Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

MCHUNGAJI AACHANA NA MKEWE KWA KUMTUHUMU NI MCHAWI MBEYA

$
0
0
Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Sabina Lameck mke wa mchungaji anaedaiwa kuachwa sababu ya uchawi 
Katikati mama mzazi wa mchungaji Elia Jongo wakiwa katika kikao hicho
Baadhi ya wazee wa kanisa wakiwa makini kusikiliza kisa hicho
“ Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa sababu alizichukua ili apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane na mchungaji lakini badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi anataka kuolewa yeye,” alisema Mwanamke huyo. ambaye alikuwa mke wa mchungaji Elia
Huyu ndiye muumini wa kanisa hilo anayedaiwa kutaka kuolewa na mchungaji Elia pia muumini huyu ni mzee wa kanisa hilo
Mchungaji Elia na dada yake wakiwa makini kumsikiliza mchawi wake
“ Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane alianza kunivurugia huduma ambapo waumini walianza kupungua kanisani na yeye kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema mchungaji huyo kwa hasira.
Askofu wa kanisha hilo Pasta Lugito 
 Hili ndilo kanisa la Calnel Centre mbeya lipo katibu na kiwanja cha ndege Mwanjelwa  Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea  katika kanisa hilo lililopo Airport Jijijini Mbeya baada ya Mchungaji huyo kupokea ujumbe mfupi katika simu yake ya mkononi kutoka kwa Mwanamke anayedai alikutwa mke wake ambaye waliachana miaka mine iliyopita.
Mchungaji huyo akiwa mbele ya wazee wa kanisa, Familia yake, waumini pamoja na wanahabari alisema sababu ya kuwakusanya watu hao kumetokana na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Sabina Lameck akitaka kutubu kwa mabaya aliyomtendea mumewe.
Hata hivyo baada ya mwanamke huyo kupewa nafasi ya kuanza kujieleza alianza kumtuhumu muumini wa kanisa hilo kuwa anauhusiano na mchungaji ambaye ni mumewe wa ndoa ambapo pia alidai kuwa mwanamke huyo alichukua nguo za mchungaji na mkewe kwa madai ya kupeleka kwa mganga ili kusudi awasaidie warudiane.
“ Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa sababu alizichukua ili apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane na mchungaji lakini badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi anataka kuolewa yeye,” alisema Mwanamke huyo.
Kwa upande wake mchungaji Jongo alimtuhumu mwanamke huyo kuwa ni mshirikina na kwamba sababu ya kutengana naye ni kutokana na mwanamke huyo kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa hali aliyosema alidhalilishwa kama mchungaji.
“ Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane alianza kunivurugia huduma ambapo waumini walianza kupungua kanisani na yeye kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema mchungaji huyo na kuongeza.
“ amekuja leo hapa baada ya kusikia mimi nataka kuoa muumini wangu ambapo yeye ameanza kumzushia kuwa ni mshirikiana kitu ambacho si cha kweli lakini kama kuna ukweli wowote utajulikana kwa sababu Mungu yupo,” alisisitiza Mchungaji huyo.
Hata hivyo usuluhishi huo haukufika mwafaka baada ya kuibuka kwa malumbano hali iliyomlazimu msimamizi wa usuluhisho huo Askofu wa kanisha hilo laiyejulikana kwa jina moja la Pasta Lugito kuahirsha mazungumzo hayo huku wakimpiga marufuku mwanamke huyo kukanyaga katika makazi ya mchungaji.


Jengo jipya la kuhifadhia maiti katika hosptali ya Bombo mkoani Tanga

$
0
0
 Eneo maalumu kwa ajili ya kuaga mwili katika hosptali ya mkoa wa Tanga ya Bombo.
 Eneo la mapumziko kwa wafiwa.
  jengo la kuhifadhia maiti katika hosptali ya mkoa wa Tanga ya Bombo.

Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ziarani Tanga

MV PANGANI II kiunganishi muhimu kati ya mkoa wa Tanga na Hifadhi ya Saadani.

$
0
0
 Kivuko cha Mv Pangani II ni kiunganishi kikubwa kati ya mkoa wa Tanga na hifadhi ya Saadani kwa watalii wanao toka Tanga. Ila vidumu si kwenye Landrover tuu hata huku pia .
 Tunajazia kidogo .

