Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Polisi : Idriss anatafutwa na akikamatwa atahojiwa

0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa Msanii wa Vichekesho Idriss Sultan hajalipoti katika kituo chochote cha Polisi kufuatia na Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam la kumtaka msanii huyo kujisalimisha katika kituo cha Polisi kwa kutumia picha yenye nembo ya alama ya taifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania.

Akizungumza na Michuzi TV Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Razaro Mambosasa amesema kuwa Msanii huyo anatafutwa na hakuna taarifa ya kuripoti katika kituo cha Polisi chochote cha jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Msanii Idriss Sultan anatafutwa na Jeshi la Polisi na mara baada kuripoti au kukamatwa lazima ahojiwe kwa kile alichokifanya kwa kutumia alama za Taifa kutumia bila mamlaka.

Msanii Idriss Sultan alipiga picha na kuweka nembo ya Kiti anachotumia Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania wakati ikiwa ni siku ya kuzaliwa kwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli Oktoba 29.

Baada ya picha Idriss Sultan kusambaa katika mitandao ya Jamii Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliandika katika mtandao wake kwa kumtaka Msanii huyo afike katika kituo chochote cha Polisi na kusema kuwa taarifa atazikuta huko.

WAZIRI JAFO AKIRI KUPOKEA BARUA YA CHADEMA, ATOA AGIZO KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI

0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amekiri kupokea barua kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilichokua kikilamikia mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mhe Jafo amesema Ofisi yake imepokea malalamiko kutoka kwa Vyama vya Siasa, Wadau mbalimbali pamoja na watu binafsi na kuwataka wasimamizi wa uchaguzi huo kufuatia kanuni za uchaguzi ili kuondoa dosari zote ambazo zimeshajitokeza hadi sasa.

Jana CHADEMA ilitangaza kuiandikia Ofisi ya Rais-TAMISEMI juu ya kuwepo kwa dosari kwenye uchaguzi huo ikiwemo wagombea wake kunyimwa fomu huku sehemu nyingine wagombea wakipewa fomu ambazo hazijasainiwa.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Mhe Jafo amesema dosari ambazo zimejitokeza ni chache na tayari wameshaanza kuzifanyia kazi ili kuepukana na malalamiko ambayo yameanza kutolewa.

Pia amevitaka vyama vya siasa vyote kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria pamoja na masharti wakati wote wa zoezi la uchukuaji na Urejeshaji wa fomu za uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya zoezi la uchukuaji fomu ikiwa Leo ni siku ya pili ya zoezi hilo.

Waziri Jafo amesema kiujumla zoezi hilo limeenda vizuri licha ya kuwa na dosari baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na baadhi ya vikwazo na zoezi hilo likashindwa kufanyika kiufasaha lakini dosari hizo zinafanyiwa kazi.

"Zoezi limeenda vizuri tuna kata 3959 na Kati ya kata hizo ni kata 72 tu ndio zilizokuwa na dosari ambapo zoezi hilo halikufanyika kifasaha na miongoni mwa maeneo yaliyokuwa na malalamiko ni Liwale Lindi, Moshi, Sengerema na Songwe baadhi ya maeneo hayo" 

"Niwatake wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao katika maeneo yote wahakikishe wanasimamia kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizowekwa kuhakikisha wanaondoa changamoto zilizojitokeza wakati wa zoezi hili" amesema Waziri Jafo.

Aidha amesisitiza vyama vyote vya siasa kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya kuepusha uvunjifu wa Sheria na kuvuruga amani wakati wote wa zoezi hilo.

Amesema zoezi hilo ni la siku Saba hivyo Wizara yake ambayo ndio msimamizi wa uchaguzi huo wanaendeleo kuzifanyia kazi dosari zote ambazo zimejitokeza katika maeneo yenye malalamiko wakati wa zoezi hilo kuhakikisha linaisha salama na kila mtu anapata haki yake.

Amesema maeneo yote ambayo zoezi hilo halikwenda vizuri wawasilishe malalamiko yao kwenye kamati za rufaa na maadili zilizopo katika maeneo yao ili kuondolewa kwa dosari ambazo wanahisi hazikuwekwa vizuri wakati wa zoezi hilo.

Aidha amesema maagizo yake aliyoyatoa hayajapuuzwa bali changamoto zilizojitokeza ni za kawaida ambazo hutokea katika uchaguzi wowote duniani na zitaendelea kutatuliwa na Ofisi yake ambayo ndio wasimamizi wa uchaguzi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma juu ya maendeleo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

MTATIRO AWACHARAZA VIBOKO WANAFUNZI WATORO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Julius Mtatiro ameendeleza kampeni ya kiwilaya ya kupambana na utoro sugu, nidhamu za wanafunzi na mimba za utotoni wilayani Tunduru, na leo amewaelekeza walimu kuwaadhibu watoro sugu mbele ya wazazi wao na amezionya pande zote zinazohusika na uzembe huo.

Katika kampeni hiyo Ndg. Mtatiro ameelekeza wazazi wa wanafunzi sugu kwa utoro na watoto wao wajisalimishe kwenye shule zote za Sekondari na Msingi katika wilaya hiyo.

Katika kutekeleza agizo hilo watendaji wa kata, waratibu elimu kata na walimu wa shule zote wameendelea kutoa adhabu kwa wanafunzi hao na kuwaonya wazazi ambao wameshindwa kuwasimamia watoto.

Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Ligoma iliyoko tarafa ya Namasakata Wilayani Tunduru Ndg. Mtatiro amewaonya wazazi wa watoto sugu kwa utoro kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika wilaya nzima ni kali mno dhidi yao.

