Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

Viwanja vya Ndege Tanzania kutumika majira yote ya mwaka

$
0
0


Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bahati Mollel leo akiwakaribisha waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) kusikiliza Mafanikio yaliyofikiwa na TAAkwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa naRais Dkt John Pombe Magufuli katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa chaJulius Nyerere (JNICC).
Kaimu Mwanasheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Pamela Mugarula akizungumzia muundo na kazi za TAA mbele ya
waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) leo wakati Mamlaka hiyo ilipozungumzia Mafanikio iliyofikia kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Mbila Mdemu
akizungumzia mafanikio ya TAA kwa kipindi cha Miaka minne ya Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli, katika
mkutano na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Meneja wa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Asteria Mushi (kulia) leo akizungumzia ongezeko la
mapato kwenye Viwanja vya ndege mbele ya waandishi wa habari wakati
Mamlaka hiyo ilipoelezea mafanikio yake kwa kipindi cha miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

*************************************

Na Bahati Mollel,TAA

VIWANJA vya Ndege Tanzania sasa vinaweza kutumika majira yote ya mwaka ya masika na kiangazi kutokana vingi barabara zake za kutua na kuruka ndege kujengwa kwa kiwango cha lami, imeelezwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu ametoa maelezo hayo leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), alipozungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakati alipozungumzia mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhandisi Mdemu amesema Mamlaka inajivunia mafanikio ya kuwa na viwanja 16 vyenye barabara za kutua na kuruka ndege za kiwango cha lami, ambazo zinaruhusu kutumika kwa kipindi chote cha mwaka bila matatizo ya aina yeyote.

Viwanja hivyo ni Arusha, Tabora, Mwanza, Bukoba, Mafia, Iringa, Songwe, Tanga, Moshi, Songwe, Kigoma, Dodoma, Mtwara, Mpanda pamoja Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA).

“Tangu kuanzishwa Mamlaka vilikuwepo viwanja nane pekee vyenye viwango vya lami, lakini sasa mpaka Novemba mwaka 2015 tumeweza kuongeza na kufikisha 16 ambavyo vinapitika kwa uhakika zaidi katika majira yote ya mwaka ya kiangazi na masika,” amesema Mhandisi Mdemu.

Mbali na barabara za kutua na kuruka ndege, pia Mamlaka hiyo imefanikiwa kufanya ukarabati na upanuzi wa majengo ya abiria na kufanikisha kuweza kuhudumia abiria wengi zaidi ya wa awali, ambapo ni pamoja na jengo la tatu la abiria la JNIA, Bukoba, Dodoma, Iringa, Mpanda, Mtwara na Mwanza.

Pia Mhandisi Mdemu amesema mafanikio mengine ni kuboresha ulinzi wa kutosha wa abiria na mizigo, kwa kufungwa kamera za kufuatilia matukio, kuwepo kwa mashine za kukagua abiria na mizigo na kujengwa kwa uzio kwenye baadhi ya viwanja,; pia kumefungwa mifumo ya kisasa ya kiyoyozi; na kuanza kusimikwa kwa taa za kuongoza ndege ili ziweze kutua usiku.

Naye Meneja Mipango na Takwimu wa TAA, Asteria Mushi amesema kuwa Mamlaka imeweza kupata mafanikio kwa kuongeza mapato kutoka Tshs. Bil. 63 kwa mwaka 2015 na kufikia Bil. 105 kwa mwaka 2018, ambazo ni ongezeko la asilimia 66, ambapo lengo la Mamlaka ni kuongeza mapato na kufikia Tshs. Bil. 130 ifikapo mwaka 2020; pia wameweza kuongeza biashara za maduka na sasa serikali wanashirikiana na taasisi binafsi kujenga hoteli ya nyota nne yenye ghorofa nane (8) itakayojengwa karibu na jengo la pili la abiria (JNIA-TBII).

Hali kadhalika Mushi, amesema Mamlaka imeongeza idadi ya ndege za abiria ambazo awali zilikuwa zikifanya safari nchini, lakini baadaye zikasitisha na zimeanza tena safari hizo, ambazo ni Air Uganda na Zimbabwe. Ndege hizo zinafanya idadi ya ndege za nje kufikia 21.

“Katika viwanja vya ndege tumetenga asilimia 30 kwenye majengo ya abiria tumetenga huduma za abiria na biashara, lakini tunaangalia na ongezeko la ndege za Air Tanzania ambapo sasa zinakwenda njia 10 za ndani ya nchi na njia tano za kimataifa,” amesema Mushi.

Article 1

$
0
0



Na Mwandishi wetu Mihambwe

Hatimaye Bibi Somoye Dadi Dabali aliyekuwa akidai shamba lake kwa muda imeamuliwa leo arejeshewe shamba lake alilochukuliwa na Mjukuu wake Sofina Salum Said Liuma. 

Maamuzi hayo yamefanywa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu mara baada ya kuzikutanisha pande zote za mshtaki, mshatakiwa na mashahidi wao na kuridhishwa Bibi Somoye apewe ardhi hiyo ambayo alimpa Mjukuu wake huyo alime Mihogo kwa muda naye Mjukuu Sofina akaamua kupanda Mikorosho ambayo ina mwaka mmoja sasa wakati ambao Bibi Somoye alikuwa anaumwa.

Baadae Mjukuu Sofina alitaka kumlipa Tsh. Laki sita Bibi yake huyo Somoye ili amwachie shamba naye Bibi akakataa na kusema Sofina arudishe shamba lake na hahitaji hela yake kwani ameonyesha utovu wa nidhamu wa kutaka kumdhulumu shamba.

*”Nimesikiliza pande zote vizuri na leo ninaamuru Sofina kurejesha ardhi ya Bibi Somoye na isitokee Bibi huyo kusumbuliwa kwa namna yeyote ile. Kuanzia sasa Shamba liwe mikononi mwa Bibi Somoye”* Alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika hatua za kusikiliza kesi hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata Miuta, Mtendaji Kijiji cha Ng’ongolo lililo shamba hilo, Mashahidi pamoja na Wajumbe wa Baraza la ardhi la Kata.

MCHANGO WA MBUNGE WA KAHAMA MJINI KUTAKA WATOTO WANAOKATAA KUTOA FEDHA KUSAIDIA WAZAZI WAO WASHTAKIWE WENGI WAUUNGA MKONO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
BAADA ya Mbunge wa Kahama Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jumanne Kishimba, kutoa mchango wake bungeni wa kuitaka Serikali kupeleka muswada bungeni utakaomwezesha mzazi kumshtaki mtoto ambaye anakataa kumpatia fedha wala kupokea simu yake wakati , umeibua mjadala mkubwa ndani ya jamii, ambapo baadhi ya wazazi na walezi wameunga mkono mapendekezo yake na kuomba yafanyiwe kazi.

Mbunge Kishimba wakati anachangia Bungeni hoja ya elimu katika mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021, amesema kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto,ipeleke muswada bungeni utakaomwezesha mzazi kumshtaki mtoto ambaye anakataa kumpatia fedha wala kupokea simu ya mzazi wake.

Wakati anajenga hoja yake katika hilo Kishimba alisema kuwa mzazi au mlezi ambaye hamsomeshi mtoto wake iko sheria ya kushitakiwa kwa kutotimiza wajibu wake wa kusomesha mtoto lakini hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kumshtaki mtoto ambaye ameshindwa kumsaidia fedha mzazi wake au hata kupokea simu, hivyo ameshauri Serikali kuangalia kwa kina suala hilo ili kuwepo na sheria inayotpa nafasi mzazi kumshitaki mtoto asiyesaidia wazazi ambao walitumia fedha nyingi kumlea na kumsomesha tena wengine kwa wazazi kuuza mifugo yao.

Alipokuwa akitoa mchango wake huo wabunge mbalimbali walionekana kufurahishwa kwa kutoa vicheko .Hata hivyo Kishimba alibaki akisimamia hoja yake. 

Akizungumza kuhusu mchango wa mbunge huyo, Damian John (62) amesema amemfuatilia mbunge huyo na mchango na kubaini ana hoja inayoeleweka na hivyo kina kila sababu ya kuiunga mkono na kwamba wabunge wenye mawazo kama ya Kishimb, ndiyo wanaotakiwa kwa sasa kwa sababu wanalenga kupatia ufumbuzi matatizo yanayoikabili jamii.

