Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

JAJI MKUU AWATAKA MAJAJI WAPYA KUWA SEHEMU YA MABORESHO

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwasilisha hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mafunzo elekezi kwa Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu.


Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika akitoa kwa Wahe. Majaji katika Mafunzo hayo.

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Mhe.Jaji  Dkt. Paul Kihwelo akizungumza wakati wa Mafunzo hayo.

 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza katika Mafunzo hayo.

Meza Kuu: Katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto,  ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald Ndika, wa pili kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Rose Teemba na wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi.
Meza kuu katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wapya wanaoshiriki katika Mafunzo elekezi.


 Sehemu ya Wahe. Majaji wapya wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa akifungua rasmi mafunzo.


Na Magreth Kinabo na Mary Gwera, Mahakama


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa sehemu ya maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama.


Akifungua rasmi Mafunzo elekezi ya awamu ya tano (5) kwa Wahe. Majaji 12 walioteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni, Mhe. Jaji Mkuu aliwaeleza Majaji hao kuendeleza maboresho ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa wananchi bila kuangalia maeneo waliyopo. 


“Mahakama ya Tanzania kwa sasa ipo katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5) pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama (CCP), kwa sasa utekelezaji wake upo katika mwaka wa tatu (3) hivyo nawaalika kuwa sehemu ya muendelezo wa utekelezaji wa maboresho hayo,” alisema Mhe. Jaji Prof. Juma.

Mafunzo hayo yanayofanyika katika Kituo cha Mafunzo na Habari za Kimahakama Kisutu yamefunguliwa rasmi na Mhe. Jaji Mkuu mapema Novemba 18 mwaka huu.

Mbali na hilo, Mhe. Jaji Mkuu aliwataka Majaji hao pia kuzingatia dira na dhima za Mahakama ya Tanzania kwa kuwataka kutoa haki kwa wote na kwa wakati bila upendeleo.


“Mnapotekeleza majukumu yenu msikubali kuingiliwa na mtu yeyote iwe rafiki, mwanafamilia au hata Jaji Mwandamizi juu ya mashauri yaliyopo mbele yenu kwani yapo chini ya mamlaka zenu kikatiba,” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.


Aliendelea kwa kuwataka Majaji hao kusoma na kuzingatia Kanuni za Mwenendo kwa Maafisa wa Mahakama ‘Code of Conduct for Judicial Officers in Tanzania, 1984’ zitakazowaongoza katika utendaji kazi na vilevile kusimamia na kuviishi viapo vyao.

Awali akimkaribisha Mhe. Jaji Mkuu kufungua rasmi Mafunzo hayo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi alimshukuru Mhe. Jaji Mkuu kwa kukubali kuruhusu kufanyika kwa mafunzo hayo yatakayoleta tija kwa Majaji hao.


Mhe. Jaji Kiongozi alisema kwa sasa kuna jumla ya Majaji wa Mahakama Kuu 77 ambao kwa wastani kila Jaji anatakiwa kusikiliza jumla ya kesi 518 kwa mwaka  na kuongeza kuwa ingawa idadi hiyo inaonekana ni kubwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika zikiwemo za kitaaluma bila kuathiri utoaji wa haki.


“Nina imani kwamba uelewa na uzoefu mkubwa walionao Majaji hawa wapya pamoja na mafunzo wanaoenda kupatiwa yatawawezesha kutoa mchango katika safari ya Mahakama kuelekea Mahakama mtandao ‘e-Judiciary’, kutoa haki kwa viwango vinavyotakiwa na kuwa wawajibikaji wazuri,” alieleza Mhe. Jaji Kiongozi.


Mafunzo ya aina hii yamekuwa yakitolewa kwa Majaji wapya ambapo hupata fursa ya kujengewa uwezo na wabobezi mbalimbali wakiwemo Majaji Wakuu Wastaafu, Majaji wa Rufani na wa Mahakama Kuu waliokwisha staafu.Katika mafunzo hayo kutakuwa na wawezeshaji mbalimbali wakiwemo Majaji waliopo kazini na Wataalamu kutoka Taasisi kadhaa katika sekta ya Sheria na Utumishi wa Umma.


KATIBU MKUU WA CCM APOKEA TAARIFA YA MAONI NA MAPENDEKEZO YA WANACHAMA WA TAWI LA CCM CHINA

$
0
0
Katibu wa tawi la CCM China ndugu Yazid Iddi amekabidhi taarifa ya maoni na Mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wanachama wa tawi la CCM China yatakayochakatwa na baadae kuingizwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya 2020-2025.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu Dr. Bashiru Ally akipokea taarifa hiyo amepongeza Viongozi Na Wanachama wa tawi la CCM China kwa kuwa mabalozi wazuri katika kufanya mambo mema yenye tija ya kujenga taifa bora —Novemba 18,2019 —Dodoma,Tanzania

Makatibu Tawala Wa Elimu Nchini Watakiwa Kuhakikisha Mashindano Ya KKKK Yanafanyika Kwa Ustadi

$
0
0
Na, Editha Edward -Tabora .

Makatibu Tawala wasaidizi wa Elimu katika maeneo mbalimbali Nchini wametakiwa Kuhakikisha Mashindano ya Kusoma, kuandika, Kuhesabu na kuchora Yanafanyika kwa ustadi mkubwa kwa kuzingatia weledi na miongozo iliyotolewa na wizara ili kuleta matokeo chanya na hatimaye kupunguza kabisa idadi ya watoto wasiojua Kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora

Akifungua Mashindano hayo ya Kusoma, kuandika Kuhesabu na kuchora Afisa Elimu mkoa wa Tabora Suzan Nusu ambaye amemuwakilisha katibu Tawala mkoa wa Tabora Msalika Makungu ametoa wito kwa wasimamizi wa Mashindano hayo kuzingatia weledi huku akibainisha kuwa Sherikali katika utekelezaji wa dira ya Taifa kuekekea uchumi wa kati ni muhimu watanzania kuweka mkazo katika utoaji wa stadi inayozingatia ujenzi wa stadi za msingi za ufundishaji na ujifunzaji

"Watahini wa kazi hii hakikisheni kuwa mnazingatia usawa na kuepuka upendeleo wakati wote mnapotekeleza majukumu yenu ili tuweze kupata wanafunzi mahiri watakaotuwakilisha vyema kitaifa"Amesema Nusu

Fatuma Shabani ni miongoni wa walimu waliopata mafunzo hayo amesema yatawasaidia kuwafundisha watoto kwa ueledi na ufanisi kwani wamepata uzoefu wa kutosha na maarifa

Aidha Mashindano hayo ya utambuzi yaliyojumuisha mikoa mitano Tabora , Simiyu, Singida Dodoma, na Shinyanga yatasaidia kuwaongezea ujuzi walimu lakini pia Ari katika utendaji wao wa kazi.
Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nusu ambaye amemuwakilisha katibu Tawala mkoa wa Tabora akitoa wito kwenye Mashindano hayo ya kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora
Wanafunzi wa shule ya za msingi mkoani Tabora waliohudhuria katika Mashindano hayo ya Kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora.
Mwalimu akiwaelekeza wanafunzi waliohudhuria kwenye Mashindano hayo kwa michoro

Tume yatakiwa kuimarisha utawala bora

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga baadhi ya machapisho kutoka tume katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Mahiga akiongea na ujumbe waTume ya Haki za Binadamu na Utawala bora uliotembelea ofini kwake mapema Novemba 18, 2019.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kulia kwake). Wengine ni Makamishna wa Tume, kutoka kulia ni Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa, Thomas Masanja, Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga (katikati) akiagana na Mwenyekiti wa tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu. Wengine pembeni waliotabasamu ni Makamu Mwenyekiti Tume, Mohamed Khamis Hamad (kulia), Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli (kushoto), nyuma yake ni Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande.




