Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WANANCHI WOTE WALIODHURUMIWA KULIPWA FIDIA

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameziagiza Halmashauri za Miji pamoja na watu wenye mashamba makubwa wahakikishe wanawalipa fidia Wananchi wote ambao hawajalipwa kwa muda mrefu tangu kufanyika kwa tathmini kwani wananchi wengi wamekuwa wakiishi ndani ya mashamba yao kwa muda mrefu na wakiamishwa hawalipwi fidia zao kwa miaka mingi na wengine kuondolewa bila kulipwa kabisa.

Waziri Lukuvi meyasema hayo alipofanya ziara Wilayani Handeni Mkoani Tanga wakati wa kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Soko la zamani Chanika maarufu Nyerere Squre Katika mkutano huo Waziri wa Ardhi aliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo Godwin Gondwe akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Handeni Omari Abdallah Kigoda na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Kupitia kampeni yake ya "FUNGUKA KWA WAZIRI" Lukuvi amesikiliza kero za ardhi za wananchi zaidi ya 200 wa wilaya ya Handeni zilizowasilishwa kwake. Kampeni hiyo iliyoanza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo wakazi wengi wa mji huo wamelalamikia suala la kulipwa fidia ndogo au kutokulipwa fidia zao kabisa.

Lukuvi amesema Halmashauri nyingi zimekuwa na pupa za kupanga viwanja bila kuwalipa wananchi fidia na hata ikitokea wakalipa fidia basi fidia itakuwa ndogo sana kwani kwa kufanya hivyo kutazidisha migogoro mingi ya ardhi isiyo ya lazima, hivyo amezitaka halmashauri kupitia upya madai ya wananchi na kuwalipa stahiki zao.

”Kwa kuwa hapa sasa mashamba mengi ya mji huu yamegeuka kuwa ni miji, lazima hawa watu muwafidie viwanja zaidi kuliko pesa kama wanataka pesa basi wauze wenyewe hivyo viwanja, hamuwezi kuwapa shilingi milioni tatu wakati nyinyi mnauza viwanja milioni kumi. Kumekuwepo na unyang’anyi na kuwalazimisha watu kupima viwanja kwa fidia kidogo. Na kwa mujibu wa sheria ya fidia kama hujamlipa mwananchi kwa miaka zaidi ya miwili basi inatakiwa ufanye tathmini upya”.

Hata hivyo Lukuvi ameshangazwa na wingi wa migogoro ya Ardhi ambayo ilikwisha patiwa ufumbuzi wake na mingine ilikwisha tolewa hukumu na Mahakama lakini cha kushangaza bado wananchi wanacheleweshewa haki zao hivyo kuwaamuru Maafisa ardhi kuhakikisha wanashughulikia swala hilo haraka iwezekanavyo kwani asingependa kuona swala hilo likijirudia tena.

Lukuvi amesema kuwa amebaini 90% ya Wananchi wa Handeni hawana uwelewa juu ya hatimiliki ya ardhi zao wanazomiliki kwani ameshangazwa sana kuona wengi wao hawafahamu mipaka ya maeneo yao hali inayopelekea kuzuka kwa migogoro ya mipaka hivyo amewaasa wananchi kuyafatilia maeneo yao na kuyapatia hati miliki ili kuyalinda na wavamizi kwani Hati ndio kielelezo namba moja kinachotambulika kisheria.

"mimi kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ipo migogoro ambayo nina uwezo wa kuitafutia ufumbuzi kutokana na mamlaka niliyonayo na ndio maana nimeamua kuwa na kampeni ya Funguka kwa Waziri ili kusikiliza kero mbalimbali za Ardhi lakini hii migogoro ya mtu na mtu inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi ndani ya ofisi zenu za ardhi au wilaya" Amesema Waziri Lukuvi.

Hata hivyo baada ya kusikiliza kero za wananchi Waziri Lukuvi ameahidi kuanzisha Baraza jipya la Ardhi na Nyumba la Wilayani Handeni kwani wananchi wamekuwa wakisafiri hadi Wilayani Korogwe kusikiliza mashauri yao jambo ambalo limekuwa na ucheleweshaji wa kusikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wakati kwani ndio chanzo cha migogoro mingi Wilayani hapo.

Aidha, akifunguka mbele ya Waziri Bi. Telessa Petro Gumbo ambae ni mkazi wa Handeni amelalamikia uvamizi wa uliofanywa katika shamba lake ambapo amemuomba Waziri Lukuvi kuingilia kati swala lake la kutolulipwa fidia baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kulimega eneo lake na kupitisha barabara hali inayomlazimu kulipwa fidia ya eneo hilo.

Naye, Bi. Amina Ali Kiale ambae pia ni mkazi wa Handeni amemlalamikia Waziri lukuvi kwa baadhi ya watendaji wa Ardhi ambao sio waaminifu kushiriki katika vitendo vya kudhurumu ardhi kwa kuwacheleweshea hati zao kwa muda mrefu wanapokuwa wanazifatilia.

Katika kutoa shukurani kwa Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amemshukuru Lukuvi kwa kitendo cha kuifanya programu hiyo ya FUNGUKA KWA WAZIRI katika Wilaya yake ya Handeni kwani imeweza kutatua migogoro ya ardhi iliyodumu muda mrefu na kuahidi kushughurikia migogoro iliyobaki katika ofisi yake ya Wilaya.
 Sharifa Mussa Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimuonesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
 Amina Ali Kiwale Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimuelezea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
 Sufian Sanyimina Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimpa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi uthibitisho wa madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WANANCHI WOTE WALIODHURUMIWA KULIPWA FIDIA.

0
0
Sharifa Mussa Mkazi wa kitongoji cha Chanika akimuonesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi madai yake ya fidia ya ardhi ambayo bado hayajalipwa wakati wa mkutano wa hadhara wa utatuzi wa kero za ardhi kwa wakazi wa mji wa Handeni katika uwanja wa Soko la Zamani Chanika maarufu Nyerere Square Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akimpa taarifa ya Wilaya ya handeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuhusu sekta ya ardhi katika Wilaya yake.

********************************

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameziagiza Halmashauri za Miji pamoja na watu wenye mashamba makubwa wahakikishe wanawalipa fidia Wananchi wote ambao hawajalipwa kwa muda mrefu tangu kufanyika kwa tathmini kwani wananchi wengi wamekuwa wakiishi ndani ya mashamba yao kwa muda mrefu na wakiamishwa hawalipwi fidia zao kwa miaka mingi na wengine kuondolewa bila kulipwa kabisa.

Waziri Lukuvi meyasema hayo alipofanya ziara Wilayani Handeni Mkoani Tanga wakati wa kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Soko la zamani Chanika maarufu Nyerere Squre Katika mkutano huo Waziri wa Ardhi aliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo Godwin Gondwe akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Handeni Mhe. Omari Abdallah Kigoda na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Kupitia kampeni yake ya “FUNGUKA KWA WAZIRI” Mhe. Lukuvi amesikiliza kero za ardhi za wananchi zaidi ya 200 wa wilaya ya Handeni zilizowasilishwa kwake. Kampeni hiyo iliyoanza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo wakazi wengi wa mji huo wamelalamikia suala la kulipwa fidia ndogo au kutokulipwa fidia zao kabisa.