Ameseam kuna watoto wengi ambao wamesomeshwa na wazazi kwa shida na kujinyima, lakini wanapopata kazi wanajichimbia mijini bila kujua wazazi wao wanaishije vijijini.

Kwa upande wake Adelina Damian (55),yeye amesema amewapongeza wananchi wa Kahama kumpata kiongozi imara, anayejua matatizo ya wananchi na kwamba amekuwa akifuatilia michango yake Bungeni, ni mtu ambaye ana mawazo ya kusaidia maendeleo ya taifa.

"Itakuwa ni jambo la kushangaza iwapo wananchi wa Kahama hawatamchagua tena Kishimba ili kuwaingoza kwenye uchaguzi wa 2020. Kama watoto wangetimiza majukumu yao hata TASAF isingekuwepo," alisema na kuwataka wananchi wa Kahama wasifanye makosa wakati uchaguzi ujao.

Kwa kukumbusha zaidi Kishimba wakati anazungumza bungeni alisema: "Unakuta wazee kijijini wanahangaika na TASAF (mpango wa kunusuru kaya masikini), lakini mtoto ana maisha mazuri Dar es Salaam kila siku anafanya siku ya kuzaliwa,"alisema Kishinmba na kuongeza.Mbona Serikali mwanafunzi anapofikisha kidato cha sita humpatia mkopo wenye riba anaolazimika kuulipa akianza kazi. 

"Mimi nina kosa gani kumdai mwanangu? Kwanini wazazi tujiandae kulalamika na kutoa radhi? Kwanini Serikali isitusaidie? Mwanasheria Mkuu wa Serikali uko hapa. Mwanangu nimemtunza, nimemsomesha kwa nini nijiandae kuja kutoa radhi? Anatakiwa kunisaidia. Niruhusiwe kama hakutoa fedha, hakupokea simu, mimi niende polisi nikamshtaki." Wakati wa mchango wake huo, Kishimba alikuwa akishangiliwa na wabunge wakuonekana kuafikiana naye.

Kishimba ambaye kwenye mchango wake alijikita kwenye suala la elimu, alisema hatuwezi kuondoa elimu ndani ya maendeleo, lazima twende nayo. Kishimba kwenye mchango wake, alijipambanua kwamba anasimama sehemu ya elimu peke yake.

Alisema suala la ajira tusielekeze kuitupia lawama peke yake, lazima tutafute ufumbuzi ambao unaweza kusaidia kuipunguza angalau kwa nusu au kuimaliza kabisa.Kabla ya kuzama kwenye jambo hilo, Kishimba alisema ataanza na utaratibu wa chini wa watoto kwenda shule abusuhi. "Kama hatuna nafasi za kazi ni vizuri tumuombe Waziri wa Elimu, afikirie upya utaratibu huo hasa kwa watu ambao ni wakulima, wafugaji, wafanyabishara ndogo ndogo," alisema Kishimba na kuongeza;

"Watoto wetu wanaondoka asubuhi saa 12 kwenda shule, wanaanza kukimbia mchakamchaka hadi saa 3, hadi kuja kuanza masomo ni saa nne, kwa nini wasiende shule saa tano wakiwa wamefanyakazi nyumbani ambazo tunatarajia kuwarudisha huko wakimaliza vyuo vikuu mheshimiwa Mwenyekiti?"

Alisema kwa kufanya hivyo watakuwa wamefanyakazi nyumbani hadi saa tano asubuhi, watarudi kutoka shuleni saa 10 hadi 11. Kwa mujibu wa Kishimba utaratibu wa watoto kwenda shule asubuhi ni wa nchi za Uingereza, Ulaya na nyinginezo.

Alitoa mfano kwamba nchi za Ulaya bwana na bibi wanafanyakazi, wanaondoka na watoto wao wanawaacha shule, wanaporudi wanawapitia.

"Kule Ulaya kuna tishio la barafu, inaweza kupiga London ukawa hauwezi kurudi nyumbani, kwa hiyo kumuacha mtoto nyumbani ni hatari, lakini kwa Ulaya kule nyumbani hakuna kazi zozote za kufanya, lakini sisi tunazo kazi nyingi za kufanya, kwa nini watoto wetu wasiende shuleni saa 5 hadi saa 6, wakiwa wamefanyakazi?

Leo hii tuna watoto wa shule za msingi za kutwa milioni 4 hadi tano, wakifanyakazi nyumbani kwa kuzalisha kilo moja moja ya mahindi, mtama au mpunga, tutakuwa tumeinua uchumi wetu kwa kiwango cha juu, lakini pia watakuwa wamepata elimu ya kutosha, hivyo watakapomaliza vyuo vikuu na tukawalazimisha wajitegemee hawatakuwa na tatizo lolote la kurudi kijijini."

Katika suala lake la pili, Kishimba alizungumzia watoro wa wanafunzi, akisema utafiti na uzoefu walionao, watoro ndiyo watu waliofanikiwa katika maisha.Hivyo alihoji kwa nini Wizara ya Elimu isianzishe mtaala wa watoto watoro na watu wazuri (wasiokuwa watoro).

"Kuna ubaya gani wa kuwa na mtaala wa watoro watakaofundishwa na watu waliokuwa watoro, ambao wameonesha mafanikio?"Alihoji.
Alitoa mfano akisema aliyevumbua Amerika hakuwa msomi, bali alikuwa kwenye safari zake kwenda India, alipopotea alijibuta Amerika, ndipo akawa amevumbua Amerika kwa kwamba sasa wote tunakwenda kuomba pesa Amerika?

"Leo hii tunashuhudia watu wakubwa wakifanya mambo makubwa, leo tuna wana michezo, wana muziki, bahati nzuri na humu ndani (bungeni) tuna zaidi ya wabunge 50 watoro, lakini wana mafanikio makubwa sana, kwa ridhaa yako kama utakubali nitaje hata 10," alisema.

Hata hivyo, alikatishwa na taarifa iliyotoka kwa mbunge wa Itilima (CCM), Njalu Siyanga aliyesema Kishimba naye hakumaliza shule ya msingi, lakini alifanikiwa sana kuchenjua dhahabu na mwaka 1992, alianzisha ununuzi wa pamba hapa nchini.

Akijibu taarifa hiyo, Kishimba alikiri kuwa hakumaliza shule ya msingi na kwamba aliishia darasa la nne, alielewa kitu wanachofundisha kina faida maeneo fulani.

"Mimi nimeishia darasa la nne nikagundua ndani ya elimu kuna faida fulani, kwa nini mzazi wangu na mimi tukamatwe kurudishwa shuleni? Tuendelee miaka 20 isiyokuwa na faida?" Alihoji na kuongeza kwamba utaratibu wote huo ambao wanahangaika nao ni wa Ulaya. Alisema katika suala la elimu ni lazima wizara ifanye utafiti kwa vitu vingi. 

"Leo hii kuna Watanzania zaidi ya milioni 10 wanaomiliki simu, lakini VETA haina mtaala wa kutengeneza simu, leo hii kuna biashara nyingi za madalali zimepatikana, lakini hatuna mtaala wa madalali, wapo mtaani na wanaendesha shughuli zao, lakini VETA vitu walivyog'ang'ania havipo," alisema.

Pamoja na wananchi kadhaa kuunga mkono mchango huo, pia video inayoonesha Kishimba akichangia Bungeni imeonekana kusambaa katika makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii yakiwemo makundi ambayo yanahusisha masuala ya familia.Walio wengi kwenye makundi hayo ya kijamii yaliyoko katika mitandao ya kijamii nao wameonekana kumpongeza na kumuunga mkono.

DIRA YA DUNIA JUMATATU 11.11.2019

ATHARI ZA MFUMO DUME KWENYE JAMII NI KUBWA-TGNP

$
0
0
 OFISA Programu na Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za jinsia kushoto ni Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John 
 Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo kulia ni Amina Omari wa gazeti la Mtanzania kushoto ni Khadija Baragasha wa EATV na Majira  na George Sembony wa gazeti la Citizen mkoa wa Tanga

Sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo kulia ni Rais Saidi wa Gazeti la Mwananchi akiwa na waandishi wengine wa mkoa huo.


ATHARI za mfumo dume kwenye jamii  ni kubwa sana kutokana na kwamba unagusa maeneo mengi ya kichumi, kijamii upatikanaji wa huduma za jamii huku akieleza jamii inatakiwa kutambua kwamba eneo ambalo kuna hali hiyo hata maendeleo yatachelewa kupatikana.


