Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

DC SIHA:KESHENI KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE.

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu akikagua ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule ya ya sekondari Songu ambapo alishangazwa  na ujenzi wa shule hiyo kusimama
Mafundi wanaojenga shule hiyo Onesmo  Lyimo na Martin Kingu  wamesema kuwa iwapo wataletewa vifaa vyote muhimu wako tayari kufanya .


Na Vero Ignatus,Killimanjaro.

Agizo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu  kuwataka  mafundi kufanya kazi mchana na usiku pamoja  kuhamishia makazi yao kwa muda katika shule ya sekondari Songu inayojengwa ili waweze kukamilisha ujenzi wa shule hiyo hadi ifikapo Novemba 27  mwaka huu .

Buswelu ameyasema hayo  wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa shule ya sekondari Songu na kushangazwa na ujenzi wa shule hiyo kusimama kwa muda licha ya halmashauri kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambapo ameiagiza Kamati ya ujenzi kununua vifaa vya ujenzi kwa muda ili kukamilisha ujenzi huo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa shule hiyo inapaswa kukamilika haraka ili Mdhibiti ubora aweze kwenda kuikagua na kuipitisha tayari kwa kuanza kupokea wanafunzi januari 2020.

Ameainisha  amesema kuwa serikali imedhamiria kusogeza huduma ya shule karibu ili wanafunzi waweze kunufaika na elimu bure inayotolewa na serikali ya awamu ya tano.

Isaya Mkilindi ni  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi   amesema kuwa kwa sasa wako kwenye hatua ya ununuzi wa mbao na saruji hivyo watakahakikisha kazi hiyo inakamilika kwa muda na kwa wakati.

Kwa upande wao mafundi wanaojenga shule hiyo Onesmo  Lyimo na Martin Yohana Kingu  wamesema kuwa iwapo wataletewa vifaa vyote muhimu wako tayari kufanya kazi hadi muda wa ziada ili kukamilisha ujenzi huo.


WATAFITI WATAKA USAWA WA KIJINSIA KWENYE UTAFITI

0
0

WASAYANSI watafiti wanaoshiriki mkutano wa mwaka wa Baraza la Sayansi Kanda ya Afrika wamezitaka nchi zao, kuhakikisha zinakuwa na Sheria na Sera ambazo zitawezesha wanawake watalaam kushiriki katika utafiti ili kuwepo usawa wa kijinsia.

Hayo yamsemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Profesa Muhammed Sheikh wakati akitoa taarifa ya mkutano huo ambao umeshamalizika.

Prof. Sheikh alisema takwimu zinaonesha uwiano kati ya wanaume na wanawake kwenye kufanya utafiti haulingani hivyo Serikali za Afrika zinapaswa kuweka mfumo ambao utarahisha usawa kisheria na kisera.

"Tumejadiliana na asilimia kubwa hoja ya ushiriki wa wanawake katika utafiti imechukua nafasi kubwa kwani takwimu zinaonesha karibu nchi zote ushiriki upo chini hivyo njia rahisi ni kuwepo mifumo ya kisheria na kisera ambayo itapendelea kundi la wanawake.

 Ili kufikia huko ni muhimu taasisi za utafiti zinakuwa na ushirikiano kikazi kwa kuwawezesha wanawake wanasayansi kufanya utafiti kama walivyo wanaume," alisema.Sheikh alisema wasayansi hao wanaamini iwapo kundi hilo litapewa msukumo dhana ya usawa wa kijinsi itaonekana na kuondoa malalamiko.

Aidha, alisema wanataaluma hao wamejadili namna ya kuwawezesha watafiti wanaoibukia fedha za kufanyia utafiti ili iwe rahisi kuwaingiza kwenye mfumo kitafiti ulio bora.

Alisema Tanzania kupitia COSTECH na nchi ya Sweden imekuwa ikiwezesha watafiti wanaochipukia kuanzia mwaka 2015 programu ambayo imeonesha matokeo chanya.

"Karibu Euro 900,000 zimeweza kutumika kuwezesha watafiti wapya hivyo ni jukumu la wenzetu kuchukua mfumo huu na kuupeleka kwao,” alisema.
Aidham alisema kupitia mkutano wamekutana na Baraza la Utafiti la Norway na kubadilishana uzoefu katika shughuli za utafiti.

Mtafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Sayansi nchini Marekani, Makyba Charles alisema nchini kwao wamekuwa wakizingatia jinsia kwenye utafiti kwa kuwepo vipengele vya sheria na sera.Charles alisema nchini Marekani sheria na sera zinaelekeza taasisi za utafiti kuzingatia usawa wa kijinsi hivyo ameshauri nchi za Afrika kuzingatia hilo.

Alisema nchini Marekani iwapo kutatokea unyanyasaji wa kijinsia sheria zinaelekeza tukio hilo liripotiwe ndani ya siku 10 ili hatua zichukuliwe.

Mtafiti Mwandamizi wa COSTECH, Hildegalda Mushi alisema washiriki wamependekeza changamoto zote ambazo zinarudisha nyuma watafiti wanawake zipatiwe ufumbuzi."Muda mwingi ulitumika kujadili namna ya kuwezesha kundi letu la wanawake kuhakikisha linaambukizwa chachu ya kufanya utafiti kama walivyo wanaume," alisema.

Alisema washiriki walisema ili kundi hilo liweze kuwa shindani linahitaji kujengewa uwezo kuanzia elimu ya msingi hadi vyuoni ambapo takwimu zinaonesha ushiriki wao umeshuka.Mushi alisema pia wamekubaliana kila nchi shiriki kukusanya takwimu za ushiriki wanawake kwenye utafiti ili kuwa na taarifa sahihi.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia, Sera na Ubunifu Afrika (ATPS), Nicholas Ozor alisema pamoja na uwezeshwaji wanawake na watafiti wanaochipukia juhudi kubwa zinapaswa kuelekezwa kwenye utafiti ulio wazi.

