Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Wanaume zaidi ya milioni nne nchini wafanyiwa tohara

$
0
0

Na Catherine Sungura -Dodoma

JUMLA ya wanaume milioni 4,456,511 wamefanyiwa tohara kinga ya kitabibu tangu 2009 ilipoanza kutolewa hadi kufikia Septemba, 2019.

Hayo yamesemwa na Afisa Mpango kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Sasan Mmbando wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wabunge wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na kamati ya Katiba na Sheria kuhusu mpango huo.

Dk. Mmbando alisema kuwa lengo la kwanza la afua hiyo lilikuwa kuwafikia wanaume na vijana milioni 2.8 kufikia Septemba, 2017.“Hadi kufikia Septemba, 2017 tumeweza kuwafikia milioni 3,303,940 na kuwatahiri,” alisema.

Aidha, alisema katika lengo la pili kuanzia mwaka 2017 hadi 2022 wana mpango wa kuwafikia wanaume milioni 2.7.Alisema hadi kufikia Septemba, 2019, tayari wameweza kuwatahiri jumla ya wanaume 1,681,070 ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya lengo.

Alisema afua hiyo inatekelezwa katika mikoa 17 yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV na kiwango kidogo cha utahiri nchini.

“Hata hivyo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ili kuwa na huduma endelevu na kupunguza matatizo ya njia ya mkojo, mfano UTI, ilianza kutoa huduma ya tohara kwa watoto wachanga wenye umri kuanzia siku moja hadi 60, 2013, kama utafiti wa kujifunzia (pilot study), katika mkoa wa Iringa hadi sasa imefikia mikoa 15 nchini,” alibainisha.

Alisema hadi kufikia Septemba, 2019 jumla ya watoto wachanga 13,603 wametahiriwa.

“Tohara ya watoto wachanga inafanyika katika mikoa 15, Iringa Njombe, Morogoro, Singida, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Rukwa, Katavi, Songwe, Mbeya na Kigoma,” alisema.
  Wabunge wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na kamati ya  Katiba na Sheria walioshiriki semina ya kujengewa uelewa wa masuala ya mpango wa taifa wa kudhibiti UKIMWI
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akifafanua jambo wakati wa semina hiyo
Wabunge walioshiriki semina hiyo iliyohusu masuala ya UKIMWI 
Waheshimiwa wabunge wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati ya semina hiyo 


UHABA WA MAJI NA UCHAFU WA MAZINGIRA CHANZO CHA UGONJWA WA TRAKOMA SINGIDA

$
0
0

 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Ernest Mugetta, akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya ugonjwa wa Trakoma cha robo  tatu ya nne ya mwaka kilicho wakutanisha wadau wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na Manyoni mkoani Singida jana.
 Afisa Mradi wa Trakoma  kutoka Shirika la Helen Keller International, Athuma Tawakal, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao hicho kuhusu ugonjwa huo.
 Washiriki wa kikao hicho wakiwa kwenye majadiliano.
 Dkt. Peter Kabangila (kushoto) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, akijadiliana jambo na Mratibu wa Huduma za Macho Wilaya ya Ikungi, Shija Mhoja katika kikao hicho.
 Majadiliano yakiendelea. Kutoka kushoto ni Kaimu Mratibu wa Huduma za Macho Wilaya ya Manyoni, Renatus Ngeze, TT Surgeon Wilaya ya Manyoni, Bukumbi Makoye na Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele (DNTDCO) Wilaya ya Mkalama DC, Dkt. Julius Nyenje.
 Kikao kikiendelea.
 Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.


CHANGAMOTO ya uhaba wa maji na usafi wa mazingira vimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea  kushamiri kwa ugonjwa wa Trakoma  kwenye baadhi ya halmashauri za mkoa wa Singida, zikiwemo Manyoni na Itigi  imeelezwa.  

Trakoma ni ugonjwa unaoathiri macho ambapo kope huingia ndani na kugusa jicho hatimaye matokeo ya hali hiyo huweza kusababisha mtu kutoona vizuri au kuwa kipofu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao cha tathmini ya robo mwaka, kilichowakutanisha wadau mbalilmbali wanaojihusisha kukabiliana na ugonjwa wa Trakoma ndani ya halmashauri za wilaya ya Manyoni na Ikungi mkoani hapa jana, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mugetta, alisema pamoja na dalili za mafanikio zilizopo lakini bado kuna jitihada za ziada zinahitajika kwa kila mdau katika kutokomeza kabisa ugonjwa huo.  

”Tunaendelea kutoa elimu hususan kwenye kuzingatia usafi wa macho, maji na kunawa uso vizuri…hivi ni vitu ambavyo tunaendelea kuvisisitiza sana kwenye jamii ili kupunguza  trakoma,”  alisema Dkt. Mugetta na kubainisha kuwa sehemu kubwa ya jamii inayoathirika na ugonjwa  huu ni ile ambayo upatikanaji wake wa maji ni mdogo. 

Alisema serikali  kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Helen Keller International kwa mda mrefu sasa wameendelea kutoa huduma za afya ya macho kwa mafanikio ndani ya Halmashauri za Manyoni na Itigi na kuhamasisha umma juu ya kuchukua tahadhari, ikiwemo kuzingatia usafi wa macho wakati wote katika kukabiliana na ugonjwa huo hatari unaowakumba watu wote wenye umri wa miaka 15 na kuendelea.   

Kikao cha wadau hao, pamoja na mambo mengine kilipitia taarifa za halmashauri zilizofikiwa na mradi huo sanjari na kujadili mwelekeo wa kuingiza halmashauri nyingine zenye changamoto ya ugonjwa huo kwa utekelezaji wa mradi.   

Afisa Mradi wa Trakoma kutoka Shirika la Helen Keller International, Athuman Tawakal, alisema tatizo lipo kwa mda mrefu lakini limekuwa likipungua kadri siku zinavyokwenda.   

“Juhudi kubwa iliyopo kwa sasa ni kuhamasisha jamii kuondokana na visababishi vyote vinavyoweza kusababisha ugonjwa huu ikiwemo kuzingatia suala la usafi wa mazingira, upatikanaji wa maji ya kutosha ndani ya jamii, ujenzi wa vyoo bora na kutoa matibabu kwa wale wote ambao wameathirika dhidi ya Trakoma

MIFUMO IMEKUWA CHANGAMOTO KWA MWANAMKE KUSHIRIKI TAFITI ZA KISAYANSI,TEKNOLOJIA,UBUNIFU

$
0
0
 Afisa Mtafiti Mwandamizi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Hildegalda Mushi kushoto, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya utafiti Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Profesa Mohamed Sheikhe na watatu ni Mkurugenzi Mkuu Mtandao wa sayansi na teknolojia kwa nchi za Afrika, Dkt. Nicholas Ozor.

Mkurugenzi Mkuu Mtandao wa sayansi na teknolojia kwa nchi za Afrika, Dkt. Nicholas Ozor kulia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa wanawake katika Tafiti za Kisayansi na ubunifu katika mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya utafiti Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Profesa Mohamed Sheikhe.
 Taasisi ya Sayansi ya Taifa-US, Makyaba Charles-Ayinde akizungumza na waandishi wa habari katika Makutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtandao wa sayansi na teknolojia kwa nchi za Afrika, Dkt. Nicholas Ozor.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya utafiti Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Profesa Mohamed Sheikhe akizungumza na waandishi wa habri jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na wanasayansi kutoka nchi15 za kusini mwa jangwa la Sahara na kutoka nchi mbalimbali. kushoto ni

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MIFUMO ya utoaji fedha za kitafiti na mifumo ya elimu imekuwa changamoto kwa wanawake kushiriki katika tafiti za kisayasi, teknolojia na ubunifu kwasababu ya kutokuwepo na vigezo vinavyompa kipaumbele mwanamke.

Afisa Mtafiti Mwandamizi Hildegalda Mushi, ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea kufanyika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kuanzia ngazi za chini za elimu wanamke anapojifunza  anakuwa na changamoto katika kujifunza masomo ya Sayansi.

