Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

WAZIRI KALEMANI ASIKITISHWA KWA KUTOKUUNGANISHWA KWA UMEME KWA TAASISI ZA UMMA

0
0
WAZIRI wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameeleza kusikitishwa kwake na suala la Taasisi za umma na maeneo yanayotoa huduma za kijamii kutounganishiwa umeme katika baadhi ya vijiji nchini huku nishati hiyo ikiwa tayari imefika kwenye vijiji hivyo.
Dkt. Kalemani aliyasema hayo tarehe 16 Oktoba, 2019, wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme kwenye baadhi ya vijiji akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Eng. Zephania Chaula, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya na watendaji kutoka TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Awali, taarifa ya TANESCO katika Wilaya ya Simanjiro ilieleza kuwa, mkandarasi wa umeme vijijini wilayani humo, tayari amewasha umeme katika vijiji 11 kati ya 21 alivyopangiwa lakini ni Taasisi chache za umma zimeunganishwa na umeme.
" Ina maana baadhi ya viongozi wa Vijiji na Halmashauri hawalipii umeme ili taasisi za umma na maeneo yanayotoa huduma za kijamii kama visima vya maji yaunganishiwe umeme, itabidi ifike mahala tuulizane na viongozi hawa kwa nini hawalipii umeme kwenye Taasisi zao." alisema Dkt Kalemani.
Kutokana na hilo, Dkt Kalemani aliendelea kuwasisitiza viongozi hao kote nchini,  kutenga fedha za kuunganisha umeme kwenye taasisi hizo ili umeme huo uweze kuleta tija kwa jamii.
Kuhusu usambazaji umeme wilayani Simanjiro, Dkt Kalemani alisema kuwa, Wilaya hiyo ina vijiji 56 na tayari vijiji 39 vimesambaziwa umeme ambapo aliagiza kuwa, ifikapo mwezi Disemba mwaka huu, vijiji vyote vilivyosalia viwe vimesambaziwa umeme.
Aidha, akiwa wilayani humo, Dkt Kalemani aliwasha umeme katika Kijiji cha Naepo na Nakweni ambapo aliagiza kuwa vitongoji vya Vijiji hivyo ambavyo havina umeme, visambaziwe umeme.
Kwa upande wake, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya, alimshukuru Rais, Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi inayofanyika ya usambazaji umeme vijijini na kueleza kuwa juhudi hizo zimepelekea umeme kusambaa katika maeneo mbalimbali nchini
Aidha, alimshukuru Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini bila kubagua maeneo na kueleza kuwa Wilaya hiyo imefaidika na miradi ya umeme vijijini kwani takriban asilimia 70 ya vijiji wilayani humo, tayari vina nishati ya umeme.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria kuwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Naepo wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara. Wa Tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Eng. Zephania Chaula na wa Pili kushoto ni Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya.
 aadhi ya wananchi katika Kijiji cha Naepo wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) aliyefika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme na kuwasha rasmi umeme kwenye kijiji hicho.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akivishwa vazi maalum la kimasai na kupatiwa fimbo maalum mara baada ya kufika katika Kijiji cha Naepo wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara ili kuwasha rasmi umeme.
Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nakweni wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara mara baada ya Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia kwa Mbunge) kufika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme. Kushoto kwa Mbunge ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Eng. Zephania Chaula.

WAZAZI WASHAURIWA KUCHANGIA CHAKULA CHA WATOTO WAKIWA SHULENI

0
0

Baadhi ya watoto wakila chakula shuleni.

Na Woinde Shizza Michuzi blog,Arusha
WAZAZI wameshauriwa kuwa na desturi ya kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao mashuleni ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwani watoto wengi wamekuwa wakifeli kutokana na utoro.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa shule ya sekondari Olmotonyi Forest iliyopo kijiji cha Emaoi kata ya Olmotonyi halmashauri ya Arusha, Anna Minja wakati akizungumza na wazazi na wanafunzi katika mahafali ya 4 ambapo jumla ya wanafunzi 141 walihitimu .

Anna amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikizikabili shule nyingi ni kutokana na wazazi kutochangia fedha kwa ajili ya chakula cha mchana kwa watoto wao hali ambayo huchangia kuwepo kwa utoro kwa watoto ambao hawali mashuleni.

Amesema kuwa kutokana na baadhi ya wazazi wengi kutokuwa na mwamko wa kuchangia chakula mashuleni, kumekuwa kukichangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kuwepo kwa division ziro shuleni hapo, hivyo amewaomba wazazi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya elimu ya watoto wao kwa kuchangia fedha kwa ajili ya chakula ili watoto waweze kusoma kwa utulivu.

"Kwa kweli uwepo wa baadhi ya wazazi wengi kutochangia chakula cha mchana kwa ajili ya watoto wao ndio wamekuwa wakichangia shule yetu kupata wanafunzi wenye division ziro, kwani wengi wa wanafunzi wanaopata ziro na wale ambao hawali chakula cha mchana hapa shuleni, hivyo tunawaomba sana wazazi wachangie chakula cha watoto ili tuhakikishe tunafuta division ziro."alisema Anna.

Aidha amesema kuwa shule hiyo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa sita ,nyumba za walimu saba,maabara moja,bwalo la chakula, vyoo vya wasichana, maktaba, pamoja na walimu wa masomo ya Sayansi.

"Tunaomba serikali utusaidie ujenzi wa mabweni mawili kwa ajili ya wavulana kwani mabweni yaliyopo ni kwa ajili ya wasichana tu,kwani wavulana wanaendelea kupata adha kubwa sana ya kuwahi shuleni kutokana na kutembea umbali mrefu ."alisema Anna.

Naye Meneja msaidizi wa Hifadhi ya misitu Meru/ Usa, Jeremiah Gumadi amewataka wanafunzi hao kujitahidi kusoma kozi mbalimbali za kujiajiri ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ajira iliyopo hivi sasa,huku akiwataka kutochagua kazi .

Aidha amewataka kujifunza zaidi maswala mbalimbali ya ujasiriamali ambayo yatawawezesha wao kuweza kujiajiri wenyewe na kujipatia kipato badala ya kutegemea kuajiriwa.

Kwa upande wa wanafunzi waliohitimu, Hawa Jaffary na Charles Mbowe wamesema kuwa, kitendo cha kuwepo kwa shule katika mazingira hayo kumeleta manufaa makubwa kwa jamii hiyo kwa kuondoa mrundikano wa wanafunzi katika shule zingine za kata.

BENKI YA NMB YAZINDUA MALIPO YA MASTERCARD KWA BODABODA

0
0

BENKI ya NMB imezindua malipo ya kimtandao kwa huduma za bodaboda ambapo mfumo huo wa malipo ni wa aina yake na wa kwanza nchini Tanzania ambao unawawezesha abiria na wateja wa bodaboda kulipa nauli zao kwa kutumia simu zao za mkononi na fedha hizo kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya NMB ya dereva husika.

Kwa mujibu wa benki hiyo huduma hiyo iliyozinduliwa jana ni mwendelezo wa juhudi za kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanatumia huduma za benki sambamba na kuhamasisha utunzaji fedha kwa njia salama na za uhakika.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa huduma hiyo inaweka msingi wa kurasimisha sekta ndogo ya usafiri wa bodaboda.