Ozor alisema ulimwengu wa leo unahitaji  ushirikiano katika kila jambo hivyo iwapo mfumo wa utafiti wa kisayansi uliowazi ukipata nafasi kutakuwa na matokeo chanya."Sisi ATPS tunaamini katika utafiti uliowazi kama njia ya kuendeleza jinsia na watafiti wanaochipukia tunachopigania ni uwepo wa miundombinu rafiki katika kitekeleza adhma hiyo," alisema.

WIZARA YA KILIMO YAKUTANA NA WADAU WA TUMBAKU KUJADILI CHANGAMOTO ZAO

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza katika mkutano wa wadau wa kilimo cha Tumbaku jijini Dodoma
baadhi wa wadau wa zao la tumbaku wakuiwa katika picha ya pamoja ndani ya ukumbi wa msekwa

Wizara ya Kilimo imekutana na wadau na wakulima wa kilimo cha Tumbaku hapa nchini ili kujadili changamoto zilizopo katika sekta hiyo nakuzitatua ili kuinua sekta ya kilimo cha Tumbaku hapa nchi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma na kuwakutanisha Wizara ya kilimo, fedha na wadau wa kilimo cha Tumbaku, wakulima na makampuni yanayonunua zao la Tumbaku na wenye viwanda vya Tumbaku, naibu Waziri wa Kilimo Husain Bashe amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha Wanakutana kwa pamoja na kujadili changamoto na vikwazo vyote vinavyopelekea kutoendelea kwa kilimo cha Tumbaku hapa nchini.

"Tumekutana hapa lengo likiwa ni kuangalia ni namna gani tunaweza kutoka hapa tulipo na kwenda mbele, ndio maana tumeshirikisha wadau wote sisi Wizara ya kilimo, fedha, wadau wa kilimo,wenye viwanda na wakulima ili kila mtu ajue nani ni kikwazo na kuanguka kwa sekta hii"

Ameongeza kuwa" zao la Tumbaku uzalishaji wake umekuwa ukishuka siku baada ya siku ukiangalia uzalishaji umeshuka kwa asilimia kubwa toka uzalishaji wa tani laki mojana ishirini (120,000) Hadi kufikia tani arobaini (40) kwa Sasa" Amesema Mhe. Bashe.

Amesema katika kikao hicho wameunda kamati ndogo ambayo itapitia sekta nzima ya kilimo cha Tumbaku na kukutana na wadau wote wa kilimo cha tumbaku na kuja na mapendekezo ya pamoja nini kitanyike na Kodi zipi zipunguzwe kwa Afya ya kilimo cha Tumbaku hapa nchini.

Amesema wameamua kuja na vikao hivyo vya kila kila zao peke yake ili kuona kila zao na tatizo lake kwa matatizo mengi yanatofautiana kwa kila zao na hivyo wameona ni vyema kukaa na wadau wa kila zao kuona namna ya kutatua changamoto za kila zao.

Amesema moja ya changamoto zilizoibuka ni baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutaka kujitoa, na wamejadili na makampuni hayo likiwamo kampuni ya TLTC kutokana na kutorudi kwa VAT return lakini baada ya mazungumzo wamekubali kuendelea na ununuzi wa zao hilo.

Lengo kubwa la serikali ni kuona kilimo cha Tumbaku kinaanza kurudi katika uzalishaji wake wa kawaida na kuleta tija kwa serikali na wakulima kunufaika na kazi wanazozifanya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, ambaye ni mdau wa kilimo cha Tumbaku amesema ni muhimu kwa taasisi za Serikali kujenga mazingira mazuri kwa wakulima na wafanya biashara wa zao la Tumbaku ili kuondoa migongano ambayo imekuwa ikitokea Mara kwa Mara.

Amesema kwa pamoja kama wakulima ni lazima lazima wasimamie ushirika katika zao hilo ili iwe rahisi katika hata katika kupanga bei, pia amesisitiza wale wanaopanga ubora wa tumbaku kuwa waaminifu na wazalendo kwa kupanga kwa usahihi.

Naye mmoja wa wakulima ambaye pia ni mwanachama wa chama Cha msingi Tabora, Uyui, Said Shabani, mbali na kumpongeza Naibu Waziri wa Kilimo kwa kuwakutanisha, amesema kwa kikao hicho ameanza kuona mwanga katika sekta ya kilimo na Sasa anaamini uzalishaji utaanza kupanda sasa.

APPS ZA KITAMBULISHO CHA TAIFA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI NI BATILI - NIDA

NHIF KUHAMISHA OFISI ZAKE ZA MKOA WA KINONDONI NA TEMEKA

CGP PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MANYARA

0
0

 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Lipina Lyimo(katikati) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Magereza, Masoud Kimolo(kulia) muda mfupi alipowasili leo Novemba 16, 2019 Mkoani humo. CGP Kasike yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua magereza yote ya Mkoa huo na kuzungumza na Maafisa na askari wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Magereza Mkoani Manyara mara baada ya kuwasili Gereza Babati kwa ziara yake ya kikazi leo Novemba 16, 2019.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(meza kuu) akiongoza kikao kazi na Maafisa wa Magereza Mkoani Manyara kabla ya kufanya Baraza la Wafungwa na mahabusu wa Gereza Babati.
 Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro(kulia) akimuonesha  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(kushoto) shamba la maharage ambalo limelimwa kwa kutumia Kilimo cha umwagiliaji Gereza Arusha.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro(kulia)alipokagua Shamba la mahindi kabla ya kuendelea na ziara  ya kikazi Mkoani Manyara leo Novemba 16, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).