Na Mbaraka Kambona,

Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuimarisha misingi ya utawala bora nchini ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa jamii.

Waziri Mahiga alitoa kauli hiyo Novemba 18, 2019 katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria baina yake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Mathew Mwaimu.

Akiongea katika kikao hicho, Waziri Mahiga alieleza kuwa tume ni chombo muhimu ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia mambo mawili ambayo ni haki za binadamu na utawala bora.

Waziri Mahiga aliendelea kusema kuwa tume katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake imekuwa ikifanya kazi kubwa katika masuala ya haki za binadamu zaidi ya utawala bora, na hivyo, kuwataka katika awamu hii ya tano wawekeze nguvu zaidi katika kuimarisha misingi ya utawala bora. 

“Tume ni chombo muhimu katika kujenga ustawi wa jamii, hususani kujenga jamii yenye utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu nchini, lakini msisahau kujenga utawala bora”, alisema Mahiga

“Mheshimiwa Rais anaposema serikali hii ni ya wanyonge, anataka wale watu walio kwenye mamlaka walijue hilo na wazingatie utawala bora katika kuhudumia jamii, na nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha misingi ya utawala bora inaimarika nchini”aliongeza Maiga

Katika hatua nyingine Waziri Mahiga aliitaka tume kuieleza na kuifafanulia jamii utekelezwaji wa haki za binadamu unavyotekelezwa kwa vitendo na serikali ya awamu ya tano.

Mahiga alisema pamoja na changamoto zinazopigiwa na kelele na wadau wa masuala ya haki za binadamu, lakini ni ukweli uliowazi kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza na inaendelea kutekeleza haki mbalimbali kwa vitendo na kuhakikisha haki hizo wananchi wanazipata.

Alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza kwa vitendo haki ya kupata elimu kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi mpaka sekondari.

Pia, alieleza kuhusu haki ya afya ambapo wazee wameanza kupata matibabu bure, na upatikanaji wa bima ya afya kwa wananchi.

“Hizi jitihada zote za serikali katika kuwapatia huduma wananchi bado hazijaelezwa vya kutosha, tume tumieni nafasi yenu kuyaeleza haya kwa jamii iweze kuelewa”alisisitiza Mahiga

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome alimueleza Mwenyekiti wa tume kuwa masuala ya haki za binadamu yanafanywa na taasisi nyingi na hivyo kipindi hiki wawekeze nguvu zao katika kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria nchini.

“Tume ni lazima muonekane mnachukua hatua, wekeni mkakati wa viashiria vya kubaini haraka changamoto zinazoelekea kuathiri utawala bora na kuzifanyia kazi”, alisema Mchome

Akizungumza mapema, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alimueleza Waziri Mahiga dhamana waliyopewa wataitumia vyema katika kusaidia serikali kutimiza lengo lake la kuifikisha nchi katika uchumi wa kati.

“Tume itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na tutatekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia taratibu, sheria na katiba ya nchi”alisema Mwaimu

Mwenyekiti huyo wa Tume alikwenda kutembelea Wizara ya Katiba na Sheria kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri Mahiga ikiwa ndio mara yake ya kwanza tangu alipoapishwa Novemba 4, 2019.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliongozana na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad, na Makamishna wengine watano ambao ni Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

MSANII RAY C ALITUMBUKIA KWENYE DAWA ZA KULEVYA, AKAJINASUA.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Oktoba, 2019.


“Kizuri hakikosi kasoro” msemo huu wa Kiswahili umejidhihirisha wazi kwa msanii Rehema Chalamila, ambaye ni mrembo mwenye sifa zote za kike, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii la Ray C.

Aliwahi kujitumbukiza kwenye ‘janga’ la matumizi ya dawa za kulevya, lakini baadaye aliamua kujinasua kwa kuachana nayo.

Ray C ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, aliyejaaliwa kuwa na umbo la kupendeza, sauti nyororo, sura nzuri inayopambwa na macho yenye mvuto.

Uhodari wake wa kuzinyonga nyonga umemfanya kuwa maarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Rahema alizaliwa mkoani Iringa, Mei 15, 1982, amejaaliwa kuwa uwezo mkubwa wa kuimba muziki wa R&B, dansi, Afro-Jazz, Taarab hata Bongo-Bhangra.

Kabla ya kujihusisha na muziki, aliwahi kufanya kazi ya utangazaji wa redio ya Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam.Mwaka 2003 Ray C alitoka na albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la ‘Mapenzi Yangu’.

Msanii huyu aliendelea kujulikana zaidi baada ya kuachia vibao vingine kadhaa kama vile, Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Nawewe Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu zaidi.Juhudi zake katika muziki, hatimaye Ray C akatokea kuwa mwimbaji maarufu aliyeutingisha muziki wa Bongo Fleva kati ya miaka ya 2003 na 2009.

Sifa zake nzuri zikatambaa kila kona, lakini akaja kuzichafua baada ya kuingia matatani, kiafya alipoanza kutumia dawa za kulevya.

Dawa hizo zilimtesa kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012, ambapo Rais wa Tanzania wakati huo, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alimpa msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu yake.

Alianza matibabu bila kuchelewa na mara baada ya kupona, msanii huyo Rehema Chalamila a.k.a Ray C, alikwenda kumtembelea Rais Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliompatia wakati alipokuwa mgonjwa.Katika ziara hiyo Ray C alifuatana na mama yake mzazi Margaret Mtweve na dada yake Sarah Mtweve.

Akiwa Ikulu, alimweleza Rais Kikwete kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za washabiki wake waliokuwa wamemkosa kwa kipindi kirefu.

Kwa apande wake, mama mzazi wa Ray C, alimshukuru Rais kwa kuokoa maisha ya bintiye.Mama huyo akatoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya matibabu ya Ray C, waache kufanya hivyo kwani yamegharamiwa na Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka Ikulu, Rais alimpongeza Ray C kwa kuikubali hali yake ya kiafya, pia kukubali kupata matibabu ambayo alikuwa akiendelea nayo chini ya uangalizi maalum.

Lakini kama Waswahili wasemavyo kuwa “Sikio la kufa halisikii dawa”, katika hali ya kushangaza na kusikitisha, Ray C, alikumbwa na mikasa mingi ukiwemo wa mwaka wa 2016, ikaripotiwa kwamba amerudia tabia yake ya kutumia dawa za kulevya!

