Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110148 articles
Browse latest View live

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipa

$
0
0

Ngoma ya P-Square ya 'Chop My Money' wakimshirikisha Akon na May D itachukua muda kuchua

WAZIRI KAGASHEKI AMEANZA KUTATUA MIGOGORO YAUVUNAJI NA UVAMIZI KATIKA SHAMBA LA SAO HILL

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AZINDUA MABASI YA KUSAFIRISHA MAHABUSU MKOA WA PWANI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima ili azungumze na Maafisa wa Jeshi hilo kabla ya uzinduzi wa magari ya 10 ya kuwasafirisha Mahabusu mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza katika hafla ya uzinduzi wa jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima akiwa ndani ya moja ya Basi la kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani mkoani Pwani.
Sehemu ya magari 10 ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima katika hafla iliyofanyika Gereza la Mahabusu Ubena mkoani Pwani.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (Kushoto) akitoa ufafanuzi zaidi kwa waandishi wa habari kuhusiana na magari 10 yaliyozinduliwa mkoani Pwani.

Wanawake waliopona Fistula CCBRT waamua kujiajiri

$
0
0

Mratibu wa Kituo cha Mabinti kilichopo chini ya Hospitali ya CCBRT Bi. Katia Geurts akiwaelezea Maafisa wa Vodacom Foundation shughuli zinazofanywa na kituo hicho wakati walipotembelea kuona miradi mbalimbalia wanaoyoifadhili ,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu ya Fistula katika Hospital ya CCBRT na Kupona ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao.
Mmoja wasichana wa kituo cha "Mabinti" aliyepata kutibiwa Fistula na kupona katika Hospitali ya CCBRT Bi. Roida George akionesha umahiri wa kushona kofia wakati Maafisa wa Vodacom Foundation ambao ndio wadhamini wa miradi yao walipotembelea katika kituo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinawawezesha mabinti hao kupata elimu ya kazi za mikono ili waweze kujikimu kimaisha pindi wanaporudi makwao.
Mratibu wa Kituo cha Mabinti kilichopo chini ya Hospitali ya CCBRT Bi. Katia Geurts akifafanua jambo Maafisa wa Vodacom Foundation jinsi shughuli zinazofanywa na kituo hicho wakati walipotembelea kuona miradi mbalimbalia wanaoyoifadhili ,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu ya Fistula katika Hospital ya CCBRT na Kupona ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao,wapili toka kuliani Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon,Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu.

========== ============= =============

Wanawake waliougua kutibiwa na hatimaye kupona maradhi ya fistula katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam wameamua kujikita katika sanaa ya kazi za mikono kwa lengo la kujiajiri sambamba na kujikwamua na wimbi la umasikini.

Takribani wanawake wapatao 62, chini ya mpango madhubuti ulioratibiwa na hospitali ya CCBRT, wamekuwa wakihitimu mafunzo mbalimbali ya kazi za mikono zikiwemo sanaa za ushonaji wa batiki, nguo za aina tofauti, utengenezaji wa mabegi, kofia, ususi na kadhalika, katika Kituo kinachoendeshwa na hospitali hiyo kijulikanacho kama 'Mabinti' tangu mwaka 2007.


Akizungumza mbele ya ujumbe wa wadhamini waliotembelea kituo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mratibu wa Kituo hicho, Katia Geurts, alisema kituo hicho kinatoa mafunzo mahsusi kwa wakinamama waliopona baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa fistula. 

"Wengi wao wanatoka katika familia duni, hivyo mafunzo haya wanayoyapata baada ya kumaliza matibabu ya Fistula yanakwenda kuwasaidia kujiajiri wao wenyewe jambo linalowasaidia kupunguza ukali wa maisha," alisema Geurts.


Aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo kituo hicho huwapatia vyeti vya uhitimu vinavyotambulika, sanjari na vitendea kazi vinavyoendana na stadi stahiki aliyohitimu mwanafunzi kwa minajiri ya kuwarahisishia upatikanaji wa mahitaji muhimu ya maisha yao.


