Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA MADINI ASHIRIKI KUJADILI CHANGAMOTO ZA BARABARA MKOANI GEITA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Grbriel Akiwasilisha Mada katika kakao cha Bodi ya Barabara Mkoani Geita.

Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Geita
Waziri wa Madini Doto Biteko akiandika faarifa katika kikako cha Bodi ya. Barabara kilichofanyika Mkoani Geita.

…………………..

Na Tito Mselem Geita,

Waziri wa Madini Doto Biteko ameshiriki katika Kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Oktoba 15,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ili kujadili changamoto za barabara mkoani hamo. 

Kikao hicho kiliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapindizi wakiwemo Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Geita akiwemo Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Doto Biteko, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma, Mbunge wa Mbogwe Augustino Masele, Mbunge wa Busanda Lolesia Bukwimba, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema Pendo Peneza.

Vingozi wengine walioshiriki ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mjini Josephat Maganga, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Mkumba, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe. Martha Mkupasi, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Geita Alhaji Said Kalidushi pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali.

Aidha Waziri Biteko amewapongeza viongozi wa TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri wayoifanya katika Mkoa wa Geita kwa kuhakikisha kuwa barabara zinatengenezwa kwa kiwango kizuri na kumalizika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Biteko amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri katika kuhakisha barabara za Mkoa wa Geita zinakamilika kwa muda uliopangwa na zinakuwa kwenye viwango vinavyotakiwa.

Imeelezwa kuwa Mji wa Geita ni kati ya miji inayokua kwa kasi sana sambamba na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi, hivyo kuwepo na msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu barabarani. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema katika awamu hii ya tano Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitupa ahadi ya ujenza wa barabara na ametekeleza ujenzi wa barabara ya Ushirombo mpaka Lusahunga kilometa 110 kwa gharama ya shilingi bilioni 114.557, Uwanja wa Ndege wa Chato kilometa 3.5 kwa gharama ya Shilingi Billioni 39.15. 

Aidha, Mhandisi Gabriel amesema kwamba, kazi ambazo zimekamilika ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Runzewe mpaka Bwanga kilometa 45 kwa gharama ya shilingi bilioni 43.357 na barabara ya Bwanga mpaka Biharamuro kilometa 65.0 miradi yote hii inatekelezwa kwa fedha za serikali.

Katika hatua nyingine Mhandisi Gabriel ameeleza kwamba katika Mkoa wa Geita TANROADS inasimamia miradi ya usanifu wa kina katika barabara za Geita mpaka Kahama yenye kilometa 139.557 kwa gharama ya shilingi bilioni 440 inatelekezwa na mkandarasi ENV Engeneering, kazi imekamilika. 

“TANROADS inasimamia pia usanifu katika barabara ya Nyamirembe mpaka Katoke yenye urefu wa kilometa 50 kwa gharama ya shilingi bilioni 861.046 na Mhandisi Consult ambapo kazi hiyo imekamilika,” Gabriel amesema Mhandisi Gabriel.

Katika hatua nyingine Mhandisi Gabriel ametoa rai kwa wananchi kutunza miundombinu ya barabara kwa kutopitisha mifugo na kunyofoa alama za barabarani pamoja na kutovamia hifadhi za barabara.

Katika bajaeti ya mwaka 2018/2019 TARURA Mkoa wa Geita unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi 6,844,393,140.37 kutoka mfuko wa barabara (Road fund) kwa ajili ya matengenezo ya barabara na shilingi 1,612,500,000.00 kwa ajili ya kazi za maendeleo, fedha hizo ni kutoka OR-TAMISEMI. 

Hadi kufikia Tarehe 03/01/2019 jumla ya shilingi 2,249,253, 616.84 sawa na asilimia 32.86 zimepokelewa kwa ajili matengenezo ya barabara na jumla ya shilingi 612,654,524.43 sawa na asilimia 37.99 zimepokelewa kwa ajili ya miradi maendeleo ya barabara za mkoani Geita.

KATIBU WA BUNGE NDG. STEPHEN KAGAIGAI AFUNGUA MAFUNZO YA NDANI KWA KAMATI INAYOHUSIKA NA KUZUIA NA KUFUATILIA VIHATARISHI KAZINI

0
0
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akifungua mafunzo ya ndani kwa kamati inayohusika na kuzuia na kufuatilia Vihatarishi kazini tukio lililofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Mkufunzi, Mtafiti na Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Ernest Mwasalwiba akiwasilisha maada wakati wa mafunzo ya ndani kwa kamati inayohusika na kuzuia na kufuatilia Vihatarishi kazini tukio lililofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Bunge Ndg. Peter Magati akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya ndani kwa kamati inayohusika na kuzuia na kufuatilia Vihatarishi kazini tukio lililofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kuzuia na kufuatilia vihatarishi kazini wakiwa katika mafunzo ya ndani yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

ATHARI YA MVUA KWA BAADHI YA NYUMBA ZA MAKAZI JIJINI DAR

0
0

Mvua zinazoendelea kunyesha katika Jijini Dar es salaam na kuleta athari kwa baadhi ya mitaa kujaa maji, kama inavyooneka pichani nyumba hizo zipo wilaya ya Kigamboni.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Nyumba zikiwa imezingirwa na maji kutokana mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

MAONESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI KUFUNGULIWA RASMI OKTOBA 16 SIMIYU

0
0
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi (wa pili kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Afisa kutoka Benki ya Tanzania (BOT), Bi. Edista Njau (kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya mitaji kutoka katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi wakitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari namna mifuko hiyo ilivyowasaidia kupata mitaji, wanufaika hao wamehojiwa katika banda la Benki Kuu ya Tanzania, katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

…………………..


Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Oktoba 16, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Mjini Bariadi Mkoani hapa, ambapo washiriki kutoka taasisi za Umma na binafsi zaidi ya 100, mifuko ya uwezeshaji zaidi ya 40 na vikundi vya kijamii (VICOBA) wanatarajiwa kushiriki.



Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy ambao ndiyo waandaaji amesema maonesho haya ni fursa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kujifunza huduma za mifuko ya uwezeshaji, taasisi za fedha na programu mbalimbali.

“Maonesho haya yameanza Oktoba 14, 2019 na yatafunguliwa rasmi Oktoba 16, 2019 na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na yatahitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2019 na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waje wajionee huduma mbalimbali za mifuko, taasisi na vikundi vya kijamii,” alisema Kessy.

Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao kujua huduma zao, huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo kupitia mpango mkakati wa miaka mitano ulioanza mwaka 2018 inatarajia kuzifikia familia 235,000 kwa kudhamini mikopo kiasi cha shilingi bilioni 210.6 .

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tanzania tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi amesema benki hiyo kwa kushirikiana na NEEC na PASS imetoa mikopo ya vikundi mbalimbali vya kijamii, vikundi rasmi na visivyo rasmi, wafanyabiashara, hivyo ni vema wananchi wafike kwa wingi kujionea fursa hizo ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naye mnufaika wa mikopo ya mifuko ya uwezeshaji, Bw. Emmanuel Nyambi Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi kutoka Kahama, ametoa wito kwa wananchi kufika katika maonesho hayo ili waweze kuona fursa za upatikanaji wa mikopo kupitia mifuko, programu na taasisi mbalimbali za kifedha huku akieleza kuwa hakuna urasimu katika utoaji wa mikopo.