"Ushiriki wa wanawake bado umekuwa kwa kiwango kidogo kutokana na changamoto za kimifumo ambazo ni katika mifumo ya utoaji wa fedha za kitafiti na kuna masuala ya mifumo ya utoaji elimu". Amesema Hildegalda.

Kwa upande wa fedha za kitafiti amesema kutokana na mila na destuli za kiafrika kuwa kuwepo na vigezo ambavyo vitamuwezesha mwanamke kupata mkopo na sio kuangajia jinsia ndio apate fedha hizo.

"Katika Utoaji wa Fedha  kuwepo na vigezo vitakavyoangalia je! hizi fedha za utafiti zinavyotoka zinawezaje zikafaidisha wanawake na wanaume kwa pamoja kwa sababu wakati mwingine mazoea ya mila na destuli za kiafrika,hata nchi za magharibi wamepita huko lakini wameweza kupita na kugundua yale mapungufu mbalimbali ambayo yamechukuliwa kuwa ni maisha ya kawaida basi wakaweza kugundua kuwa inasababisha mwanamke kuenguliwa katika kupata fedha za kitafiti, kwa kigezo hiki inahusika na jinsia na wala sio utaalamu".

Kwa upande wa Sera za nchi Hildegalda amesema kuwa miongozo ya kisera katika mabaraza yanayotoa fedha za kitafiti kuwe na vigezo na kuhakikisha kuwa mwanamke anapata nafasi ya kipekee ili waweze kufaidika na fedha za kitafiti.

Hata hivyo amesema kuwa  changamoto hizo zinaendelea hata katika taasisi za elimu ya juu na hata katika kusomea taaluma ya kitafiti changamoto zinaendelea kutokana na unyanyasaji wa kijinsia.

Katika mashauriano kwenye mkutano huo wameafikiana kuwa mwanamke anayefanya tafiti katika nchi 15 za kusini mwa jangwa la Sahara akikumbwa na unyanyasaji wa kijinsia ni lazima kutoa taarifa ndani ya siku 10 ili hatua cha kitafiti na kisheria ziweze kuchukuliwa.

"Kwa nchi ya Marekani wenzetu wamefanikiwa kwa mwanamke ambaye atafanyiwa ukatili wa kijinsia wakati akifanya utafiti wa kisayansi, kiteknolojia na ubunifu kutoa taarifa kwenye vyombo husika ndani ya siku 10 ili sheria ziweze kuchukuliwa kwa haraka sana na zimeanza kuzaa matunda".

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH), Profesa Mohamed Sheikhe amesema kuwa ili kuwa na watafiti waliobobea taasisi ya watafiti lazima iimarishwe iwekewe mipangilio bora na ziweze kuendelezwa.

BENKI YA POSTA YATOA MEZA NA VITI KWA SHULE MBILI ZA MBINGA

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania(TPB),Sabasaba Moshingi wa tatu kushoto akikabidhi moja kati ya meza 100 na viti 100 vyenye thamani ya shilingi Ml 4.8 kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye kwa ajili ya shule mbili za Sekondari za Mbambi na Makita zilizopo Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma,kushoto Afisa mahusiano wa Benki hiyo Novas Moses,

BENKI ya Posta Tanzania(TPB) imetoa msaada wa meza 100 na viti 100 vyenye thamani ya shilingi Ml 4.8  kwa shule mbili za Sekondari za Mbambi na Makita zilizopo katika Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma.

Akikabidhi samani hizo za Shule,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi alisema, Benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutenga kiasi fulani cha fedha  kila mwaka na kusaidia jamii hasa katika sekta ya Elimu katika mikoa mbalimbali hapa Nchini.

Alisema,  mwaka wa fedha 2019 Benki ya Posta imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya kuchangia huduma za jamii na itaendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazo fanywa wananchi na Serikali.

Moshingi alisema, Benki ya Posta Tanzania inajivunia sana kuona imekuwa sehemu ya mafanikio katika sekta  ya Elimu hapa Nchini  na sio mara ya kwanza kuchangia sekta ya elimu kwani mwaka jana ilitumia kiasi cha shilingi milioni 50 kukarabati shule ya Msingi Kindimba iliyopo katika wilaya hiyo.

Amewataka wanafunzi wa shule hizo, kuhakikisha  wanatumia meza na viti hivyo kusoma kwa bidi na kujiepusha na mambo yanayoweza kukatisha safari yao ya maisha na kuwataka Watanzania wengine kuunga mkono juhudi zinazo fanywa na Benki ya Posta na Serikali ya awamu ya tano ya kumarisha miundombinu ya Shule.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Cosmas Nshenye,amewataka wakazi wa  Mbinga  kuwa wazalendo, na wenye mapenzi mema kwa  kumaliza baadhi ya changamoto zinazoikabili wilaya hiyo badala ya kutegemea misaada ya Serikali na wafadhili.

 Nshenye ametoa kauli hiyo jana wakati akiongea na wanafunzi,walimu na baadhi ya wananchi katika hafla ya kupokea msaada wa viti 100 na meza 100 zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania kwa shule mbili za  Sekondari za Mbambi na Makita wilayani humo.

Alisema, sio  jambo la kufurahisha na haipendezi hata kidogo kwa jamii  ya wana Mbinga kuona wanashindwa  kuchangia ujenzi wa miradi na huduma mbalimbali za kijamii, kwani wana uwezo mkubwa wa kifedha,lakini inasikitisha kuona  kazi kubwa ya kuijenga wilaya hiyo imeachwa kwa Serikali na wadau wengine wa maendeleo.

Nshenye alisema, wakati umefika kwa wakazi wa wilaya ya Mbinga kubadilika na kujitolea nguvu kwa kuchangia  ujenzi wa miradi  ikiwemo miundombinu ya Elimu,Afya,Maji na mingineyo hatua itakayochochea na kuharakisha maendeleo ya Nchi yetu.

Kwa mujibu wake,ni aibu wilaya kama ya Mbinga ambayo wananchi wake wana nguvu kubwa ya kiuchumi inayotokana na zao maarufu la kahawa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati,viti na meza huku baadhi ya wanafunzi wa shule wakilazimika kubeba viti kutoka nyumbani kwao.

Aidha Mkuu wa wilaya ameishukuru Benki ya Posta kwa msaada wa viti na meza ambazo zinakwenda kupunguza  mahitaji ya samani  kwa shule hizo mbili, ambapo ameyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Benki hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kuchangia miundombinu ya shule kwa wilaya ya Mbinga.

Amewataka wanafunzi  kutumia meza na viti hivyo  kusoma kwa bidii, hali itakayowasaidia kufikia malengo waliyojiwekea katika safari yao ya maisha nan a viti na meza hizo wazitumie kama chachu ya mafanikio.

Awali Mkuu wa shule ya Makita Wilson Msengi alisema, shule hiyo ina upungufu wa viti 62 na meza 58,lakini msaada huo  uliotolewa na Benki ya Posta utapunguza sana changamoto hiyo.

Alisema,samani hizo zinakwenda kuhamasisha suala zima la kujifunzia na kufundishia darasani na pia kuchochea taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo.

USAJILI KILI MARATHON WAANZA KWA KASI

$
0
0
Washiriki wa mbio za kilometa 42 za Kilimanjaro Premium Lager marathon wakiwa tayari kuanza mashindano hayokatika mbio zilizopita. Usajili wa mashindano hayo umeanza kwa kasi kwa njia ya mtandao na Tigopesa.

Usajili wa mbio za 18 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, Tigo km 21 na Grand Malt Km 5 umeanza kwa kasi huku ukiwa juu kwa asilimia 30 ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana. Hili ni ongezeko la asilimia 10 ndani ya wiki moja. 

Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa mbio hizo ieeleza kuwa mwendendo ni mzuri na wamewataka washiriki kuchangamkia punguzo la bei litakalodumu hadi mwezi Januari mwakani. Washiriki wanajisajili kwa kupitia www.kilimanjaromarathon.com na kwa Tigopesa kwa kubonyeza *149*20#.

Mkurugenzi wa Mbio hizo nchini, John Bayo alisema kwa kupitia taarifa hiyo kuwa kuna idadi maalumu ya washiriki inayotakiwa kwa mbio zote tatu (Kilimanjaro Premium Lager Km 42, Tigo km 21 na Grand Malt Km 5) ili kuhakikisha kuw ambio hizo zinaendana na viwango vya Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) ili kuhakikisha usalama unazingatiwa.