Hayo yalisemwa na OFISA Programu na Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za jinsia ambapo alisema  sababu mfumo unaathiri uchumi na kupelekea maendeleo kushindwa kupatikana .


Akitolea mfano pale wanawake wanapohitaji nafasi ya kushiriki kwenye uchumi unakuta mfumo unaonyesha wanawake hawatakiwi kufanya hivyo na badala yake wanakaa nyumbani kwa hiyo wanapookaa nyumbani kwenye eneo la uchumi umaskini unaendelela kwa sababu wanaamini wanawake wapo wengi zaidi ya asilimia 50 hivyo wanaposhiriki kwenye suala la uzalishaji mali wanaongeza kipato cha familia na Taifa kwa ujumla.


“Hivyo lazima jamii ibadilike na kuacha na mfumo dume ambao umekuwa kikwazo kikubwa cha uchelewashaji wa maendeleo hivyo badala yake waweze kutoa nafasi kwa lengo la kuoindosha hali ya namna hiyo “Alisema


Hata hivyo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye chaguzi hizo zijazo wanawake popote walipo waone hiyo ni nafasi ya kujitokeza na wafahamu michakato na namna ya kuchukua fomu na kujiandaa kwa ushiriki wao.


“Tuna nafasi kubwa ya kushiriki kwenye uchaguzi hizo zijazo na kushiriki kwa sababu tunaona jinsi Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu anavyotuongoza vizuri inawezekana mwanamke akawa Rais na nchi ikaendelea vizuri kwa sababu ni waadilifu na wachapa kazi “Alisema.


Naye kwa upande wake Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John alisema kwamba mfumo dume ni mfumo uliopo kwenye jamii na wakati mwengine inatokana na nguvu aliyokuwa nayo mtu katika hali ya kumiliki rasilimali kutoa maamuzi.


Alisema sehemu kubwa kwenye jamii mfumo dume unasababishwa na wanaume wamekuwa wakinyima sauti wanawake katika kuongeza vitu na hata kumiliki rasiliamali lakini pia upo kwenye pande mbili kutokana na kwamba mwisho ya siku unaweza kuathiri pande zote mbili.

RC SINGIDA DKT NCHIMBI ASHAURI JESHI LA POLISI KUANZISHA DAWATI LA UPIMAJI MACHO

$
0
0
Mtaalamu wa macho kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Sight Saver akimwelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi wakati akimpima macho katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani uliofanyika mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovick. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi , akipuliza kifaa cha utambuzi wa kilevi kwa dereva aliyekunywa pombe. Kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt. Angelina Lutambi. 
Wananchi wakisubiri kupima macho kwenye maadhimisho hayo.
Uandikishaji majina kabla ya kupima macho ukifanyika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi , akipata maelezo alipotembelea banda la Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Singida kwenye maadhimisho hayo.
Uandikishaji majina kabla ya kupima macho ukifanyika.
Mtaalamu wa macho kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Sight Saver akimpima macho mwananchi 
Mwanahabari wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Mkoa wa Singida, Leonard Manga akisoma maandishi kabla ya kupimwa macho.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi, akizungumza kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida kwenye maadhimisho hayo, Afande Mwakalukwa.


Na Waandishi Wetu, Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi, ameshauri Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo chake cha usalama barabarani kuanzisha ‘dawati maalumu’ la upimaji wa afya ya macho ili kupunguza ajali zitokanazo na uoni hafifu.

Dkt. Nchimbi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mkoani hapa wakati wa zoezi la upimaji macho linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserkali la Sightsavers, linalokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya Usalama Barabarani.

“Kati ya dawati ambalo mnatakiwa kuwa nalo kwa sasa ni hili la afya ya macho, niwasihi shirikianeni na wataalamu wa macho nendeni mkafanye kampeni kubwa ya afya ya macho…himizeni, tuhimizeni ninyi mkisema jamii itawaelewa na ajali zote zinazotokana na tatizo hili la uoni hafifu zitapungua,” alisema Nchimbi.

Alisema, tunapoadhimisha wiki ya usalama barabarani tusisahau kuwa afya ya macho ni kati ya kipengele na mhimili muhimu katika suala zima la usalama barabarani hapa nchini.

Alieleza kuwa, endapo kila mtumiaji wa barabara atapatiwa huduma stahiki ya afya ya macho basi ni dhahiri atakuwa mwangalifu, makini na hatimaye kuweza kupiga hesabu zinazotakiwa awapo barabarani.

Akifafanua umuhimu wa uwapo wa dawati hilo la upimaji macho, alisema iwapo mtumiaji wa barabara anakabiliwa na tatizo la macho, mathalani wakati fulani badala ya kuona gari moja anajikuta anaona mawili au kwasababu huna uoni wa mbali una uoni wa karibu ukafikiri gari lipo karibu kumbe lipo mbali au kinyume chake, matokeo yake ni mfululizo wa matukio ya ajali kila kukicha.

Alisema wakati mwingine mtu yupo pembeni ya barabara lakini badala ya kusubiri anaamua kukatisha barabara akiamini chombo cha moto kilicho kulia kwake au kushoto bado kipo mbali-alisema yote hayo ni matokeo ya matatizo ya afya ya macho ambayo kwa pamoja jeshi la polisi na jamii ikiamua tatizo hilo litamalizika.

Dkt, Nchimbi aliongeza kuwa suala la usalama barabarani halimanishi wale wanaoendesha vyombo vya moto pekee bali ni kwa watumiaji wote wa barabara husika, ikiwemo watembea kwa miguu, na kuhimiza kila mtu anapaswa kuchukua tahadhari wakati wote.

“Mtumiaji wa barabara unapokuwa barabarani hakikisha kwanza macho yako yapo sawasawa, pia unapaswa kuwa wewe mwenyewe ni dereva unayejiendesha, lakini muendeshe pia na mwenzako aliye kushoto kwako, kulia kwako na nyuma yako…hii iwe kwa wote ikiwemo waendesha bodaboda, baiskeli, bajaji, wafugaji, na vyombo vingine vya moto ili tuweze kumaliza kabisa ajali hizi zinazoweza kuepukika,” alisema.

EMANUEL GEKA KINARA WA MAGOLI KIDAMALI FC

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya Kidamali inayoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa maarufu kama ASAS SUPER LEAGUE  ambapo mchezaji wa timu hii Emanuel Geka anaongoza kwa ufungaji wa magoli hukupia timu ya kidamali ikiwa imefuzu hatua ya nane bora ya ASAS SUPER LEAGUE 
 Wachezaji wa timu ya Kidamali inayoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa maarufu kama ASAS SUPER LEAGUE  ambapo mchezaji wa timu hii Riziki Kelvin anaongoza kwa ufungaji wa magoli huku pia timu ya Isiman ikiwa imefuzu hatua ya nane bora ya ASAS SUPER LEAGUE 

Na Fredy Mgunda, Iringa 
WACHEZAJI nane kutoka timu za Mafinga Academy,Kidamali fc,Kalinga Fc,Isimani Fc, Mapanda Fc na Irole fc wanafukuzia tuzo ya mfungaji bora wa mashindano ya kugombea kombe la bingwa wa mkoa yanajulikana kwa jina la Asas Super League 2019 (ASL 2019).


Wachezaji hao vinara Emanuel Geka wa Kidamali anamagoli 8, Luka Duma (Irole fc) na Riziki Kelvin wa Isimani Fc wana magoli 7 kila mmoja Baraka Athumani kutoka Mafinga Academy na Vicent Madembo (Mapanda Fc) kila mmoja wana goli 5, Kelvin Msafiri (Kalinga Fc),Conrodgers (Irole Fc)na Mohamed Rashid (Isimani fc) wameonyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu ambapo hadi sasa kila mmoja amefanikiwa kufunga magoli 4 katika michezo waliyocheza.


 Licha ya ushindani mkali katika mashindano hayo katika ufungaji mchezaji wa Kidamali fc Emanuel Geka anakimbizwa kwa karibu na mchezaji Riziki Kelvin wa Ismani ambaye anamagoli saba na alikuwa mfungaji bora msimu uliopita.


Mchezaji wa Kidamali fc Emanuel Geka amefunga magoli mengi akiwa katika uwanja wa kidamali tofauti na akiwa anacheza nje ya uwanja wao wa nyumbani hivyo amekuwa mmoja ya wachezaji ambao wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani kufumania nyavu za wapinzani.


