Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

Majadiliano kesi ya uhujumu uchumi yagonga mwamba

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.


ZOEZI la kuomba msamaha na kukiri shtaka dhidi ya kesi ya utakatishaji inzayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi  wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Takukuru, Kulthum Mansoor limeshindwa kufikia mwisho kufuatia majadiliano kati yake na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kugonga mwamba baada ya pande hizo kushindwa kufikia muafaka.

Wakili wa utetezi, Elia Mwingira amedai hayo leo Novemba 12,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevin Mhina wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai Oktoba 30, mwaka huu waliieleza mahakama kwamba mteja wake ameandika barua kwa DPP kuomba kuingia makubaliano na kukiri makosa yake na kwamba mazungumzo ya pande zote mbli yalifanyika lakini hayana mwelekeo mzuri hivyo, wanaomba kesi hiyo iendelee kama ilivyokuwa awali.

Kufuatia zoezi hilo kugonga mwamba, wakili Mwingira aliiomba mahakama itoe amri ya kusikiliza kesi hiyo haraka ili mshitakiwa apate haki yake kwa wakati kwani yupo ndani kwa muda mrefu na kesi yake haina dhamana.

Mapema mahakamani hapo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upalelezi bado haujakamilika ila wataelekeza wapelelezi kuhakikisha wanakamilisha upelelezi katika maeneo yaliyobakia kwa haraka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Mansoor anakabiliwa na mashitaka  manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshitakiwa alighushi barua ya ofa ya  Agosti  13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya  ya Bagamoyo huku akijua kuwa sieeeo kweli.

 Aidha kati ya Januari 2012 na Mei 2017  huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja  kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo,  Mansoor alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mshtakiwa pia  alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Katika mashitaka ya tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh milioni saba kutoka jwa Ekwabi Majungu  ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Mansoor anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa  alijipatia Sh1,477,243,000 wakati akijua kuwa  fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

KIKWETE ATAKA WAZEE WAHUSISHWE KUTATUA MIGOGORO YA MIPAKA.

$
0
0
Na Shushu Joel

MBUNGE wa Jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameitaka serikali kuwatumia wazee wa maeneo husika ili kuondoa migogoro ya mipaka baina ya Kijiji na Kijiji au ile ya kata kwani kwao wameishi maeneo hayo kwa kipindi kirefu.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la chalinze ambapo mbunge huyo alisisitiza kuwa endapo wazee wakipewa nafasi ya kutatua migogoro hiyo itabaki kuwa ni historia.

Aliongeza kuwa katika jimbo lake kuna changamoto ya uwepo kwa baadhi ya maeneo kuwa na matatizo hayo hivyo amewashauri wataalamu wa idara ya ardhi kuwatumia wazee wa maeneo husika kwani wanaweza wakawapa mwelekeo wa kujua jinsi ya kumaliza changamoto hizo.

“Nimefanya mikutano katika jimbo langu kwenye vijiji taklibani vyote hivyo mimi kama mbunge nimeshauri kutumiwa kwa wazee ili kutatua changamoto hiyo”Alisema Kikwete.

Aidha aliongeza kuwa kitu kingine ambacho kimekuwa kikiwachanganya wananchi ni maamuzi yanayofanywa na wataalam katika utatuzi wa migogoro hiyo kwa wao kwenda kwenye maeneo na kuwahusisha watu ambao si sahihi.

Kwa upande wake mzee Said Lufunga (79) amempongeza mbunge kwa kutambu changamoto za mipaka ambazo zimekuwa ni kero kubwa katika jamii.“Ukimuona nyani kazeeka amekwepa mishale mingi hivyo aminini wazee ni kimbilio la matatizo yote” Alisema Lufunga.

Naye Bi, Amina Ramadhani(76) amesema kuwa migogoro inatengenezwa na wataalam kutokana na kutotaka kusikiliza wazawa kwani wao wamekuwa wakitumia vifaa vya kisasa tu.Hivyo amemuomba mbunge Kikwete kuendelea kulipigia kelele Jambo hili uenda mwafaka ukapatikana.

“Wazee kwa kushirikiana na viongozi wa dini wanaweza wakawa suluhiaho la hili Jambo katika halmashauri yetu ya chalinze ” Alisema.
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akizungunza na baadhi ya wazee jimboni humo.

HAFLA YA MAKABIDHIANO YA JENGO LA MAKUMBUSHO KUU BEIT EL AJAIB KWA MKANDARASI YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khadija Bakari akimkabidhi Mkandarasi wa Kampuni ya C,G,G ya Italia Andrea Kwasolo hati ya Ukarabati wa Jengo la Makumbusho Kuu Beit El Ajaib hafla iliofanyika katika ukumbi wa Jumba hilo Forodhani mjini Unguja .
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khadija Bakari akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mji Mkongwe Issa Sariboko Makarani hati ya Ukarabati wa Jengo la Makumbusho Kuu Beit El Ajaib hafla iliofanyika katika ukumbi wa Jumba hilo Forodhani mjini Unguja .
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya Jengo la Makumbusho Kuu Beit El Ajaib iliofanyika katika ukumbi wa Jumba hilo Forodhani mjini Unguja .
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika hafla ya Makabidhiano ya Jengo la Makumbusho Kuu Beit El Ajaib iliofanyika katika ukumbi wa Jumba hilo Forodhani mjini Unguja .
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akionesha nembo ilio katika moja ya Nguzo za Jengo la Makumbusho kuu ya Beit El Ajaib katika hafla ya Makabidhiano ya Jengo hilo kwa mkandarasi iliofanyika katika ukumbi wa Jumba hilo Forodhani mjini Unguja
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya makabidhiano ya Jengo la Makumbusho kuu kwa mkandarasi iliofanyika katika ukumbi wa Jengo hilo Forodhani mjini Unguja .PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Majadiliano kesi ya uhujumu uchumi yagonga mwamba

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.
ZOEZI la kuomba msamaha na kukiri shtaka dhidi ya kesi ya utakatishaji inzayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi  wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Takukuru, Kulthum Mansoor limeshindwa kufikia mwisho kufuatia majadiliano kati yake na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kugonga mwamba baada ya pande hizo kushindwa kufikia muafaka.

Wakili wa utetezi, Elia Mwingira amedai hayo leo Novemba 12,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevin Mhina wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai Oktoba 30, mwaka huu waliieleza mahakama kwamba mteja wake ameandika barua kwa DPP kuomba kuingia makubaliano na kukiri makosa yake na kwamba mazungumzo ya pande zote mbli yalifanyika lakini hayana mwelekeo mzuri hivyo, wanaomba kesi hiyo iendelee kama ilivyokuwa awali.

Kufuatia zoezi hilo kugonga mwamba, wakili Mwingira aliiomba mahakama itoe amri ya kusikiliza kesi hiyo haraka ili mshitakiwa apate haki yake kwa wakati kwani yupo ndani kwa muda mrefu na kesi yake haina dhamana.

Mapema mahakamani hapo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upalelezi bado haujakamilika ila wataelekeza wapelelezi kuhakikisha wanakamilisha upelelezi katika maeneo yaliyobakia kwa haraka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Mansoor anakabiliwa na mashitaka  manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshitakiwa alighushi barua ya ofa ya  Agosti  13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya  ya Bagamoyo huku akijua kuwa sieeeo kweli.

 Aidha kati ya Januari 2012 na Mei 2017  huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja  kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo,  Mansoor alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mshtakiwa pia  alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Katika mashitaka ya tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh milioni saba kutoka jwa Ekwabi Majungu  ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Mansoor anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa  alijipatia Sh1,477,243,000 wakati akijua kuwa  fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

KITABU CHA UJASIRI WA PEKEE WA RAIS MAGUFULI KUZINDULIWA DESEMBA, 2019

$
0
0

"Finest Valor" Ujasiri wa Pekee" Simulizi ya Kuibuka kwa Rais John Pombe Magufuli.

