Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

MRADI WA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WENYE UALBINO NA WANAWAKE WENYE WATOTO WENYE UALBINO WATAMBULISHWA SHINYANGA

$
0
0
Mratibu wa mradi wa ‘Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun, Grace Wabanhu akitambulisha mradi huo kwa wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Under The Same Sun limetambulisha rasmi mradi wa 'Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI)' wenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga ili wawe na uelewa wa kutosha na kupata ujasiri wa kuielimisha jamii juu ya hali ya ualbino.

Mradi huo umetambulishwa leo Jumatatu Novemba 18,2019 katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu kuhusu elimu ya ualbino kwa na wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino 30 kutoka wilaya za mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa mradi wa ‘Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun, Grace Wabanhu alisema mradi huo wa miezi minne unaotekelezwa katika mkoa wa Shinyanga na Mwanza utafikia tamati mwezi Januari,2020.

“Lengo la mradi unaofadhiliwa na watu wa Canada ni kutoa elimu ya ualbino kwa wanawake hawa,tumechukua wanawake 30 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga,Mwanza hivyo hivyo wanawake 30. Wanawake hawa watapata mafunzo ya uelewa juu ya ualbino na wao ndiyo watakuwa wakufunzi kuielimisha jamii”,alisema.

“Tunatarajia kwamba wanawake watakaojengewa uwezo watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya hali ya ualbino na watakuwa na ujasiri wa kuielimisha jamii inayowazunguka kwa lengo la kuondoa unyanyapaa na ukatili dhidi yao na watoto wenye ualbino ili kuleta usawa kati ya watu wenye ualbino na wasio na ualbino”,aliongeza Wabanhu.

Alisema wameamua kuchagua kundi la wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino kutokana na kwamba kundi hilo limesahaulika lakini kwa kuzingatia kuwa akina mama hao ndiyo wanalea watoto na ni waathirika wakubwa wa vitendo vya unyanyapaa na ukatili na wamekuwa wakikimbiwa na waume zao.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga (TAS), Eunice Zabron alisema njia pekee ya kukomesha vitendo vya unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino ni kutoa elimu ya kutosha kwa jamii.

Zabron ambaye pia Mwenyekiti wa Idara na Wanawake na Watoto katika Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga aliipongeza serikali kwa kuendelea kuwa bega kwa bega na watu wenye ualbino huku akibainisha kuwa vitendo vya unyanyapaa vimeendea kupungua kutokana na elimu inayotolewa na vyombo vya habari na wadau mbalimbali kuhusu ualbino.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Lilian Kiyenze kwa niaba ya Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga aliwataka wanawake hao kutumia vizuri elimu watakayopatiwa kuhusu Ualbino ili wakawe chachu ya mabadiliko katika jamii. 
Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze akizungumza kwa niaba ya Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga wakati Shirika la Under The Same Sun likitambulisha mradi wa ‘Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’ leo Jumatatu Novemba 18,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI).
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun, Grace Wabanhu akitambulisha mradi wa 'Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)' kwa wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ Grace Wabanhu akielezea kuhusu mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI).
Grace Wabanhu akizungumza wakati akitambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga (TAS), Eunice Zabron akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI).
Wanawake wenye watoto wenye ualbino wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa.
Akina mama wakiteta jambo ukumbini.
Wanawake wenye ualbino wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa rasmi mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi zatakiwa kuwapa watumishi walioajiriwa stahiki zao

$
0
0
Joseph Kinduguyo ambaye ni muhasisi wa kampuni ya kampuni ya larittate Legal Consultants akiendelea kuwapa semina washiriki.
Washiriki wakifuatilia semina hiyo 


Na Woinde Shizza, globu ya jamii Arusha

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameagiza taasisi zilizo waajiri watumishi kuhakikisha maeneo yao ya kazi wanapa stahiki zao kutokana na namna wanavyofanyakazi kwenye idara kwa lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili za kulalamikia maslai madogo wanayolipwa,

Kwitega ametoa Agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Semina ya kuwajengea waajiri uwezo wa kufuata taratibu za kazi ikiwemo misingi bora kwa watumishi mkoani Arusha na kusema kwamba malalamiko makubwa hutokana na mashirika ya watu binafsi kushindwa kuheshimu mikataba ya kazi na kupelekea kufungua majalada mahakamani.

Ameeleza kuwa mbali na jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kutatua malalamiko kwa watumishi wa sekta binafsi kwa kutoa ushauri wa kisheria lakini bado kumekuwepo na changamoto hivyo ameitaka kampuni ya Clarittate Legal Consultants inayo endesha semina hiyo kuwapa mafunzo taasisi zinazohudumia jamii kwani kampuni hiyo imekuwa ikisaidia taasisi kufuata taratibu kanuni na miongozo jinsi ya kufanyakazi kwa mujibu wa sheria za nchi

Katibu tawala amesema kuwa waajiri waliopata mafunzo hayo endapo watatumia vyema elimu walipata itasaidia kuondoa migogoro na migongano katika taasisi hivyo mafunzo hayo ni mwanzo mzuri wa kuondokana na migogoro ya mara kwa mara kati ya mwajiriwa na bosi wake.

Awali akizungumza semina hiyo kwa waajiri hao mwanasheria Emmanuel Atonny Ngeiza amesema kwamba waajiri wengi wamekuwa wakifanya maamuzi kwa watumishi wao bila kuangalia maslahi ya mtumishi wake ni yapi na baadae wakijikuta wakitengeneza migogoro isiyo na tija kwa mtumishi kumfikisha mwajiri wake mahakamani kutafuta haki ya kulipwa stahiki zake.

Ngeiza amesema semina hiyo kwa waajiri imelenga kufuata taratibu za kazi pamoja na kuheshimu kazi zinazofanywa na mtumishi wake na endapo mtumishi ameachishwa kazi anapaswa kupata stahiki zake kwa mujibu wa sheria.

