Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Vodacom yatoa msaada wa kompyuta zilizounganishwa na intaneti kwa shule 14 wilayani Urambo, kukuza elimu ya kidigitali

$
0
0

· Yaonyesha njia katika maendeleo ya teknolojia ya Kidijitali kupitia mfumo wa e-learning

· Zaidi ya wanafunzi 7,000 kunufaika na msaada huo.

Oktoba 19, 2019 Urambo. Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania Plc, kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation leo imetoa msaada wa kompyuta na Kipanga njia (Router) vilivyounganishwa katika intaneti kwa shule 14 za Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora. Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi 67,634,000 ni sehemu ya mpango endelevu wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu katika sekta ya elimu.

Hii ni sehemu ya ushirikiano wa Vodacom na mfuko wa pamoja wa huduma za Mawasiliano (UCSAF) wa kutoa elimu shuleni kwa kutumia miundombinu bora ya teknolojia ya mawasiliano ya Vodacom kote nchini . Kupitia ushirikiano huo, jumla ya shule 300 na hasa zilizoko vijijini zitapata kompyuta zilizounganishwa katika intaneti bure.

Akipokea msaada huo, katika shule ya Sekondari Urambo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe, alisema msaada huo wa kompyuta ni hatua muhimu kuelekea mchakato wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya kidijitali.

“Maendeleo ya kuelekea kwenye matumizi ya dijitali yanaonesha kuwapo mafanikio kutokana na uwepo wa kompyuta kama hizi katika shule zetu sambamba na kasi ya matumizi ya simu za mkononi nchini,” alisema Waziri Kamwelwe.

“Shule ni mahala pazuri pa kuanzia kufundisha matumizi ya kompyuta katika maisha ya kila siku. Kompyuta zikiwa shuleni hazitatumika kwa wanafunzi pekee kujifunza matumizi yake, lakini pia walimu kutumia kompyuta hizi kupata ujuzi zaidi na kuboresha uwezo wao wa kufundisha. Walimu pia watatumia muda huo kuboresha ujuzi wao ili kwenda sambamba na ulimwengu wa kidijitali na kupata maarifa Zaidi,” aliongeza Mh Kamwelwe.

“Tunaamini kwamba kompyuta hizi ni hatua nyingine katika mchakato wa mabadiliko ya kidijitali. Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa msaada wao mzuri,” alisema Kamwelwe.

Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, bi Rosalynn Mworia, alisema msaada huo ni sehemu ya ajenda ya Vodacom Foundation yenye lengo la kusaidia sekta ya elimu ili kutoa elimu bora na kuhakikisha wanafikia malengo ya millenia na ajenda ya kitaifa kama sehemu ya mradi wa shughuli za kijamii.

“Fursa za kidijitali ni nishati muhimu katika uchumi unaokua, zina matokeo ya haraka katika uchumi na jamii kwa ujumla. Kwa pamoja zinachangia ukuaji wa uchumi, kuongeza mianya ya ajira pia ina mchango mkubwa katika kupunguza umasikini, huku ikitoa mwanya katika kuchochea ukuaji wa sekta muhimu kama vile elimu na afya,” alisema bi Mworia.

“Vodacom imeamua kuweka nguvu katika maendeleo kidigitali Tanzania. Ndiyo maana tunajivunia kutoa msaada huu leo ambao unajumuisha kompyuta, rota vyote vikiunganishwa katika mtandao vikiwa na thamani za zaidi ya shilingi milioni 67 katika shule 14 wilayani Urambo ambayo inategemea kuwafikia zaidi ya wanafunzi 7,000,” alisema Mworia.

“Vodacom imejikita zaidi katika kukuza maendeleo ya kidijitali, mawasiliano na ubunifu nchini. Tunataka kuwasaidia wanafunzi ili waende sambamba na zama hizi za kidijitali tulizomo kwa sasa na kuwashawishi zaidi kutokuwa watumiaji tu, bali kushiriki kikamilifu katika fursa za kidijitali. Tukio la leo ni mwendelezo wa utoaji wa Kompyuta chini ya ushirikiano wa Vodacom Tanzania Foundation na UCSAF kwa shule za Tanzania Bara na Visiwani,” alisema Mworia

Wiki iliyopita, Vodacom ilitoa kompyuta na router zilizounganishwa na intaneti yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 48 kwa shule 10 Mkoani Simiyu.

Kompyuta hizi zitawezesha shule hizo kupata taarifa mbalimbali za elimu kutoka katika mfumo wa kidijitali kupitia katika muundo wa foundation yetu na hivyo kuhamasisha usomaji wa kidijitali.

Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo ya teknolojia shuleni kupitia mpango wa Instant Schools, ambapo imetoa kompyuta mpakato na za kawaida 75 katika wa shule za sekondari za Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja na Kinyerezi.
 
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia akimuelekeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe jinsi mfumo wa Instant Schools  unavyofanya kazi, Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi kompyuta mpakato, router na kuunganisha intaneti yenye tahamani ya Shilingi 67m kwa shule 24 wilayani Urambo.
 

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA MAMLAKA YA MASOKO YA MITAJI NA DHAMANA PAMOJA NA SOKO LA HISA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
 Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Moremi Marwa akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Soko hilo.  
 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wakati Kamati hiyo ilipokutana na Watendaji wa Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
Meneja katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Emmanuel Nyalali akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti jinsi soko hilo linavyofanya kazi Jijini Dar es Salaam. PICHA NA BUNGE

KAMPENI YA KIJANA SMART YAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
      Na Khadija seif, Michuzi TV

MSANII wa Bongo fleva Kala Jeremiah amezindua kampeni ya kijana smart jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo Kala amesema wasanii wanatakiwa kusaidia jamii inayowazunguka kwa vitendo na kuwaandaa vijana kiakili.

Aidha, Kala ameeleza lengo la kampeni hiyo kuamsha ari, hamasa kwa vijana ili kujitambua, kutambua  majukumu yao, nafasi yao uwezo na umuhimu wao katika mstakabali wa kupata jamii bora itakayoleta matokeo chanya katika mambo yote muhimu ya kijamii na kiuchumi.

"Tunaamini vijana wakijikwamua kiuchumi jamii nzima inaelewa kwa kuwa kijana ni nguzo muhimu katika jamii na taifa kwa ujumla,"

Pia amebainisha kanuni za kijana smart  ni pamoja na kuhakikisha anapambana kwa nguvu na akili zake zote,  kuhakikisha anapinga kwa vitendo vya mimba na ndoa za utotoni na kushiriki kikamilifu kwenye maswala ya usawa wa kijinsia pamoja na kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele katika vita vya kupamabana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Hata hivyo kampeni hiyo ipo chini ya shirika lisilo la kiserikali linaloitwa wana ndoto kwa kushirikiana na wadau wengine.