Mh. Lukuvi amesema Halmashauri nyingi zimekuwa na pupa za kupanga viwanja bila kuwalipa wananchi fidia na hata ikitokea wakalipa fidia basi fidia itakuwa ndogo sana kwani kwa kufanya hivyo kutazidisha migogoro mingi ya ardhi isiyo ya lazima, hivyo amezitaka halmashauri kupitia upya madai ya wananchi na kuwalipa stahiki zao.

”Kwa kuwa hapa sasa mashamba mengi ya mji huu yamegeuka kuwa ni miji, lazima hawa watu muwafidie viwanja zaidi kuliko pesa kama wanataka pesa basi wauze wenyewe hivyo viwanja, hamuwezi kuwapa shilingi milioni tatu wakati nyinyi mnauza viwanja milioni kumi. Kumekuwepo na unyang’anyi na kuwalazimisha watu kupima viwanja kwa fidia kidogo. Na kwa mujibu wa sheria ya fidia kama hujamlipa mwananchi kwa miaka zaidi ya miwili basi inatakiwa ufanye tathmini upya”. 

Hata hivyo Mh.Lukuvi ameshangazwa na wingi wa migogoro ya Ardhi ambayo ilikwisha patiwa ufumbuzi wake na mingine ilikwisha tolewa hukumu na Mahakama lakini cha kushangaza bado wananchi wanacheleweshewa haki zao hivyo kuwaamuru Maafisa ardhi kuhakikisha wanashughulikia swala hilo haraka iwezekanavyo kwani asingependa kuona swala hilo likijirudia tena. 

Mhe. Lukuvi amesema kuwa amebaini 90% ya Wananchi wa Handeni hawana uwelewa juu ya hatimiliki ya ardhi zao wanazomiliki kwani ameshangazwa sana kuona wengi wao hawafahamu mipaka ya maeneo yao hali inayopelekea kuzuka kwa migogoro ya mipaka hivyo amewaasa wananchi kuyafatilia maeneo yao na kuyapatia hati miliki ili kuyalinda na wavamizi kwani Hati ndio kielelezo namba moja kinachotambulika kisheria.

“mimi kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ipo migogoro ambayo nina uwezo wa kuitafutia ufumbuzi kutokana na mamlaka niliyonayo na ndio maana nimeamua kuwa na kampeni ya Funguka kwa Waziri ili kusikiliza kero mbalimbali za Ardhi lakini hii migogoro ya mtu na mtu inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi ndani ya ofisi zenu za ardhi au wilaya” Amesema Waziri Lukuvi.

Hata hivyo baada ya kusikiliza kero za wananchi Waziri Lukuvi ameahidi kuanzisha Baraza jipya la Ardhi na Nyumba la Wilayani Handeni kwani wananchi wamekuwa wakisafiri hadi Wilayani Korogwe kusikiliza mashauri yao jambo ambalo limekuwa na ucheleweshaji wa kusikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wakati kwani ndio chanzo cha migogoro mingi Wilayani hapo.

Aidha, akifunguka mbele ya Waziri Bi. Telessa Petro Gumbo ambae ni mkazi wa Handeni amelalamikia uvamizi wa uliofanywa katika shamba lake ambapo amemuomba Waziri Lukuvi kuingilia kati swala lake la kutolulipwa fidia baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kulimega eneo lake na kupitisha barabara hali inayomlazimu kulipwa fidia ya eneo hilo.

Naye, Bi. Amina Ali Kiale ambae pia ni mkazi wa Handeni amemlalamikia Waziri lukuvi kwa baadhi ya watendaji wa Ardhi ambao sio waaminifu kushiriki katika vitendo vya kudhurumu ardhi kwa kuwacheleweshea hati zao kwa muda mrefu wanapokuwa wanazifatilia.

Katika kutoa shukurani kwa Mhe. Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amemshukuru Mh. Lukuvi kwa kitendo cha kuifanya programu hiyo ya FUNGUKA KWA WAZIRI katika Wilaya yake ya Handeni kwani imeweza kutatua migogoro ya ardhi iliyodumu muda mrefu na kuahidi kushughurikia migogoro iliyobaki katika ofisi yake ya Wilaya.

TAASISI YA DAWA ASILIA YAASA KUWEKEZA KWENYE TAFITI ZA DAWA ASILIA

0
0
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi na Utafiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Profesa Mohammed Sheikh aikungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mtafiti Mwandamizi wa utafiti wa Mradi wa Fellow, Dk. Francis Machumi na katikati ni Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Khadija Malima. 

 Mkurugenzi wa Utafiti wa tiba asili, Joseph Otieno akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Profesa Mohammed Sheikh na Mtafiti Mkuu Kiongozi waTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Khadija Malima. 
 Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Khadija Malima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Profesa Mohammed Sheikh na Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya Dawa asili, Dk. Khadija Malima. 

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
KUNA haja ya kuwekeza katika tafiti za ya dawa asilia nchini kwani Tanzania inamalia asili nyingi ambazo zitaweza kuimalisha afya ya kila mtu.

Hayo yamesemwa na Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Khadija Malima jijini Dar es Salaam leo wakati akingumgumza na waandishi wa habari ikiwa ni kuelekea mkutano wa mabaraza ya kitafiti utakaofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 11 hadi 15 unaondaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

"Ili kuhakikisha dawa asilia ni salama kwa binadamu, dawa hizo zinaweze kutibu na kuondoa matatizo ya magonjwa, dawa hizo zinatakiwa kufanyiwa utafiti na zitengenezwe ka kiwango cha hali ya juu na kwauwingi".

Khadija Amesema kuwa viwanda vikishiriki katika utafiti wa dawa asilia tuweze kupata dawa na kufungua soko la dawa asilia kwa nchini za Afrika mashariki na katika na nchi za kusini mwa jangwa la sahara.

Hata hivyo amesema kuwa tunaweza kujikita katika matumizi ya fedha za uuma kwaajili ya kwaajili ya kufanya tafiti ambazo zitatupatia dawa za asili lakini sio lazima ziwe zifikie kiwango cha vidonge kwani hiyo itachukua miaka mingi, lakini tukitumia maliasili  tuliyokuwa nayo tunaweza pia kuwekeza ili kujiletea maendeleo.

"Ili kuhakikisha hizo dawa ni salama kwa binadamu, ziweze kutibu na kuondoa matatizo ya magonjwa,zinatakiwa zitengenezwe kwa kiwango cha hali ya juu na kwa uwingi".

Hata Hivyo Mkurugenzi wa taasisi ya dawa asili, Joseph Otieno amesema kuwa biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza ni kwenye kitengo cha dawa asili kwani dawa huzi zinatafutwa na nchi za nje ikiwepo Marekani, Uholanzi, ujerumani, China na Kolea.

" Watu hawa wanakuja hapa Muhimbili katika Taasisi ya tiba asili wakihitaji tuweze kushirikiana nao ili waweze kujua dawa zinazotokana na miti dawa zinazoweza Kuendelezwa ili kupambana na maradhi yanayoongezeka duniani ambayo yamekuwa sugu na hayawezi kutibika kirahisi kwa dawa ambazo tayari zimevumbuliwa".

Otieno amesema kuwa Tanzania inamiti zaidi ya elfu 12 lakini kati ya hiyo zaidi ya asilimia 25 imesharekodiwa  kwamba ni ya dawa lakini kinachokosekana ni utafiti ambao unahusisha waganga wa asili, kuungwa mkono na serikali kuhakikisha kwamba hii miti inafanyiwa utafiti kwaajili ya kutibu magonjwa yanayotusumbua.

