Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

DOKTA MPANGO AIOMBA AfDB KUJENGA BARABARA NJIA NNE MOROGORO HADI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Cheptoo Amos Kipronoh (hayupo pichani) kuweka katika vipaumbele vya Benki hiyo kwa Tanzania kuhusu ujenzi wa Barabara ya Morogoro Dodoma yenye upana wa njia nne, kulia ni Kamishna Msaidizi wa Bajeti Bw. Emmanuel Tutuba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Cheptoo Amos Kipronoh, akieleza nia ya Benki yake ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato Jijini Dodoma, wakati wa Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Amos Cheptoo, baada ya mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Amos Cheptoo, (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo na Benki ya AfDB , Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Amos Cheptoo, wakiwa katika Mkutano Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)


Na Benny Mwaipaja, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika kuipatia Tanzania mkopo nafuu kwa ajii ya kujenga barabara ya njia Nne kuanzia Morogoro hadi Dodoma ili kuboresha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo


Dkt. Mpango ametoa ombi hili Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo anayewakilisha nchi nane za ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Amos Cheptoo.

“Barabara hii ilijengwa muda mrefu miaka ya 80, malori mengi yanapita hapa kwenda Mwanza, Kigoma na nje ya nchi ikiwemo Burundi, Rwanda, na unaona kabisa imeelemewa na imeanza kuharibika” Alisema Dkt. Mpango

Alisema amemwomba Mkurugenzi Mtendaji huyo wa AfDB waanze kuliweka jambo hili kwenye miradi itakayogharimiwa na Benki hiyo baadae ili barabara hiyo itakayo kuwa na uwezo wa kuelekeza magari mawili kwenda upande mmoja na mengine mawili kupita upande mwingine iweze kujengwa.

“Baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi, tunahitaji usafirishaji kwa njia ya barabara uwe na tija zaidi, uende haraka zaidi lakini pia kupunguza ajali. Hivi sasa kuna ajali nyingi sana kwa sababu magari yanayokwenda Dar es Salaam na yanayokuja Dodoma au kwenda Mwanza yanapishana kwenye haka kanjia kamoja” alisisitiza Dkt. Mpango

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Amos Cheptoo aliyeko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, alisema Benki yake itahakikisha Tanzania inapata mikopo ya miradi yake ya kimkakati na ya kipaumbele ukiwemo huo wa barabara ya Morogoro hadi Dodoma.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Cheptoo Amos Kipronoh, ameitaka Sekta Binafsi nchini Tanzania kuchangamkia fursa za mikopo nafuu zilizopo katika Benki hiyo.

Bw. Kipronoh alisema kuwa Sekta Binafsi nchini Tanzania ina nafasi nzuri ya kupata mikopo na utaalam utakaoiwezesha kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kutokomeza umasikini katika Bara la Afrika.

“Sekta Binafsi hapa Tanzania haijatumia vizuri dirisha la mikopo ya Sekta hiyo ikilinganishwa nan chi nyingine za ukanda huu wa Afrika na ninakuomba Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango uihamasishe Sekta Binafsi ikope fedha hizo ili kukuza mitaji yao na kuongeza tija” alisema Bw. Cheptoo

Aidha, alisema kuwa Benki ya AfDB ipo katika hatua za mwisho za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Dodoma na tayari benki hiyo imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko mjini Dodoma pamoja na miradi mipya ya kuzalisha Nishati ya umeme ambayo iko mbioni kuwasilishwa katika vikao vya Bodi ya Benki hiyo hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo amempongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwa kiongozi mwenye maono ambaye amesaidia katika mabadiliko makubwa ya uchumi na kuzitaka nchi nyingine barani Afrika kujifunza kutoka Tanzania.

“Nilipotua nimeona jengo la abiria la III katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, daraja la juu la Mfugale na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea kwa kasi, miundombinu ambayo miaka miwili iliyopita sikuikuta nilipotembelea hapa nchini” alisema Bw. Cheptoo.

Aidha, amempongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kwa kusimamia na kuhakikisha uchumi unaendelea kuwa imara ikiwa ni moja ya lengo la Benki hiyo katika jitihada za kuifanya Afrika kuwa na uchumi imara.

Kwa upande Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amewataka watanzania kujivunia hatua za maendeleo zinazoonekana kwa kuwa hata wageni wanaona mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini.

Ameishukuru Benki ya AfDB kwa kukubali kufadhili miradi ya barabara za mzunguko Jijini Dodoma na pia miradi mbalimbali ya kilimo ambayo inaajiri watu wengi, huku akibainisha kuwa kwa kipindi cha miaka minne miradi mbalimbali imetekelezwa kwa msaada wa AfDB na kuifanya Tanzania kukua kwa kasi kiuchumi.

Dkt. Mpango amewataka watendaji wa Wizara yake kuhakikisha wanawakutanisha viongozi wa Sekta Binafsi na Watendaji hao wa AfDB kabla ya kumaliza ziara yao nchini, ili kufanya mazungumzo yatakayosaidia kutumia fursa zilizopo katika Benki hiyo.

Aidha, Dkt. Mpango amewataka watanzania wenye vigezo kuchangamkia nafasi mbalimbali za kazi zinazotangazwa katika Benki hiyo ili kuongeza uwakilishi wa wananchi hasa kutoka Afrika Mashariki, ikizingatiwa nafasi zinazotangazwa ni za ushindani.

Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB imefadhili miradi 23 hapa nchini ikiwemo miradi 21 ya umma na miwili ya Sekta Binafsi, katika Nyanja za Nishati, miundombinu ya barabara, usafiri, kilimo, maji na usafi wa mazingira, yote kwa pamoja ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 2 nuta 1

HATMA YA KUFUTIWA AU KUTOFUTIWA DHAMANA KWA WABUNGE WANNE WA CHADEMA KUJULIKANA KESHO MAHAKAMANI KISUTU, WENYEWE WAJITETEA

$
0
0
KESHO KUTOA UAMUZI WA KUFUTA AU KUTOFUTA DHAMANA 

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jami.


MAHAKAMA ya ya Hakimu Mkazi Kisutu kesho Novemba 20, mwaka 2019  inatarajia kutoa uamuzi wa kufuta au kutofuta dhamana ya  wabunge wanne wa Chadema  baada ya kukiuka masharti ya dhamana.

Wabunge hao ni Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa,  Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya ambao wamefika mahakamani hapo leo wakitokea katika kituo cha polisi  Osterbay jijini Dar es Salaam baada ya kujisalimisha kutokana na amri ya Mahakama ya kuamuru wakamatwe.

Hatua hiyo ya Mahakama imekuja bàada ya washtakiwa hao wote wanne kutoa sababu zao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba zilizowafanya kushindwa kufika mahakamani hapo Novemba 15, saa tatu asubuhi kama Mahakama ilivyokuwa imepanga.

Wakitoa sababu kwa nini wasifutiwe dhamana, washtakiwa Heche, Msigwa na Mdee waliieleza Mahakama kuwa siku hiyo ya kesi walifika mahakamani hapo kwa kuchelewa kutokana na sababu mbali mbali.

