Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

HALMASHAURI YA NYASA YATEKELEZA AGIZO LA DC NYASA

$
0
0


Wafanyabiashara ya samaki Wilayani Nyasa,wakiwa katika soko jipya la fisheries ambalo mkuu wa wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, aliipa halmashauri ya Wilaya ya Nyasa siku saba kuanzisha soko la samaki ili kutatua changamoto iliyokuwa inawakabili wafanyabiashara ya samaki Wilayani Nyasa, ya kutokuwa na eneo maalumu ya kuuzia samaki.(picha na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa)

…………………..

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imetekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi Isabela Chilumba la kuanzisha Soko la samaki katika eneo la Fisheries Wilayani hapa, kwa kipindi cha siku saba.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa alitoa agizo hilo octoba 30 mwaka huu, wakati akiongea na wavuvi,p amoja na wachuuzi wa mazao ya uvuvi kwa lengo la kutatua changamoto ya kutokuwa na Soko la samaki wilayani Nyasa.

Uchunguzi uliofanyika na mwandishi wa habari hizi umebaini kabla ya kutimia siku saba za agizo hilo, soko la samaki lilikuwa limeshaanza katika jengo la karakana ya kutengenezea boti, ambalo lilikuwa halitumiki. wavuvi wengi wa Mbamba-bay wamefurahia uwepo wa soko hili ambalo limetatua changamoto, kero ya kutokuwa na sehemu maalumu ya kuuzia samaki, iliyokuwa inawakabili wavuvi na wachuuzi wa samaki.

Mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi Wilaya ya Nyasa Bernard Semwaiko amethibitisha kuanza kwa soko hilo la samaki Mjini Mbamba-bay na leo amefanya kikao na uongozi wa kamati ya soko la samaki Mbamba-bay kwa lengo la kutatua changamoto zingine katika soko hilo la samaki.

Wafanyabiashara wa samaki wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, na Uongozi wa Halmashauri Nyasa kwa kuanzisha Soko la Samaki , na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanatekeleza majukumu yao bila kikwazo chochote.


GANGWE MPYA KWENYE GAME??

$
0
0





Ukiona mtu anaweza kufanya jambo lake bila uoga wa kuona wale wabishi na wakubwa zaidi yake kwenye hilo jambo nao wanafanya kwa wakati huo ni lazima ikupe maswali kidogo juu yake..Ndivyo ambavyo msanii anayekuja kwa kasi anavyowapa watu mshtuko na maswali baada ya kuachia ngoma yake inayokwenda kwa jina la BWEKA inapatikana hapa

https://youtu.be/ZI8XdkybUEA

jumatano ya wiki hii huku vyuma kama Diamond Platnumz,Harmonize na Ali Kiba nao wakiwa wametoa ngoma zao zinazozidi kushika chati kila siku.SALHA ambaye mbali na kuwa bado mchanga kwenye sanaa ya muziki ameonyesha kutokuogopeshwa na uwepo wa kazi za wasanii wakubwa sokoni kwa kuachilia nyundo yake kali ambayo kwa jinsi inavyozidi kupokelewa vizuri na wasikilizaji pamoja na vituo mbalimbali inatufanya tujiulize, 
 
je huyu ni gangwe mpya wa muziki wa Tanzania??Haikuishia hapo ambapo wasanii wakubwa pia kama Benpol wameonyesha wazi kuikubali BWEKA kwa kuitupia katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram muda mchache tu baada ya kuiachilia..Kwa haraka picha anayotupa ni ya ujasiri mkubwa katika sanaa yake licha ya kuwa binti mdogo wa miaka 19 tu..
 
BWEKA ambayo imepikwa kwa mtayarishaji Aloneym ni kati ya mishale ambayo mwanadada huyu mwenye sauti ya kipekee ameanza kuirusha akiwa chini ya menejimenti yake ya The Collective Live.
 
Salha ambaye pia yupo kwenye maandalizi ya kuachia video ya ngoma hii hivi karibuni,anaweka wazi kuwa BWEKA ni moja tu kati ya ngoma zake kali ambao unapatikana sasa YouTube na anaamini watanzania wataupokea kwa mikono miwili na utawakonga nyoyo sana huku maandalizi ya video na mambo mengine ya kimuziki akiyatupia katika page yake ya instagram inayokwenda kwa jina la Salhaofficialtz 

TANZANIA NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KATIKA ENEO LA MAFUTA, GESI NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0






Na Mwandishi Maalum Dodoma Nov: 15/2019

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardusi Kilangi, jana
( alhamisi) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa
Serikali ya Angola hapa Nchini, Mhe. Balozi Sandro Renato
Agostinho de OLIVEIRA.

