Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA YA KILIMO

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 20,2019 amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo katika kikao cha kazi kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam. Pichani, Waziri Mkuu akizungumza na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba (wa tatu kulia), Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (wa pili kushoto), Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE.KANYASU AWATAKA WAZAZI WATIMIZE WAJIBU WAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasiil na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi Antony Ezekiel ambaye bingwa wa somo la Fizikia katika mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Rocks- Hill ya jijini iliyopo katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu ( kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Shule ya Sekondari ya Rocks- Hill, Meshak Mpalanga wakiangalia ratiba kabla ya mahafali ya kidato cha nne kuanza katika shule hiyo iliyopo katika wilaya ya Ilemele jijini Mwanza.





Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na jumla ya wahitimu 60 wa kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Rocks-Hill iliyopo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Rocks- Hill wakiwa katika mstari wa kuingia katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya wahitimu hao.

( PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

**************************
Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewakumbusha Wazazi wenye watoto waliowapeleka kusoma katika shule binafsi wahakikishe wanawatimizia mahitaji yao ya muhimu katika kipindi chao chote cha masomo ili waweze kufaulu mitihani yao ya mwisho.

Badala ya kuja na zawadi nyingi siku ya mahafali ajili ya kuwapongeza wanapohitimu ilhali wanafunzi hao walikuwa wakirudishwa nyumbani kila wakati wakachukue ada ya shule.

Ametoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa wanafunzi 60 yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Rocks Hill iliyopo katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Amesema wazazi lazima wawekeze kwa watoto wao ili waweze kusoma katika mazingira ya kutokuwa na hofu ya kurudishwa nyumbani kwa sababu wazazi wao hawajawalipia ada ya shule.

“Ukiamua kumsomesha mtoto lazima ukubali kwamba elimu haijawahi kuwa bure, hivyo ni jukumu la kila mzazi kukidhi mahitaji ya mwanae likiwemo suala la kumlipia ada kwa wakati.” alisisitiza Kanyasu

Amesema ni vyema wazazi hao kutambua dhamana waliyonayo katika kuwandaa watoto wao kielimu badala ya kusubili hadi watoto warudishwe nyumbani.

Mhe.Kanyasu amesema kitendo hicho cha wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa ajili ya ada kimekuwa kikiwarudisha nyuma kimasomo kwa vile wamekuwa wakikosa baadhi ya vipindi.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiweze kuharibikiwaa mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Meshak Mpalanga amesema katika kipindi chao chote cha masomo wamelelewa kimaadili hali itakayowasaidia kupambana zaidi katika kuyamudu maisha

Akizungumzia jinsi walivyoandaliwa kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho, Amesema anatarajia idadi kubwa ya wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano.

NayevMwanafunzi bora katika masomo yote aliyetajwa katika mahafali hayo, Diana Titus amesema wamejianda vyema na wapo tayari kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho.

” Tunawashuru walimu wote kwa kutulea na kutufundisha, tunaamini sote tutafanya vizuri mitihani yetu.alisisitiza Mwanafunzi huyo

BAADA YA MIAKA MINNE YA UADUI YUSUPH MAKAMBA, KHAMIS MGEJA WAFANYA DUA MAALUM, WAOMBANA MSAMAHA YAISHE

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

BAADA ya miaka ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Yusuph Makamba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Shinyanga Khamisi Mgeja kuishi wakiwa maadui hatimaye wamekutana na kusameehana na kuondoa tofauti zao kwa kusoma dua maalum.

Makada hao wa CCM wamekutana nyumbani kwa Makamba maeneo ya Kisanga Tegeta jijini Dar es Salaam na hivyo kutumia nafasi hiyo kuzungumza mambo mengi na kubwa ni kuombana msamaha na kusameehana.Baada ya dua wakacheka pamoja na kukumbatiana. 

Akizungumza Mgeja kwa upande wake amesema kilichowasukuma kuondoa tofauti zao ni maadili na misingi ya dini na kwa maslahi mapana ya dini na utu tu si vinginevyo dini imesisitiza kusameheana."Sisi siasa ilitufikisha pabaya sana na mzee wangu huyu".

Kwa upande wake mzee Makamba amempongeza Mgeja kwa kueleza miaka ya nyuma Makamba akiwa Katibu mkuu wa CCM na Mgeja akiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga walikuwa marafiki sana lakini shetani aliingilia kati na kumkumbusha umuhimu wa kusameheana na kutoa maelekezo yaliomo ndani ya dini.

Makamba ameitaka jamii izidishe upendo na kujenga utamaduni wa kusameheana kama alivyofanya yeye na Mgeja. "Tumeondoa tofauti na huko mbinguni, hizi siasa tutaaziacha hapa hapa duniani huko kila mmoja na amali zake, tujitahidi kufanya mema hapa duniani na kuzidisha upendo baina yetu,"amesema.