"Wana ndoto ni shirika changa na jipya na tutatumia njia mbalimbali ya uhamasishaji kwa vijana kupitia video kuhakikisha kijana smart imekuwa ni maisha ya kila siku ya kijana,vyombo vya habari  mitandao ya kijamii vyuo na mashule nyimbo matamasha na makongamano.

Pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono katika kuhakikisha vijana wanatimiza malengo yao na tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

HUDUMA YA MAJI KEREGE HADI AMANI BAGAMOYO KUREJEA LEO USIKU

$
0
0
MAMLAKA ya majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewahakikishia wananchi waishio maeneo ya Kerege hadi Amani, Bagamoyo kuwa jitihada za kurejesha huduma za maji zipo katika hatua za mwisho kabisa ambapo usiku wa leo kazi hiyo inatarajia kumalizika.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo iliyotolewa leo Oktoba 21, imeeleza kuwa kasi ya urekebishaji wa bomba hili imechukua muda kuliko ilivyotarajiwa kufuatia kuendelea kuwepo kwa maji mengi katika mto Mpiji.

Imeelezwa kuwa  maeneo ya Kerege, Mapinga, Kiharaka, Kiembeni, Mingoi, Kimelela, Vikawe na Amani yamekosa maji tangu Oktoba 19 siku ya Jumamosi kufuatia kukatika kwa bomba kuu la inchi 54 linalosafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini hali iliyosababishwa na uchimbaji holela wa mchanga katika mto Mpiji.

EBITOKE, LINAH NDANI YA DREAM DESTINATION KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Na Khadija Seif, Michuzi TV
KAMPUNI ya startimes imeletea rasmi kipindi cha television chenye maudhui ya kitalii kinachotarajiwa kuruka chaneli ya ST swahili pamoja na chaneli ya Tanzania Safari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malisa amesema,  kipindi hicho kinatarajiwa kuwa na watangazaji nyota kutoka nchi ya Kenya pamoja na Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Rogers Mugisha.

"Wote wataonesha na kukueleza vivutio mbalimbali vipatikanavyo nchini Tanzania na barani Afrika ikiwemo maziwa makuu, nyota hao wataongoza katika kipindi cha Dream destination kujionea fahari ya Afrika kwa ujumla," amesema.

Pia amefafanua kuwa ndani ya kipindi cha dream destination kitaonesha wasanii wawili ebitoke pamoja na linah wakiwa katika harakati za kutembelea vivutio.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa television ya Tanzania Safari Gabriel Nderuma amesema, ni wakati wa wakuangalia maudhui yenye kujenga na kufumbua bongo za watazamaji kwa vipindi vizuri hasa vya kitalii.

"Tanzania Safari imekua ikirusha vipindi vya wanyama, maporomoko ya maji pamoja na misitu iliyopo afrika ila kwa sasa tumeweza kuongeza kipindi kingine cha dream destination kitakachoruka octoba 26 mwaka huu,"

Hata hivyo Nderuma ameeleza lengo la kuandaa vipindi vya maudhui ya utalii ni kusaidia serikali kutangaza vivutio vilivopo nchini ili kuongeza pato la taifa kwa kupitia watalii wanaokuja nchini.
Meneja wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio mpya wa kipindi cha dream destination chenye maudhui ya kitalii kinachotarajiwa kuruka katika chaneli ya ST Swahili pamoja na Tanzania Safari leo  jijini Dar es Salaam.

YANGA IKO TAYARI KUWAVAA MBAO FC KESHO CCM KIRUMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao Fc, Timu ya Yanga  imeendelea kuimarika kwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo utakaochezwa kesho Jijini Mwanza.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo Yanga wana kumbukumbu ya kuondoka na ushindi wa 2-1 kwenye Uwanja huo kwa magoli ya Heritier Makambo Amisi Tambwe.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga Hassan Bumbuli na kusema kuwa wachezaji waliokuwa timu ya Taifa, Abdulaziz Makame na Metacha Mnata pamoja na Issa Bigirimana aliyekuwa mgonjwa  tayari wamejiunga na kikosi chao Mwanza.

Kwa upande wa Kocha Zahera, amesema, baada ya mazoezi ya siku mbili vijana wake wako tayari kwa mchezo huo utakaokuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia za timu kwenye mechi zilzizopita.

"Kwa kawaida naiandaa timu kwa ajili ya mchezo uliokuwa mbele yangu, hadi sasa naona timu iko vizuri sana na iko tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao FC. Tunawaheshimu Mbao ni timu nzuri, lakini na sisi ni wazuri pia na tumejiandaa kwa ushindi," amesema Mwinyi Zahera.

Daktari wa Timu ya Yanga, Shecky Mgazija amesema wachezaji wote wa Yanga wako kwenye hali nzuri na utimamu wa mchezo hivyo ji jukumu la kocha tu kuwatumia katika mchezo dhidi ya Mbao kesho.

Kuhusu hali ya beki wa kulia wa timu hiyo Paul Godfrey 'Boxer',  Dr. Mgazija amesema beki huyo anaendele vizuri na ataweza kuwa fiti kutumika katika mchezo dhidi ya Pyramids kama Mwalimu ataridhika na hali ya mazoezi yake.

"Kimsingi Boxer amepona, lakini hawezi kuingia moja kwa moja kikosini, hivyo anaendelea na mazoezi na ninamaamini baada ya kesho atajuika na wezake tayari kwa mchezo wa Pyramids kama atakuwa ameshaiva kwenye programu za kocha," amesema Mgazija.

Aidha amesema majeruhi mwengine Mohammed Issa Banka na Cleofas  Sospeter  bado hajajiunga na timu lakini matibabu yake yanaendelea vizuri na huenda akajiunga na wenzake baada ya timu kurejea kutoka Misri.

Wachezaji walipo kambini jijini Mwanza ni pamoja na Papy Tshishimbi, David Molinga, Deus Kaseke, Ramadhan Kabwili, Faouk Shikalo, Sadney Urikhob, Juma Balinya, Mrisho Ngassa, Ally Mtoni Sonso, Muharami Issa Marcelo, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Feisal Salum, Ally Ally, Jafari Mohammed, Gustafa Simon, Lamine Moro, Said Juma Makapu, Raphael Daudi, Maybin Kalengo, Mapinduzi Balama, Patrick Sibomana, Mustafa Seleman na Paul Godfrey.

Dar, Dodoma vinara wa mapato, Viongozi Kigoma watakiwa kujitathimini

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

JIJI la Dodoma limetajwa kuongoza katika kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 13.0 huku Jiji la Mbeya likiwa la mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya Shilingi Bilioni 2.7.

