Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

ALIYEHUKUMISA KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA, AHUHUMIWA TENA KULIPA FIDIA YA BILIONI 1.004

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru mwanasiasa  Salma Mtambo kumlipa fidia ya sh. Bilioni 1.004 Ridhuan Mringo kwa hasara aliyomsababishia kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mtambo ambaye Septemba 18, mwaka huu alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka 17 kati ya 24 yaliyokuwa yakimkabili yakiwamo ya kutakatisha fedha jumla ya Sh. 1.027,000,000, ameambiwa anapaswa kulipa fidia hiyo baada ya kumaliza kutumikia kifungo hicho.

Mshtakiwa Mtambo amesomewa adhabu hiyo ya fidia leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi Kevin Muhina ikiwa ni nyongeza ya adhabu ya kifungo ya miaka sita jela aliyopewa awali.

Kesi hiyo leo Oktoba 30, 2019 ilikuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka lililotaka mshtakiwa alipe fidia ya kutokana na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Ridhuan Mringo.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mhina amesema fidia inakuwa ni nyongeza ya adhabu nyingine kama kifungo au mbadala wa adhabu nyingine  pale mahakama itakavyoona na kwamba  makosa yaliyomtia hatiani mshtakiwa yalimsababishia muathirika hasara ya sh bilioni 1.027.

"Kwa maoni yangu, hasara aliyoipata victim ni kubwa haiwezi kupita hivihivi hivyo mahakama kwa mamlaka yake inaona ilipwe kama nyongeza ya adhabu" amesema Hakimu

Amesema fidia hiyo ya Sh.bilioni 1.004 ilipwe mara baada ya kumaliza kifungo.

Awali mshtakiwa huyo alitiwa hatiani katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika kosa la kugushi,  mshtakiwa Salma anadaiwa kati ya June mosi 2003 na Oktoba 31, 2011 maeneo yasiyojulikana Wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam kwa nia ya udanganyifu aligushi risiti ili kuonesha kwamba Ridhuan Mringo alinunua nyumba ya Shirika la Nyumba iliyopo Plot namba 710 mtaa wa Mfaume Upanga kwa Sh. Millioni 70 wakati akijua si kweli. 

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ndogo za Chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Oktoba 30, 2019.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM baada ya kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za Chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Oktoba 30, 2019. PICHA NA IKULU

ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA, AHUHUMIWA TENA KULIPA FIDIA YA BILIONI 1.004

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru mwanasiasa  Salma Mtambo kumlipa fidia ya sh. Bilioni 1.004 Ridhuan Mringo kwa hasara aliyomsababishia kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mtambo ambaye Septemba 18, mwaka huu alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka 17 kati ya 24 yaliyokuwa yakimkabili yakiwamo ya kutakatisha fedha jumla ya Sh. 1.027,000,000, ameambiwa anapaswa kulipa fidia hiyo baada ya kumaliza kutumikia kifungo hicho.

Mshtakiwa Mtambo amesomewa adhabu hiyo ya fidia leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi Kevin Muhina ikiwa ni nyongeza ya adhabu ya kifungo ya miaka sita jela aliyopewa awali.

Kesi hiyo leo Oktoba 30, 2019 ilikuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka lililotaka mshtakiwa alipe fidia ya kutokana na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Ridhuan Mringo.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mhina amesema fidia inakuwa ni nyongeza ya adhabu nyingine kama kifungo au mbadala wa adhabu nyingine  pale mahakama itakavyoona na kwamba  makosa yaliyomtia hatiani mshtakiwa yalimsababishia muathirika hasara ya sh bilioni 1.027.

"Kwa maoni yangu, hasara aliyoipata victim ni kubwa haiwezi kupita hivihivi hivyo mahakama kwa mamlaka yake inaona ilipwe kama nyongeza ya adhabu" amesema Hakimu

Amesema fidia hiyo ya Sh.bilioni 1.004 ilipwe mara baada ya kumaliza kifungo.Awali mshtakiwa huyo alitiwa hatiani katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika kosa la kugushi,  mshtakiwa Salma anadaiwa kati ya June mosi 2003 na Oktoba 31, 2011 maeneo yasiyojulikana Wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam kwa nia ya udanganyifu aligushi risiti ili kuonesha kwamba Ridhuan Mringo alinunua nyumba ya Shirika la Nyumba iliyopo Plot namba 710 mtaa wa Mfaume Upanga kwa Sh. Millioni 70 wakati akijua si kweli. 

BARAZA‌ ‌LA‌ ‌MADIWANI‌ ‌KINONDONI‌ ‌LAMPITISHA‌ ‌TENA‌ ‌ MANYAMA‌ ‌KUWA‌ ‌NAIBU‌ ‌KWA‌ ‌MARA‌ ‌YA‌ ‌NNE

$
0
0
BARAZA‌ ‌la‌ ‌Madiwani‌ ‌la‌ ‌Halmashauri‌ ‌ya‌ ‌Manispaa‌ ‌ya‌ ‌ Kinondoni‌ ‌limemchagua‌ ‌Mhe.George‌ ‌Manyama‌ ‌kutoka‌ ‌ Chama‌ ‌Cha‌ ‌Mapinduzi‌ ‌(CCM)‌ ‌kuwa‌ ‌Naibu‌ ‌Meya‌ ‌wa‌ ‌ Halmashauri‌ ‌hiyo‌ ‌kwa‌ ‌awamu‌ ‌ya‌ ‌nne‌ ‌tangu‌ ‌mwaka‌ ‌2016.‌ ‌ ‌ Uchaguzi‌ ‌huo‌ ‌umefanyika‌ ‌leo‌ ‌(jana)‌ ‌katika‌ ‌baraza‌ ‌ maalumu‌ ‌la‌ ‌madiwani‌ ‌la‌ ‌robo‌ ‌ya‌ ‌mwaka‌ ‌ambapo‌ ‌jumla‌ ‌ ya‌ ‌wajumbe‌ ‌21‌ ‌ambao‌ ‌ni‌ ‌madiwani‌ ‌walishiriki‌ ‌uchaguzi‌ ‌ huo.‌ ‌
Akitangaza‌ ‌matokeo‌ ‌hayo,‌ ‌Katibu‌ ‌tawala‌ ‌wa‌ ‌Halmashauri‌ ‌ hiyo‌ ‌Bi‌ ‌Stella‌ ‌Msofe‌ ‌amesema‌ ‌kuwa‌ ‌idadi‌ ‌ya‌ ‌kura‌ ‌ zilizopigwa‌ ‌ni‌ ‌21‌ ‌kulingana‌ ‌na‌ ‌wajumbe‌ ‌wa‌ ‌baraza‌ ‌hilo‌ ‌ kutoka‌ ‌vyama‌ ‌vyote‌ ‌vyenye‌ ‌madiwani‌ ‌katika‌ ‌baraza‌ ‌hilo.‌ ‌ Msofe‌ ‌amemtangaza‌ ‌Mhe.‌ ‌Manyama‌ ‌kutoka‌ ‌CCM‌ ‌kuwa‌ ‌ mshindi‌ ‌wa‌ ‌nafasi‌ ‌hiyo‌ ‌ya‌ ‌Naibu‌ ‌Meya‌ ‌kwa‌ ‌kupata‌ ‌kura‌ ‌ 13,‌ ‌huku‌ ‌mpinzani‌ ‌wake‌ ‌Mhe.‌ ‌Phares‌ ‌Lupomo‌ ‌kutoka‌ ‌ chama‌ ‌cha‌ ‌Demokrasia‌ ‌na‌ ‌Maendeleo‌ ‌Chadema‌ ‌akipata‌ ‌ kura‌ ‌nane.‌ ‌

Awali‌ ‌wagombea‌ ‌hao‌ ‌wawili‌ ‌walipata‌ ‌nafasi‌ ‌ya‌ ‌kunadi‌ ‌ sera‌ ‌zao‌ ‌kabla‌ ‌ya‌ ‌kufanyika‌ ‌kwa‌ ‌uchaguzi‌ ‌huo‌ ‌ikiwa‌ ‌ni‌ ‌ Toggle screen reader support. 