 Watumiaji wa kivuko wakishuka katika chombo hicho Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Pangani.

UNATAKA KUPATA KITABU CHA ERIC SHIGONGO BURE?

$
0
0
BAADA YA KUSUBIRIWA KWA HAMU, HATIMAYE KILE KITABU 'Kifo ni Haki Yangu' CHA MTUNZI MAHIRI WA RIWAYA NCHINI TANZANIA, Eric James Shigongo, sasa kiko tayari kuanza kuuzwa karibu yako. Mtunzi huyo ameandaa zawadi ya VALENTINE kwako wewe msomaji wa mtandao huu, hivyo utajipatia kitabu hiki BURE, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wewe ni mwanachama au umeshajisajili katika mtandao wa www.globalpublishers.info, kama bado fanya hivyo kuanzia leo kisha usubiri utaratibu wa kujipatia kitabu hiki na vingine BUREEE...Stay Tuned!

ZAIDI ya wanyama 200 hugongwa na magari katika hifadhi ya taifa ya Mikumi kila mwaka

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii aliyeko Mikumi Morogoro. 
 ZAIDI ya wanyama 200 wa aina tofauti 12, katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi,kila mwaka hufa kwa kugongwa na magari katika barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Zambia inayopita katikati ya hifadhi hiyo kwa kipande cha kilometa 50. 

Na kutokana na magari kupita hifadhini bila kulipia na kusababisha mauaji ya wanyama, serikali imekuwa ikipoteza mapato ya zaidi ya Sh billion 6 kwa mwaka, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Damiani Saru amesema.

Akiongea na waandishi wa habari 10 wa mkoa wa Kilimanjaro, walio kwenye ziara za kutembelea hifadhi za taifa Bw Saru alisema kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi hiyo kina urefu wa kilomita 50, ambapo kuna mabango mbalimbali yakiwataka madereva kwenda kwa mwendo mdogo lakini bado wameendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi unaoathiri  wanyama hao. 

 Alisema kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita wanyama zaidi ya wanyama 40 walikufa na baadhi ya magari yalikamatwa na kutozwa faini kulingana na aina ya mnyama. 

 “Faini inayotozwa si suluisho kwani si mara zote wanagogwa wakati askari wa wanyamapori wakiwepo mara nyingine inatokea wakati hawapo na wahusika kukimbia na kubaki kuokota mizoga…tumefanya utafiki kwa mwaka tungekusanya Sh billion 6 iwapo magari yote yanayopita yangelipa” alisema.

Aliainisha wanyama wanaogongwa mara kwa mara kuwa ni swala pala ambao huruka kwa wastani wa 15 hadi 20, samba, chui, twiga, tembo, nyani, nguruwe na digidigi na zaidi hutokea nyakati za usiku. 

Bw Saru aliongeza kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), limewasilisha andiko kwa serikali kuelea umuhimu wa kuondolewa kwa barabara hiyo na inavyoendelea kuwepo ina athari gani kwa mustakabali wa wanyama na wanaednelea kusubiri majibu. 

 Mhifadhi huyo alisema awali waliweka kizuia kwa magari mwanzo na mwisho wa hifadhi na kila gari kutakiwa kulipia, ili kuepusha utalii wa bure, ujangili na kugonga wanyama, lakini Walaka wa Barabara nchini (Tanroads) walipinga suala hilo kwa kuna barabara ni mali yao. “Ifike mahali tiuone wanyama wanakwishwa, kulea mnyama mmoja hadi akifie umri flani inacchukua muda mrefu, wakiendelea kuteketezwa kwa kugongwa na ujagili hifadhini ni wazi kuwa watakwisha” alisema Saru. 

 Naye, Mhifadhi Utalii, Tutindaga Mdoe, alisema uwepo wa barabara hiyo umeruhusu utalii wa bure, ambapo wageni ambao walitaka kutembelea hifadhi huacha kwa kuwa wanaweza kupita barabarani na kupiga picha. Hata hivyo, alisema hifadhi imechukua hatua na kuwakamata wanaofanya hivyo, lakini kwa wanaosafiri kwa mabasi wamekuwa wakijionea wanyama bure jambo ambalo linapunguza idadi ya watalii wa nje na ndani.



