Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 317 | 318 | (Page 319) | 320 | 321 | .... | 3272 | newer

  0 0  0 0

  Mkurugenzi wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata mwongozo wa Umoja wa Mataifa.
  Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema juhudi zinahitajika katika kuwahamasisha Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa.
  Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.


  0 0

  Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wakitoa maelezo kuhusu shughuli wanazozifanya walipotembelewa na wananchi mbalimbali waliohudhuria maonyesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye viwanja vya Betrasi mjini Unguja.

  KATIKA  kukabiliana na uhaba wa Wakaguzi wa Marubani wa Ndege, Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeajiri wataalam watatu wa kada hiyo kwa mwaka 2013.

  Ofisa Habari wa Mamlaka hiyo, Ally Changwila alisema kuwa kuajiriwa kwa wataalam hao kunaongeza idadi yao na kufikia sita kwa sasa.
  Ofisa huyo alisema hayo wakati wa maonyesho ya siku tatu ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar yaliyomalizika jana visiwani humo.
  Kwa mujibu wa Changwila kada hiyo ya wakaguzi wa marubani inakabiliwa na upungufu wa watumishi 12 ili kufanikisha ufanisi katika eneo hilo.
  Aliongeza kwamba changamoto mbalimbali zinachangia eneo hilo kuwa na watumishi wachache ni gharama kubwa za masomo ya kada hiyo nje ya nchi na uduni wa mishahara.
  Awali alibainisha kwamba mwaka 2013 katika upande wa usajili wa ndege TCAA imesajili helkopta tatu mpya ambazo sasa zinatumika kufanikisha shughuli za utafiti wa mafuta, gesi na huduma za kukodi.
  Alieleza majukumu muhimu ya mamlaka hiyo kuwa ni udhibiti wa usalama, udhibiti uchumi katika eneo la anga na utoaji wa huduma za uongozaji wa ndege.

  0 0   Jumla ya vikundi 32 kutoka ndani na nje ya nchi vimechaguliwa kufanya maonyesho ya muziki katika tamasha la 11 la Sauti za Busara ambalo limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 13 mpaka 16 Februari 2014 katika viwanja vya kihistoria Ngome Kongwe, zanzibar.
  Orodha ya wasanii imejumuisha imejumuisha wasanii maarufu kutoka Africa Mashariki, Kusini na Afrika Magharibi, pamoja na wasanii kutoka nchi za Mto Nile na hata maeneo ya Puerto Rico
  Sauti za Busara (Sound of Wisdom) linalojulikana kama  ‘Tamasha rafiki katika Sayari’ ni tamasha la kimataifa linalosheherekea muziki wa kiafrika kila mwaka  wiki ya pili ya mwezi wa Februari. Lengo likiwa ni kuwaleta watu  pamoja na kuonyesha utajiri wa muziki wa kisasa ambao umebuniwa katika nchi za Afrika Mashariki,  nchi nyingine kutoka barani Afrika na kwingineko duniani.
  Wasanii watakaopanda jukwaani kutoka hapa nyumbani ni pamoja na Jhikoman nguri wa muziki wa Rege anayesifika hapa nchini  na ambae ameshafanya maonyesho mbalimbali ya muziki ndani na nje ya nchi, ambapo kwa upande wa Sauti za Busara hii ni mara yake ya nne kupanda jukwaani. Jhikoman mpaka hivi sasa amesha toa albam tatu zinazojulikana kama Chikondi aliyoitoa mwaka 2005, Tupendane, 2008 na Yapo, iliyoingia sokoni mwaka 2009.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Jana Desemba 7, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe E. maswi ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Jana Desemba 7, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Jana Desemba 7, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe E. maswi ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2014.

  0 0

  Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
   Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.

  Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.

  Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa  Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una  muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.
   Tundu Lisu akiwatuliza na  kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
  Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini  ameshinda kesi yake hiyo aliyoifungua akiitaka Kamati Kuu ya Chadema kutojadili Uanachama wake hadi kesi ya msingi aliyoifungua itakaposikilizwa.
  Habari zaidi utaendelea kuzipata hapa
  Wafuasi wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe wakimshangilia kiongozi wao alipokuwa akiwasili Mahakamani hapo leo.
  Sehemu ya Wafuasi wa CHADEMA wasiomkubali Zitto Kabwe wakiwa na Mabango yao nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  The late Samuel Kumalija Chagula
  Beloved father, grandparent and dear friend to many Samuel Kumalija Chagula, died peacefully aged 63 on Monday 23rd December at 6:20am at the Royal Free Hospital, Hampstead, London UK.

  Samuel touched many with his great sense of humour, charm, intelligence and an uncanny ability to brighten any room he walked into. As he often remarked, ‘Life is dynamic’ and it is perhaps this that sums him up best. Fondly remembered, never forgotten, Samuel was a ‘true man of the people’ and will be dearly missed by all that knew him.

  Samuel is survived by his mother Asha, children Josephine, James, Gosbert, Henry, Diana, Caroline and grandchildren Dalvin, Denzil, Daniel and Dominic.

  If wishing to make a contribution towards funeral costs, please transfer funds into the bank account listed below. Please ensure to that you include your full name when asked for a reference.


  Account Holder: Ms Josephine Chagula

  Bank: Halifax

  Sort code: 11-04-16

  Account number: 00232703

  Funeral Details

  12pm January 17th 2014

  Hendon Cemetery Chapel

  London, Holders Hill Rd, London NW7 1NB

  *Funeral to be followed by Reception at ‘The Claddagh’ in Hendon, Church Road, NW4 4EA

   For more information please contact one of the family members listed below:
  Josephine Chagula: josephinejames04@yahoo.co.uk-07941 569 052

