Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA MIRADI YA VIJANA MKOANI IRINGA

0
0
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kusindika Mbogaboga na Malimbichi cha EatFresh Bi. Hadija Jabiry (kulia) akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati walipotembelea kiwanda hicho kilichopo eneo la SIDO, Mkoani Iringa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha EatFresh wakiendelea na kazi ya kuchambua maharage mabichi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. (Wa tatu kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya Mkurugenzi wa Kiwanda cha EatFresh Bi. Hadija Jabiry (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kutembelea miradi ya Vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb) akieleza jambo wakati Kamati hiyo ilipokutana na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa kwa ajili ya kupokea taarifa kuhusu miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya ijana.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya vikundi vya vijana vilivyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mfuko huo.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya vikundi vya vijana vilivyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mfuko huo na kutembelea miradi ya vikundi vya vijana. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Ally Saleh (kulia) akichangia jambo kuhusu miradi itakayowanufaisha watu wenye ulemavu kunufaiaka na Mfuko huo wa Maendeleo ya Vijana.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (wa pili kutoka kulia) akieleza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipofanya ziara ya kutembelea miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mkoani Iringa. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb).
Kiongozi wa Kiwanda cha vijana cha EnviBright Bw. Paul Myovela (kulia) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria namna wanavyotengeneza mbolea inayotokana na taka ngumu.
Muonekano wa Kiwanda cha EnviBright kinachojihusisha na utengenezaji wa mbolea kupitia taka ngumu.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Mamia wajitokeza kufanyiwa uchunguzi saratani ya matiti

0
0
Dkt. Ndigwake Mallango (kulia) akimuelekeza Bi. Mekitilda Wamala jinsi ya kujifanyia uchuguzi wa awali wa saratani ya matiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila.
Mtaalam wa mionzi, mawimbi sauti na usumaku wa Hospitali ya
Mloganzila Mariam Ndosa (kulia) akichukua vipimo vya urefu na
uzito kabla ya Bi. Masha Jum kufanyiwa uchunguzi wa awali wa
saratani ya matiti.
Muwakilishi kutoka MEWATA mkoa wa Pwani Dkt. Deograsia
Mkapa akitoa elimu kwa kina mama kuhusu ugonjwa wa saratani
ya matiti, ambapo zaidi ya kina mama 200 wamejitokeza kwa ajili
ya kufanyiwa uchunguzi wa awali katika Hospitali ya Mloganzila
kati ya hao 45 wamekutwa na viashiria.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili- Mloganzila,
Dkt Julieth Magandi akiwa katika picha ya pamoja na watoa
huduma mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchunguzi wa
awali wa saratani ya matiti lililofanyika kwa siku mbili.

**************************************

Dar es salaam 27-10-2019

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha
Madaktari Wanawake Tanzania-MEWATA- imefanya zoezi la uchunguzi wa awali
wa saratani ya matiti bila malipo kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya ugonjwa
huo na kuhamasisha jamii umuhimu wa kujichunguza mapema.

Zoezi la uchunguzi limefanyika kwa siku mbili ambapo kina mama zaidi ya 200
wamehudumiwa huku 45 wakigundulika kuwa na viashiria vya saratani ya matiti
hivyo wanahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Daktari Bingwa wa Radiolojia kutoka MNH-Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu ametaja
huduma zilizotolewa kuwa ni elimu ya ugonjwa wa saratani ya matiti, dalili zake
na jinsi ya kujichunguza mwenyewe.

“Kujichunguza ni muhimu hasa kwa kina mama ambao ndio waathirika wakubwa
wa saratani ya matiti kutokana na uwepo wa vichocheo (Hormone) katika miili yao
ambavyo vinaweza kuchangia kupata ugonjwa huu’’ amesema Dkt. Sakafu.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka MEWATA ambaye pia ni Daktari Bingwa
wa magonjwa ya saratani Dkt. Sikudhani Muya, amesema tatizo la saratani ya
matiti ni kubwa na huathiri wanawake kati ya umri wa miaka 28 hadi 50 kwa
asilimia kubwa, na ni asilimia moja tu ya wanaume hukutwa na ugonjwa huu.

“Uchunguzi kama huu husaidia kugundua iwapo mtu anaviashiria vya saratani ya
matiti na kisha hufanyiwa uchunguzi wa kina na kupelekwa kwa madaktari bingwa
wa magonjwa ya saratani kwa hatua zaidi” amefafanua Dkt. Muya.

Saratani ya matiti ni ya pili katika saratani zinazowapata wakina mama hapa nchini
ya kwanza ikiwa ni saratani ya shingo ya kizazi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA SEMINA YA WABUNGE WANAWAKE WA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA

0
0
 Sehemu ya wajumbe wa  Tanzania katika Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, baada ya kufungua Semina hiyo Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Grand Malya Jijini Arusha.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Gran Malia Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Gran Malia Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa  Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, baada ya kufungua Semina hiyo Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Grand Malya Jijini Arusha.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika picha ya kumbukumbu  na Wajumbe wa  Semina ya Siku nne kwa Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu  Juu ya kuhamasisha Wajumbe Wanawake katika masuala mbalimbali ya kuboresha Ushirikiano wa Wanawake katika Michakato ya kuongeza Idadi  yao kwenye Vyombo vya Maamuzi  hususan Bungeni, baada ya kufungua Semina hiyo Jumla ya wajumbe kutoka Nchi 18 za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wanashiriki kwenye Semina hiyo iliyofunguliwa  leo 27 Octoba 2019 katika Ukumbi wa  Grand Malya Jijini Arusha.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


PanAfrican Energy Tanzania Limited yasaini makubaliano na Shirika la Tumaini la Maisha kusaidia watoto wenye saratani Lindi

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa PAET, Andy J Hanna (kulia) na Mwenyekiti wa bodi ya TLM Gerald Mongella (kushoto) wakisaini mkataba wa makubaliano kusaidia watoto wenye saratani mkoani Lindi.


