Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 316 | 317 | (Page 318) | 319 | 320 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Edwin Moshi,Makete
  Jeshi la polisi wilayani Makete  mkoani Njombe linamshikilia  Fransis Pilla (36) mkazi wa kijiji cha Iwawa na kata ya Iwawa  wilayani hapa kwa makosa  mawili ya  utekaji nyara na  ubakaji  kwa binti mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.
  Akiongea na vyombo vya habari wilayani hapa afisa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya Makete Bw Gozbert Komba  amesema kuwa siku ya tarehe 15 mwezi huu walipokea taarifa  kutoka kwa msamaria mwema ambaye pia ni mwajiri wake bw. Erick Mbilinyi (34) ya      mtendewa kutekwa na kufungiwa ndani ya nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake maarufu kwa jina la pagale ambapo walifika katika jumba hilo  na kumkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.
  Amesema kuwa  mara baada ya kumkuta mtendewa huyo akiwa ametekwa walimhoji na yeye kukiri  kuwa amebakwa na  hajaoga tangu afanyiwe ukatili huo na hivyo kurahisishia  kupatikana kwa vipimo kutoka kwa madaktari kuwa ni kweli binti huyo amebakwa na kuongeza kuwa walikuwa wana mahusiano ya kimapenzi.
  Katika hatua nyingine mrakibu huyo amebainisha kuwa  mtendewa huyo alisema kuwa alitekwa nyara kwa siku tatu,   na hajala chakula kwa siku zote hizo ambapo alitekwa nyara tangu tarehe 3  mwezi Januari mwaka huu  majira ya saa saba mchana  mpaka tarehe 5 mwezi huu majira ya saa saba na nusu mchana. 
  Amesema polisi wanatarajia kumfikisha mahakamani siku chache zijazo

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries (TDL), Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi cheti cha kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hiyo, Ashura Omari  wakati wa hafla ya wafanyakzi kufurahi pamoja na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  TDL, David Mgwassa.
   Mkurugenzi Mtendajj wa Kiwanda cha Konyagi, David Mgwassa aimpatia Munisi cheti cha shukurani kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu waliotumikia kiwanda hicho.

   Mgwassa akimtunuku Michael Mrema cheti kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa TDL
   Wafanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi na familia zao wakishindana kufukuza kuku
   Sssa ni wakati wa mapumziko
  Watoto wa wafanyakazi wa TDL wakishindana mbio za magunia.

  0 0


  0 0
  0 0

  Familia ya Bwana na Bibi Moses Mwangende wanapenda kumshukuru Mungu kwa kufikisha mtoto wao  mpendwa Brayden Moses(Nsajigwa ) ametimiza miaka miwili leo. Mungu azidi kumpa afya na kumuepushia maradhi.

  0 0

  Pump ya Solar — Bei ni Tshs 5.5m wakati bei ya dukani Tshs 8.6m
  1. Pump yenye uwezo wa lita 3,000 kwa saa
  2. Ina Solar Panel 6 kila moja watts 80 bure
  3. Gurantee ya miaka 5
  4. Inafaa kwa matumizi ya nyumbani na shambani
  5. Vyuma vya kufungia solar juu ya paa BURE
  6. Installation ya pump na Solar BURE

  Solar Panel 3 - Bei ni Tshs 1.65m wakati bei ya dukani Tshs 2.4m
  1. Solar Panel 3 @ 150 Watts
  2. Zimetumika kwa mwaka mmoja tu
  3. Gurantee ya miaka 5
  4. Kila Moja Only Tshs 500,000
  5. Installation bure…
  6. Inafaa kwa matumizi ya nyumbani na shambani

  Vifaa vyote viko poa vinauzwa kwa sababu nimepata umeme wa Tanesco
  Mdau anapatikana Dar es Salaam wasiliana nae kwa 0757 245 750 au 0788 880 096

  0 0

  Tarehe 6 Januari nikiwa nimepaki gari eneo la Benaco Salasala, Dar es Salaam mida ya saa 11:30 jioni niliingia kanisani kwenye maombi.

