Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Tigo yaifikisha promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo Jijini Arusha

$
0
0


Kaimu mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi,Aidan Komba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo iliyofanyika Jijini Arusha.Pembeni yeke ni Mtaalamu wa huduma za Kidigitali wa Tigo,Fabian Felician
Mtaalamu wa huduma za Kidigitali wa Tigo,Fabian Felician akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo iliyofanyika Jijini Arusha.Pembeni yeke ni Kaimu mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi,Aidan Komba


Wateja wa Tigo wanaoshiriki katika promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo kwa mara ya kwanza wana nafasi ya kushinda hadi Sh1 milioni kila wiki huku mshindi wa jumla ataweza kujinyakulia gari mpya aina ya Renault Kwidyenye thamani ya Sh23 milioni.


Meena Ally akitoa maelezo jinsi ya kushinda Gari mpya (0kms) aina ya Renalt Kwid kwenye promosheni ya #TigoFiestaChemshaBongo. Tuma Neno "Muziki" kwenda 15571



ELIMU YA MATUMIZI YA CHAKULA VINYWAJI KWA WANAFUNZI YATOLEWA ZANZIBAR

$
0
0
Walimu pamoja na Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula wa Wakala wa Chakula na Dawa (ZFPA)Aisha Suleiman wakati akitoa Elimu ya Matumizi ya Chakula Vinywaji pamoja na Peremende kwa Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Mpendae mjini Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula wa Wakala wa Chakula na Dawa (ZFPA)Aisha Suleiman akitoa Elimu ya Matumizi ya Chakula Vinywaji pamoja na Peremende kwa Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Mpendae mjini Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Wakala wa Chakula na Dawa Mohamed Shadhil Shauri akitolea ufafanuzi baadhi ya maswala wakati akitoa Elimu ya Matumizi ya Chakula Vinywaji pamoja na Peremende kwa Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Mpendae mjini Zanzibar. 

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.


Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 23/10/2019

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar imepiga marufuku kutumia bidhaa ambazo vifungashio vyake havina maandishi ya lugha iliyokubalika kutumika kisheria nchini.

Akitoa elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Glorious Acedemy huko Mpendae kuhusiana na uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu pipi na chokleti zimeingia nchini kuwa zina madhara Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula Aisha Suleiman amesema ni marufuku kutumia bidhaa kama pipi na chokleti ambazo maandishi yake yameandikwa kwa lugha isiyofahamika.

Amesema hakuna pipi ama chokleti zinazoingizwa nchini ambazo zina madhara wala athari kwa jamii bali ni kuzingatia vifungashio, viambata vilivyomo katika bidhaa na muda wa kumalizika kwake.Ameeleza Wakala wa Chakula na Dawa ina jukumu la kuhakikisha kwamba vyakula vinavyoingia nchini viko salama kwa matumizi ya binadamu na havileti madhara kwa mtumiaji.

Mkuu huyo amewafahamisha wanafunzi hao kuwa waangalifu wanaponunua bidhaa zenye vifungashio kwa kuangalia vyema maelezo yaliyomo ili kuepuka kupata madhara. Aidha Mkuu huyo amewataka wanafunzi hao kuacha kutumia vyakula vyenye sukari kwa wingi ili kuepukana na maradhi mbali mbali na kupata taifa lililoimara.

Aidha amesisitiza wanafunzi hao kutosikiliza taarifa za uvumi uliopo na kuwa walimu kwa wenzao ili jamii iondokane na jambo hilo. Nao wanafunzi hao wamesema kuwa wataitumia vyema elimu waliyoipata na kuwa walimu wazuri kwa wenzao.

HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO YAZINDUA JENGO NA IDARA YA KUSAFISHA FIGO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

LEO OKtoba 23, Waziri wa Ulinzi na Jesh la kujenga Taifa Dkt. Hussein Ally Mwinyi amezindua rasmi idara na jengo la kusafisha figo katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo hilo Waziri Mwinyi amesema ukamilikaji wa kituo hicho umefika muda sahihi kwa kuwa unaenda sambamba na mlengo wa Serikali wa kujenga vituo vya afya kote nchini.

"Serikali ya awamu ya tano imeendelelea kuhakikisha vituo vya afya vinajengwa kote nchini na kukamilika kwa kituo hiki utarahisisha utoaji huduma kwa wananchi pia utapunguza gharama kwa kuwapeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi kwani tunaamini tutawapokea wagonjwa wengi " ameeleza.

Amesema kuwa huduma zinazotolewa na Jeshi ikiwemo elimu na afya si kwa jeshi na familia zao bali ni kwa jamii nzima hivyo watumie fursa hizo kwani ni kwa ajili ya wote.

