Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

TANZANITE GALA IN LAS VEGAS - SAVE THE DATE: SATURDAY DECEMBER 28, 2019


PROF. MWAKALILA ASEMA UTUMISHI WA UMMA NI NIDHAMU

$
0
0
MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amewataka watumishi wa Chuo hicho kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za utumishi wa umma.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imesema hayo yamesemwa na Prof. Mwakalila wakati akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya uongozi wa Chuo hicho na wafanyakazi lengo likiwa ni kukumbushana, kuelekezana na kujipanga kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo mwaka 2019/20.

"Sisi ni watumishi wa umma na utumishi  wa umma ni dhamana hivyo tusikubali kuchezea fursa hii tuliyonayo ni vyema tukatimiza Wajibu wetu kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za Utumishi wa Umma,"anasisitiza Prof. Mwakalila.

Pia Mkuu huyo wa Chuo amewataka wafanyakazi wote kuwa  na uelewa wa dira ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuwa ni kitovu cha utoaji wa maarifa bora kuhusu ubunifu, uvumbuzi na kuendeleza Amani na Umoja.

Amesema Chuo hicho pia kina jukumu la kutoa mafunzo ya uongozi na maadili,mafunzo ya Kujiendeleza na Kufanya tafiti zinazotatua changamoto katika jamii.

Profesa Mwakalila pia ameelezea baadhi ya mafanikio ya Chuo hicho kuwa ni pamoja na kuboresha  mazingira ya kujifunzia na kufundishia, ambapo tayari  vyumba vyote vya madarasa vimefungwa viti visivyohamishika, Madarasa yamefungwa vifaa vya kisasa vya kufundishia, idadi ya vitabu imeongezwa  kwenye Maktaba kwa kampasi zote mbili, ikiwemo ya Kivukoni na ile ya Karume- Zanzibar.

Pia amebainisha baadhi ya mikakati ya Chuo hicho kuwa ni  ni pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, ujenzi wa hosteli kwa kampasi ya Karume- Zanzibar na  kuongeza bajeti kwa ajili ya tafiti mbalimbali lengo likiwa ni kutatua changamoto katika jamii. 

Prof. Mwakalila amewataka  viongozi wenzake wakiwemo Manibu wa Chuo hicho, Wakuu wa idara na Vitengo katika Chuo hicho kuhakikisha wanatenda haki kwa watumishi walio chini yao ikiwa ni pamoja na kujiepushe na vitendo vyote vya ukabila, dini au Rangi.


Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
30/10/2019
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila akizungumza leo wakati anazungumzia na uongozi wa Chuo hicho
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mkutano huo

KOCHA MKUU TAIFA STARS AELEZA ANAVYOWAPATA WACHEZAJI WAKE,AGUSIA WALIOKO NJE YA NCHI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amefunga kwa kueleza mambo mbalimbali kuhusu timu ya Taifa huku akitumia nafasi hiyo kueleza vigezo anavyotumia kuwapata wachezaji wa timu hiyo.

Akizingumza leo Oktoba 31 katika mahojiano maalumu kati yake na watangazaji wa kipindi cha Sport Arena kinachorushwa na kituo cha redio cha Wasafi FM Kocha Mkuu wa Taifa ya Tanzania amesema yeye anao mfumo wake ambao anatamani kuona wachezaji wanautumia kupata mafanikio ya timu na ushindi kwa mechi wanazokutana nazo.

Hivyo amesema ili kupata kikosi kizuri amekuwa akifuatilia taarifa za wachezaji na vilabu wanavyochezea na hivyo anakuwa na taarifa za kutosha za kila mchezaji na uwezo wake wa soka uwanjani.

Amesema pamoja na mambo mengine yeye anapenda kuwa na wachezaji ambao mashambulizi yanaanza kwa mlinda mlango ili kuhakikisha wachezaji wanapeleka mashambulizi kwa timu mpinzani.Pia anapenda kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mpira kwani hiyo inasaidia kupanga mipango ya kushinda.

"Ili kupata wachezaji hao lazima ufuatilie kwa karibu kwenye klabu wanazochezea na nafasia ambazo wanapewa na baada ya hapo naangalia nimuite nani na kwa wakati gani na kubwa zaidi hawa naangalia na pia muungano wa wachezaji kati ya mchezaji mmoja na mwingine ukoje?

"Hata hivyo tukubali kuwa muda wa kuita wachezaji unakuwa mfupi kulingana na ratiba zinapotolewa, lakini cha pili ninaita wachezaji kulingana na mahitaji ya wakati huo na timu ambayo tunakutana nayo kwenye michuano.Naamini kuna wachezaji wengi ambao bado hawajapata nafasi ya kuitwa Taifa Stars lakini naamini wakati utafika,"amesema.

Ameongeza kuwa pamoja na kuita wachezaji kutokana na uwezo wanaoonesha kwenye vilabu vyao anatambua kuwa timu ya Taifa inacheza michuano ya kimataifa, hivyo lazima awe anapata wachezaji ambao wanatoka pia kwenye vilabu ambavyo vinashiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara ambapo ametolea mfano wa klabu za Yanga, Azam FC na Simba.

Alipoulizwa kwanini kwenye timu ya Taifa anaita zaidi wachezaji wa klabu ya Simba na Azam kuliko wa kutoka vilabu wengine, Kocha Ndayiragije amejibu kuwa anaamini huwa anachukua Watanzania kwa ajili ya kuisaidia timu yetu ya Taifa"Huwa nachukua wachezaji Watanzania na si vinginevyo."

Kuhusu kuwaita na kuwachezesha wachezaji walioko nje ya Tanzania, Kocha huyo amejibu kuwa anatamani wote wawepo kwenye timu ya Taifa ili kusaidia na kutoa mchango wao lakini mazingira ya rariba kwa wachezaji hao inakuwa ngumu kuwepo kikosini.

"Nimekuwa naita wachezaji walioko nje lakini changamoto kubwa ni muda, hivyo tunakosa nafasi ya kutosha ya kuepena maelekezo.Hivyo ninajaribu kuangalia kipindi cha Desemba ambako ligi nyingi zinakuwa kwenye mapumziko ambako tutaita wachezaji walioko nje ili tuje tujumuike pamoja na hapo tutakuwa na uhakika wa nani ni nani na anaweza kusaidia vipi tumu yetu.

"Hivyo ni suala la muda tu lakii natambua na kuthamini mchango wachezaji wa nje na nafuatilia kila mchezaji huko aliko,"amesema Kocha huyo wakati anazungumza kwenye kipindi hicho.

T-PESA WAZINDUWA BANDO LA TAMTAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba pamoja na Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde.
Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya muda wa maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS) leo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (kulia) akipongeza moja ya kikundi cha burudani kwenye hafla ya uzinduzi huo. 
Mmoja wa wateja wa TTCL akipata huduma kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam. 



KAMPUNI ya T-PESA imezinduwa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi (SMS).

Huduma hiyo imezinguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri huku akisisitiza kuwa bidhaa hiyo imebuniwa kwa lengo la kuendelea kurahisisha huduma kwa wananchi kwa bei nafuu zaidi. Aidha aliwaomba Watanzania na wateja kwa ujumla kuendelea kutumia huduma za T-PESA ikiwa ni pamoja na kufurahiya mawasiliano ya huduma mpya ya Bando la TamTam.

“...T-PESA inawaletea huduma bora ya kipekee kabisa ya BANDO ambalo ni NAFUU na lenye MVUTO wa aina yake kwa watumiaji. Wananchi watapata fursa ya kupata huduma kwa siku, wiki na mwezi ikiwa na muda wa maongezi, huduma ya Inatenti na ujumbe mfupi (SMS),” alisema Bw. Kimweri.

Awali akifafanua juu ya huduma ya Bando Tam Tam la T-PESA, Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde alisema huduma hiyo itakuwa na virushi vya aina tatu, ambayo ni pamoja Kifurushi cha Siku, ambacho kinampa mteja MB 500 za kutumia intaneti, SMS 50 na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa masaa 24 kwa shilingi 500 tu.

Alibainisha kuwa Kifurushi cha pili cha Wiki, ambacho kinampa mteja GB 1 ya kutumia intaneti, SMS 100 na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 7 za wiki kwa shilingi 1000, huku akikitaja Kifurushi cha tatu cha Mwezi, ambacho kinampa mteja GB 2 za kutumia intaneti, SMS 300 na dakika 20 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 30,kwa shilingi 5000 tu.

Aidha alibainisha kuwa ili kuendelea kuboresha huduma za T-PESA, kampuni imeendelea kusajili mawakala nchi nzima hadi kufikia sasa T-PESA inamawakala wanaozidi zaidi ya 19,000 nchi nzima, uwepo wa mawakala hao wamechangia katika kufikisha huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini.