Taarifa hizo zilipomfikia Rais Kikwete, zilimsikitisha na kumkera sana.

Licha ya matatizo yake hayo, Ray C, alifanya kazi kwa kuachia albam za Mapenzi Yangu ya mwaka 2003, na Wewe Milele ya mwaka 2004, Sogea Sogea ya mwaka 2006 na Touch Me ya 2008.

Ray C, alikwisha twaa Tuzo kadhaa katika kazi zake, zikiwemo za msanii bora wa kike kwa mwaka 2004.Ray C alishiriki na kufanikiwa kupata tuzo za Msanii bora Afrika ya Mashariki mwaka 2005, shindano lililoandaliwa na Channel O Music Awards.

Mwaka 2006 kampuni ya Pearl of Africa Music Awards, ilimtunuku tuzo ya Msanii bora wa kike Tanzania.Aidha alitwaa tuzo ya msanii Bora wa kike kutoka Uganda na Tanzania na mwaka 2007.

Ray C alinyakua tuzo ya Msanii bora wa kike Tanzania mwaka 2007 na 2008, zilizotolewa na Pearl of Africa Music Awards.

Mwaka 2011 Tanzania Music Awards ilimpa tuzo kwa Video bora, Wimbo bora, Wimbo bora wa Afro Pop na Wimbo bora wa kushirikishwa wa 'Mama Ntilie', akishirikiana na Gelly wa Ryme & AT.

Ray C katika baadhi ya kazi zake aliwahi kuwashirikisha wasanii wengine kama Dknob, Chid Benz, Mheshimiwa Temba, Squeezer pamoja na Nako Nako.

Mapema Januari 02, 2018 msanii huyo wa muziki wa Bongo Fleva Rehema Chalamila (Ray C), alimuomba Rais John Pombe Joseph Magufuli kupitisha sheria kama aliyofanya Sultan Qaboos wa Oman.

Rayc C aliaandika ombi hilo kupitia ukurasa wake wa instagram 

“Mzee mi na shida Moja! hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji Sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili! Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman! Hakuna mahusiano ya Kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa! 

“Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila Cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea! Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe! Utakuwa umewanyoosha kisawasawa hawa Wanaume zetu. Tutaheshimiana! 

Msanii huyo mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, alimuanika kwenye mitandao ya kijamii mpenzi wake mpya.

Ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na Rapa Lord Eyes, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumtambulisha mpenzi wake huyo.

Kila la heri Rehema Chalamila aka Ray C, baadhi ya wadau wa muziki huo wanakusihi kuachana kabisa na dawa za kulevya.


Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao ya kijamii.
Mwandaaji wa makala hii anapatikana kwa namba: 0713331200, 0736331200, 0767331200 na 0784331200.

MAMBO YA MKESAHA WA MWAKA MPYA DMV MAREKANI

WAZIRI MKUU AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA FEDHA NDANI YA BENKI YA CRDB KUJIWEZESHA KIFEDHA ILI KUMALIZA MIRADI KWA WAKATI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitambulishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela (katikati) kwa Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRD Dkt. Joseph Witts wakati alipowasili kufungua Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini lililofanyika Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.
David Jere, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi (CRDB) akihutubia wakati wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni Kanda ya Kusini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kongamano lililo andaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wakandarasi ,wazabuni na wafanyabishara wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, lilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu, mjini Mtwara. Kongamano hilo lililenga kuwapatia washiriki hao elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo wanazozichukua kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, wakandarasi ni sekta muhimu sana katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hivyo wanapaswa kuboresha utendaji kazi wao kwa kuchukua mikopo toka taasisi za fedha na mabenki. Ameongeza kuwa, changamoto kubwa inayowakabili wakandarasi wengi ni ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ambapo changamoto hiyo huchangia kutomalizika kwa miradi kwa wakati.

“Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni vilivyo, changamkieni fursa hizo ili muweze kukuza biashara zenu na kupata faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana wetu na hatimaye kulipa kodi stahiki za serikali. Ni matarajio yangu kuwa, baada ya kongamano hili tutaona utofauti mkubwa kutoka kwa wakandarasi na halmashauri, ambao wamekuwa wakipitia changamoto katika kukamilisha miradi yao, kutokana na suala la mapato na ukwasi” alisema Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Majaliwa pia alipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa miondombinu mbalimbali ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi.

Alisema “Benki ya CRDB imekuwa ina fadhili miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika jitihda zake za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Tunatambua na kuthamini sana ushikiri wa Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi wa umeme wa maji katika bonde la Rufiji (Nyerere Hydro Power Project) na ule wa kusambaza nishati ya umeme vijijini yaani REA.

Kipekee kabisa niwapongeze tena Benki ya CRDB kwa utayari wenu, ambao mmekuwa mkiuonesha katika kuisaidia Serikali, hususan katika utekelezaji wa miradii mikubwa ya kimkakati”. alisema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema kuwa,kongamano hili ni fursa pekee ya kuwakutanisha wakandarasi, wazabuni na wafanyabisahra ili kuwajengea uwezo na kuwajulisha fursa mbalimbali za kifedha zilizomo ndani ya benki ya CRDB, na namna ya kuzitumia fursa hizo ili kukuza miradi na biashara zao.

“Tuna bidhaa nyingi mahususi kwa ajili ya kundi hili la wateja ikiwamo: Purchase Order Financing, Contract financing, and Invoice Discounting ambazo hazihitaji dhamana yoyote kutoka kwa Mkandarasi au mzabuni pindi anapotaka kukopa. Zaidi ya hilo, Benki pia hutoa mikopo kwa ajili ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, magari, mashine, Mabasi na huduma nyingine kama vile dhamana ya malipo ya awali (Advance Payment Guarantee), dhamana ya Utekelezaji wa Miradi (Performance Guarantee), Barua za Mikopo (Letters of Credit), Huduma za Bima na pia tunatoa mikopo ya muda mfupi kama mitaji ya kufanyia kazi” alisema.

Naye mmoja wa Wakandarasi Henry Shimo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chibeshi constructions Ltd , amesema kuwa, swala zima la uwezeshwaji wa mikopo hiyo litawasaidia kwa kiasi kikubwa sana wakandarasi hao kumaliza miradi yao kwa wakati kwani changamoto kubwa ilikuwa ni mitaji kwa ajili ya kuendeleza miradi yao. Amesema kuwa, kinachotakiwa kikubwa ni uaminifu wa wakandarasi katika kujua fedha wanayopewa inahitaji kufanyiwa kazi na kurudishwa kwa wakati.

Benki ya NIC yatoa mchango wa magodoro kwa shule ya sekondari ya wasichana Loyola

$
0
0

 Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume, amewaasa wanafunzi wa shule ya sekondari Loyola kujifunza kwa kuzingatia mtizamo mpana wa kidunia ili kuendana na mfumo wa sasa wa kielimu wa kidunia unaohitaji wahitimu wenye uwezo mkubwa wa kuelewa mambo na matatizo mbali mbali na kisha kuyatafutia suluhisho.