"Rais Magufuli na serikali yale anatenga Shs Bilioni 23.6 za kitanzania kila mwezi ili msome bure, nyinyi na wazazi wenu mnachekeana na kupuuza masomo, mnalifanya taifa linapoteza fedha nyingi na Rais anahangaika kutumia kodi za watanzania ili watoto wenu wapate elimu wawe na maisha bora lakini mnapuuza juhudi hizo", ameeleza mhe. Mtatiro.

Ndg. Mtatiro amewaelekeza maafisa wote wanaosimamia elimu na utawala katika vijiji na kata za Tunduru kuendelea na msako mkali kuhakikisha watoto wote wanaendelea na masomo na ikibidi wazazi wachukuliwe hatua kali, maelekezo hayo yameanza kutekelezwa na wazazi wengi ambao wanawasalimisha watoro sugu kwenye shule zao.

TANZANIA KUANZISHA KITUO CHA KIMATAIFA CHA USULUHISHI WA MIGOGORO YA KIBIASHARA

0
0

Na Mwandishi wetu, Abidjan,Ivory Coast.

Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.

Prof. Kabudi amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia Tanzania kuweka mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania hasa baada ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ya muundo mpya wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ili kuiwezesha kutoa ushauri wa kina na wa kitaalam kwa serikali lakini pia kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa.

Ameongeza kuwa maombi ya Tanzania kwa taasisi hiyo kwa ajili ya kuisaidia ofisi ya mwanasheria na wakili mkuu wa serikali yamekamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni kuwasilisha maombi hayo kwa kikao cha bodi ili utekelezaji uanze.

Ameongeza kuwa eneo jingine ambalo Tanzania inahitaji msaada kutoka kwa Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni kuhusu kuisaidia Tanzania katika hatua iliyoichukua ya kutunga sheria mpya ya usuluhishi wa migogoro ya kimataifa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo kipya cha kusimamia usuluhishi wa migogoro.

Katika eneo hilo Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa wataalamu kusaidia Tanzania kupitia miswaada ambayo imeandaliwa na serikali pia kuandaa andiko la namna kituo hicho kitawekwa Tanzania na kukidhi matakwa ya kimataifa.

Kwa uoande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika Bw Stephen Karangizi amesema wamepokea ombi hilo na kwamba wanasubiri maamuzi ya kikao cha bodi ili kuweza kuanda program maalum kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

Ameongeza kuwa nchi nyingi za Kiafrika zimeshindwa katika usuluhishi wa migogoro hususani ya kibiashara,madini,mafuta na gesi na maeneo mengine na kuongeza kuwa suala hilo linapaswa kuwekewa mkakati maalum na kutekelezwa kwa haraka ili kuepuka makosa yaliyokwisha kufanywa katika siku zilizopita.

Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilianzishwa kutokana na ombi la Mawaziri wa fedha kutoka Afrika kwa lengo la kuzisaidia Nchi za Afrika kujijengea uwezo katika masuala ya kisheria hususani katika madini,mafuta na gesi pamoja na madeni ili kuziwezesha nchi za Kiafrika kuwa na uwanda sawa wa majadiliano katika ngazi za Kimataifa kuhusu masuala ya kisheria yanahusu biashara na makampuni ya Kimataifa. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi 

TANZANIA KUANZISHA KITUO CHA KIMAHAKAMA NA USULUHISHI WA MIGOGORO YA KIMATAIFA

0
0
Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.

Prof. Kabudi amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia Tanzania kuweka mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania hasa baada ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ya muundo mpya wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ili kuiwezesha kutoa ushauri wa kina na wa kitaalam kwa serikali lakini pia kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa.

Ameongeza kuwa maombi ya Tanzania kwa taasisi hiyo kwa ajili ya kuisaidia ofisi ya mwanasheria na wakili mkuu wa serikali yamekamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni kuwasilisha maombi hayo kwa kikao cha bodi ili utekelezaji uanze.

Ameongeza kuwa eneo jingine ambalo Tanzania inahitaji msaada kutoka kwa  Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni kuhusu kuisaidia Tanzania katika hatua iliyoichukua ya kutunga sheria mpya ya usuluhishi wa migogoro ya kimataifa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo kipya cha kusimamia usuluhishi wa migogoro.

Katika eneo hilo Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa wataalamu kusaidia Tanzania kupitia  miswaada ambayo imeandaliwa na serikali pia kuandaa andiko la namna kituo hicho kitawekwa Tanzania na kukidhi matakwa ya kimataifa.

Kwa uoande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika Bw Stephen Karangizi amesema wamepokea ombi hilo na kwamba wanasubiri maamuzi ya kikao cha bodi ili kuweza kuanda program maalum kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

Ameongeza kuwa nchi nyingi za Kiafrika zimeshindwa katika usuluhishi wa migogoro hususani ya kibiashara,madini,mafuta na gesi na maeneo mengine na kuongeza kuwa suala hilo linapaswa kuwekewa mkakati maalum na kutekelezwa kwa haraka ili kuepuka makosa yaliyokwisha kufanywa katika siku zilizopita.

Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilianzishwa kutokana na ombi la Mawaziri wa fedha kutoka Afrika kwa lengo la kuzisaidia Nchi za Afrika kujijengea uwezo katika masuala ya kisheria hususani katika  madini,mafuta na gesi pamoja na madeni ili kuziwezesha nchi za Kiafrika kuwa na uwanda sawa wa majadiliano katika ngazi za Kimataifa kuhusu masuala ya kisheria yanahusu biashara na makampuni ya Kimataifa.

SIMBA SC YAANDAA MKUTANO MKUU WA KAWAIDA DESEMBA 8, 2019 JIJINI Dar es Salaam

NEWS ALERT: Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) yatoa trilioni 1.5 kwa Ujenzi wa uwanja wa ndege wa msalato jijini Dodoma

0
0

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma na kuahidi kuidhinisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 455 sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato sambamba na ujenzi wa barabara za mzunguko Jijini humo.


Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina (pichani kulia) ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abijdan Nchini Ivory Coast wakati wa Mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lakini pia kwa Tanzania.



Amesema Benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha dola za marekani milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma na kwamba kiasi kingine cha dola za marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato kinatarajiwa kuidhinishwa na mapema mwezi Novemba 2019.



Dkt. Adesina ameongeza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ina imani na mageuzi ya kiuchumi yanayotekelezwa chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu bila malipo,afya na maji pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuleta uwajibikaji katika taaisisi za uma na kwamba iko tayari kuunga jitihada hizo za serikali kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu.



Aidha Dkt. Adesina ameelezea nia yake ya kutaka kushudia bara la Afrika likipiga hatua kubwa za kimaendeleo sasa na kwa haraka na sio kusubiri baadae na kwamba katika kipindi chake cha uongozi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika atapambana kuhakikisha azma hiyo inatekelezeka.



Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimae Bara zima la Afrika.



Prof. Kabudi ameongeza kuwa tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika iko tayari kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa yaani Standard Gauge Railway ya kipande cha kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda na kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara baada ya kukamilika mchakato wa utoaji wa fedha hizo ambapo mazungumzo ya awali kuhusu ufadhili huo yameanza.



Pia Prof. Kabudi amemtaka Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina kuimarisha ofisi za kanda za benki hiyo ili ziweze kutoa huduma zote za kibenki ili kusogeza huduma karibu na wanufaika wa benki hiyo sambamba na kuunga mkono miradi yote ya kimkakati inayounganisha nchi na nchi katika bara la Afrika ili kuboresha nakurahisisha huduma ya usafiri katika Bara la Afrika na hivyo kuwezesha biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na kujiletea maendeleo.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi yuko Abijdan Nchini Ivory Coast kushiriki mkutano wa siku mbili wa dharura wa Mawaziri wa fedha uliondaliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB).

SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI UZINDUZI WA KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE LA KENYA ZA LUGHA YA KISWAHILI, TAARIFA ZA MWAKA ZA UTENDAJI KAZI WA KAMATI BUNGENI JIJINI NAIROBI

0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizindua Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za lugha ya Kiswahili katika hafla iliyofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya. Kuanzia kushoto ni Kiongozi wa Walio wengi Bungeni (Majority Leader), Mhe. Aden Duale, Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi na Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Moses Cheboi.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge na Wageni waalikwa (hawapo kwenye picha) katika hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za lugha ya Kiswahili na taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati tukio lililofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya.





Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za lugha ya Kiswahili na taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati tukio lililofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za lugha ya Kiswahili na taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati tukio lililofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya. Kulia ni Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi na Kushoto ni Kiongozi wa Walio wengi Bungeni (Majority Leader), Mhe. Aden Duale.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizindua taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati katika hafla iliyofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi na Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Moses Cheboi.

RC MAKONDA AFANIKISHA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 500 WENYE TATIZO LA MOYO KWA KIPINDI CHA MWAKA MZIMA

0
0


********************************************

Ubalozi wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE umeendelea kuunga mkono kampeni ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto kutoka familia duni Iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda ambapo leo October 31 wamemkabidhi hundi ya Shilingi Milioni 27 kwaajili ya Bima za Afya kwa Watoto 500 wenye Tatizo la Moyo.

RC Makonda amesema kiasi hicho cha fedha kitawezesha Watoto 500 wakiwemo yatima na Wanaotokea familia duni Waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kupata Bima za Afya zitakazowawezesha kupata Matibabu Bure kwa kipindi cha Mwaka Mzima.

Aidha RC Makonda amesema uamuzi wa kuwatafutia Bima za Afya umekuja baada ya kubaini Watoto wengi wanaofanyiwa upasuaji wanahitajika kwenda Clinic kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya Afya na Dawa lakini kutokana ugumu wa maisha wanashindwa kumudu gharama jambo linalowafanya Wazazi au Walezi wao kuuza Mali walizochuma kwa muda mrefu ili wapate fedha na mwisho wa siku familia inazidi kuwa maskini.

Pamoja na hayo RC Makonda amemshukuru Balozi kwa kuendelea kumuunga mkono katika mambo mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto 100 wa kike kidato cha tano na sita, Kumpatia madaktari bingwa wa Moyo Waliofanya upasuaji kwa watoto 60, Kumsaidia futari kwaajili ya Maimamu wa Misikiti 800 huku akitoa wito kwa Wananchi kuwa na moyo wa upendo wa kusaidia wenye uhitaji.

Kwa upande wake Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Bw. Khalifa Abdulrahman Almarzooqi amesema kuwa Ubalozi huo unafurahishwa na kazi nzuri ya RC Makonda katika kusaidia Wananchi wenye uhitaji ndio maana wameamua kushirikiana nae kwa kila jambo kwakuwa kila msaada anaoupokea unawafikia walengwa.

kongamano la kwanza la Dar Business Expo 2019 lafana

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), Bw. Francis Nanai, akiwahutubia washiriki wa kongamano la kwanza la Dar Business Expo 2019 lililofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Kilimnjaro jijini Dar es salaam na kushirikisha wajasiriamali wa Ndani na nje ya jiji hilo


Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Donatus Richard (kulia), akitoa mada katika kongamano hilo kulia kwake ni watoa mada wenzake


Washiriki wa Kongamano hilo wakisikiliza  mada zilizokuwa zikitolewa


Washiriki wa Kongamano hilo wakirekodi na kufuatilia   mada zilizokuwa zikitolewa
Waandaaji na watoa mada wa kongamano la kwanza la Dar Business Expo 2019 lililofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Kilimnjaro jijini Dar es salaam

Picha ya pamoja ya waandaaji, watoa mada na washiriki wa kongamano la kwanza la Dar Business Expo 2019 lililofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Kilimnjaro jijini Dar es salaam

Katibu Tawala wa wilaya ya Kalambo Frank Sichalwe akiwaasa wakazi wa mpakani kudhibiti mamluki

Rais Magufuli Angoa Mizizi ya Kufanya Kazi kwa Mazoea

0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli

Na Lillian Shirima–Maelezo

Imetimia miezi 48 sasa sawa na miaka minne tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipochukua jukumu rasmi la kuiongoza nchi Novemba 5, 2015.