Mazungumzo baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa
Kilangi na Balozi Sandro Renato Agostinho de OLIVEIRA ambayo
yamefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Jijini Dodoma, yalijikita katika kuangaliana namna gani Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania itakavyoshirikiana na Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Angola.

Balozi wa Angola Mhe. Sandro Renato Agostinho de OLIVEIRA,
alimweleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus
Kilangi kwamba, Serikali yake, yaani Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ingependa kushirikiana karibu na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania katika maeneo kadhaa
likiwamo namna ya kukabiliana na tatizo la rushwa.

"Tungependa (Angola) kuanzisha mahusiano na masharikiano baina
ya Ofisi yako na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Angola.
Tunaamini kuna maeneo mengi ambayo tunaweza kubadilishana
uzoefu likiwamo hili la kukabiliana na changamoto za
rushwa". Akasema Balozi de OLIVEIRA.

Aidha Balozi huyo wa Angola alisema amefurahi sana kufika
Jijini Dodoma kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza.
Kwa upande wake Profesa Adelarus Kilangi pamoja na kushukuru
kwa Balozi huyo wa Angola kumtembelea, alimweleza kwamba
Ofisi yake ipo tayari kuanzisha mahusiano na mashirikiano na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Angola.

AG Kilangi pamoja na kukubaliana kushirikiana na kubadilisha
uzoefu katika eneo la kukabiliana na rushwa, yeye alitaka
ushirikiano pia katika eneo la mafuta na gesi na pia katika
maeneo ya kujengeana uwezo na maarifa katika maeneo
mbalimbali.

Itakumbukwa kwamba, Nchi ya Angola ni kati ya nchi chache za
Bara la Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinautajiri
mkubwa wa mafuta na gasi na wanauzoefu wa kutosha eneo
hilo.

SERIKALI YAZINDUA WIKI YA KUHAMASISHA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA ZA ANTIBIOTIKI

$
0
0
KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Eliasi Kwesi amezindua rasmi shughuli za kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa za Antibiotiki katika kuelekia wiki hiyo duniani itakayofanyika kuanzia Novemba 18-24, mwaka huu Duniani kote.

Katika tukio hilo, Dkt. Kwesi aliweza kusoma tamko rasmi akimwakilisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ambapo alitaka jamii kuelewa athari na tatizo kubwa ambalo limekuwa likiongezeka duniani kote.

“Kuanzia tarehe 18-24 Novemba, mwaka huu, duniani kote tunaadhimisha wiki ya kampeni ya dawa aina ya Antibiotiki (World Antibiotic Awareness Week).

Lengo ni kusisitiza na kuongeza uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa hizi ili kupunguza matumizi yasiyostahili na hatimaye kuzuia ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa hizi” alieleza Dkt. Kwesi akisoma tamko hilo.

Dkt. Kwesi aliitaka jamii kuzingatia matumizi sahihi ya kuepukana hasa kwenye kinga ya maambukizi kwa njia ambazo zinaweza kufanywa mahali popote ikiwemo ngono salama, kuosha mikono na chanjo.

Aidha, alisema kuwa, Serikali imendaa mipango na miongozo mbalimbali ili kutekeleza kazi kwa usahihi ikiwemo mpango wa Taifa wa kupambana na usugu wa dawa dhidi ya vimelea mbalimbali Antimicrobial ( 2017-2022).

“Aidha, niwaagize watoa dawa kote nchini kuandika dawa kwa kufuata mwongozo wa matibabu wa mwaka 2017 na kutumia majina halisi ya dawa (Generics). Pia naagiza vituo vyote vya huduma ya afya kutekeleza miongozo ya kukinga na kuzuia maambukizi ambayo ni muhimu sana kwa kuzuia usugu katika sehemu zao za kazi” alisema Dkt. Kwesi.

Akielezea ripoti ya benki ya Dunia ya mwaka 2017 inabainisha kuwa zaidi ya watu 700,000 wanafariki kila mwaka kutokana na usugu wa dawa.

“Hatua madhubuti zisipochukuliwa haraka zaidi ya watu milioni 10 watafariki kila mwaka kutokana na usugu wa dawa ifikapo mwaka 2050.

Hali hii ya usugu wa vimelea inaweka mashaka makubwa ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa hili kwa kusababisha vifo kutokana na kuongezeka kwa magonjwa sugu yasiyotibika kwa kutumia dawa zilizokuwa na uwezo wa kutibu, kuongezeka kwa umasikini kutokana na kuugua muda mrefu na kutumia dawa ghari zaidi lakini pia kuongezeka kwa vifo vya mifugo na udhalishaji hafifu wa chakula” alieleza Dkt. Kwesi.