Naye mwazilishi wa kampuni hiyo Joseph Kinduguyo ambaye ni mwanasheria wa kujitegema amesema kumekuwepo na ukiukwaji wa kutokufuata sheria kanuni na miongozo ya kazi kwa waajiri walio wengi na hii ni mara baada ya kufanya utafiti wakaona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa waajiri katika mikoa ya Arusha Kilimanjaro ili kuwapa mafunzo ya kuondoa changamoto zinazowakabili waajiri dhidi ya watumishi engo nikufikia mikoa yote nchini.

WAZIRI MKUU AMTAKA MTENDAJI MKUU TBA AJITATHMINI

$
0
0

*AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WATATU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini kuhusu utendaji kazi wake huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa wakala huo.

“TBA tunaihitaji lakini watu wake wana shida. Hatuwezi kuwaacha, TBA wasipewe miradi kwa sababu hawawajibiki na wanadhani kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ndio wataachwa wafanye mambo ya hovyo.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi wakurugenzi hao leo (Jumatatu, Novemba 18, 2019) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Arch.Humphrey Killo, Kaimu Meneja wa Miradi, Abdallah Awadh na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushauri Arch. Hamis Kileo.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika miradi mbalimbali waliyopewa na Serikali ukiwemo ujenzi wa jengo la NEC ambalo ujenzi wake ulianza Julai, 2017 na ulitakiwa ukamilike Juni 2018 kwa gharama ya sh. bilioni 13. Hata hivyo mradi huo bado haujakamilika na ujenzi wake umesimama.

Akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya NEC Waziri Mkuu alihoji sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi alisema jengo hilo limeshindwa kukamilika kwa sababu wakati walipokuwa wanaanza kazi walibaini kuwa kuna vitu vilisahaulika wakati wa uandaaji wa Bill of Quantities(BOQ). TBA ndio waandaaji wa ramani ya jengo hilo na ndio wajenzi.

“Bajeti ya awali ilikuwa sh. bilioni 10 wakati wa uandaaji wa michoro ya ujenzi gharama ziliongezeka na kufikia sh. bilioni 13 ambazo ndizo tulikubaliana katika mkataba. Wakati tunaendelea na kazi tuligundua kuna vitu vimesahaulika kwenye BOQ jambo lililoongeza bajeti ya ujenzi na kufikia sh. bilioni 32.” Amesema Arch. Killo.

Waziri Mkuu akahoji tena “kutoka sh. bilioni 13 hadi kufikia sh. bilioni 32 je unaona inakuja vizuri hiyo” sh. bilioni 10 hadi sh. bilioni 13 tena hadi sh. bilioni 32 inazungumzikaje hii na je mwenye jengo mlikubaliana naye? Awali mwenye mahitaji alisema ana sh. bilioni 10 sasa imefikaje 32 je mlimshauri muhusika kuhusu ongezeko hili?

Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi Arch. Killo alipotakiwa kueleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi huo amesema waligundua tofauti wakati wakiwa kwenye eneo la ujenzi kwamba kuna kazi zilitakiwa zifanyike lakini katika mkataba hazipo na hawakuwasiliana na muhusika.

Miongoni mwa vitu vilivyosahaulika katika BOQ ya mradi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa ghorofa ya nne katika jengo moja wanalolijenga katika mradi huo ambalo ni la ghorofa nane, pia hapakuwa na paa la jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya NEC.

Waziri Mkuu amesema miradi mingi inayojengwa na TBA katika maeneo mbalimbali imeshindwa kukamilika kwa wakati, hivyo amemwagiza Waziri wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama asitishe mkataba huo wa ujenzi na atafutwe mkandarasi mwingine aje amalizie.

“Jengo la TAMISEMI lililopo katika mji wa Serikali limejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.7, nyie wataalamu gani na kwa nini tuendelee kuwaacha ndani ya taasisi? TBA hamfanyi kazi vizuri wakuu wa mikoa na wilaya wanalalamika majengo hayakamiliki ni Serikali gani itakayowavumilia, mmeshindwa kutambua majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.  
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu), wakati alipoenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), uliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, ambao haujakamilika kwa wakati, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi (TBA), Humphrey Killo (kulia), wakati alipoenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, Novemba 18, 2019, baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mwakilishi wa Meneja Mradi, kutoka Chuo Kikuu Ardhi, Godwin Maro (kulia), wakati alipoenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, Novemba 18, 2019, baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Jaji Semistocles Kaijage. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA BIASHARA NA WAKANDARASI KANDA YA KUSINI.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako alifungua Kongamano la Biashara na Wakandarasi kwa Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye ukmbi wa Tawi la Benk Kuu - Mtwara, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Biashara na Wakandarasi kwa Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye ukumbi wa Tawi la Benki Kuu- Mtwara, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Biashara na Wakandarasi kwa Kanda ya Kusini wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Tawi la Benki Kuu- Mtwara, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

ASKARI POLISI, MTUMISHI MAHAKAMA YA TEMEKE KORTINI KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA 200,000/-

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

ASKARI Polisi Itialy Omary na mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Lezilie Koini wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. 200,000.

Hata hivyo mahakama imemsomea mashtaka mshtakiwa Koini peke yake kwa kuwa mshtakiwa Omary hajafika mahakamani, hivyo Mahakama imetoa amri ya kukamatwa kwake.

Akizungumza leo Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horombe amedai Mei 8, mwaka 2018 mshtakiwa Omary na Koini kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mussa Abdallah ikiwa kama kishawishi ili asikutwe na we na hatia katika kosa namba 211/2018 la usalama barabarani.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa Omary alikubali kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai bado haujajiandaa hivyo wanaomba ahirisho la muda kwa ajili ya kujiandaa. 

Hata hivyo, Hakimu Mmbando alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na vitambulisho halali atakayesaini bondi ya Sh. 500,000. 

Mshtakiwa ametimiza masharti ya dhamana, nje kwa dhamana.Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 21 mwaka huu.

