Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

KATIBU WA BUNGE, NDG. STEPHEN KAGAIGAI AKUTANA NA MAAFISA WAANDAMIZI KUTOKA BUNGE LA KENYA JIJINI DODOMA

$
0
0
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza na Maafisa kutoka Bunge la Kenya walipomtembelea leo Ofisini kwake Bunge Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Mahusiano na Machapisho Kutoka Bunge la Kenya, Ndg. Njenga Ruge walipomtembelea leo Ofisini kwake Bunge Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Mahusiano na Machapisho Ndg. Njenga Ruge kutoka Bunge la Kenya pale Maafisa kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo Ofisini kwake Bunge Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (watatu kulia) katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Bunge la Kenya walipomtembelea leo Ofisini kwake Bunge Jijini Dodoma. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Mahusiano na Machapisho na Kiongozi wa Msafara kutoka Bunge la Kenya 
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akisalimiana na Katibu Msaidizi Mwandamizi kutoka Bunge la Kenya, Ndg. Lawrence Amollo wakati akiwakaribisha Maafisa kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo Ofisini kwake Bunge Jijini Dodoma.

DIAMOND AZITAJA SABABU ZA KUWEPO WIZKID NA TIWASAVAGE TAMASHA LA WASAFI.

$
0
0

     Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond platinum amewapongeza wasanii,makampuni pamoja na vyombo vya habari kwa kufanikisha tamasha la wasafi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Diamond amesema hayo katika ukumbi wa Hyatt regency uliopo jijini Dar es salaam ,nakugusia swala la wasanii hao kutoka nchi ya Nigeria kuwepo kwao kulikua na lengo maalumu.

"Lengo lilikua ni kujifunza kwa wenzetu jinsi ya kutumbuiza kwao kwa kuona mubashara tofauti na wengi wetu tulikua tunaona tu kupitia televisheni au kwenye mitandao ya kijamii,"

Aidha,mbali na kujifunza kutoka kwa wasanii hao wawili Diamond amefafanua zaidi kuwa wizkid na tiwasavage wataweza kututangaza kuanzia siku walipofika,sehemu watakazotembelea ,hivyo kutaleta ushawishi kwa watu ambao wanawatazama kutamani kufika nchi ya Tanzania.

Hata hivyo amewaomba wadhamini mwakani msimu mwingine wa Tamash hilo kuwaongezea fedha ili waweze kuwa na nafasi ya wasanii wengine kushiriki kikamilifu.

"Japo fedha ilikua pungufu sio sana lakini niliweza kutazama baadhi ya wasanii kwa jicho la kipekee kutokana na mara nyingi kutopewa nafasi kwenye majukwaa mbalimbali na ndio sababu pia sisi Kama wasafi na uongozi wa lebo yetu Wcb kuwapa nafasi wakongwe wa Muziki akiwemo inspector harun,Mandojo na domokaya,Madee na wengine kutumbuiza jukwaa la wasafi,"

Pia ametoa ushauri kwa wasanii kutosikiliza minong'ong'ono ya mashabiki zao wenye lengo la kuwagombanisha hasa mitandaoni.

"Wakati mwengine Mashabiki zetu wanatufanya tugombane ,tuchukiane na hata kutoelewana tuyapuuzie hayo kwani wote wanapenda kazi zetu kiujumla akitokea kwenye tamasha langu ataimba nyimbo zangu na akija kwako ataimba na zako huoni Kama wote Ni shabiki zetu tusiweke matabaka,"


WAFANYABIASHARA WA TANZANITE WAITWA KWA RMO MIRERANI

$
0
0
Ofisa madini mkazi (RMO) wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima, akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani.
……………..
WAFANYABIASHARA maarufu wa madini ya Tanzanite 28 wakiwemo wenye asili ya bara la Asia na baadhi ya wamiliki wa migodi hiyo, wameitwa katika ofisi ya madini Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ili watoe taarifa juu ya madini waliyonayo. 

Kwa mujibu wa barua ya Ofisa madini mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima imewataka wamiliki hao wa migodi, madalali na wanunuzi wa madini hayo kufika ofisini kwake kuanzia leo jumanne ya Novemba 12.

Ntalima alisema shughuli hiyo itafanyika kwenye ofisi yake, kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 12 hadi Novemba 14.

Alisema wahusika wote wameshaandikiwa barua wakiwemo wale ambao siyo wanachama wa chama cha wafanyabiashara wa madini nchini (Tamida). 

Aliwataka wahusika wote kuhudhuria bila kukosa ili kuweka uelewa wa pamoja juu ya biashara ya madini ya Tanzanite ili kujenga Taifa bora. 

Wafanyabiashara hao walioandikiwa barua ya kutii wito huo ni Hussein Lemali, Emmanuel Wado (Sunda), Saitoti, Tarimo, Bima, Hamad Mjaluo, Manesh Kotog, Edward Mollel na George Kivuyo. 

Wengine ni Ben Nkya, Peter Periera, Sam Mollel, Rakesh, Vinal, Reno, Bima, Rajan, Saran, Salesh, Sidor, Faisal, Jitu, Muller, Shah, Sumil na Frizble. 

Oktoba 29 mwaka huu Ntalima alitaja majina ya vigogo wenye kumiliki madini ya Tanzanite ofisini kwao au majumbani mwao, kufika ofisini kwake ili watoe taarifa zao juu ya madini hayo. 

Mmoja kati ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, Hawa Athuman alisema baadhi ya watu hawakuamini kama serikali ingeweza kuwaita wafanyabiashara hao na wakatii amri. 

“Tusomeshe watoto jamani, huyu RMO Daudi Ntalima ni kijana mdogo lakini anatimiza wajibu wake ipasavyo yaani hawa wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite wametoka Arusha na kuja Mirerani kuleta taarifa zao,” alisema. 

Mkazi mwingine, Hamis Hamza alisema tukio hilo ni zuri kwa serikali kwani inapokuwa na mashaka juu ya suala lolote lile hufanya mahojiano ili kujiridhisha. 

“Hii serikali ya Rais John Magufuli inafanya kazi kweli kweli jana tumewaona vigogo wametoka Arusha na kuja Mirerani kuhojiwa na kutoa taarifa zao,” alisema Hamza.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA AONGOZA SEMINA KUHUSU NAFASI YA BUNGE KATIKA MAPINDUZI YA LISHE NCHINI JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Semina hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Agri Thamani, Mhe. Mizengo Pinda (kulia kwake), Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Sekretariat ya Kamati ya Uongozi ya Bunge
Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Ndg. Sikitu Simon akiwasilisha maada mbele ya Wajumbe Kamati za Kudumu za Bunge za uongozi, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati ya uongozi ya Bunge wakati wa semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya uongozi, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati ya uongozi ya Bunge wakiwa kwenye semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Agri Thamani Foundation, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya uongozi, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati ya uongozi ya Bunge kwenye semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Agri Thamani Foundation, Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kijarida kinachotoa uelewa mpana zaidi wa janga la udumavu na utapiamlo nchini mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge za uongozi, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati ya uongozi ya Bunge kwenye semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Agri Thamani Foundation, Mhe. Mizengo Pinda alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na Viongozi kutoka Agri thamani Foundation Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Agri Thamani Foundation na Kiongozi wa Msafara, Mhe. Mizengo Pinda, Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Neema Lugangira (katikati) na Mwenyekiti wa Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dunstan Kitandula (kulia)

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TRA YAKABIDHI VYETI VYA UTAMBULISHO WA MLIPA KODI WILAYANI KIBITI MKOA WA PWANI

$
0
0
NA RACHEL MKUNDAI, KIBITI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa kuwa inatolewa bure bila malipo yoyote.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu kwa Mlipakodi inayoendelea wilayani Kibiti katika mkoa wa Pwani, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema TRA inawakaribisha wafanyabiashara wote ambao hawajajisajili kufika maeneo maalumu yanayotoa huduma na elimu kwa mlipakodi katika wiki hii ili wasajiliwe na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi waweze kufanya biashara zao kwa Uhuru na kulipakodi stahiki bila usumbufu.

"Tunafanya wiki ya huduma na elimu kwa lengo la kusogeza huduma karibu na walipakodi na kuwatatulia changamoto zao zinazohusu ulipaji Kodi" amesema Kayombo.

Aidha, Kayombo ameongeza kuwa mbali na kutoa elimu kwa njia ya semina na matamasha maofisa wa TRA wanapita madukani kutoa elimu kwa wafanyabiasha na kuwasajili kupata namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kuongeza idadi ya walipakodi na kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari miongoni mwa watanzania. 

Amesisitiza kwamba, TRA imejipanga kufanya wiki ya elimu kwa mikoa miwili miwili kwa mwezi na hivyo amewataka wafanyabiashara wa kutumia fursa hii kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi na kuhakikisha cheti wanatundika katika maduka yao katika sehemu inayoonekana. 

Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na kuwa na wiki ya elimu lakini pia TRA imetenga siku ya Alhamis kila wiki kwa mameneja wa wilaya na mikoa nchini kote kuwasikiliza wafanyabiashara na kutatua changamoto zao ili kuchochea ari ya ulipaji kodi kwa hiari. 