“Natoa wito kwa wajasiriamali wadogo au vyama mbalimbali, wafike kwenye maonesho haya waje wajifunze namna ya kupata mikopo ya kuendeshea shughuli za kiuchumi, niwahakikishie hakuna urasimu kwenye mikopo, tunaipata kwa wakati na Benki Kuu inadhamini kikubwa ni kuwa waaminifu kurejesha mikopo,” alisema Nyambi.

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu: “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Tanzania ya Viwanda”.

ALAT yawataka vijana kuchangamkia fursa za Kilimo

0
0
Charles James, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT), Elirehema Kaaya amewataka vijana kuchangamkia fursa za kilimo badala ya kukaa vijiweni na kulalamika ajira hamna.

Kaaya amesema hayo wakati alipofika kukagua mradi wa kituo cha kilimo cha Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo alielezwa na wasimamizi wa kituo hiko juu ya uhaba wa vijana wanaoenda kujifunza kilimo.

Amesema jumuiya hiyo kwa kushirikiana na halmashauri wamewekeza fedha nyingi ili kuboresha kituo hicho ili kiweze kutoa elimu kwa vijana na jamii inayozunguka eneo hilo.

" Vijana wengi wanapenda kazi za ofisini za kuvaa suti na tai lakini niwahakikishie kilimo kinalipa sana, mnapaswa mtumie fursa hizi ambazo Serikali inawaletea hadi maeneo yenu huku.

Alat tumeleta Sh.Milioni 150 na halmashauri imechangia karibu Sh.Milioni 90 ili kuandaa kitalu,mbogamboga na kutoa mafunzo kwa nguvu kazi ambapo wakulima wamepata elimu hiyo," Amesema Kaaya.

Kaaya ametoa maagizo kwa uongozi wa kituo hiko kujenga mfumo wa kuvuna maji ya mvua kwenye majengo ya kituo hiko ili kukabiliana na upungufu wa maji kwenye eneo hilo.

Nitoe wito kwa wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi kuhamasisha wanafunzi kujitokeza kwa wingi ili waweze kupatiwa elimu ambayo itakua msaada mkubwa kwenye maisha yao katika kuajiri.

Awali, akitoa taarifa ya kituo hicho, Mkuu kituo cha Kilimo, Taaluma na Mawasiliano Kibakwe, Samson German alisema kituo hicho kinatoa huduma za kilimo na mifugo kwa wakulima katika eneo husika.

“Wanaona kama kazi sio za kwao wanataka kazi zenye kipato kikubwa ambapo tunalazimika kupata vijana wa kufundishwa wanatoka mbali lakini wao wanaotoka hapa hawapatikani.Hata kazi za kupalilia ukimuita kijana wa eneo hili aje apalilie anaona kazi haimfai kwa sababu haina kipato kikubwa na kituo chetu hakina uwezo wa kuwalipa kiasi kikubwa," Amesema German.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT), Elirehema Kaaya akikagua shamba la mradi wa kilimo Kibakwe wilayani Mpwapwa.
 Katibu wa ALAT, Elirehema Kaaya akisikiliza maelezo juu ya mradi wa Kilimo Kibakwe wilayani Mpwapwa alipofika kukagua.
Katibu wa ALAT, Elirehema Kaaya akikagua shamba la Nyanya Chungu katika shamba la mradi wa Kilimo Kibakwe wilayani Mpwapwa

ISLAMIC FOUNDATION YAFANIKISHA MIRADI YA MAJI KITETO

0
0
TAASISI ya Islamic Foundation imechimba ambayo imefanikisha mradi wa maji kwa kuchimba kisima kwenye Kata ya Matui Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imechimba kisima kingine cha maji katika shule ya sekondari Kiteto, chenye urefu wa mita 150 na thamani ya shilingi milioni 45.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, baada ya kuzindua mradi huo, Mkurugenzi wa taasisi ya Islamic Foundation, Ibrahim Twaha, alisema katika mkoa wa Manyara wametekeleza mradi wa visima vipatavyo saba vyenye thamani ya shilingi milioni 270.
Twaha alisema kati ya visima hivyo, visima vinne vimetekelezwa ndani ya wilaya ya Kiteto, kisima kimoja katika kata ya Matui na visima viwili kijiji cha Sukuro wilayani Simanjiro.

“Hili ni jambo la kumshukuru sana Mwenyezi Mungu pia ni jambo la kumshukuru kiongozi wetu, Rais wetu Dokta John Pombe Magufuli kwa juhudi zake kubwa na ndiyo maana leo mnaona tupo tunatekeleza miradi katika hali ya amani na furaha, hizi zote ni juhudi za kiongozi wetu jemedali wetu Rais John Magufuli, kwa hiyo hili ni jambo ambalo la kumpongeza sana,” alisema Mkurugenzi Twaha.
Alisema lslamic Foundation ni taasisi ambayo iko kisheria nchini imeanzishwa 1998 na hadi sasa wameweza kutekeleza miradi ya visima zaidi ya 3,000 ikiwa ni visima virefu na vifupi.

“Tumeweza kuwanusuru akina mama mbalimbali ambao walikua wanaliwa na mamba katika sehemu za kando kando ya mito, na huduma hizi katika taasisi yetu sisi tunazitoa ni huduma za raia au wananchi watanzania, nje ya kuangalia dini wala kabila, wala chama wala nani, maadamu ni Mtanzania ana haki ya kupata mradi huu, kwenye dini yetu sisi ya kiislam huwa maji ni uhai, mnyama anahitajika apate na watu wote, kwahiyo watanzania wanayo haki kupitia kiongozi wao jemedali Rais Magufuli na kupitia taasisi zote ziwe za kidini, zisiwe za kidini madamu zipo ndani ya Tanzania wanayo haki ya kupata huduma hii, kwa ajili hii napenda nikushukuru sana mheshimiwa mkuu wa mkoa nimefurahi sana leo kuungana na wewe katika zoezi hili nakushukuru sana,” alisema Twaha.
Mbunge wa jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian aliishukuru taasisi hiyo Kwanzaa kufanikisha hilo kwani walishapima kuchimba visima 19 kwenye maeneo mengi bila mafanikio ya kupata maji.


“Sisi tunaiwashukuru hii taasisi na tunadhani kwa gharama za mradi huu kwa shilingi mil.45 wanapata maji leo zaidi ya lita 3,000 kwa dakika 45, ina maana sisi tunaweza kufanya hesabu wenyewe ndani ya fedha za wizara za halmashauri zinazoingia (RUASA) ukiwapa hawa kazi wanaweza kutuchimbia maji wakatupa kutujengea visima tukapunguza migogoro ya maji na ubadhilifu wa fedha zinazotokana na wakandarasi tukawa tumepunguza migogoro tukabaki salama, tushirikiane nao hawa watuchimbie, watujengee tuwalipe waondoke tupate maji,” alisema Papian.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti aliipongeza taasisi hiyo kwa kile alichodai jambo hilo sio dogo ni kubwa kwani siyo mara yao ya kwanza kufanya shughuli kama hiyo.

