Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

MUWSA WAMUOMBA WAZIRI WA MAJI ,PROF MAKAME MBARAWA KUSAIDIA KUKUSANYA MADENI YA MAJI KWA TAASISI ZA SERIKALI .

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,(MUWSA) ,Prof Jafary Kidegesho wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo ulifanyika zilipo ofisi za MUWSA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa katibu wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,(MUWSA) ,Mhandisi Aron Joseph ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo .Hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo umefanyika zilipo ofisi za MUWSA
Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,Joyce Msiru ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ,akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Maji,Prof Makame Mbarawa mara baada ya Bodi hiyo kumaliza muda wake. 
Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akizingumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) .
Baadhi ya Wafanyakazi 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya MUWSA waliomaliza muda wao na wale wapya wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Prof Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kutamburisha wajumbe wapya wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) 
Baadhi ya Wafanyakaziw  wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya MUWSA iliyomaliza muda wake na wajumbe wapya wa Bodi hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakifuatilia kwa karibu hotuba zilizokuwa zikitolewa katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya . 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi aliyemaliza muda wake ,Prof Faustine Bee akizungumza wakati akitoa taarifa ya Bodi iliyomaliza muda wake na kukabidhi kwa Bodi mpya .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA). 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi aliyemaliza muda wake ,Prof Faustine Bee (kulia ) akikabidhi nyaraka za Bodi hiyo kwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya MUWSA ,Prof  Jafari Kidegesho mara baada ya Waziri kuizundua rasmi mjini Moshi
Wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mjini Moshi (MUWSA) . 
Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,(MUWSA) mara baada ya kuizindua .  
 Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi waliomaliza muda wao ,tukio hili limefanyika  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka hiyo.    
Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,(MUWSA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka hiyo.  
 
Na Dixon Busagaga ,Moshi

WAFANYAKAZI  wa Malmala ya Majisafi na Usafi wa MAzingira ,Moshi,(MUWSA) wamemuomba Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa kusaidia mchakato wa kufuatilia fedha za malimbikizo ya madeni ya maji kwa taasisi za serikali ambazo ni zaidi ya Sh Bil 2.3.

Mamlaka ya Majisafi an Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ni miongoni mwa mamlaka zinazotajwa kufanya vizuri katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi inaowahudumia ambapo kwa sasa imefikia wastani wa asilimia 91% kwa eneo inayohudumia.

Licha ya mafanikio hayo yanayoitamburisha MUWSA kuwa miongoni mwa Mamlaka Bora nchini ,changamoto iko kwenye Madeni yatokanayo na Ankara za maji kutoka kwa taasisi za serikali .

Akizungumza wakati wa kuzindua bodi hiyo Waziri wa Maji, Prof.Mbarawa amesema Wizara kwa sasa imelekeza nguvu zake kwenye kusimamia makusanyo katika Mamlaka za Maji nchini ili kuweza kufikisha huduma ya maji katika maeneo mengi zaidi.

Katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi (MUWSA) Waziri Mbarawa alisema ‘Wakati wangu wote natumia nguvu nyingi kusimamia makusanyo kwenye mamlaka za maji, ziko ambazo zikitaka hata kufunga nati kwenye miradi zinakuja wizarani kuomba fedha”alisema Prof Mbarawa.

Zaidi Mbarawa aliongeza: “Mamlaka hizi kama tutazisimamia vizuri zina uwezo mkubwa sana, lakini bado tuko kwenye usingizi. Nataka kila bodi mpaka watendaji wabadilike na kuiga mfano wa Mamlaka ya Maji ya Moshi Mjini”alisema .

“Mimi baada ya kuingia katika Wizara hii niliamua kuzifuatilia mamlaka kama saba ambayo ni Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro, Mbeya na mamlaka za maji ndogo ndogo za Kilwa na Makonde.”

Alisema kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa Muwsa, inampa moyo wa kuendelea kukaa katika Wizara hiyo hasa kutokana na takwimu kuonyesha kuna jitihada za kuongeza makusanyo yake kila mwezi.

“Mimi ukiniuliza, nasema Muwsa ina uwezo wa kukusanya Sh. bilioni 1.2 kwa mwezi na hilo halina ubishi, kwa sababu mwezi Januari 2019 tulikuwa tumekafika Sh. milioni 814,”alieleza Mbarawa


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Aron Joseph amesema hali ya utoaji wa huduma ya maji kwa sasa inaridhisha, kutokana na kutoa huduma katika kata 21 zilizopo ndani ya Manispaa ya Moshi na Wilaya ya Hai na Moshi Vijijini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza kabla ya Waziri Mbarawa kuhutubia, alisema kulikuwa na utitiri wa mamlaka za maji 159 nchi nzima lakini mamlaka hizo zimepungua sasa na kufikia mamlaka 83.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Muwsa aliyemaliza muda wake, Prof. Faustine Bee ambaye kwa sasa ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alimweleza Waziri Mbarawa kuwa mpaka wanaondoka katika nafasi hiyo, deni la ankara za maji katika taasisi za umma ni Sh. bilioni 2.16

Pia, alimweleza kuwa mkakati mahususi waliouacha mchakato wake uendelezwe na bodi mpya ni pamoja na upanuzi wa mabwawa ya majitaka yanayopokea majitaka kutoka maeneo mbalimbali ambao gharama zake zinafikia Sh. bilioni 7.6

