Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Wakurugenzi wa Halmashauri Watakiwa kutenga Fedha za Kutokomeza Mazalia ya Mbu

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Dorothy Gwajima akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wanaohusika katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini katika ukumbi wa Morena jijini Dodoma Meneja Mpango wa Kudhibiti Malaria nchini Dkt Ali Mohamed akizungumza kwenye mkutano huo Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wanaojihusisha na udhibiti wa malaria nchini wakimsikiliza Dkt Gwajima leo jijini Dodoma



………………..

Na Mathew Kwembe

Wakurugenzi wa Halmashauri wametakiwa kutenga fedha katika mipango ya bajeti za halmashauri zao kwa ajili kununulia dawa ya kupulizia wadudu wanaosababisha magonjwa mbalimbali nchini ukiwemo ugonjwa wa malaria, kama mkakati mmojawapo wa kuhakikisha kuwa Tanzania inatokomeza ugonjwa huo nchini kutoka maambukizo ya asilimia 7.3 hivi sasa hadi asilimia 1 ifikapo mwaka 2030.

Sambamba na hilo, Wakurugenzi wa halmashauri wametakiwa kulipa madeni yao baada ya kuchukua dawa za kupulizia wadudu katika kiwanda cha kutengeneza dawa hizo kilichopo kibaha, mkoani Pwani.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt Dorothy Gwajima mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wanaohusika katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini.

Amesema hatarajii katika bajeti zijazo, kuona halmashauri hazitengi fedha kwa ajili ya kudhibiti na kutokomeza mazalia ya mbu katika halmashauri zao kwani hazitapita.

“Haitapita bajeti ya halmashauri kama haitaweka mikakati ya kudhibiti Malaria sambamba na maelekezo tuliyokuwa tukiyapeleka na mafunzo ambayo tumekuwa tukiyatoa,” amefafanua.

Dkt Gwajima ameongeza kuwa ni muhimu fedha hizo zitengwe ili zitumike katika kutokomeza mazalia ya mbu kwani wataalamu wa halmashauri wanajua ni maeneo gani ya halmashauri yenye mazalia mengi ya mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria.

“Kwa hiyo lazima ionekane pale ni kiasi gani cha dawa kitaagizwa kutoka katika kiwanda chetu cha kibaha kinachozalisha dawa zinazotumika kupulizia kwenye mazalia ili kudhibiti ongezeko la wadudu hawa,” amesema na kuongeza:

“Wakurugenzi hawa walichukua hizi dawa kibaha hawajalipa, kwanza walipe deni, kisha wapange kwenye bajeti zao kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika.”

Amesema kuwa ni jukumu la wataalamu kuainisha maeneo yenye mazalia mengi ya mbu ili dawa zitakazonunuliwa ziweze kutumika vizuri, badala ya kupuliza kila eneo.

Amesema kuna maeneo kwenye halmashauri ambayo yanajulikana kabisa ndiyo yenye mazalia ya mbu na kwamba dawa ikipulizwa kwenye maeneo hayo tatizo linakwenda chini.

Akizungumzia zaidi kuhusu hali ya maambukizo ya ugonjwa wa malaria nchini Dkt Gwajima amesema jitihada zinazofanyika kutokomeza ugonjwa huo nchini zinafanikiwa kwani maambukizo ya malaria nchini yamepungua hadi asilimia 7.3 kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015/16.

Amesema kupungua kwa maambukizi ya malaria kumetokana na kuwepo kwa mikakati mbalimbali ya kinga pia uwepo wa dawa zinazotumika kupambana na ugonjwa huo ambapo kiwango cha matumizi yake kilifikia asilimia 98.4, huku matumizi ya kipimo cha haraka cha kupima vijidudu vya malaria (mRDTs) ikifikia asilimia 97.8, lakini pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya vyandarua vyenye dawa kwa asilimia 62.5 mwaka 2017 kulinganisha na asilimia 55.9 mwaka 2015/16.

Kwa upande wake Meneja Mpango wa kudhibiti Malaria nchini Dkt Ali Mohamed amesema kulingana na takwimu za mwaka 2017, mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mara,Lindi, Ruvuma na Mtwara inaonekana kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria.

Amesema kutokana na takwimu hizo, maeneo hayo yanayoonekana kuwa na kiasi kikubwa cha maambukizi ipo haja ya kupelekwa mikakati ya ziada mbali na mikakati ya kawaida ya kuzuia mbu, kuhakikisha kuna vitendanishi vya kupima malaria na dawa za kutosha zina ubora unaotakiwa.

Ameitaja mikakati ya ziada ni jinsi ya kutumia dawa kinga (SP) kwa ajili ya wanafunzi shuleni, pia kutoa dawa katika maeneo ambayo malaria inapatikana kwa kipindi kichache, na mikakati mingine ambayo hufanywa na Mpango wa kudhibiti Malaria nchini.

Juhudi za kuutokomeza ugonjwa wa malaria nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla bado una safari ndefu kwani kwa mujibu wa taarifa ya dunia ya malaria ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa zimeripotiwa kesi milioni 219 za malaria duniani na kusababisha vifo 435,000.

Kadhalika barani Afrika, kati ya kesi zilizoripotiwa asilimia 70 zinatoka Afrika na idadi ya vifo asilimia 71 pia inatoka barani Afrika hasa katika nchi kumi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania. Nchi nyinginezo ni Burkina Faso, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, Mali, Msumbiji, Niger, Nigeria na Uganda.


IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 24,2019

$
0
0

                 

SERIKALI YATENGA BILIONI 201 KWA AJILI YA UBORESHAJI WA ELIMU NCHINI

$
0
0
Serikali kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) imetenga takribani shilingi bilioni 201 kwa ajili ya awamu ya nane ya uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya shule nchini

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako Wilayani Chato wakati wa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule za msingi na sekodari zinazokarabatiwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ambapo amesema suala la ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya shule ni endelevu. 

“Ujenzi au uboreshaji wa miundombinu ni suala endelevu na ukiangalia katika kipindi cha uongozi wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli katika upande wa miundombinu mpaka sasa kwenye mradi wa EP4R tumeshatumia bilioni 306 ambapo zimefanya ujenzi wa madarasa katika awamu saba, ” amesema Profesa Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema katika awamu ya nane ya Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kipaumbele kitakuwa kwa Halmashauri ambazo zimepewa fedha na kufanya vizuri katika usimamizi wa fedha katika awamu zilizopita na zile ambazo hazikufanya vizuri zitapatiwa fedha baada ya kushughulikiwa wale wote ambao wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa miradi hiyo. 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Chato Charles Kabeho ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa fedha zaidi ya Bilioni 1.3 kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya shule na ukamilishaji wa maboma yaliyokuwa katika hatua mbalimbali wilayani humo.

"Kwa Kweli fedha hizi zimetusaidia tumeweza kutatua changamoto ya miundombinu iliyojitokeza baada ya sera ya elimu bila malipo kijitokeza,"alisema Mkuu wa Wilaya hiyo

Mhandisi Kabeho amesema wilaya ya Chato itaendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza katika kuchangia nguvu kazi katika uboreshaji wa miundombinu ya shule ili kuhakikisha nao wanachingia katika uwekezaji wa elimu bila malipo ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

Naye Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jikomboe Valentina Geofrey amemshukuru Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa Januari alipotembelea shule hiyo ya kuwajengea ukuta kuzunguka shule pamoja na bwalo la chakula ambavyo kwa kiasi kikubwa vinakwenda kupunguza changamoto ambayo wamekuwa wakikutana nazo. Aidha, Mwanafunzi huyo amemuomba Waziri kuwasaidia kuwajengea maabara za sayansi ili waweze kusoma masomo ya sayansi yatakayowawezesha kushiriki katika azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.

Naye mmoja wa wazazi Elizabeth Lukanyima ameupongeza uongozi wa serikali ya Awamu ya Tano kwa uboreshaji wa miundombinu ya shule na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao ili waweze kupata elimu iliyobora na kuweza kushiriki katika ujenzi wa nchi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Ndalichako katika ziara yake ya kukagua miradi ya elimu katika Halmashauri ya wilaya ya Chato ametembelea na kukagua ujenzi wa ofisi ya Uthibiti ubora wa shule, ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari ya Jikomboe, Bwina na shule ya msingi Chato aliyosoma Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Pamoja na ujenzi wa majengo mapya katika shule ya msingi ya Chato unaofanywa na Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo (EP4R), Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu na ofisi mbili za walimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Dada Mkuu wa shule ya sekondari Jikomboe Vaertina Geofrey kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ya kuwezesha kupika pilau na kuku kwa muda wa siku tatu baada ya kufurahishwa na ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo ambao walipata daraja la kwanza na la pili tu.