Mshtakiwa  Msigwa na Heche walidai kuwa walipata ajali wakiwa njiani kufika mahakamani hapo huku Mdee yeye alidai aliugua ghafla akiwa njiani na kumlazimu kupitia Hospitali kitendo kilichopelekea wote kufika mahakamani kwa kuchelewa.

Kwa upande wake, mshtakiwa Ester Bulaya alidai kuwa  hakufika  mahakamani siku hiyo kwa kuwa alifiwa na mama yake Mdogo hivyo alikwenda Singida kwa ajili ya Maziko.

"Wakati kesi inaendelea siku ya mwisho nilijaribu kunyoosha mkono lakini haukuniona Hakimu,  mimi ni Mjumbe wa kamati ya Bunge ambapo baada ya kesi, nilikimbia  kwenda Dodoma alhamisi kwenye kikao ambacho kiliisha saa moja na nusu usiku niliondoka saa mbili na nusu usiku na kuingia Dar es Salaam saa mbili asubuhi. Kwenye akili yangu nilijua kesi ni saa nne na nusu hivyo sikuwa na wasiwasi kama nitachelewa lakini wakati nikiwa njiani kuja mahakamani nikiwa na Heche, tulipata ajali", amesema Msigwa.

"Mheshimiwa ninaheshimu Mahakama na siwezi kuidharau mahakama wala wewe binafsi,
Naomba Mahakama isinifutie dhamana yangu," alisema Msigwa.

Kwa upande wake Mdee ameiomba Mahakama isimfutie dhamana yake kwani anaiheshimu sana mahakamai ila siku hiyo wakati anakuja mahakamani aliugua ghafla akapitia Hosp lakini kwa kihofia kuchelewa alimpigia mdhamini wake ambae nae alifika kwa kuchelewa.

"Mimi ninakaa karibu kilometa 1600 kutoka hapa, hapa mjini sina familia wala mke, ila tangia kianza kwa kesi hii sijawahi kuchelewa mahakamani wala kuonywa, ila siku ya kesi tukiwa njianj na Msigwa, gari iligongwa, ikabidi tutafute pa kuiweka na kisha tukachukua boda boda lakini tulipofika mahakamani tukakutana na wenzetu ndio wanatoka" amesema Heche.

Wakati  Bulaya amesema, hawezi kuidharau mahakama, ila alifikwa na msiba wa mama yake mdogo huko Singida, hivyo aliwataarifu wadhamini wake ili siku ya kesi wafike, lakini nao walipofika walikuwa wamechelewa na kukuta kesi imeahirishwa.

Hata hivyo upande wa mashtaka kupitia wakili wa Serikali Salimu Msemo akiwasilisha hoja ya kutaka washtakiwa wafutiwe dhamana amedai, ni muhimu suala muda wa kuwepo mahakamani kuzingatiwa na ni dhahiri kuwa washtakiwa hawakuwepo mahakamani wakati kesi hiyo inaahirishwa.

Hivyo ninaiomba mahakama iwafutie dhamana washtakiwa hao wanne na kuwachukulia hatia stahiki wadhamini wao.Akijibu hoja hizo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala amedai, hakuna sababu za kimazingira wala kisheria za kufuta dhamana, uamuzi wa kutoa dhamana ni mwepesi zaidi kuliko uamuzi wa kuifuta.

Hakuna ubishi kwamba wakati wa kesi hii washtakiwa walikuwa na rekodi bzuri ya kuhudhuria mahakamani na kwamba washtakiwa walitoa maelezo siku hiyo walikuja mahakamani.

Ni kweli kwamba kawaida kesi za jinai zinaanza saa tatu asubuhi lakini tangu waanze shauri hili awajawahi kuanza muda huo bali wamekuwa wakianza saa 4:30 asubuhi na kuendelea na kuongeza kuwa kuchelewa mahakamani sio na kutofika.

Mahakama sio mashine kwakuwa zipo sababu za kibinadamu na ndio maana kuna mahakimu au majaji wanaofanya maamuzi na kutafsiri sheria.

Wabunge watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya wabunge wa 4 wa chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni,  Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko.

Katika Kesi hiyo Mbowe na wenzake wanakabiliwa na  mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

Pia, wanadaiwa kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo watuhumiwa hao wanne wamepelekwa mahabusu hadi kesho uamuzi utakapotolewa.

Hata hivyo, pia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu anaumwa na amelazwa katika Hospitali ya Aghakhan chumba 507. Taarifa ya kuumwa kwa Mbowe, imetolewa mahakamani hapo na Mdhamini wake, Grayson Selestine.






BILIONI 18 ZIMETUMIKA MIRADI YA “CSR” MKOANI GEITA

$
0
0


Waziri wa Madini Doto Biteko akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la Zahanati ya Gereza Geita ikiwa ni sehemu ya miradi ya CSR mkoani Geita
Waziri wa Madini akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakielekea kukagua shuguli mbalimbali zinatekelezwa ikiwa ni sehemu ya miradi ya CSR kutoka mgodi wa GGM.
Askari Magereza akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Madini Doto Biteko kwa utaratibu wa kijeshi kwa ajili ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo la Zahanati ya Gereza Geita akiambatana na viongozi mbalimbali. Kulia kwake ni mkuu wa Mkoa Geita Mha. Robert Gabriel mwenye kofia ya CCM ni Mbunge wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu.

………………….

Na Issa Mtuwa – “WM” Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema anaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii (Corporate Social Responsibility – CSR) inayotekelezwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita – GGM ikiwa na madhumuni ya kuifanya jamii inayo zunguka mgodi huo kufaidika kutokana na uwepo wa raslimali hiyo.

“Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Yapo mambo bado sikubaliani nao hasa kwenye masuala ya Local Content hususani ajira, mishahara ya watanzania na huduma na manunuzi bado sijaridhishwa. Lakini kuhusu CSR niseme ukweli GGM wanafanya vizuri sana”. Alisema Biteko wakati akiweka jiwe la msingi la jengo la Zahanati ya Magereza Geita miongoni mwa miradi ya CSR Geita mjini.

Biteko alisema GGM wamejenga, zahanati kadhaa ikiwemo hiyo ya Magereza Geita, vyumba vya madarasa, barabara za lami, taa za barabarani, ujenzi wa soko kubwa la wamachinga geita, soko kuu la dhahabu na mirandi mingine, vyote hivyo ni miradi ya CSR inayotekelezwa na fedha za GGM.

“Hii ndio namna ya kuweka alama hata kwa vizazi vijayo kuyafanya madini kuishi na hata madini na mgodi wa GGMM kufungwa. GGM wameshatumia fedha nyingi za CSR zaid ya bilioni 18 kwa ajili ya miradi katika maeneo yetu ya Geita. Fedha hizi nyingi sana huko nyuma kabla ya serikali ya awamu ya tano hazijawahi kutolewa na huko nyuma mgodi ulikuwa unapanga nini cha kufanya lakini leo miradi hii inayotekelezwa inatokana na mipango na vipau mbele vya Halmashauri zenyewe na kumbwa utekelezaji wake unashiriki serikali zetu za mitaa”. Alisema Biteko.