Kwa mujibu wa Bw. Bayo, hii pia itahakikisha washiriki wanafurahia mbio hizo bila ya msongamano na pia kutoa nafasi kwa waandaaji waweze kutoa huduma zinazotakiwa katika njia ya mashindano na sehemu ya kumalizia pia.

Kuhusu punguzo la bei, waandaaji hao pia walitoa wito kwa washiriki wachangamkie utaratibu huo ambao ulianza Oktoba Mosi 2019 hadi Januari 14 , 2020. Kwa raia wa Tanzania na wale kutoka nchi za Afrika Mashariki watalipa Tsh 15,000 kwa mbio za Km 42 na 21 na Tsh 5000 kwa km 5 lakini kuanzia Januari 15, 2020 hadi Februari 16, 2020 washiriki watakaojisajili watalipa Tsh 20,000 kwa km 42 na 21 na Tsh 5000 kwa km 5. 

Kwa wageni wakazi au wenye vibali vya kuishi na kufanya kazi na wale wa nchi za SADC watalipa USD 35 kwa km 42 na 21 na USD 5 kwa km 5 kuanzia Octoba 1, 2019 hadi Januari 14, 2020 lakini kuanzia Januari 15, 2020 hadi Februari 16, 2020 wanaojisajili watalipa USD 45 kwa km 42 na 21 na USD 5 kwa km 5. 

Washiriki wa kimataifa watalipa USD 70 kwa km 42 na 21 na USD 5 kwa km 5 kuanzia Oktoba 1, 2019 hadi Januari 14, 2020 na kuanzia Januari 15 hadi Februari 16, 2020 watalipa USD 85 kwa km 42 na Km 21 na USD 5 kwa km 5. 

Kwa mujibu wa waandaaji hao, usajili utafungwa rasmi saa sita usiku Februari 16, 2020 au pale ambapo idadi inayotakiwa itatimia.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Chama Cha Riadha Tanzania, Baraza la Michezo Tanzania, Bodi ya Utalii Tannzania na wadau wengine wa riadha.

Washiriki pia walikumbushwa kuhusu vituo vya kuchukulia namba zao za ushiriki ambapo kwa Dar es Sallaam ni Mlimani City kuanzia February 22-23, 2020, Arusha ni Hoteli ya Kibo Palace kuanzia Februari 25-26 na Moshi ni Hoteli ya Keys kuanzia Februari 27-28. “Washiriki watatakiwa kujitambulisha na kuthibitisha kuwa wameshalipia kabla ya kukabidhiwa namba zao,” ilisema taarifa ya waandaaji. 

Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2020 ni Kilimanjaro Premium lager, Tigo, Grand Malt Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement, Barclays Bank na watoa huduma rasmi ni Kibo Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.

Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayoandaliwa na Wild Frontiers na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions, yanatarajiwa kufanyika Machi 1, 2020 katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Washiriki wa mbio za Tigo kilometa 21 wakianza mbio hizo.

SIKU YA TAKWIMU AFRIKA 2019 KUADHIMISHWA KWA SHINDANO MAALUMU LA INSHA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAADHIMISHO ya siku ya Takwimu Afrika yanayofanyika kila tarehe 18 Novemba kila mwaka yataadhimishwa tena mwaka huu yakiwa na malengo ya kuelimisha umma kote barani Afrika kuhusiana na umuhimu wa takwimu na kuongeza ufahamu juu ya nafasi na mchango wa tasnia ya takwimu na kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasnia ya takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Takwimu nchini (NBS) imeeleza kuwa Tanzania itaadhimisha siku ya takwmu ikiwa mwanachama wa Umoja wa Afrika na kila mwaka huungana na wanachama wengine wa umoja huo kuadhidhimisha siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinaakisi maudhui ya maadhimisho hayo na miongoni mwa matukio yatakayoambatana na maadhimisho hayo ni pamoja na mashindano ya kuandika Isha kwa wanafunzi wa shule za sekondari kote nchini.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo la kuweka shindano hilo ni kuongeza ufahamu kwa vijana kuhusu masuala ya kitakwimu ikiwemo umuhimu na matumizi ya takwimu katika maendeleo pamoja na kuwahamasisha vijana kupenda tasnia ya takwimu amayo ni moja ya tasnia ambayo itawasaidia nakuwawezesha kutimiza ndoto zao za maisha.

Wanafunzi wa shule za Sekondari wameshauriwa kuandika insha kuhusiana na  Mada ya 'UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA KUPANGA NA
KUIMARISHA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA' na urefu wa Insha usizidi maneno mia tano huku tarehe ya mwisho ya kuwasilisha insha hizo ikiwa ni Novemba 21 mwaka huu saa kumi kamili jioni na washindi watatangazwa na kupatiwa zawadi zao siku ya kilele cha siku ya maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika tarehe 28 Novemba, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Mtaa waShaaban Robert jijini Dar es Salaam.
 Insha zote ziwasilishwe   kwa anuani zifuatazo:
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Barabara ya Jakaya Kikwete,
S.L.P 2683,
DODOMA
AU
Ofisi za Takwimu za Mkoa ulipo
AU
Emails: sg@nbs.go.tz na nakala kwa joel.weja@nbs.go.tz, said.ameir@nbs.go.tz.

RITA KULITUMIA SHIRIKA LA POSTA KUSAFIRISHA NYARAKA NA VITENDEA KAZI, WAINGIA MAKUBALIANO RASMI KUFANIKISHA UTEKELEZAJI HUO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

WAKALA wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Shirika la Posta nchini wamesaini hati ya makubaliano kwa ajili ya wakala huo kutumia shirika hilo kusafirisha vitendea kazi na nyaraka muhimu zilipo katika ofisi mbalimbali nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa Watanzania kwa wakati.

Akizungumza wakati wa utiwaji saini wa hati hiyo ya makubaliano yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu au Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson amesema kuwa wamekutana kusaini makubaliano hayo kwa ajili ya kufanya pamoja na Shirika la Posta katika kusafirisha vitendea kazi vyao na nyaraka.

"RITA ni kifupi cha Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini ambayo inajumuisha majukumu makuu matatu ambayo tunayatekeleza , kwa wale ambao mmefika RITA kwa shughuli mbalimbali tunaamini mmeona huduma zetu.Tunasajili vizazi, vifo, ndoa, talaka, tunasimamia mirathi, tunasajili bodi za wadhamini, tunasimamia mali ambazo hazina wenyewe na tunatunza wosia na kuandika.Hivyo leo tuko hapa kwa ajili ya kusaini hati ya makubaliano kwa ajili ya kufanya kazi pamoja na Shirika la Posta katika kusafirisha vitendea kazi vyetu,"amesema Hudson.

Amefafanua kwamba kama inavyofahamika kuwa RITA ni mratibu wa shughuli za usajili wa matukio muhimu ya binadamu kama alivyozoeleka hapo awali , wanahusika na kusajili  vizazi vifo, ndoa , talaka, na watoto wa kuasili na katika kutekeleza majumu yao yote muhimu yanayowahusu wanasadiana na wadau mbalimbali kuyafanikisha kwa upande wa Tanzania Bara.

"Ili kuwezesha majukumu hayo kufanyika RITA inalojukumu la kutengeneza nyaraka na vitenda kazi ili viweze kutumika katika maeneo ambayo tunafanya  nayo kazi  na hasa katika ofisi mbalimbali ambazo shughuli zao zinafanyika.Pamoja na kutengeneza na kununua hivyo vifaa lazima vifike mahali kupitia njia ya usafiri.Tumekuwa tukitumia njia mbalimbali kusafirisha vifaa hivyo katika ofisi zetu na tumekuwa tukitumia usafiri wetu.