WAFANYABIASHARA WASHAURIWA KUTUNZA KUMBUKUMBU ILI KULIPA KODI STAHIKI

0
0
Na Veronica Kazimoto,Simiyu

Wafanyabiashara nchini wameshauriwa kutunza kumbukumbu za biashara zao ili kulipa kodi stahiki na hatimaye kupunguza kero ya madai yao kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakadiria kodi kubwa isiyoendana na uhalisia wa biashara wanazofanya.

Akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka mamlaka hiyo Diana Masalla, amesema kuwa, wafanyabiashara walio wengi hawana tabia ya kutunza kumbukumbu za biashara zao suala linalosababisha malalamiko mengi baada ya kukadiriwa kodi na TRA.

“Ndugu zangu wafanyabiashara sote tunajua kwamba, mali bila daftari hupotea bila habari hivyo basi, niwaombe mjenge tabia ya kutunza kumbukumbu za biashara zenu siyo tu kwa ajili ya TRA lakini pia kwa ajili yenu wenyewe kwani mtaweza kujua kama biashara zenu zinakua au zinashuka lakini pia mtaweza kupanga bajeti za mauzo na manunuzi yenu vizuri na mwisho wake mtalipa kodi stahiki na kuchangia maendeleo ya nchi yetu,” amesema Masalla.

Masalla ameongeza kuwa, kuna tofauti kubwa kati ya mfanyabiashara anayetunza kumbukumbu na yule asiyetunza kumbukumbu kwani asiyetunza kumbukumbu kwa mauzo ya shilingi milioni 14 atalipa kodi shilingi 450,000 kwa mwaka wakati anayetunza kumbukumbu kwa mauzo hayo atalipa shilingi 320,000 kwa mwaka.

“Tukichukulia mfano wa wafanyabiashara wawili wenye mauzo ya shilingi milioni 14, lakini mmoja anatunza kumbukumbu na mwingine hatunzi kumbukumbu tunaona kwamba, kuna tofauti ya shilingi 130,000 kwa kuwa asiyetunza atalipa shilingi 450,000 na anayetunza kumbukumbu atalipa shilingi 320,000. Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu,” amesisitiza Masalla.

Meneja huyo wa Elimu kwa Mlipakodi amewaambia wafanyabiashara hao kuwa, nyenzo muhimu inayosaidia utunzaji wa kumbukumbu ni pamoja na Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) na kama mfanyabiashara hajafikia mauzo ya kutumia mashine ya EFD ambayo ni chini ya shilingi milioni 14 anashauriwa kutumia kitabu cha risiti za kuandika kwa mkono ambapo mfanyabiashara atakwenda na kumbukumbu hizo TRA kwa ajili ya kukadiriwa kodi.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa mbao wilayani humo, Zakaria Manyilizu amesema kuwa, elimu aliyoipata ya utunzaji kumbukumbu za biashara ni nzuri hata hivyo ameiomba TRA kutoa elimu juu ya namna ya kutumia mashine za EFD kwani walio wengi hawana utalaamu wa kutumia mashine hizo.

“Kwa kweli tunaishukuru TRA kwa kutuletea elimu hii ya utunzaji wa kumbukumbu hapa wilayani Busega lakini sisi tulio wengi hatujui kutumia vizuri mashine za EFD hivyo ninaiomba TRA itufundishe namna ya kutumia mashine hizi ili na sisi tunufaike na faida za utunzaji kumbukumbu alizozieleza meneja wa TRA,” alisema Manyilizu.

Timu ya Maofisa wa kodi wakiongozwa na Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania wako Mkoani Simiyu katika Wilaya ya Busega na Bariadi ambapo wanakutana na wafanyabiashara mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi ikiwa ni pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.
   Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla akitoa elimu ya kodi wakati wa semina ya wafanyabishara wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Nyashimo.
 Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla akiwafundisha wafanyabishara wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu tofauti iliyopo kati ya mfanyabishara anayetunza kumbukumbu na asiyetunza kumbukumbu katika semina ya wafanyabishara hao iliyofanyika mjini nyashimo.
Mfanyabishara wa duka katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Paulina Hinda akichangia hoja wakati wa semina ya wafanyabishara ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanyika Mjini Nyashimo Wilayani humo.

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA JIOLOJIA

0
0
Na Asteria Muhozya, DSM
Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa wito kwa kuzitaka nchi za Afrika kujenga uwezo kwa Wataalam wa ndani wa Jiolojia ili kuwawezesha kujenga uwezo wa tafiti za rasilimali madini ili pindi nchi au taasisi wafadhili wanapoacha kufadhili, mamlaka husika ziwe kwenye nafasi ya kuendeleza shughuli hizo.

Waziri Biteko ameyasema hayo Oktoba 24, 2019 wakati akifungua Mkutano wa 36 wa Wataalam wa Jiolojia kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao wanakutana jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo unalenga katika kuwapatia wataalam hao mafunzo yanayogusa masuala mabalimbali kuhusu sekta ya Madini ikiwemo kubadilishana uzoefu katika utafutaji rasilimali madini na kuangalia namna bora ya kuendeleza rasilimali hizo ili kuhakikisha kwamba zinayanufaisha mataifa husika. 
Aidha, amewataka washiriki wa mkutano huo kujifunza na kutumia vyema uzoefu mzuri utakaotolewa na mataifa mengine ili kuwezesha kuongeza thamani  katika kutekeleza majukumu  ya taasisi zao  katika uendelezaji wa rasilimali madini.

‘’ Afrika lazima tujifunze wenyewe kuendeleza na kujenga miradi yetu wenyewe. Katika mkutano yapasa kujiuliza siku Wafadhili wetu Umoja wa Ulaya na  taasisi nyingine zinazofadhili mafunzo haya zikiacha tutaweza kujisimamia wenyewe?,’’ amehoji Waziri Biteko.
Amesema kwa upande wa Tanzania kama taifa linaamini katika kuwajengea uwezo wataalam wa ndani ambapo tayari serikali imechukua hatua kadhaa za kuhakikisha zinawendeleza wataalam wake ili kuwezesha taifa kuzalisha wataalam waliobobea katika taaluma ya jiolojia na ambao watakuwa na mchango katika utafutaji wa rasilimali madini.

Amesema mradi huo wa kutoa Mafunzo kwa Taasisi za Jiolojia Afrika unafadiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na taasisi nyingine 12 ambapo tangu kuanzishwa kwa mradi huo mnamo mwaka 2017, tayari umewezesha kuwapatia mafunzo wataalam wapatao 1,100 kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika huku wataalam 30 wa Tanzania wakiwa wamepatiwa mafunzo hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano  Kutoka Umoja wa Ulaya, Jose Dorreia Nunes, amewataka washiriki wa mkutano huo kutafakari namna rasimali hizo zitakavyozinufaisha nchi zao ikizingatiwa kwamba madini ni chanzo kikubwa cha mapato kwa nchi za Afrika hivyo ni muda sahihi kupitia mafunzo yanayotolewa na Umoja huo yawezeshe kujenga uwezo wa wataalam wa ndani katika kutafiti, kusimamia na kuendeleza rasilimali katika nchi zao.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Yorkberth Myumbilwa akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo amesema mafunzo yanayotolewa na Taasisi wafadhili yana umuhimu mkubwa kwa kuwa yanagusa moja kwa moja shughuli zinazofanywa na taasisi hizo zikiwemo tafiti, wingi wa mashapo, urithi wa Jiolojia, namna ya kuhifadhi data na masuala mengine.
Ameongeza kwamba, suala la kukutanishwa na taasisi nyingine lina umuhimu kwa GST kwa kuwa linawezesha kujenga mahusiano mapya na Taasisi nyingine za Jiolojia kutoka nchi nyingine. 