JALADA LA MFANYABIASHARA ANAYETUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA NA MAGUNIA MAWILI YA MKAA LIPO HATUA ZA UCHAPAJI

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mfanyabiashara Khamis Luwonga 'Meshack' (38), anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuwa upelelezi wa kesi hiyo kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Novemba 18, mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, na kwamba upelelezi umekamilika na  jarada lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyingine ili waweze kufatilia suala hilo.

Hakimu Ally amearisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu. Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mkewe Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.

HAMISI AWALIZA MASHABIKI WA BSS

$
0
0
  Na.Khadija seif, Michuzi TV.

 JAJI Mkuu wa shindano la kusaka vipaji (BSS) Rita paulsen ajibu malalamiko ya kijana Hamisi kutolewa kwenye mashindano hayo.

Usiku wa kuamkia leo Jumanne Novemba 18, 2019 wafuatiliaji wa kipindi cha Bongo Stars Search wamechukizwa na kitendo cha mshiriki wa shindano hilo, Hamisi kutolewa kwenye kinyang’aro hicho.

Madam Rita amesema kuwa kijana huyo, Bado yupo ila kasimamishwa kutokana na ishu za masomo na ataendelea kushiriki.

 “Yupo sana alitakiwa kuondoka ili kumalizia mitihani yake ya kidato cha nne ila yupo kambini,” Ameeleza Madam Rita kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwatuliza watazamaji wa shindano hilo.

Jana Hamisi alishindwa kuingia kwenye Top 20 ya washiriki ambao wameingia kambini na kujikuta akitolewa kwenye mashindano hayo, Huku majaji wakieleza kuwa endapo watazamaji wangependa kumuona Hamisi au washiriki wengine waliotolewa kwenye Top 10 watahitajika kumpigia kura mshiriki huyo au hao.

Washiriki wawili waliotolewa kwenye mashindano hayo, Watapata nafasi ya upendeleo kuingia kwenye fainali yaani Top 10 kwa kupigiwa kura.

MRADI WA MKAA ENDELEVU WAPELEKA NEEMA KIJIJI CHA DIGUZI, WATOA OMBI KWA SERIKALI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii 

WANANCHI wa Kijiji cha Diguzi waliopo Kata ya Matuli wilayani Morogoro ambao wanajihusisha na Mradi wa kuleta mageuzi kwenye sekta ya mkaa nchini Tanzania(TTCS), maarufu 'Mkaa Endelevu'wamesema kwa sasa maisha yao yamenoga na wanajimudu kiuchumi ukilinganisha na hapo kabla ya kuwepo kwa mradi huo. 

Wamesema mradi wa mkaa endelevu umesababisha wananchi wa kijiji hicho kuwa na uhakika wa maisha kichumi wao pamoja na kijiji chao na kwamba uwezo walionao hivi sasa wanachohitaji sio fedha za Serikali bali wanahitaji kuhakikishiwa usalama wa mradi huo ambao umeleta maendeleo makubwa. 

Wakizungumza katika mahojiano maalumu na Michuzi Globu ya jamii, wananchi hao wamesema uwepo wa mradi huo umewafanya waondokane na utegemezi kwa asilimia kubwa, kwani hivi sasa mambo mengi wanafanya kwa kutumia fedha za mradi huo. 

Mtendaji wa Kijiji cha Diguzi Redemter Matola amesema kwa maendeleo ambayo wameyapata kupitia mradi huo wanaelekea kusaidia vijiji vingine huku akifafanua kabla ya mradi wa mkaa endelevu haujafika kijijini hapo hawakuwa na mapato ya aina yoyote. 

Amesema baada ya kuingia kwa mradi huo ndani ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa mradi 2018/2019 walifanikiwa kuingiza Sh.milioni 63. "Kutokana na kuingiza kiasi hicho cha fedha, hakika tumefanya mambo mengi ya maendeleo." 

Pia amesema kutokana na mradi huo kuonesha matokeo chanya wananchi wa kijiji hicho wanaiomba Serikali kuundeleza pale wafadhili watakapofikia kikomo kwani una tija kwa kijiji na nchi. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi kupitia mradi wa mkaa endelevu Chilunda Iman amesema kwa maendeleo waliyoyapata kwa mwaka mmoja imewafanya wajiamini na hawana muda wa kusubiri Sh.milioni 50 za kila kijiji kwani wenyewe kupitia mradi huo wanao uwezo wa kupata zaidi ya fedha hizo kupitia mradi huo. 

Amesema kabla ya mradi huo maisha yalikuwa magumu, lakini baadae ndio wamegundua kumbe walikuwa wamekalia rasilimali muhimu katika kijiji chao. 

"Tuwe wakweli hapa katika kijiji chetu wala hatuna haja ya kusubiri wala kuhitaji Sh. Milioni 50 za Rais kwa kila kijiji.Katika milioni 63 ambazo tumezipata, tumetumia Sh.milioni 48 kufanya maendeleo na tunaendelea. 

"Tumejenga choo cha kijiji Sh.milioni tatu, tuweka umeme jua kwenye Zahanati kwa gharama ya Sh.milioni moja, tumefanya ukarabati wa tanki la maji kwa Sh.milioni moja na tunajenga nyumba ya mwalimu kwa Sh.milioni 13.8. 

"Pia kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutumika kulipa gharama za ulinzi wa msitu wetu wa kijiji ambao ndio tunautegemea kwa ajili ya mradi wetu wa mkaa endelevu,"amesema. 

Akizungumza kuhusu mradi huo wa mkaa endelevu, Ofisa Kujemgea Uwezo kutoka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG), Simon Lugazo ameeleza kwamba vijiji 30 ikiwemo cha Diguzi wilayani Morogoro, Kilosa na Mvomero vimenufaika na mradi huo kwa kujengewa uwezo wa kutumia rasilimali ya misitu kwa njia endelevu. 

Amesema kilichosemwa na wananchi wa Diguzi ndicho hicho hicho kinachosemwa na vijiji vingine ambavyo mradi huo upo." Lengo letu sisi kama TFCG, Mjumita na TaTEDO kupitia TTCS chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) kumtoa mwananchi wa kijijini kwenye umaskini," amesema. 