Takwimu hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo wakati akitoa taarifa ya mapato ya vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka ya mwezi Julai hadi Septemba.

Waziri Jafo pia ameipongeza pia Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuwa imekua ya kwanza Kitaifa kwa kukusanya mapato kwa asilimia 52 huku Halmashauri ya Kyerwa ya mkoani Kagera ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya kwa asilimia tatu ya makisio yake.

Katika kuzipima halmashauri zote kwa pamoja katika kipindi hiki imeonesha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko halmashauri zote kwa kukusanya Bilioni 13.10 na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ikishika mkia kwa kukusanya Shilingi Milioni 35.15.

" Kuna halmashauri ambazo kwa upande wa asilimia tumesema Msalala imekua ya kwanza lakini ukiangalia lile pato ghafi Jiji la Dodoma limeonekana ndio la kwanza ikifuatiwa na Manispaa ya Ilala ambayo imekusanya Bilioni 13.0.

Hawa Buhigwe wa mkoani Kigoma wamekusanya Shilingi Milioni 35 tu kwa kipindi chote hiki cha miezi mitatu, sasa taarifa za kimkoa zinaonesha Mkoa wa Rukwa umekua wa kwanza kwa kukusanya pato la ndani kwa asilimia 31, wakati Mtwara umekua wa mwisho kwa asilimia kwa kukusanya asilimia 13 ya mapato yake ya ndani," Amesema Mhe Jafo.

Kwa upande wa mapato ya ndani ya halmashauri kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato, Mhe Jafo amesema Mkoa wa Dar es Salaam ndio ulioongoza kwa kukusanya Shilingi Bilioni 39.5 na Mkoa wa mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Kigoma ambao umekusanya Shilingi Bilioni 2.1 katika kipindi hicho.

" Kwahiyo Mkoa wa Kigoma na halmashauri zake zote miezi mitatu wamekusanya Shilingi Bilioni mbili wakati kule Jiji la Dodoma nimezungumza wamekumapatoShilingi Bilioni 13 hawa Kigoma mkoa mzima. Kwahiyo kwa pato ghafi hawa Kigoma wameonekana ni wachovu kuliko wote hivyo niwatake wajitathimini ili waweze kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato," Amesema Jafo.

Kwa upande wa Halmashauri za Majiji kwa kigezo cha asilimia, Jiji la Dar es Salaam limeongoza kundi hili kwa kukusanya asilimia 38 ya makisio yake ya mwaka na Jiji la Dodoma limekua la mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 18 ya makisio yake.

Akizungumzia ukusanyaji wa mapato kwa Manispaa, Waziri Jafo ameitaja Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuwa kinara kwa kukusanya asilimia 42 ya makisio yake huku Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ikishika mkia kwa kukusanya asilimia Tisa ya makisio yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

" Nimpongeze sana Mkurugenzi wa Sumbawanga ndugu yangu Jacob kwa kazi kubwa anayofanya toka ateuliwe, toka tumtoe Nzega amefanya maboresha makubwa Sumbawanga na leo tunaona wanafanya vizuri kwenye mapato. Kwa Kigoma Ujiji nirudie tena wanapaswa kubadilika wamekua wamwisho kwenye mapato kila kona hii ni aibu kwao," Amesema Waziri Jafo.

Ametumia nafasi hiyo kuwaonya wakurugenzi ambao hawatumii ipasavyo nafasi zao kusimamia ukusanyaji wa mapato na kueleza kuwa wanapaswa kuangalia mabadiliko yaliyofanywa na Rais Magufuli katika nafasi za Ukurugenzi kama sehemu ya wao kujitathimini kwenye nafasi wanazohudumu.

" Wale ambao wanashindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato tunawaweka katika taa nyekundu tunapigia mstari kwa kuwa wako kwenye taa nyekundu hata wenzao walikuwa kwenye taa nyekundu na walishaondoka tukaleta watu wapya, kumbukeni juzijuzi Mhe Rais alifanya mabadiliko ya baadhi ya wakurugenzi hivyo kwa wale ambao wanasuasua kwenye utendaji wao wajitathimini," Amesema Jafo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri kwa kipindi cha robo mwaka.

AZAM FC YAMRUDISHA ARISTICA CIOABA CHAMAZI COMPLEX

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Timu ya Azam FC imemtangaza Kocha aliyewahi kukinoa kikosi cha matajiri hao wa Chamazi,  Aristica Cioaba kuja kuchukua mikoba ya Etienne Ndayiragije.

Cioaba aliwahi kuifundisha kikosi hicho kabla ya kitimuliwa ila amerejea tena na kupewa mkataba wa mwaka mmoja.

Kocha huyo  anachukua mikoba ya aliyekuwa Kocha wa Azam, Etienne Ndayiragije, ambaye anatarajia kutangazwa kama Kocha Mkuu wa kudumu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.

Kocha huyo raia wa Romania, aliyewahi kuinoa Azam FC misimu miwili iliyopita, ataanza majukumu yake mara moja tutakapokamilisha taratibu za vibali vyake vya kufanya kazi nchini.

Aidha, kama ilivyokuwa awali Cioaba, mwenye leseni ya juu ya ukocha ya UEFA Pro Licence, amerejea sambamba na Kocha wa viungo, Costel Birsan, aliyekuwa naye awali kipindi anaifundisha Azam FC.

Mara baada ya kuingia mkataba rasmi mapema leo Jumatatu, Cioaba ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi na uongozi mzima wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani naye.

 "Naushukuru uongozi wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani na mimi, kikubwa mimi sio mgeni hapa naijua timu, wachezaji wananijua na pia wanafahamu falsafa yangu, jambo kubwa ni kuendelea kuifanya timu kuwa juu pamoja na kushinda mataji," amesema.

Ndayiragije anaenda timu ya Taifa, baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC kuridhia ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanaomuhitaji awe kocha mkuu wa kudumu baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi hicho akiwa kocha wa muda.

Azam FC tunamtakia kila la kheri, Ndayiragije katika majukumu yake mapya akiwa Taif Stars, ambapo tutakuwa naye sambamba pale atakapohitaji kutoka kwetu msaada kwenye masuala yake kiufundi.
 Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akiwa sambamba na mtangulizi wake, Etienne Ndayiragije, anayekwenda kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'. Wawili hao wamekutana makao makuu ya Azam FC (Azam Complex) wakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', kukabidhiana kijiti, ikiwemo Ndayiragije kuwaaga wachezaji na kwenda kwenye majukumu yake mapya ya timu ya Taifa.
 Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akitia saini mkataba wa mwaka mmoja wa kukinoa kikosi hicho akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'
Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akitia akibidhiana mkataba wa mwaka mmoja wa kukinoa kikosi hicho akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'



Wakenya wang'ara Rock City Marathon 2019

$
0
0
  Wakati msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon ukihitimishwa kwa kushirikisha mamia ya wanariadha kutoka ndani ya nje ya nchi, Serikali imesema ipo haja ya kufanya tathmini ili kupima mchango wa mbio za aina hiyo katika kuinua sekta ya utalii hapa nchini ili iweze kuwekeza nguvu zaidi katika kuziboresha.