Kampuni ya uzalishaji gesi ya PanAfrican Energy Tanzania Limited (PAET) imesaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Shirika la kuhudumia watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha (TLM) kwaajili ya kusaidia utoaji wa huduma za matibabu kwa watoto wenye saratani katika Hospitali ya rufaa ya Sokoine mkoani Lindi.

Makubaliano hayo yalisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PAET, Andy Hanna na Mwenyekiti wa bodi ya TLM, Gerald Mongella ambapo pande zote mbili zilieleza kuwa na imani na hatua hiyo ambayo ni mwanzo katika kufikisha huduma hiyo katika maeneo mengine ya nchi.

“Ushirikiano huu utasaida katika utambuzi wa magonjwa ya saratani kwa watoto hususani kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi hapa nchini baada ya kazi hii kufanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam. Tunafarijika kuunga mkono jitihada hizi ambazo ni msaada mkubwa kwa rika la watoto hapa Tanzania,” alisema Hanna.

Aliongeza “Ushirikiano huu utaanza na uanzishwaji wa kituo cha matibabu hapo mkoani Lindi ili kuleta huduma karibu na wahitaji.Tunaamini kuwa huu ni mwanzo tu wa ushirikiano utakaofanya kufikisha huduma hizi maeneo mengi ya nchi siku za karibuni.”

Msaada huu utasaidia kuhakikisha watoto wanapata matibabu bora na ya uhakika karibu na makazi yao.

Msaada huu wa PAET kwa TLM katika utoaji wa huduma za matibabu kwa watoto ni sehemu ya uwajibikaji kwa jamii ambapo kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa afya, kampuni inategemea kuleta mchango chanya katika kuokoa maisha ya watoto wenye saratani nchini.

Tumaini La Maisha, ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo lakutoa huduma za matibabu bure kwa watoto wenye wenye saratani nchini ili kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo.

PanAfrican Energy Tanzania (PAET) ni kampuni ya uzalishaji gesi asilia inayowajibika kulinda mazingira pamoja na jamii ikijidhatiti kuleta matokeo chanya katika ukuaji wa sekta ya gesi nchini kwa wateja pamoja na jamii zinazozunguka maeneo ya uendeshaji.

Ikiwa na shabaha ya afya na elimu, kampuni hii imeendelea kufanya uwekezaji kwenye sekta hizo huku ikichochea uvumbuzi, miradi yenye kuleta manufaa kwa nchi.

Miaka 20 ya kuwekeza kwenye sekta ya gesi nchini.

Kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa zaidi ya miaka 20, PanAfrican Energy ni kampuni yakitanzania inayoongoza katika uzalishaji,uwekezaji pampoja na uendelezaji wa gesi asilia nchini.

GALOS AZINDUA KITUO CHA UJASIRIAMALI JIMBO LA JANG’OMBE.

0
0
KATIBU wa Kamati Maalumu ya NEC,idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ndugu Cassian Galos Nyimbo akihutubia wananchi katika uzinduzi wa Kituo cha ujasiriamali Jang’ombe.
MWAKILISHI wa Jimbo la Jang’ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande,akizungumza katika hafla hiyo
KATIBU wa Kamati Maalumu ya NEC,idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ndugu Cassian Galos Nyimbo(wa pili kutoka kulia),akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha mafunzo ya ujasiriamali cha Jimbo la Jang’ombe,Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe.Ramadhan Hamza Chande( wa kwanza kushoto) na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Jimbo hilo ndugu Ali Ahmad Ibrahim(wa kwanza kutoka kulia).

BAADHI ya Waalikwa na wanafunzi wa kituo hicho wakisikiliza nasahas mbali mbali kutoka kwa viongozi wa JImbo la Jang’ombe.


**********************************

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati Maalumu ya NEC,idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ndugu Cassian Galos Nyimbo,amewataka Wanawake na Vijana wa jimbo la jang’ombe kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa kujiajiri wenyewe.
Wito huo ameutoa wakati akizindua Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali cha Jang’ombe kilichoanzishwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo uko Kilimani Mnara wa mbao Unguja.

Alisema ujasiriamali ni kazi kama zilivyo kazi zingine katika jamii hivyo ujuzi unaotokana na sekta hiyo unatakiwa kuthaminiwa na kupewa kipaumbele.Galos alieleza kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali watakayopewa wananchi wa jimbo hilo kupitia Kituo hicho yawe na tija ya kujikwamua kichumi na kujiongezea kipato.

Katika maelezo ya Katibu huyo, alimpongeza Mwakilishi huyo kwa ubunifu wake wa kuanzisha Kituo kitakachozalisha wataalumu wengi wa masuala ya ujasiriamali wenye uwezo wa kutengeneza bidhaa mbali mbali zenye viwango.

“Nakuombeni hiki kituo mkitumie vizuri kwani mkipata ujuzi wa masuala ya ujasiriamali mtakuwa mmejikomboa katika wimbi la umaskini na kuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe.”, alisema ndugu Galos.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande,alisema lengo la kuanzisha kituo hicho ni kuwapatia ujuzi wa masuala ya ujasiriamali wananchi wa jimbo hilo hasa vijana na wanawake.
Alisema wakati akiomba kura za wananchi wampatie ridhaa ya uongozi aliahidi kuanzisha kituo hicho na kwa sasa ametekeleza ahadi hiyo.

Alisema katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 imeelekeza uanzishwaji wa vituo vya mafunzo ya ujasiriamali nchini, hivyo jimbo hilo wametekeleza maelekezo ya Ilani.

Alisema kituo kimesajiliwa na kupitia taratibu zote za kisheria pia wana wakufunzi waliobobe katika kufundisha utengenezaji wa bidhaa bora zinakubalika katika soko la ndani na kimataifa.