Baada ya kuondoa tofauti hizo wote pamoja kuangalia mifugo ya mzee na hasa ng'ombe wa maziwa, kuku, bata na sungura.

Mgeja baada ya kutembezwa na kujionea ufugaji wa kisasa amempongeza mzee Makamba kwa ufugaji wa kisasa wa kitaalamu na wenye tija kiasi ambacho amepata somo zuri na ujuzi huo atauchukua kuupeleka nyumbani kahama shinyanga.

"Hakika ugeni wangu huu pamoja na suluhu lakini nimepata elimu nzuri sana zitanisaidia katika shughuli zangu za ufugaji na kilimo ambazo ndizo niliko jielekeza hivi sasa huko nyumbani kijiji cha Nyanhembe kata ya Kilago halmashauri ya mji wa Kahama Shinyanga" amesema Mgeja
Mgeja ametoa mwito kwa watanzania wajielekeze katika shughuli za kilimo na ufugaji wenye tija kwani kuna fursa kubwa sana na hasa vijana kutoa ajira na ukuaji wa uchumi kuliko kubaki kijiweni na kubaki kuwa walalamikaji tu. 

Pia ameshauri Watanzania kichangamkia soko jipya la sungura ambalo linakuwa kwa kasi ndani ya nchi na nje ya nchi hasa majirani zetu nchi za Kenya na kwamba Tanzania bila umasikini inawezekana.

Mgeja amesema ni vema kila mmoja wetu akatambua maendeleo na tukitaka kuondokana na umasikini ni lazima kufahamu maendeleo hayana njia ya mkato lazima afanye kazi kwa juhudi na maarifa na ndio siri ya mafanikio.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Yusuph Makamba (aliyevaa kanzu) akiwa  na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Shinyanga wakiwa wamekaa pamoja baada ya kukutana na kuomba msamaha kutokana na tofauti walizokuwa nazo kwasababu ya mambo ya kisiasa

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI URUSI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 20, 2019) kwenda Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba 23 – 24, 2019.

Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Mkutano huo utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23, na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba 24, 2019.


Waziri Mkuu atashiriki kwenye mikutano yote miwili.

WZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONDOKA NCHINI KWENDA URUSI

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 20, 2019 ameondoka chini kwenda Urusi ambako atamwakilisha Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. Pichani, Waziri Mkuu akisalimiana na Spika wa Bunge Job Ndugai kwenye Uwanja Ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri SADC Yakamilika

$
0
0
Picha ya Pamoja ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri Mazingira,Maliasiki na Utalii wa nchi wananchama wa SADC unaotarajiwa kuanza kesho Jijini Arusha.
wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri Mazingira,Maliasiki na Utalii wa nchi wananchama wa SADC wakikagua eneo la Kituo cha Kimataifa Mikutano cha AICC ambapo mkutano huo utafanyika kuanzia kesho 21-25 oktoba 2019

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira ,Maliasili na Utalii wa nchi mwanachama wa SADC unaotajia kuanza kesho jijini Arusha  yamekamilika na tayari kutoka mataifa mbalimbali wameanza kuwasili jijini Arusha kwa ajili ya kuanza mkutano huo kesho.
Peofesa Adolf Mkenda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara  ya Maliadili na Utalii amesema maandalizi tayari yamekamilika kuanzia eneo ambalo mkutano huo utafanyikia usafiri,chakula pamoja na fursa ya kutembelea hifadhi mbalimbali za taifa itakayokuwepo katika kipindi chote cha mkutano.

Profesa Mkenda amesema kuwa siku ya kesho makatibu wakuu wa Wizara husika watakutana na kuandaa agenda za mkutano huo ambao mpaka sasa maandalizi yamekamilika.
 Dr,Omar Ali Amir  ni Naibu Katibu Mkuu ,Wizara ya Kilimo,Maliasili ,Mifugo na Uvuvi Zanzibar ameeleza kuridhishwa na maandalizi yaliyofanyika mpaka sasa na Tanzania na chi za SADC zitaweka mikakati ya kushirikiana katika kupambana na uvuvi haramu baharini na kusimamia sambamba rasilimali za uvuvi.
Mhandisi Joseph Malongo  ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Raisi ,Muungano na Mazingira ,amesema  katika mkutano huo kuna mambo makubwa ambayo watahimiza ikiwemo  nchi ambazo haziridhia kuanzishwa kwa itifaki ya SADC ziweze kuridhia ikiwa ni pamoja na kupitia na kutathmini mpango mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi wan chi za SADC.
Kwa upande wake  Katibu Mkuu wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Rashid Tamatama amesema kuwa miongoni mwa mambo muhimu watakayoyaangazia ni pamoja na  itifaki ya Sadc inayolenga kuinua maisha ya watu kupitia sekta ya uvuvi ambayo eneo la kimkakati linalochangia katika usalama wa chakula na kukuza uchumi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJULIA HALI MHANDISI DIONIZ MAJOGO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakimpa pole Mhandisi Dioniz Majogo wakati walipokwenda nyumbani kwa Waziri wa zamani, Edgar Majogo, Ununio jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia kufutia kifo cha Elizabeth Majogo, mke wa Mheshimiwa Majogo, Oktoba 20, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Bazi Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerald Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshugulikia Elimu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ali Sakila Bujiku kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakisaini Hati ya kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru wapili kutoka (kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli wa kwanza (kushoto), pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakwanza (kulia) mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa sambusa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU


MALI ZA BILIONEA ERASTO MSUYA ZAZIDI KUITESA FAMILIA...MAMA WA MAREHEMU ADAI HAKUNA MGOGORO

$
0
0

Na Woinde shizza, Michuzi TV Arusha

SAKATA la wanandugu wa familia ya narehemu bilionea Erasto Msuya ambao ni wakazi wa Arusha wanaodaiwa kugombea mali  za marehemu Msuya limechukua sura mpya baada ya upande wa baba yake kuibuka na kudai hakuna mgogoro wa kugombea mali ila suala hilo linazushwa kwa maslahi ya upande wa mke wa marehemu.

Pia imekanusha madai ya kufunga nyumba tano za marehemu na kusababisha watoto kuishi hotelini na kudai kuwa mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye  Kervin Msuya(22)aliamua kuishi mwenyewe hotelini kwa kupenda anasa zake na si kwa kufungiwa nyumba .

Akizungumza na vyombo vya habari, mama mzazi wa Marehemu Erasto, Ndeshu Msuya ameeleza bayana nyumba hizo zilifungwa kwa sababu ya usalama baada ya mke wa marehemu, Miriam Mrita kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya wifi i yake Anitha Msuya na kukosa mwangalizi kutoka na baadhi ya vitu kupotea ovyo.

Amesema hatua hiyo ilikuja kutokana na fnyumba aliyokuwa akiishi marehemu na familia yake ,upande wa mke wa marehemu kutaka kuiuza kwa kuwa haikuwa sehemu ya mali za mirathi za marehemu zilizokuwa zimeorodheshwa.

Mama Ndeshu alidai kwamba  funguo za myumba hizo zilikabidhiwa kwa ndugu hao wa Mke ambao hadi sasa bado wanazo.

Amefafanua Kervin ambaye ni mtoto mkubwa wa marehemu alikuwa akisoma nje ya nchi nchini Australia lakini walimrejesha nyumbani bila kumaliza masomo yake ili kumtumia kama mtaji wa kufuatilia mali za marehemu baba yake.

Mama huyo amedai anasikitishwa na hatua ya watoto wa marehemu wapatao wanne kutopewa haki ya mgao wa mali za marehemu baba yao kwani kwa sasa mali hizo zinawanufaisha ndugu wa uoande wa mke ambao wamejigawia kusimamia.

"Sisi kama wazazi wa marehemu tunasikitishwa sana kumtumia huyu kijana suala la mali ,kwanza wamemkatisha masomo yake na pale hotelini hana mamlaka yoyote zaidi ya kutumwa kwenye kununua vitu vya hotelini sokoni,"amesema Mama.

Hata hivyo amedai hakuna ubishi kuwa marehemu Erasto Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Agosti 7mwaka 2013. Kifo cha marehemu ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite kiliacha simanzi

Imeelezwa kuwa katika maisha yake Erasto alifanikiwa kuwa na mali mbalimbali ikiwemo vitega uchumi kadhaa magari ya kifahari,nyumba za kisasa ,mashamba makubwa ,migodi na hoteli.

Mama mzazi wa Marehemu Erasto Msuya,Ndeshu  Msuya anaeleza jinsi Mke wa marehemu Miriam Mrita jinsi alivyoweka pembeni ubinadamu na kuanza kuuza chap chap baadhi ya mali za marehemu mumewe kabla hata ya mazishi ikiwemo kuhamisha mali mbalimbali na kupeleka kusikojulikana, kubadilisha mikataba ya umiliki wa mali na  kuandika jina lake.

"Nashukuru waandishi wa habari kwa kuingilia kati jambo hili naimani nchi itaelewa ukweli .Mkuu wa Wilaya (Jerry Muro)Erasto alikuwa mtoto  wangu pekee wa kiume kwenye uzao wangu kati ya watoto saba  wakiwemo mabinti saba,mtoto wangu aliuawa Mijohoroni kila mtu anajua kwamba alipigwa risasi nyingi.

"Kilichotokea muda mfupi  baada ya kijana wangu kuuawa mke wake(Miriam) huku ndani alianza kutoa vitu vyote kwenye Selfu  zikiwemo fedha na document mbalimbali na kupeleka kusikojulikana.

"Aliondoka na kwenda kuvunja ofisi ya marehemu na kuchukua documents zote yakiwemo Madini na fedha,hamuwezi kuamini kuwa  Erasto alikuwa bilionea, mfanyabiashara wa Madini lakini hatukuona hata sample chafu ya Madini ya Tanzanite yanayomhusu Erasto labda ungesema alikuwa muuza Maandazi.

