Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

Serikali, SIDA, Unesco waanza maandalizi ya ripoti ya kitaifa uanuai wa kitamaduni

$
0
0

 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos mara baada ya kuwasili kwenye warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg.
 Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA ambaye pia ni Mtaalamu wa Taifa wa mradi unaolenga kutekeleza makubaliano ya UNESCO ya mwaka  2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Tamaduni Anuwai, Bi. Doreen Sinare akitambulisha meza kuu (hawapo hewani) wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akitoa salamu za UNESCO wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg akitoa salamu za SIDA wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA na Mtaalamu wa Taifa wa mradi unaolenga kutekeleza makubaliano ya UNESCO ya mwaka  2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Tamaduni Anuwai, Bi. Doreen Sinare cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi  Bw. Maximilian Chami kutoka Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco) cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Meneja wa Programu wa Taasisi ya Culture and Development East Africa (CDEA), Bw. Mandolin Kahindi cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Mwakilishi kutoka COSOTA Bw. Zephania Lyamula cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Mwamini Mohamed cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
Baadhi ya washiriki wakiwasilisha kazi za vikundi wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Utamaduni, Elimu, Utamaduni na Sayansi la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wamezindua mafunzo ya kuandaa ripoti ya kitaifa ya Mkataba wa UNESCO wa mwaka 2005.

Mkataba huo ambao serikali ya Tanzania umetia saini mwaka 2011 unazungumzia kulinda na kuendeleza uanuai wa kujieleza kiutamaduni.
Kwa mujibu wa matakwa ya mkataba huo kila baada ya miaka mine mataifa yanayotakiwa kuandika taarifa kuelezea utekelezaji wa mkataba huo. Mengi ya mataifa ikiwamo Tanzania haijawahi kuandika  taarifa hiyo.

Kwa kawaida taarifa hiyo ni mchanganyiko wa taarifa za serikali na wadau wengine wakiwemo wa taasisi zisizo za kiserikali (AZAKI).
Fedha za kufanyia mafunzo hayo na kuandika taarifa zimetolewa na Sweden kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (SIDA) chini ya uratibu wa UNESCO.
Taarifa hiyo ikishakamilika inatarajiwa kujadiliwa na wadau na kupelekwa serikalini ambako nako itapitiwa na kufikishwa UNESCO.

Akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini Dk. Kiagho Kilonzo, alisema kwa sasa Tanzania ipo tayari kwa taarifa hiyo ndio maana imeunda kamati na kuanza mafunzo.
Kamati hiyo ya kuandika Ripoti inaongozwa na Robert Mwampembwa ambaye ikisimamiwa na Doreen Sinare, Ofisa mtendaji Mkuu wa COSATA ambaye ndiye mtaalamu wa mradi.

Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden nchini Andres Sjoberg, ufadhili wa taifa hilo kwa nchi 16 zinazotakiwa kuandika utekelezaji wa mkataba huo umelenga kuhakikisha kuwa kuna uhuru wa wasanii kujieleza kiutamaduni na hasa wanawake.
Alisema kwa sasa dunia sio kijiji bali kutokana na mifumo ya upashanaji wa habari kuzidi kuimarika dunia imekuwa ni moja na hivyo masuala ua kujieleza yanabaki kuwa wazi kila mahali.

Naye Dk. Harrison Mwakyembe alisema kwa sasa Tanzania iko vizuri kutokana na kuridhia mkataba huo wa 2005 ambao lengo lake kubwa ni kutengeneza fursa kwa wasanii kuwa karibu na soko la dunia.
Aidha alisema kwamba nia kubwa ya makubaliano hayo ni kulinda uanuai wa kujieleza kiutamaduni na hivyo kutengeneza mazingira ya kukua kwa utamaduni kwa manufaa ya watu wote.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe ni matarajio yake kwamba ifikapo Aprili mwakani taarifa hiyo itakuwa imekamilika na tayari kutumika na tasnia ya utamaduni na ubunifu na dunia pia.
Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Dar es Salaam, Tirso Dos Santos,  alisema kwamba taarifa ya Tanzania itaunganishwa na mataifa mengine ili kuelezea dunia inavyoendelea katika kutekeleza matakwa ya mkataba.

"Sote tunajua kwamba Tanzania ni kitovu cha ubunifu na hasa kwa kuwa na matamasha mbalimbali hali inayodhirisha umuhimu wa mradi huu kwa ajili ya maendeleo maendelevu ", alisema mwakilishi huyo wa UNESCO ambapo aliyataja matamasha makubwa ya filamu nchini ikiwamo ya ZIFF na Azam kama moja ya uanuai wa utamaduni.