Kiongozi huyu amefanikiwa kuhakikisha watanzania wanatoka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo badala ya kubaki kama walivyo miaka nenda miaka rudi. Aina ya uongozi wa rais Magufuli umeonesha uwezo au karama ya kuondoa taratibu zilizooleka katika jamii na kisha kubuni, kuelekeza njia sahihi kwa vitendo ni ushindi wa mafanikio katika uongozi wake.

Katika kipindi kifupi rais Magufuli amekuwa gumzo ndani na nje ya nchi kutokana na uwezo alionao kushawishi watu kufikia maendeleo yaliyotarajiwa kwa kuondoa taratibu zisizofaa kama vile uzembe kazini, ubadhirifu wa mali ya umma, na huduma mbovu za jamii kama vile maji safi na salama, elimu, afya.

Akihojiwa na Idara ya Habari Maelezo mchambuzi na mtafiti wa wa masuala ya uchumi na siasa Dkt. Bravious Kahyoza anamuelezea Rais John Pombe Magufuli kama kiongozi mwenye uthubutu wa kuamua mambo mazito na kuyatekeleza kwa wakati kwani ameweza kuvunja taratibu zisizofaa ambazo zilikuwa kizingiti cha maendeleo ya nchi jambo ambalo limemjengea imani kwa wananchi .

“hakuna jinsi nyingine kubwa ya kuhakikisha watu wanatoka hatua moja kwenda hatua nyingine kama taratibu za maisha yao zinabaki zilivyo na tafsiri za kiuchumi duniani zinaonesha kuwa maendeleo ya watu kiuchumi yanahusiana na utaratibu wa maisha ya watu wenyewe, Rais wetu amevunja taratibu korofi ”. Anasema Dkt. Kahyoza.

Aidha, ameongeza kuwa kinachomtofautisha rais Magufuli na viongozi wengine kiasi cha kusababisha awe gumzo ndani na nje ya nchi ni muda mfupi aliotumia kuleta mageuzi makubwa nchini. Pia namna alivyoonesha mfano wa kubana matumizi katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa nchi. 

Mwandishi David Lender katika kitabu chake cha ‘The Wealth and Poverty of Nations: why some are so rich and some are so poor (Utajiri na Umasikini wa Mataifa: kwanini mengine ni tajiri na mengine masikini. Kitabu hicho kimeeleza kwamba mataifa ambayo yameweza kuwa na sehemu kubwa ya mabadiliko kati ya miaka 1961 na 2014 ni yale yaliyobadilisha taratibu na tabia za watu zilizooeleka na kuzielekeza kwenda kwenye mtazamo wenye tija kwa taifa lao, miongoni mwa mataifa hayo ni ulaya na Asia katika nchi za Uingereza, Japan na Afrika ni nchi za Namibia, Botswana, Rwanda na Ethiopia.

Anasema, mfano hai ni kama vile uandaaji wa sherehe za kitaifa za gharama kubwa, sherehe wakati wa uteuzi wa viongozi mbalimbali, kumbukumbu za kitaifa, sherehe za uhuru, muungano na uzinduzi wa miradi ambapo fedha nyingi hutumika kusherehesha wakubwa serikalini na baadhi ya jamii.

Rais Magufuli alichukua hatua ya kubatilisha taratibu za ufanyaji wa sherehe hizo kwa kufanya kazi za kijamii kama vile usafi, kuhudumia wagonjwa na mara kadhaa kutumia fedha husika kwa ajili ya manufaa ya taifa ambapo sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru aliagiza fedha zitumike kwenye ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco. 

Pia, Rais Magufuli alipounda Baraza la Kwanza la Mawaziri 2015, Baraza lilikuwa mawaziri 19 tu huku baadhi ya wizara zikibaki bila naibu mawaziri. Rais aligiza kiasi cha shilingi bilioni 2 zilizokuwa zitumike kwaajili ya semina elekezi kwa viongozi wapya zipelekwe Wizara ya Elimu kutunisha fungu la elimu bure ikiwa ni pamoja na kununua madawati ya wanafunzi.

Rais hakuishia hapo, alizuia safari za viongozi nje ya nchi zisizokuwa za lazima na yeye mwenyewe kupunguza safari zake nyingi nje ya nchi na kuagiza balozi kumwakilisha katika masuala ya Kimataifa.

Aidha, uzoefu wake katika kulitumikia taifa kwa muda mrefu, aligundua ndani ya utumishi wa umma yapo makundi mawili ya wafanyakazi wanaolipwa mshahara kwa mazoea. Kundi la kwanza ni watumishi ambao kwenye kumbukumbu za utumishi wanaonekana waajiriwa wa serikali wanaolipwa stahiki zote za utumishi lakini si watumishi ambao kwa idadi walikuwa 20,000.

Kundi la pili ni watumishi ambao kwa mazoea wanafanya kazi lakini hawana sifa kwa nafasi walizonazo kwa idadi walikuwa 14,000. Watumishi hao baadhi walitumia vyeti visivyo sahihi kuajiriwa na wengine walifanya kazi za taaluma ambazo hawakuwa na ujuzi nazo.

Kwa mamlaka aliyonayo, Rais Magufuli alitoa agizo kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha watumishi wa aina hiyo wanaondolewa sehemu zao za kazi. Zaidi ya watumishi 10,000 walipoteza ajira na serikali iliokoa zaidi ya shilingi Bilioni 15 za mishahara hewa huku Wakuu wa Mikoa walioshindwa kutekeleza agizo hilo kwa usahihi nyadhifa zao zilitenguliwa.