CBE YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI BORA WA MAPATO NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHUO cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam kimepongezwa kwa usimamizi bora wa mapato pamoja na uanzishaji wa kampasi mpya na uboreshaji wa miundombinu ya elimu.

Akihutubia katika mahafali ya 54 ya Chuo hicho Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi. Stellah Manyanya amesema kuwa Chuo hicho kimeendelea kupiga hatua mwaka hadi mwaka na hiyo ni pamoja na kuanzisha na kuboresha Kampasi mbalimbali na kubwa ni kwa kuwapokea wanafunzi wa ngazi za astashahada kwa kushirikiana na TAMISEMI.

Aidha Mhandisi Manyanya amekipongeza Chuo hicho kusimamia vyema mapato ya Chuo hicho.

"Nimefurahi kuwa Chuo changu hakiendekezi ufisadi na kwa mwaka huu mmepata hati safi kutoka ofisi ya CAG na mmeshika nafasi ya pili katika taasisi zinazosimamia manunuzi, hili ni jambo jema sana na ninawaomba muendelee ivyo ivyo" amesema.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inatambua mchango na mafanikio ya Chuo hicho na kuhusiana na Changamoto za miundombinu Serikali ipo tayari na tatizo hilo litatatuliwa.

Pia amekipongeza Chuo hicho kwa kutoa elimu ya biashara na ujasiriamali jambo ambalo litawasaidia wahitimu hao na amewashauri wahitimu hao kuvuka mipaka na kutumia vyema mitandao kwa kupenya katika masoko ya nje.

Pia Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema amesema kuwa maarifa yanayotolewa na Chuo hicho yameendelea kuleta na tija kwa watanzania na hadi kufikia sasa kuna wanafunzi wapatao 80000 katika Kampasi zote nchini.

Amesema kuwa katika mahafali hayo ya 54 asilimia 50.1 ya wahitimu hao ni wanawake waliohitimu katika ngazi za Astashahada, Shahada  na Shahada za Uzamili.

Prof. Mjema amesema kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu katika kampasi zote na kwa sasa katika kampasi ya Dar es Salaam inajengwa maktaba kubwa ya kisasa yenye vyumba vya mihadhara na ofisi na itabeba wanafunzi 11000 kwa mara moja pamoja na ofisi 30 za walimu.

Pia ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi bilioni 1.5 ambazo zimetumika kununua iliyokuwa Shule ya New Hellen na sasa kuwa Kampasi ya CBE jijini Mwanza na kuahidi kuendelea kusimamia vyema Elimu ya Biashara nchini ili kuweza kujenga uchumi wa viwanda na kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati.

Akieleza Changamoto za Chuo hicho Makamu mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho  Prof. George Shumbusho amesema kuwa miundombinu bado haitoshelezi hasa katika Kampasi ya Mbeya.

"Miundombinu iliyopo iliandaliwa kwa kuwahudumia wanafunzi 600 pekee na hadi sasa tunahudumia wanafunzi zaidi ya elfu sita na licha ya Chuo kutumia mapato ya ndani bado changamoto ya miundombinu bado" ameeleza.

Pia ameishukuru Serikali kwa mchango wao na kuiomba kuendelea kushirikiana nao ili kuweza kuendeleza biashara na hiyo ni pamoja na kupatiwa fungu la maendeleo kutokana na uhitaji mkubwa wa fedha wa kuendeleza elimu ya biashara hatimaye kujenga uchumi wa kati na viwanda.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi. Stellah Manyanya akizungumza na wahitimu wa chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa  mahafali ya 54 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) tawi la Dar es Salaam, Prof. Emanuel Mjema akisoma hotuba yake kwa mgeni rasmi na wahitimu waliofika kwenye mahafali ya 54 ya chuo hicho yalifanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi. Stellah Manyanya wakati wa  mahafali ya 54 ya chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi. Stellah Manyanya akiwatunuku wahitimu Astashahada, Stashahada na Shahada waliofika kwenye mahafali ya 54 ya chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo.
  Baadhi ya wahitimu wakishangilia mara baada ya kutunukuwa Shahada  zao wakati wa  mahafali ya 54 ya chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo.

 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi. Stellah Manyanya akiwatunuku baadhi  ya wahitimu Shahada ya Uzamili waliofika kwenye mahafali ya 54 ya chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo.
Picha za pamoja

Bw. Jianpo Zhang na mkewe Shamsa Shaban Zhang wafurahia ndoa yao

0
0
Bw. Jianpo Zhang akiwa na mkewe Shamsa Shaban Zhang wakiwa katika hafla hiyo wakifurahia pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Bw. Jianpo Zhang akiwa na mkewe Shamsa Shaban Zhang wakiwa katika hafla hiyo wakifurahia pamoja na wageni waalikwa mbalimbali wakipata burudani ya muziki.
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo ya kuwapongeza.

……………………………………………

MWANAFUNZI wa Chuo cha Mzumbe ambaye ni raia kutoka China Jianpo Zhang amesema anajisikia fahari kuoa Tanzania akidai kufanya hivyo mbali na kudumisha undugu baina ya familia hizo pia kunazidi kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na China.

Aliyasema hayo wakati wa sherehe ya kuwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kwa namna moja au nyingine kufanikisha harusi yake na mkewe Shamsa Shaban Zhang iliyofanyika wiki iliyofanyika Jijini Dar es Salaam juzi na kuudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi mstaafu Robert Mboma.