Nchi zinazoshiriki mkutano unafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 24 – 25 Oktoba, 2019 ni pamoja na Tanzania, Namibia, Sengel Morroco, Kenya, Afrika Kusini , Rwanda, Zambia na Ghana.
 Waziri wa Madini Doto Bteko akifungua Mkutano wa 36 wa Watalaam wa Jiolojia kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
 Wataalam wa Jiolojia kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wataalam wa Jiolojia. 
 Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na baadhi ya Wataalam wa Jiolojia kutoka Mataifa mbalimbali.
Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa 36 wa Wataalam wa Jiolojia kutoka nchi mbalimbali za Afrika unaofanyika Jijini Dar es Salaam

KAMATI YA BUNGE YA PAC YARIDHISHWA NA HESABU ZA SEKTA YA UJENZI

0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
Mhe. Nangenjwa Kaboyoka, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius
Mwakalinga, (hayupo pichani) mara baada ya Sekta yake kuwasilisha
taarifa ya hesabu zake mbele ya Kamati hiyo, jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, (hayupo pichani), wakati
akiwasilisha taarifa ya hesabu za Sekta yake mbele ya kamati hiyo.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Singida, Mheshimiwa Asha-Rose
Matembe, akitoa maoni yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga
(hayupo pichani), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuwasilisha taarifa ya
hesabu za Sekta yake kwa Kamati hiyo.

PICHA NA WWUM

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,imekubali maombi ya Chama cha ACT

0
0
 MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imekubali maombi ya Chama cha ACT- Wazalendo kujiunga katika kesi ya kikatiba inayohusu ukomo wa urais, iliyofunguliwa na mwananchi anayejitambulisha kama mkulima, Dezydelius Patrick Mgoya.

 Uamuzi huo umetolewa leo Alhamis, Oktoba 24, 2029 na Jaji Dk. Benhajj Masoud , baada ya kuridhika na hoja za chama hicho kuwa kina maslahi katika shauri hilo.

Kesi hiyo ya Mgoya imefungua mahakamani hapo, masjala Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiiomba mahakama itoe tafsiri ya maana sahihi na athari za masharti ya Ibara ya 40(2) ya Katiba ya Nchi inayoweka ukomo wa mtu kuchaguliwa kuwa rais.

Katika Maombi hayo, Mgoya anadai kuwa masharti ya ibara hiyo ya 40(2) ya mihula miwili tu ya raia kuchaguliwa kuwa rais yaani miaka 10 tu yanakiuka haki za kikatiba za Ibara za 13, 21 na 22(2) hasa kushiriki katika shughuli za utawala kwa kuchagua na kuchaguliwa.

Hata hivyo Serikali kupitia kwa AG tayari imeshamwekea pingamizi la awali ikiiomba mahakama hiyo iitupilie mbali pamoja na mambo mengine ikidai kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, na kwamba kesi hiyo ina kasoro za kisheria ambazo haziwezi kurekebishika.

Pia inadai kuwa mwombaji hana haki ya kisheria kufungua na kwamba nafuu anazoziomba mwombaji haziwezi kutolewa kwa kuwa zinakiuka kifungu cha 44 cha Sheria ya Mawakili, Sura ya 341, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo, kabla ya mahakama hiyo kusikiliza pingamizi hilo la Serikali Bodi ya Wadhamini wa ACT, iliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kujiunga katika kesi hiyo, kama mdaawa mwenye maslahi, kwa madai kuwa wana maslahi nayo na kwamba wanataka kutetea kile wanachokiita maslahi yao.

 Muombaji Mgoya kwa upande wake alipinga maombi hayo, pamoja na mambo mengine akidai kuwa chama hicho hakina sababu za msingi za kuunganishwa katika kesi hiyo hoja ambazo zinetupiliwa mbali na mahakama kuu ikisema kuwa chama hicho kina haki ya kuunganishwa.

Jaji Masoud amesema kuwa katika mashauri ya kikatiba mtu yeyote awe na maslahi binafsi au asiwe na maslahi binafsi anaweza kuwasilisha maombi mahakamani na kwamba kwa kuwa shauri lililoko mahakamani ni la kikatiba basi mwombaji (ACT_Wazalendo) kina maslahi katika shauri hilo.

Katika shauri la msingi linalosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Kiongozi, Dk. Elieza Feleshi, akishirikiana na Jaji Dk. Masoud na Jaji Seif Kulita, limepangwa kutajwa mahakamani hapo kesho kwa ajili ya mahakama kutoa maelekezo maalum.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuendelea na kesi ya IPTL

0
0
Na Karam Kenyunko, globu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power (IPTL), Herbinder Seth na Mfanyabiashara, James Rugemarila, kwa sababu mshtakiwa Rugemarila ni mgonjwa na hajaweza kufika mahakamani.

Hata hivyo, licha ya kwamba Rugemarila kuumwa bado kesi hiyo iko kwenye sintofahamu hususani juu ya Washtakiwa hao kuandika barua kwa  DPP wakitaka kufikia makubaliano jinsi ya kumaliza shauri lao.

Sintofahamu inakuja pale ambapo Sethi anadaiwa kuandika barua lakini hajawahi kuifahamisha mahakama kama ambavyo sheria inamtaka kufanya hivyo baada ya kuandika barua.

Mapema leo Oktoba 24,2019  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika  na kwamba mshtakiwa Rugemarila anaumwa.

Hata hivyo baada ya maelezo hayo ya wakili Wankyo, ambayo hayakueleza   chochote kuhusiana na kinachoendelea kwa DPP,  mawakili wa utetezi nao hawakuzungumza chochote

 Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Seth na mwenzake Rugemarila wanakabiliwa na mashitaka  12 ya uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha Serikali hasara ya USD  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

RASHFORD NYOTA WAKUTAZAMWA ENGLAND

0
0
   Na.Khadija seif, Michuzi TV
MFULULIZO  wa kupachika Magoli muhimu kwa Timu ya Taifa ya England na Klabu yake ya Man United hivi karibuni kwa msimu huu wa 2019/2020.

Hatimae imemtambulisha upya kinda Marcus Rashford Kama mmoja ya Nyota vijana wakutazamwa Sana katika Soka Ulimwenguni kwa Sasa.

Alhamisi  hii Mashetani wekundu watatua Nchini Ubelgiji kukipiga na Partizan Belgrade katika Europa League mapema saa 1:55 usiku.

Mechi hii  itaoneshwa mubashara kupitia King'amuzi cha startimes  pekee kwenye chaneli  ya World Football. 

Hata hivyo Mashabiki wanabaki na sitonfahamu Kuhusu Rashford kuiongoza Vema Man United katika Mchezo huu.

HARMONIZE AUZA MALI ZAKE ILI KUPATA MILIONI 500 YA KUWALIPA WCB

0
0
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul 'harmonize'.

MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul 'harmonize' amesema ameuza baadhi ya mali zake na kulipa fedha kwa Uongozi wa WBC ili aweze kutumia nyimbo zake kama zamani.