Akizungumza wakati wa kilele cha mbio hizo zilizofanyika kwenye viunga vya jengo la Biashara la Rock City Mall ambapo ilishuhudiwa wakimbiaji kutoka nchini Kenya wakiendelea kutamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla alisema wingi wa wawashiriki kutoka ndani na nje ya nchini ni kiashilio tosha kuwa mbio hizo zikitumika vizuri kutangaza utalii zitachochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu kiuchumi.

“Nimeshuhudia mamia ya washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamekuja kushiriki mbio hizi,tayari hiyo ni sehemu ya utalii wa ndani. Zaidi imeshuhudiwa ushiriki wa wenzetu kutoka nje ya nchini ikiwemo Kenya,Rwanda na wengine nje ya bara la Africa nao wamekuja.’’

“Ili kupata mchango hasa wa mbio kama hizi kwenye sekta ya Utalii na ukuaji wa uchumi naagiza ufanyike utafiti wa kisayansi ili Serikali tujue namna ya kuziunga mkono ziendelee kufanya vizuri zaidi,’’ aliagiza Dr Kigwangalla ambae pia alishiriki kukimbia mbio za Km 21.

Tangu kuanzishwa kwa mbio miaka 10 iliyopita zimekuwa zikivutia zaidi washiriki kutoka mataifa ya Kenya na Rwanda ambapo ilishuhudiwa Mwanariadha Kutoka Kenya Ibrahimu Too akiibuka mshindi wa mbio za km 42 upande wa wanaume baada ya kutumia muda wa 2:18:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Willium Koskei na John Muthui waliotumia muda wa 2:19:06 na 2:21:30 kila mmoja.Mtanzania pekee kwenye kumi bora wanaume alikuwa Hamis Athumani aliefanikiwa kushika nafasi ya nne huku akitumia muda wa 2:21:36

Kwa upande wa wanawake katika mbio hizo za km 42 ilishuhudiwa mwanariadha Elilither Tamui kutoka Kenya akiibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 2:42:50 akifutiwa na wakenya wenzake Joan Rotich (2:46:07) na Lydia Wafula (2:48:57) ambapo Watanzania Fabiola John na Zainabu Hamis walifanikiwa kushika nafasi ya 6 na nafasi ya 10.

Katika mbio za Km 21 mshindi wa kwanza upande wa wanaume ni Bernard Musau kutoka Kenya alietumia muda wa 01:11:26 akifuatiwa na Ochieng Julius kutoka Uganda alitumia muda wa 01:11:36 huku mshindi wa tatu akiwa ni Alex Nizemana kutoka Rwanda alitumia muda wa01:12: 21

Kwa upande wanawake katika mbio hizo za km 21 mshindi wa kwanza hadi wa nne wote ni kutoka Kenya ambao ni Ester Kakuri alietumia muda wa 1:21:44 , Vane Nyaboke (1:22:13), Ronah Nyabochoa (1:23:10) na Martha Njoroge(1:23:17) huku mshindi wa tano ni Grace Jackson kutoka Tanzania alietumia muda wa 1:24:23

Akizungumzia matokeo hayo Mshauri wa Masuala ya Ufundi wa Mbio hizo Bw John Bayo pamoja na kuwapongeza wanariadha kutoka Kenya kwa kufanya vizuri alisema kuwa Tanzania haikupata ushiriki wa wanariadha wakubwa kutokana na wengi wao kushiriki kwenye mbio za kimataifa na hivyo kutoa mwanya kwa wanariadha hususani wa Kenya kuweza kutamba kwenye mbio hizo.

Mbio hizo zilipambwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau mbalimbali wa utalii pamoja na wadhamini wa mbio hizo ikiwemo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) sambamba na wadhamini wa mbio hizo ambao ni pamoja na kampuni za TIPER na Pepsi.

Wadhamini wengine ni pamoja na, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM, Mwanza Water, Pigeon Hotel, The Cask and Grill, SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla (katikati) akimpatia zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 4/- mshindi wa mbio za Rock City Marathon Km 42 kwa upande wa wanawake Bi Elilither Tamui kutoka Kenya alieibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 2:42:50. Wengine ni pamoja na Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (kulia) ambao ni moja ya wadhamini wakubwa wa mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall jijini Mwanza.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (katikati) akimpatia zawadi ya fedha taslimu mmoja wa washindi wa mbio za Rock City Marathon Km 21.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla (wa pili kulia) akishiriki mbio za km 21 za RockCity Marathon sambamba na mamia ya washiriki wengine wa mbio hizo.
Baadhi ya matukio yaliyopamba mbio za Rock City Marathon msimu wa 10 jijini Mwanza.














WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA KIPINDI CHA SPORTS ARENA NDANI WASAFI MEDIA,ATOA NENO LEO JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akizungumza leo wakazi wa Uzinduzi wa kipindi kipya cha michezo cha Sports Arena,sambamba na kuwatangaza watangazaji wapya wa kipindi hicho,hafla hiyo fupi umefanyika makao makuu ya ofisi za Wasafi Media,jijini Dar

Waziri Mwakyembe amempongeza Msanii mahiri wa muziki C.E.O wa Wasafi Media, Nassib Abdull almaarufu Diamond Platnumz kwa kuanzisha kipindi cha michezo na mchango wake mkubwa kuutangaza muziki nje ya mpaka wa Tanzania na kwingineko Duniani.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba 21,2019 kwenye uzinduzi wa kipindi hicho cha Sports Arena, Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa taasisi ya Wasafi, imekuwa ikihamasisha hata wasanii wachanga kutaka kufikia mafanikio yake.“Nawashukuru sana Wasafi kwanza kwa kuweka hamasa kwenye muziki,Mtu yeyote anayeingia kwenye muziki sasa hivi anataka awe kama Diamond ni nzuri na hayo ndio maendeleo",ameeleza Dkt Mwakyembe.
C.E.O wa Wasafi Media, Nassib Abdull almaarufu Diamond Platnumz akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe kuzungumza na Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ikiwemo na kuzindua rasmi kipindi hicho,ambacho kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa
C.E.O wa Wasafi Media, Nassib Abdull almaarufu Diamond Platnumz akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe kuzungumza na Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ikiwemo na kuzindua rasmi kipindi hicho,ambacho kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa .
Meneja wa Wasafi Media atambulikae kwa jina la Babu Tale akizungumza jambo huku akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyowakutanisha wadau wa michezo,masumbwi,muziki na michezo mingine.
Mtangazaji mahiri atakaeongoza jahazi la kipindi cha Sports Arena Maulid Kitenga akizungumza jambo mara baaya kutambulishwa kwao na kipindi kuzinduliwa.
Kikosi kamilia cha kipindi cha Sports Arena ndani ya Wasafi Media
Ilikuwa ni burudani tuu na shangwe za hapa na pale
Watangazi nyota wa kpindi hicho kilichozinduliwa leo 
Baadhi wageni waalikwa na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua tukio la hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo

Magari yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuwabeba watangazaji wa kipindi hicho mara watakapokuwa wameshuka kwenye helikopta.
Helikopta iliyokuwa imewabeba Watangazaji mahiri wa kipindi cha Sports Arena ikiwa imetua uwanjani jirani na ofisi za Wasafi Media.




Wageni waalikwa

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 22,2019

WIZARA YA KILIMO YAJA NA MKAKATI WA KUZALISHA MICHE MILIONI 20 YA KAHAWA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la kahawa linalomilikiwa na Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) wakati alipotembelea  makao makuu ya Taasisi hiyo Lyamungo Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 21 Octoba 2019.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikata utepe kuzindua vitabu vya Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo, leo tarehe 21 Octoba 2019. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Dkt Anna Mghwira na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) Ndg Aloyce Mdalavuma (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikata utepe kuzindua vitabu vya Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo, leo tarehe 21 Octoba 2019 eneo la Lyamungo Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikabidhiwa zawadi ya Kahawa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) Ndg Aloyce Mdalavuma mara baada ya  kuzindua vitabu vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo, leo tarehe 21 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Dkt Anna Mghwira na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Khatib Kazungu wakikagua shamba la kahawa linalomilikiwa na Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) wakati alipotembelea  makao makuu ya Taasisi hiyo Lyamungo Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 21 Octoba 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro


Moja ya changamoto katika kuimarisha ubora wa Kahawa ni uzalishaji mdogo ya Miche ya Kahawa huku mahitaji yakiwa ni makubwa kwa wakulima.

Wizara ya Kilimo imekusudia kuzalisha mbegu mpya ambazo ni bora za kahawa kwa lengo kubwa la kubadilisha mikahawa ya zamani ipatayo milioni 240 kwa kutumia aina mpya za kahawa. 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 21 Octoba 2019 wakati wa uzinduzi wa vitabu vya kanuni bora na mitaala ya ufundishaji katika zao la Kahawa katika Ofisi za Taasisi ya utafiti wa Kahawa TACRI Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa uzalishaji wa idadi ya miche milioni saba (7) kwa mwaka ni kidogo, ambapo itatuchukua takribani Miaka 35 kubadili aina hizi za zamani hivyo aliahidi kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo itahakikisha kunakuwa na mapinduzi ya Kilimo cha kahawa nchini.

Katika kuifikia dhamira ya kubadili mikahawa ya zamani serikali kupitia wizara ya kilimo imejipanga kuanza kuzalisha Miche milioni 20 ya kahawa mpya ili kuongeza tija na uzalishaji wa kahawa.

Amesema kuwa sekta ndogo ya kahawa ina umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa taifa na huchangia takribani asilimia 24 kwa mwaka ya mapato ya mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi, ambapo ni wastani wa asilimia 4 ya pato la taifa. 

Hata hivyo, pamoja na mchango huo wa sekta ndogo ya kahawa uzalishaji bado ni mdogo sana, ambapo kwa mwaka wastani wa tani 50,000 huzalishwa. Aliongeza kuwa hali hiyo inasababishwa na tija ndogo ambapo mpaka sasa mti mmoja wa kahawa unatoa gramu 250 ikilinganishwa na wastani wa gramu 1,000 inayotakiwa kuvunwa kwa mti. 

Moja ya changamoto inayosababisha tija kuwa chini katika sekta ndogo ya kahawa ni ukosefu wa elimu ya kanuni bora ya kilimo cha kahawa kwa wakulima ambapo amewataka maafisa kilimo kote nchini kuanza kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa mikahawa mipya.

Alisema ili kuhakisha kuwa mkulima anapata tija kubwa na kuongeza kipato kutokana na kilimo cha kahawa, ni muhimu kupata elimu ya uzalishaji wa kahawa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya kanuni bora za kilimo cha kahawa. 

Waziri Hasunga ameipongeza TaCRI kwa kuandaa vitabu vilivyozinduliwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo ambavyo vitatumika kwa Maafisa Ugani, Wakulima na Wananchi wote wenye nia ya kujifunza mbinu bora za kilimo cha kahawa chenye tija. 

Mhe Hasunga amesema kuwa Vitabu hivyo vyenye picha na maelezo ya kutosha vimelenga kuwapa wakulima wa kahawa utaalamu wa kukuza zao la kahawa katika lugha rahisi ambapo lengo la vitabu hivyo ni kuhakisha kuwa kaya za wakulima wa kahawa zipatazo 420,000 nchini; wanakuwa na rejea ya haraka na rahisi wakati wote wawapo shambani, mahali ambapo hawana wataalamu; na pale ambapo kutakuwa na mtaalamu vitakuwa vichocheo vya mazungumzo ili kuweza kujua zaidi au kupata ufafanuzi wa kitaalamu wa masuala ya kilimo cha kahawa.

SHERIA IMERUHUSU KUDAI ZAWADI ULIZOTOA UCHUMBA UNAPOVUNJIKA.

$
0
0


Una mahusiano na mwanaume au mwanamke  ambaye kimsingi mpo katika uchumba. Unampa zawadi nyingi naye anakupa zawadi.  Mnayo ahadi ya kufunga ndoa na kuishi kama mme na mke . Na kwasababu hiyo unajitoa sana kimatumizi kwa mtu huyo.

Lakini katika mazingira usiyoyaelewa unaona sasa mambo hayaendi vizuri. Hayaendi vizuri katika kiwango ambacho sasa mahusiano yamevunjika kabisa. Hakuna tena mahusiano. Au bado yapo lakini kwa mambo unayofanyiwa unaona kabisa hutakiwi tena.

Kumbuka huko nyuma umegharamia sana. Umegharamia kwa fedha na mali. Swali ni je vitu hivi haviwezi kurudishwa ?. Vitu hivi haviwezi kufidiwa ?. Na je sheria imeongelea kuhusu jambo hili ?.