 KITABU cha Mafanikio ya Rais Dr.John Pombe Magufuli, kuanzia mchakato wa kumpata kama mgombea, kampeni ya Urais 2015, kuapishwa Novem Ba 5 2015, sera na mipango yake. 

Ujasiri wa kusimamia rasilimali za nchi, kufufua shirika la ndege, kujenga misingi ya uzalendo, sera ya mambo ya nje na kufanikiwa kupambana na rushwa na ufisadi kwa kiwango cha juu.

Kitabu hicho kimeandikwa na Novatus Joseph Igosha Mwanasheria Wizara ya katiba na sheria na kinatarajiwa kuzinduliwa Disemba 2019.

Kimehaririwa na Spika mstaafu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, kitabu hicho kwa sasa kimepitishwa katika kampuni ya Afrika kusini inaitwa Reach Publishers.

Kitabu hicho kinalengo la kujenga uzalendo kwa kuonesha ujasiri wa serikali ya Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya maamuzi kijasiri katika kusimamia rasilimali za nchi, kupambana na rushwa na ufisadi kizalendo.

 Ila pia kutambulisha upekee wa serikali hii katika kujenga uchumi wa kati na wa viwanda kwa siku zijazo.

WAFANYABIASHARA IFAKARA WAELIMISHWA KUHUSU KODI YA ZUIO

$
0
0
Na Veronica Kazimoto ,Ifakara 

Wafanyabiashara wa Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameelimishwa kuhusu Kodi ya Zuio katika eneo la ukodishaji majengo na ardhi ambapo mpangaji anapaswa kukata kodi na kuwasilisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) asilimia kumi ya kiasi cha malipo walichokubaliana katika mkataba wa upangishaji.

Akizungumza wakati wa Kampeni ya Usajili, Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayofanyika mkoani Morogoro, Afisa Kodi Mkuu, Julius Mjenga amewataka wapangishaji kutowazuia wapangaji kukata asilimia 10 ya malipo ya mkataba kwakuwa kodi hiyo inatozwa kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato na inasimamiwa na TRA. 

“Kodi ya zuio inatozwa kwa mujibu wa sheria na anayeisimamia sheria hiyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania hivyo wapangishaji wote mnapaswa kutowazuia wateja wenu ambao ni wapangaji wa majengo na ardhi kuwasilisha asilimia kumi ya malipo kufuatana na mkataba mlioingia,” alisisitiza Mjenga. 

Mjenga ameeleza kuwa, kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wapangishaji kuwakatalia wapangaji wao kukata asilimia hiyo na pale wapangaji wanapolazimisha husitishiwa mkataba au kupewa notisi ya siku 90. 

“Iwapo mpangishaji atakaidi malipo hayo ya asilimia kumi yasikatwe na mpangaji kwa lengo la kuyawasilisha TRA, mpangishaji huyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015,” alisema Mjenga.

Kodi ya zuio inatozwa katika maeneo tofauti ikiwa ni pamoja na malipo ya mishahara, mirabaha, hisa, upangishaji na gawio mbalimbali ambapo kila eneo limepangiwa kiwango cha asilimia kinachotakiwa kulipwa.

Kampeni ya usajili, huduma na elimu kwa mlipakodi imeanza tarehe 11 na itamalizika tarehe 17 Novemba, 2019 na inafanyika katika wilaya zote za Mikoa ya Morogoro na Pwani.
Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rahabu Kibona (kulia) akiwakabidhi Namba za Utambulisho kwa Mlipakodi (TIN) mara baada ya kusajiliwa wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa Mikoa ya Morogoro na Pwani.
 Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Julius Mjenga akiwaelimisha Wafanyabiashara wa Ifakara mjini mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa Mikoa ya Morogoro na Pwani.
Afisa TEHAMA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Shukuru Bathoromeo akimsajili Mfanyabiashara wa Rupiro mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa Mikoa ya Morogoro na Pwani.

JAJI MKUU ATOA NENO MIMBA ZA UTOTONI RUKWA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (Kulia) baadhi ya vipeperushi vinavyoelezea sheria za watoto ili aweze kujielimisha zaidi ikiwa ni moja ya utamaduni wake kufanya hivyo anapofika katia ofisi za mihimili mingine ya serikali.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (Katikati) Katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa (kuliani kwake) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushotoni kwake) Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrango na viongozi wengine.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (Katikati) Katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa (kuliani kwake) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushotoni kwake) Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrangona viongozi wengine.
………………….

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kufanya tathmini ya kazi inayofanywa na wapelelezi pamoja na waendesha mashitaka katika kesi iwapo wanatekeleza wajibu wao ipasavyo. 

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim Wangabo alipomtembelea ofisini kwake akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kesi kutomalizika kwa wakati na wakati mwingine haki kutotendeka kutokana na wapelelezi pamoja na waendesha mashitaka kutotekeleza wajibu wao ipasavyo.

Aidha Jaji Mkuu ameishauri Serikali kuwabana wapelelezi na waendesha mashitaka ili wawe wanajiandaa vizuri katika kesi mbalimbali.

Alisema endapo kutakuwa na maandalizi hafifu ya hati ya mashitaka katika kesi huweza kusababisha upelelezi wa kesi hiyo kutofanyika inavyotakiwa na hivyo kupelekea wakati mwingine haki kutotendeka na kusababisha mfumo wa sheria kutoaminiwa na wananchi.

Alisema matumizi ya Tehama katika kesi yatarahisha na kusaidia haki kutendeka na kesi kumalizika kwa wakati huku akitolea mfano wa matumizi ya kipimo cha DNA kwenye kesi kubwa kama vile za mauaji na ubakaji. Alisisitiza umuhimu wa hivyo kuchukuliwa mapema kabla ya ushahidi haujapoa.

Akitolea mfano wa kesi kwenye Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu alisema wakati mwingine Majaji hukutana na changamoto ya maandalizi hafifu ya hati ya mashitaka kwa kuwa inakuwa haiendani na tukio lenyewe.

Alisema kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia, hivi sasa wapelelezi hawana budi kuchukua maungamo ya kesi kwa njia ya picha video. “Upelelezi bado uko karne ya 16 wakati wahalifu wako karne ya 21”, alisema Jaji Mkuu. 

Kuhusu Mahakama kuanza kutoa hukumu kwa lugha ya Kiswahili, Jaji Mkuu amesema suala hilo ni muhimu na Mahakama italifanyia kazi. Aliongeza kuwa hivi sasa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kinatoa mafunzo kwa Mahakimu ya uandishi wa hukumu kwa lugha nyepesi na inayoeleweka zaidi. 

Awali akizungumza, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliiomba Mahakama kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati hususani zile zinazohusiana na mimba za utotoni kwa wananfunzi wa shule za msingi pamoja na Sekondari zilizopo kwenye mkoa wake.

Alisema tayari kesi 40 za makossa hayo zimefikishwa mahakamani lakini kati ya hizo ni kesi tatu tu ambazo zimesikilizwa na kutolewa maamuzi. Alisema katika kipindi cha mwaka moja kanzia Julai 2018 mpaka Oktoba 2019 katika mkoa wake kuna jumla ya wanafunzi 294 waliopata mimba wakiwemo 209 wa shule za sekondari na 85 wa shule za msingi. 

Naye Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Mhe. Halfan Haule aliiomba Mahakama kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa hukumu kwa lugha ya kishwahili hasa kwenye ngazi ya Mahakama za wilaya ili kuwawezesha wananchi kuzielewa kwa urahisi.

Alisema hivi sasa wananchi walio wengi hutumia muda mwingi kuzunguka kwenye ofisi mbalimbali za wanansheria ili kupewa tafsiri za hukumu zao hatua inayowafanya kuchelewa kupata haki ikiwemo kuchelewa muda wa kukata rufaa endapo wanakuwa hawajaridhishwa na hukumu zilizotolewa. 

Jaji Mkuu ameanza ziara ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga ambapo awali alikagua miradi ya ujenzi katika mkoa wa Songwe pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga. Jaji Mkuu anaendelea na ziara kukagua shughuli za Mahakama katika wilaya za Nkasi na Kalambo.