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji Jonathan Biko amesema pamoja na mafanikio kuna baadhi ya changamoto ambazo nazo zimekuwa sehemu ya kuwafanya kuongeza jitihada kuhakikisha mradi wao unakuwa salama na endelevu. 

Ametaja baadhi ya changamoto ni uelewa finyu kuhusu utunzaji misitu kwa maendeleo endelevu, uhaba wa vifaa duni vya ulinzi na wafugaji kuingiza mifugo kwenye misitu hali inayoibua migogoro zaidi. 

" Unaenda kukamata muhalifu kwa kutumia vyombo vya asili huku yeye ana silaha ya moto hii ni changamoto kubwa,"amesema. Aidha, Biko amesema pamoja na changamoto hiyo wameendelea kulabiliana nazo kwa kufuata taratibu za kisheria. 

Amesema katika msimu wa 2019/2020 wanatarajia kuKusanya mapato zaidi ya Shilingi Milioni 60 ambazo zitatekeleza miradi mipya na kumalizia ya zamani.
 Sehemu ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Diguzi ambao umetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mkaa endelevu unavyoonekana.
 Mweka Hazina wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji, Angelina Mugasa kizungumza kuhusu namna ambavyo kijiji chao kimepiga hatua kimaendeleo kutokana na utekelezaji wa mkaa endelevu kijijini hapo
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Diguzi wilayani Morogoro wakiwa kwenye kikao cha kuelezea mafanikio yaliyopatikana kupitia mradi wa mkaa endelevu.
Mtendaji wa Kijiji hicho cha Diguzi wilayani Morogoro Redemter Matola akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa kijiji cha Diguzi kuhusu maendeleo yaliyopatikana kupitia mradi wa kuleta mageuzi kwenye sekta ya mkaa nchini Tanzania(TTCS).


WAZIRI MKUU AMTAKA MTATIRO AWASHUGHULIKIE WALIOKULA FEDHA ZA KOROSHO TUNDURU

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Julius Mtatiro ahakikishe anaondoka na Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho hadi Tunduru ili wakahakiki ni kwa nini wakulima hawajalipwa.

"Nimefurahi kusikia minada ya korosho inakwenda vizuri. Lakini sijafurahia habari ya Tunduru. Mheshimiwa Rais aligiza sh. milioni 40 zipelekwe kwa wakulima. Na ninajua kwamba zimeshalipwa. Sasa ni kwa nini wakulima bado wanadai?, alihoji.

"Ukitoka hapa kwenye mkutano nenda pale jengo la Bodi ya Korosho. Ondoka na Mtendaji Mkuu wake, mwende Tunduru akafuatilie ni kwa nini malipo ya mwaka jana hayajalipwa hadi sasa." Bw. Mtatiro ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.

"Nataka afuatilie fedha zimekwama kwa nani. Kaimu Mkuu wa Mkoa ukigundua wanaokwamisha ni viongozi wa ushirika, shughulika nao hukohuko kama ambavyo umekuwa ukifanya," amesisitiza. 

Ametoa agizo hilo leo mchana wakati akifungua kongamano la siku moja la Wakandarasi na Wazabuni wa mikoa ya Kusini lilioandaliwa na benki ya CRBD kwenye ukumbi wa Benki Kuu (BoT) mjini Mtwara.

Akizungumzia kuhusu kongamano hili ambalo kaulimbiu yake ni "Pamoja nawe kukuza uchumi", Waziri Mkuu amewataka wakandarasi hao baada ya kupata elimu kidogo kuhusu shughuli za benki hiyo, anataraji kuwa wataenda kwenye Halmashauri zao na kutafuta ........

"Serikali inajenga miradi mikubwa kama vile bwawa la kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji la Mwalimu Nyerere, bomba la mafuta la kutoka Hoima hadi Tanga na miradi ya maendeleo kama ile ya barabara, reli, ujenzi wa hospitali, madarasa na nyumba za walimu. Miradi yote hii inawatarajia ninyi wakandarasi mkaijenge."

Alisema Serikali imeendelea kuimarisha na kusogeza karibu kwa wananchi huduma za jamii ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu. "Katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019, kwa shule za msingi, Serikali imejenga madarasa 473, matundu ya vyoo 1,405, nyumba za walimu 24 na kukamilisha maboma ya madarasa 2,760. Kwa shule za sekondari, Serikali ilijenga madarasa 465, matundu ya vyoo 736, nyumba za walimu 23 na kukamilisha maboma ya madarasa 2,392," alisema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hii kutoa wito kwa viongozi na watendaji wazingatie utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma kwa kutenga zabuni zenye thamani ya chini ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya wazabuni Watanzania ili kuwajengea uwezo na kushiriki katika zabuni. Alisema Serikali kwa upande wake itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa CRDB kwa kubuni programu hiyo ya tofauto ambayo imelenga kuwainua wakandarasi wadogo na wa kati. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki qa kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa alisema hadi sasa jumla ya tani 67,000 za korosho zimeuzwa mkoani humo kupitia minada mitatu.

Oktoba 30, mnada wa kwanza ulipofanyika bei ilikuwa sh. 2,468/- kwa kilo na mnada wa tarehe 15 Novemba, ulishihudia bei ikipanda na kufikia sh. 2,890/- kwa kilo, alisema.

Alisema katika msimu huu, korosho zimeingiza sh. Bilioni 1.75 ambapo kati ya hizo, sh. Bilioni 1.20 zimeshaingizwa kwenye akaunti na kupelekwa kwa wakulima.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CRDB, Bw. Abdulmajjid Nsekela alisema bei hiyo inamsaidia mteja kwa kutoa ushauri, kumwezesha na kushirikiana naye kuijenga nchi.

"Leo tuko Mtwara, lakini tumeshaendesha makongamano kama haya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza. Na hapa Mtwara tumejumuisha pia mikoa ya Lindi na Ruvuma," alisema.