“... T-PESA imekuwa miongoni mwa kampuni zenye gharama nafuu za miamala kulinganisha na watoa huduma wengine. Hivyo watanzania wanahaki ya kujivunia zaidi na kutuunga mkono zaidi kwa kutumuia huduma zetu za T-PESA.” Alisisitiza.

“...Vifurushi hivi vinapatikana kwa mteja wa T-PESA. Jinsi ya kujiunga ni rahisi, mteja anatakiwa kupiga*150*71#. kuchagua namba 3 kununua Muda wa Maongezi au Vifurushi, halafu namba 2 kununua Vifurushi, kisha kuchagua namba 1 Bando Tam Tam.”

NBC kuendelea kuwapiga jeki wanawake wajasiriamali nchini

$
0
0


Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kushoto), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akizungumza na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Chiku Chambuso (kushoto), pamoja na mwenzake, Lena Mwakisale katika banda la benki hiyo wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lena Mwakisale pamoja mwenzake Isdory Maumba (kushoto), alipokutana nao wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akihutubia wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo Benki ya NBC ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. 
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kulia), akishikana mikono na Kaimu Mwenyekiti Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.

Baadhi ya wanawake waliohudhuria wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.









BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wanawake nchini kuondoa hofu ya kutembelea na kuzungumza na wataalamu wa masuala ya fedha na biashara katika matawi ya benki hiyo ili kufahamu huduma zao na jinsi wanavyoweza kupata huduma za kifedha zitakazoweza kuinua biashara na maisha yao.





Akizungumza wakati wa Kongamano la Kwanza la Wafanyabiashara Wanawake wakubwa na wa kati jijini Dar es Salaam jana ambao benki hiyo ililidhamini, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Benjamin Nkaka, alisema ni vyema kwa wafanyabishara hao wanawake kuzoea kufanya kazi na benki kwani ni njia rahisi na pekee itakayoweza kustawisha biashara zao. 



“Kuna hofu imejengeka kwa wengi kuja benki. Hofu hiyo iondoke. Njooni benki muweze kufahamu ni nini tunakitoa katika kusapoti wajasiriamali hasa wanawake,” alisema Nkaka.



Alisema miongoni mwa majukumu ya benki hiyo ni kusaidia katika kukuza uchumi hasa wa wanawake wajasiriamali, na kuongeza:



“Kwa zaidi ya miaka 50 ya huduma za benki hii nchini, tunafahamu kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiriamali wanawake ni elimu ya mikopo. Sisi tunatoa elimu hiyo pamoja na ushauri kwa wateja wetu wafanyabiashara kadri biashara yao inavyoendelea na kuwaunganisha na mnyororo wa thamani.



“NBC pia huwakutanisha wateja na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA) na taasisi nyingine. Katika harakati zetu za kuwasapoti wanawake, tumeanzisha Vikundi Akaunti ambazo hazina makato yoyote, huku pia tukishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) kutoa mikopo yenye garantii ya hadi asilimia 80 kuwawezesha wanawake kuingia kwenye kilimo kwa nguvu.”



Mkutano huo ulihudhuriwa na takriban wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara 1,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.



Wanawake hao walikutanishwa kupitia mwavuli unaofahamika kama ‘Madirisha’ huku wadau mbalimbali wa maendeleo wakipata nafasi ya kuwaonyesha wanawake hao fursa mbalimbali zilizopo nchini katika kuboresha uchumi wao kama vikundi.



Kampuni ya GS1 iliandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) pamoja na taasisi ya PASS.





Tigo yaingiza sokoni ‘Kitochi 4G Smart’ ’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu

$
0
0


Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu ,Pembeni yeke ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu ,Pembeni yeke ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam .




Wateja wataweza kuipata kwa gharama ya Sh49, 000/-


Dar es Salaam. Oktoba 30, 2019. Kampuni inayoongoza katika mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo, leo imezindua simu yenye sifa za smartphone ‘‘Kitochi 4G Smart’ ya kwanza kwenye soko la simu Tanzania yenye uwezo wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote ili kufungua fursa za kijamii na kiuchumi.

Simu hiyo inayojulikana kama ‘Kitochi 4G Smart’ inapatikana sokoni kwa gharama nafuu ya Sh49, 000/- na inakuja na Applications kama WhatsApp, Facebook, Twitter na YouTube.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema “Kama waanzilishi wa kwanza wa mtandao wa kasi wa 4G hapa nchini tangu mwaka 2014, tunavunja mipaka tena kwa kuhakikisha kila mmoja anapata simu ya 4G kwa gharama nafuu ili kuwa sehemu ya mabadiliko ya kidigitali na hatimaye kuchangia ujumuishwaji wa kidigitali hapa nchini,” alisema Boudiaf.

Boudiaf aliongeza kuwa kwa muda mrefu gharama kubwa ya simu zenye uwezo wa 4G imekuwa kikwazo kwa watanzania wengi kumiliki simu zenye uwezo wa intaneti ya kasi hivyo ujio wa simu hiyo ni msaada kwa watanzania wengi.

“Kwa ujio wa simu hii ya ‘Kitochi 4G Smart’ kwenye soko yenye uwezo wa Facebook ya bure kwa miezi mitatu itawapa wateja wetu uwezo wa kujumuika kwenye mitandao na hivyo kufanya kila mmoja kuwa sehemu ya mageuzi ya kidigitali,” alisema.

Naye, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema “Kitochi 4G Smart inadhihirisha dhamira ya Tigo ya kuwahudumia wateja wake katika kila hatua ya maisha.Kwa hatua hii ni imani yetu kuwa hakuna mtu ambaye atashindwa kupata manufaa yatokanayo na intaneti ya kasi ya 4G.”

Aliongeza, “Kitochi 4G Smart itaongeza wigo wa upatikanaji wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote na kusaidia katika ufikiwaji wa taarifa na maarifa yatakayosaidia katika kutumia vema fursa za kijamii na kiuchumi.”

Tigo inapanua wigo wa uvumbuzi kwa kuendelea kutoa bidhaa na huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja sokoni na zaidi kuchangia mageuzi ya kidigitali nchini.Kitochi 4G Smart ni hatua nyingine kutoka Tigo baada ya Smartphone ya Kiswahili, Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa Pesa na App ya Tigo.

Wateja wa Tigo wanaweza kujipatia simu ya Kitochi 4G kwa kuweka oda kwa kupiga namba 100 na kufanya malipo ya awali.itochi 4G Smart inakuja na App kama Facebook, WhatsApp, YouTube,Twitter, Gmail, Google Map na zingine nyingi zinazopatikana kwenye kaiOS App store.

NAIBU WAZIRI AONGOZA UJUMBE WA WIZARA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisoma taarifa kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe

Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro leo ameongoza ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Bunge jijini Dodoma. Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), kwa pamoja wameipongeza Wizara kwa kutekeleza vyema mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo katika vikao vilivyopita, sambamba na utekelezaji mzuri wa vipaumbele na malengo ya Wizara.

Kikao hicho kilitoa fursa kwa Wizara kuwasilisha kwa kamati taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, kikao hicho hutoa fursa kwa kamati kupokea na kujadili taarifa za Wizara pamoja na kutoa mapendekezo yake kuhusu masuala mbalimbali. 
Kikao cha Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kikiendelea. 
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao. 
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), akichangia jambo wakati wa kikao. 
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia kikao. 

TAASISI ZA SERIKALI ZATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI ZA MADAI

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi ( AG) akifungua Mkutano baina yake na wakati akifungua mkutano baina yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.Mkutano huu wa siku mbili unafanyia Jijini Dododma.
Sehemu ya Wajumbe wanaohudhuria Mkuwano wa Siku mbili ambao umeitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Washiriki wa Mkutano huu ni Mawakili wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi za Serikali, Mashirika na Halmashauri za Miji.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Clement Mashimba naye akichangia majadiliano wakati wa Mkutano ulioitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi

*********************************

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo kwa
Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba, zinawasilisha
taarifa zote zinazohusu mashauri ya madai zinazohusiana na
taasisi hizo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi,
ameyasema hayo leo jumatano, wakati akifungua mkutano baina
yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za
Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka za Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi
mbalimbali za Serikali.

Zaidi wa wajumbe 300 kutoka taasisi hizo wamehudhuria Mkutano
huu ambao ni wa siku mbili, unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma,akiwamo pia Wakili Mkuu wa
Serikali, Dkt.Clement Mashimba (SG).

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,taarifa hizo
zinatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Profesa Kilangi, amewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba,
Ofisi yake imeamua kutoa maelekezo hayo kutokana na kuwepo kwa
changamoto ya baadhi ya taasisi za serikali kuendesha kesi
zake bila taarifa ya uwepo wa kesi hizo kuwasilishwa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa
Serikali.

