Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

BARAZA LA KILIMO LAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MFUMO WA UAGIZAJI WA MBOLEA.

$
0
0
 Mratibu Taifa wa Programu ya Ubia wa Kilimo Tanzania chini ya Baraza la Kilimo Bw. Mark Magila akifungua Warsha ya siku moja iliyofanyika Mkoani Morogoro na kujumuisha Wadau wa Kilimo ilikujadili matokeo ya Utafiti kuhusu Mfumo wa uagizaji Mbolea kwa Pamoja. 

 Makamo Mwenyekiti wa Chama cha wasambazaji wa Pembejeo nchini TADCOS Bw. Iddi Madeni akichangia kuhusu Mfumo huo wa uagizaji wa Mbolea kwa pamoja, ambapo pamoja na masuala mengine amesema ni muhimu serikali ikawa inawashirikisha kabla ya upangaji wa bei elekezi .

 Mkulima wa Tumbaku kutoka Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Bw. Juma Phesto akichangia mada kuhusu uagizaji wa Mbolea kwa pamoja ambapo amekiri kuwa mfumo huo umesaidia mbolea kuwafikia wakulima kwa wakati, Mkutano huo umefanyika Mkoani Morogoro.
Sehemu ya washiriki wa Warsha hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada katika mkutano huo uliofanyika Mkoani Morogoro.

 Washiriki wa Warsha ya wadau wa Kilimo iliyofanyika Mjini Morogoro na kuratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.


SERIKALI imeelezea kuridhishwa na mfumo wa uagizaji wa Mbole kwa pamoja licha ya uwepo wa changamoto kadhaa zikiwemo za ucheleweshaji wa mbolea kuwafikia wakulima ikiwa ni pamoja na suala la bei elekezi.


Kauli hiyo ya Serikali imetolewa jana Mjini Morogoro na Afisa Kilimo Idara ya Mazao Kitengo cha Pembejeo kutoka Wizara ya Kilimo Bw Joseph Lyafwila wakati wa Warsha ya wadau wa Sekta ya Kilimo iliyokuwa ikiangazia matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu Mfumo wa uagizaji wa Mbolea kwa Pamoja ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.


“Kwetu kwenye Sekta ya Kilimo Mfumo huu ni mpya na tayari  tumeona mafanikio yake ndani ya kipindi cha miaka mitatu, hivi sasa Mbolea inafika nchini kwa wakati na wakulima pia inawafikia kwa wakati na kama nilivyosema ni ukweli kwamba bado kunachangamoto kadhaa,


“Tunajua pia wakulima wamekuwa wakilalamikia suala la bei na hii inatokana na ukweli kwamba kuna baadhi ya vijiji viko mbali sana na inafanya bei inapanda kidogo inagwa Serikali bado inangalia changamoto zote  zinazoendelea kujitokeza katika mfumo huu ili tuweze kuzishughulikia “ alisema Bw Joseph.


Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Timothy Mmbaga alisema kuwa waliamua kufanya utafiti huo kuhusu maendeleo ya mfumo ili kuona namna inavyoweza kuishauri Serikali namna bora zaidi ya kuendelea na mfumo huo.


“Kabla ya mfumo huu kulikuwa na changamoto nyingi sana watu walikuwa wanauziwa mbolea feki wengine walikuwa wanauziwa hadi siment, lakini Baraza la Kilimo tulipiga sana kelele na tunaishukuru Serikali ililiona hili na hatimaye kuja na mfumo huu,


“Tunajua mahitaji ya mbolea kwa sasa yanazidi kuongeka hivi sasa inakadiriwa kufikia tani laki nne ingawa kupitia mfumo huu ni tani 70,000 pekee ndio inayoagizwa ingawa tunajua kuna njia nyingine nyingi za uagizaji wa mbolea zaidi ya DAP na UREA zinazoagizwa kupitia mfumo huu” alisema Bw. Mmbaga.



DKT. MPANGO AIOMBA BENKI YA DUNIA KUSAIDIA SEKTA YA KILIMO NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Ramadhani Kissimba na Eva Valerian, Washington Dc 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) ameitaka Benki ya Dunia kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania ili kuweza kuwainua kiuchumi wakulima hasa wale wa kati na wadogo.

Dkt.Mpango aliyasema hayo wakati wa kikao cha majadiliano na timu nzima ya Benki ya Dunia ambayo inafanya kazi nchini Tanzania na wengine kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo nchini Marekani. 

Mhe.Mpango alisema katika mkutano huo walipitia kwa pamoja utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hivi sasa inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, lakini pia walipitia na kujadili miradi ambayo inaanza kufikiriwa kwa ajili ya utekelezaji kwa mwaka utakaofuata.

‘’Moja ya vitu vilivyonifurahisha mwaka jana kwenye mjadala niliwaaomba sana kwamba hatuwezi kuendelea kuitaka Benki ya Dunia isaidie kwenye miradi mingine tu ni lazima nguvu kubwa ielekezwe pia kwenye miradi ya kilimo ambayo kwa sasa msaada wa Benki ya Dunia katika miradi hiyo ni kidogo sana’’ alisema Dkt.Mpango.

Aidha Dkt.Mpango alielezea dhamira ya Tanzania kushirikiana na Benki ya Dunia ili kuanzisha programu itakayohakikisha kuwa tija inapatikana kwenye sekta nzima ya kilimo na mifugo, lakini pia kuweza kuyafikia masoko kwa mazao yanayozalishwa nchini, hasa yale yenye thamani kubwa duniani.

Dkt. Mpango amefafanua kuwa Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya mabdiliko inayofanyika katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka, lakini vile vile wakulima wa kati wamezidi kuongezeka. 

Aidha, kuongezeka kwa maeneo ya kilimo imewafurahisha wataalamu wa Benki hiyo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa aina ya mazao yanayolimwa   hasa yale yenye thamani kubwa ambayo yanalimwa kwa kasi kubwa sana kuliko ilivyokuwa awali.

Pia Dkt. Mpango alisisitiza kuwa, Benki ya Dunia imeshafanya utafiti wao wa kutosha ambao umeonesha kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka.

Mhe. Mpango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali tena kuleta timu ya wataalamu nchini Tanzania ambayo itakaa na sekta nzima ya kilimo na ufugaji ili kuona ni namna gani hasa Benki ya Dunia itasaidia kuinua sekta hiyo, na kuwasaidia wakulima hasa katika matumizi ya nguvu kazi kwa upande mmoja na kuwaongezea kipato kwa upande mwingine.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifuatilia majadiliano katika Mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika uliofanyika Jijini Washington DC. Kulia kwa Mhe.Mpango ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru na anayefuatia ni Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Msafiri Mbibo.
Mtaalam wa Masuala ya Kilimo kutoka Benki ya Dunia Bw. Holger Krag akifafanua jambo kwa ujumbe wa Tanzania.