KUMBUKUMBU YA DAFROSA SABINUS KWEKA

$
0
0


Dafrosa Sabinus Kweka
1970 - 1999

Ni miaka ishirini(20) sasa toka
umerudi kwa baba.

Ninapokosa maneno yako ya busara na
hekima, ucheshi na ujasiri.

Ninakukumbuka sana na kukuombea mimi
mtoto wako wa pekee Jesca, pia

unakumbukwa sana na mume wako
mpendwa, Ibrahim Msengi, kaka zako
Festo na Thade, dada zako Jane, Eugenia,
Elizabeth na Cesilia pamoja na Mjukuu
wako Dafrosa Michael Chenza.

“Msijisumbue kwa neno lolote, bali
katika kila neno kwa kusali na
kuomba pamoja na kushukuru,
haja zenu zijulikane na

Mungu.” Fil: 4:6

PINDA AIMWAGIA SIFA SERIKALI AWAMU YA TANO UTEKELEZAJI MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO YA KUAKISI UCHUMI WA VIWANDA.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesifu Serikali ya awamu ya tano kwakuendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016 /2021 kwa kukuza uchumi wa viwanda hali ambayo itafanya wananchi kuondokana nan a umasikini kutokana na viwanda hivyo kutumia malighafi zilizopo nchini.

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliyasema hayo wakati akifunga maonesho ya bidhaa za viwandani vilivyoko Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Kibaha Mjini.

Amesema, moja ya mpango huo ni ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam- Morogoro na makutopora na kwamba kukamilika kwake itakuwa na mchango mkubwa kwa Taifa ambapo mkoa wa Pwani utakuwa umepata fursa kubwa itakayokuwa inawasaidia wawekezaji wake katika kufanya biashara kutokana na mnyororo wa usafiirishaji.

Pinda amesema uwepo wa Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kwa kuwa na ndege mchango wake mkubwa kwa faida ya maendeleo ya Taifa na kuiingizia nchi fedha za kigeni kutokana na wafanyabiashara wengi kuja nchini kwa ajili ya uwekezaji pamoja na fursa za utalii.

" Baadhi ya watu walikuwa wanasema maneno ya hovyo sana,mara vindenge vyenyewe vidogo,havijazi watu na maneno mengine mengi ya kubeza juhudi hizo lakini sasa hivi watu wanaruka moja kwa moja kutoka India kwa ndege hizohizo kwahiyo lazima tukubali matokeo,"alisema Pinda

Mbali na miradi lakini alisema Rais Magufuli ,anajenga mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere huko Rufiji Mkoani Pwani ambao kukamilika kwake utakuwa na uwezo wa kufua umeme zaidi ya megawati 2000 ambao utasaidia kuboresha mazingira ya uendeshaji kwa wamiliki wa viwanda nchini.

Alisema kuwa,mradi huo wa umeme ulibuniwa miaka mingi ya nyuma tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini Rais Magufuli amefanikiwa na sasa anajenga kwa fedha nyingi kwahiyo lazima watu wakubali matokeo hayo ya maendeleo na ikiwezekana waunge mkono juhudi za Serikali.

Hatahivyo,Pinda alizipongeza taasisi wezeshi kwa namna zilivyojipanga kuendeleza shughuli za uwekezaji wa viwanda hapa nchini kwakuwa jambo hilo litasaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ,alisema chimbuko la maonesho hayo limetokana na wamiliki wa viwanda kuonyesha changamoto za ukosefu wa masoko kupitia bidhaa wanazozalisha na hata kutofahamika kwa Wananchi.

Ndikilo,alisema malengo mahususi ni kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya mkoa wa Pwani pamoja na kusaidia kutafuta masoko kwa bidhaa hizo na kwamba mpaka maonesho hayo yanakamilika zaidi ya watu 10,000 wametembelea.

alisema kuwa,kupitia maonesho hayo wawekezaji wamepata masoko mbalimbali na hata baadhi ya wananchi wamenufaika kwa kutambua bidhaa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Pwani huku akisema kupitia kauli mbiu ya ujenzi wa viwanda mkoa umetenga zaidi ya ekari 53,000 kwa ajili ya wawekezaji.

Ndikilo,aliongeza kuwa juhudi nyingine ni kuendelea kuwavutia wawekezaji zaidi pamoja na kushirikiana na taasisi wezeshi ili waweze kuona namna ya kufikia malengo ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha .
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza namna walibyoweka mazingira ya uwekezaji wa viwanda katika mkoa katika maonesho ya viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha .
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akimkabidhi Tuzo mmoja wa wadhamini ya maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero 
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero akiwa na watendaji wa kanda hiyo kwa pamoja wakifurahia tuzo walioipata katika maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha .
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akitoa maelezo katika Banda huduma za pamoja katika Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha .
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu nMstaafu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa maonesho ya wiki ya viwanda mkoa.



Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesifu Serikali ya awamu ya tano kwakuendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016 /2021 kwa kukuza uchumi wa viwanda hali ambayo itafanya wananchi kuondokana nan a umasikini kutokana na viwanda hivyo kutumia malighafi zilizopo nchini.

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliyasema hayo wakati akifunga maonesho ya bidhaa za viwandani vilivyoko Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Kibaha Mjini.

Amesema, moja ya mpango huo ni ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam- Morogoro na makutopora na kwamba kukamilika kwake itakuwa na mchango mkubwa kwa Taifa ambapo mkoa wa Pwani utakuwa umepata fursa kubwa itakayokuwa inawasaidia wawekezaji wake katika kufanya biashara kutokana na mnyororo wa usafiirishaji.

Pinda amesema uwepo wa Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kwa kuwa na ndege mchango wake mkubwa kwa faida ya maendeleo ya Taifa na kuiingizia nchi fedha za kigeni kutokana na wafanyabiashara wengi kuja nchini kwa ajili ya uwekezaji pamoja na fursa za utalii.

" Baadhi ya watu walikuwa wanasema maneno ya hovyo sana,mara vindenge vyenyewe vidogo,havijazi watu na maneno mengine mengi ya kubeza juhudi hizo lakini sasa hivi watu wanaruka moja kwa moja kutoka India kwa ndege hizohizo kwahiyo lazima tukubali matokeo,"alisema Pinda

Mbali na miradi lakini alisema Rais Magufuli ,anajenga mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere huko Rufiji Mkoani Pwani ambao kukamilika kwake utakuwa na uwezo wa kufua umeme zaidi ya megawati 2000 ambao utasaidia kuboresha mazingira ya uendeshaji kwa wamiliki wa viwanda nchini.

Alisema kuwa,mradi huo wa umeme ulibuniwa miaka mingi ya nyuma tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini Rais Magufuli amefanikiwa na sasa anajenga kwa fedha nyingi kwahiyo lazima watu wakubali matokeo hayo ya maendeleo na ikiwezekana waunge mkono juhudi za Serikali.

Hatahivyo,Pinda alizipongeza taasisi wezeshi kwa namna zilivyojipanga kuendeleza shughuli za uwekezaji wa viwanda hapa nchini kwakuwa jambo hilo litasaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ,alisema chimbuko la maonesho hayo limetokana na wamiliki wa viwanda kuonyesha changamoto za ukosefu wa masoko kupitia bidhaa wanazozalisha na hata kutofahamika kwa Wananchi.

Ndikilo,alisema malengo mahususi ni kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya mkoa wa Pwani pamoja na kusaidia kutafuta masoko kwa bidhaa hizo na kwamba mpaka maonesho hayo yanakamilika zaidi ya watu 10,000 wametembelea.

alisema kuwa,kupitia maonesho hayo wawekezaji wamepata masoko mbalimbali na hata baadhi ya wananchi wamenufaika kwa kutambua bidhaa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Pwani huku akisema kupitia kauli mbiu ya ujenzi wa viwanda mkoa umetenga zaidi ya ekari 53,000 kwa ajili ya wawekezaji.