"Hata hivyo kumekuwepo na changamoto ya kufikisha vifaa na nyaraka muhimu kwa wakati, hivyo tumeona fursa iliyopo kwa Shirika la Posta ambao wamesambaa nchi nchi nzima, tumeona tuingie nao makubaliano kwa ajili ya kusafirisha vitendea kazi na nyaraka zetu.Kwa hiyo kimsingi kama nchi ilivyokuwa kubwa nasi tumekuwa tukisafirisha tani 10 kwa mwaka.Nyaraka ambazo tunasafirisha nusu yake zinatakiwa kurudi tena Ofisi ya RITA Makao Makuu kwa ajili ya kuzitunza,"amesema na kuongeza jukumu la kutunza nyaraka hizo ni lao ili ziweze kutumika katika matumizi ya Serikali na mtu binafsi.

Amesema kuwa wanatambua kuwa wanayo mifumo imara ya Tehama ya kutunza kumbukumbu lakini bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na nyaraka halisi. Ametoa mfano kuwa Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama wakati anataka kugombea aliwekewa vikwazo kuhusu mahali alipozaliwa."Tunafahamu Marekani teknolojia yao iko juu lakini Obama alilazimika kupeleka cheti halisi kuthibitisha kuwa amezaliwa katika nchi hiyo.Hivyo tunaona umuhimu wa nyaraka halisi na hivyo kwetu lazima tuhakikishe inasafiri katika mikono salama,"amesema.

Ameongeza hivyo mashirikiano hayo ambayo wameingia na Shirika la Posta wanaamini kwamba nyaraka hizo zitawafikia kwa wakati na  kubwa zaidi iliyopewa jukumu hilo i taasisi ya umma na hivyo wanaamini kutakuwa na usalama, uadilifu na nidhamu kubwa.

"Tulikutana  siku moja tukazungumza na hatimaye tukakubaliana na leo tupo hapa kwa ajili ya kuweka makubaliano ili haya ambayo tumezungumzwa yawe kwenye utekelezaji kwa vitendo.Ni matarajio yetu  huu utakwenda vizuri na tumeanza kwa makubaliano ya mwaka mmoja na huko mbele tutaangalia kama tuendelee au tusiendelee maana tunafahamu makubaliano si Msahafu au Biblia,"amesema.

Kwa upande wake Posta Master Mkuu Hassan Mwang'ombe amesema jambo ambalo linafanyika leo halijawaji kufanyika huko nyuma na kwamba ni muhimu sana kwani linahusu ushirikiano kati ya Shirika la Posta na RITA katika kusafirisha nyaraka na vitendea kazi.

Amesema kuwa makubaliano hayo yanakwenda kurahisisha utoaji huduma kati ya eneo moja ya jingine na kwamba makubaliano hayo ni sehemu ya magizo ambayo wamepewa , kwamba wananchi wa Tanzania wanapaswa kupata huduma bora na kwa haraka.

"Tunaamini mambo yatakuwa mazuri yatarahisisha utoaji huduma na kwa haraka.Sisi Posta kwa sasa tupo katika kipindi cha mabadiliko makubwa na haya tunayafanya katika eneo zima la usafirishaji.Nitoe  mfano mmoja zamani tulikuwa tunatumia mawakala kusafirisha bidhaa lakini sasa tumenunua magari yetu wenyewe, tunakwenda katika mikoa mbalimbali nchini.Tuko kila mahali ili kuhakikisha tunasafirisha bidhaa za Watanzania,'amesema.

Amesema ndani ya saa 36 wanakuwa wamefika na kufanya huduma na kuongezawanatumia muda mchache, hivyo RITA hawajakosea kuwatumia Posta katika kufanikisha huduma hiyo inatekelezwa kwa wakati."Kwa makubaliano haya tunasema RITA wamelamba dume na hatuko tayari kuona watu wanaharibu uhusiano  huu."amesema.

Amesema kuwa Watanzania wanaweza kufanya mambo makubwa na kueleza kuwa ile dhana ya mambo mazuri yanafanywa na Wazungu tu inapaswa kuondewa kwani sio kweli.Hata Watanzania wanaweza kufanya mambo makubwa kuliko hata yanayofanywa na Mzungu.

ASASI YA KIRAIA YATOA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA KATIKA MAGEREZA YA ARUSHA, TANGA NA KILIMANJARO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP -  Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bw. Charles Shang’a alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya  wafungwa  leo Novemba 15, 2019.
Meza kuu wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike (wa pili toka kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania ikiashiria ufunguzi wa hafla fupi ya kupokea misaada ya Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa iliyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ. Tukio hilo limefanyika leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania Bw. Joseph Kumwembe akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya Wafungwa nchini. Dorcas Aid International Tanzania hushirikiana na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ katika kutoa misaada ya namna hiyo.
Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP - Phaustine Kasike akitoa hotuba kwa wageni mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria hafla fupi ya kupokea msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa  kutoka kwa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ  leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike akipokea msaada wa baiskeri ya walevu pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa  na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Novemba 15, 2019 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi.
Muonekano wa baadhi ya misaada ya Kibinadamu iliyotolewa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ iliyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi. Misaada imekabidhiwa leo kwa ujumla wake ina thamani ya zaidi ya milioni 183.
Mhandisi ujenzi wa Jeshi la Magereza, SP. Julius Sukambi akitoa maelezo ya kitaalam kwa Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP - Phaustine Kasike alipotembelea katika eneo hilo la ujenzi wa Kiwanda Kipya cha bidhaa za ngozi kinachojengwa nje ya eneo la Gereza Kuu Karanga, Moshi(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Na ASP Lucas Mboje, Moshi

ASASI ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi kwa Jeshi la Magereza misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 183 ambayo itawanufaisha wafungwa na Mahabusu waliopo magerezani katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Akizungumza kabla ya kukabidhi misaada hiyo ya wahalifu waliopo magerezani, Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania, Bw. Joseph Kumwembe amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni magodoro, sabuni, nguo za watoto, mabranketi, vipeperushi, vifaa vya usafi na vitabu vya kiroho. 

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameishukru Asasi hiyo isiyo ya Kiserikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa ikiwemo mafunzo ya Kijasiriamali kwa wafungwa hivyo kulisaidia Jeshi la Magereza katika suala zima la urekebishaji wa wafungwa.

“Niwashukru sana Asasi hii kwa moyo wao wa upendo na kujitolea na niwapongeze sana kwa kutambua kwamba wahalifu waliopo magerezani ni Binadamu kama walivyo Binadamu wengine na wanahitaji misaada ya ki-binadamu kama hii,” Amesema Jenerali Kasike. Aidha, Jenerali Kasike ametoa wito kwa Asasi nyingine zisizo za Kiserikali kuiga mfano uliooneshwa na New Life in Christ na Dorcas Aid International Tanzania ili ziweze kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa manufaa ya Taifa.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewataka Wakuu wote wa Magereza yaliyonufaika na misaada hiyo kuhakisha kuwa misaada inawanufaisha walengwa kwa maeneo yaliyokusudiwa samabamba na kusimamia vyema vifaa hivyo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mara baada ya kupokea misaada hiyo ametembelea eneo la mradi mkubwa wa uwekezaji wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi ambacho ni cha ubia kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF. Kiwanda hicho kinajengwa katika eneo lililopo nje ya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo amewasisitiza wakandarasi wa ujenzi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

AT ATOA MASIKITIKO YAKE KWA WAANDAAJI WA MATAMASHA

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.

MSANII wa Muziki wa kizazi kipya miongoko ya mduara kutoka Zanzibar, Ally Ramadhani a.k.a  AT ametoa masikitiko yake kwa waandaaji wa matamasha na majukwaa kutoshirikishwa kwa wasanii wa kizanzibar.

AT amezungumza hayo leo na Ripota wetu katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JNCC, jijini Dar es salaam na nakueleza kuwa Sanaa yeyote ile ili ipanuke na kukua zaidi ni muhimu wasanii na wadau kushirikiana kwa pamoja na kutengeneza umoja ambao utaleta faida katika jamii na kupelekea sanaa kuimarika na kutangazika kimataifa.

"Tunatengwa sana hasa sisi wazanzibar kwani matamasha mengi hatushirikishwi wanajichagua wenyewe kwa wenyewe,"

Aidha, amewatoa hofu wasanii wachanga  kutokata tamaa katika vipaji vyao na kuvipigania .