Nae Mkufunzi wa Kituo hicho ambaye awali alikuwa mmoja wa waathirika wa ugonjwa wa fistula hospitalini hapo, Jane Rugalabamu, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aanze kufundisha wenzake kituoni hapo amebaini kuna idadi kubwa ya wanawake wenye matatizo ya fistula ndani ya jamii lakini waume zao wamekuwa wakiwaficha kwa dhana ya kufisha aibu.


"Kuna haja kubwa ya kuelimisha akinababa wawaruhusu wake zao wenye matatizo waje kutibiwa. Ugonjwa huu unatibika na wala sio wa kurogwa kama wengi wanavyodhani, sisi sote hapa kwenye kituo cha mabinti tulikuwa na maradhi hayo na sasa tumepona kabisa wanawake jitokezeni," alisema Rugalabamu.


Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Grace Lyon, baada ya kukagua shughuli mbalimbali za mafunzo zinazoendelea kituoni hapo, alisema kwa niaba ya wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone duniani kote, wataendelea kuwasaidia akinamama wote wanaopatwa na maradhi ya fistula hatua kwa hatua, sanjari na kuhakikisha wanazidisha kasi katika kampeni inayoendelea dhidi ya maradhi hayo.



"Tutaendelea kuwa karibu zaidi na waathirika wa fistula kuanzia hatua ya kuwasafirisha kutoka vijijini na mikoani kwa kuwatumia fedha kupitia huduma yetu ya M-Pesa, pia tutakuwa pamoja wakati wote wa matibabu na baada ya kupona tutawaunga mkono kwenye mafunzo kama haya ili kuwaletea ustawi ulio bora kwa maisha bora kwa ajili yao na familia zao," alisema Lyon.

PRESIDENT KIKWETE AT WORLD ECONOMIC FORUM 2013 IN DAVOS

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets Belgium Princess Astrid in Davos Switzerland during the World Economic forum. The two leaders later participated in a Global Health and Diplomacy Dinner.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Global Fund Executive Director Dr.Mark Dybul(second left) at Hotel Sheraton in Davos Switzerland during the World Economic forum. Left is Global Fund’s Director for Resource Mobilization Dr.Christoph Benn.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete speaks with Germany Federal Minister for Development Mr. Dirk Niebel at Hotel Sheraton in Davos During the World Economic Forum(WEF) meeting yesterday.(photos by Freddy Maro).

UJUMBE WA SEKRETARIETI YA CCM WAWASILI SALAMA MKOANI KIGOMA LEO

$
0
0
Wananchi wa Mkoa wa Kigoma leo wameupokea kwa shangwe Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliowasili mkoani Kigoma ukitokea jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa Treni ya Reli ya Kati.

Wajumbe hao ambao wanaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana ni pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela.

Akizungumza baada ya kuwasili Mkoani Kigoma leo, Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana alisema kuwa lengo la wao kutumia usafari huo wa Treni ni kuwadhihirishia wananchi wa Tanzania kuwa Usafiri wa Treni ni Usafiri wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara ya Uchukuzi, itasimamia kikamilifu usafiri huo na kuendelea kuuboresha zaidi ya ilivyo sasa na kuhakikisha safari zinaongezeka na kuwa za kila siku na si kuwa kwa wiki mara mili kama ilivyo sasa.

Nao baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wao wa kusafiri kwa kutumia Treni kutoka jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Kigoma na kujionea hali halisi ya usafiri huo.

Ujumbe huo upo Mkoani Kigoma kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama pamoja na wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida wakati Treni iliposimama kwa muda mfupi katika mji huo.
Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akizungumza nao.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akipena mkono na Dereva wa Treni ya TRL,Bw. Kambi Ali (wa pili kulia) aliyewasafirisha kutoka Jijini Dar es Salaam mpaka Mjini Kigoma salama. Wengine pichani ni Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye.
Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakielekea kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati ukiwasili Mjini Kigoma leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.
Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma ya utamaduni ya mkoa wa Kigoma iliyokuwa ikipigwa Stesheni leo,huku Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akipiga moja ya ngoma hizo.

