Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUSITISHWA KWA HUDUMA ZA USAFIRI WA RELI UKANDA WA KASKAZINI (TANGA & KILIMANJARO) KUANZIA LEO


RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuaga baada ya kuongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine na wadau akikata utepe kuashiria kupokewa kwa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakisiliza maelezo toka kwa Kepteni Dennis Mshana mmoja wa Marubani walioileta ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Seattle Marekani hadi katika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na marubani na wanaanga waliokuja na ndege wakati alipoongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini alipoongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wa Taasisi Mbalimbali za Umma na Binafsi alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mzee Omary Mkali, mmoja wa wazee waliofika katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kiti cha rubani Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kepteni saidi Hamadi mmoja wa Marubani walioleta ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner kuoka Seattle Marekani alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuipokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo kwenye viti vya marubani wa Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019 PICHA NA IKULU

PSPTB yatoa mafunzo wa Wafanyakazi wa VETA Makao Makuu

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanayakazi wa VETA Makao mkuu mara baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyofanyika siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akizungumza jambo wakati wa kufunga  mafunzo ya wafanyakazi wa VETA ya kuwajengea uelewa wa pamoja kati ya wadau wa ndani(Idara tumizi, kamati za tathimini ya Bodi ya Zabunu) kuhusu utaratibu wa kuzingatia katika kutekeleza miradi na shughuli mbalimbali kwa ufanisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu akziungumza wakati wa kufunga mafunzo ya wafanyakazi wa VETA yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) pamoja na VETA Makao Makuu yaliyofanyika katika ukumbi wa VETA Makao Mkuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam leo.

Mshauri wa masuala ya Ununuzi na ugavi, Hamis Mpinda akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa VETA yaliyokuwa yanahusu sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akichangia mada wakati wa mafunzo ya ya wafanyakazi wa VETA ili  kutatua changamoto zilizopo ili kuongeza tija na kupata thamani ya fedha katika ununuzi wa bidhaa, huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Baadhi ya Wafanyakazi wa VETA Makao makuu wakichangia mada wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na PSPTB pamoja na VETA Makao yalikuwa yanahusu sheria ya Ununuzi wa Umma oamoja na kanuni zake yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa VETA Makao makuu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na PSPTB pamoja na VETA Makao yalikuwa yanahusu sheria ya Ununuzi wa Umma oamoja na kanuni zake yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26, 2019 katika ukumbi wa ofisi za VETA Makao Makuu, Chang`ombe jijini Dar es Salaam.

Serikali kukarabati miundombinu ya Barabra iliyoathiriwa na Mvua mkoani Tanga.

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Serikali imesema kuwa Wananchi wawe wanachukua tahadhari katika kipindi cha mvua wakati wanatumia vyombo vya usafiri.

Hayo ameyasema Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi  Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe  wakati akizungumza na waandishi habari leo kuhusiana kukatika kwa mawasiliano katika Barabara mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Tanga.

Amesema kufuatia kwa mvua hizo wamesitisha safari za train ya mizigo kwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro.

Kamwelwe amesema kuwa mvua zilizonyesha kwa Mkoa wa Tanga ,miundombinu ya Barabara imekuwa na changamoto na kufanya serikali na vyombo vyake kuweka kambi.

Aidha amesema kuwa mvua zikiisha tu watajenga kwa haraka kwani fedha zipo za kufanya ujenzi huo.

Amesema Tanga imeaathiriwa sana katika miundombinu ya Barabara   na hizipitiki katika Wilaya za Handeni,Korogwe,Pangani,Mheza Pamoja na Lushoto.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua iliyochukua kufuatia na Mvua ilyoharibu miundombinu ya Barabara katika Mkoa wa Tanga leo jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar( ZAPEA ) safarini Oman