MWENYEKITI WA CWP DUNIANI MHE. SHANDANA KHAN AWASILI KUSHIRIKI SEMINA YA CWP KANDA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Mwenyekiti  wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani (CWP International), Mhe. Shandana Gulzar Khan akipokelewa na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Saidi Yakubu, baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki warsha ya Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region) iliyoanza leo tarehe 26 - 29 Oktoba, 2019 Katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani, Mhe. Shandana Gulzar Khan (wa pili kushoto) akiongozana  na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Saidi Yakubu (kushoto) baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki warsha ya Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika iliyoanza leo tarehe 26 - 29 Oktoba, 2019 Katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Herman Berege
 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani, Mhe. Shandana Gulzar Khan (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Saidi Yakubu (wa pili kushoto) baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki warsha ya Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika iliyoanza leo tarehe 26 - 29 Oktoba, 2019 Katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Herman Berege

Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani, Mhe. Shandana Gulzar Khan (kulia) akizungumza na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Saidi Yakubu, Katika Ofisi za uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili  kwa ajili ya kushiriki warsha ya Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika iliyoanza leo tarehe 26 - 29 Oktoba, 2019 Katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

NAIBU WAZIRI ULEGA AHUDHURIA MKUTANO WA MAWAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA JIJINI ADDIS ABABA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega yuko nchini Ethiopia ambapo anahudhuria mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo, mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.
Mkutano huo ulioitishwa na Kamisheni ya Afrika kupitia Shirika lake la kusimamia Maendeleo ya Rasilimali za Wanyama Barani Afrika (AU-IBAR), unafanyika kwa siku mbili mjini Addis Ababa ambapo mbali na mambo mengine mkutano huo utapokea ripoti na maazimio mbalimbali kutoka kwa wataalam wa sekta hizo kujadili na kuyapitisha ili waweze kupeleka Halmadhauri Kuu ya AU kwa maamuzi na utekezaji.
Moja ya mikakati, ripoti na maazimio na mapendekezo yanayotarajiwa kujadiliwa na kuridhiwa na baraza hilo la mawaziri wa AU wa sekta ya mifugo, uvuvi, kilimo, mazingira na maji ni ripoti ya miaka miwili ya Tathmni ya Azimio la Malabo (Malabo Declaration) lenye lengo la kuondoa njaa katika bara ka Afrika ifikapo Mwaka 2025 na ripoti ya Tathnimi ya kuwasiliana na Majanga ya asili kama mafuriko na ukame.
Maazimio na mapoendekezo mengine ni ripoti ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi, juhudi za nchi wanachama kuzuia matumizi ya bidhaa za plastiki, mkakati wa kupanda mazao yenye viini lishe vya kutosha na mkakati wa kukabiliana na upotevu wa mazao ya mimea na samaki baada ya kufunga (Post harvest Loss).
Katika kikao hicho pia kitajadili mkakati wa kupambana na magonjwa na vimelea sugu kwa mifugo, mpango wa kuanzisha maabara za kupima ubora wa chakula katika bara la Afrika, mpango wa pamoja wa kuwa na kusimamia na kuweza katika wazo la uchumi wa bahari (Blue economy), mpango mkakati wa miaka 10 kuendeleza uvuvi mdogo mdogo (small scale fisheries) na mpango mkakati wa miaka 10 wa kuendeleza sekta ya ukuzaji viumbe maji.

Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi Bi. Josefa Correia Sacko Mkuu wa Kamisheni ya Afrika ya Kilimo na maendeleo vijijini, ambapo zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi 49 za bara la Afrika wanahudhuria wakiwepo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kama FAO, WWF, Benki ya Dunia na NEPAD.

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo anahudhuria mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo, mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa Addis Ababa nchini Ethiopia akiwa katika mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo, mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa Addis Ababa nchini Ethiopia akiwa na mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo, mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.

TASWIRA ZA MAANDALIZI YA KUANZA SAFARI YA KUJA NYUMBANI KUTOKA MAREKANI KWA NDEGE YETU YA DREAMLINER BOEING 787

$
0
0
Marubani na wanaanga wenzao wakipata staftahi kabla ya kuanza safari ya saa 17 kutoka Seattle, Marekani, kuja Dar es salaam ambapo wanatarajiwa kutia mchana huu.












MAFURIKO YAKATA MAWASILIANO YA BARABARA, MAMIA YA WASAFIRI WAKWAMA ENEO LA MANDELA MKOANI TANGA

$
0
0
Wasafiri kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine wamekwama katika eneo la Mandela kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara katikati ya wilaya ya Handeni na Korogwe, Mkoani Tanga baada ya kufurika kwa mto Mandera kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini.  Hii ni mara ya pili sasa kukatika kwa mawasiliano katika eneo hilo.

SUKAMAHELA: KIJIJI AMBACHO KIPO KATIKATI YA NCHI YA TANZANIA

$
0
0


Hapa ndio  Sukamahela kijiji kilichopo Kata ya Solya katika Wilaya ya  Manyoni mkoani Singida.  Na hapa ndipo inaposemekana ni katikati kabisa ya nchi ya Tanzania Bara. Kuna alama iliyo  kuleeee juu ya miamba katika picha hapo chini ambako ukaingalia kwa makini juu ya mwamba uliochomoza kulia pana alama kama ya nyani aliyesimama inayoashiria jambo. Basi hapo ndipo katikati ya Tanzania.