Zhang alisema anajivunia kuoa mtanzania huyo akisisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na kwamba kitendo chake cha kufunga ndoa hiyo kitazidi kumfanya ajisikie kuwa kama yupo nyumbani huku akiwataka watanzania kuona fahari pia kwenda kuoa raia kutoka China.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu aliyoishi hapa nchini ameona mambo mengi mazuri na kiasi cha kumfanya ajihisi yupo ‘nyumbani’ na zaidi akidai kuwa amani na upendo kutoka kwa watanzani ndiyo hasa jambo linalozidi kumuongezea hamasa ya kuona undugu unazidi kukua baina ya mataifa yote mawili.

Alisema furaha kwake Tanzania inazidi kukua kimaendeleo siku hadi siku chini ya uongozi wa Rais John Magufuli ambaye pia anasema katika utawala wake ameona wazi wazi ushirikiano baina ya Tanzania na China ukizidi kuhimarika.

“Naipenda Tanzania, nawapenda watu wake na zaidi Rais John Magufuli ambaye katika utawala wake naona mambo mengi mazuri ukiwemo ujenzi wa miradi mbalimbali ikifanyika katika kiwango cha hali ya juu” alisema Zhang.
Alisema mipango yake ya baadae ni kufanya biashara mbalimbali zinazoakisi mahitaji uhimu ya kijamii ili ziweze kuzidi kumuweka karibu na watanzania anaodai kuwa kwa sasa ni ndugu zake hasa baada ya kumuoa mtanzania.

SERIKALI YASEMA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2019 UKO PALEPALE...KAMPENI KUANZA RASMI KESHO HADI NOVEMBA 23 

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotangaza msimamo wa serikali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji ambapo Kampeni zinatarajiwa kuwanza kesho.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga alipokuwa akizungumza nao leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change ADC Bw. Doyo Hassan Doyo akizungumza na waandishi wa habari katika makao mkuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam wakati alipotangaza msimamo wa chama hicho kushiriki uchaguzi huo amesema chama hicho kinashiriki kikamilifu, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change ADC Bw. Doyo Hassan Doyo Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga wakiwa katika picha ya pamoja na wagombea wao wanaoshiriki katika nyazifa mbalimbali za uchaguzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga akizungumza na kusisitiza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wagombea wa chama cha Chama cha ‘Alliance For Africa Farmers Party’ (AAFP) wameenguliwa katika uchagzui huo kwa makosa mbalimbali ya kikanuni na kisheria.
Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai akizungumzzia kuhusu makosa mbaimbali ambayo wagombe wa chama chake walifanya na kisha kuengeuliwa kikanuni na wasimamizi wa uchaguzi.
Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu yao yaliyopo Tandika wilayani Temeke jijini Dar es salaam.

……………………………………………………….

SERIKALI YASEMA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2019 UKO PALEPALE...KAMPENI KUANZA RASMI KESHO HADI NOVEMBA 23 


*Vyama vya siasa ambavyo vitashiriki vyatakiwa kupeleka ratiba ya mikutano ya kampeni Polisi wapewe ulinzi

*Watakiwa kufanya kampeni za kistaarabu katika maeneo yote, wagombea 12319 wapita bila kupingwa

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

SERIKALI imeweka wazi kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka 2019 uko pale pale huku ikitangaza kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi huo zikitarajiwa kuanza kesho. 

Hivyo vyama vyote ambavyo vitashiriki uchaguzi huo zimetakiwa kupeleka ratiba ya mikutano yao ya kampeni kwa wakuu wa Polisi wa Wilaya kwa lengo la kupatiwa ulinzi kuhakikisha kampeni hizo zinakuwa salama na wagombea kupata fursa ya kujinadi kwa wapiga kura.

Wakati Serikali ikitoa msimamo huo baadhi ya vyama kadhaa vya upinzani kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Chama cha Wananchi(CUF) ,Chama cha ACT Wazalendo , Chama cha Chauma na NCCR Mageuzi wao walishatangaza kujitokea ,huku Chama Cha Mapinduzi(CCM) na vyama kadhaa vya upinzani vimetangaza kutoshiriki.

Akizungumza leo Novemba 16,mwaka 2019 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga amesisitiza uchaguzi huo utafanyika kama ambavyo imepangwa na kampeni itaanza kesho nchini na kila kitu kiko sawa.

Amefafanua kuwa kwamba Watanzania waajiandae kusikiliza mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na kisha Novemba 24 wakachague viongozi wao .Tunaomba vyama ambavyo vitashiriki kujiandaa na kampeni ambazo zinaanza kesho( leo) , ushauri wetu kwa vyama hivyo ni kupeleka ratiba ya mikutano yao ya kampeni za uchaguzi huu kwa wakuu wa polisi wa wilaya ili wapatiwe ulinzi,”alisema.

Kuhusu kampeni za uchagzi huo, ameeleza kuwa baada ya kuanza kesho,zitahitimishwa Novemba 23 mwaka huu ambayo itakuwa siku moja kabla ya upigaji wa kura kwa vyama vyote ambavyo vimebakia katika uchaguzi huo.Amesisitiza hakuna sababu ya uchaguzi huo kuusogeza mbele wala kuuahirisha.

Ameongeza kuwa kampeni za uchaguzi huo zinazoanza kesho zitafanyika katika maeneo yenye wagombea pekee na kuyaacha maeneo ambayo wagombea wake wamejitoa au kupita bila kupingwa jambo ambalo pia limevifanya vituo vya uchaguzi kupungua kwa kiwango fulani kutoka vituo 1,10000.

Nyamuhanga amesema kwa ujumla wagombea waliopita bila kupingwa katika mchakato wa uchaguzi huo nchi nzima ni 1,2319 sawa na asilimia 55 ya wagombea wote waliokuwa wamejitokeza kuomba kuteuliwa huku akitoa msisitizo kwa vyama vyote kufanya kampeni za kistaarabu.
Amesisitiza kuwa Wasimamizi wa uchaguzi, askari Polisi, mgambo wote wanapaswa kuwa katika sare kipindi chote cha kampeni hadi uchaguzi utakapofanyika ili kuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kujitokeza huku akitoa onyo kwa vyama hivyo na kuvitaka kuacha kutumia vikundi vya sungusungu na vinginevyo na kwamba sheria itachukua mkondo wake pale ambapo agizo hilo utekelezaji wake utakiukwa.