$
0
0

Na Khadija Khamis –Maelezo    Zanzibar              
Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar( ZAPEA ) umeishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia fursa ya kushiriki mkutano wa kimataifa nchini  Oman kwa lengo la kukuza ajira nchini .
Hayo yameelezwa na Kiongozi wa Msafara Amani Khamis Fakih (pichani juu) huko Uwanja wa Ndege wai Abeid Amani Karume wakati wakiondoka  kuelekea nchini Omani .
Amesema wataitumia vyema  fursa walioipata kwani wataweza kuondoa  changamoto wanazokumbana nazo  katika kazi zao kwa  vijana wanapokuwa nchini huko. 
Alieleza kuwa changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya vijana wanaokwenda kufanyakazi huko nchini Oman ni pamoja na kutofuata utaratibu wa ajira jambo ambalo husababisha migogoro na usumbufu wafanyakazi na waajiri wao.
Aidha alifahamisha kuwa Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar unapeleka wafanyakazi mbalimbali katika Serikali ya Oman kwa kuzingatia Sifa, Mkataba Sheria na vigezo ambavyo vinakubalika kisheria.
“Vijana  wanaopelekwa na Umoja wetu katika nchi tofauti kwa masuala mazima ya ajira tunahakikisha tunazingatia vingezo muhimu vinavyohitajika na kutiliana saini Mkataba na Kampuni  husika pamoja na kushirikiana na Serikali ya Zanzibar na Ubalozi”Alisema Amani 
Nae Bi Khadija Said amewataka vijana kutokata tamaa katika kutafuta ajira nje ya nchi kwani serikali inafursa nyingi kupitia kwa wawekezaji.
Mkutano huo wa Kimataifa ni wa Siku tatu unafanyika nchini Oman ambao  umetayarishwa kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Oman na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mwana FA anogesha Tamasha la 38 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kwa bonge moja la show

$
0
0

Msanii wa kizazi kipya Khamisi Mwijuma ‘Mwana FA’ amepiga shoo moja matata ndani ya Tamasha la 38 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.
Katika onesho hilo, ukumbi huo wa TaSUBa ulifurika watu mbalimbali wadau wa burudani waliokuwa na hamu ya kumshuhudia msanii huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo ya ‘We endelea tu’.
Akiwa jukwaani pia alitumia wasaa huo kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele za haki akiwemo marehemu Mangwea na kumuelezea kuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa na uwezo mkubwa sana na kumuenzi kwa kupiga wimbo wake wa "Mikasi".
Aidha, Mwanafa aliimba nyimbo zake kama "Asante kwa kuja", "Ya Laiti" na "Unanisikia".
Mwana FA aliwashukuru wadau hao kwa kupokea sanaa yake na kisha kuwaomba kuwaombea wasanii waliotangulia mbele za haki akiwemo Sharo milionea, Complex, King Majuto na wengine wengi.


IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO OKTOBA 27,2019

MWAKYEMBE AWATAKA WASANII KUEPUKA MIKATABA FEKI

$
0
0
     Na.Khadija seif, Michuzi TV

WAZIRI wa habarii, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini  Dk Harrison Mwakyembe amezindua rasmi awamu ya pili ya kamati ya kusimamia haki za wasanii.

Aidha, Mwakyembe amefafanua zaidi kuwa kamati hiyo ipo kwa ajili ya kusaidia wasanii na katika awamu ya Kwanza ya kamati hiyo imeweza kusaidia wasanii wenye malalamiko kwa kiasi kikubwa na kufanikisha kupata haki zao.

" Mama Kanumba,Marehemu mzee majuto Ni miongoni mwa watu ambao tuliweza kutatua matatizo yao ambapo baadhi ya makampuni yalikua yakilegalega kufanya malipo kwao,"

Pia amewataja wasanii kama Ay na Mwana Fa kuwa Ni miongoni mwa wasanii ambao kamati ilisaidia  wapate haki zao na kutokana na uvumilivu wao waliweza kupata jasho lao.

Hata hivyo Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii ambao wanaingia mikataba bila kuweka wakili au wanasheria kuacha mara moja kwani wanajidhurumu jasho lao na kupelekea kudhurumiwa wao wenye.