Pia amewataka wataalamu watakaoendesha huduma hiyo kutumia vifaa hivyo kwa uangalifu ili kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi na kuvifanya vifaa hivyo vidumu kwa muda mrefu zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama nchini Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya jeshi na jamii kwa ujumla.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka 2016 na kumalizika 2017 na  Rais Dkt. John Joseph Magufuli alitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na hadi kukamilika kwake kimegharimu shilingi Milioni 431, laki nane ishirini na saba elfu mia tisa na thelathini na tano na tayari lina mashine bora zilizonunuliwa nchini ujerumani kwa gharama ya shilingi milioni 633 huku wakiwa na mpango wa kujenga kituo cha utambuzi kwa wagonjwa (diagnosis centre.)

Amesema kuwa kituo hicho ni cha kwanza kuwepo jeshini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 na hiyo itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya taifa Muhimbili pamoja ma kuipunguzia gharama serikali ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Awali akitoa taarifa ya kituo hicho Daktari bingwa wa magonjwa ya pua, koo na masikio na msimamizi Mkuu wa hospitali kuu ya Jeshi Lugalo Brigedia Jenerali Gabriel Mhidze amesema kuna wataalamu wa kutosha pamoja na mashine kumi za kuchuja wagonjwa wa figo na hadi sasa wamefanya michujo kumi na tisa huku wakiwa na uwezo wa kuwahudumia wagonjwa arobaini kwa siku.

Amesema kuwa gharama kwa huduma hiyo ni nafuu na amewashauri wananchi kufuata sheria za afya ili kuepukana na tatizo la figo ikiwemo kuzingatia vyakula pamoja na kucheki afya zao ili kujilinda zaidi.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda atembelea Banda la Benki ya Maendeleo TIB wakati wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani

$
0
0
Meneja Mipango na Utafiti wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Samwel Marko (kulia) akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi wa Ufungaji wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani, Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Mizengo Pinda (wapili kulia). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo.
Mgeni Rasmi wa Ufungaji wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani, Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Mizengo Pinda (wapili kulia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mipango na Utafiti wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Samwel Marko (kulia) wakati akitoa maelezo kuhusu uwekezaji uliofanywa na benki hiyo mkoani Pwani. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo (katikati), Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani, Bw. Ramadhani Maneno (kushoto) na Meneja Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Bw. Saidi Mkabakuli (wapili kushoto).
Mgeni Rasmi wa Ufungaji wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani, Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Mizengo Pinda (wapili kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Mipango na Utafiti wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Samwel Marko (kulia) wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo (wapili kushoto) na Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto).
Meneja Mipango na Utafiti wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Samwel Marko (kulia) akipokea Tuzo ya Udhamini wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Mizengo Pinda. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani, Bw. Ramadhani Maneno (kulia).
Wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo TIB walioshiriki ufungaji wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamojamara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Udhamini wa Maonesho hayo.

KORTI YAMTAKA MDHAMINI WA TUNDU LISSU KUPELEKA UTHIBITISHO WA MAENDELEO YA AFYA YA TUNDU LISSU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka mdhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ifikapo Novemba 21, mwaka huu kuleta mahakamani uthibitisho wa maendeleo ya afya ya Lissu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefikia hatua hiyo baada ya kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu kusimama kusikilizwa kwa takribani miaka miwili kwa sababu mshtakiwa huyo anaumwa yuko Ubelgiji.

Mapema, wakili wa Serikali, Estazia Wilson alidai mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya usikilizwaji wa ushahidi wa shahidi wa upande wa mashtaka lakini haiwezi kuendelea kwa sababu mshtakiwa Lissu hayupo.


Mdhamini wa mshtakiwa huyo, Robert Katula alidai Lissu bado anaumwa yuko nje ya nchi.Kufuatia taarifa hiyo, hakimu Simba amemuamuru mdhamini tarehe ijayo ya kesi afike na uthibitisho wa maendeleo ya mshtakiwa na kesi imeahirishwa hadi Novemba 21 mwaka huu.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokua na taarifa za uchochezi.

Alidai mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Mbali na mashtaka hayo washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016, Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote, waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

AFRIKA NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA DUNIA-PUTIN

$
0
0

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amefungua Kongamano la Biashara baina ya Urusi na Afrika (Russia Business Forum) ambapo amesema Bara la Afrika ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa dunia na ni kivutio kikubwa kwa wafanyabiashara wa Urusi.


Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 23, 2019) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Olympic Park katika mji wa Sochi nchini Urusi. Rais Putin amesema takwimu zilizotolewa na watalaamu wa masuala ya uchumi zinaonyesha kwamba pato la Afrika (GDP) litafikia dola trilioni 29 ifikapo 2050.

Amesema biashara kati ya Urusi na Afrika imeongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kufikia dola za Marekani bilioni 20 na kwamba nchi yake inaunga mkono wazo la kuanzishwa eneo huru la biashara katika bara la Afrika ukiwa ni mkakati wa Umoja wa Afrika (AU) na kwamba itatoa ushirikiano ili kufanikisha wazo hilo.

Kadhalika, Rais Putin ameongeza kuwa nchi yake inatekeleza kwa vitendo mpango kuzifutia madeni nchi za Afrika na hadi sasa imeshafuta madeni ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 20. 