“Nakumbuka nikiwa mkuu wa wilaya Arumeru mlituchimbia visima vingi sana, taasisi hii imekuwa ikitoa msaada mkubwa na tunawashukuru na tunazidi kuwaombea muendelee kufanya hii huduma, kwa sababu hii najua ni ibada kwenu, kwani watoto hawa walikuwa wanateseka sana kutafuta maji, na niwaombe haya maji msiyachezee ovyo ovyo na wala msiyatoe nje ya shuleni hapa kwa sababu Lita 3,000 kwa mahesabu yangu ya haraka haraka bado yanawatosheleza watoto walio hapa, mtoto mmoja kwa siku anatumia lita 60, Lita 20 asubuhi, jioni lita 20 na hapa katikati.

Hata hivyo, alisema taasisi hiyo imekuwa ikihudumia nchi nzima hivyo, hivyo aliwaomba waendelee kuongeza visima vingine ndani ya mkoa huo ili kuweza kupunguza adha ya upatikanaji wa maji, ili kuwapunguzia kusaidia jamii hasa wanawake.

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA KUHUISHA TAARIFA ZA MAKAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA NDANI YA SIKU 90

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA UPATIKANAJI WA NIN KWA AJILI YA USAJILI WA KUHUISHA KAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA


Nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu Zajadili Halia ya Amani, Usalama

0
0
Baadhi ya vinongozi kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu wakifuatilia mkutano ulipokuwa unaendelea jijini Brazzaville.
Mwenyekiti wa Kikao cha nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu, akiongoza mkutano jijini Brazzaville.
Ujumbe kutoka Tanzania ukielezea jambo wakati wa mkutano wan chi wanachama ukanda wa maziwa makuu ulipokuwa unaendelea.


Baadhi ya vinongozi kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu wakifuatilia mkutano ulipokuwa unaendelea jijini Brazzaville.
……………………

Na  Ripota wetu, Brazzaville

Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakutana jijini Brazzaville na kujadili hali ya amani na usalama katika maeneo yaliyokubwa na ugonjwa wa ebola.

Wanachama hao walikutana na pamoja na wataalamu wa afya kutoka nchi hizo kuanzia tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2019, jijini Brazzaville Jamhuri ya Kongo 

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Jamhuri ya Kongo, Mhe. Jean Claude Gakosso ambapo alisema kuwa mkutano huo uliitishwa kwa ajili ya kujadili masuala makuu mawili ikiwemo hali ya ugonjwa wa ebola katika ukanda wa maziwa makuu pamoja na hali ya usalama katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa wa ebola.

Kuhusu hali ya ugonjwa wa ebola, ilielezwa kwamba nchi ya DRC ndiyo iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo. Ikielezwa kwamba zaidi ya watu 3000 wameathirka na ugonjwa huo na kati yao zaidi ya 2000 wamepoteza maisha ambapo maeneo yaliyoathika zaidi ni yale ya mashariki mwa DRC ambayo ni Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini.

“Juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya DRC hadi sasa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wengine katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa chanjo ya kinga ya ugonjwa huo na elimu kwa wananchi wa maeneo yaliyoathirika na ugionjwa huo” alisema Waziri Gakosso

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya kutoka ukanda wa maziwa makuu, imeelezwa kuwa hali ya maambukizi kwa sasa imepungua katika maeneo hayo.

Aidha, pamoja na jitihada hizo za serikali ya DRC kwa kushirikiana na wadau wengine katika mapambano hayo kumekuwa na changamoto ya usalama kutokana na kuendelea kuwepo kwa makundi ya waasi katika maeneo hayo ambayo yamekwamisha jitihada hizo

Katika hatua nyingine, mkutano wa waratibu wa kitaifa kutoka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kutoka nchi zote 12 walikutana na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo, michango ya wanachama, suala la ajira, hali ya ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa pamoja na suala la watu wasio na utaifa

Mikutano hiyo miwili imetangulia mkutano mkuu wa mawaziri wa mambo ya Nje kutoka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu utakao fanyika leo, Brazzaville ambapo ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro

Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.

Kiswahili chapendekezwa kutumika Ukanda wa Maziwa Makuu

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha pendekezo la Kiswahili kutumika katika ukanda wa maziwa makuu mjini Brazzaville jana
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Vicente Muanda wakiwa katika ukumbi wa mikutano, mjini Brazzaville jana
Balozi wa Tanzania Nchini DRC Luteni. Jen. Paul Mella akimueleza jambo balozi wa sudan wakati wa mkutano wa ukanda wa maziwa makuu mjini Brazzaville jana
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakifuatilia mkutano ulifanyika jana Brazzaville jana
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Bwn. Clement Mouamba jijini Brazzaville jana

…………………….

Na Mwandishi wetu, Brazzaville,

Katika jitihada za kukuza lugha ya Kiswahili barani Afrika, Tanzania imeziomba nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya kazi

Wito huo umetolewa katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu, uliofanyika mjini Brazzaville leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro 

“Tumewaomba wenzetu wa maziwa makuu wakubali lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha rasmi na lugha ya kazi katika nchi zote za maziwa makuu. Pia nchi sita ambazo zipo hapa na hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuruhusu Kiswahili kutumika kama lugha rasmi katika Afrika (AU) nchi hizo zimetuhakikishia kuwa zitaridhia mabadiliko hayo ili kuhakikisha kuwa Kiswahili kinaanza kutumika kama lugha rasmi ya kazi,” Alisema Dkt. Ndumbaro

Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda huo ni fursa ambayo italeta umoja wa kitaifa, na katika ukanda wa maziwa makuu lakini pia umuhimu wa Kiswahili kwamba ni lugha pekee ambayo haina uhusiano na ukoloni barani afrika. 

“Tunatumaini kwamba tutazipata sahihi za nchi sita na tukisha zipata tutabakiwa na sahihi ya nchi moja tu ili Kiswahili kiwe rasmi lugha ya kazi katika mikutano itakayo kuwa inafanyika barani Afrika,” aliongeza Dkt. Ndumbaro 

Nchi sita ambazo hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika kama lugha rasmi ya kazi ni pamoja na Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani, Uganda na Zambia. 

Kwa sasa hivi ni lugha rasmi lakini siyo lugha ya kazi kwa hiyo tumekwenda vizuri kwenye Kiswahili tunaamini ni fursa nzuri ya kuanza kukuza lugha ya Kiswahili katika bara la Afrika

Wakati huo huo, Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa, katika mkutano huo nchi wanachama waliweza kuongelea agenda kuu za nchi wananchama wa ukanda wa maziwa makuu ambazo ni Amani, Utulivu na Usalama hususani katika eneo la mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Sanjari na hilo, nchi nyingi zimeusifu uongozi wa Rais wa DRC, Felix Tshisekedi kuwa tangu alipoingia madarakani amejitahidhi kuhakikisha kuwa kuna kuwa na amnai ndani ya DRC pamoja na majirani zake. Pia Uganda, Rwanda pamoja na Angola zimesifiwa kufanikisha kusaini makubalianao ya kuleta amanai kati ya Uganda na Rwanda.

Akiongea awali wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje Mgeni rasmi ambae alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Bwn. Clement Mouamba alisema kuwa mkutano wa leo, umelenga kuisaidia nchi ya DRC katika changamoto inazopitia hasa katika ukanda wa mashariki.

“Nawapongeza sana kwa kazi ambayo mmekuwa mkiifanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa ugonjwa wa ebola unatokomezwa, kwani naamini kuwa umoja wetu tunaweza,” alisema Mouamba.