"Nilikua na kipato duni sana ila nilijitahidi kununua nguo za mitumba ili ni shoot video zangu kwani niliamini mdogo mdogo ndio mwendo na hatimae nimefika hapa hivyo kwa wasanii wachanga watumie vitu ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi"

Aidha, AT ameeleza kuwa wasanii wasichoke kuwaomba wasanii waliotoboa kimuziki kuwasaidia kimawazo ili kuboresha kazi zao .

"Mimi nilikua msanii wa kwanza mchanga kumpandisha Alikiba kwenye daladala kutoka alipokua anaishi kariakoo hadi masaki kwa mtayarishaji wa Muziki Allen Mapigo nilijishusha na kumyenyekea kutokana na uhitaji wa Jambo likamilike,"

Hata hivyo amesema anajisikia faraja kuona bado ana nguvu na maono ya kuona ana nafasi ya kuwasaidia wasanii chipukizi wakike na kuwakuza kimuziki na kimaadili.

"Kwa Sasa wasanii wakike baadhi wamekua wakijiacha utupu ili tu wajulikane kwa haraka zaidi kutokana na kukosa nafasi wao wenyewe kupenya Kama wasanii wengine wakubwa walivopata nafasi,"

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI NA MILLENIUM WOMEN'S GROUP WAKABIDHI MISAADA MBALIMBALI KITUO CHA KULEA WAZEE CHA NUNGE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ameungana na wake wa viongozi mbalimbali katika kusherehekea miaka 10 ya umoja wao uitwao New Millenium Women’s Group kwa kutoa misaada katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.

Mama magufuli, ambaye aliambatana na Mlezi wa umoja huo Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Magufuli, Mwenyekiti wake Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda na Mama Asina Kawawa aliungana na wajumbe hao kutoa misaada mbali mbali ya ujenzi, chakula na nguo.

Mama Magufuli alichangia jumla ya gypsum 178 huku Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akituma mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Bwalo la kituo hicho kikongwe ambacho hadi leo Novemba 15, 2019 kilikuwa na wazee 26.

Umoja huo wa New Millenium Women’s Group ulichangia ujenzi wa mnara wa kisima cha maji kwa gharama ya shilingi milioni 1.9, vyakula na nguo vyenye thamani ya shilingi milioni 3.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group akiwasili katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Mama Tunu Pinda, Mama Mary Majaliwa, Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mama Asina Kawawa.
Wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group wakiwa katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo walikofika kutoa misaada mbalimbali katika kuadhimisha umoja huo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada ya nguo na vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akitoa misaada ya nguo na vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s na wakaaazi wa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAENDELEA NA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA ILI KUPISHA UJENZI WA NGUZO ZA UMEME WA SGR

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania laendelea na zoezi la ulipaji fidia ili kupisha ujenzi wa Miundombinu ya kusafirisha umeme katika mradi wa reli ya kisasa - SGR kipande cha Dar es Salaam - Morogoro, hivi karibuni Novemba, 2019.

Zoezi linaendeshwa na Maafisa kutoka Shirika la Reli Tanzania, Shiirika la Usambazaji Umeme nchini - TANESCO, Chuo Kikuu cha Ardhi na viongozi wa serikali za mitaa na vijiji husika katika kijiji cha Mtego wa Simba, Kinonko, Kidugalo, Mikese, Sinyaulimbe, Ngerengere, Mgude, Mhungamkola na mtaa wa Pangawe.

Malipo ya fidia yanahusisha wananchi wote ambao maeneo yao yamepitiwa na ujenzi wa miunbominu ya usafirishaji wa umeme kutoka katika chanzo cha uzalishaji kwenda katika vituo vya kuhifadhi na kupoza umeme ambavyo vitapeleka umeme katika treni za kisasa.

Aidha wananchi wa mitaa na vijiji hivyo wameonesha ushirikiano katika zoezi hili ambapo zaidi ya wananchi 200 watapatiwa hundi zao kwa ajili ya fidia za ardhi na makazi mkoani Morogoro. Mkazi wa kijiji cha Mtego wa Simba Bwana Rashid Said ambaye eneo lake limetwaliwa amesema kuwa manufaa ya mradi wa SGR ni makubwa kuliko fidia ambazo zimekuwa ziilipwa hivyo anaunga mkono jitihada za serikali.  

Shirika linaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za Mradi wa Ujenzi w Reli ya kisasa, kwani mradi huu ni wa kimkakati na wenye maslahi kwa taifa katika sekta za uchumi, utawala na jamii, pia linawashukuru wananchi wote wanaoshiriki kwa namna yoyote katika kuhakikisha mradi huu unaotumia fedha za watanzania haukwami.
 


RC Tanga, awaasa Watumishi wa Nishati

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati,Raphael Nombo,(kulia)akibadilishana jambo na viongozi wengine mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela(katikati) kufungua kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani humo.kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela ( watatu kushoto waliokaa) akiwa
katika Picha ya pamoja ya washiriki wa Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani humo.
Sehemu ya Sekretarieti ya kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani tanga, kutoka wizara ya nishati, kutoka kushoto ni Zaituni Nkya( katikati), Lilian Lumbila na Talkisia Eriyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (katikati)akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani humo.
 Mkuregenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Dkt.Tito Mwinuka( katikati) akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani Tanga.

************************************

Na Zuena Msuya, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela amewataka watumishi wa Umma
kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi, Uadilifu, utiifu, weledi,
taratibu na sheria za kazi katika kutumiza majukumu yao kila siku.

Shigela alisema hayo, Novemba 14, 2019 kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais, Utumishi, Dkt. Laurian Ndumbaro, wakati akifungua Kikao kazi cha
Wakurugenzi,Mameneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa
Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kilichofanyika mkoani Tanga.

Akizungumza katika kikao hicho, Shigela aliwaeleza washiriki wa mkutano
huo kuwa pia wanatakiwa kufanya kazi kwa kutumia Lugha safi na sahihi
kulingana na huduma wanayoitoa kwa mtumishi au mteja katika eneo
husika.

Alisema endapo Wakurugenzi na Mameneja wa Rasilimaliwatu watafanya
kazi zao kwa misingi inayotakiwa, hakika kazi zote na miradi mbalimbali
inayotekelezwa na serikali itafanyika kwa umakini mkubwa na kukamilika
kwa wakati.

Vilevile itasaidia wao pamoja na watumishi na wafanyakazi waliochini yao
kujilinda na kuwaepusha na vishawishi dhidi ya rushwa katika sehemu zao
za kazi.

Alifafanua kuwa Wakurugenzi na Mameneja ndiyo wenye dhamana kubwa
ya kusimamia watendaji na watumishi walio chini yao sehemu za kazi,
hivyo wanapaswa kutimiza majukumu kwa weledi ili kuwawezesha
watumishi wanaowaongoza kutekeleza majukumu kwa ufanisi na bila
malalamiko.

Aidha, Shigela aliipongeza Wizara ya Nishati, kwa kuwa wizara ya kwanza
kutekeleza agizo la Katibu Mkuu, ofisi ya Rais, Utumishi lililoelekeza wizara
zote nchini kuweka utaratibu wa kufanya vikao kazi na taasisi zilizochini
yake ili kubaini changamoto na kuboresha mambo mbalimbali katika
Utendaji kazi na usimamizi wa Rasilimaliwatu.

“Watumishi wa umma wanahitaji kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao,
kwa kuwa wao ni kiungo muhimu cha kufinikisha na kuwafikia wananchi
moja kwa moja yale mengi mazuri yanayotekelezwa na serikali kwa
wananchi wake, pia ni watu wanaotumia muda kazini kuliko katika familia zao, hivyo wasiposimamiwa vizuri na kupata miongozo sahihi , yale mazuri
yanayofanywa na serikali hayata wafikia wananchi kama inavyotakiwa”,alisisitiza Shigela.

Akizungumzia suala la kuwaongezea uwezo watendaji na watumishi,
Shigela alizishauri Wizara na Taasisi mbalimbali kuweka utaratibu wa
kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara watumishi wao ili kuendana na
teknolojia inayokuwa kila siku na kuwapa motisha kazini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Dkt.Tito Mwinuka, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati, Dkt.Khamis Mwinyimvua, alisema kuwa utaratibu wa
kufanya vikao na kuzungumza na Tasisi zilizochini ya Wizara imesaidia
sana kuongeza ushirikiano kati ya mtumishi na muajiri.