  James Chagula: jchagula@hotmail.com– 07453 816 484


  Gosbert Chagula: gosbertc@gmail.com– 07779 263 188


  0 0

  Na Othman Khamis Ame,
   Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  Skuli za Msingi na Sekondari zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa katika sehemu mbali mbali za Visiwa vya Unguja na Pemba ni maeneo maalum yaliyotengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzalisha vijana wengi wa elimu ya juu watakaotegemewa kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa hili. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiifungua rasmi Skuli ya Sekondari ya Mpendae ikiwa ni muendelezo wa sherehe za Maadhimisho ya Kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. 
  Balosi Seif alisema Wananchi wanaposherehekea miaka 50 ya Mapinduzi wanajinasibu kwa kuwa na Skuli za Sekondari 144 zenye jumla ya wanafunzi 76,706 ikiachiwa Chuo cha Ualimu cha Beit-el-Ras, ambacho kilichukua na idadi ndogo ya wanafunzi wa kusomea ualimu. 
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kazi nzuri iliofanya katika kipindi cha miaka 50 takeo kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964. 
   Balozi Seif alizitaja Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na kuendelea kuimarisha miundombinu ya elimu, kuipandisha hadhi sekta ya elimu hasa katika ujenzi wa skuli za msingi, sekondari pamoja na vyuo vya amali. 
   Aliwasihi vijana kutozichezea fursa zilizopo za kusoma na kuwataka kuongeza bidii ya ushindani ili wende sambamba na vijana wenzao wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki. “ Skuli sasa ipo nyumbani, kilichobaki ni juhudi yao tu ya kufanya vizuri katika masomo ya msingi ili waweze kuingia katika Skuli hii “. Alisema Balozi Seif. 
  Alieleza kwamba kwa vile Serikali ina mpango wa kutoa kompyuta za kutosha kwa kila skuli ili wanafunzi waweze kutumia mitandao kwa ajili ya masomo yao aliwashauri kujifunza somo la kompyuta litakalowarahisishia kujifunza kwa urahisi zaidi. 
   Akizungumzia suala la kupanua kiwango cha taaluma Balozi Seif aliushauri Uongozi wa skuli ya Mpendae pamoja na masomo ya kawaida wakajipangia kuwa na mafunzo ya ziada ambayo yatasaidia wanafunzi kuchemsha bongo ili kuondokana na kuwa na mambo kila siku darasani. Alieleza kwamba Skuli za sekondari zinaweza kuanzisha midahalo, michezo ya kuigiza kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili kurejesha mfumo ulokuwepo ambao ulisaidia kuimarisha kiwango cha elimu kilichoipatisa sifa kubwa Zanzibar wakati huo. 
   “ Pamoja na masomo ya kawaida, ni muhimu pia kuwa na mafunzo ya ziada ambayo yatasaidia wanafunzi kuchemsha bongo ili kuondokana na kuwa na mambo yale yale (routine) kila siku darasani, ili waongeze motisha wa kusoma “. Alisisitiza Balozi Seif. 
   “ Mathalan, skuli za sekondari zinaweza kuanzisha “debating societies”, michezo ya kuigiza kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Mambo haya ambayo zamani yalikuwepo sasa hayapo tena. Ni vema kurudishwa katika skuli zetu za sekondari “ Aliendelea kufafanua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. 
   Katika risala yao walimu, wanafunzi na wazazi wa skuli ya Mpendae iliyosomwa na Mwalimu Muhaymina Talib Omar wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo katika jitihada za kukamilisha ujenzi wa Skuli hiyo. 
  Walisema ujenzi wa skuli hiyo umewapa faraja kubwa kutokana na uwepo wa huduma muhimu za lazima anazopaswa kuzipata mwanafunzi ikiwa ni pamoja na Maabara, Maktaba, Kompyuta pamoja na huduma za maji safi na salama. Hata hivyo Walimu, Wanafunzi na Wazazi wa Skuli hiyo walizitaja baadhi ya changamoto zinazowasumbua ndani ya skuli hiyo ikiwemo ukosefu wa uzio wa skuli hiyo jambo ambalo linawapa wakati mgumu katika yulinzi wa skuli yao. 
  Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Mwanaidi Saleh alisema ujenzi wa skuli hiyo ya ghorofa ya sekondari Mpendae ni miongoni mwa skuli Mpya 19 za Sekondari zilizojengwa hapa Zanzibar. 
  Alisema skuli hizo zimo ndani ya mradi wa uimarishaji wa elimu ya lazima ambao unatekelezwa kwa pamoja kati yua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Benki ya Dunia { World Bank } kwa gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 48. 
  Bibi Mwanaidi alisema uwepo wa skuli hiyo ya sekondari ya Mpedae utasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi uliopo katika skuli mbali mbali za jirani zilizopo Mwanakwerekwe. Ujenzi wa skuli ya Mpendae ambao Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Salum Turky na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Mohammed Said Mohammed Dimwa walioahidi kuweka mafeni kwenye madarasa yote ya skuli hiyo katika kipindi kifupi kijacho imegharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Bilioni 1.6. Skuli hiyo yenye madarasa 12 ina uwezo wa kuhudumia wnafunzi wapatao 660 ambapo wanafunzi 40 kila darasa kwa mikondo miwili ikiwa kwa sasa ina wanafunzi sitini na moja. 
   Jengo la Skuli mpya ya Ghorofa ya Mpendae lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ikiwa ni muendelezo wa shamra  shamra za maadhimisho ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kulifungua rasmi jengo jipya la skuli ya Ghorofa ya Sekondari ya Mpendae.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua sehemu mbali mbali za skuli ya ghorofa ya Sekondari ya Mpendae mara baada ya kuifungua rasmi.
   Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mpendae MwalimuMbarouk Rashid Habib akimpatia maelezo Balozi Seif mara baada ya kuifungua rasmi skuli hiyo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua sehemu mbali mbali za skuli ya ghorofa ya Sekondari ya Mpendae mara baada ya kuifungua rasmi.
  Jengo la Skuli mpya ya Ghorofa ya Mpendae lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ikiwa ni muendelezo wa shamra  shamra za maadhimisho ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0
 • 01/07/14--20:34: Article 22


