Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

DC CHONGOLO AWAWEKA NDANI WAKANDARASI WA KAMPUNI YA CRJE KWA KUSHINDWA KUKAMILISHA MRADI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA KWA WAKATI.

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo amewashikilia wakandarasi wawili wenye asili ya china wa Kampuni ya CRJE kwa kushindwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande.

Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo leo mara baada ya kampuni hiyo kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati huku Mhandisi mshauri wa Manispaa Emanuel Tilya akisisitiza kuwa wamekuwa hawatoi ushirikiano wowote licha ya kwamba yupo kwenye eneo la mradi.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya leo ya kukagua miradi inayojengwa na Halmashauri hiyo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa kwa muda mrefu amekuwa akizungumza na mkandarasi huyo kuhusu kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa lakini hawakufanya hivyo.

Ameeleza kuwa halmashauri inahitaji kiwanda hicho haraka ili kiweze kutumiwa na wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo lakini mkandarasi aliyepewa kazi hiyo anawarudisha nyuma.

Ameeleza kuwa halmashauri imeshawalipa fedha kwa ajili ya ujenzi huo lakini kinachofanyika ni fedha hizo kuzipeleka kwenye miradi yao mingine jambo ambalo limefanya hadi sasa kusuasua kwa mradi.

“ Nimekuja hapa zaidi ya mara tatu, mara ya kwanza nilikuja nikaongea nao wakaniahidi watakamilisha kwa muda uliopangwa, mara ya pili nilikuja hapa nikafoka hadi nikakasirika lakini hali imeendelea hivi hivi, sasa sijawakamata nimewashikilia hadi pale watakapoleta mpango kazi wao uliojitosheleza.“ amesema Mhe. Chongolo.

”Hatuwezi kukaa na watu wa namna hii, tumetoa pesa nyingi, kwa ajili ya kukamilisha mradi huu mapema halafu wanatuchezea, ,kama wakileta leo, kesho nitawaachia, kadiri watakavyowahi kuniletea huo mpango kazi wao ndio na mimi nitawaachia, Askari kamata hao waweke ndani.

Askari huyo wa kituo cha polisi Mabwepande alitii agizo hilo na kuwapakiza kwenye gari kuelekea kituoni huku Mhe. Chongolo akiwafuata nyuma ili kuhakikisha kuwa wamefikishwa mahali husika.

Mhe. Chongolo alisisitiza kuwa hajaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa kiwanda hicho na kuagiza wasiachiwe hadi atakapotoa agizo ikiwa ni baada ya kutekeleza walichoambiwa.

Awali Mhandisi mshauri wa Manispaa, mhandisi Tilya ,amesema kuwa walikubaliana kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati lakini kilichotokea ni tofauti huku mafundi wanne tu ndio waliokuwa wanafika eneo hilo la mradi.

Alifafanua kuwa “ wakati mwingine huwa tunagombana wenyewe kwa wenyewe, kama angekuwa na uwezo wakufanya kazi kama msambazaji wake ingekuwa sawa, kwani anauwezo wakubeba kiubiki mita. 150 hadi kufikia saa 8.00 mchana, inamana tukifanya kazi usiku na mchana tunaweza kufikia kiubiki mita .300 kwa siku.

Alifafanua kuwa eneo la kiwanda hicho kinaukubwa wa mita zaidi ya 4070 ambapo hadi sasa tayari imeshafanyika kiubiki mita 491 sawa na asilimia 12 na kwamba iliaweze kufanikisha hanabudi ndani ya mwezi mmoja kwa usiku na mchana jambo ambalo alisema mkandarasi huyo hawezi kufanya.

Mhandisi huyo alifika mbali zaidi nakusema kuwa “ hakuna ushirikiano ambao anapata kutoka kwao , wanachoendelea kukifanya hapa ni kukudanganya mkuu. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akiwa sambamba na wakandarasi wa kampuni ya CRJE katika eneo la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa Mabwepande alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya ujenzi wake.
 Eneo la juu la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa ndani ya Manispaa ya Kinondoni katika kata ya Mabwepande.
 Mafundi wakiendelea na kazi katika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa Kata ya   Mabwepande katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Samweli Lyiza wakati wakikagua mradi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa katika Kata ya Mabwepande


Rais Magufuli ateua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TMA

WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA SADC KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA SEKTA YA KAZI NA AJIRA

0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wataalamu waliohudhuria mkutano wa SADC wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wajumbe wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane akieleza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe akizungumza wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (kushoto) kwenye meza kuu akisikiliza taarifa ya Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane (hayupo pichani). Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe, Mwakilishi wa Vyama vya Kibiashara vya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Bw. Michael Akuupa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Waajiri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt, Aggrey Mlimuka
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) waliohudhuria mkutano wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

……………….

Na; Mwandishi Wetu

Wataalamu wa Sekta ya Kazi na Ajira kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika wamedhamiria kuboresha na kuendeleza sekta ya kazi na ajira kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alipomwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa mkutano SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira na kueleza kuwa mkutano huo umewakutanisha kwa wataalamu wa nchi wanachama wa SADC kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha sekta ya kazi na ajira ikiwemo sera ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira.

“Mustakabali wa sekta ya kazi na ajira unategemea jinsi ambavyo tunashughulikia fursa na changamoto zitokanazo katika mazingira ya sekta hiyo, hivyo mada zitakazo jadiwa katika mkutano huu zitatoa mwelekeo kwa wajumbe kuona namna ya kuwa na sera rafiki za kazi na ajira,” alieleza Massawe

Alifafanua kuwa kulingana na taarifa ya mwenendo wa ajira ulimwenguni ya mwaka 2019 iliyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeelezea hali ya ajira inayoonesha zaidi ya watu milioni 170 hawana kazi ikiwa ni sawa na asailimia 5.1, na wafanyakazi bilioni 2 wapo katika ajira isiyo rasmi ikiwa ni sawa na asilimia 61.2.

“Ni matumaini yangu ajenda zitakazo jadiliwa zitatoa mwelekeo wa namna bora ya kutatua changamoto zilizopo sasa na mapendekezo yatakayotolewa na wataalamu kutoka nchi wanachana yatakuwa yanazingatia vipaumbele na malengo endelevu katika sekta ya kazi na ajira,” alisema Massawe

Sambamba na hayo alieleza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kutoa elimu ya sheria za kazi ili kuongeza uelewa kwa wananchi kufanya kazi zenye staha na kuboresha mazingira ya kazi.

Akitolea mfano Ofisi ya Waziri Mkuu inavyotekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa wanavyoshiriki katika kufanya kazi za staha kupitia mafunzo wanayopatiwa chini ya programu hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane alieleza kuwa ukuaji wa sayansi na teknolojia umechangia kwa kiasi kikubwa nchi wanachama za SADC kukuwa kiuchumi hivyo kumekuwa na hitaji la kuwa na miongozo sahihi, sera na sheria zitakazo wawezesha kushirikiana kwa pamoja katika kukuza sekta ya kazi na ajira.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Waajiri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt, Aggrey Mlimuka alisema kuwa ajenda zitakazojadiliwa zitatoa fursa kwa nchi wanachama kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo kwa wafanyakazi ambao ni chachu ya ukuaji uchumi.

Mkutano huo unafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 18 hadi 22 Novemba, 2019 na umeshirikisha wajumbe kutoka nchi ya Angola, Botswana, Eswatini, Malawi, Msumbiji, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe. Wajumbe wengine kutoka Shirika la Kazi Dunianai (ILO), SATUCC, SPSF, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), ZANEMA na ZATUC.