Aliongeza kwa kuzitaka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuendelea kulinda amanai na umoja walionao ili kuweza kuendelea na shughuli mbalimbali za maendeleo kwani bila amani ni vigumu sana kwa umoja huo kuendelea.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Jamhuri ya Kongo, ambae pia alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo Mhe. Jean Claude Gakosso aliwasisitiza mawaziri wa nchi wanachama kuwa amani na umoja katika ukanda huo ni nguzo muhimu sana na hivyo waendelee kuishika amani hiyo.

Pia aligusia ugonjwa wa ebola na kuwataka nchi wanachama kutokata tama ya kupambana na ugonjwa huo licha ya changamoto zinazojitokeza. 

“Juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya DRC hadi sasa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wengine katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa chanjo ya kinga ya ugonjwa huo na elimu kwa wananchi wa maeneo yaliyoathirika na ugionjwa huo” alisema Waziri Gakosso.

Mkutano wa leo ulitanguliwa na mikutano miwili ambayo ilianza tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2019, jijini Brazzaville ambapo pamoja na mambo mengine ilijadiliwa suala la ugonjwa wa ebola na hali ya amani katika maeneo yenye mlipuko wa ugonjwa huo.

Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.

Mwezi Augusti, 2019 Umoja wa Maendeleo ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Africa (SADC) ulifanyika Tanzania Jijini Dar es Salaam nchi wananchama waliridhia na kuipitisha kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya Umoja huo baada ya Kiingereza, Kireno na Kifaransa.

DKT. MPANGO AITAKA BENKI YA DUNIA KUSAIDIA SEKTA YA KILIMO NCHINI TANZANIA

0
0
Na Ramadhani Kissimba na Eva Valerian, Washington Dc 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) ameitaka Benki ya Dunia kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania ili kuweza kuwainua kiuchumi wakulima hasa wale wa kati na wadogo.

Dkt.Mpango aliyasema hayo wakati wa kikao cha majadiliano na timu nzima ya Benki ya Dunia ambayo inafanya kazi nchini Tanzania na wengine kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo nchini Marekani. 

Mhe.Mpango alisema katika mkutano huo walipitia kwa pamoja utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hivi sasa inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, lakini pia walipitia na kujadili miradi ambayo inaanza kufikiriwa kwa ajili ya utekelezaji kwa mwaka utakaofuata.

‘’Moja ya vitu vilivyonifurahisha mwaka jana kwenye mjadala niliwaaomba sana kwamba hatuwezi kuendelea kuitaka Benki ya Dunia isaidie kwenye miradi mingine tu ni lazima nguvu kubwa ielekezwe pia kwenye miradi ya kilimo ambayo kwa sasa msaada wa Benki ya Dunia katika miradi hiyo ni kidogo sana’’ alisema Dkt.Mpango.

Aidha Dkt.Mpango alielezea dhamira ya Tanzania kushirikiana na Benki ya Dunia ili kuanzisha programu itakayohakikisha kuwa tija inapatikana kwenye sekta nzima ya kilimo na mifugo, lakini pia kuweza kuyafikia masoko kwa mazao yanayozalishwa nchini, hasa yale yenye thamani kubwa duniani.

Dkt. Mpango amefafanua kuwa Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya mabdiliko inayofanyika katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka, lakini vile vile wakulima wa kati wamezidi kuongezeka. 

Aidha, kuongezeka kwa maeneo ya kilimo imewafurahisha wataalamu wa Benki hiyo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa aina ya mazao yanayolimwa hasa yale yenye thamani kubwa ambayo yanalimwa kwa kasi kubwa sana kuliko ilivyokuwa awali.

Pia Dkt. Mpango alisisitiza kuwa, Benki ya Dunia imeshafanya utafiti wao wa kutosha ambao umeonesha kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka.

Mhe. Mpango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali tena kuleta timu ya wataalamu nchini Tanzania ambayo itakaa na sekta nzima ya kilimo na ufugaji ili kuona ni namna gani hasa Benki ya Dunia itasaidia kuinua sekta hiyo, na kuwasaidia wakulima hasa katika matumizi ya nguvu kazi kwa upande mmoja na kuwaongezea kipato kwa upande mwingine.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifuatilia majadiliano katika Mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika uliofanyika Jijini Washington DC. Kulia kwa Mhe.Mpango ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru na anayefuatia ni Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Msafiri Mbibo.
Mtaalam wa Masuala ya Kilimo kutoka Benki ya Dunia Bw. Holger Krag akifafanua jambo kwa ujumbe wa Tanzania.

WADAU MVIWATA WATAKIWA KUTULIA ILI MGOGORO UTATULIWE

0
0
Na.Joseph Lyimo

WADAU na wanachama wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) wametakiwa kuwa makini, watulivu, na wavumilivu wakati huu kukiwa na mgogoro wa kiusajili na kikatiba wa taasisi hiyo. 

Mwenyekiti wa MVIWATA Mkoani wa Arusha, John Safari ameyasema hayo wakati akisoma taarifa ya MVIWATA ya mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro na bodi ya wadhamini juu ya mgogoro huo. 

Safari alisema Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania ni shirika la wanachama lililoanzisha mwaka 1993 na wakulima wakiwezeshwa na Chuo Kikuu cha Sokione ili kutetea maslahi ya wakulima wadogo na waweze kunufaika na shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa na mtandao wao. 

Alisema MVIWATA ilisajiliwa mwaka 1995 chini ya sheria ya vyama (Society Ordinance Act) kwa usajili namba SO 8612 na Mwaka 2000 ilisajiliwa Bodi ya Wadhamini ili kukidhi matakwa ya kisheria. Mwaka 2007 MVIWATA ilipata cheti cha ukubalifu (Certificate of compliance) chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiseriali na kusajiliwa kwa namba 1930.

Alisema MVIWATA ilipitisha azimio na kuliweka kwenye katiba linalotaka kuundwa kwa mitandao ya kati na kuisajili katika ngazi mikoa na wilaya lengo kubwa lilikuwa ni kuimarisha nguvu ya MVIWATA, kusogeza madaraka kwa wanachama, kuimarisha ushirikishwaji na kuboresha huduma kwa wanachama. 

“Katika mikoa ambayo usajili umefanyika, mafanikio yamejionesha wazi, mwaka 2016, serikali kupitia wizara husika ilifanya uhakiki wa asasi za kiraia na kushauri mitandao ya MVIWATA kusajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kama Chama cha Kijamii,” alisema Safari.

Alisema sababu kubwa kwa nini MVIWATA isajiliwe kama Chama cha Kijamii ni kuwa, MVIWATA ni chombo kinachoundwa na wanachama na hao hao wanachama ndiyo wanufaikaji wa shughuli na huduma za MVIWATA. Hii ndio tofauti inayoifanya MVIWATA isifae kusajiliwa kama Shirika lisilo la Kiserikali (NGO).

“Kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyo ya Kiserikali, Na. 24/2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na marekebisho ya sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 3/2019 na kwa kuwa malengo ya MVIWATA ni kuwanufaisha wanachama wake, tumeshauriwa tena na wataalam katika ofisi za usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kusajili MVIWATA chini ya Sheria ya Vyama vya Kijamii (Societies Act) Sura 337 ya Sheria za Tanzania,” alisema Safari.