Amesema utoaji wa mafunzo ya taaluma mbalimbali umekuwa ni utamaduni wa ushirikiano kati ya Urusi na Afrika. “Hadi katikati ya miaka ya 80 nchi yake imejenga taasisi zipatazo 100 za mafunzo mbalimbali Barani Afrika na watu 500,000 wampata mafunzo katika taasisi hizo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshiriki katika mkutano huo akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli. Pamoja naye idadi kubwa ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika Bara la Afrika wamehudhuria mkutano huo.

Miongozi mwa viongozi hao ni Rais Yoweli Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais wa Misri na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Abdel Fattah al Sissi, Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na viongozi wengine kutoka Bara la Afrika.

Kesho (Alhamisi, Oktobba 24, 2019) Waziri Mkuu anatarajia kushiriki katika mkutano baina ya Urusi na Wakuu wa nchi na Serikali wa Bara la Afrika. 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin akihutubia katika Mkutano wa uchumi kati ya Afrika na Urusi (Russia -Africa Economic Forum) kwenye Kituo cha Olympic Park, Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC MNYETI AWAFAGILIA VIONGOZI MBULU

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Mbulu wakiongozwa na DC wao Chelestino Simbalimile Mofuga kwa namna wanavyowatumikia wananchi hadi kupunguza kero kila mahali anapopita kwenye mikutano yake anakutana na changamoto chache.

Mnyeti akizungumza na wananchi wa Mbulu mjini amesema viongozi wa wilaya hiyo wamejitahidi kupunguza kero za maeneo inayowazunguka hadi yeye wanampunguzia kazi katika eneo hilo. 

“Jana nilipita Kainam na kuzungumza na wananchi baada ya kukagua mabweni ya wasichana kwenye shule ya sekondari kisha nikaenda Hhaynu nikaweka jiwe la msingi la shule ya sekondari na kuzungumza na wananchi ambapo watu wawili walijitokeza kutoa kero,” alisema Mnyeti. 

Alisema watu hao walizungumzia barabara na umeme hivyo kudhihirisha kuwa viongozi wa Mbulu wanawatembelea wananchi na kusikiliza kero zao. 

“Nimefika Tlawi jana na leo nimekwenda Qatesh, Titiwi, Gehandu na Gedamar huko kero za wananchi ni chache na hapa Mbulu mjini watu watatu wamejitokeza kutoa kero hapa mmeonyesha kazi imefanyika,” alisema Mnyeti. 

Aliwapongeza Mofuga, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Sarah Sanga, Mkurugenzi wa Mji wa Mbulu Anna Mbogo na viongozi wengine wa eneo hilo kwa kutatua migogoro, kero na changamoto za wananchi. 

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mofuga alishukuru kwa hatua hiyo ya kutambuliwa kazi nzuri wanayofanya kwani kila alhamisi wametenga kukutana na wananchi wenye matatizo ofisini kwake na pia kuwatembelea kwenye maeneo yao. 

“Tutahakikisha jamii inasaidiwa kwenye kutatuliwa kero zao ili kuhakikisha wananchi wanaipenda serikali yao inayoongozwa na Rais John Magufuli,” alisema Mofuga. 

biashara ya samaki soko la feri jijini dar leo

$
0
0

Wachuuzi wa Samaki katika Soko kuu la samaki la kimataifa Feri wakiendelea na shughuli zao mbalimbali katika soko hilo kama wanavyoonekana pichani leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Michuzi Tv).
Mchuuzi wa Samaki wa soko la Samaki feri akimkata kata samaki aina ya  Changu kwa ajili ya kupeleka mtaani kuuzwa,amapo Changu mmoja huuzwa kati Elfu tatu mpaka 20,000/= kulingana na ukubwa/uzito
Wachuuzi wa samaki katika Soko kuu la samaki la kimataifa Feri jijini Dar es Salaam wakitayarisha Samaki kwa lengo la kuwauza kwa wateja mbalimbali watakaofika katika soko hilo kama inavyoonekana pichani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

BENKI YA CRDB YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU, YAHUDHURIA MAHAFALI YA 53 SHULE YA SEKONDARI KIBAHA MKOANI PWANI