Changa moto hii ya baadhi ya Taasisi kuendesha kesi zake pasipo
kutoa taarifa kwa Ofisi hizo mbili kumeisababishia serikali
hasara ambayo ingeweza kuzuilika.

“Ipo changamoto ya baadhi ya taasisi za serikali kuendesha kesi
zake bila taarifa kuwasilishwa Ofisi ya yangu na ofisi ya Wakili
Mkuu wa Serikali, ,utaratibu huu umeisababishia hasara
serikali hasara ambayo inegeweza kuzuilika”.

“Hivyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo
kwa taasisi zote za serikali kuwasilisha taarifa zote za mashauri ya madai kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali Mkuu wa Serikali kwa hatua zake
stahiki”.Amesisitiza AG.

Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema,
Ofisi yake pia ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa
mfumo maalum wa kieletroniki wa uwasilishaji wa taarifa kwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka katika Taasisi mbalimbali
baina ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara na
Taasisi zake.

Vile vile Profesa Kilangi ameeleza kwamba, Ofisi yake imesajili
Jarida litakalochapisha masuala Muhimu ya sheria yanayohusu
Mihimili ya Dola ( The Journal of Government Law). Lengo la
jarida hilo litakuwa ni kutoa fursa kwa mawakili wa Serikali
kuchapisha makala mbalimbali zinazohusu mihimili ya Dola.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Kilangi ameitisha Mkutano
huu kwa madhumuni kadhaa yakiwamo ya kuiwezesha Ofisi yake
kujadiliana na kubadilishana mawazo na Wajumbe kutoka Taasisi
hizo juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na uoaji wa huduma
za kisheria hapa nchini.

“Kama mnavyofahamu jukumu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni
kutoa ushauri katika masuala yote ya kisheria jukumu ambalo pia
nyinyi mnalifanya kwa katika maeneo yenu kwa niaba ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hivyo kikao hiki ni muhimu sana
kwetu sote ili tupeane taarifa na miongozo mbalimbali
inayohusiana na utekelezaji wa majukumu hayo kwa lego la
kuongeza tija na ufanisi wa kazi”. Akasema Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.

Kuhusu kuanzishwa kwa Daftari la Mawakili, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali amesema, Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Kifungu cha 16A kama
ilivyorekebishwa, inampa mamlaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuanzisha Daftari la Mawakili wote walioko kaitka Utumishi wa
Umma nchini ( Rolle of State Attorneys).

Akasema, Daftari hilo, litakuwa lina taarifa mbalimbali za
Mawakilil hao na pia litasaidia sana kufahamu wakili gani yupo
wapi na ana taaluma gani au amebobea katika fani gani ili hatimaye pale serikali inapomhitaji kwa jambo fulani aweze kupatikana kwa urahisi.

Aidha kupitia Dafteri hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ataweza kutambua mahitaji ya aina ya mafunzo kwa ajili ya
kuongeza uwezo na ubobezi wa mawakili wa Serikali katika maeneo
mbalimbali.

Mada mbalimbali zikiwalishwa katika siku hii ya kwanza ya
mkutano zikiwamo zinazohudu vazi maalum ( joho) litakalovaliwa
na Wanasheria wa Serikali wanapokwenda Mahakamani au katika
shughuli maalum za kitaaluma.

Lengo la kuwa na Joho maaluma kwa Mawakili wa Serikali
wanaokwenda Mahakamani pia litawezesha kutambuliwa kirahisi kwa
Mawakili wa Serikali, pia litawaongezea kujiamini, kuaminika na
kukubalika.

Dkt. Abbasi, Bosi PSSSF Watatua Kero ya Walimu Papo kwa Papo Simiyu

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jana mkoani Simiyu. Mkutano huo umewakutanisha walimu kutoka mikoa ya Kagera, Mwanza, Kigoma, Mara, Tabora, Shinyanga, Geita na wenyeji Simiyu.

******************************

Na Immaculate Makilika- MAELEZO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, jana jioni alilazimika kumpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hoseah Kashimba ili kutatua kero za walimu waliodai kuna wenzao wamestaafu hawajalipwa mafao yao.

Tukio hilo lilijitokeza wakati Dkt. Abbasi akijibu hoja za walimu mara baaya ya kuwasilisha mada wakati wa Mkutano ulioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na walimu kutoka mikoa ya Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera 

Katika mkutano huo walimu walitaka kujua ni lini Serikali italipa pesheni kwa wastaafu ambao hawajalipwa kwa muda mrefu.

Dkt. Abbasi alionesha kushangazwa na hali hiyo kwani aliwaeleza wanasemina hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, imeachana na utamaduni wa zamani wa kulimbikiza madeni yasiyo na sababu.

Alitoa mfano kuwa licha ya TZS Bilioni zaidi ya 40 zilozotolewa mwaka 2017 kulipa madeni ya wastaafu, Serikali ya Rais Magufuli pia ilihakikisha kati ya hizo TZS Bilioni 16 zinahusu walimu.

Akaongeza kuwa hata mwaka huu kati ya Julai na Septemba Serikali imelipa madeni yanayofikia TZS Bilioni 85.62 ambapo kati ya hizo TZS Bilioni 50 ni madai ya pensheni, Bilioni 22 ni madai mbalimbali ya watumishi wa umma na nyingine ni wadai wa sekta binafsi.

Kutokana na madai ya kuwepo wastaafu wa kada ya elimu ambao hawajalipwa muda mrefu, baadhi wakidai kuwa ni mwaka mzima, Dkt. Abbasi alimpigia simu na kumuunganusha moja kwa moja kwenye kipaza sauti Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.

Akijibu hoja hiyo, Bw. Kashimba alisema kuwa Serikali kupitia PSSSF imeendelea kuwalipa pensheni wastaafu wote kwa wakati na kutoa ofa kwa mwalimu yeyote ambaye hajalipwa kwa muda mrefu alete vielelezo suala lake litafanyiwakazi haraka.

“Mmesikia wenyewe, kama nilivyosema, Serikali ya Rais Magufuli ni ya kisayansi. Hili sasa limekwisha, sio kulalamika tena lete ushahidi wa majina na namba ya malipo ya mishahara ya mtumishi husika, suala lake litatatuliwa haraka,” alisema Dkt. Abbasi kuwaeleza walimu hao waliokuwa na furaha tele baada ya ofa ya Mkurugenzi wa PSSSF.

Baadhi ya walimu hawakuwa na vielelezo husika lakini wachache waliwasilisha nyaraka zao na zinafanyiwa kazi.

Dkt. Abbasi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Mkoa wa Simiyu, ambapo awali aliudhuria hafla ya kufunga Kambi za Kitaaluma kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne katika mwaka 2019.

BAKWATA MWANZA YAZINDUA SHEREHE ZA MAULIDI KITAIFA

$
0
0
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hassani Kabeke akizungumza na Waislamu kwenye Ukumbi wa Sheikh Salum Ferej kabla ya kuzindua maulidi ya kitaifa ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W.
Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji sheikhe Hassani Kabeke akipandisha bendera ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ikiwa ni ishara ya kuzindua maonyesho na sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W yanayofanyika kitaifa jijini humu.


NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limezindua sherehe na maonyesho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.W.A. na kuwataka waumini wa dini zote kuhudhuria.

Pia limewataka Watanzania kwa umoja wao kujitokeza kupira kura kwenye uchaguzi a serikali za mitaa mwaka huu ili kuchagua viongozi waadilifu weny hofu ya Mungu kwa sababu uimara wa serikali unaanzia chini.

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hassani Kabeke alisema jijini humu wakati akizindua sherehe za Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.W.A zinazofanyika kitaifa mkoani humu.

Alisema wananchi na wakazi wa Jiji la Mwanza waislamu na wasio waislamu wajitokeze kwenye maulidi hayo ya kuzaliwa kwa Mtume na waonyeshe ukarimu wao kwa wageni wa ndani na nje ya nchi watakaohudhuria sherehe hizo ambazo mgeni rasmi atakuwa Mufti Abubakar Zuberi.

Sheikhe Kabeke alieleza kuwa Novemba 9, kabla kutafanyika matembezi ya amani (Zafa) yatakayoongozwa na Ngamia wawili na kupokewa na Mutfi, yakianzia BAKWATA mkoa kupitia barabara ya Nyerere hadi Viwanja vya Furahisha, Manispaa ya Ilemela ambapo kabla maandamano hayo kutakuwa na siku maalumu ya kuombea nchi idumu katika amani na utulivu.

“Tumezindua rasmi leo maonyesho na sherehe za maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W ambayo ni siku yake ya kuzaliwa na kilele chake kitakuwa Novemba 9, mwaka huu, kutakuwa na maonyesho ya shughuli za kijamii,upimaji wa kisukari,macho, shinikizo la damu na uchangiaji wa damu wa hiari unaolenga kukusanya chupa 8,000 ili kuokoa maisha ya watu kama alivyofanya Mtume,”alisema Sheikhe Kabeke.

