Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu azindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Pwani

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa (MB) amezindua Mwongozo wa  Uwekezaji wa Mkoa wa Pwani katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Mkoa wa Pwani sambamba na kufungua rasmi Kongamano la Uwekezaji katika Mkoa Pwani mwishoni mwa wiki.
Katika Uzinduzi Mwongozo huo, Waziri Mkuu alichukua fursa hiyo pia kuitaka mikoa ambayo bado haijatekeleza agizo lake la kuandaa makongamano ya uwekezaji ihakikishe inafanya hivyo mara moja. 
 “Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa mkoa wa Pwani kwa kutekeleza agizo nililolitoa Juni 18, 2018 wakati wa Kongamano la tatu la uwezeshaji wananchi kiuchumi la kuhakikisha mikoa yote inaandaa Kongamano la Uwekezaji na inakuwa na Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa. Mikoa ambayo haijatekeleza agizo hilo, ifanye hivyo mara moja,” amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe wanasimamia miundombinu inayoelekea kwenye viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa Kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angella Kairuki alisema kwamba Serikali imeanza kutekeleza mapendekezo ya mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (Blueprint for Regulatory Reforms for Improving the Business Environment) kwa kuondoa tozo zaidi ya 163 zilizokuwa zikilalamikiwa na wawekezaji.
“Pia tumetenganisha majukumu ya TBS ya TFDA ambayo sasa ni TMDA. TBS itashughulika na vyakula na TMDA itashughulika na dawa na vifaatiba. Vilevile, tumeondoa ada za usajili sehemu za kazi ambazo zamani ilikuwa ni sh. 28,000 na sasa hivi zinatolewa bure,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mhandisi Evarist Ndikilo aliwataka watu wote wanaotaka kuwekeza nchini waufikirie kwanza mkoa wa Pwani kwa sasabu uko kimkakati na una fursa nyingi ikiwemo hali nzuri ya usalama na kwa maana hiyo mitaji yao italindwa.
“Mkoa wetu uko kwenye eneo la kimkakati la kuwezesha biashara kwa kuwa uko karibu na bandari ya Dar es Salaam na uwanja wa ndege; uko karibu na soko kubwa ambalo ni Dar es Salaam; unapitiwa na reli zote kwenda mikoani na nchi jirani; unapitiwa na barabara kuu itokayo Dar es Salaam na pia una bandari kavu ya Kwala.”
Mbali ya hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema faida nyingine ambayo mkoa huo unayo ni uwepo wa miundombinu ya maji, umeme na nishati ya gesi asilia ambayo imeanza kutumiwa na baadhi ya viwanda kama Goodwill na Lodhia Steel.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida alisema, Taasisi yake ikishirikiana na Serikali ya Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) imekuwa wa ikiandaa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa kwa lengo la kuchambua na kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa husika ili kuwavutia wawekezaji.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji ESRF Dkt. Tausi Kida wakati akizungumzia mchango wa Taasisi yake kwenye uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Pwani, kazi ambayo imewezesha kuwapo wa Kongamano la Uwekezaji katika Mkoa huo.
Dkt. Kida alisema kwamba tayari Taasisi hiyo imesaidia Mikoa 17 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa 12 imekamilisha na Mikoa 5 iko katika hatua mbalimbali.
“Hadi sasa tumekwishaisadia mikoa 17 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji na kwa sasa mikoa 12 imeshakamilisha na mikoa mitano iko kwenye hatua mbalimbali,” alisema.
Akizungumzia Mkoa wa Pwani, Dkt Kida alisema Mkoa Pwani una fursa nyingi katika Sekta za; Viwanda, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Utalii, Madini, Miundombinu na Huduma za jamii na  kusema maelezo ya kina yapo katika Mwongozo ambao Waziri Mkuu aliouzindua.
Kwa mujibu wa Dkt. Kida, timu ya ESRF iliyoshiriki kuandaa Mwongozo huo ilijumuisha Prof. Samuel Wangwe, Bi. Margareth Nzuki, Dk Hussein Nassoro, Bw. Mussa Mayala Martine, na Bw. James Kasindi wakishirikiana na wataalam wa Mkoa wa Pwani.
Mwongozo huo ulielezwa kwa kina katika kongamano, katika mada iliyowasilishwa na Prof Samuel Wangwe.
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela ambao ni wadhamini wakuu wa kongamano hilo, Ofisa Mkuu wa Biashara, Benki ya CRDB, Dk Joseph Witts alisema benki hiyo imeendelea kugusa sekta zote za uchumi na hivyo kuongeza tija kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji. Alisema huduma zao zimelenga kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya viwanda nchini ikiwemo utoaji wa mikopo ya biashara kwa ajili ya kuongeza mikopo ya uendeshaji (working capital loans) na mikopo ya uwekezaji (investment loans).
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akitoa hotuba wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizundua Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angellah Kairuki (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto).
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akionyesha nakala za Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angellah Kairuki (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto).
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi nakala Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kuzindua Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mh. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa salamu za ukaribisho kwa wageni waalikwa na wananchi (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Mwakilishi wa timu ya ESRF iliyoshiriki kuandaa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani, Prof. Samuel Wangwe akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki walipokuwa wakisubiri kuwasili kwa mgeni wa heshima kwenye Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Wawakilishi wa timu iliyoshiriki kuandaa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki (katikati) na Prof. Samuel Wangwe (kushoto)wakibadilishana mawazo walipokuwa wakisubiri kuwasili kwa mgeni wa heshima kwenye Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Baadhi ya viongozi wa taasisi za serikali na sekta binafsi walioshiriki Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na timu ya ESRF wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wa mkoa wa Pwani wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wawekezaji wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilioenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Pwani uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha.


