Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

Mhe Lowassa Anusurika Kwenye Ajali Mkoani Morogoro

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa
 Gari la  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa likiwa limebonyea kwa ubavuni baada ya kupata ajali Jumapili asubuhi.
-- 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa Mh. Edward Lowassa amenusurika kifo, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la Bwawani mkoani Morogoro.

Gari hilo la Mhe  Lowassa liligongwa na basi la Morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na kukutana uso kwa uso na gari lakini dereva wa  Mh. Lowasa kwa ustadi mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa  mzee na kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva na hakuna aliyejeruhiwa.


Mhe Lowassa na msafara wake aliendelea na safari hadi morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Kilakala ambapo yeye na Marafiki Zake Wamechangia Shilingi Milioni 18


WANAFUNZI WA DARASA LA MUZIKI LA THT WAKABIDHIWA VYETI BAADA YA KUHITIMU MASOMO YAO

$
0
0
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Guan Fabian, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments). Sherehe hiyo ya kuwaaga ilifanyika THT jijini Dar Jana.
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Hawa Lipapapa, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments).
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Ramadhani Rashid, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments). Sherehe hiyo ya kuwaaga ilifanyika THT jijini Dar Jana.
Wanafunzi wa darasa la muziki pamoja na Sauti (vocal) wakiwa na walimu wao mara baada ya kupata vyetu vya vya kuhitimu masomo yao.

UN YAENDESHA MAFUNZO KUHUSU SHUGHULI ZA UNDAP NA HAKI ZA BINADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho katika mkutano na waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar ambapo amesema wanatarajia kupata mawazo mengi zaidi ya kujenga kutoka kwa waandishi ambapo yatasaidia Umoja wa Mataifa pamoja na Serikali kuihudumia nchi kwa upeo wa juu zaidi.
Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga akizungumza na waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wao kama UN katika kutekeleza hoja za mipango wa maendeleo (UNDAP) kutokana na kuchelewa kupewa majibu na uchelewashaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja wakimsikiliza Afisa Mawasilano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.

Death and Funeral Announcement

Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) apata dhamana leo Mahakama kuu jijini dar

$
0
0
Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akizungumza na wakili wake Peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana leo asubuhi kwenye Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ambapo dhamana hiyo imepatikana kwa mashart ya mashahidi wawili wafanyakazi wa Serikali kwa bondio ya fedha Tsh20 Millioni kila mmoja na masharti mengine tumeorodhesha kwenye habari hapo chini.
Msanii Lulu (katikati) akisubiri kusikiliza maombiyake ya dhamana kusomwa na Jaji anaesikiliza kesi hiyo Zainabu Mruke leo jijini Dar es Salaam.
Lulu akiwasili kwenye kizimba cha Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo.
Wakili wa Lulu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kupatiwa dhamana.
Ndugu jamaa na marafiki wa msanii huyo na baadhi ya watu wengine wakiwa kwenye Chumba cha mahakama kuu jijini Dar es Salaam wakisubiri kusikiliza maombi ya dhamana.
Msanii Muhusin Awadi (Dk.Cheni) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutolewa kwa dhamana ya msanii huyo.

 HATIMAYE Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu mchana wa leo amepata dhamana na kuachiliwa kutokana na kesi inayo mkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu marehemu Steven Kanumba  mwaka jana.

Akisoma mashart ya dhamana Jaji anaesikiliza Kesi hiyo Zainabu Mruke, alitaja mashart kadhaa ambayo mtuhumiwa atatakiwa kuyatekeleza kabla ya kupewa dhamana hiyo. 

Mruke alisema mtuhumiwa atatakiwa kuwasilisha hatizake za kusafiria zote mahakamani hapo, atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali ambao kila mmoja atatakiwa kuweka udhamini wa Tsh20Millioni kama bondi na sio keshi.

Aidha Jaji Mruke aliongeza kuwa mtuhumiwa hataruhusiwa kusafiri nnje ya jiji la Dar es Salaam isipokuwa kwa ruhusa maalum ya mahakama.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala alisema amefurahishwa na dhamana aliyopatiwa mtejawake na wataendelea na kazi ya kumtetea hadi mwisho wa kesi hiyo.