WANANCHI ZAIDI YA 1000 WAPATIWA MSAADA WA KISHERIA MKOANI SIMIYU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa mkoa mkoa huo(hawapo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.


Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jarida la msaada wa kisheria katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktioba 21, 2019.

………………………

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi amesema takribani wananchi 1018 wamepata huduma ya msaada wa kisheria katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba 25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.



Mushi ametoa taarifa hiyo katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi na yameshafikishwa mahakamani na yako katika hatua mbalimbali.

Amesema huduma walizopata wananchi katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi, ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu sahihi ya kwenda pindi wanapopata migogoro.

“Mbali na huduma kwa wananchi mafunzo yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao 1300 wakiwemo, wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe wa kamati ya parole, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji, wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakimu, askari polisi na magereza, wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa vijiji na kata, “ alisema Mushi.

Kwa upande wake Hakimu Mary Nyangusi akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo mingi inatokea mara nyingi wanaume( baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto kudhulumiwa haki zao.

Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi waliofika kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema, “nashukuru nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba mwenye mji anapokuwa amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana mamlaka juu ya mali iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake wakati mzee hakuacha hata wosia”.

Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, ili wananchi wapate uelewa wa masuala ya kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana.

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya kimeenda sambamba na uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

KARIBU AIR TANZANIA;BOEING 787-8 DREAMLINER

$
0
0
Ndege Inatua Leo Katika Ardhi ya Tanzania  ni Ndege ya 8 KWENYE Orodha ya Ndege za AIR TANZANIA 

1. Boeing 787-8 Zipo 2
2. Forker 50 Ipo 1 
3. Bombardier Dash 8-400 Zipo 3
4. Bombardier Dash 8-300 Ipo 1 
5. Airbus  A220-300 Zipo 2 


Ndege Hii Mpya Imesajiliwa Kwa Usajili Namba 5H-TCJ na Imepewa Brand Name ya Visiwa vya RUBONDO ISLAND Vilivyopo  Mkoani Mwanza Vyenye Ukubwa wa Kilometre za Mraba 456.8 Sawa na Kushabihiana Ukubwa wa Manispaa ya KINONDONI Mkoa wa DAR ES SALAAM

Ndege Mpya ya Air TANZANIA Boeing 787-8 Ina Uwezo  wa Kutembea Kilometres 13620 Sawa na saa zaidi ya 12 Hewani Bila ya Kusimama 

Inabeba Lita 101,000 za Mafuta na Ina Ukubwa wa MITAA 56.72 Yaani Ni Sawa na Nusu ya Uwanja wa Mpira wa Miguu

Inabeba Jumla ya Abiria 262 

Ina Uwezo wa Kubeba Uzito wa Tani 227 Yaani 227,930Kg Wakati wa Kupaa Uzito wa Hujumuisha Uzito wa Chombo,Mizigo,Mafuta na Inapotua Inatakiwa Iwe na Tani  172 za Uzito, Hii Inatokana na Kupungua Kwa Kiasi Cha Mafuta Wakati wa Kutua .

Sifa ya Ndege Hii Ina Uwezo Mkubwa wa Kuhimili Hali Nzito ya Hewa Ikiwa KWENYE Umbali Mrefu Kwenda Juu 

Leo Tunaipokea Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA 



Mgeni RASMI ni Mhe RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, H:E Dr JOHN POMBE MAGUFULI

DC MURO MGUU KWA MGUU MRADI WA MAJI BILIONI 8

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arumeru amefanya ukaguzi wa nane wa mradi wa maji wa Bilioni 8 * katika Halmashauri ya wilaya ya *Arusha, ambapo amewataka wakandarasi kuhakikisha mradi huo wa maji *unamalizika Haraka iwezekanavyo *

Dc Muro ambae ametembelea eneo la ujenzi wa pampu kubwa za kuchujia maji yenye Fluoride na kutembelea Tanki kubwa la kuhifadhi maji mbali na kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na wakandarasi amesema Muda wa utekelezaji wa mradi huo umekwisha na sasa ni zamu ya wananchi zaidi ya kaya elfu 50 kupata maji safi na salama na si vinginevyo 