KAMPENI YA KUTOKOMEZA UKEKETAJI YAANZA KUFANIKIWA IKUNGI MKOANI SINGIDA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAMPENI ya kutokomeza mila potovu za ukeketaji, mimba za utotoni na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake wilayani Ikungi mkoani Singida imeanza kufanikiwa.

Mafanikio hayo yamekuja kufuatia kamati za ulinzi wa mama na mtoto na klabu za kupinga vitendo hivyo zilizoundwa na Shirika la Save Mother and Children for Central Tanzania (SMCCT)  kuanza kuibua vitendo hivyo na  kufanyiwa kazi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kampeni maalumu ya siku sita ya kupinga vitendo hivyo na tathmini ya mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu na udhalilishaji wa kijinsia,  Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika hilo la Save Mother, Evaline Lyimo alisema kampeni hiyo imeanza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Alisema kampeni hiyo ambayo imefadhiliwa na Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) inayolenga kutokomeza ukeketaji, ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni  dhidi ya watoto pamoja na udhalilishaji wa kijinsia wilayani Ikungi  imeanza kufanikiwa baada ya klabu zilizofunguliwa mashuleni na kamati za kumlinda mama na mtoto kuibua vitendo hivyo na kuanza kufanyiwa kazi.

Alisema katika kampeni hiyo shirika hilo limetembelea kata sita  na vijiji 18 pamoja na shule 25 zilizopo wilayani  humo pamoja na kutathmini  mradi huo ambapo waliwa tembelea wahanga wa matukio ya ukatili kama kukeketwa, kubakwa,  kulawitiwa na   wale ambao wamerudishwa shuleni baada ya kupatiwa elimu na shirika hilo kwa msaada wa kamati za ulinzi wa mama na mtoto na klabu za wanafunzi katika shule za sekobdari na msingi.

SMCCT ni Shirika lisilo la kiserikali ambalo pia Ni mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania( THRDC), ambalo limejikita Katika kupinga matukio ya ukatili kupitia mradi huo.
 Mratibu wa Mradi wa kupinga vitendo vya mila potofu ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya  mama na mtoto kutoka Shirika la Save Mother and Children Central Tanzania (SMCCT) Evaline Lyimo (katikati) akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Masinda wakati wa tathmini ya mradi huo wilayani Ikungi mkoani Singida mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwezeshaji wa mradi huo, Aloyce Kalegeya. 
 Diwani wa Kata ya Makhonga Sombi Majuta akizungumza katika kikao cha kutahmini mradi huo akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mama na mtoto wa kata hiyo.
 Lyimo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makhonga  wanaounda klabu ya kupinga vitendo vya ukatili.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lainichungu wakiwasikiliza viongozi wa SMCCT walipokuwa katika tathmini ya mradi huo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lainichungu wakiwa katika mkutano wa tathmini.
 Wanafunzi wanaounda Klabu ya kupinga ukatili wa Shule ya Msingi ya Lainichungu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shirika la SMCCT na  walimu wao.
 Viongozi wa SMCCT wakiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mama na mtoto wa Kata ya Ihanja wakati wakifanya tathmini ya mradi huo.
 Hapa Lyimo akizungumza na wanafunzi wanaounda klabu ya watoto ya kupinga ukatili wa Shule ya Msingi  Ihanja.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano wakisubiri kuzungumza na viongozi wa SMCCT.
 Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la SMCCT,  Evaline Lyimo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano. .
 Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la SMCCT, Evaline Lyimo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano. 
Kushoto ni Mwezeshaji wa Shirika hilo,  Aloyce Kalegeya
 Wanafunzi wa Klabu ya kupinga ukatili katika Shule ya Sekondari ya Masinda wakijaza fomu maalumu ya tathmini ya mradi huo.
 Hapa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Iseke wanaounda klabu hiyo.
 Hapa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Unyangwe wanaounda klabu hiyo.
Hapa akizungumza na kamati ya ulinzi wa mama na mtoto wa Kata ya Iseke.

DIT YATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU

$
0
0

TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Dar es Salaam (DIT) kuanzia 21 hadi 25 Oktoba 2019 inaendesha mafunzo ya TEHAMA ya siku tano kwa walimu wa shule za serikali nchini. 
 Lengo la mafunzo hayo ambayo yanajulikana kitaalamu 'Basic ICT Devices Maintenance and Repair' ni kuimarisha utunzaji wa vifaa vya TEHAMA ambavyo hutolewa kwa shule mbalinbali nchini na serikali pamoja na wadau wengine, vifaa hivyo ni ambavyo ni pamoja na kompyuta, printa na vifaa vya mawasiliano. 
 Mafunzo hayo yanayotolewa na wataalamu wa DIT yamefadhiliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (UCSAF). 
Walimu wanaohudhulia mafunzo hayo ni wa shule za Msingi na Sekondari. 
“Serikali hutoa vifaa mashuleni kama kompyuta, printa au vifaa vya mawasiliano kupitia UCSAF, imeonekana kuwa ni muhimu vifaa hivyo vikatunzwa vizuri hivyo tutoe mafunzo kwa walimu hawa ili waweze kutunza na kufanya ukarabati.
“Walimu tuliowapokea hapa ni 540 na mafunzo haya yanaanza leo Jumatatu na yatafungwa Ijumaa, ni mafunzo ya siku tano,” alisema Mratibu wa Mafunzo kutoka DIT, Daudi Mboma. 
Walimu hao ni kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Pwani, Mtwara, Ruvuma, Lindi, Kilimanjaro, Kilimajaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Zanzibar na Tanga. Mwisho