"Wapo vijana 10 ambao walifanyishwa kazi na mtu asiejulikana na kukimbilia nchini kwao lakini tutafanya juu chini kuhakikisha tunamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwani tunaamini wasanii wanapigana usiku na mchana kutafuta riziki na kuendesha maisha yao Kama kazi zingine,"

Kwa upande wake Mwanasheria katika kamati hiyo Dora  Mwenegoha amebainisha changamoto walizokumbana nazo wakati wa kutatua matatizo kwa awamu ya kwanza.

"Baadhi ya makampuni yalikua hayatoi  ushirikiano wakutosha katika kusuluhisho migorogoro na wasanii walioingia nao mikataba,"

Aidha, Mwenegoha amewapongeza makampuni Kama startimes kwa kutii agizo la Waziri Mwakyembe kwa kuwalipa stahiki zao wasanii ambao walikua wakidai haki  zao na kutaka makampuni mengine kutekeleza Jambo mara moja .
 Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akizindua Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi. Sarah Nsangizyo Zilahulula na kushoto ni mjumbe Dkt. Dorah Mwenegoha
   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini wakimsikiliza Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati waziri alipokuwa akizindua kamati hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mara baada ya kuizindua mapema hii leo jijini Dar es Salaam



RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 30 MWAKA “C” KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mkate wa Ekaristi alipoungana na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki kushiriki Misa Takatifu Dominika ya 30 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Oktoba 27,2019.
 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 30 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Oktoba 27,2019.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 30 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Oktoba 27,2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Waumini wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph baada ya Misa Takatifu Dominika ya 30 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Oktoba 27,2019. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi pamoja na Mzee wa Kanisa Dkt. Adelhelm Meru baada ya Misa Takatifu Dominika ya 30 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Oktoba 27,2019.


PICHA NA IKULU

Benki ya DCB yadhamini Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania

$
0
0
 Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jaffo, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Godfrey Mweli.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa, Joseph Kandege (kulia), akishiakana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa baara ya kupokea cheti cha shukurani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, kutoka na udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania  kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki. 
 Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akimfahamisha Angel Lomwai kuhusu faida ya akaunti maalumu ya mpango wa elimu ya ‘DCB Skonga’ iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki. 
 Ofisa Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Dalila Issa (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu  akaunti maalumu ya masuala ya elimu ya DCB Skonga iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania  kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.

 Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini. 
 Baadhi ya wahudhuriaji katika  hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini wakifuatilia matukio mbalimbali ya utoaji tuzo hizo.

WAJUMBE KAMATI YA UONGOZI CWP KANDA YA AFRIKA WAKUTANA JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani, Mhe. Shandana Gulzar Khan akielezea jambo katika kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo katika hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Wabunge wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Saidi Yakubu akizungumza na Wajumbe wa kamati ya uongozi wakati wa kikao kilichofanyika leo katika hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani, Mhe. Shandana Gulzar Khan na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Zainab Gimba
 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region), Mhe. Zainab Gimba akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo katika hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani, Mhe. Shandana Gulzar Khan

NAIBU WAZIRI MABULA AAGIZA KUPITIWA VIWANJA VINAVYODAIWA KUMILIKIWA NA JIJI LA TANGA

$
0
0
 Na Munir Shemweta, WANMM TANGA
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji kupitia viwanja vyote vinavyodaiwa ni mali ya jiji hilo lakini vinamilikiwa na watu wengine.
 Hata hivyo, wakati Dkt Mabula akitoa agizo hilo eneo maarufu la ufukwe katika jiji la Tanga la Bathing Club lililopo Raskazone Tanga limerejeshwa kwa halmashauri ya jiji la Tanga baada ya mmili wake kulitumia kwa muda mrefu.
Eneo hilo la ufukwe ambalo wananchi walikuwa wakienda kwa kulipia limeelezwa kuwa ni moja ya maeneo ambayo nyaraka zake zilikuwa zikioonesha linamilikiwa na Jiji la Tanga lakini lilikuwa chini ya watu wengine.
 Dkt Mabula aliagiza kupitiwa kiwanja kimoja baada ya kingine na kuwataka wamiliki wake kwenda na nyaraka zinazoonesha umiliki wa maeneo yao kama ni halali na kama ni halali walipataje maana bado yanasomeka kama mali ya jiji la Tanga.
 ‘’ Ikibainika kuwa wamiliki wake wanamiliki isivyo halali maeneo hayo basi mali hizo zote lazima zirudi serikalini maana kumbukumbu zinaonesha maeneo hayo bado ni mali ya jiji la Tanga’’ alisema Dkt Mabula.

Akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shighela wakati wa kutembelea baadhi ya maeneo hayo, Dkt Mabula aliitaka Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenda mtaa kwa mtaa, kuyatambua maeneo husika na kupata nyaraka zinazoonesha umiliki wa maeneo hayo kama ni halali na kama ni halali ifahamu yalipatikanaje wakati hadi sasa kumbukumbu zinaonesha ni mali ya jiji la Tanga.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, agizo hilo ni kwa halmashauri zote hasa katika yale maeneo yaliyotaifishwa na serikali na kuwa mali ya umma lakini bado yanaendelea kumilikiwa na watu wengine huku wengine waliouziwa maeneo wakishindwa kukamilisha malipo yao.

‘’ Kuna baadhi ya maeneo serikali iliwarudishia  wenyewe na mengine serikali ilipangisha kama rasilimali zake lakini bado maeneo hayo yanamilikiwa na watu wengine.’’ alisema Naibu Waziri.

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji alimueleza Naibu Waziri kuwa katika jiji lake kuna maeneo yanaoyoonesha kuwa yanamilikiwa na jiji lakini maeneo hayo bado yanamilikiwa na watu wengine na jiji lake lilifanikiwa kurejeshewa eneo la Bathing Club lililopo Raskazone. Aidha Mayeji alisema jiji lake linakabiliwa na chanagamoto ya baadhi ya maeneo yake kumilikiwa na taasisi za serikali ambazo zimeshindwa kulipa fidia maeneo iliyotwaa kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe alitaka kuwekwa kwa gharama halisi za upimaji kwa kuwa hivi sasa kumekuwa na tofauti kubwa ya gharama za upimaji jambo linalowafanya wanapotoa maagizo ya upimaji na kutaka kutolewa muongozo wa gharama za upimaji, upangaji kwa nchi nzima ili kuondoa sintofahamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Gracian Makota ameomba kupatiwa Afisa Ardhi Mteule kwa kuwa anayewahudumia sasa kutoka Korogwe wakati mwingine anashindwa kufanya hivyo kutokana na changamoto au geographia ya wilaya ya Kilindi hasa pale inapotokea miundombinu kuharibika.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewajia juu watunza kumbukumbu wa Masijala ya Ardhi katika halmashauri za Jiji la Tanga na ile wilaya ya Pangani mkoani Tanga kwa kushindwa kuzingatia taratibu za utunzaji majalada ya ardhi jambo alilolieleza kuwa linasababisha migogoro ya ardhi.

Akiwa katika ziara yake mkoani Tanga, Dkt Mabula alibaini utunzaji wa kumbukumbu za Majalada ya ardhi usiozingatia taratibu za utunzaji na kuagiza ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini kuhaskikisha inatoa mafunzo kwa watunza kumbukumbu za Majalada ya ardhi kwa halmashauri zote za mkoa mzima wa Tanga ili waweze kutunza kumbukumbu vizuri.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya Majalada ya Ardhi katika Ofisi za ardhi za jiji la Tanga mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Tanga. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Strawton Thobias.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya Jiji la Tanga Strawton Thobias mwishoni mwa wiki alipowasili katika jiji hilo wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Tanga.

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya eneo lenye mgogoro lililopo Mtaa wa Independence katikati ya jiji la Tanga wakati wa kutembelea maeneo yenye mgogoro wa ardhi katika jiji hilo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shighela na kushoto ni mtoto wa mmiliki wa eneo hilo Paul Charles. 
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na uongozi na watendaji wa sekta ya ardhi wilaya ya Pangani mkoani Tanga mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Tanga. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Issa.