Alisema pamoja na ushauri makini uliotolewa na wataalam wa wizara husika, suala hilo bado limeleta mivutano baina ya MVIWATA Taifa (Bodi ya Wakurugenzi), Mitandao ya Kati iliyosajiliwa na wanachama. Mivutano hii imesababisha Halmashauri ya MVIWATA kuunda Kamati kwa lengo ya kuangalia mivutano hii na changamoto zake na kutoa ushauri wa nini kifanyike.

“Jambo la kusikitisha ni kwamba, baada ya Kamati kufanya kazi yake, mambo yafuatayo yamejitokeza na yanaendelea kujitokeza:
Muda wa kamati kufanya kazi (siku 7) ulishapita na kamati haijapewa nafasi haijawasilisha taarifa kwa Halmashauri ya MVIWATA, hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu ucheleweshwaji huu,” alisema Safari. 

Alisema kikao cha Halmashauri ya MVIWATA hakijaitwa kupokea taarifa ya Kamati. Pia, hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu sababu za kutofanya hivyo.
Kutofanyika kwa Mkutano Mkuu wa MVIWATA ambao awali ulipangwa kufanyika tarehe 9 – 11 Oktoba 2019. 

Alisema hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya kuahirishwa kwa mkutano huu na sababu za kuahirisha.Badaya yake, sasa inafanyika mikutano ya upotoshaji katika mikoa mbalimbali inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Watumishi kwa lengo la kupotosha ukweli kuhusu usajili unaopaswa kwa MVIWATA na kujenga mgawanyiko kati ya mitandao iliyosajiliwa na ambayo haijasajiliwa.

Kuendelea kusambazwa kwa taarifa za uongo kwamba mitandao ya kati iliyosajiliwa ina nia ya kujitenga na MVIWATA (mtandao wa kitaifa) jambo amblo si kweli Kuendelea kushinika mabadiliko ambayo hayatokani na wanachama na yaliyo kinyume na dhana na makusudi ya kuanzishwa kwa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania.

Kuleta mgawanyiko na kutengeneza matabaka ndani ya mtandao kitu kinachoondoa umoja ambalo ni kusudui la msingi kwa ajili ya kujenga taasisi yenye nguvu yenye sauti ya pamoja Kuonekana dhahiri kwa dhamira ya kufuta mitandao ya kati ya MVIWATA kunakojionesha katika mapendekezi ya Bodi ya Wakurugenzi yaliyowasilishwa kwa Halmashauri.

“Jambo hili linaongeza mashaka kwamba kuna baadhi ya watu wachache wanataka kumiliki mtandao badala ya wanachama wenyewe na kutokana na changamoto hii na kile kinachoendelea sasa, tunapenda wanachama wa MVIWATA kote nchini, wadau wetu na umma uelewe kwamba:
MVIWATA ni moja na itaendelea kuwa moja katika muundo wake wa kimtandao unaoanzia kwenye vikundi, Mitandao ya Msingi, Mtandao ya Kati na Mtandao wa Taifa,” alisema. 

Alisema ieleweke wazi kuwa, muundo huu haufanyi na haujawahi kufanya uwepo wa MVIWATA nyingi bali umewezesha ukuaji wa MVIWATA na kuimarisha sauti ya pamoja.

Alisema wanachama na Mitandao ya Kati ya MVIWATA imekusudia kufanya usajili wa MVIWATA kama chama cha Kijamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kubakiza madaraka kwa wanachama ambao ni wakulima wadogo.

Alisema wanachama wasikubali upotoshaji unaofanyika sasa katika mikutano inayoendelea maeneo mbalimbali na kwamba wanachama wanapaswa kuhoji uhalali wa mikutano hiyo inayofanyika sasa na kuuliza kwa nini haikuwa inafanyika huko nyuma. 

Alisema ni vyema ikaeleweka wazi kwamba, mikutano inayoendelea sasa kupotosha ukweli kuhusu wapi MVIWATA ijisajili ni matumizi mabaya ya fedha ambazo zingefaa kufanya shughuli za utetezi wa maslahi ya wakulima. 

Alisema kama bodi ina nia ya dhati ya kufanya maboresho, inapaswa kuruhusu mjadala mpana wa wanachama unaowapa fursa ya kusikiliza mawazo na hoja za pande zote ili wanachama wafanye uamuzi sahihi wenye taarifa za kutosha.

Alisema waelewe wazi kwamba Mitandao ya Kati iliyosajiliwa, haina nia wala kusudi la kujitenga, kujiondoa ama kukiuka katiba ya MVIWATA, badala yake inasimama kidete kutetea maslahi ya wanachama na azma ya kuundwa kwa mtandao.

“Ieleweke pia kwamba, Mtandao huu ni wa wanachama, unaomilikiwa na wanachama na kuongozwa na wanachama wenyewe na sio watumishi wake, na kitendo chochote cha kuruhusu baadhi ya watumishi kuchukua madaraka ya uongozi wa mtandao, kunaleta hatari ya ustawi na lengo la mtandao, hatukubaliani na mabadiliko ya mfumo na muundo wa shirika ikiwa ni pamoja na kuondoa usajili wa ngazi za kati,” alisema.

“Hatukubaliani na muundo wa mabaraza na mikutano ya wanachama ambayo inaondoa nia ya uanzishwaji wa mtandao na kupora madaraka ya wanachama, hatuna imani na Bodi ya Wakurugenzi kwa kuleta mabadiliko yanayopora madaraka ya wanachama, kubadili dhana ya mtandao na kutaka kuondoa mtandao kwenye makusudi ya kuundwa kwake,” alisema. 

Alisema kutokana na maelezo hayo hapo juu, wao viongozi na wanachama wa Mitandao ya Kati iliyosajiliwa, wanaomba wasajili katika wizara husika kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro huo na wanawaomba wanachama na wadau wao kuwa makini, watulivu na wavumilivu wakati mgogoro huu unapotatuliwa.

WANAWAKE WA KIJIJI CHA GEHANDU WAIOMBA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MWANAMKE WA KIJIJINI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu (Kulia) akitazama bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na wanawake waishio vijijinikatika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika katika Wilaya ha Hanang mkoani Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu (Kushoto) akitazama bidhaa za sabuni zinazotengenezwa na wanawake waishio vijijinikatika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika katika Wilaya Hanang mkoani Manyara.Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitoa salamu za Wizara na kuahidi kutoa fursa ya elimu kwa wanawake wawili kujifunza kuhusu Elimu ya utengenezaji wa umeme wa upepo nchini India katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika katika Wilaya ha Hanang mkoani Manyara.

????????????????????????????????????

Baadhi ya wanawake na wananchi wa Kijiji cha Gehandu wakifuatilia hotuba na salamu mbalimbali za viongozi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika katika Wilaya ha Hanang mkoani Manyara.



Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Gehandu katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika katika Wilaya ha Hanang mkoani Manyara.
…………………

Picha zote na Kitengo cha Mawasilino WAMJW


Na Mwandishi Wetu Hanang Manyara

Wanawake waishio katika Kijiji cha Gehandu wameiomba Serikali kutatua changamoto za Wanawake waishio kijijini hapo ikiwemo uhaba wa maji yanayopatikana umbali wa Kilometa 30 na ukamilishaji wa jengo la Kituo cha Afya litakaosaidia kutatua upatikanaji wa huduma za Afya.

Wakizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini wanawake wa Kijiji cha Gehandu mmoja wa Mwanamke Bi. Ate Giegon amesema kuwa wanawake wa kijiji hicho wanakabiliwa na tatizo la kutafuta maji kwa umbali mrefu ambayo ni changamoto kubwa kwani husababisha kusimama kwa shughuli nyingine za kiuchumi.

Ameongeza kuwa wanaume wamekuwa wakiwakandamiza wanawake kwa kuwaachia kushugulika na shughuli zote za nyumbani na za kiuchumi.“Wanaume hawana mchango wowote kwetu bali wamekuwa wakitukandamiza na kuturudisha nyuma katika maendeleo”alisema Bi. Ate

Bi. Ate ameiomba Serikali kutoa elimu kwa wanaume kuachana na vitendo vya ukatili na ukandamizaji kwa wanawake hasa wale waishio vijijini kwani kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakirudisha nyuma kimaendeleo.

Naye Bi Happy Gwarugwa ameeleza kuwa njia pekee ya kumkomboa mwanamke ni kumuelimisha kwa kumpatia elimu itakayomsaidia kupambanua fursa zilizopo zikamsaidia kujikwamua kiuchumi na kuindeleza familia na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa wanawake waliofanikiwa kupata elimu wasidie wanawake wenzao hasa waishio vijijini kupata elimu ya kutambua haki zao ambazo zinakandamizwa na wanaume kwa asilimia kubwa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Bw. Brayson Kibasa amesema kuwa Wilaya imejipanga katika kutatua changamoto za wananchi wa kijiji cha Gehandu haswa wanawake kwa kuhakikisha wanatekelza miradi ya maji itakayosaidia kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji kijijini hapo.

Bw. Kibasa ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang inajipanga kuhakikisha Boma la Kituo cha Afya lililojengwa kwa nguvu za wananchi linamalizika ili kuwezesha upatikananji wa huduma za Afya hasa huduma ya Mama na Mtoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi ameeleza kuwa Maadhimisho haya yanalenga kuwawezesha wanawake wanaoishi vijijini kutatua changamoto zinazowakabili wanawake wanaoishi kijijini kupitia rasilimali zinazowazunguka.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha Mwanamke hasa aishie kijijini kuondoka na vitendo vya ukatili amesema Wizara iimeanzisha na kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ambao unaeleza jinsi Jamii na Serikali inavyotekeleza wajibu wao katika kumlinda Mwanamke na vitendo vya ukatili dhidi yao.

Akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Gehandu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu ameiagiza Halmshauri ya Wilaya ya Hanang kuhakikisha changamoto zilizotolewa na wanawake wa kijiji cha Hanang zinapatiwa ufumbuzi na haswa suala la upatikanaji wa maji na huduma za Afya.

Aidha ametoa rai kwa wadau kuwawezesha wanawake wanaoishi kijijini ili waweze kujitegemea na kujiamini na hata kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kupunguza changamoto zinazowakabili.

Ameongeza kuwa wanawake hawana sababu ya kuogopa kujitokeza katika jamii kusimama na kupigania haki zao kwani italeta nguvu ikiwa wanawake wataungana pamoja kutetea haki zao.

Ameitaka jamii ya Mkoa wa Manyara kuachana na mila zisizofaa hasa vitendo vya ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni zinazosababisha kukatiza ndoto za watoto wengi wa kike nchini.

Aidha Afisa kutoka Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto Mkoa wa Manyara Pili Serieli amesema kuwa Mwanamke na Mtoto ndio waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili hivyo jamii inatakiwa kuripoti vitendo vya kikatili ili kumsaidia Mwanamke na mtoto na vitendo vya ukatili dhidi yao.

Ameongeza kuwa wananchi hawana haja ya kukata tamaa endapo mtuhumiwa akiwa ameachiwa huru kwa dhamana bali waendelee kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili kwani Jeshi la Polisi linaendelea kupambana na vitendo vya ukatili.

JUKWAA LA UTAWALA WA MTANDAO LAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MAFANIKIO, CHANGAMOTO ZA MTANDAO, WANAWAKE WATAJWA KUONGOZA KWA KUFANYA BIASHARA ZA MTANDAONI

0
0
Mtaalam wa Masuala ya mtandao ambaye pia nia Mhadhiri kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza wakati akifungua kongamano la wadau wa mtandao linaloendelea jijini Arusha.
Mratibu wa Kamati ya Jukwaa la Utawala wa Mtandao(IGF) Nazar Nicholas akifafanua jambo mbele ya wadau wa mtandao wakati wakongamano la kujadili mafanikio na changamoto za matumizi ya mtandao nchini.Kongamano hilo linafanyika jijini Arusha na kushifrikisha wadau kutoka taasisi za Serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada ambazo zinaendelea kujadiliwa katika kongamano la masuala la matumizi ya mtandao.Kongamano hilo linaendelea jijini Arusha ambalo limeanza leo 


Na Said Mwishehe, Arusha 

JUKWAA la Utawala wa Mtandao Tanzania (IGF), limewakutanisha wadau, taasisi za Serikali na asasi mbalimbali za kiraia kujadili mafanikio na changamoto zinazotokana na matumizi ya mtandao huku wanawake wakitajwa kuongoza katika matumizi ya mtandao biashara mara mbili Zaidi ya wanaume duniani. 

Akizungumza leo Oktoba 16,2019 katika ufunguzi wa kongamano hilo linaloendelea jijini Arusha, Mtaalam wa masuala ya mtandao na mkufunzi katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kasi ya matumizi ya biashara mtandao imekuwa kubwa sana katika miaka ya karibuni tofauti na hapo awali. 

Amesema katika utafiti alioufanya mwaka jana nchini, aliweza kugundua kuwa wanawake wamekuwa wakitumia fursa za uwepo wa mitandao katika kutangaza, kununua na kuuza kwa njia ya mitandao mara mbili Zaidi ya wanaume. 

Profesa Sedoyeka kupitia kongamano hilo ametoa mwito kuwataka watumiaji wa mitandao kuitumia katika njia salama ili kuepuka kutapeliwa hususani kwa wanaotumia kwa ajili ya kufanya biashara. 

Hata hivyo amesema mtandao kama rasilimali muhimu bado haitumiki vizuri kwani kuna tatizo la baadhi ya watumiaji kutoamini kama njia sahihi ya kufikisha ujumbe na ndio maana baadhi ya watu wakitumiwa barua kwa njia ya mtandao lazima watapiga simu kwaajili ya kuhakiki. 

Amewataka watumiaji wa mtandao kuweka nywila (password), ili kuepuka watu wanaotumia vibaya mitandao kwa kufanya uhalifu na kwamba endapo utapenda kumpatia mwenza wao nywila hiyo lakini lazima kuhakikisha simu au kompyuta imewekwa nywila. 

Kwa upande wake Mratibu wa Kamati ya Jukwaa la utawala mtandao Tanzania, Nazar Nicholaus, amesema matumizi ya mtandao yamekuwa na changamoto kubwa sana ambapo watu wamekuwa wakiitumia vibaya bila kujua athari za baadae. 