  Muda mfupi baadae nilitoka nikakuta gari yangu imevunjwa lock ya mbele. Wezi waliiba bag jeusi lenye laptop na vitu vingine kama hard disc, lazer pointers na vitu vingine zikiwepo nyaraka muhimu. Miongoni mwa vitu vingine ni vyeti vya chuo kikuu cha Dar es Salaam na taarifa muhimu za tafiti mbalimbali.

  Ninaomba kama kuna yeyote anayeweza kusaidia kupatikana au kwa vitu hivyo au baadhi awasiliane nami kwa SIMU namba 0687375296. zawadi nono itatolewa kwa atakayefanikisha upatikanaji wa vitu hivyo.

  Computer ni aina ya PANASONIC ambazo hazipatikani hapa nchini kwa wingi, hata key za operating systems zake hazipatikani kwa vendors.

  Nitashukuru sana kwa msaada au taarifa yoyote.
  Wenu Mdau

  0 0  0 0

  Mwandishi na mwanamuziki Mtanzania, Freddy Macha, katoa video ya wimbo unaoyasifia mazingira, mandhari, watu, asilia na uzuri wa Tanzania kupitia mlima Kilimanjaro. Kibao hiki alichokitunga akiishi Brazil (na kurekodi mjini London 2001) kimeshirikisha wanamuziki wa Ulaya, Afrika Mashariki na Kati ambao wengi ni marafiki zake wa karibu sana. "Kilimanjaro" ni kati ya nyimbo zinazotazamiwa kufungua kinywa cha Albam mpya ya Macha, baadaye mwakani. 
  Pata maelezo zaidi : http://kitoto.wordpress.com/  0 0

  Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi (kulia) akinyanyua kwa furaha zawadi ya kinyago ambayo ni moja  ya zawadi alizokabidhiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto).Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria  Mhe  Youcef Yousfi ikiwa ni pamoja na ujumbe wake wamewasili nchini Tanzania. Nia na madhumuni ya ziara hiyo ni kudumisha ushirikiano katika sekta za nishati na gesi.
   Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Nishati na Madini (kulia) Profesa Sospeter Muhongo mara baada  ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini  Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi  akichangia mada kwenye kikao hicho
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia ) akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani). Aliyekaa upande wa kushoto ni Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wakuu wa mashirika na idara wa Wizara ya Nishati na Madini ikiwa ni pamoja na ujumbe wa Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria uliowakilishwa na wakuu wa taasisi na mashirika
   Baadhi ya wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wakuu wa Idara kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

  0 0
  0 0

   
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef  Yousfi (wa kwanza kushoto kwake) aliyeongozana na Ujumbe wake kutoka Kampuni ya Sonatrach na Sonalegaz za nchini Algeria, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumo leo Jan 7, 2014.
   Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef  Yousfi, aliyeongozana na Ujumbe wake kutoka Kampuni ya Sonatrach na Sonalegaz za nchini Algeria, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumo leo Jan 7, 2014. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Kampuni ya Sonatrach na Sonalegaz za nchini Algeria, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014. 
  Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef  Yousfi,  baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Mhongo. Picha na OMR