Ndikilo,aliongeza kuwa juhudi nyingine ni kuendelea kuwavutia wawekezaji zaidi pamoja na kushirikiana na taasisi wezeshi ili waweze kuona namna ya kufikia malengo ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASALIMIANA NA RAIS WA URUSI VLADIMIR PUTIN

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaiana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika wanaoshiriki katika Mkutano baina ya Urusi na Afrika unaofanyika Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATUMIZI YA TEHAMA YAMEIMARISHA USALAMA WA TAARIFA NA HUDUMA ZA SERIKALI

$
0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

SERA ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003, pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya Serikali kutumia fursa za TEHAMA katika utendaji kazi wa kila siku na utoaji huduma kwa wananchi.

Katika kutekeleza sera hiyo, mwaka 2004 Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) ilianza kuchukua hatua mbalimbali kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kuimarisha mifumo ya utoaji habari na huduma kwa wananchi.

Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kuanza utekelezaji wa dhana ya Serikali Mtandao iliyokuwa sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Mabadiliko katika Utumishi wa Umma (Public Service Reform Programu – PSRP).

Programu hiyo ililenga kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na uboreshaji wa utoaji huduma kwa umma. Pamoja na mambo mengine, Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ziliwezeshwa kuwa na mifumo imara ya Menejimenti ya Habari.

Aidha, Serikali iliziwezesha taasisi za umma kuwa na Tovuti zake ambapo hadi kufika mwaka 2010 takribani Taasisi zote za Serikali zilikuwa na Tovuti, ambapo kwa sasa matumizi ya TEHAMA yameongezeka kwa kasi Serikalini na zimeongeza uwazi, ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika anasema Serikali imeendelea kusimamia matumizi ya mifumo na miundombinu ya TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi na usalama wa taarifa za Serikali.

Anaongeza kuwa mifumo na miundombinu hiyo ni pamoja na Vituo Vikuu vya Kuhifadhi Mifumo na Taarifa za Serikali kwa kuongeza Taasisi mpya 13 hivyo kufanya jumla ya taasisi zilizohifadhi mifumo na taarifa zao kufikia 43, Mfumo wa barua pepe Serikalini (GMS) kwa kuongeza taasisi mpya 39 na kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 398.

Anaitaja mifumo na miundombinu mingine ni Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-office) kwa kuongeza taasisi mpya 15 na kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 48, Mfumo wa kutoa huduma kwa Umma kupitia simu za Mkononi (Government Mobile Platform (GMP) kwa kuongeza taasisi mpya 24 na kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 146.

Kwa mujibu wa Mkuchika anasema Serikali ilitoa mafunzo ya utekelezaji wa Serikali Mtandao kwa kwa Viongozi, Wasimamizi wa TEHAMA na watumiaji wa huduma za Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma 98 ili kuongeza uelewa na uwezo wa Taasisi hizo katika kutumia TEHAMA, kuongeza ufanisi wa kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuchika anasema Serikali pia ilitoa ushauri wa kitaalam kwenye maeneo ya Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma 23 ili kuhakikisha kwamba uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye TEHAMA unatoa matokeo yaliyokusudiwa.

‘‘Msaada wa kiufundi umetolewa kwa Taasisi za Umma 252 kupitia Mfumo wa Kutoa Msaada na Huduma kwa Wateja (Helpdesk System) unaopatikana saa ishirini na nne (24/7)’’ anasema Waziri Mkuchika.

Akifafanua zaidi Waziri Mkuchika anasema Mifumo mikubwa ya TEHAMA imetengenezwa kwa Taasisi za Umma kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, kuboresha utoaji huduma kwa umma, kurahisisha ukusanyaji wa mapato na kuondoa mianya ya rushwa.

Anaitaja baadhi ya mifumo iliyotengenezwa ni pamoja na Mfumo wa Tiketi za Kieletroniki kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mfumo wa kusajili wahandisi kwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Mfumo wa kufanya usajili wa wataalam wa ununuzi na ugavi kwa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

‘’Wataalam wa Wakala ya Serikali Mtandao 11 wamewezeshwa kupata mafunzo yanayotolewa na Bodi mbalimbali za Kitaalam kwenye maeneo ya usalama mtandao, miundombinu na utengenezaji wa Mifumo na Vile vile watumishi 7 wamewezeshwa kupata mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Stashahada, Uzamili na Uzamivu’’ anasema Waziri Mkuchika.

Matumizi ya TEHAMA yameisaidia Serikali kuongeza uwazi, ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi hususani katika zama hizi ambazo taarifa na huduma za Serikali zimekuwa zikitolewa kwa njia ya nyaraka kupitia muundo wa karatasi.

MWANARIADHA FARAJA DAMAS ATINGA FAINALI MASHINDANO YA MAJESHI YA DUNIA NCHINI CHINA, SIMBU AJIPANGA MARATHON

$
0
0
Mwanariadha Faraja Damas wa JWTZ Mwenye namba 1505 akichuana vikali na wanaridha kutoka mataifa Mbalimbali katika mashindano ya Dunia ya Majeshi yanayoendelea nchini China Faraja aliibuka mshindi wa kwanza na kuingia Fainali. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu, China.

Mwanaridha kutoka Tanzania Faraja Damas amefuzu kuingia fainali ya Mita 5000 katika mashindano ya majeshi ya dunia yanayoendelea nchini  China huku akiwapita wanariadha wengine 24.

Faraja alishika nafasi ya kwanza baada ya kukimbia kwa dakika 14:39.24   huku akiwaacha nyuma wakimbiaji wengine katika kundi la pili la wakimbiaji waliokuwa wakisaka nafasi ya kuingia fainali.
Hata hivyo siku haikuwa Njema kwa mwanaridha Joseph Panga baada ya kushindwa kufuzu katika hatua ya Fainali baada ya kukimbia nafasi ya sita nyuma kwa dakika 14:10.47 katika kundi ambalo pia lilikuwa na wakimbiaji 24.

Katika kundi hilo Mkenya  Peter Ndegwa aliongoza baada ya kukimbia kwa dakika 14:04.67 na kufanikiwa kutinga fainali huku akiwa na kibarua cha kukabiliana na wanaridha wengine Tisa waliofuzu kwa Fainali.

Wanariadha hao wa mbio za Mita 5000 wanatarajia kuchuana Oktoba 26 ili kumpata mshindi wa kwanza wa pili na watatu watakaonyakua Medali. Wakati huo huo Mwanariadha Private Gisamoda Emannuel ameshika nafasi ya nne kati ya wanariadha 39 kutoka nchi 46 zilizoshiriki mbio za mita elfu kumi akitanguliwa na El aaraby Mohamed kutoka Moroko  aliyeshika nafani ya kwanza.

Petros  Amanal  wa Ujerumani akishika nafasi ya pili na tatu ikishikwa na  Sahli Hamza naye wa Moroko huku Mtanzania Mwingine Marco Sylvester aliyeshika nafasi ya sita. Mwanariadha Private  Magdalena Shauri aliyeshinda mashindano ya Majeshi Afrika Mashariki anatarajiwa kukimbi leo usiku  sambamba na katika fainali za mbio za Mita 5000 huku  wanariadha wa Marathoni wakiongozwa na Private Felix Simbu wakitarajiwa kukimbia tarehe 27.

Wakati huo huo bondia selemani kidunda ametolewa katika hatua ya robo fainali baada mpambano mkali ambapo  kidunda alipambana  muda wote na kumrushia mpinzani wake makonde mazito.
Hata hivyo mpaka mwisho wa Mpambano Kidunda alipata pointi 26 huku mpinzani wake Ghousoon Ahmad wa syria akipata pointi 30 na kutangazwa mshindi baada ya maamuzi ya majaji wote watano.

Dun&Bradstreet wazindua alama ya mkopo kurahisisha utoaji wa mikopo nchini

$
0
0
Taasisi inayoongoza kuandaa taarifa za mikopo nchini Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Ltd. imezindua mfumo wa alama ya kwanza ya utabiri wa deni la mteja ili kuwawezesha wakopeshaji kama vile benki na taasisi za huduma ndogo za fedha kupata taarifa sahihi za wakopaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu Mtendaji wa Dun & Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas alisema kuwa alama hiyo imezinduliwa ili kutatua changamoto zinazowakabili wadau wote katika soko la mikopo nchini.