Wasanii wenzake waliojitokeza na kuonekana mahakamani hapo ni pamoja na Muhusin Awadh (Dk.Cheni) na Steve Nyerere. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo Dk.Cheni alisema yeye binafsi amefurahishwa na dhamana hiyo na yuko tayari kufanyanae kazi.

“Lulu nilimchukua kwao akiwa na miaka mine na kuanza kufanyanae kazi hadi sasa akiwa na umri wa miaka 18 amekua msanii mkubwa nan i Director mzuri pia kwahiyo nitaendelea kufanyanae kazi”Alisema Dk.Cheni.

Alipoulizwa kuhusu kutimiza Mashart ya dhamana Dk.Cheni alisema kila kitu kilikuwa kimetimia ispokuwa passport tu ndio hawakutarajia kama ingehitajika lakini tayari alishapigiwa simu mtu ailete kutoka nyumbani kwao Tabata na kukamilisha mashart ya dhamana hiyo. 

April saba mwakajana msanii huyo alifikwa na kadhia hiyo ya tuhuma za kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa Filamu nchini marehemu Steven Kanumba kutokana na mgogoro uliotokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kuelezwa kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. 

MEYA WA ILALA AHIMIZA KUKAMILISHWA KWA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA PUGU KAJIUNGENI

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akitoa taarifa wakati akizindua Mradi wa Maji Pugu Kajiungeni ambapo amesema mradi huo unatokana na kisima cha maji chenye urefu wa mita 122 toka usawa wa ardhi.
Mstahiki meya amesema kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita 60,000 kwa saa. Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na mtandao wa mabomba wa kilometa 9, vituo 25 vya kuchota maji, nyumba ya pampu, fensi pamoja na uzio.
Aidha amewataka wananchi wa maeneo husika ya Pugu Kajiungeni ni kuitunza miradi hii na kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili kuweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Pugu Emelda Samjela na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kassim Mjesa na Kulia ni Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd inayoshughulikia mradi huo Method Mlay.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akimkabidhi Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) barua rasmi ya mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni unaotekelezwa kwa ushirikiano na wahisani /wafadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Tanzania, Halmashauri ya manispaa ya Ilala na wafadhili wengine mbalimbali. Anyeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Kassim Mjesa.
Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) akitoa neno la shukrani baada Mstahiki Meya kumkabidhi barua rasmi ya ujenzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni na kuahidi kutoa ajira kwa Vijana wa maeneo ya Pugu kuanza sasa mpaka mradi utakapokamilika.
Sehemu ya wakazi wa Pugu Kajiungeni waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo utakaochukua miezi Sita kukamilika na kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa sita kushoto) akikagua sehemu ya mradi huo kilipojengwa kisima chenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita elf 60,000 kwa saa.
Muonekano wa Kisima hicho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa nne kushoto) na Diwani wa Kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela katika picha ya pamoja na viongozi wa kata hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akingumza na vyombo vya habari ambapo amesema mradi huo wa maji wa Pugu Kajiungeni uhahudumiwa na tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 140,000 lilipo katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto na matenki mnegine ya maji yenye ujazo wa lita 45,000 na 100,000 ambayo yanapatikana Pugu Kajiungeni karibu na Zahanati ya Pugu.
Amefafanua kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imechangia kiasi cha Shilingi 378,000,000 na kiasi kingine kinachobaki kinatolewa na Serikali Kuu pamoja na wahisani.
Mradi wote utagharimu kiasi cha shilingi 1,024,000,000/=.
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa kata ya Pugu Kajiungeni Nuru Daniel akitoa shukrani zake za pekee kwa Serikali ya awamu na uongozi kwa kutekeleza ilani za Chama ikiwemo kuwapatia maji wakazi wa Pugu Kajiungeni.