KUFIKIA JUMATATU WANANCHI WA KISARAWE KUANZA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kufikia mapema wiki ijayo, Wakazi wa mji mdogo wa Kisarawe wanaondoka na na adha ya maji ya muda mrefu baada ya ujenzi wa mradi wa Kisarawe kukamilika kwa asilimia 99.

Hatua hiyo imefikiwa, baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kukamilisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita Milioni 6 kukamilika.

Mradi huo wenye thamani ya Bilioni 10.6 uliojengwa kwa fedha za ndani za Dawasa unaotoa maji kutoka Tanki la maji la Kibamba hadi Kisarawe.

Kuanza kwa mradi huo kutawanufaisha wananchi wengi zaidi na maunganisho mapya 1000 watakaounganishwa maji kwa mkopo na kulipa ndani ya mwaka mmoja.

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameupongeza uongozi wa Dawasa kwa jitihada kubwa walizozifanya ndani ya muda mfupi kwa kuhakikisha maji yanafika katika mji mdogo wa Kisarawe.

"Naupongeza uongozi wa Dawasa, Mwenyekiti, Mkurugenzi na watendaji wengine kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wanajenga mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Bilioni 10.6 kwa fedha za ndani na kuleta maji kwenye Mji mdogo wa Kisarawe,"

"Mradi huu umechukua muda mfupi sana, na ndani ya siku tatu hizi nataka kuhakikisha wananchi wanapata maji kesho nitaandamana na baadhi ya viongozi kuelekea Kibamba maji yanakoanzia ili kujionea mwenyewe," amesema Aweso.

Amesema, kuna changamoto ya umeme ambapo amewahakikishia wananchi wa Kisarawe mita itapatikana na maji yataanza kuingia kwenye tanki na huduma ya maji itaanza.

Kaimu Mkurugenzi Uwekezaji Miradi Dawasa Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema mradi wa maji Kisarawe umekamilika kwa asilimia 99 na kazi iliyobaki ni ndogo sana na Dawasa wanaendelea kuhakikisha ndani ya muda mfupi maji yanafika kama agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwengelo amewataka wananchi wa mji mdogo wa Kisarawe kuwa na subira ndani ya siku chache wataanza kupata maji safi na salama.

" Niwatake na kuwaomba wananchi wa Kisarwe na wale walio nje ya mji huu kwamba kwa sasa nawakaribisha kuja kuwekeza kwenye Mji mdogo wa Kisarawe, maji yatakayokuwa hapa yanatosheleza mahitaji ya wakazi wote ambapo kwa sasa ni Lita Milion 1.2 zinazohitajika ila Dawasa wametuletea Lita Milion 6," amesema.

Mji mdogo wa Kisarawe unapata maji kutoka Mtambo wa Ruvu Juu na umeweza kufanikishwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ukitekelezwa na Dawasa ambapo kufikia Septemba Mwaka huu Mji huo umekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka hiyo.

Mbali na mradi huo, Naibu ameweza pia kutembelea shule aliyosoma ya Pugu Sekondari, Shule aliyofundisha Kisarawe pamoja na Kisima alichokuwa anatumia kwa ajili ya matumizi ya maji sambamba na mradi wa maji wa Jet Buza wenye thamani ya Bilion 2 unaotarajia kuanza hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akionesha Kisima cha Mani alichokuwa anakitumia wakati anafundisha shule ya Msingi Kisarawe na bado kinaendelea kutumika na wananchi wa Kisarawe.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji Miradi DAWASA akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso baada ya kutembelea mradi wa Jet Buza utakaoanza Jeti na kulaza mabomba hadi Buza.

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo ya miradi ya maji kwa Wilaya ya Ilala kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema baada ya kufika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu ambapo amewaahidi kero ya maji ya miaka mingi itafikia ukingoni baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kisarawe hadi Pugu wenye thamani ya Bilion sita unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira. Aweso amesoma shule hiyo katika mchepuo wa Sayansi PCB na kuhitimu kidato cha sita mwaka 2007.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa amekaa kwenye dawati alilolitumia wakati anasoma kwenye shule ya sekondari Pugu mchepuo wa Sayansi PCB na kuhitimu kidato cha sita mwaka 2007.M
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumzia maendeleo ya mradi wa maji wa Kisarawe unaotarajiwa kuanza kutoa huduma ya maji safi na majitaka kufikia Mwanzoni mwa Mwezi Novemba. Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea mradi huo uliokamilika kwa asilimia 99.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa maji Kisarawe Kutoka DAWASA Mhandisi Ishmael Kakwezi na kuangalia matoleo mojawapo yaliyopo kwenye tanki la maji la Kisarawe linaloweza kuhifadhi maji Lita Milion 6 kwa siku.

Naibubu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitembelea ujenzi wa mradi wa maji Kisarawe uliokamilika kwa asilimia 99, utakaohudumia wakazi wa Mji mdogo Kisarawe wenye thamani ya bilion 10.6 uliojengwa kwa fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA.

SHULE YA SEKONDARI PUGU KUONDOKANA NA KERO YA MAJI YA MIAKA MINGI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewahakikishia wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu kuwa watapata maji safi na salama.

Hayo ameyasema baada ya kutembelea shule hiyo ambayo alisoma mchepuo ya Sayansi PCB na kuhitimu elimu yake ya kidato cha sita mwaka 2007.

Aweso, amesema kuna mradi wa maji kutoka Kisarawe kwenda Pugu wenye thamani ya Bilion 6 ambapo amewaagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA kupeleka maji shuleni hapo.

"Nafahamu changamoto ya maji katika shule hii, mimi nimesoma hapa ilifikia kipindi unakaa hadi wiki tatu hujayapata maji, kero ilikuwa kubwa sana," amesema.

"Kuna mradi mkubwa wa maji unaotoka Kisarawe hadi Pugu, nilishawaagiza Dawasa wakati nafanya Mkutano kuwa maji lazima yafike Shule ya Pugu," 

 Aweso amesema, kuna watu mashuhuri, viongozi wamepita hapa Pugu Sekondari na mimi nawaomba wasiache kuja kutembelea hapa na kuhakikisha wanaisaidia kwa namna moja au nyingine.

 "Kuna Viongozi wengi na watu mashuhuri wamepita hapa Pugu Sekondari na mkuu wa Shule usisite kuwaalika kwa ajili ya kuja kuisaidia shule yao na mimi nawahakikishia kuwa ntarudi tena hapa," 

"Mimi nimesoma hapa, hata katibu Mkuu wangu wa Wizara ya Maji Kitila Mkumbo amesoma hapa na kutokana na hilo lazima nihakikishe maji yanafika kwenye shule hii, mwalimu Mkuu usisite kusema lolote kwani wengi tumepita kwenye shule hii," amesema Aweso.

Aweso ametembelea shule hiyo na kusalimiana na wanafunzi wa Mchepuo wa Sayansi PCB, na kuwataka wasome kwa bidii ili waje kuisaidia shule yao hapo baadae.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso  akiwa amekaa katika meza aliyokuwa anaitumia wakati anasoma shule ya Sekondari Pugu, leo ametembelea shule hiyo na kuwahakikishia wanafunzi wa hapo watapata maji safi na salama.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisalimiana na walimu waliomfundisha wakati anasoma shule ya Sekondari Pugu, leo ametembelea shule hiyo na kuwahakikishia wanafunzi wa hapo watapata maji safi na salama.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa amepiga picha ha pamoja na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Pugu baada ya kutembelea shule hiyo.