Pengine hali hii ndio iliyokuwa inasababisha hasira dhidi ya serikali kwakuwa wananchi hawakuona huduma zinatolewa kama zinavyostahili. Dkt. Kayhoza alisema kuwa nanukuu maneno ya rais Magufuli “Naagiza wakuu wote wa mikoa hakikisheni watumishi hewa yaani ambao hawapo wanaondolewa kwenye orodha ya utumishi na sehemu zao za kazi’. 

Pia, matokeo yake ndani ya kipindi kifupi serikali iliweza kutangaza nafasi za kwa wenye sifa katika sekta nyingi mathalani Tamisemi ilitangaza ajira mpya kwa walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na sekta ya afya na nyingine nyingi. 

Hii leo watanzania tunaona mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika utumishi wa umma.

Dkt. Kayhoza anasema, Rais Magufuli ameonyesha dhahiri kuwa kiongozi bora asiye mlalamishi bali ni kiongozi anayetafuta ufumbuzi wa kila changamoto anayokutana nayo. Aidha, ni kiongozi mwenye uthubutu , maamuzi sahihi, mtekelezaji, mfuatiliaji wa maamuzi yake mpaka yanapokamilika. 

“Hii inaonesha dhahiri uwezo alionao wa kuzisoma nyakati na kuhakikisha nyakati hizi zinaweza kutafsiriwa si tu kwa nchi anayoiongoza lakini pia kuangalia uchumi wa nchi unategemea masuala gani yanatokea na namna gani yanaweza kusaidia nchi kwenda mbele”. Amesema Dkt Kahyoza.

Maamuzi mengine aliyoyafanya ni serikali yake kuhamia Dodoma. Hadi sasa Mawaziri wote chini ya Waziri Mkuu, Naibu Mawaziri, Makatibu na Kurugenzi zote muhimu zimehamia Dodoma.

Uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma haukupewa kipaumbele kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita tangu ulipoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye 1970. Kutokana na umuhimu wa kuhamia Dodoma watumishi wa serikali waliokuwa makao makuu walihamia Dodoma. Hili ni funzo kwetu ambapo tukiamua tunaweza kwani ndani ya matumizi na mazingira yetu ya kawaida inawezekana tukapanga na tukatekeleza mambo yetu wenyewe kwa ufanisi.

Akitoa mfano juu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kufua umeme katika Mto Rufiji Dkt. Kahyoza amesema “Licha ya mradi huu utakaozalisha kilowati 2115 za umeme kupingwa na kukabiliwa na vizingiti ndani na nje ya nchi, Rais Magufuli ameweza kuvunja vizingiti hivyo ambapo Julai mwaka huu alizindua rasmi ujenzi wa bwawa la mto Rufiji utakaogharimu fedha za Tanzania za shilingi trilioni 6.5. 

Suala lingine ambalo rais Magufuli aliahidi kupambana nalo ni ukusanywaji wa kodi ambapo ukaguzi kwa kila sekta umekuwa mkubwa na matokeo yake ni kuongezeka kwa mapato ya taifa kutoka shilingi milioni mia nane kwa mwezi hadi kufikia shilingi trilioni 1.7 Septemba, 2019.

Rais alisema“unapouza toa risiti na unaponunua dai risiti”. Alianza kwa kusisitiza kwa mtu mmoja mmoja kudai risiti kwa kila huduma anayopatiwa na baadaye akahimiza wafanyabiashara kulipa kodi ikiwa ni pamoja na taasisi za serikali kulipa kodi baada ya kupatiwa huduma au bidhaa.

Hali hii imeleta mageuzi kwa kila mfanya biashara kuwa na mashine ya EFD (Eletronic Fiscal Divice) kitu ambacho hakijawahi kutokea miaka iliyopita. Amemalizia Dkt. Kayhoza

Naye Projestus Rwegarulila Mkurugenzi wa Mradi wa Utamaduni na Uzalendo anasema, Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kutumia lugha ya Kiswahili kwenye mikutano mbalimbali ya Kimataifa anayoshiriki jambo halijawahi kufanyika kwa viongozi wetu hivi karibuni. 

“Kitendo cha Rais kuongea Kiswahili kwenye mikutano ya kimataifa kimewalazimu wasiojua lugha hiyo kutafsiriwa na wengine kuamua kujifunza Kiswahili”. Anasema Rwegarulila.

Anasema, pamoja na watu kuvutiwa na kile anachozungumza Rais kwenye mikutano, kasi ya maendeleo ya Tanzania kwenye sekta mbalimbali ndiyo inawavuti wageni kuja kujifunza namna ambavyo nchi imepiga hatua kama vile mradi kama vile mwendo kasi, kuanzishwa kwa sera sera mpya ya madini, ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme ni baadhi ya baadhi ya mambo yanayoamsha kiu ya mataifa mengine kujifunza kutoka kwetu.

Na hakuna lugha nyingine isipokuwa kutafsiri Kiswahili katika lugha zao.

Naye mwanafunzi Hamida Khamis wa shule ya msingi Bunge jijini Dar es Salaam amesema kabla ya serikali ya awamu ya tano shule yao haikuwa na madawati ya kutosha, wanafunzi walikuwa wanasukumana kutafuta nafasi za kukaa kwenye dawati lakini mpango wa elimu bure umefanikisha shule kupata madawati ya kutosha. 

Mkazi wa Mugumu Serengeti Herman Peter yeye anasema, kabla Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani huduma za afya zilipatikana katika Halmashauri ya Serengeti tu lakini sasa huduma zimesogezwa karibu baada Serikali kujenga Kituo cha Afya katika kata yao ya Nata kwa gharama ya shilingi milioni 400. 