Ameongeza kuwa, zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi la Zahanati hiyo ya Magereza tarehe 18/11/2019 ni moja ya kielelezo hicho na amefurahi kusikia ujenzi huo unaendelea na utakamilika bila kukwama. .

“Naomba nitumie fursa hii, kuwakumbusha wenye leseni za uchimbaji madini kote nchini watambue CSR ipo kwa mujibu wa sheria na kila mwenye leseni popote alipo ana wajibu wa kuchangia maendeleo ya jamii kwenye eneo la leseni ilipo, sio suala la migodi mikubwa pekee,” aliongeza Biteko.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo, mkuu wa Gereza Geita, SSP. Mussa Mkisi alimwambia mgeni rasmi Waziri wa Madini Doto Biteko kuwa ujenzi huo unaendelea vizuri na jumla Tshs. milioni 50,000,000/- zimetengwa kutoka mfuko wa CSR –Geita mjini kukamilisha ujenzi huo. Aliongeza kuwa hadi kukamilika kwake, ujenzi huo utakamilika kwa gharama ya jumla ya Tshs. milioni 170,000,000/- na Zahanati hiyo ya kisasa itakuwa inatumiwa na wafungwa, mahabusu na jamii nzima inayozunguka Zahanati hiyo.

Kwa upande wa mgodi wa GGM kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa mgodi, Richard Jordanson amesema wanaona fahari kutekeleza miradi inayo walenga wananchi wote moja kwa moja kwani miradi hiyo inakuwa ni kielelezo na kwamba wataendelea kutekeza miradi mbalimbali kwa kuzingatia miongozo ya utekelezaji wake.

Jordanson ameongeza kuwa mgodi wa GGM utaendelea kushirikiana na serikali huku akimuahidi Waziri wa Madini kumshangaza kwa maajabu atakayoyafanya kuhusu utekelezaji wa Local content katika mwaka ujao.

Wakati huo huo Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa kiasi cha Tsh. Milioni 1,500,000/- kwa ajili ununuzi wa mchele, Ng’ombe na Vinywaji baridi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wa gereza hilo kwa siku hiyo. Ametoa fedha hiyo alipotembea Gerezani hapo na kuzungumza nao, huku akiwatia moyo kwamba wasivunjike moyo na kwamba mungu anampenda kila mtu na siku moja watarudi uraiani.

Nae Mbunge wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amewafariji kwa kuwaambia wasikate tama na kwamba hata walioko nje ni wafungwa au mahabusu watarajiwa huku akibainisha kuwa hata yeye aliwahi kukaa mahabusu siku tano baada ya yeye na wenzake kufanya fujo na vurugu wakiwa shuleni lakini leo maisha yanaendelea.

KERO YA MIAKA 59 YA MAJI KITUO CHA AFYA NASSA YATATULIWA

$
0
0
Mkazi wa Kijiji ha Bukabile, Specioza Mahondola akitwishwa ndoo ya maji na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera baada ya kupokea mradi kisima cha maji uliojengwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TDCF).Kushoto anayehushudima ni mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee.


NA BALTAZAR MASHAKA, BUSEGA

TAASISI ya The Desk & Chair Foundation imetumia sh.milioni 20 kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka 59 ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha Bukabile na Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu.

Kisima hicho kirefu cha maji kitatumiwa na wananchi wa kijiji hicho, wakiwemo wajawazito, wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa kwenye kituo hicho cha afya huku taasisi hiyo ikitoa sh. 800,000 kugharamia vitambulisho vya wazee 800 vitakavyowatambulisha kupata matibabu.

Mwenyekiti wa TDFC, Sibtain Meghjee, akikabidhi mradi huo kwa serikali, alisema kisima hicho kirefu cha maji kimegharimu sh. milioni 20 na kimefungiwa pampu ya kusukuma maji inayotumia nguvu ya umeme jua na hivyo kukiwezesha kituo cha Afya Nassa na wananchi kupata maji ya uhakika muda wote.

“Tumeridhishwa na mfumo wa mitambo iliyofungwa kisimani hapo kuwa inasukuma maji vizuri hadi kituoni baada ya majribio kufanyika.Kwa niaba ya wafadhili na uongozi wa The Desk & Cair Foundation, tunaikabidhi serikali mradi huu, hatutakuwa na mamlaka nao isipokuwa kwa matengenezo ya mitambo itakapoharibika,”alisema.

Meghjee alisema taasisi hiyo imetekeleza miradi mbalimbali ya kijamii mkoani Simiyu ikiwa ni pamoja na kuboresha visima vifupi 11 vya maji na kuchimba vipya 12, kufunga mitambo ya umeme jua kwenye Kituo cha Afya Nassa, mradi wa maji safi na salama Lamadi, baiskeli 5 kwa walemavu wa viungo na moja ya kawaida.

Mingine ni mradi wa nyumba 10 za nyasi vijijini kufungiwa mfumo wa umeme jua,vyoo kwenye shule ya Malayele,vibebeo 300 kwa wajasiriamali na vitambulisho vya afya kwa wazee 800 huku miradi kama hiyo ikifanyika pia kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati.

“Naishukuru serikali kwa kutoa vibali na ushirikiano wa dhatiwakati tunapotekeleza shughuli zetu kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya nchi,kama ilivyo kauli mbiu yetu ya Tupo pamoja Iwe Dhiki Iwe Faraja:Huduma kwa Jamii Bila Kuchagua Bila Kubagua,”alisema Meghjee.

Aidha, baadhi ya akinamama wa Kijiji cha Bukabile ambao ni wanufaika wa mradi huo, Nadhifa Yusuf, Specioza Mahondola naWinfrida Masalu,walisema utainufaisha jamii na umewakomboa na adha ya kufuata maji umbali mrefu,ambapo wakati wa kujifungua walipata shida ya kwenda na maji .

Walieleza kuwa wameteseka miaka mingi kufuata maji umbali wa km 4 kutokana na kijiji hicho kuwa mbali na Ziwa Victoria, walikuwa wakinunua maji sh.1000 kwa ndoo tano ama kuyateka kwenye madimbwi hivyo kwa sasa wataweza kushiriki shughuli za uzalishaji na maendeleo.

Kwa upande wa vitambulisho vya bima kwa wazee, mmoja wa wanufaika hao Kitula Kubangwa (71) aliishukuru The Desk & Chair Foundation kuwaondolea changamoto ya vitambulisho vya matibabu na kuishauri serikali iendelee kuwatizama kwa jicho la huruma.

Akipokea mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Busega,Tano Mwera, alisema The Desk & Chair Foundation ni wadau wakubwa wa maendeleo kutokana na misaada yao kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma mbalimbali kwa jamii.

Alisema mradi huo wa maji utabadilisha maisha ya wananchi na wagonjwa wanaotibiwa kwenye kituo cha afya Nassa kwani lengo la serikali ni kumtua mwanamke ndoo ya maji kichwani.

