Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 315 | 316 | (Page 317) | 318 | 319 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014
   Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao mwisho kwa mwili wa marehemu Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu na familia yake wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014. 
  Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiwa wamebeba sanduku lenye mwili wa marehemu Dkt William Mgimwa  kwenye  viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014 tayari kwa kusafirishwa kuelekea mkoani Iringa ambako ndiko mazishi yake yatafanyika.PICHA NA IKULU

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Afisa Mawasiliano wa TASAF Zablon Bugingo 
  Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la TASAF
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisikilkiza  maelezo kuhusu  faida na matumizi ya asali ya masega kutoka kwa  Khamis Suleiman Masoud wa kikundi cha JUKUNUM Cooperative cha Vitongoji Kibokoni Pemba 
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipewa maelezo ya namna ya kutengeneza lulu toka kwenye gamba la Chaza Bahari na Mwajuma Haji Sharif (wa kwanza kulia mwenye kofia) toka kikundi cha Tujikomboe Co-operative Makombeni Pemba . Wa pili kulia ni Nasra Yusuf Yakuob wa kikundi cha Mwendapole Co-operative Mangapwani Unguja  .PICHA ZIADI BOFYA HAPA

  0 0
 • 01/05/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Los Lobos wanatamba hadi leo na 'La Bamba'

  0 0


  MAAZIMIO YA KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU HATUA ZA KINIDHAMU DHIDI YA WANACHAMA ZITTO ZUBERI KABWE, DR. KITILA MKUMBO NA SAMSON MWIGAMBA
  UTANGULIZI

  Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilikaa kikao cha dharura ili kupokea, kujadili na kuamua juu ya utetezi wa mashtaka ya ukiukaji wa Katiba, Kanuni na Mwongozo wa Chama yaliyokuwa yanawakabili aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Zuberi Kabwe, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu Dr. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba. Kikao hicho cha dharura kilifanyika Dar es Salaam kati ya tarehe 3-4 Januari, 2014. Kabla ya kuanza kwa kikao, Kamati Kuu ilipokea taarifa kwamba Zitto Zuberi Kabwe amefungua mashtaka dhidi ya CHADEMA katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam. Aidha, Kamati Kuu ilijulishwa kwamba Mahakama Kuu imetoa amri ya zuio la muda ya kuizuia Kamati Kuu au chombo kingine cha Chama kutokukaa, kujadili na kuamua suala la uanachama wa Zitto Zuberi Kabwe. Kutokana na amri hiyo ya Mahakama Kuu, Kamati Kuu haikujadili na kuamua juu ya mashtaka dhidi yake.
  MASHTAKA
  Watuhumiwa wote watatu walishtakiwa jumla ya mashtaka 11 yanayohusu ukiukaji wa vifungu mbali mbali vya Katiba ya Chama, Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama, Kanuni za Kusimamia Shughuli, Mwenendo na Maadili ya Wabunge wa Chama na Mwongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Chama, Mabaraza na Serikali. Mashtaka yote yalitokana na watuhumiwa kuandaa kile kinachoitwa Mkakati wa Mabadiliko, 2013 kama ifuatavyo:

  0 0

   Rafiki wa mpendwa wetu Catherine Nyongole akishindwa kujizuia  mara tu alipomuaona mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera alipofika nyumbani kwa marehemu kutoa pole na kujumuika nao katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao Zainab Buzohera aliyefariki jana jioni Jan 4, 2014 katika hospitali ya Doctor's Community iliyopo Goodluck Rd, Lanham, Maryland. Msiba upo nyumbani kwa wafiwa 5030 57th Ave, Bladensburg, Maryland na leo baadae kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha ilikusaidia kuusafirisha mwili wa marehemu harambee itafanyika 5401 Anapolis Rd, Bladensburg, Marland kuanzia saa 10 jioni(4pm) Lengo ni kujitahidi kumsafirisha mpendwa wetu siku ya Jumatano Jan 8, 2014.Watanzania wakiamua hawashindwi na jambo.
   Watanzania wa DMV wakijumuika na wafiwa nyumbani kwa marehemu.
   Catherine Nyangole mwenye kilemba cheusi pamoja na WanDMV wakimpa pole mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera nyumbani kwa marehemu.
   Watanzania wa DMV wakiendelea kutayarisha makulaji kwa ajili ya wageni watakaofika nyumbani kuwapa pole wafiwa.
   Watanzania DMV wakijumuika pamoja na wafiwa nyumbani kwao
  Watanzania wa DMV wakiwafariji wafiwa.