Alisema mfumo wa alama hiyo utaongeza uwajibikaji katika kukopesha na kukopa, pia utasaidia wakopeshaji na wadai kusimamia vitabu vyao vya mkopo na kuhakikisha viwango vya riba hulingana na maelezo husika ya mkopaji na kukuza bidhaa za mkopo katika soko la wakopeshaji.

Alisema Alama ya Mikopo hutoa faida nyingi kwa mkopaji kwani humwezesha kujua kama anavyo vigezo vya kukopa au kutokukopa.

“Pia inapunguza muda wa kupata mkopo kulingana na taarifa za mkopo zilizopo kwenye ripoti zake hivyo kukuwezesha kama dhamana ya mkopo wako mpya na kukupatia mkataba bora na wenye kiwango stahiki cha riba.

"Inampa mkopeshaji taarifa sahihi za mchakato wa utoaji wa mikopo; ujumbe na mwongozo wa tathmini ya mkopaji, pia kuwezesha kasi ya utoaji mkopo na usimamizi wa wateja husika. "Pia mtoaji wa huduma anaweza kuongeza kasi ya upatikanaji wa wateja, kuelekeza na kusimamia mipaka ya mkopo yao na kuboresha utoaji wa huduma hizo.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hizo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Adebowale Atobatele alisema lengo lao kila wakati limekuwa kutoa suluhisho la usimamizi kuelekea mikopo isiyolipika katika sekta mbalimbali na kutoa taarifa sahihi kwa watoa mikopo kufanya maamuzi sahihi ya kutoa au kutokutoa mikopo.

"Lakini pia kuharakisha kasi yao ya kuchukua maamuzi; kurahisishaji upatikanaji wa haraka wa bidhaa za mikopo kwa kampuni zinazostahiki, watu binafsi na hivyo kukuza fursa za ukuaji kwa uchumi kwa wote.

“Pia tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote na wahusika wote nchini ili kusaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za mkopo nchini, "alisema. Alisema alama ya mkopo ni maelezo ya kihesabu ambayo wakopeshaji hutumia, pamoja na ripoti ya mkopo kutathmini hatari ya kutoa mkopo.

"Alama za mkopo ni njia muhimu za kukopesha ambayo inaweza kuamua ikiwa unapata mkopo, viwango gani vya riba unalipa kwa deni husika, "alisema.

Naye Ofisa Mkuu wa masuala ya Ufundi wa kampuni hiyo, Kelyn Pena alisema alama ya mkopo ya watumiaji wa D & B ni ya kipekee nchini Tanzania kwa sababu inatoa taarifa halisi za kitakwimu. "Alama hii ya mkopo ni rahisi kutumiwa na taasisi za kifedha na watumiaji kwa jumla kwani iko thabiti katika mpangilio wa wakati na utofauti wa historia ya mikopo ya watumiaji. " alisema.


Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa fedha kutoka BOT, Jerry Sabi akizungumza namna mfumo wa alama za mkopo kwa wakopaji na wakopeshaji unavyosaidia kukuza sekta ya fedha na uchumi nchini.


Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun&Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfumo wa alama ya mkopo kwa wakopaji na wakopeshaji nchini. Mfumo huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam kuwawezesha wakopeshaji kuwa na taarifa sahihi za wakopaji.

Meneja Mkuu wa kampuni ya Dun&Bradstreet Credit Bureau, Adebowale Atobatele akifafanua namna mfumo wa alama kwa mteja unavyozisaidia taasisi zinazokopesha wateja kupata taarifa sahihi za mkopaji.
 

KASI YA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI TANGA YAIRIDHISHA BODI

$
0
0
Na Veronica Simba – Tanga
Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB) imekiri kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa wakandarasi Derm Electrics (T) Ltd na JV Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd; wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, Oktoba 23, mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi hiyo, Mhandisi Styden Rwebangila alisema wakandarasi hao wanafanya kazi nzuri kwani mpaka sasa wamevuka asilimia ya utekelezaji waliyopaswa kuwa wamefikia.

“Mkandarasi Derm Electrics amefikia asilimia 83.5 kati ya 66 aliyopaswa kuwa amefikia wakati mwenzake akiwa amefikia asilimia 67 kati ya 66 aliyopaswa kuwa amefikia,” alibainisha Mwenyekiti.

Akifafanua, Mhandisi Rwebangila alisema Kamati yake imefarijika kuona mabadiliko makubwa aliyofanya Mkandarasi huyo wa pili (JV), kwani awali alikuwa akisuasua kiasi cha kuwa kwenye hatari ya kufutiwa mkataba wake.

“Kwa niaba ya Bodi, tumeridhishwa na utendaji wa wakandarasi katika Mkoa wa Tanga.”

Hata hivyo, Mhandisi Rwebangila alisema katika ziara ambayo Kamati yake imefanya mkoani humo kwa muda wa siku mbili, imebaini changamoto kadhaa ikiwemo wakandarasi kutokugawa vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wenye uhitaji kama serikali ilivyowaelekeza.

Kufuatia changamoto hiyo, alisema, Kamati yake imetoa maelekezo kwa Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Mkoa na Wilaya, waweke mkakati utakaohakikisha vifaa hivyo vinafungwa kwa wananchi husika kama ilivyoelekezwa.

Aidha, alitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa nyaya za umeme suala ambalo alisema limekwishafikishwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ambaye naye amechukua hatua kwa kupanga kukutana na wazalishaji wote wa nyaya nchini Oktoba 29 mwaka huu, ili kujua tatizo linalosababisha kutopatikana kwa nyaya hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, ambaye amefuatana na Bodi husika katika ziara hiyo, alitoa wito kwa wakandarasi kuhakikisha wanapeleka nguzo zote maeneo ya kazi na kuzisimika ili kuepuka changamoto ya kukwama kutekeleza hilo kutokana na kipindi cha mvua kinachoendelea ambacho mara nyingi huharibu miundombinu ya barabara.

Pia, aliwataka wakandarasi kuwaunganishia umeme wateja wote waliopo ndani ya wigo pasipo kisingizio cha mteja kutotandaza mfumo wa nyaya (wiring) kwenye jengo lake kwani kuna kifaa cha UMETA kinachofaa kwa wateja wa aina hiyo.

“Natamani wakandarasi watuambie wamegawa vifaa vyote 250 ambavyo kila mmoja kapewa kwa kila eneo ili sisi tuwaongezee vingine badala ya kukaa navyo tu pasipo kuwafungia wananchi,” alisema Olotu.

Awali, Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Sebastian Masanja, alitoa pongezi kwa Rais John Magufuli na Serikali kwa ujumla, hususan Wizara ya Nishati, kwa kutekeleza mkakati wa kupeleka umeme vijijini.

Alisema, umeme vijijini umekuwa ni mkombozi kwa vijana ambao hawakuwa na kazi na kuzurura hovyo. “Sasa wengi wamejiajiri katika shughuli mbalimbali ikiwemo saluni na kuchomelea vyuma na wanajipatia kipato kuendesha maisha yao na familia zao.”

Wakandarasi wote wameahidi kukamilisha kazi kwa viwango stahiki na kwa wakati kama serikali ilivyoagiza, yaani Desemba 31, mwaka huu.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Styden Rwebangila akizungumza, wakati Kamati hiyo ilipokutana na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga (hawapo pichani), Oktoba 23, 2019.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Styden Rwebangila (meza kuu – katikati), akiongoza kikao baina ya Kamati hiyo na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga, Oktoba 23, 2019.
 Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Louis Accaro, akifuatilia kikao baina ya Kamati hiyo na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga (hawapo pichani), Oktoba 23, 2019.
  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, akizungumza wakati Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), ilipokutana na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga (hawapo pichani), Oktoba 23, 2019.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuyuni, wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, Zihirwani Mbwambo (kushoto), akizungumzia hali ya upatikanaji umeme kijijini hapo alipotembelewa na Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), ofisini kwake, Oktoba 23, 2019.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Styden Rwebangila (katikati) na Ujumbe wake, wakiwa katika kikao cha ndani na mameneja wa TANESCO mkoani Tanga pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi husika mkoani humo, walipokuwa katika ziara ya kazi, Oktoba 23, 2019.

JAFO AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUFUNGUA AKAUNTI MAALUM YA FEDHA ZA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo akiongea wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii lilofanyika jijini Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

*******************************

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jafo ametao mwezi mmoja kwa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinafungua akaunti maalum ya Benki kwa ajili ya fedha za maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo jana wakati akifunga kongamano la wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma nakuwataka wataalam hao kuhakikisha wanakwenda kusimamia zoezi hilo na kukamilisha katika kwa kipindi cha mwezi mmoja.