Hata hivyo Dkt. Kwesi alizitaka Wizara zingine wadau wakiwemo Mawaziri wa Mifugo na uvuvi,, Kilimo na Mazingira kwa pamoja kufanya kampeni zinazolenga kuongeza uelewa wa jamii juu ya matumizi sahihi na athari zitokanazo na matumizi holela ya dawa kwa binadamu na mifugo.

Kwa upande wao wadau walioshiriki katika tukio hilo wakiwemo wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya(WHO), Shirika la Chakula (FAO) na Shirika la Wanyama (OIE) walieleza wanashirikiana kwa pamoja na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya tatizo hilo.

MAHAFALI YA 33 CHUO CHA VETA SHINYANGA YAFANA

$
0
0


Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog 

Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Shinyanga, kimefanya Mahafali ya 33, huku wahitimu wakishauriwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili wapate mikopo na kujiajiri wenyewe, kuliko kukaa mitaani na kusubiri ajira na wakati ujuzi wanao wa kuwapatia kipato na hatimaye kuendesha maisha yao.

Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 15, 2019 kwenye viwanja vya chuo hicho, huku mgeni rasmi akiwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi. Akizungumza kwenye Mahafali hayo,Kifizi amewataka wahitimu hao kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kupata fedha za halmashauri za mapato ya ndani asilimia 10, ambazo hutolewa kwa vijana asilimia nne, ili wapate mitaji na kujiajiri wenyewe kuliko kupoteza ujuzi wao kwa kusubiri kuajiriwa na kuanza kulalamika maisha magumu. 

“Natoa wito kwa wahitimu wa fani mbalimbali ambao mnahitimu leo muache tabia ya kutegemea kuajiriwa, bali mjijenge kujiajiri wenyewe kwani ujuzi mnao,muutumie kujipatia kipato na kuinuka kiuchumi,” amesema Kifizi.


“Pia mjiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili mpate mitaji na kufungua ofisi zenu na kujiajiri wenyewe, kuliko kumaliza masomo yenu hapa na kuishia kukaa mitaani na kulalamika hakuna ajira na wakati ujuzi mnao,”ameongeza. Katika hatua nyingine amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kujenga hosteli jirani na chuo hicho cha Veta, ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kupanga kwenye Magheto na kuambulia ujauzito, pamoja na wengine kuwa watoro sugu na kuacha masomo. 

Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Magreth Edward amesema changamoto kubwa ambayo hukabiliana nayo ni ukosefu wa ajira, huku wakiomba Serikali kulegeza masharti ya upataji wa mikopo asilimia nne kwa vijana ili wapate kujiunga kwenye vikundi na kupata mitaji ya kujiajiri wenyewe. 

Amesema wakati wanaanza kusoma mafunzo walikuwa 142, lakini wamehitimu wanafunzi 118, huku wanafunzi 24 wakishindwa kumaliza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo utoro sugu pamoja na wengine kuambulia ujauzito na kuacha masomo sababu ya kuishi kwenye Magheto. Aidha mratibu wa mafunzo chuoni hapo Rashid Ntahigiye, amesema wanafunzi hao 118 wamehitimu fani mbalimbali ikiwemo umeme, uselemala, uchomeleaji, ubunifu na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi pamoja na mafundi wa mitambo. 

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta mkoani Shinyanga Magu Mabelele, amesema chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 400, wasichana 133 na wavulana 267, huku akitoa wito kwa wazazi wa Shinyanga kupeleka watoto wao chuoni hapo ili wakapate ujuzi ambao utatimiza ndoto zao. TAZAMA PICHA HAPA CHINI Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akizungumza kwenye Mahafali ya 33 ya Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) Mkoani Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Kaimu mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mkoani Shinyanga Magu Mbelele akisoma taarifa ya chuo hicho na kumkaribisha mgeni rasmi. Mratibu wa mafunzo wa chuo cha Veta mkoani Shinyanga Rashid Ntahigiye akisoma taarifa ya chuo. Mwanafunzi Magret Edward akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake. Wahimitu wakiwa kwenye Mahafali. Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali. Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali. Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali. Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali. Wazazi wakiwa kwenye Mahafali. Wageni waalikwa na baadhi ya walimu wa chuo cha Veta wakiwa kwenye Mahafali. Awali Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhitimu wa fani ya ushonaji Magreth Edward namna wanavyoshona nguo wenyewe. Mwalimu Yona Mwambopa akimwelezeaMkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi namna wanavyofundisha fani ya ukataji na ung'arishaji wa madini ya Vito. Mwanafunzi Suzana Obed akikata madini ya Vito. Kaimu mkuu wa chuo cha Veta Magu Mabelele akimwelezea mgeni rasmi Mkurugenzi wa SHUWASA Flaviana Kifizi namna wanavyofundisha fani ya utengezaji wa magari kwa njia ya mitambo. Wanafunzi wakitoa burudani na kuonyesha mitindo mbalimbali ambayo wamebuni na kushona wenyewe. Burudani ya kuonyesha mitindo ikiendelea kutolewa. Burudani ya kuonesha mitindo ikiendelea kutolewa. Awali wahitimu wakiingia ukumbini Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Wabunge Wapitisha Azimio la Kumpongeza Rais Magufuli