  0 0

  Joe Kahama (mwenye miwani na shati la draft) akiwa na waumini katika ibada na baadaye harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisda la Kimkunda,Kyaka,mkoani Kagera. Katika shughuli hiyo, Joe aliwatia homa wabunge wa majimbo ya eneo hilo pale alipoeleza kuwa hatoongea sana lakini watarajie kumsikia sana siku za mbele. Katika hafla hiyo, Joe alichangia shilingi milioni 3 na kushiriki mnada kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo. Picha zifuatazo ni za tukio hilo.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Mrembo wa  Redds  Miss Kanda ya Mashariki , Diana Laizer , ambaye ni Miss  Morogoro 2013  akimkabidhi  zawadi ya vyakula Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watu  wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo  , Padri Beatus Sewando ( kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho siku ya kwanza ya mwaka mpya  2014 akiwa na mshindi wa tatu wa Miss Morogoro, Muzne Abduly  pamoja na Mratibu wa  Miss Kanda ya Mashariki , Alex Nikitas ili kuwafariji na kusherekea kwa kula chakula nao.( Picha na John Nditi).
  Picha ya pamoja
  ========  ======  =========
  REDDS MISS KANDA YA MASHARIKI AMBAYE PIA NI MISS MORO 2013 ASIFIWA ALIVYOJITOA KUSAIDIA  WATU WENYE ULEMAVU WA VIUNGO NA MTINDIO WA UBONGO KITUO CHA AMANI.
  Na John Nditi, Morogoro
  KITUO cha Amani kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro  na kinachowahudumia  Watu  wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo, kutoka sehemu mbalimbali mkoani hapa  kimepongeza  Redds Miss Kanda ya Mashariki , Diana Laizer  , kutokana na kuonesha upendo na kulijali  kundi la watu wa aina hiyo  kwa kutoa msaada wa  vyakula.
  Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Kituo hicho,  Padri Beatus Sewando , siku ya kwanza ya mwaka mpya 2014,  kwa Miss Kanda ya Mashariki  ambaye pia ni Miss Morogoro 2013.
  Mrembo huyo ambaye  kwa sasa ni Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) siku hiyo alikitembelea  Kituo hicho  akiwa na   mshindi wa tatu Miss Morogoro, Muzne Abduly , pamoja  na  Mratibu wa Miss Kanda ya Mashariki, Alex Nikitas ambapo alitumia siku hiyo kula na kucheza nao burdani za ngoma.
   Mkurugenzi wa Kituo hicho  alisema ,  watoto wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo wanayo mahitaji  mengi ukiwemo kuwaonesha  upendo na wanapotembelewa  na wageni hasa nyakati za sikukuu na kupatiwa  zawadi  wanapata faraja kubwa kwa kujiona nao ni sehemu ya jamii.
  “ Binafsi yangu nikiwa Mkurugenzi wa Kituo hiki , walengwa na wazazi wao tumefurahi na tumefarijika  kwa uamuzi wako kututemebela siku ya mwanzo ya kuanza mwaka huu wa 2014 , umetuletea zawadi ya vyakula” alisema na kuongeza.
    Japo wewe mwenyewe umesema ni kidogo , lakini kwetu sisi tunakiona ni kikubwa , watoto wamefurahi , kutoa ni moyo na si utajiri , kikubwa umejitoa kujakushinda nasi  leo hii” alisema Padri Sewando.
   Hata hivyo alisema , kituo hicho cha Amani kina  watoto 42  wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo na hakina ufadhili wa n je  na wadani , kinawategemea watu wenye kujitoa na kitendo cha Miss Kanda ya Mashariki kukitembelea na kutoa zawadi ya vyakula ndiyo ufadhili wenyewe.
  Pamoja na hayo alisisitiza kwa kusema “ Kituo hakina ufadhili na nina  waomba wote wanaoshinda kuwa Miss Morogoro  waige mfano wa Miss Diana , ambaye amejitoa  na kuutumia muda wake  kusaidia jamii  isiyojiweza” alisema na kusisitiza kuwa.
  “ Jambo hili ni kubwa na linayapa hadhi  mashindano haya  ambayo  jamii yetu  siku zote imekuwa na  fikra potufu ya kuwa Ma Miss  ni wapenda  starehe na anasa, lakini sivyo ilivyo miaka ya hivi sasa ” alibainisha.
  Naye Redds Miss Kanda ya Mashariki, alisema kuwa , moja ya majukumu yake ni kusaidia jamii hasa makundi ya watoto yatima na wenye ulemavu sambamba na wanaishi  katika mazingira magumu , wakiwemo wa Kituo hicho.
  Hivyo alisema, kwa kutambua jukumu hilo, siku hiyo ya mwaka mpya aliamua kukitembelea Kituo hicho  na kutoa  msaada wa vyakula ,kula nao na kuburudia kwa pamoja ili kuonesha upendo.
  Hivyo alitoa wito kwa washiriki wengine wa Urembo wajitokeza kusaidia makundi kama hayo kile kidogo wanachokuwa nacho kwani wao pia ni sehemu ya jamii inayohitaji kutunzwa kiafya , kielimu na kijamii.