MSEMAJI WA SIMBA SC HAJI SUNDAY MANARA AKITOKA NYUMBANI LEO

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI MKUTANO WA AALCO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungua Mkutano wa siku tano wa  58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) katika Ukumbi wa Mwalim Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Octoba 21, 2019.
 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa siku tano wa  58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao ni Viongozi wa Serikali, Mawaziri, Wanasheria, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na Mabalozi kutoka Nchi 48 Wanachama wa Shirika hilo wamsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati  akifungua Mkutano wa siku tano wa  58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Octoba 21,2019.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Sheria na Katiba Balozi Augustine  Mahiga alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa Mwalim Julius Nyerere Jijini Dar Es salaam Leo Octoba 21, 2019 kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tano wa  58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.  Palamagamba Kabudi alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Es salaam Leo Octoba 21, 2019 kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tano wa  58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO).(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Anaedaiwa kumuua mkewe kwa moto wa magunia ya mkaa apata wakili upelelezi umekamilika

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

WAKATI upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said (38) anayedaiwa kumchoma mke wake na magunia mawili ya mkaa umekamilika, wakili Mohamed Majaliwa amejitambulisha mahakamani hapo kama wakili wa utetezi wa mshtakiwa .

Mapema wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiarifu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika na kwamba jalada la kesi hiyo liko kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya kuletwa ofisi ya taifa ya mashtaka kusoma.


Simon alidai kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo aliiomba mahakama  hiyo ihairishe kesi hiyo.

Kufuatia taarifa hiyo, hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4,2019

katika kesi ya msingi mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la mauaji ambapo anadaiwa  Mei 15, 2019 katika oneo la Geza Ulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.

RC MNYETI AZINDUA BARABARA ZA KITETO

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amezindua barabara za Wilaya ya Kiteto za urefu wa kilomita 19.14 zilizotengenezwa kwa gharama ya shilingi 380,883,000.

Meneja wa wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kiteto mhandisi Edwine Magiri akizungumza baada ya RC Mnyeti kuzindua barabara hizo alisema zimefanyiwa matengenezo kwa kuanzia April 2019 hadi Julai 2019. 

Mhandisi Magiri alisema kati ya barabara hizo kilomita 19.14 zimewekewa changarawe na nyinginezo zimefanyiwa ukarabati wa kawaida. 

Alisema katika ujenzi wa kilomita hizo za barabara hizo kumewekewa na kujengewa kalvati 22 na pia kumejengwa madrifti mawili. 

"Kazi zimefanyika kwa wakati na kiwango kinachotakiwa ikiwemo vipimo kwani tulisimamia ujenzi ipasavyo wakati wa shughuli hiyo," alisema mhandisi Magiri. 

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza wakati akizindua mojawapo kati ya barabara hizo aliwapongeza Tarura Kiteto kwa namna walivyotengeneza barabara hizo. 

Hata hivyo, Mnyeti alitoa wito kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kuwa na tabia ya kusafisha mazingira ili ziwe safi kwa kuondoa uchafu. 

"Kuna ule utaratibu wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, tumieni nafasi hiyo kwa kuhakikisha mnaondoa uchafu uliopo pembezoni hasa katika mitaro," alisema Mnyeti. 

Pia, Mnyeti aliipongeza Tarura na wakala wa barabara za nchini (Tanroads) mkoani humo kwa namna wanavyotengeneza barabara na kuzikarabati pindi kukitokea matatizo. 

"Ukipita Manyara unakuta barabara zake zinapitika bila shida hongereni kwa hilo kwani ukipita sehemu nyingine unaona changamoto kwa wenzetu namna barabara zao zilivyo," alisema Mnyeti. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza baada ya kuzindua mojawapo ya barabara za Wilaya ya Kiteto. 
Meneja wa Wakala wa barabara wa Mijini na Vijiji (TARURA) Wilaya ya Kiteto mhandisi Edwine Magiri (kushoto) akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (katikati) kuzindua mojawapo ya barabara za eneo hilo. 

MKUTANO WA MAKATIBU ,WATENDAJI WAKUU WA SADC UNAOHUSU MASUALA YA MAZINGIRA MALIASILI NA UTALII WAANZA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu wakuu na Watendaji Wakuu katika Mkutano unaoendelea Katika Kituo cha Kimataifa cha mikutano AICC Jijini Arusha.
Domingos Gove Mkurugenzi Mkuu wa Idaravya Chakula na Kilimo na Maliasili kwenye Sekretatieti ya SADC
Makatibu wakuu na Watendaji wakuu kutoka nchi za SADC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo kufunguliwa rasmi.
Mkutano ukiendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkutano wa Makatibu wakuu na watendaji wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC Unaohusu masuala ya Mazingira Maliasili na Utalii umeanza leo Jijini Arusha

Aidha Mkutano huo ukiwa na lengo la kujadili mabadiliko ya tabianchi kwa nchi wananchama ambapo watapokea pia taarifa mbalimbali kuhusiana na kukabiliana Ujangili unaovuka mipaka ,kuwalinda wanayama pori na misitu.

Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Profesa Adolfu Mkenda alisema kuwa kwa sasa upo mjadala mkubwa ambao unaendelea kama utekelezaji wa itifaki mbalimbali za jumuiya hiyo ikiwemo ya vizuizi itifaki ya maeneo ikiwemo pia viendelee kuwepo na vizuizi vingine vipya vilivyowekwa kama vinafaa kwa maendeleo ya nchi hizo za SADC

Katibu Mkuu wa Wizara ,Profesa Adolfu Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa makatibu wakuu kutoka nchi mwanachama amesema kuwa mkutano huo utajadili mambo mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ujangili ambayo inapaswa kuungwa mkono kwa nchi zote mwanachama badala kuachwa kwa nchi moja.

“Ifahamike kuwa Tanzania ni miongoni mwa wananchama wa SADC wanaotekeleza mkakati kuhusu usimamizi wa sheria na vita dhidi ya ujangili wa wanayamapori na maeneo mengine yanayohusu mipango ya uhifadhi yaliovuka mipaka wan chi moja kwenda nyingine kwenye maeneo ya misitu uvuvi mazingira na mabadiliko ya tabianchi”alisema Prof.Mkenda

Mkenda amesema kuwa nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za kupambana na ujangili.“Tunahitaji kuwa na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC hii ni moja kati ya agenda muhimu zitakazojadiliwa” Alisema Profesa Mkenda

Mkurugenzi wa idara ya Chakula ,kilimo na Maliasili kutoka Sektretarieti ya SADC ,Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya kimazingira,Utalii na Wanyamapori 

Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Raisi ,Muungano na Mazingira ,Mhandisi Joseph Malongo amesema kuwa watajadili mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa pamoja na jinsi ambavyo wananchi wanaweza kutumia uchumi wa bluu kwa maana ya bahari katika kuchangia maendeleo .


MAKATIBU WAKUU WA SADC KUJADILI MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UJANGILI

$
0
0
Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Maliasili,Utalii na Mazingira wa nchi za SADC wameanza vikao vya kujadili na kuweka agenda za mkutano wa Mawaziri wa sekta husika kutoka umoja huo ambapo wanatarajia kujadili mpango mkakati wa pamoja wa kukabiliana na ujangili ili kutomokeza ujangili katika nchi mwanachama.
Katibu Mkuu wa Wizara ,Profesa Adolfu Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa makatibu wakuu kutoka nchi mwanachama  amesema kuwa mkutano huo utajadili mambo mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ujangili ambayo inapaswa kuungwa mkono kwa nchi zote mwanachama badala kuachwa kwa nchi moja.
Mkenda amesema kuwa nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za kupambana na ujangili.
“Tunahitaji kuwa na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC  hii ni moja kati ya ajenda muhimu zitakazojadiliwa” Alisema Profesa Mkenda
Mkurugenzi wa idara ya Chakula ,kilimo na Maliasili kutoka Sektretarieti ya SADC ,Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya kimazingira,Utalii na Wanyamapori .
Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.

Waziri Mhagama yazitaka TBS, SIDO kushirikiana kuendeleza wajasiriamali

$
0
0


Waziri wa Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama, akizungumza na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)juzi mkoani Simiyu alipotembelea banda la shirika hilo kwenye kilele cha maonesho ya tatu ya mifuko ya uwezeshaji program na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi. Picha na mpiga picha wetu.




SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetakiwa kushirikiana na Shirika la kuendeleza viwanda vidogo (SIDO) ili wajasiriamali kupata maeneo bora ya kuzalishia katika karakana za SIDO





Waziri wa Sera,Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama ametoa wito huo jana mkoani Simiyu alipotembelea banda la TBS wakati wa kilele cha maonesho ya tatu ya mifuko ya uwezeshaji program na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi.





Mhagama alitoa wito huo kufuatia maelezo kutoka kwa ofisa wa shirika hilo, Roida Andusamile kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozizalisha kutokana na kutokuwa na majengo bora ya kuzalishia.


Akizungumza na washiriki wa maonesho hayo, Mhagama ameitaka mifuko inayotoa mikopo kwa wajasiriamali kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo hiyo ili iweze kufikia wajasiriamali wengi nchini.





“TBS mnapaswa kushirikiana na SIDO ili kuwawezesha wajasiriamali kuzalishia katika kalakana za SIDO na hatimaye waweze kuzalisha kwa kuzingatia viwango na kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo," alisisitiza Mhagama.


Naye mtenndaji Mkuu wa Baraza hilo, Beng'I Issa amewataka wananchi wa Simiyu kuchangamkia fursa zilizotolewa katika maonesho haya kwani uwepo wa maonesho haya utaibua chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Simiyu.


Mhagama alisema utoaji huo wa mikopo uwe na riba nafuu ili wajasiriamali wengi wanufaike nayo na amelitaka Baraza la Uwezeshaji kusimamia mifuko ya uwezeshaji kuendelea kujitambulisha na kujitangaza kwa wananchi kupitia programu mbalimbali.


Katika maonesho hayo TBS ilipata fursa ya kuwatembelea wajasiriamali wapatao 60 wanaozalisha bidhaa mbalimbali na kuwapatia utaratibu ili waweze kusajili majengo wanayozalishia , bidhaa na kuthibitisha ubora wake.


Alisema maonesho haya pia yanakutanisha wajasiriamali na taasisi za serikali lengo likiwa ni kuwawezesha kurasimisha biashara zao na kuhamasisha matumizi ya mifuko ya ya kijamii pamoja na mtandao kwa wajasiriamali.

Maonesho haya yaliyoanza Oktoba 14,2019 mpaka Oktoba 20 2019 mbali na wajasiriamali yameshirikisha taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zipatazo 48.


Pia wananchi waliotembelea banda la shirika hilo walielimishwa umuhimu kwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora na TBS na kuangalia muda wa matumizi wa bidhaa wanazozinunua badala ya kuangalia bei.