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuhairisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 11 leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuhairisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 11 leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha 17 cha Mkutano wa 11 wa Bunge leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_48975" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mhe. Jason Rwekiza akiwasilisha hoja binafsi ya kuazimia Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya wakati wa kuhitimisha kikao cha 17 cha Mkutano wa 11 wa Bunge leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Goodlucky Mlinga akichangia hoja kuhusu azimio la Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya wakati wa kuhitimisha kikao cha 17 cha Mkutano wa 11 wa Bunge leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Mhe Charles Mwijage akichangia hoja kuhusu azimio la Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya wakati wa kuhitimisha kikao cha 17 cha Mkutano wa 11 wa Bunge leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Sumve, Mhe Richard Ndassa akichangia hoja kuhusu azimio la Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya wakati wa kuhitimisha kikao cha 17 cha Mkutano wa 11 wa Bunge leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Mbunge wa Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Amina Mollel akichangia hoja kuhusu azimio la Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya wakati wa kuhitimisha kikao cha 17 cha Mkutano wa 11 wa Bunge leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Mawaziri mara baada ya kumaliza hotuba yake ya kuhairisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 11 leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma.Aliyeshikana naye mkono ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye ulemavu Jenista Mhagama. Kikundi cha Brass Band kikiongoza kuimba wimbo wa taifa wakati wa kuhairisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 11 leo tarehe 15/11/2019 jijini Dodoma.(Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

VOA SWAHILI: Duniani Leo November 15, 2019

VOA SWAHILI:Zulia Jekundu Episode 252


MEYA SITA ASHAURI WANANCHI KUPENDA BIDHAA ZINAZO ZALISHWA NYUMBANI, ASEMA ZINAUBORA WA HALI YA JUU

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita wa pili kulia mwenye suti, akikagua bidhaa za ngozi zinazozalishwa na wajasiriamali wa Halmashauri hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Patricia Henjewele.

…………………….

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni, Mhe. Benjamini Sita amesema kuwa kunahaja ya kuangalia namna ya kuwajengea uwezo wananchi kuwa natabia ya kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Meya Sita ametoa kauli hiyo leo, wakati akikagua mabanda ya maonesho ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na Manispaa nakuwezeshwa na Mamlaka ya Biashara Tanzania Tan Tredi.

Meya sita amesema kuwa amefurahishwa na manispaa kuandaa maonesho hayo kwani kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuwatia moyo wajasiriamali na hivyo kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao.

Amefafanua kuwa Tanzania inauwezo mkubwa wakuzalisha bidhaa zangozi zenye ubora kutoka kwa wajasiriamali wa ndani na hivyo itaondoa dhana ya watu kwenda kununua bidhaa hizo nje ya nchi.

“ Tanzania tunauwezo mkubwa wakuzalisha vitu vizuri,tunapaswa kushirikiana kwa pamoja ili tuhakikishe bidhaa zetu zinapata soko la kutosha , lazima tutengeneze mazingira ya wenzetu kupata miundombinu ya vifaa ili waweze kuzalisha bidhaa nyingi nakupata soko nje ya nchi.

Meya sita alishauri kuwepo kwa masoko ya kati ya bidhaa( Supermarket) ili kuwezesha wananchi kupata bidhaa hizo kwa urahisi pindi wanapokwenda kununua mahitaji mengine jambo ambalo litaweza kuleta uzalendo na hivyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia bidhaa za ngozi.

Kwaupande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi,Dk. Patricia Henjewele alisema kuwa maonesho hayo yamekwenda sambamba na mafunzo ya utangazaji wa bidhaa ambapo wajasiriamali kutoka Manispaa ya Kinondoni wameshiriki.

Alifafanua kuwa baada ya kumalizika kwa maonesho hayo na mafunzo, halmashauri imeandaa maonesho mengine yatakayofanyika Disemba 12 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Pekazi ambapo wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali watashiriki.