Sheikhe huyo wa mkoa aliwahamasisha wananchi wa jiji hili kufanya usafi kwenye mitaa yao, makazi, barabara na kupaka rangi nyumba huku akiwashauri waumini wa dini ya Kiislamu kuunda vikundi vya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwaalika waumini wa dini zingine washiriki maulidi.

Aidha, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, aliwataka wanasiasa wasiharibu nchi kwa uchu wa madaraka, bali wafahamu kuna watanzania zaidi ya watu milioni 55 ilhali vyama vyao vikiwa na wananchama wasiozi milioni 30.

Pia aliwahamiza watanzania hasa wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu kwani uimara wa serikali unaanzia chini na itakuwa busara wanasiasa wakaongeza juhudi ili uchaguzi ufanyike kwa amani,usalama na utulivu badala ya kusababisha migogoro inayoweza kuharibu nchi.
Sheikhe Kabeke alionya wananchi kuwa, kuwachagua watu wasio na uadilifu ni kukaribisha matatizo kwenye jamii na hivyo siku ikifika wachague viongozi wenye mshikamano na uadilifu watakaoimarisha maendeleo yaliyopatikana chini ya serikali ya awamu ya tano.

BAKWATA MWANZA YAZINDUA SHEREHE ZA MAULIDI KITAIFA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limezindua sherehe na maonyesho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.W.A. na kuwataka waumini wa dini zote kuhudhuria.

Pia limewataka Watanzania kwa umoja wao kujitokeza kupira kura kwenye uchaguzi a serikali za mitaa mwaka huu ili kuchagua viongozi waadilifu weny hofu ya Mungu kwa sababu uimara wa serikali unaanzia chini.

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hassani Kabeke alisema jijini humu wakati akizindua sherehe za Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.W.A zinazofanyika kitaifa mkoani humu.

Alisema wananchi na wakazi wa Jiji la Mwanza waislamu na wasio waislamu wajitokeze kwenye maulidi hayo ya kuzaliwa kwa Mtume na waonyeshe ukarimu wao kwa wageni wa ndani na nje ya nchi watakaohudhuria sherehe hizo ambazo mgeni rasmi atakuwa Mufti Abubakar Zuberi.

Sheikhe Kabeke alieleza kuwa Novemba 9, kabla kutafanyika matembezi ya amani (Zafa) yatakayoongozwa na Ngamia wawili na kupokewa na Mutfi, yakianzia BAKWATA mkoa kupitia barabara ya Nyerere hadi Viwanja vya Furahisha, Manispaa ya Ilemela ambapo kabla maandamano hayo kutakuwa na siku maalumu ya kuombea nchi idumu katika amani na utulivu.

“Tumezindua rasmi leo maonyesho na sherehe za maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W ambayo ni siku yake ya kuzaliwa na kilele chake kitakuwa Novemba 9, mwaka huu, kutakuwa na maonyesho ya shughuli za kijamii,upimaji wa kisukari,macho, shinikizo la damu na uchangiaji wa damu wa hiari unaolenga kukusanya chupa 8,000 ili kuokoa maisha ya watu kama alivyofanya Mtume,”alisema Sheikhe Kabeke.

Sheikhe huyo wa mkoa aliwahamasisha wananchi wa jiji hili kufanya usafi kwenye mitaa yao, makazi, barabara na kupaka rangi nyumba huku akiwashauri waumini wa dini ya Kiislamu kuunda vikundi vya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwaalika waumini wa dini zingine washiriki maulidi.

Aidha, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, aliwataka wanasiasa wasiharibu nchi kwa uchu wa madaraka, bali wafahamu kuna watanzania zaidi ya watu milioni 55 ilhali vyama vyao vikiwa na wananchama wasiozi milioni 30.

Pia aliwahamiza watanzania hasa wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu kwani uimara wa serikali unaanzia chini na itakuwa busara wanasiasa wakaongeza juhudi ili uchaguzi ufanyike kwa amani,usalama na utulivu badala ya kusababisha migogoro inayoweza kuharibu nchi.

Sheikhe Kabeke alionya wananchi kuwa, kuwachagua watu wasio na uadilifu ni kukaribisha matatizo kwenye jamii na hivyo siku ikifika wachague viongozi wenye mshikamano na uadilifu watakaoimarisha maendeleo yaliyopatikana chini ya serikali ya awamu ya tano.sssss
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hassani Kabeke akizungumza na Waislamu kwenye Ukumbi wa Sheikh Salum Ferej kabla ya kuzindua maulidi ya kitaifa ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W.
 Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji sheikhe Hassani Kabeke akipandisha bendera ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ikiwa ni ishara ya kuzindua maonyesho na sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W yanayofanyika kitaifa jijini humu.
 Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki pamoja na kaimu sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, alhaji Hassani Kabeke kuimba qaswida wakati wa uzinduzi wa sherehe nza maulidi zilifanyika kwenye ukumbu wa Sheihe Salum Ferej jana .

WAZIRI NDALICHAKO AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA HUDUMA YA MTANDAO JAMII

$
0
0
Serikali ya Tanzania imesema inatambua umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya mawasiliano kama mkakati mmojawapo wa kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda inafikiwa.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa Kongamano la Nne la Huduma ya Mtandao Jamii linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo amesema sekta ya mawasiliano ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.

"Kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 sekta ya mawasiliano ilikua kwa asilimia 13.1 na ilikuwa sehemu ya pili katika kuchangia ukuaji wa uchumi nchini," amesema Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako amesema katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika mpaka vijijini, mwaka 2014 serikali iliingia mkataba na kampuni kutoka Vietnam wa kuhakikisha huduma hiyo inafika katika vijiji 4,000 ambapo kufikia Januari 2019, vijiji vyote vilikuwa vimefikiwa na huduma hiyo.

Waziri huyo ameendelea kuelezea kuwa serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefanya kazi kubwa katika kuhakikisha inafikisha mawasiliano vijijini ambapo mpaka sasa imeweza kupeleka huduma ya mawasiliano katika Kata 562 zenye vijiji 2,132.

Aidha, Profesa Ndalichako amesema kwa upande wa elimu, mfuko huo umewezesha kufika kwa huduma za mawasiliano katika baadhi ya shule na taasisi za kielimu pamoja na  kutoa mafunzo ya huduma za mawasiliano kwa walimu wapato 1,229.

Akizungumza katika Kongamano hilo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Faustine Bee amesema kongamano hilo linatoa nafasi kwa washiriki kujifunza namna ya kuendelea kuboresha huduma ya mawasiliano kwa jamii hasa jamii ambayo haijafikiwa na huduma hiyo.

"Lengo kubwa  ni kuhakikisha ifikapo 2025 taasisi zote za serikali ziwe zimefikiwa na  huduma ya mawasiliano ikiwemo vyuo vyote, shule zote za msi ngi na sekondari pamoja na ofisi zote za serikali," amesema Profesa Bee.

Kongamano hilo la wiki moja linahusisha nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Internet Societ Association for Progressive Community na ufanyika mara moja kwa mwaka, ambapo kwa mwaka huu limefanyika nchini Tanzania likiwa na washiriki kutoka Kenya, Uganda, Liberia, Cameroon, Ghana, Spain na mwenyeji Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako leo Oktoba 30, 2019 amefungua Kongamano la Nne la Huduma ya Mtandao Jamii lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa niaba ya Waziri Mkuu wa   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Faustine Karrani Bee wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Huduma ya Mtandao Jamii lilofanyika Chuoni hapo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la huduma ya Mtandao Jamii

CRDB Bank announces the highest profit in the market for the Third Quarter of the year 2019

$
0
0
 Dar es Salaam, Thursday  31st  October 2019 – Tanzania's leading commercial Bank, CRDB Bank PLC, today announces a 76% jump in its net profit for the year ending September 2019.

During the period, CRDB Bank Group reported a net profit of TZS 92.16 billion from its operations, up from TZS 52.25 billion recorded in the same period in 2018. 

CEO and Managing Director, Abdulmajid Nsekela attributes the impressive performance to dedicated and committed staffs, responsible lending that led to improved loan quality and loan repayments, growth of CRDB Wakala business and Trade Finance through guarantees.

“Our  focus on operational efficiency and sales optimization is paying off. We have embarked on the digitalization journey while adhering to good governance, reduce operational costs, and improve our service delivery. As you can see, our earnings from credit books, trade finance, and foreign currency dealings have significantly increased, showing our commitment to serving each segment in the market," says Nsekela.

Nsekela affirms that the Bank's continued pursuit for business excellence portends even higher financial performance in the last quarter of the year. "We are focusing on the customer, and this means that we are re-engineering our products and services to respond to the changing needs in the marketplace, we are optimistic about our targets, come end of the year," he quips.
  