MKUU WA MKOA WA PWANI KUZINDUA ALBAMU YA KAMANDA WA POLISI KESHO

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kesho anatarajia kuzindua tamasha kubwa la dini linalojulikana kwa jina la Kipaji change thamani yangu kwa Kibaha salama ambali pia litaambatana na uzinduzi rasmi wa albamu mpya ya video inayoitwa nilipigwa picha ikiwa na nyimbo tisa katika ukumbi wa Filberti bayi uliopo  Wilayani Kibaha.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa tamasha hilo Kadnas  Nassir alisema kwamba onyesho hilo limeandaliwa na kwa ushirikiano wa umoja wa makanisa Wilayani Kibaha pamoja na mwimbaji maarufu wa  wa nyimbo za injili Eva Stesheni ambaye pia ni mkuu wa Kituo cha polisi Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
“Kwa kweli mpaka sasa maandalizi yote tunashukuru Mungu yanaendelea vizuri kwani mipango yote ambayo tumeipanga inakwenda vizuri na kitu kikubwa siku hiyo kutakuwa na burudani mbali mbali kutoka katika kwanya za Mkoa wa Pwani pamoja na nyingine kutoka Jijini Dar es Salaam sambamba na wasanii wengine wa nyimbo za injili.
Pia alisema kwa lengo la kuandaa tamasha hilo kubwa katika Wilaya ya Kibaha ni kuyakutanisha makanisa mbali mbali kwa ajili ya kuweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika novemba 24 mwaka huu pamoja na kuzindua albamu hiyo ya video yenye nyimbo za injili.
Aidha katika hatua nyingine mratibu huyo alibainisha kuwa tamasha hilo lina lengo la kuweza kutoa fursa kwa vijana  mbali mbali wa wilayani Kibaha na mkoa wa Pwani wanaoimba mziki wa injili kuweza kukuza vipaji vyao pamoja na kuonyesha uwezo wao wa kuimba.
Mratibu huyo aliongeza kuwa tamasha hilo pia litapambwa na waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili wakiwemo Joel Lwaga, Jane Miso, Sifael Mwabuka na mtoto wa Yohana Antony, pamoja na kwaya ya Haleluya , KKT Tumbi,Anglikaana.AIC sambamba na kwaya ya RC Tumbi na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa shilingi elfu 50 kwa viti maalumu pamoja na shilingi elfu 5 kwa kawaida na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo.
Mratibu wa Tamasha la injili linalokwenda kwa jina la Kipaji change yhamani yangu kwa kibaha saalama  Kadnas Nassir akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na maandalizi ya onyesho hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis Evarist Ndikilo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kepteni saidi Hamadi mmoja wa Marubani walioleta ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner kuoka Seattle Marekani alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo kwenye viti vya marubani wa Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Mke wa Rais Mama janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuipokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuaga baada ya kuongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine na wadau akikata utepe kuashiria kupokewa kwa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakisiliza maelezo toka kwa Kepteni Dennis Mshana mmoja wa Marubani walioileta ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Seattle Marekani hadi katika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na marubani na wanaanga waliokuja na ndege wakati alipoongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini alipoongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wa Taasisi Mbalimbali za Umma na Binafsi alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mzee Omary Mkali, mmoja wa wazee waliofika katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Oktoba, 2019 ameungana na wananchi wa Dar es Salaam kuipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamlineriliyonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha usafiri wa anga na kukuza uchumi hapa nchini.


Mapokezi ya ndege hiyo yamefanyika jengo namba moja (Terminal One) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Mabalozi wa Nchi mbalimbali, Wabunge, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa taasisi mbalimbali na wafanyabiashara.


Akizungumza na wananchi mara baada ya kutua kwa ndege hiyo kutoka Seattle nchini Marekani ilikotengenezwa, Mhe. Rais Magufuli ameelezea furaha yake ya kufanikiwa kwa mpango wa kuimarisha usafiri wa anga baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kununua ndege 11 kwa ajili ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambapo 7 zimeshawasili na zingine 4 zitawasili kwa vipindi tofauti hadi kufikia June 2020.

Mhe. Rais Magufuli amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa kwa fedha zinazotokana na kodi zao na hivyo ametoa wito kwa kila Mtanzania kuendelea kuchapa kazi na kulipa kodi ili Serikali iweze kufanya mambo mengi zaidi ya kuwaletea maendeleo.


“Kwa hiyo fedha zenu zinajulikana hadi kule Marekani kwamba Watanzania wanaweza kununua kitu kizito kama hiki, hongereni sana Watanzania, siku zote mtembee kifua mbele ndugu zangu Watanzania, mnaweza, Watanzania tunaweza na Waafrika tunaweza, hakuna kinachoshindikana.


Kikubwa kinachohitajika ni matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana kutoka kwa wananchi, hongereni Watanzania, kwangu mimi najisikia raha sana, ninajisikia raha kuwa kiongozi wa Tanzania, lakini najisikia raha zaidi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu haya yamezungumzwa kwenye Ilani ya Uchaguzi.


We mi ndege kama hii inashuka hapa? kwa sababu ni lazima tujiulize kwa nini hayakushuka zamani? Huo ndio ukweli bila kuficha, kwa nini mi dege hii isubiri Magufuli awepo ndio ishuke” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Amemshukuru Rais wa Marekani, Mhe. Donald Trump kwa kutambua juhudi za Tanzania katika maendeleo na kununua ndege kutoka Marekani kwa ajili ya kuimarisha huduma za usafiri wa anga.


Balozi wa Marekani hapa nchini Dr. Inmi Patterson ameipongeza Tanzania kwa kuboresha usafiri wa anga na ameelezea juhudi hizo kuwa zitaboresha uchumi na zitavutia uwekezaji.