Harmonize ameyasema hayo wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm leo alipokwenda kutambulisha nyimbo yake mpya ya Uno.

Amesema, amefuata sheria ya taratibu za Mkataba, alitakiwa kulipa Milioni 500 na baadhi gharama ambapo hakuwa na fedha ikambidi auze mali zake.

 "Kiukweli kule sijaondoka kwa ubaya, tumefuata sheria na taratibu za mkataba! Nilitakiwa kulipa million 500 na baadhi ya gharama, kiukweli sikuwa na pesa lakini nimeuza baadhi ya mali zangu ili nifanikiwe kulipa hiyo pesa na kwa asilimia kubwa nimelipa bado asilimia chache tu ili niweze kutumia kitu chochote kinachomuhusu Harmonize"

Harmonize amesema kuwa,  mahusiano yake na uongozi wake uliopita hauko sawa, na kuhusu kutokuhudhuria kwa ndoa yake na Mkewe Sarah ni kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameiweka ya kutaka ndugu zake walioishi vizuri Kijijini kwao ndio wawe wahudhuriaji.

“Sitaki kusema uongo, Mahusiano yangu na uongozi wangu uliopita sio kama zamani, na kuhusu wao kushindwa kuhudhuria ndoa yangu mimi niliweka nadhiri kuwa siku ya ndoa yangu ningependa wahudhuriaji wawe ni ndugu zangu niloishi nao vizuri kijijini”

Akizungumzia msiba wa Ruge, Harmonize amesena nyuma ya Harmonize kuna Rajabu na lazima ahusike kwenye masuala ya kibinadamu   na alikuwa anaumia sana nyimbo zake kutokupigwa kwenye Redio hiyo.

"Mimi ni Harmonize, lakini nyuma yangu kuna Rajabu, Kwenye mambo ya kibinadamu Rajabu lazima ahusike ndio maana nilishiriki kwenye mazishi ya Ruge, Nilichokifanya hakikuniletea matatizo kwenye uongozi wangu uliopita” 

“Amani ndio kitu nilikimiss kipindi ngoma zangu hazipigwi  Clouds, nilikuwa natamani kama hivi nikutane na na nyie tupige story, Naheshimu misingi ya kibiashara lakini sasa tuko good” 

Harmonize ameweka wazi kuwa, "Jembe ni mtu aliyekuwa akinisupport tangu kitambo, Baada ya kuvunja mkataba na lebo yangu ya nyuma! Jembe akaamua kuanza kunisupport japo watu wengi wamekuwa wakimtafsiri vibaya na kuhisi kwamba yeye ndio chanzo cha kunifanya niondoke kule lakini sio kweli”

Harmonize ameanza kufanya ziara ya Vituo vya redio kutambulisha nyimbo yake na kueleza masuala mbalimbali baada ya kuachana na uongozi wake wa zamani WCB.

Mwamoto ametoa vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki ligi ya Asas Super League

0
0

 Nahodha wa timu ya IroleFc akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020
 Nahodha wa timu ya Mbega Mwekundu akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020.
 Nahodha wa timu ya IroleFc akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020.
Mchezaji wa timu ya Mbega Mwekundu akikabidhiwa vifaa na mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava kwa ajili ya ligi ya Asas Super League 2019/2020.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
MBUNGE wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto ametoa vifaa vya michezo kwa timu mbili zinazoshiriki ligi ya Asas Super League ambazo ni Irole Fc na Mbegu Mwekundu ambazo zinatoka katika wilaya ya Kilolo


Akizungumza wakati wa kukabidhi jezi,viatu na mipira mbunge huyo alisema kuwa ametoa vifaa hivyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri kwenye ligi ya Asas Super League ya msimu wa mwaka wa 2019/2020.


Hivi vifaa viwaongezee hali ya kupambana ili kuhakikisha mnakuwa mabingwa wa league hii ambayo imekuwa na ubora sana tofauti na ilivyokuwa hapo awali,nawaombeni sana hakikisheni mnapambana kupata matokeo chanya kila mechi mnayoicheza”alisema Mwamoto


Mwamoto aliwataka wachezaji wa timu zote mbili kucheza kwa nidhamu ya juu kwa kuwa mpira miguu ndio unataka hiyo.


“Timu ya Mbega Mwekundu na wenzenu Irole Fc hamjaonyesha nidhamu kwenye mechi hii zenu hivyo mnatakiwa kulinda nidhamu yenu ili muwezekufika mbali kisoka” Mwamoto


Mwamoto alisema kuwa jezi na vifaa vingine vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi milioni mbili na vyote vimetolewa na ofisi ya mbunge kwa lengo la kuwasaidia timu hizo kwenye ligi hiyo.


Naye Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava alisema kuwa ataendelea kuzichangia timu hizo nauli pamoja na maji ya kunywa kwenye kila mchezo hivyo wachezaji wanapaswa kucheza kishindani ili wapate matokeo.


“Mimi nitatoa laki moja kwa kila mechi ambayo mtashinda hivyo kazi imebakia kwenu kuhakikisha mnashinda michezo yote iliyobakia na kufanikiwa kuingia nane bora” alisema Kuyava


Aidha Kuyava alisema kuwa mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto ameongeza kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa kila mechi ambayo watashinda hivyo inakuwa laki moja na nusu kwa kila mchezo watakaoshinda .


Kuyava alimalizia kwa wachezaji na viongozi kuwa na nidhamu kwenye michezo mbalimbali ili kuwa timu bora na yenye ushindani wa kweli.

Wakuu wa vituo vya Polisi waitwa Mahakamani

0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaamuru Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay na cha Kijitonyama kufika mahakamani hapo kesho kueleza  kwanini wamekaa na mshitakiwa kituo cha polisi badala ya kumpelekeka gerezani.

Oktoba 10, mwaka huu mahakama ilitoa amri kwa mshitakiwa ambaye ni msimamizi wa mirathi wa mke wa marehemu, Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) kwenda gereza la Segerea kwa sababu anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana.

Amri hiyo imetolewa leo Oktoba 24,2019 na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kevin Mhina baada ya wakuu hao kukaa na mshitakiwa huyo kituo cha polisi badala ya kumpeleka gerezani kama amri ilivyotolewa.

Kesi hiyo leo ilikuja mahakamani hapo lakini  haikuweza kusikilizwa kutokana na mkanganyiko uliokuwepo baada ya mshitakiwa huyo kubainika hakuwepo gereza la Segerea na kwamba alikuwa kituo cha polisi.

Mshitakiwa huyo aliletwa mahakamani akitokea Kituo cha Polisi Kijitonyama alikokuwa amekaa kwa siku saba na Kituo cha Oysterbay alikaa siku saba.

Katika kesi hiyo, Elizabeth ambaye ni Mkazi wa Boko Magengeni,  anakabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh milioni 25 kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Awali wakili Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai  kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk Roderick Kisenge kwa ulaghai.

Mshitakiwa anadaiwa  kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambalo halijapimwa lililopo eneo la Boko Dovya Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Wankyo alidai katika kipindi hicho  mshitakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Katika Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka, Elizabeth hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya Uhujumu Uchumi na Hakimu Mhina alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana kisheria.