TAMASHA LA WASAFI KURINDIMA DAR, MASHABIKI WATEGEMEE KUBURUDIKA

$
0
0
 Na. Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond platnum amewaasa wasanii kutumia Sanaa yao kuongeza pato la taifa.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam wakati akitangaza rasmi ujio wa Tamasha la wasafi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam amesema kwa mwaka huu imekua neema kwa wasanii wasanaa mbalimbali kupewa nafasi na Waziri wa utalii Hamisi kigangwala kutembelea vivutio vilivopo nchini hasa mlima Kilimanjaro nakujifunza vingi zaidi.

" Tumeanza kupanda mlima Kilimanjaro lakini vingine vingi vitafata lengo likiwa ni kuutangaza utalii wetu kwa nchi za nje ili kujua vitu tulivobarikiwa sisi Kama watanzania,"

Hata hivyo platnum ameeleza ujio huo wa Tamasha utakua ni mara ya Kwanza kwake kutumbuiza Dar  es Salaam kwani hakuweza kufanya hivyo kutokana na kukosa kibali kwa mwaka Jana kutokana na utovu wa nidhamu uliofanyika .

"Niliweza kutumbuiza uwanja wa Taifa katika Tamasha la jamaa lililoandaliwa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ,Basi pale niligusa gusa tu balaa lenyewe mashabiki na wapenzi wa lebo ya wasafi (WCB) wajitokeze novemba 9 mwaka huu katika viwanja vya posta jijini Dar es salaam,"

Pia amegusia swala la vijana kupima afya zao nidhahiri wamekua wakipata ushirikiano wakutosha kutoka Taasisi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi (TACAIDS) na kupewa fursa Kila mkoa kuungana nao na kutoa elimu juu ya kujikinga na kuepuka maambukizi ya ukimwi.

Hata hivyo amefafanua kuwa Wana lengo la kuwa tofauti katika Tamasha la mwaka huu hasa la Dar es salaam na mashabiki wategemee uwepo wa  wasanii wengine wengi kutoka nje ya nchi lengo ni kupata burudani kabambe.

AfDB kuipatia Tanzania zaidi ya shilingi 1trln kujenga uwanja wa ndege msalato

$
0
0

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abidjan Nchini Ivory Coast.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi wakati alipowasili ofisini kwake katika makao makuu ya Benki hiyo Abidjan, Ivory Coast.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi baadhi ya maafisa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Wizara ya fedha na Mipango mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Abidjan, Ivory Coast.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma na kuahidi kuidhinisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 455 sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato sambamba na ujenzi wa barabara za mzunguko Jijini  humo.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abijdan Nchini Ivory Coast wakati wa Mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lakini pia kwa Tanzania.

Amesema Benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha dola za marekani milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini  Dodoma na kwamba kiasi kingine cha dola za marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato kinatarajiwa kuidhinishwa na mapema mwezi Novemba 2019.

Dkt. Adesina ameongeza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ina imani na mageuzi ya kiuchumi yanayotekelezwa chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu bila malipo,afya na maji pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuleta uwajibikaji katika taaisisi za uma na kwamba iko tayari kuunga jitihada hizo za serikali kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu..

Aidha Dkt. Adesina ameelezea nia yake ya kutaka kushudia bara la Afrika likipiga hatua kubwa za kimaendeleo sasa na kwa haraka na sio kusubiri baadae na kwamba katika kipindi chake cha uongozi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika atapambana kuhakikisha azma hiyo inatekelezeka.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimae Bara zima la Afrika.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika iko tayari kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa yaani Standard Gauge Railway ya kipande cha kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda na kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara baada ya kukamilika mchakato wa utoaji wa fedha hizo ambapo mazungumzo ya awali kuhusu ufadhili huo yameanza.

Pia Prof. Kabudi amemtaka Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina kuimarisha ofisi za kanda za benki hiyo ili ziweze kutoa huduma zote za kibenki ili kusogeza huduma karibu na wanufaika wa benki hiyo sambamba na kuunga mkono miradi yote ya kimkakati inayounganisha nchi na nchi katika bara la Afrika ili kuboresha nakurahisisha huduma ya usafiri katika Bara la Afrika na hivyo kuwezesha biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na kujiletea maendeleo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi yuko Abijdan Nchini Ivory Coast kushiriki mkutano wa siku mbili wa dharura wa Mawaziri wa fedha uliondaliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB).

DC KINONDONI AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUSHUHUDIA RC MAKONDA AKIZINDUA UJENZI WA BARABARA YA MAKONGO JIJINI DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KERO ya barabara Makongo jijini Dar es Salaam inatarajia kufika ukingoni baada ya Serikali ya Rais Dk.John Magufuli kutoa Sh.bilioni 8.9 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kipande cha kilometa tano ambazo zilizokuwa zimebakia ili kuunganisha maeneo ya Goba, Mbezi Massana, Mbezi mwisho na Wazo kwa lami.

Akizungumza leo na wananchi wa Kilimahewa Juu na Salasala katika Kata ya Wazo wilayani kinondoni, Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anatarajiwa kuzindua ujenzi wa barabara hiyo Ijumaa ya wiki hii.

Chongolo amefafanua kuwa wananchi wa Makongo walikuwa wakifanyiwa kila aina ya utani na wenzao wa maeneo yenye miundombinu mizuri ya barabara ikiwa ni pamoja na kuwachora kwenye vibonzo kuwa ni watu wanaofika mjini wakiwa wamechafuka vumbi kila mahali, lakin sasa muda mfupi ujao hali hiyo itakoma na wao wataanza kutereza kama wengine.

Ameongeza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo ya Makongo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya barabara unaoendelea ndani ya Wilaya ya Kinondoni huku akitumia nafasi hiyo kueleza  Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kutatua kero za wananchi wakiwamo wa wilaya hiyo. "Miradi mingine ya barabara ni pamoja na ule wa Ununio kwenda Mbweni ambako ujenzi wake unaendelea kwa awamu, umaliziaji wa kipande cha barabara ya Wazo kiwandani mpaka Kisauke shule kata ya Wazo.

"Pia upanuzi wa barabara ya Morocco kwenda Mwenge, upanuzi wa barabara ya Shekilango kwa njia nne, na uboreshaji wa barabara zaidi ya 46 za mitaa kwenye maeneo ya Tandale, Mburahati, Ndugumbi, Mwananyamala, Makumbusho, Kijitonyama na Magomeni,"amesema.

Chongolo ametoa mwito kwa wananchi wa Makongo na maeneo yanayozunguka eneo hilo kujitokeza kwa wingi katika shughuli hiyo ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo muhimu ya Makongo siku ha ijumaa."Wananchi tunaomba mjitokeze kwa wingi siku ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo.