  0 0
 • 01/05/14--20:14: Article 17


 • 0 0

  Wakurugenzi Wa Kampuni Ya Maxcom Africa Wakitoa Taarifa Ya Utekelezaji Kwa Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda Nyumbani Kwake Kijiji Cha Kibaoni, Mpanda Mkoani Katavi. Maxcom Africa Inamiliki Na Kuendesha Mtandao Wa Malipo Ya Kielektroniki Wa Maxmalipo

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akisikiliza Kwa Makini Wakati Mkurugenzi Mtendaji Wa Maxcom Africa Bwana Juma Rajabu Akisisitiza Jambo Wakati Akitoa Taarifa Ya Utekelezaji Walipomtembelea Nyumbani Kwake Kijiji Cha Kibaoni, Mpanda Mkoani Katavi.

  Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akiagana Na Wageni Wake Wakurugenzi Wa Kampuni Ya Maxcom Africa Wanaomiliki Mtandao Wa Malipo Ya Kielektroniki Wa Maxmalipo Baada Ya Kupokea Taarifa Ya Utekelezaji Walipomtembelea Nyumbani Kwake Kijiji Cha Kibaoni, Mpanda Mkoani Katavi

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Eneo Huru la Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru (aliyekaa kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Madeni Kipande (aliyekaa kulia) wakitia saini makubaliano ya uendelezaji wa hekta 10 za eneo huru la bandari ya Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Wanaoshuhudia ni Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia); Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw.Gregory Teu (kushoto) na mwanasheria wa TPA, Bi. Koku Kazaura (katikati).
   ===========  =========  ========
  EPZA, TPA zafikia makubaliano kuendeleza eneo huru la Bandari Mtwara
  Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zimefikia makubaliano ya uendelezaji wa hekta 10 za eneo huru la bandari ya Mtwara.Makubaliano haya ni awamu ya kwanza ya uendelezaji wa jumla ya hekta 110 za eneo hilo huru la bandari ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali.
  Hekta hizo 10 zitaendelezwa kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa na kisha kugawiwa kwa makampuni ya kimataifa yanayofanya kazi za kutoa huduma mbalimbali kwa makampuni yanayofanya kazi ya utafiti wa mafuta na gesi katika mkoa wa Mtwara.
  Kitakapomalizika, kituo hiki cha huduma kwa makampuni yanayofanya utafiti wa gesi na mafuta mkoani Mtwara kitakuwa cha kipekee si kwa Tanzania pekee bali katika ukanda mzima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
  Utiaji saini makubaliano hayo ya kihistoria mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Madeni Kipande na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw.Gregory Teu.
  Akiongea wakati wa tukio hilo, Dkt. Mwakyembe alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa makampuni ya kimataifa yanayotoa huduma kwa kampuni za utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta kuwekeza Mtwara na pia kutoa huduma zake katika eneo hili la Afrika.