RAIS KABILA ATUA DAR MCHANA HUU KWA ZIARA YA SIKU MOJA

$
0
0
 Ndege iliyomchukua Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013. Kiongozi huyo amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

 Matarumbeta ya Mzee Hozza ndani
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

KINANA ATINGA WILAYANI KAKONKO MKOANI KIGOMA, APOKEWA NA DIWANI WA CHADEMA KATA YA KASANDA

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwalisha kiapo cha utii Wanachama wapya 45 wa CCM mara baada ya kuwapa kadi za chama hicho kwenye mkutano uliofanyika Kata ya Kasanda, Kakonko mkoani Kigoma

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya, Elizabeth Gwimo, alipokwa wanachama wapya 45, katika mkutano uliofanyika Kata ya Kasanda, Kakonko Kigoma.

Wanachi wakishangilia jambo kwa pamoja
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika Kata ya Kasanda, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na mabalozi wa mashina na wazee katika Kata ya Kasanda, Kakonko mkoa wa Kigoma.

Diwani wa kata ya Kasanda, Kakonko mkoani Kigoma, Dickson Barutwa (CHADEMA), akimpa maelezo ,Ndugu Kinana kuhusu ujenzi wa nyumba za zahanati ya kata hiyo unaofanywa na serikali.


zahanati ya kata ya Kasanda iliyojengwa na Serikali,picha zaidi bofya Michuzijr.blogspot.com.

Dkt MIGIRO MKUU WA CHUO KIKUU HURIA, NYAMBACHA AWA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 

 Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.
Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.

Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU

DAR ES SALAAM


30 Januari, 2013


death and funeral announcement

$
0
0

The late Moses Tito Kachima

It is with sorrow the family of Moses Tito Kachima announces the death of their loved one Mr. Moses Tito Kachima which occured on the 29th January 2013 at Mama Ngoma Hospital, Mwenge Dar es Salaam.
Family, relatives and friends are gathering at the deceased residence at Lugalo Street plot no. 314 Upanga for funeral and burial arrangements.
There will be a mass at the St. Immaculate Church on United Nations road, Upanga on Friday 1st February 2013, thereafter the body will be laid to rest at the Kinondoni Cemetery at 1600 hrs.
         "Blessed are the pure in heart for they shall see the Lord"

News alert:MOTO WATEKETEZA KIWANDA CHA CHEMI COTEX DAR

$
0
0

Moto mkubwa umezuka na unakiunguza kiwanda cha vipodozi cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha moto huo hakijafahamika ingawaje inahisiwa kuwa huenda ni hitilafu iliyotokana na fundi aliyekuwa akichomelea kitu ndani ya kiwanda hicho.

Wahusika wakuu wa kiwanda hicho hawakuwa katika eneo husika ili kutoa maelezo zaidi. Taarifa zinasema kuwa magari ya kikosi cha zima-moto yalipowasili, watu walianza kuyarushia mawe kiasi cha kutishia usalama wa watu wengine ambao waliamua kuondoka kutoka katika eneo la tukio.

Jitihada  za  kumtafuta kamanda  wa  polisi  wa  kanda maalum ya Dar es Salaam Suelein Kova  bado zinaendelea baada ya simu yake  kuita bila  kupokelewa 

WAZIRI MKUU: MTWARA CORRIDOR KUPEWA UZITO WA PEKEE

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali italipa uzito wa kipekee suala la uendelezaji wa Ukanda wa Kiuchumi wa Mtwara (Mtwara Corridor) kama ilivyo kwa Ukanda wa Kilimo wa Nyanda za Juu Kusini Tanzania (SAGCOT).

 
Amesema Serikali itachukua hatua hiyo ili kuiendeleza kiuchumi mikoa ya kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma.
 
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Januari 30, 2013) mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ili kutoa ufafanuzi juu ya suala alilokwenda kufuatilia mkoani Mtwara kufuatia vurugu zilizozuka hivi karibuni kuhusiana na suala la uchimbaji gesi mkoani humo.
 
Mbali na hilo, Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha Wizara ambazo zinawajibika kutoa maelezo kuhusu uwekezaji na uendelezwaji wa miradi mkoani Mtwara zinaweka ratiba maalum ya kwenda huko na kutoa maelezo ya kina kwa wananchi.
 