Karume aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 21 ya shule hiyo alitoa wito huo, sambamba na kukabidhi mchango wa magodoro 100 kwa ajili ya kuboresha mazingira wanayoishi wanafunzi wa shule hiyo.

Mkurugenzi huyo pia aliwaambia wanafuzi wa Loyola kuwa ili kuendana na dunia ya sasa, wanatakiwa kufanya jitihada binafsi za kutafuta maarifa na ujuzi na siyo tu kutegemea kile wanachofundishwa na waalimu wao darasani  na kusisitiza kuwa bado wana safari ndefu.

“Elimu mliyoipata bado ni ya hatua za mwanzo tu, hasa ukizingatia kukua kwa utandawazi. Kutokana na mabadiliko makubwa yanayoenda sambamba na ukuaji wa haraka wa Sayansi na Teknalojia yanayomgusa kila mtu na katika kila nyanja ya maisha, sote tutalazimika kuendelea form 6 kujifunza mambo mapya hadi mwisho wa maisha yetu,” alisema

Karume aliwaambia wahitimu hao watarajiwa kwamba ni wajibu wao kuendelea kujifunza mbinu mpya za kuyakabiliana na maisha na pia kujijengea uwezo wa kujiajiri pindi watakapomaliza elimu ya juu

Elimu mliyopata na ambayo mtaendelea kuipata itafungua maisha yenu na ya jamii nzima ikiwa ni pamoja na familia zenu na watoto wenu. Elimu hii pia itawapa uwezo wa kiuchumi, itawapa uwezo wa kuwa na sauti, mtaongea, mtasikika na kusikilizwa, pia itawajengea heshima katika jamii na kuwapa uwezo wa kuchangia mambo mbali mbali katika maisha. 

Aliwataka kuiga mifano ya wanafunzi waliosoma shuleni hapo na ambao wamefanikiwa kimaisha baadhi yao wakiwa ndani na wengine nje ya nchi

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Padri Obwanda Meyo, SJ alimuhakikishia mgeni rasmi kuwa wanafunzi wake wamejiandaa vizuri kwa ajiili ya mitihani ya mwisho na hivyo watafanya vizuri 
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (kushoto) akiwa ni mgeni rasmi wa sherehe ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Loyola akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi  milioni 4.7/- kwa mkuu wa shule hiyo Father Ubwanda Meyo jana, ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki ya NIC kwa ajili ya kununulia magodoro 100 yatakayotumika kwenye mabweni ya wasichana wa  shule hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akizungumza na wageni waalikwa , wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Loyola waliohudhuria kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne shule hiyo jana jijini Dar es salaam
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari Loyola, Padri Obwanda Meyo (wa tatu kulia), mwakilishi wa wazazi watoto wa kidato cha nne, Joseph Tadayo (kulia), Brigitte Asenga na Annah Lupembe (kushoto) ambaye ni meneja wa tawi la NIC Kariakoo.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akifurahi na wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Loyola.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili kulia mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Loyola, Mkuu wa Shule Padri Obwanda (aliyebeba mtoto), Mwakilishi wa wazazi, Joseph Tadayo , Mwenyekiti wa PTA Luyola, Brigitte Asenge na Meneja wa Tawi la NIC Kariakoo, Annah Lupembe (mwisho kushoto)
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume akiwa na kikombe alichopewa zawadi na uongozi wa shule ya sekondari Loyola.












WANAODHANI CCM ITANGO’KA MADARAKANI WAMECHELWA-KALLI

$
0
0

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, amesema CCM wanaodhani itaondoka madarakani wamechelewa bali itaendelea kuongoza nchi kutokana na misingi yake na kukubalika kwa wananchi.

Alisema vipo vyama barani Afrika vilianguka na kuondoka madarakani sababu ya viongozi wake kushindwa kusimamia misingi lakini si kwa CCM.

Kalli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bwiru jana kuwa, CCM itendelea kuongoza na kushika kwa miaka 100 kutokana na uimara wa misingi yake na jinsi inavyokubalika kwa wananchi.

“Zipo nchi zinaongozwa kifalme,kidini na kisiasa.Tanzania inaongozwa kisiasa chini ya Chama Cha Mapinduzi , hivyo kitendelea kuongoza kwa muda mrefu kutokana nakutekeleza mmbo mengi ya kijamii, wenye ndoto kuwa kitaondoka madarakaniwamechelewa sana,”alisema.

Katibu wa CCM mkoani humu alisema tangu nchi ipate Uhuru mwaka 1961 ni mengi yamefanywa katika sekta mbalimbali ukiwemo ujenzi wa shule, hospitali, vituo vyaafya na zahanati, reli,miundombinu ya barabara na maji, yote hayo si miujiza nikazi ya CCM.
Alisema wakati nchi inapata Uhuru akina mama walijifungulia vichakani, kulikuwa na shule 22 za sekondari lakini leo kila kata ina shule ya sekondari na nyingine zaidi yamoja na akina mama wanajifungulia vituo vya afya na hospitali.

Kallia alifafanua kuwa Mwalimu Nyerere aliweka misingi ya usimamizi wa elimu wakiwemo viongozi wengine waliofuata baada yake na sasa Rais John Magufuli anatoa elimubure huku wazazi wakibaki kuangalia mahitaji mengine ya watoto, malezi na nidhamu.

“RaisMagufuli amenunua ndege lakini wapo wanaopinga hazina maana, si lazima tuzipande wote la hasha.Wataokazipanda watalipa nauli na serikali itaongeza shule nyingine na kutoa huduma zingine kwa wananchi,”alisema Kalli.

Alielea kuwa elimu wanayoitafuta itawapa heshima wanafunzi haona hivyo hawana budi kujibibidisha kwenye masomo ili wapatikane wana sayansi wakumrithi Rais Magufuli, maprofesa,madaktari na watalaamu wa kada zingine lakini pia wajenge uzalendo kwa nchi yao kabla na baada ya masomo .
Aidha,Kalli ambaye alikuwa shuleni hapo kushiriki na wanafunzi wa klabu ya Jogging kufanya mazoezi ya kujenga mwili alitumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi hao pamoja na jamii kufanya mazoezi yakuimarisha miili yao na kujenga afya ili kuepukana na maradhi.sss

WANAFUNZI WA SHULE YA BWIRU GIRLS WAFANYA JOGGING

$
0
0
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana jana baada ya kufanya nao mazoezi ya kiungo pamoja. PICHA ZOTE NA BALTAZAR MASHAKA MWANZA.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana akiwaongoza wanafunzi wa shule hiyo kufanya mazoezi pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, wa tatu kutoka kukaa akishikiru mazoezi ya viungo pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana jana.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana wakifanya mazoezi ya kujenga mwili pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, wa pili kutoka kila jana.

MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA KUZUNGUMZIA NAMNA YA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mbele) wakiwa kwenye kikao kazi na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kikao kazi hicho kilikuwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Waziri huyo ndiye mwenye dhamana ya kushughulikia masuala ya muungano.