Zingatieni Maadili ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yenu – CGP Kasike

$
0
0
Na ASP Lucas Mboje, Masasi
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike amewaasa Maafisa na askari wote wa Jeshi hilo kuendelea kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi na nidhamu Jeshini. 
Amesema hayo leo alipotembelea katika magereza ya Namajani, Masasi na Gereza Newala katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara yenye lengo la kujionea utendaji kazi wa Jeshi hilo katika vituo mbalimbali vya Jeshi hilo.

Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa wapo baadhi ya maafisa na askari ambao wanatatizo la kimaadili na hawataki kubadilika hali ambayo inaharibu taswira ya Jeshi hilo katika jamii.
 "Taswira ya Jeshi la Magereza inategemea zaidi utekelezaji mzuri wa majukumu yenu kwa kuzingatia maadili na nidhamu. Jukumu letu ni kusimamia wafungwa ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza adhabu zao kwa mujibu wa Sheria, " alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amekemea tabia ya ulevi wa kupindukia kwa baadhi ya maafisa na askari kwani tabia hiyo inachangia sana katika kushuka kwa maadili ndani ya Jeshi hilo.
“Nitaendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuwafukuza kazi Maafisa na askari ambao hawataki kubadilika kwani vitendo vya ukiukaji maadili havikubaliki Jeshini,” Amesisitiza Kamishna Jenerali Kasike.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Varisanga Msuya amemhakikishia Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza kuwa atahakikisha kuwa Maafisa na askari katika Mkoa wake wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa Jeshi hilo. 

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, kesho Oktoba 17, 2019 ataendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara ambapo anatarajia kutembelea Gereza Kiwanda Chumvi kabla ya kuhitimisha ziara yake Gereza Kuu Lilungu.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Namajani lililopo Wilayani Masasi, leo Oktoba 16, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya  kikazi Mkoani Mtwara.
 Baadhi ya askari wa Gereza Namajani wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Masasi, leo Oktoba 16, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya  kikazi.
 Mkuu wa Gereza Masasi, Mrakibu wa Magereza, Juma Mkumba akitoa taarifa fupi ya Gereza  mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) alipotembelea Gereza hilo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) akikagua Mifugo katika Gereza Namajani lililopo Wilayani Masasi, leo Oktoba 16, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya  kikazi Mkoani Mtwara.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiwasili Gereza Newala, leo Oktoba 16, 2019 alipotembelea gereza hilo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Gereza Namajani alipotembelea leo Oktoba 16, 2019 katika ziara yake ya  kikazi. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Varisanga Msuya(Picha zote na Jeshi la Magereza).

WAFANYABIASHARA MANYARA WAKUNWA NA UTENDAJI WA RAIS MAGUFULI-WAAHIDI KULIPA KODI KWA HIARI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza jambo alipofanya kikao na wafanyabiashara wa Mkoa wa Manyara kujadili fursa na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao katika kikao kilichofanyika Ofisi za Halmashauri ya Mji wa Babati, mkoani Manyara
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Mhe. Esther Mahawe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Nicodemus Tarmo, wakifuatilia mjadala kati ya wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipotembelea mkoa huo na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akisindikizwa na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara baada ya kuzungumza nao Mjini Babati Mkoani humo
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara, Mjini Babati.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)

………………..

Na Benny Mwaipaja, WFM, Manyara

WAFANYABIASHARA mkoani Manyara, wameahidi kuendelea kulipa kodi kwa hiari baada kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wafanyabiashara hao wamemweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji aliyekutana nao Mjini Babati ili kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta binafsi pamoja na kuwaelimisha namna Serikali ilivyofuta kodi lukuki kwa lengo la kuwawezesha kufanyabiashara zao kwa tija Zaidi.

Pamoja na ahadi hiyo ya kulipa kodi kwa hiari, wafanyabiashara hao wamemwomba Dkt. Ashatu Kijaji awasaidie kufikisha kilio chao kwa Serikali ili idadi kubwa ya taasisi za Serikali zinazowabana kulipa kodi zipunguzwe, ama kodi zinazodaiwa ziunganishwe ili kumwondolea mfanyabiashara adha ya kudhibitiwa na Mamlaka nyingi.

Baadhi ya Mamlaka zilizotajwa ni pamoja na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Wakala wa Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) na nyingine nyingi ambazo wamesema mbali na kuwatoza kodi kubwa lakini wamekuwa wakipata usumbufu wa aina mbalimbai.

Akijibu hoja mbalimbali za wafanyabiashara hao, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amewapongeza wafanyabishara hao kwa kulipa kodi ambayo imeiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, mwezi Septemba, tumekusanya Zaidi ya shilingi trilioni 1.76 kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru” alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyajibiashara ambapo mpaka sasa imeondoa Zaidi ya kodi 50 zilizokuwa zikiwakwaza wafanyabiashara lengo likiwa ni kuwawezesha kufanyabishara yao kwa ufanisi zaidi ili waendelee kulipa kodi

“Tumepunguza kodi nyingi sana!, Mwaka uliopita wa fedha (2018/2019) tulipunguza kodi 108 na mwaka huu wa fedha (2019/2020 tumepunguza kodi na tozo 54 kwa makusudi, Dkt, John Pombe Magufuli ameamua kuwawezesha watanzania, kila mmoja kwenye eneo lake la kazi afyanye kazi vizuri” alisisitiza

Aidha, Dkt. Kijaji aliwataka wafanyabiashara waliopata msamaha wa riba kwenye kodi mbalimbali walizokuwa wanadaiwa, walipe madeni yao kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na kwamba hakutakuwa na muda mwingine utakao ongezwa.

Aliwataarifu wafanyabiashara hao kwamba Serikali imesitisha kwa muda utoaji fedha kwenye miradi mikubwa ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI yenye lengo la kuziwezesha Halmashauri kujitegemea kimapato hadi pale mfumo madhubuti wa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo utakapo wekwa.

Dkt. Kijaji alitoa kauli hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul, aliyeomba shilingi bilioni 5.5 kutoka Serikalini kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi ili kuboresha mazingira ya biashara na utoaji huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu Kamishna Operesheni ya Kodi Bw. Simon Kingu, alisema TRA iko tayari kushirikiana na wafanyabishara na kuhakikisha wanatatua kero zao ili walipekodi kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Alisema juhudi kubwa inayofanywa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati wa viwanda unategemea mchango mkubwa wa wafanyabiashara katika kulipa kodi stahiki.