Pia vimesaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili
wafanyakazi na watumishi ikiwemo kuondoa ama kupunguza malalamiko
kati ya wafanyakazi na waajiri katika maeneo ya kazi.

Vilevile, imeboresha na kuinua ari ya utendaji kazi kwa watumishi na
wafanyakazi wa maeneo husika kwa kuwa haki zao za msingi zinatatuliwa
wakati sahihi.

Sambamba na hilo, Dkt.Mwinuka alisema kuwa imesaidia wafanyakazi na
watumishi wengi kuzungumza na kuweka wazi changamoto zinazowakabili
kwa kuwa zinasikilizwa, na kupatiwa majawabu pamoja na kuelezwa
hatua zinazochukuliwa dhidi ya changamoto hizo kabla ya kutatuliwa.

“Utaratibu huu ni mzuri sana umeleta matokeo chanya, Taasisi na Wizara
tunajua uhitaji na changamoto zinazowakabili wafanyakazi na watumishi
wa sekta zetu kila inapotea, na tunafahamu ni namna gani
tunazishughulikia kwa pamoja na kwa haraka zaidi tofauti na ilivokuwa
huko nyuma, naupongeza sana huu utaratibu” alisema Dkt. Mwinuka.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo, alimshukuru Mkuu
wa Mkoa huyo na kumuhakikishia kuwa wao kama wasimamizi wa
watumishi na wafanyakazi katika Wizara, Taasisi na Idara mbalimbali za
Serikali watafanya kazi zao kwa uadilifu, weledi,ubunifu na kujituma kwa
kuzingatia misingi na taratibu za kazi.

Alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa, Wizara ya Nishati ni moja ya nguzo
kubwa na muhimili muhimu Sana katika kuchangia maendeleo ya uchumi
kwa kuwezesha kupatikana kwa Nishati ya Umeme nchi nzima, hivyo
wanajukumu kubwa la kuwasimamia vyema watendaji, watumishi na
wafanyakazi ili na wao wafanye kazi zao kwa weledi ,kujituma, ubunifu kwa
maslahi makubwa ya Taifa.

“Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kujenga uchumi wa viwanda kila
kona ya nchi yetu, Wizara ya Nishati, sisi ndiyo tunadhamana kubwa
sababu tunazalisha umeme unaotumika katika viwanda hivyo,
tunawahakikishia watanzania kuwa tunatekeleza majukumu yetu usiku na
mchana bila kuchoka kuhakikisha umeme mwingi na wakutosha
unapatikana wakati wote katika maeneo ya uzalishaji hasa viwandani
kutimiza lengo lililokusudiwa,” alisisitiza Nombo.

Nombo alisema kuwa hicho ni kikao cha tatu kufanyika ambapo kikao cha
kwanza kilifanyika Mikoani Dar ES salaam, cha pili mkoani Mwanza,
ambavyo vinafanyika kila robo mwaka, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea
katika wizara hiyo na Tasisi zake ili kuzungumza na kujadili mambo kadha
yanayojikeza kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kutatua changamoto
endapo zimejitokeza.

MISA YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA KURUDI DARASANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Africa (MISA) tawi la Tanzania Salome Kitomari akienelea kutoa elimu juu ya waandishi wa kujua umuhimu wa kuendelea kusoma kwa kuwa elimu haina mwisho
Waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa makini kusikiliza mjadala ambao ulikuwa unaendelea kuhusu umuhimu wa elimu ya uandishi wa habari
Waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa makini kusikiliza mjadala ambao ulikuwa unaendelea kuhusu umuhimu wa elimu ya uandishi wa habari 
Waandishi wa habari na wadau wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa MISA Tanzania



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wanahabari mkoa wa Iringa wametakiwa kuongeza kiwango cha elimu ili kuweza kufanya kazi kwa kujiamini na kwa weledi wa hali ya juu katika kazi zao.

Akizungumza kwenye majadiliano ya kubaini changamoto za waandishi wa habari mkoani Iringa mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Africa (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews,Salome Kitomari alisema kuwa waandishi wa habari mkoani Iringa wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi kutokana na elimu uliyonayo.

“Waandishi wakiwa na elimu ya uandishi wa habari wanapaswa kuishi maisha yaliyo mazuri kwa manufaa ya jamii kwa kuwa waandishi wa habari ni kioo cha jamii,mwandishi unapaswa kujiuliza kwenye jamii unaonekanaje kutokana na kazi yako” alisema Kitomari

Kitomari alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuwa nadhifu muda wote kutokana na taaluma inavyotaka ili kuweza kutambulika kisheria kama taaluma nyingine ambazo zinatambuliwa vizuri kwa muonekano wao kwa wanataaluma wao.

“Waandishi wa habari mnatakiwa kuvaa mavazi nadhifu kama ilivyo wanasheria ambavyo wamekuwa wanaonekana wawapo kazini ndio maana wanaaminika zaidi ya waandishi wa habari hivyo inatupaswa kubadilika kimuonekano” alisema Kitomari 

Aidha Kitomari alisema ikifika 2021 kama huna elimu ya stashada ya elimu ya uandishi wa habari hautakuwa na fursa ya kuendelea kufanya kazi ya uandishi wa habari kwa mujibu wa sheria za nchi hii.

“Kama ujaanza kusoma stashada ya elimu ya uandishi wa habari basi ikifika 2021 utakuwa hujamaliza hivyo hutakuwa na sifa za kuwa mwandishi wa habari hasa usisubili changamoto hiyo ikukute jiongeze kitaaluma.” Alisema Kitomari

Lakini katika majadiliano ya kubaini changamoto kwa waandishi wa habari mkoani Iringa kuliibuka changamoto kama tatizo la uchumi kwa mwandishi mmoja mmoja ambapo ilionekana waandishi wengi hawaandiki habari kiweledi kutokana na na tatizo la kiuchumi.

Raymond Minja mwandishi wa gazeti la Mtanzania alisema kuwa waandishi wengi wa sasa wamekuwa wakiandika habari za kusifu na kuabudu kutokana na tatizo la uchumi kwa kuandika kile kitu anachokita mtoa habari.

“Tunaandika sana habari za kusifu na kuabudu kutokana na waandishi wengi kuwategemea watoa habari ambao mara nyingi wanakuwa viongozi wa kada mbalimbali na kupelekea kutoka katika misingi ya taaluma ya uandishi wa habari” alisema Minja

Waandishi wa habari wanachuki wao kwa wao,hawapendani na wanaubinafsi kutokana na tatizo la changamoto ya uchumi duni hiyo kupelekea waandishi wengi kuanza kutoka kwenye weledi wa taaluma hiyo, alisema Denis Mlowe mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima

WATUMISHI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA NIDHAMU YA HALI YA JUU

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt Emmanuel S. Shindika katikati mwenye suti ya kijivu wakati akifunguarasmi kikao cha Baraza la Wafanyakazi linaloendelea katika ukumbi wa VETA Dodoma  

 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wwaUmma wakifuatilia  Mkutano

 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wakimsiliza 
Mwenyekiti wa Baraza

 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia mada kuhusuSera ya Mafunzo ambayo imetolewa kwenye Mkutano huo

 Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya kupiga kura kumchagua Katibu na KatChuo cha Utumishi wa Umma Tanzania

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt Emmanuel S. Shindika mwenye suti ya kijivu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.

************
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Emmanuel Selemani Shindika amewataka watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu.

Dkt Shindika ameyasema hayo Jjini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa VETA Dodoma.

Alisema Chuo cha Utumishi wa Umma kimebeba majukumu ya kuhakikisha kuwa mafunzo yenye ubora yanatolewa kwa watumishi wa umma. Katika kutoa mafunzo hayo ni lazima kuonesha ushirikiano, umoja, mshikamano, ufanisi na uadilifu mkubwa kwa kuzingatia sheria, kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali ya Chuo.