……………………..

Na James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman wamefanya kikao kazi kujadili namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma kwa umma pamoja na kuimarisha Muungano ili uendelee kuwa na tija kwa wananchi.

Akifungua kikao kazi hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema pamoja na kujadili masuala ya kuboresha huduma pia kililenga kuimarisha muungano ili kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa taifa letu Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, katika kikao kazi hicho wameweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wa pande zote mbili za muungano ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema wao kama mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wanataka ushirikiano wa taasisi zinazoshughulikia masuala ya kiutumishi na utawala bora uendelezwe kwa vitendo kwa ajili ya manufaa ya wananchi.



Mhe. Suleiman amesisitiza kuwa, ushirikiano huu una manufaa katika kuboresha huduma zitolewazo na taasisi za umma kwa wananchi na una tija katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Taasisi za Umma nchini.



Mhe. Suleiman amewataka wajumbe wa kikao hicho, kuhakikisha misingi madhubuti ya kiutendaji iliyojengwa katika kikao kazi hicho inaimarishwa ili utekelezaji wake uwe wa vitendo na uweze kuwa chachu ya kutoa huduma bora kwa wananchi.



Masuala yaliyojadiliwa katika kikao kazi hicho kudumisha ushirikiano katika masuala ya Ajira, Serikali Mtandao, Udhibiti wa rushwa, Usimamizi wa Maadili ya Viongozi, Mafunzo kwa Watumishi wa Umma, Utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Utumishi wa Umma, Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma, Uandaaji wa Miundo na Mifumo ya Taasisi na Utawala Bora kwa ujumla.

Mwekezaji sekta ya Utalii, akabidhi Serikali shule aliyokarabati Babati

$
0
0
Shule ya msingi vilima vitatu, ambayo amekarabati madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo na kuweka madawati na vitatu ukarabati ambao umefanywa na Taasisi ya Chemchem Association na amekabidhi umegharimu zaidi ya sh 54.2 milioni.
 Mkuu wa wilaya Babati Elizabeth Kitundu akiwa na watendaji wa taasisi ya chemchem na viongozi wa kijiji cha vilima vitatu wakiwa wanatembelea shule ya msingi Vilima vitatu.

Mwandishi wetu,Babati. 

Mwekezaji katika sekta ya Utalii, wilayani Babati mkoa wa Manyara,Taasisi ya chemchem association, amekabidhi shule ya msingi vilima vitatu, ambayo amekarabati madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo na kuweka madawati na vitatu ukarabati ambao umegharimu zaidi ya sh 54.2 milioni.

Shule ya msingi vilima vitatu ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madarasa, vyoo, nyumba na walimu na madawati na kusababisha wanafunzi kusoma chini.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi shule hiyo, mkuu wa wilaya babati Elizabeth Kitundu ,kukarabatiwa na kujengewa majengo mapya katika shule hiyo, ni mchango wa mwekezaji huyo katika kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha elimu.

Kitundu ameipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika sekta ya elimu pia amewataka waendelee kushirikiana na wananchi wa Kijiji hicho ambacho kampuni hiyo, imewekeza katika utalii wa picha na hoteli.

" Maendeleo yanakuja kwa kuletwa na elimu hivyo ninaomba muendelee kushirikiana ili kuleta maendeleo katika Kijiji hiki ili kutatua changamoto zilizopo hapa". alisema

Alisema hata hivyo, kampuni hiyo ambayo imewekeza ndani ya hifadhi ya jamii ya Burunge, inahimiza wananchi kutunza wanyamapori na kuacha vitendo vya ujangili lakini pia kutunza na mazingira ili watalii waendelee kufika katika maeneo yao na hivyo kupatikana fedha za misaada.

“kama tukiendelea kutoa ushirikiano kwa mwekezaji huyo, kuacha kuharibu mazingira watalii watakuja zaidi na hivyo wao wanafaidika na sisi wananchi na serikali tutaendelea kunufaika”alisema

Afisa maendeleo ya jamii ya taasisi ya Chemchem ,Walter Pallangyo alisema pallango alisema wataendelea kushirikiana vizuri na wananchi katika kusaidiana elimu Bora pamoja na mahitaji mengine .

Pallango aliwaomba wananchi kuendelea kutunza mazingira na uhifadhi wa wananyama kwani mazingira yanapokuwa mazuri tunapata wageni wengi maana fedha hizo zinatokana hifadhi hiyo ili wazidi kufanya maendeleo

Afisa mtendaji wa Kijiji Husna Shabani amesema kuwa taasisi hiyo inatijitoa kwa hali na Mali katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo , ikiwa marekebisho yaliyofanyika ni vyumba vya madarasa nane ,ofisi za walimu mbili, nyumba za walimu tatu,ujenzi wa vyoo vya matundu manne pamoja na madawati Mia moja 100 vyote hivyo vikiwa na thamani ya sh 54.2 milioni.

Husna aliendelea kusema hata hivyo taasisi hiyo imeweza kuwaletea vitabu vya kufundishia vyenye gharama ya sh 325,700 hivyo shule hiyo imekuwa na mafanikio katika taaluma Kila mwaka mwaka.

“mwaka ,2017 walifanya mtihani 23 na walifaulu wote pia 2019 walifanya mtihani 20 na walifaulu 19 kwa wastani alama ya 150 kupitia maboresho hayo hali ya taaluma itaboreka na utoro unapungua k na matunda ya ukarabati huo umetokana na hifadhi ya jamii burunge”alisema

Akizungumza mkuu wa shule vilima vitatu Denis Mtui alishukuru chemchem kwa kuweza kukarabati shule hiyo maana awali shule hiyo ilikuwa chakavu Sana katika sekta zote tofauti na Sasa shule hiyo inatia hamasa ya kuonekana shule Bora kimuonekano na kielimu pia.

Mtui alisema aliahidi watatunza shule hiyo na kuendelea kukarabati inapopata shida pia anaomba wananchi kuwa naushirikiano mzuri katika kuleta maendeleo yaliyonatija katika jamii ikiwepo kuacha matukio ya kuvamia maeneo ya mwekezaji kuingiza mifugo.

WAZIRI KAMWELWE: AfDB ENDELEENI KUFADHILI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BARABARA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo katika kikao kilichomkutanisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Wakurugenzi kutoka Sekta ya Ujenzi, jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa taarifa ya miradi ya barabara iliyotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Amos Cheptoo, alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amos Cheptoo (kushoto), akisisitiza jambo katika kikao kilichomkutanisha Mtendaji huyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na wakurugenzi kutoka Sekta ya Ujenzi, jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kulia), akimwonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amos Cheptoo (kushoto), miradi ya barabara iliyotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki hiyo, jijini Dodoma.
Wakurugenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (hayupo pichani), katika kikao kilichomkutanisha Waziri huyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amos Cheptoo, alipofika ofisini kwake na kufanya mazumgumzo nae kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya barabara inayofadhiliwa na Benki hiyo, jijini Dodoma.