CDF MABEYO AONGOZA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA TAIFA KUKAGUA VIPENYO SALAMA NAA VISIVYO SALAMA KATIKA MPAKA WA TANZANIA NA MSUMBIJI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akiongea na wananchi wa kijiji cha Kitaya baada ya kutoka kutembelea eneo la kumbukizi ya shujaa UD 5826 L/CPL Ahamad Mzee, alipoangushia Ndege mbili za Ureno april 1972, katika Msafara huo umeongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mwenyekiti wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama CDF, General Venance Salvatory Mabeyo. 
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mwenyekiti wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama CDF, General Venance Salvatory Mabeyo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama, ameyasema hayo leo alipokuwa katika kijiji cha Kitaya baada ya kutoka kutembelea eneo la kumbukizi ya shujaa UD 5826 L/CPL Ahamad Mzee, alipoangushia Ndege mbili za Ureno april 1972 .
 Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mwenyekiti wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama CDF, General Venance Salvatory Mabeyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa, Kamishna Diwani Athuman wakiwa katika eneo Kitaya mkoani Mtwara katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji ilipo  kumbukizi ya shujaa UD 5826 L/CPL Ahamad Mzee, alipoangushia Ndege mbili za Ureno april 1972.
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mwenyekiti wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama CDF, General Venance Salvatory Mabeyo, katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa, Kamishna Diwani Athuman alie mkono wa kushoto wa IGP Sirro wakiwa katika hifadhi ya bandari ya Ghuba ya Mnazi na maingilio ya mto Ruvuma baada ya kukagua kipenyo cha Kilambo kinachotumiwa na wahalifu kutoka nchi jirani ya Msumbiji. (PICHA NA JESHI LA POLISI)

MRADI WA HPSS WASAIDIA KUBORESHA SEKTA YA AFYA NCHINI

$
0
0

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii

KATIKA kutatua Changamoto ya wahudumu wa ugawaji dawa katika vituo vya Afya nchini mradi wa HPSS tuimarishe Afya umesaidia kusomesha baadhi ya wahudumu wa vituo vya afya nchini.

Kupitia mradi wa kuboresha na kuimarisha Afya nchini wa HPSS wakishirikiana na chuo kikuu cha Afya cha Mtakatifu John kilichopo makao makuu ya nchi Dodoma wamesaidia kuwapa mafunzo wahudumu wa vituo vya afya vilivyopo vijijini katika kutoa elimu ya msingi ya famasia.

Hayo yamesemwa na Mkufunzi wa Chuo cha mtakatifu John, Romuald Mbwasi wakati akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam leo katika kongamano la wadau wa afya kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini na nchi za nje.

"Ili kuweza kuondoa tatizo la kuwafanya watu wanaotoa dawa katika vituo vya afya na Zahanati huko vijijini tukaanzisha kozi ya mwaka mmoja ya watoa dawa (Wafamasia) ambao wanapata mafunzo ya kifamasia". Amesema Mbwasi.

Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba wanaotoa elimu ya wafamasia ni kutokutambuliwa kwa kozi ya mwaka mmoja na utumishi kuajili moja kwa moja serikalini lakini wanaweza kuwaajili kama wahudumu wa saidizi wa afya lakini Serikali inaweza kuwaajili kama wasaidizi wa afya wanaotoa dawa katika vituo vya afya.

Iki kuweza kuziba pengo la wahudumu wa afya wanaweza kuajiliwa kwa kazi maalumu kwa kutoa dawa kuagiza dawa kwa ufasaha zaidi kwa kuwa ndivyo wanavyofundishwa.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Josephat Kandege amewaasa wadau wa afya nchini kote watumie mafunzo waliyofundishwa kwa ufasa hasa wakizingatia takwimu na Uvumbuzi.

 Mkufunzi wa Chuo cha mtakatifu John, Romuald Mbwasi akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamano la wadau wa afya kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani. Amesema kuwa katika Mradi wa HPSS wameweza kuwezesha maliasili watu wengi ili kuoresha huduma za afya katika vituo vya afya nchini kote.
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Josephat Kandege akizungumza na wadau wa afya wakati wa kufunga kongamano la Afye lenye ujumbe "The Future of Tanzania Health Supply chain Perfomance Driven by Data and Innovation "  (Tanzania ijayo katika utoaji huduma kwa kuzingatia Takwimu na Uvumbuzi).
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Josephat Kandege akizungumza wakati wa kufunga kongamano la wadau wa Afya jijini Dar Es Salaam. 


Baadhi ya wadau wa Afya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Josephat Kandege jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yakutana na Wadau wa Uchaguzi Dodoma

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano Kati ya Tume na wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma, kuelekea kuanza maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Dodoma.Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera, akizungumza wakati wa mkutano Kati ya Tume ya uchaguzi na Wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma, kuelekea kuanza maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage, katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Dodoma, Mara baada ya kufungua mkutano Kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage, katikati akiwa na wahariri wa vyombo vya habari Mkoa wa Dodoma, baada ya kufungua mkutano Kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma.
…………….

Na.Boniphace Richard

Tume ya taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema imekamilisha maandalizi yote ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Dodoma, huku wakibainisha kuwa ili kupata mafanikio katika zoezi hilo linahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau.

Na ili kuhakikisha elimu ya mpiga kura inawafikia wananchi kikamilifu, wametoa vibali kwa asasi zisizokuwa za kiserikali katika kueneza elimu hiyo katika jamii.

Haya yamebainishwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (rufaa) Semistocles Kaijage, wakati wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi katika jiji la Dodoma wakiwamo wahariri wa vyombo vya habari asasi za kiraia, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Amesema tume tayari imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Dodoma maandalizi yake yamekamilika zoezi hilo linategemea ushirikiano wa wadau mbalimbali .

“Lengo la kukutana nanyi leo ni kuwafahamisha kuwa tume imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoa wa Dodoma na tunaamini mafanikio ya zoezi hilo linategemea ushirikiano wa wadau” amesema Jaji Kaijage.

Aidha amebainisha kuwa zipo asasi za kiraia ambazo zimepewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura kwa madhumuni hayo, hivyo wananchi watakapoona asasi hizo watumie nafasi hizo kujifunza kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema kwa upande wa Mkoa wa Dodoma zoezi la uhakiki liliongeza vituo vya uandikishaji wa daftari l kudumu la wapiga kura kutoka vituo 2,606 vilivyokuwemo mwaka 2015, hadi kufika 2,686, hivyo kuwa na ongezeko la vituo 80.

Zoezi hilo lilizinduliwa July 18, 2019 Mkoani Kilimanjaro, na baada ya uzinduzi huo zoezi hilo liliendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali, pia baada ya mwaka 2015, tume imekamilisha zoezi kwa awamu ya kwanza katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara, Simiyu,Mara,Mwanza,Geita,Shinyanga,Kagera na Kigoma.