Mwisho


Vodacom Tanzania Plc Yasogeza Huduma kwa Wateja wa Tandahimba na Korogwe

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba (mwenye suti) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom wilayani humo juzi. Kushoto kwake ni Mkuu wa mauzo kanda ya Pwani wa kampuni ya Vodacom Liston Clay Chale.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba (mwenye suti) akizungumza na wageni waalikwa na wafanyakazi wa Vodacom wilayani Tandahimba mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mkuu wa mauzo kanda ya Pwani kampuni ya Vodacom Liston Clay Chale.
Mkuu wa mauzo kanda ya Pwani kampuni ya Vodacom Liston Clay Chale akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba namna Vodacom Tanzania ilivyowekeza kufikisha huduma kwa wateja kote nchini.
Wafanyakazi wa duka la Vodacom Korogwe mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa wilayani humo juzi
Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi duka jipya la Vodacom mjini Korogwe juzi. Kulia ni Brigita Stephen mkuu wa kanda ya kaskazini Vodacom
Wafanyakazi wa Vodacom wakiendelea na zoezi la usajili wa laini za simu kwenye uzinduzi wa duka jipya mjini Korogwe

CHUO CHA CBE CHAPATA HATI SAFI KUTOKA KWA CAG

$
0
0
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Injinia Stela Manyanya akizungumza kwenye mahafali ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Kampasi ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri aipongeza CBE kwa kupata hati safi

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Profesa Emanuel Mjema akizungumza kwenye mahafali ya 54 ya chuo hicho mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stela Manyanya ambapo wahitimu walikuwa 2,439 katika fani mbalimbali kwa kiwango cha Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili.
Wahitimu wa fani mbalimbali katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Injinia Stela Manyanya kwenye mahafali ya 54 ya chuo hicho mwishoni mwa wiki.


Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imepongeza mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Chuo cha Biashara cha CBE katika maendeleo ya taaluma na miundombinu tangu kuanzishwa kwake miaka 54 iliyopita.

Pia imepongezwa kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu zake kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya kwenye mahafali ya 54 ya chuo hicho yaliyofanyika Kampasi ya Dar es Salaam.

Kwenye mahafali hayo wahitimu walikuwa 2,439 katika fani mbalimbali kwa kiwango cha Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili.

Manyanya aliwapongeza kwa kukarabati jengo la utawala katika kampasi ya Dar es salaam na kuanzisha ukarabati mwingine wa jengo la Cafeteria ambalo baada ya kukamilika litakuwa na maktaba kubwa ya kisasa na kumbi za mihadhara kwa kutumia fedha za ndani.

“Nimeelezwa na pia nilipata fursa ya kutembelea na kujionea eneo hilo kubwa lenye Majengo ya kutosha yanayohitaji kufanyiwa ukarabati katika kampasi ya Mwanza,”

“Pia nawapongeza kwa maendeleo mazuri ya mradi mkubwa wa ujenzi wa hostel katika Kampasi za Dar es Salaam na Dodoma ambao mchakato wake unaendeshwa na Benki ya Dunia kwa ajili “Public Private Partnership” (PPP) umefikia mahali pazuri,” alisema.

Waziri aliwapongeza pia kwa kusimamia Mapato na Matumizi ya fedha za Chuo na kupata hati safi za Mkaguzi Mkuu wa fedha za Serikali (CAG), pamoja na hati safi katika manunuzi ya umma kutoka Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), ambapo mwaka huu CBE imeshika nafasi ya pili na kupata hati safi katika manunuzi ya umma.

Alisema CBE imepanda kwenye ubora wa vyuo vikuu, yaani “University ranking”, kutoka nafasi ya 53 hadi ya 15 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mkuu wa chuo cha CBE, Profesa Emanuel Mjema chuo kinaendelea kuwasomesha wanataaluma wake kufikia kiwango cha shahada ya uzamili na uzamivu PhD kwa kutumia fedha za ndani.

Alisema pamoja na jitihada za chuo kuwasomesha wahadhiri wake hivi sasa kinawanataaluma 16 tu wenye shahada za uzamivu na kati ya wahadhiri 178 na kwamba mpaka sasa wanasomesha wahadhiri 44 kwa ngazi ya uzamivu na sita uzamili.

Profesa Mjema aliipongeza serikali kwa kutoa vibali vya kuajiri wahadhiri mara kwa mara ingawa idadi ya wanachuo waliopo chuo kinahitaji kuwa na wahadhiri 240 wakati waliopo ni 178 tu.

Alisema hali hiyo inasababisha kuwepo kwa changamoto katika kutoa taaluma na kufanya tafiti mbalimbali nan chi inapoelekea kwenye uchumi wa viwanda tafiti mbalimbali zinahitajika kwenye sekta ya biashara.

Pia Profesa Mjema aliipongeza serikali kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wote wa CBE hali inayosababisha chuo hicho kujiendesha vizuri kwani kazi kubwa ya vyuo ni kufundisha, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu.

Alisema chuo kimetuia fedha za ndani kimefanikiwa kukarabati majengo yake katika kampasi zake Dar es Salaam na Dodoma na kuanzisha ujenzi mwingine wa maktaba ya kisasa ambalo litakuwa na kumbi za mihadhara.

Profesa Mjema aliishukuru serikali kwa kufanikisha mchakato wa mradi mkubwa wa ujenzi wa hosteli katika kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma ambao umefikia pazuri.