The CEO says the Bank has instituted internal reforms that are aimed at improving service delivery and optimizing processes for enhanced customer experience. "We have reviewed critical areas of our operations and deployed a new business model that taps into the

Bank's greatest strengths, while taking advantage of the opportunities in the market,our philosophy still stands at 30/70 where the first stands for back-office dealings, and later for business solicitation and relationship management” the CEO explains.  

The Bank - together with its subsidiaries - continued to maintain a healthy balance sheet with Group total assets appreciating by 5% to reach TZS 6.2 trillion up from TZS 5.9 trillion reported in September 2018.

The Group Loan portfolio witnessed a slight positive change to close at TZS 3.25 trillion in the third Quarter of this year, representing an increase of 2.5% from TZS 3.17 trillion reported in the Second quarterquarter, 2019.


“Our total customer deposits increased by 7% to TZS 4.8 trillion, up from TZS 4.5 trillion reported in the third quarter of 2018, while  Net Interest Income increased by 22% year on year to reach TZS 389.66 billion from TZS319.09 billion reported in September 2018," says  Nsekela.  

Nsekela notes that CRDB Bank Group continues to command a 22% market share of industry deposits, owing to its robust network of 240 branches, 551 ATMs, over 2,400 Point of Sales (POS) terminals.

CRDB Wakala agents increased by 7,260 years on year to reach 11,612 by the end of September 2019, who spread across the country.

The Bank’s MD further attributes the Bank’s sustained performance to a robust digital banking proposition through the SimBanking and SimAccount platforms, which continue to provide unrivaled convenience.  The Bank also has reliable Internet banking services. 

Summary of  Key Highlights for the quarter ended September 30th, 2019: 
Loans and advances grew by 6% to reach TZS 3.25 trillion (Q3 2018: TZS 3.08 trillion) 
Net Interest Income increased by 9% to reach TZS 131.86 billion (Q3 2018: TZS 121.28 billion) 
Operating profit grew by 39% to reach TZS 45.09 billion (Q3 2018: TZS 32.37billion)
• Profit for the quarterquarter(after-tax) grew by 36% to reach TZS 31.08 billion (Q3 2018: TZS 22.92 billion).





NAIBU WAZIRI IKUPA APONGEZA UBUNIFU WA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, amefunga rasmi kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu, ambapo amewapongeza viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka kwa ubunifu huo ambao utawasaidia wanafunzi hao kufanya vizuri katika mitihani yao.

Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo Oktoba 30, 2019 wakati wa kuhitimisha kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambayo imefanyika kwa muda wa siku 60 katika Shule ya sekondari Simiyu na Chuo cha Ualimu Bariadi Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwaandaa na mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika kuanzia Novemba 04, 2014.

“Nampongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu mkubwa wa kuandaa kambi hizi kwani, naamini wanafunzi mmejifunza mambo mengi na mtafanya vizuri katika mtihani wenu, ningeshauri watu wengine waige jambo hili, niwakumbushe wanafunzi mtakaoanza mtihani wenu Novemba 4, 2019, kumuomba Mungu ili awaongoze kipindi chote cha mitihani,” alisema Ikupa.

Aidha, Ikupa amesema Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu nchi kwa kuongeza bajeti katika shule, kujenga madarasa, na anaamini kuwa itaendelea kutatua changamoto ya walimu katika mkoa wa Simiyu, na nchini kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema uongozi wa Mkoa, walimu, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo wamefanya uwekezaji mkubwa kwa wanafunzi wote waliokuwa katika kambi za kitaaluma na kupitia kazi nzuri iliyofanywa na walimu anaamini kwamba watafanya vizuri katika mtihani wa Taifa utakaoanza Novemba 4, 2019.

Ameongeza Serikali mkoani Simiyu itaendelea kuwapa motisha walimu, wanafunzi na shule zote zitakazofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa, huku akiahidi kuwalinda walimu wote, ambapo ameahidi kuwa kuanzia Desemba Mosi, 2019 viongozi wa mkoa watawatembelea walimu katika Halmashauri zote na kuzungumza nao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amewaomba wadau kuendelea kuunga mkono kambi hizi ili waweze kutimiza ndoto zao huku akibainisha kuwa kupitia kambi hizo watapatikana viongozi mahiri wa baadaye.

Katibu Mkuu, Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif amesema walimu wana imani na Serikali na wameamua kufanya kazi yao kwa bidii na wanaiomba Serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kupandishwa madaraja na mishahara kwa wakati na malipo ya fedha za likizo na malimbikizo ya mishahara.

Naye Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju amesema tangu kambi hizi zianze mwaka 2016 zimesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo kwa kidato cha nne mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 70.68% na mwaka 2019, ufaulu umekuwa 86.46%.

Naye Diana Boniphace mwanafunzi kutoka Shule ya sekondari Kidinda amesema, “kupitia kambi hii wanafunzi tumejifunza mambo mengi kupitia kwa walimu mahiri na kiwango cha ufaulu kimeongezeka tofauti na tulivyoingia hivyo tunaahidi kuwa tutafanya vizuri katika mtihani wa Taifa tutakaoanza Novemba 04, 2019.”

Kambi ya Kitaaluma iliyohitimishwa Oktoba 30, 2019 ilihusisha wanafunzi 1512 ambao walikuwa na ufaulu hafifu(daraja sifuri), wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa Mkoa(Mock) na wanafunzi kutoka shule zenye wanafunzi chini ya 30 na wamekaa kambini siku 60.
 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, mara baada ya kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi hao kuhitimishwa Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha nne kutoka shule mbalimbali mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, wakati wa kufunga kambi yao ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa, Bw. Jumanne Sagini, Afisa Elimu Mkoa, Ernest Hinju na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakifurahia jambo, wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wananfunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wanafunzi Kidato cha nne kutoka shule mbalimbali mkoani Simiyu wakicheza na kufurahi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya viongozi wakifuatilia kitu wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi , kutoka kulia walioketi mbele, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas, Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif na Mbunge la Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko ,
 Baadhi ya walimu mahiri waliofundisha kambi ya kitaaluma ya kidato cha nne wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

WANANCHI NAMTUMBO KUONDOKEWA NA MATUMAINI YA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI

$
0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA, NAMTUMBO
Urani ni metali ya asili yenye kawaida ya kutoa mionzi ambapo imekuwepo ardhini tangu kuumbwa kwa dunia miaka bilioni tatu na nusu(3,500,000,000) iliyopita.

Upatikanaji wa urani ikiwa ardhini inaanza na tani mbili na kuendelea katika sehemu mbalimbali ikiwa ndani ya miamba , ndani ya maji ya ardhini na baharini

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya kigeni zilifanya utafiti wa madini katika ardhi ya wilaya ya Namtumbo mwaka 2006 na kugundua uwepo wa madini ya Urani katika mto mkuju kijiji cha Likuyusekamaganga.

Ugunduzi wa madini ulileta matumaini kwa wananchi wa wilaya ya Namtumbo licha ya kutolewa taarifa kuwa mionzi ya madini hayo ni hatari kwa afya ya binadamu .

Mionzi ya madini hayo zikiingia kwenye mwili wa binadamu hufanya kazi ya kuharibu mfumo wa ukuaji wa seli ,lakini wananchi Wilayani Namtumbo wanalalamikia kuchelewa kuanza kwa uchimbaji wa madini , wakiamini kuanza kwa uchimbaji wa madini hayo kutawanufaisha kiuchumi.

Uchimbaji wa madini ya urani yenye mionzi na hatari kwa afya za binadamu huchimbwa kwa njia ya shimo lililowazi au kwa njia ya kuingia ndani ya ardhi yaliko madini .

Licha ya madhara yanayoelezwa na wataalamu kuhusu madini ya urani wananchi Wilayani Namtumbo hususani vijana wanashauku kubwa ya kupata ajira ya kuchimba madini ya urani waweze kujipatia kipato.

Madini ya Urani katika mto mkuju yanapatikana karibu na uso wa dunia kiasi ambacho kitarahisisha uchimbaji wake na uchimbaji wa njia ya shimo lililowazi ndio utakaotumika.

Katika Madini ya Urani kuna mionzi hatari ya aina tatu, Alfa,Beta na mionzi aina ya Gamma kwa pamoja mionzi hiyo inamadhara kwa afya ya binadamu iingiapo mwilini .

Mionzi aina ya Alfa ina madhara mara ishirini zaidi ya madhara yanayoweza kutolewa na mionzi aina ya beta na gamma katika mwili wa binadamu wakati wa uchenjuaji .

Mionzi huingia katika mwili wa binadamu kwa njia ya hewa au kwa njia ya kumeza chembechembe za urani wakati wa uchenjuaji wa madini baada ya kuchimbwa kutoka ardhini.