Nimalizie kwa kusema vema tukafahamu Rais John Pombe Magufuli ameweza kuondoa taratibu zilizokuwa zikichelewesha nchi kusonga mbele. Hakuleta sheria mpya au sera mpya, alichokifanya ni kuhakikisha yeyote anayepewa dhamana ya uongozi anatimize wajibu wake, anaposhindwa kuleta mabadiliko ndani ya muda mfupi anamwondoa katika madaraka aliyokuwa nayo. 

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Tanzania na ALSF zakubaliana kuandaa mkakati wa mafunzo ya kisheria

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa kishheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) mara baada ya kumaliza majadiliano kuhusu kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa kishheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) mara baada ya kumaliza majadiliano kuhusu kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP). Wa pili kutoka kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.

Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bwana Stephen Karangizi(kulia) akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) wakati wa majadiliano kuhusu kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) anayefuatia baada ya Bw. Stephen Karangizi ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.

MTUHUMIWA SUGU WA UHALIFU AJISALIMISHA

0
0
Na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri ameahidi kumsaidia fedha shilingi milioni moja mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi,baada ya kujisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya waandishi wa habari na Kamati ya Ulinzi na Usalama  wa Manipsaa hiyo mara baada ya Ali Mtemi ambaye ni mtuhmiwa sugu wa uhalifu kufika na familia yake mbele ya kamati hiyo na kukili kuhusika kwa baadhi ya matukio huku akitubu na kuomba msamaha kwa kujutia kile alichokifanya kwa muda wote.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kulia) akizungumza mbele ya waandishi wa habari, ambapo ameahidi kumsaidia fedha shilingi milioni moja mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi ambapo amejisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akimpongeza mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi ambapo amejisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.

 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwapongeza ndugu wa mtuhumiwa sugu aliyekili na kuhusika kwenye makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi ambapo amejisalimisha mbele ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Manispaa hiyo.kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija.

MSANII HARMONIZE ALIVYOUTAMBULISHA WIMBO WAKE UITWAO UNO KWA WAKAZI WA MBAGALA

0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Msanii wa Kizazi kipya nchini, Rajabu al maarufu kwa jina la Harmonize ametambulisha kibao chake kipya cha UNO kwa wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kwa mara ya kwanza kujitokeza kwa mashabiki wake tangu ajitoe kwenye Kundi la Wasafi.

Harmonize katika utambulisho huo amesindikizwa na Wasanii wa Bongo Fleva na Wasanii wa Hip Hop pamoja na Wasanii wa mziki wa Singeli wakiwakilishwa na Msanii maruufu wa miondoko hiyo ya Singeli, Mzee wa Bwax.

Harmonize amedai miaka minne iliyopita alifika jijini Dar es Salaam ambapo alifikia eneo la Mzinga, Mbagala akitokea nyumbani kwao Mtwara, amesema kabla yakuanza kuimba alifanya kazi yakuuza Mitumba kabla yakujiunga na Kundi la WCB Wasafi.

Katika utambulisho huo, Msanii aliyewahi kutamba na Wimbo wa Mpenzi wangu Bubu, H BABA amemtunuku Tuzo ya heshima, Harmonize baada yakutambua mchango wake kwenye mziki kwa kumtaja kwenye kibao chake.

Hata hivyo, Harmonize ameomba kura kwa mashabiki wake katika Tuzo za MTV EUROPEAN MUSIC AWAARDS 2019 katika Kipengele cha Best African Act zitakazotolewa hivi karibuni wakati yeye akiwa ni mmoja wa Wasanii wanaowania tuzo hizo.

Pia, Harmonize ameahidi kwa mashabiki wake kuwa atafanya 'Show' kama hiyo, Desemba 25 ya mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 










BENKI YA CRDB YAKIPOIGA JEKI CHUO CHA POLISI MOSHI KWA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 10

0
0
Picha ikionyesha wa kwanza kushoto mkurugenzi wa ununuzi na ugavi wa benki ya CRDB Pendason Philemon akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 iliotolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanawake chuoni hapo , kwanza kulia kaimu mkuu wa chuo cha polisi moshi SACP Gemini Mushy hafya iliyofanyika chuoni hapo. Picha na Woinde Shizza


Na Woinde Shizza Michuzi TV, Kilimanjaro 

 Kufuatia changamoto kubwa ya uchakavu wa vyoo vya askari wanafunzi wa kike katika chuo cha polisi moshi (CCP) ambayo imekuwa ikihatarisha afya ya wanafunzi hao wawepo chuoni hapo benki ya CRDB imetoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo vya chuo hicho ili kuwapunguzia adha hiyo wanafunzi wa kike. 

 Msaada huo unakuja wakati mwafaka kutokana na chuo hicho kuwa na majengo ya muda mrefu akikabidhi msaada huo mkurugenzi wa ununuzi na ugavi wa benki ya CRDB Pendason Philemon amesema msaada huo ni moja ya sera maalum iliyojiwekea ya benki hiyo ya kusaidia jamii yenye kuagiza na kuelekeza kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka. 

 “Dhamira hii ya kusaidia jamii kunaifanya benki ya CRDB kuendelea kuwa mdau wa maendeleo kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa jamii inayotuzunguka pamoja na kusaidia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kupeleka huduma za kijamii zenye kukidhi mahitaji ya wananchi hususani katika kuliunga mkono jeshi la polisi katika jitihada zake za kulinda wananchi na mali zao.”alisema Philemon. 

 Alisema benki ya CRDB inafahamu fika kuwa vyoo ni afya na usafi katika maisha ya binadamu yoyote yule duniani hivyo basi waliposikia chuoni hapo na kukuta kina uhitaji wa ujenzi na maborsho ya vyoo vya wananwake hawakusita kama benki kuunga mkono ombi hilo ili kuwezesha ujenzi huo.