WASHIRIKI BUNGE LA VIJANA 2019 WAPATIWA MAFUNZO JIJINI DODOMA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo akizungumza na Wajumbe wanaoshiriki katika Bunge la Vijana 2019 wakati wa mafunzo yaliyoanza leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Bunge hilo linategemewa kufunguliwa rasmi na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, 19 Novemba, 2019 katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma
Mwandishi mwandamizi wa Taarifa rasmi za Bunge kutoka Ofisi ya Bunge, Ndg. Patson Sobha akitoa mafunzo kwa Wajumbe wanaoshiriki katika Bunge la Vijana 2019 lililoanza leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za Bunge Ofisi ya Bunge, Ndg. Joshua Chamwela akitoa mafunzo kwa Wajumbe wanaoshiriki katika Bunge la Vijana 2019 lililoanza leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Bunge hilo linategemewa kufunguliwa rasmi na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, 19 Novemba, 2019 katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo akizungumza na Wajumbe wanaoshiriki katika Bunge la Vijana 2019 wakati wa mafunzo yaliyoanza leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Bunge hilo linategemewa kufunguliwa rasmi na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, 19 Novemba, 2019 katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma
Washiriki Mbalimbali wa Bunge la Vijana 2019 wakiwa katika mafunzo ya Bunge hilo yaliyoanza leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea maelezo kutoka kwa Muuguzi kiongozi katika Wadi ya Watoto Njiti, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Cleopatra Mtei (kushoto), wakati alipotembelea Wadi hiyo baada ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti yaliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel, Novemba 14, 2019. Wengine ni Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe (wa pili kulia), Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (katikati) na kulia ni Dkt. Isaack Maro.
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, akimkabidhi zawadi mmoja wa Mama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti), Felista Nyambala, wakati alipotembelea Wadi hiyo Novemba 15, 2019, Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es salaam. Katikati ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel pamoja na Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe.
Mama Getrude Mongela ambaye pia ni Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, akizungumza katika halfa hiyo, Mama Mongela alisema anatambua changamoto za Watoto Njiti kwani Mmoja wa Wajukuu zake alizaliwa akiwa Njiti. Katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini na kushoto ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel.
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Novemba 14, 2019, Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es salaam.

BENKI YA CRDB YAKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI KOREA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya Watanzania waoishi nchini Korea, wakati alipokutana nao kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini humo na kuzungumza nao masuala mbalimbali yanayohusu Benki hiyo. Uongizi wa Benki ya CRDB ulifika ubalozini hapo kwa mualiko wa Balozi Matilda Masuka (kushoto), kwa nia ya kuipongeza Benki hiyo kwa kuwa Benki ya kwanza Afrika Mashariki na Kati, Kupokea kibali cha Umoja wa Mataifa cha Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani (Green Climate Fund - GCF) itakayoweza kupitisha fedha za utekelezaji wa ufadhili wa kijani nchini Tanzania. Benki ya CRDB ilipata kibali hicho hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 24 wa Bodi ya Hali ya Hewa ya Kijani (GCF), huko Songdo, Korea Kusini. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipeana mkono na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Balozi Matilda Masuka, baada ya hotuba yake kwa Umoja wa Watanzania waoishi nchini Korea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza katika Mkutano huo.

Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Korea wakiwa kwenye Mkutano huo.

Mkoa wa Lindi Wajivunia Mafanikio Miaka 4 ya JPM

$
0
0
Mkoa wa Lindi umetumia zaidi ya bilioni 10.4 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka minne kuboresha sekta ya afya. 

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amesema kuwa baadhi ya miradi iliyonufaika na fedha hizo ni pamoja na ujenzi wa Hosptali za Wilaya, Vituo vya Afya, na Zahanati ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya. 

“Ujenzi wa miundombinu katika sekta hii umeenda sambamba na upatikanaji wa dawa ambao umefikia zaidi ya asilimia 95 katika maeneo yote ya kutolea huduma katika mkoa wetu,” alisisitiza Zambi. 

Akifafanua,amesema kuwa kuimarishwa kwa huduma za afya katika mkoa huo kumesaidia kuwawezesha wananchi kushiriki katika kukuza uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula, hivyo kukuza uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla. 

Akizungumzia elimu bure Mhe. Zambi amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 4 zimetolewa kugharamia elimu bure katika mkoa huo hali iliyowezesha kuongeza maradufu kiwango cha wanafunzi wanaosajiliwa kujiunga na shule za msingi. 

Kwa upande wa chuo cha ualimu Nachinge, Mhe. Zambi amesema kuwa zimetumika kukarabati chuo hicho kwa kuboresha miundombinu yake ikiwemo mabweni, maktaba na madarasa. 

Katika sekta ya maji, Mradi wa Ngapa umewezesha uzalishaji wa maji kufikia lita milioni 7.5 ikilinganishwa na lita milioni 2 zilizokuwa zikizalishwa awali kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo. 

Mhe. Zambi amebainisha kuwa mkoa huo umepiga hatua katika sekta ya uwekezaji kutokana na kuwepo kwa nishati ya uhakika baada ya mkoa huo kuunganishwa na gridi ya Taifa hali inayowezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, gesi na uchimbaji wa madini. 

“Mkoa wa Lindi umepata wawekezaji katika sekta ya uchimbaji wa madini ya graphite na bado tunaendelea kuwakaribisha wawekezaji wengine kuja kuwekeza katika mkoa wetu kutokana na kuimarishwa kwa miundombinu na upatikanaji wa umeme wa uhakika,” alisisitiza Zambi. 

Mkoa wa Lindi ni moja ya mikoa iliyofanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayolenga kuleta mageuzi na ustawi wa wananchi katika sekta za afya, elimu, maji, barabara na nyingine zinazolenga kukuza uchumi. 

MKANDARASI WA UMEME WILAYANI CHATO ATEKELEZA MAAGIZO YA BODI YA REA

$
0
0
Mafundi wakifanya kazi ya kuvuta nyaya katika Kijiji cha Mnekez wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA III).
Zahanati katika Kijiji cha Mutundu ambayo imefikiwa na miundombinu ya umeme ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA III).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (wa Tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga (katikati) na Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt Andrew Komba (wa kwanza kulia) wakiwa mbele ya zahanati katika Kijiji cha Mutundu wilayani Chato mara baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme kijijini hapo.
Kazi ya kuvuta nyaya ikifanyika katika Kijiji cha Kakindo wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA III).
Kazi ya kuvuta nyaya ikifanyika katika Kijiji cha Kakindo wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA III).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (katikati), na Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt Andrew Komba ( wa pili kulia) wakiwa katika Kijiji cha Kakeneno wilayani Chato ambapo walifika kukagua kazi ya usambazaji umeme kijijini hapo. Wengine katika picha ni watendaji kutoka REA, TANESCO na Kijiji cha Kakeneno.