Hamu ya wananchi wa Namtumbo hasa vijana ya kupata ajira ya kuchimba madini ya Urani licha ya madini hayo kuwa hatari kwa afya za binadamu zinaendelea kupotea baada ya kampuni iliyotegemewa kuanzisha kuchimba madini Mantra Tanzania Limited kutoonesha dalili za kutaka kuchimba madini hayo.

Wananchi katika wilaya ya Namtumbo kupitia vikao vya serikali hawajachoka kuhoji kuhusu ajira zinazosemwa kuwa kuanza kwa uchimbaji wa madini ya urani katika mto mkuju utasaidia vijana kupata ajira huku wakibaki bila majibu sahihi juu ya lini madini hayo yataanza kuchimbwa rasmi.

Afisa Mahusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania Limited Adija Pallangyo anadai kampuni ya Mantra haijaanza uchimbaji wa madini kutokana na madini hayo kushuka bei katika soko la dunia kiasi ambacho kitaifanya kampuni kupata hasara endapo wataanza kuchimba madini kulingana na gharama za uendeshaji.

Kampuni ya mantra inakadiriwa kuwepo katika eneo la mto mkuju kwa zaidi ya miaka 12 hali inayopelekea wananchi kuhoji viongozi wa serikali Wilayani Namtumbo mara kwa mara uwepo wao katika eneo hilo huku hakuna shughuli za uchimbaji zinazoendelea.

Mbunge wa jimbo la Namtumbo Edwin Amandus Ngonyani pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Daniel Magnus Nyambo katika ziara zao za kuzungumza na wananchi Wilayani hukutana na swali mara kwa mara linalohusiana na lini madini ya urani katika mto mkuju yataanza kuchimbwa? Ambapo majibu yakiendelea ya kuwataka wananchi kuendelea kuvuta subira .

Bwana Ngonyani kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha mapinduzi mkoa wa Ruvuma amewafafanulia wajumbe wa kikao kuwa ajira asilimia 99.5 za vijana zinasubiriwa kupatikana katika uchimbaji wa madini ya urani huku makampuni ya uchimbaji wa madini hayo yakiendelea kusuasua katika uchimbaji na wananchi wameanza kupoteza matumaini juu ya uchimbaji wa madini hayo kutokana na kusubiri kwa muda mrefu.

Wananchi Wilayani Namtumbo matumaini yao kwa kampuni ya Mantra kuwa ingeanza kuchimba madini hayo kutokana na mwelekeo wake wa kushiriki kikamilifu kuwezesha shughuli za kijamii na ghafla kampuni hiyo inaonekana kuanza kutoweka taratibu kwenye kushiriki shughuli za kijamii na kupunguza wafanyakazi waliopo kwa kiasi kikubwa na kuleta sintofahamu kwa wananchi kuhoji kama uchimbaji wa madini hayo utafanyika .

Wapo wananchi Wilayani hapa wanabishana wao kwa wao wakihoji uhalali wa kampuni hiyo kukaa zaidi ya miaka 12 bila kufanya kazi ya uchimbaji lakini pia wanabiashana kuhusu aina ya kibali kinacho tolewa na wizara inayohusiana na madini ni cha utafiti au cha uchimbaji na kama ni cha utafiti ni kwa muda wote huo na kama cha uchimbaji mbona uchimbaji haufanyiki.na kuacha wananchi katika maswali magumu wakibishana wao kwa wao.

Eneo linalotumiwa na kampuni ya Mantra lipo katika Hifadhi ya misitu ya Undendeule (undendeule forest reserve) ambalo lina urani nyingi wananchi wanahoji kauli ya profesa Dos Santos Silayo katibu mkuu wakala wa misitu Tanzania aliyoitoa katika mkoa wa katavi kuwa hakuna uchimbaji wowote wa madini utakaofanyika katika Hifadhi bila kibali ,kampuni hiyo inawezaje kukaa katika Hifadhi bila kibali na wanahoji ni kibali gani cha utafiti au uchimbaji kinachotolewa kwa muda wa zaidi ya miaka 12 na uchimbaji usifanyike.

Barani afrika urani huzalishwa kwa asilimia 18 ya urani yote duniani na hatua ya uchimbaji na uchenjuaji wa urani Afrika ulianza mwaka 1952 Afrika kusini na mwaka 1976 nchini Namibia .

Nchi za Afrika ambazo zina kiasi kikubwa cha madini ya urani ni Algeria,Botswana,Jamhuri ya kidemokrasia ya kati , Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ,Gabon,Guinea,Eguatorial guinea,Malawi na Mali.

Zingine ni nchi ya Mauritania ,Morocco,Namibia ,Niger ,Afrika kusini ,Tanzania ,Zambia pamoja na Zimbabwe

Nchini Tanzania madini ya urani yanapatikana Wilayani Namtumbo,Bahi,Galapo,Minjingu,Mbulu,Simanjiro,Ziwa Natron,Manyoni,Songea,Tunduru ,Madaba na Nachingwea

Katika wilaya ya Namtumbo madini ya urani yanapatikana katika kijiji cha Likuyuseka katika mto mkuju yenye jumla ya tani 58,500 ambayo inaizidi wilaya zingine kwa uwingi wa urani Nchini Tanzania.

Kitendawili cha uchimbaji wa madini ya Urani katika mto mkuju Wilayani Namtumbo kilianza kutolewa na waziri wa viwanda na biashara wa Urusi bwana Denis Manturov kwa kudai kuwa uchimbaji wa madini ya urani katika Mto mkuju utaanza mapema mwaka 2018 kupitia kampuni ya Russian”s Uranium one Inc ya nchini humo.

Katika eneo la mto mkuju kampuni ya Mantra Tanzania Limited ilionekana ndio kampuni yenye dhamira ya dhati ya kutaka kuanza uchimbaji wa madini hayo na kuwatumainisha wananchi katika kutegemea kupata ajira lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea na chakushangaza zaidi wafanyakazi wa kampuni hiyo imeanza kuwaondoa wafanyakazi wake katika eneo hilo na kuwafanya wananchi Wilayani Namtumbo kuanza kupotelewa na matumaini ya ajira kutokana na kuchimba madini hayo.

PAMOJA NA KUWEPO KWA SHERIA YA HAKI YA MTOTO KWA MIAKA 30,TAKWIMU ZINAONESHA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO UKO JUU-MKURUGENZI IDARA YA MAENDELEO YA WATOTO

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MKURUGENZI wa Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mwajuma Maguiza amesema pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Haki ya Mtoto kwa miaka 30 sasa lakini bado takwimu za Jeshi la Polisi hapa nchini za mwaka 2018 zinaonesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto kuongezeka kutoka matukio 13457 kwa 2017 hadi matukio 14419 kwa 2018 ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.6.

Ametaja baadhi ya vitendo vya ukatili ni ulawiti, ubakaji, mimba, ndoa za utotoni, vipigo na ukeketaji vitendo hivi vyote vinagandamiza haki za mtoto zilizosainiwa na Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi ambapo zilisainiwa ili kulinda haki za mtoto na kwamba utekelezaji wa Sheria ya mtoto (CRC), utekelezaji wake upo lakini hautiliwi mkazo ndio maana vitendo vya ukatili vinaongezeka mwaka hadi mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 31 mwaka 2019, Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii na familia ndio imekuwa sababu kubwa. “Tumekuwa tukishuhudia watoto wakifanyiwa ukatili katika familia zetu, ukatili wa aina mbalimbali ikiwa wanaofanya ukatili  huo kwa kiasi kikubwa wakiwa watu waliokaribu na mtoto kama familia, dugu, jamaa na rafiki”. 

Hata hivyo utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa watoto kwa kipindi cha Desemba mwaka 2017 hadi Januari mwaka 2018 katika halmashauri 12 hapa nchini zinaonesha kuwa ilibaini uwepo wa watoto 6,393 wanaofanya kazi mitaani, kati ya hao wasichana ni 1528 na wavulana 4,865.

Pia utafiti huo ulibaini kuwa watoto 1,385 ilibaini wanaishi na kufanya kazi mitaani usiku hii ni kutokana na kutokuwajibika kwa familia katika kumudu majukumu yao ya kuwalea watoto, hivyo jamii inapaswa kuwajibika katika malezi ya watoto ili kujenga taifa lenye kutengemeana kuwepo na wazazi, watoto, vijana pamoja na wazee.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya, Mwajuma Magiza akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wakitoa semina ya malezi ya watoto na msingi wa malezi ya watoto na familia
 Frank Odhiambo akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa mafunzo ya malezi bora ya watoto na malezi bora ya watoto.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja.

Wachimbaji Madini Ujenzi watakiwa kuwa na Mikataba ya Utoaji Huduma kwa Jamii

$
0
0
Na Greyson Mwase,  Morogoro
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amewataka wachimbaji wa madini ya ujenzi kuwa na mikataba ya utoaji wa huduma kwa jamii inayotambulika kisheria ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza baina yao na wananchi wa  vijiji vinavyozunguka machimbo.