SIMA ATOA AGIZO KITUO CHA KUPOKEA GESI ASILIA CHA SONGAS KUWASILISHA MPANGO KAZI WA USIMAMIZI MAZINGIRA

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akiwasili katika kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kwa ajili ya kukagua na kupokea taarifaya madhara yaliyotokana na kuvuka kwa nishati hiyo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai.
Meneja wa kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas Salehe Kifunga (aliyesimama mwenye shati jeupe) akitoa maelezo kuhusu kituo hicho kinavyofanya kazi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima aliyeambatana na viongozi wengine.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akizungumza wakati wa ziara katika kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akitoa maelekezo baada ya kukagua kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas.
Eneo la kituo cha Songas kama linavyoonekana wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima pamoja na viongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC).
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai akizungumzia kuhusu tukio la kuvuja kwa gesi lilivyotokea mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai mara baada ya kukagua kituo cha Songas.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai mara baada ya kukagua kituo cha Songas.

…………….

Na Robert Hokororo, Kilwa

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima ameagiza kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga kuwasilisha mpango kazi wa usimamizi wa mazingira unaoonesha madhara na hatua zinazochukuliwa pindi yanapotokea maafa.

Sima ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara yake akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnath Chagu na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Samuel Gwamaka kukagua kituo hicho ambacho Novemba 3 mwaka huu kilipata tatizo la kuvujisha bomba la mafuta katika eneo hilo wilayani Kilwa mkoani Mtwara.

Katika ziara hiyo inayohusisha mikoa ya Lindi na Mtwara alisema kuwa ni muhimu wananchi wa vijiji zaidi ya 60 vilivyopitiwa na mradi wa bomba la gesi asilia licha ya kujua faida zake lakini pia wanatakiwa wapate elimu sahihi ya madhara pindi yanapotokea matatizo kama haya.

Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na hasa ya gesi asilia na kutaka mikataba ambayo inaingia na wakandarasi lazima ioneshe wananchi wameshirikishwaje na kuelewa kuhusu madhara yatakajitokeza endapo gesi itavuja.

Alisema kuwa lazima kama nchi tujuie mikataba hii ili kama yakitokea maafa wao wanawajibikaje kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza hususana kwa wananchi wanaopitiwa na miradi hiyo.

“Tumekuja hapa tuone kama mkiradi hii inafuata sheria ya mazingira yam waka 2004 na hapa tunataka tuone kwenye eneo hili yakitokea madhara ni hatua gani zinachukuliwa, tunataka kuona taarifa kamili na tuangalie kwenye eneo letu la mazingira mnachukua hatua gani.

“Hebu turudi kuangalia mkataba huu makubaliano gani tunawekeana sio valvu mpya imetoka maabara imekuja ikawekwa hapa halafu ikajivusha gesi, hapana lazima tuje na majibu sahihi. Natambua wizara husika imefanya kazi yao na sisi tunaoratibu shughuli za mzingira lazima tufanye kazi yetu,” alisema Sima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC) Prof. Chagu alisema ni muhimu kwa watalamu kuhakikisha vifaa vinavyototumika vinakuwa na viwango.

Prof. Chagu alisema kuwa matumizi ya vifaa vyenye viwango yatasaidia katika kuhakikisha matatizo kama haya hayatokei na kuleta madhara kwa wananchi na hata kama yakitokea basi lazima tujue hatua za kuchukua. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai alisema hili ni tukio baya kutokea na kama wasingekuwa makini kuzuia cheche ingekuwa hali ya hatari na kusababisha maafa makubwa. 

Ngubiaga alibainisha kuwa katika siku ya tukio hilo wananchi wanaotumia Barabara ya Kilwa hususan wasafiri wa mabasi ya kwenda au kutoka Mtwara na Songea waliathirika kutokana na kutoendelea na safari.

Pia alisema kuwa athari za kiuchumi zilionekana kutokana kuzimwa kwa kituo cha umeme Kilwa kutoka muda wa jioni hadi usiku hivyo wananchi walikosa huduma hiyo na kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi.

BENKI YA TPB YAMWAGA VIFAA SHULE MBILI ZA SEKONDARI MBILI

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania(TPB) Sabasaba Moshingi wa tatu kushoto akikabidhi moja kati ya meza 100 na viti 100 vyenye thamani ya shilingi Ml 4.8 kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye kwa ajili ya shule mbili za Sekondari za Mbambi na Makita zilizopo Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma,kushoto Afisa mahusiano wa Benki hiyo Novas Moses. 
****************

BENKI ya Posta Tanzania(TPB) imetoa msaada wa meza 100 na viti 100 vyenye thamani ya shilingi Ml 4.8  kwa shule mbili za Sekondari za Mbambi na Makita zilizopo katika Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma.

Akikabidhi samani hizo za Shule,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi alisema, Benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutenga kiasi fulani cha fedha  kila mwaka na kusaidia jamii hasa katika sekta ya Elimu katika mikoa mbalimbali hapa Nchini.

Alisema,  mwaka wa fedha 2019 Benki ya Posta imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya kuchangia huduma za jamii na itaendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazo fanywa wananchi na Serikali.


Moshingi alisema, Benki ya Posta Tanzania inajivunia sana kuona imekuwa sehemu ya mafanikio katika sekta  ya Elimu hapa Nchini  na sio mara ya kwanza kuchangia sekta ya elimu kwani mwaka jana ilitumia kiasi cha shilingi milioni 50 kukarabati shule ya Msingi Kindimba iliyopo katika wilaya hiyo.

Amewataka wanafunzi wa shule hizo, kuhakikisha  wanatumia meza na viti hivyo kusoma kwa bidi na kujiepusha na mambo yanayoweza kukatisha safari yao ya maisha na kuwataka Watanzania wengine kuunga mkono juhudi zinazo fanywa na Benki ya Posta na Serikali ya awamu ya tano ya kumarisha miundombinu ya Shule.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Cosmas Nshenye,amewataka wakazi wa  Mbinga  kuwa wazalendo, na wenye mapenzi mema kwa  kumaliza baadhi ya changamoto zinazoikabili wilaya hiyo badala ya kutegemea misaada ya Serikali na wafadhili.

 Nshenye ametoa kauli hiyo jana wakati akiongea na wanafunzi,walimu na baadhi ya wananchi katika hafla ya kupokea msaada wa viti 100 na meza 100 zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania kwa shule mbili za  Sekondari za Mbambi na Makita wilayani humo.

Alisema, sio  jambo la kufurahisha na haipendezi hata kidogo kwa jamii  ya wana Mbinga kuona wanashindwa  kuchangia ujenzi wa miradi na huduma mbalimbali za kijamii, kwani wana uwezo mkubwa wa kifedha,lakini inasikitisha kuona  kazi kubwa ya kuijenga wilaya hiyo imeachwa kwa Serikali na wadau wengine wa maendeleo.

Nshenye alisema, wakati umefika kwa wakazi wa wilaya ya Mbinga kubadilika na kujitolea nguvu kwa kuchangia  ujenzi wa miradi  ikiwemo miundombinu ya Elimu,Afya,Maji na mingineyo hatua itakayochochea na kuharakisha maendeleo ya Nchi yetu.

Kwa mujibu wake,ni aibu wilaya kama ya Mbinga ambayo wananchi wake wana nguvu kubwa ya kiuchumi inayotokana na zao maarufu la kahawa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati,viti na meza huku baadhi ya wanafunzi wa shule wakilazimika kubeba viti kutoka nyumbani kwao.