 • 0 0


  0 0

   
   Mkurugenzi mtendaji wa Daraja Fonndation Bi. Arsheen Dhalla yenye Makao Makuu yake Canada akiitambulisha Jumuiya yao inayojishuhulisha na sekta ya Afya, Elimu na Watoto mayatima katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Amore Mio Mjini Zanzibar.
   Baadhi ya watoto yatima na walezi wao waliofika katika uzinduzi wa Jumuiya ya Daraja Fonndation katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Amore Mio Mjini Zanzibar.
   Afisa wa Afya wa Daraja Fonndation Bwa. Ahmed Said Suleiman akielezea jinsi ya Jumuiya yao inavyofanya kazi zake hapa Zanzibar katika sherehe iliyofanyika Hoteli ya Amore Mio Mjini Zanzibar.
  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0
 • 01/08/14--01:40: Article 19


 • 0 0

  Meneja wa Fedha wa Benki ya NMB, Deogratias Usangira akipokea Tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Goodluck Ole Medeye. Benki ya NMB imepokea tuzo hii ya ushindi wa kwanza wa kuwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2012 kutoka kwenye Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu nchini. Hafla hii ya makabidhiano ilifanyika hivi karibuni mkoani Arusha.

  Maafisa wa benki ya NMB (toka kushoto) Evarist Webby, Jonathan Eliamlisi, Deogratias Usangira na Israel Kingu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea tuzo hii ya ushindi wa kwanza wa kuwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2012 kutoka kwenye Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu nchini katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni mkoani Arusha.

  0 0

  Wilaya ya  chunya  - wizi wa gari.


  Mnamo tarehe 06.01.2014 majira ya  saa 15:00hrs huko eneo la kuegesha magari ya  Kampuni ya  Sunshine Mining LTD katika kijiji cha Matundasi, kata ya Matundasi,  tarafa ya  Kiwanja, Wilaya ya Chunya   mkoa wa Mbeya.  Msabaha s/o Rashid  Kafulama, fundi mkuu wa kutengeneza  magari wa Kampuni hiyo aliiba gari lenye nambari za usajili T 421 CHG aina ya  Toyota L/Cruiser ingle cabin rangi nyeupe chases no JCLB-715407036705 lenye thamani ya  USD 35,000 na kwenda mahali kusikojulikana. Mbinu ni kujaribu kuendesha gari hilo baada ya  kulifanyia matengenezo.  Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mbeya  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi   anatoa  wito kwa yeyote mwenye taarifa juu ya  mahali alipo mtuhumiwa pamoja na gari azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake,vinginevyo ajisalimishe mwenyewe.


  Wilaya ya  Mbarali  - Ajali ya  Moto.


  Mnamo tarehe 06.01.2014 majira ya  saa 20:15hrs huko katika Shule ya Wasichana ya  Sekondari Igumbilo inayomilikiwa na Kanisa la Lutherani, iliyopo  kata ya  Chimala, tarafa ya  Ilongo wilaya ya  Mbarali mkoa wa Mbeya. bweni moja la shule hiyo liliungua moto na  kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani ya  bweni hilo. chanzo bado kufahamika, ingawa uchunguzi wa awali unaonyesha ni hitilafu ya  umeme. hakuna madhara ya  kibinadamu yaliyotokea. thamani halisi ya  mali iliyoteketea bado kufahamika. Kamanda wa Polisi  mkoa wa Mbeya  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi   anatoa  wito kwa jamii kuwa makini na kuchukua tahadhari dhidi ya  majanga ya  moto.


  Wilaya ya Mbeya Mjini – kupatikana na pombe haramu ya  moshi
                                                             [gongo].


  Mnamo tarehe 07.01.2014 majira ya saa 12:50hrs huko katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Mponzi kilichopo kata ya  Kagera, tarafa ya  Sisimba jiji na   mkoa wa Mbeya.    Askari Polisi wakiwa doria /msako walimkamata Prisca d/o Godwin, miaka 27, Kyusa, Mkulima, mkazi wa mtaa wa Kagera    akiwa na pombe haramu ya  moshi [gongo] ujazo wa lita 1.5. mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa pombe hiyo. taratibu zinafanywa ili afikishwe Mahakamani. Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mbeya  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi   anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia pombe haramu ya  moshi[gongo] kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya  mtumiaji.

  signed by:

   [Ahmed Z. Msangi -SACP].