Mhe. Rais Magufuli ameipongeza menejimenti na wafanyakazi wa ATCL kwa kazi wanazofanya ikiwemo kuingiza mapato ya kiasi cha dola za Marekani Milioni 14 (sawa na shilingi na shilingi Bilioni 31 na Milion 892) na amewataka kuzitunza ndege hizo vizuri na kuhakikisha Shirika linaendeshwa kwa ufanisi.


Ndege hiyo mpya ina uwezo wa kubeba abiria 262 na kusafiri saa 18 bila kutua, Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiikabidhi kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dr. Leonard Chamriho ili itumike kwa ATCL.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amekubali ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Makonda la kupatiwa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam na amemuagiza Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kutafuta fedha hizo ili ujenzi uanze.


“Hatuwezi kuwaacha wananchi wa Ubungo wateseke, wakitaka kutibiwa mpaka waende Wilaya za jirani, hapana, tutajenga Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Ubungo hoyeee” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

26 Oktoba, 2019



JAJI KIONGOZI AIPA SOMO MAHAKAMA SACCOS

$
0
0
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi(katikati) akifungua   Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo  cha Mahakama ya Tanzania(MAHAKAMA SACCOS) leo Oktoba 26, mwaka huu  wakati akiwa mgeni rasmi wa kufungua mkutano huo, uliofanyika katika ukumbi namba moj uliopo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Kulia wa pili ni Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Edwin Protas na wa kwanza ni Makamu Mwenyekiti,Bi.Haluwa Kivuma. Kushoto wa pili ni Bi. Herodia Kambanga na wa kwanza kushoto ni Bi. Irene Ngowi wote ni Maafisa Ushirika kutoka Manispaa ya Ilala.  
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Mahakama ya Tanzania (MAHAKAMA SACCOS) wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka, uliofanyika leo, uliofanyika katika ukumbi namba moj uliopo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Magreth Kinabo – Mahakama)

……………………….

Na Magreth Kinabo- Mahakama

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewashauri viongozi na wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Mahakama ya Tanzania(MAHAKAMA SACCOS) kukinadi chamam hicho ili kiweze kuwa na idadi kubwa ya wanachama na kuiwezesha Mahakama kuwa Taasisi bora inayoongoza kwa utoaji kwa riba nafuu kitaifa na kimataifa.

Akizungumza leo Oktoba 26, mwaka huu wakati akiwa mgeni rasmi wa kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, uliofanyika katika ukumbi namba moj uliopo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, Jaji Kiongozi alisema ni vema viongozi hao na wanachama kuweka mikakati ya kuweza kuongeza idadi ya wanachama ili kufikia azima hiyo.

Alisema idadi ya majaji saba waliojiunga na chama hicho, bado ni ndogo, wakiwemo mahakimu na wasajili.

“Mnapaswa kuweka mikakati ya kukinadi chama hiki ili kuweza kuwa na angalau nusu ya idadi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania, chama hakijafanyiwa uhamasishaji wa kutosha, hivyo kila mwanachama anaowajibu wa kuhamasisha watu kujiunga,” alisema Jaji Kiongozi.

Jaji Kiongozi aliongeza kwamba chama hicho, kinatakiwa kutumia mitandao ya kijamii na tovuti ya Mahakama ili kiweze kufahamika na kutangaza shughuli za kupitia mitandao hiyo, ikiwemo kuwa na vijarida na vipeperushi vya chama, kwa kuwa ni nyezo za kukifanya kiweze kufahamika.

Aidha Jaji Kiongozi alikishauri chama hicho, kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli zake, ikiwa ni hatua ya kuweza kuwafikia watumishi wengi na kupunguza gharama za uendeshaji.

Dkt. Feleshi alisema pia chama hicho, kitumike kama sehemu ya kudumisha, amani, upendo, ushirikiano na mshikamano miongoni kwa watumishi hao ili kiweze kusaidia changamoto za kiuchumi na kijamii hali itakayosaidia wanachama kuweza kufanya kazi za utoaji haki kwa hisia.

Awali akizungumza kabla ya kukaribisha, Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Edwin Protas alisema kilianzishwa mwaka 1970 kikiwa na wanachama 84 na hivisasa kina wanachama 372, kati ya watumishi zaidi ya 5000 wa Mahakama.

Protas alisema kwamba baadhi wanachama wake, ambao si maafisa wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na mishahara midogo, hivyo aliiomba Tume ya Utumishi ya Mahakama ya Tanzania kuweza kuliangalia suala hilo, ili chama kisiweze kuzorota.

Kwa upande wake, Afisa Ushirika kutoka Manispaa ya Ilala,Bi. Herodia Kambanga alikitaka chama hicho kuwa ushirikiano na vyama vingine ili kuweza kubadilisha uzoefu na kutatua changamoto mbalimbali.

BONANZA LA WATUMISHI WA UMMA MKOA WA SINGIDA LILIVYOFANA

$
0
0
Mchezaji wa Timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Singida, Donald Kaene (kushoto) akimtoka Bill David mchezaji  wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tabroad) katika  bonaza la michezo ya watumishi wa umma mkoani Singida.
Timu ya Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, wakionesha umahiri wa kufanya mazoezi ya kuruka.