Aidha Mkuu wa wilaya ameishukuru Benki ya Posta kwa msaada wa viti na meza ambazo zinakwenda kupunguza  mahitaji ya samani  kwa shule hizo mbili, ambapo ameyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Benki hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kuchangia miundombinu ya shule kwa wilaya ya Mbinga.

Amewataka wanafunzi  kutumia meza na viti hivyo  kusoma kwa bidii, hali itakayowasaidia kufikia malengo waliyojiwekea katika safari yao ya maisha nan a viti na meza hizo wazitumie kama chachu ya mafanikio.

Awali Mkuu wa shule ya Makita Wilson Msengi alisema, shule hiyo ina upungufu wa viti 62 na meza 58,lakini msaada huo  uliotolewa na Benki ya Posta utapunguza sana changamoto hiyo.

Alisema,samani hizo zinakwenda kuhamasisha suala zima la kujifunzia na kufundishia darasani na pia kuchochea taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Serikali Kuanza Mikakati Ya Kuwa Na Masoko Ya Uhakika Ya Asali

0
0
Na, Editha Edward -Tabora

Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii imesema inaendelea na mikakati ili Kuhakikisha kunakuwa na Masoko ya Uhakika ya Asali kwa kuanzisha viwanda katika maeneo mbalimbali Nchini ambapo tayari imetenga bajeti ili Kuanza ujenzi wa viwanda viwili na kukarabati viwanda vingine vitano vilivyopo

Akizindua kamati ya kitaifa ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki mjini Tabora yenye wajumbe wapatao kumi waziri Kigwangala amebainisha kuwa kuna haja ya kuwa na viwanda vya kuchakata na kufungasha Asali vitakavyosaidia kuwa na Masoko huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo thabiti wa vyama vya ushirika ili visimamie viwanda hivyo ambapo ametoa muda wa mwezi mmoja Kuhakikisha kuna mifumo ya ushirika

"Pesa zimetengwa taasisi zipo na zipo tayari kuchangia mizinga zipo tayari kwa ajili ya kujenga hivyo viwanda lakini mfumo haupo mimi nilichokitaka nikuwepo na mfumo thabiti wa ushirika kwani ndiyo msingi wa kufanikiwa kwenye utekelezaji wa mpango huh"Amesema Kigwangala 

Katika hatua nyingine Waziri Kigwangala amekabidhi Mizinga miasita kwa kikundi chat ufugaji nyuki IPOLE na mizinga miatano katika chuo cha ufugaji nyuki Tabora huku akiziagiza taasisi zilizo chini ya wizara yake zikuwemo TANAPA, TAWA na TFS kutengeneza mizinga elfusita Kila taasisi ili zigawiwe katika vyama vya ushirika vitakavyoanzishwa 

Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Ezekiel Mwakalukwa Amesema takwimu zilizopo za mizinga katika kikundi chat Ipole ni takribani elfu kumi na mbili ya magome ya miti na mizinga ya maboxisi ni mizinga miamoja licha ya kuwepo na juhudi kubwa ya ufugaji nyuki lakini kwa sehemu kubwa inaharibu Mazingira

Aidha pamoja na kukabidhi mizinga Huyo waziri wa maliasili na utalii pia ameiomba bodi kumshauri kuhusu ujenzi wa viwanda na muundo mzuri ambao utafaa katika kuvisimamia na namna ya upatikanaji wa Masoko ya Uhakika. 
Mizinga ya nyuki miatano iliyokabidhiwa kwenye chuo cha ufugaji nyuki Tabora
Waziri wa maliasili na utalii Dkt Hamis Kigwangala akikabidhi mizinga miasita kwa kikundi cha ufugaji nyuki IPOLE
Waziri wa maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza katika uzinduzi wa kamati ya kitaifa ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki mjini Tabora
wajumbe wa kamati ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki.

DKT KALEMANI ATANGAZA NEEMA NYAMAGANA

0
0
Veronica Simba - Mwanza

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwaunganishia umeme wananchi wa mitaa 14 ya Kata ya Lwanima na mitaa 9 ya Kata ya Buhongwa, wilayani Nyamagana, Mkoa wa Mwanza, kwa gharama ya shilingi elfu 27 pekee sawa na miradi ya umeme vijijini.

Alitoa maagizo hayo Novemba 19 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo, ambapo aliwasha rasmi umeme katika Mtaa wa Mwang’haranga.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Waziri Kalemani alisema neema hiyo ya kuunganishiwa umeme wa elfu 27 imewafikia kutokana na mpango unaotekelezwa na serikali katika maeneo yaliyoko pembezoni mwa miji, yenye kushabihiana na vijiji, maarufu kama Peri-Urban.

“Kwakuwa maeneo haya yanashabihiana na vijiji, mtaunganishwa kwa bei ya vijiji. Mumshukuru sana Rais Magufuli kwa kuendelea kuwapigania wananchi wanyonge na kuhakikisha wanapelekewa huduma za maendeleo.”

Aidha, Waziri alimpongeza Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, ambaye alimwelezea kuwa amepambana sana kuhakikisha wananchi wa maeneo husika wanapata nishati ya umeme kwa gharama hiyo nafuu.

Aliwataka TANESCO kukamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi ujao wa Desemba ili kuwawezesha wananchi hao kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka wakiwa na umeme.Kwa upande wake, Mbunge Mabula aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa usikivu wa changamoto za wananchi na utatuzi wa haraka.

Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani alifanya ziara wilayani Magu ambapo aliwasha umeme katika vijiji vya Mahaha na Nyasato huku akitilia mkazo taasisi za umma kuunganishwa na nishati hiyo kwa ajili ya uboreshaji wa huduma kwa wananchi.

Aliwataka viongozi wa Halmashauri za Wilaya na Vijiji kuhakikisha taasisi zote za umma zilizo katika maeneo yao, zinaunganishiwa umeme. “Hilo litatekelezeka ikiwa ninyi viongozi mtatenga fedha na kulipia gharama za kuunganishwa ambazo ni shilingi elfu 27 tu,” alisisitiza.

Akiwa katika Shule ya Msingi Nyasato (eneo ambalo waliishi babu na bibi yake), Dkt Kalemani alilipa kwa TANESCO shilingi elfu 27 ikiwa ni gharama za kuiunganishia umeme shule hiyo ambayo tayari ilikwishatandaza mfumo wa nyaya (wiring). Aliagiza umeme uunganishwe siku hiyohiyo.

Kwa nyakati tofauti, Waziri alipongeza jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Magu, Desdery Kiswaga, katika kuhakikisha wananchi wake wanapata nishati ya umeme kwa ajili ya maendeleo yao.

Naye Mbunge huyo alipongeza uchapakazi wa Dkt Kalemani huku akimpambanua kuwa mmoja kati ya mawaziri wachapakazi, wenye weledi na kasi ya kazi katika Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.

Alimwomba Waziri kufikisha salamu za shukrani za wana-Magu kwa Rais Magufuli kutokana na namna anavyowapigania katika masuala ya kimaendeleo.Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati, alimpongeza Waziri Kalemani kwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kusitisha uagizaji nje wa vifaa mbalimbali vya umeme zikiwemo transfoma na kutumia vinavyozalishwa nchini.

Alisema kwa kutumia vifaa vya ndani, kumekuwa na mabadiliko chanya ya zoezi la uunganishaji umeme katika maeneo mbalimbali tofauti na ilivyokuwa awali.

Katika ziara hiyo, Waziri alifuatana na viongozi mbalimbali waandamizi kutoka wizarani, TANESCO na REA.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme katika Zahanati ya Kijiji cha Nyasato, wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza, akiwa katika ziara ya kazi, Novemba 19, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyasato iliyopo wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara ya kazi, Novemba 19, 2019. Waziri aliagiza shule hiyo iunganishiwe umeme siku hiyohiyo.
 Baadhi ya watoto wakazi wa Buhongwa mkoani Mwanza, wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo akiwa katika ziara ya kazi, Novemba 19, 2019.