Waziri Mukangara atembelea Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) jijini dar leo

$
0
0
Meneja Uchapishaji wa Shirika la Magazeti la Serikali(TSN) John Mcharo(kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara(wa pili kushoto) jinsi wanachapisha magazeti leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Profesa Moses Warioba( wa tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Magazeti ya Serikali(TSN) Gabriel Nderumaki (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (kulia).
Kaimu Mhariri Mteandaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara(katikati) jinsi wanavyohariri habari mbalimbali leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki(wa pili kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (kushoto) jana leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali. Wengini ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Profesa Moses Warioba( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.
Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akijionesha jinsi kurasa za magazeti ya Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) zinavyosanifiwa na wasanifu jana leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali.Picha na MAELEZO- Dar es salaam

SEKRETARIETI YA CCM YATEMBELEA MRADI WA DARAJA LA MAlAGARAsI MKOANI KIGOMA LEO

$
0
0

Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,ukiongozwa na Katibu Mkuu,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ukiwa katika matembezi ya kuangalia maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Malagarasi na Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kidawe mpaka Uvinza kwa kiwango cha lami leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa ujenzi wa Daraja hilo,Bw. Jung-Sik You kutoka nchini Korea.
Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Malagarasi na Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kidawe mpaka Uvinza kwa kiwango cha lami,Bw. Jung-Sik You (kushoto) akitoa maelezo machache juu ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana na kuahidi kuwa mpaka ifikikapo mwezi Septemba ama Oktoba,Daraja hilo litakuwa limeshakamilika na kulikabidhi kwa Serikali.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo,waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza na pia kusikiliza shida zao wakati alipofanya ziara ya kutembelea vijiji viwili vya Wilaya hiyo ya Uvinza.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Uvinza,Wilayani Uvinza mkoani Kigoma leo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Evans Bukuku's Comedy Club - 29th January 2013

$
0
0

Greetings All,

Hope this email finds you all in the best of spirits!!

I have attached, the poster design for the upcoming comedy show so please forward and post on your respective platforms. Please also include the facebook event page for more details on this link:http://www.facebook.com/events/493354444050359/ 

Thanks and Kind Regards,


Evans.

happy birthday mtoto Eskia David

$
0
0

FAMILIA  YA  BWANA NA BIBI DAVID  KISSENGE INAMPONGEZA MTOTO WAO  MPENDWA ESKIA DAVID KWA KUTIMIZA  MWAKA MMOJA TAREHE 27.01.2013, MWENYEZI MUNGU  AMJALIE AFYA NJEMA, HEKIMA, BUSARA NA MIAKA MINGI  YENYE KUMPENDEZA MACHONI  PA BWANA

manufaa na faida ya gesi kwa wananchi wa lindi na mtwara

$
0
0

SERIKALI imetaja manufaa na faida ambazo wanatarajia kuzipata wananchi wa Mtwara pamoja na Lindi endapo gesi itasafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam.

Imesema Mkoa wa Mtwara ndipo utakapo jengwa mtambo mkubwa wa kusafishia gesi hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa matumizi ya uzalishaji umeme na matumizi ya moja kwa moja viwandani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipokuwa akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Radio One jijini Dar es Salaam.

Naibu waziri huyo ameweka wazi kuwa mkoani Mtwara licha ya Serikali kupanga kujenga viwanda vingine kadhaa, inajenga mtambo wa megawati 250 ambao utakuwa ukizalisha umeme na mwingine kujengwa mkoani Lindi eneo la Somanga Funga utakao kuwa ukizalisha megawati 520.

Akifafanua zaidi Simbachawene alisema eneo la Mikindani katika Kijiji cha Msijute mkoani Mtwara kinatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha saruji Afrika Mashariki na Kati chenye uwezo wa kutoaji ajira kwa watu 6000 jambo ambalo ni manufaa ya Wanamtwara.

Alisema pia tayari kuna wawekezaji wa viwanda vya mbolea wamejitokeza kujenga viwanda mkoani Mtwara na Serikali itaviacha vinu vya kuchimba na kusindika gesi eneo hilo jambo ambalo bado ni manufaa makubwa kwa wananchi.

“Viwanda vya kusindika gesi hii vimepangwa kujengwa maeneo ya Lubasi, Kishere, Mchinga Bay, Lindi, Sudi Bay, Airport pamoja na Mikindani…viwanda vyote hivi vitatoa ajira kubwa sana,” alisema Naibu Waziri.

Alisema licha ya manufaa hayo, gesi itakapopelekwa Dar es Salaam itazalisha umeme wa uhakika pamoja na kutumika moja kwa moja viwandani jambo ambalo litailetea taifa tija kubwa ikiwa ni pamoja kupunguza ukali wa maisha.