Majibu ya maswali haya yote ni ndiyo. Ni ndiyo, na gharama pamoja nazo zawadi zinaweza kurejeshwa. Unaweza kushangaa kuona sheria imeongelea hata mambo ya uchumba lakini ndio ukweli.
Wengi tunaijua sheria katika kuongelea wizi, dhamana, mikataba, mirathi, ndoa, na mengine. Lakini ni vyema tukajua kuwa sheria ni pana na imeongelea mambo mengi mno. Hili la uchumba nalo ni sehemu ya yaliyoongelewa.

1 KUVUNJA UCHUMBA
.
Kifungu cha 69( 1 ) cha Sheria ya Ndoa iliyofanyiwa marekebisho 2010 kinasema kuwa mtu anaweza kufungua shauri na kudai fidia baada ya uchumba kuvunjwa.

Kwa haraka utaona kuwa tafsiri ya kifungu hiki sio kufungua shauri ili kumlazimisha mtu akurudie, hapana. Mahakama haiwezi kutoa maamuzi kuwa fulani lazima amrudie fulani. Isipokuwa lengo lake ni kumtaka yule aliyeumizwa katika hili kudai fidia kutokana na maumivu aliyoyapata. Hapa hatujaongelea kurudisha zawadi.

Kudai fidia na kurudisha zawadi ni vitu viwili tofauti. Fidia inahusu kulipwa maumivu uliyoyapata kutokana na tukio hilo la kuachwa pamoja na muda uliopoteza na huyo mtu. Wakati zawadi ni kurejesha kile ulichotoa. Kwahiyo la zawadi tutaliona baadae.

Aidha masharti ya kufungua shauri la kudai fidia ni kuwa , moja anayefungua shauri awe ni yule aliyeumizwa, pili ahadi ya kuoana lazima iwe ilikuwa imefanyika Tanzania, tatu wakati mnaingia kwenye mahusiano iwe mlikuwa nyote mmetimiza miaka 18 .

2. KURUDISHA ZAWADI.

Kifungu cha 71 cha Sheria ya ndoa kinasema kuwa mtu anayo haki ya kufungua shauri kudai kurejeshewa zawadi ambazo alizitoa kwa mtu ambaye alikuwa ana ahadi ya kufunga naye ndoa lakini ndoa haikufungwa.

Zawadi ni pamoja na fedha, nyumba, magari, nguo na kila kitu chenye thamani(valuable). Haijalishi mali hiyo ipo kwenye jina la nani suala la msingi ni kuthibitisha kuwa wewe ndiye uliyetoa hiyo zawadi.

Shauri la namna hiyo unaweza kulifungua mahakama yoyote ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi au hata mahakama kuu. Itategemea na thamani ya kiwango cha mali unazodai.

Kama mali hizo zitakuwa zimekwishatumika au hazipo tena pengine zimeuzwa au kutolewa zawadi kwa mtu mwingine basi itatakiwa kulipwa fedha zinazolingana na mali hizo au mali hizo zikanunuliwe tena kwingine ili kumrudishia anayedai.
Ukishindwa kabisa kurudisha basi mali zako binafsi ambazo hazikuwa sehemu ya zawadi zitauzwa ili kupata kiwango kinachodaiwa na kama huna mali yoyote ya kuuza utatakiwa kwenda jela kama mfungwa wa madai.

Kwa hiyo watu wanatakiwa waelewe kuwa uchumba na ahadi za kuoana si jambo jepesi kama wanavyolitamka na kuliahidi .

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI URUSI KUMWAKILISHA JPM MKUTANO BAINA YA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA NA URUSI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa mkate na chumvi  ikiwa ni utamaduni wa kukaribisha wageni wa Warusi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sicho nchini humo Oktoba 21, 2019 ambako  anamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sicho nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, Oktoba 21, 2019. Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi (kushoto) na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sicho nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, Oktoba 21, 209.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Aisee...!!!! Mlinzi Takukuru aua mchumba baada kukataliwa ndoa

$
0
0

Alikuwa amemsomesha unesi,alipomaliza kusoma akasema sitaki tena ndoa,nimepata mchumba mwingine

Taarifa ya RPC mkoa wa Ruvuma
BEATA Kafuru mkazi wa Mtaa wa NHC, Tunduru Mkoani Ruvuma, mwenye umri wa miaka 26 amefariki kwa kinachodaiwa amepigwa risasi 3 kichwani na Mchumba wake James Paul(27) mlinzi wa TAKUKURU na kufariki papohapo ndani ya nyumba wanayoishi, chanzo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Marehemu alikuwa Muuguzi Hospitali ya Wilaya Tunduru na ameacha Mtoto mchanga wa miezi 11 aitwae Aviera, mtuhumiwa anasema wameishi pamoja kwa miaka 4 hadi wakazaa na walipanga kuoana, Beata akaenda kujiendeleza kimasomo Peramiho aliporudi akabadilika na kudai hamtaki.

Kwahiyo chanzo ni wivu wa kimapenzi na kulipiza kisasi kwasababu James anadai marehemu alikuwa anamtamkia Waziwazi kwamba hamtaki wakati alikuwa anampenda sana na hakuwa tayari kushare na mwingine, ila Binti kasema amepata mwingine na akataka waachane.

Kabla ya tukio mtuhumiwa alikuwa lindoni Ofisi za TAKUKURU na akatoka lindoni kwenda kutimiza adhima yake, James alipoua akataka kujiua pia, lakini kumbe risasi zilikuwa zimedondoka Housegirl akamuwahi kwa kupiga kelele Askari waliokuwa Doria wakafika.

Katika eneo la tukio tumekuta Pistol aina ya Browing (mali ya TAKUKURU), risasi nne ambazo hazikutumika na maganda matatu ya risasi, James tunamshikilia na tutamfikisha Mahakamani, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Wilaya Tunduru...
Toka kurasa wa Benjamin Kasenyenda Andongolile.....

MGOGORO WA KUGOMBEA MALI ZA MAREHEMU BILIONEA ERASTO MSUYA WAPATIWA UFUMBUZI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Mgogoro wa kugombea mali wa Familia ya Marehemu Bilionea Erasto Msuya uliodumu kwa zaidi ya Miaka sita ,umepata ufumbuzi Mara baada ya upande mmoja kukubali kuondoa kesi ya Miradhi mahakama ili kujadili jambo hilo mezani.

Akiongea mbele ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro aliyekuwa akiongoza kikao cha familia hizo,ofisini kwake,mama wa marehemu,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu wamekubali kuondoa kwa muda shauri hilo mahakamani ili kurejea meza ya mazungumzo.