Profesa Kikula alitoa kauli yake katika nyakati tofauti  mkoani Morogoro leo tarehe 30 Oktoba, 2019 kwenye ziara yake  yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini  ujenzi pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini hayo.

Katika ziara yake Profesa Kikula aliambatana  na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Shija, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Morogoro (MOREMA), Dk. Omari Mzeru, Mwenyekiti wa  Madini ya Ujenzi na Wachimbaji Wasio Rasmi, Aquilin Magalambula na  Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Yahya Nania.

Wengine ni pamoja na Wawakilishi kutoka katika Kurugenzi ya Manispaa ya Morogoro, Kurugenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Maafisa kutoka Tume ya Madini.

Profesa Kikula mara baada ya kusikiliza  kero za wachimbaji wa madini ya ujenzi katika maeneo tofauti alielekeza kuwa ni vyema wachimbaji wa madini ya ujenzi wakahakikisha wanaingia makubaliano ya kisheria na wanavijiji wanaozunguka machimbo yao  kuhusu utoaji wa huduma kwa jamii kama vile  maji, barabara, ujenzi wa madarasa ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza mbeleni.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula aliwataka wamiliki wa machimbo ya mchanga kuhakikisha wanakuwa na mipango ya  maandalizi ya ufungaji wa machimbo mara baada ya shughuli za uchimbaji kumalizika na kuanza kuitekeleza kwa kurudishia mashimo vizuri.

“Mnatakiwa kuwa na mpango wa kuanza kurudishia mazingira katika hali nzuri  kabla ya shughuli za uchimbaji wa mchanga kuisha ili kuepuka mashimo ambayo ni hatari kwa wananchi,” alisisitiza Profesa Kikula.

Aidha, aliwataka wamiliki wa machimbo  ya mchanga kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyakazi hao kwa kuhakikisha wanakuwa na nyumba na vyoo salama ikiwa ni sehemu ya usalama kwenye machimbo hayo kama Sheria ya Madini na kanuni zake inavyofafanua.

Profesa Kikula aliongeza kuwa, wamiliki wa machimbo hayo wanatakiwa kuhakikisha  wanakuwa na mpango wa huduma ya kwanza kwenye machimbo pamoja na kuhakikisha wachimbaji wanavaa vifaa vya kujikinga na madhara mbalimbali kwenye shughuli zao.

Wakati huohuo, Profesa Kikula alifanya ziara kwenye viwanda vidogo vya kufyatua matofali vya Vibrate Block na Nak Vibrate vilivyopo Wilayani  Morogoro na kuwataka wamiliki wake kuhakikisha wananunua mchanga kwa wachimbaji wenye leseni za madini.

“Ikumbukwe tu kuwa ni kosa la kisheria kununua mchanga kwa mchimbaji asiye na leseni ya madini, adhabu yake ni faini pamoja na kutaifishwa kwa mchanga pamoja na vifaa,”alisisitiza Profesa Kikula.

Profesa Kikula alimwelekeza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Morogoro (MOREMA), Dk. Omari Mzeru kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini ya ujenzi kuhusu umuhimu wa kuendesha shughuli za madini  kwa kuwa na leseni za madini, umuhimu wa kuwa na mpango wa utoaji wa huduma ya kwanza kwenye machimbo.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wachimbaji wa madini ya ujenzi pamoja na wamiliki wa viwanda vidogo vya kufyatua tofali Wilayani Morogoro walimpongeza Profesa Kikula kwa  kusikiliza na kutatua kero zao.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kulia) akikagua risiti ya malipo kwenye machimbo yanayomilikiwa na Mathayo Mkude yaliyopo katika eneo la Kiegea B Wilayani Morogoro kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani humo tarehe 30 Oktoba, 2019 yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi. Kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Shija.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kulia) akitoa maelekezo  kwa wachimbaji wa madini ya ujenzi  kwenye machimbo yanayomilikiwa na Mathayo Mkude yaliyopo katika eneo la Kiegea B Wilayani Morogoro kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani humo tarehe 30 Oktoba, 2019 yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Shija (mbele) akimwongoza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula pamoja na  msafara wake kwenye ziara katika machimbo yanayomilikiwa na Mathayo Mkude yaliyopo katika eneo la Kiegea B Wilayani Morogoro kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani humo tarehe 30 Oktoba, 2019 yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi.

SERIKALI KUBORESHA MIFUMO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI ILI KURAHISISHA UPATIKANAJI WA TAARIFA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akifunga mafunzo ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Hassan Kitenge akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.

Na Happiness Shayo – Dodoma
Serikali kwa kushirikiana na Asasi Zisizo za Kiserikali inatarajia kuboresha mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa manufaa ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Nolasco Kipanda wakati akifunga mafunzo ya wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.

Bw. Kipanda amesema kuwa mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini iliyoko sasa haiwasiliani hivyo kuleta changamoto ya upatikanaji wa taarifa ya pamoja ya utekelezaji wa miradi mbalimbali serikalini.

“Kuna mifumo mingi ya Ufuatiliaji na Tathmini ambayo haiongei, hivyo kwa kushirikiana na AZAKI tunajipanga kuboresha mifumo hiyo ili iweze kuwasiliana na kutoa taarifa ya pamoja inayoweza kutumiwa na wadau wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali” Bw. Kipanda amesema.

Bw. Kipanda amefafanua kuwa, ili kufikia azma ya kuboresha mifumo hiyo, unahitajika muda wa kutosha, rasilimali fedha, rasilimali watu na mikakati thabiti, hivyo kupitia mafunzo hayo wadau wametoa maoni yatakayowezesha maboresho.

Bw. Kipanda ameongeza kuwa, maoni ya wadau yaliyopatikana katika mafunzo hayo yatawasilishwa kwenye mamlaka nyingine za serikali ili yatumike kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Bi. Esther Ngulwa ambaye ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa taasisi ya Aga Khan Foundation East Africa  amesema, ili Serikali ifanikiwe kuboresha mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini ni vema ikawa na mikakati endelevu ya kuwakutanisha wadau wa kada hiyo kwa ajili ya kukusanya maoni kwa lengo la kuisaidia Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi.

Bi. Ngulwa ameongeza kuwa, endapo mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini itaunganishwa pamoja itawezesha upatikanaji wa taarifa na kubaini maeneo yenye mapungufu na hatimaye kuangalia namna bora ya kufikia malengo ya Taifa.

Naye, Meneja wa Uchambuzi wa Sera na Bajeti wa taasisi ya Policy Forum Bw. Nicholaus Lekule ameipongeza serikali kwa kuwa na mifumo mizuri ya Ufuatiliaji na Tathmini na kuitaka Serikali kufanyia kazi pendekezo la kuwa na mifumo inayozungumza.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na “Centre for Learning on Evaluation and Results CLEAR-AA” ya Chuo cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAZINDUA RASMI MFUMO WA KIELETRONIKI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA TAARIFA ZA UKAGUZI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

WIZARA ya Fedha na Mipango imtangaza kuwa sasa mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi umezinduliwa rasmi huku ikisisitiza kuwa wakaguzi wa ndani wa taasisi za umma wataanza kuutumia mfumo huo kikamilifu na kuachana na utamaduni wa kuwalisha taarifa za ukaguzi kwa mlipaji mkuu wa Serikali kwa kutumia nakala ngumu.

Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa mfumo huo leo Oktoba 31 jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango aliyekuwa mgeni rasmi Amina Shaaban amesema kuwa mfumo huo utafanyiwa maboresho ili kuwaingiza wadau wengine wa umma walio katika ofisi ya Msajili wa Hazina, wasimamizi wa wakaguzi wa ndani na mamlaka za Serikali za Mitaa walio katika sekretarieti za mikoa TAMISEMI na hata wakaguzi wakuu ili kurahisisha utendaji kazi serikalini.

Pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo kutenga fedha kupitia idara ya mkaguzi wa ndani mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha mfumo huo  kuhakikisha kuwa watumiaji wote wanapata mafunzo stahiki ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza bado kuna watumishi wengi hawana mafunzo kuhusu mfumo huo na hivyo wataendelea kuelimishwa siku hadi siku.

"Nipende kumshukuru Kaimu Mkurugenzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kwa kunialika katika kuzindua mfumo huu muhimu wa kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi katika taasisi za umma(GARIITS).Natambua mkaguzi mkuu wa ndani wa Serikali na wataalam wake kwa jinsi walivyoonesha umuhimu wa suala hili na kuhakikisha kuwa wanasaidia mfumo huo wa kieletroniki wa kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya wakaguzi wote wa ndani na nje yanayotolewa kwenye taarifa zao za mara kwa mara. Pia natambua sheria ya fedha ya mwaka 2010 iliweka jukumu la kumsaidia mlipaji mkuu wa Serikali katika ya ukaguzi wa ndani katika masuala ya ukaguzi wa ndani katika taasisi zote za umma,"amesema Shaaban.