‘’Natoa maagizo ifikapo Novemba, 30 kila Halmashauri Nchini iwe imefungua akaunti maalum ya Benki kwa ajili fedha ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuwa fedha zikitolewa katika mfumo wa sasa zinakuwa kama zinaelea’’. Alisitsiiza Waziri Jaffo.

Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa fedha hizi zinapotelewa bila akaunti hiyo inakuwa vigumu kwa serikali kuzifanyia tathimini hivyo kuwaimiza wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii katika Halmashauri zao kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo ili malengo na matumizi ya fedha hizo yaweze kufanyiwa tathimini.

Pamoja na kutoa agizo hilo Waziri Jafo pia ameongeza kuwa ili jamii iweze kuleta mabadiliko yanayotakiwa suala la kutumia wataalam wa maendeleo ya jamii halikwepiki kwa sasa wakati jamii inataka mabadiliko ya haraka kuelekea Tanzania ya viwanda.

Wataalam hawa ni chachu ya mabadiliko na katika mashirika makubwa duniani wataalam wa maendeleo ya jamii wamekuwa wakitumiwa sana ili kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali na wamekuwa msaada mkubwa kitaifa na kimataifa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika hotuba yake kwa Waziri huyo aliongeza kuwa kongomano hilo lilikuwa na mjadala mkubwa kuhusu kuhamasisha jamii kujiletea maendeleo kwa kutumia istilahi zilizoko katika jamii akitolea mfano wa istilahi maalufu kwa mikoa ya ya kati ijulikanayo kama Msalagambo.

Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa matokeo ya kongamano hilo pia nikuwafanya wataalam hao wajione kuwa wao ni chachu ya maendeleo katika kuhamasisha wananchi kuwa na ari ya kujiletea maendeleo.



Wakati huo huo Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka TAMISEMI aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara yake katika Kongomano hilo Bw.John Miayo Cheo aliwataka wataam wa maendeleo ya jamii kutumia taaluma yao kuhamasisha wananchi kugombea nafasi za uongozi ili waweze kuwa viongozi wa kufuatia uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. 

Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wamekutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne

NAIBU WAZIRI MABULA AWATULIZA WANANCHI WA KIJIJI CHA SINDENI HANDENI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM HANDENI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewatuliza wananchi wa kijiji cha Sindeni kilichopo Tarafa ya Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga kufuatia mgogoro kati yao na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuhusu mpaka baina ya kijiji cha Sindeni na Shamba la Miti la Korogwe.

Dkt Mabula aliwatuliza wananchi hao baada ya kufika katika shamba la Miti la Korogwe lililopo wilayani Handeni kukagua maendeleo ya Ujenzi wa ofisi na Nyumba za Watumishi za TFS zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwa katika ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Tanga.

Dkt Mabula ametaka idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Handeni ikisimamiwa na Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini kuhakikisha inafanya uhakiki wa mpaka kati ya TFS na kijiji cha Sindeni na kuweka alama ili kukomesha mgogoro huo unaozuka mara kwa mara.

‘Kitakachofanyika ni uhakiki wa mipaka ya kijiji chenu kinaishia wapi, TFS wanaishia wapi, NARCO wanaishia wapi, tutaheshimu mipaka na nyaraka zilizoanzisha vijiji vyenu’’ alisema dkt Mabula.

Uamuzi wa Dkt Mabula kutoa maagizo hayo unafuatia wananchi wa kijiji hicho kulalamika mbele ya Naibu Waziri kuwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) uliongeza eneo inalomiliki katika shamba hilo kwa kuingia ndani ya eneo la kijiji cha Sindeni jambo linalochochea mgogoro kati ya pande hizo.

Ally Mhina mkazi wa kijiji cha Sindeni alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa, TFS iliacha eneo lake la asili na kuongeza eneo lingine kuingia kijiji cha Sindeni wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Miti la Korogwe Pregreen Mushi alisema, wenyeji wa Sindeni walivamia eneo la Wakala wa Huduma za Misitu huku wale wa Kwamatuko na Kwaingoma wakiuza maeneo ya hifadhi kwa jamii ya wafugaji na Mkuu wa Wilaya ya Handeni alishatoa agizo wote waliovamia kuondoka eneo la hifadhi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema alishashughulikia mgogoro huo na kuwataka wasioridhika wasioridhika na utatuzi wake kwenda mahakamani na kufafanua kuwa katika jitihada zake za kutafuta suluhu ya mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali kuwepo msitu huo na sasa wananufaika kwa kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mustafa Beleko alisema pamoja maagizo ya Naibu Waziri kuhusiana na uhakiki wa mpaka kati ya kijiji cha Sindeni na TFS lakini wao kama halmashauri watachukua ramani ya kijiji wakati wa uhakiki mipaka ili kukomesha kuibuka kwa mgogoro huo mara kwa mara.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza pia kuweka alama za mpaka kati ya Wakala wa Huduma za Misitu na NARCO kufuatia suluhu ya mpaka kati ya taasisi hizo mbili za serikali kushindikana kutekelezwa kwa madai kuwa NARCO ilikaa kimya katika utekelezaji makubaliano ya kuchangia gharama za ubainishaji mipaka.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Shamba la Miti la Shume Lushoto mkoani Tanga linalomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu katika wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sindeni katika eneo la Shamba la Miti la Korogwe lililopo Handeni aliposikiliza malalamiko yao ya mpaka kati yao na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa jana usiku akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayofanywa na Shirika hilo katika mkoa wa Tanga. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Mawanaasha Tumbo.

NAIBU WAZIRI MABULA AWATULIZA WANANCHI WA KIJIJI CHA SINDENI HANDENI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM HANDENI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewatuliza wananchi wa kijiji cha Sindeni kilichopo Tarafa ya Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga kufuatia mgogoro kati yao na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuhusu mpaka baina ya kijiji cha Sindeni na Shamba la Miti la Korogwe.

Dkt Mabula aliwatuliza wananchi hao baada ya kufika katika shamba la Miti la Korogwe lililopo wilayani Handeni kukagua maendeleo ya Ujenzi wa ofisi na Nyumba za Watumishi za TFS zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwa katika ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Tanga.

Dkt Mabula ametaka idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Handeni ikisimamiwa na Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini kuhakikisha inafanya uhakiki wa mpaka kati ya TFS na kijiji cha Sindeni na kuweka alama ili kukomesha mgogoro huo unaozuka mara kwa mara.

‘Kitakachofanyika ni uhakiki wa mipaka ya kijiji chenu kinaishia wapi, TFS wanaishia wapi, NARCO wanaishia wapi, tutaheshimu mipaka na nyaraka zilizoanzisha vijiji vyenu’’ alisema dkt Mabula.

Uamuzi wa Dkt Mabula kutoa maagizo hayo unafuatia wananchi wa kijiji hicho kulalamika mbele ya Naibu Waziri kuwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) uliongeza eneo inalomiliki katika shamba hilo kwa kuingia ndani ya eneo la kijiji cha Sindeni jambo linalochochea mgogoro kati ya pande hizo.

Ally Mhina mkazi wa kijiji cha Sindeni alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa, TFS iliacha eneo lake la asili na kuongeza eneo lingine kuingia kijiji cha Sindeni wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Miti la Korogwe Pregreen Mushi alisema, wenyeji wa Sindeni walivamia eneo la Wakala wa Huduma za Misitu huku wale wa Kwamatuko na Kwaingoma wakiuza maeneo ya hifadhi kwa jamii ya wafugaji na Mkuu wa Wilaya ya Handeni alishatoa agizo wote waliovamia kuondoka eneo la hifadhi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema alishashughulikia mgogoro huo na kuwataka wasioridhika wasioridhika na utatuzi wake kwenda mahakamani na kufafanua kuwa katika jitihada zake za kutafuta suluhu ya mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali kuwepo msitu huo na sasa wananufaika kwa kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mustafa Beleko alisema pamoja maagizo ya Naibu Waziri kuhusiana na uhakiki wa mpaka kati ya kijiji cha Sindeni na TFS lakini wao kama halmashauri watachukua ramani ya kijiji wakati wa uhakiki mipaka ili kukomesha kuibuka kwa mgogoro huo mara kwa mara.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza pia kuweka alama za mpaka kati ya Wakala wa Huduma za Misitu na NARCO kufuatia suluhu ya mpaka kati ya taasisi hizo mbili za serikali kushindikana kutekelezwa kwa madai kuwa NARCO ilikaa kimya katika utekelezaji makubaliano ya kuchangia gharama za ubainishaji mipaka.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Shamba la Miti la Shume Lushoto mkoani Tanga linalomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu katika wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sindeni katika eneo la Shamba la Miti la Korogwe lililopo Handeni aliposikiliza malalamiko yao ya mpaka kati yao na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa jana usiku akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayofanywa na Shirika hilo katika mkoa wa Tanga. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Mawanaasha Tumbo.