Huku akibainisha kuwa ya Tabora,Katavi,Rukwa na Dodoma zoezi hilo likiwa bado kinaendelea, uboreshaji kwa mwaka huu utafanyika kwa kutumia Technolojia ya kielectronic ya Biometriki(BVR) mfumo huo itachukua taarifa za mtu za kibaiolojia na kuzihifandhi katika kanzi data.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt Wilson Mahera, amesema tume ya taifa ya Uchaguzi imepewa jukumu la kikatiba la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge kwa Jamhuri ya Muungano, na Madiwani kwa Tanzania bara.

Na kwa kila Kijiji/Mtaa kutakuwa na angalau na kituo kimoja cha kuandikisha wapiga kura, na vituo vya kuandikisha wapiga kura vimepangwa katika majengo ya Umma na maeneo ya wazi.

SAMIA KUFUNGUA MAONYESHO YA PILI YA VIWANDA MKOANI PWANI

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MAKAMU wa Rais wa Jamhur ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua maonyesho ya viwanda ambayo yanafanyika kwa mara ya pili mkoani Pwani, octoba 17 mwaka huu.

Katika maonyesho hayo ,wenye viwanda 206 wamejitokeza kushiriki .
Maonyesho hayo yataambatana na kongamano la uwekezaji litakalofanyika octoba 19 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Wazir Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo, mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema, waratibu wa maonyesho hayo watakuwa ni wabobezi wa masuala ya maonyesho kama hayo kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya viwanda (TANTRADE) .

Alieleza, malengo ya matukio hayo ni kuonyesha kwamba mkoa wa Pwani ,umedhamiria kuwa ukanda wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya.

Aidha Ndikilo alifafanua lengo la kongamano hilo ,kuwa ni kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii,uchumi,kijamii,kilimo,uvuvi na viwanda.

“Kufanyika kwa kongamano hili italeta picha halisi ya fursa zote zilizopo mkoani Pwani,na kuonyesha namna mkoa ulivyopiga hatua katika sekta ya viwanda,uwekezaji na fursa za miradi mikubwa ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa uzalishaji umeme megawatts 2,100 STIGO ,huko Rufiji”alibainisha Ndikilo.

Hata hivyo,mkuu huyo wa mkoa alisema wenye viwanda maonyesho ya mwaka jana walikuwa 166 mwaka huu wanatarajia wameongezeka 206.
Nae Januarius Maganga wa TSN alisema ,wanakwenda kuratibu maonyesho hayo ikiwa ni maonyesho ya kumi .

Maonyesho hayo pia yatafungwa octoba 23 mwaka huu na Wazir Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda


WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA WALIOKIUKA MAAGIZO YA SERIKALI WAFUTIWE VIBALI VYA KUINGIZA NA KUSAFIRISHA VYUMA CHAKAVU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene akiongea katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi yake jijini Dodoma na Wajumbe wa Kikosi kazi ( hawapo pichani) kilichoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa makontena ya kusafirisha vyuma chakavu yaliyokamatwa bandarini jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt Gwamaka Mafwenga akiongea wakati wa kikao cha kumkabidhi ripoti ya uchunguzi wa makontena ya vyuma chakavu yaliyokamatwa bandarini aliyekaa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene akipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa wa Mazingira (NEMC) ripoti ya uchunguzi wa makontena ya vyuma chakavu yaliyokamatwa bandarini jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikosi kazi kilichoundwa kwa ajaili ya uchunguzi wa makontena ya vyuma chakavu yaliyokamatwa katika jiji la Dar Es salaam.

………………….

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene ameagiza kufutwa kwa vibali vya wafanyabiashara wote wanaosafirsha vyuma chakavu ambao hawakufuata maelekezo na maagizo ya Serikali.

Amesema hayo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda kwa ajili ya uchunguzi wa makontena ya bidhaa za chuma chakavu yaliyokua yamekamatwa kwa uchunguzi katika bandari ya jiji la Dar Es Salaam. Ninaagiza wafanyabiashara wote waliokiuka maagizo na maelekezo ya Serikali wafutiwe vibali vyao.

Waziri Simbachawene ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya na amepokea mapendekezo yote yaliyopendekezwa na kamati hiyo. “Nawapongeza sana mmefanya kazi kubwa na mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati nimeyapokea na ninaagiza NEMC kama msimamizi mkuu kusimamia jambo hili’ alisema Waziri

Aliongeza kuwa Wafanyabiashara wa vyuma chakavu siyo wakweli mana wengi wanasafirisha bidhaa zingine tofauti na vyuma chakavu huku wakisingizia kuwa wamebeba vyuma chakavu wakati siyo kweli. Vitu mbalimbali vinasafirishwa kama vile mifuniko ya chemba, injini za vifaa vya moto, mita za maji, vipande vya bomba na vingine ni vipya kabisa na haviko kwenye kundi la vyuma chakavu.

Akiongea wakati wa kumkaribisha Mh. Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa hifadhi ya mazingira (NEMC) Dkt Gwamaka Mafwenga alisema kuwa ziko Kampuni sita ambazo makontena yao yalikamatwa Bandarini na yalikua yakifanyiwa uchunguzi. Makampuni hayo ni J. M Kambi and General Services(makontena 88), JBR Group of Companies(makontena 35), Villa Plast L.td(makontena 3) , Three Star Metal Group(makontena 12) na Steel Com Ltd(makontena 2).

Waziri Simbachawene alifanya ukaguzi katika bandari ya Dar Es salaam na kuagiza makontena yote ya Kampuni tajwa hapo juu yaliyokua yamebeba shehena ya vyuma chakavu kuzuiliwa kusafirisha bidhaa hizo na kufanyike uchunguzi wa haraka sana juu ya makontena hayo.

RAIS DKT MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE MIKOA YA KUSINI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akifurahia na wananchi wa Lukuledi wilayani Masasi Mkoani
Mtwara wakati akiendelea na ziara yake mikoa ya kusini Leo Oktoba 16,
2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Lukuledi Maalumu wenye ulemavu wa kusikia wakati aliposimama kusalimia wananchi wa Lukuledi wilayani Masasi Mkoani Mtwara wakati akiendelea na ziara yake mikoa ya kusini Leo Oktoba 16, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiserbuka na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Rw3angwa mkoa wa Lindi wakati akiendelea na ziara yake mikoa ya kusini Oktoba 18, 2019

Picha na IKULU

WASHINDI WA TIGOPESA WAKALA PROMOSHENI WAKABIDHIWA ZAWADI

$
0
0


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo, Angelica Pesha (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 5/- kwa mshindi wa kwanza promosheni ya 'Tigopesa Wakala', Suleiman Husein kutoka Zanzibar katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi watatu wa promosheni hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo, Angelica Pesha (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2/- kwa mwakilishi wa mshindi wa tatu wa promosheni ya 'Tigopesa Wakala', Anna Mosha katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi watatu wa promosheni hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa.
Washindi wa promosheni ya Tigopesa Wakala wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo, Angelica Pesha (kulia) na Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa (kushoto).
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo, Angelica Pesha (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3/- kwa mshindi wa tatu wa promosheni ya 'Tigopesa Wakala', Vicky Ibrahim katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi watatu wa promosheni hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa.



Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi watatu wa promosheni ya Tigopesa Wakala, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa (kushoto). 



Dar-es-Salaam Oktoba 16, 2019. Kampuni ya simu ya Tigo leo imetoa zawadi kwa washindi watatu wa promosheni ya tatu ya mawakala wa Tigo Pesa ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa mawakala wao nchi nzima.

Promosheni hiyo ijulikanayo kama ‘Tigo Pesa Wakala promosheni’ ilianza mwezi Septemba 2019 ambapo washindi 12 wametoka katika kanda nne za Tigo(kanda ya Ziwa, Pwani, Nyanda za juu kusini na Kaskazini).

Promosheni hii ni kwaajili ya kutoa shukrani kwa mawakala wa Tigo Pesa zaidi ya 100,000 nchi nzima.Promosheni hiyo ambayo inafayika kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja inamzawadia wakala ambae amefanya miamala mingi katika kanda yake kwa mda wa mwezi mmoja.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Kaimu Mkuu wa kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema “Kwanza niwashukuru na kuwapongeza sana mawakala wetu wote kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia wateja nchi nzima na pili niwapongeze mawakala hawa watatu kwa kuibuka na ushindi kwa kuwapiku maelfu ya mawakala kweye mikoa yao.”

Pesha alisema huduma ya Tigo pesa imekuwa zaidi ya mfumo wa kutuma na kupokea pesa bali ni sehemu ya shughuli zilizoanzishwa na Tigo Pesa katika kuhakikisha inachangia agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi hapa nchini hasa kwa njia ya kuwawezesha mawakala wa Tigo Pesa.

“Kama kampuni ya kidigitali tunahakikisha tunakuja na mikakati mbalimbali ambayo itawafanya mawakala nchi nzima kunufaika na huduma hii.Tuna furaha kuchangia agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kupitia huduma ya Tigo Pesa kwa kurahisisha huduma za kifedha jambo linalochochea ukuaji wa uchumi kwa mawakala, jamii pamoja na nchi kwa ujumla,” alisema Pesha.

Baaa ya kutangazwa,washindi walijawa na nyuso za furaha akiwamo Suleiman Hussein kutoka Zanzibar aliyeshinda Sh5 Milioni, Vicky Ibrahim wa Temeke aliyeibuka na Sh3 milioni na Anna Mosha kutoka Ilala aliyejishindia Sh2 milioni.

Tigo Pesa inashika nafasi ya pili hapa nchini kama mtoa huduma za kifedha mkubwa kwa njia ya simu. Tigo Pesa pia imefungua milango ya ugunduzi wa kidijitali Afrika Mashariki ikiwa ni kampuni ya kwanza kuanzisha huduma ya kutuma fedha kwa njia ya simu kwa nchi nyingine, kutuma pesa kwenda mitandao mingine na kuingia kwenye pochi moja, huduma ya jihudumie mwenyewe pamoja na App ya kisasa ya Tigo Pesa inayorahisha sana kufanya miamala.

Ikiwa imezinduliwa mwaka 2010, Tigo Pesa imepiga hatua kutoka kuwa huduma za kutuma na kupokea pesa hadi kutoa huduma zote za kifedha ikiwamo malipo ya kibishara suala linalochangia ustawi wa watu kiuchumi nchini.

Tigo Pesa ni huduma ya kifedha inayokua kwa kasi zaidi nchini ikiwa na wateja waliosajiliwa zaidi ya 7 milioni na wafanyabiashara 50,000 pamoja na mawakala zaidi ya 100,000 nchi nzima.

KASI YA KUJIANDIKISHA CHALINZE YAMRIDHISHA DAS.

$
0
0
Na Shushu Joel

KATIBU tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kasilda Mgeni amefurahishwa na wananchi wa halmashauri ya chalinze kwa kuweza kuitikia wito wa kujiandikisha kwenye daftali la kupiga kura.

Wananchi wamekuwa mstali wa mbele katika zoezi la kujiandikisha kutokana na uelewa wa kutumia fursa ya kuwachagua viongozi wao.

Akizungumza na baadhi ya wananchi katika moja ya vituo vya kujiandikishia alivyotembelea kwenye kata ya ubena,halmashauri ya chalinze katibu tawala huyo aliwapongeza wananchi waliojiandikisha na kuwataka wawahamasishe na wenzao ambao bado ili nao wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa na vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi na moja.

"Kwa kweli chalinze wananchi hongereni sana kwa kujiandikisha kwa wingi nadhani kufikia mwisho wa zoezi hili mtakuwa mmevuka lengo lenu" Alisèma.Aidha Mgeni amempongeza mbunge wa jimbo la chalinze mh Ridhiwani Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhamasisha wananchi wake ili wakajiandikishe.

Aliongeza kuwa Kikwete ni kiongozi wa pekee aliyefanikisha kazi ya hamasa kwa wananchi kwani watu wamejitokeza na wanazidi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha na kwa baadhi ya vituo kuonekana wamemaliza kuandikisha huku wakiwa wamevuka malengo yaliyokuwa yamekusudiwa.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa ujio wa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na katibu tawala imemuongezea nguvu na mzuka zaidi.

Alisema kuwa wananchi wa chalinze wamehamasika wenyewe mara baada ya kutangaziwa na gari maalum lililotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwahamasisha wakazi wa chalinze kuweza kujitokeza.Aidha Aliongeza kuwa kila kazi inachangamoto zake lakini kwa chalinze changamoto kubwa ni mfululuzo wa mvua zilizokuwa zikinyesha hivyo kupelekea wananchi kutojitokeza huku wengine wakiwa mashambani. 

"Kwa jinsi hali inavyoelekea wanachalinze tutavuka malengo tuliyokuwa tumejiwekea kwani kwa sasa tuna zaidi 80% huku siku chache zikiwa zimebaki.Naye msimamizi mkuu wa uchaguzi katika halmashauri hiyo Shabani Milao amempongeza mbunge kwa jinsi alivyojitolea kutoa hamasa kwa wananchi katika zoezi zima la kujiandikisha.

Aliongeza kuwa zoezi linaenda vizuri na kile kichokuwa kimekusudiwa na serikali.