"Mnachokifanya leo kina baraka zote za Serikali. Hiki kitawasaidia vijana kuongeza umakini kwenye shughuli zao na kuchangia uchumi wa Taifa," amesema Mhagama.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema huduma hiyo inatoa fursa kwa maelfu ya madereva wa bodaboda nchini kutumia huduma za benki hatua ambayo itaimarisha usalama wa fedha zao pamoja na wao wenyewe.

“Hii ni namna bora zaidi ya kurudisha uwajibikaji kwa shughuli za madereva wa bodaboda ambao mchango wao kwenye uchumi wa Taifa unatambulika,"amesema na  kuongeza huduma hiyo itaanza kwa Jiji la  Dar es Salaam kisha itaenda Mwanza, Arusha, Ruvuma, Dodoma na Mbeya wiki chache zijazo.

 Zaipuna ameongeza kuwa mfumo huo wa malipo utawasaidia madereva bodaboda kukuza biashara zao kwa kuwapunguzia adha ya kuhifadhi fedha taslimu na kuwapa fursa ya kuepuka matumizi yasiyokuwa na mpangilio.

“Kwa kutumia MasterCard QR, tunatoa huduma ya uhakika wa malipo kwa madereva bodaboda kutoka kwa watoa huduma wote na benki za biashara wanaotumia huduma hii.

" Malipo yatafanywa kwa kutumia simu ya mkononi yenye programu ya MasterCard QR na kupunguza hatari za kumiliki fedha taslimu. Huduma hii kwa bodaboda ni sehemu ya mkakati wa benki kufikisha huduma zake kwa watu wengi zaidi,” amesema Zaipuna .

Wakati huo huo Mwakilishi wa MasterCard Tanzania  Frank Molla amesema mfumo huo wa malipo ya kidijiti unakusudia kuwapa uhuru dereva na abiria wake wakati wote wa safari huku ukimuepushia dereva uwezekano wa kuporwa au kupoteza fedha zake.

“MasterCard inakusudia kuhamasisha na kuwezesha malipo ya kidijiti hapa nchini. Benki ya NMB inayo dira inayofanana nasi katika ujenzi wa miundombinu itakayoiwezesha jamii kufurahia ulimwengu wa malipo ya kimtandao kwa kutumia teknolojia ya kisasa,” amesema.

Tayari Benki ya NMB imewajengea uwezo zaidi ya madereva 1,000 wa jinsi ya kutumia QR kufanikisha malipo kwa kutumia simu za mkononi. Mfumo huo unatarajiwa kuongeza usalama wa malipo ya kimtandao kwa sekta hiyo ndogo ya watoa huduma.

Kumlipa bodaboda, abiria anatakiwa kwenda kwenye simu yako – NMB Mkononi, piga *150*66# kupata menu na kuchagua kufanya malipo halafu ‘Scan to Pay.’ Pia ukiwa na simu janja nenda kwenye programu (App) ya NMB Mkonini ambako atachagua ‘Scan to Pay’ na kuendelea na maelekezo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwa kwenye boda boda baada ya kuzindua Mastaboda ambao ni mpango maalum wa benki ya NMB kwa kushirikiana na Mastercard ambao utawawezesha waendesha boda boda kukopa piki piki ,wengine ni kaimu Mkurugenzi mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna,Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma makao Makuu ya Usalama Barabarani ,Mrakibu wa Polisi Abel Swai.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwa kwenye boda boda baada ya kuzindua Mastaboda ambao ni mpango maalum wa benki ya NMB kwa kushirikiana na Mastercard ambao utawawezesha waendesha boda boda kukopa piki piki ,wengine ni kaimu Mkurugenzi mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna,Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma makao Makuu ya Usalama Barabarani ,Mrakibu wa Polisi Abel Swai.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza mbele ya wageni waalikwa na Waendesha piki piki kutoka sehemu mbalimbali ndani ya jiji la Dar,kabla ya kuzindua huduma ya Mastaboda,jana jijini Dar.Huduma hiyo ni maalum kwa  waendesha boda boda.
Mgeni rasmi (wanne kushoto) ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiongoza uzinduzi wa huduma hiyo ya Mastaboda,jana jijini Dar.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna  akimshukuru Mgeni rasmi ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama  mara baada ya tukio la uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akifafanua jambo mbele ya Waendesha piki piki (hawapo pichani),kuhusu huduma ya Mastaboda,alisema kuwa huduma hiyo inatoa fursa kwa maelfu ya madereva wa bodaboda nchini kutumia huduma za benki, hatua ambayo itaimarisha usalama wa fedha zao pamoja na wao wenyewe.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa hudma hiyo ya Mastaoda.

HALI YA FOLENI KWA SASA JIJINI DAR, MVUA INAENDELEA KUNYESHA

0
0
JIJI la Dar es Salaam leo hali ya mvua imekuwa kizungumkuti na usafiri nao umekuwa shida kutokana na maji kutatapakaa kila mahali na hivyo kusababisha usafiri kuwa Mgumu kwa kuwa na foleni.

Kwa wanaopita barabara mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kuelekea eneo lenye ofisi nyingi la Posta chukueni tahadhali kabla ya kutoka kwa kuangalia ni barabara itakayokuwa na unafuu wa kufika eneo hilo.

Picha hapo juu inaonyesha rangi mbalimbali katika barabara za hapa mjini.
Rangi hizo  zinaashiria namna barabara ilivyo kwa sasa kwakuwa rangi nyekundu zaidi ya nyingine zote inaonyesha foleni ambayo inaenda lakini taratibu.

Hivyo chukua maamuzi ya kubadilisha njia kwa kuangalia yenye unafuu wa kufika mahali ambapo unataka kufika bila kupoteza muda mwingi.


Hivyo ndivyo hali ilivyo ya foleni.

Madhara ya Zebaki ni makubwa wananchi watakiwa kuwa makini.

0
0
 Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wananchi hususani wachimbaji wadogo wa dhahabu kuwa makini na matumizi ya Zebaki kwenye uchenjuaji wa madini hayo wakati Serikali ikitafuta njia mbadala ya kemikali hiyo.

Waziri Biteko ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) Mkoa Geita, kilichofanyika Oktoba 16, 2019.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwenye kikao hicho.
 Afisa Madini Mkazi Mkoa Geita, Daniel Mapunda akiwasilisha taarifa ya Madini ya Mkoa huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.

RC MAKONDA AMTAKA MKANDARASI KUKABIDHI JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA MWANANYAMALA KABLA YA DESEMBA 30.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  jana Oktoba 16,2019 ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Gorofa tano la Mama na Mtoto Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala na kumtaka Mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.

RC Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona hilo changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Aidha RC Makonda amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari.


Pamoja na hayo RC Makonda amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SEKTA ZA MAZINGIRA, MALIASILI NA UTALII NCHI ZA SADC

0
0
Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
IKIWA Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC wanaotekeleza Mkakati wa SADC kuhusu Usimamizi wa Sheria na Vita Dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori, inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Hayo yameelezwa katika taarifa kwa umma ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu iliyotolewa Oktoba 16. 

Taarifa hiyo inaeleza kuwa mkutano huo utafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuanzia tarehe  21 hadi 25 Oktoba, 2019.