$
0
0
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 53 ya Shule ya Sekondari ya Kibaha ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck akikabidhi cheti kwa Mwanafunzi Winson Mahenge aliyeshika nafasi ya kwanza kitaaluma kwa wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibaha Mkoani Pwani, yaliyofanyika Oktoba 23, 2019 shuleni hapo. Benki ya CRDB ambayo imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kila mwaka kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya elimu nchini, kama kuchangia vyumba vya madarasa, kuboresha mazingira ya shule ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu katika mazingira yaliyo rafiki kwao, Imepongeza jitihada za kitaaluma zinazofanywa na shule hiyo pamoja na kuwasihi wanafunzi wanaohitimu kuwa bado safari yao kimasomo inaendelea kwani Benki inaimani ya kuwa wote watafaulu katika DARAJA LA KWANZA na kujiunga na kidato cha sita.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 53 ya Shule ya Sekondari ya Kibaha ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck akikabidhi cheti kwa Mwanafunzi Akimu Christopher aliyeshika nafasi ya pili kitaaluma kwa wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibaha Mkoani Pwani, yaliyofanyika Oktoba 23, 2019 shuleni hapo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 53 ya Shule ya Sekondari ya Kibaha ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck akikabidhi cheti kwa Mwanafunzi Shaban Mussa aliyeshika nafasi ya tatu kitaaluma kwa wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibaha Mkoani Pwani, yaliyofanyika Oktoba 23, 2019 shuleni hapo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 53 ya Shule ya Sekondari ya Kibaha ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibaha, Mwalimu Chrisdom Ambilikile.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 53 ya Shule ya Sekondari ya Kibaha ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck akizungumza katika mahafali hayo, yaliyofanyika Oktoba 23, 2019 shuleni hapo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibaha, Mwalimu Chrisdom Ambilikile akizungumza.
































MAADHIMISHO YA MIAKA 74 YA UMOJA WA MATAIFA KUFANYIKA DODOMA

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe akizungumzia maadhimisho ya miaka 74 ya Umoja wa Mataifa yatakayofanyika Kitaifa kesho jijini Dodoma.
Kaimu Mratibu wa Umoja wa Mataifa, Michael Dunford akizungumza na wandishi wa habari kuelezea siku ya Umoja wa Mataifa ambapo hufanyika kila Oktoba 24 ya kila mwaka. Kesho Umoja huo unatimiza miaka 74 tangu kuanzishwa kwake.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akizungumza jambo na Kaimi Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Michael Dunford wakati wa mkutano wao na wandishi wa habari kuelezea maadhimisho ya miaka 74 ya UN yatakayofanyika kesho.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa umoja wa mataifa (UN)



Charles James, Michuzi TV

Kuelekea maadhimisho ya miaka 74 ya Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania imesema imepiga hatua kubwa katika suala la usawa kwenye jinsia kwa kutoa kipaumbele wa nafasi za uongozi kwa wanawake.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe alipokua akizungumzia maadhimisho hayo ambayo kitaifa yatafanyika jijini Dodoma.

Dk Mnyepe amesema maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya Wanawake na Wasichana kuwa kipaumbele kufikia malengo ya Dunia ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi.

" Tunashukuru ushirikiano ambao tunaoneshwa na ndugu zetu wa UN hasa katika kutoa elimu juu ya nafasi ya mwanamke katika uongozi. Tunaomba wananachi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kesho katika viwanja vya Nyerere ambapo itakua mara ya kwanza kwa maadhimisho haya kufanyika jijini hapa.

Kama Taifa tumekua mstari wa mbele kupigania haki ya mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla. Tunaamini katika usawa hivyo nitoe rai kwa watanzania kuendelea kuwaamini wanawake katika mambo mbalimbali kielimu, kisiasa, kitamaduni na hata kiuchumi," Amesema Dk Mnyepe.

Amesema licha ya Prof Kabudi kuwa mgeni rasmi sherehe hizo zinatarajiwa pia kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa, viongozi wa serikali na waakilishi wa makundi mbalimbali likwemo la wenye mahitaji maalumu.  

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini, Balozi Michael Dunford amesema sherehe hizo zimelenga kuhimiza usawa wa kijinsi huku akiipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ambalo linazunguzia usawa wa kijinsia.

 “ Tunaamini kama nchi itafanikiwa katika lengo la usawa wa kijinsia basi malengo yote ya maendeleo endelevu yatafanikiwa. Kwa upande wa Tanzania imepiga hatua katika lengo hili katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu na afya, hivyo sisi kama Umoja wa Mataifa tutashirikiana na serikali katika kufikia lengo hili.”

Umoja wa Mataifa umekua ukifanya maadhimisho haya kila ifikapo Oktoba 24 ya kila mwaka ambapo mwaka huu yatafanyika jijini Dodoma na kushuhudiwa gwaride maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na bendera ya UN itapandishwa kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni Makao Makuu ya Nchi.

MAHAKAMA YA RUFAA YABARIKI MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR KUHUSU VIFUNGU VYA SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Rufaa imebariki maamuzi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyoelekeza serikali kubadilisha kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kwa kuwa vinakiuka Katiba ya Tanzania.

Vifungu hivyo, vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 lakini mtoto wa kiume ameruhusiwa kuoa akiwa na miaka 18 hivyo, sheria haiweki usawa kati ya watoto hao na kwamba ni ya ubaguzi na ni kinyume na Ibara ya 13 na ya 12 ya katiba inayozungumzia usawa.

Hukumu hiyo imetokana na Serikali kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa mwaka 2016 ambao ulibatilisha kifungu cha Sheria ya Ndoa kinachoruhusu ndoa za utotoni.