Hata hivyo wakati anaeleza uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo, wananchi wa Kilimahewa na Salasala wamemuhakikishia Mkuu wa wilaya hiyo kwamba watajitokeza kwa wingi ili nao kuwa sehemu ya kushuhudia kazi ambayo itafanyika katika kuijenga barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu. 
Mkuu wa Wilya ya Kinondoni ,Daniel Chongolo akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Kilimahewa Juu,kata ya Wazo wilayani Kinondoni changamoto zake,mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa eneo alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ya barabara na maji,lakini pia aliwaeleza tukio la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Makongo unaotarajiwa kufanywa na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Ijumaa wiki hii.
  Wananchi wa Kilimahewa Juu katika Kata ya Wazo wilayani kinondoni, wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo amesema kuwa Mkuu alipokuwa akizungumza na wakazi hao kuhusu uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Makongo unaotarajiwa kufanywa na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Ijumaa wiki hii.DC Chongolo aliongeza kusema kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo ya Makongo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya barabara unaoendelea ndani ya Wilaya ya Kinondoni huku akitumia nafasi hiyo kueleza  Serikali ya Awamu ya Tano kudhamiria kwa dhati kutatua kero za wananchi wakiwamo wa wilaya hiyo. "Miradi mingine ya barabara ni pamoja na ule wa Ununio kwenda Mbweni ambako ujenzi wake unaendelea kwa awamu, umaliziaji wa kipande cha barabara ya Wazo kiwandani mpaka Kisauke shule kata ya Wazo.
Wananchi wa Kilimahewa Juu katika Kata ya Wazo wilayani kinondoni, wakimshukuru Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo  kwa kukutana nao ikiwemo sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabbili katika maenno yao,alkini pia kuwapa taarifa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Makongo unaotarajiwa kufanywa na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Ijumaa wiki hii. Picha na Michuzi JR (MMG).

MAHAKAMA KISUTU YAMHUKUMU ALIYEKUWA MHASIBU CHUO KIKUU HURIA KWENDA JELA MIAKA MITANO AU KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 700

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

ALIYEKUWA Mhasibu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Engels Mrikaria amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani au kulipa faini ya Sh milioni 700 baada ya kukutwa na hatia  katika makosa ya kughushi na utakatishaji fedha zaidi ya sh. Milioni 500.

Pia mahakama imeamuru mshitakiwa huyo kulipa fidia ya Sh milioni 566.4 kama hasara aliyoisabisha  kwa chuo hicho. Pia Mahakama umeamuru kutaifishwa  kwa ardhi iliyopo mkoani Morogoro.

Kwa upande mwingine,  mahakama hiyo imewaachia huru mke wa Mrikaria, Lucy Mrikaria  Boniface Msofe, Stanley Msofe na Rose Maungu baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile amesema amezingatia ushahidi wa mashahidi 35 pamoja na vielelezo 48 amba uliletwa na upande wa mashtaka ambapo walimeweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya Mrikaria ambaye ndie alikuwa akilipa mshahara kwa wafanyakazi wa OUT.

Amesema mshitakiwa amekutwa na hatia katika mashitaka 53 ya kughushi, saba ya utakatishaji fedha na moja la kuisababishia chuo hicho hasara ya Sh 566,446,500.

Hakimu Rwizile alisema katika mashitaka ya kwanza hadi ya 53, mahakama inamuachia huru mshitakiwa huyo kwa sababu amekaa rumande kwa miaka saba na kwa mujibu wa sheria  mashitaka ya kughushi kifungo cha juu ni kifungo cha miaka saba.

Akifafanua adhabu hiyo, Hakimu Rwizile amesema katika shtaka la utakatishaji fedha kila moja mshitakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 100 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Pia katika shtaka la kusababisha hasara mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela na kulipa hasara ya Sh 566,446,500 alizosababisha kwa chuo hicho na kwamba adhabu za vifungo zitakwenda kwa pamoja. Hivyo atakaa jela miaka saba. "Pia mahakama inataifisha ardhi iliyopo mkoani Morogoro na kuhusu kiwanja kilichopo Arumeru mkoani Arusha mahakama haiwezi kukitaifisha kwa sababu bado haijajulikana kama kiliingia mikononi mwa mshitakiwa," amefafanua Hakimu Rwizile.

Ameongeza kuwa, kama upande wa mashitaka utataka mali hiyo itaifishwe basi ipeleke maombi ikiwa ni pamoja  na kuorodhesha mali zote wanazotaka zitaifishwe.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Theophil Mutakyawa ameiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine kwa sababu makosa aliyoyafanya ni makubwa.

Pia ameiomba mahakama kutoa amri y kuamuru mshitakiwa kulipa fidia ya hasara aliyosababisha na kutaifisha mali hizo.

Katika utetezi wake, mshitakiwa kupitia wakili wa Utetezi, Peter Kibatala ameiomba mahakama impunguzie adhabu mshitakiwa kwa sababu ni kosa lake la kwanza na kwamba tayari amekaa gerezani kwa miaka saba hivyo, asitengwe na familia yake.

Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya Julai 2009 na Aprili 2011 mshitakiwa Mkaria alighushi nyaraka ya malipo ya mshahara na kuwatumia fedha watu mbalimbali kupitia akaunti za CRDB na NBC ambao hawakuwa wafanyakazi wa OUT.

Inadaiwa kati ya Julai 15 na 31, 2009 makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), jijini Dar es Salaam, alighushi  nyaraka ya malipo ya mshahara (payroll) lengo kuonesha S. M January alilipwa mshahara wa Sh milioni mbili, B. J Msoffe (1,983,000) na A. Mrakari (1,603,000) wakati akijua sio wafanyakazi wa chuo hicho.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa Julai 2009 na Aprili  Mrikaria na mke wake, walijipatia  28,776,750 zilizoingia kwenye akaunti ya familia kama mshahara.

Pia inadaiwa mshitakiwa aliingiza fedha kwenye akaunti ya Kampuni ya Kyungu Hill kama mshahara.

Aidha, Aprili 2011 maeneo ya Dar es Salaam na Dodoma mshtakiwa alijipatia shamba lenye ekari 130 katika Kijiji cha Muungano kilichopo Kongwa mkoani Dodoma fedha ambazo zililipwa na chuo hicho kama mshahara kupitia akaunti zake. Anadaiwa kununua kiwanja Kijiji cha Kiharaka kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, pia alinunua kiwanja kilichopo Kijiji cha Meru wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Kati ya Julai 2009 na Aprili 2011 maeneo ya jiji la Dar es Salaam, Mrikaria alisababisha hasara ya 566,446,500 kwa chuo Kikuu huria (OUT).

SARATANI YA MATITI YAWEZA KUSHIKA NAMBA MOJA

$
0
0
Na. Catherine Sungura, WAMJW-DSM

Endapo hatua zisipochukuliwa za saratani ya matiti inaweza kushika namba moja kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa nchini.

Hayo yanesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Kinga ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispian Kahesa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwezi wa uhamasishaji , uelimishaji na uchunguzi wa saratani ambao huadhimishwa kila mwezi oktoba kila mwaka.

“Idadi ya saratani ya matiti inaonekana kuongezeka nchini ambapo hivi sasa wanawake wenye umri kuanzia miaka 20 na kuendelea nao wanagundulika kuugua ugonjwa huu”. Alisema Dkt. Kahesa.

Alisema kuwa endapo hatua zisipochukuliwa saratani hiyo itazidi kuwa tishio zaidi na kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo wanatoka katika maeneo ya mjini ambapo mkoa wa Dar es salaam unaonekana kuongoza.

“Tathimini ya miaka 10 iliyopita saratani hii ilikua inashika nafasi ya tano ,hivi sasa ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa,zamani tulikua tunawaona wagonjwa kuanzia miaka 55 ukashuka hadi miaka 50 na sasa tunaona hadi wenye umri wa miaka 20”.

Dkt. Kahesa alisema kuwa kwa mwaka huu pekee wameweza kuona wanawake 1443 ambapo kati ya 342 wamekutwa na uvimbe 170 walikuwa na dalili za awali za saratani.