PINDA AMWAGIA SIFA SERIKALI YA AWAMU YA TANO UTEKELEZAJI MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO YA KUAKISI UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu wa Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mjini Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza namna walibyoweka mazingira ya uwekezaji wa viwanda katika mkoa katika maonesho ya viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mjini Kibaha.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akimkabidhi Tuzo mmoja wa wadhamini ya maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero akiwa na watendaji wa kanda hiyo kwa pamoja wakifurahia tuzo walioipata katika maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akitoa maelezo katika Banda huduma za pamoja katika Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali maonesho ya wiki ya Viwanda vya Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mjini Kibaha.
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa maonesho ya wiki ya viwanda mkoa.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesifu Serikali ya awamu ya tano kwakuendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016 /2021 kwa kukuza uchumi wa viwanda hali ambayo itafanya wananchi kuondokana nan a umasikini kutokana na viwanda hivyo kutumia malighafi zilizopo nchini.

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliyasema hayo wakati akifunga maonesho ya bidhaa za viwandani vilivyoko Mkoa wa Pwani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Kibaha Mjini.

Amesema, moja ya mpango huo ni ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam- Morogoro na makutopora na kwamba kukamilika kwake itakuwa na mchango mkubwa kwa Taifa ambapo mkoa wa Pwani utakuwa umepata fursa kubwa itakayokuwa inawasaidia wawekezaji wake katika kufanya biashara kutokana na mnyororo wa usafiirishaji.

Pinda amesema uwepo wa Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kwa kuwa na ndege mchango wake mkubwa kwa faida ya maendeleo ya Taifa na kuiingizia nchi fedha za kigeni kutokana na wafanyabiashara wengi kuja nchini kwa ajili ya uwekezaji pamoja na fursa za utalii.

" Baadhi ya watu walikuwa wanasema maneno ya hovyo sana,mara vindenge vyenyewe vidogo,havijazi watu na maneno mengine mengi ya kubeza juhudi hizo lakini sasa hivi watu wanaruka moja kwa moja kutoka India kwa ndege hizohizo kwahiyo lazima tukubali matokeo,"alisema Pinda
Mbali na miradi lakini alisema Rais Magufuli ,anajenga mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere huko Rufiji Mkoani Pwani ambao kukamilika kwake utakuwa na uwezo wa kufua umeme zaidi ya megawati 2000 ambao utasaidia kuboresha mazingira ya uendeshaji kwa wamiliki wa viwanda nchini.

Alisema kuwa,mradi huo wa umeme ulibuniwa miaka mingi ya nyuma tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini Rais Magufuli amefanikiwa na sasa anajenga kwa fedha nyingi kwahiyo lazima watu wakubali matokeo hayo ya maendeleo na ikiwezekana waunge mkono juhudi za Serikali.

Hatahivyo,Pinda alizipongeza taasisi wezeshi kwa namna zilivyojipanga kuendeleza shughuli za uwekezaji wa viwanda hapa nchini kwakuwa jambo hilo litasaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ,alisema chimbuko la maonesho hayo limetokana na wamiliki wa viwanda kuonyesha changamoto za ukosefu wa masoko kupitia bidhaa wanazozalisha na hata kutofahamika kwa Wananchi.

Ndikilo,alisema malengo mahususi ni kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya mkoa wa Pwani pamoja na kusaidia kutafuta masoko kwa bidhaa hizo na kwamba mpaka maonesho hayo yanakamilika zaidi ya watu 10,000 wametembelea.

Alisema kuwa,kupitia maonesho hayo wawekezaji wamepata masoko mbalimbali na hata baadhi ya wananchi wamenufaika kwa kutambua bidhaa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Pwani huku akisema kupitia kauli mbiu ya ujenzi wa viwanda mkoa umetenga zaidi ya ekari 53,000 kwa ajili ya wawekezaji.

Ndikilo,aliongeza kuwa juhudi nyingine ni kuendelea kuwavutia wawekezaji zaidi pamoja na kushirikiana na taasisi wezeshi ili waweze kuona namna ya kufikia malengo ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.

MAHAKAMA YA RUFAA YABARIKI MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR KUHUSU VIFUNGU VYA SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Rufaa imebariki maamuzi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyoelekeza serikali kubadilisha kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kwa kuwa vinakiuka Katiba ya Tanzania.

Vifungu hivyo, vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 lakini mtoto wa kiume ameruhusiwa kuoa akiwa na miaka 18 hivyo, sheria haiweki usawa kati ya watoto hao na kwamba ni ya ubaguzi na ni kinyume na Ibara ya 13 na ya 12 ya katiba inayozungumzia usawa.

Hukumu hiyo imetokana na Serikali kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa mwaka 2016 ambao ulibatilisha kifungu cha Sheria ya Ndoa kinachoruhusu ndoa za utotoni.

Rufaa hiyo imesikilizwa na Jopo la majaji watatu, Augustine Mwarija, Winfrida Korosso na Dk Mary Lavira ambapo miongoni mwa sababu za serikali za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ni kwamba mahakama ilikosea kutoa uamuzi huo kwa sababu ililenga kuwasaidia kuwalinda watoto wa kike dhidi ya ngono na kupata watoto nje ya ndoa.

Pia walidai mtoto wa kike anakua mapema kabla ya mtoto wa kiume.
Akisoma uamuzi uliotolewa na majaji hao, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eddie Fussi amesema watoto wote ni sawa bila kujali jinsia na kwamba sheria hiyo haiwezi kumkinga mtoto wa kike kwa kumruhusu kuolewa kwa madai huko kuna ulinzi zaidi wakati kuna madhara makubwa kwake.

Amesema miongoni kwa madhara ambayo mtoto wa kike akiolewa chini ya umri wa miaka 18 ni mimba za utotoni, magonjwa na unyanyasaji wa kijinsia.Pia sheria mbalimbali zinakataza mtoto wa chini ya umri wa miaka 18 kuingia mkataba wowote hivyo ni pamoja na mkataba wa ndoa kwa sababu ni mgumu zaidi.

"Mahakama inaelekeza kifungu cha 13 na 17 vinakiuka katiba ya Tanzania hivyo, serikali ifuate maelekezo ya Mahakama Kuu ya kubadilisha vifungu hivyo," alisema Fussi.

Kesi hiyo ya kikatiba ilifunguliwa na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi.

MAKAMU WA PILI WA RAIS AZINDUA SERA YA VIWANDA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Vitabu vya Sera ya Viwanda katika hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akitoa Hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Muakilishi kutoka Ubalozi wa Sweden Jenny Akeback akitoa hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Muakilishi kutoka UNIDO Steven Cargbo akitoa hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Juma Hassa Reli akitoa hotuba ya Makaribisho katika hafla ya uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029-iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya waheshimiwa na Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Sera ya Viwanda iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull wakil kikwajuni Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

………………….

Na Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaomba Washirika Binafsi wa Sekta ya Viwanda pamoja na Wadau wa Maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Viwanda Nchini ya Mwaka 2019 – 2029 ili ifikie lengo la kuifanya Zanzibar kuwa ya Viwanda.

Balozi Seif alitoa ombi hilo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vitabu Vitano vya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema Sera ya Viwanda ikiwa ni miongoni mwa Vitabu vilivyozinduliwa na kupata baraka zote za Serikali itachangia kuimarika kwa Sekta hiyo kwa kuzingatia utayarishaji wake imewashirikisha wadau wote wa Maendeleo ya Viwanda na kuzingatia maoni na michango iliyotolewa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Sera hiyo ni matokeo ya mapitio ya Sera ya Viwanda ya Mwaka 1998 iliyokuwa imepitwa na wakati ambayo pia inakwenda sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 – 2020 ibara ya 84 {d} inayozungumzia kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara.