BARABARA YA KIVULE YAANZA KUJENGWA BAADA YA RC MAKONDA KUWASWEKA LUPANGO WAKANDARASI

$
0
0
Katapila likisawazisha vifusi vilivyomwagwa wakati wa ujenzi wa barabara hiyo katika kona ya Kitunda kwenda Kivule. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA


Daraja lililopo katika barabara hiyo ambalo ni takribani mwaka sasa ujenzi wake haujakamilishwa


Katapila la Kampuni ya Nyanza likiwa kazini katika daraja hilo


Kifusi kimwagwa tayari kwa ujenzi wa barabara hiyo
Kizuizi cha muda kilichichowekwa kurahisisha ujenzi

Na Richard Mwaikenda,Ukonga.

HATIMAYE Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza imeanza ujenzi wa Barabara ya Kitunda-Kivule, Ukonga Dar es Salaam, baada Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutoa amri ya kuwasweka lupango viongozi wa kampuni hiyo.

Makonda alitoa amri hiyo Dar es Salaam Alhamisi, baada ya kampuni hiyo iliyopewa zabuni ya kuchelewa kuanza ujenzi licha ya kulipwa malipo ya awali ya sh. bil. 4.8. Mkataba wa ujenzi umeanza Oktoba Mosi.

Akizungumza na vyombo vya habari, RC Makonda alisema kuwa wakandarasi hao, watakuwa akienda kujenga barabara hiyo wakitokea mahabusu.

Pilikapilika za ujenzi zimeanza ijumaa katika eneo la Kitunda, ambapo yalionekana makatapila yakikwangua sehemu ya barabara hiyo, huku mengine yakisawazisha vifusi vilivyokuwa vinamwagwa na malori.

Kampuni hiyo itajenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara chenye urefu wa km 3.2 kuanzia Kituo cha Polisi Kitunda hadi Mwembeni.

Ubovu wa barabara hiyo ya kutoka Banana, Kitunda hadi Kivule Fremu Kumi, imekuwa ni kero na kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo. Ujenzi wa kipande hicho cha barabara unatarajiwa kukamilika Oktoba mwakani.

Kila msimu wa mvua kama huu barabara hiyo uharibika na kuwa na mshimo yanayosababisha daladala nyingi kusita kwenda huko, hali ambayo inawafanya abiria kulipa kiasi kikubwa cha nauli hadi sh.3000 kutoka Banana hadi Flemu Kumi kwa kutumia usafiri wa Bajaji na Bodaboda.

Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwaonea huruma kwa kuhakikisha ujenzi wa kipande hicho kukamilika haraka kabla ya mvua za masika, lakini pia kumalizia kipande kingine cha barabara kutoka Mwmbeni hadi Flemu kumi.

SWAHILI SOCIETY USA FEST. 2019

TAARIFA MUHIMU KUHUSU PASSPORT KWA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI

$
0
0

Image result for PASSPORT MPYA ZA TANZANIAUnataarifiwa kwa wale wote ambao Pasi za kusafiria zimeisha muda wake mnaombwa kuzibadilisha na kupata pasi mpya.

INASHAURIWA
 Usisubiri dharula itokee badilisha Passport yako sasa, hata kama ni hati ya dharula ya kusafiria huchukua siku 3 mpaka 4 kua tayari.

Kila kitu kinafanyika matandaoni, kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico www.tanzaniaembassy-us.org . Fomu za passport na za hati ya dharura zinajazwa kupitia www.immigration.go.tz sehemu ya e-services.Fomu ya maombi iliyokamilika na nyaraka zote ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa ama affidavit, cheti cha kuzaliwa ama affidavit ya mzazi mmoja wapo, nakala ya passport na nakala ya kitambulisho vinapokelewa ubalozini kupitia barua pepe  ubalozi@tanzaniaembassy-us.org. Tafadhali pitia viambatisho vya maelekezo kwa uelewa zaidi hapo chini.

Kwa taarifa zaidi na maelekezo USISITE wasiliana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington, DC simu 202 884-1080 ASANTE.