Amefafanua kuwa kuwamoja ya lengo kuu katika mpango mkakati wa Wizara ya Fedha na Mipango wa mwaka 2017-2022 ni kuimarisha usimamizi wa masuala ya fedha na uwajibikaji , hiyo inajumuisha kuimarisha mifumo ya kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa ndani na wakaguzi wa nje wa taasisi zote za umma.

Aidha amesema Serikali imeweka utaratibu wa kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma kupitia kufanya tathimini ya utendaji."Kwa mantiki hii wakaguzi wa ndani katika taasisi zote za umma wanatakiwa kutekeleza wajibu wa kuthamini na kutoa taarifa za utekelezaji wa mapendekezo yaliyo katika taarifa za ukaguzi zilizotolewa na wao hata zile zilizotolewa na wakaguzi wa nje na maelekezo yanayotolewa na waangalizi wengine kama mamlaka za usimamizi na kamati za Bunge,"amesema.

Pia amesema ikumbwe kwamba Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa kuishia mwaka 2025 unasisitiza kuhusu  utawala bora ni msingi muhimu na uwekaji wa utamaduni wa uwajibikaji.Utawala bora ni msingi muhimu katika kusuma mbele ajenda ya maendeleo ya nchi yetu.

Hata hivyo amesema ili kuwezesha utekelezaji kikamilifu wa mapendekezo yaliyotolewa katika taarifa za ukaguzi katika mnyororo wa uwajibikaji na usimamizi bora wa masuala ya fedha ni wazi kuwa Serikali ilihitaji mfumo madhubuti wa kukusanya taarifa sahihi za mapendekezo ya wakaguzi yaliyotekelezwa na mapendekezo ambayo hayajatekelezwa kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi.

"Mfumo huu ambao nimeuzindua utakapatikana kwa njia ya mtandao mahali popote alipo mkaguzi wa ndani wa taasisi za umma , utakuwa rafiki katika kuutumia , utaweza kuboreshwa bila kutumia gharama kubwa na kuwaongeza watumiaji wengine watakaoonekana ni muhimu na hauna gharama za mara kwa mara za leseni,"amesema Shaaban.

Ameongeza anazo taarifa kuwa pamoja na kuwa na Serikali inao wakaguzi wa ndani zaidi ya 1,200 ni wakaguzi wakuu wachache tu wasiozidi 200 waliopatiwa mafunzo ya matumizi ya mfumo huo na ambao kwa sababu wanautumia kuwalisha taarifa zao kwa mlipaji mkuu wa Serikali.Pia amesema amefuatilia mfumo huo bado unachangamoto chache zilizojitokeza baada ya kuutumia kwa majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ametaja baadhi ya changamoto hizo ni kutotambua  wadau muhimu kama maofisa masuuli, wasimamizi wa mashirika ya umma walioko katika ofisi ya Msajili wa Hazina, wasimamizi wa wakaguzi wa ndani.Hivyo ni matarajio yake baada ya uzinduzi huo changamoto hizo zitapata ufumbuzi wake kwa mfumo kufanyiwa marekebisho ili kuwaungiza wadau wengi zaidi. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi. Amina Shaaban akizungumza mbele ya Wageni waalikwa (hawapo pichani), leo jijini Dar wakati wa kuzindua rasmi mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa Taarifa za ukaguzi (Goverment Audit Report Implementation Information Tracking Systtem-GARIITS). Wageni waalikwa hao pia Washirika wa Maendeleo  kupitia mpango  wa kuboresha  usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa na mfumo huo.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mhandisi Amin Mcharo akieleza namna ya kutumia mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa Taarifa za ukaguzi (Goverment Audit Report Implementation Information Tracking Systtem-GARIITS) mbele Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi Amina Shaaban na Wageni waalikwa mbalimbali ambao ni Washirika wa Maendeleo kupitia mpango huo wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa na mfumo huo.
Sehemu ya Washirika wa Maendeleo kupitia mpango wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),wakifuatilia aliyokuwa akizungumza mgeni rasmi kuhusina na mpango huo muhimu kwa Serikali.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi. Amina Shaaban  akiwa katika picha ya pamoja na Washirika wa Maendeleo kupitia mpango huo wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa na mfumo huo.Picha na Michuzi JR (MMG).

WATAFITI NCHINI WATAKIWA KUWASILISHA ANDIKO LA UTAFITI KWA WADAU

$
0
0
Watafiti nchini wameshauriwa kuwasilisha andiko lolote la utafiti kwanza kwa wadau wa utafiti kabla ya kuomba kibali Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH ili wadau hao waweze kutoa ushauri wao kuhusu utafiti unaofanywa kwenye sekta yao na hivyo kufanya tafiti kuwa na tija zaidi kwa taifa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu na taasisi za Utafiti na maendeleo nchini kujadili kuhusu maadili, Taratibu,Sheria na kanuni za kufanya utafiti nchini iliyoandaliwa na COSTECH kwenyew ukumbi wa Taasisi ya elimu ya kujiendeleza kwenye Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.

Amesema ili tafiti ziweze kuleta tija zaidi na kuondoa changamoto za kurudia kufanya utafiti kuna kila sababu ya Watafiti kuwasilisha kwanza mawazo yao kwenye wizara au sekta husika kabla ya kupeleka maombi ya kufanya utafiti wowote kwenye Tume hiyo kwaajili ya kupitiwa na kupata kibali.

Dkt. Nungu amesema kumekuwa na lawama nyingi kwa baadhi ya watafiti kwamba vibali vya kufanya utafiti vinacheleweshwa na COSTECH kitu ambacho amesema inatokana na wao kuwasiliana na taasisi husika ama wadau wa utafiti kabla ya kupeleka kwenye kamati maalumu ya kitaifa kupitia na kuwapa ruksa ya kutoa kibali husika cha utafiti.

’’Mathalani unafanya utafiti kwenye Elimu tunategemea Utafiti wako utakuja kubadilisha ua kuboresha sera hivyo ni muhimu Wizara ya Elimu iweze kujua kinachofanyika ili nao waweze kutoa neno maana inawezekana ukafanya utafiti ambao majibu yao wanayo tayari’’ Alisema Dkt. Nungu.

Mkurugenzi huyo Mkuu wa COSTECH ameongeza kuwa eneo lingine ambalo  wadau hao watajadiliana na kutoa mapendekezo ya pamoja ni namna ambavyo Mtafiti wa ndani anavyotakiwa kushiriki kwenye utafiti wa watu kutoka nje ya nchi hasa baada ya kugundua kuwa watafiti wa ndani huandikwa tu kwenye makaratasi kukithi vigezo vya kufanya utafiti lakini hawashiriki na hawafahamu lolote kuhusiana na hatua na utafiti unavyofanyika.

‘’ Taratibu za mtu kufanya utafiti kutoka nje ya nchi zinamtaka mtafiti huyo kuwa na mtafiti kutoka Tanzania lakini cha ajabu mtafiti wa ndani unapomuuliza kuhusu utafiti unavyoendelea na hatua zilizofikiwa hana majibu anakuambia anajua mtafiti wa nje kitu ambacho sio sawa katika taratibu za vibali vya kufanya tafiti za aina hizo’’ Alifafanua Dkt. Nungu.

Dkt. Nungu amesema haya na mambo mengine mengi ndiyo yaliyotufanya tukusanyike hapa kama wadau ili tuweze kufahamishana na kupeana ushauri wa namna ya kuboresha namna ya utendaj kazi kwenye eneo la utafiti ili ziweze kuleta tija nchini.

Kwa upande wake makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka ambaye ni mshirki wa warsha hiyo amesema utafiti unasaidia kutatua changamoto za nchi lakini pia lazima uzingatie vigezo na maadili ya kufanya taifi ili ulete tija kwa taifa.

Amesema ili Utafiti uingie na kutambuliwa na Taifa lazima upitie COSTECH ambao ndio waratibu wa tafiti zote ili kuweza kufikia malengo na serikali iweze kuutumia kwa manufaa ya jamii na Taifa badala ya watafiti kuishia kwenye taasisi zao kabla ya kushirikisha wadau.

Amesema kukutana kwao kwenye warsha hiyo kutasaidia sana wakuu wa taasisi kuweza kuwasaidia watafiti wake kutimiza vigenzo na masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za tafiti ili kuwa na Utafiti bora lakini pia kuwahisha kupata kibali kutoka COSTECH.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Dkt. Amos Nungu akizungumza na Waandishi wa habaru nje ya ukumbi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Dkt. Amos Nungu akifungua Warsha hiyo.
 Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mkutano.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Dkt. Amos Nungu akizungumza na Waandishi wa habari nje ya Mkutano.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images