Kwaupande wao washiriki wa maonesho hayo wameipongeza manispaa ya Kinondoni kwakuandaa mafunzo hayo kwani imekuwa fursa kutangaza bidhaa ambazo wamezizalisha wenyewe na hivyo kuomba wananchi kuwaunga mkono.

MAJALIWA Atokwa MACHOZI MAGUFULI Alivyomwaga MAMILION kwa WASANII

TAKUKURU Yakabidhiwa Jalada la kufanyia Uchunguzi Upotevu wa Fedha Katika Ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe akimkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti ya upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia leo jijini Dar es Salaam

…………………..

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeikabidhi TAKUKURU jalada la kulifanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe amekabidhi jalada hilo kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo katika ofisi ndogo za Wizara jijiji Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja kutokana na jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za uma.

Uchunguzi huo unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Kuhusu kiwango cha fedha kilichopotea Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe, amesema kitajulikana mara baada ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walililokabidhiwa.

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI NA MILLENIUM WOMEN'S GROUP WAKABIDHI MISAADA MBALIMBALI KITUO CHA KULELEA WAZEE CHA NUNGE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ameungana na wake wa viongozi
mbalimbali katika kusherehekea miaka 10 ya umoja wao uitwao  New
Millenium Women’s Group kwa kutoa misaada katika kituo cha kulea wazee
cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.

Mama magufuli, ambaye aliambatana na Mlezi wa umoja huo Mke wa Waziri
Mkuu Mama Mary Magufuli, Mwenyekiti wake Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu
Mama Tunu Pinda na Mama Asina Kawawa aliungana na wajumbe hao kutoa misaada mbali mbali ya ujenzi, chakula na nguo.

Mama Magufuli alichangia jumla ya gypsum 178 huku Makamu wa Rais Mhe
Samia Suluhu Hassan akituma mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya
ukarabati wa Bwalo la kituo hicho kikongwe ambacho hadi leo Novemba
15, 2019 kilikuwa na wazee 26.

Umoja huo wa New Millenium Women’s Group ulichangia ujenzi wa mnara wa kisima cha maji kwa gharama ya shilingi milioni 1.9, vyakula na nguo
vyenye thamani ya shilingi milioni 3.

.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group akiwasili katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Mama Tunu Pinda, Mama Mary Majaliwa, Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mama Asina Kawawa.


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada ya nguo navyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar essalaam leo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akitoa misaada ya nguo na vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar essalaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada wa gypsum 178 kaajili ya ujenzi wa bwalo la kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja nawajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja nawajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s na wakaaazi wa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo
Wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao NewMillenium Women’s Group wakiwa katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo walikofika kutoa misaada mbalimbali katika kuadhimisha umoja huo.PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI APIGA SIMU NA KUONGEA NA WASANII UKUMBINI

JESHI LA POLISI LATOA NENO KUELEKEA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS RAIS. MAGUFULI TAMASHA LA MWALIMU ARTS FESTIVAL 2019

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza kwa simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihotubia katika Kongamano la Sanaa la Mwalimu (Mwalimu Arts Festival) lililofanyika katika kituo cha Mikutano wa Kimatifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam , ambapo Mhe. Rais ameahidi kutoa Tsh Milioni mia moja (100) kwaajili ya Mfuko wa Sanaa. Novemba 15, 2019



Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe .Kassim Majaliwa( hayupo pichani), katika Tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019, lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Juilius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisikiliza simu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli alipopiga kuwapongeza wasanii kwa kuanzisha tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019, aliyeshikilia simu hiyo ni Rais wa Shirikisho la Muziki Nchini Ado Novemba.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na kumkaribisha Mgeni Rasmi katika Tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019 ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Juilius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza na Washiriki wa Tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019, lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Juilius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia washiriki wa Tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019, lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Juilius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019.

Wasanii na wadau mbalimbali wa Sanaa wakishangilia baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kuongea kwa simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihotubia katika Kongamano la Sanaa la Mwalimu (Mwalimu Arts Festival) lililofanyika katika kituo cha Mikutano wa Kimatifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam , ambapo Mhe. Rais ameahidi kutoa Tsh Milioni mia moja (100) kwaajili ya Mfuko wa Sanaa. Novemba 15, 2019
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza katika Kongamano la Sanaa la Mwalimu (Mwalimu Arts Festival) lililofanyika katika kituo cha Mikutano wa Kimatifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam , ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ameahidi kutoa Tsh Milioni mia moja (100) kwaajili ya Mfuko wa Sanaa. Novemba 15, 2019.