Wiki ya elimu kwa mlipakodi inafanyika katika mikoa ya Morogoro na Pwani kuanzia tarehe 11 hadi 17 Novemba, 2019 ambapo wananchi na wafanyabiashara watapata fursa ya kuelimishwa masuala ya ulipaji kodi

Huduma zinazotolewa katika wiki hii ni usajili wa wafanyabiashara na utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, Ulipiaji wa kodi ya majengo, elimu ya kodi na kutatua changamoto mbalimbali za walipakodi ili kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.Richard Kayombo (kulia), akimkabidhi Cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) Bw. Abdallah Juma, ambaye ni mkazi wa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika stendi ya Kibiti wilaya humo.
Mkazi wa Kibiti mkoani Pwani, Mahamoud Hemed Mpikage akionesha Cheti cha Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kukabidhiwa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika stendi ya Kibiti wilaya humo. 
Afisa Mtendaji Kata ya Kibiti wilaya ya Kibiti Ramadhani Mtulia akifungua semina ya elimu ya ulipaji kodi iliyofanyika katika stendi ya Kibiti kama sehemu ya wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea wilayani humo. 
Elimu ya mlipa kodi ikiendelea kutolewa na wataalamu wa TRA huko Kibiti 

WAZIRI LUKUVI AFUNGUA MKUTANO WA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ARDHI NA UHIFADHI WA MANDHARI ZA AFRIKA, ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (Mb) akifungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za Ardhi katika Mandhari ya Afrika (African Landscapes Dialogue) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) jijini Arusha
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akimkaribisha Waziri kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ambaye ndiye mwenyeji wa Mkutano huo Dkt. Stephen Nindi akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu malengo na matarajio ya mkutano kabla ya kufuguliwa na Mh. Waziri
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo kutoka Serikali ya Uholanzi Bw. Hayo Haastra akitoa maelezo kwa washiriki namna Serikali ya Uholanzi inavyoshiriki kwenye mijadala ya matumzi ya ardhi katika mandhari mbalimbali za Afrika.
Mkurugenzi wa Eco Agriculture Sara Scherr, akitoa maelezo ya namna taasisi yake ilivyoshiriki katika maandalizi na kufanikisha kufanyika kwa Mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Boris Buechler akizungumza na washiriki kuhusu ushiriki wa Shirika hilo kwenye masuala mbalimbali ya matumizi ya rasilimali ardhi katika mandhari za Afrika
 Mwakilishi kutoka Senegal Chimmere Diaw wa African Model Forest Network akiwasilisha mada ya jinsi ya kusimamamia mandhari jumuishi ya matumizi ya ardhi
 Bwana John Recha kutoka programu ya mabadiliko ya Tabianchi akiwasilisha mada kuhusu upangaji matumizi ya ardhi katika mandhari mbalimbali kwa kuzingatia Sera na mabadiliko ya tabianchi
 Mkurugenzi wa Shirika la Solidaridad Afrika Mashariki na kati Rachel Wanyoike, akiendesha moja ya mijadala kuhusu matumizi ya ardhi katika mandhari mbalimbali za Afrika
 Washiriki wakifuatilia Mkutano
 Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za Ardhi katika Mandhari ya Afrika (African Landscapes Dialogue).(Picha na Fredy Njeje)

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi, amefungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi bora ya rasilimali ardhi kwenye Mandhari mbalimbali za Afrika wenye lengo la kujadili hali halisi na kubadilishana uzoefu katika upangaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Mandhari hizo.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mh. Lukuvi amewapongeza Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kama muandaaji mwenyeji, Asasi zisizo za Kiserikali za Eco Agriculture Partners pamoja na wadau wengine wote waliofanikisha kufanyika kwa mkutano huo na Tanzania kuwa mwenyeji kwa mwaka huu.


Aidha, Mh. Lukuvi amewataka wadau hao kutoka ndani na nje ya nchi kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kisekta yenye lengo la kuimarisha Mandhari Duniani hasa katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kushamiri na kuathiri uzalishaji na maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali Duniani.


Mkutano huo wa siku nne, unatarajiwa kujadili masuala ya uanzishwaji na utawala wa mandhari, utekelezaji na upangaji wa mandhari kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi, uimarishaji wa biashara, ajira na ujasiriamali katika uchumi wa kijani. Masuala mengine ambayo yanatarajiwa kujadiliwa ni pamoja na usimamizi wa wanyamapori na bionuai katika mandhari pamoja na udhamini kifedha, Uwekezaji, haki za miliki na matumizi ya ardhi katika mandhari. 


Inategemewa kuwa, kufanikiwa kwa utekelezaji wa masuala hayo yote katika nchi mbalimbali za Afrika na dunia kwa ujumla itakuwa ni chachu katika kuimarisha uchumi na kuleta maendeleo ya nchi na hatimaye kufanikiwa kwa malengo endelevu ya maendeleo (Sustainable Development Goals)


RAS TANGA AWAONYA WATUMISHI WA UMMA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MAGENDO

$
0
0
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati wa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akigawa sehemu ya bidhaa ambazo zilikamatwa na kutaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu za forodha ambazo ni sukari mifuko 278 na mafuta ya kupikia madumu 1241na hivyo kamisha wa Idara ya forodha na Ushuru wa Bidhaa ameamua kutoa kama msaada kwa taasisi mbalimbali hususani vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu na magereza kwa mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamisha Msaidizi wa Jeshi la Magereza Emanuel Lwenga
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakikagua vitu hivyo kabla ya kugawa kwa walengwa
Sehemu ya bidhaa ambazo ziligawiwa ambazo ni mafuta ya kula 
Sehemu ya sukari ambayo iligawanywa leo

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said amewaonya watumishi wa umma mkoani humo kuacha kujihusisha na masuala ya magendo huku akiwaambia kwamba kufanya hivyo ni kudhoofisha juhudi za serikali kukusanya mapato.

Mhandisi Zena aliyasema hayo leo wakati akikabidhi msaada kwa magereza yaliyopo mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto, watu wenye mahitaji maalumu na vuti vya kulea wazee ambavyo vimetolewa na Kamisha wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA nchini kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 217(2)(a) cha sheria za forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki cha mwaka 2004.

Kupitia kifungu hicho Kamisha huyo ameamua kutoa msaada ya vyakula ambavyo ni sukari na mafuta ya kupikia kwa magereza yaliyopo mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto, watu wenye mahitaji maalumu na vituo vya kulea wazee

Vyakula hivyo vinatokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo mkoani Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo kutokutoa mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa.

Alisema kwamba lazima watumishi hao wa umma wawe mstari wa mbele kuwafichua watu wanaohusika na biashaza magendo badala ya kushirikiana nao katika kuingiza bidhaa hizo kwa njia za panya ambapo wanachangia kuikosesha serikali mapato ambayo ndio yanasaidia kuchochea ukuaji wa maendeleo kwa wananchi.

“Ndugu zangu watumishi wa umma jiepusheni na magendo na anzeni kuwafichua wanaoingia magendo na wananchi endelee kutoa taarifa kwani tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kumaliza kabisa suala la biashara za namna hiyo “Alisema Ras Mhandisi Zena.

Hata hivyo Katibu tawala huyo aliipongeza mamlaka hiyo kwa kujielekeza kwa taasis hizo kwa kuzipa ahueni kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa waledi kwenye kukamata bidhaa hizo.

“Bidhaa hizo zimekatwa kwa sababu zilitakiwa kulipa kodi ya serikali imeshindikana na kama zingekuwa zimepita kinyemela zingeipa hasara serikali hivyo niwapongeza TRA kwa na Kamishna wa Forodha kwa kufanya kazi kubwa na nzuri kupambana na vitendo vya namna hiyo”Alisema

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitu hivyo Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoani Tanga (TRA) Speciaoza Owure alisema kwamba mzigo huo ulitaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu za forodha hivyo kamisha wa Idara ya Forodha kuamua kutoa msaada kwa taasisi mbalimbali.

Alizitaja taasisi hizo ni vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu na Magereza ambao waligawiwa vyakula hivyo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi katika halfa iliyofanyika mjini Tanga

“Kwa niaba ya Kamisha wa Forodha tunaomba uridhie kugawa vyakula hivyo vinavyotokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo mkoani Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo kutokutoa mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa”Alisema Meneja huyo wa TRA Mkoa wa Tanga.

Alizitaja bidhaa ambazo ziligawiwa ni mifuko ya sukari 278 yenye ujazo wa kg 50 ambazo thamani yake ya kiforodha ni milioni 12.7 na kodi ya forodha ilitakiwa kuwa milioni 12,791,391.60 na VAT milioni 4,604,900.97 .

Aidha waligawa pia madumu 1241 ya mafuta ya kula yenye lita 20 kila mmoja thamani yake ya forodha ni milioni 43, 191, 652.14 na ushuru wake ni milioni 15,117,078.24 na VAT yake ni milioni 10,495,571.44 kwa hiyo thamani ya vifaa vilivyogawiwa ni vyenye thamani ya bilioni milioni 55,983,043.74 zenye thamani ya ushuru wa forodha miloni 27,908,469.84 na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ni miloni 15,100,472.41.

Hat hivyo alisema vifaa vyote hivyo ambazo viligawiwa vilikuwa na thamani ya milioni 55,983,043.74 na kodi ni sh.milioni 43,008,942.25.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Magezera Mkoa wa Tanga Kamisha wa Msaidizi Emanuel Lwenga alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo kutokana na wao kuwa na wanawahitaji wengi jumla ya wafungwa 1508 wote wanahitaji kupata chakula.

Alisema hivyo wanashuruku kiasi walichowapatia ambapo sukari wamepata jumla ya kilo 9400 na hivyo itasaidia kuwalisha wafungwa kwa kipindi cha miezi sita mkoa wa Tanga mzima huku mafutaa kilo 17442 waliokabidhiwa itasaidia kuwalisha wafungwa mkoa mzima kwa mwaka mzima.

“Lakini pia nitoe wito kwa wakati mwengine msisite kutuma msaada kwani bado tunauhitaji mkubwa kwani wafungwa bado wapo na wataendelea kuwepo hivyo misaada ni muhimu sana kwao “Alisema .