Wafanyakazi wa Tanroad wakishindana kuvuta kamba na wafanyakazi kutoka Halmashaurj ya Wilaya ya Manyoni.
Wafanyakazi wa Tanroad wakishindana kuvuta kamba na wafanyakazi kutoka Halmashaurj ya Wilaya ya Manyoni.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manyoni wakishindana kuvuta kamba na wafanyakazi kutoka Wilaya ya Manyoni.
Bonanza likiendelea.
Wafanyakazi wa kike kutoka Manyoni wakivuta kamba dhidi ya wafanyakazi wa Tanroad.
Wafanyakazi wa Tanroad wa kike wakivuta kamba dhidi ya wafanyakazi wa kike wa Manyoni.
Timu ya Tanesco ikiwa viwanja vya Singidani Beach lilipofanyika bonanza hilo.
Mchezaji wa Hospitali ya Mkoa Singida, Frank Meza (kushoto) akimtoka Issa Ahmed kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida katika bonanza hilo.
Wacheza karate kutoka Singida Shotokaki Karate wakionesha ukakamavu katika bonanza hilo.
Wafanyakazi wa Vodacom wakivuta kamba dhidi ya wafanyakazi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Timu ya ofisi ya mkuu wa mkoa ikivuta kamba.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wakishangilia.
Mfanyakazi wa Tanesco akisakata kabumbu.
Wafanyakazi wa Tanesco wakifanya mazoezi kabla ya kuingia mchezoni dhidi ya Tanroad.
Wachezaji wa Netball kati ya Manyoni na Tanroad wakimenyana uwanjani.
Mchezaji wa Tanroad Doroth Ogutu akifunga bao.
Wafanyakazi wa Tanesco wakifanya mazoezi.
 Timu ya Standard Radio katika picha ya pamoja.
 Timu ya Watumishi  katika picha ya pamoja.
 Timu ya Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ikifanya mazoezi.
Timu ya Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika picha ya pamoja

MWAKILISHI JIMBO LA JANG'OMBE AZITEMBELEA MASKANI ZA CCM JANG’OMBE

$
0
0
MWAKILISHI wa Jimbo la Jang’ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande (wa pili kutoka kulia), akikabidhi mabati saba kwa Katibu wa maskani ya Butihama ndugu Ali Mabrouk Makashari (kushoto) katika ziara hiyo.

MWAKILISHI wa Jimbo la Jang’ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande (kushoto) , akimkabidhi fedha taslimu shilingi 70,000 Mjumbe wa maskani ya Karume ndugu Ibarahimu Abass Faki kwa ajili ya matengenezo ya maskani hiyo.
MWAKILISHI wa Jimbo la Jang’ombe Zanzibar Mhe.Ramadhan Hamza Chande (kushoto),akimkabidhi seti moja ya jezi Meneja wa timu ya mpira wa miguu ya Kidongo chekundu City ndugu Omar Shamna (kulia).
MWAKILISHI wa Jimbo la Jang’ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande (kushoto) ,akimkabidhi mabati saba ya kuezekea maskani ya Bora Imani iliyopo Urusi Jang’ombe ndugu Omar Said Salum ‘Saa nane’ (wa nne kutoka kulia).(PICHA NA IS-HAKA OMAR-ZNZ)

……………………

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

MWAKILISHI wa Jimbo la Jang’ombe Zanzibar Mhe.Ramadhan Hamza Chande, ametoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 1.5 kwa maskani nane za Chama Cha Mapinduzi zilizomo katika jimbo hilo.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara zake katika maskani mbali mbali za CCM jimboni humo, Mhe.Ramadhani alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo ni Mabati ya kuezekea nyumba, Jezi za mpira wa miguu na fedha taslimu ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake alizowaahidi wananchi katika kampeni za uchaguzi zilizopita.

Alisema kwamba wakati akiomba ridhaa ya wananchi katika jimbo hilo aliahidi kuzipatia vifaa hivyo maskani za Chama Cha Mapinduzi zilizokuwa na changamoto mbali mbali zilizotakiwa kutatuliwa na viongozi wa Chama.

Alieleza kuwa katika uongozi wake ndani ya jimbo hilo ataendelea kuwa karibu na Wananchi wa makundi yote, bila kubagua rika zao kwani kila mmoja ana umuhimu wake katika maisha ya kisiasa.

Katika maelezo yake Mwakilishi huyo Mhe.Ramadhan, aliwambia viongozi na makada wa maskani hizo kuwa Chama Cha Mapinduzi kinawathamini kutokana na mchango wao wa kuimarisha taasisi hiyo Kisiasa na Kiuchumi.

Alitoa nasaha zake kwa wanachama mbali mbali wa maskani hizo kubuni miradi ya ujasiriamali ili Vijana,Wanawake na Wazee wapate sehemu mbadala ya kujiingizia kipato.