"Madhumuni ya mkutano huu ni pamoja na kuangalia mwenendo wa hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi, kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira, kupitia Mkakati wa SADC wa Uchumi wa Bahari (SADC Strategy on Blue Economy); na kutathmini maendeleo katika sekta za misitu, wanyamapori na utalii".

Mkutano huo utahusisha Mawaziri wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utatanguliwa na mikutano ya wataalam wa sekta ya wanyamapori utakaofanyika tarehe 18 hadi19 Oktoba, 2019 na Mkutano  wa Makatibu Wakuu wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utafanyika tarehe 21 hadi 24 Oktoba, 2019.

 Aidha Mikutano hii miwili itajadili na kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 25 Oktoba, 2019 kwa maamuzi na maelekezo.

Mkutano wa Mawaziri  unatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ijumaa Oktoba 25, 2019, ukumbi wa mikutano wa AICC, Arusha na Mkutano wa Makatibu Wakuu unatarajiwa kufunguliwa na Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Oktoba 21, 2019 katika ukumbi wa AICC, Arusha.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Maeneo mengine yanahusu Programu za uhifadhi yaliyovuka mpaka wa nchi moja hadi nyingine kwenye maeneo ya misitu, uvuvi, mazingira na mabadiliko ya tabianchi, utalii, ukuzaji viumbe maji na Mkakati wa Ubora wa Afya wa wanyama wa majini (SADC Transfontiers Conservation Areas,forestry, fisheries, environment and climate change, tourism,  regional Aqua culture strategy and action plan, and SADC Aquatic Animal Health Strategy) pamoja na Programu ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.

Mapema mwezi Agosti mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la  uenyekiti wa Jumuiya hiyo. 

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ni moja kati ya jumuiya za  kikanda katika bara la Afrika. Jumuiya hii iliundwa kwa dhumuni la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi,  ulinzi, siasa na usalama.  Jumuiya hii inaundwa na  nchi wanachama 16 ambazo ni Angola, Botswana, Comoros, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

UJERUMANI YAMWANGA MABILIONI MFUKO WA BIMA YA AFYA NCHINI (NHIF).

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na Kaimu Balozi Bw. Jorg Herrera Wakionesha nakala za Mikataba ya Msaada baada ya kutia saini .Hafla hiyo fupi ilifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akisaini Mkataba wa Msaada wa Shilingi Bilioni 20 Kati yake na Kaimu Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bw.Jorg Herrera, Hafla hiyo fupi ilifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na akimpa mkono wa shukurani Kaimu Balozi Bw. Jorg Herrera mara baada ya kutia saini mikataba hiyo,hafla hiyo fupi ilifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam. Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya shughuli hiyo kuisha


………………………….


Na.Mwandishi Wetu –MAELEZO.

Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani limetoa msaada wa Euro milioni 8 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 20 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwaajili ya kuboresha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa msaada huo, Kaimu Balozi wa Ujerumani nchini Bw.Jorg Herrera amesema msaada huo ni kwaajili ya kuimarisha mfuko wa Bima ya Afya ili uweze kuwahudumia watanzania wengi zaidi hasa wale wa vijijini.

Amesema lengo la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani ni kuisaidia Serikali ya Tanzania katika azma yake ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Bima ya Afya ili hatimaye kufikia lengo la kutoa huduma ya Afya kwa wote .

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Doto James amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya Awamu ya Tano inajitahidi kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wake ili waweze kufanya kazi kwaajili ya kuelekea Tanzania ya Viwanda.

“Msaada huu ni wa masharti nafuu kabisa na hatulazimiki kulipa fedha yoyote, na sisi kama Serikali tumeupitia na kujiridhisha kwamba hauna chembe yoyote ya masharti ndio maana leo hii tumetoka hadharani kusaini ” Alisema.

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha alisema msaada wowote ambao serikali inapatiwa hupitiwa na wataalam makini ambao wanahakikisha hakuna masharti ambayo yatakuja kusumbua baadaye na pia ni kwa kuzingatia Sheria na Katiba ya nchi.Pia amesema kwa upande wa Ujerumani wamekuwa marafiki wazuri sana ambao mara kwa mara wameendelea kuisidia Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

Aidha Bw. James amesema uimarishaji wa mfumo wa TEHAMA katika mfuko wa Bima ya Afya una manufaa makubwa ikiwemo,kuongeza usajili wa wanachama wa bima ya Afya ikiwajumuisha walioko kwenye sekta isiyo rasmi pia kuboresha namna ya kuwatambua ,kuwasajili na kuwalipa watoa huduma.

Faida nyingine ni kuboresha utendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli zake za kila siku pamoja na kuwajengea uwezo wa watumishi wa mfuko wa Bima ya Afya.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeazimia kutoa huduma za Afya kwa wote na ili kufikia lengo hili, kuna mpango wa kuwa na mfuko mmoja wa Bima ya Afya utakaojulikana kama “Single Health Insurance Fund” (SNHIF) ambapo itakuwa ni lazima kila mtanzania kujiunga.

Serikali ya ujerumani siyo mara ya kwanza kuisaidia Tanzania, kwani imekuwa ikisaidia katika sekta za Maji, Nishati,Uhifadhi wa maliasili,Usimamizi wa fedha za umma pamoja na kuijengea uwezo Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania imeshuhudia mashirika ya kimataifa nchi mbalimbali pamoja na wahisani wakiendelea kumimina misaada kwaajili ya shughuli za maendeleo kutokana na uongozi wa Rais Dkt.John Magufuli , ambao umejitahidi kupambana na ufisadi na kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wengi.

MAVUNDE AWATAKA VIJANA KUJIAJIRI, AWAPONGEZA BENKI YA KCB

0
0
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , vijana na ajira, Anthony Mavunde(kushoto), akimkabidhi ruzuku ya gari aina ya kirikuu kwa Janeth Kipangula,mfanya biashara wa vifaa vya ujenzi wakati wa ambaye ni mmoja wa wanawake 256 ambao walipokea mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kupitiaprogramu ya 2jiajiri. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa KCBFoundation, Jane Mwangi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB,Cosmas Kimario(kulia).
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , vijana na ajira, Anthony Mavunde(kushoto), akimkabidhi ruzuku ya komputa na vifaa vingine nya ofisini kwa Halima Haji Sasya, ambaye ni mmoja wa wanawake 256 ambao walipokeamafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kupitia programu ya 2jiajiri.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa KCB Foundation, Jane Mwangi(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Cosmas Kimario(wa pili kushito).
 
Mwakilishi wa vijana wanaopokea mafunzo kutoka VETA na kudhaminiwa na Benkiya KCB, Nd. Baraka Konkara,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu yaKCB 2jiajiri Youth Scholarship kwa vijana inayoendeshwa na VETA nakudhaminiwa na Benki ya KCB katika hafla ya uzinduzi huo umefanyika jijini Dares Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya KCB, Cosmas Kimario,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarshipkwa vijana inayoendeshwa na VETA na kudhaminiwa na Benki ya KCB katika haflaya uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , vijana na ajira, Anthony Mavundeakizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarshipkwa wanafunzi wa Veta yaliyodhaminiwa na Benki ya Biashara ya KCB hafla yauzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amewataka vijana kuondokana na dhana ya kwamba ili waonekane wana ajira lazima wafanye kazi ofisini badala yake amewaasa wajiajiri na kufanya biashara.