………………….


Na Teresia Mhagama, Geita

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa kwa Mkandarasi anayefanya kazi ya kusambaza umeme vijijini wilayani Chato kampuni ya Whitecity Guangdong JV ambayo yalilenga kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo tarehe 17 Novemba, 2019, wilayani Chato, Mkoa wa Geita mara baada ya kukagua kazi za usambazaji umeme zinazoendelea wilayani humo akiwa ameambatana na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt Andrew Komba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.

Alieleza kuwa, maagizo ya Bodi hiyo yalitolewa Siku 14 zilizopita ambapo Mkandarasi huyo alielekezwa kutekeleza kazi ambazo alikuwa hajafanya kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo kuchimba mashimo, kusimika nguzo na kuvuta nyaya ili kuweza kuwasha umeme katika Vijiji alivyopangiwa kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA III).

” Tulitoa maagizo haya Wiki mbili zilizopita baada ya kufanya ziara wilayani hapa na kukuta nguzo zimelala na Mkandarasi alikuwa haonyeshi kama alikuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa kasi tunayotaka lakini baada ya kukagua leo tumeona nguzo zimesimikwa na nyaya zimeanza kuwekwa kwenye nguzo, hivyo ameweza kutekeleza maelekezo.” Alisema

Aliongeza kuwa, Mkandarasi huyo pia ameanza kazi ya kufunga transfoma kwa ajili ya kusambaza umeme kwa wananchi hivyo Bodi hiyo ilimtaka kuendelea kuongeza kasi ili maeneo yote muhimu pamoja na wananchi waunganishiwe umeme.

Aidha, Bodi hiyo ilimwelekeza Mkandarasi huyo kuwasha umeme katika Kijiji cha Kakeneno na ifikapo mwishoni wa wiki ijayo wananchi wawe wameunganishwa na umeme kwani miundombinu imeshafika kijijini hapo na wananchi wameshafanya wiring kwenye nyumba zao.

Vilevile, baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Mutundu, Bodi hiyo iliagiza umeme uwashwe tarehe 18 Novemba, 2019 kwani kuna miundombinu yote ya umeme na kilichobaki ni kuwasha tu umeme.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni Whitecity Guangdong JV, Nuhu Mringo alisema kuwa kampuni hiyo imejitahidi kutekeleza maagizo ya Bodi yaliyotolewa Wiki mbili zilizopita na kuahidi kuendelea kutekeleza kazi hiyo kwa kasi na kwa viwango.

Ikiwa wilyani Chato, Bodi hiyo ilikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Mutundu, Kakindo, Kamanga, Mnekez, Kakeneno na Matofali.

Kampuni ya Bia Serengeti kuendelea kudhamini michezo nchini

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto), akipokea tuzo ya udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara trophy 2019 kutoka kwa mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo, Brigedia Generali mstaafu, Michael Luwongo (kulia) katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Dar es Salaam jumamosi.

Mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta  akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza mashindano ya Gofu ya Waitara trophy 2019, Samuel Kileo aliyeshinda kwa NET 64

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta  akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti kwa kampuni ya hiyo kudhamini mashindano ya Gofu ya Waitara trophy 2019
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula jioni iliyoambatana na  kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Gofu ya Waitara trophy 2019.
 Wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha jioni

Mkapa: Mpango wa bima ya afya nilijifunza kwa Rostam Aziz

$
0
0
Na Ripota Wetu, Dar es Salaam 

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameweka wazi kuwa uamuzi wa kuwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni mpango ulioasisiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz.

Katika kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ alichokizindua wiki iliyopita jijiji Dar es Salaam, Mkapa ameeleza alijifunza mpango huo wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga alikouasisi mwaka 1996 kabla ya kutangazwa rasmi kuwa wa kitaifa.

“Njia nyingine ya moja kwa moja ya kuwasaidia masikini ni kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ambao umejitolea kuzipatia familia hizo bima za afya.

“Nilijifunza kuhusu mpango huu kutoka kwa Rostam Aziz, Mbunge na mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa.

“Mwaka 1996 alianzisha mpango wa bima ya afya kwa wananchi wake wa Jimbo la Igunga kwa kiwango kidogo cha fedha ya Sh 10,000 ambacho kilisaidia familia yenye watoto wanne kutumia bima hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima. Tuliamua kuutangaza mpangohuu kitaifa,” ameeleza Mkapa katika kitabu chake hicho.

Amesema ingawa mpango huo ulipoanzishwa haukueleweka vizuri kwa watu kwani wengine walisema “sitaumwa sasa kwanini nitoe fedha yangu kwenye mfuko huu,” lakini waliendelea kusisitiza juu ya mpango huo.

KUPANDA KWA BEI YA WALI MAHARAGE,CHIPS KUKU CHUO KIKUU DAR, WANAFUNZI WAJA JUU

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

BAADA ya kupanda kwa bei ya vyakula na hasa vilivyozoeleka vikiwemo vya Wali maharage na chipsi kuku katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Serikali ya Wanafunzi Chuo hicho(DARUSO) imeamua kufanya mazungumzo na watoa huduma ya vyakula ili kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya vyakula ambayo wamedai iko juu.

Hata hivyo tayari Serikali hiyo ya wanafunzi imetoa waraka unaoeleza kwa kina kuhusu kupanda kwa bei ya vyakula na kusababisha athari za kisaikolojia kwa wanafunzi kwa kile walichoeleza hali ya maisha si rafiki kwao kumudu gharamu hizo.

Sehemu ya waraka huo wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliosainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya DARUSO Mliman Hamis Hamis umesema kupitia ofisi ya Rais imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mfumo wa bei za vyakula kiholela kwa baadhi ya vyakula pendwa.