"Baada ya kuzika kijana wetu tulikaa kikao cha ukoo pale Boma,tukamuuliza Mwali(Miriam) utaolewa ama unabaki kwenye boma ,akasema atabaki kwenye boma(Nyumbani kwa Marehemu),"amesema.

Ameongeza kikao cha ukoo kilikaa na kuorozesha mali zote za marehemu kwa kuziona na kuelezwa, wakaviweka kwenye mirathi na kumwandikia Miriam, kwamba asimamie mji wako kama ambavyo mlikuwa mkiendesha mji na Mume wako.

Pia amesema baadaye kabla yakuzika wakaambiwa kuwa  baadhi ya vitu yakiwemo mabegi yamesombwa usiku wa manane na Gari aina ya Rand cruise na kupelekwa kusikojulikana.

"Ndipo tulipojua huyu mwanamke ni mpumbavu hata Bibilia inasema mwanamke mpumbavu huvunja mji wake mwenyewe uliona wapi mali zako halafu unajiibia mwenyewe ,lakini hatukutaka kumuuliza chochote.

"Baada ya kukabidhiwa kama msimamizi wa mirathi alianza mizengwe akidai ni wakati wake wa kula good time(Kula raha) ,alianza kujigawa na kukata mawasiliano na sisi ,alianza kuuza vitu ikiwemo viwanja huko Njiro ,Magari na kubadilisha majina na kuandika Miriam Stephano Mrita.

"Tulimchagua Miriam kama msimamizi wa mirathi ili akusanye na kama kuna madeni alipe na baadae agawe mali kwa watoto wake wanne na yeye mwenyewe, lakini akaona kama amechaguliwa kuwa mmiliki wa Mali na kufanya atakavyo ,"amedai.

Ameongeza fedha zilizopo kwenye akaunti mbalimbali za marehemu kwenye mabenki ,Marehemu aliacha maelezo ya maandishi  kuwa iwapo atafariki dunia wazazi wake wakiwa bado hai,asilimia 40 wagawane wazazi pamoja na Dada zangu na  asilimia 60 ibaki kwenye akaunti kwa ajili ya mke wake  na watoto.

Amesema wao kama wazazi wanaona dariri mbaya za watoto wa marehemu kukosa haki yao ndio maana wameingilia kati jambo hili na si kwa kutaka mali za Marehemu kijana wetu bali tunataka Mali ya Marehemu igawanywe kwa watoto

Kwa upande wake Bahati Msuya ambaye ni dada wa marehemu amesema kuwa wao kama ndugu wa marehemu hawana nia ya kugombea mali za marehemu kaka yao isipokuwa wanachotaka ni watoto wa marehemu wapewe haki ya kumiliki Mali za Marehemu baba yao.

Amesema mtoto wa marehemu aitwaye Glory  Msuya ambaye yupo masomoni nchini  Canada ameshindwa kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu baada ya ndugu wa mama yake wanaosimamia hoteli na miradi mingine kukataa kumlipia ada wakimtaka arejee nchini.

Awali mtoto mkubwa wa Marehemu,Kervin Msuya alilalamikia ndugu wa upande wa baba yake kutaka kumpora Mali za baba yake na kumfungua nyumba ya marehemu baba yake jambo ambalo lilimfanya akose makazi na kulala hotelini .

Hata hivyo suala hilo lilitatuliwa na Mkuu wa wilaya Jerry Muro kwa kuamuru kijana huyo nanwenzake  kurejea katika nyumba hiyo ili kuendelea na makazi .

Muro aliagiza pande zote zinazozozana kufika ofisini kwake kesho jumatatu SAA nne asubuhi  ili kufikia mwafaka wa changamoto zilizojitokeza.


TANZANIA KUNUFAIKANA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIANINFRASTRUCTURE INVESTMENT’.

$
0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika mazungumzo na Bw. Danny Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’  yaliyofayika katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC. Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.
Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) kulia, na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Mohammed Abdiwawa. Kulia kwa Mhe. Mpango ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Mashimba Ndaki na kushoto kwa Mhe.Abdiwawa ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga.


TANZANIA KUNUFAIKAcNA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIAN INFRASTRUCTURE INVESTMENT’.

$
0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika mazungumzo na Bw. Danny Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’  yaliyofayika katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC. Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.
Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) kulia, na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Mohammed Abdiwawa. Kulia kwa Mhe. Mpango ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Mashimba Ndaki na kushoto kwa Mhe.Abdiwawa ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga.


WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HALMASHURI KUHAKIKI TAASISI NDOGO ZA FEDHA KUBAINI TAASISI ZINAZOWAIBIA WANANCHI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Bi. Efrancia Kabuga kutoka Wilaya ya Kishapu mfano wa Hundi ya shilingi 50,000,000/=mkopo kutoka benki ya CRDB , ambao amefadhiliwa na Taasisi ya PASS, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ( katikati) akikata utepe kama ishara ya kuzindua Mpango mkakati wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa kipindi cha 2018/2019 mpaka 2022/2023, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na kulia ni Mwenyekiti wa NEEC, Dkt. Festus Limbu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza baadhi ya wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo(SIDO), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza baadhi ya wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo(SIDO), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza mwakilishi wa Kiwanda cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu asali inayotengeenzwa na kiwanda hicho, wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.




Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama , ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya uhikiki wa kina wa taasisi ndogo za kifedha zinazotoa mikopo kwa wananchi na vikundi, ili kuzibaini taasisi zinazowaibia Watanzania badala ya kuwanufaisha kiuchumi..

Waziri Mhagama ametoa agizo hilo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Oktoba 20, 2019.

“Ninajua baadhi ya taasisi ndogo za fedha badala ya kuwasaidia wanachama zimekuwa ziifanya kazi ya kuiba fedha za wanachama na kuwafanya wanachama warudi nyuma badala kusonga mbele, agizo hili Baraza la Taifa la Uwezesheshaji wananchi Kiuchumi mlifuatilie kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alisema Mhagama.

Katika hatua nyingine ameitaka mifuko/programu za uwezeshaji wanachi kiuchumi kutoa mikopo kwa riba nafuu tofauti na taasisi nyingine za kifedha, ambapo amebainisha kuwa takribani wajasiriamali 1,237,984 wamenufaika na mikopo ya mifuko hiyo na hadi kufikia Juni 2019 jumla shilingi bilioni 388.4 zimetolewa.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za kifedha kuhakikisha zinajibu changamoto za wananchi huku akiwataka wananchi (wajasiriamali) walioshiriki maonesho haya kutumia vema fursa walizoziona katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili wakuze uchumi wao

Baadhi ya wanufaika wa mikopo wilaya ya Bariadi na Busega mkoani Simiyu na Chato Mkoani Geita wamezishukuru Taasisi za kifedha zilizowakopesha mitaji jambo ambalo limewasaidia kuimarsisha shughui zao za kiuchumi wanazofanya ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.

“Naishukuru Benki ya AZANIA na wadhamini wangu Taasisi ya PASS kwa kuniwezesha kupata mkopo wa shilingi milioni 20, kuanzia sasa nitalima kisasa na nitaenda kuongeza miundombinu ya maji kwenye shamba langu maana nilikuwa nalima ekari 10 kwa kumwagilia badala ya ekari 30 nilizo nazo,” alisema Elisha Malugu kutoka wilayani Busega.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) Dkt. Festus Limbu amesema NEEC inaendelea kufuatilia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa Juni 2019 la kila mkoa kuwa na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi, lengo likiwa kuvifanya vituo hivyo kuwa kitovu cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’ Issa amesema Maonesho haya yameshirikisha Taasisi 45, wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya, Pwani, Mwanza, Tabora, Kagera , Mara, Singida na Dar es Salaam na kutoka nchi jirani za Burundi na Kenya.

Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii chini ya Kauli Mbiu, “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda” yametanguliwa na maonesho ya kwanza yaliyofanyika Mbeya mwaka 2017, ambapo ya pili yalifanyika mwaka 2018 jijini Dodoma.

INAKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 21,2019

TCRA YASHIRIKI KUTOA ELIMU YA MAWASILIANO MAONESHO YA VIWANDA

$
0
0
MKUU wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidhi kitabu cha mongozo wa mawasiliano kwa mwananchi aliyetembelea maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa pwani yanayofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa.
Afisa Mwandamizi wa Mitambo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki Kenneth Chitemo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TCRA katika maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Wakuu wa Taasisi wakiwa katika Kongamano la wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akiwa picha pamoja na wadhamini wa maonesho ya viwanda.

*****************

Na Mwandishi WETU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imeshiriki maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani katika utoaji wa elimu ya mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza katika maonesho hayo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa katika maonesho hayo wananchi watembelee banda la TCRA kuweza kupata elimu namna ya kutumia l simu katika kupata maendeleo ya Taifa.

Mhandisi Odiero amesema kuwa uchumi wa viwanda unakwenda na mawasiliano ya simu na kutaka wadau kutumia simu katika biashara zao kwa kutangaza biasha kwa kutumia simu hizo.

Aidha amesema TCRA iko katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kujisajili kwa laini za simu kwa lama za vidole kwa muda uliopangwa na usajili huo utafungwa Desemba 31 mwaka huu.

“Tunataka wananchi wajisajili simu zao kwa alama za vidole kwa muda uliopangwa na wasije wakapata usumbufu wakati zoezi hilo likiwa limefungwa kwa laini za simu kutopata mawasiliano.amsesema Mhandisi Odiero.