Msanii wa Mashairi ya Kughani, Mrisho Mpoto akitoa burudani katika Tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019 lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Juilius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019
Msanii wa Mashairi ya Kughani, Mrisho Mpoto akiingia kutoa burudani katika Tamasha la Mwalimu Arts Festival 2019 lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Juilius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019.

TAIFA STARS YAANZA VYEMA,YAIKUNA EQUATORIAL GUINEA 2-1

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya mataifa Afrika AFCON 2021 kati ya Tanzania na Equatorial Guinea umemalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Taifa Stars leo imeanza vema michuano ya Afcon kwa kuibuka kidedea mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Stars ilianza kwa kasi kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kuweza kutumia nafasi walizozipata na katika dakika ya 15 Equatorial Guinea aliweza kupata bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Pedro Obiang.

Kipindi cha pili Stars ilianza kwa kulazimisha mashambulizi na iliwapeleka mpaka dakika ya 68 ambapo Simon Msuva aliandika bao la kwanza akimalizia pasi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala' na kuweka mzani sawa.

Taifa Stars iliendelea kushambulia ikitafuta goli la ushindi na kupitia kwa Kiungo Salum Abubakari kwenye dakika ya 90 aliandika bao la lipi na la ushindi akiwa nje ya 18.

Ushindi huo unaifanya Stars kujikusanyia pointi zake tatu leo ikiwa kwenye uwanja wa Taifa na Novemba 20, Taifa Stars watashuka tena kucheza na Libya ukiwa ni mchezo wa pili.

Kikosi cha timu ya Taifa Stars
Equatorial Guinea








IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 16,2019

WATOTO WAPATAO ELFU SITA WAISHI NA KUFANYA KAZI MITAANI NCHINI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiongea na wadau pamoja na wataalam wa ustawi wa jamii mkoani Mwanza kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja kupambana na tatizo la watoto wa mitaani Jijini Mwanza.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katikati akifuatilia jambo pamoja na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ngondi kulia pamoja na Bw. Kizito Wambula kushoto ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wakifuatilia kwa Makini mada mojawapo kuhusu tatizo la watoto wa mitaani.


Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara aya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftali Ngondi akifafanua jambo kuhusu tatizo la watoto wa mitaani wakati wa kikao kazi kati ya Wizara na Wadau wa watoto Jijini Mwanza.


Wadau wa ustawi wa jamii, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Katibu Mkuu Wizara ya Afya na viongozi wengine Mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha kupambana na tatizo la watoto wa mitaani Jijini Mwanza.

…………………


Anthony Ishengoma- Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka wadau mkoani humo kwa kushirikiana na serikali kutokomeza kabisa tatizo la watoto takribani 1,254 wanaoishi na kufanya kazi mitaani jijini Mwanza kwa kutumia mifumo na rasilimali zilizopo kumaliza kabisa tatizo hilo.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema lengo la kutaka kupunguza tatizo hilo sio la kuwaonea bali pia ni kuwasaidia watoto hao kuondoka na madhara na madhira wayapatao watoto hao ili waweze kurudi katika familia zao na kuondokana na maisha ya mashaka yanayowakabili.

Aidha Bw. Mongella amesema hayo leo Jijini Mwanza wakati wa Kikao Kazi cha wadau wa Mkoa wa Mwanza na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kilichokaa leo kujadili mpango Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani Nchini.

Bw. Mongella ameonya tabia ya baadhi ya taasisi na watu binafsi wanaotoa misaada kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao na kutaka kuwepo utaratibu wa kuangalia namna bora ya utoaji misaada hiyo mabayo amedai inachangia uwepo wa tatizo sugu la watoto wa mitaani.

‘’Unakuta mtoto anakuja mtaani na kupewa msaada unaotosha kwa wiki moja kwa msingi huu mtu huyu anazoea na kujenga tabia ya kutochukia maisha ya namna hii hivyo misaada hii inajenga usugu kwa baadhi ya watu hawa kutoona sababu ya kuachana na tabia ya kurudi au kendelea kuishi mitaani hivyo razima suala misaada liangaliwe upya.’’Alisisitiza Bw. Mongella.

Aidha kiongozi huyo wa Mkoa wa Mwanza ameongeza kuwa mkoa wa mwanza unaweza kutokomeza vitendo hivi kwa kuwa unayo mifumo mizuri ya ufuatiliaji kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa na kuwataka wadau mkoani humo kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha watoto hawa wanarudi katika familia zao na kuwafuatilia kupitia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

Wakati huo huo katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 iko wazi kwani inawataka watoto kuishi na kulelewa katika familia hivyo suala hili linaweza kutokomezwa kwa mjibu wa sheria hiyo.

Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa watoto hawa lazima warudishwe katika familia zao na uchambuzi ufanyike ili kubaini wale wote ambao hawataweza kurudi katika familia zao basi wapelekwe katika makao ya serikali ya wattoto ili waweze kupatiwa huduma bora ikiwemo chakula na maradhi.

Dkt. Jingu amewataka watoto hao kutambua kuwa wao ni azina ya Taifa hivyo wanatakiwa kuishi katika malezi bora na kuonya kuwa baadhi ya walezi kwa sasa ni waharifu na hivyo kuwafundisha watoto hao uharifu na kujiona wao sio sehemu ya jamii wanamoishi.

Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii hapa Nchini Dkt. Naftali Ngondi wakati akimkaribisha katibu Mkuu katika kikao kazi hicho amsema lengo la kikao kazi hicho ni kuja na mpango mkakati utakaowezesha kufuatilia utekelezaji wa kutokomeza swala la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kuisha kabisa kwa kuanzia na mkoa wa mwanza.

Aidha Dkt. Ngondi ameongeza kuwa idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani nchini ni takribani elfu sita na kati ya hao asilimia tisini tayari wazazi na walezi wao wanatambulika hivyo kazi iliyopo ni kutafuta namna bora ya kuwaunganisha watoto hao na familia zao.

Wadau wa mashirika pamoja na wataalam wa ustawi wa jamii wanakutana jijini mwanza ili kukubaliana na kuja na mpango mkakati utakaowezesha utekelezji kwa vitendo namnan bora ya kuondokana na tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Mkuu wa Mkoa Morogoro kuwapiga Jeki Wahitimu Mikumi VETA katika ajira

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameahidi kuwa Balozi wakusaidia wahitimu wa Chuo cha VETA Mikumi kwa wale wataokafanya vizuri kwenye masomo yao baaada yakumaliza mitihani yao kwa mwaka huu

Kauli hiyo Ameitoa wakati wa mahafali ya 22 ya chuo cha ufundi stadi mikumi mkoani morogoro nakueleza kuwa mkoa wa morogoro unayo miradi mikubwa inayotekelezwa kama ule mradi wa kufua umeme wa bwawa la mwl nyerere ambao unahitaji watalaamu wanaozalishwa kutoka vyuo vya ndani na hivyo yeye akiwa kiongozi atahakikisha watakaofaulu vizuri wanapata ajira kwenye miradi hiyo

Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuwaendeleza vijana kwakutoa wataalumu ambao wanatoka kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo Veta na hivyo kila mwanafunzi anayesoma veta anatakiwa kufahamu kuwa ipo miradi inayowahitaji wao kuitumikia ikiwemo kujiajiri mwenyewe pamoja na kupenda kazi,kutafyta fursa,kuwa wajasiliamali, na kujiendeleza kitaaluma ili kumudu mabadiliko ya sayansi na teknolojia

Nae kaimu mkuu wa chuo Veta Mikumu Emmanuel Munuo ameziomba asasi zisizo za serikali na wadau kuifaga mfano wa shirika la plan international kwa kutafyta vijana walioko vijijini kutambua mahitaji yao na kasha kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na elimy ya ujasiliamali ili kuwatengenezea fursa za kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

Nao baadhi ya wazazi na walezi wamewataka vijana wanaohitimu masomo kuwa waadilifu nakuutumia ujuzi waliupata kwa manufaa kwa jamii na taifa pamoja nakusoma kwa bidiii ili kuitumia fursa yakauli ya mkuu wa mkoa yakutumia miradi iliyopo Morogoro kwakupata ajira

Jumla ya wahitimu 240,Wavulana 176 na Wasichana 64 wanahitimu kwa fani mbalimbali chuoni hapo.
 Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akipata maelezo kutoka mwanafunzi wa ngazi ya tatu katika ya uunganishaji Stanford Ngozo namna walivyotengeneza kabati wakati mkuu wa mkuu huyo alipotembelea karakana hiyo, mahafali ya 22 ya Chuo cha VETA Mikumi Mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare akizungumza katika mahafali ya 22 ya Chuo cha VETA Mikumi Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Adam Mgoi akizungumza kuhusiana na faida ya Chuo hicho kwa wakazi wa Kilosa kupata stadi za ufundi wakati wa Mahafali ya Chuo cha VETA  Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo akizungumza kuhusiana na historia ya chuo  hicho na mafanikio waliyoyapata katika kuandaa vijana wenye ujuzi .
 Sehemu ya wahitimu wa chuo cha VETA Mikumi wakifurahi wakati wakiingia katika viwanja vya Mahafali katika Chuo hicho