Hivyo Ofisi ya Rais DARUSO inawapa pole wanafunzi wote walioathirika na changamoto hizo kwa namna moja au nyingine.

Pia waraka huo umesema Serikali ya wanafunzi inatambua kuwepo kwa changamoto hiyo kubwa japo hatua za mazungumzo zimekwishafanyika mara kadhaa na imeonekana kutozaa matunda kutokana na wawekezaji kusimamia mikataba yao waliyoingia na Chuo kama inavyowaelekeza bila kujali uwezo wa wanafunzi kumudu bei elekezi katika mikataba hiyo.

Akizungumza na Michuzi Globu ya jamii jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2019, Katibu Mkuu DARUSO Hamis Hamis amesema kwa sasa wanaendelea na mazungumzo kati yao na watoa huduma ya vyakula.

"Tunaendelea na mazungumzo kati yetu na watoa huduma ya vyakula hapa chuoni.Mazungumzo yanakwenda vizuri na tutafikia pazuri.Mfuko wa bei ya vyakula hapa chuoni umekuwa mkubwa sana na maisha yetu yanafahamika,"amesema Hamis.

Ameongeza wanafunzi walio wengi hawana fedha mfukoni na hata wale ambao wamepata mkopo wa Serikali fedha bado hazijaingia katika akaunti zao , na hivyo kuongeza kwa bei ya vyakula kumesababisha changamoto za kimaisha.

Hata hivyo ametoa ombi kwa wanafunzi kuendelea kuwa na subira wakati mazungumzo yakiendelea na wawe na imani na Serikali yao ya wanafunzi ambayo inashughulikia malalamiko hayo.

Hata hivyo wakati DARUSO wakitafuta ufumbuzi wa kushuka kwa bei ya vyakula chuoni hapo, mwishoni mwa wiki Waziri wa Kilimo na Chakula Japhet Hasunga amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza amesikia kuna watu wanalalamika kuhusu kupanda kwa bei ya vyakula ambapo amewataka wafahamu Serikali haiwezi kumpangia bei mkulima.

Wakati anafafanua kupanda kwa bei ya vyakula Waziri Hasunga alieleza kwamba mkulima anapokuwa katika shughuli zake za kilimo hadi anavuna hakuna mtu anayejua gharama anazotumia mkulima katika kuandaa shamba , kupanda, kupalilia hadi kuvuna mazao yake , sasa iweje Serikali iwapangie bei.

Katika hilo Katibu huyo wa DARUSO amesema ni kweli Waziri alichoongea mkulima anapata changamoto nyingi wakati analima lakini hiyo haina maana aachwe apange bei anavyotoka.

"Ifahamike mkulima hapeleki sokoni, hivyo kuna mtu anakwenda kununua na kuleta mazao sokoni na hapo ndipo yanakutana na wanunuzi au walaji ambao itabidi wabebeshwe mzigo wote na kufanya maisha kuwa magumu.Tunaomba hili la bei ya vyakula liangaliwe vizuri na sisi tunaimani na Serikali pamoja na watoa huduma,"amesema Hamis.

Hata hivyo DARUSO kupitia Katibu Mkuu huyo amesema Serikali yao imeapa kuwatumikia na kuyatetea maslahi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa namna yoyote ile.

"Rais wa DARUSO 2019/2020 Hamis Mussa ametoa amri kwa watoa huduma ya vyakula wote hapa chuoni kurudisha haraka bei za awali kama ilivyozoeleka,"amesema Katibu Mkuu kupitia waraka wao na kuongeza iwapo amri hiyo haitatekelezwa watatumia ustaarabu mwingine.

WATANZANIA WAASWA KUPENDELEA MAVAZI YA UBUNIFU

$
0
0
   
    Na Khadija seif, Michuzi TV

MUASISI wa jukwaa la wiki ya Maonesho ya mavazi Afrika Mashariki na kati Mustafa Hassanali ameweka wazi lengo lake la kukuza lugha ya kiswahili kupitia Sanaa ya ubunifu.

 Hassanali amesema hayo wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo la Maonesho la ubunifu wa mavazi( Swahili fashion week), ambapo kila mwaka huwakutanisha wabunifu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

"Mbali na kuonesha mavazi katika jukwaa hilo, kuna kuwepo na vitu vya kiubunifu vilivyobeba majina, kwa mfano mishono ya nguo ,Mwanamke nyonga,kibwaya ,mikufu,hereni ambavyo ni vya Kitanzania hivyo kwa namna moja au nyingine tunakua tumetangaza vitu vya kinyumbani zaidi kwa kupitia Sanaa ya ubunifu pamoja na lugha ya Kiswahili,"

Aidha jukwaa hilo la 12 tangu kuanzishwa kwake limepanga kufanyika desemba 6 hadi 8 katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam na litawakutanisha wabunifu 34 wa Afrika Mashariki na Ulimwenguni.

Hata hivyo Muasisi huyo amesema lengo la kuendeleza tasnia ya ubunifu Afrika bado linabaki mstari wa mbele kwa kupitia jukwaa Hilo na kwa Sasa wataweza kuona thamani ya bidhaa za ubunifu wa kitanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la Sanaa za ubunifu na uchongaji (TAFCA) Adrian Nyangamale ameeleza kuwa jukwaa hili ni mojawapo ya njia ya kukuza vipaji vya wabunifu kwani inawashirikisha hata wale wanaochipukia.

"Watu wanakutana pamoja kutoka sehemu mbalimbali lakini hata wale chipukizi wanapewa nafasi ya kuonyesha ujuzi wao wakibunifu pia wanapata nafasi ya kuona wabunifu wakubwa nakujifunza vitu vingi ili kuboresha Sanaa zao"

Pia Nyangamale amesema mbali na kupewa fursa kwa chipukizi kuonyesha ubunifu wao ,fursa nyingine wanapatiwa wanamitindo kupita majukwaani hivyo kwa namna moja ama nyingine Mustafa ana unga Mkono Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya hapa kazi tu.