Akitoa shukrani katika hafla hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini ndugu Kamaria Suleiman Nassor, aliwapongeza viongozi wa jimbo la Jang’ombe kwa ushirikiano wao uliozaa matunda ya kuanzisha kituo hicho kitakachowanufaisha Vijana.

Alisema vijana wa jimbo hilo wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga kituo hicho ili wapate ujuzi utakaowawezesha kutengeneza bidhaa zitakazowapatia kipato.

BARABARA YA KIVULE YAANZA KUJENGWA BAADA YA RC MAKONDA KUWASWEKA LUPANGO WAKANDARASI

0
0
 Katapila likisawazisha vifusi vilivyomwagwa wakati wa ujenzi wa barabara hiyo  katika kona ya Kitunda kwenda Kivule. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

 Daraja lililopo katika barabara hiyo ambalo ni takribani mwaka sasa ujenzi wake haujakamilishwa

 Katapila la Kampuni ya Nyanza likiwa kazini katika daraja hilo

 Kifusi kimwagwa tayari kwa ujenzi wa barabara hiyo

Kizuizi cha muda kilichichowekwa kurahisisha ujenzi


                              Na Richard Mwaikenda,Ukonga.


HATIMAYE Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza imeanza ujenzi wa Barabara ya Kitunda-Kivule, Ukonga Dar es Salaam, baada Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutoa amri ya kuwasweka lupango viongozi wa kampuni hiyo.


Makonda alitoa amri hiyo Dar es Salaam Alhamisi, baada ya kampuni hiyo iliyopewa zabuni ya kuchelewa kuanza ujenzi licha ya kulipwa malipo ya awali ya sh. bil. 4.8. Mkataba wa ujenzi umeanza Oktoba Mosi.


Akizungumza na vyombo vya habari, RC Makonda alisema kuwa wakandarasi hao, watakuwa akienda kujenga barabara hiyo wakitokea mahabusu.


Pilikapilika za ujenzi zimeanza ijumaa katika eneo la Kitunda, ambapo yalionekana makatapila yakikwangua sehemu ya barabara hiyo, huku mengine yakisawazisha vifusi vilivyokuwa vinamwagwa na malori.


Kampuni hiyo itajenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara chenye urefu wa km 3.2 kuanzia Kituo cha Polisi Kitunda hadi Mwembeni.


Ubovu wa barabara hiyo ya kutoka Banana, Kitunda hadi Kivule Fremu Kumi, imekuwa ni kero na kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo. Ujenzi wa kipande hicho cha barabara unatarajiwa kukamilika Oktoba  mwakani.


Kila msimu wa mvua kama huu barabara hiyo uharibika na kuwa na mshimo yanayosababisha daladala nyingi kusita kwenda huko, hali ambayo inawafanya abiria kulipa kiasi kikubwa cha nauli hadi sh.3000 kutoka Banana hadi Flemu Kumi kwa kutumia usafiri wa Bajaji na Bodaboda.

Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwaonea huruma kwa kuhakikisha ujenzi wa kipande hicho kukamilika haraka kabla ya mvua za masika, lakini pia kumalizia kipande kingine cha barabara kutoka Mwmbeni hadi Flemu kumi.





YANGA SC YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA WA KOMBE LA SHIRIKISHO DHIDI YA PYRAMIDS FC

0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Yanga imepoteza mchezo wake wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho, hatua ya mchujo baada yakukubali kipigo cha bao 2-1 mbele ya Pyramids FC ya Misri katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta mikuvute dakika zote 90, dakika ya kwanza mchezo ulianza kwa kasi zaidi kwa Yanga SC kuanza kwa spidi ya hali juu kwa kufanya mashambulizi ya hapa na pale kwenye lango la Pyramids.

Dakika ya Tisa ya mchezo, Ally Mtoni Sonso alipiga Shuti kali kwa guu la kushoto lilookolewa na Golikipa wa Pyramids, Ahmed Elshenawy kama ilivyo dakika ya 10, Kelvin Yondani kuokoa mpira kwenye chaki baada ya shambulizi golini kwa Yanga.

Dakika ya 38 ya mchezo, Beki wa Yanga SC, Ally Ally alitaka kujifunga mwenyewe  baada yakupishana na Kipa, Farouk Shikhalo kwa mpira mpira uliopigwa langoni kwao na Mchezaji wa Pyramids.

Dakika ya 42 ya mchezo huo, Pyramids FC walipata bao lililofungwa na Nyota wao, Eric Traory baada ya kupokea mpira safi ulitokea pembeni kwa lango la Yanga SC.

Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, Pyramids walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 katika dimba la CCM Kirumba Mwanza, Yanga SC wakiwa na mashabiki lukuki zaidi ya Pyramids FC.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa timu zote, Yanga SC walianza kulisakama lango la Pyramids, dakika ya 56, Feisal Salum (Fei Toto) anapiga Shuti kali lakini Golikipa wa Pyramids, Elshenawy anaruka juu juu nakuucheza mpira huo.

Katika kipindi hicho, Pyramids walirudi tena mchezoni dakika ya 59, Yanga SC wanapata kona dakika ya 61 lakini baada ya kona hiyo makosa ya Nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa yanapelekea Pyramids kupata bao la pili kupitia kwa Nahodha wao, Abdallah Elsaid kuunganisha pasi safi iliyotoka kwa Mohammed Farouq.

Mshambuliaji wa Yanga SC, Juma Balinya aliingia kuongeza nguvu katika mchezo huo kuchukua nafasi ya Feisal Salum baada ya Yanga kuwa nyuma kwa jumla ya mabao 2-0, dakika ya 71 pia Mrisho Ngassa anatoka na kuingia, Deus Kaseke wakati upande wa John Antwi aliingia upande wa Pyramids kuongeza nguvu zaidi na Nahodha Abdallah Elsaid kutoka nafasi yake kuchukuliwa na Ahmed Tawfiq.