Katika mashindano hayo hadi sasa timu ya soka ya Irole Fc ndio kinara wa magoli mengi kwa kuwa na magoli 18 katika michezo 7 iliyocheza ikifatiwa na timu ya soka ya Isiman Fc yenye mabao 17 huku Kidamali Fc wakiwa na mabao 13 na hizi timuzote zinatoka katika kundi B na zimefuzu hatua ya nane bora ya Asas Super League.


 Timu za Acosato ndio timu iliyoruhusu magoli mengi kwenye michezo yao kwa kufungwa goli 15 huku ikifuatiwa na timu ya African wonders ambao wamefungwa magoli 14 huku zikifuatiwa na Magulilwa na mapanda fc ambazo zote zimefungwa magoli 12 kila. 


Aidha ligi hiyo hadi kufikia sasa jumla ya magoli 170 yamefungwa na timu zote zinazoshiriki ligi ya Asas Super League msimu wa 2019/2020


Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas bingwa atapata kombe na sh. 2,000,000,jezi seti moja,mipira mitatu na cheti, na nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa.


Mshindi wa Pili shilingi 1,000,000, Mipira 2, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki huku Mshindi wa Tatu - Tsh 500,000/=, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki na zawadi nyingine ni kwa  wanahabari wameyatangaza vyema mashindano hayo kama ifuatavyo Mwandishi bora blog, Mwandishi bora wa luninga , Mwandishi bora Redio kipindi cha michezo na Mwandishi bora gazeti watapata sh. 50,000 kila mmoja.


Lakini pia kutakuwa na zawadi kwa kipa bora, mchezaji bora wa mashindano, mwamuzi bora,mfungaji bora , timu yenye nidhamu itaondoka na zawadi pia.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 12,2019


SHIRIKA LA KUHIFADHI MISITU ASILI TANZANIA(TFCG) LAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI 28 WA KUANDIKA HABARI ZINAZOHUSU UHIFADHI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu-Morogoro

SHIRIKA la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) limeamua kuandaa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari nchini wapatao 28 kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazohusu usimamizi shirikishi wa wa misitu nchini.

Mbali ya kutoa mafunzo hayo shirika hilo limetumia nafasi hiyo kueleza hatua mbalimbali wanazofanya katika kuhakiksha jamii ya Watazania inakuwa na uelewa mzuri wa utunzaji misitu ya asili pamoja na kuongeza thamani ya misitu hiyo kwa jamii inayowazunguka.

Mafunzo hayo yametolewa leo mkoani Morogoro chini ya chini ya Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (Mjumita), Shirika la Kuendeleza Nishati Asili Tanzania (TaTEDO) ambayo yanatekeleza Mradi wa Kuleta Mageuzi Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC).

Katika mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo amefafanua mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo waandishi hao wa habari kuhusu rasilimali misitu inavyoweza kutunzwa na kutumika kwa faida ya jamii husika.

"Tunafahamu waandishi wa habari in kiungo muhimu kati ya jamii na watunga sera hivyo wao wanaamini kundi hilo likipata uelewa litarahisisha jamii nzima kuelewa lengo lao.Tumekuwa na utekelezaji wa mradi wa TTCS kwa takribani miaka saba sasa, hivyo wakati tunatekeleza mradi kwa wananchi waandishi wa habari ndio kiungo sahihi ya kufikisha ujumbe kwa jamii bila kupindapinda.

Hivyo tumekutana hapa kujengeana uwezo kwa kutambua waandishi wa habari ni wadau muhimu, wanafahamu mambo yanayohusu utunzaji wa misitu ya asili lakini tunataka kuelezana kwa kina kuhusu uhifadhi huo na hatimaye tuwe na lugha na tafsiri moja kati yetu sisi na wadau hasa vyombo vya habari na hii itasaidia jamii kupata ujumbe sahihi," amesema.

Amefafanua zaidi waliamua kuja na mradi huo ili kuhakikisha misitu ya vijiji inakuwa salama na endelevu jambo ambalo limeweza kuonekana kivitendo na katika maeneo ambayo mradi huo upo wamefanikiwa kiuchumi kutokana na ukweli kwamba mbali ya kutunza misitu hiyo wamekuwa wakinufaika nayo kwa kupata fedha nyingi kutokana na shughuli za uvunaji misitu unaofanywa na wanakijiji kwa utaratibu uliowekwa.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea mradi wa mkaa endelevu ambao unasimamiwa na shirika hilo na kwamba kupitia mkaa huo endelevu umeweza kuleta mageuzi makubwa mageuzi ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wengi vijijini.Hivyo ni vema hicho ambacho wanakifanya jamii ikaelewa vema na wenye kufikisha ujumbe huo ni waandishi wa habari.

Hata hivyo amesema  misitu ni rasilimali inayoweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwa jamii, hivyo wamekuwa wakijengea uelewa kwa wanavijiji kuhusu faida za matumizi endelevu ya rasilimali hiyo.

Kuhusu utafiti ambao umefanywa na shirika hilo, Lyimo amesema kwamba matokeo ya jumla yameonesha kuwa shughuli za kilimo ndizo zinachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa misitu ya asili na hiyo inatokana na uandaaji wa mashamba mapya makubwa kwa ajili ya kilimo na hasa cha mahindi.

"Tumetembelea wilaya 67 na mikoa 22 matokeo yanaonesha ukataji wa misitu unasababishwa na uandaaji wa mashamba mapya na mkaa ni sehemu ndogo hali ambayo inachangia upotevu wa hekta 469, 000 kila mwaka,"amesema Lyimo.

Ameshauri kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira na hasa ukataji wa misitu ni vema wanavijiji wakapewa fursa ya kuanzisha au kutenga maeneo ya uhifadhi wa misitu kwani wamebaini katika maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya hifadhi, misitu imekuwa salama kuliko ile misitu ambayo haina wa kuiangalia ambayo ndio inaharibiwa kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Ofisa wa Kujengea uwezo wa TFCG, Simon Lugazo ameongeza kuwa mradi huo umechochea kwa kiasi kikubwa jamii kutambua umuhimu wa kutunza misitu ya asili na kupata faida ya kiuchumi.Amesema hadi sasa vijiji,halmashauri na wanavijiii wamefanikiwa kuingiza zaidi ya Sh.bilioni tatu ambazo zimefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo. "Fedha hizo ambazo zimepatikana kupitia mradi huo zimetumika katika miradi ya afya, elimu, kilimo, maji na uhifadhi wa misitu ukiimarika".

Wakati huo huo Ofisa Mawasiliano wa TFCG, Bettie Luwuge ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari kujikita katika kuandika habari zinazohusu uhifadhi wa misitu ya asili nchini.Ukweli kupitia miradi ambayo tunaisimamia kuna mafanikio makubwa katika vijiji ambavyo tunashirikiana na wananchi katika hili, tumefanikiwa sana."


Kwa upande wake Mwandishi wa Habari Mkongwe, Allan Lawa amewataka waandishi wa habari nchini kuwa wabunifu kwa kuandika habari ambazo zinagusa jamii na nchi kwa ujumla zikiwemo habari za uhifadhi wa mazingira."Iwapo waandishi wa habari watatumia kalamu zao kwa ufasaha watakuwa na mchango mkubwa kwenye sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya jamii".
Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Bettie Luwuge akizungumza leo kuhusu sababu za kuamua kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya waandishi wa habari nchini.

 Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Bettie Luwuge (wa kwanza kulia) akiwa na maofisa wengine wa shirika hilo pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mada wakati wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kuandika habari zinazohusu usiamizi shirikishi wa misitu.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) Emmanuel Lyimo akifafanua jambo wakati wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari 28 kutoka vyombo mbalimbali yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za uhifadhi wa mazingira na hasa misitu ya asili.
 Baadhi ya wahariri wakongwe nchini ambao wamebobea katika masuala mbalimbali yakiwemo ya uandishi wa habari za mazingira wakiwa katika mafunzo hayo.Wahariri hao ni sehemu ya watoa mada kuhusu waandishi wa habari wanavyoweza kujikita kuandika habari za mazingira na kuleta mabadiliko ndani ya jamii kujenga utamaduni wa kutunza na kuhifadhi misitu na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla
 Ofisa wa Kujengea uwezo wa TFCG Simon Lugazo akitoa mada kwa waandishi wa habari inayohusu umuhimu wa vyombo vya habari kujikita katika kuandika habari za uhifadhi wa misitu ya asili nchini.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada zinazotolewa na wataalam wa masuala ya uhifadhi wa misitu ya asili wakati wa mafunzo hayo.