Katika ziara hiyo aliwakumbusha Wananchi hasa Wana CCM kuhakiki vitambulisho vyao vya mzanzibar mkaazi sambamba na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate uhalali kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha kinashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alieleza kwamba kutokana na kazi aliyopewa na Wananchi wa Jimbo hilo ametekeleza Ilani ya Chama kwa zaidi ya asilimia 70 na anaendelea kukamilisha ahadi zake ili ifika mwishoni mwa mwezi Desemba awe amemaliza utekelezaji wa ahadi zake.

“Nawashukru sana Viongozi wenzangu wa jimbo letu wakiwemo mbunge ,madiwani na viongozi wote wa Chama na Jumuiya zake kwa ushirikiano wenu, ulioteta tija kubwa kwa wananchi wetu wote.

Naye Diwani wa wadi ya Kwaalinatu Mhe.Fatma Suleiman Juma, aliwataka wananchi kuendelea kujali na kuitunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na viongozi wa CCM ili idumu kwa muda mrefu kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Diwani wa wadi ya Urusi Mhe.Ibrahimu Abass Faki, alisema kwamba jimbo hilo limeendelea kuimarika kimaendeleo kutokana na ushirikiano wa viongozi wake katika kutekeleza Ilani ya CCM.

Akizungumza Katibu wa Siasa na Uenezi wa Jimbo hilo Ali Hamad Ibrahim, alisema ziara hiyo imeongeza hamasa kubwa wa wana maskani hao kwani changamoto zao za muda mrefu zimetafutiwa ufumbuzi na kudumu na mwakilishi huyo.



Aliongeza kuwa kila mwanachama na viongozi wa CCM ndani ya jimbo hilo anatakiwa kuandaa vizuri zana zake za mapambano ya vita ya kisiasa kuelekea 2020,kwani muda kusema kwa maneno umepita na kilichobaki ni kutekeleza kwa vitendo.

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI CP LIBERATUS SABAS AZUNGUMZA NA WATENDAJI KATA PAMOJA NA MAAFISA TAARAFA WA WILAYA YA KASULU MKOANI KIGOMA

$
0
0
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas wa pili kutoka kulia akiongea na Askari wa kutuliza Ghasia katika Kituo cha Polisi cha Kasulu mapema leo kabla ya kuingia kwenye kikao chake na Watendaji Kata na Maafisa Taarafa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas wa tano kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Watendaji Kata na Maafisa Taarafa baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi uliopo kituo cha Polisi Kasulu mkoani Kigoma.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, akikagua kitabu cha kufunfulia mashtaka katika kituo cha Polisi cha Nyarugusu baada ya kutembelea kambi hiyo na kuongea na askari wa kituo hicho.(PICHA NA JESHI LA POLISI


Majaliwa Aitetea Zimbabwe Mkutano wa NAM

$
0
0

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amehimiza mjadala wenye tija kutoka Jumuiya ya Kimataifa ili kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbambwe.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na kwingineko duniani uliofanyika Baku, Azerbaijan.

“Uwekwaji wa vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Zimbambwe unalemaza ukuaji wa uchumi,ufanyaji wa biashara,uwekezaji na ustawi wa watu”Aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa.

Hatua hiyo imekuja wakati China ikiunga mkono wazo la Rais Dkt. Magufuli la kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuindolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi ambapo kupitia Balozi wake hapa nchini Wan Ke aliitaka jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo hivyo katika kongamano maalum kuhusu vikwazo vya kiuchumi na hatma ya maendeleo ya Afrika lililofanyika Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Masauni asikiliza kero za Wananchi wa Kijiji cha Chikongo Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Chikongo wilayani Tandahimba wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa idara zilizopo chini ya wizara mkoani Mtwara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwananchi wa Kijiji cha Chikongo wilayani Tandahimba,Hassan Mkeli akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kutoka kulia), wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Mwananchi wa Kijiji cha Chikongo wilayani Tandahimba, Stanley Alphonce akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WANAFUNZI WENGINE 11,378 WAPANGIWA MIKOPO

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa imetoa orodha ya Awamu ya Pili yenye jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza 11,378 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 35.06 bilioni.

Taarifa iliyotolewa leo (Jumamosi, Oktoba 26, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru imesema idadi hii ya awamu ya pili inafanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo kufika 42,053 na wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 148.56 bilioni.

Katika orodha ya awamu ya kwanza iliyotangazwa wiki iliyopita, wanafunzi wa mwaka wa kwanza 30,675 walipata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.

Badru amesema katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali imetenga TZS 450 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, wanafunzi zaidi ya 45,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wanafunzi wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, TZS 427.5 bilioni zilitengwa na kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,285 wakiwemo wanafunzi 41,285 wa mwaka wa kwanza.

“Tumeboresha sana mifumo yetu, na sasa mwanafunzi anaweza kufungua akaunti yake aliyoombea mkopo maarufu kama SIPA - Student’s Individual Permanent Account - na kupata taarifa zake zikiwemo za kiwango cha mkopo alichopata,” amesema Badru.