Rufaa hiyo imesikilizwa na Jopo la majaji watatu, Augustine Mwarija, Winfrida Korosso na Dk Mary Lavira ambapo miongoni mwa sababu za serikali za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ni kwamba mahakama ilikosea kutoa uamuzi huo kwa sababu ililenga kuwasaidia kuwalinda watoto wa kike dhidi ya ngono na kupata watoto nje ya ndoa.

Pia walidai mtoto wa kike anakua mapema kabla ya mtoto wa kiume.
Akisoma uamuzi uliotolewa na majaji hao, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eddie Fussi amesema watoto wote ni sawa bila kujali jinsia na kwamba sheria hiyo haiwezi kumkinga mtoto wa kike kwa kumruhusu kuolewa kwa madai huko kuna ulinzi zaidi wakati kuna madhara makubwa kwake.

Amesema miongoni kwa madhara ambayo mtoto wa kike akiolewa chini ya umri wa miaka 18 ni mimba za utotoni, magonjwa na unyanyasaji wa kijinsia.Pia sheria mbalimbali zinakataza mtoto wa chini ya umri wa miaka 18 kuingia mkataba wowote hivyo ni pamoja na mkataba wa ndoa kwa sababu ni mgumu zaidi.

"Mahakama inaelekeza kifungu cha 13 na 17 vinakiuka katiba ya Tanzania hivyo, serikali ifuate maelekezo ya Mahakama Kuu ya kubadilisha vifungu hivyo," alisema Fussi.

Kesi hiyo ya kikatiba ilifunguliwa na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI MKUTANO WA UCHUMI KATI YA URUSI NA AFRIKA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnagangwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (kulia) wakimsikilza Rais wa Urusi, Vladimir Putin wakati alipohutubia katika Mkutano wa uchumi kati ya Afrika na Urusi (Russia -Africa Economic Forum) kwenye Kituo cha Olympic Park, Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa uchumi kati ya Afrika na Urusi (Russia -Africa Economic Forum) wakimsikiliza Rais wa Urusi, Vladmir Putin wakati alipohutubia mkutano huo kwenye Kituo cha Olympic Park, Sochi chini Urusi, Oktoba 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Urusi, Vladimir Putin akihutubia katika Mkutano wa uchumi kati ya Afrika na Urusi (Russia -Africa Economic Forum) kwenye Kituo cha Olympic Park, Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WASHIRIKI WA MKUTANO WA SADC WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA(ANAPA)

$
0
0
Washiriki wa Mkutano wa  Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za SADC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye hifadhi ya Taifa Arusha(ANAPA)wakiongozana na Ujumbe kutoka Tanzania 
Wataalamu kutoka sekta za Utalii na Mazingira na Maliasili walioshiriki mkutano huo wa SADC wakiwa katika Hifadhi ya Taifa Arusha (ANAPA )
wajumbe wa mkutano wakitazama wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA)

Na Vero Ignatus,Arusha

Washiriki wa Mkutano wa  Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za SADC wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA) wakiongozana na ujumbe wa Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo makundi ya wanyamapori kama vile nyati, nyumbu, pundamilia pamoja na maporomoko ya maji.
Ziara hiyo imelenga kuhamasisha utalii katika nchi wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania ambayo ina vivutio vingi vya utalii ambavyo ni mbuga za wanyama, hifadhi pamoja na utalii wa utamaduni.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Agnes Kayole ameeleza kufurahishwa na hifadhi ya Taifa ya Arusha ambayo ipo karibu na Mjini na ina vivutio vingi ikiwemo wanyama na maporomoko ya maji  jambo ambalo linahitaji kutangazwa ili kupata watalii wengi zaidi.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Kitengo cha Utalii kutoka Wizara ya Utalii nchini Msumbiji Bw. Nosto Mazivile amefurahishwa na vivutio hivyo vizuri na kusisitiza kuwa vikitangazwa vizuri vitasaidia  kukuza uchumi wa Tanzania na kutoa rai kwa Tanzania kuendelea na juhudi za kutunza na kuhifadhi kwa maendeleo endelevu.
Mhifadhi wa Masuala ya Utalii  na Masoko kutoka Afrika Kusini , Rollen Fovak amesema kuwa ni mara ya kwanza kutembelea hifadhi hiyo ambapo wamejionea Ngurudoto Kreta, nyani weupe maarufu kama mbega pamoja na mapromoko ya maji ya Tululusia hivyo anajukumu la kuhamasisha mataifa mengine kutembelea hifadhi.
Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii zinandelea na vikao vyake kwa nchi wanachama wa SADC ambavyo vimeanza tarehe 21/10/2019 na vinatarajiwa kukamilika siku ya Ijumaa tarehe 25/10/2019 Jijini Arusha.