Mfumuko wa bei wa Taifa waongezeka kutoka asilimia 3.4 hadi asilimia 3.6

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO,Dodoma
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unaoishia mwezi Oktoba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.4 mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza takwimu za bei, Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Bibi. Ruth Minja amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019. 

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 115.84 mwezi Oktoba, 2019 kutoka 111.83 mwezi Oktoba, 209 

“Ongezeko hili la mfumuko wa bei limetokana na ongezeko la bei za bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.1 toka asilimia 4.0 mwezi Septemba, 2019.” Alisema Bibi. Ruth. 

Aidha amesema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo hazijumuishi chakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2019 umepungua kidogo hadi asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.7 Septemba, 2019 

Fahirisi za Bei kati ya mwezi Septemba, 2019 na mwezi Oktoba, 2019 zimepungua kwa asilimia 0.1 ambapo badiliko ni sawa na badiliko lilivyokuwa kati ya mwezi Agosti, 2019 na mwezi Septemba 2019 

Alizitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirishi kuwa ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 2.5, dieseli kwa asilimia 2.1, petrol kwa asilimia 4.0. vifaa kwa ajili ya uchakataji wa taarifa kama kompyuta kwa asilimia 5.1 na baadhi ya huduma binafsi. 

Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo ndiyo mamlaka ya kutangaza takwimu pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mfumuko wa bei kila mwezi ambapo ambapo mfumuko wa bei katika nchi hizo utangazwa.

DIAMOND AZITAJA SABABU ZA KUWEPO WIZKID NA TIWASAVAGE TAMASHA LA WASAFI.

$
0
0

     Na.Khadija seif, Michuzi TV

MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond platinum amewapongeza wasanii,makampuni pamoja na vyombo vya habari kwa kufanikisha tamasha la wasafi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Diamond amesema hayo katika ukumbi wa Hyatt regency uliopo jijini Dar es salaam ,nakugusia swala la wasanii hao kutoka nchi ya Nigeria kuwepo kwao kulikua na lengo maalumu.

"Lengo lilikua ni kujifunza kwa wenzetu jinsi ya kutumbuiza kwao kwa kuona mubashara tofauti na wengi wetu tulikua tunaona tu kupitia televisheni au kwenye mitandao ya kijamii,"

Aidha,mbali na kujifunza kutoka kwa wasanii hao wawili Diamond amefafanua zaidi kuwa wizkid na tiwasavage wataweza kututangaza kuanzia siku walipofika,sehemu watakazotembelea ,hivyo kutaleta ushawishi kwa watu ambao wanawatazama kutamani kufika nchi ya Tanzania.

Hata hivyo amewaomba wadhamini mwakani msimu mwingine wa Tamash hilo kuwaongezea fedha ili waweze kuwa na nafasi ya wasanii wengine kushiriki kikamilifu.

"Japo fedha ilikua pungufu sio sana lakini niliweza kutazama baadhi ya wasanii kwa jicho la kipekee kutokana na mara nyingi kutopewa nafasi kwenye majukwaa mbalimbali na ndio sababu pia sisi Kama wasafi na uongozi wa lebo yetu Wcb kuwapa nafasi wakongwe wa Muziki akiwemo inspector harun,Mandojo na domokaya,Madee na wengine kutumbuiza jukwaa la wasafi,"

Pia ametoa ushauri kwa wasanii kutosikiliza minong'ong'ono ya mashabiki zao wenye lengo la kuwagombanisha hasa mitandaoni.

"Wakati mwengine Mashabiki zetu wanatufanya tugombane ,tuchukiane na hata kutoelewana tuyapuuzie hayo kwani wote wanapenda kazi zetu kiujumla akitokea kwenye tamasha langu ataimba nyimbo zangu na akija kwako ataimba na zako huoni Kama wote Ni shabiki zetu tusiweke matabaka,"


SERIKALI YAOKOA BILIONI 34 /- KWA KUTUMIA MFUMO WA UNUNUZI KWA NJIA YA KIELETRONIKI-KATIBU MKUU

$
0
0
SERIKALI imesema imeokoa wastani wa Sh.bilioni 34 katika miaka mitano ya kwanza kutokana na kutumia mfumo  wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 11,2019,  Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Doto James amesema kwa kuzingatia mfumo huo imeiagiza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu kuwa taasisi zote za ununuzi nchini ziwe zimeungwa katika mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki na kuanza kuutumia bila kisingizio chochote.

Katibu Mkuu James amesema kuwa kuzingatia kwa fedha zitumikazo katika utekelezwaji wa miradi ya Serikali kwa kiasi kikubwa hutumika kupitia mifumo ya ununuzi wa umma na kwamba jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuliimarisha eneo hilo ili kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kupitia  ununuzi wa bidhaa.

Amesema taasisi za  umma  ambazo tayari  zimeunganishwa  katika mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki ni jumla ya taasisi nunuzi 418 kati ya taasisi 540 sawa na asilimia 77.4 ya taasisi nunuzi zilizopo nchini zimeunganishwa na mfumo huo.

James amesema tangu kuanza kwa mfumo huo kumeongeza ushindani kwenye michakato  ya ununuzi ,kuongeza ufanisi na hivyo kupunguza muda unaotumika katika michakato ya zabuni  pamoja kuongeza uwazi hivyo kupunguza vitendo vya rushwa.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Mhandisi  Leonard Kapongo amesema baada ya kupewa maagizo na Serikali waliingia kazini kuongeza katika kutoa mafunzo kuhusiana na mfumo kwa maafisa  Ununuzi na Tehama wa Taasisi za Umma.

Amesema hawataruhusu taasisi za umma kufanya nunuzi nje ya mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki kufikia Januari 31 mwaka ujao.

Mhandisi Kapongo amesema taasisi ambazo hazjaunganishwa wajiunge ikiwa ni pamoja na kugharamia mafunzo maakumu ya namna ya kutumia mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki.

 Pichani kati ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dar,kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS)  ikiwa pamoja na Utekelezaji wa Maagizo ya Waziri wa Fedha kuhusu matumizi ya mfumo huo.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Bodi  wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Balozi Dkt Matern Lumbanga na kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Mhandisi Leonard Kapongo.
 Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiwaonesha Waandishi wa Habari moja ya Nyaraka iliyokuwa na maelekezo ya uanzishwaji mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS),ambapo amesema Serikali imeagiza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) ifikapo Disembe 31,2019 ihakikishe taasisi zote za ununuzi hapa nchini ziwe zimeungwa katika mfumo huo na kuanza kuutumia bila kisingizio chochote. Picha na Michuzi JR.(MMG).
 Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

TAASISI 418 ZA UMMA ZAUNGANISHWA TANePS, OFISA MTENDAJI MKUU PPRA ATOA MWITO

$
0
0
JUMLA ya Taasisi 418 zimeunganishwa kwemye Matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (TANePS).


Hayo yamesemwa Novemba 11,2019 jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leonard Kapongo alipokuwa akielezea  utekelezaji wa magizo ya Waziri wa Fedha, Dk.Philip Mpango kuhusu mfumo wa TANePS.

Alisema wakat waziri anatoa maagizo hayo taasisi nunuzi zilizokuwa zimeunganishwa zilikuwa 303 huku jumla ya wataalam wa nunuzi na tehama wapatao 924 walikuwa wamepatiwa mafunzo.

"Kutokana na juhudi kubwa zilozofanyika hadi kufikia leo hii Novemba 11, 2019 jumla ya taasisi 418 zimeunganishwa huku idadi ya watalaam waliopatiwa mafunzo kutoka taasisi nunuzi wakifikia 1,600. Hii inamaanisha kuna ongezeko la taasisi 115 zilizounganishwa toka siku tuliyopewa maagizo Septemba 28 mwaka huu," amesema Kapongo.

Mhandisi Kapongo amefafanua utaratibu wanaotumia kwa sasa ni kuwa mara baada ya taasisi nunuzi kupatiwa mafunzo taasisi zao huunganishwa kwenye mfumo na taasisi hizo huagizwa na PPRA kuanza kuutumia mfumo wa TANePS kwa kuweka mipango yao ununuzi kama hatua ya awali.