ANANIA NGOLIKA MWENYE UWEZO MKUBWA KATIKAMUZIKI LICHA YA ULEMAVU WAKE WA MACHO.

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi,Tabora.

Novemba, 2019.
Nchini Marekani yupo mwanamuziki Steve Wonder mwenye ulemavu wa macho aliye na ukwasi mkubwa unaomuweka katika nafasi ya kuwa miongoni wa wanamuziki matajiri duniani.

Miaka ya 1980 na 1990 alikuwepo mtunzi na mwimbaji katika bendi ya Juwata raia kutoka nchini Kenya, Niko Zengekala, aliyekuwa na ulemavu wa macho pia. Aliweza kuzikonga nyoyo za wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi kwa tungo halikadharika uimbaji wake. Hii ni kudhihirisha kuwa ulemavu siyo sababu ya kubweteka.

Makala haya yanamzungumzia mwanamuziki Anania Ngoliga, mwenye talanta nyingi katika muziki. Amepitia vikwazo vingi vikiwamo vya kubezwa na kufuatia ulofa na ulemavu wake wa macho.

Wasifu wa Ngoliga aliwahi kuelezea kuwa pamoja na kuwa yeye ni mwanamuziki, hajui alikojifunza ala inayoitwa Kalimba, inayotumiwa na wasanii wa eneo lao la Mpawapwa mkoani Dodoma ila alijikuta tu analijuwa.

Ngolinga yaelezwa kuwa alipozaliwa baada ya kupata ufahamu, aliwaona baba pamoja na baba zake wadogo wote wakipiga ala hiyo.

Alisema kuwa hata dada zake watoto wa baba yake mdogo walikuwa mabingwa wa kupiga Kalimba. Kwa kawaida Anania nimcheshi kila wakati, anakumbuka wakati akiwa bado mdogo yeye na ndugu zake walikuwa wakishindana kupiga ala hiyo.

Anania alizaliwa akiwa na udhifu wa kuona vizuri, tatizo hilo liliendelea hadi alipofikisha umri wa miaka mitano, macho yake yakaanza kupoteza uwezo wa kuona kabisa.

Alipelekwa kwenda kuanza shule ya Wasioona ya Buigiri, lakini anakiri na kutoa shukurani nyingi kwa mwalimu wake Abel Mbata. Mwalimu Mbata alikuwa anafundisha hapo Buigiri ndiye aliyemshawishi babu yake ili aweze kujiunga na shule hiyo.

Baba yake Ngoliga baada ya ushawishi huo akafanya mipango yote ya yeye kujiunga na shuleni hapo rasmi.Katika shule ya Buigiri kulikuweko na magitaa na piano na vyombo vingine vya kisasa, hivyo Anania akajifunza pia kupiga vyombo hivyo.

Kufikia darasa la nne tayari alikuwa kiongozi wa kwaya ya shule yake hiyo ya Buigiri.Aliendelea na masomo shuleni hapo hadi alipomaliza darasa la saba mwaka 1976, mara baada ya kumaliza alirudi kwao Mpwapwa mkoani Dodoma.

Anania alipofika Mpwapwa akajiunga na kwaya ya Kanisa Kuu la Anglican la Mpwapwa, ambako hata huko baada ya muda mfupi akawa mwalimu wa Kwaya hiyo.

Mwaka 1987 aliamua kwenda katika jiji la Dar es Salaam akasindikizwa na rafiki yake kwa ajili ya kumsalimia dada yake aliyekuwa kaolewa huko, aliyekuwa akiishi maeneo ya Msasani. Kwa bahati nzuri jirani na alipofikia kukawa na jamaa aliyekuwa na gitaa.

Hivyo Anania Ngoliga akawa anaachiwa kupiga gitaa hilo mara kwa mara, jambo ambalo likamfanya shemeji yake amuulize kwanini asijiunge na mojawapo ya bendi.

Kwakuwa mmiliki wa hilo gitaa alikuwa anawafahamu baadhi ya wanamuziki wa bendi iliyojulikana kama Jambo Stars, iliyokuwa mali ya Dk. Vulata, ikiwa na makao makuu huko Komakoma maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Hivyo Anania akaenda kuonana na wanamuziki wa bendi hiyo na kujitambulisha kama yeye anauwezo wa kuimba, huku akilazimika kuficha kuwa anajua kupiga gitaa.Alifanya hivyo baada ya kuingiwa na hofu alipowasikia wapigaji wa magitaa waliokuweko katika bendi hiyo wakati ule, ambao walikuwa wazuri sana.

Ngoliga aliwakuta wanamuziki walikuwapo katika bendi hiyo ya Jambos Stars akina Kazembe wa Kazembe, Cobra wa Bilumba ambao wote walikuwa wapigaji wazuri wa magitaa.Alikuwapo Omari Gendaeka aliyekuwa akiliungurumisha gitaa la besi na mwingine aliyekuwa akijulikana kwa majina ya Cheo Ali.

Anania Ngoliga alifanyiwa usaili na akaonekana anafaa, hivyo akawa mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo ya Jambos Stars.Aliendelea kupiga katika bendi hiyo mpaka siku moja ambapo mwanamuziki aliyekuwa raia toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lovy Longomba, alipita kuangalia mazoezi yao.

Baada ya kumshuhudia Ngoliga na kubaini uwezo wake, Lovy muda uleule akatamani kumchukuwa awe katika bendi yake ya Afriso Ngoma.Lovi Longomba akaenda kwa shemeji yake Anania, kumuomba amshawishi Anania ajiunge na Afriso Ngoma. Bendi hiyo ilikuwa ni mali ya mzee Mwendapole na Lovy akiwa kiongozi wa bendi.

Anania alitamka kuwa kitendo hicho aliona kama ni ndoto, kwakuwa hakikupita kipindi kirefu tangu afike katika jiji hilo akitokea Mpwapwa. Aidha alikuwa hajawahi kupigia bendi yoyote, ikaona maajabu pale alipoombwa na mwanamuziki kama Lovy Longomba kwenda kujiunga na bendi yake ilikuwa kama ndoto.

Anania Ngoliga hakufanya ajizi alienda kuripoti katika bendi hiyo ya Afriso Ngoma. Lakini kwa bahati mbaya siku alipofika huko, ilikuwa ndio siku Lovy alikuwa anasafiri. Hata hivyo Lovy aliacha maagizo kwa wanamuziki wenzake kuwa wampokee Anania, kwa uhakika zaidi wamfanyie mahojiano.

Kama Waswahili wasemavyo kuwa “Hakika asiyekujuwa hakuthamini…” hakuna mwanamuziki yeyote miongoni mwao aliyeshughulika naye.

Fikra tele zikamjaa Anania akidhani kuwa yawezekana wenzake hao walimdharau kufuatia udhalili aliokuwa nao,hakuwa hana hata viatu, alikuwa amevaa viatu vya matairi alivyotoka navyo Mpwapwa.

Alienda mbali zaidi akijihisi kuwa labda ulemavu wake wa macho umewafanya wasimtilie maanani.

Baada ya wiki mbili Lovy alirejea akakuta mahojiano hajafanyiwa. Akamuomba aimbe, nae akaimba vizuri baadhi ya nyimbo za Afriso, nakujikuta yuko katika neema kubwa kwani baada ya jaribio hilo akapata ajira mara moja.Wakati huo huo waimbaji wawili wa bendi hiyo Kasavubu na Anderson Supa wakaachishwa kazi.

Bendi ya Afriso Ngoma ilikuwa na imesheheni wanamuziki waliokuwa na uwezo mkubwa katika muziki. Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja na John Maida, Robert Tumaini Mabrish, Mjusi Shemboza, Kasongo Kalembwe, Peter Kazadi wote hao walikuwa wakishika ala za muziki.

Kwa upande wa waimbaji walikuwa Lovi Longomba, Ramadhani Kinguti ‘Systeme’, Tofi Mvambe na mwenyewe Anania Ngoliga.Bendi hiyo iliweza kurekodi nyimbo nyingi ikiwemo ya ‘Elly wangu’ vilevile ilipata fulsa ya kusafiri karibu wilaya zote hapa nchini.

Ngoliga baadaye aliamua ‘kuitosa’ Afriso Ngoma, akahamia katika bendi ya Legho Stars iliyokuwa imeanzishwa.Kwa mara ya kwanza bendi ya Legho Stars ilipoanzishwa waimbaji walikuwa yeye Anania Ngoliga, Tshibanda Sonny, Marcelino Vitalis na Lucy Emea. Kwa upande wa wapiga vyombo walikuwapo akina Stamili Uvuruge, Chris Chiwaligo, George Mtully na Hemed Mganga.

Bendi ya Legho Stars nayo ilionja hamahama ya wanamuziki wake. Kama ilivyo kawaida ya wanamuziki kuhamahama, Legho Stars iliondokewa na wanamuziki wake akina Stamili Uvuruge pamoja na Tshibanda Sonny.

Ili kuiamarisha bendi hiyo, iliwasajiri wanamuziki wengine akiwemo mtunzi na mwimbaji Tshimanga Kalala Assosa, Jemsia Msuya, John Maeda na Shaaban Manyanya kwa pamoja wakaianza Legho Stars ya awamu ya pili.

Ngoliga bado safari yake ya kutafuta ilikuwa haijakamilika. Hakukaa sana katika bendi hiyo ya Legho Stars akaenda kujiunga na kundi la Ram Choc Stars liliyokuwa linaongozwa na mwanamama Rukia Mtama.