Mavunde amesema kuwa Serikali inatarajia ifikapo mwaka 2025, asilimia 40 ya nguvu kazi ya nchi ambayo ni vijana itakuwa imeajiriwa katika sekta ya viwanda.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla iliyowakutanisha vijana zaidi ya 100 Waliochanguliwa kujiunga na programu ya Vijana 2jiajiri inayoratibiwa na Benki ya KCB,

Mavunde amesema Serikali inatengeneza mazingira wezeshi kwa vijana yatakayowasaidia Kuweza kujiajili na wengine kuajiliwa na kuongeza kuwa ukuaji wa viwanda nchini utafanikisha jambo hilo.

Amesema pamoja na serikali kutengeneza mazingira hayo vijana wanapaswa kuondokana na dhana ya kufikiria kwamba ili waonekane wana ajira ni lazima wafanye kazi maofisini badala yake amewataka wahakikishe wanajiajiri.

" Tatizo vijana wengi wanafikra mbaya ya kuajiriwa na wanawaza kuwa lazima wavae chati jeupe asubuhi suruali nyeusi na kwenda ofisini, mimi nawaomba wabadirike na waondokane na fikra hiyo kuanzia sasa, mnapaswa kujiajiri jamani kwa kufanya shughuli yeyote inayowaingizia kipato," amesema Mavunde.

"Tafiti za mwaka 2014 zinaonesha nchi inauwezo wa watu Milioni 24.3 wa kufanya kazi hivyo watu hawa kila mwaka wanaingia katika soko la ajira, kwahiyo wewe kijana ukikaa

nyumbani na kujiaminisha kuwa siku moja utaajiliwa Benki nikwambie unaendelea Kupoteza muda wako, tambua kuwa ajira aina mataili wala haiwezi kukufuata ulipo,"

Aidha amesema Serikali ya awamu ya tano inatambua elimu ya ufundi na ndio maana imetenga fedha kwa ajili ya kujenga vyuo vingi vya Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) ili wanafunzi wapate elimu na kuweza kujiajiri.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam, Violet Fumbo amesema programu ya Vijana 2jiajiri inayosimamiwa na Benki ya KCB ni mkombozi kwa vijana wengi kwani itawasaidia kuweza kupata elimu ya ufundi stadi itakayowawezesha waweze kufanyakazi.mbalimbali za ujasiriamali.

Amesema kijana yeyote atakayepata fursa ya kupata elimu ya ufundi na ujasiriamali anapaswa kuondokana na dhana ya kuajiliwa na kuongeza kuwa VETA ipo tayari

kushirikiana na KCB ili kuweza kuwasaidia vijana kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB,Cosmas Kimario amesema jumla ya Sh. Milioni 80 wamezitoa ili kuwasaidia vijana 123 kuwezakupata elimu ya ufundi stadi katika chuo cha VETA na baadae waweze kujiajiri.

NDALICHAKA ATOA SIKU 15 KWA SUMA JKT NA KAMPUNI YA BICO KUPITIA UPYA FEDHA SH.BILIONI 10 ZA MRADI WA UJENZI CHUO CHA WALIMU KABANGA,KASULU MKOANI KIGOMA

0
0
Moureen Rogath, Kasulu

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametoa  siku 15 Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), na  mhandisi mshauri Fred Abel kutoka kampuni ya BICO na mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa chuo cha ualimu Kabanga wilaya ya Kasulu, mkoa wa Kigoma kupitia upya fedha Sh. Bilioni 10 za mradi huo baaada ya kutowiana na majengo ya chuo hicho.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa majengo ya  chuo hicho amesema mbali na kutoa siku hizo pia Profesa Ndalichako amesikitishwa na kasi ya ujenzi wa chuo hicho na kusema umekuwa ukisua sua na kwenda polepole na kwamba wamekwamisha wanafunzi wa chuo hicho kuhamia kwa wakati.

Profesa Ndalichako amesema pamoja  na maagizo hayo pia ametaka kupatiwa gharama za ujenzi za kila jengo katika chuo hicho, huku akidai  ujenzi wa  majengo ya chuo hicho hauendani na kiasi hicho cha fedha ambazo tayari wameomba kwa serikali. 

"Kama chuo hichi kingewahi kumalizika haraka nilitamani walimu waweze kuhamia kutokana na majengo ya chuo wanachosoma sasa yapo hatarini kuwadondokea , "amesema profesa Ndalichako.Akitoa taarifa kwa waziri Ndalichako , Kaimu Mkuu wa Kanda ya ujenzi Luteni Kanali Onesmo Njau amesema chuo hicho chenye majengo 10 , muda wa ujenzi ni miezi 15 na  mpaka sasa umefikia asilimia 25.

Mratibu wa mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu kutoka wizara hiyo Ignas Chonya  amesema anashindwa kuelewa kwanini ujenzi huo umekuwa ukienda taratibu wakati fedha za ujenzi huo zipo na zimeshapitishwa tayari na serikali.Waziri Ndalichako yupo mkoani Kigoma kukagua miradi mbalimbali ya elimu katika halmashauri ya Buhigwe na Kasulu, ambapo miradi hiyo inatokana na fedha za mradi wa lipa kwa matokeo(EP4R).


Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia , ametembelea na kukagua miradi ya elimu katika shule ya sekondari Kigodya, Chuo cha ualimu Kabanga , shule ya sekondari Ruhita, Shule ya sekondari ya Nyantare ,Shule ya msingi Kasyenene, shule ya sekondari Kasangezi na chuo cha kilimo cha Bubondo wilayani Kasulu na kutoa maagizo.
Waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia akikagua ujenzi wa chuo cha ualimu Kabanga kilichopo wilayani kasulu mkoani Kigoma kinachojengwa kwa fedha za serikali.

WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA UKAGUZI WA MIRADI YA ELIMU WILAYANI BUHIGWE IFANYIKE

0
0
Moureen Rogath-Buhigwe. 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, amemuagiza katibu Mkuu wa wizara hiyo Leonard Akwilapo, kwenda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma kufanya ukaguzi maalumu wa miradi ya elimu kama utekelezaji wake ulifata utaratibu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya waziri huyo kufanya ziara katika wilaya hiyo katika miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa na fedha za mpango wa lipa kwa matokeo (EP4R), miradi yenye thamani ta fedha zaidi ya Sh .1.

Waziri Ndalichako amesema katika baada ya kukagua miradi hiyo aliweza kubaini kasoro mbalimbali za ujenzi wa majengo ya elimu yanayoendelea kujengwa katika wilaya hiyo.

"Nimeweza kubaini kasoro mbalimbali katika miradi ya elimu ikiwemo matumizi ya vifaa vya ujenzi vilivyochini ya kiwango pamoja na kutumia ramani ya michoro yao binafsi na kuacha ya wizara katika majengo ya utawala", amesema Ndalichako.

Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina amesema kabla ya kuja waziri aliweza kubaini baadhi ya mapungufu na kuyatolea maelekezo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Anosta Nyamoga na kuzichukulia hatua.