Dakika ya 88 Yanga SC walipata baokupitia kwa Nahodha Pappy Tshishimbi baada yakuwalamba chenga Beki wa Pyramids nakufunga bao hilo. Hata hivyo, Beki wa Yanga, Kelvin Yondani alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada yakucheza rafu wakati timu hiyo ikiwa na shinikizo lakusawazisha bao wakiwa nyumbani.

Kwa matokeo hayo, Yanga SC watakuwa na kibarua kizito zaidi ugenini Novemba 3, 2019 kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo nakusonga mbele, Yanga SC wanatakiwa kupata ushindi zaidi ya mabao 3-1 ili kujihakikishia nafasi ya makundi ya Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup).

WAZIRI LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WABADHIRIFU WA VYAMA VYA USHIRIKA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kata ya Neruma, Wilayani Bunda, leo. Kushoto ni Mwenyekiki wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Isaac Mahela. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Kata ya Neruma,Wilayani humo, Deonatus Makongo.





Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiki wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isaac Mahela, wakati alipokuwa anawasili Wilayani humo, leo.
…………………….

Na Felix Mwagara, MOHA, Bunda.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwakamata viongozi wa vyama vya ushirika nchini ambao wamekuwa wakihujumu fedha za wakulima.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo, katika Mkutano wa Viongozi wa Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, jana, kufuatia Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili kuwakamata viongozi wa vyama vya ushirika walioshindwa kurejesha fedha za Serikali zaidi ya bilioni moja na milioni mia nne atua ambayo imemfanya.

“Nawaagiza Polisi kuendesha operesheni ya kuwakamata wabadhirifu wa fedha na mali mbalimbali za umma, na agizo hili si la hapa Bunda tu, bali nchi nzima, makamanda wawasake na kuwatia mbaroni ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia hizo,” alisema Lugola.

Pia Waziri Lugola, alitoa onyo kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika kote nchini kuwa Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara yake haitamuacha mtu salama atakayechezea fedha za Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alisema wamewakamata viongozi wa vyama vya ushirika walioshindwa kurejesha fedha za Serikali na watawafikisha mahakamani.

“Fedha za vyama vya ushirika zimeliwa, tukaamua kuwakamata watuhumiwa wote na tayari tumefanya hizo, na tutawafungulia mashataka ili iwe fundisho kwa wananchi ambao wanatabia ya kuchukua fedha za umma,” alisema Lydia.

Waziri Lugola yupo Wilayani Bunda kwa ajili ya ziara ya kikazi, kuzungumza na wananchi, na pia kutatua kero mbalimbali zinazohusu Wizara yake Wilayani humo.

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MASHINDANO YA MICHEZO NA SANAA KWA VYUO VYA UALIMU NCHINI

0
0
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini mapema hii leo mkoani Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi wa ualimu wakiandamana kuelekea katika uwanja wa Nangwanda mkoani Mtwara wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini mapema hii leo mkoani Mtwara.
Baadhi ya walimu wa vyuo vya ualimu na viongozi mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo picchani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini mapema hii leo mkoani Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi wa ualimu wakiingia katika uwanja wa Nangwanda mkoani Mtwara wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini mapema hii leo mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini mapema hii leo mkoani Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evodia Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini mapema hii leo mkoani Mtwara.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu nchini wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo mapema hii leo mkoani Mtwara.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na washiriki wa mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu
Picha na WHUSM – Mtwara

MBUNGE ELIBARIKI KINGU AONGOZA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SEKONDARI YA MIANDI IKUNGI SINGIDA

0
0
 Mgeni rasmi akimpatia zawadi ya madaftari mwanafunzi anayefanya vizuri kimasomo, Ashura Jumanne.
 Mgeni rasmi akinkabidhi cheti mhitimu, Peter Paul.
 Wazazi wakiwa katika  mahafali hayo.
 Mratibu wa sherehe ya mahafali hayo, Gedion Samuel akizungumza.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kituntu, Shabani Kilakunu akizungumza.
 Wanafunzi wakiwa katika mahafali hayo.
 Kiongozi wa dini ya kiislam wa kata hiyo, Ramadhan Hamli,  akiomba dua la kufunga hafla ya mahafali hayo.
 Mwalimu wa dini,Daniel Ngoi kutoka Kanisa la EPCT kijiji cha Miandi akiomba wakati wa kufunga sherehe za mahafali hayo.
 Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wahitimu.
Umati wa wanafunzi wazazi waliohudhuria mahafali hayo.

 Kijana wa Skauti, Benadeter Fadhil  wa Shule ya Sekondari ya Miandi iliyopo Wilayani Ikungi mkoani Tabora akimvika Skafu ngeni rasmi Wa mahafali ya nane ya kidato cha nne, Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu wakati alipowasili kwenye mahafali hayo mwishoni mwa wiki.
 Mbunge Kingu akilakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wazazi wakishiriki mahafali hayo.
 Wazazi wakishiriki mahafali hayo.
 Wanafunzi wa shule hiyo katika mahafali hayo.
 Viongozi wakiwa meza kuu.
 Wazazi wakishiriki mahafali hayo.
 Taswira ya mahafali hayo.
 Wahitimu wakiimba wimbo maalumu.
 Mshereheshaji  wa mahafali hayo Mwalimu, Hamad Selemani akiwajibika.
 Afisa Elimu wa Kata ya Kituntu, Kassim Mayoho akizungumza na wahitimu hao.
 Vijana wa Skauti wakiwa katika mahafali hayo.
 Afisa wa Shirika la Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) Mkoa wa Singida, Peragia Nshema akizungumza katika mahafali hayo.
 Mkuu wa shule hiyo wa zamani, William Ipini akizungumza.
 Vijana wa Skauti wakionesha umahiri wa kukanyaga miguu katika gwaride.
 Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Hajira Ramadhani,  akizungumza.
 Wahitimu wakionesha umahiri wa kucheza mziki.
 Mkuu wa shule hiyo, Juma Maatu akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi.
 Mgeni rasmi Elibariki Kingu akihutubia.