…………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuendelea kutekeleza mkakati wake wa ufadhili wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya barabara.

Ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati Waziri huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo kuhusiana na maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara inayofadhiliwa na benki hiyo.

“Tunawashukuru AfDB kwakuwa miongoni mwa wadau muhimu katika kutoa ufadhili wa utekelezaji na uboreshaji wa barabara nyingi nchini, tunaomba muendelee na ufadhili kwani bado tunahitaji kuendelea kuunganisha mtandao wa barabara kati yetu na nchi jirani”, amesema Waziri Kamwelwe.

Aidha, Waziri huyo amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka 11 iliyopita Benki hiyo imetoa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi Trilioni mbili (2) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 1,655 ambapo kati ya hizo kilometa 1,168 zimeshakamilika na kilometa 487 bado zinaendelea na ujenzi wake.

Ametaja baadhi ya miradi ya barabara iliyofadhiliwa na Benki hiyo na ambayo imekamilika kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo ni ukarabati wa barabara ya Arusha – Namanga (km 105), barabara ya Singida – Babati – Minjingu ( km 223.5), barabara ya Iringa – Dodoma (km 260) na barabara ya Namtumbo – Tunduru (km 193).

Ameongeza kuwa miradi mingine ya barabara inayoendelea kutekelezwa kupitia ufadhili wa Benki hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 349), barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka kwa Awamu ya II, barabara ya Tanga – Pangani – Bagamoyo (km 246), barabara za mzunguko katika jiji la Dodoma, na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Msalato jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB, Amos Cheptoo, amesema kuwa AfDB itaendelea kuunga mkono na kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara lengo ni kuifanya Afrika kuendelea kiuchumi.

Amesema kuwa lengo la kuja kwake Tanzania ni kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki hiyo ili kuona maendeleo yake.

MBINU ZA WIZARA YA MAJI ZIMEKUJA NA UTATUZI WA HUDUMA YA MAJI MIJI MIKUU YA MIKOA

$
0
0

Na Ismail Ngayonga,MAELEZO
DAR ES SALAAM


Maji ni hitaji muhimu sana katika ukuaji wa uchumi  na hii inatokana na ukweli kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote duniani  yawe ya viwanda, kilimo na kadhalika yanategemea maji.
Aidha Maji ni hitaji muhimu sana katika uhai wa mwanadamu na viumbe wengine na ndio maana maji hayana  mbadala na pia bila maji hakuna uhai na hivyo serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji ili kuimarisha uendeshaji na utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.
Huduma za maji mijini hutolewa kupitia Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwenye Miji Mikuu ya Mikoa 23 pamoja na Dar es Salaam; Miji Mikuu ya Wilaya 99, Miji Midogo 14; na miradi 8 ya maji ya Kitaifa ili kufikia malengo yaliyopo ya kuboresha huduma hiyo katika Miji Mikuu ya Mikoa kutoka asilimia 86 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020
Taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Maji inaonesha kuwa mwaka 2016, Uzalishaji wa majisafi maeneo ya mijini umeongezeka kutoka lita milioni 385 kwa siku mwezi Aprili 2015 hadi kufikia lita milioni 470 kwa siku mwezi Machi, 2016 sambamba na ongezeko la idadi ya wateja waliounganishiwa huduma ya maji kuongezeka kutoka kutoka 362,953 mwezi Aprili, 2015, hadi wateja 405,095 mwezi Machi, 2016 ambapo wateja 392,942 sawa na asilimia 97 wamefungiwa dira za maji.
Aidha makusanyo ya maduhuli kwa mwezi yatokanayo na yatokanayo na mauzo ya maji yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 7.28 mwezi Aprili, 2015 hadi kufikia Tsh. Bilioni 8.50 mwezi Machi 2016 sawa na ongezeko la asilimia 17.
Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika sekta ya maji nchini, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikuu ya Mikoa ili kufikia asilimia 95; na Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2020.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa anasema katika mwaka 2018/2019, Serikali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini kwa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi na majitaka pamoja na kuzijengea uwezo Mamlaka za Maji Mijini.
Akbainisha baadhi ya Miradi inayotekelezwa na Serikali katika Miji Mikuu ya Mikoa, Waziri Mbarawa anasema katika Manispaa ya Kigoma Serikali kwa kushirikiana na  na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya inatekeleza mradi wa usambazaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa gharama ya Euro milioni 16.32, ambapo hata hivyo mwaka 2018 Serikali imesitisha mkataba na mkandarasi wa mradi huo kutokana na uwezo mdogo wa mkandarasi.
‘’Hadi kuvunjwa kwa mkataba, utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 87 na mradi ulikuwa umeanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi, kutokana na hali hiyo, Wizara imechukua jitihada za kuhakikisha huduma iliyokuwa ikitolewa kwa wakazi wa Mji wa Kigoma inarejeshwa kwa kuajiri mkandarasi wa kuweka mitambo ya muda ya kusukuma maji’’ anasema Waziri Mbarawa.
Kuhusu Jiji la Arusha,, Waziri Mbarawa anasema Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji majisafi na uboreshaji wa huduma ya uondoaji wa majitaka katika Jiji la Arusha kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 233.9.
Anaongeza kuwa Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na uchimbaji wa visima virefu 56, ujenzi wa matanki 10; ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji, upanuzi na ukarabati wa mtandao wa mabomba ya majisafi, upanuzi na ukarabati wa mtandao wa majitaka, ujenzi wa mabwawa mapya 18 ya majitaka, ujenzi wa ofisi ya Mamlaka; ununuzi wa vitendea kazi na kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi.
Akifafanua zaidi Waziri Mbarawa anasema hadi mwezi Aprili 2019, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020, ambapo kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 200 kwa siku na muda wa upatikanaji wa huduma ya majisafi utaongezeka kutoka wastani wa saa 12 za sasa kwa siku hadi saa 24.
Waziri Mbarawa anasema katika Manispaa ya Lindi, Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya inatekeleza mradi wa majisafi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Lindi unaogharimu Euro milioni 11.7 ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017 lakini haukukamilika kutokana na uwezo mdogo wa kiutendaji wa mkandarasi.
Anasema kuwa Serikali ilichukua hatua ya kuvunja Mkataba na Mkandarasi huyo mwezi Oktoba 2018 ambapo utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 92.3 na unatoa huduma ya maji kwa wakazi wapatao 81,343 wa Mji wa Lindi, ambapo kazi zilizobaki ni kufunga mfumo angalizi wa uzalishaji maji, ununuzi wa gari la uondoaji majitaka na kurekebisha maeneo yenye mapungufu katika mradi huo.
Aidha Waziri Mbarawa anasema katika mpango wa muda mfupi wa kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Njombe, Serikali imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa chemchemi ya Kibena uliogharimu Tsh. bilioni 1.1, ukihusisha  ujenzi wa kidakio cha maji, ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa kilomita 2.2 na ufungaji wa pampu mbili za kusukuma maji zenye uwezo wa kuzalisha lita 72,000 kwa saa.
Kukamilika kwa mradi huo kumeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 480,000 hadi lita 864,000 kwa siku na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika Hospitali ya Kibena, Chuo cha Uuguzi, na Ofisi za Makao Makuu ya Mkoa na hivyo kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Njombe kutoka asilimia 69 mwaka 2016 hadi asilimia 87 za sasa.
Ili kufanikisha malengo yaliyopo, ni wajibu wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika miji mikuu ya Mikoa kuimarisha hali ya Uzalishaji wa majisafi pamoja na kupunguza kiwango cha upotevu wa maji pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma iliyo bora na endelevu kwa wananchi.

TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA AALCO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akizungumza wakati hafla ya Maadhimisho ya Miaka 63 ya kuanzishwa kwa Shirika la Mashauriano ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (AALCO) yaliyofanyika jijini New Delhi tarehe 15 Novemba 2019. 
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda [kushoto] akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Shirika la Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika [AALCO], Prof. Kennedy Gastron wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 63 ya kuanzishwa kwa shirika hilo, Jijini New Delhi tarehe 15 Novemba 2019 
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika meza moja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 63 tangu kuanzishwa kwa Shiriko la AALCO 
Wageni waalikwa wakiwa kwenye maadhimisho 
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi pamoja na Maafisa Ubalozi wa nchi wanachama wa AALCO walioshiriki hafla ya maadhimisho ya miaka 63 ya kuanzishwa kwa shirika hilo, Jijini New Delhi tarehe 15 Novemba 2019.


Ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Mashauriano ya masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (AALCO) kuendelea kuimarika


Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amemwakilisha Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria na Rais wa sasa wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (Asia-Africa Legal Consultative Organization-AALCO) kwenye sherehe ya miaka 63 ya kuanzishwa kwake. Sherehe hiyo imefanyika Jijini New Delhi tarehe 15 Novemba 2019 na kuhudhuriwa na nchi wanachama wageni waalikwa, wenyeji na mashirika ya kimataifa yaliyopo New Delhi.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mhe. Mahiga, Balozi Luvanda alielezea uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na AALCO na kueleza kuwa utaendelea kudumishwa kwa manufaa ya pamoja.

AALCO ilianzishwa tarehe 15 Novemba 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika. Toka kuanzishwa kwake AALCO imewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.

Ushirikiano kati ya Tanzania na shirika hilo ulianza tangu mwaka 1965 ambapo Tanzania ilishiriki katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AALCO kama nchi Mwangalizi na baadaye mnamo mwaka 1973 kama nchi mwanachama rasmi. 

Mpaka sasa Tanzania imeshaandaa Mikutano mikubwa 3 ya Mwaka ambapo Mkutano wa 25 wa AALCO ulifanyika mwaka 1986 jijini Arusha, Mkutano wa 49 ulifanyika Jijini Dar es Salaam mwaka 2010 na Mkutano wa 58 ulifanyika hivi karibuni, jijini Dar es Salaam tarehe 21 hadi 25 Octoba 2019. 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS WA AFRIKA KUSINI PAMOJA NA MJUMBE MAALUM KUTOKA KWA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed Waziri wa Nchi wa Ethiopia Hirut Zemene mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum wa Rais huyo Waziri wa Zamani wa Nishati wa Afrika Kusini Jeffrey Radebe mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe Maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed iliyowasilishwa kwake na Waziri wa Nchi wa Ethiopia Hirut Zemene mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaa .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Waziri wa Zamani wa Nishati wa Afrika Kusini Jeffrey Radebe mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Waziri wa zamani wa Nishati wa Afrika Kusini Jeffrey Radebe mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

WAMILIKI WA KUMBI ZA MIKUTANO WATAKIWA KUKIMBILIA FURSA YA KUTANGAZA UTALII WA NDANI.

$
0
0
     
   Na.Khadija seif, Michuzi TV

WAMILIKI wa kumbi za mikutano na starehe wametakiwa kuutangaza utalii wa ndani pindi wageni na wenyeji wanapotembelea sehemu hizo.

Akizungumza na Michuzi tv Meneja wa Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam Shaban Karuse amesema wakati mwengine tusione wasanii tu na watu maarufu ndio wenye dhamana ya kuutangaza utalii na vivutio vingine peke yao bali hata wamiliki wa kumbi wanatakiwa waione fursa hiyo mara moja.

"Kwa kuthamini mchango wa utalii sisi tumeamua kunyanyua sanaa ya ubunifu ikiwemo ya mavazi na vitu mbalimbali na ukifika hoteli yetu ya serene iliyopo hapa Dar es salaam utapata vitu vya kibunifu na vya asili ya kitanzania na hata nakshi nakshi na mapambo yaliyopambwa katika hoteli hii ni ya asili ya kitanzania mfano milango,viti pamoja vitu vingine ni vya kinyumbani.

Aidha, Karuse amefafanua mbali na vitu hivyo karuse ameeleza kuwa hoteli hiyo imeona fursa pekee ya kunyanyua na kukuza Sanaa ya ubunifu na ndio maana kila siku ya jumamosi kunakuwepo wabunifu na meza zao ili kuuza bidhaa zao kwa watu wanaofika hotelini.

"Ipo wazi kuwa kila jumamosi ni sikukuu ya wabunifu kwa hapa hoteli ya Serena na hakuna malipo yoyote kwa mbunifu anaetaka kushiriki katika gulio hilo,"

Pia ametoa wito kwa watanzania kuwa wazalendo na kuthamini vitu vya kinyumbani na kuacha kununua nguo kutoka nchi za wenzetu kwani kununua vya kinyumbani ni mojawapo ya kuwa mzalendo.

"Batiki,vitenge,kaniki ,vibwaya ni mavazi ambayo yanapatikana hapa nchini na watalii wakifika hapa nchini wanaonyesha uzalendo kwa kuvinunua kwanini sisi wenye tusivinunue na tusiwatie moyo wabunifu wetu ambao wapo na wanatengeneza vitu vizuri na vya kiasili na vyenye ubora,"

Hata hivyo karuse amesema kwa kuthamini mchango wa wabunifu hoteli hiyo imeamua kudhamini wiki ya Maonyesho ya  12 ubunifu wa Mavazi (Swahili fashion week) ya mbunifu mkongwe hapa nchini Mustafa Hassanali.
Meneja wa hoteli ya serena ya jijini Dar es salaam akitolea ufafanuzi juu ya kutangaza utalii kwa wamiliki wa kumbi za mikutano na starehe pamoja na kudhamini wiki ya Maonyesho ya 12 ya ubunifu wa mavazi ya Mustafa Hassanali yanayotarajia kuanza desemba 6 hadi 8 mwaka huu jijini Dar es salaam.

WARSHA KUHUSU MAJADILIANO YA PAMOJA YA SHERIA MOJA UDHIBITI KATIKA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI YAFANYIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki anzania(TAEC),Pro.Lazaro Busagala (aliyekaa katikati)katika pamoja na washiriki wa warsha ya majadiliano ya pamoja ya sheria ya udhibiti wa uchimbaji salama wa madini ya Urani.
Warsha ikiendelea.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Ulaya (EU) inaendesha warsha ya kuboresha shughuli za kisheria na uhakiki ili kuboresha uwezo uliopo katika kudhibiti madini ya urani. 