 Wananchi wa kijiji cha Mahaha, wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza, wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuwasha rasmi umeme, Novemba 19, 2019.

 Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula (wa pili-kulia), akimwonesha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa tatu-kulia), baadhi ya mitaa ya Buhongwa, wilayani humo ambayo inashabihiana na vijiji na haijafikiwa na umeme. Waziri aliiagiza TANESCO kuipelekea mitaa hiyo umeme wa elfu 27 sawa na inavyotozwa vijijini. (Novemba 19, 2019)

 Mbunge wa Magu, Desdery Kiswaga, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijiji cha Mahaha, wilayani humo. Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Novemba 19, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijiji cha Mahaha, wilayani humo. Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Novemba 19, 2019.

TAMISEMI Queens yaichapa JKT Mbweni na kutwaa ubingwa wa Muungano

0
0
Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI Queens) hii leo wamefanikiwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 baada ya kuifunga timu ya JKT Mbweni magoli 40 kwa 23 katika mchezo wafainali wa michuano hiyo.

TAMISEMI Queens wamekabidhiwa kikombe cha ubingwa huo na kuweza kutoa pia mchezaji bora (MVP) na mchezaji bora wa katikati (center).

Akizungumza mara baada ya mchezo huo wa Fainali uliyofanyika katika Viwanja vya Gym Kana visiwani Zanzibar Mwalimu wa Timu ya TAMISEMI Queens Maimuna Rajabu Kitete amesema kuwa mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na wachezaji wake wameweza kufanya vizuri kutokana na alivyokuwa amewaandaa katika michuano hiyo.

“Wachezaji wangu niliwataka kucheza mpira na so kucheza na waamuzi wa mchezo ndo maana tuliweza kufanya vizuri katika mchezo waleo na kuibuka mabigwa wa michuano hii” ameeleza Mwalimu Kitete

Kwa kuongezea Mwalimu Kitete ametoa shukrani kwa Uongozi wa TAMISEMI,wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano wao mpaka kufanikiwa  kutwaa ubigwa huu.

Mwalimu Kitete ameendelea kusema kuwa baada ya Ubingwa huu wanajipanga vizuri kuaangalia michuano ya Afrika mashariki inayokuja mbele yao baaada ya kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Muungano 2019

Lakini pia mchezo huo wa fainali timu ya JKT Mbweni walishindwa kucheza vizuri kutokana na wao kucheza na waamuzi wa mchezo huo kitu kilichowapa changamoto na kufanya kupoteza mchezo huo. 

Kwa upande mwingine zikiwa zimesalia dakika saba mchezo wa fainali hizo kumalizika timu ya JKT Mbweni waligomea mchezo na kutoka nje ya uwanja wakidai waamuzi wa mchezo huo kutokuwa sawa katika maamuzi huku timu ya TAMISEMI Queens wakibaki uwanjani mpaka dakika za mchezo huo kumalizika na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.

TAMISEMI Queens ilikuwa kundi B ikiwa na timu za JKT Mbweni, Mafunzo ya Zanzibar, Eangle ya Dar es salaam, Makotopola ya Dodoma na Zimamoto ya Zanzibar na katika hatua ya makundi walipata kushinda michezo yote na kuingia hatua inayofata mpaka kufikia fainali na kuwa mabingwa wa michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa TAMISEMI Queens ni timu pekee ya wizara kutokea Tanzania Bara iliyoshiriki michuano hii na kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Muungano Zanzibar 2019.
Kikosi cha Timu ya TAMISEMI Queens kikiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanikiwa kuichapa JKT Mbweni katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Muungano na kutwaa ubingwa huo.

WATAALAM FIZIOTHERAPIA WAKUTANA MLOGANZILA

0
0
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Sara Maongezi akifungua kongamano la kitaifa la wafiziotherapia nchini.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (Kulia) akizungumza katika kongamano la wafiziotherapia linalofanyika katika Hospitali ya Mloganzila, kushoto ni Dkt. Sara Maongezi.
Rais wa Chama cha Kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA), Bi. Remla Shirima akisoma risala wakati wa Kongamano la Wafiziotherapia linalolenga kuangalia maendeleo ya taaluma hiyo nchini.
Wataalam wa Fiziotherapia wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizotolewa katika mkutano huo.
Dkt. Sara Maongezi na Dkt. Julieth Magandi wakiwa katika picha ya pamoja na wafiziotherapia mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa mwaka wa wataalam hao.

…………………..

Wataalam wa Fiziotherapia wamekutana katika kongamano la kitaifa la taaluma ya tiba kwa vitendo lengo likiwa ni kuangalia maendeleo ya taaluma hiyo nchini.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Sara Maongezi amesema kuwa Wizara ya Afya inazitambua kisheria huduma zinazotolewa na wafiziotherapia nchini.

“Huduma ya tiba kwa vitendo na wanataalauma wake wanatambuliwa rasmi na sheria ya kusimamia huduma na watoa huduma wa taaluma katika sheria mpya ya madaktari, madakari wa meno na huduma shirikishi ya 2017 (Medical, Dental and Allied Health Professionals Act 2017),” Amesema Dkt. Maongezi.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi ametaja kuwa hospitali ina jumla ya vitanda 608 ambapo kwa siku inahudumia wagonjwa wa nje 400 hadi 450, na wagonjwa wa ndani takribani 300 ikiwa ni pamoja na kufanya upasuaji kwa wagonjwa 200 hadi 300 kwa mwezi.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania, Bi. Remla Shirima ametaja moja kati ya changamoto ambayo taaluma hiyo inapata ni kukosekana kwa vyuo vinavyotoa shahada ya taaluma ya tiba kwa njia ya vitendo ambapo hadi sasa vyuo vingi hapa nchini vinatoa elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada tu.

“Tunaiomba Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ianzishe vyuo vinavyotoa shahada ya tiba kwa njia ya vitendo kutokana na idadi ya wataalam hawa kuwa wachache, ambapo hadi sasa wapo takribani wataalam 400 nchini na kati ya hao 182 tu ndio wanaofanyakazi kwenye taasisi za Serikali kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mapema mwaka huu,” Amesema Shirima.

Kongamano limejumuisha washiriki wanaotoka sehemu mbalimbali nchini ikiwamo wataalam kutoka MNH, Chuo cha Fiziotherapia KCMC, Benki ya NMB, Wawakilishi kutoka Chuo cha Fiziotherapia SOMT nchini Netherlands, Bodi ya Usajili wa Hospitali Binafsi za Afya nchini (PHAB), Taasisi za Hospitali Binafsi (APHTA), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Wawakilishi wa vyama mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, Kamati tendaji ya Chama cha Kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA), Dawati la utengamao-Wizara ya Afya na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

VIGOGO WAWILI WA CHADEMA HANANG’ WAJIUNGA CCM

0
0
Mwenyekiti wa CCM Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Mathew Darema (kushoto) akinyanyua juu mkono wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Wilayani Hanang’ Yuda Bwanjida aliyeondoka Chadema na kujiunga CCM.
Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Balang’dalalu Mkoani Manyara, Emmanuel Gamasa akipeana mkono na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Wilayani Hanang’ Yuda Bwanjida.

………………………
VIGOGO wawili wa Chadema Wilayani Hanang’ wameondoka kwenye chama hicho na kujiunga na CCM ili kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. 