Hivyo alielekeza mshitakiwa huyo kurudishwa rumande katika gereza la segerea hadi leo kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

TRA YAPITISHA MASHINE ZA EFD, KWA WAENDESHA MALORI

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kati na Wadogo wa Malori nchini (TAMSTOA), Chuki Shaaban akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada yakufanya mazungumzo na Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhusu Magari hayo yanayosafirisha mizigo nje ya nchi kuhakikisha wanapata Mashine za EFD na kupata Leseni ya usafirishaji mizigo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Madalali Wanaosafirisha Mizigo Tanzania, Rajabu Masasi akizungumzia malengo yao kwa Wamiliki wa Malori nchini.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
CHAMA Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shaaban (TAMSTOA) kimeeleza kufika mwafaka na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhusu Magari hayo yanayosafirisha mizigo nje ya nchi ili kuondoa vikwazo katika usafirishaji nje ya nchi. 

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo kati ya Uongozi wa Chama hicho na Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Abdul Mapembe kwa Madereva wa Malori hawatakamatwa tena kwa ajili ya Mashine ya EFD lakini madereva hao wanapaswa kuwa na Risiti ya Mashine hiyo ya EFD ili kupata Leseni mpya ya usafirishaji mizigo nje ya nchi ifikapo 2020.

Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shaaban amethibitisha kufika makubaliano hayo, amesema wamekubaliana na TRA, ili kupata leseni ya sasa ya usafirishaji mizigo Nje ya Nchi kwa Dereva lazima awe na Risiti ya yakununulia Mashine ya EFD ili kuondoa vikwazo katika usafirishaji mizigo.

''Wenzetu wanaotoka Nje ya Nchi wanaotumia Bandari yetu wanalalamika mzigo haifiki kwa wakati kwa sababu ya mambo yetu ya ndani, kwa hiyo Kamishna akasema tukutane, tujadili sual hilo''; amesema Chuki. 

Pia amesema TAMSTOA imepunguza ada ya kupata Cheti, amesema wamebaini Wanachama wao wanashindwa kutatua changamoto zao kutokana hawana anuani kamili ya Chama hicho kupata taarifa. Chuki amesema ili kupata cheti katika Chama hicho lazima uwe na Kitambulisho cha Mmiliki wa Lori, Picha ya Mmili, Anuani (Address) na taarifa zozote za mawasiliano. 

Nao Chama cha Madalali Wanaosafirisha Mizigo Tanzania, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Rajabu Masasi amesema chngamoto walizokuwa nazo kwenye udalali tayari wamezijadili kwa kina, wana lengo lakuwaweka Wamiliki kuwa sehemu salama, amasema wamejadiliana kuwa na ushirikiano na Wamiliki wa Malori.

Mmoja wa Dereva wa Malori, Said Mascat ameishukuru Serikali kupunguza kero, changamoto nyingi kwa Madereva kwa kiasi kikubwa, amempongeza Rais Magufuli katika utawala wake kutokana na haki inayotendeka wanapokuwa katika majukumu yao ya udereva.

MSANII ALI KIBA AIOMBA SERIKALI KUTHAMINI MCHANGO WA WASANII KATIKA KUKUZA SEKTA MBALIMBALI.

0
0

  Na Khadija Seif, Michuzi TV

 MSANII wa Bongofleva Ally Saleh a.k.a Alikiba atunukiwa cheti cha ubalozi wa utalii wa ndani  na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.

"Nina  furaha kubwa kutunukiwa Cheti cha ubalozi wa Utalii wa ndani ili kuongeza chachu zaidi katika kukuza utalii wa Zanzibar na Tanzania kiujumla kwa Watanzania wenzangu na hata watalii kutoka nchi mbalimbali..." amesema Kiba.

Ali Kiba ametoa Shukrani za dhati kwa Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwa kuona mchango wake utafaa katika hilo.

"Nazidi kuziomba serikali zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar ziendelee kuthamini mchango wa wasanii wa Tasnia mbalimbali na watutumie katika kukuza sekta mbalimbali katika Nchi yetu,"

 Ali Kiba amekua akitumia baadhi ya vivutio vingi katika kutangaza utalii wa Tanzania Kama vile kutumia wanyama kama tembo na wengine kwenye Sanaa yake ya muziki.

DC KASESELA ATATUA MGOGORO WA ARDHI BAINA YA CHUO KIKUU CHA IRINGA NA WANANCHI

0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifurahia jambo na bi Mwaija Ngaga mara baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wako
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye meza moja na walalamikiwa pamoja na walalamika wakati wa kutatua mgogoro
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutatua mgogoro


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi saba dhidi ya chuo kikuu cha Iringa uliodumu toka mwaka 1992

Akizungumza kwenye ofisi za mkuu wa chuo hicho,Kasesela alisema kuwa amefanikiwa kuutatua mgogoro huo kutokana na kuzikutanisha pande mbili ambazo zilikuwa zinagombana kuhusu ardhi ya chuo hicho ilipochukuliwa mwaka 1992.

“Huu mgogoro ni wa miaka mingi na mimi nimeukuta hivyo leo nimefanikiwa kuumaliza kwa njia ya busara kabisa kitu ambacho pale zilizokuwa zinalalamika zimefikia muafaka” alisema Kasesela

Aidha Kasesela alisema kuwa wamefanikiwa kumaliza mgogoro kwa kuwatafutia kila mmoja kiwanja kimoja ili kufidia maeneo ambayo serikaliilikipatia chuo kikuu cha Iringa.

“Nimewaagiza uongozi wa chuo kuwa ikifika siku ya jumatatu waje ofisini kwangu ili wawalipe nauli zao hawa wananchi kwa kuwa wanawajibu kwa mujibu wa makubaliano yetu ambayo tulikuwa tumefikia kwenye kikao hiki” alisema Kasesela

“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema Kasesela

Kwa upande wa waliokuwa wanalalamika wakiwakilishwa Mwaija Ngaga pamoja na Zuhura Balama walisema kuwa wamelidhishwa na maamuzi yaliyofikiwa na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa kwa kumaliza mgogoro huo.

“Kwa kweli mkuu wa wilaya tunaomba ufikishe salamu zetu kwa Rais kwa kuchagua viongozi kama nyie wenye maono ya kushughulikia kero za wananchi maana la sivyo tulipanga kwenda Dodoma kumuona Rais” walisema wazee hao.

RC ALLY HAPI ATOA SIKU SABA UJENZI WA SOKO LA MLANDEGE KUKAMILIKA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wa mkoa Iringa juu ya hatma ya soko kuu la Mlandege lililopo katika manispaa ya Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akimsikiliza kwa makini mkandarasi wa soko la kisasa la Mlandege Manispaa ya Iringa
Moja ya eneo la soko kuu la kisasa la Mlandege lilopo Manispaa ya Iringa



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally salumu hapi amefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa soko kuu na la kisasa mlandege mjini Iringa na kuagiza kasi ya ujenzi iongezwe na mkandarasi wa Home Africa Constractions Engineering Ltd anayejenga soko hilo ili hadi kufikia October 31 mwaka huu liwe limekamilika tayari kwa matumizi ya wafanyabiashara.

Katika Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya kutembelea na kukagua ujenzi wa soko jipya unaoendelea hivi sasa mjini Iringa Hapi alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo huku akitoa agizo la kuhakikisha linakamilika mwishoni mwa mwezi huu Mwaka Huu.