"Ni wachache wenye Moyo  wa kipekee na kujitolea kuwajengea uwezo na kuwapa moyo vijana ambao hawana ajira ila vipaji wanavyo na ndio maana hata katika swala la ubunifu wa mavazi Mustafa amechukua jukumu la kuwapatia ajira vijana wengi,"

 Hata hivyo Nyangamale ametoa wito kwa wadau, wabunifu na wapenzi wa ubunifu wa mavazi kutoa mchango wao,kuthamini na kuvipenda vya nyumbani ili kuendelea kujitangaza zaidi kimataifa kupitia mavazi y ubunifu.
Rais wa shirikisho la Sanaa za ubunifu na uchongaji akizungumza na waandishi wabunifu pamoja na waandishi wahabari wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Maonyesho la  ubunifu wa mavazi (Swahili fashion week) katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.

Jinsi Watanzania wanavyoendesha magari 'gharama ya chini'

$
0
0
Kugunduliwa kwa mafuta na gesi katika baadhi ya nchi za Afrika kumeweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kununua nishati nje kwa matumizi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa kipindi cha miaka 15, toka Tanzania ilipoanza kuzalisha na kusambaza gesi, imeokoa kiasi cha shilingi Trilioni 30, ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje kwa ajili ya kuzalisha umeme na uendeshaji wa viwanda.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio, takriban asilimia 60 ya umeme unaozalishwa nchini unatumia gesi asilia, huku nishati hiyo pia ikitumika viwandani mbali na kutumika kuendesha magari katika siku za hivi karibuni.

Kulingana na Mwanahabari wa BBC Halima Nyanza magari yanayotumia mfumo wa gesi, yamekuwa yakiongezeka nchini Tanzania kila uchao.

Katika eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam, kunakopatikana kituo pekee kinachotumia mfumo wa gesi katika uendeshaji wa magari, Mwanahabari huyo alikutana na Augustin - dereva wa UBA, aalimwelezea ni nini haswa kilichomshinikiza kuanza kutumia mfumo wa gesi katika gari lake.

Dereva huyo anasema kwamba alilazimika kutumia nishati ya gesi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi mbali na bei ya juu ya mafuta

''Ninatumia gesi kwa kuwa ni bei rahisi kulingana na hali ya uchumi ya sasa ilivyo, lakini pia ukitazama kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha mafuta ambayo unaweza kutumia mengi kwa siku huku gesi ukitumia fedha chache lakini kwa muda mrefu''.

''Hii gesi nikijaza dola saba na Marekani in maana ninaweza kutembea kilomita 150 ukichanganya na foleni za mjini'', aliongezea.PICHA KWA HISANI YA  GETTY IMAGES

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio anasema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji vituo vingine viwili vikubwa vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya kusambaza gesi kwenye vituo vingine vidogo katika maeneo mbalimbali.

Bwana Mataragio anasema kwamba takriban magari 300 nchini Tanzania yamelkuwa yakitumia gesi badala ya mafuta , huku mengi zaidi yakiendelea kubadilishga mifumo yao ya mafuta hadi kuwa ile ya gesi

''Kufikia sasa zaidi ya magari 300 yanatumia gesi .Tulianza mwaka 2009 ambapo kituo cha kwanza cha gesi kilijengwa hapa Dar es salaam ambacho kinatumika katika kujaza magari gesi. Tangu kipindi hicho kumekuwa na karakarana ambazo zimekuwa zikibadilisha mifumo ya mafuta hadi gesi''.

kusoma zaidi bofya BBCSwahili.com

Shida ya Udumavu Rukwa inaanzia kwenye fikra hizi – Meya wa Sumbawanga

$
0
0

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbwanga Mh. Justin Malisawa amewataka wanawake mkoani Rukwa kuachana na dhana kuwa familia zinazopendelea kula mboga za majani ni masikini na hivyo kupelekea kinamama wengi kushindwa kula mboga za majani kuhofia kuitwa masikini jambo linalopelekea udumavu kuendelea kuwepo kaika mkoa wa Rukwa.

Amesema kuwa udumavu unatokana na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kula mlo wa aina moja pamoja na kuwa ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa uzalishaji nchini na kusisitiza kuwa mboga za majani ni muhimu kwa wanawake hasa wajawazito kwani huwasaidia kuwajenga na kumjenga kiumbe aliyemo tumboni mwake kukua kiafya na kiakili. 

“Na bahati mbaya tumejijengea utaratibu kwamba familia ambayo inayokula mboga za majani kwa wingi ni familia masikini, huo ndio ukweli ukimkuta mama Fulani kakarangiza mboga za majani, kesho mboga za majani, keshokutwa mboga za majani, majirani watamwita masikini wa kutupwa,” Alisema.

Mstahiki Meya ameyasema hayo kwenye kongamano la wanawake wajasiriamali lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Sumbawanga, kongamano ambalo lilihudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali ikiwemo mabenki, bima ya afya, SIDO, TRA, TBS na watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga George Lupilya amesema kuwa Manispaa Sumbawanga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imejipanga kuhakikisha inatekeleza maagizo na Sera mbalimbali za nchi ili kuhakikisha Mwananchi anafikiwa kwa huduma za Kijamii na kujikwamua Kiuchumi.