Katika bendi hiyo ilikutana na waimbaji wengine ‘wakali’ akina Banza Tax, Salim Shaaban, Adiel Makula, Chris Chiwaligo, Ado Mpoloto , Geofrey Charahani na kwenye upigaji wa gitaa la rhythm, alikuwa ni Yahaya Mkango.

Ram Choc Stars ilipata mkataba katika Iringa hotel,iliyopo mjini Iringa.
Wanamuziki takribani wote walitimka wote kwa pamoja siku ya mwaka mpya 1991, wakaiacha bendi hiyo wakilalamika kutolipwa mishahara.

Ule msemo wa Waswahili kwamba “Usiache mbachao kwa msala upitao” Ngoliga baada ya ‘mtiti’ wa wanamuziki wa bendi nzima kuhama Ram Choc Stars, aliamua kurejea tena Legho Stars wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Joseph Mulenga ‘King Spoiler’ aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo.

Wanamuziki wengine waliokuwepo ni John Maida, alikuwa akipiga gitaa la rhythm na Christopher Chiwaligo na gitaa la besi lilikuwa likiungurumishwa na Adolf Mpoloto.

Waimbaji walikuwa Ana Mwaole, Banza Tax, Salim Shaban na yeye Anania Ngoliga.

Lakini kama nilivyokujuza msomaji wa makala haya kwamba Anania alikuwa mtafutaji. Kwa mara nyingine tena akaiacha bendi hiyo na kuhamia kwenye bendi iliyokuwa mbioni kuanzishwa ya Ngoza Makayota.Juhudi za kuanzisha bendi hiyo ziligonga ukuta baada ya danadana za ahadi zikawa nyingi bila kununuliwa vyombo vya muziki.

Wanamuziki hao wakawa wanafanya mazoezi bila kupiga dansi. Hali hiyo ilipelekea yeye na wanamuziki wenzake wakaondoka tena kundi zima na kwenda Iringa. Huko wakajiunga na bendi iliyokuwa inaendeshwa na kanisa Katoliki la Mshindo iliyokuwa inaitwa VICO Stars (Vijana Catholic Stars). Hata huko hawakukaa muda mrefu katika bendi hiyo kufuatia masharti magumu na pia haikuwa na fedha za kuwalipa, maonyesho yake yalikuwa machache sana ambayo karibu yote yalifanywa vijijini.

Wanamuziki hao watano wakakimbilia kwenda mji mkuu wa Tanzania Dodoma. Wakati walipokuwa safarini kwenda Dodoma na kujiunga na bendi ya Materu Stars, kwa bahati mbaya hawakupata nafasi ya kufanya onyesho lolote kutokana na tatizo la kukosekana kwa vyombo.

Wakati wakihangaika siku moja wakatembelewa na mwanamuziki Kasaloo Kyanga wakiwa mazoezini. Kasaloo aliwaambia kuwa wanahitajika tena mjini Iringa ambako kulikuwa na bendi ikitarajiwa kuazishwa.

“Mtafuta hachoki akichoka kaisha pata” mseomo huu ulijionesha wazi baada ya Ngolika na wenzake wakaamua karudi Iringa, wakaanzisha bendi ya Living Light mwaka 1993 mwishoni.Bendi ihiyo ilianza kupiga katika hoteli ya Living Light, iliyokuwepo eneo la Wilolesi mjini humo.

Bendi yao hatimaye ikapata mkataba wa kupiga muziki Dodoma Hoteli, tatizo lilikawa kwa mmiliki wa bendi aliyetoa amri kuwa wanamuziki wapige muziki bila kulipwa chochote hadi pale atakaporudisha fedha alizonunulia vyombo.

Amri hiyo ililikuwa gumu wakikumbuka kuwa hakukuweko na makubaliano yoyote kati ya wanamuziki na mwenye mali katika mkakati wa kununua vyombo.Kafuatia haIi hiyo ikalazimu wanamuziki waondoke kwenye bendi hiyo baada ya kufanyaka ‘Varangati’ kubwa.

Wakapata taarifa kuwa kuna shirika lilioitwaTACOSODE lilikuwa na vyombo vya muziki, hivyo kundi hilo lilijiunga na na kutengeneza bendi ya TACOSODE mwaka 1995.

Anania aliweza kuendeleza bendi hiyo hadi mwaka 2002, vyombo vyao vilipo chakaa kufika hali ya kutoweza kutumika tena.Tahfif katika maisha yalianza kuonekana baada ya kujiunga katika bendi ya Tango Stars, ambapo walikuwa wakilipwa mishahara. Lakini ghafla mwenye bendi akaamua kushusha mishahara yao.

Wanamuziki hao wakawa hawana jinsi ila kuiacha bendi hiyo ambapo Anania akahamia katika bendi ya Karafuu huko Zanzibar.Anania Ngolika aliamua kwenda kujiunga katika bendi ya Kalunde inayoongozwa na Deo Mwanambilimbi ambako ndiko yuko mpaka sasa.

Kwa makala haya natumani mpendwa msomaji utakuwa umemfahamu Anania Ngolinga, jinsi alivyofanya kila aina ya jitihada kutimiza malengo yake ya kuwa mwanamuziki pasipo kukata tamaa. “Penye nia pana njia”

Hili ni fundisho tosha kwa wanamuziki wanaochipukia kuto bweteka baada ya kutoa single moja!


Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba 0784331200 na 0713331200.


DICOTA 2019 HEALTH FORUM IN PICTURES

$
0
0
MOBILZE4HEALTH

On November 9th, 2019, The Diaspora Council of Tanzanians in America (DICOTA) hosted a health forum: Mobilize4Health: Galvanising Diaspora Action to Advance Health in Tanzania at Howard University Law School, Washington, DC. Professionals attended from Tanzania and within the U.S. Diaspora, Germany, the United Kingdom and Canada encompassing government Officials, healthcare professionals (doctors, nurses and administrators), public health interventionists, business and non-profit leaders. Event proceedings will be released next week, in the meantime we would like to share these photos.

We are thankful for all those who made this event possible.
DICOTA 2019 Health Forum Planners and guests 

Registration desk volunteers

Dr. Mary Banda with Ambassador Liberata Mulamula

Ambassador Liberata Mulamula with Ms. Elvira Williams of AHEAD Inc.

Dr. Frank Minja, DICOTA President presenting on his work on Intervention Radiology. Collaboration between Yale University and Muhimbili University of Health and Allied Sciences

Mr. Salum Omar of Greenlight Foundation Tanzania

Kevin White, Globan Vision 2020

Gale O'Sullivan, George Washington University McDonough School of Business

Dr. Seche Malecela, Dr. Mary Banda and Dr. Henry Ziegler

Panel on Health Ventures in Tanzania;Representatives from USAID, Greenlight Foundation, Health Tanzania Foundation, St. Francis Hospital, Georgetown University.

Panel on Human Resources for Health

Click soma zaidi for more photos

Dr. Harieth Gabone-Mwalupindi-South University

Dr. Martha Mkony- Muhimbili University of Health and Allied Sciences

Dr. Gideon Mlawa-Tanzania UK Healthcare Diaspora Association - TUHEDA

Dr Eliford Kitabi-U.S. Food and Drug Administration

Dr.Vincent Rwehumbiza, Munich Germany (YEBI Health)

Joyce Matondane- Azania Capital/Physiocare

Allen Chacha- Blue Cross & Blue Shield

Mr. Tony Goodesmith- Standard Med

Dr. Imani Kondo- Tanzania UK Healthcare Diaspora Association - TUHEDA

Dr. Mohamed Manekia 

Christina Lasway- DICOTA Board Member/Azania Capital/DAMAX Solutions

Mr. Lunda Asmani- Past Board Chair DICOTA

Dr. Kurwa Nyigu-Past DICOTA Board Member

Justa Lujwangana, founder of Curious on Tanzania

David Mrema-Pamoja We Can Harambee USA

Dr. Anita Mwalui- Montgomery College

Patrick Liganga -AmericaCargo Express LLC

Dr. Charles Bishota- Past DICOTA President/Bishota Law

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Dr. Seche Malecela, Lunda Asmani, Dr. Ndaga Mwakabuta, Fred Mjema and Patrick Liganga 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Delegate lunch and networking at Howard Law School Cafeteria 

Kwame Kinabo, Conrad Kwayu, Lunda Asmani- DICOTA Board of Trustee Members 

Jameela Baruti and Shufaa Misana from the DMV Community 

Ms. Asinath, Dr. Susan Nkurlu and Justa Lujwangana 

Ms. Asinath, Dr. Susan Nkurlu and Justa Lujwangana 

Oliva Kavishe leading the Howard University student volunteers 

The After Party at Serengeti Club 


Huduma Ya Matibabu Bure Yatolewa Wilayani Urambo

$
0
0

Na Editha Edward -Tabora 

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amezindua huduma ya Matibabu ya bure ya kibingwa wilayani Urambo Mkoani Tabora ambapo huduma hiyo inatolewa kwa siku tano na timu ya madaktari bingwa 45 wa JITOLEE group ambayo yanaratibiwa na familia ya hayati Samweli Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri Ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kuenzi mchango wake katika jumbo la Urambo

Akizindua Matibabu Hayo Mwanri amesema huduma hiyo ni muhimu sana hivyo wananchi wa urambo wanatakiwa kutoipuuzia na wajenge utamadumi wa kwenda hospitali ili waweze kuangalia afya zao na kufata masharti watakayo pewa na madaktari 

"Sisi tunapenda mambo ya kupuuza watu zamani tulikuwa tunakula magimbi viazi mchemsho magimbi mboga za majani matunda lakini siku hizi tumekalia kula chipsi Ndo maana magonjwa makubwa kama presha tunayapata tunatakiwa tupunguze"Amesema Mwanri