Ameongeza kuwa wao kama wazazi hawana nia ya kupoka Mali za marehemu ila wanachopigania ni haki ya urithi wa Mali kwa watoto wanne walioachwa na marehemu Bilionea Erasto Msuya, ambazo hadi sasa hazijagawanywa huku ikidaiwa kuwanufaisha ndugu wa upande wa Mke wa marehemu.

"Nitakwenda mahakamani na mwanasheria wangu tukalitoe kwa muda jambo hilo na kurejea meza ya mazungumzo" Alisema mama Ndeshu

Awali mtoto mkubwa wa marehemu,aitwaye Kelvin Saimoni Msuya alisema kuwa yupo tayari kukaa meza moja ya mazungumzo na upande wa wazazi wa baba yake na kuwataka ndugu hao kuwa na upendo na mama yake anayesota Gerezani kwa kesi ya mauaji.

Katika kikao hicho dada wa marehemu aitwaye Dkt Easter Msuya naye akatoa wosia kwa watoto wa marehemu ambapo aliwataka kupendana na kumtanguliza Mungu katika kila jambo

Baadae Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro akahitimisha kikao hicho kwa kumwaga maombi mazito huku akiishukuru familia ya Msuya kwa kuondoa shauri hilo mahakamani ili kufanya mazungumzo ya kugawanya Mali hizo na watoto warejee masomoni.
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akisuluhisha mgogoro wa miradhi uliokuwa ukiikabili familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya.


 Wanafamilia ya marehemu Erasto Msuya wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ofisini kwake jana 
mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimkumbatia mtoto wa marehemu Erasto Msuya kijana anaejulikana kwa jina la Kelvin Saimoni Msuya mara baada yakusuluhisha

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE AKAGUA ZAHANATI YA SHELUI MKOANI SINGIDA NA KUTOA MSAADA

$
0
0

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akimkabidhi mashuka kwa Muuguzi wa Zahanati ya Kata ya Shelui, Cecilia Emmanuel alipokuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Diwani wa kata hiyo Kinota Khamis (JB)
Mhe.Aysharose Mattembe akisaini katika kitabu cha wageni katika Zahanati hiyo.
Diwani wa Kata ya Shelui Kinota Khamis akitoa taarifa fupi kuhusu zahanati hiyo. Kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu wa kata hiyo, Jenipher Miano.
Muuguzi wa zahanati hiyo, Cecilia Emmanuel akisoma taarifa fupi ya zahanati hiyo mbele ya Mbunge Mhe. Aysharose Mattembe.
Mhe.Mattembe akizungumza na wagonjwa waliokuwepo kwenye zahanati hiyo kupata matibabu.
Mhe Mattembe akigawa sabuni kwa wagonjwa.
Mhe.Mattembe akimpatia sabuni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Alex Paulinus (wa pili kulia) kwa niaba ya watumishi wenzake.
Hapa Mhe. Mattembe akikagua chumba cha maabara.
Mhe.Mattembe akionesha upendo kwa kuwapakata watoto waliozaliwa katika zahanati hiyo.
Diwani wa Kata hiyo, JB akizungumza na wanawake waliowapeleka watoto wao kliniki katika zahanati hiyo.
Mhe. Mattembe akizungumza na wanawake waliowapeleka watoto wao kliniki katika zahanati hiyo.
Mhe.Mattenbe akiwakabidhi mashuka wanawake hao kwa ajili ya zahanati hiyo.
Mhe.Mattenbe akiwakabidhi mashuka wanawake hao kwa ajili ya zahanati hiyo.
Majengo ya zahati mpya iliyoanza kujengwa kwa msaada wa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ambao ujenzi wake umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.



Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kata ya Shelui Wilayani Iramba mkoani Singida wameiomba Serikali iwasaidie kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kata hiyo ili waondokane na adha wanayoipata ya kupata huduma za matibabu 

Wananchi hao walitoa ombi hilo kwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata hiyo mwishoni mwa wiki.

Akizungumza mbele ya mbunge huyo mkazi wa Kijiji cha Kibigiri Mussa Kizugulu alisema wanachangamoto kubwa ya kutokuwa na zahanati kwani iliyopo ni ndogo na inaelemewa na wingi wa watu wanaokwenda kupata huduma.

Alisema zahanati hiyo inatoa huduma kwa wananchi kutoka Kijiji cha Kisonso ambacho kipo kilomita 10, Masagi kilometa nane, wembere kilometa tisa na Tintigulu kilometa nane ambao hulazimika kutembea umbali huo hadi kufika katika zahanati hiyo kupata matibabu.

Mwadawa Salum kutoka Kijiji cha Nselembwe alisema changamoto nyingine waliyonayo ni pale inapotokea ajali katika barabara kuu ya kutoka Singida kwenda Mwanza ambayo inapita jirani na zahanati hiyo kuwa watumishi huzidiwa kutoa matibabu na kulazimika kuwapeleka majeruhi Igunga na Tabora kwa matibabu.

Mkazi wa Kijiji cha Kyala Mwajuma Permena alisema zahanati hiyo kwa sasa imezidiwa hivyo kuwa changamoto kwa wajawazito wanaokwenda kujifungua kutokana na chumba cha wazazi kuwa kidogo.

Diwani wa kata hiyo Kinota Khamis (JB) alisema jengo la zahanati hiyo ni chakavu kwani lilijengwa toka enzi ya ukoloni mwaka 1937 lakini mwaka 2010 Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alianza kuwajengea zahanati nyingine ambayo ujenzi wake bado haujakamilika ambapo anaiomba serikali iwasaidie kukamilisha ujenzi huo na kuifanya zahanati hiyo kuwa kituo cha afya ili kuwapunguzia adha wananchi.

Mbunge Aysharose Mattembe baada ya kuambiwa changamoto hiyo aliahidi kuifanyia kazi kwa kuwapelekea wahusika ambapo pia alitoa mashuka kwa ajili ya zahanati na sabuni ambazo alizigawa kwa wagonjwa na watumishi wa zahanati hiyo. 