Na Lydia Churi-Mahakama Sumbawanga

WAJASIRIAMALI TABATA WAKICHAKALIKA

$
0
0


 Wajasiliamali maarufu kama machinga wakiandaa biashara zao leo kama wanavyo onekana pichani  katika kituo cha Mabasi Tabata Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Da es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

 Wafanya biashara wa viazi katika kituo cha  Tabata Segerea  wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwahudumia wateja wanaotoka sehemu mbalimbali,ambapo fungu moja la viazi limauzwa shilingi 1000 mpaka 2000 na Nazi moja  kuanzia mia tano mpaka 1500.



THAMINI UHAI WON TANZANIA CSO OUTSTANDING IMPACT IN SOCIAL SERVICES DELIVERY AWARD

$
0
0
The CSO Excellence Awards 2019 ceremony was held on 8th November 2019 at Morena Hotel, Dodoma organized by Foundation for Civil Society(FCS), in order to celebrate, recognize and honor achievements and contributions made by different institutions or individuals that have influenced development policy and practice in Tanzania. The award ceremony gives an opportunity for organizations to showcase their activities and impact for the sake of their own public relations and fundraising activities. The awards also offer the larger group a chance to learn about the unique approaches applied by different actors in the field of development for the sake of replication of change and innovation in the sector.

Thamini Uhai won the CSO Excellence Award of Outstanding Impact in Social Services Delivery category for their outstanding work to improve women’s and newborn babies’ health especially in rural areas and marginalized communities in Kigoma, Morogoro and Pwani regions. The awards organizer received 166 nominations of people and organizations that have had an outstanding impact in a number of areas and in the category of social services delivery the finalists were Thamini Uhai, KCE and FAWOPA.

The selection for this award was made on the basis of the development impact, scale, sustainability, impact to marginalized/vulnerable groups, creativity and innovation. The CSO Excellence Award for Outstanding Impact on Social Services Delivery category was presented by the President of FCS, Dr. Stigmata Tenga and was delivered to the Executive Director of Thamini Uhai, Dr. Nguke Mwakatundu.

In his comment about the award Thamini Uhai received at CSO Excellence Awards 2019 ceremony, Dr. Nguke Mwakatundu said “We are happy to receive this award recognizing our work. Our team has been working tirelessly to improve maternal and newborn health outcomes of rural and marginalized communities and we are grateful to see the impact contributed by our organization being recognized. We take the award as a motivation towards our commitment to further help our country to meet its maternal and newborn health goals”

SBL mdhamini mkuu mashindano ya Waitara Gofu 2019

$
0
0
Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti kwenye mashindano ya Waitara Gofu ya mwaka 2019 yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumamosi viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam. Wengine ni Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo Gofu Brigedia Generali Mstaafu, Michael Luwongo (katikati) na Nahodha wa klabu ya Gofu ya Lugalo , Kapt. Japhet Masai
Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi akipeana mkono wa pongeza na Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo Gofu Brigedia Generali Mstaafu, Michael Luwongo mara baada ya kutangaza udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti kwenye mashindano ya Waitara Gofu ya mwaka 2019 yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumamosi viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam. Wengine ni Nahodha wa klabu ya Gofu ya Lugalo , Kapt. Japhet Masai (kulia) na Afisa Utawala wa klabu hiyo Luteni. Samwel Mosha.



Jumla ya wachezaji 120 wa gofu kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini, wanatarajiwa kuchuana vikali mwishoni mwa wiki katika mashindano ya Waitara Gofu ya mwaka 2019 yanayodhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Mashindano hayo ya siku moja, yatafanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam, Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi aliwaambia waandishi wa habari kuwa udhamini wa SBL kwenye mashindano hayo maarufu, unalenga kuendeza mchezo wa gofu hapa nchini.

“Kampuni ya SBL kupitia bia yake pendwa ya Serengeti Premium Lager inayofuraha kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya gofu ya Waitara ya mwaka huu. Udhamini huu unaonyesha nia yetu ya dhati ya kuendeleza michezo hapa nchini,” alisema Anitha.

Kupitia bia ya Serengeti Premium Lager, kampuni ya SBL ni mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars Serengeti na pia inadhamini ligi ya taifa ya wanawake kupitia bia yake ya Serengeti Lite.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo aliishukuru kampuni ya SBL kwa udhamini huo na kuyataka makampuni na taasisi nyoingine kuiga mfano wa SBL na kujitokeza kusaidia michezo wa gofu nchini.

“Tunaishukuru sana kampuni ya SBL kwa mchango wake kwenye kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini na hususani gofu. SBL imekuwa mdhamini mkubwa wa mashindano haya,” alisema.

Mashindano ya Waitara Golf hufanyikja kila mwaka yakilenga kutambua mchango wa Genelrali mstaafu George Waitara aliyekuwa mkuu wa majeshi kwa kuanzisha klabu ya golf ya Lugalo.

Klabu ya Golf ya Lugalo ilianza mwaka 2006 kutokana na mchango mkubwa wa Waitara ambo pia uliendelezwa na Generali Davis Mwamunyange ambaye alimfuatia baada ya kustaafu.

MRADI WA KIWANDA KIKUBWA CHA DAWA TANZANIA WAVUTIA WAWEKEZAJI WA KIMKAKATI AFRIKA KUSINI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Johannesburg 

Tanzania imewasilisha miradi 13 ya Kipaumbele kwa wawekezaji wa kimkakati wanaoshiriki kongamano la Jukwaa la Uwekezaji Mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango anayemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo, amesema Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa mchanganyiko kitakachogharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 408 umewavutia wawekezaji wengi.

Amewataja wawekezaji waliovutiwa na mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho kitakachojengwa Kibaha mkoani Pwani, kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya aina 230 za dawa kwamba wanatoka nchi za Korea, Uturuki, taasisi za fedha za kimataifa na kwamba hadi kufika mapema mwakani (2020) mwekezaji mmoja au zaidi watakuwa wamepatikana kwa ajili ya kuanza kujenga mradi huo.

"Pamoja na kupunguza tatizo la uhaba wa dawa na dawa bandia zinazoingizwa nchini, kiwanda hiki pia kitazalisha ajira kwa watanzania" alisema Dkt. Mpango. 

Dkt. Mpango amesema Serikali inatenga zaidi ya sh bilioni 230 kwenye Bajeti kila mwaka kwa ajili ya kununua dawa huku mahitaji halisi ya dawa nchini ni takriban shilingi trilioni 1.4 ndio maana mkazo umewekwa kwenye ujenzi wa kiwanda hicho kitakachotatua changamoto za upatikanaji wa dawa nchini.

Alifafanua kuwa miradi mingine 12 iliyowasilishwa mbele ya wawekezaji hao iko katika hatua za maandalizi na iko katika sekta za Nishati ya umeme unaotumia nguvu ya maji, viwanda vya kuchakata pamba ili kuiongezea thamani na hatimaye kuzalisha nguo, ambavyo vinaendana na dhamira ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake, Meneja Miradi kutoka Bohari ya Dawa ya Taifa Mhandisi Fredrick Pondamali ameeleza kuwa usanifu wa mradi huo wa kiwanda cha kuzalisha dawa mchanganyiko umekamilika pamoja na viwanda vingine viwili zaidi vinavyotafutiwa wawekezaji.

Alisema kuwa mradi wa kiwanda cha kuzalisha dawa ulichaguliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa lengo la kuupeleka mbele ya wawekezaji ili uweze kupata fedha kutokana na umuhimu wake kwa Tanzania na nchi jirani.