“Ndani ya tarehe 31 mwezi huu kumi taa zote,umaliziaji vitu vyote ya soko hili viwe vimekamilika,nataka ifikapo mwezi wa 11 tarehe 1 tayari muwe tayari kukabidhi mradi huu wa kisasa kwa halmashauri ili iweke utaratibu wa mzuri wa matumizi kwa hiyo nawapa siku saba tuu soko hili liwe imekamirika”alisema hapi.

Aidha Hapi alisema kuwa mradi huo unagharimu shilingi bilioni 3.7 huku akimtaka mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa na wataalamu kuhakikisha wanaweka mpangilio mzuri wa watu kupata vibanda na maduka kwa halali bila manung’uniko na waliokutwa mwanzo ndio wapewe kipaumbele.

Alisema mkoa wa Iringa hauna duka kubwa la kisasa la kuuza bidhaa ,hivyo halmashauri iangalie katika soko hilo eneo wanaloweza kuweka kwajili ya uwekezaji wa duka kubwa litakalokuwa linatoa bidhaa zenye ubora ili kuongeza pato la hamashauri.

“Naomba nitumie fursa hii kuwapongeza sana mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela,mkurugenzi na mkandarasi kwa kazi kubwa mliyoifanya kuhakikisha soko hili linakamili hivi karibuni” alisema Hapi 

Simon s. bahegwa ni mkandarasi wa kampuni ya home Africa constractions alimesema kuwa thamani ya mradi ilikuwa shilingi bilioni 3.72 na ifikapo tarehe 31 october watakuwa wamekamilisha kama alivyoagiza mkuu wa mkoa.

“ mheshimiwa kufikia tarehe 31 mwezi huu tutakuwa tumekamilisha mradi huu kwa asilimia 100 kwa tukimaanisha kufunga taa ,na thamani ya mradi huu ilikuwa ni shilingi bilioni 3.72 na fedha iliyotumika mpaka sasa ni bilioni 2.6 tunategemea kukabidhi mradi huu mwishoni mwa mwezi huu”alisema bahegwa

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya iringa HAMID NJOVU alisema kuwa soko hilo la Mlandege linaukubwa wa Squermeter 3182 ambapo wanatarajia likianza kutumika litakuwa likiingiza mapato ya shilingi million 55 mpaka milioni 80 kwa mwezi.

Mradi wa ujenzi wa soko jipya la Mlandege Manispaa ya Iringa unagharimu taklibani shilingi bilioni 3.7 kwa fedha za serikali unaotarajiwa kuwa na jumla ya wafanyabiashara 2000 .

KIPANDE CHA PILI MOROGORO-MAKUTOPORA UJENZI WA SGR WAZIDI KUNOGA.

0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Elias John Kwandikwa amezindua utandikaji wa Reli ya kisasa kipande cha Pili Morogoro – Makutopora hivi karibuni oktoba 2019.

Katika gafla hiyo Naibu Waziri alimtaka mkandarasi aongeze kasi ili kuweza kumaliza kwa wakati.Aliongeza wakati wa uzinduzi wa zoezi la utandikaji reli katika eneo la Mkata mkoani Morogoro, Naibu Waziri Kwandikwa amesema kuwa, pamoja na kasi kubwa ya ujenzi wa Reli hiyo, lakini watanzania wamefaidika na fursa za Ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu nne na viwanda vilivyopo nchini kuweza kuongeza mapato kama viwanda vya Saruji na Nondo kea kupata fursa ya kuuzia wakandarasi

Naibu Waziri Kwandikwa ameongeza kuwa, ujenzi wa Reli ya kisasa unaotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano una lengo la kuboresha miundombinu ya reli na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za usafiri wa reli nchini na nchi jirani.

Katika gafla hiyo naye, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa, asilimia 90 ya eneo linalohitajika kwa ajili ya ujenzi wa Reli hiyo kipande cha Morogoro – Makutopora limekabidhiwa kwa Mkandarasi kampuni ya Yapi Markezi na kinachoendelea ni utekelezaji ili wamalize kwa wakati.

Sambamba na hafla ya utandikaji wa Reli kwa kipande cha pili Morogoro-Makutipora Naibu Waziri Kwandikwa akiongozwa na mwenyeji wake Mkurugenzi mkuu TRC Ndugu Masanja amepata fursa ya kutembelea eneo linapojengwa handaki refu zaidi kwenye ujenzi huo, lenye urefu wa Kilomita 1 na mita 31.

Kipande cha Pili ya ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipa
Morogoro -. Trilioni 4.4 kwa ajili ya utelekeza wa ujenzi wa SGR

UJUMBE WA CPC ZANZIBAR.

0
0
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou, akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Sheikh Abeid Amani Karume hapo Kisiwandui Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, akizungumza na ujumbe wa watu watano kutoka Chama cha Kikoministi cha China (CPC), walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou,akivishwa sikafu na Vijana Maalumu wa UVCCM baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou(kulia, akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kushoto).

(PICHA NA JOHN BOSCO EMILIAN).

TANZANIA YAKABIDHIWA URAIS WA AALCO

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga akiongoza Mkutano wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) Uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Katika Mkutano huo Waziri Mahiga alikabidhiwa kuwa Rais wa AALCO
Katibu Mkuu kutoka Wazira ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akizunguma na wageni wa Mkutano wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) kuhusu kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko tanzania bara na Zanzibar mara baada ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO), Prof. Kennedy Gastorn akiteta jambo na Mjumbe kutoka Sekritarieti ya AALCO mara baada ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga, akisalimia na Mmoja wa Washiriki wa Mkutano wa AALCO mara baada ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga, akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO), Prof. Kennedy Gastorn na Mkurugenzi Mkuu wa Sheria za Kimataifa kutoka Nigeria, Mhe.Wilfred Ikatari


Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga, akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa AALCO mara baada ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

…………………….

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambalo kikao chake cha 58 kimemalizika hapa Jijini Dar es Salaam safari hii kimeteua Tanzania kuwa Rais wa Shirika hilo na kwa maana hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania, Balozi Augustine Mahiga anashika nafasi hiyo.



Kikao hicho kilichoanza jumatatu, wiki hii kimemalizika leo naajenda mbalimbali zilijadiliwa huku msukumo ukilenga kuimarisha sheria za ukanda wao na Kimataifa kwa Ujumla.



Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Katiba na Sheria kutoka Tanzania ambaye ameanza wadhifa wake Rais Mpya wa AALCO amesema kuwa katika mfululizo wa vikao vyao kitu kikubwa kilichojadiliwa ni suala la vikwazo dhidi ya mataifa ambalo limekuwa tatizo kwa nchi mbalimbali.



“Mkutano huu ulikuwa unaangazia masuala mbalimbali na muhimu kwa nchi za Afrika na Asia na kwingineko duniani na suala ambalo lililpewa kipaumbele ni kuhusu vikwazo ambavyo nchi mbalimbali kubwa duniani zimekuwa zikiziwekea nchi ndogo, kitu ambacho kinaumiza wananchi katika nchi hizo”, amesema, Balozio Mahiga.



Balozi Mahiga, amesema kuwa Mkutano huo ambao washiriki wake ni kutoka Asia na Afrika unazingatia masuala mengi ya kisheria, likiwemo lile la vikwazo kwa nchi kama za Zimbabwe, Palestine, Iran na nyinginezo duniani.