Warsha hii ya siku tatu ambayo imeanza tarehe 19 hadi tarehe 21, Novemba 2019 katika makao makuu ya TAEC yaliyopo Njiro, Arusha 

Lengo la warsha hii ni kujadili tathimini ya ripoti ya Sheria ya udhibiti na mahitaji na ya leseni ya uchimbaji wa madini ya urani. Pia katika warsha hii muhitasari wa uwepo wa madini ya urani pamoja na utayari wa utoaji wa leseni ya uchimbaji wa madini ya urani katika siku zijazo pia utajadiliwa. 

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mhe. Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, amesema majadiliano ya warsha yanalenga kuja na sheria mpya itakayoweza kutumika katika uchimbaji wa madini ya Urani pamoja na kumlinda mwananchi wa kawaida na madhara ya madini hayo. 

“Kunahitajika udhibiti wa hali ya juu katika madini ya urani, hivyo sheria mpya itakapokamilika itaanza kutumika “alisema Prof.Lazaro . 

Jumla ya washiriki 29 wanashiriki katika warsha hii ambapo washiriki ishirini (20) ni kutoka TAEC na washiriki wengine tisa (9) ni kutoka taasisi nyingine ambazo zinahusika katika maswala ya madini ya urani kama vile, Wizara ya Madini, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Tume ya Madini 


Imetolewa na; 

Peter G. Ngamilo 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano 
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

NEWZ ALERT : MEYA WA ARUSHA KALISTI LAZARO AJIUNGA NA CCM

$
0
0
Wakati kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zikiendelea nchini, aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Ndugu Kalisti Lazaro aliyefika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam ameeleza amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu akiwa katika Wadhifa wake wa Meya wa Jiji la Arusha.

Ndugu Kalisti amesema amepokea barua za maonyo mara kadhaa kutoka Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano na Viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri ambayo ameifanya Nchini ikiwamo katika Mkoa wa Arusha.

Vitisho vya mara kwa mara ikiwamo dhidi ya uhai wake ndio vimepelekea kujivua nafasi zake zote katika Chadema na kujiunga na CCM, Chama ambacho kinashughulika na utatuzi wa kero za wananchi. Ndg. Lazaro pia amechukizwa na Chama chake kujitoa katika uchaguzi huku akiita kitendo hicho uvunjaji wa demokrasia ambacho ndani ya masaa mawili uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema iliwanyima mamilioni ya wapenda demokrasia haki ya kushiriki katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

Ndg. Kalisti Lazaro amesema sasa yuko tayari kuchapa kazi ya wananchi akiwa ndani ya Chama ya Mapinduzi na kwamba yuko tayari kwa maelekezo ya kazi kutoka Uongozi wa CCM.

Ndg. Kalisti kwa kujiunga na CCM amejiuzuru nafasi ya Udiwani, Umeya wa Jiji la Arusha, Uenyekiti wa Mameya na Madiwani wote wa Chadema Nchini na Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Ndugu Kalisti Lazaro atapokelewa rasmi na wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha katika tarehe itakayopangwa hivi karibuni.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Uzinduzi Wa Tawi Jipya Benki Ya Exim: BOT Yaipongeza Exim Kwa Ukuaji.

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeipongeza benki ya Exim Tanzania kwa jitihada na mafanikio inayoyapata katika kujitanua ndani na nje ya nchi huku ikitoa wito kwa benki hiyo kuhakikisha inawekeza zaidi katika kutoa huduma maalumu na zenye ubunifu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ili waongeze nguvu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse wakati akifungua rasmi tawi jipya la benki ya Exim Tanzania lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam ikiwa ni baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania. Katika uzinduzi huo, Dk Kibesse alimuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

“Ni fahari kwetu kuona benki ya kizalendo inafanya mambo makubwa kama haya. Mmekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mabenki hapa nchini jinsi inavyojizatiti kujiimarisha ndani na nje ya mipaka ya nchi.Hatua hii ni sawa na kuitikia kilio cha wadau wa huduma za kifedha hapa nchini wanaohitaji huduma zinazokidhi mahitaji yao pia huduma zinazolingana na zile za kimataifa na kwenye mazingira yaliyobereshwa.’’ Alisema.

Alitoa wito kwa benki hiyo kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara wadogo na wa kati ili waweze kuongeza nguvu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini ili kulisaidia taifa kufikia malengo yake ambayo ni pamoja na kufikia pato la kati ifikapo mwaka 2025.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na msimamo wa Rais Dk John Magufuli ambae amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na benki kubwa zaidi na ndogo nchini kwa kuwa ni hatua muhimu kwa afya ya kifedha katika ukuaji wa uchumi hususani katika kutoa huduma kamili na zenye ubunifu kwa wateja.

“Aidha ufunguzi wa matawi mapya kama hili utasaidia kuimarisha uwepo wa Benki ya Exim kiushindani katika maeneo mbalimbali ili kutoa kwa urahisi huduma zetu kwa wakazi na wamiliki wa biashara wa maeneo haya’’

"Tunafurahi kuwakaribisha wateja wa Benki ya UBL, wafanyakazi na jamii yote ya UBL kwenye familia ya Benki ya Exim. Hatua hii si tu inaongeza uwepo wetu kwenye soko kubwa bali pia inatuongezea timu kubwa ya wafanyakazi wenye weledi katika masuala ya kibenki,’’ alisema.

Alisema Dar es salaam ni soko muhimu kwa Benki ya Exim na tawi hilo jipya la Mkwepu limeambatana na matumzi ya teknolojia mpya na muundo ambao utawasaidia wateja wa benki hiyo kuwasiliana na maafisa wa benki hiyo kwa njia inayowafaa na katika mazingira ambayo ni bora na salama zaidi.

Akielezea mpango wa benki hiyo Bwana Matundu alisema kuwa wanalenga kutoa kasi ya juu katika suala la utoaji huduma ili kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma haraka na zisizo na usumbufu kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na hali ya soko.

Ikiwa na jumla ya matawi 33 kwasasa Benki ya Exim Tanzania ni moja wapo ya benki kubwa nchini. Katika kipindi kifupi cha zaidi ya miaka 22 ya uwepo wake benki hiyo imetoa huduma za kifedha kwa wateja wa wadogo, wa kati na wakubwa.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse (Kulia) akipongeza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (Kushoto) wakati akifungua rasmi tawi jipya la benki ya Exim Tanzania lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.


Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse (Kulia) akijipongeza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (Kushoto) wakati akifungua rasmi tawi jipya la benki ya Exim Tanzania lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania. Wengine ni pamoja na maafisa waandamizi wa benki hiyo, wateja na wageni waalikwa.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse akzungumza wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (katikati) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse (wa nne kulia) pamoja na na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa benki ya Exim, wateja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images