“Ni kweli gesi imepatikana Mtwara lakini ni lazima uipeleke sokoni ili iweze kupata soko (wateja)…Dar es Salaam ndio kwenye soko, huwezi ukaiacha Mtwara ambako hakuna soko; mbali na kuzalisha umeme kuna viwanda 37 na hoteli kadhaa zinataka ziitumie moja kwa moja ni lazima iletwe huku, Mtwara pale hakuna soko,” alisema.

Aidha alitolea mfano kuwa zipo nchi mbalimbali ambazo zimegundua gesi lakini zimelazimika kuisafirisha kwa mabomba kwenda eneo la soko. Alibainisha kuwa nchi ya Urusi inasafirisha gesi yake hadi nchini Ujerumani huku Iran ikisafirisha hadi India gesi yake kutafuta soko lilipo.

Alisema miundombinu mikubwa ya umeme ipo jijini Dar es Salaam hivyo kuna kila sababu ya gesi hiyo kuletwa jijini humo ili iweze kuzalisha umeme na matumizi ya viwandani moja kwa moja pamoja na matumizi mengine, ambapo tayari wateja wamepatikana.

Aidha aliongeza kuwa uzalishaji umeme wa kutosha kwa kutumia gesi utapunguza bei ya umeme na kuuzwa kati ya senti 6 na 8 za Marekani jambo ambalo litapunguza ugumu wa maisha na pia bei ya bidhaa nchini.

Pamoja na hayo amevitaka baadhi ya vyama vya siasa na taasisi zisizo za Serikali (NGO’s) zinazowapotosha Wanamtwara juu ya mradi huo kuacha kitendo hicho kwani hakuna asiyejua umuhimu wa gesi hiyo kuja Dar es Salaam.

“Hivi ni nani asiyejua kuwa tatizo la kutokua na umeme wa uhakika nchini ndilo linalokwamisha uchumi wa nchi…Tanzania inapoteza bilioni 4.5 kwa ajili ya kununua mafuta ya kuzalisha umeme kwenye mitambo yake, sasa gesi itaokoa fedha hizi,” alisema Simbachawene.

Hata hivyo amesema Serikali haiwezi utekeleza mradi huo kwa nguvu bali itaendelea kuwaelimisha Wanamtwara umuhimu na manufaa ya gesi hiyo kuletwa Dar es Salaam na inaimani wataelewa na malumbano kumalizika.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Ayoub mzee with Palestine leader Mahmood Abbas

$
0
0

Ben TV's reporter Ayoub  mzee with  Palestine  leader Mahmood  Abbas.Chairman of the Palestine Liberation Organization and President of the  State of Palestine 
Mr Abbas on Sunday attended the African Union Summit as a special guest and reiterated the call for Israel's withdrawal from occupied territory.
Mr. Abbas was speaking in Addis Ababa during the opening of the 20th African Union Summit at which some 40 African heads of state and government and UN Secretary General Ban Ki-moon were present.
While on his first visit to Africa after the admission of Palestine into the UN with an observer status through the support of the African countries, the Palestinian leader reaffirmed his opposition and that of all the Palestinian people to the illegal occupation and colonization carried out by Israel on the Middle-East territory.
"The continued colonization only reflects a racist and an apartheid regime that is applied on the Palestine territory," Abbas said.
He called for the stoppage of the occupation policy, the release of Palestinian prisoners in Israel, the withdrawal of the Israeli forces from the occupied territory and the termination of the policy of confiscating Palestinian taxes by its powerful neighboring state.

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0

Ngoma ya I Am A Disco Dancer  iliyomtoa Mithun Chakraborty mwaka 1983 ilitamba sana enzi za picha za kihindi katika kumbi za sinema za Cameo, Odeon, New Chox  na Avalon ambazo siku hizi ni marigiyo...

ngoma azipendazo ankal - Kizazi kipya

$
0
0

Ngoma ya 'Mtu Pesa' ya Twanga Pepeta itabakia mojawapo ya Classic ya bendi hiyo

UMOJA WA WANATAALUM WA KIISLAM TANZANIA (TAMPRO) NA WANAZUONI WA KIISLAMU (HAYAT-ULAMAA) WAHAMASISHA UTEKELEZAJI WA NGUZO YA ZAKAT UL-MAAL

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayat-ulamaa) Shk. Suleiman Amran Kilemile Akitoa Nasaha Juu ya Umuhimu wa Waislam Kiimarisha utekelezaji wa Ibada ya Kutoa Zakat kwa Makundi yaliyotaja Katika Qur'an kwani ndio Njia rahisi ya Kuimarisha Uchumi wa Jamii na Nchi kwa Ujumla.  
 