Balozi Seif alisema utekelezaji wa kazi zitaimarisha mazingira bora ya Uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa kupitia Viwanda vilivyopo ndani pamoja na kuanzisha vipya ili Taifa lifanikiwe kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana, kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza uagizaji bidhaa kutoka nchi za nje.

“ Ninatambua kwamba kuitekeleza Sera ya Viwanda ni lazima kila Mshirika apate fursa ya kusoma vitabu hivyo ili aweze kutimize wajibu wake ipasavyo”. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba kwa vile Sera ya Viwanda Zanzibar imeshapata baraka zote na kukubalika katika ngazi ya juu, hivyo Serikali Kuu itajitahidi kuyatekeleza na kuyasimamia kwa upande wa Sekta ya Umma.

Alielezea kuwa vitabu vilivyozinduliwa vinategemewa kuwa na mwanzo mzuri wa kukuza sekta ya Viwanda ambapo Wafanyabiashara watapata uelewa kuhusiana na mazingira ya ufanyaji wa biashara pamoja na kupata muongozo maalum utakaowasaidia wafanyabiashara na bidhaa kupitia daftari maalum.

Balozi Seif aliwahakikishia Washirika wa Sekya ya Viwanda na Biashara kwamba Serikali Kuu itazifanyia kazi changamoto zote zilizopo katika urahisishaji biashara katika maeneo ya usafirishaji na uagizaji bidhaa, usajili na uhaulishaji wa mali pamoja na upatikanaji wa vibali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizitaka Mamlaka za utoaji wa leseni na Mamlaka za usimamizi kuchukuwa hatua katika maeneo yote ambayo hayakufanya vizuri ili kurahisisha ufanyaji biashara.

Balozi Seif alisema bado ipo kazi kubwa iliyo mbele kwa Taifa ya kuwaomba Wawekezaji wengi zaidi kutumia fursa za Uwekezaji katika ujenzi wa Viwanda Vipya huku akiwataka Wananchi waendeleze amani iliyopo itakayowapatia ushawishi Wawekezaji hao.

Akitoa salamu Mwakilishi kutoka Sekta Binafsi Bwana Ahmed Yussuf alisema Kundi lao limepata faraja kubwa kutokana na ushiriki wao kwenye utayarishaji wa Vitabu hivyo muhimu kwa Maendeleo ya Sekta ya Biashara Zanzibar.

Bwana Ahmed alisema mchakato huo umeanza kwa muda kiasi, licha ya kuchelewa lakini kilichozingatiwa ni umakini wa kusonga mbele na akashauri uwepo wa ulinzi makini wa Viwanda vitakavyoanzishwa Nchini ili lile lengo lililokusudiwa likamilike vyema.

Nao kwa upande wao wakiwasilisha Salamu wa Taasisi zao, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Viwanda {UNIDO} Bwana Stephen na Mwakilishi wa Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Bibi Jane Akebak walisema mafanikio makubwa ya uimarishaji wa Sekta ya Viwanda utafanikiwa vyema endapo Sera za Sekta hiyo zitaimarishwa na kuwa wazi.

Wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuliona hilo kwa uamuzi wake wa kuandaa Sera, Miongozo na masuala mengine muhimu yanayojenga mazingira bora ya kuendeleza Sekta ya Viwanda sambamba kwa kushirikisha Sekta Binafsi.

Walieleza kwamba Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Viwanda {UNIDO} pamoja na Washirika wengine wataendelea kuiunga mkono Zanzibar katika Mikakati yake ya kuvifanya Visiwa vya Zanzibar kuingia katika Mfumo wa Viwanda katika uendeshaji wake wa Uchumi.

Walisema Tafiti zitafanywa zinazokwenda sambamba na Wataalamu wa Taasisi hizo kuendelea kutoa mafunzo kwa Vijana wa Zanzibar katika kuona Sekta ya Viwanda inaendelea kusonga mbele kwa kipindi kirefu ikilenga kupunguza tatizo la Ajira hasa kwa Vijana.

Walifahamisha kwamba Sekta ya Viwanda Duniani imeanza tokea Karne ya 19 kwa kujikita zaidi katika masuala ya Kilimo jambo ambalo wataalamu walipelekea kubadilisha mfumo huo na kuelekeza nguvu zaidi katika furza zaidi za ajira kwa kuanzisha uzalishaji wa biadhaa mbali mbali.

Akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Vitabu hivyo Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali alisema uzinduzi wa Vitabu vya Sekta ya biashara umetoa mwanga kwa safari ya Zanzibar kuelekea kwenye Maendeleo ya uhakika.

Balozi Amina alisema Wizara ya Biashara itaendelea kubeba dhima ya kuiona Zanzibar inastawi na kufanikiwa katika mwenendo mzima wa Sekta ya Biashara inayotowa fursa kubwa katika utoaji wa ajira miongoni mwa Wananchi walio wengi.

Wajasiri amali wadogo wadogo wamezingatiwa katika mfumo wa Miongozo ya Sera na Vitabu hivyo watakaokuwa na fursa pana zaidi ya kujengewa mazingira mazuri wa bidhaa zao zitakazokuwa na muelekeo wa kuuzwa katika Masoko ya Kimataifa likiwemo lile la AGOA.

Waziri wa Biashara na Viwanda ameushiriki Uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa unaoshughulika Viwanda {UNIDO} na Ubalozi wa Sweeden Nchini Tanzania kwa michango yao iliyofanikisha kukamilika kwa Vitabu hivyo.

Jumla ya Vitabu Vitano vimezinduliwa kuhusiana na Sera ya Viwanda, Ripoti ya tathmini ya mazingira ya ufanyaji wa biashara, Daftari la Wafanyabiashara, Muongozo wa usafirishaji na uagizaji pamoja na Taarifa za Wazalishaji wa Kazi za Mikono Zanzibar zinazotarajiwa kuuzwa katika Soko la AGOA.

MAJALIWA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA YA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA MATAIFA YA AFRIKA NA RAIS WA URUSI, VLADIMIR PUTIN

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa urusi, Vladimir Putin kabla ya kuanza kwa Mkutano baina ya Urusi na Afrika unaofanyika, Sochi nchini Urusi, Oktoba 24, 2019.


(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZITAKA HALMASHAURI KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI KUPITIA ZABUNI ZA HALMASHAURI

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na vijana wa Chuo cha Ufundi cha Mt. Anthony ambao wanasomeshwa kwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Programu ya Ukuzaji Ujuzi Nchini iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Sehemu ya vijana wa Chuo cha Ufundi cha Mt. Anthony wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) alipowatembelea vijana hao kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano akieleza jambo wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na vijana wanaojifunza fani ya Uchomeleaji na uungaji vyuma alipotembelea karakana kujionea mafunzo ya vijana hao.
Baadhi ya vijana wanaojifunza ufundi wa magari wakijishughulisha ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na vijana wanaojifunza fani ya Ushonaji alipotembelea kujionea mafunzo ya vijana hao.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

………………….

Na; Mwandishi Wetu

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amezitaka Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji nchini kuwawezesha Vijana kiuchumi kwa kutumia Vikundi na Kampuni za Vijana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa kuzipa zabuni kampuni na vikundi hivyo kupitia utaratibu wa “force account” hasa katika utengenezaji wa madawati na ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, zahanati na vituo vya Afya.

Naibu Waziri Mavunde kayasema hayo Wilayani Musoma wakati alipotembelea Chuo cha Ufundi cha Mt. Anthony ambapo jumla ya Vijana 240 wanasoma hapo fani mbalimbali kwa ufadhili wa Serikali kupitia Programu ya Ukuzaji Ujuzi Nchini iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo mwaka huu wa fedha 2019/2020 inatrajiwa kuwajengea uwezo Vijana 46,000 katika fani mbalimbali.

“Serikali inayo nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba tunaijengea Ujuzi stahiki nguvukazi ya Taifa hili ili vijana wengi zaidi waweze kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za uzalishaji mali.Mamlaka za Serikali za Mitaa ziwe kichocheo katika kuwawezesha Vijana kiuchumi kwa kutoa zabuni kwa vikundi na makampuni ya Vijana nchini kote hasa zile zinapitia katika mfumo wa manunuzi wa force account,” alisema Mavunde

Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano amewahakikishia Vijana hao kupata mikopo ya asilimia 4 na asilimia 2 kwa wenye ulemavu itokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri na kuwataka kuunda vikundi kutokana na fani zao za Ufundi.