Pamoja na SIPA, Badru amesema majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo katika awamu hii ya pili yanapatikana katika mtandao wa HESLB wa uombaji mkopo (https://olas.heslb.go.tz) na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kwa awamu inayofuata ukiendelea.

NAIBU WAZIRI SHONZA ASHIRIKI UFUNGAJI TAMASHA LA 38 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikagua bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni alipotembelea mabanda ya wajasiliamali wakati wa hafla ya kufunga Tamasha la 38 la Sanaa na Utamadani la Chuo cha Sanaa Bagamoyo lililofanyika chuoni hapo leo tarehe 26/10/2019 mjini Bagamoyo.



TANZANIA YATAKA VIKWAZO DHIDI YA CUBA NA ZIMBABWE VIONDOLEWE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Mkutano wa Nchi zisizofungamana na uapande wowote kwenye Kituo cha Mikutano cha Baku nchini, Azerbaijan alikomwakilisha Rais Dkt. John Bombe Magufuli, Oktoba 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu, wa Azerbaijan, Ali Ahmedov (kulia) kwenye Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu huyo iliyopo Baku nchini humo, Oktoba 27, 2019. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi ambaye pia ni Balozi wa Azerbaijan, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mimwi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu, wa Azerbaijan, Ali Ahmedov (kulia) kwenye Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu huyo iliyopo Baku nchini humo, Oktoba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



SERIKALI ya Tanzania imelaani vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Serikali ya Marekani dhidi ya Cuba na Zimbabwe kwa sababu vinadhoofisha biashara, uwekezaji na ustawi wa wananchi na imetaka vikwazo hivyo viondolewe.

Tamko hilo limetolewa leo (Jumamosi, Oktoba 26, 2019) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye Mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) ulioanza leo huko Baku, Azerbaijan.

“Vizuizi na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya Cuba na Zimbabwe vinadhoofisha maendeleo ya uchumi, uwezo wa kufanya biashara, fursa za uwekezaji na ustawi wa wananchi wake.”

“Tanzania inaungana na Jumuiya ya Kimataifa kutaka yawepo majadiliano ya msingi ambayo yataondoa vizuizi kwa Serikali ya Cuba na vikwazo kwa Serikali ya Zimbabwe ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa manufaa ya watu wa nchi hizo,” amesema.

Mwaka 2001, Marekani na Jumuiya ya Ulaya (EU) ziliweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe baada ya Serikali ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Rais Robert Mugabe kuamua kuchukua ardhi yote iliyokuwa ikimilikiwa na wageni.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, aligusia mambo kadhaa ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, masuala ya Sahara Magharibi, usalama wa Palestina na msimamo wa Tanzania kwenye Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM).

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, Waziri Mkuu amesema suala hilo ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili dunia na wanadamu kwa sasa. “Tunaiomba Jumuiya ya Kimataifa iweke njia muafaka ambazo zitasadia kurekebisha tishio ambalo tunakabiliana nalo hivi sasa. Tunazitaka nchi zilizoendelea zitimize ahadi zao na michango ya kifedha, zisaidie kujenga uwezo na kutoa wataalamu watakaozisaidia nchi zinazoendelea,” amesema.

  Akizungumzia Sahara Magharibi, Waziri Mkuu amesema suala la kujitawala kwa nchi hiyo limeingia sura mpya baada ya Morocco kujiunga tena na Umoja wa Afrika na kwamba hivi sasa imekuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

“Ipo fursa kubwa hivi sasa kwa Umoja wa Mataifa pamoja na mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuweza kushirikiana na chombo kipya cha Troika kilichoundwa na Umoja wa Afrika katika kuliangalia suala zima la Sahara Magharibi. Tanzania inaunga mkono jitihada hizo,” amesema Waziri Mkuu.

Kwenye suala la Palestina, Waziri Mkuu amesema Tanzania inatambua kwamba nchi hiyo ina haki ya kufurahia amani na uhuru wake kama ilivyo kwa Israeli, kwa mujibu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa. “Ni matumaini yetu kwamba kuendelea kuwepo kwa jitihada za kimataifa, mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi katika muda muafaka na mataifa haya mawili yataishi kwa amani na utulivu.”

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuelezea msimamo wa Tanzania kwenye umoja huo na kusisitiza kwamba Tanzania bado ina imani na chombo hicho. “Tanzania itaendelea kuheshimu kazi zinazofanywa na umoja huu kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa miaka 58 iliyopita. Tunaomba ushirikiano baina ya nchi za Kusini uimarishwe. Ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea nao pia uimarishwe.”

Amesema: “Serikali ya Tanzania inapongeza uhusiano ulipo baina ya Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), kundi la nchi 77 (G77) na China na kwamba tunatamani ujizatiti zaidi kutetea maslahi ya umoja huu ambao wanachama wake wengi ni nchi zinazoendelea.”

Waziri Mkuu Majaliwa ameambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Tanzania nchini Urusi ambaye pia ni Balozi wa Azerbaijan, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi. 
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live


Latest Images