Katibu Mkuu Nyamuhanga amesema maandalizi ya uchaguzi huo yameshakamilika ikiwemo wino maalumu utakapakwa kidoleni mara baada ya kupiga kura pamoja na rakiri itakayotumika kufungia masanduku mara baada ya kuhitimishwa kwa zoezi la kupiga kura.

Wakati Serikali ikisisitiza kufanya uchaguzi huo, vyama vya ‘Alliance For Democratic Change’ (ADC) pamoja na Chama cha ‘Alliance For Africa Farmers Party’ (AAFP) vimetangaza kushiriki uchaguzi huo kwa kudai havioni sababu yoyote ya wao kujitoa.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Vyama vya Tanzania Labour Party(TLP) na chama cha National Reconstruction Party (NRA) kutangaza kushiriki mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa vikidai kuwa kufanya hivyo ni kuitendea haki demokrasia iliyopo nchini.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo amesema Chama chao kitashiriki uchaguzi huo licha ya ‘figisu figisu’ zilizojitokeza zilizosababisha baadhi ya wagombea wake kukosa kuenguliwa huku akikiri kuwa baadhi yao ‘walijichanganya’ katika mchakato wa ujazaji fomu za uteuzi.

Amesema ni kweli wapo waliofanya makosa ya aina mbalimbali katika ujazaji fomu hatua iliyosababisha kukiuka kanuni, kilichosababisha hayo kutokea hatuwezi kukilaumu kwa kuwa mengine yalitokana na uzembe wao kwa kutowapa elimu wagombea wao kabla ya kuzijaza fomu hizo.

Wakati Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai, pamoja na kusisitiza kushiriki katika uchaguzi huo, amesema changamoto iliyojitokeza katika chama chake na kusababisha wagombea wake kuenguliwa ni kukiuka kanuni katika ujazaji fomu.

Hata hivyo amesema licha ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali wao bado watashiriki katika uchaguzi huo kwa kuwa bado wanao wagombea katika baadhi ya maeneo nchini.'Kwetu hata tukipata mtaa mmoja ni ushindi wa zaidi ya asilimia hamsini, haijarishi wenzetu wameshinda viti vingapi,"ameongeza.

Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ulioanza Oktoba mwaka huu kwa mchakato wa uandikishaji wapiga kura na baadae uchukuaji fomu, urejeshaji wa fomu, ukataji rufaa na sasa.kuanza kwa kampeni ambazo zitahimitishwa kwa kufanyika uchaguzi huo Novemba 24 kwa wananchi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.

KAHUNDI AONGOZA SHEREHE ZA MAHAFALI YA 11 KIDATO CHA NNE 2019 KOM SEKONDARI

0
0
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi ameongoza sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 189 kati yao wasichana 80 wavulana 109 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.

Mahafali hayo yamefanyika leo Jumamosi Novemba 16,2019 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya wazazi,wageni waalikwa,wanafunzi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

Akizungumza wakati wa Mahafali,Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalipia ada watoto wao kwa wakati.

“Nimeambiwa kuna baadhi ya wazazi wanachelewa kulipa ada.Niwakumbushe tu kuwa ukimpeleka mtoto katika shule binafsi maana yake una uwezo wa kulipa ada, sasa lipeni. Elimu ni gharama, hata kwenye shule za serikali ‘ Public Schools’ kuna gharama,kuna nguvu za wananchi”,alisema Kahundi.

“Ni muhimu kumpeleka shule mtoto mara tu shule inapofunguliwa,kwani shule ikifunguliwa masomo yanaanza. Usimuweke mtoto nyumbani,anafanya nini nyumbani muda wa shule?,alihoji Kahundi.
Afisa Elimu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuwakatia bima ya afya watoto wao ili kurahisisha matibabu pindi wanapougua. 

“Vijana mnarudi nyumbani mnatakiwa kuwa watii kwa wazazi wenu,nanyi wazazi msijaribu kuwaozesha wanafunzi hawa waliohitimu kidato cha nne.Msiende kuozesha watoto hawa”,alisema Kahundi. 

Kahundi aliipongeza shule ya Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma na kinidhamu kwani imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali ngazi na mkoa na taifa.

Awali Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi alisema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 wanafunzi 179 walihitimu kati yao 167 walijiunga na kidato cha tano.

Aidha kwa kipindi cha miaka 10 kati ya mwaka 2009 hadi 2018,Koyi alisema jumla ya wanafunzi 1420 wamehitimu kidato cha nne kati yao wanafunzi 1093 walichaguliwa kuendelea na kidato cha tano.

Alisema wanafunzi waliobaki 327 wengi wao wamejiunga na vyuo mbalimbali vikiwemo vya uhasibu,biashara,ualimu,uuguzi,sheria n.k huku akibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na walimu darasani pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya wanafunzi.

Akisoma taarifa ya shule,Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba alisema shule hiyo iliyosajiliwa mwaka 2006 ikiongozwa na kauli mbiu ‘ Elimu bora kwa wote – Quality Education for All’,alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 579 kati yao wavulana ni 314 na wasichana 265 huku walimu wakiwa ni 32 hivyo uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:18.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji zinazosababishwa na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha,baadhi ya wazazi kutolipa ada kwa wakati hivyo kuwafanya watoto wachelewe kufika shule inapofunguliwa na baadhi ya watoto kutowalipia watoto wao bima ya afya. 