  0 0

  Mkoa wa Kilimanjaro unatarajia kujenga mji wa viwanda na biashara katika eneo la Lokolova ili kuchochea uongezaji thamani mazao na kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nchi jirani.
  Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Bw. Leonidas Gama aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni mjini Moshi kuwa eneo hilo ambalo tayari limebainishwa litatoa fursa kubwa ya biashara.“Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na sekta binafsi tumepanga mipango hii ili kuboresha biashara,” alisema, na kuongeza kuwa eneo hilo litajengwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.
  Alisema mji huo utakuwa nguzo kubwa kwa soko la kisasa la kimataifa linalotarajiwa kujengwa katika eneo hilo la Lokolova kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.“Mkoa wetu huu upo mpakani na ni mashuhuri sana katika biashara lakini bado tunauza mazao ambayo ni ghafi ambayo hayana tija kubwa ya kibiashara,” alisema.
  Alisema kama ilivyo katika maeneo mbalimbali nchini, bado wananchi wa mkoa huo wanauza mazao ghafi na kuwa ujio wa viwanda hivyo utasaidia kusindikwa kwa mazao hayo na hivyo kuleta tija zaidi.Alibainisha kwamba wakati wa kuuza mazao ghafi umepitwa na wakati, hivyo mipango hiyo imekuja katika kipindi sahihi ambapo mazao yataongezwa thamani na kupangwa katika madaraja ili kupata soko zaidi.
  Mkoa huo ni maarufu kwa mazao mbalimbali kama nyanya, ndizi, maparachichi na mbogamboga.Akizungumzia mradi mwingine alisema katika wilaya ya Siha wanatarajia kuanzisha kituo kikubwa cha kisasa cha utalii ili kuongeza utalii katika mkoa wao.
  “Kituo hiki kitajengwa katika maeneo yaliyokuwa ya Serikali ambayo kwa sasa hayatumiki, na kujengwa vivutio vizuri vya utalii mbalimbali,” alisema.Kwa mujibu wa Bw. Gama, mpango huo ukikamilika utaongeza idadi ya watalii na kusaidia kukuza mapato ya sekta binafsi na umma na kukuza uchumi wa nchi.
  Alifafanua kuwa vivutio vitakavyojengwa ni pamoja na eneo la maonyesho, bustani mbalimbali ikiwemo ya wanyama, maua, mahoteli ya kisasa na maeneo ya michezo.Pia utajegwa mfano wa mlima Kilimanjaro kwa ajili ya watalii ambao hawawezi kwenda kuona na kuupanda mlima huo maarufu barani Afrika.
  Alisema miradi yote hiyo itafanywa kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na biafsi kwa faida ya pande zote mbili.Alisistiza kuwa mkoa wake na halmashauri zote zimebainisha maeneo ya biashara na kuyatenga ambapo sekta binafsi itayatumia kufanya biashara bila vikwazo vyovyote.

  0 0

    Binti Aida Nakawala (miaka 25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya,akiwa na watoto wake wanne aliojifungua hivi karibuni katika hospitali ya Wazazi ya Meta,Jijini Mbeya.Mama huyo alijifungua Watoto hao wa wanne kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya na anaendelea vizuri kabisa.Mama huyo jana alitembelewa na baadhi ya Wadau wa Habari wakiongozwa na Mwanalineneke wa Blog ya Mbeya Yetu,Joseph Mwaisango,ambapo waliwasilisha mchango wao mdogo waliokuwa nao,wengine alioambatana nao katika kuwasilisha msaada huo ambao ni pesa taslim,simu ya mkononi na nguo za watoto hao toka kwa wasamaria wema ambao ni Yassin Kapuya , Hassan Othman,Mwanalibeneke Othman Michuzi pamoja na Dada Pendo Fundisha.
  Mwanalibeneke Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog (kulia) na Dada Pendo Fundisha wa New Habari (kushoto) wakiwasilisha msaada wa nguo kwa Mama aliejifungua watoto wanne kwa pamoja,Bi. Aida Nakawala.
  Mdau Ezekiel Kamanga pamoja na Mwanalibeneke Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog wakikabidhi msaada wa pesa taslim pamoja na simu ya mkononi kwa kwa Aida Nakawala,mama aliejifungua watoto wanne kwa pamoja.Utaratibu wa kumpatia mama huyo namba ya simu unafanyika hivi sasa na iwapo itakuwa tayari italetwa hapa hapa ili kwa yeyote atakaetaka kumsaidia mama huyo,aweze kufanya hivyo.
  Wakipata maelezo ya Maendeleo ya Mama huyo kutoka wa Muuguzi,Terecia Bahari (kushoto).

  Baadhi ya wadau waliomtembelea mama huyo hospitali ya Wazazi ya Meta,jijini Mbeya.

