Justice and all institutions of the bloc.
 A section of the youth who attended the launch of the EAC Citizens’ Engagement Campaign at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.
 EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko addresses participants before he officially launched the ‘EAC I Deserve Campaign’ at the EAC Headquarters in Arusha. 
EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (centre), Director of Trade Alhaji Rashid Kibowa (in grey suit), and participants hold campaign booklets shortly after the launch outside the EAC Headquarters.


21ST ORDINARY MEETING OF THE SUMMIT OF THE EAC HEADS OF STATE POSTPONED

$
0
0

EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko addressing a media briefing at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania shortly before he unveiled the EAC 20th Anniversary Logo. With him is the Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote.
The Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote, gestures as he addressed journalists in Arusha. On the left is EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko.
EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (right) and the DSG in charge of Planning and Infrastructure shortly after the SG unveiled the EAC 20th Anniversary Logo at the EAC Headquarters in Arusha.
East African Legislative Assembly MP Hon. Eng. Mnyaa Mohamed Habib is assisted by a nurse from the Mt Meru Hospital in donating blood at the EAC Headquarters in Arusha. The blood donation drive was organised by the EAC as part of activities to mark its 20th Anniversary.

East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 20th November, 2019The 21st Ordinary Meeting of the EAC Heads of State Summit initially scheduled for Saturday, 30th November, 2019 has been postponed to a later date in either January or February next year.

EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko said Wednesday that the 21st Summit was postponed after a request by one of the Members of the Summit, adding that the postponement had nothing to do with a dispute or disagreement among any of the EAC Partner States.

Amb. Mfumukeko said that a new date for the 21st Summit meeting would be communicated later after consultations among the EAC Heads of State.

Amb. Mfumukeko, however, said that the 39th Meeting of the Council of Ministers slated for 21st to 27th November, 2019 would proceed as initially planned.

The Secretary General was addressing a media briefing at the EAC Headquarters where he among other things launched a Blood Donation Drive and unveiled the EAC 20th Anniversary Logo as part of activities to commemorate the Community’s two decades of existence.

The blood donation drive, which drew participation from EAC Staff and Members of Parliament from the East African Legislative Assembly, and was organized in collaboration with the Mt. Meru Hospital, Arusha, is part of the Community’s initiative to give back to the society by saving lives.

The Secretary General said that the overall objective of the EAC 20th Anniversary celebrations was to commemorate the achievements of the Community over the past 20 years.

“The celebrations are a joint undertaking by all EAC Organs, Institutions and Partner States’ Ministries responsible for EAC Affairs. The theme of the 20th Anniversary is EAC@20: Deepening Integration, Widening Cooperation,” he said.

Amb. Mfumukeko observed that the Community had expanded in the last 20 years, growing from the original three Partner States in 1999 to six today, with the Federal Republic of Somalia and the Democratic Republic of Congo having made applications to join the bloc.

He said the desire by other countries to join the six-member bloc was due to the achievements made by the Community over the years that have made it more attractive for investment and in the process raised the living standards of the people of East Africa.

On the Customs Union, the Secretary General said that the intra-EAC trade had increased from US$2.7 billion in 2016 to US$2.9 billion in 2017 and to US$3.3 billion in 2018.

“The increase in intra-regional trade can be attributed to the resolution of multiple Non-Tariff Barriers to trade by the Partner States and the establishment and operationalization of 13 One-Stop Border Posts to facilitate the cross-border movement of persons and goods,” he said.

“The implementation of the EAC Single Customs Territory has, for instance, resulted in drastic reduction in the period taken to clear goods from over 20 days to three (3) days on the Central Corridor and from 21 days to four (4) days on the Northern Corridor,” he added.

Under the Common Market, the Secretary General singled out the abolition of visa fees for EAC nationals traveling within the region, the ongoing issuance of the new internationally recognised East African e-Passport by all the Partner States except the Republic of South Sudan and the ongoing harmonisation of mobile calling and data charges within the region as some of the achievements of the Community.

“Various professional associations in the region have also signed Mutual Recognition Agreements (MRAs) to ease cross border movement of professionals within the region,” said Amb. Mfumukeko.

He noted that infrastructure development remains a priority for the EAC Heads of State as evidenced by their biennial retreats on infrastructure development and financing.

He disclosed that the Community had negotiated a total of US$2.5 billion from the African Development Bank for development projects to be implemented by the Partner States with US$1.6 billion earmarked for various regional infrastructure development projects, namely: road and railway transport connectivity, energy infrastructure and ICT connectivity.

“A total of US$271 million was set aside for the construction of the multinational 301 km Nyakanazi-Kasulu-Manyovu road in Tanzania and the 78 km Rumonge-Rutunga-Bujumbura road in Burundi,” said Amb. Mfumukeko.

“For Tanzania and Kenya, the Malindi-Mombasa-Lunga Lunga-Tanga-Bagamoyo road will be constructed at the cost of US$585 million,” he added.

On the East African Monetary Union, Amb. Mfumukeko disclosed that EAC Partner States were in the process of harmonizing critical policies and establishing the necessary institutions to ensure the realisation of a single currency for the entire region by the year 2024.