Jukwaa hilo la Uwekezaji Afrika linalofanyika kwa mwaka wa pili sasa limeandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kwa kushirikiana na wadau wake mbalimbali ambapo mwaka huu limevuta wawekezaji wa kimkakati zaidi ya 4000 kutoka kila pembe ya dunia ikiwa na lengo la kuongeza uwekezaji kwenye ujenzi wa miundombinu ili kuchochea kasi ya mabadiliko ya kiuchumi katika nchi za Bara la Afrika.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Dkt. Alex Mubiru, kando ya Kongamano la Jukwaa la Wawekezaji Afrika (Africa Investment Forum), unaoendelea Mjini Johannesburg, Afrika Kusini
 Msimamizi wa Dawati la Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Said Nyenge (wa pili kulia) akimweleza Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika Dkt. Alex Mubiru (kulia) kuhusu miradi ya kipaumbele iliyowasilishwa na Serikali kwenye Kongamano la Jukwaa la Uwekezaji Afrika), linalofanyika Johannesburg, Afrika Kusini. Kulia ni Bw. Frank Sanga kutoka AfDB na wa pili kulia ni Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipangp Bw. Abel Philip.
 Mkuu wa Idara ya Huduma za Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Abubakar Ndwata, akimweleza mwekezaji kutoka Kampuni ya Burhani Engineers kutoka Zoher Pirbhai kutoka nchini Kenya kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa Kongamano la Jukwaaa la uwekezaji la Afrika, linalofanyika Johannesburg nchini Afrika Kusini,
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (aliyeipa mgongo kamera kushoto) akizungumza na wawekezaji wa kimkakati walioonesha nia ya kuwekeza kwenye Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza dawa chenye thamani ya dola za Marekani milioni 408, kutoka nchi za Korea, Uturuki na taasisi za fedha za kimataifa, wakati wa Jukwaa la Africa Investment Forum), unaoendelea Mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Baadhi ya wawekezaji wa kimkakati kutoka nchini Korea, Uturuki na Taasisi za Fedha za Kimataifa, wakielezea nia yao ya kuwekeza kwenye Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha dawa nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Marekani milioni 408, walipokutana na kufanya kikao na Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Philip Isdor Mpango, mjini Johannesburg, Afrika Kusini

WAZIRI LUGOLA AWAONGOZA WATENDAJI WAKUU UHAMIAJI, NIDA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA, JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akisoma Taarifa ya Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dtk. Anold Kihaule (kushoto) akiwa na Maafisa wake, wakifuatilia taarifa iliyokuwa inasomwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), kuhusu Mamlaka hiyo, katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akisoma Taarifa ya Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Katibu wake, Nelson Kaminyoge alipokuwa akimfafanulia jambo kabla ya kuingia katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YA RAIS MSTAAFU MHE. MKAPA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akizindua kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa
Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akishuhudiwa na Rais wa
Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan
Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Finland nchini Tanzania
Mhe. Antila Sinikka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne Novemba 12, 2019
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William akihutubia
wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Maisha yake katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Jumanne Novemba 12, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli baada ya kuzindua kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na Rais waZanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan
Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne Novemba
12, 2019





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza kwa hotuba nzuri Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe.
Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya
Mhe. Mkapa huku akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed
Shein na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete pamoja na Balozi wa Finland nchini Mhe. Antila Sinikka katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam


leo Jumanne Novemba 12, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiongoza kunyanyua glasi na kumtakia maisha marefu Rais Mstaafu wa
Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa katika kuadhimisha siku ya
kuzaliwa kwake wakati wa sherehe za uzinduzi wa kitabu cha historia ya
Maisha ya Mhe. Mkapa. Wengine hapo meza kuu ni Rais wa Zanzibar Dkt.
Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Anna Mkapa katika Ukumbi wa Mikutano waKimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne Novemba
12, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin
William Mkapa baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Mhe. Mkapa.
Wengine ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu
Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Balozi
wa Finland nchini Mhe. Antila Sinikka na Mama Anna Mkapa pamoja na
maafisa wa Ofisi Binafsi ya Mhe. Mhe. Mkapa katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne
Novemba 12, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin
William Mkapa baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Mhe. Mkapa
wakiwa na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne Novemba 12, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin
William Mkapa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Marais wastaafu Alhaj
Ally Hassan Mwinyi na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuzindua
kitabu cha Historua ya Maisha ya Mhe. Mkapa katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne
Novemba 12, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin
William Mkapa baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Mhe. Mkapa.
Wengine ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu
Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Balozi
wa Finland nchini Mhe. Antila Sinikka na Mama Anna Mkapa na familia ya
Mhe. Mkapa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumanne Novemba 12, 2019



WADAU WALIOMBA BUNGE KURIDHIA ITIFAKI YA MITANDAO YA TEHAMA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe 


Na Prisca Ulomi, WUUM

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewasilisha Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mitandao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (EAC Protocol on ICT Networks) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ili waweze kuipitia na kuridhia kabla ya kuiwasilisha kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baada ya Kamwelwe kuwasilisha Itifaki hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, Kamati ilipokea Itifaki hiyo na kualika wadau wa Sekta ya Mawasiliano ili waweze kufika mbele ya Kamati hiyo na kutoa maoni yao.

Kamwelwe aliwaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa madhumuni ya Itifaki hiyo ni kuendeleza uunganishaji wa miundombinu ya TEHAMA mipakani; kuwezesha matumizi ya pamoja ya miundombinu ya TEHAMA, ikiwa pamoja na masafa na namba; kuwezesha matumizi ya huduma za mitandao ya TEHAMA bila upendeleo; kuendeleza matumizi ya huduma za mitandao ya TEHAMA Serikalini na kwenye sekta binafsi ikijumuisha Serikali Mtandao, Biashara Mtandao, mfumo wa “Geospatial Information.

System (GIS)” na utangazaji; kuwianisha sera, sheria na programu za TEHAMA zitakazowezesha kufikiwa kwa malengo ya itifaki; kutoa elimu bora na mafunzo yanayohitajika kwa ajili ya uongozi wa kimkakati, usimamizi, utafiti na ujuzi katika eneo la mitandao ya TEHAMA ndani ya Jumuiya; kuendeleza mashirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi; kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa wote hususan kuunganisha visiwa na nchi zisizopakana na bahari; na kuhakikisha usalama na ubora wa huduma za mawasiliano na kuwezesha matumizi salama ya mtandao.

Aliongeza kuwa kwa upande wa Tanzania, nchi yetu imejiimarisha kwa kuweka miundombinu muhimu ya TEHAMA ambayo ni pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao umejengwa na kufika katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar na kufikisha kwenye maeneo tisa ya mipaka na nchi jirani ikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda ambapo kuna watoa huduma za mawasiliano wa nchi hizo wanaotumia Mkongo wa Taifa. Pia, nchi za Rwanda, Uganda, Zambia na Malawi zinategemea uwepo wa miundombinu ya TEHAMA ya Tanzania kuwasiliana kimataifa.

Vilevile, watoa huduma wa nchini Kenya wanatumia Mkongo wa Taifa wa Tanzania kupitisha mawasiliano yake kwenda nchi nyingine. Miundombinu mingine iliyopo ni Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data, Vituo sita vya maunganisho ya watoa huduma za intaneti (Internet Exchange Point – IXPs), miundombinu ya utangazaji pamoja na Mfumo wa Kuratibu na Kusimamia Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System-TTMS). Pia, Serikali inaendalea kukamilisha Mkakati wa Taifa wa Mtandao wa
Kasi (National Broadband Strategy).

Wakitoa maoni yao kuhusu Itifaki hiyo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wadau mbali mbali wakiwemo Kampuni ya Simu ya Airtel, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC) wameridhia Itifaki hiyo na kuomba Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliridhie na kupitisha Itifaki hiyo Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi alisema kuwa, “Itifaki hii nimekuja wakati muafaka, Tanzania imekuwa mdau wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, imejenga miundombinu na kuwezesha nchi za jirani zisizopakana na bahari kupata
mawasiliano.