"Kamati ya usalama ya wilaya iliweza kubaini mapungufu katika miradi mbalimbali na tulitoa maelekezo kupitia kwa mkurugenzi na vyombo vyetu vilishaangizwa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki,"amesema mkuu wa wilaya hiyo Ngayalina.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amekiri kuwepo kwa mapungufu hayo katika ujenzi wa majengo hayo ya elimu na kusema kuwa tayari ameshaanza kuchukua hatua kwa waliohusika katika ujenzi huo .

Waziri Ndalichako amekagua miradi ya elimu wilaya ya Buhigwe katika shule ya msingi Bwega , shule ya sekondari Janda, shule ya sekondari Muyama , shule ya msingi Kasumo na shule ya sekondari Mwibuye wilayani Kasulu na kubaini kasoro mbalimbali .
 Waziri wa Elimu,  sayansi na teknolojia akikagua ujenzi wa  chuo cha ualimu Kabanga kilichopo wilayani kasulu mkoani Kigoma kinachojengwa kwa fedha za serikali.

The British Council Tanzania launches its new programme for Children aged 6-11

0
0
Primary Plus represents a unique formula for how kids learn English and establishes regional standards for Sub Saharan Africa for all aspects of its work with children and young people.

This new programme targets every aspect of the learning environment for Young Learners of English – how teachers are recruited, how timetables link with the school system, how course content matches age and culture. 

Primary Plus focuses on developing life skills and confidence in English. Communication, teamwork and creativity are promoted in the classroom, giving children the essential language and social skills, they need to succeed in today’s world. Interesting and motivating topics will be used and implemented through engaging activities in a positive and supportive learning environment.

The British council draws on over 50 years of experience of working with Young Learners, with over 109,000 young people in its 65 Teacher Centres worldwide, with expertise from within and from partners.  

Child Protection is a key focus for the British Council globally and for our Young Learner programmes in Sub Saharan Africa region. We have a ‘Child friendly School’ agenda. Children can only fulfil their potential in safe, non-threatening learning environments where building strong relationship with parents is highly valued and learning content challenges and engages, and teaching approaches recognise individual needs and differences.  As Head of the Teaching Centre, Doris Likwelile says, ‘Our aim is to be the most trusted global/local provider of English language services for children in Tanzania.’  

The courses will be launched on Saturday 19 October 2019 from 09:00am, all parents interested are encouraged to bring their children and learn more about the course. 

CHAGUENI VIONGOZI WA KUENDANA NA KASI YA RAIS MAGUFULI -DC. MWEGELO

0
0
Na Shushu Joel
MKUU wa wilaya ya kisarawe ambaye anakaimu Ukuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Joketi Mwegelo amewataka wananchi wa Halmashauri ya Chalinze kuwachagua viongozi wenye Utayari na Uwezo wa kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Bwilingu kwenye viwanja vya kituo cha mabasi Cha Barabara ya Morogoro.

Mkuu huyo wa wilaya aliwakumbusha na kuwasisitiza wananchi hao kutambua dhamani kubwa waliyonayo na yupi ni kiongozi atakayekuwa ni kiungo kikubwa kwa viongozi wa juu na anayeweza kuendana na utendaji wa Raisi Magufuli.

"Jambo hili niwewatahadharisha mapema kabla ya kufanya uchaguzi wa serikali za mtaa mwisho mwa mwezi wa kumi na moja"

Pia Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftali la kupiga kura huku akiwapa msisitizo kuwa ni wale watakaokuwa kwenye orodha ndani ya Daftari la Wapiga kura tu ambao watapata fursa ya kupiga kura. 

" Wananchi wenzangu wale ambao wanadhani kuwa kile kitambulisho cha kupiga kura kitawawezesha kushiriki uchaguzi huu, hapana. Uchaguzi huu tunatumia daftari hivyo ni muhimu kwenda kuniandikisha".

Alisema," jambo la kuwa na Vitambulisho kuwa kigezo si kweli bali ni wewe tu kuweza kufika kituoni na inakuchukua dakika 2 tu.

Mbali na kuwahimiza Wananchi kujitokeza katika zoezi hilo Mh.Mkuu wa Wilaya, amempongeza Mbunge wa jimbo hilo Mh.Mbunge wa Chalinze Ndg.Kikwete kwa utekelezaji na ufanikishaji wa miradi mbalimbali katika jimbo lake na juu ya yote alivyojitokeza yeye akishirikiana na wananchi kuhamasisha uandikishaji.

Hivyo amewataka wananchi hao kuwa na viongozi watakaochaguliwa vitongojini na vijijini wawe wachapakazi kama Mh. Mbunge na Mh.Raisi wanavyoshirikiana kufanya kazi nzuri ya kuleta Maendeleo." Ninyi wenyewe Mashuhuda na Mbunge ameeleza jinsi Miradi mikubwa kama ya maji,afya,madarasa, miundombinu na umeme ilivyotekelezwa kwa asilimia kubwa sana. Nakupongeza Mh. Mbunge kwa utekelezaji Mzuri wa majukumu.

Naye mzee Zaidi Lufunga (78) akizungumza kwa niaba ya Wana Chalinze amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kujionea mafanikio makubwa yalifanywa na serikali ya awamu ya tano katika jimbo la chalinze.

"Miaka yetu changamoto zilikuwa nyingi sana lakini kipindi hiki cha Rais Magufuli kwa kushirikiana na mbunge wetu Ridhiwani Kikwete mafanikio tunayapata na kazi nzuri inaonekana.Aidha amemwakikishia Joketi kuwa kwa hali hii ya utekelezaji wa miradi mikubwa na iliyokuwa ndio ndoto zao ni tu watachagua viongozi wenye hofu ya Mungu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa ujio wake wa kujionea jinsi wanachalinze wanavyojitokeza katika zoezi la kujiandikisha.Amewapongeza wakazi wa kata ya Bwilingu kwa kujitokeza kwa wingi ili kumsikiliza mkuu wa wilaya. Kwake Mbunge amelielezea hili jambo kubwa na kwa hakika linatoa dalili kuwa wananchi wako tayari. 


Hadi kufikia jana Halmashauri ya Chalinze ilikuwa imefikia Asilimia 74 ya Uandikishaji na baada ya kukatika kwa mvua kumekuwa na wingi mkubwa wa wananchi kujiandikisha. Zoezi hili linatarajiwa kuisha tarehe 17 October ambapo matarajio ya kuandikisha watu 136,000 utafikiwa huku hadi jana watu zaidi ya 90,000 wakiwa wamejitokeza kujiandikisha.



WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA RUANGWA

0
0
*Akemea ujenzi mbovu wa kuta, aagiza zibomolewe na kurekebishwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi na kusema kwamba hajaridhishwa na baadhi ya majengo.

Amemwagiza Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Tengamaso Wilson abomoe kuta zenye hitilafu na kurekebisha kasoro zilizopo kwenye majengo hayo ikiwemo kutonyooka kwa kuta za majengo hayo.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatano, Oktoba 16, 2019) wakati akikagua majengo ya hospitali hiyo, na kumweleza mhandisi huyo kwamba kuta zimepishana unene kwa sababu hakusimamia kazi yako ipasavyo. “Ukuta huu ni mbovu kwa sababu hukuwasimamia vizuri mafundi wako. Kuna mahali juu unaona ukuta ni mdogo na huku chini ni mnene.”