Alisema benki hiyo ina hisa trilioni 6.3 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya hisa za mabenki yote na kwa upande wa amana, Mkurugenzi Mkuu huyo alisema amana za benki hiyo zinafikia trilioni 4.9 ambazo ni sawa na asilimia 23 ya amana za benki zote nchini.

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE ATOA KOMPYUTA KWA WANAHABARI SINGIDA

$
0
0
Katibu wa Mbunge wa Viti Maalumu ( CCM) Mkoa wa Singida, Mariam Ntembo (kulia), akimkabidhi Kompyuta Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (Singida Press Club), Seif Takaza aliyoitoa mbunge huyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari hao katika shughuli zao za kila siku. Katikati ni Katibu wa Chama hicho, Revocatus Phinius.


Na Dotto Mwaibale, Singida.

MBUNGE wa Viti Maalumu ( CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ametoa kompyuta moja kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (Singida Press Club).

Akikabidhi kompyuta hiyo kwa niaba ya mbunge huyo katika mkutano wa kawaida wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki, katibu wa mbunge huyo, Mariam Ntembo alisema kompyuta hiyo imetolewa na Mattembe ili kuwasaidia katika shughuli za kila siku za waandishi wa habari wa mkoa wa Singida.

" Mbunge Mattembe amenituma nije kuwakabidhi kompyuta hii kwani anatambua mchango wenu wa kuhabarisha umma kupitia kalamu zenu juu ya maendeleo ya mkoa wetu wa Singida na Taifa kwa ujumla" alisema Ntembo.

Ntembo alisema Mbunge Mattembe yupo pamoja na waandishi hao na kuwa anawapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwa ataendelea kukisaidia chama chao kadri atakapopata nafasi ya kufanya hivyo ambapo pia alichangia shilingi laki mbili kwa ajili ya kuwezesha mkutano huo.

Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Seif Takaza akipokea msaada huo alimshukuru mbunge huyo kwa kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari wa mkoa huo na kumuomba wakati mwingine asisite kuwapa msaada.

DK.SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 20 YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa hutuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya (kulia) Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico (kushoto) Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Hassan Khamis Hafidh ,[Picha na Ikulu.] 18/11/2019.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa hutuba yake katika viwanja vya Fumba Mji mpya mkoa wa Mjini Magharibi. [Picha na Ikulu.] 18/11/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Tanzania Nd,Josphat Rweyemamu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Wajasiriamali baada ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico wakiangalia Gazeti la Zanzibarleo alipotembelea madanda ya maonesho ya wajasiriamali baada ya kuyafungua rasmi Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya Mkoa wa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico wakifuatana na viongozi wengine wakati alipotembelea madanda ya maonesho ya wajasiriamali baada ya kuyafungua rasmi Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo katika viwanja vya Fumba Mji mpya Mkoa wa Mjini Magharibi 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico mara alipowasili katika viwanja vya Fumba Mji mpya katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.] 18/11/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Maudline Cyrus Castico mara alipowasili katika viwanja vya Fumba Mji mpya katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Maonesho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo (wa pili kulia) Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Hassan Khamis Hafidh ,[Picha na Ikulu.] 18/11/2019.

WAKANDARASI MRADI WA REA WAASWA KUITEKELEZA KWA WAKATI

$
0
0
.Mh Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(kulia) pamoja na Mkuu wa
Wilaya Ya Kilosa Mh Adamu Mgoyi (mwenye shati ya draft )na baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa rea katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza katika kijiji cha mabana kata ya mbigiri wilaya ya kilosa mkoani morogoro hapo jana .
Mh Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu pamoja na Mkuu Wa Wilaya ya
Kilosa Mh Adamu Mgoyi na baadhi ya wananchi wa kijiji cha mabana kata ya mbigiri wakizungumza na wananchi kabla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa rea katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza wilayani kilosa mkoani morogoro 
Mkuu Wa Wilaya Ya Kilosa Mh Adam Mgoi (Aliesimama) Akizungumza Na
Wananchi Wa Kata Ya Mvuha Ndani Ya Wilaya Hiyo Baada Ya Ugeni Wa Naibu Waziri wa Nishati Mh Subira Mgalu Kutembelea Wilaya Hiyo.
Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Makwambe Kata Ya Mvumi Wilayani
Kilosa Wakimskiliza Naibu Waziri Wa Nishati Bi Subira Mgalu Alipotembelea Kijiji Hicho.

*********************************

NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.

Wakandarasi Wa Mradi Wa Rea Katika Awamu Ya Tatu Mzunguko Wa Kwanza Wametakiwa Kutekeleza Majukumu Yao Kikamilifu Ili Kufanikisha Adhma Ya Serikali Ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo Katika Maeneo Yao Ikiwa Uunganishwaji Wa Umeme Huo Katika Vijiji Utaleta Manufaa Makubwa Ikiwemo Uuanzishwaji Wa Viwanda Vidogo Vidogo Kuelekea Uchumi Wa Kati.

Kauli Hiyo Imetolewa Na Naibu Waziri Wa Nishati Bi Subira Mgalu
Alipotembelea Katika Kijiji Cha Mabana Kata Ya Mbigiri Wilayani Kilosa
Mkoani Morogoro Kwa Ajili Ya Uzinduzi wa Uwashaji Wa Umeme, Na kuongea na wananchi wa kijiji Makwambe Kata Ya Mvumi Wanaotarajiwa Kupatiwa Umeme Kupitia Mradi Huo.

Mh.Mgalu Amesema Kumekuwa Na Malamiko Mengi Kutoka Kwa Wananchi
Hasa Kuhusu Michoro Inayoidhinishwa Na Bodi Katika Uwekaji Wa Nguzo Za Umeme Hivyo Limekwisha Tatuliwa Tatizo Hilo Na Kama Wizara Wametoa Maelekezo Ya Namna Ya Michoro Hiyo Kama Ilivyoidhinishwa Na Bodi Ya Wakala Wa Vijijini Rea.