Mhandisi Odiero amesema kuwa Kanda ya Mashariki ya TCRA itapita Wilaya zote zilizo katika kanda hiyo katika kutoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja na huduma nyinginezo za bidhaa za mawasiliano.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi waepuke kufanya maawsiliano na watu wasiowajua kwa kuwaomaba fedha ni mpaka pale watakapojiridhisha na katika mawasiliano kwani baadhi yao wanafanya utapeli.

JAMII YASHAURIWA KUONDOKANA NA MILA POTOFU ZA KUAMINI KWAMBA CHANJO HUSABABISHA MADHARA KWA WATOTO

$
0
0
Na, Jumbe Ismailly IKUNGI 

JAMII imeshauriwa kuondokana na mila potofu na zilizopitwa na wakati za kuamini kuwa endapo mtoto akipatiwa chanjo ya ugonjwa wa Surua Rubela na Polio upo uwezekano wa kupata madhara katika siku za baadaye na haitaweza kumkinga na magonjwa yatakayomkabili.

Akiongea wakati wa Uzinduzi wa kampeni za chanjo ya kuzuia magonjwa ya Surua,Rubela na Polio uliofanyika kwenye Kituo cha Afya cha Ikungi,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Huduma za jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Abeli Richard Sui alisisitiza kwamba ni wakati muafaka kwa wataalamu wa Afya kwa kushirikiana na wanasiasa kwenda kuwahamasisha wananchi kwa kuwapatia elimnu sahihi ili waweze kuondokana na dhana hiyo potofu.

“Yapo mambo ambayo yapo katika jamii ambayo kwa umoja wetu sisi kama alivyosema mheshimiwa mgeni rasmi twende tuiathiri jamii kufahamu umuhimu wa hiki kwamba jamii kule wanaona mtoto akichanjwa pengine anaweza akapata madhara pale baadaye na wala si kwamba inamkinga na maradhi yatakayomkabili.”alisisitiza mwenyekiti huyo wa kamati.

Kwa mujibu wa Sui dhana hiyo ni potofu ambayo kwa umoja wao wanapaswa kuikemea ikiwa ni sambamba na kutoa elimu sahihi ili wananchi wa wilaya hiyo waweze kuelewa kikamilifu pamoja na kuondokana na dhana hiyo inayokwamisha kupeleka watoto kwenye chanjo hizo.

“Kwa hiyo twende kusambaza ujumbe huu,lakini mgeni rasmi tukuombe kwa wakati mwingine endelea kushiriki nasi kwani suala la huduma za jamii ni pana na lina mambo mengi kama nilivyotangulia kusema kwamba ili tufike mahali sasa huduma hizi zimfikie mlengwa kwa karibu ni lazima tuongeze vituo vya kutolea huduma.”aliweka bayana Mwenyekiti.

Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya,Honest Nyaki alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi na walezi wa watoto wenye sifa za kupatiwa chanjo ya magonjwa ya surua rubella na polio wawapeleke watoto wao kupatiwa chanjo.

Aidha Mwakilishi huyo alibainisha kwamba mzazi au mlezi yeyote yule ambaye hataweza kumpeleka mtoto wake kupatiwa chanjo atahesabika kufanya vitendo vya hujuma kwa watoto wao ambapo alitoa mfano wa hujuma hizo kuwa ni pamoja na kushindwa kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo inayoendelea kutolewa nchi nzima.

Akizindua kampeni ya chanjo hiyo ya Surua Rubela na Polio,Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Edward Mpogoro aliwapongeza wazazi pamoja na walezi wote waliojitokeza na kupeleka watoto wao kupata chanjo kwa kile alichodai kwamba wanatekeleza sera za Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Akitoa taarifa fupi ya maandalizi ya chanjo ya magonjwa hayo,Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Godeliva Mutasa aliweka bayana kwamba Halmashauri hiyo inatarajia kuchanja jumla ya watoto 48,245 kwa chanjo ya Surua Rubela na Polio na jumla ya watoto 23,833 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya polio.

“Magonjwa haya yanasababisha ulemavu,upofu pamoja na vifo kwa watoto kinga yake ni chanjo kabla ya mtoto hajaugua na tunategemea kutoa chanjo ya Surua Rubela kwa watoto wote walio katika umri wa miezi tisa mpaka miaka minne na miezi 11.”alifafanua Mratibu huyo.

Wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida inatarajia kutoa chanjo ya Surua Rubela kwa watoto 48,245 wenye umri wa kati ya miezi 9 mpaka miaka 4 na miezi 11 wakati zaidi ya watoto 23,000 wenye umri wa mwaka mmoja na nusu mpaka miaka mitatu na nusu watapatiwa chanjo ya Polio.
 baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye sifa za kupatiwa chanjo ya Surua Rubela na Polio wakiwa kwenye Kituo cha Afya cha Mji mdogo wa Ikungi wakishuhudia uzinduzi wa Kampeni ya chanjo ya Surua Rubela na Polio.


Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye sifa za kupatiwa chanjo ya Surua Rubela na Polio wakiwa kwenye Kituo cha Afya cha Mji mdogo wa Ikungi wakishuhudia uzinduzi wa Kampeni ya chanjo ya Surua Rubela na Polio.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Bwa.Edward Mpogoro akizindua kampeni ya chanjo ya Surua Rubela pamoja na Polio uliofanyika katika kituo cha afya cha Mji mdogo wa Ikungi.

KUMEKUCHA MKUTANO WA SADC WA MAZINGIRA MALIASILI NA UTALII JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkutano wa SADC ambao unaendelea umebeba madhumuni ya kuangalia mwenendo mzima wa hali ya mazingira na mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni pamoja na kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi ya usimamizi wa mazingira

Mkutano huo leo utaingia hatua ya pili ya makatibu wakuu baada ya wataalamu kumaliza ngwe yao jana na utafunguliwa na Waziri mwenye dhamana ya utalii Dkt.Khamis Kigwangalah kwenye Kituo cha mikutano ya Kimataifa AICC  jijini hapa

TBS Yaondoa Sokoni Vipodozi Vyenye Viambata Sumu

$
0
0
Maofisa wa Shirika La Viwango Tanzania (TBS) wakichambua vipodozi vyenye viambata sumu wakati walipofanya ukaguzi wa kushtukiza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Vipodozi hivyo vimepigwa marufuku kutokana na kuwa na madhara kwa watumiaji.

Na Mwandishi Wetu 
AINA mbalimbali za vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu vimeondolewa sokoni na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza jijini Dar es Salaam.

Maofisa shirika hilo walifanya ukaguzi huo mwishoni mwa wiki kwenye maduka mbalimbali yaliyopo Kariakoo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi huo,Mkaguzi Mwandamizi wa Shirika hilo,Mhandisi Donald Manyama, alisema wauzaji wa vipodozi hivyo wameonesha ushirikiano wa kutosha,kwani wamevitoa kwa kadri ambavyo walielekezwa.

Alipoulizwa kama kuingia nchini kwa vipodozi hivyo, kunachangiwa na kutokuwepo udhibiti wa kutosha mipakani,Mhandisi Manyama, alisema udhibiti upo wa kutosha,lakini vitu ambavyo vimepigwa marufuku nchini vinaingia kwa njia ambazo sio halali.

Alisema waingizaji wamekuwa wakitumia njia za panya kuingiza vipodozi hivyo. Alisema vipodozi walivyovikamata wamevichukua kwa ajili ya kwenda kuviharibu.

"Zoezi hili sio kwamba litaishia hapa (Dar es Salaam) baada ya kumaliza hapa tutaendelea na ratiba yetu mikoani kuondoa vipodozi hivi," alisema Mhandisi Manyama.

Alipoulizwa madhara ya vipodozi hivyo vyenye viambata sumu kwa matumizi ya binadamu,Manyama alisema vina madhara kwenye ngozi ya binadamu.

"Kwanza vinaichubua hiyo ngozi na kuifanya kuwa laini kiasi kwamba mtumiaji akifanyiwa operesheni ushonaji wake unakuwa ni mgumu," alisema na kuongeza;

"Vingine vinasababisha saratani ya ngozi, kupunguza kinga ya ngozi na kuathiri mfumo wa homoni za mwili. Hivyo tunawashauri hata watumiaji kuacha kutumia vipodozi hivyo. Wengine wanavitumia bila kufahamu, wakiona mwenzao amebadilika ngozi,wanadhani havina madhara.

Alisema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waache kutumia vipodozi hivyo.Alitoa wito kwa wasambazaji wa vipodozi hivyo kuacha, kwani wakikamatwa watawasababishia mitaji yao kupotea na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.

Lakini pia alitoa wito kwa watumiaji kuacha kuvitumia kwa sababu ni hatari kwa afya zao. Baadhi ya vipodozi vilivyokamatwa kwenye ukaguzi huo na kuondolewa sokoni ni Carolight,Movate,Coco Pulp, Diproson,Viva White, Carotone, Bronz na Eclair.

Vingine ni Citrolight, Tent Clear, Tender White, Clinic Clear, TCD, Baby Face,Light up,Dermotyl na Top Lemon. Mmoja wa wauzaji wa vipodozi hivyo, Rose Joseph, alishauri udhibiti uimarishwe zaidi mipakani,kwani kama vitaendelea kupatikana vitazidi kupata soko.

Aliipongeza TBS kwa kuendelea kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye masoko, kwani hatua hiyo inawasaidia kujua aina ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kuwa na viambata sumu.

TPDC KUUNGANISHA GESI ASILIA KATIKA NYUMBA 400 MWAKA HUU

$
0
0

Mtaalamu mwandamizi wa masuala ya Petroli(Geologist) kutoka TPDC Simon Zablon.