Itifaki hii itatuweka mahali pazuri na tutashirikiana vema, kwa sasa
tunaingia makubaliano baina ya nchi mbili na kupeleka mawasiliano, ila tukitofautiana hakuna pa kwenda, ila kupitia itifaki hii tutaendelea kufungua masoko EAC na nchi za SADC ambapo hadi sasa tumeunga Malawi na tunaendelea Msumbiji,”.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa TCRA, Dkt. Phillip
Filikunjombe alisema kuwa Itifaki hii ikipitishwa, nchi wanachama wa EAC tutakuwa na fursa ya kukaa pamoja na kuja na sheria zinazofanana na zinazoendana na matakwa ya nchi yetu katika kudhibiti uhalifu mtandaoni

Filikunjombe alifafanua kuwa Tanzania tumefunga mtambo wa TTMS ambapo Itifaki hii inazungumzia mifumo ya kudhibiti usalama wa mtandao kwa kuwa Tanzania sio kisiwa na uhalifu mtandao hauna mipaka, tutahakikisha nchi za wenzetu wanakuwa na mifumo yenye viwango vinavyohitajika kudhibiti usalama kwa kuwa hawana mfumo kama TTMS hivyo tutahakikisha nao wanafunga mifumo ya kudhibiti uhalifu wa mtandao na usalama.

Mwakilishi wa Airtel, Delfina Martin alisema kuwa kampuni yao imeridhia Itifaki hii na itapunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wao wanaowasiliana kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine kwa kuwa hadi sasa Airtel wapo nchi 16 za Afrika na wana makubaliano ya moja kwa moja ya kutumia miundombinu na huduma za mawasiliano.

Baada ya kupokea maoni ya wadau, Kakoso amesema kuwa Kamati yake imeridhia Itifaki hiyo na itawasilisha taarifa yake Bungeni na kuunga mkono Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili Itifaki hiyo iweze kuridhiwa kupitishwa na Bunge

WAZIRI MKUU KUZINDUA MKAKATI MPYA WA KITAIFA WA KIDIJITALI NOVEMBA 14, DODOMA

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI MKUU Mhe Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkakati mpya wa kitaifa wa Afya wa kidijitali utakaofanyika Novemba 14 mwaka huu jijini Dodoma.

Mkakati huo wenye lengo la kufanya maboresho kwenye sekta ya Afya umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais-TAMISEM ambapo unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa mojawapo ya wa Nchi viongozi ulimwenguni katika afya ya kidijitali.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Mkurugenzi Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya, Dk Grace Magembe amesema mojawapo ya mambo muhimu kwenye mkakati huo ni muundo wa utawala ambao unaongeza meno na ufanisi katika mkakati tekelezaji wa mkakati huo.

" Viungo viwili vikuu vitawajibika kimsingi katika mkakati huu navyo ni Kamati ya usimamizi wa afya ya kidijitali na Sekretarieti ya Afya ya Kidijitaki Kitaifa," Amesema Dk Grace.

Amesema mkakati huu mpya wa kitaifa ni wa miaka mitano hadi 2024 na utaenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2024, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (2015-2020) na sera zingine muhimu zinazohimiza juhudi Nchi kujenga mifumo madhubuti ya kidijitali inayoweza kuwasiliana na sekta ya afya.

Vilevile amesema Serikali inatarajia kuzindua maktaba ya kidijitali kuhakikisha kuwa kuna uwazi na wadau wanapata taarifa juu ya mipango iliyopo ya afya na hati zote.

" Sambamba na wiki hii kutarajia kuzindua mpango huu kuna Kazi nyingi ambazo zinaendelea kwenye viwanja vya Jamhuri ikiwemo kupika afya ya magonjwa yasiyoambukiza na tunashukuru mwamko wa wananchi umekua mkubwa ingawa tunasisitiza waziri kujitokeza kwani hakuna malipo yoyote.

Pia tutazindua mpango wa magonjwa yasiyoambukiza ambapo moja ya Kazi ya mkakati huu wa kidijitali ambao pia tutauzindua itakua kuhifadhi takwimu za magonjwa yasiyoambukiza, lazima tuweze kufuatilia rasilimali zote zinazoingia kwenye huo mpango je zinaleta tija? Lakini pia tuwe na taarifa muhimu za haya magonjwa je zinaongezeka au zinapungua," Amesema Dk Grace.

Amesema wao kama Wizara wameamua kwenda na mpango huo wa kidijitali ili kuwa na Benki ya takwimu lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa sekta ya afya nchini.Mpango huo unatajwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 100 na umeandaliwa kwa muda wa miezi sita hadi kukamilika.

Dk Grace amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kupima afya zao sambamba na kufanya mazoezi ambayo yamekua muarobaini wa magonjwa yasiyoambukiza." Sekta ya afya ni sekta ambayo inabadilika sana, kila siku magonjwa mapya na tiba mpya zinakuja, mpango huu utakua msaada kwenu tutakapohitaji kufanya tafiti maana tutakua na takwimu ya kile tunachohitaji kukifanyia utafiti.

Sasa mfumo huu wa kidijitali utatusaidia sasa kuangalia zile takwimu zetu na kuzifuatilia kuona kama kuna mambo mapya yanatokea ni kwanini kwahiyo tutatumia takwimu zetu kufanya tafiti. Mpango huu wa kidijitali unaenda kuwa mkombozi kwenye sekta hii muhimu ya Afya," Amesema Dk Grace.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Grace Mapunda akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo kuhusiana na uzinduzi wa mkakati mpya wa kitaifa wa afya ya kidijitali utakaofanyika Novemba 14 mwaka huu jijini Dodoma.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUANZISHA KAMPUNI YA UJENZI KUPITIA VIKOSI VYAKE VYA ULINZI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa Kuanzisha Shirika au Kampuni ya Ujenzi itakayovishirikisha Vikosi vyake vya Ulinzi ili kupunguza gharama katika masuala ya Ujenzi wa Majengo ya Taasisi za Umma Nchini.

Alisema tabia iliyozoeleka ya kuyatumia Makampuni pamoja na Washauri elekezi wa nje ya Nchi katika kusimamia Majengo ya Taasisi za Serikali unapaswa kuepukwa kwa vile unasababisha kutumia gharama kubwa ambazo wakati mwengine zinaweza kutumika katika ujenzi wa majengo mengi zaidi.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akimalizia ziara yake Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kukagua Miradi ya Maendeleo na kuangalia changamoto zinazowakwaza Wananchi akimalizia Wilaya ya Kaskazini “B” kwa kuanzia ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Wananchi wa Kijiji cha Dundua walioamua kupisha Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Bandari huko Mwangapwani.

Alisema upo ushahidi wa wazi unaoshuhudiwa na Serikali pamoja na Watendaji wa Taasisi za Umma wa jinsi Vikosi vya SMZ vinavyowajibika vyema wakati vinapopewa tenda za ujenzi wa Majengo ya Taasisi mbali mbali ambapo umefika wakati nguvu zao zikaunganishwa pamoja ili kuleta tija na faida zaidi.

Balozi Seif alisema Wahandisi wa Vikosi hivyo vya Mafunzo, KMKM na JKU wanastahiki kupongezwa kwa Uzalendo wao uliopelekea kuanza kuaminika wakatui wanapokabidhiwa kazi za Ujenzi pale inapofikia wakati Serikali au Taasisi za Umma na hata Binafsi zinapohitaji huduma hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru Wananchi wa Kijiji cha Dundua kwa mapenzi yao ya kuiridhia Serikali Kuu kwa kupisha Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Gati ya Mafuta na Gesi kwenye Makaazi yao ambapo kwa kitendo hicho ndipo Serikali ilipoamuwa kuwajengea Nyumba za Kudumu katika Kijiji cha Gongoni.

Alisema Serikali iliamua kujenga Nyumba za kudumu badala ya kuwapa Fedha kama fidia ambazo hatma yake zingeishia katika matumizi mengine ya kawaida na kuziacha Familia za Wananchi wao kusambaratika bila ya kuwa na Makaazi ya Kudumu.

Balozi Seif alisisitiza kwamba Wananchi hao wa Dundua ambao baadae watahamia katika Makaazi yao mapya yaliyopo Kijiji cha Gongoni wameanza safari ndefu ya Maendeleo kwa vile eneo lao limeshaingizwa ndani ya Mipango Miji itakayokiwezesha Kijiji hicho kuwa Mji Mdogo.