Akizungumza kwa niaba ya Vijana wenzake wanafuika ya Programu ya kukuza Ujuzi, Bw. Baraka Emmanuel ameishukuru Serikali kwa kuwajali Vijana na kuwawezesha kupata Ujuzi kupitia mafunzo wanayoyapata hapo Chuoni ambayo pia yatawafanya waweze kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUBORESHA MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Raphael Waida, akisisitiza umuhimu wa kuwa na tabia ya kujali wateja, wakati wa mafunzo ya maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja kwa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Arusha. Kushoto ni mtaalam wa uchambuzi wa masuala ya Utawala, Bi. Beltila Mgaya
Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Fortunata Soka, akielezea umuhimu wa kufanya maboresho ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Wizara hiyo, wakati wa mafunzo ya maboresho ya mkataba huo, Jijini Arusha.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Raphael Waida (kulia) na mtaalam wa uchambuzi wa masuala ya Utawala, Bi. Beltila Mgaya, wakifuatilia kwa makini hoja za washiriki wa mafunzo ya maboresho ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Arusha.
Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Henrico Ndagula (kushoto) akiomba ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya mkataba wa huduma kwa wateja kwa Wizara hiyo, wakati wa mafunzo ya maboresho ya mkataba huo, Jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja kwa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Arusha, wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)

…………………….

Na. Peter Haule, WFM, Arusha

Wizara ya Fedha na Mipango inaboresha Mkataba wa utoaji Huduma kwa wananchi kwa kupata maoni katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma lengo likiwa kuongeza ufanisi na kufikia maendeleo stahiki kwa wakati.

Hayo yamebainishwa na Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Fortunata Soka, wakati wa mafunzo ya ukusanyaji wa maoni ya maboresho ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja kwa wadau wa Wizara hiyo yaliyofanyika Jijini Arusha na kuwakutanisha wadau kutoka Wizara hiyo pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Bi. Soka alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imekuwa na Mkakati wa Utoaji huduma kwa wananchi ambao sasa unahitaji maboresho ili kuongeza ufanisi wa huduma na kuharakisha maendeleo ya wananchi.

‘’Muundo wa Wizara umebadilika na pia wadau wanaongezeka hivyo kuna kila sababu ya kuboresha mkataba wa huduma kwa wateja ili kukidhi uhitaji, tunalazimika kufanya mafunzo ya namna ya kufanya tafiti kwa wadau ili kuja na mkataba bora uliosheheni weledi na kuleta matokeo chanya kwa walengwa.’’, alieleza Bi. Soka

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua kwa kufikisha huduma kwa haraka kwa wananchi hivyo Wizara inalengo la kupata mrejesho wa utoaji wa huduma zake ili kuweza kuandaa mipango yenye manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla

Bi Soka alisema kuwa maboresho ya Mkataba wa huduma kwa wateja ni sehemu ya kujali wananchi hasa wa hali ya chini ambao wanataka kupata huduma bora kwa ufanisi kwa maendeleo yao kwa kupunguza urasimu usio wa lazima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni mtoa mada, Bw. Raphael Waida, alisema kuwa ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi lazima mikataba ya huduma kwa wateja ikafanyiwa maboresho kila inapobidi kwa kuwa teknolojia na mazingira ya kihuduma yanabadilika.

Aidha, ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa jitihada zake za kuhakikisha inatoa huduma kwa wadau kwa wakati hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali imejidhatiti kufikia uchumi wa Kati uliojikita katika viwanda kwa manufaa ya wananchi.

Naye Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Henrico Ndagula ambaye ni mmoja wa Washiriki wa Mafunzo amesema kuwa, mafunzo hayo yanasaidia kufanya tathmini ya utoaji huduma na kuangalia maeneo ambayo Wizara imefanikiwa na yanayohitaji maboresho, hivyo kuwa na umuhimu hasa katika wakati huu ambao mabadiliko makubwa yakiuchumi yanafanyika nchini.

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA JIOLOJIA

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko akifungua Mkutano wa 36 wa Watalaam wa
Jiolojia kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Wataalam wa Jiolojia kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa
Mkutano wa 36 wa Wataalam wa Jiolojia.
**************************************

Na Asteria Muhozya, DSM

Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa wito kwa kuzitaka nchi za Afrika
kujenga uwezo kwa Wataalam wa ndani wa Jiolojia ili kuwawezesha
kujenga uwezo wa tafiti za rasilimali madini ili pindi nchi au taasisi wafadhili wanapoacha kufadhili, mamlaka husika ziwe kwenye nafasi ya kuendeleza shughuli hizo.

Waziri Biteko ameyasema hayo Oktoba 24, 2019 wakati akifungua
Mkutano wa 36 wa Wataalam wa Jiolojia kutoka nchi mbalimbali za Afrika
ambao wanakutana jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unalenga katika kuwapatia wataalam hao mafunzo
yanayogusa masuala mabalimbali kuhusu sekta ya Madini ikiwemo
kubadilishana uzoefu katika utafutaji rasilimali madini na kuangalia namna
bora ya kuendeleza rasilimali hizo ili kuhakikisha kwamba zinayanufaisha
mataifa husika.

Aidha, amewataka washiriki wa mkutano huo kujifunza na kutumia vyema
uzoefu mzuri utakaotolewa na mataifa mengine ili kuwezesha kuongeza
thamani katika kutekeleza majukumu ya taasisi zao katika uendelezaji wa
rasilimali madini.

‘’ Afrika lazima tujifunze wenyewe kuendeleza na kujenga miradi yetu
wenyewe. Katika mkutano yapasa kujiuliza siku Wafadhili wetu Umoja wa
Ulaya na taasisi nyingine zinazofadhili mafunzo haya zikiacha tutaweza
kujisimamia wenyewe?,’’ amehoji Waziri Biteko.

Amesema kwa upande wa Tanzania kama taifa linaamini katika
kuwajengea uwezo wataalam wa ndani ambapo tayari serikali imechukua
hatua kadhaa za kuhakikisha zinawendeleza wataalam wake ili kuwezesha
taifa kuzalisha wataalam waliobobea katika taaluma ya jiolojia na ambao
watakuwa na mchango katika utafutaji wa rasilimali madini.

Amesema mradi huo wa kutoa Mafunzo kwa Taasisi za Jiolojia Afrika
unafadiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na taasisi nyingine 12 ambapo
tangu kuanzishwa kwa mradi huo mnamo mwaka 2017, tayari
umewezesha kuwapatia mafunzo wataalam wapatao 1,100 kutoka Mataifa
mbalimbali ya Afrika huku wataalam 30 wa Tanzania wakiwa wamepatiwa
mafunzo hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano Kutoka Umoja
wa Ulaya, Jose Dorreia Nunes, amewataka washiriki wa mkutano huo
kutafakari namna rasimali hizo zitakavyozinufaisha nchi zao ikizingatiwa
kwamba madini ni chanzo kikubwa cha mapato kwa nchi za Afrika hivyo ni
muda sahihi kupitia mafunzo yanayotolewa na Umoja huo yawezeshe
kujenga uwezo wa wataalam wa ndani katika kutafiti, kusimamia na
kuendeleza rasilimali katika nchi zao.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini
Tanzania (GST), Yorkberth Myumbilwa akizungumza na waandishi wa
habari waliohudhuria mkutano huo amesema mafunzo yanayotolewa na
Taasisi wafadhili yana umuhimu mkubwa kwa kuwa yanagusa moja kwa
moja shughuli zinazofanywa na taasisi hizo zikiwemo tafiti, wingi wa
mashapo, urithi wa Jiolojia, namna ya kuhifadhi data na masuala mengine.

Ameongeza kwamba, suala la kukutanishwa na taasisi nyingine lina
umuhimu kwa GST kwa kuwa linawezesha kujenga mahusiano mapya na
Taasisi nyingine za Jiolojia kutoka nchi nyingine.

Nchi zinazoshiriki mkutano unafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 24 –
25 Oktoba, 2019 ni pamoja na Tanzania, Namibia, Sengel Morroco, Kenya,
Afrika Kusini , Rwanda, Zambia na Ghana.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images