Ameongeza baada ya hapo kuendelea na kutekeleza michakato yote ya ununuzi inayofuatia ikiwemo kuweka matangazo ya zabuni ili wazabuni waweze kushiriki kwa njia ya kieletroniki na kwamba kati ya taasisi 418 zilizounganishwa, taasisi 200 zimekwisha anza mfumo huo hadi leo kwa kuwasilisha mipango ya ununuzi ya mwaka yenye jumla ya zabuni 11,343 zenye thamani takribani shilingi Trilioni 11.3.

"Kwa zile taasisi za umma ambazo hazijaunganishwa kwenye mfumo huo, PPRA inatoa mwito kwa taasisi hizo kudhuria mafunzo maalum yakutumia mfumo huu yanayoendeshwa na PPRA.

Orodha ya taasisi hizo itawekwa kwenye tovuti ya PPRA yaani www.ppra.go.tz," amesema.

Mhandisi Kapongo amesisitiza awamu ya mwisho ya mafunzo itazihusisha taasisi hizo na yanatarajiwa kuanza Novemba 16 mwaka huu na kuendelea hadi kufikia wiki ya pili ya Desemba na matarajio yao baada ya kukamilika kwa awamu hiyo taasisi zote nunuzi zitakuwa zimeunganishwa kwenye mfumo wa TANePS.

Hata hivyo amesema kwa upande wa taasisi nunuzi ambazo zingependa kufanyiwa mafunzo maalum zinaweza kuwasilisha maombi PPRA kwa ajili ya kupatiwa maelekezo zaidi kuhusu taratibu za utoaji wa mafunzo hayo.

"Nirudie tena kutoa rai kwa wakuu wa taasisi nunuzi kuwa matimizi ya mfumo wa TANePS ni ya lazima kwa sababu ni takwa la kosheria na kanuni zake na sio suala la utashi wa taasisi. Hivyo sisi PPRA hatutaishia kutoa mafunzo na kuziunganisha tu kwenye mfumo taasisi nunuzi bali tutafuatilia kwa karibu kuhakikisha matumizi sahihi na kamilifu ya mfumo, hatutasita kuchukua hatua stahiki," amesema.

Aidha, ametoa mwito kwa watoa huduma mbalimbali, wazabuni na makandarasi wote nchini kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye michakato ya zabuni kwa kujisajili kwenye TANePS kupitia tovuti ya mfumo ambayo ni www.taneps.go.tz.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua umuhimu wa kuanzishwa kwa mfumo huo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS) kwa Waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam,ambapo alisema kuwa  jumla ya Taasisi 418 zimeunganishwa kwemye Matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (TANePS) kati ya Taasisi 540.Pichani kulia ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James .
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Balozi Dkt Matern Lumbanga akizungumza mbelee ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar,kwa kuishukuru Serikali kwa kuanzisha mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS),ambao utaongeza ufanisi ndani ya Serikali na kuongeza zaidi pato la Taifa katika mustakabali mzima wa kuwaletea Wananchi maendeleo. 

Airtel Africa yaingia ushirikiano na Mastercard kuwezesha wateja wa Airtel Money kufanya malipo kidigitali

$
0
0
• Wateja wa Airtel Money, hata wale ambao hawana akaunti za benki kwa sasa wanaweza kufanya malipo ya kimtandao/kidigitali wakiwa popote duniani kwa kutumia Airtel Money virtual card

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania  imetangaza kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao (kama Netflix) wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard. Wateja wa Airtel Tanzania wataweza kufurahia huduma hii ya kipekee kutokana na usalama na uhakika kwa kufanya malipo kidigitali popote kupitia ushirikiano huu.

Vile vile, wateja wa Airtel Money wataweza kufanya malipo binafsi kwa watoa huduma popote kwa kutumia huduma ya Quick Response (QR) kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali au watoa huduma kupitisha QR akaunti ya Airtel Money au kuandika namba ya wakala/mtoa huduma anaekubali malipo kwa Mastercard .

Uzinduzi wa huduma hii unalenga kuendelea kukuza sekta ya fedha hapa Tanzania huku taarifa za hivi karibuni za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zikionesha kuwa, nchini Tanzania watumiaji wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu za mkononi wanaongezeka ambapo hadi kufikia mwezi machi mwaka huu wamefikia takribani milioni 22 wakiwa wamefanya miamala inayofikia thamani ya zaidi ya TZS trilioni 8. 

Vile vile, kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na maendeleo makubwa katika baadhi ya huduma kama utumaji wa fedha kupitia mitandao mbalimbali kutoka ule wa zamani uliokuwa ukifanyika kwa kumtuma mtu ili kusafirishae fedha ndani au nje ya nchi, ubunifu umefanyika hata kwenye kununua muda wa maongezi kwa mtandao na hivyo kufanya huduma ya fedha wa njia ya mtandao kuwa moja ya huduma yenye tija katika sekta ya kifedha nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo ya Airtel Money Mastercard Virtual card, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchuda alisema “Kwa sasa tunaishi kwenye dunia ambapo malipo yanafanyika kila sekunde. 

Ushirikiano wetu na Mastercard unatufanya tuendelee kukamilisha dhamira yetu ya kutoa huduma na bidhaa ambazo ni za kipekee na zenye unafuu zaidi ili kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wetu.’ Alisema Nchunda huku akiongeza kuwa uzinduzi wa Airtel Money Mastercard Virtual card unaonyesha ni kiasi ngani Airtel inaunga mkono juhudi za Serikali za kurahishisha na kupanua sekta na huduma za kifedha hapa nchini.

Airtel Money Mastercard inamuwezesha mteja wa Airtel kufanya malipo kwa urahisi kwenye sehemu zote ambazo Mastercard inakubalika hata kama mteja huyo hana akaunti ya benki au kadi ya malipo. Ili mteja wa Airtel Money aweze kupata Airtel Money Mastercard Virtual card piga *150*60# chagua 6 kisha 1 na ufuate maelekezo kuapata Airtel Money Mastercard Yako. Pale Airtel Money Mastercard inapokamilika pia inakuwa tayari kwa malipo ya kupitia mtandao.

Kwa upande wake, Makamu Rais na Mkurugenzi wa Biashara Afrika Mashariki wa Mastercard Adam Jones alisema “Ushirikiano wetu na Airtel utarahishisha huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania. Kwa kupitia ushirikiano wetu huu wa huduma za kidigitali, nia yetu ni kuendelea kuboresha utoaji huduma kiditali zaidi kwa kuzingatia urahisi, unafuu na usalama ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kidigitali. 

Mastercard ni njia ya malipo kwa mtandao inayotumia teknolojia ya kisasa kwa kushirikiana na washirika wake ukanda wa kati pamoja na bara la Afrika kwa lengo la kumfanya mteja kufurahia huduma za kimataifa za malipo”.

“Huduma za fedha kwa mitandao ya simu imesaidia sana kupuguza gharama za miamala na kuongeza ukuaji wa uchumi kwa kuondoa gharama za kusafiri mpaka kwenye matawi ya benki ili kufanya miamala ya malipo. Airtel Money Mastercard sasa itapanua wingo wa matumizi ya akaunti za Airtel Money kufanya malipo kwa njia ya mtandao, alisema Jones.

Airtel Money Tanzania kwa sasa imeunganisha kwa zaidi ya watoa huduma 1000 pamoja na taasisi za kifedha zaidi ya 40 kwa kumfanya mteja kutoa na kuweka fedha. Vile vile, Airtel inazidi kutanua wigo wake hapa nchini kwa kuwa na Zaidi ya Airtel Money branch 80ambazo zinatoa huduma na bidhaa za Airtel.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirji alisema taasisi yake imejipanga vyema na kwakudhihirisha hilo kwa inaendelea kuwekeza kwenye miundo mbinu na kujiweka kwenye sehemu nzuri kwenye soko ili kuendelea kutoa huduma ya malipo ya uhakika kwa washirika wake kama Mastercard na Airtel ambao dhamira zao ni kutoasuluhisho kwenye huduma za malipo. 

“Selcom imekuwa moja ya taasisi imara kwenye huduma ya malipo kwa zaidi ya muongo mmoja na kutoa mageuzi makubwa kwenye malipo ya kimtandao hapa nchini na wakati tukiendelea kukua tunakua pamoja na washirika wetu kwenye kurahshisha malipo ykidigitali.