Benki ya DCB yashinda tuzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto), akikabidhi tuzo ya  mshindi wa tatu katika kitengo cha makampuni bora ya mwaka katika eneo la uwekezaji katika sekta za  kibenki  kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya Biashara ya DCB, Regina Mduma wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanachama wa DSE jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Wengine pichani kutoka kushoto ni;  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es salaam, Moremi Marwa,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama na Ofisa katika kitengo cha Sheria wa DCB, Grace Ringo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akishikana mikono  Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria was Benki ya DCB, Regina Mduma, baada ya kumkabidhi iliyoshinda benki hiyo ya  mshindi wa tatu katika kitengo cha makampuni bora ya mwaka katika eneo la uwekezaji katika sekta za  kibenki  wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanachama wa DSE jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa katika kitengo cha Sheria wa DCB, Grace Ringo.
Mkurugenzi katika Kitengo cha Sheria wa Benki ya DCB, Regina Mduma (kulia), na Ofisa wa Kitengo hicho Grace Ringo wakionesha tuzo hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha

NAIBU WAZIRI MABULA AAGIZA KUTAMBULIWA WAMILIKI WA MAENEO WASIOTAKA KUMILIKISHWA HAI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM HAI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini kuwatambua wamiliki 2,019 wa maeneo katika halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambao hawataki kumilikishwa maeneo yao na kupatiwa hati.

Agizo hilo linafuatia Dkt Mabula kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri hiyo Jacob Muumba kuwa pamoja na halmashauri hiyo kupima viwanja 2,019 lakini wamiliki wake hawajajitokeza kumilikishwa jambo lililomstua Naibu Waziri wa Ardhi.

‘’Watu wana maeneo lakini hawataki kumilikishwa, wanakwepa kitu gani maana hawalipi kodi’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza wale wote wenye maeneo yaliyopimwa katika halmashauri ya wilaya ya Hai kutambuliwa na kujulikana wanamiliki maeneo yao toka muda gani na kusisistiza kuwa hakuna atakayeachwa na zitaangaliwa hatua za kuchukua.

Katika hatua nyingine Dkt Mabula ameagiza kufuatiliwa kwa maeneo yote ya biashara ya hamashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambayo hayalipiwi kodi ya pango la ardhi ili yaweze kulipiwa.

Alisema, pamoja na halmashauri hiyo kuwa na maeneo ya kibiashara yaliyopimwa kama vile Stendi na Soko lakini hakuna hata eneo moja lililolipiwa kodi ya pango la ardhi hivyo basi Mkurugenzi wa halmashauri lazima ahakikishe analipia maeneo yake ya biashara.

‘’DED wa Hai hujawahi kulipia kodi ya pango la ardhi ya Stendi na Soko wakati vimepimwa na kama halamashauri hailipi je mtu wa kawaida itakuaje? alihoji Dkt Mabula.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya aliagiza kupatiwa taarifa ya maandishi kuhusiana na halmashauri ya wilaya ya Hai kushindwa kulipia kodi ya pango la ardhi katika maeneo yake ya biashara na kumuahidi Naibu Waziri Mabula kuwa atalifanyia kazi suala hilo katika kipindi cha muda mfupi pamoja na lile la wamiliki wa maeneo wasiotaka kumilikishwa.

Hata hivyo, Ole Sabaya alimueleza Dkt Mabula kuwa pamoja na changamoto mbalimbali katika sekta ya ardhi wilayani humo Ofisi yake kwa kushirikiana na idara ya ardhi imeweza kuzipatia ufumbuzi kero za ardhi za wananchi wa wilaya hiyo zipatazo 350 kati ya 432 zilizowasilishwa wakati wa siku maalum ya ardhi maarufu kama Ardhi Day. 

Wakti huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekagua ujenzi wa mradi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo ambapo alilitaka Shirika la Nyumba kukamilisha ujenzi katika muda uliopangwa.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Kilimanjaro Mradi huo unaogharimu takriban shilingi milioni 910 unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka 2019.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozana na Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya kuelekea kukagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya hiyo kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
 Mhandisi anayesimamia ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Peter Mwaisabura akimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hiyo jana wakati Naibu Waziri alipofanya ziara kukagua mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifafanua jambo wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa  Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro unaosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua jalada la ardhi katika ofisi ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Kulia ni Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Jacob Muumba.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Kanisa la Arusha Praise center laandaa maombi ya kuombea Taifa

$
0
0
Na woinde shizza, Michuzi blog, Arusha
TAASISI ya Kanisa la Arusha Praise Center  limeandaa Maombi makubwa ya kuliombea Taifa kwa ajili ya uchaguzi mkuu na amani ya nchi litakalofanyika tarehe 17 mwezi wa November jijini Arusha kwenye ukumbi wa Hotel ya Mount Meru eneo la kata ya Sekei jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari Askofu wa kanisa hilo Aminiel  Mgonja alisema kuwa Kongamano hilo litaenda sambamba na kuombea nchi hususani kuona umuhimu wa wananchi kuchagua na kuchaguliwa wakiwa kwenye Amani na utulivu.

Amesema Taifa lolote lisilo na Amani na utulivu haliwezi kuwa na uchaguzi huru na haki hivyo kwetu sisi kama watanzania ndio tumeona tuliombee taifa letu wakati huu linaenda kwenye uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa na baadae uchaguzi wa madiwani wabunge na Rais hapo mwakani.

Ameeleza kuwa kwa msingi huo ili kuwapata viongozi lazima wapewe kibali na Mungu ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kuchagua viongozi kila baada ya miaka mitano hivyo maombi yetu ni kuombea taifa letu wakati huu tunapoenda kuchagua viongozi.

“Niwasihi sana viongozi wetu na watanzania kuona umuhimu wa kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka huu na mwakani sisi tumejipanga kuombea taifa kupita salama kwenye chaguzi hizi”

Amesema kuwa maombi hayo yatawashirikisha wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro pamoja na masheikh na Maaskofu wa makanisa ya KKKT Katoriki na madhehebu mbalimbali.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo la kuombea uchaguzi Mkuu, Zacharia Isack amesema kuwa tamasha hilo ni sehemu ya kuwaleta jamii kuwa wamoja wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa.

Amesema kuwa wanatoa rai kwa jamii ya mikoa ya kaskazini bila kujali itikadi zao kushiriki kwa pamoja kwenye tamasha hilo ambalo limelenga kuliombea taifa Amani na utulivu kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu na hakutakuwa na malipo kwenye tamasha hilo.

Amesema kuwa mziki wa injili ndio utabeba tamasha hilo na wamejipanga sana kuwapokea wageni hao kwa ajili ya tamasha hilo katika ukumbi wa Hotel ya Mount Meru na kuwataka watu wa dini zote kujitokeza kuja kuliombea taifa lao kipindi hichi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na baadae uchaguzi mkuu 2020.

Mkurugenzi wa Kismart Media ya Jijini Arusha Mary Mollel amesema kwamba tamasha hilo litabeba vyombo vya habari kwa lengo la kutoa taarifa kwa jamii juu ya kuombea Amani pamoja na kufikia uchaguzi wenye amani na utulivu
Askofu wa kanisa la Arusha Praise center,  Aminiel  Mgonja akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Arusha.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images