Wiki Hii Katika The Sporah Show

MASASI YAZIDI KUCHAFUKA,WATU SABA WADAIWA KUPOTEZA MAISHA

$
0
0
Na Abdulaziz Video.

WATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwa zimebeba sura ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.

Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu saba.

Majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete Vurugu kubwa zilianza majira ya saa 4 asubuhi leo baada ya polisi waliokuwa wakiendesha pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano,Hata hivyo hoja hiyo ilihamia kwenye gesi na kundi la vijana mara moja walivamia nyumba ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari mawili.

Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na kuiteketeza kwa moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma moto pamoja na magari matatu.Hasira za wananchi hao zilifika kituo kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma moto magari matano ya halmashauri ya wilaya.

Pia walichoma moto ofisi ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma ofisi ya maliasili.

Polisi kutoka maeneo mbalimbali yandani na nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na kusababisha vifo vya watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi….

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI ATOA MAONI YA KATIBA MPYA KWA TUME

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walioongozwa na Mwenyekitiwa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba (kulia). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo mstaafu leo ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika leo katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa maoni yake kuhusu KatibaMpya kwaTume. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
Rais mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akibadilisha mawazo na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) na Makamu Mwenyekiti,Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani (katikati). Wajumbe wa Tume walikuta na Rais huyo mstaafu leo ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali ya Tanzania, Mhe. Andrew Chenge akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika leo katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu AugustinoRamadhani.

Rais Kikwete ahudhuria Mkutano wa AU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na jopo la APRM kuhusu Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Mhe. Rais alitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Wengine katika picha ni Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwemo pia wajumbe na Wabunge waliofuatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano huo.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe aliofuatana nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM, Tanzania.

Rais Kikwete ahudhuria Mkutano wa AU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na jopo la APRM kuhusu Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Mhe. Rais alitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Wengine katika picha ni Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwemo pia wajumbe na Wabunge waliofuatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano huo.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe aliofuatana nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM, Tanzania.

UTULIVU WAREJEA MTWARA, ZAIDI YA 40 WAKAMATWA, PINDA NA NCHIMBI WATIA TIMU

$
0
0
 
Sehemu ya watuhumiwa wa vurugu za Mtwara wakikamatwa 
mmoja baada ya mwingine

Hali ya  utulivu  inadaiwa  kurejea katika wilaya ya Masasi  mkoani Mtwara baada ya   vikosi  vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na  polisi  kuungana  kuweka ulinzi huku  watu  zaidi ya 40  wakikamatwa  kuhusika na matukio  ya vurugu za jana.

Mwandishi  John Kasembe anaripoti  kuwa kutokana na vurugu  hizo  waziri mkuu Mizengo Pinda na  waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku  huu wapo Mtwara  wakiendelea na vikao  vya  kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.

Pia inadaiwa  mida ya asubuhi  leo  polisi  walilazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  vijana ambao  walikuwa  wamefunga barabara na  kuwatoza ushuru  batili  wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.

Mbali ya tukio  hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara  kwa siku ya leo shughuli  zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara zimesimamishwa kwa  muda  ili  kukwepa vurugu kama za jana  japo shughuli za ibada  zimeendelea kwa  utulivu  zaidi.

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Piga ua lakini mwamba wa muziki toka Nigeria Fela Anikulapo Kuti hatosahaulika katika safu ya nyota wa muziki halisi wa bara la Afrika. Msikilize katika ngoma hii ya 'Lady'

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0

Bibie Hafsa Kazinja alitia Presha watu sana akiwa na Banana Zorro

MTANZANIA KUSIMAMIA PAMBANO LA UBINGWA WA DUNIA KWA VIJANA

$
0
0

Ngowi akiwa na mwamuzi Jaap Van Niewenhuizen wa Afrika ya Kusini.

Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Matanzania Onesmo Ngowi atasimamia pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.

Mpambano huo utawakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini akipambana na bondia Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia. Georgia ilikuwa kati ya nchi zilizokuwa Umoja wa nchi za Kisoshalisti wa Sovieti (USSR).

Mabondia hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight tarehe 15 February, 2013.

Mpambano wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg, nchini South Africa.

Ngowi kama kamishna mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao: Refarii: Wally Snowball (Afrika Kusini). Jaji Namba moja:Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar (Spain) na Jaji namba tatu: Jaap Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini).

Mpambano huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya mradi wa IBF wa “Utali wa Michezo”
Imetolewa na:
UTAWALA
IBF/ AFRIKA

MEYA WA KINONDONI AHAMASISHA USAFI ENEO LA NDUGUMBI.

$
0
0


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amefanya ziara ya uhamasishaji utunzaji wa usafi wa mazingira kwa wakazi wa kata ya Ndugumbi, jijini leo (Jan 27). Pamoja na Mambo mengine ameahidi kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu ambapo kila mwisho wa wiki, wakazi wanaoishi kwenye Kata mbalimbali za Manispaa hiyo watakuwa wakitekeleza zoezi hilo. Pichani ni zoezi hilo lilivyotekelezwa leo kwa viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (Suruali ya njano) akisimamia uondoaji wa taka zilizokuwa zimetelekezwa pembezoni mwa Barabara ya Mandela.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.


Meya wa Manipaa, Yusuph Mwenda (kulia) akimkabidhi shilingi 10,000 bibi kizee ambaye ni mkazi wa mtaa huo baada ya kufurahishwa na hatua yake ya kujitolea kufanya usafi wa mazingira.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi wa Kata ya Ndugumbi wakikatiza mitaa mbalimbali ya Kata hiyo wakiwa na mifagio na machepeo.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.
Mifereji ilizibuliwa.
Moja ya vitendea kazi vilivyotumika kwenye zoezi hilo.

MEYA WA KINONDONI AHAMASISHA USAFI ENEO LA NDUGUMBI.

$
0
0


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amefanya ziara ya uhamasishaji utunzaji wa usafi wa mazingira kwa wakazi wa kata ya Ndugumbi, jijini leo (Jan 27). Pamoja na Mambo mengine ameahidi kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu ambapo kila mwisho wa wiki, wakazi wanaoishi kwenye Kata mbalimbali za Manispaa hiyo watakuwa wakitekeleza zoezi hilo. Pichani ni zoezi hilo lilivyotekelezwa leo kwa viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (Suruali ya njano) akisimamia uondoaji wa taka zilizokuwa zimetelekezwa pembezoni mwa Barabara ya Mandela.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.


Meya wa Manipaa, Yusuph Mwenda (kulia) akimkabidhi shilingi 10,000 bibi kizee ambaye ni mkazi wa mtaa huo baada ya kufurahishwa na hatua yake ya kujitolea kufanya usafi wa mazingira.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi wa Kata ya Ndugumbi wakikatiza mitaa mbalimbali ya Kata hiyo wakiwa na mifagio na machepeo.
Mifereji ilizibuliwa.

JOOMLA! CMS WEBSITE DESIGN AND DEVELOPMENT TRAINING FROM 18– 22 FEBRUARY, 2013

$
0
0
The University of Dar es Salaam (UDSM), Center for Virtual Learning(CVL) is organizing a 5 days training to equip participants with the skills, knowledge and techniques for designing and developing good websites without even being experts by using Open Source Content Management System (CMS) called Joomla! CMS 2.5.8

Joomla is an award-winning CMS, which enables people to build Websites, as well as Web based applications. A summary of course outline can be found from the College website: www.coict.udsm.ac.tz


Target Audience

  • Individuals who would like to have their very own website.