 Mgeni rasmi akiserebuka sanjari na wahitimu wa kidato cha nne.

TGNP MTANDAO YAKUTANA NA VIONGOZI WA CCM KISHAPU KUJADILI USHIRIKI WA WANAWAKE NAFASI ZA UONGOZI KWENYE UCHAGUZI

0
0
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) umeendesha mkutano na wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kishapu, kujadili ushiriki wa wanawake katika kuwa nia nafasi za uongozi kwenye uchaguzi.

Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 27, 2019 kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Maganzo wilayani Kishapu, ambao ulihudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya siasa ya CCM wilayani humo, ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Shija Ntelezu. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilayani Kishapu Shija Ntelezu, ameupongeza mtandao huo wa jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), kwa kutoa elimu za kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ili kuleta usawa wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi. Amesema kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawajitokezi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, lakini sasa hivi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi, na kubainisha chama hicho wilayani humo kimejiwekea mikakati ya kuwapatia kipaumbele wanawake ambao watakuwa wakitia nia ya kutaka uongozi.

 “Nalipongeza sana Shirika hili la TGNP Mtandao kwa kutoa elimu kwa wanawake kujitokeza kushiriki kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, ili kufikia 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi, ambapo na sisi kama CCM tumekuwa tukiliunga mkono, na ndio maana mwanamke akayetia nia tunampa kipaumbele,”amesema Ntelezu. 

Naye mjumbe wa kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo , amesema chama chao kinathamini sana usawa wa kijinsia, na kutolea mfano katika vijiji 117 wilayani humo ambapo kati ya vijiji 25 ambavyo walijitokeza wanawake kuchukua fomu za kuwania nafasi za uenyekiti wa kijiji, kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 24,2019 wamewapitisha wote kugombea nafasi hizo.

 Amesema hata katika nafasi za kuwania ujumbe, kama kuna watu nane wanataka nafasi hiyo wakiwemo na wanawake wawili, lazima wapitishwe wanawake hao, na baada ya hapo ndipo wanaanza kuchagua wanaume ili kujazia nafasi. Aidha mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) CCM wilayani Kishapu Rahel Madundo, amewapongeza wanawake ambao wamejitokeza kuwa nia nafasi za uongozi kweye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, na kutoa wito pia wajitokeza kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu mwakani. 

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao EvaHawa Juma, amesema wameendesha mkutano huo na wajumbe wa kamati hiyo ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi CCM wilayani Kishapu, ambapo jana wamefanya na vyama vingine vya siasa, na kubainisha lengo lake kubwa ni kutoa nafasi kwa wanawake kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi. 

Amesema wanawake wamekuwa wahawajitokezi kwa wingi kuwania nafasi hizo za uongozi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo na kukatwa majina yao, kutopitishwa kwenye kura za maoni ndani ya chama, kutokana na imani iliyojengeka ni viumbe dhaifu hawawezi uongozi, na ndiyo maana wanatoa elimu kwa viongozi wa vyama vya siasa, ili kuitokomeza dhana hiyo na kumpatia nafasi mwanamke kugombea uongozi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani kishapu Shija Ntelezu akifungua mkutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao)pamoja na wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilayani Kishapu, ili kujadili ushiriki wa wanawake kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Katibu wa CCM wilayani Kishapu Helena Chacha akiupongeza mtandao huo wa Jinsia Tanzania -TGNP Mtandao Kwa kutoa elimu ya kuwajengea ujasiri wanawake kushiriki kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, na kutoa wito elimu hiyo iendelee kutolewa zaidi. Mwanaharakati kutoka mtandao huo wa jinsia Tanzania (TGNP) Eva Hawa Juma, akielezea madhumuni ya mkutano huo na viongozi wa vyama vya siasa. Wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa TGNP Mtandao. Wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa TGNP Mtandao. Wajumbe wa Kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa TGNP Mtandao. Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Gregory Kibusi akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Boniphace Butondo akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Joseph Kwilasa akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Rahel Madundo akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Kashinje Bulugu akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu Jiyenze Sheleli akichangia mada kwenye mkutano wao na TGNP Mtandao juu ya ushiriki wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi. Wajumbe wakiendelea kuchangia mada, na kuwataka wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, ukiwemo uchaguzi mkuu 2020. Kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanaharakati kutoka mtandao wa TGNP mara baada ya kumaliza mkutano wao, huku mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu katikati akiwa ameshika kitabu cha ilani ya uchaguzi kwa wanawake. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Mchungaji Dkt Kipangula Tunataka Viongozi Wenye Sifa Kama Rais Dkt Magufuli

0
0
Mkuu wa eneo la maandalio la kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayoyosi ya Mufindi Mchungaji Dkt Antony Kipangula (wa pili kushoto ) akiwa ameshikana mikono na wachungaji na viongozi wa dayosisi hiyo jana kuonyesha umoja wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kutengwa kwao na dayosisi ya kusin
Mhubiri wa kimataifa kutoka Israel,Rabbi Abshalom akihubiri katika mkutano wa injili kijiji cha Ikongosi Mufindi ulioandaliwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzani (KKKT)eneo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi juna (PICHA NA FRANCIS GODWIN)
Wachungaji na viongozi wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) eneo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi wakiwa katika mkutano wa injili kijiji cha Ikongosi wakimsikiliza mhubiri wa kimataifa kutoka Israel ,Rabbi Abshalom(hayupo pichani) jana
………………..

NA Francis Godwin , Iringa 

MKUU wa eneo la maandalio la kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Mufindi mkoani Iringa Mchungaji Dkt Antony Kipangula amewataka wakristo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ili kupata viongozi wenye sifa za kizalendo watakaofanya kazi na Dkt John Magufuli ya kuwaletea maendeleo watanzania pasipo ubinafsi na kuendekeza migogoro.