Kwa Upande Wake Kaimu Meneja Tanesco Bw.Martin Schilima Na Mkuu Wa
Wilaya Ya Kilosa Mh Adam Mgoi Wameishukuru Serikali Kupitia Naibu Waziri Mh Subira Mgalu Kwa Hatua Na Jitihada Zinazofanyika Katika Kuwafikia Wananchi Kwa Kuwaunganishia Umeme Na Kuahidi Kushirikiano Nao Pamoja Na Wananchi Kwa Kila Hatua Ili Kuwafikia Kwa Wakati.

Nao Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Mabana Kata Ya Mbigiri Wametoa
Shukrani Zao Kwa Kuwashiwa Umeme Katika Kijiji Hicho Na Kuahidi Kufanya Makubwa Katika Kuwaletea Maendeleo Hasa Uanzishwaji Wa Viwanda Vidogo Vidogo Kama Kusindika Nyanya.

Mradi Huu Upo Katika Awamu Ya Tatu Mzunguko Wa Kwanza Ambapo Kuna
Vijiji Mia Moja Na Sitini Na Tano Katika Mkoa Wa Morogoro Ambapo Katika
Wilaya Ya Kilosa Kuna Vijiji 24 Na Mpaka Sasa Vijiji Kumi Vimeshawashwa
Umeme Na Vijiji Vilivyosalia Kumi Na 4 Vinakwenda Kuwashwa Umeme Kabla Ya Mwezi Desember Mwaka Huu.

MBUNGE AZZA AKUTANA NA WANAWAKE WA MWAKITOLYO KUKOMESHA BIASHARA YA NGONO 'CHEMSHA CHEMSHA'

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiongozana na madiwani 11 wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamekutana na wanawake na mabinti wanaoishi katika kata ya Mwakitolyo ili kuzungumza nao namna ya kukomesha vitendo vya baadhi ya mabinti wenye umri kuanzia miaka 12 na wanawake watu wazima wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘Chemsha chemsha’.

Hatua ya mbunge na madiwani hao kukutana na wanawake na mabinti wa Mwakitolyo leo Jumatatu Novemba 18,2019 inatokana na azimio la kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichofanyika Mwezi Agosti mwaka huu ambapo Mhe. Azza aliomba aongozane na madiwani wanawake kwa ajili ya kwenda kuzungumza na mabinti na akina mama ili kukomesha biashara ya ngono katika kata hiyo.

Akizungumza katika kikao cha ndani na wanawake hao wakiwemo wanaomiliki gesti na nyumba za kupanga kilichofanyika katika kijiji cha Nyaligongo,Mhe. Azza amesema biashara ya ngono inadhalilisha utu wa mwanamke lakini pia kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya zinaa hivyo inapaswa kupingwa na kila mtu.

“Ndugu zangu biashara ya ngono ni biashara ya kujidhalilisha naomba wanawake na mabinti wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo. Tutafute kazi za kufanya ambazo siyo za kujidhalilisha,kazi yeyote ukiipenda na ukaifanya kwa moyo mmoja ni lazima utafikia malengo yako”,amesema Azza.

“Acheni biashara hii. Wanawake tutambue heshima tuliyopewa na mwenyezi Mungu,mama ndiyo anayejua kila kitu katika nyumba,mama ndiye aliyebeba majukumu makubwa katika familia,kwa hiyo tunatakiwa tuibebe heshima tuliyonayo badala ya kujidhalilisha”,alisema mbunge huyo.

Mhe. Azza ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni ‘gesti’ na wanaopangisha vyumba kutoruhusu watu wanaofanya biashara ya kuuza miili.

Aidha amewashauri kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili ili waweze kupata mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na kwamba hata kama wana biashara zingine basi wajishughulishe pia na kilimo ili wawe na uhakika wa chakula katika familia zao.

“Nitumie fursa hii kumpongeza mtendaji wa kata ya Mwakitolyo na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kwenda kuwatafuta wanawake na mabinti waliokuwa wanafanya biashara na kuwapa elimu ya kuondokana na biashara hiyo na kuwapatia vyerehani ili waweze kufanya biashara ambayo ni halali,jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa biashara hiyo”,ameongeza Azza. Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake akiwasili katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 18,2019. Picha zote na Said Nassor - Malunde 1 blog 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake akiwasili katika kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake katika kata ya Mwakitolyo 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipokelewa katika kata ya Mwakitolyo. Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na wanawake wa kata ya Mwakitolyo.

Wanawake wa Mwakitolyo wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na wanawake wa kata ya Mwakitolyo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja akisoma taarifa ya kata ikiwemo biashara ya Chemsha chemsa
Mbunge wa Azza Hilal na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakisikiliza taarifa ya kata ya Mwakitolyo.
Diwani wa kata ya Mwakitolyo Limbe Augustine Limbe akizungumza katika kikao hicho.
Akina mama wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa viti maalumu Chausiku Hassan akizungumza katika kikao hicho. 
Wanakikundi wakisoma risala mbele ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akimkabidhi Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja Eploni 50 kwa ajili ya Mama Lishe katika kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na baadhi ya mama lishe baada ya kuwakabidhi Eploni nyekundu zitakazowasaidia kwenye kazi yao.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na baadhi ya mama lishe waliohudhuria kikao cha ndani cha mbunge,madiwani wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja na Mama lishe pamoja viongozi wa halmashauri na kata.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wachimbaji wadogo wanawake kata ya Mwakitolyo.Chama hicho kimemuomba Mbunge kuwa Mlezi wa chama hicho.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja viongozi wa kikundi cha hiari ya Moyo kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo kinachojihusisha na kuweka na kukopa.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja viongozi wa kikundi cha hiari ya Moyo kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha na kikundi cha wanawake na maendeleo kilichoanzishwa kwa lengo la kuwafanya akina mama kuachana na biashara ya kuuza miili yao.Dhamira ya kikundi hicho ni kushusha Punda 200 'ndoo za mawe ya dhahabu' ili kusafisha senga 'mchanga wa dhahabu" 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na akina mama wa Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na akina mama wa Mwakitolyo. 