Majengo ambayo Waziri Mkuu aliyakagua na kuonesha kutoridhishwa nayo ni ya utawala, wagonjwa wa nje (OPD) na maabara. Majengo mengine yanayojengwa ni jengo la wazazi, la X-ray, la utoaji dawa na la kufulia nguo.

Alipouliza ni kwa nini kumetokea tofauti baina ya kuta hizo, Waziri Mkuu alijibiwa kwamba tatizo ni upigaji wa lipu. “Mhandisi wa Wilaya simamia hili, kagonge upya kuta za jengo hili na lile. Hatuwezi kuwa na jengo la Serikali la aina hii. Tukitoa fedha ya Serikali ni lazima mjiridhishe kama kilichojengwa ndicho sahihi.”

“Tunahitaji majengo yote yawe smart, hata ujenzi wake nao uwe smart. Usikubali kutoa certificate kama kazi haijakamilika. Kama kuna kazi haujaridhika nayo, usikubali certificate itoke. Zile sentimeta 30 ni lazima zirekebishwe la sivyo, itaonekana huku uliweka matofali mengi kuliko upande ule,” alisisitiza.

Akiwa hospitalini hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba katika awamu ya kwanza, Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 na kuelekeza yajengwe majengo saba ya kipaumbele ambayo ni jengo la wazazi, la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, la X-ray, la utoaji dawa, la kufulia nguo na la utawala.

Ujenzi wa hospitali hiyo unafanyika kwa kutumia njia ya manunuzi inayoitwa ‘Force Account’ ambapo Halmashauri inanunua vifaa vya ujenzi na kuajiri mafundi wa kujenga majengo yaliyoelekezwa wakisimamiwa na wataalam wa halmashauri na kamati mbalimbali. 

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemwagiza mweka hazina wa Halmashauri hiyo, Bw. Frank Chonya ajiridhishe na kazi za ujenzi zinazofanyika kabla hajaamua kutoa fedha za malipo.

“Mweka hazina, wakati wote ukiambiwa kuwa certificate imeletwa ni lazima uende ukakague mradi na kama haujaridhika, sema wazi kwamba hujaridhika na kazi iliyofanywa,” alisema Waziri Mkuu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Andrea Chezue alisema kiasi chote kilichotolewa na Serikali cha sh. bilioni 1.5 kimeshatumika, na kwamba Halmashauri illitumia zaidi ya sh. milioni 100 ili kusafisha eneo na kulipa fidia ili wapate eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 56.

“Mchango wa Halmashauri ya Wilaya kwenye ujenzi wa hospitali hii, mpaka sasa ni kwamba tumelipa sh. milioni 88.266 zikiwa ni fidia ya eneo la ujenzi na sh. milioni 14.418 zimetumika kusafishia eneo lote,” alisema.

IAPR BIDS FAREWELL TO AMBASSADOR MODEST MERO OF TANZANIA AS HE RETIRES FROM OFFICE.

0
0
Farewell party hosted by the International Association of UN Permanent Representatives Committee (IAPR) for Amb. Modest J. Mero of Tanzania and Amb. Gustavo Meza Cuadra of Peru at the Residence of Hungary by the Chairperson Amb. Katalyn, in Manhattan, New York on 15 October 2019

BRITISH COUNCIL YAJA NA KOZI YA WATOTO

0
0
 Mkuu wa kitengo cha Ufundishaji cha taasisi ya kimataifa ya British Council , Doris Likwelile akizungumza na waandhi wa habari kuhusu taasisi hiyo kuanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha  na kushoto ni Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden -Watkinson.
Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga kuwahudumia watoto wataojiunga kwenye kozi za taasisi hiyo wakati wa Taasisi hiyo ilipokuwa inatangaza siku ya kuanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha 
 Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kuwaondoa wananchi hofu kuhusu malipo ya kozi zitolewazo na Shirika hilo wakati wa kutangaza siku ya uzinduzi wa mafunzo ya kiingereza kw watoto kuanzia miaka 6 hadi 11. Wa kwanza kushoto ni  Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson  na katikati ni  Mkuu wa kitengo cha Ufundishaji cha British Council Tanzania, Doris Ndewa Likwelile.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KATIKA kukabiliana na changamoto ya watu wengi kutokuwa na ujasiri wa kujieleza mbele za watu taasisi ya kimataifa ya British Council imeanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha ufundishaji wa taasisi ya kimataifa ya British Council, Doris Likwelile jijini Dar Es Slaam leo, amesema kuwa programu kwaajili ya watoto itazinduliwa Jumamosi ya Oktoba 19,2019.

"Kwa mara ya kwanza  kabisa tunaanza kuwa na kozi za kingereza kwa watoto lakini hii kozi itakuwa zaidi kwa mtoto kujifunza kingereza". Amesema Doris

Amesema kuwa ni jambo nzuri kuanzisha kozi hiyo kwa watoto wa kuanzia miaka sita hadi 11 kwani kwa mara ya kwanza itaanza kutolewa hapa nchini ikiwa  taasisi hiyo ilishaenea kwenye nchi zaidi ya 65 duniani kote.

"Mtoto zaidi ya kujifunza Kingereza  mtoto ataongezewa ujuzi ambao unahitajika kwa karne hii ya sasa ya 21 kwa kufanya mawasiliano pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwa na mawazo mapana,na kuwawezesha kuwa na ujasiri na kuwa wabunifu". Amesema Doris


Nae Meneja wa Huduma ya wateja na mauzo wa Taasisi ya kimataifa ya British Council, Bernard Mosha, amesema kuwa kozi hiyo kwa watoto itakuwa gharama nafuu na mtihani kwaajili ya kiwango utafanyika bila gharama yoyote yaani ni bure kabisa.

"Naomba niwaondoe wasiwasi wazazi kuhusiana na bei zetu kwani wanawezakufikiri kuwa bei zetu zinaweza kuwa za kimataifa hii ni hapana bei zetu zitakuwa za kawaida kwani tumefanya utafiti na kugundua kuwa wazazi kiwango cha uchumi cha wastani kwahiyo gharaama za kozi hii kwa mtoto itakuwa ni nafuu.

Pia amewaomba mzazi au mlezi kumpele mwanaye katika taasisi hiyo ili mtoto aweze kufanya mtihani wa kiwango kwaajili ya kuweza kujua kiwango chake na kuangalia namna ambavyo wanaweza kumfundish kwa ufasaha zaidi.

Kwa Upande wa Usalama wa watoto Mosha amewaondoa wasiswasi wazazi kwani ni sehemu salama kwa watoto.

Hata hivyo Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil,Richard Watkinson amesema kuwa wazazi wawapeleke watoto wakafundishwe lugha ya Kingereza na waingereza wenyewe.
Amesema kuzi hiyo itakuwa na awamu tatu ambapo mtoto atasoma wakati yupo likizo.

HESLB yatangaza wanafunzi 30,675 waliopata mikopo awamu ya kwanza

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.

Katika mwaka huu wa masomo, Serikali imetenga TZS 450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, fedha zilizotengwa na kutolewa zilikua TZS 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar e Salaam na   Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).