“Tumekuwa tukifuatilia yanayoendelea mtandaoni, bado kuna baadhi ya watu wanaitumia vibaya na wengine kutoa taarifa ambazo si sahihi.Kwa mfano hivi karibuni kuna mtu aliamua kutumia mtandao kutoa taarifa za kwamba mmoja ya Waziri Mkuu mstaafu nchini (akamtaja) amefariki dunia wakati sio kweli.Kuna mifano mingi tu ya matumizi yasiyo sahihi. 



“Ni jukumu la kila moja wetu kuhakikisha tunaitumia mitandao vizuri na ukweli uliopo katika mitandao kuna mambo mengi yenye tija Zaidi kwa maendeleoe ya nchi yetu.Mtandao ni zakidi ya kutuma picha katika Whtsap na facebook, hiyo ni sehemu ndogo sana na tunaweza kusema kama ni asilimia basi ni 0.0001,”amesema Nicholas. 

Kuhusu kongamano ambalo limewakutanisha wadau hao Nicholas amesema IGF inatambua umuhimu wa kuwakutanisha wadau wa masuala ya mtandao kwa ajili kukaa pamoja kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu njia bora ya kutumia mtandao na hivyo anaamini kupityoia kongamano hilo watatoka na mawazo yaliyo bora. 



“IGF tutaendelea kuwakutanisha wadau wa mtandao kwa ajili ya kujadiliana kwa pamoja.Tulikuwa tumesinzia kidogo lakini sasa tumeamka na binafsi niliamua kuchukua jukumu la kuhakikisha wadau wanakutana.
amesema Nicholas. 



Kuhusu nafasi ya watu wenye mahitaji maalumu wakiwamo wenye ulemavu kushirikishwa katika IGF, Nicholas amesema kwa kutambua nafasi yao imekuwa ikiwashirikisha na hata kwenye kongamano linaloendelea wameshirikishwa kikamilifu na mawazo na maoni yao yatapewa kipaumbele.

RAIS DKT MAGUFULI AENDEL:EA NA ZIARA YAKE MIKOA YA KUSINI

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia na wananchi wa Lukuledi wilayani Masasi Mkoani Mtwara wakati akiendelea na ziara yake mikoa ya kusini Leo Oktoba 16, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Lukuledi Maalumu wenye ulemavu wa kusikia wakati aliposimama kusalimia wananchi wa Lukuledi wilayani Masasi Mkoani Mtwara wakati akiendelea na ziara yake mikoa ya kusini Leo Oktoba 16, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiserbuka na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Rw3angwa mkoa wa Lindi wakati akiendelea na ziara yake mikoa ya kusini Oktoba 18, 2019 Picha na IKULU

Balozi Kairuki awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Vietnam

0
0
Balozi wa Tanzania nchini China ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Watu wa Vietnam, Mhe. Mbelwa Kairuki akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Vietnam, Mhe. Nguyen Phu Trong katika Ikulu ya Vietnam leo jijini Hannoi
Balozi wa Tanzania nchini China ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Watu wa Vietnam, Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Vietnam, Mhe. Nguyen Phu Trong katika Ikulu ya Vietnam leo jijini Hannoi.

Airtel yaja na huduma ya Tuma na ya Kutolea, huna haja ya kukokotoa gharama za kutolea tena

0
0
·Wateja wa Airtel Money kutuma pesa bila kuhofia makato ya kutolea

Ukitumia AIRTEL MONEY huna haja ya kukotoa gharama za kutolea, Menu imerahisishwa kukufanyia hayo yote.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua huduma ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money. Huduma hiyo inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’ itakuwa ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money pale wanapotuma hela. Huduma ya Tuma na ya Kutolea itawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kujisumbua kukokotoa gharama ya hela ya Kutolea.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda alisema, ‘Tunazindua huduma hii ikiwa ni kuadhimisha yale tuliohaidi katika wiki ya huduma kwa wateja ambapo ilianza tangu Oktoba 7 mwaka huu. Airtel imedhamiria kuendelea kuhakikisha ya kwamba inatoa huduma bora muda wote na hii ndio sababu tumekuwa tukiwaletea wateja wetu huduma na bidhaa ambazo ni za kiwango cha juu kabisa’.

Kwa muda mrefu, tumekuwa tukiona wateja wa Airtel Money wakituma pesa pamoja na ya ziada ambayo lengo lake ni kufidia gharama za Kutolea ambazo ni maarufu kama Tuma na ya Kutolea. Sisi Airtel nia yetu ni kuwapa wateja wetu kilicho bora, leo Airtel imekuja na huduma ambayo ni suluhishi wakati wa kutuma pesa kwani gharama za Kutolea zitakuwa zikikatwa wakati wa kutuma kwa kupitia menu ya Airtel Money. Nia yetu ni kuifanya huduma hii kuwa rahisi, nafuu na ya haraka pale mteja anapofanya miamala yake,’ Nchunda alisema.

Airtel imekuwa ikizundua na huduma na bidhaa za kipekee ambazo zinakidhi matakwa ya wateja wetu pamoja na kugusa maisha yao ya kila siku. Tuma na ya Kutolea ni huduma ya kipekee ambayo inawafanya wateja wetu kuendelea kufurahia huduma za Airtel Money, Nchunda aliongeza.

Nchunda alisema kuwa huduma hii inapatikana kwa urahisi. Kuanzia sasa, wateja wa Airtel Money hawatakuwa na hofu yoyote kuhusu gharama za Kutolea pesa kwani kupitia Tuma na ya Kutolea huduma ya kutuma pesa sasa imerahisisha kwa kutuma pesa pamoja na ya Kutolea.

Kwa mteja wa Airtel Money kufurahi huduma ya kutuma pamoja ya Kutolea, atatakiwa kufuata maelekezo yafuatavyo; · Kupiga menu ya Airtel Money *150*60# · Changua 1 Tuma Pesa · Changua 3 Tuna na ya Kutolea · Changua namba ya Kutuma ya Airtel · Ingiza namba ya kutuma · Weka kiasi cha kutuma · Weka namba yako ya siri

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema, Airtel inatambua kuwa ni muhimu kuweka mahitaji ya wateja wetu mbele. Ni kwa kupitia Airtel Money ambapo mteja anaweza kutuma pesa bure na sasa tumekuja na huduma suluhishi kwenye gharama za Kutolea. Tunajivunia kuwa na huduma zenye uwazi ambapo kwa sasa wateja watakuwa na uhakika wa kujua gharama halisi ya kutolea pale wanapotumia huduma ya Tuma na ya Kutolea. Airtel itaendelea kutoa huduma ambazo utapatikanaji wake ni rahisi, nafuu na za haraka ili kukidhi mahitaji ya wateja.

Kwa sasa, Airtel inaendelea kuwekeza kwenye mtandao ili uendelee kuwa mpana zaidi na kutoa huduma za kifedha bora zaidi hapa nchini. Airtel sasa inajivunia kuwa na zaidi ya 1,000 Airtel Money branches na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 60,000 ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma zote za Airtel kama vile kusajili kwa alama ya vidole, simu mpya za smartphone, vifaa vya simu pamoja huduma nyingine nyingi.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua huduma ya ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money. Huduma hiyo inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’ itakuwa ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money pale wanapotuma hela na itawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kujisumbua kupiga hesabu za gharama ya hela ya Kutolea. 
  Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua huduma ya ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money. Huduma hiyo inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’ itakuwa ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money pale wanapotuma hela na itawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kujisumbua kupiga hesabu za gharama ya hela ya Kutolea.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania na Mkurugenzi wa Airtel Money wa kampuni hiyo Isack Nchunda wakionyesha bango baada ya kuzindua huduma ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money. Huduma hiyo inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’ itakuwa ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money pale wanapotuma hela na itawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kujisumbua kupiga hesabu za gharama ya hela ya Kutolea.