Mwamvua Mwinyi, Pwani
SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) linatarajia kuunganisha nyumba 400 kupitia mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ,ambapo kati ya nyumba hizo nyumba125 zitakuwa mkoa wa Mtwara na nyingine mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha mpaka sasa viwanda 45 vinafanya uzalishaji kwa kutumia gesi inayosambazwa na TPDC na miongoni mwa viwanda hivyo ni DANGOTE kilichopo mkoani Mtwara na Goodwill kilichopo Mkiu wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani.

Mtaalamu mwandamizi wa masuala ya Petroli(Geologist)kutoka TPDC Simon Zablon,alisema hayo katika maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani Mjini Kibaha.

Alisema, nyumba hizo zinatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu.

Zabron alisema,katika upande wa viwanda ambavyo vitanufaika na mradi huo ni kiwanda cha Lodhia, NAF na Cokacola .

"TPDC tupo tayari kutoa huduma ya gesi kwa urahisi kwenye viwanda vyote vilivyopo katika Mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na ambavyo miundombinu ya bomba la gesi imepita"

Katika hatua nyingine, alifafanua magari yanayotumia gesi hadi sasa yamefikia 200, na kwamba magari yanayounganishwa na huduma hiyo ni yale yaliyokuwa kwenye mfumo wa kutumia petroli.

Alisema, awali mradi wa kuunganisha gesi kwenye magari ulianza miaka saba iliyopita lakini ulikuwa unasuasua kutokana muamko kwenye vituo vya mafuta kuwa mdogo.

Zabron alielezea pia kumetokana na kituo kimoja kilichokuwa Ubungo jijini Dar es salam pekee kutoa huduma hiyo tofauti na hali ilivyo sasa.

TFF YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU UCHAGUZI MDOGO

$
0
0


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWITIKIO mdogo kwa wanaochukua na kurudisha fomu za uchaguzi mdogo wa bodi ya ligi Tanzania (TPLB) umepelekea kamati ya uchaguzi ya mpira wa miguu nchini (TFF) kupitia kikao kilichofanyika Oktoba 19,2019 kuongeza siku za kuendeleza zoezi hilo.

kupitia taarifa ilitotolewa na Afisa haari na Mawasiliano wa shirikisho la mpira nchini (TFF) Cliford Mario Ndimbo imeeleza kuwa zoezi hilo la kuchukua na kurejesha fomu litaanza leo Oktoba 21 na kuhitimishwa Oktoba 23, 2019 saa kumi jioni.

Ndimbo ameeleza kuwa maamuzi hayo yamezingatia kanuni 10 (6) ya kanuni za uchaguzi TFF toleo la 2013.

MAKAMPUNI YA KOKOTO CHALINZE YALIA NA USHURU WA SH. 60,000 KWA LORI-MODEST

$
0
0


Mwamvua Mwinyi, Pwani
KAMPUNI ya uchimbaji wa mawe na kusaga kokoto ya Gulf Aggregates(T), Lugoba imeitaka halmashauri ya Chalinze na serikali kuangalia uwezekano wa kuwashirikisha wawekezaji, kabla ya kufanya mabadiliko ama kuwapandishia ushuru.

Aidha imeiomba halmashauri ya Chalinze, kuboresha miundombinu ya barabara ambayo imekuwa changamoto hususani kipindi cha mvua huku barabara hiyo ikiwa tegemeo la magari ya kokoto zaidi ya 500 yapitayo njia hiyo kila siku.

Akielezea changamoto wanazokabiliana nazo wakati akizungumza na waandishi wa habari ,katika maonyesho ya viwanda yanayoendelea mkoani Pwani, ofisa muajiri wa kampuni hiyo,Agustine Modest alisema,kwasasa halmashauri hiyo imepandisha ushuru kutoka sh.20,000 hadi 60,000 kwa lori kiasi ambacho ni kikubwa kwao .

"Ushuru huu ni mkubwa kwa mwekezaji lakini pia unatuumiza kwani lazima gharama ya kuuza itapanda, tunaomba ushuru upunguzwe hadi sh.30,000 aliomba.

Modest alisema,ushirikishwaji ni muhimu kwakuwa wamekuwa wakipandishiwa ushuru tofauti na faida wanayoipata hivyo kupata hasara.

Nae Ramadhani Siasa ambaye ni meneja masoko wa Lake Gas alieleza, pia wanatarajia kuanza uzalishaji wa mitungi ya gesi ambapo maandalizi yanatarajia kukamilika mwezi desemba mwaka huu.

"Lake gas itakuwa ya kwanza kwa uzalishaji wa mitungi hiyo hapa nchini ambapo awali mitungi yote ilikuwa ikiagizwa kutoka nje ya nchi"alieleza Siasa.

Gulf Aggregates ni kati ya makampuni yanayomilikiwa na Lake Group, makampuni mengine ni Lake gas, Lake Oil, Lake Trans ,Lake petrolium,Lake steel na Lake Cylinders.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>