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE MBELE YA AZAM FC, YAILAZA BAO 1-0

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Klabu ya Soka ya Simba imeendeleza ubabe mbele ya Azam FC baada ya kuichapa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) uliopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute dakika zote 90, ubabe ukitawala ndani ya dimba, Simba SC walipata matokeo hayo ya ushindi kupitia kwa Mshambuliaji wake, Meddie Kagere (MK 14) dakika ya 49 kipindi cha pili baada yakuunganisha kwa Kichwa pasi safi ya guu la kushoto ya Kiungo Mshambuliaji, Fransic Kahata.

Dakika za lala salama, Azam FC walionekana kuwa bora kutaka kusawazisha bao hilo baada yakuwaongeza Mshambuliaji, Shaaban Iddi 'Chulunda' na Donald Ngoma kuongeza mashambulizi, na kufanikiwa kuisumbua ngome ya ulinzi ya Simba ilikuwa chini ya Serge Wawa Pascal na Erasto Nyoni waliokuwa wanasaidiwa na Gadiel Michael na Haruna Shamte pembeni.

"Sisi tumengeneza nafasi nyingi sana ambazo hatukuweza kuzitumia, lakini wenzetu wamepata bahati, wametengeza nafasi chache wametumia moja na wamepata ushindi", amesema Nahodha wa Azam FC, Salum Aboubakar 'Sure Boy'.

"Ugumu wa mchezo ulikuwa, kwanza timu zote mbili ni nzuri, zote zinacheza, zinaweza kucheza, kikubwa sisi tulifuata maagizo ya Kocha wetu ndio maana tukapata ushindi huu", amesema Nahodha wa Simba FC, Erasto Nyoni.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana zilikutana August 17, 2019 kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani, ambapo Simba SC iliibuka na ushindi wa bao 4-2 mbele ya Azam.

Kwa ushindi huo, Simba SC wanakuwa kileleni mwa msimamo wa VPL kwa alama 15 baada ya ushindi wa michezo yake mitano ya Ligi hiyo wakati Azam FC wanabaki na alama zake 9 akiwa na michezo minne.



 

Kikosi cha Simba FC 
 Kikosi cha Azam FC

TIMU YA YOUNG STARS MABINGWA WA KOMBE LA FA MKOA WA IRINGA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto pamoja mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava wakimkabidhi kombe la ubingwa wa FA mkoa wa Iringa nahodha wa timu ya Young Stars baada ya kuwafunga timu ya mbega mwekundu goli 5-1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa mkwawa
Mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto pamoja mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava wakimkabidhi kombe la ushindi wa pili wa FA mkoa wa Iringa nahodha wa timu ya mbega mwekundu baada ya kufungwa goli 5-1 na timu ya Young Stars kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa mkwawa
Mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto alitoa pia zawadi ya kitamba cha unahodha kwa timu ya Young stars


Na Fredy Mgunda,Iringa.

TIMU ya Soka ya Young Stars imefanikiwa kuwa mabingwa wa kombe la FA mkoa wa Iringa baada ya kuibuka na ushindi ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Mbega Wekundu fc ya wilaya ya kilolo.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa chuo kikuu cha Mkwawa timu ya Young Stars walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji hatari Zacharia Mwipopo.

Mchezo huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Young Stars walikuwa wakiongoza bao 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha kufika fainali ya FA Mkoa wa Iringa kwa Mbega wekundu kusawazisha goli kwa njia ya penati iliyopigwa na Gibo Laurence dakika ya 51 kipindi cha pili,lakini timu ya Mbega Mwekundu dakika 61mchezaji wao Nick King akipata kadi nyekundu nakuifanya timu hiyo kuwa pungufu na vua ya magoli ilipo waangukia timu hiyo 

Baada ya kadi nyekundu waliyopata timu ya Mbega Mwekundu,timu ya Young Stars waliongeza mashambuli kwa kasi kubwa na kuanza kushusha vua ya magoli kwa timu pinzani ikiwa dakika ya 62 mchezaji Johnson Mwakatumbula aliipatia goli timu yake huku Zacharia Mwipopo akirudi tena kambani 72 na shughuli ilimaliziwa na mchezaji Maulid Chitonela alifunga magoli mawili katika dakika ya 84' 86 hadi mwisho wa mchezo Young Star 5-1 Mbega Wekundu

Baada ya mchezo huo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava aliwataka wachezaji wa timu zote mbili kucheza kwa nidhamu ya juu kwa kuwa mpira wa miguu ndio unataka hiyo.

Timu ya Mbega Mwekundu leo hii hamjaonyesha nidhamu kwenye mechi hii ya leo hiyo mnatakiwa kulinda nidhamu yenu ili muwezekufika mbali kisoka.
Naye mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amewapongeza wachezaji wa timu zote mbili kwa mchezo huo na kuwaomba waendelee kulinda nafasi yenu katika soka

WANAWAKE WAPEWA MBINU ZA KUGOMBEA NA KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya akizungumza katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka vitongoji na vijiji kwenye baadhi ya kata wilaya Kishapu mkoani Shinyanga. 