MWENYEKITI HALMASHAURI SINGIDA DC AENDESHA HARAMBEE UJENZI WA MSIKITI

$
0
0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha, akizungumza juzi katika Harambee ya ujenzi wa Msikiti wa Zaharau uliopo katika Kata ya Ughadi "B" Halmashauri ya wilaya hiyo.
Msikiti wa Zaharau uliopo katika Kata ya Ughadi "B" Halmashauri ya wilaya hiyo ambao unatakiwa kujengwa.
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye harambee hiyo.
Michango ikihesabiwa.
Katibu wa Msikiti huo Sheikh Ismail Issa, akizungumza.
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye harambee hiyo.



Na Boniphace Jilili Singida. 


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha ameitaka jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea kujitokeza katika jamii. 

Elia Digha aliyasema hayo juzi wakati akiendesha harambee ya ujenzi wa jengo la Msikiti wa ZAHARAU uliopo katika kata ya Ughadi "B" Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo alichangia Mabati 50, na sh. laki 3.

Mwenyekiti huyo alisema kumekuwa na vitendo vya wanaume kuwalawiti watoto, ambapo akasema vitendo hivyo havikubaliki katika jamii, na kuwaomba viongozi wa kidini kusaidiana kukemea jambo hilo huku wakimwomba mwenyezi Mungu kuondoa roho za vitendo hivyo mioyoni mwa watu. 

"Baadhi ya wanaume wamekuwa washenzi hawamuongopi hata Mungu wanawalawiti watoto wadogo, wanabaka watoto jamani wapi tunakoelekea"alisema Digha. 

Hata hivyo aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, pamoja na kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa wenye sifa za kuandikishwa, ambapo ni wapiga kura wapya, waliopoteza ama kuharibikiwa kadi zao na sifa zingine zilizoaishwa na tume ya uchaguzi. 

Digha alikusanya jumla ya sh. milioni 5 laki 5 na 100,kwenye harambee hiyo,fedha taslimu ikiwa ni sh.milioni 1 laki 8 na elfu 31 Mia moja,huku ahadi ikiwa ni sh.milioni 2 na nusu ambapo aliwataka viongozi wa msiki huo kusimamia na kutumia fedha hizo kwa matumizi yaliyotarajiwa ili kukamilisha jengo hilo na waumini waanze kulitumia kwa shughuli za ibada. 

Aidha Katibu wa Msikiti huo Sheikh Ismail Issa wakati akisoma taarifa ya Msikiti alisema jumla ya sh. Milioni 20 zinahitajika kukamilisha jengo hilo ambapo mpaka sasa zaidi ya sh.milioni 9 zimekwisha tumika.

SHIRIKA LA INADES FORMATION LIMEITAKA JAMII KUTAMBUA HAKI NA SHERIA ZA MNYAMA PUNDA

$
0
0
Mnyama aina ya Punda ambaye anapiganiwa kupata haki na sheria zake na Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz).
Na Fredy Mgunda Iringa
SHIRIKA la Inades Formation Tanzania (IFTz) limeitaka jamii kutambua haki na sheria za mnyama punda pamoja na kutambua mchango wa punda katika maisha ya jamii.


Akizungumza na vyombo vya habari  mratibu wa kuboresha maisha kupitia ustawi wa mnyama kazi punda Fadhili  Nyingi  ambapo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mnyama punda pamoja na  kurasimisha sekta ya punda katika halmashauri ya wilaya ya iringa.


Lengo la kwa la mradi ni kuongeza uelewa wa watu juu ya haki za wanyama na ufugaji bora wa Punda,mwisho wa siku watu wanatakiwa kujua punda anatakiwa kula nini,analala wapi na anahaki gani za msingi kutoka kwa binadamu” alisema Nyingi


Nyingi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza uelewa kwa wananchi juu ya mnyama punda na kuwa sekta rasmi kama zilivyo sekta nyingine.


Aidha ameeleza mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kubadili mitizamo ya wananchi na kupunguzwa ukatili dhidi ya mnyama punda.


“Mafanikio yapo toka tumeanza mradi huu,maana wananchi wengi waliopo vijijini wameanza kubadilika kimtadhamo juu ya mnyama punda ndio maana sasa wameanza kuacha kuuza punda” alisema Nyingi


Kwa upande wake afisa mfawidhi nyanda za juu kusini bwana Nong’ona Solomoni amebainisha baadhi ya magonjwa yanayokumkumba mnyama punda ni pamoja na pepo punda,homa ya farasi na vidonda.


Hata hivyo kupitia mradi huo wa Inades Formation Tanzania wamefanikiwa kuunda vikundi 6 vya kukopeshana pamoja kutoa elimu juu ya haki za wanyama.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya Mkoani Rukwa ajisalimisha polisi kwa tuhuma za kubaka

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Rukwa kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya iliyopo kata ya Kaengesa, Wilayani Sumbawanga Dastan Mlelwa anafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa tuhuma ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na cha tatu katika shule hiyo.

Amesema kuwa anataarifa kuwa mwalimu huyo tayari amekwishajisalimisha katika mikono ya polisi na hivyo kumtaka kamanda wa polisi mkoa, Kamanda wa TAKUKURU mkoa pamoja na Mkuu wa Usalama wa mkoa kufuatilia jambo hilo ili mwalimu huyo asitoke kwenye mikono ya polisi bali apelekwe mahakamani.