Kwa upande wa saratani kwa wanaume Dkt. Kahesa alisema kuwa saratani hiyo huathiri asilimia moja kwa wanaume hata hivyo kwa upande wao ni hatari zaidi na endapo isipogundulika huweza kuathiri mapafu yao kwa haraka.

“Saratani hii huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume kwa asilimia 99 na wanaume ni asilimia 1 tu,ambapo dalili kwa wanaume ni tofauti kidogo na wanawake,hivyo kwa mwanaume ni rahisi kugundua kuliko mwanamke kwa kuwa kifua chake kina mafuta mengi.

Aliongeza kuwa kati ya wanawake 170 waliofanyiwa vipimo zaidi ya 68 waligundulika na vivimbe ambavyo ni ugonjwa wa saratani.Hapa nchini saratani ya shingo ya kizazi inaongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti,saratani ya njia ya chakula,saratani ya tezi dume na saratani nyingine ni zile zinazoathiri mfumo wa kinga.
Mkurugenzi wa huduma ya kinga Dkt.Kahesa

WANAFUNZI 170 WA WILAYA YA TUNDURU WAACHA SHULE

$
0
0

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TAKWIMU zinaonesha Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo jumla ya  wanafunzi 170 wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameacha shule kwa sababu mbalimbali.

Hata hivyo kupitia taarifa ya ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imesema kuwa wanafunzi 20 walihama kwenda katika shule nyingine, wanafunzi 15 waliacha masomo baada ya kupata ujauzito, wanafunzi 63 waliacha masomo kutokana na sababu mbalimbali na wanafunzi 72 waliopewa nafasi ya kurudia masomo baada ya kufeli kidato cha pili baadhi yao wazazi waliamua kuwapeleka katika vyuo vya Ufundi stadi kama (VETA) na shule binafsi.


Hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 170 kwa kipindi cha miaka minne ndio hawapo shuleni tofauti na taarifa ilivyoonesha jumla ya wanafunzi 350 wa shule hiyo wameacha masomo.

Aidha kuhusu suala la utoro wa reja reja Halmshauri inaendelea kushirikiana na wazazi pamoja walezi wa wanafunzi katika kuahikisha utoro mashuleni unadhibitiwa.

Taarifa ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imekanusha habari ya upotoshaji iliyotolewa na Gazeti la Habari Leo la tarehe 28 Oktoba 2019 na Kituo cha Televisheni cha ITV ikisomeka kuwa “Wanafunzi 350 waacha shule kwa utoro, mimba,” habari hii haina ukweli wowote kama ilivyoripotiwa.

"Tunapenda kuuarifu umma kuwa baada ya kuwepo kwa taarifa hiyo Ofisi ya Mkurugenzi imefanya ufuatiliaji wa kina katika Shule ya Sekondari Marumba ambayo imetajwa katika habari hiyo iliyosema kuwa wanafunzi 350 wa shule hiyo wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya utoro na mimba kwa kipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2016 hadi 2019". Taarifa hiyo inaeleza.

Taarifa hiyo inaseka kuwa ni vyema umma ukafahamu kuwa katika kipindi cha miaka minne yaani 2016 hadi 2019, shule hii ilipangiwa idadi ya wanafunzi 603 ikiwa wavulana 320 na wasichana 283, waliosajiliwa kwa kipindi hicho ni wanafunzi 515 ikiwa pungufu ya wanafunzi 88 kati ya waliopangwa.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi waliopo katika shule ya Sekondari Marumba hadi kufikia tarehe 28/10/2019 ni 345 ikiwa wavulana 208 na wasichana 137 kukiwa na upungufu wa wanafunzi 170.

 Mkurugenzi Mtendaji Halmasahuri ya Tunduru Gasper Balyomi amesema hii ni wazi kuwa idadi ya wanafunzi 350 wa sekondari ya Marumba walioripotiwa hawajulikani walipo hazina ukweli wowote kufuatia takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari hivyo.

WAZIRI JAFO AKIRI KUPOKEA BARUA YA CHADEMA, ATOA AGIZO KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amekiri kupokea barua kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilichokua kikilamikia mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mhe Jafo amesema Ofisi yake imepokea malalamiko kutoka kwa Vyama vya Siasa, Wadau mbalimbali pamoja na watu binafsi na kuwataka wasimamizi wa uchaguzi huo kufuatia kanuni za uchaguzi ili kuondoa dosari zote ambazo zimeshajitokeza hadi sasa.

Jana CHADEMA ilitangaza kuiandikia Ofisi ya Rais-TAMISEMI juu ya kuwepo kwa dosari kwenye uchaguzi huo ikiwemo wagombea wake kunyimwa fomu huku sehemu nyingine wagombea wakipewa fomu ambazo hazijasainiwa.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Mhe Jafo amesema dosari ambazo zimejitokeza ni chache na tayari wameshaanza kuzifanyia kazi ili kuepukana na malalamiko ambayo yameanza kutolewa.

Pia amevitaka vyama vya siasa vyote kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria pamoja na masharti wakati wote wa zoezi la uchukuaji na Urejeshaji wa fomu za uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya zoezi la uchukuaji fomu ikiwa Leo ni siku ya pili ya zoezi hilo.

Waziri Jafo amesema kiujumla zoezi hilo limeenda vizuri licha ya kuwa na dosari baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na baadhi ya vikwazo na zoezi hilo likashindwa kufanyika kiufasaha lakini dosari hizo zinafanyiwa kazi.

"Zoezi limeenda vizuri tuna kata 3959 na Kati ya kata hizo ni kata 72 tu ndio zilizokuwa na dosari ambapo zoezi hilo halikufanyika kifasaha na miongoni mwa maeneo yaliyokuwa na malalamiko ni Liwale Lindi, Moshi, Sengerema na Songwe baadhi ya maeneo hayo" 

"Niwatake wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao katika maeneo yote wahakikishe wanasimamia kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizowekwa kuhakikisha wanaondoa changamoto zilizojitokeza wakati wa zoezi hili" amesema Waziri Jafo.

Aidha amesisitiza vyama vyote vya siasa kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya kuepusha uvunjifu wa Sheria na kuvuruga amani wakati wote wa zoezi hilo.

Amesema zoezi hilo ni la siku Saba hivyo Wizara yake ambayo ndio msimamizi wa uchaguzi huo wanaendeleo kuzifanyia kazi dosari zote ambazo zimejitokeza katika maeneo yenye malalamiko wakati wa zoezi hilo kuhakikisha linaisha salama na kila mtu anapata haki yake.

Amesema maeneo yote ambayo zoezi hilo halikwenda vizuri wawasilishe malalamiko yao kwenye kamati za rufaa na maadili zilizopo katika maeneo yao ili kuondolewa kwa dosari ambazo wanahisi hazikuwekwa vizuri wakati wa zoezi hilo.

Aidha amesema maagizo yake aliyoyatoa hayajapuuzwa bali changamoto zilizojitokeza ni za kawaida ambazo hutokea katika uchaguzi wowote duniani na zitaendelea kutatuliwa na Ofisi yake ambayo ndio wasimamizi wa uchaguzi huo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo 

WANANCHI SALASALA WAMTUMA DC CHONGOLO KUFIKISHA UJUMBE WAO KWA RAIS DK.MAGUFULI

$
0
0
*Wachekelea kupata maji safi na salama ya bomba, Kilimahewa nako yanukia 

Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

WANANCHI wa Salasala Juu wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam  wamemtuma Mkuu wa Wilaya hiyo Daniel Chongolo kufikisha ujumbe wao 
shukrani zao za dhati kwa Rais Dkt.John  Pombe Magufuli baada ya changamoto ya kukosa  maji kwa muda mrefu kupata ufumbuzi.