Vigogo hao akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chadema (Bavicha) wilaya ya Hanang’ Yuda Bwanjida na aliyegombea udiwani kwa Chadema mwaka 2015 kata ya Balang’dalalu Daudi Mathayo walipokewa na Mwenyekiti wa CCM wilayani Hanang’ Mathew Darema. 

Bwanjida akizungumza sababu za kujitoa Chadema, alisema zipo nyingi ikiwemo maendeleo mengi yanayofanywa na Rais Magufuli na usimamizi wa mkuu wa mkoa huo Mnyeti. 

Bwanjida alisema baada ya kuona viongozi wa chama chake wameangukia kwenye uanaharakati badala ya maendeleo aliamua kuachana nacho na kujiunga na CCM. 

“Nimejiunga na kukutana na vijana wenzangu ambao tutashirikiana kufanya kazi za kijamii kwani CCM ipo karibu na wananchi kupitia mikakati mbalimbali ya kutetea wananchi wa Taifa hili kuliko kuwa kwenye chama cha uanaharakati,” alisema. 

Kwa upande wake, Mathayo ambaye aligombea udiwani wa kata ya Balang’dalalu na kuangushwa na Paulo Marmo (CCM) alisema anarudi CCM ili kuwaunga mkono Rais Magufuli na Mnyeti katika kufanikisha maendeleo. 

Mathayo alisema yale mambo waliyokuwa wanapigia kelele wakiwa upinzani hivi sasa yanatekelezwa na Rais Magufuli hivyo haoni umuhimu wa kumpinga. 

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) kata ya Balang’dalalu, Emmanuel Gamasa aliwapongeza viongozi hao wa upinzani kwa kuondoka Chadema na kujiunga na CCM. 

“Nawakaribisha viongozi hawa ambao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 walitupa changamoto kubwa na hivi sasa tutaendelea kujenga chama chetu kwa umoja na upendo,” alisema Gamasa. 

Mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani Manyara, Carol Gisimoy alisema viongozi hao wameona mbali kwa kuondoka Chadema na kujiunga CCM kwani wananchi wengi wanaiunga mkono. 

“Hakuna mtu ambaye aliwashawishi kujiunga na CCM ni wao wenyewe wameona maendeleo ya Rais Magufuli na usimamizi mzuri wa mkuu wa mkoa Mnyeti wakaona hakuna sababu ya kubaki upinzani,” alisema Gisimoy. 

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Hanang’ Mathew Darema alisema chama hicho kinazidi kupiga hatua na wananchi wengi zaidi wanazidi kuwaunga mkono kutokana na maendeleo yanayofanywa. 

“Chini ya jemedari wetu Rais Magufuli tunaendelea kutembea kifua mbele kutokana na kuendelea kuungwa mkono katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania,” alisema Darema.

MAKUSANYO KODI YA ARDHI GAIRO HAYAMFURAHISHI NAIBU WAZIRI MABULA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia wamiliki wa viwanja walioingizwa katika Mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya Kieletroniki katika ofisi za Ardhi za Halmashauri ya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya hiyo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe na aliyekaa ni Afisa Ardhi Msaidizi wa Halamashauri ya Wilaya ya Gairo Salivius Sarapion.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Agnes Mkandya kuhusiana na makusanyo ya kodi ya ardhi wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Gairo mkoani Morogoro jana. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe akiangalia sehemu ya Mizinga ya Nyuki katika eneo la Msingisi Gairo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Gairo jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akielekea katika Shamba la Miti la Ukaguru kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi na nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jana. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe na Kulia ni Meneja wa Shamba la Miti la Ukaguru Mohamed Msalu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka kukagua ujenzi wa ofisi na nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jana katika hifadhi ya Msitu wa Ukaguru. Anayemfuatia ni Mkuu wa wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo wakitembea katika hifadhi ya Msitu wa Ukaguru wilaya ya Gairo jana alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi na nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jana.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Gairo kwenye Maporomoko ya hifadhi ya Msitu wa Ukaguru wilayani Gairo jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Gairi Sirieli Mchembe.



……………………

Na Munir Shemweta, WANMM GAIRO

Kasi ndogo ya ukusanyaji mapato ya Kodi ya pango la ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro imemsononesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ta Makazi Dkt Angeline Mabula na kuagiza halmashauri hiyo kuongeza kasi ili kufikia lengo la mapato ya kodi ya ardhi.



Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika wilaya hiyo jana tarehe 19 Novemba 2019 Dkt Mabula alielezwa na Afisa Ardhi katika halmashauri ya Gairo Nicolaus Matsuva kuwa halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka 2018/2019 imekusanya shilingi milioni 12.3 na mwaka huu kufikia Novemba imekusanya milioni 10 ya kiwango ilichopangiwa cha milioni 55.



Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, kiwango hicho cha makusanyo katika halmashauri ya Gairo ni kidogo na hakijafikia hata nusu ya makadirio ya shilingi milioni 55 iliyowekewa halmashauri hiyo kukusanya kwa mwaka na makadirio hayo hayalingani na uhalisia wa makusanyo ya halmashauri.



Aliitaka halmashauri ya Gairo kupitia idara yake ya ardhi kuongeza kasi ya makusanyo ya maduhuli ya kodi ya pango la ardhi kwa kuwa kodi hiyo ndiyo inayoisaidia serikali kutekeleza miradi mikubwa aliyoieleza kuwa mingi inataegemea kodi ya ndani.



‘’Msipokusanya kodi ya ardhi mjue mnamkwamisha Mhe Rais kutekeza miradi mikubwa kama vile mradi wa kufufua umeme wa Mwl. Nyerere maarufu kama stiglers hivyo ni lazima tuongeze kasi ya makusanyao’’ alisema Dkt Mabula.



Sambamba na hilo Dkt Mabula aliitaka halmashauri ya wilaya ya Gairo kuhakikisha kufikia Desemba 2019 inarejesha fedha shilingi milioni 31 ilizopatiwa mwezi Juni 2019 kama mkopo kwa ajili ya upimaji viwanja katika halmashauri hiyo.



Hatua hiyo inafuatiwa Naibu Waziri Mabula kuhoji kuhusiana na marejesho ya fedha za mkopo huo na kuelezwa na Afisa Ardhi kuwa, halmashauri hiyo hajarejesha kiasi chochote cha fedha za mkopo iliopatiwa kwa ajili ya upimaji viwanja na kuomba kuongezewa muda wa kurejesha hadi mwezi Machi 2019.



‘’ Toka mwezi Juni hadi leo Desemba hamjarejesha wakati ulitakiwa kurejeshwa ndani ya miezi mitatu, Mkopo huu unazunguka kwa nini hamjarejesha hadi leo? Kazi mliyopewa hamjamaliza naagiza hadi kufikia Desemba fedha hiyo iwe imerejeshwa’’ alisema Mabula.



Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshangazwa na idara ya ardhi katika halmashauri ya Gairo kuingiza viwanja 155 kati ya 1,198 kwenye mfumo wa makusanyo ya kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki jambo alilolieleza linaikosesha serikali mapato yataokanayo na kodi ya pango la ardhi sambamba na kushindwa kutoa ilani kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi ingawa ilani hizo zilizndaliwa tangu mwezi Machi 2019.



Dkt Mabula alielezwa na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Nicolaus Matsuva kuwa, baadhi ya wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi walishindwa kupatiwa ilani hizo kutokana na maeneo wanayomiliki kukutwa wakiishi watu wengine tofauti na wamiliki waliopo kwenye kumbukumbu zao jambo lilimfanya Naibu Waziri kumuagiza Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda Maalum ya Morogoro Erick Makundi kufuatilia suala hilo kwa kwenda uwandani na kupatiwa taarifa kufikia Desemba mwaka huu.



Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe alisema, wilaya yake ina changamoto kubwa ya ujenzi holela na kubainisha kuwa hata zoezi la urasimishaji katika wilaya hiyo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo sebule za baadhi ya nyumba kuelekezwa kwenye vyoo vya nyumba nyingine.



Hata hivyo, alimuahidi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa ofisi yake itayafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo uandaaji wa Mpango Kabambe katika wilaya hiyo iweze kupangika kimji sambamba na kuwa na Mji wa Serikali utakaojumuisha taasisi zote za serikali zilizopo katika wilaya hiyo.



Ktika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alitembelea hifadhi ya Msitu wa Ukaguru uliopo Tarafa ya Nongwe kata ya Mandege wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba na ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unaofanywa na Shirika la nyumba la Taifa (NHC).



Akiwa kwenye ukaguzi wa ujezi huo, Dkt Mabula alipata malalamiko ya baadhi ya vibarua wanaojenga ofisi hiyo kutopatiwa malipo kwa wakati jambo walilolieleza kuwa linawakatisha tamaa kuendelea na kazi hiyo. Hata hivyo, Naibu Waziri Mabula aliwataka vibarua hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuahidi kulifuatialia suala hilo haraka ili vibarua hao walipwe fedha kwa wakati.



Aidha, Dkt Mabula alipata fursa ya kutembelea Maporomoko katika hifadhi ya shamba la Miti la Ukaguru ambapo alijionea namna eneo hilo linavyoweza kuwa moja ya vyanzo vya umeme sambamba na kuwa kivutio kikubwa cha utalii kinachoweza kuingizia serikali mapato yatokanayo na sekta hiyo.



Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe alielezea ziara ya Naibu Waziri Mabula kwenye Maromoko hayo kuwa ni ya kwanza kufanywa na Waziri na kubainisha kuwa ziara hiyo inaweza kuwa chachu ya hifadhi ya Msitu huo kutumika kwa shughuli mbalimbali kama vile za kitalii.

DIWANI ALALAMIKIA TEMBO KUVAMIA MAKAZI YA WANANCHI

0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA,NAMTUMBO.

Diwani wa kata ya Mgombasi Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma,Mrisho Mbawala aamelalamikia tembo kuvamia makazi ya wananchi wa kitongoji cha Masimango katika kijiji cha Nambecha.

Akizaungumza katika vikao mbalimbali Wilayani hapa pamoja na mkutano wa baraza la madiwani la hivi karibuni Mrisho alisema tembo katika kitongoji cha Masimango katika kijiji cha Nambecha kinawanyima wananchi uhuru wa kufanya shughuli za maendeleo ,Wanashindwa kwenda shambani wakihofia tembo .

Mrisho alidai tembo katika kitongoji hicho wametengeneza mazoea ya kuja katika kitongoji hicho mara kwa mara sio usiku tu hata mchana wanakuja na kuleta taharuki kwa wananchi alisema Mrisho.

Amedai kuwa kitendo cha kuwatumia askari wasaidizi wa vijiji (VGS) ambao hawana vifaa vya kuwafukuza tembo kinafanya tembo kuona ni jambo la kawaida kwao na kuendelea kufika katika makazi ya wananchi na kufanya uharibifu.

Mtendaji wa kata ya Mgombasi Benadetha Ndunguru alikiri kuwepo kwa tembo katika kijjiji cha Nambecha kitongoji cha Masimango ambao wanaharibu mazao ya wakulima yakiwemo mihogo,migomba na kuingia katika makazi ya wananchi .

Ndunguru alidai kikao cha maendeleo ya kata kilijadili kwa kina jambo hilo na kumtaka mheshimiwa diwani wa kata hiyo kuliwasilisha swala hilo katika vikao vya kisheria vya Halmashauri ambapo naye alifanya hivyo.

Obi Abeid Tindwa mkazi wa kijiji cha Nambecha alisema yeye anashindwa kwenda shambani kwake kutokana na tembo kufanya makazi katika mashamba yake na kuharibu mihogo,mbaazi,mapapai ,maembe,ndizi na kuvamia mahindi aliyoyahifadhi katika ghala .

Aidha kaimu mtendaji wa kijiji cha Nambecha Hamisi Rashidi Ulaya pamoja na mambo mengine alisema wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuomba askari walioajiriwa kufanya kazi ya kuwaondoa tembo hao kwani askari wa wanyamapori wa kijiji hicho (VGS) wanasusa kazi hiyo kwa madai kuwa hawana mshahara na kazi hiyo kwani hata wao wanakazi zao za shambani alisema kaimu Mtendaji huyo.

Afisa Ardhi na Maliasili wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Saimon Sambalu alidai kijiji cha Nambecha ni miongoni mwa vijiji vilivyopakana na Hifadhi ya wanyama ya Selou ambapo mara kwa mara tembo huvuka mipaka yao na kuingia katika maeneo ya karibu ya wananchi yaliyopo jirani na Hifadhi .

Hata hivyo bwana Sambalu alidai askari wao katika vijiji (VGS)pamoja na uhaba wa vitendea kazi wanajitahidi kufanyakazi ya kuwafukuza tembo hao mara kwa mara na kuwarudisha mbugani na kudai changamoto kubwa iliyopo ni kujua lini tembo hao watakuja tena baada ya kufukuzwa maana wakati mwingine wakifukuzwa humaliza hata mwezi mzima wasirudi na siku msiyotarajia wanatokea kijijini hali inayopelekea (VGS ) kuendelea kufanyakazi zao za kujipatia kipato kijijini wakidhania tembo hao wameacha kufika alisema Sambalu.

Ofisa wanyamapori wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Ernest Nombo alisema kitengo cha wanyamapori katika Halmashauri hiyo kinaendelea kuhakikisha watumishi wake wanafanya doria katika maeneo ya vijiji vilivyozunguka mbuga ya wanyama ya Selous kwa kushirikiana na askari wa vijiji waliopatiwa mafunzo kuhakikisha wanyama waharibifu wasilete madhara kwa wananchi na malizao.

Kikao cha baraza La madiwani katika Halmashauri ya Namtumbo kilitoa agizo katika idara inayohusika na wanyamapori kuwaondoa wanyama hao katika makazi ya wananchi na kuitaka idara hiyo kuacha kufanyakazi yake baada ya kutokea matukio..

RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA YAKE DODOMA KESHO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake wakati akitoa taarifa kuhusiana na ziara ya kikazi ya Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,itakayoanza kesho tarehe 21 hadi Novemba 25,mwaka huu jijini Dodoma,upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobasi Katambi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka.

Rais Dk John Magufuli anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Dodoma Novemba 21,2019 ambapo katika ziara hiyo ataweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya mandeleo ikiwemo Hospitali ya Uhuru, Stendi Kuu ya mabasi pamoja na soko kuu Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge amesema ziara hiyo itaanza Novemba 21 mwaka huu ambapo Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya kumi (10) ya Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga, Chuoni hapo.

Dk Mahenge amesema Novemba 22, 2019 Rais ataweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Hospitali ya Uhuru, Wilayani Chamwino, ujenzi wa nyumba 118 za Askari Polisi katika maeneo ya FFU Nzuguni na Medeli East, Ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi iliyopo Nzuguni.

Miradi mingine ni Soko Kuu linalojengwa katika eneo la Nzuguni  pamoja kuzungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika stendi ya mabasi Nzuguni.

“Jumatatu Novemba 25, 2019 mheshimiwa Rais ataweka mawe ya msingi kwenye miradi ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania Kikombo, ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji na Ujenzi wa jengo la Makandarasi katika eneo la National Capital City.