  Waziri huyo alisema tayari kampuni saba ziko tayari kuwekeza katika eneo hilo na akazitaka mamlaka husika kuhakikisha zinafanya haraka na kwa usahihi matayarisho yote yanayotakiwa ili kampuni hizo ziweze kuanza kufanya kazi mara moja.“Mamlaka husika hazina budi kumaliza haraka na kwa usahihi matayarisho yanayotakiwa ili uwekezaji huu uanze mara moja,” alisema.
  Alisema kabla ya hapo kampuni hizo zilikuwa zikitoa huduma zake kutokea Mombasa, Kenya na Afrika ya Kusini.Waziri Teu alisema hatua hiyo ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania.“Mtwara na Tanzania sasa vinafunguka zaidi,” alisema, na kuongeza kuwa baada ya kuanza kazi, kampuni hizo zitazalisha ajira kwa watanzania na kuongeza wigo wa kodi kwa serikali.
  Kwa upande wake, Dkt. Meru alisema hatua hiyo ni muhimu sana kwa kuwa kampuni hizo zitatoa huduma kwa makampuni yanayofanya utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta katika nchi za Kusini na Mashariki ya Afrika.Alisema ujio wa kampuni hizo pia utasaidia katika kuendeleza sekta nyingine kama hoteli na kilimo katika mkoa wa Mtwara.
  Baadhi ya kampuni zilizoonyesha nia ya dhati kuwekeza katika eneo hilo la hekta 10 ni pamoja na Schlumberger, Weatherford and Halliburton International Inc toka Marekani; Lena, FFF (T), Alpha group and Queensway toka Dubai na Uingereza; Altus Tanzania Ltd toka Singapore; Tans Ocean Industries & Services Ltd toka Dubai na Intershore Tanzania Ltd ya Afrika ya Kusini.

  0 0

  Mume wa marehemu Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera wakiwa kwenye harambee ya kuchangisha fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa mpendwa wetu marehemu Zainab Buzohera aliyefariki Jumamosi Jan 4, 2014 saa 2 usiku (8pm ET) WanaDMV walijumuika katika harambee iliyofanyika Bladensburg, Maryland na kuchangisha $22,938 kiasi kilichokuwa kinatakiwa ni $15,000 hii inamaanisha wanaDMV wanapoamua hufanya kweli shukurani kwa wote walioshiriki harambee hii kwa njia moja au nyingine lengo ni kufanikisha na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema tunashukuru kwa kutuwezesha kufanikiwa harambee hii ya mpendwa wetu Zainab Buzohera. WanaDMV tunawashukuru wenzetu wa New York waliofika kwenye harambee hii kuja kusaidia kutimiza malengo.
  Shangazi wa marehemu Jasmine Bernett akiongea kwa niaba ya familia ya Buzohera huku akiwa amejawa na uso wa huzuni aliwashukuru  wote waliofika kwani lengo ni kusaidia kuchangia ili mwili wa marehemu Zainab uweze kusafirishwa nyumbani Tanzania kwa mazishi na matarajio ni kusafirisha siku ya Jumatano na kisomo kinatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne jioni mahali patatangazwa baadae.
  Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akielezea utaratibu wa harambee.
  Umati wa Watanzania waliokuja kwenye harambee.