 Awali Gemini Mushy kaimu mkuu wa chuo cha polisi Moshi alisema msaada huo uliotolewa na Benki ya CRDB ni muhimu kwa kuwajengea Askari polisi mindombinu bora ambapo licha ya kutumia bajeti ya serikali bado wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundo mbinu chuoni hapo kufuatia majengo hayo kuwa ya muda mrefu. 

 “Ni ombi letu pia katika mipango yenu kuzidi kuangalia mtakavyoweza kutia shime ili kuborsha mazingira ya kuwafundishia askari wetu ili watokapo hapa wawe na ari kubwa Zaidi ya kuwalinda raia na mali zao kwa ufanisi Zaidi ili pato binafsi la mtanzania liweze kukua Zaidi na utashi wa kuwekeza kupitia CRDB uweze kukua sawia”alisema SACP MUSHY 

 Kwa upande wake meneja wa benki ya CRDB kanda ya kaskazini Chiku Issa alisema CRDB iliguswa na hali mbaya ya vyoo vya wanachuo wa kike hivyo kuamua kuasaidia kutatua changamoto hiyo. 

 “Mimi kama mama kwa kweli nilipofika hapa baada ya kupokea maombi kwa mmoja wa wadau ambae ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka niliguswa na kwa kutambua kauli mbiu ya choo ni nyumba niliona ipo haja ya kuwasaidia askari wetu ambao ndio walinzi wa mali zetu na raia” alibainisha Chiku.

Nae mlezi wa wanafunzi wa kike na mkufunzi katika shule ya polisi Tanzania mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Pili Misungwi ameshukuru benki hiyo kwa msaada huo ambao amesema wanaishukuru benki hiyo kwa wepesi na uharaka wa nanma walivyolishughulikia suala hilo ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa kwa wanafunzi askari wa kike. 

 “Tulihusisha wadau mbali mbali lakini mmoja wa wadau waliojitokeza kwa haraka na kuamua kutusaidia ni CRDB kwa kwa kweli kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi nchini na mkuu wa chuo tunaishukuru sana CRDB kwa kutambua umuhumu wa kusaidia askari wanafunzi wa kike kwa sababu maumbile ya kike na kiume ni tofauti kwa kuwa watoto wa kike ni rahisi sana kupatwa na magonjwa endapo mindombinu haitakuwa misafi”alisema SSP Misungwi 

JIJI LA DODOMA LATOZWA FAINI KUTOKANA NA UCHAFU WA MACHINJIO

0
0

Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea machinjio ndogo ya Msalato na kujiona hali mbaya ya mazingira katika eneo hilo. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC imefunga machinjio hiyo na kupiga faini Jiji la Dodoma ya kiasi cha Shilingi Milioni 5.

*****************************

Na Lulu Mussa

Dodoma

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) hii leo imefunga machinjio ndogo ya Msalato kwa muda usiojulikana na kupiga faini kwa kosa la kukithiri kwa uchafu wa mazingira na miundombinu chakavu.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo na kujionea Mazingira yasiyoridhisha kwa usalama wa afya za binadamu.

Katika ziara hiyo, wabunge wamejionea mazingira yasiyoridhisha na kuhatarisha afya za watumiaji wa nyama inayochinjwa machinjioni hapo ikiwa ni pamoja na kurundikana kwa samadi, kukithiri kwa harufu kali na kukosekana kwa maji safi.

Bw. Gratius Mwesiga, Afisa Mifugo wa Jiji la Dodoma ameieleza Kamati hiyo kuwa ukarabati katika eneo hilo umeanza na unaendelea kwa awamu, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa mifumo ya maji taka.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima amesema lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa manufaa ya afya za walaji. "Sisi watu wa Mazingira afya za binadamu ni kipaumbele namba moja, hali hii haikubaliki" Sima alisisitiza.

Waziri Sima amemuagiza Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka kufanya tathmini ya haraka na kina na kuhakikisha kuwa machinjio yanazingatia taratibu zilizopo katika Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Kanali Mstaafu Masoud Ali amesema hali ya usafi katika machinjio hiyo haidhirishi na kuwataka NEMC kuchukua hatua. "NEMC msingechukua hatua, sisi Kamati tungechukua, haiwezekani hali hii haikubaliki" Alisisitiza Mhe. Masoud Ali.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC amelitoza faini Jiji la Dodoma ya kiasi cha Shilingi Milioni tano (5) kwa mujibu wa kifungu namba 194 cha sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kutakiwa kuilipa ndani ya wiki mbili.

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Yabuni Chanzo Kipya Cha Mapato

0
0
Mlango wa kuingilia ndani ya Stendi kuu ya mabasi ya Tabora mjini.

 Muonekano wa  Stendi kuu ya mabasi ya Tabora mjini.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Joseph Kashushula akizungumza kuhusiana na halmashauri hiyo kubuni chanzo kipya cha mapato

Na Editha Edward, Michuzi TV Tabora 

Halmashauri ya manispaa ya Tabora mjini imepata chanzo kipya cha mapato ya ndani kupitia Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na wilayani  ambapo  kila mtu anayeingia ndani ya Stendi hiyo atatozwa kiasi cha shilingi 200 ili kupata huduma ya kusafiri.

Akizungumza ofisini kwake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri Tabora manispaa  Joseph Kashushula (pichani) amesema chanzo hicho kimebuniwa hivi karibuni ambapo pesa ambayo itapatikana hapo itaweza kusaidia huduma ambazo ni bora kwa wananchi wa manispaa hiyo zikiwemo za kiuchumi kiafya na kielimu 

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara ndani ya Stendi hiyo  Juma Iddy na Fadhili Hussein wamesema utaratibu waliouweka halmashauri ni mzuri kwani unaongeza mapato ya ndani na uchumi kwa ujumla ila unachangamoto za kjuimarisha miundombinu ya stendi.