Alitumi fursa hiyo kuwasihi wakazi wa mkoa huo kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinaimarishwa kama kweli wanataka mkoa huo uendelezwe.
 
“Ninawasihi wakazi wa Mtwara waimarishe amani na utulivu sababu fursa walizonazo ni kubwa sana. Ni vizuri viongozi na wananchi wa mkoa huo wakajipanga vizuri ili waangalie namna watakavyonufaika na uwekezaji huo,” alisema.
 
Akifafanua kuhusu mgogoro uliosababisha vurugu hizo, Waziri alisema katika muda wa siku mbili alizokuwa Mtwara aliweza kukutana na vikundi tisa vilivyojumuisha viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, madiwani, wafanyabiashara na vyombo vya dola.
 
Alisema baada ya kusikiliza pande zote, Waziri Mkuu aliwaita mawaziri wa Elimu, Uchukuzi, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Viwanda na Biashara na Kaimu Mkurugenzi wa TIC ili watoe ufafanuzi kwenye kikao cha majumuisho ambacho kilifanyika jana (Jumanne, Januari 29, 2013) mjini Mtwara.
 
“Ni bahati mbaya hali ilikuwa hivyo. Ni jambo ambalo lisingetakiwa kufika hapo. Ni bahati mbaya kwamba elimu kuhusu uwekezaji mkoani Mtwara haikuwa imefika kwa wananchi walio wengi, ni wananchi wachache waliofikiwa wakati wa kutoa taarifa. Wabunge walijua jambo hili na walikuwa na wajibu wa kuwaelimisha wananchi…,” alisema.
 
Waziri Mkuu alisema hoja kuu iliyotolewa na wakazi hao ni kwamba walikuwa hawapingi gesi kwenda Dar es Salaam isipokuwa walikuwa wakitaka kijengwe kiwanda cha kusafisha gesi pale Mtwara ili mabaki yanayotokana na usafishaji huo yatumike palepale mkoani kutengenezea bidhaa nyingine kama vile mbolea na vifaa vya plastiki.
 
Akielezea kuhusu hasara zilizosababishwa na vurugu hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alisema nyumba, ofisi na magari vilichomwa moto katika sakata hilo lililohusisha wilaya za Mtwara na Masasi Januari 25 na 26 mwaka huu.
 
Alibainisha kwamba kwa wilaya ya Masasi pekee gharama za kurekebisha uharibifu huo zinafikia sh. bilioni 1.5/-. Hata hivyo, alisema gharama halisi za uharibifu uliotokea kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara pamoja na Manispaa ya Mtwara hazikuweza kupatikana kwa haraka.
 

Joett - Color Me Beautiful Video TEASER

Dkt. Migiro afanya ziara wilaya mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

$
0
0
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.

kinana akagua miradi ya maendeleo ikiwemo soko la kimataifa la pamoja na ujenzi wa daraja mpakani mwa tanzania na burundi, kibondo mkoani kigoma leo .

$
0
0
 

Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma  Magango (shoto) na baadhi ya Wanachi wakielekea kukagua  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.




Wakielekea kukagua ujenzi wa mradi wa darja la pamoja.
Pichani ni  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.

Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika februari 20,2013 utagharimu kiasi cha shilingi 260,000,000/=,aidha imeelezwa kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu nne,awamu ya kwanza imeshaanza ambayo unahusisha ujenzi wa daraja,barabara KM1 inayotoka kwenye soko hadi darajani na hifadhi ya Mazingira,utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia 70% mpaka sasa.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai alipokwenda kukagua mradi  wa ujenzi wa  daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai akitoa ufafanuzi mbele ya Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana kuhusiana na ujenzi wa Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.


Jengo la Soko la Pamoja lililokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo jioni,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.Picha na habari zaidi bofya JIACHIE BLOG.

UNIC YASHIRIKISHA VIJANA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WAHANGA WA MAUAJI YA KIMBARI YA HOLOCAUST.