Ziara hii ya mheshimiwa  Rais (John Magufuli) kwetu ni fursa ya kumwonesha hatua tulizofikia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyotupatia na kupokea maelekezo ya namna ya kusonga mbele kwa uhakika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake,” Amesema Dk Maheng

KADUGUDA ATEULIWA KUWA KAIMU MWENYEKITI KLABU YA SIMBA

0
0
Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedy Mkwabi, Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simba Sports Club Limited imemteua, Mwina Kaduguda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Klabu hiyo.

Taarifa kwa Umma iliyotolewa mapema leo na Klabu hiyo, imeeleza uteuzi huo umeanza leo Novemba 19, 2019. Tarehe ya Uchaguzi kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu hiyo utatangazwa na Bodi ya Wakurugenzi hapo baadae.

Hata hivyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simba Sports Club imemteua, Salim Abdallah Muhene kuwa Makmu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo, kwa uteuzi huo kuanza leo.

Taarifa hiyo imeeleza teuzi hizo zimefanywa kwa mujibu wa Mamlaka ya Bodi chini ya Ibara ya 50 ya Katiba ya Klabu ya Simba yam waka 2018.

KOCHA JOSE MOURINHO ATAJA KUWA KOCHA MKUU WA TOTTENHAM

0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Tottenham rasmi imemtaja Kocha raia wa Ureno, Jose Mourinho kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo baada yakumtimua aliyekuwa Kocha wake, raia wa Argentina Mauricio Pochettino.

Tottenham inakuwa timu ya tatu ya Uingereza kufundishwa na Kocha Mourinho baada ya awali kuzifundisha Manchester United na Chelsea.

Mourinho ametajwa kuwa Kocha wa Tottenham akichukua mikoba iliyoachwa na Kocha Mauricio Pochettino kwa kusaini kandarasi hadi mwisho wa msimu wa 2022-23.

Kupitia Tovuti ya BBC Sport, Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy amenukuliwa akisema kuwa “Kwa Jose tumepata Kocha mwenye mafanikio katika Soka na mwenye uzoefu kufundisha Soka”.

Baada yakutangazwa kuwa Kocha wa timu hiyo, Mourinho amesema “Navutiwa na ubora wa Kikosi chao kikubwa na Kituo chao cha Vijana (Academy). Kufanya kazi na Wachezaji wa Tottenham ni furaha kwangu”.
   
Mourinho akiwa Kocha nchini Uingereza alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu Soka nchini humo, Kombe la FA mara mbili akiwa na Chelsea, pia alishinda Europa League na Carabao Cup akiwa na Manchester United.

RAIS MAGUFULI ASEMA WAKULIMA WAPANGE BEI KULINGANA NA SOKO, SERIKALI HAITAWAPANGIA

0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amewataka wakulima wote nchini kuuza mazao yao kwa bei wanayotaka na kwamba Serikali haitapanga bei na badala yake jukumu hilo libaki kwa mkulima mwenyewe.

Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo Novemba 20, mwaka 2019 akiwa katika eneo la Dumila mkoani Morogoro.Rais alisimama kuzungumza na wananchi hao akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma kikazi.

Akiwa na wananchi hao, Rais Magufuli amekumbusha kuwa mvua zimeanza kunyesha, hivyo watu wajihusishe na kilimo huku akieleza kuwa kuna watu wanalalamika kupanda kwa bei ya mahindi lakini ifahamike Serikali haitapanga bei.

Amesema mkulima mwenyewe ndio ataamua anataka kuuza bei gani kulingana na mahitaji ya soko kwa wakati husika.

"Nataka Mkoa wa Morogoro uwe kinara katika kuzalisha mazao.Serikali ninayoingoza katika kipindi changu sitapanga bei ya vyakula, wakati mkulima analima hakuna anayempangia bei, hivyo anapouza mazao yaake aachwe aamue anataka kuuza bei gani mazao yake,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza hata kama mkulima ataamua kuuza debe moja la mahindi kwa Sh.milioni moja sawa tu auze. "Hakuna kumpangia bei, wanaotaka bei nafuu wakalime wao."

Amefafanua ni kama ilivyo kwa mfugaji, anapouza ng'ombe huangalia bei ya soko , kama bei ya ng'ombe itakuwa juu atauza kwa bei ya juu, hivyo wakulima nao waachwe wapange bei wenyewe."Soko liachwe liamue bei na sio kupangiwa na Serikali."

Amesisitiza watu waache kulalamika mahindi yamekuwa juu na hiki ndio kipindi cha wakulima kunufaika na kilimo chao."Hata anayekuwa ofisini bado anaweza kulima kwa kutumia fedha zake kumtuma mtu amlimie badala ya kulalamika tu."

Rais Magufuli amesema kwa sasa soko la mahindi na mazao mengine ni nzuri na kuongeza nchi nyingi zinahitaji kununua mazao kutoka kwa wakulima wa Tanzania, hivyo ni wakati wao kutajirika.

WAKAZI JAMII YA WAFUGAJI CHAMAKWEZA WAANZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, Chamakweza

WAKAZI jamii ya Wafugaji wa Kijiji cha Chamakweza Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo Pwani, wameanza ujenzi wa shule ya sekondari ambayo ikikamilika itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye shule mbalimbali.

Hatua hiyo itahamasisha baadhi ya jamii hiyo wanaoshindwa kusomesha watoto wao na wengine kushindwa kuwapeleka kwenye shule za Moreto na Chalinze ambazo ni za bweni na kutwa.

Wakizungumza kwenye eneo la ujenzi, Michael Kashina,
Lepa Mumbi na Solomon Madongo walisema ,ujenzi huo umeanza kutokana na juhudi za Lekope Langw'esi diwani wa Kata ya Pera, kata ambayo kwa sasa baadhi ya vijiji vyake vilivyokuwa katika kata hiyo vimehamishiwa Kata ya Vigwaza.

Kashina alieleza, katika harakati hizo wametumia shilingi milioni 13 kwa ajili ya kuweka bati kwenye vyumba vitatu na ofisi moja, ili wakipata ridhaa toka halmashauri waanze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani, hatua inayopunguza msongamano katika shule zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.

"Langw'es akishirikiana na viongozi wenzake pamoja na wananchi walikaa kisha kuzungumza na mkazi aliyekuwa ameanza ujenzi wa sekondari binafsi, ambapo aliishia njiani ili awaachie majengo hayo yaliyopo ndani ya eka 50 kisha wampatie eneo mbadala"

Nae Mumbi alisema , miliki wa jengo hilo alilolenga kuwa sekondari ya binafsi, ameshindwa kulimalizia, hatua iliyowalazimu wao kumfuta wakamuomba ili wajenge shule ya Kata, kisha wao kumpatia eneo lingine lenye ukubwa wa eka 50 sawa na hilo. 

Diwani Langw'esi aliwashukuru wananchi wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wao kwa kukaa kisha kuibua mradi huo unaolenga kuwaondolea wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.


DKT.MAGUFULI AAGIZA MAJENGO YOTE YA OFISI ZA TANROAD DUMILA YAWE KITUO CHA AFYA

0
0











Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza majengo yote yaliyokuwa ya Ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania(TANROAD)eneo la eneo la Dumila mkoani Morogoro yakabadilishwe na kuwa Kituo cha Afya Dumila. 

Ametoa maagizo hayo leo Novemba 20,mwaka 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Dumila akiwa safari kuelekea mkoani Dodoma. Akiwa hapo wananchi hao kupitia diwani wao walitoa maombi yao kadhaa kwa Rais ambayo kwao yamekuwa changamoto ikiwemo ya kukosa kituo cha afya, uhaba wa maji safi na salama na umeme. 