ULINZI NA USALAMA WAKATI WOTE WA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA NA KUPIGA KURA KUIMARISHWA MKOANI ARUSHA

$
0
0


Na Ahmed Mahmoud Arusha

JESHI la polisi mkoa wa Arusha,limewahakikishia wananchi kwamba litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote wa zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa zoezi ambalo limeanza Oktoba 8 na litakalohitimishwa Oktoba 17 saa 12 jioni.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana, ameyasema hayo leo ofisini kwake mara baada ya kukamilisha ziara ya kuangalia hali ya usalama kwenye vituo vya kujiandikisha wapiga kura katika jiji la Arusha.

Alisema kuwa jeshi la polisi litaendelea kuimarisha usalama na hivyo kuwezesha wananchi kujiandikisha na kuhakikisha kuwa kipindi chote cha kampeni mpaka uchaguzi na kutangazwa matokeo hakuna matukio ya jinai ambayo yanalenga kuvuruga zoezi hilo.

Kamanda Shana,akisema kuwa amekuta zoezi likiwa limedorora na hivyo akatoa wito kwa wananchi watumie muda wa nyongeza wa siku tatu uliotolewa na serikali ili waweze kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili wawachague viongozi wao .

Kamanda,Shana,alisema serikali imeongeza siku tatu ambapo zoezi hilo lilikuwa lifikie mwisho Oktoba 14 sasa limesogezwa mbele hadi Oktoba 17 saa 12,000 jioni kutokana na kubainika kuwa wananchi wengi walikuwa hawajajitokeza kujiandikisha .

Alisema kuwa jeshi la polisi litaendelea kuimarisha usalama na hivyo kuwezesha wananchi kujiandikisha na kuhakikisha kuwa kipindi chote cha kampeni mpaka uchaguzi na kutangazwa matokeo kutakuwa salama.

Kamanda,Shana,alisema hadi sasa hakuna tukio lolote la uhalifu ambalo limetokea kwa ajili ya kuvuruga zoezi hilo na kuonya kuwa jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakae jihusisha na uvunjifu wa amani kwa kufanya makosa ya jinai.

Amesema katika kuhakikisha usalama unaimarishwa jeshi la polisi litatumia vitabu vitatu ambavyo ni kuzingatia kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka 2019,mwongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa pia watazingatia sheria na taratibu za polisi zilizoko kwenye mwongozo wa jeshi hilo yaani PGO ,wakati wote wa kampeni kupiga kura, kutangazwa matokeo.

Alisema wasimamizi wa uchaguzi kwenye halmashauri zote za wilaya katika mkoa wa Arusha watawasilisha ,miongozo,kanuni na taratibu za uchaguzi kwa wakuu wa polisi wa wilaya OCD ili kuhakikisha kuwa usalama wakati wote wa uchaguzi huo unakuwepo na unaenda bila viashiria vya uvunjifu wa amani.

WAALIMU RUDISHENI NIDHAMU MASHULENI KWA WANAFUNZI WATOVU WA NIDHAMU

$
0
0

Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Gabriel Daqarro awataka walimu wa shule zote jijini hapa kutosita kuwaadhibu kwa viboko wanafunzi wenye nidhamu mbaya ili kurejesha nidhamu Mashuleni jambo litakalosaidia kuongeza ufaulu.

Gaqarro ametoa rai hiyo wakati akiongea na walimu wa shule mbalimbali za jiji la Arusha katika maadhimisho ya siku ya walimu duniani yanayofanyika Oktoba 5, kila mwaka ,yaliyoenda sanjari na kutoa zawadi za fedha tasilimu na vyeti kwa shule na walimu waliofanya vizuri.

Amesema suala la utii na nidhamu Mashukeni halina mjadala , hivyo walimu wanao wajibu wa kutumia viboko pale kunapolazimika bila kumwonea mwanafunzi na wasikubali wanafunzi kuwazoee.

“Ninacho waomba walimu ,mrejeshe nidhamu kwa wanafunzi na msikubali kuzoeana sana na mwanafunzi ,hiyo itasaidia ila msimwonee mwanafunzi na kutumia nguvu kupita kiasi hapo utakuwa umetenda jinai” Amesema Daqarro.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo aliagiza kutohamishwa ovyo kwa walimu bila kupewa fedha za uhamisho huku akiwataka walimu wanaoidai serikali kuwa wavumilivu wakati madai yao ya msingi yanashughulikiwa .

Awali walimu hao kupitia risala yao iliyosomwa na katibu Mkuu wa Chama cha walimu mkoa wa Arusha,CWT,Abraham Kamwela wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabilib ikiwemo mazingira ya kazi yao.

Pia wamedai kucheleweshewa kubadilishiwa mishahara yao kwani tangu wamepewa barua za mabadiliko ya mishahara bado mabadiliko hayo hayajafanyika ikiwemo suala la kupandishwa madaraja.

Aidha wameiomba halmashauri ya jiji la Arusha kuwakopesha viwanja ili wajenge nyumba za kuishi kwani baadhi yao wanaishi kwenye mazingira magumu na kujikuta wakikosa morari wa kufundisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,Dkt Maulid Madeni pamoja na kuwapongeza walimu hao kwa jitihada zao na kuufanya mkoa wa Arusha kuwa kinara wa ufaulu kitaifa amewaomba walimu hao wazidi kujituma zaidi huku akiahidi mazingira mazuri zaidi ya kazi yao.

Hata hivyo dkt Madeni amewatupia lawama kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo kwa kutowatendea haki walimu hao kwa kufanya mkutano wao usiku huku wakinyeshewa mvua na kung’atwa na mbu jambo ambalo aliahidi kipindi kijacho halmashauri yake itatoa fedha ili wafanyie kwenye kumbi za kisasa.

Dkt Madeni amewataka walimu hao kumkumbuka mwasisi wa taifa hili Hayati Mwl.Julius Nyerere ambaye ndio baba wa taifa hili aliyewatoa wananchi wake kwenye ujinga kwa kuhimiza elimu.

Amewataka pia walimu kumkumbuka rais John Magufuli ambaye serikali yake imefuta ada kwa shule zake nchini jambo ambalo limeongeza morari kwa wazazi kupeleka watoto wao kusoma.

Katika hatua nyingine dkt Madeni amesisitiza walimu kujiandikisha ili kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Gabriel Daqarro 

BRELA KURASIMISHA HUDUMA ZA BIASHARA JIJINI DODOMA

$
0
0
Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Emanuel Kakwezi akizungumza

WAKALA wa Usaji wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) unatarajiwa kutoa huduma za urasimishaji wa biashara Octoba 18 na Octoba 19 Jijiji Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma wakati wa Fursa 2019

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Emanuel Kakwezi ambaye pia alifanya ukaribisho kwa wana Dodoma alisema watatoa huduma mbalimbali wakati wa fursa 2019 huku wakiwataka wakazi wa mkoa huo kuchangamkia fursa hiyo muhimu

Alisema kwamba huduma ambazo zitatolewa wakati wa Fursa Dodoma ni usajili wa Majina ya Biashara, Kampuni, Nembo za Biashara na huduma, Hataza, Leseni Daraja A, 
Leseni za Viwanda.