 Kijana Mfanyabiashara Ndogo Ndogo Ambae amekuwa akitoa Zakat mara kwa Mara akitoa ushuhuda jinsi gani utoaji wa Zakat Umemsaidia kulinda na Kukuza Biashara yake katika Mkutano wa Ugawaji Zakat.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Baytul -ulmaal (Charity Fund) Tanzania akisisitiza Umuhimu wa Matajiri na Wasomi wa Kiislam Kushiriki Kikamilifu kuimarisha Mfuko huo kwa Maslahi ya Ustawa wa Jamii hasa Masikini na wenye mahitaji maalum ili kuleta uiano wa kimaendeleo.
 Baadhi akina Mama wakifuatilia kwa Makini Mada Juu ya Utekelezaji wa Ibada ya Zakat ambayo ni Nguzo Muhimu katika dini ya Kiislam yenye lengo la kupambana na Umasikini ndani ya Jamii ya eneo husika.
   Kijana Mwanafunzi Yatima anayejiunga na Shule ya Serikali Akipokea Tshs 100,000 Kutoka kwa Sheikh Suleiman Kilemile kama Fungu la Zakat lililotolewa Katika Ukumbi wa Lamada Ilala. Mfuko wa Baytul –ul maal Unaendeshwa pamoja kati ya Wanataalum wa fani mbali mbali za kimazingira pamoja na Wanazuoni wa Kiislam kukuzanya Zakat pamoja na Waqfu kwa manufaa ya Jamii ya Kiislam.
      Waumini wa Kiislam wakimsikiliza Shk Twaha Bane wakati akieleza Umuhimu wa Waislam kuitekeleza Nguzo ya Zakat kwani inaleta Upendo, Amani na Uimara wa Biashara kwa Mtoaji na Anayepokea.

ABIRIA WAITAKA SUMATRA KUFANYA UKAGUZI WA MARA KWA MARA

$
0
0
Mahmoud Ahmad Arusha

Baadhi ya Abiria wanaosafiri na mabasi kwenda mikoani wameitaka mamlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu Sumatra kuangalia wezekano wa kuwa na ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mabasi yatokayo mikoani kwani kumekuwa na ukiukwaji wa sheria za usafirishaji mara kwa mara na Abiria kuendelea kupata matatizo wawapo safarini.

Hayo yamezungumzwa wakati abiria hao wakisafiri kutoka singida kuelekea Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwenye basi la Mtei Coach na kumtaka kondakta kuelezea Tiketi ya Arusha mwisho wake wapi?kwani abiria anayetoka singida hadi usa river je anatakiwa kulipa nauli hadi usa au la.

Tukio hilo limetokea wakati mwandishi aliposafiri na basi hilo kutoka Stand kuu kuelekea Usa River kwani ndani ya basi alikuwepo abiria na familia yake waliokuwa wanasafiri kutoka Singida hadi usa River na kutakiwa kusimama ili kuwapisha Abiria wengine kwani tiketi yake iliangikwa singida Arusha.

Taarifa zinadai kumekuwapo na changamoto mbali mbali kwenye usafiri wa Mabasi ya mikoani kwa abiria kukosa masaada pindi yanapojitokeza matukio ya ukiukwaji wa sheria za usafirishaji huku mamlaka husika ikijitokeza kwenye wakati wa siku za mwisho wa mwaka hadi pale wanapopelekewa taarifa ndipo hustuka na kuja njiani na kutakiwa kuacha ofisi zao kuja kushughulikia kero mbali mbali za Abiria.

Abiria hao wakamtaka waziri wa uchukuzi kuliangalia suala hilo kwa ukaribu kwani matatizo wayapatayo ni makubwa zaidi ya ukaguzi wa nauli pekee huku wengine wakiwa hawajapewa tiketi za kuonyesha wanasafiri hadi wapi haya yamekuwa ni matatizo ya kawaida kwa abiria wengi wasafirio kwenye baadhi ya mikoa hiyo ya kanda ya kaskazini.