Kwa upande wake Mbunge Wa Urambo Magreth Sitta amesema yeye na familia yake walikubaliana kuendesha zoezi hilo Ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Samweli Sitta kwa wananchi wa wilaya ya Urambo"kama mapenzi ya Mungu Yametimizwa hivyo tumeamua kuangalia jinsi gani tunaweza kusaidia jamii inayotunzunguka katika kuangalia afya za kina mama na kupimwa magonjwa mbalimbali yakiwemo meno, macho na kupima afya zao kwa ujumla "Amesema Magreth

Nae Mwenyekiti wa JITOLEE group Daktari Erick Muhumba amesema wanategemea kuona watu wengi zaidi katika huduma hiyo ambapo ametoa takwimu kwa mwaka 2017 wananchi waliojitokeza kuangaliwa afaya zao walikuwa Elf moja Mia moja kumi na nane na mwaka 2018 walikuwa Elf moja mia nne thelathini na nane

Aidha huduma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa Wilaya ya Urambo hivyo wananchi hao wanatakiwa kutosita kwenda kuangaliwa afya zao ili kupunguza adha ya kwenda kutibiwa nje ya Mkoa Wa Tabora. 
Madaktari bingwa 45 wa JITOLEE group ambao wanatoa huduma ya kupima magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya ya Urambo
Mbunge wa jimbo la Urambo Magreth Sitta akizungumza katika uzinduzi huo wa Matibabu bure ambayo unaratibiwa na familia ya hayati Samweli Sitta.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza katika huduma ya Matibabu bure wilayani Urambo

JAJI MKUU AWATAKA MAHAKIMU KUANZA KUZIPITIA SHERIA ZA UCHAGUZI

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mohamed Mtanda kitabu kinachoonyesha Mpango wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania alipofika ofisini kwake kumtembelea akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Rukwa.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya  ya Nkasi alipomtembelea Mkuu wa wilaya hiyo ofisini kwake akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Rukwa.
 Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nkasi wakimsikiliza Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa wilaya ya Nkasi waliofika Mahakamani kupata huduma za kimahakama.


Na Lydia Churi-Mahakama Rukwa


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mahakimu nchini kuanza kuzipitia Sheria na kanuni zinazohusu uchaguzi ili kujiandaa kusikiliza kesi za uchaguzi.


Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi wakiwemo Mahakimu, Jaji Mkuu amewataka Mahakimu kuanza kujiandaa kusikiliza kesi za uchaguzi kwa kuwa mwaka huu nchi itafanya uchaguzi wa Serikali za mitaana baadaye mwakani uchaguzi mkuu.


Aidha, Jaji Mkuu pia ameagiza Mahakimu kutochelewesha kesi za uchaguzi kwani alisema kwa kufanya hivyo wataweza kuiingiza Mahakama kwenye migogoro. Aliongeza kuwa endapo kesi hizo zitasikilizwa kwa mujibu wa sheria na kumalizika kwa wakati zitasaidia kuifanya Mahakama kuendelea kuaminiwa zaidi na wananchi.


Alisema endapo Mahakimu watazipitia sheria na kujiandaa vema kusilikilza kesi hizo kni wazi kuwa hawatababaishwa mahakamani. “Hakimu anayefahamu sheria na taratibu hawezi kubabaishwa awapo Mahakamani”, alisema Jaji Mkuu.


Jaji Mkuu pia amewataka Mahakimu kutojihusisha na masuala ya siasa ili waweze kuwa huru katika kutatua migogoro mbalimbali itakayoletwa kwao. Alifafanua kuwa Sheria inamkataza Jaji, Msajili, na Hakimu kujiunga na chama chochote cha siasa ili waweze kutatua migogoro inayoletwa kwao. 

Awali akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Said Mohamed Mtanda, Jaji Mkuu amesema Mahakama ya Tanzania inao mpango wa kuwa na mahakama za Mwanzo za kisasa kwenye kwenye kila tarafa kwa nchi nzima ili kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi.


“Tutahakikisha tunajenga Majengo ya kisasa ili endapo tarafa husika itakuwa wilaya basi majengo hayo yawe na hadhi ya kuwa Mahakama za wilaya”, alisema Jaji Mkuu. Alisema Mahakama itaiomba Serikali Kuu kupeleka fedha za ujenzi wa majengo hayo kwenye halmashauri ili halmashauri zijenge.


 “Sisi tutatoa ramani za majengo, tutatafuta na fedha ili halmashauri zijenge kwa kuwa tayari zinao uzoefu katika kujenga vituo vya afya hivyo na jukumu la kujenga Mahakama za Mwanzo mlibebe.”


Awali akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Said Mohamed Mtanda alipomtembelea ofisini kwake, Prof. Juma alihimiza ushirikiano wa Mahakama na mihimili mingine kwa kuwa Katiba ya nchi pia inatambua na imegawa majukumu kwa kila mhimili ambapo mihimili yote humtumikia mwananchi.


Naye Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Said Mohamed Mtanda amesema Serikali wilayani humo itashirikiana na Mahakama ya Tanzania kwa karibu ili kuhakikisha wananchi wa wilaya hiyo wanapata huduma zote muhimu zikiwezo huduma za mahakama.


Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Rukwa ambapo leo alitembelea Mahakama za wilaya ya Nkasi na Namtumbo.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 13,2019

USHIRIKISHWAJI WENYE USAWA KATIKA UTAFITI KULETA MATOKEO CHANYA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika wiki ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. kulia ni Mratibu wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Theophilus Mlaki.

Mratibu wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Theophilus Mlaki akifafanua jambo katika mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
USHIRIKISHWAJI wenye usawa kwa nchi 15 zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu utaleta matokeo chanya katika tafiti za masuala ya kisayansi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika wiki ya   Sayansi, Tenkolojia na Ubunifu. Katika Mkutano huo amesema kuwa mijadala iliyopo ni katika kushirikiana na kuafikiana ili tafiti zinazofanywa ziwe na matokeo chanya.

Dkt. Nungu amesema kuwa ili kuwe na matokeo chanya ya tafiti za kisayansi lazima kuwe na data wazi ili kuweza kushirikisha nchi nyingine kwaajili ya kupata matokeo mazuri zaidi.

"Katika tafiti na ubunifu kwa maendeleo lazima malengo ambayo serikali na wawekezaji wameyaweka lazima yaonekane hata kwa mwananchi wa kawaida aweze kuona nini kinatokea". Amesema Dkt. Nungu.

Hata hivyo Dkt Nungu amewaomba nchi zilizoendelea kiutafiti kutokuficha baadhi ya vitu katika kufanya utafiti ili nchi za Afrika zikakosa ndio maana mkutano unasisitiza tafiti shirikishi na zenye usawa ili kuwepo na usawa kwa nchi zinazotoa ufadhili na nchi zinazopokea ufadhili katika tafiti za kisayansi.

"Tukiwa na Tafiti wazi na shirikishi mtafiti aweze kuomba takwimu  au data zilezile ambazo mwingine amezitumia akazifanyia kazi  kama sio wazi aliyefanya utafiti kwa mara ya kwanza atazifungia na mwingine atakayetaka kufanya utafiti ule ule lazima aanze mwanzo". Amesema Dkt. Nungu

Katika mjadala huo changamoto iliyojitokeza ni miundombinu ya maabara za kisasa kwa nchi za Afrika ukilinganisha na nchi nyingine.

Ili serikali ipate matokeo mazuri na makubwa lazima wanasayansi kuonyesha kuwa wanaweza na wajitume.

WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKO LA MIKINDANI MKOANI MTWARA WAOMBA KUJENGEWA CHOO

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Balozi Mushi (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG ambao wapo katika ziara ya kuwahamasisha wanawake wafanyabiashara masokoni wa mkoa huo kujiunga katika umoja wa kitaifa.
Afisa mradi wa shirika EfG, Susan Sitta akimkabidhi mfuko wenye machapisho mbalimbali kutoka EfG, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Balozi Mushi.
Meya wa Manispaa ya Mkoa wa Mtwara, Geofrey Mwanchisye (kushoto), akiwa amebeba mfuko wenye machapisho mbalimbali kutoka EfG.
Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG wakimsikiliza Meya wa Manispaa ya Mkoa wa Mtwara, Geofrey Mwanchisye (hayupo pichani)
Meya wa Manispaa ya Mkoa wa Mtwara, Geofrey Mwanchisye (wa tatu kutoka kulia walioka), akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake wajasiriamali kutoka katika masoko ya jijini Dar es Salaam ambao wapo ndani ya Shirika la EfG ambao wapo katika ziara ya kuwahamasisha wanawake wafanyabiashara masokoni mkoa huo kujiunga katika umoja wa kitaifa. 



Na Mwandishi Wetu, Mtwara.

WANAWAKE wajasiriamali katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo (Sauti ya Mwanamke Sokoni) wameiomba halmashauri hiyo kuwaboreshea mazingira ya vyoo kwenye kazi zao hizo hususani matundu ya vyoo kwani yaliyopo ni machache ikilinganishwa na uwingi wao.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki na wanawake hao wakati wa ziara ya mafunzo kwa wajasiriamali hao iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na shughuli ya kuinua maendeleo ya sekta isiyo rasmi hapa nchini hasa kwa wanawake la Equality for Growth (EfG ) lenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo yameambatana na kutambulishwa kwa mradi huo wa Sauti ya Mwanamke Sokoni mkoani hapa wenye lengo la kuhamasisha wanawake wafanyabiashara katika manispaa hiyo na mkoa kwa ujumla kujiunga na umoja wa wanawake sokoni wa kitaifa ambapo kwa sasa Mtwara mradi unatekelezwa kwenye Soko Kuu, Saba saba pamoja na Magomeni.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake kutoka Soko Kuu la Mtwara Magdalena Malembe alisema masoko yao kwa sasa yanakabiliwa na changamoto hiyo kutokana hayana vyoo vya kutosha kwani wanawake wametengewa matundu mawili ya vyoo sokoni hapo lakini tundu moja tu ndio linalotumika.