Waombaji wafungue ‘SIPA’ kupata taarifa za mikopo
Badru amefafanua kuwa waombaji mikopo wafunfue akaunti zao binafsi (SIPA – Student’s Individual Permanent Account) walizofungua kuomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz) ili kupata taarifa za mikopo. 

Aidha, orodha kamili ya wanafunzi hao inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na pia inatumwa vyuoni ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.

“Pamoja na tovuti, wanafunzi wanaweza kufungua akaunti zao walizooombea mkopo mtandaoni maarufu kama SIPA na kuona walivyopangiwa … na tunaanza kupeleka fedha vyuoni kesho kwa kuwa Serikali imeshatukabidhi TZS 125 bilioni ambazo tuliomba kwa malipo ya kati ya Oktoba hadi Disemba mwaka huu,” amesema Badru.

Kwa mujibu wa Badru, HESLB inakamilisha orodha ya awamu ya pili ambayo itatangazwa kabla ya mwisho wa wiki ijayo na fedha zao zitatumwa vyuoni mapema kabla vyuo havijafunguliwa.

Makundi Maalum – Yatima, Wenye ulemavu n.k
Kuhusu makundi maalum yenye uhitaji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675, wapo wanafunzi 6,142 ambao ni yatima au wamepoteza mzazi mmoja, wenye ulemavu 280 na wengine 277 wanaotoka katika kaya zinazofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

“Katika makundi maalum pia tuna wanafunzi 1,890, sawa na asilimia 6 ya wanafunzi 30,675 wa awamu ya kwanza ambao walisoma shule binafsi lakini kutokana na hali duni ya uchumi, walifadhiliwa na walithibitisha kwa kuweka nyaraka sahihi,” amesema Badru.

Kutangazwa orodha ya awamu ya pili Kuhusu awamu ya pili, Badru amesema HESLB kabla ya Oktoba 25 ya wiki ijayo baada ya kukamilishwa kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliochelewa kukamilisha taratibu za udahili au kuchelewa kurekebisha maombi yao ya mkopo mtandaoni.

Wito kwa wanafunzi 

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa HESLB Dr. Veronica Nyahende amewataka wanafunzi ambao taarifa zao hazijakamilika, kukamilisha ili wenye sifa wapangiwe mkopo. 

“Kuna kama wanafunzi 1,000 ambao maombi yao hayajakamilika, watumie muda huu hadi tarehe 19 kukamilisha ili wenye sifa nao tuwapangie mkopo," amesema.

HESLB pia imewataka wanafunzi kuwa watulivu na kuendelea kufuatilia vyombo vya habari na akaunti zao ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu uombaji mikopo na wanapokua na maswali, wawasiliane na HESLB kuopitia namba za simu zinazopatikana katika tovuti (www.heslb.go.tz).
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul Razaq  Badru akitangaza wanafunzi wakipata Mikopo kwa vigezo vilivyoanishwa na Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Uchambuzi wa upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Veronica Nyahende akizungumza na waandishi habari kuhusiana na upangaji Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa kwanza leo jijini Dar es Salaam.

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KUBADILISHA UZOEFU MATUMIZI YA MITANDAO

0
0
Na Said Mwishehe,Arusha-Michuzi TV 

JUKWAA la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAGF) wamekutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili kwa pamoja ukuaji wa matumizi ya mtandao kwa maendeleo ya jamii ya nchi hizo.

Kupitia mkutano huo wawakilishi na wadau wa nchi hizo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda ,Burundi na Sudani Kusini wametumia nafasi hiyo kujadili kwa kina kuhusu matumizi sahihi ya mitandao katika kuleta maendeleo huku kila nchi ikilezea namna inavyotumia mtandao.

Akizungumza katika kongamano hilo Mwakilishi kutoka Burundi Joel Nkurunzinza amesema kutokana na kukua kwa teknolojia kumeifanya Dunia kuwa kijiji hivyo EAGF zimeona ni vema kutumia jukwaa la majadiliano ili kuwaelimishana na kubadilishana uzoefu.

"Lengo la nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuhakikisha tunakwenda pamoja katika eneo hili la matumizi ya mtandao,"amesema na kuongeza matumizi hayo yaende sambamba na kuheshimu sheria zilizopo kwa kila nchi.

Ameongeza kuwa kupitia kongamano hilo, kuna mambo mengi ya kujifunza na yatatoa muelekeo sahihi kuhusu namna bora ya kutumia mitandao. "

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Rwanda Grace Ingabine ambaye ni Mkurugenzi wa RICTA amesema amefurahishwa na majadiliano ya kongamano la EAGF huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa nchi yao imepiga hatua kwani asilimia 96 ya wananchi wa mjini na vijijini wanatumia mtandao.

"Kwetu wadau wa mtandao tumekuwa tukikutana kujadili kuhusu teknoloji ya mawasiliano kila ifikapo Novemba, lakini kupitia kongamano hili la EAGF tumeamua na sisi tutakuwa tukikutana la nchi kwetu kila ifikapo Juni na hiyo itatoa nafasi ya kushiriki katika kongamano la EAGF ambalo linafanyika Oktoba,"amesema.

Mwakilishi wa Tanzania wa EAGF Nazar Nicholas amesema kwa upande wa Tanzania kumekuwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha mitandao inatumika kwa usahihi na baadhi ya hatua ambazo zimechukuliwa ni pamoja na kuwepo kwa sheria ya mtandao .

Mwisho 

Wakati huo huo Getrude Mweta kutoka Chama cha Viziwi Tanzania ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa EAGF kuhakikisha watu wenye ulemavu wanakuwa na mazingira rafiki ya kushirikishwa katika majadiliano yanayoyaandaa.

Amesema watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wamekuwa wakishirikishwa katika makongamano lakini changamoto kubwa inayowakutana ni kukosekana kwa mawasiliano ya majadiliano"Hapa leo tunao viziwi , watu wenye matatizo ya uono na walemavu wa viungo na wanahitaji kujua kinachoendelea lakini changamoto ni nani anawasaidia kuwafikishia ujumbe."

Mwakilishi wa EAGF kutoka nchini Kenya Barrack Otieno amesema nchini kwao wanaendelea na kupiga hatua katika matuminzi ya mitandao na kwamba kongamano hilo limesaidia kuwapa nafasi ya kujua kipi ambacho wanatakiwa kukiboresha.
Wadau wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAGF) wakiwa katika kongamano la majadiliano kuhusu matumizi ya mtandao
Wawakilishi wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAGF) kutoka nchi za Tanzania,Kenya,Burundi,Rwanda,Sudan Kusini na Uganda wakiwa meza kuu wakati wa majadiliano hayo wakiendelea leo Oktoba 17,mwaka 2019 jijini Arusha
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia majadiliano wakati majadiliano hayo
Mmoja wa wakalimani akitoa ufafanuzi kwa watu wenye ulemavu waliohudhuria kongamano la majadiliano ya mtandao ambayo yameandaliwa na Jukwaa la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAGF)
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akitoa maoni yake wakati wa majadiliano hayo

MAJALIWA AKAGUA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA KIWALALA KATIKA HALMASHAURI YA MTAMA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua skimu ya umwagiliaji ya Kiwalala katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi, Oktoba 17, 2019. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga na wa tatu kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda ya Kusini, wafike ofisini kwake Dar es Salaam kesho asubuhi na taarifa kuhusu skimu wa umwagiliaji wa Narunyu.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) wakati alipoenda kukagua skimu hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa tangu 2017. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama ni Bw. Warioba Gunze na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda ya Kusini, ni Mhandisi Mndeme.