“Utakuta wakati mwingine unasafiri kutoka sehemu Fulani kwenda sehemu nyingine unapitishwa kituo na unapohoji unaambiwa umelala hivyo unashushwa sehemu nyingine kama huna fedha nyingine unafanyaje”alihoji Fadhill Kibwana makazi wa jiji la Arusha.

Fadhili alienda mbali kwa kuzitaka mamlaka husika ikiwemo jeshi la polisi kuwa makini na madereva na makondakta wa mabasi ya Abiria hapa jijini kwani wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kinyama kwa kuwapandishia nauili wakati wa jioni wanaporudi majumbani kwao wakati wanapotoka kwenye mihangaiko tyao ya kujipatia ridhiki zao za kila siku.

“Nauli ya Usa River ambayo kihalali ni sh.500 inageuka sh,1000 huku wahusika wakiyafumbia macho bila ya kuchukuliwa hatua sehemu mbali mbali huko vijijini wananchi wamekuwa wakipata taabu bila ya msaada utakuta mahali pa nauli ya 500 inatozwa hadi 2500 huu sasa ni wizi wa mchana kweupe”alisema Hadija Kichwa mkazi wa Magugu mkoani manyara.

Matatizo ya usafiri kwenye mikoa mbali mbali hapa nchini yamekuwa kero kwa wananchi hasa wa vijijini kwani imeonekana kuwa wananchi hao wamesahauliwa huku wakizitaka mamlaka husika kwenda huko kila mara ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo hiyo ya usafiri.

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti hili unaonyesha matatizo yamekuwa mengi kwa wasafirisha abiria humu nchini na zaidi kwenye vijiji huku wamiliki hao wakikiuka nauli halali za abiria kwa kuwatoza nauli hadi 65% ya nauli halali kwa kilometa

KIJIWE CHA UGHAIBUNI

MICHUANO YA KINONDONI MEYA CUP YASHIKA KASI

$
0
0
Manispaa ya Kinondoni ni moja ya wateja wakubwa wa NMB lakini pia Manispa ya kinondoni inaongoza kwakua na wakazi wengi zaidi ya manispaa nyinginezo. Hivyo basi kwa kulizingatia hili na kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri kati ya NMB na Manispaa ya Kinondoni NMB imedhamini mashindano yanayoendelea katika wilaya ya kinondoni . Mashindano ambayo yanawahamisisha vijana katika kuimarisha ulinzi na usafi.Michuano hii ambayo inazinduliwa katika awamu tatu tofauti na katika sehemu tatu tofauti, mwishoni mwa wiki ikiwa ndio uzinduzi wa pili ulishirikisha kata ya Mzimuni na Ndugumbi ambapo Ndugumbi waliibuka kidedea kwa 1-0

Mheshimiwa Iddi Azan Mbunge wa Jimbo la kinondoni akikagua vikosi vya mpira wa miguu kata ya Ndugumbi na Mzimuni mwishoni mwa wiki ambao wapo katika michuano ya kinyang’anyiro cha Kinondoni Meya Cup 2013 inayoendelea katika kata tofauti wilayani humo.Mashindano haya yakiwa na kusudi la kuhamasisha Usafi na ulinzi Benki ya NMB ikiwa ndio wafadhiri wakuu na TVS King watatoa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu kwa mshindi wa kwanza

Mchezaji Abdul Hussein wa timu ya Ndugumbi akiwakabili vilivyo wachezaji wa timu ya Mzimuni katika michuano ya kuwania kombe la meya wa kinondoni 2013 katika mechi zinazoendelea kwenye wilaya ya kinondoni Katika mechi zilizochezwa mwishini mwa wiki Ndugumbi waliibuka kidedea kwa 1-0

WIZARA ITASHIRIKIANA NA WADAU KUTATUA MIGOGORO YAUHIFADHI WILAYANI LOLIONDO - KAGASHEKI

VURUGU NA UHARIBIFU MTAA WA ISENGO KATA YA IZIWA. MBEYA

$
0
0
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ATHUMANI DIWANI ENEO LA TUKIO