HATUA ZA UOMBAJ][ E-PA88PORT

' Kabla ya kujaza Fomu Mwombaji ahakikishe amefanya scanning ya picha yake Ipassport size) na
viambatisho vyote (Cheti cha kuzaliwa, naKala ya passport, cheti cha kuzaliwa cha Baba au Mama na
kitambulisho). Viambatisho hivyo viwe kwenye
mfumo wa picha (image- jpegJng) na kila kiambatishi Ki nzidi ukubwa wa IMB. Viambatisho
hivyo atatakiwa kum'upload wakati anajazafomu

' Awe na Kadi yake ya bank ambayo atatumia
Kufanya malipo wakati wa kujazafomu hiyo

' Kwa Waombajl‘: walio miji ya mbali lazima watume
bahasha ama Walipie Ubalozini gharama za
kutumiwa passport zao zikifi!ka

1. Mwombaji ajaze fomu online kupitia www.imm ation. o.tz Ce-services) ataona sehemu ya passport application form

2. Aprint fomu yake na kuituma kwa mail, email (ubalozi tanzaniae ass -us.or ) ama kwa kuiwasilisha Ubalozini

3. Ikishapokelewa na kuthibitishwa kwenye mfumo atatumiwa bill ya malipo katika email address aliyojaza kwenye fomu

4. Bill hiyo ya malipo itamwonyesha link ya kufanya malipo kwa njia ya mtandao

5. Kwenye link hiyo ataweka control number na kiasi cha malipo kama Bill inavyoonyesha

6. Akikamilisha malipo atume risiti yaks Ubalozini ili malipo yahakikiwe na kupangiwa miadi ya kuja kwa ajili picha na kuchukuliwa alama za vidole

7. Wakati anakuja Ubalozini ahakikishe anakuja na nakala halisi za viamhatisho vyake na atapatiwa risiti yaks ya malipo

8. Passport ikipokelewa kutoka Uhamiaji Mhusika atatumiwa kwa njia ya mail ama kwa kuchukua mwenyewe Ubalozini.

HATUA ZA UOMBAJX ETD

1. Mwomhaji ajaze fomu online kupitia www.imm ation. o.tz (e-services)

2. Aprint fomu yake na kuituma kwa mail ama kwa kuiwasilisha Uhalozini

3. Xkishapokelewa na kuingizwa na kuthihitishwa atatumiwa hill ya malipo kwa email

4. Risiti ya malipo itamwonyesha link ya kufanya malipo kwa njia ya mtandao

S. Malipo Fake yakikamilika na kupokelewa ETD itatolewa

6. ETD husika atatumiwa kwa njia ya mail ama kwa kuchukua mwenyewe.

NOTE:

* Kwa Waombaji walio miji ya mbali lazima watume
bahasha ya karadishia ETD yake

' Kabla ya kajaza Toma Mwombaji ahakikishe
amefanya scanning ya picha yake(blue ba`. kgroand) na viambaHsho vyote (Cheti cha kazaliwa, nakala ya passport, cheti cha kazaliwa cha babe` na baraa ya maombi).

WAZIRI JENISTA: WAAJIRI ZINGATIENI USALAMA WA WAFANYAKAZI WENU MAHALA PA KAZI KUEPUSHA AJALI NA MAGONJWA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, amewataka wamiliki wa maeneo ya kazi kuzingatia usalama na Afya mahali pa kazi kwa Wafanyakazi wao.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo maalumu ya Usalama na Afya mahali pa Kazi kwa wakaguzi wa OSHA yaliyofanyika jijini Arusha, Mhe. 
Mhagama amesema kila ajira zinapozalishwa zinaenda sambamba na ajali pamoja na magonjwa, amesema hivyo waajiri wanapaswa kuhakikisha wanazingatia usalama wa wafanyakazi wao, amesema  kukua kwa haraka kwa teknolojia inayotumika viwanda na maeneo mengine ya kazi kunagusa moja kwa moja afya na usalama wa wafanyakazi. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda amesema, walishirikiana na Shirika la Kimataifa la Workplace Health Without Borders (WHWB) katika mafunzo hayo kwa Wakaguzi, Khadija amesema Shirika hilo linalofanya kazi nchi mbalimbali dunia ikiwemo Tanzania  pia limejenga uwezo kwa wakaguzi  wa OSHA kuhusu masuala ya usalama na Afya, hivyo kupelekea na mabadiliko ya Teknolojia, amesema Shirika hiloa limetoa msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo vitatumika kwaajili ya kufanya kaguzi mbalimbali meeno ya kazi.
Nao Washiriki wa Mafunzo hayo kutoka OSHA, wamesema elimu waliyoipata wataitumia kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi, hususan kaguzi mbalimbali watakazokuwa wanazifanya.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiwa na kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda kwenye Kufunga Mafunzo Kwa Wakaguzi wa OSHA jijini Arusha.