“Maji ni muhimu, mradi huu unaunga mkono juhudi za serikali za kuhudumia wananchi na kuwaletea maendeleo lakini pia sasa watayapata maji karibu na akinamama watatumia muda wao mwingi kufanya shughuli za maendeleo,”alisema Mwera. 

Awali Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nassa, Fred Mruma, alisema changamoto ya maji tangu kujengwa kwa kituo hicho mwaka 1960 imekwisha ingawa bado wana tatizo la nishati ya umeme kwenye chumba cha upasuaji, mashine ya kufua nguo za wagonjwa na mashine ya kupima damu (Full Blood picture machine).

BUNGE LA VIJANA LAANZA HII LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu katika Bunge la sita la Vijana Tanzania kwa mwaka 2019 Ndg. Alvin Maro akifafanua jambo kwenye kikao cha Bunge hilo lililozinduliwa rasmi hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la sita la Vijana Tanzania kwa mwaka 2019 Ndg. Ramadhan Singa akiendesha kikao cha Bunge hilo lililozinduliwa rasmi hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la sita la Vijana Tanzania kwa mwaka 2019 wakiwa katika Mjadala wa Bunge hilo lililozinduliwa rasmi hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Bunge/.

Dk.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE WA CCM WILAYA KASKAZINI A UNGUJA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Hutuba yake wakati alipokuwa akizungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini(A) (hawapo pichani) katika Ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni leo (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Saadala(Mabodi)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Hutuba yake wakati alipokuwa akizungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini(A) katika Ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni leo
Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini (A) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa Hutuba yake kwa Wazee hao wakati wa mkutano katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni leo
Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini (A) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa Hutuba yake kwa Wazee hao wakati wa mkutano katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni leo
Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini (A) wakiitikia dua iliyoombwa baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuimarisha Chama uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Mafunzi ya Amali Mkokotoni leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini(A)baada ya kumalizika kwa mkutano alioufanya leo na Wazee hao akiwa katika Ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Unguja, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Saadala(Mabodi) pamoja na Viongozi wengine wa Chama alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa kuimarisha Chama na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini (A) Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Nd,Laila Burhan Ngozi pamoja na Viongozi wengine wa Chama alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa kuimarisha Chama na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini (A) Mkoa wa Kaskazini Unguja leo

Vodacom yakutanisha Wadau kujadili ustawi wa huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi Afrika

$
0
0
Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd, Epimack Mbeteni akizungumza kwenye kongamano hilo 
Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Albert Cesari (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (wa kwanza kulia), Mtendaji mkuu, Sheria na Udhibiti kutoka Vodacom Group, Judith Obholzer (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Rosalynn Mworia wakati wa kongamano na uzinduzi wa ripoti kuhusu kuhakikisha ukuaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia (kulia) na Mtendaji mkuu, Sheria na Udhibiti kutoka Vodacom Group, Judith Obholzer (katikati) wakizungumza na mdau wa huduma za kifedha aliyehudhuria kongamano hilo.

*************************************

Novemba 19, 2019, Dar es Salaam. Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 8 Afrika wanakutana leo katika kongamano maalumu lililoandaliwa na Vodacom kujadili mwenendo na maendeleo kwaajili ya kuboresha sekta ya huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi Afrika. Kampuni hiyo inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano pia imetoa ripoti yake ya kuhakikisha ukuaji wa Huduma za Kifedha kupitia simu za mkononi katika kongamano hilo.

Ripoti hiyo ambayo ni ya kwanza ya Mwendelezo wa Sera ya Umma kwa Vodacom, inafafanua jinsi ambayo huduma ya pesa kwa simu ya mkononi inayoendesha ukuaji wa uchumi na kuinua kiwango
cha maisha kupitia huduma ya kifedha.

Mkurugenzi Mtendaji, Sheria na Udhibiti wa Vodacom Group, Judith Obholzer, alisema Nchi za Afrika zilizoko Kusini Mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania zimeshuhudia ukuaji wa haraka katika huduma za pesa kupitia simu ya mkononi, sambamba na uvumbuzi na kuwezesha ushiriki mpana wa utoaji wa huduma za kifedha.

Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kinara ambapo watu wazima wengi wanamiliki akaunti za simu ya mkononi kuliko zile za taasisi za kifedha. Mabadiliko haya katika ukanda huo yanazidi kuendesha kukua kwa uchumi na faida za kijamii kwa kutoa huduma za kifedha kwa mamilioni ya watu wanaomiliki simu ya mkononi, lakini pia wakiwa umiliki mdogo sana wa akauti za benki.

“Lengo letu ni kutoa jukwaa kwa wataalamu wa sekta hii kutoa maoni yao jinsi ya kuboresha sekta.Sekta hii inaendelea kukua kwa kasi, watunga sera pamoja na wasimamizi wana jukumu la kuweka mazingira ya biashara hii ya kifedha,” alisema Obholzer.

Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni Meneja Msaidizi katika idara ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bwana Albert Cesari alieleza umuhimu wa huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni za simu katika utowaji wa fursa pamoja na ajira na ukuwaji wa uchumi.

“ Serikali imeweka mazingira bora na endelevu kuhakikisha huduma za kifedha zinaendelea kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi ikiwemo ajira na mabadiliko katika mfumo wa ulipiaji huduma nchini. Kanuni za malipo ya simu kupitia simu ya mkononi hutolewa ili kuongoza soko bila kuzuia ubunifu au kukwaza mafanikio ambayo yanaletwa na wavumbuzi hawa.”

M-Pesa imekuwa moja ya huduma bora zaidi ya pesa ya simu ya mkononi barani Afrika. Tafiti zinaonesha kwamba huduma ya pesa kupitia simu ya mkononi imechangia kwa kiasi kikubwa katika uwezeshaji wa jamii, kukua kwa uchumi na kupunguza umasikini.

Inatoa huduma kwa njia salama, Uhakika na ya bei nafuu kwa kutuma na kupokea pesa, kuongeza muda wa maongezi, kufanya malipo ya bili, kupokea mishahara na kupata mkopo wa muda mfupi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utafiti mpya juu ya matumizi ya huduma ya pesa kupitia simu ya mkononi Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, alisema “ Huduma ya pesa kwa simu ya mkononi imeongezwa nguvu matumizi ya simu ya mkononi, imeonekana kuwa kama jukwaa la kutoa fursa kiuchumi na kubadlisha mazingira ya huduma za kifedha na hasa katikabara la Africa,”

Hendi aliongeza kusema kuwa, “Nimefurahi kwamba ripoti hii inaleta pamoja michango ya wataalam wanaoongoza na ndio wazungumzaji katika mada hizi tatu pana. Wana maoni na mitizamo tofauti, ili kuleta msukumo wenye tija na wa kujenga.”