  0 0

   Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini
  Moshi,MUWSA,Injinia Cyprian Luhemeja akimsindkiza waziri wa maji
  Jumanne Maghembe kujionea shuguli za uchimbaji wa kisima katika eneo
  la tanki la maji la Kilimanjaro.
   Waziri Maghembe akitoa maelekezo kutoka kwa mkandarasi anaye chimba
  kisima katika eneoo la tanki la maji la Kilimanjaro.

   Mitambo ya kuchimbia visima ya kampuni ya DDCA ikiendelea na shughuli
  za uchimbaji katika eneo la tanki la maji la Kilimanjaro.
  ========  ========  ==========
  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  TAASISI za serikali nchini zikiwemo hosptali ,majeshi ya Polisi na
  Magereza zimetajwa kuwa ndio wadaiwa wakubwa wa Ankara za maji ambazo hadi sasa zinafikia kiasi cha zaidi ya shilingi ya sh bilioni  10
  jambo linalosababisha baadhi ya mamlaka za maji kupata changamoto
  kutekelezaji mipango yake

  Waziri wa maji, Profesa Jumanne Maghembe, alisema hayo akijibu baadhi
  ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari sanjari mwenyekiti wa bodi
  ya mamlaka ya majisafi na majitaka mjini Moshi(MUWSA) baada ya
  kutembelea tanki la maji Kilimanjaro na chanzo coffe curing mjini
  hapa.

  Tayari deni hilo limewasilishwa serikalini kwa utaratibu maalum na
  kwamba mipango ni kuona kwamba kila fedha zinapopatikana zinalipwa ili
  kupunguza ama kumaliza kabisa deni hilo.

  “Madeni haya ni kero,lakini tangu tumeyawasilisha serikalini, yapo
  mashiriki ambayo tayari yameanza kulipwa fedha hizo,sielewi ni kwanini
  MUWSA haijalipwa….nadhani baada ya mkutano wetu huu watasikia na
  kuanza kuyalipa kwa kasi Zaidi”alisema Maghembe.

  Hata hivyo,Profesa Maghembe,alipongeza juhudi za mamlaka katika
  kuongeza vyanzo vya maji na kuondokana na mgawo uliokuwepo awali huku
  akitaka maeneo ya Majengo,Bomambuzi, Kiborlon na maeneo mengine ya
  pembezoni kupewa kipaumbele Zaidi.

  Awali katika swali lake la msingi,mwenyekiti wa bodi ya MUWSA, Shally
  Raymond, alitaka kufahamu juhudi za serikali katika kulipa madeni ya
  Ankara za maji kwani kutolipwa kwa fedha hizo ni kikwazo katika
  utekelezaji wa baadhi ya shughuli za mamlaka hiyo.

  Mapema katika taarifa yake kwa waziri Maghembe,mkurugenzi wa mamlaka hiyo,mhandidsi Cyprian Luhemeja alisema wamefanikiwa kuongeza chanzo cha coffe curing chenye lita za ujazo wa 1500 huku juhudi za kuchimba kisima katika tanki la Kilimanjaro kitakachokuwa na lita za ujazo 1800 kwa siku zikiendelea.

  Alisema mamlaka ilijipa muda wa siku 180 kutekeleza mipango yake
  ambapo walikusudia kukarabati miundombinu na kuondoa mtandao mbovu
  wenye urefu wa Km 85 lakini hadi kufikia juzi mchakato wa kuondoa Km
  24 umekamilika ambapo vifaa vimeshanunuliwa.