Kwa mujibu wa wananchi hao ni kwamba pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingine lakini kukosekana kwa maji ilikuwa kero na ilisababisha mateso makubwa kwao lakini wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na hasa Rais Magufuli kwa kutatua kero hiyo.

Wananchi hao wamesema kupata maji safi na salama kwao ilikuwa ni ndoto ya miaka mingi hatimaye chini ya utawala wa Rais Magufuli nao wameonja ladha ya maji ya bomba baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) kukamilisha mradi wa kusambaza maji katika eneo hilo la Salasala Juu.

Akizungumza leo Oktoba 30, 2019 baada ya kuzindua rasmi maji ya bomba, 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amewaaambia wananchi hao wa Salasala Juu kwamba Serikali ya Rais Magufuli imeamua kumtua ndoo mwanamke kichwani na hivyo imedhamiria kutatua changamoto ya upatikanaji maji katika Wilaya hiyo na maeneo mengine.

Wakati Chongolo anazungumza na wananchi hao, wengi wao walionekana wenye furaha kubwa kwa kupata maji ambapo baadhi yao walisikika wakieleza waziwazi kufurahishwa na utawala wa Rais Magufuli ambao umeamua kujikita kutatua kero za wananchi.

" Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumtua mama ndio kichwani katika Jiji la Dar es Salaam. Katika kutatua changamoto ya uhaba wa maji kuna maeneo ambayo yamepewa kipaumbele na hasa maeneo yenye muinuko ambayo maji hayafiki kwa uraihisi.

"Hivyo DAWASA ilianza kwa kuweka miundombinu ikiwemo kujenga matenki ya kuhifadhi maji matano ambayo manne yanauwezo kuhifadhi lita milioni sita na moja linauwezo wa kuhifadhi lita milioni tano.Hivyo niwahakikishie wananchi tuna uhakika wa maji ya kutosha na ya uhakika na hii yote imewezekana chini ya Rais Magufuli ambaye ameamua kutoa Sh.bilioni 72 kutatua changamoto ya maji,"amesema Chongolo.

"Uwekezaji wa Sh.bilioni 72 ndugu zangu wananchi si mdogo lakini Rais wetu kwa mapenzi mema aliyonayo kwetu ameamua kutoa fedha hizi kuhakikisha tunatatua changamoto ya maji na kwa Kinondoni nina uhakika ukosefu wa maji itabaki kuwa historia ili tuanze kushughulika na mambo mengine,"amesema Chongolo.

Mbali ya kutatua changamoto ya maji Salasala, Chongolo pia amepata nafasi ya kwenda kuzungumza na wananchi wa Kilimahewa ambako nako tayari 
usambazaji wa mabomba umeanza kutekelezwa kwa lengo hilo hilo la kutatua kero ya ukosefu wa maji ndani ya Wilaya ya Kinondoni ambapo amewahakikishia wananchi kuwa mradi huo utamfikia kila mtu.

"Tunaendelea kutatua changamoto ya maji, niwaombe wananchi hakikisheni mnajiandikisha kuomba kuwekewa maji, pili miundombinu ya maji ambayo inasambwaza ilindeni kama mboni ya jicho.Mkiona mtu anaharibu miundombinu hii toeni taarifa na atakeyabainika kuharibu hana tofauti na mhujumu uchumi,"amesema Chongolo wakati anazungumza na wananchi wa Kilimahewa.

Hata hivyo amesema Dawasa wanafanya kazi kubwa ya kusambaza miundombinu ya maji na wataendelea na kazi hiyo bila kuchoka, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

Kuhusu gharama ya bei ya ndoo ya maji, amesema haizidi Sh.35 wakati hivi sasa wananchi wananunua ndoo ya maji hadi Sh.500, hivyo ni vema ikafahamika dhamira ya Serikali ni kuona maji yanapatikana kwa uhakika na gharama nafuu maana sio biashara bali ni hitaji muhimu

Mkazi wa Salasala Juu Ashura Suleiman na mkazi  Bakari Joshua wa 
Kilimahewa wamesema Rais Magufuli kwa mambo anayoyafanya 
amethibitisha yeye ni Rais wa wanyognge, hivyo watamuunga mkono kwa kila jambo la maendeleo analofanya kwa ajili ya Watanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akimtwisha ndoo  Ashura Seleman wakati wa uzinduzi rasmi wa maji ya bomba ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) eneo la Salasala Juu  wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Philemon Boniface.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa Salasala Juu mara baada ya kuzindua bomba la maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Philemon Boniface (katikati) akitoa ufafanuizi wa kutandaza mabomba ya DAWASA katika eneo la Kilimahewa Juu wakati Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo alipofanya ziara maeneo hayo ambayo yalikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu,katika wilaya hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Boko, Mhandisi Felchesm Kimaro.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza jambo na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Philemon Boniface(katikati) pamoja na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Boko Mhandisi Felchesm Kimaro wakati wa ziara ya kukagua miundo mbinu ya Maji kwa wananchi wa eneo hilo.Picha na Michuzi JR (MMG).

Baadhi ya mambomba yatakayotandikwa kwenye eneo la Kilimahewa Juu lililokuwa na tatizo kubwa ya upatikanaji wa maji wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa eneo la Kilimahewa Juu mara baada ya kufanya ukaguzi wa mabomba yatakayotandikwa kwenye eneo hilo ili kuweza kupata maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),wakati wa ziara hiyo. Wa kwanza kushoto ni  Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Mhandisi Philemon Boniface na kulia ni Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Boko Mhandisi Felchesm Kimaro.Picha na Michuzi JR (MMG).
Baadhi ya wananchi wa Kilimahewa Juu wakimsilikiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo alipofanya ziara kwenye miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuweza kujionea na kuhakikisha maji yanawafikia wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akichimba mtaro kwa ajili ya kupitisha mabomba ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili wananchi wa Kilimahewa Juu kupata maji safi. Picha na Michuzi JR (MMG).

Tigo yaingiza sokoni ‘Kitochi 4G Smart’ ’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu

$
0
0


Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu ,Pembeni yeke ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu ,Pembeni yeke ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam .




Wateja wataweza kuipata kwa gharama ya Sh49, 000/-


Dar es Salaam. Oktoba 30, 2019. Kampuni inayoongoza katika mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo, leo imezindua simu yenye sifa za smartphone ‘‘Kitochi 4G Smart’ ya kwanza kwenye soko la simu Tanzania yenye uwezo wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote ili kufungua fursa za kijamii na kiuchumi.

Simu hiyo inayojulikana kama ‘Kitochi 4G Smart’ inapatikana sokoni kwa gharama nafuu ya Sh49, 000/- na inakuja na Applications kama WhatsApp, Facebook, Twitter na YouTube.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema “Kama waanzilishi wa kwanza wa mtandao wa kasi wa 4G hapa nchini tangu mwaka 2014, tunavunja mipaka tena kwa kuhakikisha kila mmoja anapata simu ya 4G kwa gharama nafuu ili kuwa sehemu ya mabadiliko ya kidigitali na hatimaye kuchangia ujumuishwaji wa kidigitali hapa nchini,” alisema Boudiaf.

Boudiaf aliongeza kuwa kwa muda mrefu gharama kubwa ya simu zenye uwezo wa 4G imekuwa kikwazo kwa watanzania wengi kumiliki simu zenye uwezo wa intaneti ya kasi hivyo ujio wa simu hiyo ni msaada kwa watanzania wengi.

“Kwa ujio wa simu hii ya ‘Kitochi 4G Smart’ kwenye soko yenye uwezo wa Facebook ya bure kwa miezi mitatu itawapa wateja wetu uwezo wa kujumuika kwenye mitandao na hivyo kufanya kila mmoja kuwa sehemu ya mageuzi ya kidigitali,” alisema.