Mtandao wa Jinsia Tanzania 'TGNP Mtandao' umetoa mafunzo ya uongozi kwa Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 ili kuwajengea uwezo,ujasiri,mbinu na mikakati ya kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi na kushinda.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo Jumatano Oktoba 23,2019 kwenye ukumbi wa BM uliopo katika kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na kukutanisha watia nia 65 kutoka baadhi ya kata za wilaya ya Kishapu.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Theresia Sawaya ambaye ni Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kugombea na kushinda kwa kishindo.

"Tumekutana na watia ni kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi ili kuwafundisha kuhusu dhana za jinsia na namna zinavyotumika na athari zake katika masuala ya uongozi lakini pia kuwajengea uwezo namna ya kufanya kampeni kwenye uchaguzi,namna ya kupata rasilimali fedha na ulinzi na usalama wa wagombea",alieleza Sawaya.

Alisema kupitia mafunzo hayo wanatarajia wanawake ambao katika miaka ya nyuma wamekuwa nyuma kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi watahamasisha na kupata ujasiri wa kugombea na kushinda katika uchaguzi na kushiriki katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Kwa upande wake, Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa ambaye pia ni mwezeshaji katika mafunzo hayo aliwataka wanawake watia nia kugombea kwenye uchaguzi kuhakikisha wanawashirikisha waume zao ili kupata matokeo mazuri zaidi.

"Wanawake tunapogombea madaraka ni vyema kuwashirikisha watu wanaotuzunguka,washawishini waume zenu wawaunge mkono ikibidi muwaombe wawe makampeni meneja wenu,wataongea na wanaume wenzao ili wawape kura na mtapata ushindi mnono",alisema Juma.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya akielezea kuhusu mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka vitongoji na vijiji kwenye baadhi ya kata wilaya Kishapu mkoani Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya ambaye ni Mwezeshaji katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akiwahamasisha wanawake kujiamini kwani wanaweza kuongoza jamii kutokana na kwamba mwanamke ni kiongozi kuanzia ngazi ya familia.
Wanawake watia nia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwa ukumbini. Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa ambaye pia ni mwezeshaji katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akiwasisitiza kuepuka rushwa ya ngono kwenye uchaguzi. 
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa akizungumza wakati wa mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akiwasisitiza kuepuka rushwa ya ngono kwenye uchaguzi.
Diwani wa Kata ya Mwadui Luhumbo,Mhe. Sarah Masinga akiwatia moyo wanawake waliotia nia kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa wajiamini,wamtangulize Mungu na kushirikiana na jamii ili kushinda katika nafasi wanazogombea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisiliza nasaha mbalimbali.
Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo akiwasisitiza wanawake kupendana na kuacha tabia ya kukwamishana wao kwa wao.
Mtia nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,Mary Richard Nzingula akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Mlezi wa wanawake watia nia ya kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wilaya ya Kishapu,Mhe. Suzana Makoye ambaye ni Diwani wa Viti Maalum kata ya Maganzo akiwasisitiza wanawake watia nia kutokata tamaa pale wanapokutana na changamoto mbalimbali. 

MAADHIMISHO YA SIKU YA UMOJA WA MATAIFA KUFANYIKA KESHO, DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza na wanahabari  (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma.

Katika mkutano huo Dkt. Mnyepe amewajulisha waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba, 2019
jijini Dodoma kwenye uwanja wa Nyerere square.  

Dkt. Mnyepe amebainisha kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho hayo, yatakayofanyika kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi 5.00 asubuhi.

Maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana kuwa Kipaumbele katika kufikia Malengo ya Dunia. Kauli mbiu hii inalenga kusisitiza uwajibikaji na ushirikishwaji wa Wanawake katika kufikia malengo ya dunia.

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mnyepe amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuheshimu na kusimamia misingi ya kulinda na kutetea maslahi ya Wanawake na Wasichana ikiwemo kuwashirikisha katika mipango ya maendeleo ya kijamii na uchumi.

Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa hufanyika kila mwaka tarehe 24 Oktoba. Maadhimisho ya mwaka huu ambayo yatapambwa na shamrashamra kutoka vikundi mbalimbali vya sanaa, yanatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wawakilishi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa nchini, vijana, asasi za kiraia na wadau wengine mbalimbali.
Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika ofisi za Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.   
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (katikati) Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakisikiliza maswali kutoka kwa Wanahabari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja baada ya mkutano na waandishi wa habari

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA AALCO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea  ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Bw. Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran) pamoja na Amon Mpanju Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania), ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina) mara baada ya mazungumzo na Viongozi hao wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Amon Mpanju Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania) mara baada ya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina) mara baada ya mazungumzo na Viongozi hao wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Wang Liyu Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria wa China mara baada ya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou,  ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Wang pamoja na Kanali Ngamela Lubinga Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimatifa wa Ccm  ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Wang  na Kanali Ngamela Lubinga Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimatifa wa Ccm  mara baada ya mazungumzo yao ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akigana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa (Wakwanza kulia) na Balozi wa China hapa nchini  Wang (wakwanza kushoto) mara baada ya Mazungumzo  ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019. PICHA NA IKULU

SBL yatimiza miongo miwili ya ukuaji kwa kuzindua nembo mpya

$
0
0
 Waziriwa Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Serengeti Breweriers kwenye hoteli ya Coral Beach jana.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL John Ulanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Serengeti Breweriers kwenye hoteli ya Coral Beach jana.



 Mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Serengeti Breweriers kwenye hoteli ya Coral Beach jana.
 Nembo mpya ya Serengeti Breweries ikizinduliwa
 Cheerrsssss baada ya uzinduzi







Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.

Ikiwa ni zaidi ya miongo miwili tangu ianze kufanya shughuli zake hapa nchini, kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua nembo mpya itakayoitambulisha na kuonyesha historia ya ukuaji wake tangu ianzishwe mwaka 1996.

“Nembo mpya ya SBL inasimama ikiwakilisha ubora, ubunifu, utaalaum, urafiki na kujiamini. Nembo hii pia inaonyesha kuwa kampuni yetu inatengeneza bia zake kwa viungo asilia,” Mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti aliwaambia wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa nembo hiyo mpya jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, nembo hiyo ni kielelezo cha historia pamoja na vipindi ilivyopitia kampuni hiyo kwa miaka yote tangu ikimiliki kiwanda kimoja kidogo cha kuzalisha bia jijini Dar es Salaam hadi kufikia kampuni kubwa inayomiliki viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza huku ikitoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 800.

Bia zinazozalishwa na SBL ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Kibo Gold, Guinness pamoja na Senator. Bia hizi zimefanikiwa kushinda tuzo mbali mbali za kitaifa na kimataifa kutokana ubora pamoja na ubunifu unaotumika kuzitengeneza. SBL pia inasambaza pombe kali zinazoongoza kwa ubora na mauzo duniani kama Johnnie Walker, Smirnoff, White Horse, Gordons, Baileys na nyinginezo.

IIkijulikana kama mdhamini mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars), SBL katika kipindi cha miaka 10 imetekeleza miradi 17 ya maji nchi nzima kwa kuchimba visima kwenye sehemu zenye shida ya maji na kuwawezesha watu zaidi ya milioni 2 kupata maji safi na salama. Kwa mujibu wa Ocitti, kampuni hiyo inashirikiana na Wizara ya Kilimo kuwasaidia wanafunzi wanaofanya vizuri kutoka familia za wakulima kupata elimu ya chuo kupitia ufadhili chini ya mpango wa SBL Kllimo-Viwanda Scholarship.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL John Ulanga alisema nembo hiyo mpya inaakisi lengo jipya la ukuwaji wa kampuni hiyo na kuongeza kuwa SBL imewekeza Paundi za Uingereza milioni 14 katika shughuli zake na upanuzi. “Uwekezaji huu mkubwa, utasaidia kutengeneza ajira mpya zaidi, utaongeza mchango wa SBL kwenye kodi kwa Serikali,”alisema.

Tukio la uzinduzi lilifanywa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa aliyeelezea kuridhishwa kwake na mchango wa SBL kwa uchumi wa nchi na kuahidi kuwa Serikali itandelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa ajili ya malkampuni pamoja na biashara. Bashungwa alisema maboresho yanayaofanywa kwa sasa kwenye sera yanalenga kuondoa urasimu usio wa lazima kwa taasisi za umma ambao ni kikwazo kwa maendeleo na ukuaji wa biashara.

DC JERRY MURO MGENI RASMI TAMASHA LA MUZIKI NA FURSA MERERANI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Dodoma

MKUU wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la muziki na fursa litakalo fanyika Mererani mkoani Arusha.

Akizunguza na waandishi wa habari jijini Dodoma juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMOFA) Stella Joel alisema tamasha hilo limeandaliwa na Tamofa na kuwa litafanyika Oktoba 28 hadi Novemba 3 mwaka huu.

" Tamasha ili litafanyika Oktoba 28 hadi Novemba 3, 2019 Viwanja vya Kanisa la International EAGT Mererani na litahudhuriwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka sehemu mbalimbali" alisema Stella.

Alisema lengo la tamasha hilo ni kwa ajili ya kuwapa fursa kwa wanamuziki wa mikoa ya Manyara na Arusha kuweza kuelewa faida zitokanazo na kazi zao pamoja na kuhakikisha wanasajili kazi zao Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)

Joel aliwataja baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili watakao toa burudani katika tamasha hilo kuwa ni Mary Nyerere, Emmanuel Mbasha, Faraja Ntaboba, Evmagreth Sembuche, Stella Joel na Dkt.Tumaini Msowoya.

Stella aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwepo na madaktari ambao watakuwa wakitoa ushauri wa kitabibu na upimaji wa afya na kuwaomba wananchi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images