Akizungumza jana wakati wa kilele cha mkutano mkubwa wa injili ulifanyika katika kijiji cha Ikongosi chini ya mhubiri wa kimataifa Rabbi Abshalom kutoka Israel , jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli zinaliletea heshima kubwa Taifa na kila mtanzania anaona kasi kubwa ya maendeleo ambayo imekuwa ikifanywa na serikali katika kuliwezesha Taifa kujitegemea pasipo kutegemea wahisani .

Hivyo alisema mwendo huo ambao Rais Dkt Magufuli amekuwa akiendanao katika kuliwezesha Taifa kupiga hatua ni vema watanzaia kama walivyojitokeza kwa wingi kujiandikisha na viongozi wa dini kama walivyohamasisha waumini wao kujiandikisha ndivyo wanapaswa kufanya uhamasishaji mkubwa wa watu kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali na siku ya kupiga kura kila mmoja kufika kituoni kuchagua kiongozi mwenye sifa ya Rais Dkt Magufuli ya kuwatumikia wananchi na wale wasio na sifa wasiwapigie kura .

“ Eneo la dayosisi yetu ya maandalio dayosisi ya Mufindi tumejiwekea mkakati wa kila jumapili tunapokutana katika ibada zetu kuwa na kipengele cha kuwaombea viongozi wetu akiwemo Rais ,makamu wa Rais waziri mkuu ,mawaziri ,wakuu wa mikoa na wilaya na hadi viongozi wa ngazi za vitongoji lengo la kufanya hivyo ni kumwomba Mungu awaongoze katika utendaji kazi wao wa kila siku na wasijikwae katika kuwatumikia watanzania na tumekuwa tukiona unyofu nauadilifu wa Rais wetu katika kuwatumikia watanzania “ alisema Dkt Kipangula

Kuwa hakuna mtu ambae ambae haoni kazi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt Magufuli kwenye utawala wake miradi mikubwa ya kimaendeleo imefanyika kwa miaka hii mitano kwa kuwa na ndege za kutosha ,reli imeimarishwa , mradi mkubwa wa umeme Rufiji , miundo mbinu ,afya ,elimu bila malipo na mambo mengi makubwa ambayo yote hayo yanafanyika kutokana na uzalendo mkubwa kwa Taifa ambao Rais ameonyesha .

Alisema pamoja na kuendelea kuliombea Taifa kuzidi kuwa na mshikamano na umoja bado jukumu la kila mtanzania kuendelea kumuombea Rais afya njema na wale wasiolitakia mema Taifa kwa kutoa maneno yasiyo faa kwa serikali na Rais kuombewa ili roho mbaya kwa Taifa zisiweze kujiinua .
Mchungaji Dkt Kipangula alisema watu wenye roho mbaya sasa wameanza kuingia hadi kwenye nyumba za ibada kwa kutengeneza migogolo na chuki jambo mbalo ni hatari na serikali haina budi kuingilia kati kwa kuchukua hatua za haraka pale penye chuki na migogolo maana migogolo ndani ya nyumba za ibada ni mibaya zaidi na inajenga chuki mbaya zaidi na kama amani haitakuwepo kwenye nyumba za ibada ni vigumu Taifa kuwa na amani .

“ Mfano KKKT dayosisi ya Kusini kwa sasa ipo kwenye mgogolo na jimbo la Mufindi ambalo sasa ni eneo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi toka mwaka 2015 ilipotengwa na uongozi wa juu ya dayosisi ya kusini ila kwa kuwa tunamwamini Mungu sisi Mufindi tumesimamia imara na kuupa kisogo mgogolo huo pamoja na kutengwa kwetu sisi kazi ya Mungu inasonga mbele tena kwa kufanya mambo makubwa zaidi kufanya kazi ya kitume tuliyotumwa kuifanya na kuhubiri injili isonge mbele “
Aidha alisema jukumu la kuliombea Taifa na viongozi wake ni la dini zote na kila mtanzania anawajibu wa kumuombea Rais na serikali pia kila mmoja ana nafas ya kukemea wale wanaovuruga amani ndani ya nyumba za ibada na nje ya nyumba za ibada maana nchi hii ni moja amani ikivurugika wote tutaangamia .

Kwa upande wake mchungaji mstaafu wa KKKT Antony Mabena alisema kuwa kutengwa kwa waumini wa jimbo la Mufindi na dayosisi ya kusini kwao si hoja kubwa ya kushindwa kumwabudu Mungu na kuwa kwa kuwa wanamwamini Mungu si mwanadamu mambo yote ya ibada na maendeleo ya eneo hilo la maandalio ya dayosisi ya Mufindi yanakwenda vizuri .

Alisema Mungu si wa machafuko wala chuki bali ni Mungu wa upendo na mshikamano na kutengwa na mwanadamu si tija kwani Mungu ni wa upendo hivyo wamesimama kidete kwa kuwa wanajua wanayemtegemea si mwanadamu ni Mungu .

Martine Ngwembe mwenyekiti wa mchakato wa jimbo la Mufindi kuelekea kuwa dayosisi ya Mufindi kuwa wanaamini kabisa kupiga hatua mbele kwa kumtanguliza Mungu na tayari hata kama bado mkuu wa KKKT hajabariki rasmi Mufindi kuwa dayosisi ila kazi zinazofanyika kwa kimaendeleo ni kubwa na zinazidi hata zile za dayosisi yenyewe na kuwa wao lengo ni kusonga mbele na hawataangalia nyuma wasije wakageuka jiwe la chumvi.

Alisema kuna hoja ya askofu mstaafu wa dayosisi hiyo Isaya Mengele kuwa kuna wachungaji 18 ambao amewakabidhi kwa askofu mpya kuwa hoja hiyo haina ukweli kwani wachungaji 18 anaosema ni wale alioagiza polisi wakamatwe na kuwekwamahabusu Octoba 6 mwaka 2015 kituo cha polisi cha Mdandu ambao bado wako huko kwani hakuna aliyekwenda kuwatoa .