Naye, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema “Kitochi 4G Smart inadhihirisha dhamira ya Tigo ya kuwahudumia wateja wake katika kila hatua ya maisha.Kwa hatua hii ni imani yetu kuwa hakuna mtu ambaye atashindwa kupata manufaa yatokanayo na intaneti ya kasi ya 4G.”

Aliongeza, “Kitochi 4G Smart itaongeza wigo wa upatikanaji wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote na kusaidia katika ufikiwaji wa taarifa na maarifa yatakayosaidia katika kutumia vema fursa za kijamii na kiuchumi.”

Tigo inapanua wigo wa uvumbuzi kwa kuendelea kutoa bidhaa na huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja sokoni na zaidi kuchangia mageuzi ya kidigitali nchini.Kitochi 4G Smart ni hatua nyingine kutoka Tigo baada ya Smartphone ya Kiswahili, Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa Pesa na App ya Tigo.

Wateja wa Tigo wanaweza kujipatia simu ya Kitochi 4G kwa kuweka oda kwa kupiga namba 100 na kufanya malipo ya awali.itochi 4G Smart inakuja na App kama Facebook, WhatsApp, YouTube,Twitter, Gmail, Google Map na zingine nyingi zinazopatikana kwenye kaiOS App store.

WAZIRI MPINA ATANGAZA NEEMA KUBWA KWA WAFUGAJI UOGESHAJI WA MIFUGO

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akishirikiana na wafugaji kuingiza ng'ombe kwenye josho la Kijiji cha Kikonko wilayani Mlele mkoani Katavi wakati wa uzinduzi wa uogeshaji mifugo awamu ya pili na kutangaza ng'ombe mmoja sasa ataogeshwa kwa sh 50 tu badala ya sh 500 waliokuwa wanatozwa miaka ya nyuma.Picha na Mpiga Picha Wetu


Na Mwandishi Wetu, Katavi

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua kampeni ya kitaifa ya uogeshaji mifugo nchini na kutangaza neema kubwa kwa wafugaji ambapo sasa ng’ombe mmoja ataogeshwa kwa shilingi 50 badala ya sh 500 huku Mbuzi na Kondoo wakiogeshwa kwa sh 10 kila mmoja.

Uamuzi huu wa Serikali utawawezesha kuokoa shilingi bilioni 19 ambazo wafugaji wangezitumia kuogesha mifugo yao lakini ambapo sasa itatumika shilingi bilioni 2.16 tu huku Serikali ikiwapatia wafugaji ruzuku ya asilimia 90 ambapo kama wafugaji wangeendelea na bei hiyo ya miaka ya nyuma wangelazimika kutumia sh bilioni 21.6.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya uogeshaji mifugo awamu ya pili katika Josho la Kikonko wilayani Mlele na baadae mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Majimoto, Waziri Mpina alisema kupitia  mpango huo Serikali itasambaza dawa ya ruzuku lita 12, 546 kwenye majosho yanayofanya kazi 1,733 nchini kote.

Huku Mvua kubwa ikinyesha kwenye mkutano huo, Waziri Mpina alitumia zaidi ya saa moja kuhutubia huku akinyeshewa na mvua na kuwathibishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuleta mageuzi kwa vitendo hasa katika sekta ya mifugo.

Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ibara ya 25 kipengele  inaiagiza Serikali kuhakikisha mifugo yote inaogeshwa ili kuweze kuzuia magonjwa yote yanayoenezwa na kupe ambapo asilimia 72 ya vifo vya mifugo vinasababishwa na kupe.

Hivyo uogeshaji huo utawezesha mifugo kujikinga na maradhi na vifo ambapo Serikali itaogesha michonyo milioni 38 kwa Ng’ombe, michonyo milioni 18 ya Mbuzi, michovyo milioni 7 ya Kondoo, na michovyo 2500 ya Punda hivyo utaliwezesha taifa  kupata mifugo bora ambayo haina magonjwa.

Waziri Mpina alibainisha kuwa katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja Serikali imekarabati majosho 400 na kwamba majosho yaliyobaki ambayo  hayajakarabatiwa ni 639 na kusisitiza kuwa yote yatakarabatiwa ili kuongeza kasi ya uogeshaji mifugo.

Waziri Mpina alisisitiza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya magonjwa ya binadamu yanasababishwa na mazao ya mifugo ikiwemo nyama na maziwa hivyo uamuzi wa Serikali kuogesha mifugo pia umelenga kupambana na magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Hivyo juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono na watendaji wote wa Serikali, wafugaji wote ili kuboresha afya za mifugo na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo ikiwemo nyama, maziwa na ngozi sambamba na kuwakinga wananchi na maradhi yanayoweza kuambizwa kutoka kwenye mifugo.

Kufuatia uzinduzi huo, Waziri Mpina ameagiza kila kijiji nchini kiwe na josho kwenye  vijiji vyote zaidi ya 12,000 ili kila kijiji kiweze kuogesha mifugo na kusisitiza kuwa Serikali ya Rais Magufuli itakuja na mkakati wa kuhakikisha kila kijiji kinapata josho kama sehemu ya kuboresha afya za mifugo.

Pia ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha majosho yote yamekarabatiwa ndani ya mwezi mmoja na wizara itahakikisha inasambaza dawa kwenye majosho yote mabovu.

Aidha amesisitiza wanaokwenda kuogesha mifugo wafuate sheria za uogeshaji kuhakikisha mifugo inaogeshwa lakini kwa fedha ambayo Serikali imeitangaza ya sh 50 kwa kichwa na ng’ombe na sh 10 kwa kichwa cha mbuzi na zoezi hili litafanyika mfululizo kwa kipindi cha miezi 6 na kumuagiza  Mkurugenzi wa huduma za mifugo, Madaktari ya Mifugo wa Mikoa, na Wilaya kuhakikisha zoezi hilo linasimamiwa vizuri kuhakikisha wananchi hawatapeliwi

Pia Waziri Mpina ameweka wazi kuwa Serikali itatangaza bei elekezi ya chanjo ifikapo 15 Novemba mwaka huu na hakuna mtu mwingine atakayekwenda kuwaibia wafugaji tena na kwamba  chanjo ya homa ya mapafu ya ng’ombe itauzwa kwa sh 350 tofauti na siku za nyuma ambapo walichanja kwa sh 2000 kwa kichwa cha ng’ombe.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Homera amemhakikishia Waziri Mpina kuwa Serikali ya mkoa huo inatasimamia maagizo yote na kwamba hakuna mfugaji atakayeonewa au kudhulumiwa na kwamba bei elekezi iliyotangazwa ya sh 50 kwa kichwa ngombe na 10 kwa mbuzi italeta neema kubwa kwa wafugaji.

Pia kuhusu malalamiko ya wafugaji kupigwa faini kubwa kuuawa kwa mifugo yao amemkabidhi nyaraka za malalamiko hayo Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Katavi na kuwakamata watu wote waliotajwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Hezron Nonga amesema zoezi hilo la ugeshaji litafanyika nchi nzima na kuwataka wafugaji kujitokeza kuogesha mifugo yao ili kuikinga na maradhi.

MAVUNDE:SERIKALI KUENDELEA KULIWEZESHA KWA UJUZI KUNDI LA VIJANA NCHINI

$
0
0

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,Vijana na ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa akifunga mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana yaliyofanyika mkoani Tanga

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa akizungumza wakati wa mafunzo hayo 

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo

Serikali imesema itahakikisha inaendelea kuliwezesha kwa ujuzi kundi la Vijana ili waweze kushiriki kwa vitendo katika shughuli za kiuchumi na ujenzi wa Taifa


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,Vijana na ajira Anthony Mavunde Leo wakati wa kufunga mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana yaliyofanyika mkoani Tanga

Alisema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi wa mwaka 2014 inaonyesha kuwa ukosefu wa ajira kwa Vijana ni asilimia 11.7% duniani ambapo kitaifa ni asilimia 10.3%.