“Hili jambo hatutalifumbia macho, Mkuu wa shule kuwatafuta wanafunzi kimapenzi na mpaka kuwatia mimba, yeye kama mzazi na mwalimu haikubaliki hata kidogo, huu ni ubakaji kwasababu wale wanafunzi wa kidato cha pili na cha tatu hawana umri wa miaka 18 ni chini ya hapo, ni ubakaji,” Alisisitiza.

Katika kusisitiza suala hilo pia ameitaka kamati hiyo kufuatilia kesi ya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpui iliyoopo Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga aliyembaka na kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili na baadaye mwanafunzi huyo kuhamishwa katika shule ya Sekondari Mazwi iliyopo Manispaa ya Sumbawanga.  

Katika hatua nyingine Mh. Wangabo amewaagiza wajumbe hao wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa kufuatilia kesi ya wizi wa mifugo inayomhusisha Afisa mifugo wa mji mdogo wa laela, wilayani Sumbawanga Emanuel Tluwey baada ya kukamatwa akiwa anachinja ng’ombe wa wizi kesi ambayo ilifikishwa polisi na kuonya kuwa kesi hiyo isifinyangwe finyangwe ili mwizi huoy asichukuliwe hatua. 

“Lakini kuna Mazingira tata huenda kesi ikafinyangwa finyangwa na mwizi huyu asichukuliwe hatua, sasa narudisha kwa timu hii hapa, TAKUKURU yuko pale, jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama fuatilieni suala hili kule Laela huyu mwizi wa mifugo lazima achukuliwe hatua ya kisheria afikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo,” Alisema.
Mh. Wangabo ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika kikao maalum kilichowajumuisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na watumishi wa seksheni ya Elimu na watumishi wa seksheni ya uchumi na uzalishaji inayojumuisha watumishi wa  mifugo katika Mkoa.

Mh. Wangabo amesema kuwa nia ya kuyafanya hayo ni kupiga vita uhalifu ndani ya mkoa pamoja na ubakaji wa wanafunzi na kuonya kuwa itafika wakati kutakuwa na kura za maoni mashuleni kwa wanafunzi ili kumbaini anayewashawishi wanafunzi hao kujiingiza katika suala la mapenzi katika umri mdogo. 

MAKATIBU WAKUU WA NCHI 16 WAKUTANA ARUSHA KUWEKA AGENDA YA MKUTANO WA SADC KWA MAWAZIRI WA SEKTA ZA MAZINGIRA,MALISILI NA UTALII .

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa Sekretarieti ya SADC,Domingos Gove akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.  
  Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira ,Joseph Malongo akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.
Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi  wa Sekta ya Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC ,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika kituo cha kimataifa cha Mikutano cha AICC jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Malisili na Utalii ,Prof ,Adolf Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu wakuu na Maafisa Waandamizi wa Sekta za Mazingira ,Malisili na Utalii kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo , kusini mwa Afrika (SADC) . 
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .
Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa  Sekretarieti ya SADC ,Domingos Gove akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaoshirikisha Makatibu Wakuu kutoka nchi 16 za SADC.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wanaoshiriki Mkutano huo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,prof ,Adolf Mkenda akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.

Na Dixon Busagaga,Arusha .

MAKATIBU wakuu wa Sekta na Maafisa waandamizi wa Wizara zinazo shughulika na Mazingira ,Maliasili na Utalii wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kuweka agenda za Mkutano wa Mawaziri wa sekta husika kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) .

Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kikao hicho cha awali ni pamoja na mpango mkakati wa pamoja wa kukabiliana na ujangili kwa nchi za SADC ,hoja inayo paswa kuungwa mkono nan chi wanachama.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof,Adolf Mkenda amesema  nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za kupambana na ujangili.

“Tunahitaji kuwa na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC,  hii ni moja kati ya agenda muhimu zitakazojadiliwa” alisema Profesa Mkenda.

Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili kutoka Sekretarieti ya SADC, Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya Mazingira,Utalii na Wanyamapori .

Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira,Mhandisi Joseph Malongo amesema kuwa watajadili mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa pamoja na jinsi ambavyo wananchi wanaweza kutumia uchumi wa bluu kwa maana ya bahari katika kuchangia maendeleo .

MICHUANO YA BASHUNGWA KARAGWE CUP YAHITIMISHWA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV

Michuano ya Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Karagwe Innocent Ruga Bashungwa (Mb) ambae pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara imefikia tamati leo hii toka ilipoanza mwanzoni mwa mwezi Agost 2019 kwa timu ya Kata ya Nyakahanga kuchukua ubingwa huo katika msimu wa pili wa ligi hiyo, baada ya kuifunga timu ya Kata ya Kamagambo kwa penalti 3-2 Katika Uwanja mpya wa Bashungwa uliopo mjini Kayanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

Kilele cha mashindano hayo  kilitanguliwa na mchezo wa awali wa  mshindi wa tatu kwa kuzikutanisha Timu za kata ya Nyakabanga na Kayanga, ambapo Nyakabanga wameibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Kata ya Kayanga baada ya Timu hizo kutoshana Nguvu kwa Dakika 90 za mchezo.

Mgeni rasmi katika mchezo wa Fainali hizo Constantine Kanyasa (Mb) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema amefurahishwa na Fainali hizo na huku akiduwazwa na umati wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo,  ikiwa ni ishara ya upendo mkubwa wa wananchi hao dhidi ya Mbunge wao pamoja na michezo kwa ujumla, licha ya mambo mengine Kanyasu amesisiitiza juu ya Vijana na wananchi kuendelea kutangaza Utalii kupitia michezo hususani hifadhi mbili za Burigi - Chato na Ibanda - Rumanyika zilizopo katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa.