“ Wananchi mnapaswa kutokuwa na wasi wasi wowote kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote inawajali Raia wake wote katika kuimarisha ustawi wao”. Alisisitiza Balozi Seif.

Mapema Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Wananchi wa Dundua Mhandisi Hawa Natepe alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Mradi huo unahusisha Nyumba 31 zinazosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa Mafuta {ZURA}.

Bibi Hawa alisema Nyumba hizo zinazojengwa kwa pamoja na Vikosi vya Mafunzo na KMKM vikitanguliwa na JKU kwa ufyatuaji wa Matofali ya Nyumba hizo zitakuwa na Vyumba Vitano kwa Nyumba 29 na Vyumba Vitatu kwa Nyumba Mbili.

Alisema ujenzi huo kwa awamu ya kwanza tayari umeshafikia asilimia 65% ambazo kwa sasa kazi ya uwezekaji inaendelea vyema licha ya changamoto ya upatikanaji wa Kifusi kuweka sawa Vyumba vya Nyumba hizo.

Alieleza kwamba Awamu ya Pili ya Mradi huo wa Ujenzi wa Nyumba za Wananchi wa Dundua inatarajia kuhusisha ujenzi wa Msikiti, Soko, Kituo cha Afya pamoja na uwekwaji wa mahitaji muhimu ya Kibinaadamu kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu Wananchi hao.

Akikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Tangi la Kuhifadhia Maji safi na salama katika Kijiji cha Kitope uliofikia asilimia 40%, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ina hamu kuona kwamba Mradi huo wa maji unamalizika kwa wakati ili kutoa huduma kama ulivyokusudiwa.

Balozi Seif alisema Sera ya Chama cha Mapinduzi iliyonadiwa kwa Wananchi wakati wa Kampeni za Uchaguzi wa Mwaka 2015 – 2020 na hatimae kupata ridhaa ya kuongoza Dola Nchini Tanzania Bara na Zanzibar iliweka wazi umuhimu wa wa Serikali kuwahudumia Wananchi katika upatikanaji wa Maji safi na salama sehemu zote Mijini na Vijijini.

Aliwataka wahandisi na wasimamizi wa Mradi huo muhimu kwa ustawi wa Jamii kuhakikisha kwamba kipindi kilichopangwa kumalizika ujenzi wake kinazingatiwa vyema ili kuwapa moyo mkubwa Wafadhili waliojitolewa kugharamia ujenzi wa Mradi huo.

Katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pia alipata wasaa wa kulikagua shamba la Muwekezaji Mzalendo la Kampuni ya Al- Zara Agriculture liliopo katika Kijiji cha Kirombero linalotarajiwa kujishughulisha na kilimo cha Biashara.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Ahmed Saleh Mbarouk alimueleza Balozi Seif kwamba mradi wao umechelewa kuanza kama ulivyokusudiwa kutokana na changamoto kadhaa zinazotokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu zinazopaswa kupata baraka kutoka kwa baadhi ya Taasisi.

Hata hivyo Bwana Ahmed alimuhakikishia Balozi Seif kwamba taratibu hizo zitakapokamilika Mradi huo wa Kilimo unaweza kuanza ndani ya kipindi kifupi kisichozidi miezi Mitatu na kutoa ajira kwa Wakaazi wanaolizunguuka eneo hilo wasiopungua Mia Mbili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuagiza Uongozi wa Wilaya ya Kaskazini “B” pamoja na Mkoa mzima wa Kaskazini Unguja kufuatilia changamoto hizo na kutafuta mbinu zitakazosaidia kuanza kwa mradi huo ulioshindwa kuanza kazi zake kwa kipindi cha Miaka Tisa sasa.
 Harakati za Ujenzi wa Tangi la Kuhifadhia Maji safi na salama katika Kijiji cha Kitope linakalosambaza Maji katika Vijiji vya Kitope Mbaleni na Vijiji jirani lililokaguliwa na Balozi Seif.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini B wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kujua changamoto zinazowakabili.
Muwekezaji Mzalendo ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Al- Zara Agriculture Bwana Ahmed Saleh Mbarouk  akimpatia maelezo Balozi Seif juu ya mradi wao wa Kilimo cha Biashara katika shamba lao liliopo Kirombero.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimaliza ziara yake Mkoa wa Kaskazini kwa kukagua Nyumba zinazojengwa kwa ajili ya Wananchi wa Kijiji cha Dundua walioamua kupisha mradi mkubwa wa ujenzi wa Gati ya Mafuta na Gesi huko Mangapwani.
  Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Wananchi wa Dundua Mhandisi Hawa Natepe akimpatia maelezo Balozi Seif hatua iliyofikiwa ya Ujenzi wa Nyumba hizo.
Picha na – OMPR – ZNZ.

MC HAMMER ALIANZA MUZIKI KWA KURAP MITAANI.

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi,Tabora.

Msanii wa muziki wa Hip hop MC Hammer, alianza safari yake katika muziki kwa kurap mitaani na katika kumbi zisizo na hadhi, kisha akakopa dola 20,000 sana na shilingi milioni 45.8 za Kitanzania, akaanzisha lebo ya Bust it Production huko Marekani.

Alizaliwa miaka 57 iliyopita, akapewa jila la Stanley Kirk Burrell, ambaye hadi sasa anakumbukwa kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kuupelekea muziki wake kukubalika na watu wakafurahia.

Aidha MC Hammer anakumbukwa kutokana na aina ya muziki aliyokuwa akiifanya nchini mwake Marekani na kutamba duniani kote.

Licha ya kuwa masanii, nyota huyo ni maarufu kwa muziki wa Hip hop, aliyewahi kuwa mnenguaji, mtayarishaji wa muziki ma mjasiriamali katika muziki.

Ni kijana miongoni mwa vijana wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika ambao walitumia muda wao mwingi kufungua na kuweka milango ya muziki kulekea katika faida kubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

MC Hammer alianza kufanya muziki mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi katikati ya 1990, wakati huo ilikuwa ngumu watu kushondwa kujitokeza kwenye shoo yake kutokana na ngoma kali ambazo alikuwa akiimba na kunengua jukwaani.

Watu walikuwa wakijazana ukumbini kumshuhudia ambapo katika kipindi hicho, haikuwa rahisi mtu kushindwa kujitokeza kwenye onyesho la ngoma zake kali.

Wakati huo ilikuwa kama umeenda disco kujirusha halafu DJ eti asipige wimbo wake, vijana wa mjini ‘wanamfanyizia’ DJ huyo.

Vijana wengi wa enzi hizo walikuwa wakimuiga sana kwa kuimba, wengine waliona ni fahari kumuiga kwa mavazi hata uchezaji wake.

MC Hammer alitamba wakati wake na vibao vikali vya U Can’t Touch This na 2 Legit 2 Quit. Vibao hivyo vilitamba na kummfanya afahamike miongoni mwa wapenda muziki duniani.

Baada ya kuwa na uwezo wa kurekodi kazi zake, MC Hammer alifanikiwa kutenganeza albamu yake ya kwanza iitwayo Feel Power ya mwaka 1986.

Albamu hiyo ilirekodiwa mwaka 1986 na kuachiwa mwaka uliofuatia wa 1987 akitumia studio yake mwenyewe, Nyingine ilikuwa ikiitwa Oaktown Records chini ya mtayarishaji Felton Pilate.

Albamu hiyo iliuza zaidi ya nakala 60,000 ka ilisambazwa na City Hall Records. MC Hammer pia aliachia singo yake iitwayo “Ring Em”, ambayo iklifanya vizuri wakati huo na kuzidi kumpa jina.

Kuanzi hapo studio kibao zikawa zinataka kufanya kazi na MC Hammer lakini yeye aliamua kuingia mkataba na studio ya Capital Records wa kurekodi albamu yake nyingine huku akikunja dola milioni 1.7 ambazo sawa na shilingi bilioni 3.9za Kitanzania.