Mbali na shule ya sekondari Kom,pia kuna shule ya awali na shule ya msingi Kom iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo nyuma ya ofisi za KASHWASA umbali wa takribani mita 500 kutoka shule ya sekondari Kom. Hali kadhalika wameanzisha kituo cha watahiniwa wa kujitegemea wa kidato cha nne na wale wa QT ‘Private candidates & Qualifying test”.

Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akikata utepe kwenye mahafali hayo.Aliyevaa nguo nyeusi nyuma ni Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akiwasalimia wazazi na wageni waalikwa kwa kuwapungia mkono.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga. Jumla ya wanafunzi 189 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom, ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza shule ya Sekondari Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma kwani imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa neno la salamu wakati wa Mahafali ya 11 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba akisoma historia ya shule ya Sekondari Kom. Warioba aliwaomba wazazi kuwaongoza na kuwaelekeza vizuri vijana waliomaliza elimu ya kidato cha nne wakati wakisubiri matokeo yao yatakayowawezesha kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na vyuo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikata keki maalumu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikabidhi zawadi ya keki kwa walimu wa shule ya sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Onesho la mitindo ya ubunifu wa mavazi likiendelea.. Pichani ni vijana wakionesha ubunifu wa mavazi ya Mama Afrika wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Onesho la vazi mavazi ya wahudumu wa kwenye Ndege likiendelea wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Vijana wa Skauti wakionesha michezo ya ukakamavu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2019.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom,ambapo makadirio ya gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo ni milioni 6.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akichangia pesa wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akimpa Kampani ya kucheza mzee aliyejitokeza kuchangia pesa huku akicheza muziki wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.

Ukawadia muda wa kugawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne 2019 katika shule ya Sekondari Kom.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Walimu wa shule ya sekondari Kom wakikabidhi zawadi kwa Mgeni rasmi ,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi.
Mshereheshaji 'MC' wakati wa mahafali akiendelea kutoa utaratibu wakati wa mahafali hayo.
Wazazi wakifurahia na kijana wao.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA UKAGUZI WA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DODOMA

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (Wa pili kushoto), akikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akipokea maelezo kutoka kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza jinsi ujenzi unavyoendelea wakati ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akitoa maelekezo kwa Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma leo. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

HATIMAYE DK BARIKI ZACHARIA KINGU ALA NONDOZ LEO KCMC

0
0
Mdau wetu Dk Bariki Zacharia Kingu akifurahia mara baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari katika Chuo kikuyu cha udaktari KCMC mjini Moshi mapema leo .Mtandao huy tunampa hongera na kumtakia kila la Kheri katika maisha yake mapya ya kuhudumia watanzania katika kituo chake cha kazi
Matina Nkurlu ambaye ni kaka yake Dk Bariki Zacharia Kingu akimpongeza mdogo wake mara baada ya kutunukiwa leo Shahada ya udaktari katika Chuo kikuyu cha Udaktari KCMC Mjini Moshi mapema leo
Matina Nkurlu na dada yake Blandina Zacharia Kingu wakifurahia Pamoja na mdogo wao Dk Bariki Zacharia Kingu mara baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari katika Chuo kikuu cha udaktari KCMC mjini Moshi mapema Leo.

DK.SHEIN AMEZUNGUMZA NA WAZEE WA CCM WILAYA YA AMANI

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono Wanachama na Viongozi wa CCM cha wakati alipohudhuria katika mkutano wa ndani na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu wa CCM Wilaya ya Amani Kichama Nd,Abdalla Mwinyi Hassan pamoja na Viongozi wengine wakati alipohudhuria katika mkutano wa ndani na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwaangalia wasanii wa kikundi cha ngoma cha Chama mara alipowasili katika viwanja Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Amani leo wakati alipohudhuria katika mkutano wa ndani na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadala (Mabodi) pamoja na Viongozi wengine wakati alipohudhuria katika mkutano wa ndani na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake alipofanya mkutano wa ndani na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani


Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alioufanya na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani


Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake katika mkutano na Wazee hao, uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani


Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake katika mkutano na Wazee hao, uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Kichama Juma Khamis Haji alipokuwa akitoa salamu zake na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama katika Mkutano wa ndani uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati alipofanya Mkutano wa ndani na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Amani Kichama uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Ofisi ya Chama Mkoa Amani,[Picha na Ikulu] 16/11/2019

TISER WAJA NA MWAROBAINI WA MIGOGORO YA ARDHI MVOMERO

0
0
Picha ya pamoja baada ya kumaliza semina iliyowakutanisha wajumbe wa
balaza la ardhi kata ya Dakawa, na wasuruhishi wa mabalaza ya ardhi.
Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania initiative for social and economic relief
( TISER) Otana Nicholus akisalimia na mzee Bwana Philipo Kipuyo mjumbe wabalaza la wasuruhishi kata ya Dakawa.

****************************************

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

Licha ya Rais wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania Dk Jonh Pombe Magufulikumuagiza mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata Ole Sanare kuhakikishaanamaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika mkoa wamorogoro baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa mkoa huo, lakini imeonekanaelimu ya matumizi bora ya ardhi ndio kikwazo kikubwa kwa wananchi.

Hayo yamebainika baada ya asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania initiative forsocial and economic relief ( TISER) linashughurikia utatuzi wa migogoro ya ardhikati ya wakulima na wafugaji pamoja na jamii kwa ujmla, kufanya semina katikakata ya Hembeti, Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, yenye lengo la kupeanauzuefu wa utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Semina hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata ya Hembeti,wajumbe wa balaza la ardhi kata ya Dakawa, wasuruhishi wa mabalaza ya ardhi kutoka katika kata hizo,pamoja na wawakirishi kutoka taasisi ya TISER.