Kwa upande wake Mwenyeji na muandaaji wa  mashindano hayo  Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Luga Bashungwa, amewashukuru wote waliofanikisha mashindano hayo kubwa akizidi kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo amekuwa akimsaidia kwa kumuunga mkono, lakini pia kwa jinsi alivyoendelea kumuamini na kwamba hatomuangusha 
Huku akiongeza kuwa kupitia michezo ataendeleza mshikamano na mahusiano kati ya Vijana na Serikali, ikiwa pia michezo ni ajira, afya na Utalii.

Bingwa wa michuano hiyo Timu ya Nyakahanga wameibuka na Kitita cha Shilingi  amejipatia Tsh 2,500, 000/=, jezi seti 1 na Kombe, 
Mshindi wa pili amejipatia Tsh 1,650,000/= na jezi seti 1.
Mshindi wa tatu amejipatia Tsh 450,000/= na jezi seti 1.
Mshindi wa nne amejipatia Tsh 300,000/ na jezi seti 1, huku Zawadi hizo zikinogeshwa na Zawadi kutoka Kwa Mgeni rasmi Aliyeongeza Laki mbili Kwa Mshindi wa kwanza na pili, wakati Mke wa Waziri Bashungwa Mama Alaska akiongeza Milioni Moja katika Zawadi za washindi .Zawadi nyingine ni Timu yenye nidhamu imejipatia jezi seti 1, Zawadi nyingine zilikuwa za: 
Golikipa bora, Mfungaji bora na Mchezaji bora kila mmoja amejinyakulia Tsh 50,000/=

Kupitia mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti ametangaza mechi kati ya Bukoba combine na Karagwe Combine mchezo utakaochezwa wiki tatu zijazo na Mshindi atazawadiwa Milioni Mbili, na atakaeshindwa atapata kifuta jasho shilingi Milioni Moja.

Awali ligi hiyo ilishirikisha timu zote za kata  23 zilizopo Wilaya ya Karagwe huku kila timu ikipewa seti moja ya jezi na mpira mmoja kwa ajili ya michuano hiyo. Pia viongozi wengine waliohudhulia fainali hiyo ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka viongozi  wa Chama na Serikali
na watu Mashuhuri.
Baadhi ya wananchi na mashabiki wa michezo waliojitokeza kushuhudia fainali za Kombe la Bashungwa Karagwe Cup.
 Mkuu Wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti akiwasili katika viwanja vya Kayanga kuungana na maelfu ya wapenda soka katika Kilele cha Michuano ya Bashungwa Karagwe Cup, Pembeni ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka na Mwenyekiti Wa Ccm Karagwe Robinson Mutafungwa.
 Picha ya pamoja wamuzi pamoja na manahodha Wa Timu zilizotinga Fainali, Nyakahanga na Nyakabanga, ambapo mwamuzi Wa kati aliechezesha mchezo huo ni Ahmada Simba.
 Mgeni Rasmi Naibu Waziri Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (MB) akiwa na Mwenyeji wake Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara (MB) wakielekea uwanjani kukagua timu mapema kabla ya kuanza mchezo wa Fainali
 Mikakati ikiwekwa sawa ya kuwa na Mechi kati ya Karagwe Combine, na Bukoba Combine ambapo baada ya Wiki tatu kuanzia sasa Itapigwa mechi hiyo na Mshindi akiondoka na Milioni 2, na Milioni moja kwa atakaefungwa, hiyo ni kwa Mujibu wa Marco Gaguti RC - Kagera.
 Kinyuri nyuri cha Bashungwa, Mama Alaska akifuatilia mtanange, mbali na yote amemuunga mkono Mumewe kwa kutoa zawadi ya Shilingi Laki tano kwa mshindi wa kwanza na laki tano kwa mshindi wa pili.
 Mwali akiletwa uwanjani mapema kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo wa fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
 Kipa wa Nyakabanga akipangua mkwaju wa mwisho wa penati, kutoka kwa mchezaji wa Kayanga na kupelekea kuipa ushindi Timu yake kwa Kuibuka mshindi wa Tatu, Mchezo huo ulitangulia mapema kabla ya mchezo wa Fainali.
 Mgeni Rasmi Costantine Kanyasu Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Akikabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Tatu, nahodha wa timu ya Nyakabanga, Kiasi cha Shilingi Laki Nne na Nusu na jezi seti moja.
 Mgeni Rasmi Costantine Kanyasu Naibu Waziri Maliasili na Utalii, akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili, nahodha wa Timu ya Kamagambo Milioni moja Laki sita na Nusu na Seti moja ya Jezi
Mabingwa wa Mashindano ya Bashungwa Karagwe Cup 2019, Timu ya Kata Nyakahanga wakishangilia ushindi Mara baada ya kukabidhiwa Zawadi zao

MAHAKAMA YA KISUTU IMEUTAKA UPANDE WA MASTAKA KUWATENDEA HAKI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuitendea haki kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Mhasibu Mkuu wa zamani Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake watatu kwa kuwa mashtaka yanayowakabili watuhumiwa hao hayana dhamana.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba  ameeleza hayo leo Oktoba 21, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini upande wa mashtaka kupitia wakili wa Serikali Silivia Mitanto kudai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa  ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mawakili wanaosimamia kesi hiyo hawapo wapo mahakama ya mafisadi.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alisema hajafurahi kuona kesi hiyo inaahirishwa kwani lazima waitendee haki  kwa sababu mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga na Leonard.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake wawili, wanakabiliwa na mashtaka 40, kati ya hayo, makosa 20 ni ya utakatishaji fedha na 19 ya kughushi.