Hivyo kutokana na changamoto hiyo serikali imeweza kuja na mikakati endelevu ya kuliwezesha kundi Hilo kupata ujuzi wa kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa.


"Tunatambua kwamba kikwazo kikubwa kwa Vijana kushindwa kunufaika na fursa hasa za miradi ya kimkakati ni kutokuwa na ujuzi stahiki ,hivyo kwa mafunzo hayo Nina imani yatakwenda kumaliza changamoto ya ajira nchini"alisema Naibu Waziri Mavunde.


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana kwani wanayahitaji kwa kutambua kuwa ujuzi ndio msingi mkubwa wa maendeleo.


Alisema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea ubunifu na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya.


Mpaka Sasa jumla ya vijana 1,222 wamenufaika na mafunzo hayo katika mikoa ya Dodoma,Ruvuma,Geita, Mwanza, Mbeya, Lindi na Tanga

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 31,2019

$
0
0

                 

WAZIRI HASUNGA AWAASA WATUMISHI WIZARA YA KILIMO KUWA WAADILIFU

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua kitabu cha muongozo wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi alipotembelea kitengo cha mazingira wakati akizungumza na watumishi Jijini Dodoma alipotembelea ofisi za wizara hiyo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo tarehe 30 Octoba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa kitengo cha Uhasibu alipotembelea kitengo hicho  kwenye ofisi za wizara hiyo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Jijini Dodoma leo tarehe 30 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na watumishi wa kitengo cha Masijala ya siri wa wizara ya Kilimo alipotembelea ofisi za wizara hiyo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lijini Dodoma Leo tarehe 30 Octoba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Watumishi wa Wizara ya Kilimo wameaswa kuwa waadilifu na kuzingatia ubora wa kazi wakati wanatoa huduma kwa wananchi.


Mwito huo umetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 30 Octoba 2019 wakati akizungumza na watumishi Jijini Dodoma alipotembelea ofisi za wizara hiyo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Mhe Hasunga amesema kuwa udilifu, nidhamu na weledi kwa watumishi wa umma ni kinga dhidi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na ni moja kati ya njia zinazowawezesha watumishi wa umma kuwa wachapakazi hodari.


“Kiwango cha juu cha Ubora wa kazi zetu na utendaji wa kazi unaozingatia weledi vitaweza tu kufikiwa kwa kuajiri watumishi wenye sifa stahiki, maadili, na bidii ya kuchapa kazi na wanaoweza kwenda sambamba na kasi kubwa ya mageuzi katika wizara ya kilimo,” Alisisitiza Mhe Hasunga


Alisema kuwa utekelezaji mzuri wa majukumu yao ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam  mwaka 2015-2020.


Amewataka watumishi hao kusimama imara katika kufanya kazi na kutumia weledi wao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kwamba uadilifu ndiyo silaha muhimu katika kufanya kazi ya Umma.

Amesema mtumishi atakayetumia vibaya rasilimali za serikali atahesabika adui namba moja wa Serikali na eneo analofanyia kazi huku akibainisha kuwa mtumishi wa aina hiyo kamwe hatohamishwa badala yake ataachishwa kazi.

Ziara ya waziri wa Kilimo kukutana na watumishi hao ilikuwa na lengo la kusalimiana na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi.

KAMISHNA MKUU TRA AWAPA NENO WAJUMBE WA KAMATI YA MAMLAKA ZA MAPATO AFRIKA MASHARIKI (EARATC) KUHUSU MAADILI

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dr. Edwin Mhede akiwahutubia baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 10 wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki (EARATC) kuhusu Maadili unaofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 10 wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki (EARATC) kuhusu Maadili wakifuatilia mada mbalimbali zikizowasilishwa na wachangiaji toka nchi wanachama.
(PICHA ZOTE NA TRA)

……………………..

Na. Benedict Liwenga-Dodoma.

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hazinabudi kutilia mkazo suala la maadili ili kujenga uelewa wa pamoja na kuwa na mikakati shirikishi ya kutokomeza vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa mamlaka za mapato vinavyokwamisha ukusanyaji mzuri wa mapato.

Dkt. Mhede ameeleza hayo wakati akifungua mkutano wa 10 wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki (EARATC) kuhusu maadili unaoendelea Jijini Dodoma.

Amefafanua kwamba, katika mkutano huo masuala mbalimbali yanajadiliwa zikiwemo fursa mbalimbali pamoja na changamoto kama vile masuala ya upitishaji wa mapato haramu mipakani pamoja na namna ya kushirikiana katika kutoa adhabu kwa wafanyaji makosa hayo.

“Katika mkutano huu tunajadili masuala mbalimbali, mfano suala la maadili kama vile utovu wa nidhamu kwa watumishi wetu wa mamlaka za mapato, lakini pia tutaona namna ya kushirikishana katika kutoa adhabu kwa wafanyaji makosa katika upande mmoja aweze kudhibitiwa na upande mwingine”, alisema Dkt. Mhede.

Kwa upande wake, Mwenyekiti anayeongoza Mkutano huo, Dkt. Protazio Begumisa kutoka Uganda amesema kwamba, sababu inayowafanya kukutana mara mbili kila mwaka ni kukaa na kujadili na kuja na mikakati itayosaidia kupambana na rushwa ili kuhakikisha kwamba inapungua ama inatokomezwa kabisa.

“Tunakutana mara mbili kila mwaka kwasababu sisi sote tunafahamu kwamba rushwa haiheshimu mipaka na tusipokuwa makini Wafanyabiashara wengi wataendeleza rushwa toka Dar es Salaam, Mombasa, Burundi hadi Rwanda kwani hawa watu wanatafuta mianya katika kazi zetu na endapo tukizubaa kidogo tunapoteza mapato’’, alisema Dkt. Begumisa.

Naye Katibu wa Kamati ya Mamlaka hizo za Mapato za Afrika Mashariki (EARATC), Bi. Esther Masibayi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) ameeleza kuwa, katika Mamlaka za Mapato kupambana na rushwa ni jambo muhimu sana na suala la kukusanya kodi pia ni jambo muhimu, hivyo tunapokusanya kodi tujue kuwa kuna wengine wanakwepa kulipa kodi na kuendeleza vitendo hivyo viovu ndiyo maana lengo letu ni kuondoa hiyo tabia ya ukwepaji kodi ili tuongeze mapato katika Serikali zetu.

“Tunapopambana na rushwa lazima tukamate na tuwafunge watu, lakini hatuna magereza ya kutosha hivyo kikubwa ni kuwaelimisha ili wabadilike, ndiyo maana tunapaswa kubadili fikra zao ili waache kukwepa kodi na wakibadilika hii itawafanya wawe watu wema wenye kulipa kodi na Serikali zetu zitapata mapato ya kutosha’’, alisema Bi. Masibayi.

Mkutano wa 10 wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki kuhusu maadili (EARATC) hufanyika mara mbili kwa kila mwaka ukiwa na lengo la kujadiliana fursa mbalimbali pamoja na masuala ya maadili kwa watumishi wa Mamlaka za Mapato ikiwemo kupeana mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji katika kukusanya mapato ya serikali. 

Sambambamba na hilo, mkutano huu hukutanisha jumla ya nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi pamoja Sudani ya Kusini.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images