Hivyo alisema hakuna sababu ya kuwatambua wachungaji hao wakati hakuna kiongozi aliyekwenda kuwatoa polisi wala kuwa na mawasiliano na jimbo la Mufndi hadi leo na mkutano mkuu huo wenye maamuzi ya juu jimbo la Mufindi halikushirikishwa na hadi leo hakuna ushirikiano wowote hivyo ndio maana wapo kwenye eneo la maandalio ya dayosisi yao ya Mufindi chini ya uangalizi wa askofu wa mstaafu wa dayoyosi ya Iringa

ROSTAM, Dogo janja WAFUNIKA Tigo fiesta saizi yako 2019 Arusha

0
0


Msanii wa Bongofleva Roma akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana Jijini Arusha.
Msanii wa Bongofleva Mario akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana Jijini Arusha.
Roma na Stamina Wasanii wanaounda kundi la Rostam wakitumbuiza katika jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana Jijini Arusha
Msanii Rosaree akitumbuIza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo Arusha
Msanii wa bongoflava Jux akiwa jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo jijini Arusha.
Msanii wa bongoflava DogoJanja akinogesha wimbo na Roma jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia Leo Arusha.



NA Ally Mvungi, Arusha

TAMASHA la Muziki, Msimu wa Tigo Fiesta2019 jana liliwafurahisha wana chugga kwa kishindo jijini Arusha huku Rostam likifunika kwa kuwapagawisha washabiki luluki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Mbali na wasanii hao kukonga vilivyo nyoyo za washabiki wa muziki wa kizazi kipya wasanii wengine walikuwa Rosa Ree, Juma Jux,Ruby, Country boy,Fid Q,Weusi.

Washabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid walishindwa kujizuia kutokana na makamuzi ya nguvu yaliyowaacha hoi yaliyofanywa na kundi la Rostam, na huku Dongo janja akijiunga nao kufanya makamuzi ya kipekee.

Tamasha hilo limefanyika Arusha lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa ambapo mashabiki kutoka viunga vya jiji hilo la kitalii walisuuzika nyoyo na mara kadhaa walishiriki kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali hasa kundi la Rostam.

Akizindua tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema waandaaji wa Tigo Fiesta 2019 kwa ubunifu na uamuzi wao wa kuzindua tamasha hilo hawakukosea ikizingatiwa jiji hilo ni kitovu cha utalii kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati.

“Arusha ni kisima cha burudani kutoka na kuwa na wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya hivyo niwapongeze Clouds na Tigo kwa ubunifu wao wa kuandaa na kuzindua tamasha lao hapa.Sisi kama mkoa tutaendelea kuwaunga mkono.Pia tamasha hili mbali na kutoa burudani lina umuhimu kiuchumi, linatoa ajira za muda mfupi,linaongeza kipato cha wananchi wetu na waandaaji nao wananufaika,”alisema Gambo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba, kampuni hiyo ya mawasiliano itaendelea kushirikiana na kuiunga mkono Clouds ili kuhakikisha wanawapatia Watanzania burudani yenye vionjo na ladha tofauti tofauti.

Tamasha hilo sasa linaelekea mjini Tanga.

Trump atangaza kuuawa kwa kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdadi Syria

0
0
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuuawa kwa kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) kaskazini magharibi mwa Syria.

Akizungumza kutoka Ikulu ya White House, bwana Trump amesema Abu Bakr al-Baghdadi alijilipua wakati alipozingirwa na kikosi maalum cha Marekani.

Katika hutuba isioyakawida siku ya Jumapili , Rais Trump alisema Baghdadi alikufa baada ya ya kufika ukingoni alipokuwa akitoroka huko "akilia na kupiga mayowe wakati anafukuzwa na mbwa wa Marekani".

Baghdadi wakati huo alikuwa anatoroka akiandamana na watoto wake watatu wadogo ,lakini hatimae akajilipua kwa bomu alilokuwa amevaa baada ya kugundua kuwa amezingirwa. 

Katika mlipuko huo Baghdadi na hao watoto wake wote watatu walifariki papohapo.Rais Trump alisema japo mwili wa Baghdadi ulikuwa umechanika lakini waliweza kumtambua baada ya kuufanyia uchunguzi.

"Jambazi ambae alijitahidi sana kuwaogofya na kuwahangaisha wengine siku zake za mwisho alionekana mwenye mahangaiko ,taharuki kubwa na kuchanganyikiwa ,alionekana mwenye uoga kupindukia alipogundua kikosi cha Marekani kilikuwa kinamkaribia , Rais Trump alisema.

Baghdadi alipata umaarufu mwaka 2014, alipotangaza kubuniwa kwa "himaya ya Kiislamu" katika maeoneo Iraq na Syria.Wapiganaji hao walianzisha utawala wa kikatili dhidi ya watu wapatao milioni nane katika maeneo waliokuwa wanayashikilia. 

Kundi hilo pia linalaumiwa kwa kufanya mashambulizi kadhaa katika miji mbalimabli duniani.Kundi hilo la IS linalaumiwa kwa udhalimu pamoja na maovu yaliyosababisha vifo vya maelefu ya watu

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi

0
0
Real Madrid iko tayari kuipatia Manchester United £90m pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30, ili kumsajili Paul Pogba, lakini inataka mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kuimarisha kiwango chake cha mchezo uwanjani . (El Desmarque, in Spanish)

Real Madrid ina mpango wa kumuuza mshambuliaji Bale na kiungo wa Colombia James Rodriguez 28 ili kupata fedha za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylina Mbappe 20. (Calciomercato)

Wakati huohuo, rais wa Real Madrid Florentino Perez ana mpango wa kufanya kila kitu katika uwezo wake ili kumnyakua Mbappe katika uwanja wa Bernabeau msimu ujao. (AS)

Bayern Munich inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa beki wa Atletico Bilbao na Uhispania Unai Nunez na wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal na Everton. (Goal.com)


TASWIRA YA MJI WA LINDI KUTOKA ANGANI

BALOZI KAIRUKI AYAKARIBISHA MAKAMPUNI YA SADC KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI SOKO KUBWA LA SASC NDANI YA JIMBO LA JIANGSU-CHINA

0
0
Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ua SADC Bi Mapolao Mokoena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Ndugu Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana  na fursa za soko kubwa la SASC lenye idadi ya watu milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alitoa mada kuu ambapo alielezea mazingira ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini, utalii nk.  

Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80.  Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda. Habari/Video kwa hisani ya Mdau Phelista Wegessa.

KIFO CHA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MTOA MACHOZI MBUNGE ELIBARIKI KINGU

0
0
 Wakina mama wakiwa kwenye dua hiyo.
 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu (katikati) akishiriki dua hiyo.
 Katibu wa Msikiti Mkuu Kata ya Sepuka, Juma Mwango akizungumza kwa huzuni.
 Mmoja wa wanafamilia ya marehemu, Ahmed Shabani akilia kabla ya kuanza kwa dua hiyo.
 Vijana wakilia.
 Ni  vilio.
 Ni huzuni tu
 Wazee wakiwa na huzuni wakati wa dua hiyo
 Mwalimu wa Msikiti wa Mtunduruni mjini Singida, Hamisi Ndida akizungumza.
 Wakina mama wakiwa kwenye dua hiyo.
 Ni huzuni tupu.
 Diwani Mstaafu wa Kata hiyo, Juma Ntandu akizungumza.
 Vijana wakiwa wamebeba chakula kwa ajili ya dua hiyo.
Waombolezaji wakiwa kwenye dua ya kumuombea Mzee Jumanne Njoghomi aliyefariki Oktoba 22 nyumbani kwake Kata ya Sepuka mkoani Singida. Marehemu enzi za uhai wake alikuwa ni  aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Musini Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka 15.

Na Dotto Mwaibale, Singida

KIFO cha Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji Cha Musini na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Sepuka Mkoani Singida,  Mzee Jumanne Njoghomi kimeleta simanzi kubwa kwa watu waliokuwa wakimfahamu na kumtoa machozi Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu wakati wa kumuombea dua marehemu.

Wengine walioshindwa kujizuia na kuanza kulia kufuatia kifo cha mwenyekiti huyo ni pamoja na wazee,vijana,wanawake na hali hiyo imetokana na uchapaji kazi, ukarimu na upendo aliokuwa nao kiongozi huyo kwa wananchi.

Mbunge Kingu akimuongelea marehemu katika dua hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki alisema kifo chake kimewagusa watu wengi pamoja na yeye kwani alikuwa ni mshauri wake kwa mambo mengi.
"Huyu mzee kwangu alikuwa ni baba na mshauri wangu kwa kweli nimepata pigo sana nashindwa namna ya kumzungumzia" alisema Kingu huku akitokwa machozi.

Mkazi wa kata hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lissu alisema hakika kila mtu atavuna alichokipanda akiwa hapa duniani kwani mzee Njoghomi alipanda mema na yameonekana baada ya kifo chake hivyo watu tuliopo baki duniani hatuna budi kujichunguza na kubadilika kwa kutenda mema ya kumpendeza mwenyezi mungu.

Ahmed Shabani akizungumza katika dua hiyo alisema ni wakati wa kila mtu kubadilika na  kuachana na vitendo vinavyomchukiza mwenyezi mungu kama kugombea ardhi,uchoyo,wizi,dhuluma na kujivuna kutokana na utajiri na kueleza kuwa vyote hivyo tutaviacha hapa duniani.

Mwalimu wa Msikiti wa Mtunduruni uliopo Singida mjini, Hamis Ndiba alisema alichopanda marehemu enzi za uhai wake ndicho kinachojidhihirisha baada ya kifo chake kwani alikuwa mnyenyekevu kwa watu wote na msuluhishi wa migogoro mbalimbali katika mkoa huo.

" Marehemu enzi za uhai wake hakumbagua mtu awe mkristo au muislam aliwasikiliza na kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kuwajulia hali wagonjwa na kuhudhuria misibani hakika tumempoteza mtu ambaye alikuwa muhimu sana kwetu" alisema Ndiba.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sepuka, Juma Mghenyi alisema marehemu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Musini Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka 15 na mpaka anafikwa na mauti alikuwa ni mjumbe wa kamati ya siasa wa kata hiyo..

KARIBU MGENI:RC GAMBO ALIVYOMPOKEA MISS WORLD JIJINI ARUSHA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimpa zawadi ya maua Miss World, Vannesa Ponce mara baada ya kuwasili mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kulia ni Miss Tanzania, Sylivia Sebastian.

MNUSO WA JUMUIYA YA WATANZANIA JIJINI NEW YORK KUMUAGA BALOZI MERO

0
0

Mwenyekiti wa NYCT, Bwana Seif Akida akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu Mh. Balozi Mero, Balozi Mero anaestahafu baada ya kufanya kazi kwenye majengo ya Umoja wa Mataifa New York kama mwakilishi wa kudumu. Community ya Watanzania New York inathamini sana mchango wake wa kujitoa kwa hali na mali kila alivyopata nafasi ya kuudhulia sehemu mbalimbali ndani ya community. Community ya Watanzania New York itamkosa sana na inamtakia maisha mema na afya njema huko nyumbani Tanzania.


Mwenyekiti wa NYCT Bwana Akida akimkaribisha Mh. Balozi.

Mh. Balozi Mero akiongea mbele ya Watanzania waliojitokeza kuja kumuuga.
Mh. Mero kipata ukodak na viongozi walioteuliwa kujaza nafasi ambazo zilikuwa wazi.

Zawadi kutoka New York Tanzania Community kwa Mh. Balozi. Balozi Mero ulikuwa mtu wawatu na chapa kazi, kwa picha zaidi nenda chini.


Mama Balozi akiwaaga wanacommunity.

Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images