$
0
0
Afisa Habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkoma akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka wahanga wa Mauaji ya Kimbari ya Holocaust kwa vijana wanafunzi wa shule za sekondari na baadhi ya vyuo.
Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuwakumbuke watu wote wasio na hatia ambao walipoteza maisha wakati mauaji ya kimbari ya Holocaust.
Ameongeza kuwa vilevile tuhamasishe na wale ambao walikuwa na ujasiri wa kujali watu wa kawaida ambao walichukua hatua zisizo za kawaida kulinda heshima ya binadamu. Mfano wao unaweza kutusaidia sisi kujenga dunia bora zaidi leo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uokoaji wakati wa Mauaji ya Kimbari: Ujasiri wa Kujali”.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkoma (hayupo pichani) alipokuwa akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka wahanga wa Mauaji ya Kimbari ya Holocaust iliyofanyika jijini Dar leo katika ukumbi wa British Council.
Wanafunzi wa shule za Sekondari, vyuo na wafanyakazi wa UN wakifuatilia Filamu 'The Rescuers' inayosimulia kwa undani kuhusiana na stori zinazowahusu wanadiplomasia 13 waliofanya vitendo vya kishujaa na kijasiri ambao waliowaokoa maelfu ya Wayahudi wakati wa vita vya pili vya Dunia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji wa filamu maarufu na mshindi wa tuzo EMMY Michael King.
Mjumbe wa Chama cha Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bernadetha Mshana akisoma shairi lenye ujumbe wa kupiga vita mauaji na kuhamasisha vijana kudumisha amani.
Burudani ya ngoma za asili.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akiendesha mjadala na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari kutoka katika vilabu vya UN kuhusiana na siku ya kimataifa ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya Holocaust baada ya kutazama filamu iliyokuwa ikielezea mauaji hayo inayoitwa “ The Rescuers” iliyotengenezwa na mtengenezaji filamu maarufu Michael King.
Dakika moja ya ukimya: kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Holocaust.
Baadhi ya vijana wa UN Clubs wakimsikiliza kwa makini Bi. Stella Vuzo.
Pichani Juu na Chini Wanafunzi wakitoa maoni yao baada ya kutazama filamu hiyo wakati wa Mjadala ulioendesha na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi Stella Vuzo (hayupo pichani).
Bi. Usia Nkoma akitoa neno la shukrani kwa washiriki.


Ndizi za Buhegwa Mkoani Kigoma

$
0
0
Kina Mama wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwi,Mkoani Kigoma wakionekana wakifanya biashara ya Ndizi katika soko kuu la Kijiji hicho.Eneo hili ni maarufu sana kwa kilimo cha Ndizi.

Kibonzo cha Kijasti Bikozi leo

LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE

Article 7

AWAMU YA PILI MRADI WA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA.

$
0
0

AWAMU ya pili ya mradi wa Mazingira Bora kwa Elimu Bora, kwa kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam inatarajiwa kuzinduliwa hapo kesho ambapo wadau mbalimbali wakiwemo Watu wa Marekani wamealikwa kushiriki kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo diwani wa kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, alisema lengo la mradi huo ni kuboresha Mazingira ya elimu ya Msingi na Sekondari kwenye kata yake.

Aidha Kaluwa alifafanua kuwa Uboreshaji huo wa mazingira ya Elimu unafanyika kwenye Shule saba za Msingi na Sekondary za kata hiyo kwa kuwapatia madawati, maji safi na salama, kujenga vyoo na madarasa pamoja na kuwapatia wanafunzi na walimu vifaa vya elimu.

Awamu ya kwanza ya Mradi huo ilizinduliwa Machi 17,2012 ambapo kwenye awamu hiyo kulifanyika kampeni za kuhamasisha wadau kuchangisha pesa na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh.155.5Million, ambazo zilitumika kwa kununua madawati 500 ya Shule ya Msingi, 480 Shule za Sekondari na viti 100 vya shule ya awali pamoja na kufanikiwa kuchimba kisima cha maji katika kila shule.
Awamu hii ya pili ya mradi itajihusisha zaidi kwenye ujenzi wa vyoo na madarasa.
Diwani wa Kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam Bonna Kaluwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuanza kwa awamu ya pili ya mradi wa Mazingira bora kwa elimu bora itakayozinduliwa rasmi hapo kesho kwenye kata hiyo, kulia ni Mtendaji wa serikali ya mtaa wa Kipawa Said Fundi.


Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images