Kaimu Mkurungezi Mkuu alisema wameamua kishiriki kwenye Fursa mwaka huu kutokana uhitaji wa wananchi juu ya ujarasimishaji Biashara zao Pia wameamua kushiriki kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Leta Solution” ikiwa kama Taasisi ya Brela ni moja ya solution kwenye Biashara na ubunifu wa wasajiriamali ili kuendana na Serikali ya Viwanda ya sasa

Kikubwa zaidi kilichofanya kushiriki ni kuwafikia wananchi kwa ukaribu 
zaidi na kuwahidumia kwa ukaribu zaidi

Kakwezi alisema Brela pia itashiriki kwenye Fursa mikoa yote ambayo imebaki baada ya Dodoma na watakuwa wanatoa huduma zote zinazotolewa na Brela, ambapo mikoa hiyo ni Tanga, Arusha na Dar Es Salaam 

Hata hivyo alitoa rai kwa wananchi wote kutumia fursa hii ili kuweza kupata huduma za Brela kwani kutakuwa na team ya Brela ambayo itatowa huduma zote na wananchi watakao kidhi masharti kama ya kuwa na Namba ya Kitambulisho cha NIDA na vingezo vingine wataweza kuondoka na vyeti vya Usajili

Dar yatajwa kuongoza zoezi la uandikishaji, Jiji la Arusha laendelea kushika mkia

$
0
0
Dar yatajwa kuongoza zoezi la uandikishaji, Jiji la Arusha laendelea kushika mkia

Charles James, Michuzi TV

JIJI la Dar es Salaam limetajwa kuongoza katika zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku Jiji la Arusha likiendelea kushika mkia.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza wakuu wa Mikoa na viongozi wote kwa namna ambavyo wamekua wakihamasisha zoezi hilo.

Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Mkurugenzi wake kujitathimini kutokana na Jiji hilo kushindwa kufikisha lengo lililopangwa ambapo mpaka leo wameshindwa kufikia asilimia 50 ya uandikishaji.

" DC Arusha, Mkurugenzi, msimamizi wa uchaguzi wana jambo LA kujitathimini mpaka takwimu ya jana hawajafika asilimia 50 wako asilimia 37. Wengine ni Moshi lakini hawa wamefika angalau asilimia 51 wamefikia lengo kidogo. Wamejitahidi.

Halikadhalika Korogwe mjini wamejitahidi sana, kwahiyo Manispaa ya Moshi na Korogwe Mji wako asilimia 51 lakini Jiji LA Arusha kwa kweli viongozi wao wanapaswa kuongeza hamasa ili kufikia walau asilimia tulizojiwekea," Amesema Waziri Jafo.

Amewashukuru viongozi wa Kiserikali, Kisiasa na wadau wote kwa namna ambavyo wameshirikiana kuhamasisha zoezi hilo huku akisema uchaguzi huu unaweka historia ya kuwa uchaguzi ambao wananchi wanapata ujumbe wa kutosha na maandalizi yake yamekua makubwa zaidi.

Waziri Jafo amesema baada ya siku ya kwanza ya nyongeza baada ya zoezi hilo kuongezewa siku tatu idadi ya waliojiandikisha imeongezeka hadi kufikia Milioni 16.9 sawa na asilimia 74 ya lengo.

" Kwa mara ya kwanza tukumbuke uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 malengo yalikua kuandikisha watu Milioni 18.7 lakini waliokua wameandikishwa ni Milioni 11.8 sawa na asilimia 63 ya lengo. Mwaka huu kufikia Oktoba 14 kabla ya ile nyongeza watu waliokua wameandikishwa ni Milioni 15.9 sawa na asilimia 68 ya lengo hivyo mtaona tulizidi hata uandikishaji wa mwaka 2014," Amesema Jafo.

Aidha Waziri Jafo amesema siyo kweli kwamba watumishi wa Serikali wamekua wakilazamishwa kujiandikisha kama ambavyo wanasiasa wamekaririwa wakisema bali kinachofanywa na Serikali ni kuhamasisha zoezi hilo na kutoa elimu juu ya faida za kujiandikisha na kwenda kupiga kura.

Ameitaja Mikoa iliyofanya vizuri kuwa ni pamoja na Dar es Salaam yenye asilimia 89, Pwani asilimia 86, Tanga wakiwa nafasi ya tatu. Kwa upande wa mikoa ambayo inashika mkia licha ya kufikia asilimia 50 ni Mkoa wa Kigoma wenye asilimia 57, Kilimanjaro asilimia 58 mikoa ya Arusha na Shinyanga ikiwa na asilimia 66.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma wakati akitoa tathimini ya zoezi la uandikishaji wa wananchi kwenye orodha ya wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Waziri Ndalichako atilia shaka gharama za ujenzi Chuo cha Ualimu Kasulu

$
0
0
Wakati Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga kilichopo Wilayani Kasulu mkoani Kigoma ukiendelea kwa kusuasua Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku 15 kwa Mshauri Elekezi BICO kupitia upya gharama za ujenzi wa mradi huo ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni kumi ili kujiridhisha kama fedha hiyo inaendana na ukubwa wa mradi.

Prof. Ndalichako ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mradi huo ambapo pamoja na kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi ametilia shaka gharama ya ujenzi ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni kumi kutumika ndivyo sivyo kutokana na aina ya majengo yanayojengwa katika chuo hicho kuwa ya thamani ndogo.

"Hivi ni vighorofa mtoto na narudia ni vighorofa mtoto huwezi kuniambia kwamba majengo haya ambayo kwanza ni machache, pili siyo ghorofa zile kubwa kama tulizojenga katika miradi mingine tena kwa gharama ndogo ya shilingi bilioni sita zinazidiwa na vighorofa hivi hapa kuna kitu hakipo sawa nataka ndani ya siku kumi na tano gharama za mradi zipitiwe upya kwa kila jengo na nipewe taarifa vinginevyo mratibu wa miradi hii utafute kazi nyingine," amesema Prof. Ndalichako.

Kuhusu kusuasua kwa Mradi Waziri Ndalichako amemtaka Mkandarasi huyo ambaye ni Kampuni ya SUMA JKT kuongeza kasi ya kufanya kazi akisisitiza ziletwe mashine za kisasa ambazo zitarahisisha kazi pamoja na kuongeza vibarua kwenye eneo la kazi.

"Huwezi kutekeleza mradi wa zaidi ya shilingi bilioni kumi kama nyumba yako unayojenga, yaani una kamashine kamoja tena kakusukuma,vibarua wenyewe inaonekana umewaleta leo baada ya kusikia nakuja kukagua, hii haikubaliki tunataka kazi ifanyike usiku na mchana kwa sababu pesa zipo lazima mradi ukamilike haraka," amesema Waziri Ndalichako.