Aidha, Kaimu huyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Kilimo amewaasa kinamama hao kuhakikisha wanajishughulisha na kilimo cha bustani za mboga mboga kwa kulima walau tuta moja ama mawili ili kuweza kupambana na udumavu pamoja na utapiamlo katika mkoa.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Manispaa ya Sumbawanga Frank Mateni amesema kuwa dhumuni la kufanya kongamano hilo ni kuamsha ari, kuwajengea uwezo wanawake wajasiliamali kuona ni fursa gani ambazo wanazo katika mazingira yao wanayoishi wanayoweza kuyatumia kujiongezea kipato.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na wanawake wajasilimali zaidi ya 570 wakiongozwa na viongozi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Rukwa.
 Mstahiki Meya wa Manispaa  ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa
 Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa (kaunda suti ya bluu) akifurahi pamoja na washiriki wa kongamao la wanawake wajasiliamali kuwezeshwa kiuchumi katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga.
 Baadhi ya Wanawake wajasiliamali waliohudhuria katika kongamano lililolenga kutoa mafunzo ya kurasimisha shughuli zao paoja na kutambua fursa mbalimbali za kujipatia kipato zilizopo katika maeneo yanayowazunguka katika mji wa Sumbawanga.

UMWAKIKA BADO WANAHITAJI NGUVU YA WADAU KUFIKIA MALENGO.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Miongoni mwa masuala ya Kijamii yanayopewa kipaumbele kwa sasa ni pamoja na suala la Afya, ambapo kwa kutambua hilo Umoja wa Maendeleo ya Wanawake wa Kiislamu Kagera (UMWAKIKA) Kupitia Sadaka zao na waumini wengine pamoja na madhehebu mengine, wanaendelea na Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto inayojengwa katika Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.

Hajat Faidha Kainamula ni Mwenyekiti wa UWT - CCM Mkoa Kagera, akiwa Mgeni Rasmi katika Jaula na Harambee ya Uchangiaji wa Ujenzi iliyofanyika Hamugembe Manispaa ya Bukoba, amefurahishwa na jitihada za akina na mama Hawa zenye lengo la kumkomboa Mwanamke juu ya huduma anayopatiwa, akiongeza kuwa Hospitali zimekuwa zikiwadhalilisha akina mama katika utoaji wa huduma, bila kujali Dini zao, lakini kukamilika kwa Hospitali ya Nyanga utakuwa mkombozi juu ya stara ya akina Mama wote.

Katika Tamasha hilo jumla ya Shilingi Milioni Moja na laki tatu zimechangwa kupitia Michango yao na mnada wa mazao na vitu mbalimbali vilivyoletwa na akina Mama wa Misikiti tofauti. 

Ujenzi huo, ulioanza miaka ya Nyuma, umekuwa ukisua sua kutokana na Nguvu ya akina mama hawa kuwa kidogo, na Mara nyingi wamekuwa wakifanya matamasha na Harambee mbalimbali ili kuona kama Shughuli ya Ujenzi itasogea, na tayari maandalizi na mipango inaendelea kwa Tamasha kubwa la Mwisho wa Mwaka litakalofanyika Desemba 27 hadi 29 Mwaka huu.
 Pichani Katibu wa UMWAKIKA Hajat Nuriat Kaboyo, akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani), kubwa ikiwa ni Taarifa ya Ujenzi ilipofikia na kile kinachotarajiwa siku za mbeleni.
 Pichani sehemu ya akina mama waliohudhuria Jaula hiyo, kutoka Misikiti Mitano kama wanavyoonekana wakifuatilia Ratiba.
 Pichani ni Mgeni Rasmi Katika Jaula ya Akina mama wa Kiislam Hajat Faidha Kainamula Mwenyekiti wa UWT Mkoa Kagera, akitoa salaam zake kwa akina mama waliohudhuria Jaula hiyo (hawapo pichani)
 Pichani sehemu ya akina mama waliohudhuria Jaula hiyo, kutoka Misikiti Mitano kama wanavyoonekana wakifuatilia Ratiba.
Pichani Miongoni mwa Mazao na Vitu mbalimbali viliouzwa kwa njia ya mnada ili kukusanya pesa za Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto, inayosimamiwa na Umoja wa maendeleo ya wanawake wa Kiislamu Kagera (UMWAKIKA) Inayojengwa Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.

Ujerumani, Uholanzi, Austria, Croatia zatinga Euro 2020

$
0
0
Mabingwa hao mara tatu walijikatia tiketi baada ya kuwazaba Belarus mabao manne kwa sifuri, huku Toni Kroos akifunga mawili na kuiongoza timu yake kukamata usukani wa Kundi C.

Nambari mbili Uholanzi pia ilifuzu licha ya kutoka sare tasa na Ireland Kaskazini mjini Belfast. Nahodha wa Ireland Kaskazini Steven Davis alipoteza penalti katika kipindi cha kwanza. Kwa Waholanzi, itakuwa mara yao ya kwanza kushiriki mashindano makubwa tangu Kombe la Dunia 2014. 

Austria waliungana na Poland ambao tayari wamefuzu katika Kundi G kwa ushindi wa 2 - 1 dhidi ya Macedonia Kaskazini. Poland ilishinda 2 - 1 katika ushindi wao wa kwanza nchini Israel tangu 1998. Croatia walifuzu kama washindi wa Kundi E kwa ushindi wa 3 -1 dhidi ya Slovakia.

Ujerumani ambayo inakumbwa na majeruhi kikosini, ilianza na safu ya ulinzi isiyo ya kawaida ambapo Matthias Ginter wa Borussia Moenchengladbach alipangwa na Robin Koch wa Freiburg. Ilikuwa mechi ya pili kwa Koch katika timu ya taifa nay a kwanza ya ushindani. Safu ya mashambulizi ya timu hiyo ya Joachim Loew ilikuwa moto wa kuotewa mbali huku Timo Werner, Serge Gnabry na Toni Kroos wakitamba.

Ujerumani ilipata bao la kwanza kupitia Ginter katika dakika ya 41, Leon Goretzka akafunga dakika nne baada ya kipindi cha pili kuanza. Kroos akatupa kambani bao la tatu baada ya kuandaliwa pasi na Ginter katika dakika ya 55. Manuel Neuer aliokoa penalty ya Belarus kabla ya Kroos kufunga kazi kwa kutikisa wavu kwa mara ya pili katika ya 83.