Katika semina hiyo wasuruhishi wa mabalaza ya ardhi wamesema kuwa
wanaishukuru taasisi ya TISER kwa kuwapatia semina ambayo imewajengeauwezo mkubwa katika kutatua migogoro ya ardhi katika vijiji vyao, kwani awali hawakuwa na uwezo mkubwa katika utatuzi wa migogoro hiyo,hivyo wataendakufainyia kazi na wanaamini migogoro ya ardhi itaisha katika vijiji vyao.

Hata hivyo wameimba serikali kushirikiana na asasi mbalimbali katika
kuwaelimisha wananchi hususani wakulima na wafugaji juu ya athari za migogoro ya ardhi katika jamii.

Kwa upande wake Bwana Philipo Kipuyo mjumbe wa balaza la wasuruhishi kataya Dakawa lakini pia anatokea katika jamii ya wafugaji amesema kuwa TISERimewasaidia kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo,ambapo kwa sasawakulima na wafugaji wanakaa kwa amani na familia zao zinaweza
kuona(kuchumbiana baaina ya familia ya mkilima na mfugaji) na kuishi pamoja.

Aidha amesema kuwa mbinu zilizotumika katika kutatua migogoro hiyo ni pamoja na kuwakutaisha wakulima na wafugaji pale mgogoro unapotokea, jambo ambalo limesaidia kumaliza kabisa migogoro katika kijiji chao.

Nae mkurugenzi wa taasisi ya TISER bwana Otana Nicholus amesema kuwa mladi wa kutatua migogoro ya ardhi na kudumisha amani wilaya ya mvomro unalengo la kumaliza kabisa swala la migogoro ya ardhi katika wilaya ya mvomero.

Ambapo kwa sasa mladi huo unatekelezwa katika vijiji mbalimbali ikiwemo
milama,hembeti,dakwa sokoine, mpapa,ruhindo na mkambala,aidha amesemaTISER imeona mvomero kuna migogoro ndio maana wamejikita wilayani humo ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya migogoro ya ardhi.

MZEE WA KARATU ATILIA MKAZO MAELEKEZO YA KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU ALLY.

0
0
Jioni ya leo tarehe 16 Novemba, 2019 Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally amekutana na wananchi mbalimbali wenye changmoto  kutoka mikoa ya Arusha na Morogoro nyumbani kwake Jijini Dodoma.

Miongoni mwa wananchi aliokutana nao ni Mzee wa Karatu Bw. Shauri Gwandu ambapo pamoja na kueleza changamoto za migogoro ya ardhi  zilizokuwa zikimkabili na Katibu Mkuu kutoa  maelekezo kwa viongozi wa Chama na serikali mkoa wa Arusha kushughulikia. 

Katika mazungumzo hayo, Mzee huyo pia amepongeza na kukazia msimamo wa Chama Cha Mapinduzi wa kila mwanachama kijinunulia sare za chama kwa fedha zao wenyewe tofauti na awali ambapo sare za CCM zilikuwa zikigawiwa bure na wakati mwingine kuzua upendeleo.

Huu ni utaratibu wa Dkt. Bashiru kukutana na wananchi wenye changmoto mbalimbali wakati wowote na siku zote za wiki katika kutekeleza maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa kila kiongozi  kwa nafasi yake kukutana na wananchi, kuwasikiliza changamoto zao na kuzitafutia majawabu kwa wakati.

Imetolewa na;
Katibu wa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
Chama Cha Mapinduzi.

DAWASA FC YAZIDI KUFANYA VIZURI LIGI YA MASHIRIKA

0
0

Timu ya mchezo wa Mpira wa miguu ya Mamlaka ya Majisafi nan Usafi wa Mazingira Dar esSalaam (DAWASA) imeendelea kuibuka kidedea katika ligi inayoendelea ya mashirika mballimbali yakijumuisha Umma, binafsi ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Mhandisi Boniface Philemon amesema ligi hiyo inayoendelea kupigwa  katika viwanja vya Gymkhana,   DAWASA FC waliweza kuibuka na ushindi ww 1-0 dhidi ya  Global Publishers FC.

Philemon ameeleza kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa tayari na alama 7 tangu mzunguko wa ligi uanze.

“DAWASA FC tumekuwa vinara katika mechi nyingi tulizoshiriki katika ligi hii kwa kuwa wachezaji wetu wamejituma hivyo tunategemea kuondoka na kombe mwisho wa ligi”

Aidha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA FC Bakari Makilagi amewaasa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza na kushiriki katika mechi zinazoendelea katika ligi hiyo ili waweze kuwashangalia na kuongeza morali kwa wachezaji.

Amesema, kuja kwao kwa wingi kutaifanya timu yao kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Timu ya DAWASA FC inawachezaji 54 waliosajiliwa lakini katika ligi hiyo wameshiriki wachezaji 22 ambapo kuna vikosi viwili na kila kikosi kina jumla ya wachezaji 11.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Yafanya Uhakiki Mali za Baadhi ya Wabunge,Majaji

DK.SHEIN KATIKA ZIARA ZA KUIMARISHA CHAMA CHA CCM

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Mjini patika mkutano wa ndani akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Amani Mkoa,[Picha na Ikulu] 16/11/2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Mjini patika mkutano wa ndani akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Amani Mkoa,[Picha na Ikulu] 16/11/2019.

WAKULIMA MBOGA MBOGA NA MATUNDA WATAJA CHANGAMOTO ZINAZOWAKWAMISHA

0
0
Msimamizi wa Miradi wa taasisi ya TCRS mkoa wa Morogoro,Rehema Samweli, akizungumza na wakulima wa kijiji cha Diovuva, kata ya Kiloka, Halmashauri ya Morogoro vijiji.