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

  0 0


  0 0

  Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa binti wa Mratibu wa Dua maalum ya kuiombea Zanzibar, Clare Allen Mbaga walipomtembelea na kumuombea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Mratibu wa Dua Maalum ya kuiombea Zanzibar kwa ajili ya mwaka mpya wa 2014 Allen Mbaga akizungumza na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipomtembelea na kumuombea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Picha ya pamoja ya Kamati maalum ya kuiyombea Zanzibar kwa ajili ya mwaka mpya 2014 na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi ilipomtembelea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpinduzi ya Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

  0 0

  The Martha Shani Foundation on June 2014 will be supporting The  Ocean Road Cancer Hospital in Tanzania the following items: 1. Sanitary needs of the patients 2.  Health Care supplies: Both hospital wall-mounted hand sanitizers and portable sanitizers, hand wash soaps, exam and surgical gloves , alcohol swabs, wound bandages and sunscreens for protection of the skin plus many others stuff. As we count down to the event you can be the part of it by donating the above items to us. Please share this great news and feel free to ask for more info on how you can participate.

  CONTACTS
  Program coordinator
  Alex Kassuwi
  301 305 9685
  EMAIL
  kassuwi@gmail.com

  0 0

  NA RAMADHANI JUMA,OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO

  MKUU wa mkoa wa Rukwa  Mhandisi Stella Manyanya ameziagiza Halmashauri zote Mkoani hapa pamoja na taasisi nyingine za serikali kutotoa kazi yoyote ya ujenzi kwa kampuni ya ujenzi ya ‘Juin Constructions Company Limited ’ kutokana na kampuni hiyo kuonekana  kufanya kazi zake chini ya kiwango.

   Alitoa maamuzi hayo wakati alipokuwa akikagua jengo la bweni la wasichana linalojengwa katika shule ya sekondari ya Kasanga iliyopo kata ya Kasanga wilaya ya Kalambo Mkoani  Rukwa .

  Alisema wakandarasi wengi wamekuwa wakiihujumu mikoa ya pembezoni mwa nchi ukiwemo Mkoa wa Rukwa kwa kujenga miradi isiyo na viwango kwa muda mrefu sasa, na kwamba umefika wakati wa kupambana na hali hiyo.

  Aliagiza kampuni hiyo  iwekwe kwenye orodha ya makampuni yasiyotakiwa kupewa kazi katika mkoa wa Rukwa mara moja ili iwe fundisho kwa makampuni mengine yanayolipwa fedha za umma kwa kazi zilizo chini ya kwango.

  Mbali kutekeleza jengo hilo chini ya kiwango, Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema mkandarasi huyo amekuwa hafuati ushauri wa wataalam wa Halmashauri ya Kalambo iliyompa kazi hiyo.

  “Mkandarasi huyu hajawahi kupatikana katika eneo la mradi wakati wa ukaguzi hata siku moja..kila mara wakaguzi wakitembelea mradi huu yeye huwa hayupo kwahiyo huyu hatufai katika mkoa wetu” alifafanua.

  Kwa upande wake mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Issa Liyanga alisema wamekuwa wakimsimamia mkandarasi huyo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo ambapo hata hivyo amekuwa na ushirikiano hafifu katika kuzingatia ushauri unaotolewa.
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya (kulia) akizungumza wakati akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo. Pembeni yake ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Philbert Ngaponda.
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya akizungumza wakati akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo. Kulia ni mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Sumbawanga Vijijini ndugu Mtapima na katikati ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga.
  Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga akimuonesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya alipokagua jengo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo.

older | 1 | .... | 317 | 318 | (Page 319) | 320 | 321 | .... | 3272 | newer