 icha ya pamoja na wahitimu waliopata tuzo mbalimbali

DKT.NDUMBARO AIPONGEZA NISHATI KUWA YA KWANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro( aliyesimama) akizungumza na washiriki wakati akifunga Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo(kushoto) akizungumza na Washiriki wa Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake(hawapo pichani) kabla ya kufungwa kwa kikao hicho.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro( katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake , baada ya kufunga kikao hicho kilichofanyika mkoani Tanga.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro( kushoto) akiwa amembatana na Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake ambao wanaofanya kikao kazi mkoani Tanga ,kilichofungwa na Katibu Mkuu huyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,( GASCO), Mhandisi Baltazar Mroso akitoa neno la Shukrani baada ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro, kufunga kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake

……………………

Na Zuena Msuya, Tanga

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurian Ndumbaro ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake kwa kuwa ya kwanza kutekeleza agizo la Rais kwa kufanya vikao vya pamoja vya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utumishi wa umma ,utendaji kazi na utawala bora kati ya watumishi, wafanyakazi pamoja na viongozi katika sehemu za kazi.

Dkt. Ndumbaro alisema hayo Novemba 15, 2019, wakati akifunga Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani Tanga.

Alisema kuwa kwa kufanya mikutano ya namna hiyo, ni dhahiri Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake imelenga kutekeleza agizo la Rais na dhima ya serikali inayoelekeza utumishi wa umma wenye uwajibikaji, uadilifu, unaofanya kazi kwa juhudi na maarifa,uzalendo, na ule ambao watumishi wake wanakuwa na sifa stahiki.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa Wizara ya Nishati inatekeleza agizo hilo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Wizara na Taasisi zilizochini yake kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, utumishi wa Umma na Utawala bora sehemu za kazi.

Alisema kuwa utumishi wa umma unaozingatia misingi yake hujenga utawala bora kwa taifa na wananchi wake, kwa kuimarisha mahusiano mazuri kati ya wananchi, watumishi wa umma, wafanyakazi pamoja na viongozi katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kupata matokeo chanya kwa taifa na wananchi wake.

Sambamba na hilo alisema kuwa wizara hiyo na taasisi zake inatekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi na taifa, hivyo kuwepo kwa utumishi wa umma wenye kuzingatia misingi imara sehemu za kazi ni chachu ya kuongeza ari ya watumishi katika kila sekta kufanya kazi kwa bidii na kujituma bila kuchoka na kuweka mbele uzalendo na maslahi taifa.

Aliwaelekeza wasimamizi wa rasilimaliwatu kutoa motisha kwa watumishi au wafanyakazi wanaofanya kazi vizuri kwa kuwapatia vyeti au barua maalumu ya utambuzi ambazo zitaweka katika eneo la mapokezi ili kuinua ari ya kufanya kazi kwa bidii kwa kila mtumishi au mfanyakazi, na pia kutoa adhabu ya namna hiyo kwa wale ambao hawafanyi vizuri kazini.

Aliwasisitiza watumishi wa umma kutofanya kazi kwa mazoea na kwamba watambue kuwa mtumishi wa umma unaweza kufanya kazi katika ofisi yoyote ya umma iliyopo nchini, na kwamba wasikariri kuwa watakaa sehemu moja siku zote.

“Watumishi wa umma muwe na tabia kama ya kuvaa na kuvua makoti tofauti, kwa maana leo utakuwa katika kutuo cha kazi A, kesho utapelekwa Y, au P na baadaye G, huu ni utaratibu uliowekwa kwa manufaa ya kujenga na kuboresha utumishi wa umma”,alisisitiza Dkt.Ndumbaro 

Aidha aliendelea kukumbusha kuwa watumishi pamoja na wafanyakazi wapewe nafasi za kwenda kusoma yale yenye tija kwa wizara ama taasisi husika, na mafunzo hayo yatolewe kwa watu wote wa kila idara na siyo kupendelea mtu mmoja.

Vilevile alirudia kuwaeleza watumishi wa umma kuendelea kutunza siri za serikali na kulinda mali ya umma bila kusahau kupiga vita vitendo vya rushwa.

Katika zoezi linaloendelea la kuhakiki watumishi wa umma, serikali imebaini kuwa kuna watumishi ambao majina yaliyopo katika vyeti walivyosomea na majina katika barua walizoajiriwa ni tofauti, hivyo wanaendelea kufanya utafiti kwa kushirikisha vyombo vya serikali ili kubaini kama vyeti hivyo ni vya watumishi hao kihalali au ni vya watu wengine ili waweze kutoa maamuzi sahihi wakati ukifika.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>