Baadhi ya wakulima wakimsikiliza kwa makini Msimamizi wa Miradi wa taasisi ya TCRS, mkutano uliolenga kubaini changamoto zinazowakabili na kutafuta nmana ya kuwaunganisha na masoko ya mijini.



NA VICTOR MAKINDA. MOROGRORO 

Wakulima wa mboga mboga na matunda wa kijiji cha Diovuva kata ya Kiloka, Halmashauri ya Morogoro vijijini wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto lukuki zinazo kwamisha juhudi zao za kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya kilimo, sekta inayoajiri zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania. 

Wakizungumza katika mkutano wa wakulima hao uliondaliwa na Taasisi ya kuwahudumia wakimbizi ya Tanganyika (TCRS), mkutano uliolenga kuzibaini changamoto za wakulima hao na kutafuta namna ya kuzitatua, wakulima hao walisema kuwa ukosefu wa soko la uhakika, bei duni ya mazao sambamba na ujazo mkubwa maarufu kama rumbesa ni miongoni mwa changamoto zinazo wakabili. 

“ Sisi wakulima wa mboga mboga na matunda wa kijijini hapa tunakabiliwa na changamoto nyingi. Kubwa ni kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yetu. Kijiji hiki hakina soko. Lipo gulio tu ambalo hufanya kazi mara mbili kwa wiki. Kama ujuavyo baadhi ya mazao tunayozalisha huoza haraka. Tunaposubiri siku mbili kwa wiki kwa ajili ya kuuza mazao hayo kwenye gulio hutusababishai hasara ya kuoza au tunauza kwa bei ya chini kwa kuhofu kuwa hakuna mahali na siku nyingine tunawez kuuza. Alisema Siraji Rajabu mkulima wa Nyanya kijijini hapo. 

Siraji aliongeza kusema kuwa ukosefu wa barabara ya uhakika ya kusafirishia mazao yao ni kikwazo kingine kinachowafanya kuuza mazao yao kwa bei ya chini hali inayowasababishia hasara. 

Naye Kudra Jumanne mkulima wa mboga mboga wa kijijini hapo alisema kuwa ukosefu wa huduma za ugani ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili na kupelekea kuzalisha kwa hasara kwa kuwa mazao yao hushambuliwa na wadudu. 

“ Sijui kama tunaye afisa ugani hapa kijiji kwetu. Hatumjui na hatijawahi kupata huduma zake. Tunalima kienyeji tu, hatujui namna sahihi ya kutumia mbegu, madawa ya kuulia wadudu na mbole. Mazao yetu yanashambuliwa sana na wadudu.Hatujui nani tumweleze kwa kuwa ukimtafuta mtaalamu wa kilimo kwa ajili ya kupata maelezo ya kitaalamu hapatikani. Alisema Kudra. 

Naye Imani Idy mkulima wa vitunguu saumu na tangawizi kijiji hapo alilalamikia ujazo mkubwa wa mazao maarufu kama lumbesa kuwa ni kikwazo kwa ukuaji wa uchumi wao. 

“Wanapokuja wanunuzi siku ya gulio, ni tatizo kubwa. Hawataki ujazo wa kawaida. Kinyume chake wanatutaka wakulima kujaza lumbesa. Lumbesa inatufanya kuuza mazao mengi kwa bei ndogo ambayo haifanani na gharama za uzalishaji. Tunashangaa serikali ya kijiji na kata wamekaa kimya kuhusu kadhia hizi ambazo wakulima tunazipata. Alisema Imani. 

Akizungumzia changamoto hizo, Diwani wa kata ya Kiloka, Jamila Taji, alisema kuwa ni kweli wananchi wa kijiji hicho wanakabiliwa na changoto ya barabara ya Kiloka Diovuva, ambayo haipitiki hasa masika, ukosefu wa soko la kijiji. Yeye kama diwani amekuwa akisisitiza masuala hayo katika vikao ya Halmashauri kwa kipindi kirefu na kwa sasa mipango ya ujenzi wa soko na barabara hiyo ipo mbioni. 

“ Kuhusu huduma za ugani yupo mtaalamu wa kilimo wa kata, lakini hakuna wa kijiji. Labda wakulima hawamtumii lakini yupo na ninaahidi kumsukuma aende kwa wananchi kuwahudumia. Na hili la ujazo wa lumbesa nitamwelekeza mtendaji kufuatilia. Alisema Taji. 

Msimamizi wa miradi wa shirika la TCRS mkoani Morogoro, Rehema Samweli akieleza madhumuni ya mkutano huo, alisema kuwa shirika lake limedhamiria kuwasaidia wakulima wa kijiji hicho kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo changamoto ya masoko kwa kuwaunganisha na wafanyabisahara wa mijini ili wawe na uhakika wa kuuza mazao yao kwa kwa bei yenye tija.

SIMIYU KUWA NA VIWANDA VICHACHE VITAKAVYOAJIRI MAELFU YA VIJANA

0
0
Anasema Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka; Matarajio yetu ni kuwa Mkoa ambao hatutakuwa na maelfu ya viwanda,-Bali Kuwa na Viwanda vichache vitakavyoajiri Maelfu ya Vijana wa Kitanzania- (One Factory Athousand Employees) .

Pichani juuu ni Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof.Elizabeth Kiondo akiwa na Mwekezaji ambaye amefika Simiyu kwa ajili ya kuwekeza kiwanda cha Nguo pamoja na kiwanda cha vyombo vya udongo(Sahani,vikombe,Glass nk) viwanda vyote viwili vinatarajia kutoa ajira zaidi ya elfu mbili kwa vijana wa Kitanzania ,pichani Mwekezaji  huyo akikagua eneo atakalojenga viwanda vyake ndani ya mji wa Bariadi) Mwaka 2020-Ni Mwaka wa Kutenda-Tuendelee Kumpa Mungu Nafasi.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images