Hivyo wakati anajibu changamoto hizo, Rais amesema kuanzia leo hii, majengo hayo ya ofisi za TANROAD yatakuwa Kituo cha afya Dumila na nyumba 11 za ofisi hizo ziwe nyumba za watumishi wa kituo hicho. 

"Hoja zote ambazo zimetolewa na diwani wenu hapa ni za msingi na zitafanyiwa kazi, hili la kituo cha afya, naagiza majengo ya ofisi ya Tanroad yawe kituo cha Afya, kuhusu madaktari, dawa na vifaa tiba hilo nitatoa maagizo kwa Wizara ya Afya. 

"Kesho Diwani mje mfungue kituo cha afya na andika jina lako kwa niaba yangu, nimekuruhusu.Yale majengo yalijengwa kwa fedha za Serikali, kuna nyumba 11 nazo zote ziwe za kituo cha afya Dumila,"amesema Rais Magufuli. 

Pia Rais amesema changamoto nyingine ambazo zimeelezwa na wananchi hao zitafanyiwa kazi huku akitumia nafasi hiyo kutoa ruhusa ya wananchi hao kuchimba mchanga katika daraja la Mto Dumila ingawa ametaka kuwepo na utaratibu mzuri ambao uchimbaji huo hautaharibu daraja hilo. 

"Nawaruhus mchimbe mchanga, lakini tukubaliane kwa utaratibu mzuri, tusiharibu hili daraja.Ikitoke mkachimba mchanga na kuharibu daraja matipa yote nitayakamata,"amesema Rais Magufuli. 

Wakati huo huo Rais Magufuli amewataka viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo kutafuta ufumbuzi wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji ambao ametumia nafasi hiyo kueleza anayo matumaini makubwa kuwa ufumbuzi utapatikana.

WACHUNGAJI WATATU KANISA LA EAGT WAWASILISHA KUSUDIO LA KUKATA RUFAA MAHAKAMA KUU

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

WACHUNGAJI watatu wa Kanisa la EAGT (Tanzania) wamewasilisha kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu ili waweze kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Novemba 15, mwaka 2019 na Jaji Leila Mgonya.

Kusudio hilo la rufaa limewasilishwa mahakamani hapo na Wakili Edwin Swalle anayewawakilisha, wachungaji, Yared Lesilwa, Gilbert Weja na Petrol Kapama kwà niaba ya wenzao 543 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Wakili Swale amesema wanakata rufaa kwa sababu hawajaridhika na uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa kuwataka wateja wake kuandika barua kwanza ili kuona kama wanaweza kusuluhishwa nje ya Mahakama kupitia viongozi wa Kanisa ama la.

Amedai, wao wanaamini Mahakama ilijipotosha vibaya kwa kutoa uamuzi huo kwa sababu maombi yaliyokuwepo mbele yake ni kutoa kibali kwa wachungaji hao watatu waweze kuwawakilisha wenzao 543 na siyo kujadili undani wa tuhuma.

Ameongeza wateja wake walikwishajaribu kutafuta mwafaka bila mafanikio, hivyo chombo pekee cha kutatua mgogoro huo ambao ni tuhuma za ubadhirifu wa mali za Kanisa na ukwepaji wa kodi ni mahakama pekee.

Ameendelea kudai kuwa, kwa sababu hiyo hapakuwa na sababu ya kujadili ama kuzungumzia tena jambo lingine nje ya mahakama au kujadili hoja ambazo Mahakama ilishazitolea uamuzi tarehe 9 Agosti, 2019. 

Ambapo Jaji Mgonya baada ya kuangalia kama wadaiwa wanastahili kushtakiwa binafsi ama bodi ya wadhamini ya kanisa hilo,alisema wanastahili kushtakiwa mahakamani.

“Lengo la kwenda Mahakama ya Rufaa ni ili iruhusu wapewe kibali cha kuendelea kwa niaba ya wachungaji wenzao 543 kutoka maeneo mbali mbali nchini ambao ni ngumu kwao wote kufika Mahakamani na ni upotevu wa fedha na muda,"amesema Swalle.

Katika shauri hilo, Wachungaji hao ambao wanatetewa na Wakili Swalle walikuwa wakiomba kuruhusiwa kuwashtaki viongozi wa Kanisa la EAGT (Tanzania ) ambao ni wadaiwa katika kesi hiyo.

Wachungaji hao ni mchungaji Christomoo Ngowi ambaye ni mdhamini wa kanisa hilo, mchungaji Asumwisye Mwang'mbola ambaye naye alikuwa mdhamini wa kanisa hilo lakini kwa sasa ni marehemu.

Wengine ni mchungaji Brown Mwakipesile ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Mchungaji Leonard Mwizarubi Katibu Mkuu na mchungaji Praygod Mgonja ambaye ni muweka Hazina wa kanisa hilokwa tuhuma za ubadhilifu wa mali za kanisa, ukwepaji wa kodi kwa kuingiza magari kinyume cha taratibu.

Ambapo walipata msamaha wa kodi ya Serikali wakati magari hayo hayapo kwenye orodha ya mali za kanisa na uvunjifu wa katiba kwa kuwafukuza wachungaji bila ya kufuatia katiba ya kanisa na sheria za nchi.

Hata hivyo kwa upande wa wadaiwa walipinga maombi hayo wakidai kuwa wao hawapaswi kushtakiwa kwa mashtaka hayo ila bodi ya wadhamini ya kanisa hilo ndiyo ishtakiwe siyo wao kama viongozi kwa majina yao.

CHANGAMOTO UPATIKANAJI VITAMBULISHO...MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI MKUU NIDA,AMPA SIKU TATU

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

BAADA ya wananchi wa Msamvu mkoani Morogoro kutoa malalamiko kuhusu mchakato wa utolewaji wa vitambulisho vya Taifa, Rais Dk.John Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dk.Arnord Kihaule kufika leo leo Novemba 20,2019 mkoani hapo kutafuta ufumbuzi haraka ili wananchi wapate vitambulisho.

Mbali ya kwenda mkoani Morogoro Mkurugenzi huyo wa NIDA,Rais Magufuli amemtaka ndani ya siku tatu kuandaa utaratibu mzuri ambao utatumika nchi nzima katika kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho hivyo ili wananchi wasajili laini zao za simu.

Akiwa eneo la Msamvu leo Novemba 20,2019, akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma, Rais Magufuli alipata malalamiko ya wananchi kutopata vitambulisha vya NIDA na kumekuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao wanatoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Hivyo ,Rais Magufuli aliamua kumpigia simu Mkurugenzi huyo na kumuelezea changamoto na baada ya kumaliza kuzungmza naye akatoa maagizo ambayo ametayaka yafanyiwe kazi haraka.

"Nataka Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ufike hapa Morogoro ili ushughulikie hii changamoto ya vitambulisho , nimeelezwa ofisi ya NIDA mkoa wote wa Morogoro iko moja tu, hivyo watu wanatoka mbali kuja mkoani kufuata vitambulisho.

"Haiwezekani watu wasafiri kutoka wilayani kuja mkoani.Ofisi za NIDA ziwe kila mahali huko wilayani.Kama vipi muwape nauli na hela ya gesti.Ufumbuzi wa changamoto hii ufanyike hapa Morogoro lakini na wilaya zote nchini,"amesema Rais Magufuli.

Amesisitiza watu wanataka kusajili laini zao na mambo mengine, hivyo haiwezekani waliopewa jukumu hilo watashughulikie ili wananchi wapate vitambulisho na kisha waendelee na majukumu yao.
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images