Alieza kuwa suala la kuweka vikwazo halijadiliwi na nchi moja , wala mbili au tatu ambazo ni kubwa na kuwa zinajiweza kiuchumi, bali suala hilo ni la Chombo cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na hufikiwa ikiwa kuna wasiwasi wa kiusalama kwa nchi moja hiyo inayowekewa vikwazo, kwa hiyo suala la vikwazo lilikuwa kipaumbele kwenye mkutano wa AALCO.



Aidha Mkutano huo wa 58 wa AALCO ulijadilii mambo mengine sita, likiwemo lile la matumizi na utajiri ulioko baharini, rasilimali kama vile mafuta, madini na samaki ambavyo vinahitajika sana duniani, “kwa hiyo lilikuwa ni jambo jema kujadili vitu hivyo muhimu kwa nchi za Afrika na Asia.” Amesema Rais wa AALCO.



“katika Mkutano huu wa AALCO tumezungumza na kubadilishana mawazo kuhusu utajiri ulioko kwenye bahari, ambapo kila mmoja anautaka, hivyo tunatakiwa tuweke sheria nzuri na vyombo vya kisheria ambavyo vitatufanya kutumia vitu hivyo bila kugongana sehemu” Balozi Mahiga.



Aliongeza kuwa katika masuala saba yaliyojadiliwa, suala la vikwazo na matumizi ya bahari ni busara kuyajadili hayo katika majukwaa mbalimbali ikiwemo AALCO; ili kuiambia dunia kuhusu kukua kwa maendeleo ya Sheria za Kimataifa.



Tanzania itakuwa Rais wa AALCO kwa muda wa mwaka mmoja, ambapo Mkutano wa 59 unaotarajiwa kufanyika Bara la Asia, Nchini China, ambapo Tanzania itakabidhi kiti hicho kwa China.

WALIMU SHULE YA MSINGI BUHANGIJA, IBINZAMATA WAFANYA SHEREHE KUJIPONGEZA MATOKEO DARASA LA SABA

0
0

Walimu wa Shule za Msingi Buhangija na Ibinzamata zilizopo katika manispaa ya Shinyanga, wamefanya sherehe ya kujipongeza kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.

Hafla hiyo ya kujipongeza imefanyika leo Oktoba 24, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya msingi Buhangija, ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga. 

Akizungumza wakati wa sherehe hiyo,Nyeriga amewataka walimu wa shule hizo waongeze juhudi na maarifa katika ufundishaji, pamoja na kujiwekea malengo ya kuendelea kufanya vizuri zaidi, ili shule hizo kwenye matokeo ya darasa la saba mwakani 2020 ziingie kwenye kumi bora kitaifa. 

Amewapongeza walimu wa shule hizo mbili kwa kufanya vizuri kwenye matokeo hayo ya darasa la saba, licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye shule hizo ikiwemo ubovu wa miundombinu na upungufu wa walimu, lakini wamekuwa na moyo wa kujituma na hatimaye kufaulisha wanafunzi wengi tofauti na miaka ya nyuma.

 “Mimi kama afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga, nawapongeza sana walimu wa shule hizi mbili kwa juhudi ambazo mmezionyesha kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2019, nawaomba pia muongeze maarifa katika ufundishaji pamoja na kumaliza tatizo la mwanafunzi kutokujua kusoma, kuandika, na kuhesabu, ndipo mtafanikiwa kuingia kumi bora kitaifa 2020,”amesema Nyeriga. 

Naye Afisa elimu wa shule maalumu manispaa ya Shinyanga Edward Mdagata, ameipongeza Shule ya msingi Buhangija ambayo inafundisha pia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, kwa kufanya vizuri kufaulisha wanafunzi hao kwa asilimia 93,huku akiahidi kutatua changamoto ya upungufu wa walimu uliopo shuleni hapo hasa wenye uhitaji maalumu. 

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Buhangija Selemani Kipanya, amesema wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 139, wavulana 68 na wasichana 71, ambapo wamefaulu 129 sawa na asilimia 93, ambapo wavulana wakiwa 67 na wasichana 62 na kufanikiwa kushika nafasi ya 13 ngazi ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kati ya shule 41 ambapo mwaka jana walikuwa nafasi ya 18.

 Pia amesema kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliofanya mtihani walikuwa 18, wenye ualbino sita ambapo wamefaulu wote, wasioona wanne nao wakifaulu wote, viziwi walikuwa nane ambapo walifaulu watano huku watatu wakifeli. 

Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Ibinzamata Daniel Malwa amesema wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 94, wavulana 46 na wasichana 48, ambapo wamefaulu 92, wavulana 45 na wasichana 47 sawa na asilimia 98, na kufanya kushika nafasi ya Saba manispaa ya Shinyanga kati ya Shule 41 ambapo mwaka jana walikuwa wa nafasi ya 15. 

Nao baadhi ya wazazi akiwamo Martha Mahulu, wamewapongeza walimu kwa kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo ya darasa la saba, na kubainisha ufaulu wa mwanafunzi ndiyo furaha ya mzazi. TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga akiwapongeza walimu wa Shule za Msingi Buhangija na Ibinzamata kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la Saba mwaka 2019. Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga, akiwataka walimu wa Shule ya Msingi Buhangija na Ibinzamata kuongeza juhudi na maarifa katika ufundishaji, ili waweze kufikia malengo yao ya kuingia kwenye nafasi ya kumi bora kitaifa. Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Selemani Kipanya akisoma taarifa ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwenye shule hiyo, ambapo wamefaulisha kwa asilimia 93. Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Ibinzamata Daniel Malwa, akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 kuwa wamefahaulisha kwa asilimia 98. Afisa elimu wa shule maalumu manispaa ya Shinyanga Edward Mdagata akiipongeza Shule ya Msingi Buhangija kwa kufaulisha vizuri wanafunzi wenye uhitaji maalumu. Afisa elimu Kata ya Ibinzamata Mackline Shija, akiwapongeza walimu wa shule hizo mbili ya Buhangija na Ibinzamata kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Mtendaji wa Kata ya Ibinzamata Victor Kajuna ,akiwapongeza walimu wa shule hizo mbili na kuwataka waongeze juhudi katika ufundishaji. Mwalimu wa taaluma katika Shule ya msingi Buhangija Mohamed Makana, akizungumza kwenye hafla hiyo, ambapo amesema majaribio ya mitihani ya mara kwa mara baina ya wanafunzi wa Shule hizo mbili ndiyo yamefanya ufaulu kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma. Mwalimu wa taaluma katika Shule ya msingi Ibinzamata Elice Ndosa Mohamed, akizungumza kwenye hafla hiyo, anasema majaribio ya mitihani ya mara kwa mara baina ya wanafunzi wa Shule hizo mbili ndio yamefanya ufaulu kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma. Mzazi Martha Mahulu akipongeza juhudi ambazo wamezionyesha walimu wa shule hizo mbili katika ufindishaji wao na hatimaye kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba. Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Keki iliyoandaliwa na walimu wa Shule za Buhangija na Ibinzamata manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokea ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Afisa elimu taaluma mansipaa ya Shinyanga Essau Nyeriga akimlisha Keki Afisa elimu Kata ya Ibinzamata Mackline Shija kutokana na kusimamia elimu vizuri kwenye Kata hiyo na hatimaye kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019. Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga akigawa vyeti kwa walimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao na kusababisha shule kupata ufaulu mzuri kwenye matokeo hayo ya darasa la saba. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog 
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images