Mkaguzi wa Afya ya Mazingira kutoka OSHA, Bi Glory Boniventure akimuelezea Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, matumizi ya Vifaa ambavyo vimetolewa na Shirika la Kimataifa la Workplace, Health Without, Borders (WHWB) vitakavyotumiwa na Wakaguzi


 Mhandisi  Maria Ndaskoy akimuelezeaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama vifaa vya Umeme vilivyotolewa na WHWB kwa OSHA

MWIGIZAJI YUSUF MLELA AWEKA WAZINUHUSIANO WAKE NA EBITOKE

BILIONI 10.7 KUJENGA CHUO CHA VETA WILAYANI CHATO

$
0
0

Wizara ya Elimu, Sayansi na  Teknolojia imetenga jumla ya Shilingi bilioni 10.7 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa chuo hicho, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema ujenzi wa chuo huo unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani.

"Nawapongeza viongozi wa Halmashauri ya Chato kwa usimamizi mzuri kwani mpaka sasa mradi huu umefikia asilimia 78 huku mkandarasi akiwa ameshalipwa asilimia 41 ya pesa yote  jambo linaloonyesha kwamba kuna fedha itabaki ambayo itasaidia kuongeza majengo mengine," amesema Waziri Ndalichako.

Aidha, Waziri Ndalichako amewataka Wakandarasi na Washauri Elekezi wanaofanya kazi za Wizara ya Elimu kuwa wazalendo na kuacha kuongeza gharama za miradi inayotekelezwa na wizara hiyo.

"Tumegundua katika mikataba mingi malipo ya washauri elekezi yanalipwa kulingana na kiwango anacholipwa mkandarasi hivyo kufanya mkandarasi  kuongeza gharama na kutokukagua vizuri miradi hiyo," ameelezea Profesa Ndalichako.

Waziri huyo amesema Wizara inafanya mapitio hata kwa miradi iliyoishakamilika  ili kujiridhisha na gharama halisi za utekelezaji na kuwezesha kutoa fedha zinazolingana na gharama na kuhakikisha miradi inakamika kwa viwango vinavyotakiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema ujenzi wa chuo hicho cha kipekee mkoani humo ni mwendelezo wa mageuzi makubwa yanayoshuhudiwa katika sekta ya elimu kwa kipindi cha uongozi wa serikali ya Awamu ya Tano.

"Chuo cha VETA Chato kitakuwa cha kwanza chenye ubora wa juu katika kanda ya ziwa kwa kuwa ni kikubwa  na kitakuwa na  karakana zenye vifaa vya kisasa ambavyo vitawezesha vijana wa Chato kuwa na ujuzi na maarifa," amesisitiza Mhandisi Gabriel.

Aidha, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameishukuru serikaki kwa kujenga chuo hicho na kuahidi kuhakikisha anahamasisha vijana wa Chato kujiunga katika chuo hicho ili kupata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda.

Kalemani amemuomba mkandarasi wa mradi huo kuongeza vijana wa Chato katika mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na hatimaye mafunzo yaanze kutolewa Januari 2020.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu amesema mradi wa ujenzi chuo hicho ni miongoni mwa miradi 40 ya ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi pamoja na upanuzi wa vyuo vilivyopo lengo likiwa ni kutimiza azma ya serikali ya kuongeza upatikanaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi na hatimaye kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 200,000 ya mwaka 2016/17 hadi 700,000 ifikapo mwaka 2020.