Hafla hiyo iliwashirikisha wawakilishi kutoka kwa waendeshaji wa mitandao ya simu wakiwamo wadau wa mawasiliano, watoa huduma za kifedha, benki, Asasi za Kiraia na washiriki wengine walioshiriki kuchangia mada mbalimbali kama vile; Uthibitisho wa baadaye wa Uwepo wa Huduma za Kifedha za simu ya Mkononi, Mfumo wa Ushirikiano, Mfumo wa Malipo, Ushirikiano wa kikanda
na fursa za mipaka, Jinsi ya kutatua matatizo ya kisheria, Tabia ya kupeana mawazo na fursa za ushindani.

SIKU YA PILI YA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA VYUO NA TAASISI ZA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike (kushoto) akizungumza katika siku ya pili ya kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilichofanyika mkoani Morogoro.

Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Mawasiliano Bw. Mulengwa Munaku akitoa mada kuhusu ubunifu na Teknkolojia katika siku ya pili ya kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilichofanyika mkoani Morogoro.


Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George akitoa mada kuhusu ushiriki wa vyuo vya Maendelo ya Jamii katika kutatua changamoto za jamii inayovizunguka katika siku ya pili ya kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilichofanyika mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawalana Rasilimali Watu kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Marko Masaya (wa pili kushoto) akizungumzia masuala ya kiutawala katika siku ya pili ya kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilichofanyika mkoani Morogoro.

GIZA LATIBUA MCHEZO BALANG’DALALU

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Mathew Darema akikagua timu ya soka ya City Boys kabla ya mpambano na timu ya Young Boys kwenye uwanja wa shule ya sekondari Balang’dalalu.

Mwenyekiti wa CCM Wilayani Hanang’ Mathew Darema akikagua timu ya Young Boys.

………………………….
Mshindi wa tamasha la michezo Kata ya Balang’dalalu Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, ameshindwa kupatikana baada ya City Boys na Young Boys kufungana mabao 10-10 na kumalizika kutokana na giza.

Tamasha hilo liliandaliwa na Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa CCM (UVCCM) kata ya Balang’dalalu, Emmanuel Gamasa lilifikia fainali jana na litarudiwa leo kwenye uwanja wa shule ya sekondari Balang’dalalu, baada ya bingwa kutopatikana. 

Katika fainali hiyo hadi dakika 90 za mchezo huo zilipomalizika timu hizo za zilikuwa hazija fungana hivyo kulazimika kupigiana penalti tano kwa kila timu. 

Wachezaji wa timu hizo walipigiana penalti tano kwa tano na kila moja wakakosa mabao mawili hivyo kuendelea kupiga wakiwemo magolikipa na kufungana mabao 10 -10 hadi giza likaingia na kuhitimisha mpambano huo. 

Mgeni rasmi wa mpambano huo, Mathew Darema alizipongeza timu hizo na kuzipatia sh100,000 ili zigawane 50,000 kila moja baada ya kutopatikana mshindi. 

“Fainali inabidi irudiwe kesho kwani giza limesababisha tukose uhondo nawazawadia sh100,000 kwa mchezo mzuri mgawane pia nitarudi kuona mchezo mwingine tupate bingwa” alisema Darema. 

Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Balang’dalalu, Emmanuel Gamasa alisema tamasha hilo limekuwa na mafanikio makubwa kutikana na hamasa kubwa ya jamii ya eneo hilo. 

Gamasa alisema imedhihirika kuwa michezo ni furaha, amani na upendo ndiyo sababu watu wengi wamejitokeza kushuhudia pambano hilo.

STEPS WARUDI KWA KISHINDO NA FILAMU YA KASHINDE

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi TV

KAMPUNI ya kusamabaza filamu nchini  Steps Entertainment imeahidi kuziba pengo lililoachwa kwa muda mrefu katika soko la filamu.

Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa DVD wa filamu ya kashinde Meneja kutoka Kampuni hiyo Kambarage Ignatius amesema wasanii na wadau wa filamu walikua wanapata tabu kusambaza kazi zao lakini kwa Sasa muafaka umepatikana .

"Hapo awali Kampuni ya steps ilikua ikisambaza kazi za filamu lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo ilibidi isimame kwa muda ili kurekebisha baadhi ya vitu,"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza filamu (LUGWA COMPANY) Luckyness mokiwa amesema ni wakati wa wadau, wasanii na waandaaji wa filamu kujinua upya kutokana na kurudi kwa wasambazaji hao .

"Ni kishindo kikubwa ambacho wamefanya Kampuni ya steps na wameanza na kusambaza kazi yangu mpya ya filamu ya kashinde ambayo nilizindua mwaka huu,"

Hata hivyo Mokiwa amesema anatarajia kufanya uuzaji wa mfumo wa DVD wa filamu ya kashinde desemba 29 mwaka huu katika ukumbi wa uliopo kibaha.

Ndani ya filamu hiyo wapo wasanii kama gabo,patcho Mwamba,frola Mvungi,husna sajenti na wengine wengi huku maudhui ya filamu hiyo ikimuelezea msichana kashinde ambae ni kondakta wa daladala ambae anafanya jitihada zote ili aweze kujikwamua kimaisha.

"Lengo la kuuza filamu hiyo kibaha ni kutokana na sehemu nyingi za mandhari katika filamu hiyo imefanyika kibaha hivyo tumeona sio vibaya tukafanya shughuli ya kuuza filamu hiyo huko huko ili kuonyesha kuwa wapenzi na wadau wasanaa pia wanapatikana sehemu mbalimbali sio Dar es salaam peke yake tu japo ndio jiji la starehe,"
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lugwa Luckyness Mokiwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uuzwaji wa filamu ya kashinde kwa mfumo wa DVD ambapo Kampuni ya usambazaji wa kazi za filamu (steps entertainment) itakua ndio kazi ya kwanza kusambaza baada ya kurudi kwa kishindo

Halmashauri ya Tandahimba yapokea wakimbizi 165 kutoka Msumbiji

$
0
0
Halmashauri ya Tandahimba imepokea wakimbizi 165 ambao wameingia Wilayani humo kwa madai ya kukimbia machafuko yanayoendelea nchini kwao.

Akizungumza Jana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Said Msomoka alieleza kuwa  wakimbizi hao wameingia kwa kupitia Mto Ruvuma hivyo halmashauri imewahifadhi katika Kijiji Cha Lipalwe B

"Tumewatoa kule bondeni tumewaleta hapa kijijini na tumewaandalia sehemu kwa ajili ya malazi na vile vile tumewaletea chakula ," alisema Msomoka

Naye Mkaguzi  Msazidizi wa Uhamiaji Raymond Mapunda alieleza kuwa Kati ya idadi hiyo wanaume 37,wanawake 47,watoto wa kiume 33 ,watoto wa kike 28 na hivyo kufikia idadi ya 143 ,22 ni idadi ya raia wa Tanzania ambao nao walikuwa wakiishi huko 

"Kabla ya kuwapokea wanakaguliwa ili kujiridhisha ili kuepuka kuwapokea wengine ambao huenda wakawa waharifu,lakini hata hivyo wanachi wafuate utaratibu wanapotaka kwenda nchi hiyo jirani kwa kufika katika ofisi za Uhamiaji Wilaya,"alisema Mapunda
 
Wakimbizi raia wa Msumbiji
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Wilaya ya Tandahimba Raymond Mapunda 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka

WAZIRI KIGWANGALLA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA USHAURI WA UFUGAJI NYUKI NCHINI NA KUGAWA MIZINGA YA KISASA 1000 MKOANI TABORA.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akigawa jumla mizinga ya kisasa 1000 kwa Chuo cha Mafuzo ya Ufugaji Nyuki Tabora na Jumuiya ya Wafugaji wa Nyuki wa Ipole WMA mkoani Tabora.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiweka nta maalum inayotumika kuwavutia nyuki kuingia kwenye kwenye mizinga ya kisasa ya maoksi pale inapotudikwa wakati akigawa jumla mizinga ya kisasa 1000 kwa Chuo cha Mafuzo ya Ufugaji Nyuki Tabora na Jumuiya ya Wafugaji wa Nyuki wa Ipole WMA mkoani Tabora.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watedaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wajume wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Ufugaji Nyuki nchini iliyoziduliwa .

Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu ufugaji wa nyuki wadogo na mazao yake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji wa Nyuki Bw. Daniel Charles Pancras alipotembelea na kukagua kituo cha Utafiti na Mafunzo cha kuzalisha nyuki wadogo katika Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora.

Picha/ Aron Msigwa – WMU.

Uturiki kuwekeza ujenzi wa viwanda vyenye thamani ya dola milioni 50 Simiyu

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka (katika) akiwa na mwekezaji kutoka Uturuki,Bw. Mustafa Albayram (mwenye shati jeusi) pamoja na maafisa wa serikali pamoja nabaadhi ya wafanyakazi wakitembea ndani ya kiwanda cha kuchambua pamba chaAlliance Ginnery Ltd mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akioneshwa pamba inavyochambuliwa na mwekezaji kutoka Uturuki, Bw. Mustafa Albayram (mwenye shati jeusi).

********************************

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

Katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania nchini Uturukiumeambatana na wawekezaji kutoka nchini humo kwa ajili ya kuwekeza katikaviwanda mkoani Simiyu ambavyo vinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 2000.

Uwekezaji huo utajumuisha kiwanda cha nguo pamoja na kiwanda cha kutengeneza vyombo vya majumbani ambao una thamani ya dola za kimarekani milioni 50. Viwanda hivyo vitajengwa katika eneo la Isanga Mjini Bariadi Mkoani Simiyu na vinatarajiwa kuanza uzalishaji mwaka 2020.

Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo ambalo linatarajiwa kujengwa viwanda hivyo mkoani Simiyu, mwekezaji huyo kutoka Uturuki, Bw. Mustafa Albayram ameahidi kujenga viwanda viwili kimojawapo kikiwa ni cha nguo na kingine cha kutengeneza vyombo vya nyumbani ikiwemo vikombe, sahani na glasi.

Bw. Albayram amesema ameridhishwa na mazingira ya uwekezaji baada ya
kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kuangalia mazingira wezeshi kwauwekezaji wa viwanda, akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo mkoani Simiyu.

Aidha ameitaka serikali kutatua baadhi ya changamoto ili kuuwezesha uwekezaji huo kufanyika ikiwa ni pamoja na miundombinu yote muhimu hususani ya umeme ili uwekezaji huo uanze mara moja baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu zinazohitajika ikiwa ni pamoja na usajili wa kampuni na kutafuta hati miliki ya ardhi.

“Tumeamua kuwekeza Simiyu, kila kitu kikienda sawa kiwanda cha nguo kinaweza kujengwa na kufanya kazi ndani ya miezi tisa mpaka mwaka mmoja, kiwanda cha vyombo vya nyumbani miezi nane baada ya usajili wa kampuni nitarudi tena Simiyu kukamilisha masuala ya hati miliki ya ardhi, sitaki kumuangusha Mhe. Balozi maana amefanya mengi kwa ajili yetu,” alisema Albayram.

Nae Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo amesema mwekezaji ameridhishwa na eneo hilo na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kutoa ardhiya kujenga viwanda hivyo huku akibainisha kuwa ombi kubwa la mwekezaji niupatikanaji wa nishati ya kutosha kwa kuwa viwanda hivyo hutumia umeme mwingi.

Balozi Kiondo ameongeza kuwa, hayo ni matokeo ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa vitendo, hivyo Ubalozi utaedelea kuhamasisha wawekezaji wengine zaidi kuja kuweza nchini, hatimaye kufanikisha azma ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alimhakikishia mwekezaji huyo upatikanaji wa mahitaji yote muhimu na kuahidi kushirikiana na taasisi za Serikali zinazohusika kuhakikisha anapata huduma zote kwa wakati na pasipo urasimu wowote.

Kuhusu suala la Umeme Mtaka amesema katika Bajeti ya mwaka 2019/20 Wizara ya Nishati kupitia Shirika la umeme TANESCO imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupozea umeme (substation) ambacho kitajengwa karibu na eneo la uwekezaji huo.

Mtaka ameongeza kuwa mtazamo wa mkoa wa Simiyu ni kuwa na viwanda vichache vitakavyoajiri maelfu ya watanzania badala ya kuwa na viwanda vingi vinavyoajiri watu wachache ili kuwezesha watanzania wengi kupata ajira.

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa wakulima wa pamba kulima pamba kwa wingi kwa kuwa kiwanda cha nguo kitakuwa mkombozi wa kuongeza thamani ya zao la pamba na itauzwa kwa bei ya uhakika.

Naye Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema kujengwa kwa kiwanda cha nguo mkoani Simiyu kutasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika kuondoa changamoto ya bei ya pamba kwa kuwa kitapanua wigo wa soko la pamba, ambapo pamba inayotumika ni chini ya asilimia 20 – 25 ya pamba yote inayozalishwa nchini.

Katika tukio jingine kampuni ya Kawasaki Heavy Industries Ltd kutoka Japanimeonesha nia ya kuanzisha kiwanda nchini ambapo kiwanda hicho kitahudumia soko la Afrika na Nje ya Afrika.

Kawasaki Heavy Industries Ltd ni kampuni nchini Japan ambapo imewekeza katika sekta mbalimbali kama vile sekta ya usafiri (anga, reli na majini) nishati (cogeneration, energy plants, gas tuibines, gas engines), vifaa vya viwandani (hydraulic components and systems, robotics, industrial plants, environmental and recycling), pamoja na leisure (motorcycle, off-road four wheel,JET SKI).

Naibu Meneja wa Idara ya Mkakati wa Kimataifa, Kitengo cha Biashara cha Kampuni ya Kawasaki Bw. Michio Kambe anatarajia kufanya ziara nchini Tanzania kuanzia tarehe 21 hadi 26 Novemba 2019 ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Waziri wa Viwanda na Biashara.