Mapema akitoa taarifa ya mradi huo, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT, Luteni Kanali Onesmo Njau amesema mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia thelathini na kudai kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo usumbufu wa kupata vifaa vya ujenzi kama saruji na mchanga.

"Mheshimiwa Waziri tulikuwa tukitegemea kupata saruji kwa kampuni ya Dangote lakini kwa sasa inabidi tufuate wenyewe Dodoma na hivyo kutumia muda mwingi kusubiri vifaa vifike kwenye eneo la mradi," amesema Kanali Njau.

Naye mshauri elekezi wa mradi huo kutoka BICO, Fred Munishi amekiri kuwa kazi inasuasua na kusema kuwa tayari ametoa maelekezo kwa Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi taarifa ambayo hata hivyo imeonekana kukinzana na taarifa ya Mkandarasi na hivyo kutakiwa kufanya kazi kwa karibu na Mkandarasi.

"Inaonekana hapa hakuna maelewano mazuri baina ya Mkandarasi na mshauri elekezi, sitaki mivutano kazini kaeni pamoja fanyeni kazi ya serikali na mkiendelea hivi tutawaondoa," amesema Waziri Ndalichako.

Akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Waziri Ndalichako pia amekagua miradi mingine minne ya elimu katika shule za sekondari na msingi za Kigodya, Ruhita, Nyantare na Kasyenene na kueleza kuridhishwa na kazi huku akisisitiza kuwa serikali inatoa fedha ili kuona matokeo.

Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako ameambatana pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Dkt. AveMaria Semakafu pamoja na Mratibu wa Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo pamoja na ule wa TESP.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akikagua ujenzi moja ya jengo katika shule ya sekondari Kasangezi iliyoko Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Injinia wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga akimuonesha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako namna chuo cha Ualimu Kabanga kitakavyoonekana baada ya ujenzi kukamilika

WAKULIMA WA KOROSHO NACHINGWEA KUANZA KUNEEMEKA WIKI IJAYO

BAJAJ YA MAXIMA 3 YAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
WASAMBAZAJI wa pikipiki za miguu mitatu maarufu kama bajaj wa mikoa yote hapa nchini wamejumuika na kampuni ya Sunbeam jijini Dar es Salaam leo kuzindua bajaj mpya aina ya Maxima Z 3 ya ikiwa ni katika mwendelezo wa uboreshaji soko la bajaj sasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Mauzo wa kampuni ya Sunbeam, Jestas Kyolike amesema kuwa ameweza kuwaita wasambazaji wa mikoani ili kuja kushiriki pamoja uzinduzi wa bajaj mpya ili waweze kusambaza mikoa mingine.

"Bajaj iliyozinduliwa leo ni bajaj ya kisasa kabisa haijawahi kuwepo hapa Tanzania ni bajaj ambayo ina ingine kubwa na inanafasi kubwa inaweza inaweza ikapita kwenye aina za barabara zetu za Tanzania"
Amesema Kyolike.

Hata hivyo baadhi ya wasambazaji wa bajaj katika Mikoa ya Tanzania wamesema kuwa babaj inaweza kumwinua Mjasiliamali kiuchumi hasa akinunua kwaajili ya biashara ya kubeba abiria katika maeneo yake ya biashara bila kuwa na kikwazo cha jua ama mvua.

 Bajaj aina ya Maxima Z 3 baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa babaj aina ya Maxima Z 3.


 Baadhi ya wasambazaji wa bajaj katika mikoa tofauti hapa nchini wakishuhudia uzinduzi wa babaj aina ya Maxima Z 3 jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Mauzo wa kampuni ya Sunbeam, Jestas Kyolike  akizungumza na wafanyabiashara wa bajaj wa mikoa ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo. 
 Baadhi ya wasambazaji wa bajaj.

Meneja Mkuu wa Kitengo cha Ufundi wa Kampuni ya Sunbeam, akizungumza ni namna gani wanafanya matengenezo ya bajaj zikiharibika pamoja na kukabiliana na changamoto ya kupatikanaji wa vifaa baada ya bajaj kuharibika.

WAFANYAKAZI WATATU WA TIGO NA WAFANYABIASHARA WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA KWA KOSA LA KUTAPELI WATEJA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
WAFANYAKAZI watatu wa kampuni ya simu za mkononi Tigo, na wafanyabiashara wawili, wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi sita nje baada ya kukiri na kutiwa  hatiani kwa kosa la kutapeli wateja wa mtandao huo kwa njia ujumbe wa maandishi.

Wafanyakazi wa Tigo kutoka tawi la  Mlimani City  na Makao Makuu ya Kampuni hiyo waliohukumiwa ni Kokubelwa Karashani, Godfrey Magoye na Khalfan Milao ambao ni watoa huduma kwa wateja huku washitakiwa wengine ni Mohamed Abdallah na Moses Kilosa (mume wa Karashani) ambao walikuwa hawana kazi lakini walikuwa marafiki wa wafanyakazi hao wa Tigo.
 Hukumu hiyo imesomwa leo Oktoba 16, 2019 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambae,  amewatia hatiani washitakiwa hao baada ya kukiri kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hukumu hiyi, hakimu Rwizile amesema amesikiliza hoja za pande zote  na kwamba makosa waliyofanya washitakiwa si mepesi na kwa mujibu wa sheria anayepatikana na hatia katika makosa hayo anatakiwa kutumikia kifungo  hivyo, lazima adhabu kali itolewe ili kupunguza makosa ya mtandao.

Amesema washitakiwa watatakiwa kutumikia kifungo cha miezi sita nje na pia  simu 31 na laini zake pamoja na sare ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) vinataifishwa na kuwa mali ya serikali.

Kabla ya kutolewa kwa  adhabu hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa alidai washitakiwa waliingia makubaliano na DPP hivyo hawatarajii wapewe adhabu kubwa.
Katika utetezi wao,washitakiwa hao   waliiomba mahakama iwahurumie na kuwapa adhabu ndogo kwani hilo ni kosa lao la kwanza.

Awali Mbagwa alisoma hati mpya ya mashitaka ambapo mashitaka matano likiwemo la kutakatisha fedha liliondolewa na kusomewa mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma mashitaka hayo, Mbagwa amedai Januari Mosi 2018 na Juni 20,2019 maeneo ya Dar es Salaam na Arusha walijipatia  Sh 20,378,627 kutoka kwa wateja mbalimbali wa tigo kwa kutoa kwenye akaunti zao zao za Tigopesa bila idhini.

Mashtaka yaliyoondolewa  ni, kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti za wateja ,kuingilia mifumo ya kifedha ya Tigo pesa bila kibali, kupatikana na mavazi ya JWTZ.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images