Fedha hizo alizopata MC Hammer aliamua kuwekeza katika mambo mbalimbali ikiwemo kampuni ya mavazi mbalimbali na biashara nyingine ili aweze kujiongezea kipato mbali na muziki.

Akiwa na Capitalm Records, mwaka 1989, MC Hammer aliachia albamu ya Let’s Get It Started, iliyouza nakala million mbili huku ikiwa na vibao vikali kama Pump It Up, Turn This Murtha Out, Let’s Get Started na They Put Me in The Mix.

Baadhi ya albamu zingine za MC Hammer ni Please Hammer, Don’t Hurt ‘Em ya mwaka 1990, Too Legit to Quit ya mwaka 1991, New Venture ya mwaka 1992, The Funky Heahunter ya mwaka 1994, Inside Out ya mwaka 1995 na Too Tight ya mwaka 1996.

MC Hummer aliendelea kutoa albamu mbalimbali lakini singo yake ya mwisho aliitoa mwaka 2014, ikiitwa All in my Mind, aliyoimba na kundim lake la zamani la Oakland, wakimshirikisha Mistah F.A.B

Miaka hiyo ya 1990, MC Hammer aliigeukia dini na kuwa muhubiri wa dini ya Kikristo na kuendesha kipindi chake cha M.C. Hammer and Friends.

Aidha kuna mradi wake wa Katuni za televisheni ziitwazo Hmmerman, zilitoka mwaka 1991 na amewahi kuwa na kipindi chake cha kuzungumzia maisha kilichoitwa Hammertime mwaka 2009.

MC Hammer bado anapanda kimuziki, lakini wajuvi wa mambo wamesema hawezi kurejea katika viwango vyake vya zamani.

Mtayarishaji wa makala haya anapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200, 0713331200 na 0736331200.

GSM to address nations’ thirst for good quality furnishing

$
0
0

Dar es Salaam based GSM group of companies, is set to launch its biggest furniture store dubbed ‘GSM HOME’, aimed at addressing the existing gaps in the market in supply of wide range of good quality furniture’s.

Occupying about 1,200 square feet space, the new store is located along Mwai Kibaki road in Mikoche B area and is expected to cater for growing needs of office and home furniture in the country.

Speaking at HQ in Dar es Salaam GSM group of Companies Chief Commercial Officer Mr. Allan Chonjo said, the plan to unveil of the new store is the company’s long-time dream that will come true.

“We are very excited that soon we will launch this great store in Dar es Salaam. In addition to offering customers a convenient shopping experience, GSM HOME will have a number of contemporary furniture including shelving, sofas, sideboards, coffee tables, dining furniture, beds & bed room furniture, wardrobes & a wide range of cash N carry items everything to make your house perfect,” he said.

Chonjo added “And for the Office, we have a large selection of fabulous office furniture including reception area, waiting area, chairs, ergonomics, tables, conferences, workstations, storage and filing cabinets,”

The CCO noted that, the contemporary furniture collections which will be found at GSM HOME are carefully chosen for value and practicality as well as design; with the ethos that good design must work as well as being great to look at adding that a considerable amount of time has been spent looking for just the right.

He urged people to be prepared to visit the new store shortly after the lunch which will be this month and enjoy new furniture shopping experience adding that the store has everything to cater for their furniture needs.

“When choosing furniture, it’s important to pick timeless, functional pieces that fit your space and budget! Choose from contemporary and modern, traditional or a bit of both in a unique eclectic mix – there are no rules, so don’t be afraid to get creative and buy furniture you love,” he said.

We have launched our two shops in Mlimani City as well as Pugu Mall, and this 3rd one will be our iconic version aimed at driving user experience. We have packages for both individuals as well as corporate clients – with facilities to pay by card so you don’t have to carry a lot of cash with you for security purpose.

ASHA BARAKA ASIYESITA KUTHUBUTU

$
0
0

Na: Kiyungi Moshy.Tabora.

Novemba, 2019

Asha Baraka ni mwanamke wa mfano wa kuingwa kwa ujasiri wa kuthubutu kufanya jambo, akafanikiwa.

Amejaaliwa kuwa na talanta lukuki ambazo kwa kauli yake anasema zingine bado hajazionesha.

Baadhi ya vipaji vyake hivyo vilianza kujitokeza akiwa katika shule ya sekondari ya Wasichana Tabora, alipokuwa katika mchezo mpira wa Pete na kikapu, iliyomfikisha kuchaguliwa timu ya shule.

Umahiri wake katika michezo hiyo, Asha alichaguliwa kuwa mmoja kati ya wanafunzi waliounda timu ya UMISETA mkoani Tabora.

Akiieleza historia ya maisha yake, Asha alisema kuwa alizaliwa katika kijiji cha Mwandiga, kilichopo katika Wilaya Kigoma Vijijini, Mkoani Kigoma.

Masomo yake ya msingi aliyapata katika shule mbili tofauti. Darasa la kwanza hadi la tatu alisoma katika shule ya msingi Kipampa iliyopo Ujiji, mjini Kigoma.

Baba yake Mzee Ramadhani Baraka alikuwa Daktari hivyo alihamishwa kwenda kufanya kazi katika hospitali nyingine ya Nguruka, mkoani humo.

Asha alilazimika kuandamana na wazazi wake kwenda Nguruka, akiwemo mama yake mzazi, maliyemtaja kwa jina maarufu la Mama Ali Baraka.

Alisoma katika shule ya msingi Nguruka darasa la nne hadi alipofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Asha Baraka alikuwa ‘Kichwa’ kweli kweli darasani, alifaulu mtihani wa darasa la saba, akachaguliwa kwenda kusoma katika shule ya sekondari ya vipaji maalum ya Tabora Girls, iliyopo mjini Tabora.

Akiwa shuleni hapo alicheza mpira wa pete na kikapu hatimaye alichaguliwa kuwakilisha mkoa huo, akiwa katika timu ya mpira wa Pete.

Licha ya kucheza mchezo wa Pete na kikapu, Asha Baraka alikuwa mwanariadha mashuhuri akikimbia mbio za mita 100, na kuwa kati ya mwanamichezo bora shuleni hapo.

Alipomaliza masomo ya sekondari mwanzoni mwa miaka ya 1980, aliajirawa katika Shirika la Bima la Taifa (NIC) la jijini Dar es Salaam katika Idara ya mauzo na masoko.

Asha ni mama mwenye familia ya mume na watoto wawili wa kiume. Aliwataja kwa majina kuwa ni Mope mwenye umri wa miaka 25 sasa, ambaye alisema amefuata nyayo zake za uhezaji wa mpira wa kikapu.

Aliwahi kuchaguliwa katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18. Mwingine ni Imani mwenye umri wa miaka 20.

Asha licha ya majukumu yake ya kazi, pia alikuwa akijishughulisha na uongozi wa kundi la vijana waisopungua 45, katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’

Miaka ya nyuma kulikuwa na mipango mzuri ambapo baadhi ya mashirika ya umma yalikuwa na vikundi vya burudani za ngoma za asili, dansi na michezo.

Shirika la Bima la Taifa lilikuwa mojawapo ambalo lilikuwa na timu ya mpira wa pete halakadharika ilikuwa na bendi ya Bima Lee Orchestra.

Asha Baraka alicheza mpira wa pete na kikapu katika timu ya Bima, pia alichaguliwa katika timu ya wilaya hadi ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kipaji kigine cha mama huyo ni kile cha kuchaguliwa katika timu ya ya taifa ya riadha. Enzi zake alikuwa akikimbia mbio za mita 100.

Wakiwa kambini mjini Arusha wakati huo, kulifanyika mchujo, naye akawa miongozi walioondolewa katika timu hiyo.

“ Siwezi kumshau Juma Ikangaa ambaye aliniletea viatu mahsusi kwa ajili ya kukimbilia (Sparks) toa Japan. Kabla ya hapo, nilikuwa ninakimbia nikiwa na viatu vya raba” alisema Asha Baraka.