  Kuhusu upotevu wa maji,mkurugenzi huyo alisema kwa kipindi cha Juni
  2013 kulikuwa na upotevu wa mai wa asilimia 38 lakini hadi kufikia
  disemba mwaka 2013 kiwango hicho kilishuka hadi kufikia asilimia 24 na
  mipango ni kufikia asilimia 9 ifikapo Juni 2014.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mbarak Abdulwakil akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu wakati IGP alipokwenda kujitambulisha ofisini kwake kwa lengo la kufahamiana na kupanga mikakati mbalimbali ya kuzuia na kupambana na uhalifu.Katikati ni Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Mwamini Malemi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mbarak Abdulwakil akisalimiana Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP) Abdulrahman Kaniki (kulia) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na  Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Mwamini Malemi wakati IGP alipokwenda kujitambulisha ofisini kwake kwa lengo la kufahamiana na kupanga mikakati mbalimbali ya kuzuia na kupambana na uhalifu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mbarak Abdulwakil akizungumza  na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu  na Naibu IGP Abdulrahman Kaniki wakati Viongozi hao wa Jeshi la Polisi walipokwenda kujitambulisha ofisini kwake kwa lengo la kufahamiana na kupanga mikakati mbalimbali ya kuzuia na kupambana na uhalifu.Katikati ni Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Mwamini Malemi .
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mbarak Abdulwakil akisalimiana na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki  wakati alipokwenda kujitambulisha ofisini kwake kwa lengo la kufahamiana na kupanga mikakati mbalimbali ya kuzuia na kupambana na uhalifu.DIGP.

  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam,imeahirisha kutoa au kutotoa zuio la muda kwa kamati Kuu ya CHADEMA kutojadili uanachama wa Zitto Kabwe mpaka kesho mnamo  majira ya saa nane mchana.


  0 0


  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani) alipowaita kwa kuijitambulisha kwao na kutoa taarifa ya matukio mbali mbali yaliyotokea kwa kipindi cha Mwaka 2013.
   Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali jijini Mbeya,wakiendelea kuchukua taarifa aliyokuwa akiitoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi. 
   Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi (hayupo pichani).
  Mwanalibeneke Othman Michuzi (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa Habari toka vyombo mbali mbali jijini Mbeya mara baada ya Mkutano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.kutoka Kulia ni Ezekiel Kamanga (Bomba FM),Freddy Jackson (Mbeya FM),Freddy Njeje (Tone MultMedia Group),Joseph Mwaisango (Mbeya Yetu Blog),Dada Pendo Fundisha (New Habari) pamoja na Shomi Mtaki (Uhuru/Mzalendo).

  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Ilala, Jesca Njau (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbindo, Phillemon Haule (kulia), mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 68 ikiwa ni msaada wa kugharamia ukarabati wa miundombinu ya maji katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mhandisi wa TBL, John Malisa (wa pili kushoto) na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela.
   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Dk. Meshack Shimwela (wa pili kulia), mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 68 ikiwa ni msaada wa kugharamia ukarabati wa miundombinu ya maji katika Wodi ya Wazazi ya katika hospitali hiyo.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika hospitalini hapo Dar es Salaam juzi, ni Mhandisi wa TBL, John Malisa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbindo, Phillemon Haule.

  0 0

   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa maelezo ya utangulizi katika ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (MB) akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga (MB) akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga   (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungua rasmi Mafunzo ya wiki mbili ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini. (Picha zote na Veronica Kazimoto – Morogoro).


  =========  =======  ======
  OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAWANOA WAKUFUNZI WA UTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI
  (Na Veronica kazimoto – Morogoro)
  06 Januari, 2014.

  Ukosefu wa Ajira umekuwa ni changamoto kubwa kwa sasa duniani kote ambapo ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu hali ya ajira duniani, inaonesha kuwa takribani  watu milioni 197 sawa na asilimia 5.9 ya nguvu kazi duniani hawana kazi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga   wakati akifungua Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.

  Dkt. Mahanga amesema kati ya watu 197 ambao hawana kazi vijana ni milioni 73.8 sawa asilimia 12.6 ambayo ni nguvukazi inayopaswa kutumika ipasavyo kwa kuwa kuna mahusiano makubwa kati ya ukuaji wa tija na matumizi ya nguvukazi. Ameongeza kuwa, kutokana na changamoto hiyo ya ajira, ni muhimu kufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya kazi ili kuisaidia Serikali kufuatilia mwenendo wa mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira.