Amechukua uamuzi huo baada ya kufika eneo la mradi na kupokea malalamiko ya wanajumuiya ya umwagiliaji kutoka kwa Mwenyekiti wao, Bw. Bakari Awadhi juu ya kusuasua kwa mradi huo lakini alipotaka apate maelezo ya wataalamu hakuna hata mmoja ambaye alikuwepo.

"Nilitaraji niwakute hapa Mkurugenzi wa Halmashauri, Afisa Umwagiliaji wa Wilaya na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda. Nimeagiza wanikute uwanja wa ndege Lindi au Dar es Salaam na kesho asubuhi waje ofisini kwangu wanipe taarifa kamili ya mradi huu. Nataka nijue fedha zilizobakia zaidi ya sh. milioni 240 ziko wapi."

"Walipaswa niwakute hapa wananisubiri kwa sababu nilitoa taarifa tangu jana kwamba nitapita hapa. Nimepata taarifa kwamba wamesafiri kutoka Mtwara na leo asubuhi walikuwepo Lindi mjini. Waje ofisini kesho, wakishindwa, nitachukua maamuzi mengine," amesema.

Akielezea umuhimu wa mradi huo wakati akizungumza na baadhi ya wanaushirika waliokuwepo, Waziri Mkuu amesema ni wa muhimu kwa sababu unatiririsha maji wakati wote. "Huu ni mradi wa kuringia. Mradi huu unatiririsha maji wakati huu wa kiangazi, tena mengi tu."

Amesema kutokana na umuhimu wa mradi huo, hivi sasa wangekuwa wanazalisha mazao ya kila aina. "Hapa ni mahali pa kuzalisha mazao mengi, leo unalima mahindi, ukivuna unapanda matikiti, ukitoa unapanda nyanya. Sasa nitapasimamia mwenyewe," amesisitiza.

Amewataka wanaushirika wanaounda jumuiya ya umwagiliaji wahakikishe kila mmoja anatambua eneo lake na mara kazi ikianza wawe tayari kuanza kilimo. "Huu mradi una manufaa kwa watu wa Ruo, Mahumbika hadi Mnazi Mmoja. Lazima tuung'ang'anie kwa sababu kuna idadi kubwa ya wakulima wanaoutegemea. Huu mradi lazima tuuvalie njuga."

Waziri Mkuu alipofika uwanja wa ndege wa Lindi, maafisa hao walikuwa hawajafika kwa sababu simu zao hazikupatikana, na akaagiza waje Dar es Salaam kesho asubuhi. 

Mapema, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Shaibu Ndemanga alimweleza Waziri Mkuu kwamba katika mafaili aliyoyapitia ofisini kwake alibaini kwamba mradi huo ulitengewa sh. milioni 788 ambapo mkandarasi wa kwanza Chest Investments Company alilipwa sh. milioni 121 lakini akashindwa kazi.

"Mkandarasi wa pili ambaye ni D & L naye alilipwa zaidi ya shilingi milioni 400 naye pia akashindwa kazi ya kuondoka tope. Kwenye ripoti, inaonesha zilibakia sh. milioni 249," alisema.

Naye Mwenyekiti wa wanajumuiya ya umwagiliaji ya Narunyu, Bw. Bakari Awadhi alisema skimu hiyo yenye ukubwa hekta 1,200 imekuwa ikijaa maji na kufunika mitaro na hatimaye kujaa mchanga.

Alimwomba Waziri Mkuu awasaidie kuifufua skimu hiyo kwa sababu inawanufaisha wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

DKT. MPANGO: BENKI YA DUNIA IWEKEZE FEDHA KWENYE MIRADI YA KIMKAKATI YA SERIKALI

0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington Dc
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Dunia-WB iwatume wataalam wake nchini Tanzania ili waainishe miradi mikubwa ya kimkakati inayotakiwa kutekelezwa kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP) badala ya taasisi hiyo ya Fedha Duniani kutaka Serikali itekeleze miradi midogo isiyo na tija kubwa kwa Taifa

Dkt. Mpango ametoa ushauri huo Mjini Washington DC nchini Marekani baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem ambapo aliwasilisha miradi mbalimbali ambayo Serikali inatekekeleza na ambayo ameiomba Benki hiyo isaidie rasilimali fedha.

‘’Nisingependa kuona Taasisi kubwa ya Kifedha kama Benki ya Dunia inakimbilia kufadhili utekelezaji wa vimiradi vidogo vya kujenga hostel au hotel za nyota tano; Kwa sasa nchi yetu inahitaji kujikita zaidi katika miradi mikubwa  ambayo itawaletea maendeleo ya haraka wananchi wetu’’ alisisitiza Mhe.Mpango.

Mhe. Mpango aliendelea kusisitiza kuwa kwa sasa Tanzania inatekeleza miradi mikubwa na inayohitaji fedha nyingi kuikamilisha, hivyo ni vyema Benki hiyo ikajielekeza katika kusaidia utekelezaji wa miradi hiyo. 

Dkt. Mpango alianisha miradi kama ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme la Julius Nyerere katika Mto Rufiji mkoani Pwani, Mradi wa Ujenzi wa Reli kutoka Mtwara kwenda Mbamba Bay, Mchuchuma na Liganga ambako kuna rasilimali kubwa ya Madini ya Chuma na Makaa ya Mawe. 

Aidha Dkt. Mpango alisema katika kutekeleza vyema miradi ya PPP Serikali imejikita katika mambo mawili moja ni kuwa na programu ya kujenga uwezo kwa maana ya wataalamu wa kuitambua hiyo miradi lakini pia, kuwa na uwezo wa kufanya uchambuzi wa kina ili kujenga uwezo wa majadiliano na Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi hiyo.

‘’Nimewahimiza kwamba; kama kweli tunataka kutekeleza kwa ufanisi mpango wa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP) ni lazima tutekeleze miradi mikubwa, na kwa kuanzia, wangekuja kuanza kutekeleza ule mradi wa kujenga reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbaba-Bay, Mchuchuma hadi Liganga’’ alisema Mhe.Mpango.

Aliongeza kuwa ukamilishaji wa ujenzi wa reli hiyo utasaidia kuchochea kwa kasi maendeleo ya nchi  kutokana na rasilimali zilizopo katika maeneo inapopita reli hii.

Dkt. Mpango alimshukuru Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem kwa kukubali maombi mengi kutoka Tanzania ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango(katikati) akiwa na ujumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano na Benki ya Dunia kwenye Mkutano uliofanyika Jijini Washington DC.
 Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akichangia jambo kwenye kikao kati ya Benki ya Dunia na Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) kwenye Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia-WB na Shirika la Fedha la Kimataifa -IMF inayofanyika Jijini Washington nchini Marekani.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika, Nd.Hafez Ghanem akifuatilia majadiliano kati ya ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki hiyo, Jijini Washington DC. Kulia kwa Nd.Hafez ni Mshauri Mwandamizi  Maendeleo Endelevu kwa  Afrika, Bw.Thomas O’Brien.

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images