LUSHOTO WAHITAJI NAKALA 3000 ZA KITABU CHA MKAPA

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga January Lugangika amesema kwamba wilaya hiyo wanahitaji nakala 3000 ya kitabu kilichoandikiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamini Mkapa kutokana na kwamba uwepo wa maeneo mengi ya kuuzia vitabu hivyo.

Kitabu hicho ambacho kimeandikiwa na Rais Mstaafu huyo ni cha “My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu)” ambacho kilizinduliwa Jumanne iliyopita na Rais Dkt John Magufuli.

Akizungumza na mtandao huu DC January alimpongeza Rais huyo mstaafu kwa kuamua kuandika kitabu hicho huku akieleza kwamba kwenye wilaya hiyo kuna maeneo mengi ya kuuzia kitabu hicho ikiwemo hoteli za kitalii na kwenye makazi yake

“Kwanza nimpongeze Rais awamu ya tatu Mstaafu Benjamini Mkapa hapa Lushoto ana makazi yake pia ni sehemu ya utalii anampongeza kwa kuandika kitambu ambacho kitakuwa ni hazina kubwa sana kwa kuwa watanzania hapa kwetu sisi tunapokea watalii wengi”Alisema

“Kwa mwaka 2018 tulipokea watalii 1400 na mwaka huu 2019 mpaka sasa tumepokea watalii 3000 na mtalii anapokuja lushoto awe na kumbukumbu nzuri ni vuziri akanunua kitabu cha Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kwa ajili ya kumbukumbu”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kumbumbuku nzuri hiyo ya kitabu mtu anaweza kuwa na kitabu anapotembelea makazi yake akikisoma anaweza kumuuliza swali lolote lile kuhusu kusudio la kuandika kitu ambacho amekiandika kwenye kitabu hicho.

Aidha alisema pia watajitahidi kila mwana Lushoto awe na nakala moja ya kitabu kuanzia maofisini, watumishi wa umma wote na sekta binafsi ili kuhakikisha kila mkazi wa wilaya hiyo anafuatilia maisha ya kiongozi huyo

“Lakini pia tutajitahidi kuongeza na watu wa vitabu wapate wakala mmoja na nisema sisi Lushoto tunahitaji si chini ya nakala 3000 tutaviuza kwa wakati”Alisema

Hata hivyo aliwataka watanzania waone umuhimu wa kununua vitabu vinavyoandikwa na viongozi wastaafu hasa ambao bado wapo duniani ni rahisi kuvisoma na kumpigia kumuuliza alipoandika jambo Fulani alikuwa na maana gani ni sehemu ya utalii na kumbukumbu.

“Lakini pia niseme tu kwamba Mkapa ni Lushoto na lushoto ni Mkapa hivyo sasa tupo tayari kusoma maisha ya kiongozi huyo kupitia kitabu chake na ndio maana tunahitaji nakala hizo “Alisema DC

VIONGOZI WA DINI DAR WATOKA NA AZIMIO LA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza mbele ya Viongozi wa dini katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini hapa nchini katika Mkutano uliowahusisha viongozi hao pamoja na Mkuu wa Mkoa huyu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa Dini Mbalimbali hapa nchini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Paul Makonda katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.

**********************************

Viongozi wa Dini wakiwemo Maaskofu, Mashekhe, Wachungaji,Manabii, Maimamu na Wainjilisti Mkoa wa Dar es salaam leo November 18 wametoka na azimio la pamoja la kumuunga Mkono Rais Dkt. John Magufuli katika jitiada zake za kuleta maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kumaliza kero za Wananchi.

Hatua ya Viongozi hao wa dini imekuja baada ya Kuvutiwa na taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda dhidi ya Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mkoa huo chini uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli jambo lililowakosha Viongozi wa Dini na Kuamua kuja na tamko hilo.

Katika mkutano huo RC Makonda amewasilisha kwa Uhalisia wa Video taarifa ya miradi iliyotekelezwa na serikali katika sekta zote muhimu ikiwemo Afya, Barabara, Maji, Umeme, Elimu, Viwanda, Usafirishaji na sekta anyinginezo jambo lilikowagusa viongozi wa dini.

Pamoja na hayo Viongozi hao wa Dini wamesema wataendelea kumuombea Rais Dkt. John Magufuli azidi kuwa na Nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi.

WABUNGE WATATU WA CHADEMA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KUFUATIA AMRI YA MAHAKAMA YA KISUTU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jami.

WABUNGE  watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotaka wabunge wanne wa 4 chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Wabunge waliokamatwa leo Novemba 18,2019 ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa huku a Mbunge wa Kawe, Halima Mdee yeye alishakamatwa wiki iliyopita

Heche na Msingwa wamekamatwa leo mara baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuonana na Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza kesi inayowakabili, Thomas Simba.

Wabunge hao wameunganishwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika kituo hicho cha Osterbay huku Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akidaiwa kuwa anaumwa na amelazwa.

Novemba 15, mwaka huu 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru wabunge hao wanne wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kutokufika mahakamani hapo bila ya kutolewa taarifa yoyote wakati kesi yao ya uchocgezi ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Kesi hiyo inatarajia kuendelea Novemba 19, 2019 (Kesho) kwaa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizwaji.

Kabla ya kutoa amri hizo, Novemba 15, mwaka huu kesi  hiyo ilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, ambapo washtakiwa wengine waliwahi lakini wabunge hao wanne hadi saa 4:05 asubuhi walikuwa hawajafika mahakamani bila sababu za msingi.

Washtakiwa waliofika mahakamani Novemba 15, 2019 ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko.

Katika Kesi hiyo Mbowe na wenzake wanakabiliwa na  mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

Pia, wanadaiwa kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salaam..