Kwenye mashtaka hayo 29 yanamkabili Gugai peke yake ikiwemo ya kumiliki mali zilizozidi kipato halali yenye thamani ya Sh.Bilioni 3.6 inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembeaahirishwa  2015.

Pia Gugai na Makaranga wanashtakiwa kutakatisha fedha. Aidha Gugai na Aloys wanakabiliwa na mashtaka manane ikiwamo manne ya kughushi na manne ya utakatishaji fedha.

VIONGOZI CHADEMA WAPEWA WIKI MBILI

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa wiki mbili kwa viongozi tisa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kujiandaa ili waweze kuanza kujitetea kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 4,5 na 8 mwaka huu.

Pia Mahakama imeagiza kielelezo cha video kilichotolewa na upande wa mashtaka, kinachoonesha maandamano ya viongozi hao kilichoombwa na upande wa utetezi, kisitumike nje ya mahakama bali kitumike kwa kutumia  miundombinu ya mahakama chini ya usimamizi wa uongozi wa mahakama.

Akisoma uamuzi hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema ni kweli washitakiwa hao wanahitaji muda wa kufanya maandalizi na kwamba kipindi muafaka cha kujiandaa ni siku 14 na ameongeza kuwa, idadi ya mashahidi waliotajwa ni kubwa na wasipokuwa waangalifu kesi haitaisha hivyo, ni lazima kuwa na ratiba maalum ya kusikiliza kesi hiyo.

"Kielelezo mlichokiomba hakitaenda popote isipokuwa kitatumika kwa kutumia miundombinu ya mahakama ili iwe huru katika kuandika hukumu hivyo wakati upande wa utetezi wakitumia kielelezo hicho kuwaandaa washitakiwa, itakuwa chini ya usimamizi wa utawala ili kuhakikisha usalama wa kielelezo na miundombinu inazingatiwa, amesema Simba

Aidha, upande wa utetezi wametakiwa kutoa taarifa siku tatu kabla juu ya matumizi ya kielelezo hicho katika ukumbi wa mahakama na kusema kesi  hiyo itaanza kusikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia  Novemba 4,5 na 8 na baadaye itapangiwa ratiba maalum.

Mbali na Mbowe washitakiwa wengine  katika kesi hiyo,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na  Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini,  Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

UTIAJI SAINI UJENZI WA MAHAKAMA KUU TUNGUU WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama Zanzibar Kai Bashir Mbaruk kulia akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advent Construction ltd Mkataba wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Unguja hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga Zanzibar
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama Zanzibar Kai Bashir Mbaruk kulia wakibadilishana hati ya saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advent Construction ltd Mkataba wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Unguja hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga Zanzibar.
 Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Maalim akitoa hotuba katika hafla ya utiliaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Unguja ambayo itakayojengwa na Kampuni ya Advent Construction ltd hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Vuga Zanzibar.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hotuba katika hafla ya utiliaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Unguja ambayo itakayojengwa na Kampuni ya Advent Construction ltd hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Vuga Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Rubondo Island ikiwa katika hatua za mwisho ya kuletwa

DC NAMTUMBO AWATAKA WANANCHI KUWAPATIA WATOTO CHANJO YA SURUA, POLIO NA RUBELLA

$
0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA, NAMTUMBO
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo amewataka wananchi Wilayani Namtumbo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao waliochini ya miaka mitano kupata chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya Wilayani humo.

Akiongea na wananchi wa kata ya minazini katika ofisi ya serikali ya kijiji cha Minazini Mkuu wa wilaya huyo aliwataka wananchi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya ugonjwa wa Surua,Polio na Rubella ili kuwakinga na kuambukizwa na magonjwa hayo.

Aidha Mkuu wa wilaya huyo aliwathibitishia wananchi na kuwatoa hofu kuwa wasiwe na hofu yoyote kwani chanjo hizo zimethibitishwa na shirika la afya ulimwenguni , wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kuwa ni salama .

Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo Godwin Luta alimthibitishia mkuu wa wilaya huyo kuwa wataalamu wa afya wilayani humo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuwapatia watoto chanjo katika vituo vya kutolea huduma ili kuwakinga na magonjwa ya surua Rubella na Polio.

Luta alidai mwitiko wa wananchi kuwapatia chanjo watoto waliochini ya miaka mitano Wilayani humo umekuwa mkubwa kutokana na wananchi hao kuelewa umuhimu wa chanjo hizo na kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kutolea huduma za afya .

Adinani Nyoni mkazi wa minazini alisema elimu iliyotolewa na wataalamu wa afya na wataalamu wenyewe kuonesha mfano kwa kuwapatia chanjo watoto wao iliondoa woga kwa wananchi na kusababisha wananchi hao waondoe hofu na kujitokeza kuwapeleka watoto wao kuwapatia chanjo hizo.

Watoto 637 walipatiwa chanjo ya Surua ikiwa wanaume 227 na wanawake 410 na waliopatiwa chanjo ya polio ni 692 ikiwa wanawake 330 na wanaume 362 katika uzinduzi wa chanjo hiyo katika viwanja vya ofisi ya kijiji cha Minazini .
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo  akizungumza na wananchi wa wakati wa ufunguzi wa chanjo katika kijiji cha Minazini.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo akiwa na mtoto aliyepata chanjo wakati wa ufunguzi wa chanjo katika kijiji cha Minazini.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images