"Halafu humo humo sisi wanawake huwa tunakutana na changamoto kwani wanaume wanaingia mle mle kwenye chumba chetu inatukwanza lakini kwa vile sisi inaonekana ni viumbe dhaifu basi tunatumia hivo hivo",Alisema Malembe

Hata hivyo ameongezs kuwa, " Ila halmashauri yetu mnapaswa mtambue sisis akina mama wafanya biashara wa sokoni tunafanya kazi katika mazingira yasiyo rafiki",

Wanawake hao ni viwanda lakini pia wanazalisha Taifa kwani rasirimali watu hutokana na akina mama kwahiyo shimo hilo moja la choo huingia akina mama hao na watoto sssa wakiingia akina baba huwa wanaharibu mazingira hivyo upo uwezekano mkubwa watu hao kuweza kupata madhara kiafya.

Charles Chambea, Katibu wa Soko la Saba saba ametilia mkazo na kusisitiza juu ya changamoto hiyo na kwamba kutokana na uwingi wa wajasirimali hao kwa siku za usoni halmashauri kuona umuhimu wa jambo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitoka kwa watu hao.

Afisa mradi wa shirika hilo Susan Sitta alisema, mradi huo unalenga kuwakomboa wanawake kwani wanaonekana kupata faida, thamani ndogo ya bidhaa zao na wengi wao wanapata chini ya shingi elfu 7000/- kwa siku na asilimia 86.2 hawabaki na kiasi chochote au hubaki na kiasi kudogo kwa ajili ya chakula na mahitaji ya lazima.

Meya wa Manispaa hiyo Geofrey Mwanchisye amewatoa hofu na kuahidi kufanyiwa kazi changamoto hiyo inayowakabili wajasiriamali katika maeneo hayo huku akiwaomba kuwa na matumaini katika hilo.

Mradi huo kwa sasa unatekelezwa katika mikoa tisa hapa nchini ikiwemo Iringa, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Lushoto-Tanga, Musoma, Lindi, Mtwara na Dar es salaam yenye jumla ya wanachama 6500.

MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA KATAZO LA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0

Ndugu Wanahabari, 

Kama mnavyofahamu Serikali ilipiga marufuku uingizaji, uzalishaji, usafirishaji, na matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini tangu tarehe 01 Juni, 2019. 

Chimbuko la katazo hili lilitokana na changamoto za kiafya na mazingira zitokanazo na mifuko ya plasitiki ambazo ni pamoja na: Kudumu katika mazingira 

kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 500 na hivyo kuleta athari za muda mrefu; Kusababisha vifo vya mifugo, wanyama na viumbe wa baharini wanapokula na kumeza mifuko ya plastiki; Kuchangia uchafuzi wa mazingira kutokana na kuzagaa ovyo katika mazingira; na Kuziba mitaro ya maji ya mvua, miundombinu ya maji na majitaka na kusababisha mafuriko na kuenea kwa magonjwa ikiwemo malaria na kipindupindu. 

Katika kuratibu katazo hili Ofisi ya Makamu wa Rais imeunda kikosi kazi chenye jumla ya wajumbe 32 kwa nia ya kufuatilia kwa kushirikiana na vyomo vingine vya Serikali, utekelezaji wa Sheria na changamoto za katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki. 

Kufuatia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, pamekuwepo na fursa mbalimbali za kuwekeza katika kuzalisha na kuingiza nchini mifuko mbadala wa plastiki ikiwemo mifuko ya karatasi, nguo, katani pamoja na mifuko ya non- woven. Wadau wengi wamejitokeza kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko husika. Kabla ya katazo, katika kipindi cha mwezi Januari-Mei, 2019 jumla ya tani 197.8 za mifuko ya non-woven ziliingizwa nchini .Aidha, katika kipindi cha mwezi Juni – Oktoba, 2019 jumla ya tani 757.1 za mifuko mbadala ziliingizwa nchini. 

Pamoja na mafanikio hayo, changamoto mbalimbali zimejitokeza ikiwemo wimbi la uingizaji wa mifuko mbadala aina ya non-woven ambayo haikidhi mwongozo wa viwango vilivyowekwa na TBS na pia; matumizi ya vifungashio vya mifuko laini ya plastiki (plastic tubings) kama vibebeo vya bidhaa mbalimbali kama vile nyanya, karoti na njegere; na Uingizaji wa magazeti yaliyotumika kwa ajili ya kufungashia bidhaa katika maeneo ya masoko, maduka na maeneo mengine ya biashara. Hali hii ni makosa kisheria kuingiza nchini bidhaa ambazo hazikidhi matakwa ya kisheria pamoja na kubadili matumizi ya vifungashio kufanya vibebeo vya bidhaa. 

Mwongozo wa Viwango vya vya ubora wa mifuko ya non-woven umekwishatolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na umeainisha kuwa mifuko hii inapaswa kuwa na sifa zifuatazo: 
Uzito usiopungua GSM 70 (Gram per Square Metre) 
Iwe inaweza kurejelezwa (Recyclable) 
Ioneshe uwezo wa kubeba (Carrying capacity) 
Iwe na anuani ya mzalishaji au nembo ya biashara 
Iwe imethibishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) 

Hata hivyo kumekuwepo na waingizaji na wazalishaji wanaokaidi kwa makusudi matakwa ya viwango hivi hali ambayo inasababisha wazalishaji wa mifuko inayokidhi viwango kukosa soko na kukosesha Serikali mapato yatokanayo na uzalishaji wa bidhaa husika, kutishia ajira katika viwanda hivyo vya ndani, uharibifu wa mazingira na ukwepaji wa kodi utokanao na bidhaa kutotambulika na hivyo kuathiri mapato na uchumi wa nchi kwa ujumla. 

Katika jitihada za kudhibiti hali hii, shehena za mifuko mbadala isiyokidhi viwango vya ubora zimekamatwa katika maeneo mbalimbali. Kwa mfano, NEMC kwa kushirikiana na TBS wameendesha ukaguzi katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata mifuko ya Non-Woven isiyokidhi viwango zaidi ya pieces milioni 2 na rollers zaidi ya 200 kwa ajili ya kutengeneza non-woven. 

Mifuko hiyo imezuiliwa kuingia sokoni na hatua za kisheria zinaendelea. Vilevile, mifuko laini ya plastiki (plastic tubings) pieces 9,600 zimekamatwa Mwanza zikiwa kwenye magunia 8. Napongeza juhudi zinazofanywa na Mamlaka mbalimbali za Serikali ikiwemo NEMC, TBS na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudhibiti wimbi la uingizaji wa mifuko mbadala aina ya non- woven isiyokidhi viwango.

 Hata hivyo, nasisitiza ukaguzi uendelee kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini hususan kwa wazalishaji wa mifuko laini ya plastiki (plastic tubings), masokoni na maduka makubwa ili kudhibiti matumizi ya mifuko hiyo. Vilevile, napenda kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki kikamilifu na kutoa taarifa katika kutekeleza katazo hili la Serikali. 

Agizo! Naelekeza NEMC, TBS pamoja na kikosi-kazi cha kitaifa washirikiane kwa karibu na Kamati za ulinzi na usalama za mikoa, wilaya na mitaa nchini kuendelea kufanya kazi bila kuonea mtu yeyote katika kudhibiti matumizi ya mifuko mbadala aina ya non-woven na kudhibiti uingizaji, uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya non-woven isiyokidhi vigezo vinavyokubalika kisheria. 

Aidha, viko viwanda vinavyozalisha kwa kificho mifuko laini ya plastic na kuingiza sokoni kwa magendo, ufuatiliaji ufanywe na kuwabaini wazalishaji hao na hatua zichukuliwe dhidi yao zikiwemo kuteketeza bidhaa hizo ili iwe fundisho kwa wengine. 

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE 

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA.

UCHUMI WA VIWANDA KUPAISHA SEKTA YA USHIRIKA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Usirika Dkt. Titus Kamani akiongea na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Hivi karibuni Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Bw. Athanas Mutwe akiongea na watumishi wa Tume wakati wa Kikao cha Watumishi hivi karibuni
Kaimu Mrajis wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akisisitiza jambo wakati wa kikao na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Jijini Dodoma
 Bi. Veneranda Mugoba mtumishi wa Tume akichangia mada iliyokuwa ikiendelea wakati wa kikao cha Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma 
Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Watumishi na Viongozi wa Tume.
Kikao kikiendelea


Sekta ya Ushirika imetajwa kuwa moja ya maeneo muhimu ambayo yana fursa kubwa katika kushiriki na kuendeleza Uchumi wa Tanzania kupitia maendeleo ya Viwanda ili kuifikisha nchi katika Uchumi wa kati ifikapo 2025.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Dkt. Titus Kamani wakati wa kikao cha Watumishi wa Tume kilichofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni. Dkt. Kamani alieleza hayo alipokuwa akifafanua vipaumbele vya kuzingatiwa na Tume katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ni pamoja na kuhakikisha kuwa ajenda ya viwanda inakuwa ni miongoni mwa masuala muhimu katika mipango na mikakati ya Taasisi hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti huyo alieleza Sekta ya Ushirika katika harakati za kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye kuendeleza viwanda ni wakati muafaka sasa kwa kila mtumishi kuangalia namna bora anavyoweza kuja na ubunifu wa namna bora ya kusaidia kuongeza thamani ya mazao ya wakulima. Viwanda hivyo vikichakata mazao mbalimbali ya Kilimo, uvuvi, madini na mengine. Akiongeza kuwa viwanda hivyo vianzishwe kwa kuzingatia masuala yanayoleta changamoto sana katika Sekta ya Ushirika akitolea mfano eneo la vifungashio vya mazao eneo ambalo bado lina uhitaji mkubwa nchini.

“Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuchangia mawazo na utekelezaji wa maeneo ya kuendeleza, kuanzisha au kuboresha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao. Hivyo kuongeza mnyororo wa thamani,” alisema Dkt. Kamani

Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiongea na watumishi wa Tume katika kikao hicho alisema baada ya Vyama 4,413 kukaguliwa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika hivi karibuni Tume ichukue fursa hiyo kuendelea kuboresha taswira ya Sekta ya Ushirika kwa kutumia matokeo ya kaguzi zilizofanyika kwakuwa kaguzi hutoa picha na muelekeo wa utendaji.

Aidha, Dkt. Ndiege alisisitiza watumishi kufanya kazi kwa weledi na kutumia taaluma zao vizuri katika kutimiza wajibu na majukumu yao ili Tume iweze kutekeleza wajibu na matarajio makubwa ya wananchi na wanaushirika nchini.

Kaimu Mrajis aliongeza kuwa watumishi waendelee kuwa wabunifu kubuni miradi mipya, njia bora za utendaji ili huduma za Ushirika ziendelee kuwa bora na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za Ushirika katika maeneo mengi zaidi. Mrajis alishauri watumishi kuendelea kuibua tafiti na mawazo ya kuendeleza na kuanziasha viwanda vitakavyotumia malighafi kutoka vyama vya Ushirika. Akieleza kwa kufanya hivyo tutaisaidia Serikali kwa kuongeza ajira na kukuza pato la Taifa.

“Tuongeze hamasa na elimu ya Ushirika kwa wale ambao bado hawajajiunga na Vyama vya Ushirika ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wananufaika na Ushirika ili kupitia Ushirika wananchi waweze kupata maendeleo kwa urahisi pamoja na kunufaika na viwanda kupitia Sekta ya Ushirika. watumishi niwaombe muendelee kuandika mapendekezo mbalimbali yenye lengo la kutafuta ushirikiano na wadau wa maendeleo ili tukuze na kuendeleza viwanda vya Ushirika, alisema Dkt. Ndiege ” 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Bw. Athanas Mutwe akiongelea masuala ya kiutumishi katika kikao hicho alisema Watumishi ni kiungo muhimu sana chenye mchango mkubwa katika kuendeleza Sekta ya Ushirika na hatimaye kufikia Tanzania ya Viwanda. Bw. Mutwe aliwataka watumishi hao kuendelea kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma kwa manufaa yao binafsi na Taifa lote.

“Niwaombe watumishi wote kila mmoja wetu kuzingatie maadili ya utumishi wa Umma, tufanye kazi tukijua tumepewa dhamana ya kusimamia rasilimali na sekta muhimu ya Ushirika,” alisema Mutwe 

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilitoa fursa kwa watumishi wa Tume kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali ya mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Ushirika nchini ili kuongeza tija na ufanisi zaidi wa Sekta hiyo.

TASAF YAPONGEZWA NA KAMATI YA BUNGE KWA MAFANIKIO YA MALIPO YA RUZUKU KIELEKRONIKI KWA KAYA MASKINI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jasson Rweikiza (Mb) akifungua kikao kazi cha kamati yake naviongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mada kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodo
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Rehema Migilla (Mb) akichangia hoja kuhusu mada ya matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilshwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Mb) akifunga kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.

……………………..

Na. James K. Mwanamyoto – Dodoma

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umepongezwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa kupata mafanikio ya kulipa ruzuku kielektroniki kwa wakati, ufanisi na uwazi kwa kaya maskini katika maeneo 16 ya majaribio nchini ambapo ufanisi wa kuzihudumia kaya hizo umeboreka kwa kiasi kikubwa.

Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF kuwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Bw. Mwamanga amesema, malipo kwa njia ya kielektroniki katika maeneo 16 ya utekelezaji ambayo ni sawa na asilimia 10 ya walengwa yameongeza ufanisi na uwazi katika malipo, yanakwenda moja kwa moja kwa mlengwa aliyekusudiwa, yanawezesha uhakiki wa malipo kwa urahisi na kwa wakati, yanaongeza muda wa kufanya shughuli za maendeleo kwa walengwa, yanatoa fursa kwa walengwa kupata huduma bila usumbufu na yameipunguzia TASAF gharama za kuwasilisha ruzuku kwa walengwa.

“Asilimia 95 ya walengwa wanalipwa kwa njia ya mtandao kupitia simu za viganjani na asilimia 5 ya walengwa wanalipwa kupitia akaunti za benki”, amefafanua Bw. Mwamanga.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Angelina Malembeka (Mb) ameipongeza TASAF kwa ufuatiliaji mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Nchini hususani kwenye eneo la malipo kwa njia ya kielektroniki, hivyo kusaidia kuondoa udanganyifu uliokuwa ukifanywa kipindi cha nyuma na baadhi ya watendaji na walengwa wasio na uadilifu.

Naye, Mhe. Mwantum Haji ameipongeza TASAF kwa kufanya kazi vizuri na weledi hususani kwenye Mfumo wa Kupokea na Kushughulikia Malalamiko ya Walengwa ambapo wametoa elimu ya kutosha kwa walengwa kiasi cha kuwahamasisha kuutumia ipasavyo ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo ya malipo kwa njia ya kielektroniki na kuitaka TASAF kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuzikwamua kaya maskini kiuchumi.

Kwa upande wake, Mhe. Saada Mkuya (Mb) ameipongeza TASAF kwa utendaji kazi mzuri kwani faida ya utekelezaji mzuri wa mpango hauzinufaishi kaya maskini pekee bali ni msaada kwa Serikali katika jitihada zake za kuwawezesha wananchi wake kukua kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi na jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ameitaka TASAF kutumia vema mifumo ya TEHAMA kuongeza ufanisi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Mb) amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika na Naibu waziri wake, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa usimamizi mzuri wa majukumu yanayotekelewa na TASAF.

Mhe. Mchemba amempongeza pia Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwa kutekeleza vema maagizo na ushauri ya kamati yake na hatimaye TASAF kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kupitia Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo imekuwa na manufaa kwa walengwa na tija kwa Serikali katika kusimamia malipo ya fedha za ruzuku kwa walengwa.

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa imeridhishwa na utendaji kazi wa TASAF kupitia mifumo ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na na malipo kwa njia ya kieletroniki uliofanyiwa majaribio kwa mafanikio katika maeneo 16 ya utekelezaji ambayo ni Arusha jiji, Unguja, Ilala Manispaa, Temeke manispaa, Kigoma Manispaa, Bahi, Urambo, Songea manispaa, Bagamoyo, Mkuranga, Kilwa, Kisarawe, Muheza, Siha na Mpanda mji.

BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA MAHAKAMA KWA MABORESHO

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma,akisalimiana na watumishi wa mahakama ya wilaya ya Kalambo mara baada ya kuwasili kukagua shughuli za mahakama akiwa katika ziara ya kikazi Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Jengo la Mahakama ya mwanzo Msanze lililopo wilayani Kalambo likiwa limemalizika.Mahakama inaendelea na ujenzi wa majengo ya mahakama katika maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma za mahakama karibu zaidi na wananchi.


Lydia Churi Ntambi

……………………

Na Lydia Churi-Mahakama Rukwa

Benki ya Dunia imeipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kutekeleza vizuri mradi wa maboresho ya huduma za mahakama kupitia Mpango mkakati wake wa miaka mitano (2015/16-2016/2019). 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma aliwasilisha pongezi hizo kutoka Benki ya Dunia kwa watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kalambo alipokuwa akizungumza nao akiwa katika ziara ya kikazi kukagua shughuli za Mahakama mkoani Rukwa. 

Alisema taarifa ya ukaguzi iliyoandaliwa na ujumbe wa Benki ya Dunia uliofika nchini Februari 4 hadi 15, 2019 kufanya ukaguzi imetoa pongezi hizo kufuatia Mahakama kuzipitia sheria na kanuni zaidi ya 50 na kuzifanyia marekebisho ili kurahisisha utoaji wa haki nchini.

Jaji Mkuu aliyataja maeneo mengine yaliyopongezwa na Benki ya Dunia kuwa ni hatua iliyochukuliwa na Mahakama ya kutunga kanuni mpya zinazoongoza Madalali wa pamoja na zile zinazoongoza Mawakili.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, maeneo mengine ni matumizi sahihi ya mfumo wa taarifa za kusajili mashauri (JSDS II), kwa kuwa katika mfumo huo hakuna taarifa chafu iliyowahi kuingizwa na kila shauri linalosajiliwa huingizwa kwenye mfumo siku hiyo hiyo linaposajiliwa. 

Aidha, Benki ya Dunia imeisifu na kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kujiwekea malengo na kufanya kazi inayoonyesha matokeo na kujiwekea viwango au mikakati ya kupunguza mashauri ya mlundikano. Benki hiyo pia imeipongeza Mahakama kwa aina ya ujenzi wa majengo ya mahakama kwa kuwa yanazingatia kukua kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa. 

Maeneo mengine yaliyoonyesha mafanikio na kupongezwa na Benki ya Dunia ni kitendo cha Mahakama kujiwajibisha yenyewe katika utendaji kazi wake hasa kwa kujiwekea mifumo ya kujiwajibisha na kufanyiwa tathmini ya utendaji wake na Taasisi inayojishughulisha na masuala ya utafiti ya Repoa.