“Plans are at an advanced stage to put in place the East African Statistics Bureau, one of the four institutions required to make the Monetary Union a reality,” said Amb. Mfumukeko, adding that recruitment was already underway for staff who will run the Bureau.

On progress towards the East African Political Federation, the fourth and ultimate stage in the integration process, the Secretary General revealed that a team of 18 Constitutional Experts and Legislative Draftsmen had already been tasked with drafting a Constitution for the Political Confederation, a transitional model to the Political Federation.

“President Yoweri Museveni of Uganda on Monday, 18th November, 2019 launched the National Stakeholder Consultations for Drafting the Constitution of the Confederation,” he said, adding that the constitution-making process would be as consultative as possible with no Partner State being forced into the Confederation against their will.

He said that the envisaged Federation would boost the region’s profile politically, economically and militarily thereby guaranteeing national security of all the Partner States besides enabling them to negotiate better deals on the proceeds from exploitation of their natural resources versus the more developed countries

KIJIJI KUHAMISHWA KUPISHA ATHARI ZA MAAFA YA MAFURIKO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Kasongwa akipokea msaada kwa ajili ya waathirika wa maafa wilayani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, msaada huo umetolewa na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mapangoni kilichopo Kata ya Kerenge wakishirikiana na wanajeshi kushusha baadhi ya vitu vya msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akipokea msaada kwa ajili ya waathirika wa maafa mkoani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, msaada huo umetolewa na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wilayani Korogwe wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Kasongwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe hawapo pichani wakati walipopeleka misaada kwa waathirika wa maafa ya mafuriko kutoka Ofisi ya waziri Mkuu, Mfuko wa maafa
************************************

Kamati ya menejineti ya Maafa wilayani Korogwe imeelekezwa kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wananchi wa kijiji hicho chenye kaya zaidi ya 250 ambazo ziliridhia kuhama kijiji hicho baada ya baadhi ya nyumba zao kuvunjwa na mawe makubwa yanayoporomoka na maji kutoka milimani na mmomonyoko wa ardhi uliozingirwa na mifereji ya maji, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa takriban siku 40 mfululizo kijijini hapo.

Akiongea mara baada ya kukagua shughuli za urejeshaji wa hali na kabla ya kukabidhi misaada kutoka Mfuko wa Maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shuhghuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amesema katika menejimenti ya maafa hatua za urejeshaji hali baada ya maafa zinazingatia urejeshaji ulio bora zaidi kuliko wa awali hivyo kwa kuwa kijiji hicho kipo eneo hatarishi wananchi hawanabudi kuishi eneo salama kwa afya zao na mali zao.

“Kwa kuwa utabiri wa hali ya hewa unaonesha mvua za juu ya wastani zitaendelea kunyesha hadi mwanzoni mwa mwakani, niitake Kamati ya maafa ya wilaya kuhakikisha taratibu za kupima maeneo salama kwa wakazi wa kijiji hiki zinakamilika kabla ya mwak huu kuisha ili wakazi wa kijiji hiki waendelee kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa Taifa” amesisitiza Kanali Matamwe.

Kanali Matamwe ameeleza kuwa kwakuwa serikali imeamua kukihamisha kijiji hicho ili wananchi hao waweze kuishi maeneo salama na wameanza kuwasaidia wananchi hao kupitia Mfuko wa maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, amewataka wadau wengine kuendelea kuwasaidia wananchi hao ili waweze kukamilisha ujenzi wa nyumba bora na salama katika eneo litakalo ainishwa na serikali.

Ofisi ya Waziri Mkuu , Kupitia Mfuko wa Maafa imeikabidhi Kamati ya Menejienti ya Maafa ya Wilaya hiyo misaada kwa kaya zilizoathirika na maafa ya wa mafuriko Wilayani humo ikiwa ni pamoja na magodoro100, bati 200,mikeka 200,blangeti 200,ndoo 200, sleeping bag 100 vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,
Kissa Kasongwa aliishukuru ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu wa maafa kwakuona umuhimu wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo Wilayani humona kwamba mahitaji hayo yemewafikia walengwa kwa wakati muafaka.

“Tumekuwa tukifanya jitihada mbalimbali za kurejesha hali na sasa tayari Kamati ya maafa ya wilaya tumeshaainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 150 kwa ajili ya kuanzisha kijiji kipya, lakini nimefuatilia nimeona bado Halmashauri haijaenda kupima eneo hilo, nimemuelekeza mkurugenzi jumatatu hii aende kwenye wnwo hilo nw upimaji uanze mara moja na zoezi hili likamilike ” alisistiza Kasongwa

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava alimshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, kazi, ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ambaye ana dhamana ya kuratibu maafa nchini kwa kumsikiliza baada ya kuwasilisha matatizo ya wananchi wake na hatimaye kuwatuma wasaisdizi wake kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo ambapo maombi ya wananchi hao yametekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

Kwa nyakati tofauti wakazi wa kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge, Aliamini Mrutu na Asha Hizza wameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa misaada waliyowapatia na kubainisha kuwa wako tayari kuhamia katika kijiji kipya kitakacho anzishwa na serikali kwa kuwa wanapoishi sasa maisha yao yako hatarini kw akuwa tayari kaya 63 nyumba zao zimeathirika huku kaya 38 hazina mahala pa kuishi.

Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika.
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images