  0 0


  0 0

   Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula, akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam, kuwataka NSSF kufungua Ofisi zitakazotoa huduma za Westadi nchini Marekani ambazo zitawasaidia watanzania waishio nje ya nchi kusafirisha mwili wa marehemu pamoja na kupata huduma ya matibabu kwa ndugu wanne waliopo nchini. Kushoto ni Kaimu Meneja Kiongozi na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Theopista Muheta. 
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula (kulia), akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam, kuwataka NSSF kufungua Ofisi zitakazotoa huduma za Westadi ambayo itawasaidia watanzania waishio nje ya nchi kusafirisha mwili wa marehemu ikiwemo huduma ya matibabu kwa ndugu wanne waliopo nchini. Kushoto niKaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matessa.   
   Ofisa Mwandamizi wa huduma za Westadi, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. 
   Maofisa wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
   Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (kulia),   Ofisa wa NSSF, Neila Kambaya na  Halima Mgala.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa NSSF, Abdalah Mseli akizungumza katika mkutano huo. 
   Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja 
   Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Westadi. 
   Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matessa.

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Jumanne Januari 07, 2014 saa 3 usiku kwenda bara imeahirishwa hadi keshokuwa siku ya Alhamis Januari 09, 2014, saa 3 usiku.

   Taarifa hiyo imefafanua kuwa dharura hiyo ya kuahirisha safari imetokana na ajali ya treni ya mizigo iliyotokea juzi saa 2 usiku kati ya Stesheni za Luiche na Kigoma na kusababisha treni ya abiria kutoka Kigoma kushindwa kuondoka kuja Dar. 

   Wakati huo huo taarifa iiliyopatikana mchana huu imethibitisha kuwa ukarabati wa eneo lililoathirika na ajali ya treni ya mzigo ya juzi umekamilika na njia imefunguliwa saa 8:45 mchana huu. Aidha treni ya abiria kutoka Kigoma kuja Dar imeshaondoka mjini Kigoma tokea saa 9:20 alasiri ya leo. 

   Aidha taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

   Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji 
   Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu. 
   TRL Makao Makuu, 
   Dar es Salaam. 
   Januari 07, 2014

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinnduzi,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja jana, kuhudhuria katika Kikao cha Kamati Maalum ya CCM (NEC) kilichofanyika jana,(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinnduzi,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya CCM (NEC) kilichofanyika jana, Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja, (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
  Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM (NEC) wakipitia mada mbali mbali zilizoingizwa katika makbrasha waliyopewa katika kikao kilichofanyika jana katika ukumbi Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
  Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM (NEC) wakipitia mada mbali mbali zilizoingizwa katika makbrasha waliyopewa katika kikao kilichofanyika jana katika ukumbi Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinnduzi,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akizungumza na wajumbe wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya CCM (NEC) kilichofanyika jana, Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja, (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

   
   Mwakilishi  kutoka  Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo  ya Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa  shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za  Tuzo  za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST  zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.   
  Mwakilishi  kutoka  Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo  ya Singida, Fidel Samwel mmoja wa washindi wawili wa jumla wa  shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Fidel pamoja  na mwenzake Jafari Ngadula wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za  Tuzo  za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST  zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.   

  0 0

  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Martha Qorro akimkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara (wa kwanza aliyekaa kulia) kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo.wapili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa mara alipozindua Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa Bw. Selemani Hegga akitoa shukrani zake kwa wajumbe wa Bodi hiyo hawapo( pichani) katika shughuli ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akipata maelezo mafupi kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza kuhusu Ukumbi wa ndani wa Maonyesho wa Sanaa alipotembelea BASATA leo jijini Dar es Salaam (jana), watatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleao ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akitoa maelekezo kwa Wadau wa Sanaa alipotembelea Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kujionea shughuli zinazofanywa na Baraza hilo,nyuma ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.

older | 1 | .... | 316 | 317 | (Page 318) | 319 | 320 | .... | 3272 | newer