Kufuatia pongezi hizo, Jaji Mkuu amewataka watumishi wa Mahakama kuendelea kutambua nafasi pekee ya Mahakama katika jamii kwa kuwa Mahakama hutoa uamuzi kwa kuzingatia taratibu ilizojiwekea.

KAMATI YA BUNGE YATOA MAONI KUHUSU MKATABA WA UMEME JUA

$
0
0
Hafsa Omar - Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wametoa maoni mbalimbali kwa Wizara ya Nishati, kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA).

Walitoa maoni hayo Dodoma, Novemba 12, 2019 wakiwa ni sehemu ya wadau wa sekta husika ili kuboresha Mkataba huo kabla haujawasilishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Novemba 14 mwaka huu ili kuomba uridhiwe.

Akifafanua hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mariam Ditopile, Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alisema kuwa manufaa ya ISA yanaonesha kuwa ni makubwa zaidi kwa nchi ya Tanzania na yanaweza kuendelea kuwepo kwa kipindi kirefu zaidi.

Waziri alikuwa akijibu hoja kuhusu uhakika wa Tanzania kutojitoa kwenye Mkataba huo kama ambavyo imekuwa ikitokea katika baadhi ya mikataba iliyowahi kuridhiwa.

Akieleza zaidi, alisema, Tanzania imekuwa ikijitoa kwenye mikataba kama hiyo baada ya kuona kuwa manufaa ni kidogo ikilinganishwa na majukumu ya uanachama, hata hivyo, alisema kwa upande wa ISA, uwezekano wa kujitoa haupo kutokana na faida ambazo nchi itapata.

Kuhusu hoja kwamba kwanini imechukua muda mrefu kuridhia Mkataba husika tangu uliposainiwa; Waziri alieleza kuwa, ulikuwepo umuhimu wa kufahamu vizuri zaidi mazingira ya utekelezaji wa Mkataba huo na pia kupata uzoefu wa kutosha kutoka nchi nyingine ambazo zilikuwa zimeridhia.

“Kwa sasa inaonekana kuna haja ya kuridhia hasa ikizingatiwa kuwa tayari Tanzania imetengewa Mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 385 kwa ajili ya miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua. Aidha, Tanzania inaendelea kupata nafasi za masomo ili kujenga uwezo wa wataalamu.”

Aidha, Kamati pia ilitaka kufahamu ni kwa namna gani Tanzania imejiandaa katika kuhakikisha inanufaika ipasavyo na ISA, ambapo Waziri Kalemani alieleza kuwa Wizara ya Nishati inaendelea kubainisha maeneo mbalimbali nchini ambayo yanafaa kwa uendelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme wa jua.

Alitaja maeneo ambayo yamebainishwa hadi sasa kuwa ni Manyoni (Singida), Same (Kilimanjaro) na Zuzu (Dodoma).

Vilevile, alifafanua kuwa, ili kunufaika na fedha zilizotengwa, ni lazima upembuzi yakinifu ufanyike. “Hivyo, Wizara kwa kushirikiana na TANESCO, imefanya upembuzi yakinifu wa awali ambapo eneo la Mkwese wilayani Manyoni, limeonekana linafaa kwa ajili ya mradi wa kuzalisha megawati 150 za umeme.

“Umoja wa Ulaya upo katika hatua za mwisho kutoa msaada wa kulifanyia upembuzi yakinifu wa kina, eneo la Mkwese, Manyoni.”Aliongeza kuwa, kutokana na rasilimali kubwa ya jua iliyopo nchini, Wizara inaendelea kuainisha maeneo ambayo yataandaliwa Mpango wa Utekelezaji utakaohusisha upembuzi yakinifu ili kuyaandaa kunufaika na fedha za ISA.

Alisema, mpango wa utekelezaji utakaoandaliwa utahusisha sekta na Nyanja nyingine za matumizi ya nishati jua ikiwa ni pamoja na kilimo na umwagiliaji.

Hoja nyingine iliyoibuliwa ni kuhusu namna gani serikali inawahakikishia wazalishaji binafsi wa umeme hususan wanaozalisha kwa kutumia nguvu ya jua, kuendelea kupata fursa za uwekezaji, katika mazingira ambayo gridi ya Taifa inazidi kusambaa katika maeneo mengi zaidi nchini.

Akitoa ufafanuzi kwa hoja hiyo, Waziri Kalemani alieleza kuwa, serikali inawahakikishia wawekezaji hao kuwa fursa zitaendelea kuwepo kwani yako maeneo ambayo pamoja na uwepo wa gridi ya Taifa, yataendelea kuhitaji umeme mbadala.

Akitaja maeneo hayo, alisema ni pamoja na visiwa mbalimbali nchini ambavyo vitachukua muda mrefu kufikiwa na gridi ya Taifa. Mengine ni katika hospitali, ambazo alisema hata kama zina umeme wa gridi bado zinahitaji umeme mbadala. Pia, katika mitambo mbalimbali ya maji ambayo inahitaji umeme wa gharama nafuu.

Akitoa msimamo wa Kamati, Makamu Mwenyekiti Mariam Ditopile, pamoja na kuipongeza Wizara kwa hatua hiyo, aliiasa kuyatumia makubaliano ya ISA kama kichocheo cha kuupa kipaumbele uzalishaji wa umeme jua nchini ili uzalishwe kwa kiwango kikubwa zaidi nchini ambacho kitaweza kuingizwa katika gridi ya Taifa.

Kwa upande wao, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na Katibu Mkuu Dkt Hamisi Mwinyimvua, waliishukuru Kamati kwa ushirikiano na miongozo mbalimbali ambayo wamekuwa wakiitoa kwa Wizara.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akitoa ufafanuzi kwa hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA), Novemba 12, 2019. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mariam Ditopile na kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
 Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini Mariam Ditopile, Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt Hamisi Mwinyimvua, wakiwa katika kikao cha kupokea maoni ya wadau (Kamati) kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA), Novemba 12, 2019.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini Mariam Ditopile (katikati), akiongoza kikao cha kupokea maoni ya wadau (Kamati) kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA), Novemba 12, 2019. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani.

TRA: WANANCHI LIPENI KODI YA MAJENGO, VIWANGO VIMEPUNGUZWA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Kilombero.

Wito umetolewa kwa wananchi kulipa kodi ya majengo kwa kuwa viwango vilivyopangwa katika kodi hiyo ni rafiki na vinalipika kwa urahisi ukilinganisha na hapo awali.

Wito huo umetolewa na Afisa Kodi Mkuu, Julius Mjenga kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Kampeni ya Usajili, Huduma na Elimu kwa Mlipakodi katika Kata ya Mlimba Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Mjenga amesema kuwa, sasa hivi viwango vya kulipia kodi ya majengo ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000 kwa kila sakafu ya ghorofa katika Majiji, Miji na Manispaa na shilingi 20,000 kwa ghorofa zima katika Halmashauri za Wilaya.

“Sasa hivi viwango vimepunguzwa wale wenye nyumba za kawaida wanalipia shilingi 10,000 tu na wale wenye nyumba za ghorofa zilizopo kwenye manispaa, miji na majiji wanalipia shilingi 50,000 kwa kila sakafu wakati wale wenye nyumba za ghorofa zilizopo halmashauri ya wilaya wanalipia shilingi 20,000 kwa ghorofa zima,” alisema Mjenga.

Mjenga amefafanua kuwa katika majiji, manispaa na halmashauri za miji, iwapo kuna nyumba zaidi ya moja kwenye kiwanja kimoja, kila nyumba itatozwa shilingi 10,000 wakati katika halmashauri za wilaya, endapo kiwanja kimoja kina nyumba zaidi ya moja, nyumba yenye thamani ya juu ndio itakayohesabika na kutozwa shilingi 10,000.

Aidha, majengo yasiyotozwa kodi ya majengo ni pamoja na nyumba zilizoezekwa kwa nyasi na makuti, nyumba zilizojengwa kwa udongo (nyumba za tope) na majengo ya ibada kama vile misikiti na makanisa.

Julius Mjenga amewataja wazee wenye miaka 60 na kuendelea kuwa wamesamehewa kulipa kodi ya majengo kwa nyumba moja ambayo wanaishi na si vinginevyo na wazee hao wanapaswa kufika Ofisi za TRA kuomba kusamehewa kodi hiyo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea na kampeni ya usajili, huduma na elimu kwa mlipakodi katika Mikoa ya Morogoro na Pwani na itamalizika tarehe 17 Novemba, 2019.
 Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro, Bw. Morgan Njama (kulia) akimuelimisha Mlipakodi wa Kata ya Mlimba mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Usajili, Huduma na Elimu kwa Mlipakodi mkoani hapo.
 Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Lameck Ndinda (kushoto) akiwaelimisha Vijana wa Bodaboda wa kata ya Mlimba mkoani Morogoro kuhusu umuhimu wa kuhamisha kadi za vyombo vya moto wakati wa Wiki ya Usajili, Huduma na Elimu kwa Mlipakodi mkoani hapo.
 Mfanyabiashara wa kata ya Mlimba mkoani Morogoro, Bibi Justina Rugwana akitoa hoja wakati wa Kampeni ya Huduma, Elimu na Usajili kwa Mlipakodi mkoani hapo.
Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Lameck Ndinda (kushoto) akichukua taarifa zilizopo kwenye Cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa ajili ya kujiridhisha kama ni ya biashara wakati wa Wiki ya Usajili, Huduma na Elimu kwa Mlipakodi mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA TRA)
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images