Alitolea mfano wa mwanariadha wa zamani ambaye aliyepata mafanikio makubwa licha ya kutokuwa na zana, Mwinga Mwanjala.Mwanjala alishinda mashindano ya kitaifa ikikimbia bila viatu ‘Pekupeku’

Asha alibaisha kwamba hata kuchaguliwa kwake kukimbiza mwenge wa Olympic, haukufanyika kwa upendeleo, anasema yeye ni mwanariadha wa siku nyingi mwenye rekodi kitaifa.

Kama nilivyokueleza hapo awali kuwa Asha ana vipaji vingi mno, alionyesha maajabu baada ya kuendesha gari akiwa na umri mdogo wa miaka 14, wakati huo alikuwa kidato cha pili hapo Tabora Girls.

Alieleza kwamba hata alipoanza kazi Shirika la Bima, watu wengi wakiwemo wafanyakazi wenzake, walikuwa wakimshangaa kumuona binti mdogo wakati huo akiendesha ‘mkoko’ kuja kazini.

Mama Asha kupitia uzoefu wake wa muda mrefu wa kuendesha magari, aliwahi kupatwa na shauku ya kushindana katika mbio za magari hapa Tanzania.

Asha alikosa gari maalumu la mashindano hayo, licha ya kufanya mazoezi makali kupitia maeneo mbalimbali hadi Chalinze.

“Nilikuwa napenda sana kuendesha magari, nilifanya mazoezi ya kushindana nikapitia maeneo mengi hadi Chalinze. Anajisifu Asha Baraka.

Analisema kwamba Pamoja na kukosa gari, alijichomeka katika katika gari la wasindikizaji na kuweza kuzunguka toka mwanzo wa safari hadi mwisho wa mashindano hayo.

Ujasiri wa mama Asha ulionekana mwaka 2010, baada ya kuacha kazi yake nzuri katika Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kuamua kujikita katika Biashara na Siasa.

Shirika la Bima la Taifa mwaka 2000, liliwataka waajiriwa wote kuomba kazi upya. Japo yeye alikuwa nje ya mji kikazi wakati huo, lakini aliporejea hakutaka kuendelea na kazi, hivyo akaamua kutoandika barua ya maombi ya kazi hatimaye akacha kazi rasmi 2010.

Asha baada ya kuacha kazi Shirika la Bima la Taifa (NIC) aliamua kujikita katika Biashara na Siasa.

Kwa upande Siasa, Asha Baraka hivi sasa ni mjume wa National Executive Committee (NEC) kupitia wilaya mpya ya Uvinza, iliyopo mkoani Kigoma.

Anajuvunia kuwa karibu na wanamuziki wake wa African Stars, wana ‘Twanga Pepeta’ kwa kuwa anapata muda wa kuzungumza na kuelewa matatizo yanayoikabiri bendi sanjari kujua mafanikio.

Historia inaeleza kwamba kabla ya kuwa kampuni African Stars Entertainment Tanzania (ASET), kulikuwa na bendi ya African Stars iliyoanza mnamo tarehe 01 July 1994, katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Baadaye bendi za M.K.Group, M.K. Beat na M.K. Sound zikaanzishwa na Alli Baraka, aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Zambia (Zambia Airways).

Baadaye akawachia uongozi nduguze Msilwa Baraka, aliyekuwa Mwenyekiti na Asha Baraka akawa Mkurugenzi Mtendaji.

Kampuni ya African Stars Entertaiment Tanzania (ASET) iliyoasisiwa mwaka 2000 , Asha akawa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.

Kufuatia juhudi za kuongoza kwa umakini mkubwa kundi la vijana wa kiumena kike pasipo kuteteleka, walimpachika jina bandia la ‘Iron Lady’

Alijinasibu kuwa ASET ni mithiri ya Chuo ambacho kinatengeneza vipaji kwa vijana, kisha kuwaruhusu kwenda popote wanapohitajika pasipo masharti.

“Tuna Academy ya kuendeleza vipaji vya vijana, inayoitwa Twanga Pepeta Academy.

Vijana hao walikuwa wakipewa nafasi ya kupiga muziki siku za Jumamosi pale Mango Garden, kabla haijavunjwa wakapiga muziki wao, baadaye bendi African Stars ‘Wana Twanga Pepeta’ kupanda jukwaani” Alisema Iron Lady.

Akiyaelezea mafanikio katika kampuni yake ya ASET, Asha alisema ni makubwa sana licha ya kuwa wana Academy, pia ina wanamuziki wa kuingia na kutoka wapatao 45.

Vilevile wamekwisha tunukiwa tuzo kibao zikiwemo za BBC, BASATA, ile Mascut huko Arabuni ambako kulifanyika festival.

ASET imekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii katika matatizo mbalimbali ya kijamii.

Mojawapo ni lile la Iron Lady Asha Baraka kuandaa onesho maalum la muziki ambalo pesa zilizopatika hapo, alizikabidhi kwa aliyekuwa mwanamuziki mkongwe Maalim Gurumo ambaye hali yake ya kiafya ilikuwa tete, kabla ya kifo chake.

Mwaka 2000 wakati wa shindano la Tanzania Musical Awards, The African Stars Band, ilifanikiwa kuwa bora ya mwaka kwa mwaka 2000/2002. Wimbo wa Kisa cha Mpemba ukawa ndiyo mwibo bora namba mbili.

Asha Baraka ni mmoja wa viongozi wa klabu ya Simba yenye makao yake makuu Msimbazi jiijini Dar es Salaam. 

‘Iron Lady’ Asha Baraka mwaka 2019 aling’atuka akamkabidhi Luiza Mbutu wadhifa wa kuongoza bendi African Stars ‘Twanga Pepeta, baada ya Asha Baraka ‘Iron Lady’ kung’atuka.

Kabla ya kupewa nafasi hiyo, Mbutu alikuwa Katibu wa bendi ambaye amedumu katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kwa zaidi ya miaka 20.


Kila la heri Iron Lady Asha Baraka.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba: 0784331200, 0713331200, 0767331200 na 0736331200.

Bunge labariki kujipima VVU Mwenyewe

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha sheria ya mtu kujipima virusi vya UKIMWI mwenyewe.

'Sheria hiyo itamruhusu mtu kujipima mwenyewe kwani Maambukizi mapya yamehamia kwa vijana’

Leo Novemba 12, 209 Bunge limepitisha Sheria hiyo ambayo inampa  mamlaka kwa mtu kujipima Virusi vya UKIMWI mwenyewe.

Sheria hiyo, Itaruhusu mtu yeyote kuanzia miaka 15 na kuendelea kujipima mwenyewe jambo ambalo awali lilikuwa linafanyika kwenye vituo vya afya pekee.

Naibu Waziri wa Afya, Faustine Ndugulile amesema Sheria hiyo itasadia watu wengi hususani wenye uoga wa kwenda vituo vya afya kujipima wenyewe na kwa urahisi.

Ndugulile amesema kuwa kwa sasa kundi linaloongoza kwa maambukizi mapya ya VVU ni vijana ambapo wasichana ndio wanaoongoza kwa asilimia kubwa huku wanaume wakitajwa kuwa kundi linaloongoza kuogopa kupima virusi vya UKIMWI.

"Katika asilimia 40 ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi ni vijana, na katika hiyo asilimia 80 ni wasichana kwahiyo tumeona mfumo huu utasaidia sana kwa mtu kutambua afya yake," amesema

Ndungulile amesema, "tumeshapitisha sheria tunasubiri Rais asaini na na mchakato huo unaweza kufika January 2020 na utakapopitishwa vifaa hivyo vitapatikana katika maduka ya madawa,"

" Mtu hatahitajitaki kutumia damu, ila sampuli zitakazotumika ni mate na pindi mtu atakapoenda kuchukua kipimo katika duka la dawa atapatiwa ushauri nasaha na maelekezo ya namna ya kukitumia  kikubwa ni kumbukumbu ya majibu atakayoyapata," 

Sheria hiyo  itaanza kutumia pindi Rais atakapoipitisha.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images