  Mahanga amefafanua kuwa utafiti huu utasaidia pia kuboresha sera na program mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA. Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo amesema lengo kuu la Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi ni kukusanya takwimu zinazohusu hali ya soko la ajira nchini.

  Kwesigabo amesisitiza kuwa utafiti huo utawezesha  kupata viashiria vinavyohusu ajira na ukosefu wa ajira kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii na hivyo kuisaidia Serikali kuboresha sera ya kukuza ajira nchini. Mafunzo hayo ya wiki mbili yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaendelea kupewa mafunzo juu ya Utafiti huo  wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka 2014.  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP)  Faustine Shilogile, aliyesimama, akitoa neno wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya namna ya kupambana na makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto na kuhusisha askari Polisi kutoka katika kanda tatu za mikoa ya Dodoma, Pwani pamoja na Morogoro mafunzo hayo ni ya siku tano yanayoendelea kufanyika mjini Morogoro.( picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi).

  ========  =======  ========
  JESHI LA POLISI NCHINI LAENDESHA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA.

  Na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Morogoro

  Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa, maendeleo ya nchi yeyote duniani yanategemewa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji katika elimu na ulinzi wa mtoto, dhidi ya aina zote za unyanyasaji katika ngazi ya familia pamoja na jamii inayomzunguka.

  Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na washiriki wa mafunzo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayofanyika mkoani hapa ya namna ya kushughulikia makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto,  Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro,  (SACP), Faustine Shilogile, amesema kuwa, kwa sasa kumekuwa na taarifa nyingi zinazotolewa katika vituo vya Polisi kote nchini, taarifa ambazo nyingi zikihusisha watu mbalimbali kufanyiwa vitendo vya kikatili.

  Pamoja na kudharirishwa  kijinsia ambapo kamanda Shilogile, amesema kuwa,  jamii inatakiwa kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto kwa kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani hususan aina zote za  ukatili wa majumbani, jambo ambalo litaongeza tija katika maendeleo, alisema.

  Aidha, kamanda Shilogile, amesema kuwa, kupitia mafunzo haya kwa askari wa Dawati la jinsia na watoto kuhusu kushughulikia makosa yanayohusu ukatili ambapo itasaidia kuongeza ujuzi na kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi kwa askari Polisi katika kushughulikia makosa yanayohusiana na ukatili wa kijinsia, alisema.

  Hata hivyo, Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amesema kuwa, licha ya Jeshi la Polisi kuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, hivyo dawati la jinsia linawajibu wa kuhakikisha linatoa huduma bora kwa jamii, alisema.

  Kamanda Chialo, ameongeza kuwa, kutokana na mafunzo haya kutolewa kwa watendaji wa jeshi la Polisi na kuwahusisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa ya Dodoma, Pwani pamoja na Morogoro,  na kudhaminiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), yatasaidia zaidi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuifanya jamii kutokuwa na takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia.


  0 0

   Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi  akipokewa na walimu wa Philter Federal School ya Fuoni Meli Tano kwenye hafla ya wazazi wa skuli hiyo pamoja na maadhimisho ya kutimia miaka Mitano ya Skuli hiyo.
   Baadhi ya Wazazi waliohudhuria hafla wazazi na maadhimisho ya miaka Mitano ya Federal School ya Fuoni Meli tano zilizofanyika Hoteli ya bwawani Mjini Zanzibar.
   Wanafunzi wa  Maandalizi wa Federal School ya Fuoni wakionyesha umahiri wao katika kudumisha utamaduni wa Zanzibar ukianmbata na vazi maarufu la Kanga ya Kisutu.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


  =========  ========  =======
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi ameiasa Jamii kwamba uigaji wa hulka na Tabia za kigeni zinazoonekana kulikumba zaidi kundi kubwa la Vijana unazalisha malezi mabovu yanayokwenda kinyume na Utamaduni wa Taifa hili.