Alisema uzoefu unaonesha kwamba vikao vya Baraza la Wafanyakazi vimekuwa na faida mkubwa mahala pa kazi. Kwa kupitia Baraza la wafanyakazi Chuo kimefanikiwa kuongeza ufanisi na mshikamano mkubwa kati ya Watumishi na Menejimenti pamoja na wadau wetu” alisema Dkt Shindika.

Hata hivyo Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili kwa muda mrefu ikiwemo ya uhaba wa majengo kwa ajili ya madarasa, na akasema kwamba juhudi mbalmbali ili kutatua changamoto hiyo.

MANISPAA YA SINGIDA YAKUSANYA ZAIDI YA SH.MILIONI 200 KWA MWEZI

$
0
0
 Mkurugenzi wa  Manispaa ya Singida,  Bravo Lyapembile, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi jana mkoani hapa. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Alhaji Chima Mbua na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili.
Mtahiki Meya  wa Manispaa ya Singida, Alhaji Chima Mbua, akiongoza kikao hicho. Kulia ni  Mkurugenzi wa  Manispaa ya Singida,  Bravo Lyapembile.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili, akizungumza kwenye kikao hicho.
 Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
 Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
 Kikao kikiendelea.
 Kikao kikiendelea.
 Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdamu, akiuliza swali kwenye kikao hicho. Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu, Margaret Malecela na Diwani Hadija Simba.
 Madiwani wakifuatilia kikao hicho kwa umakini.
 Watendaji na wakuu wa idara wakiwa kwenye kikao hicho.
 Vijana wa Kikundi cha Familia Moja, wakionesha mikate wanayoitengeza baada ya kuwezeshwa na Manispaa hiyo. Kutoka kulia ni Katibu wa Kikundi hicho, William Mollel, Mweka Hazina, Bonaventure Njiku, Katibu Msaidizi, John Chacha, Mjumbe wa Kikundi, Cleophace Okulo na Mwenyekiti, Benard Mahenge.
 Diwani wa Kata ya Unyami, Said  Athuman , akizungumza  kwenye kikao hicho.
 Diwani wa Kata ya Kisaki, Moses Ikaku , akizungumza  kwenye kikao hicho.
 Naibu Meya, Shabani Mkata, akizungumza  kwenye kikao hicho. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lucia Mwiru, akizungumza  kwenye kikao hicho. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Shabani Karage.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida kwa mwezi wa Oktoba 2019  imefanikiwa kukusanya sh.milioni 248,858, 234.12 za mapato.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilicho keti mjini hapa jana baada ya kupata nafasi ya kuzungumza.
" Napenda kuwapongeza kwa ukusanyaji huu wa mapato tuna kwenda vizuri na tupo ndani ya wastani wa kila mwezi wa ukusanyaji wa mapato yetu" alisema Muragili.
Alisema kwa siku 14 zilizopita hadi kufikia jana saa nne asubuhi halmashauri hiyo imeweza kukusanya sh.milioni 72.594,308.06.jambo ambalo linaashiria kuwepo kwa kazi nzuri ya kukusanya mapato.
Muragili alisema mpaka Oktoba 31 mwaka huu halmashauri hiyo ilikuwa na zaidi ya sh milioni 190 zilizokuwa nje kama madeni lakini kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa deni hilo limepunguzwa hadi kufikia sh.64.6 milioni ambapo aliomba ziongezeke juhudi waweze kulipunguza  hadi lifikie sh.milioni 10.
Katika hatua nyingine Murigili amewata madiwani wa halmashauri hiyo katika kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha kwenda kwa wananchi kuwahimiza kilimo si kwa mazao ya chakula pekee bali walime na mazao ya kimkakati pamba, korosho na zao linalochukua alama ya mkoa wa Singida la alizeti.
Murigili alitumia nafasi hiyo kuwaomba madiwani hao kwenda kuwaeleza wananchi wao kutouza chakula walichokihifadhi baada ya bei katika soko kwa hivi sasa kupanda kwani kuna viashiria vya uhaba wa chakula kati ya Januari na Februali.
Katika suala la utunzaji wa mazingira aliwataka madiwani hao mbali na shughuli za kilimo waende kuhimiza upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali na kwenye maeneo ya taasisi kama za shule na ofisi za serikali.
Akizungumzia maandalizi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2020 alisema mwaka jana waliingia katika mchakato wa kutengeneza madawati hivyo aliiomba halmashauri hiyo kujipanga katika jambo hilo ili msimu wa masomo utakapoanza vijana hao wakae kwenye madawati.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bravo Lyapembile akizungumza kwenye kikao hicho wakati akiwakaribisha vijana wajasiriamali wa kikundi cha Familia Moja waliowezeshwa na manispaa hiyo kwa kukopeshwa sh.milioni 10 kwa ajili ya mradi wa kutengeneza mikate na maandazi alisema halmashauri imetenga zaidi ya sh.milioni 100 kwa ajili ya kusaidia vikundi mbalimbali na alitumia nafasi hiyo kuwaomba waliokopa kurejesha fedha kwa wakati ili ziweze kukopeshwa kwa vikundi vingine.

MANISPAA YA LINDI KUTENGA BILIONI 4 KWA AJILI YA KUJENGA SOKO LA KISASA

$
0
0
Afisa mradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Equality for Growth (EfG) , Susan Sitta akimkabidhi mfuko wenye machapisho mbalimbali , Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge. 
Afisa Utawala wa shirika hilo la EfG, Eva Buhemba, akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge. 
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG ambao wapo katika ziara ya kuwahamasisha wanawake wafanyabiashara masokoni wa mkoa huo kujiunga katika umoja wa kitaifa.


Na Mwandishi Wetu, Lindi.

HALMASHAURI Manispaa ya Lindi mkoani hapa inatarajia kutumia sh. Bil.4 kwajili ya kujenga soko la kisasa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Lindi, Joumary Satura ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG), kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Lindi, alisema kuwa ukamilikaji wa soko hilo litaweza kuwanyanyua kina mama wajasiriamali ambapo kwa sasa bado wanatumia soko la zamani ambalo ndilo linatakiwa kubomolewa.

Aidha alisema kwamba licha ya ujenzi wa soko hilo jipya ambalo litakuwa la ghorofa moja ramani na michoro kadhaa ilishakamilika.Satura alisema fedha hizo zitatokana na vyanzo vya ndani na serikali kuu na taasisi za kifedha benki taratibu mbalimbali zinafanyika.

Aliongeza kwa kusema kuwa hivi sasa miundo mbinu ya soko hilo la zamani sio mizuri kutokana na idadi ya watu wanaongezeka.Alisema kwamba kwa hiyo ukamilikaji wa soko hilo itawezesha makundi mbalimbali kutumia fursa hiyo hasa wale akina mama wajasiriamali wanaochuuza samaki mbogamboga watanufaika.

Hata hivyo aliwaambia viongozi hao kuwa makundi yanayokopeshwa fedha hasa hivi vikundi vya uzalishaji mali huwa wagumu kurudisha deni.Mpaka sasa ni zaidi ya shs mil.200 zilishakopeshwa kwa vikundi vya uzalishaji mali lakini mpaka mwaka huu havijarudisha deni hilo tangu miaka 2014 hadi 2019.

Naye Afisa Utawala wa shirika hilo la EfG, Eva Buhemba alisema madhumuni wa shirika hilo kuwakutanisha kina mama wajasiriamali kuwa na sauti moja katika masoko.Ambapo wanaonekana wanakuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji, kumiliki vizimba wanakuwa watu wanaohangaika hata biashara yenyewe anayoifanya jkwa siku anapata shs 7,000 tu.


Buhemba alisema hata kuwa na sifa ya kukopesheka huwa hawana kwani hata kizimba chenyewe alishakodi inabidi alipe, miliki huwa wanaume.
Alisema hata hivyo uongozi wa soko huwa kina baba sio wanawake ni wachache mno kwahiyo shirika huwa linawezesha kuwapa elimu kina mama.

Aliongeza kwa kusema kwamba mpaka sasa shirika linafanya kazi katika mikoa tisa nayo ni Mtwara, Lindi, Mbeya, Iringa, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam katika halmashauri ya manispaa ya Ilala na Temeke.