Mwisho

DIRA YA DUNIA JUMATATU 18.11.2019

DAWASA YAWASHUSHA NDOO WANANCHI WA SALASALA KILIMAHEWA JUU

$
0
0
Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jacob Ezekiel(kushoto) na  Ramadhan Sammata(kulia) wakisaidiana kukata bomba kwa ajili ya kuunga kwenye bomba litakalokuwa linahudumia eneo la Salasala Kilimahewa Juu.
 Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)  Jacob Ezekiel(kushoto) na  Ramadhan Sammata(kulia) wakiunga bomba kwenye moja ya bomba kubwa la maji la bomba kwa ajili kusambaza maji kwenye eneo la Salasala Kilimahewa Juu eneo lililokuwa na ukosefu wa maji ya DAWASA.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Ole Philemon  akitoa maelezo kwa Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Everlasting Lyaro alipokuwa wanashuhudia ufungwaji wa bomba kubwa la maji ya DAWASA yatakayoweza kuhudumia eneo la Salasala Kilimahewa Juu jijini Dar es Salaam.

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakitandaza mabomba ya inchi 6  kwa ajili ya kusambaza maji kwenye eneo la Salasala Kilimahewa Juu kwa takribani kilometa 1.5 katika eneo hilo.
Muonekano wa bomba  la inchi sita la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) likiwa tayari limeishaunganishwa kwenye bomba kubwa na kutandazwa kwa takribani kilometa 1.5
na kufunguliwa kwa ajili ya kuanza kusambaza maji katika eneo la Salasala Kilimahewa  Juu lililokuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Maji yakitoka kwenye bomba kubwa la inchi 6 eneo la Salasala Kilimahewa Juu mara baada ya kufunguliwa kwa bomba la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi wa eneo hilo.
Baadhi ya wananchi wa Salasala Kilimahewa Juu wakichota maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) mara baada ya maji hayo kufika katika eneo hilo leo jioni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi hao waliokuwa wanapata changamoto ya maji ya DAWASA.
Mkazi wa Salasala Kilimahewa Juu Seleman Issa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa maji wa DAWASA katika eneo hilo pamoja na kutoa shukrani kwa Mamlaka hiyo kuweza kuwafikia wananchi hao.
Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Tegeta Ole Philemon akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mamlaka hiyo ilivyojipanga kwenye usambazaji wa maji katika eneo la Salasala Kilimahewa Juu ambalo lililokuwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa maji safi na salama.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 19,2019

KUELEKEA SIKU YA VYOO DUNIANI,WADAU WATAKIWA KUTAMBUA CHANGAMOTO ZA WAZIBUAJI MITALO/WATAPISHA VYOO.

$
0
0

Kuelekea siku ya Vyoo Duniani wadau mbalimbali wa Afya nchini wametakiwa kutambua changamoto zinazowakabili watu ambao wanajihusisha na uzibuaji wa mitalo mikubwa pamoja na kutapisha mashimo ya Vyoo.


Imeelezwa kuwa katika jiji la Dar es Salaam zaidi ya asimilia 70 ya wakazi wake yapo katika maeneo ambayo si rasmi. Maeneo hayo sifa zake kunakuwa na changamoto za upatikanaji wa maji safi na Salama, upatikanaji wa huduma za usafi pamoja na huduma za utupaji wa taka maji.


Hayo yamebainishwa na Meneja miradi mwandamizi wa Taasisi ya WATER AID Tanzania, Bw.Twaha Mubarak  alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wake na Waandishi wa habari kwenye ofisi za taasisi hiyo ya WATER AID jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na wanahabari Bw. Twaha amesema kuwa inakadiliwa asilimia 10 ya jiji la Dar es Salaam limeunganishwa katika mfumo wa maji taka hivyo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuibuka magonjwa mbalimbali yanayoambukiza.


"Tukizungumzia katika asilimia hizo, asilimia 90 zilizobaki tunatumia aina nyingine za mifumo, moja kwa moja tunatakiwa kufahamu wanaofanya kazi hizo (kutapisha vyoo) ni wale ambao wanaitwa majina mengi kama vyura ama wavamiaji lulu". Amesema Bw. Twaha.

Aidha Bw. Twaha amesema kuwa katika ripoti ambayo imeandaliwa imezungumzia changamoto hizo kwa mfanya usafi na imesheheni na kudadavua mkanganyiko wanaopitia wafanyakazi katika sekta ya usafi kwenye nchi zinazoendelea.

Twaha amesema kuwa ripoti hiyo  imeandikwa kwa pamoja kwa shirika la kazi Umimwwnguni, Shirika la Water Aid, Benki kuu ya Dunia na Shirika la Afya Duniani, lengo hasa ni kuinua ufahamu  kuhusu Mazingira hatarishi ambayo wafanyakazi hao wanayapitia.

Amesema Wafanyakazi hao mara nyingi hugusa kinyesi cha binadamu pasipokuwa na vifaa vya kujikinga wala vitendea kazi vilivyobora, kitu ambacho kinawaweka kwenye hatari za kupata magonjwa mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira na Watu (UMAWA) inayofanya biashara ya usafi wa mazingira katika upakuaj wa vyoo na uchakatishaji wa maji taka, Bw.Mathias Milinga amesema kuwa biashara hiyo imekuwa kwa kiasi tangu kuanzishwa kwake kwani mpaka sasa katika maeneo mengi hasa wilayani Kigamboni upakuaji holela wa vyoo umepungua kwa kiasi kikubwa.

"Wapakuaji wa kienyeji wakipata kazi mara nyingi wanakuja kwenye kituo, tumefauru kupanua huduma hiyo kwa kufanya matangazo katika vipeperushi lakini pia tunafanya kazi na halmashauri hasa kamati za afya". Amesema Bw.Milinga.
 Meneja Miradi Mwandamizi wa Taasisi ya WATER AID Tanzania, Bw.Twaha Mubarak akizungumza na wanahabari katika ofisi za taasisi hiyo  jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira na Watu (UMAWA) inayofanya biashara ya usafi wa mazingira na uchakatishaji wa maji taka, Bw.Mathias Milinga akizungumza na wanahabari katika ofisi za taasisi ya WATER AID jana  jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images