Bunge laahidi ushirikiano kwa tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai akiongea na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (hawapo pichani) walipotembelea ofisini kwake Wilayani Kongwa Novemba 19, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa , Deogratius Ndejembi.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa , Deogratius Ndejembi akiongea na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilayani humo pamoja na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora waliotembelea ofisini kwake Novemba 19, 2019.
Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiagana na Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kongwa ambayo inaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Deogratius Ndejembi (wa kwanza kulia anayewatazama)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akimtambulisha mmoja wa wananchi wanaishi Wilayani Kongwa aliyejitokeza katika ofisi hizo kuwasalimia viongozi wa tume.

******************************

Na Mbaraka Kambona,

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai ameihakikishia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuwa itaipatia kila aina ya ushirikiano itakayohitaji kutoka kwa taasisi ya Bunge.

Ndugai alieleza hayo mapema leo (Novemba, 19, 2019) alipokutana na Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu aliyemtembelea katika ofisi yake ya jimbo iliyopo Wilayani Kongwa jijini Dodoma.

Akiongea katika kikao hicho, Ndugai alimueleza Mwenyekiti kuwa tume ni taasisi muhimu katika kusimamia na kuhamasisha masuala ya haki za binadamu nchini.

“Tume ni taasisi muhimu ambayo imepewa dhamana ya kusimamia haki za binadamu nchini, nawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya japo mnachangamoto nyingi katika kutekeleza kazi zenu”, alisema Ndugai.

Ndugai aliendelea kueleza kuwa anatambua eneo ambalo tume inalifanyia kazi ni gumu kwa kuwa linahusiana na masuala ya usimamizi wa haki za watu, na kuwataka changamoto hizo zisiwakatishe tamaa,pale watakapokuwa na jambo lolote wasisite kuwasiliana na ofisi ya Bunge ili kushirikiana kuzitatua.

“Najua katika utekelezaji wa majukumu yenu mtakutana na changamoto nyingi hususani migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji naamini mtaisaidia serikali katika kuipunguza kama sio kuimaliza kabisa”aliongeza Ndugai.

“Naamini mtaenda kushughulikia pia migogoro ya wafugaji wanaokaa karibu na maeneo ya hifadhi, haiwezekani na haiingii akilini mifugo ikiingia katika hifadhi adhabu yake ni kunyang’anya mifugo yote ya mwananchi, nadhani hii sio sawa wala sio haki, nendeni mkayashughulikie haya”alisisitiza.

Aidha, Ndugai alimueleza Mwenyekiti wa tume kuwa wasisite kupeleka mapendekezo yoyote pale watakapoona kuna sheria ambazo wataona ni kandamizi waziwasilishe na kushirikiana na Bunge katika kuzirekebisha.

Naye Mwenyekiti wa tume , Jaji Mwaimu alimueleza Spika Ndugai kuwa dhamana waliyopewa na Mheshimiwa Rais John Magufuli ni kubwa na hivyo wanaahidi kuitendea haki kwa kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kutimiza ndoto ya nchi ya kufikia uchumi wa kati.

“Sisi kama viongozi wa tume, tunaunga mkono jitihada za serikali katika kukomboa wananchi kiuchumi, tunachokiomba kutoka kwenu na wadau ni ushirikiano kwani tukishirikiana kwa pamoja tutaweza kufanikisha jitihada hizo” alisema Jaji Mwaimu.

Mwenyekiti huyo wa Tume alikwenda kumtembelea Mheshimiwa Ndugai katika ofisi zake za jimbo Wilayani Kongwa jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha ikiwa ndio mara yake ya kwanza tangu alipoapishwa Novemba 4, 2019.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliongozana na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad, na Makamishna wengine watano ambao ni Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

WAZIRI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA AKIPANDA MITI KATIKA ENEO LA WIZARA HIYO

$
0
0
 
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akichagua miti kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika maeneo ya Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akijiandaa kupokea mti kabla ya kuupanda katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akimwagilia mti baada ya kuupanda katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.

Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) akirudishia udongo baada ya kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.


Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) akirudishia udongo baada ya kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo


Afisa Ugavi wa Wizara ya Katiba na Sheria Amani Goha akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Mh. Dkt Balozi A. Mahiga Waziri wa Wizara hiyo.


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari (HGCU) wa Wizara ya Katiba na Sheria Karimu Meshack akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo


Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria {kushoto} Prof. Sifuni Mchome akimsaidia Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Balozi A. Mahiga katika zoezi la upandaji mti eneo la Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo


Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria {wa kwanza} Prof. Sifuni Mchome akimuongoza Waziri wa Wizara hiyo kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya upandaji miti Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.


Mtumishi (Dereva) wa Wizara ya Katiba na Sheria Kassim Abdallah akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.


Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Philp Makenzi (kushoto) na Stephen Malimiru (kulia) wakipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini.


Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akiandaa shimo kabla ya kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.




Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akijiandaa kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.




EALA RESUMES SITTING IN ARUSHA

$
0
0
 
EAST AFRICAN LEGISLATIVE ASSEMBLY

 The East African Legislative Assembly (EALA) today resumed its 2nd Meeting of the 3rd Session in Arusha, Tanzania.  The three-week Session which runs until December 6th, 2019, commenced with Committee engagements prior to the actual Plenary Sitting.

Topping the agenda at the Sitting is the debate and enactment of the EAC Anti-Corruption Bill, 2019, that seeks among other things, at providing impetus in order to promote good governance, transparency and accountability in the EAC Organs and Institutions.

The object of the Bill is to promote integrity and ethical values within the Organs and Institutions of the Community; to strengthen the legal framework for preventing and combating corruption in the Community; to provide for co-operation by the national anti-corruption agencies in preventing and combating corruption and related matters.

The Bill further envisages that corruption and corrupt practices undermine the effective and efficient utilization of the resources available to the Organs and Institutions of the Community and derail the Community from deepening and widening integration. It is on this score that the Bill is been proposed to strengthen the legal framework for preventing and combating fraud and corruption within the Organs and Institutions of the EAC.

In February this year, the Chairperson of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution, Hon Victor Burikukiye, moved a motion under Rule 26 (1) and Rule 64 (9), seeking leave from the Assembly to introduce the Bill.

Hon. Burikukiye underlined Article 6 (d) of the Treaty for the Establishment of the East African Community which states that “the fundamental principles that shall govern the achievement of the objectives of the Community by the Partner States shall include: good governance, including adherence to the principles of democracy, the rule of law, accountability, transparency, social justice, equal opportunities, gender equality, as well as the recognition, promotion and protection of human and people’s rights in accordance with the provisions of the African Charter on Human and Peoples’ rights. 

Also on the agenda for consideration at this session, are a number of reports that emanate from workings of various Committees.  The report of the Committee on Legal Rules and Privileges on Compliance of Laws is set to be considered.  This follows activities of the Committee undertaken on October 9th -12th, 2019, in Kampala, Uganda, where the Committee held consultations with a host of institutions inter alia, the Inter-University Council for East Africa (IUCEA), the Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency (CASSOA), Lake Victoria Fisheries Organization (LVFO) and the East African Development Bank (EADB).