Kusoma zaidi Bofya Hapa

UPELELEZI WA KESI YA ANAYEDAIWA KUMUUA MKEWE UNACHAPISHWA

$
0
0
Mfanyabiashara, Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack.

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara, Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuwa upelelezi wa kesi hiyo kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Novemba 18, mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa 

Wakili Wankyo amedai, shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi umekamilika na  jarada lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyingine ili waweze kufatilia suala hilo.

Hakimu Ally amearisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu .

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.

CGP KASIKE AFANYA MAZUNGUMZO NA RC. MNYETI KABLA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MANYARA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akitambulisha ujumbe alioambatanao kabla ya mazungumzo mafupi na na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisini kwake kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18, 2019. Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipotembelea Ofisini kwake leo Novemba 18, 2019.

 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisi kwake leo kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18, 2019. 

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akizungumza na wafungwa na mahabusu wa Gereza Mbulu(hawapo pichani) leo Novemba 18, 2019 alipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo(Picha zote na Jeshi la Magereza).

 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Mbulu, SP. Danson Mpinga alipowasili Gereza Mbulu leo kwa ziara ya kikazi. Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.

ASKALI POLISI KIZIMBANI KWA KUPOKEA RUSHWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
ASKARI Polisi Itialy Omary na  mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Lezilie Koini na wamefikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kupokea rushwa ya Sh. 200,000/-

Hata hivyo mahakama imemsomea mashtaka mshtakiwa Koini peke yake kwani mshtakiwa Omary hajafika mahakamani hivyo mahakama imetoa amri ya kukamatwa kwake.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horombe amedai Mei 8, 2018 mshtakiwa Omary na Koini kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mussa Abdallah ikiwa kama kishawishi ili asikutwe na we na hatia katika kosa namba 211/2018 la usalama barabarani.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa Omary alikubali  kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai  bado haujajiandaa hivyo wanaomba ahirisho la muda kwa ajili ya kujiandaa. 

Hata hivyo Hakimu Mmbando alitoa masharti ya dhamana  kwa mshtakiwa ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na vitambulisho halali atakayesaini bondi ya Sh. 500,000. 

Mshtakiwa ametimiza  masharti ya dhamana, nje kwa dhamana, kesi itatajwa tena Novemba 21 mwaka huu.

TAALUMA YA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII IWE CHACHU YA MABADILIKO KATIKA JAMII: DKT. JINGU

$
0
0


Na Mwandishi Wetu Morogoro

Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amevitaka Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu kuleta mabadiliko katika jamii zao na kuweza kujiajiri na kuajiri watu wengine kuliko kutegemea kuajiriwa.

Dkt.John Jingu ameyasema haya leo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilicholenga kubadilishana uzoefu kwa wakuu hao wa vyuo katika utendaji kazi na kujengeana uwezo ili Taasisi na Vyuo viweze kufanikisha malengo ya Taifa.

Dkt. Jingu amesema kuwa taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii lazima iwe nyenzo ya kutatua changamoto zilizopo katika jamii ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana kwa kutoa taaluma itakayowapa fursa wahitimu kujiajiri kutokana na taaluma waliyopata.

“Umefika wakati sasa Taasisi na Vyuo kuja na Mpango Mkakati wa namna ya kutekeleza dhana ya kujiajiri kwa lengo la kuzalisha wahitimu mahiri " alisema Dkt. Jingu.

Ameongeza kuwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii vimetoa mchango mkubwa sana katika kutatua changamoto za jamii na hivyo jamii kuthamini uwepo wa vyuo katika jamii na mafanikio yaliyoonekana kwa vyuo hivyo yaonekane kwa kila chuo.

Aidha Dkt. Jingu amevitaka Vyuo hivyo kuanzisha Vituo vya kielektroniki vya ubunifu na maarifa (Digital Innovation Centre) ambao utarahisisha upatikanaji wa maarifa na ujuzi kwa haraka zaidi kuliko kusoma vitabu na itatoa fursa ya kupata maarifa katika muda mfupi. 

“Natumaini ushiriki wetu katika kikao kazi hiki utatuongezea ari na ubunifu wa kazi katika maeneo yetu na mtazingatia mafunzo na maelekezo yatakayotolewa katika kuhakikisha vyuo vinatoa matokeo chanya kwa kuzalisha wataalam wenye ujuzi na maarifa ya kazi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii nchini Patrick Golwike amesema kuwa ili kujipambanua katika jamii umuhimu wa Kada ya Maendeleo ya Jamii inatakiwa kuwa na mbinu ya namna ambayo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii itatoa wataalam wakaosaidia kuleta mabadiliko kwa jamii.

Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa Kada ya Ustawi wa Jamii ni moja kati ya Kada ambazo zina uwanda mpana wa kujiajiri na kuajiriwa hivyo Vyuo na Taasisi ya Ustawi wa Jamii zijikite katika kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu hasa kujiajiri.

Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wamekutana mkoani Morogoro katika kikao kazi kilicholenga kutafuta namna bora ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii katika kuleta mabadiliko katika jamii.
 Katibu Mkuu maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole Bw. Rajab Kaleranda wakati alipowasili mkoani Morogoro kufungua mkutano uliowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza na Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini wakati wa kikao kilichowakutanisha wakuu hao katika kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike akielezea jinsi Kada ya Maendeleo ya  Jamii inavyosaidia katika kueta mabadiliko na kusaidia jamii wakati kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akielezea jinis a Kada ya Ustawi wa Jamii inavyosaidia katika kueta mabadiliko na kusaidia jamii wakati kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
 Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini wakisikiliza mada mbalimbali katika kikao kilichowakutanisha kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images