"Mradi huu na mingine kama hii inayotekelezwa nchini inachangia utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kuwa vijana wanapata ujuzi stahiki utakaowawezesha kuajiriwa  au kujiajiri ili kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa viwanda," amesisitiza Bujulu.

Akitoa taarifa ya Mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya ziwa, Michael Ikongoli amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo 27 ambayo ni pamoja na madarasa, karakana, nyumba 4 za walimu, bwalo la chakula, jengo la utawala na kwamba samani zote za Chuo hicho zitatengenezwa na Chuo cha VETA Mwanza kwa gharama ya shilingi milioni 693.

RC MTAKA: TRA ONGEZENI ELIMU YA KODI YA MAJENGO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, akiongea na timu ya maofisa wa TRA kutoka mkoa wa Simiyu na Makao Makuu Dar es Salaam walipomtembelea ofisini kwake Mjini Bariadi kwa ajili ya kumpa taarifa ya semina za wafanyabiashara zilizofanyika mkoani humo.
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, wakati timu ya maofisa wa TRA kutoka mkoa wa Simiyu na Makao Makuu Dar es Salaam walipomtembelea ofisini kwake Mjini Bariadi kwa ajili ya kumpa taarifa ya semina za wafanyabiashara zilizofanyika mkoani humo.
Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akiwasilisha mada ya Kodi ya Zuio kwa baadhi ya maofisa wa taasisi za Serikali mkoani Simiyu.
Baadhi ya maofisa wa taasisi za Serikali wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mada ya Kodi ya Zuio kutoka kwa Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine katika semina iliyofanyika mjini Bariadi mwishoni mwa wiki.

………………….


Na Veronica Kazimoto,Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuhamasisha wananchi kulipa kodi ya majengo na kuishauri kuongeza elimu zaidi juu ya umuhimu wa kodi hiyo.

Akizungumza ofisini kwake wakati timu ya maofisa wa TRA kutoka mkoani Simiyu na Makao Makuu Dar es Salaam walipomtembelea kwa ajili ya kumpa taarifa ya semina za wafanyabiashara zilizofanyika mkoani humo, Mtaka amesema licha ya kazi kubwa ya uhamasishaji wa kodi ya majengo inayofanyika, bado kuna baadhi ya maeneo ambapo wananchi hawajapata elimu ya kutosha kuhusu kodi hiyo.

“TRA mnajitahidi sana kuhamasisha kodi ya majengo lakini bado kuna maeneo mengi elimu hii haijafika kama inavyotakiwa hivyo tumieni kila njia ya mawasiliano kuhakikisha kuwa elimu ya kodi ya majengo inawafikia wananchi wote,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ameongeza kuwa, kuna haja ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kufungua ofisi katika baadhi ya wilaya ambazo hakuna ofisi za TRA ili kusogeza huduma karibu na wananchi ikiwa ni pamoja na kodi ya majengo. 

“Kuna baadhi ya wilaya hazina ofisi za TRA hapa nchini, kwa mfano mkoani kwangu Simiyu, kuna Wilaya ya Itilima na Busega ambazo hazina ofisi za TRA na hivyo wananchi wa wilaya hizi hulazimika kufuata huduma kwenye ofisi za TRA zilizoko makao makuu ya mkoa,” alifafanua Mtaka.

Naye, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa ushirikiano anaoutoa kwa TRA katika kutekeleza majukumu yake ya ukusanyaji mapato mkoani humo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania ndio yenye jukumu la kukusanya kodi ya majengo kisheria na viwango vya kodi hiyo ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 20,000 kwa ghorofa zima katika Halmashauri za Wilaya na shilingi 50,000 kwa kila sakafu ya ghorofa katika Majiji, Miji na Manispaa.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGUA SEMINA YA WABUNGE WANAWAKE AFRIKA

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Gran Malia Jijini Arusha.  

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa  Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, baada ya kufungua Semina hiyo Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Grand Malya Jijini Arusha.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images