“Matokeo ya uzinduzi huu wa Airtel Money Mastercard ni mafanikio makubwa sana kwa kuwa utarahisisha mambo mengi kwa wateja wa Airtel Money”.alimaliza kusema Sameer.
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchuda akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard. 
Makamu Rais na Mkurugenzi wa Biashara Afrika Mashariki wa Mastercard Adam Jones wakati wa kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akisisitiza jambo wakati wa kuingia ushirikiano na Mastercard kwa kuzindua huduma ya Airtel Money Mastercard Virtual card ambayo itawawezesha wateja wa Airtel Money kulipia huduma, bidhaa, applikesheni, hoteli, gharama za usafiri pamoja na kulipia huduma za mtandao wakati wowote kidigitali zaidi kupitia watoa huduma wote waliounganishwa au wanaokubali malipo kwa Mastercard .

SERIKALI IPO TAYARI KUPOKEA MAPENDEKEZO YATAKAYOTOLEWA KWENYE MKUTANO WA SAYANSI,TEKNOLOJIA,UBUNIFU

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wageni wanaohudhulia Mkutano wa Sayansi,Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua mkutano unaokutanisha wadau wa sayansi kutoka nchi mbalimbali za Jangwa la Sahara jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi (COSTECH) Dk.Amos Nungu akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Ngoma zilizotumuiza katika ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa Sayansi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Sayansi wakiwa katika Ufunguzi wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.

 Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kupokea Mapendekezo ambayo yatatolewa katika Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea katika Hoteli ya Srena jijini Dar es Salaam.

Hayo ameyasema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akifungua mkutano wa Sayansi, teknolojia na Ubunifu mkutano huo unaounganisha nchi mbalimbali za kusini mwa Jangwa la Sahara amesema Mkutano huo unalengo la kukutanisha tasisi zinazo fadhiri tafiti za Kisayansi pamoja na kuangalia ni namna gani wanaweza kufanya kazi pamoja.

"Serikali ipo tayari kupokea maoni na mapendekezo ambayo yatatolewa katika Mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha tafiti katika nchi yetu na katika nchi za Afrika unaleta tija na chachu ya maendeleo katika nchi za Afrika."

Hata hivyo Prof .Ndalichako amesema kuwa nchi ya Ujerumaji imetangaza rasmi kufadhili utafiti hapa nchini ili kuongeza chachu ya utafiti na maendeleo ya kisaya na kiteknolojia kwa kuungana na taasisi mbalimbali hapa nchini kwaajili ya kukuza na kuendeleza tafiti za kisayansi ili kuibua vitu vipya zenye kuzalisha katika jamii.

Amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko tayari kuunga mkono tafiti za kisayansi, kiteknolojia pamoja na ubunifu ili kuwepo na masoko mapya na yenye rasilimali watu wa kutosha katika jamii yetu.

Prof Ndalichako amewaalika wageni 250 waliopo hapa nchini Kutembelea Vivutio vilivyopo hapa nchini kwani watafurahia pamoja na kuburudisha akili zao.

Katika mkutano huo mada zinazoendelea kujadiliwa ni pamoja na kukuza ushirikiano kati ya taasisi ambazo zinafadhili tafiti katika nchi za afrika, kubadilishana uzoefu wa kitafiti katika taasisi zinazofadhili tafiti,kujadiliana mashirikiano mapya ya kufanya tafiti pamoja na miradi mipya ya kitafiti.

CWT KUJENGA OFISI ZA WILAYA 40

$
0
0
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kukamilisha ujenzi wa ofisi za CWT za wilaya 40 ili kuboresha utendaji kazi wa walimu wa sehemu mbalimbali hapa nchini. 

Katibu mkuu wa CWT, Deus Seif aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya mwalimu wilayani Simanjiro mkoani Manyara. 

Seif alisema hadi mwezi Aprili mwakani, ofisi 40 ikiwemo ya CWT Simanjiro zitakuwa zimejengwa ili kuondokana na adha ya kupanga ofisi wakati uwezo wa kujenga ofisi wanao.

"CWT ni taasisi kubwa ya tatu nchini ukiondoa Kanisa Katoliki na CCM, hivyo lazima tujenge ofisi ili yasitupate mambo ya majengo tunayopanga yakiuzwa na sisi tunauzwa huko huko," alisema. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula alisema kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kimepanda wilayani humo kupitia walimu. 

Mhandisi Chaula alisema kiwango cha ufaulu wilayani Simanjiro kwa shule za msingi mwaka 2017 kilikuwa asilimia 49.96 na mwaka jana ilikuwa asilimia 69.01.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi alisema wana miaka mitatu kwenye wilaya hiyo na wamefanikisha uanzishwaji wa shule mbili za sekondari za kidato cha tano na sita. 

"Tunatarajia kuanzia shule nyingine ya tatu ya kidato cha tano kwenye tarafa ya Moipo pia tumeanzisha chuo cha Veta kilichopo Emboreet kupitia ufadhili wa mdau wa maendeleo Peter Toima," alisema Myenzi. 

Mwanachama wa heshima wa CWT, Peter Toima alisema kupitia shirika lake lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, anajitolea matofali 3,000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CWT Simanjiro. 

Toima ambaye kitaaluma ni mwalimu alisema yeye ni mdau wa elimu ndiyo sababu huwa anashirikiana na serikali kuunga mkono maendeleo mbalimbali ikiwemo kujenga madarasa ya shule. 

Katibu wa CWT wilaya ya Simanjiro, mwalimu Nazama Tarimo alisema Simanjiro ina walimu 892 wakiwemo 622 wa shule za msingi na 270 wa shule za sekondari. Tarimo alisema katika awamu ya tano ya serikali ya Rais John Magufuli, walimu 249 wamepandishwa madaraja kati ya walimu 355 waliokasimiwa kupandishwa. 

Hata hivyo alisema tayari walimu 222 wamebadilishiwa mishahara yao hadi mwezi Oktoba, bado walimu 106.
Katibu Mkuu wa CWT, mwalimu Deus Seif (katikati) akikagua eneo litakalojengwa ofisi ya chama hicho Wilayani Simanjiro.
Katibu Mkuu wa CWT, mwalimu Deus Seif akipokewa na walimu wa Mkoa wa Manyara, alipofanya ziara ya siku moja wilayani Simanjiro.

Faida za muungano wa Tigo na Zantel kwa watumiaji wa simu za mkononi nchini

$
0
0
IMETANGAZWA mapema wiki hii kuwa kampuni mbili kubwa za mawasiliano ya simu nchini Tanzania za Tigo na Zantel zimeungana. 

Muungano huo wa kampuni hizi mbili unafanya ziunganishe huduma zao maeneo yote mawili ya Muungano kwa maana ya Bara na Visiwani na ni muungano ambao umekuwa ukisubiriwa kutokea. 

Mapema mwaka huu wakurugenzi wa kampuni hizo mbili waliweka bayana kusudio hilo la kuungana katika mahojiano na jarida maarufu duniani la Forbes toleo maalumu la kujenga Tanzania yenye mafanikio. 

Waliweka wazi namna gani muungano huo utaleta faida kwa wateja wa kampuni hizo mbili kupitia kuboresha huduma kwa kiwango cha juu na sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi kwa ujumla. 

Swali ni je muungano huu una faida gani hasa kwa mteja? 
Kwa ufupi, wateja wa kampuni hizi zote mbili sasa wataweza kufurahia huduma bora zaidi ambazo zitatolewa kutokana na muungano huu. 

Muungano huu unaleta nguvu za kampuni zote mbili pamoja na kutoa kilicho bora zaidi kote bara na visiwani, mijini na vijijini. 

Pia unaongeza wigo wa kufanya biashara toka pande zote mbili,lakini ni vyema pia kufahamu faida hizi za muunganiko si tu kwa wateja wa Tigo na Zantel pekee. 

Akielezea kuhusu muungano huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania , Simon Karikari, amesema kuwa anaamini “utatengeza sekta bora zaidi ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania kwa sasa na siku za usoni.” Ameongeza pia kuwa soko lenye kampuni zilizoungana kama hivi litasukuma mbele ubunifu. 