  Kauli hiyo aliitowa kwenye halfa ya mahafali ya wazazi pamoja na maadhimisho ya kutimia miaka mitano ya Philter Federal School  iliyopo Fuoni Meli Tano nje kidogo ya Mji wa Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.

  Mama Asha alisema wakati dunia inaendelea kupitiwa na mabadiliko makubwa ya mitandao ya Teknolojia wazazi wanapaswa kuwa makini  kipindi hichi cha mpito katika kufuatilia nyendo za watoto wao.

  Alisema licha ya muda mwingi wa watoto hao unakuwa ndani ya himaya ya walimu lakini bado Wazazi wanawajibu mkubwa wakuhakikisha wanashirikiana  na walimu hao katika kuwafinyanga watoto wao kuelekea katika njia sahihi. Katika kuimarisha kiwango cha elimu maskulini hasa kwa zile skuli za binafsi zinazojitegemea zenyewe Mama Asha alisema wazazi wahakikishe wanalipa  ada za watoto wao kwa wakati ili kutoa nafasi kwa walimu kuendelea kusomesha kwa utulivu.

  Aliupongeza Uongozi wa Philter Federal School kwa juhudi unaochukuwa wawafinyanga watoto wao na kuwa mahiri kimasomo na hata ushiriki wao wa michezo mbali mbali.

  Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuahidi Uongozi wa Skuli hiyo kwamba atakuwa tayari kusaidia nguvu za skuli hiyo katika kuona lile lengo walilojipangia la kutoa elimu bora na safi linafanikiwa vyema.

  Akisoma Risala ya Skuli hiyo Mwanafunzi Hassan Hassan Lukoma alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya skuli hiyo katika kipindi cha miaka mitano tokea ilipoanzishwa mwaka 2009.

  Mwanafunzi Hassan alisema Philter Federal School imekuwa ikiendelea kutoa wanafunzi mbali mbali wa michepuo kuingia kiwango cha sekondari katika masomo ya sanaa, Sayansi pamoja na biashara.

  Alisema katika kuimarisha ufaulu wa wanafunzi wa Skuli hiyo juhudi zimechukuwa na uongozi wa skuli hiyo katika kujiandaa na ufundishaji wa Lugha za kigeni zitakazotoa furtsa na wigo wa kuimarika kwa kiuchumi kutokana na kukomaa kwa kiwango cha elimu Kimataifa.

  Hata hivyo mwanafunzi Hassan Hassan alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili skuli hiyo kuwa ni pamoja na upungufu wa vifaa vya sayansi, uhaba wa vikalio pamoja maslahi duni ya walimu kutokana na wazazi kuchelewa kulipa ada za watoto wao.

  Mapema Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Elimu an maafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Vuai Khamis Juma alisema katika kusaidiana na Skuli Binafsi Wizara ya Elimu imeandaa utaratibu maalum wa kugawa vitabu ilivyonavyo kwa kuzipatia skuli binafsi.

  Nd. Vuai alitoa wito kwa walimu wa skuli hiyo kusomesha kwa bidii na uadilifu na kuwaomba wanafunzi wao kuepuka tabia ya kughushi mitihali yao jambo ambalo litachangia kuviza kiwango cha  elimu pamoja na upatikanaji wa wataalamu waliobobea.

  Katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa na wazazi kadhaa wa wanafunzi Mama Asha alikabidhi  vyeti kwa wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi na wale wa Darasa la kumi na mbili { Form IV } waliomaliza masomo yao. Pia hafla hiyo ilijumuisha michezo mbali mbali iliyochezwa na wanafunzi hao wa maandilizi na Sekondari wakionyesha umahiri wao uliotoa burdani safi katika viunga vya Hoteli ya Bwawani.

   Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  6/1/2014.

older | 1 | .... | 315 | 316 | (Page 317) | 318 | 319 | .... | 3285 | newer