WANAKIJIJI ISENGO IZIWA WAKIWASIKILIZA WANAUSALAMA HUKU WAKIWA NA SIRAHA ZAO ZA JADI

CHANZO CHA MAJI IZIWA

MAMA WA KISAFWA AKIWA AMEFICHA PANGA


SIRAHA ZA JADI ZILIZOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
MNAMO TAREHE 28.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS MAAFISA WA HIFADHI YA MALIASILI NA UTALII  WAKIONGOZWA NA MENEJA WA HIFADHI HIYO KASMIR S/O NGOWI NA AFISA MISITU WA JIJI  LYOWA S/O WAYANGA KWA KUSHIRIKIANA NA  ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA WALIFIKA KATIKA MTAA WA ISENGO KATA YA IZIWA KWA AJILI YA KUENDELEA NA OPERESHENI YAO YA KUWAONDOA WATU WALIOVAMIA NA KULIMA  NDANI YA HIFADHI YA SAFU YA MLIMA MBEYA [MBEYA RANGE FOREST RESERVE] ENEO AMBALO NI CHANZO CHA MAJI NA VIUMBE HAI ZOEZI LILILOANZA TANGU TAREHE 28.12.2012.
 HATA HIVYO KABLA ZOEZI HILO KUANZA KUNDI KUBWA LA WANANCHI WA ENEO HILO WAPATAO 400 WAKIWA NA SILAHA ZA JADI WALIFIKA ENEO HILO WAKIWA WAMEJIANDAA KUFANYA VURUGU WAKISHINIKIZA KUTOFANYIKA KWA ZOEZI HILO. KATIKA VURUGU NDOGO ILIYOTOKEA  YOHANA S/O MDEWA,MIAKA 54,MSAFWA,MWANACHAMA WA ASASI YA KIRAIA YA KUTUNZA MAZINGIRA  MKAZI WA KIJIJI CHA IHOMBE , ALIJERUHIWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI , WAKIDAI NDIYE MSALITI ALIYEWALETA WATU HAO ,HIVYO POLISI WALIMUOKOA NA KUMHIFADHI KATIKA OFISI YA MTENDAJI KATA.
 PIA KATIKA VURUGU HIZO KULITOKEA UHARIBIFU KATIKA GARI STJ 1830 MALI YA WAKALA WA HIFADHI YA MISITU NYANDA ZA JUU KUSINI  KWA KUPASUKA WIND SCREEN YA MBELE NA SIGHT MIRROR YA KUSHOTO  NA MAGARI MENGINE YA IDARA HIYO STJ 1821 NA STJ 1832 KURUSHIWA  MAWE PIA  KUBOMOA MADARAJA MAWILI  YALIYOPO KIJIJINI HAPO. KUFUATIA HALI HIYO  KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA MKOA WA MBEYA  WALIFIKA ENEO HILO HATA HIVYO WANANCHI WALITAWANYIKA KWA KUKIMBIA. POLISI  KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA ENEO HILO WALITOA WITO KWA           WANANCHI KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI AMBAPO WALIKIRI NA KUDAI HAWAKUELEZWA JUU YA ZOEZI HILO NA WAMEAHIDI KUJENGA  WAO WENYEWE MADARAJA WALIYOKUWA WAMEBOMOA.
UONGOZI WA SERIKALI YA WILAYA YA MBEYA CHINI YA MKUU WA WILAYA DR NORMAN SIGALA NA MSTAHIKI MEYA WA JIJI ATHANAS KAPUNGA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO  MHE DIWANI NA MTENDAJI  KATA YA IZIWA KATIKA KIKAO KILICHOFANYIKA BAADAE WAMEKUBALIANA KUWA WATU WOTE WALIOVAMIA ENEO HILO WAHAKIKISHE WAMEHAMA KABLA YA MWEZI AGOST – 2013.  KWA SASA HALI IMEREJEA KUWA SHWARI KIJIJINI HAPO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA. PIA ANAZIDI  KUSISITIZA KUWA MAZUNGUMZO NDIO  NJIA MUHIMU NA SAHIHI YA KUWASILISHA MALALAMIKO/KERO BADALA YA FUJO NA VURUGU ZISIZOKUWA NA TIJA KWANI ZINAWEZA KULETA MADHARA  NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YAO. KAMANDA AMEAHIDI KUWA WALIOVUNJA SHERIA KWA KUMJERUHI YOHANA S/O MDEWA NA KUFANYA UHARIBIFU WA MADARAJA WATAFUATILIWA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images