ASASI YA KIRAIA YATOA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA KATIKA MAGEREZA YA ARUSHA, TANGA NA KILIMANJARO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akipokea msaada wa baiskeri ya walevu pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Novemba 15, 2019 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi.

Muonekano wa baadhi ya misaada ya Kibinadamu iliyotolewa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ iliyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi. Misaada imekabidhiwa leo kwa ujumla wake ina thamani ya zaidi ya milioni 183.
Mhandisi ujenzi wa Jeshi la Magereza, SP. Julius Sukambi akitoa maelezo ya kitaalam kwa Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike alipotembelea katika eneo hilo la ujenzi wa Kiwanda Kipya cha bidhaa za ngozi kinachojengwa nje ya eneo la Gereza Kuu Karanga, Moshi
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bw. Charles Shang’a alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya wafungwa leo Novemba 15, 2019.
Meza kuu wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike (wa pili toka kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania ikiashiria ufunguzi wa hafla fupi ya kupokea misaada ya Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa iliyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ. Tukio hilo limefanyika leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania Bw. Joseph Kumwembe akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya Wafungwa nchini. Dorcas Aid International Tanzania hushirikiana na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ katika kutoa misaada ya namna hiyo.
Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike akitoa hotuba kwa wageni mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria hafla fupi ya kupokea msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa kutoka kwa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
(Picha zote na Jeshi la Magereza).

…………………..

Na ASP Lucas Mboje, Moshi

ASASI ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi kwa Jeshi la Magereza misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 183 ambayo itawanufaisha wafungwa na Mahabusu waliopo magerezani katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga. 

Akizungumza kabla ya kukabidhi misaada hiyo ya wahalifu waliopo magerezani, Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania, Bw. Joseph Kumwembe amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni magodoro, sabuni, nguo za watoto, mabranketi, vipeperushi, vifaa vya usafi na vitabu vya kiroho. 

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameishukru Asasi hiyo isiyo ya Kiserikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa ikiwemo mafunzo ya Kijasiriamali kwa wafungwa hivyo kulisaidia Jeshi la Magereza katika suala zima la urekebishaji wa wafungwa.

“Niwashukru sana Asasi hii kwa moyo wao wa upendo na kujitolea na niwapongeze sana kwa kutambua kwamba wahalifu waliopo magerezani ni Binadamu kama walivyo Binadamu wengine na wanahitaji misaada ya ki-binadamu kama hii,” Amesema Jenerali Kasike.

Aidha, Jenerali Kasike ametoa wito kwa Asasi nyingine zisizo za Kiserikali kuiga mfano uliooneshwa na New Life in Christ na Dorcas Aid International Tanzania ili ziweze kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa manufaa ya Taifa.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewataka Wakuu wote wa Magereza yaliyonufaika na misaada hiyo kuhakisha kuwa misaada inawanufaisha walengwa kwa maeneo yaliyokusudiwa samabamba na kusimamia vyema vifaa hivyo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mara baada ya kupokea misaada hiyo ametembelea eneo la mradi mkubwa wa uwekezaji wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi ambacho ni cha ubia kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF. Kiwanda hicho kinajengwa katika eneo lililopo nje ya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo amewasisitiza wakandarasi wa ujenzi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

JAMII YAASWA KUWATUNZA WAZEE

$
0
0

Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza katika Kituo cha kulelea wazee cha Nunge, kilichopo katika kata ya Vijibweni, wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, kabla ya kutoa msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa wazee waliyopo kituoni hapo, Novemba 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

………………..

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema jamii inatakiwa kuwajali na kuwatunza wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwani hilo ni jukumu la watu wote na si kuiachia Serikali pekee.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 15, 2019) wakati wa kikundi cha wake wa viongozi nchini cha New Millenium Group kilipotembelea makazi ya wazee ya Nunge katika kata ya Vijibweni Wilaya ya Kigamboni jijini, Dar es Salaam na kutoa misaada wa vitu mbalimbali.

Waziri Ndalichako amesema kuwa ‘’jukumu la kutunza wazee ni letu sote, nawashukuru wake wa viongozi kwa umoja wenu, nawaomba muendelee na moyo huu wa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu.”

Amesema Serikali imefanya ukarabati wa nyumba 10 kati ya 50 zilizopo katika makazi hayo ya wazee na itaendelea kuzikarabati nyumba zote zilizobaki na kujenga uzio ili makazi hayo yasiingiliwe na watu wanaozunguka eneo hilo.

Naye,Mwenyekiti wa New Millenium Group, Mke wa Waziri Mkuu Msaafu, Mama Tunu Pinda amesema akinamama hao wamekesha usiku na mchana kuhakikisha wazee hao wanapata mahitaji na wametoa walichobarikiwa na Mwenyezi Mungu.

‘’Kikundi chetu katika kutimiza miaka 10 tangu kianzishwe tumeamua kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa tulichobarikiwa. Ikumbukwe kuwa nasi ni wazee watarajiwa ni asilimia nne tu ya wazee wanapata mafao wengine hawana msaada wowote. Wazee kuanzia miaka 60 hunyemelewa na magonjwa mbalimbali hivyo jamii isiwasahau.”

Kwa upande wake, Mlezi wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewashukuru akinamama wenzake wanaounda umoja huo na kuiomba jamii iwaunge mkono.

“Akina Mama wa Millennium mmekuwa mfano bora kwa wenzetu nawaomba tudumishe umoja wetu na tunamshukuru Mama yetu Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa kuungana nasi katika kuwapa tabasamu wazee wetu wa Nunge.”

Awali, Afisa Mfawidhi wa kituo hicho Jacklina Kanyamweri amewashukuru akinamama kikundi cha New Mellinium Group kwa kuwakumbuka wazee na watu wenye uhitaji ambapo amewaomba wasichoke kwani wazee wana mahitaji mengi ikiwemo ujenzi wa uzio katika makazi hayo na ukarabati wa barabara.

Akina Mama wanaounda umoja huo wametoa misaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni, nguo, gypsum, baiskeli za watoto, mafuta. Wametembelea kituo hicho wakiwa katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Kadhalika, akinamama hao wameahidi kukarabati bwalo la wazee hao na kujenga mnara wa tenki la kuhifadhia maji pamoja na kutengeneza mfumo wa maji unaopeleka katika nyumba za wazee hao kadri Mwenyezi Mungu atakavyowajaalia.

Kwa upande wao, wazee wanaotunzwa katika makazi hayo wameiomba Serikali kutowatupa na wamewashukuru akinamama wa New Millennium Group kwa moyo wao wa pekee kwa walivyojitoa.

WATUMISHI 44,800 WA KADA YA AFYA KUAJIRIWA NCHINI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Silafu Jumbe Maufi Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.

………………….

Happiness Shayo-Dodoma

Serikali imepanga kuajiri Watumishi 44,800 wa Kada ya Afya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi wa kada hiyo na kuboresha huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mhe. Silafu Jumbe Maufi (Viti Maalum) aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele cha ajira kwa kada ya afya na imekuwa ikitoa vibali vya ajira kwa kuzingatia ukomo wa bajeti kuu ya mshahara na vipaumbele vya mwajiri husika.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameweka bayana kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali ilitoa vibali vya ajira 8,000/= kwa kada ya afya, lakini lengo halikufikiwa kwa sababu ya kuwepo kwa wataalamu wachache wa kada hiyo waliojitokeza kuajiriwa Serikalini.

Ili kukabiliana na upungufu wa Watumishi wa kada ya afya, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamasisha wananchi katika majimbo yao kusoma masomo yatakayowawezesha kuajiriwa katika kada ya afya kwa lengo la kuwahudumia Watanzania.

Wizara ya Katiba Yaunga Mkono Kampeni ya Kuikijanisha Dodoma

$
0
0



Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Amon Mpanju wakimwagilia maji mti walioupanda wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Amon Mpanju wakipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome (kushoto) akisaidiwa na mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo Bw. Novatus Igosha wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw.Deogratias Yinza (kushoto) akishiriki katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakaziwakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.


Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katikazoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani. (Picha na Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)



Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw.Deogratias Yinza akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa wizara hiyo kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani. 
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images