WAFANYAKAZI WATATU WA TIGO NA WAFANYABIASHARA WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA KWA KOSA LA KUTAPELI WATEJA

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
WAFANYAKAZI watatu wa kampuni ya simu za mkononi Tigo, na wafanyabiashara wawili, wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi sita nje baada ya kukiri na kutiwa  hatiani kwa kosa la kutapeli wateja wa mtandao huo kwa njia ujumbe wa maandishi.

Wafanyakazi wa Tigo kutoka tawi la  Mlimani City  na Makao Makuu ya Kampuni hiyo waliohukumiwa ni Kokubelwa Karashani, Godfrey Magoye na Khalfan Milao ambao ni watoa huduma kwa wateja huku washitakiwa wengine ni Mohamed Abdallah na Moses Kilosa (mume wa Karashani) ambao walikuwa hawana kazi lakini walikuwa marafiki wa wafanyakazi hao wa Tigo.
 Hukumu hiyo imesomwa leo Oktoba 16, 2019 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambae,  amewatia hatiani washitakiwa hao baada ya kukiri kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hukumu hiyi, hakimu Rwizile amesema amesikiliza hoja za pande zote  na kwamba makosa waliyofanya washitakiwa si mepesi na kwa mujibu wa sheria anayepatikana na hatia katika makosa hayo anatakiwa kutumikia kifungo  hivyo, lazima adhabu kali itolewe ili kupunguza makosa ya mtandao.

Amesema washitakiwa watatakiwa kutumikia kifungo cha miezi sita nje na pia  simu 31 na laini zake pamoja na sare ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) vinataifishwa na kuwa mali ya serikali.

Kabla ya kutolewa kwa  adhabu hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa alidai washitakiwa waliingia makubaliano na DPP hivyo hawatarajii wapewe adhabu kubwa.
Katika utetezi wao,washitakiwa hao   waliiomba mahakama iwahurumie na kuwapa adhabu ndogo kwani hilo ni kosa lao la kwanza.

Awali Mbagwa alisoma hati mpya ya mashitaka ambapo mashitaka matano likiwemo la kutakatisha fedha liliondolewa na kusomewa mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma mashitaka hayo, Mbagwa amedai Januari Mosi 2018 na Juni 20,2019 maeneo ya Dar es Salaam na Arusha walijipatia  Sh 20,378,627 kutoka kwa wateja mbalimbali wa tigo kwa kutoa kwenye akaunti zao zao za Tigopesa bila idhini.

Mashtaka yaliyoondolewa  ni, kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti za wateja ,kuingilia mifumo ya kifedha ya Tigo pesa bila kibali, kupatikana na mavazi ya JWTZ.

Mawakili wa mpemba wa magufuli, wakwamisha kesi kuendelea

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kutolewa maamuzi kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Ali maarufu kwa jina la Mpemba wa Magufuli na wenzake, kwa sababu mawakili wanao wawakilisha ashitakiwa hawapo.

Katika kesi hiyo Mpemba anashtakiwa pamoja na, Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.

Mapema leo Oktoba 16, 2019 wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maamuzi na kuendelea na usikilizwaji hata hivyo, alidai mawakili wa washtakiwa hao hawapo mahakamani.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21,(jumatatu) na kusema kuwa, kesi haiwezi kurndela sababu mawakili hawapo hivyo, aliwataka washitakiwa kuhakikisha mawakili wao wanafika siku hiyo.

Washitakiwa hao  wanaokabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6  na tayari wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) wakiwa na lengo la kuomba msamaha na kukiri kosa hilo.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh  milioni 392.8  bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia inadaiwa Oktoba 26, mwaka huu, washitakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo10 vyenye   uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya USD 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Wanadaiwa kuwa  Oktoba 27, mwaka huu, wakiwa Tabata Kisukuru washitakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya USD 15,000  sawa na Sh milioni 32.7 .

Aidha, Oktoba 29, mwaka huu walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh  milioni 294.6   bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Askari wapelelezi wanaotuhumiwa kushawishi rushwa ya sh. Milioni 200 wafikia wanne

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

OFISA Upelelezi wa Kituo cha Polisi Kawe, Emmanuel Njegele  leo Oktoba 16,2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa na maofisa wenzake watatu  katika kesi ya kushawishi rushwa ya Sh milioni 200 iliyoko mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.  Mbali na Njegele, washtakiwa aliounganishwa nao ni, Maofisa Upelelezi, Shaban Shillah, Joyce Kitta na Ulimwengu Rashidi.  

Mapema, wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Nickson Shao alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika ila pia ameomba  kumuunganisha mshitakiwa Njegele katika kesi hiyo. 

Akisoma hati ya mashitaka Shao amedai Desemba 17, 2018 maeneo ya Rainbow Social Club, Kinondoni, wakiwa maofisa wa uchunguzi, waliomba rushwa ya Sh milioni 200 kutoka kwa Diana Naivasha kama kishawishi cha kutokuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali. 

Alidai washitakiwa hao wakiwa maeneo ya Kituo cha Polisi Kawe, wakiwa waajiriwa wa Jeshi la Polisi, walipokea rushwa ya Sh milioni sita kutoka kwa Naivasha.  Alidai Desemba 18, 2018 washitakiwa hao walipokea rushwa ya sh. milioni sita kutoka kwa Naivasha na Desemba 19, 2018 washitakiwa hao wakiwa Kituo cha Polisi Kawe, walipokea Sh milioni mbili kutoka kwa Naivasha.

Pia inadaiwa Desemba 23, 2018 washitakiwa walipokea rushwa ya Sh milioni mbili na Januari 3, mwaka huu maeneo ya Tamarind Restaurant wilayani Kinondoni, walipokea rushwa ya Sh milioni mbili.

Aprili 13, mwaka huu maeneo ya Tripple 7 Bar and Restaurant, wakiwa maofisa wa jeshi la polisi Idara ya Upelelezi walipokea rushwa ya Sh milioni moja Naivasha kama kishawishi cha kutokuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Katika mashitaka ya nane, inadaiwa kati ya Desemba 17,2018 na Aprili 13, mwaka huu maeneo yasiyojulikana jijini Dar es Salaam, Kitta alighushi maelezo ya Naivasha ya Desemba 17, 2018 ili kuonesha kuwa maelezo hayo ni ya kweli na yalisainiwa na Naivasha wakati si kweli.

Pia inadaiwa mshitakiwa Shillah na Njegele, Aprili 13, mwaka huu wakiwa maeneo ya Triple 7 walikiuka amri halali ya kukamatwa na Mpelelezi wa Takukuru, Colman Lubis.

Washitakiwa wote walikana mashitaka na upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Rwizile aliwataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya taifa ambapo kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni 10.

Pia aliwataka kuwasilisha mahakamani hapo hati za kusafiria na mmoja kati ya wadhamini hao ametakiwa kuwa na hati au uthibitisho wa mali isiyohamishika.

Washitakiwa wote wametimiza masharti ya dhamana na kesi imeahirishwa hadi Novemba 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images