Aidha hivi karibuni kwa mujibu wa kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Joseph Kashushula amesema halmashauri itakuwa inakusanya zaidi ya shilingi Milioni 408 kwa mwezi huku ikiendelea na mikakati ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ya ndani. 

Wachimbaji Madini Ujenzi Morogoro wafurahishwa na kasi ya utoaji huduma Tume ya Madini

0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (mbele) akiangalia moja ya kokoto zinazozalishwa na kampuni ya Kiswila Minerals iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro kwenye ziara yake aliyoifanya katika kampuni hiyo yenye lengo la kukagua shughuli za uzalishaji wa madini ujenzi tarehe 31 Oktoba, 2019.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati mwenye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na vikundi vya Kiwakoki na Kiwako vinavyojihusisha na shughuli za uchimbaji wa mawe kwa ajili ya kutengeneza kokoto katika eneo la Lugono Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, katika ziara yake aliyoifanya tarehe 31 Oktoba, 2019.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiswila Minerals, Ivan Kingu (kushoto) akimwongoza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ( wa pili kushoto) pamoja na msafara wake kwenye machimbo yake ya kokoto yaliyopo katika eneo la Mlandizi Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro tarehe 31 Oktoba, 2019.
*********************************

Na Greyson Mwase, Morogoro

Wachimbaji wa Madini Ujenzi katika Wilaya ya Mvomero wamempongeza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula pamoja na Uongozi wa Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro kwa kuwatembelea na kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

Wachimbaji hao wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula aliyoifanya katika Wilaya ya Mvomero leo tarehe 31 Oktoba, 2019 yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ujenzi pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini hayo.

Katika ziara yake Profesa Kikula aliambatana na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Shija, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Morogoro (MOREMA), Dk. Omari Mzeru, Mwenyekiti wa Madini ya Ujenzi na Wachimbaji Wasio Rasmi, Aquilin Magalambula, Mkaguzi wa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Seif Msangi pamoja na Maafisa kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini.

Akizumza kwa niaba wa wamiliki wa machimbo ya mchanga yaliyopo katika eneo la Luwe Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Ibrahim Zakaya alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro wameona mabadiliko makubwa kwa kuwa wamekuwa wakipata ushirikiano wa kutosha hivyo kuhisi sehemu ya wamiliki wa rasilimali za madini na kuchangia kwenye pato la taifa.

“Binafsi nimekuwa nikiwasiliana na hata kwenda kwenye Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Shija nakusaidiwa, jambo jingine ni ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula ambayo imezaa matunda kwa changamoto zetu kutatuliwa mara moja,” alisema Zakayo.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akizungumza mara baada ya kusikiliza kero za wamiliki wa machimbo hayo, alielekeza wamiliki wa machimbo kuhakikisha wanakuwa na mpango wa ufungaji wa machimbo ili kuepuka madhara ya mazingira yanayoweza kujitokeza mara baada ya kumalizika kwa shughuli za uchimbaji wa mchanga.

Aidha, Profesa Kikula alielekeza wachimbaji wa mchanga kuhakikisha wanafuata Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake ikiwa ni pamoja na kuzingatia masuala ya afya, mazingira kwenye shughuli za uchimbaji wa mchanga.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula aliwataka wamiliki wa machimbo hayo, kuwa na mikataba ya utoaji wa huduma kwa jamii inayotambulika kisheria ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza baina yao na wananchi wa vijiji vinavyozunguka machimbo.

Alisema kuwa ni vyema wamiliki wa machimbo hayo wakahakikisha wanaingia
makubaliano ya kisheria na wanavijiji wanaozunguka machimbo yao kuhusu utoaji wa huduma kwa jamii kama vile maji, barabara, ujenzi wa madarasa ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza mbeleni.

Awali akiwasilisha changamoto zilizopo katika machimbo hayo, Mkaguzi wa Madini ya Ujenzi katika Machimbo ya Luwe, Ester Choloi alieleza kuwa ni pamoja na baadhi ya wachimbaji wasiokuwa na leseni za madini kuvamia machimbo usiku na kuchukua mchanga kinyume na taratibu.

Wakati huohuo Profesa Kikula mara baada ya kusikiliza na kutatua kero za vikundi vya Kiwakoki na Kiwako vinavyojihusisha na shughuli za uchimbaji wa mawe kwa ajili ya kutengeneza kokoto katika eneo la Lugono Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, wachimbaji hao walimpongeza kwa kazi nzuri kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini.

“Kwa kweli sasa tunaona Sekta ya Madini inafanya kazi hasa baada ya kuona kero mbalimbali zikitatuliwa na Serikali kupitia Tume ya Madini,” alisema Mwenyekiti wa Kikundi cha Kiwakoki, Juma Makusi kwa niamba ya wenzake.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Kiwako, Barnabas Gidion mbali na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Madini kwenye usimamizi wa rasilimali za madini

aliwasilisha kero za vikundi husika ikiwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya vifaa duni na kuiomba Serikali kuwasaidia kupitia ruzuku.Alieleza kero nyingine kuwa ni pamoja na miundombinu mibovu ya barabara hali inayokwamisha usafirishaji wa kokoto hususan katika kipindi cha mvua.

Katika hatua nyingine Profesa Kikula alitembelea Mgodi wa Kuchimba Kokoto unaomilikiwa na Kampuni ya Kiswila Minerals uliopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro ambapo mbali na kupongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri kwenye uchimbaji wa kokoto aliitaka kampuni kufanya kazi kwa kufuata Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.

Aliitaka kampuni kuwa mabalozi kwa wachimbaji wengine wa madini ya ujenzi kwenye uendeshaji wa shughuli zake.

DIRA YA DUNIA ALHAMISI 31.10.2019

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images