Similarly, to be presented to the House for debate, is a report of the Committee on Communication, Trade and Investments on the One Area Network  Within the health sector, as the region puts out all arsenal in containing the deadly EBOLA virus, the Assembly is to receive a report by the Committee on General Purpose on the oversight activity that sought to assess the level of preparedness of Partner States in management of EBOLA and Dengue Fever outbreaks.

The assessment took place in the Republics of Rwanda and Uganda and in the United Republic of Tanzania between September 12-16th, 2019.  The Committee on General Purpose, is also set to table its report on the EAC Annual Report 2016/17, which it reviewed recently.

Other significant issues at the forthcoming Plenary are key meetings with different stakeholders including participation at the East African Business Summit, organized by the East.

Mhe. Jenista Mhagama atembelea Nyumba za Shirika la Hifadhi za Taifa (NSSF), aamuru zikamilishwe ili Watanzania waanze kuzitumia

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama na Katibu Mkuu wa Wizara, Andrew Masawe wakitembelea miradi ya nyumba za Shirika la Hifadhi za Taifa (NSSF) zilizoko Kijichi jijini Dar es salaam na kuagiza kukamilishwa kwa miundombinu ya Nyumba zilizokamilika ili kuwezesha watanzania kuanza kuzitumia kwa makazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama akitoka kwenye moja ya nyumba za miradi ya nyumba za Shirika la Hifadhi za Taifa (NSSF) zilizoko Kijichi Wilayani Kigamboni  ambapo ameagiza kukamilishwa kwa miundombinu ya Nyumba zilizokamilika ili kuwezesha watanzania kuanza kuzitumia kwa makazi, Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Andrew Masawe na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Wiliam Erio.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama, akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa NSSF kuhusu gharama za ujenzi wa mradi wa Nyumba zilizoko kijichi Wilayani Kigamboni, Waziri ameagiza ameagiza  kukamilishwa kwa Miundombinu ya Nyumba zilizokamilika ili kuwezesha watanzania kuanza kuzitumia kwa makazi.

Mradi wa Nyumba wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) zilizoko kijichi Wilayani Kigamboni kama zinavoonekana kwenye picha, Nyumba hizo zimekamilika isipokuwa miundombinu yake, Waziri ameagiza ameagiza  kukamilishwa kwa Miundombinu ya Nyumba zilizokamilika ili kuwezesha watanzania kuanza kuzitumia kwa makazi.

Mradi wa Nyumba wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) zilizoko kijichi Wilayani Kigamboni kama zinavoonekana kwenye picha, Nyumba hizo zimekamilika isipokuwa miundombinu yake, Waziri ameagiza ameagiza  kukamilishwa kwa Miundombinu ya Nyumba zilizokamilika ili kuwezesha watanzania kuanza kuzitumia kwa makazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama, akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa NSSF kuhusu gharama za ujenzi wa mradi wa Nyumba zilizoko Ndungu  Wilayani Kigamboni, Waziri ameagiza ameagiza kukamilishwa kwa Miundombinu ya Nyumba zilizokamilika ili kuwezesha watanzania kuanza kuzitumia kwa makazi

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

Shabiki wa Simba asimulia alivyoshinda Mil 393 za M-Bet

$
0
0
Mkazi wa mkoa wa Iringa, Salvatory Kambaulaya amejishindia kitita cha Sh 393,200,750 baada ya kubashiri kiusahihi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-bet Tanzania.

Kambaulaya ambaye ni shabiki wa Simba na Manchester City alisema kuwa hakuwa na wasiwasi mara baada ya kupigiwa simu na Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa ni mshindi wa fedha hizo.

“Niliamini kuwa ni mshindi kwani mimi siyo mtu wa kwanza kushinda droo ya Perfect 12 ya M-Bet kutoka mkoa wa iringa, kuna mwanafunzi alishinda na kupatiwa fedha zake,

“Niamini M-Bet kwa kuwa na washindi wa uhakika katika michezo yao, ndiyo maana nilicheza ‘mikeka’ saba, mmoja nikipatia mechi tisa na mwingine mechi 12,” alisema Kambaulaya. Alisema kuwa kiasi cha fedha alichoshinda ni kikubwa sana na anatakiwa kutuliza akili ili kujua nini anafanya kwa upande wa maendeleo.

“Nimeshinda zawadi ya kwanza, lakini nimeumia sana na matokeo kati ya timu yangu, Manchester City ilipofungwa na Liverpool, niliweka Manchester kuwa ni washindi, hata hivyo alifungwa mchezo huo. Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa Kambaulaya ambaye ni afisa polisi mkoani Iringa ataweza kubadili maisha yake kupitia mchezo wao wa Perfect 12.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa ambao wamefaidika na msemu huo tokea kuanza kwa ubashiri. “Tumetoa washindi wengi mpaka sasa ambao wamejishindia mamilioni ya fedha na kuweza kubadili maisha yao ya kila siku,” alisema Mushi.
 Mshindi wa Sh milioni 393 wa mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Salvatory Kambaulaya ( wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania Allen Mushi (wa pili kushoto) mara baada ya kukabibidhiwa mfano wa hundi kwa kushinda kitita hicho cha fedha. Wengine katika picha ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubashiri na Kulia ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala. 

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 20,2019

TAIFA STARS YAPOTEZA MCHEZO WAKE DHIDI YA LIBYA UGENINI

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wake wa pili wa Kundi J dhidi ya Timu ya Taifa ya Libya kwa kipigo cha bao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Mustapha Ben Jannet nchini Tunisia.

Katika mchezo huo wakuwania kufuzu Michuano ya Mataifa barani Afrika yatakayofanyika mwakani nchini Cameroon, Stars ilianza kupata bao lake kupitia kwa Nahodha, Mbwana Samatta kwa mkwaju wa Penalti baada ya Mshambuliaji, Saimon Msuva kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha Pili, Libya wakionyesha kukata tamaa na matokeo baada ya kipindi cha pili kuanza, hata hivyo dakika ya 68 wenyeji wa mchezo huo, Libya walisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa Penalti kupitia kwa Sand Masoud baada ya Mwamuzi wa mchezo huo kudai Beki wa Stars, Bakari Mwamnyeto aliunawa mpira katika harakati za kuokoa mpira langoni.

Libya wakiwa nyumbani nchini Tunisia walionekana kupata hamasa katika dimba hilo wakianikizwa na mashabiki lukuki walifika uwanjani hapo, walipata bao la pili dakika za lala salama, dakika ya 81 kupitia kwa Mshambuliaji machachari, Anias Saltou baada ya gongana gongana ya hapa na pale katika lango la Stars.

Kwa matokeo hayo, Stars bado inabaki katika nafasi ya pili kwenye Kundi hilo J kwa alama zake 3, Kundi likiongozwa na Tunisia wenye alama 6 kibindoni baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea ya Ikweta katika mchezo uliopigwa nchini Guinea.

Katika michezo ya kwanza, Taifa Stars iliifunga Guinea ya Ikweta bao 2-1 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Tunisia wakipata ushindi wa bao 4-1 dhidi ya wageni Libya nchini Tunisia.

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images