Wataalamu wa uchumi na teknolojia wameweka bayana athari hasi za kuwa na soko vipande vipande au lenye kampuni nyingi za mawasiliano ya simu za mkononi mijawapo ikiwemo kushindwa kuwekeza mitaji mikubwa yenye kukuza tija kwa mtumiaji kwa muda mrefu. 


Muungano wa Tigo na Zantel ni hatua kubwa na muhimu katika kukuza sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania na kuleta mabadiliko chanya katika sekta hii. Sasa zimebaki kampuni tano badala ya sita kutokana na kuondoka kwa kampuni ya Smart mwezi jana. Hatua ya Tigo na Zantel sio tu muhimu kwa wateja wao bali pia uchumi wa nchi na sekta ya mawasiliano kwa ujumla.

Wateja watano wajishindia bodaboda na Ibuka Kidedea na NBC Malengo

$
0
0
 Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni  ya akaunti ya Malengo ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya bodaboda  kila mmoja.  Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo na kulia kabisa ni mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha .
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (mbele kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati  NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni  ya akaunti ya Malengo ya NBC ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya pikipiki aina ya Yamaha kila mmoja.  Washindi wa leo ni;  Augustine Hatari kutoka Pwani, Williumu Pendaeli Isack wa Moshi,  Scholastica Peter Yamawasa, Honest Christopher Kimaro na  Daudi Majani wote kutoka Dar es Salaam.



WATEJA Watano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wameibuka washindi wa bodaboda mpya aina ya Yamaha katika droo ya kwanza ya kampeni ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC” kupitia akaunti ya Malengo ya benki hiyo kongwe hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwenye droo ya kwanza ya kampeni hiyo iliyoanza mwezi wa Oktoba, Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo alisema kwamba akaunti ya malengo inampa mteja njia rahisi ya kuweka akiba kidogo na kupata faida kubwa kila mwezi.

“kwenye akaunti hii ya malengo kila Tsh 100,000 atakayoweka mteja kwenye akaunti hii inampa nafasi ya kushida zawadi kemkem ikiwemo bodaboda ambapo leo droo ya kwanza itashuhudia wateja hawa watano wakipata zawadi zao,” alisema Kimaryo.

Aliongeza kwamba katika kipindi chote cha kampeni bodaboda tano aina ya Yamaha zitatolewa kila mwezi na safari tatu za kwenda kufanya utalii Serengeti na safari tano za kwenda Seychelles mwezi wa Disemba na washindi wanaruhusiwa kwenda na mtu mmoja kwenye safari hizo.

“ukiwa na akaunti ya NBC malengo unapata faida nyingi ikiwemo ya kuhifadhi fedha kwa ajili ya kutimiza malengo na ndoto zako pamoja na mambo mengine ya kupata riba ya hadi asilimia 7 ya pesa uliyoweka kila mwezi,’ alisisitiza Kimaryo.

Washindi kwenye droo ya jana walikuwa ni Augustine Hatari kutoka Pwani, Daudi Majani, Dar es Salaam, Williumu Pendaeli Isack, Moshi Kibololoni, Scholastica Peter Yamawasa, Dar es Salaam, na Honest Christopher Kimaro wa Dar es Salaam.

Katika kampeni hii wateja watakao ongeza salio kwa kiasi Tsh milioni moja kwenye akaunti ya Malengo watapata nafasi ya kushinda zawadi kuu ya TOYO na jumla ya TOYO tatu zitatolewa kwenye kampeni hiyo ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC MALENGO”

AVEVA NA WENZAKE KUANZA KUJITETEA NOVEMBA 20

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

ALIYEKUWA rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake wanatarajia kuanza  kujitetea Novemba 20, mwaka huu.

Aveva na wenzake wanakabiliwa na mashitaka ya kughushi na matumizi mabaya ya madaraka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, 

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa. 

Hakimu Simba amehoji kwanini kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa wakati ilipangwa kwa kusikilizwa? Na Wakili Mitanto amedai katika  shauri lililopita waliitaarifu mahakama kuwa wamekata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo hivyo, wanaomba tarehe nyingine kusubiri uamuzi wa rufaa.

Baada ya kutoa taarifa hiyo, Hakimu Simba amesema watapanga tarehe ya kusikilizwa kwa utetezi na kama kutakuwa na masuala ya rufaa waijulishe mahakama.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amehairisha kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu kwa utetezi.

Mbali na Aveva washitakiwa wengine ni makamu wa rais, Geofrey Nyange maarufu Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka saba na kuondolewa mashitaka mawili ya utakatishaji fedha.

Katika mashitaka ya kwanza,  Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Inadaiwa Aveva na Kaburu wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Pia inadaiwa Aveva na Kaburu  wanadaiwa kwa pamoja kughushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.

Aveva anadaiwa katika benki ya CRDB anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000

Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Barclays Mikocheni alijipatia Dola za Marekani 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia Dola za Marekani 187,817 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi. 

Aveva, Kaburu na Hans Poppe  wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Marekani 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli

Katika mashitaka ya nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo  kwa Levison Kasulwa  kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577

Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577.

SAMATTA, MSUVA WATUA KUIMALIZA EQUATORIAL GUINEA NOVEMBA 15

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta na Mshambuliaji, Saimon Msuva rasmi wametua nchini kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mchezo wakuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea, mashindano yatakayofanyika nchini Cameroon.

Samatta na Msuva watawaongoza wenzao 27 wa Kikosi cha Stars kwenye mchezo huo wa kwanza wa Kundi J utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Novemba 15 mwaka huu.

Baada yakutua nchini akitokea kwenye majukumu ya Klabu yake ya KRC Genk, Samatta amesema kama Nahodha hafahamu chochote kuhusu Guinea ya Ikweta, amesema hawezi kuzungumzia wao, amesema wataandaa kikosi kipindi hiki cha wiki moja kuhakikisha wanaimaliza Guinea katika mchezo huo.

"Nakumbuka mwaka juzi, katika michezo yakufuzu AFCON, tulicheza na Lesotho mchezo wetu wa kwanza lakini tulitoka sare ya 1-1, kitu ambacho tulijutia sana sisi kama timu wakati tulikuwa nyumbani", amesema Samatta.

Samatta amesema Taifa Stars itaandaa Kikosi vizuri ili kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wa kwanza, amesema kwa upande wake yupo vizuri kuwavaa Guinea ya Ikweta pamoja na Msuva.

"Miaka michache ijayo natamani kuona Wachezaji hata 8 tunacheza Ulaya ili wote tuje kuitumikia Timu ya Taifa, Watanzania watambue wanapokuja Uwanjani watambue kuwa wao ni Mchezaji wa 12, waje kwa wingi kuhakikisha timu yao inapata ushindi katika mchezo huo", amesema Samatta.

Kwa upande wake, Saiamon Msuva amewaomba Watanzania kufika kwa wingi Uwanjani siku hiyo ya Novemba 15 kuishangilia Taifa Stars ili iweze kupata ushindi wake katika mchezo wake wa kwanza, amesema Tanzania tunahitaji kusonga mbele kisoka.

"Tumejiandaa vya kutosha katika Kikosi chetu chini ya Kocha Mkuu, Ndayiragije kilichobaki kufanya kazi hiyo Novemba 15 tukisaidiana na wenzetu waliotangulia kujiunga na Kikosi", amesema Msuva.

Wachezaji watakaoivaa Equatorial Guinea, Novemba 15 ni Mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta, Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya nchini Morocco Simon Msuva, Kiungo wa Tenerrife ya Hispania Farid Mussa. Beki wa Kulia wa Nkana ya nchini Zambia Hassan Kessy , David Kisu (Gor Mahia )na Eliuter Mpepo kutoka Buildcon Zambia.

Magolikpa Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga) na mabeki ni Salum Kimenya (TZ Prisons), Mohamed Hussein (Simba), Gadriel Michael (Simba), Erasto Nyoni (Simba)Bakari Nondo (Coastal Union), Kelvin Yondani (Yanga), Dickson Job (Mtibwa).

Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Abdul Aziz Makame (Yanga), Iddi Suleimani (Azam), Salum Abubakar (Azam),  Mzamiru Yassin (Simba), Frank Domayo (Azam), Miraji Athuman (Simba), Hassan Dilunga (Simba).

Kwa upande wa safu ya Usambuliaji ni Ditram Nchimbi (Polisi TZ), Shaban Iddi (Azam),Kelvin John ( Football House) na Ayoub Lyanga (Coastal Union).

Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images