  • Owner of an existing Joomla website built by another 3rd party.

  • SMEs and small businesses who wish to cut down the costs of web development projects and manage their own websites.

  • Individuals who wish to be self-employed in Website development


  • Web masters, website administrator, computer systems analysts, public relationship officers, communication officers and entrepreneurs.


Training fee:  Tsh. 500,000/= (excluding breakfast and lunch)

Venue:  UDSM Kijitonyama Campus (Former TTCL Staff College), Dar Es Salaam

Registration:Please register NOW through the College website: www.coict.udsm.ac.tz

Certificate of attendance:  will be provided upon completion of the course.

For more information contact us at saganda@udsm.ac.tz; Telephone: +255715471705

CRDB YAKOPESHA UJENZI WA KITEGA UCHUMI CHA KANISA

$
0
0
Mkuu wa Jimbo Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Anta Muro akizungumza katika hafla ya kuangalia jengo jipya la Kitega Uchumi cha Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani.
 Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa.wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi  la Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka CRDB. Benki hiyo pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa.akizungumza wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi  la Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka CRDB. Benki hiyo pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka benki hiyo. Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Alex Malalusa na Naibu Katibu Mkuu Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chadiel Sendoro. CRDB pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipokea ufunguo kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya  kukagua jengo la kitega uchumi la kanisa hilo Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka benki hiyo. CRDB pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba.
 Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo akipeana mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa.wakati wa  ziara ya kukagua jengo la kitega uchumi  la Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka CRDB. Benki hiyo pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba. 
 Mkuu wa Jimbo Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Anta Muro akiomba baraka. kwa ajili ya jengo jipya la Kitega Uchumi cha Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani.
 Askofu Malasusa akitoa baraka.
 Mandhari ya Ukumbi wa mikutano katika jengo la kitega uchumi la Msasani Multpurpose Development Centre (MMDC)
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa akikagua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usaharika wa Msasani, lililogharimu sh. bilioni 9.909 ambazo sehemu ya fedha hizo ni mkopo  kutoka benki ya CRDB. CRDB pia ni sehemu ya wapangaji katika jengo hilo lenye ghorofa saba.

Sekretarieti ya CCM yatembelea uwanja wa ndege wa kigoma

$
0
0
 


Meneja uwanja wa Kigoma Elipid Tesha,wa pili kuli akifafanua jambo kwa ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),uliofanya ziara fupi ya kuukagua uwanja huo na kujionea ujenzi wake unavyoendelea kwa kasi,kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh Issa Machibya akishuhudia tukio hilo adhimu, na shoto ni  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, pamoja na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na 
Ujenzi ukiendelea.
Mafundi ujenzi wakipaka rangi sehemu ya barabara ya kurukia na kutua ndege mapema jana jioni.

Sehemu ya eneo ambalo linaendelea kupanuliwa ikiwa ni sehemu ya ongezeko ya marekebisho ya kiwanja hicho cha Kigoma
Pichani kati Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.
 Sehemu ya kuruka na kutua ndege ikiwa katika hutua ya mwisho mwisho,Kwa mujibu wa Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo ameeleza kuwa unatarajiwa kukamilika mnamo juni mwaka huu,ambapo kwa asilimia 80 maeneo mengi yatakuwa yamekwishakamilika.

Pichani kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa   Machibya,akimtambulisha  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana kwa baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot) kuwapokea,ambapo Mh Kinana na ujumbe wake waliwasili mapema jana  jioni kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje. 
Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wakiwemo wanachama wa CCM,waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma mapema jana jioni walipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.

Pichani kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akipokea  Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ulioongozwa na  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana uliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot),kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.UJumbe huo umewasili mapema jana kutoka jijini Dar kwa njia ya Treni ( reli ya kati),ambako wamekuja kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.
Viewing all 110148 articles
Browse latest View live




Latest Images