Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA RUANGWA MKOANI LINDI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Shule ya Msingi Likangala kwa ajili ya kuhutubia wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi leo tarehe 15/11/2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Ruangwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Shule ya Msingi Likangala kwa ajili ya kuhutubia wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi leo tarehe 15/11/2019.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Ruangwa mara baada ya kuwasili Wilayani humo wakati akitokea Lindi mjini.

  Wananchi wa Ruangwa wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili Wilayani humo. PICHA NA IKULU


SWEDEN YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUFANYA VIZURI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0
Na Mary Mwakapenda, Dar es Salaam
Serikali ya Sweden imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuongoza nchi ikizingatia utawala bora hususani katika mapambano dhidi ya rushwa.
Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjobers alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wa nchi yake katika masuala ya utumishi wa umma kwa wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Dar es Salaam.

Balozi Sjobers amesema, katika nchi yao tatizo la rushwa halipo kabisa kwani Serikali iliongoza vema mapambano dhidi ya rushwa, hivyo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania inavyoendesha vizuri mapambano dhidi ya rushwa kwa ajili ya maslahi ya umma na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Katika mada yake, Mhe. Balozi amefafanua kuwa, nchini Sweden suala la Watumishi wa Umma kuwajibika kwa wananchi limepewa kipaumbele kwani wananchi wote wanahitaji huduma sawa bila ubaguzi wa aina yoyote.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mary Mwanjelwa (Mb) 
ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kutambua juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwenye eneo la utawala bora.

“Tunaishukuru Serikali ya Sweden kwa kutambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha utawala bora nchini hasa katika mapambano dhidi ya rushwa,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema.
Aidha, katika eneo la uwajibikaji, Mhe. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza  Watumishi wa Umma nchini kuwahudumia wananchi vizuri na kwa wakati kama Serikali inavyosisitiza kila mara.

“Ukiwa Mtumishi wa Umma, tambua wazi kuwa wewe ndio injini kwani wananchi wanahitaji huduma bora kutoka kwako, hivyo unatakiwa muda wote kuwahudumia wananchi kwa uadilifu na bila ubaguzi wa aina yoyote,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Kuhusu uhusiano uliopo kati ya Sweden na Tanzania, Mhe, Mwanjelwa amesema Nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano mzuri tangu utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza na uhusiano huo umeendelea kushamiri hadi sasa kwenye utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

“Uhusiano kati ya Sweden na Tanzania umeanza tangu mwaka 1970 walipojenga Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kwa asilimia 80 na bado tumeendelea kuwa na uhusiano mzuri,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza. 
Mhe. Balozi Sjoberg alitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)  jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania na kesho atatembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Tawi la Tabora ili kuona chuo hicho kilichojengwa na Serikali yao na kuangalia jinsi watakavyokienzi.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg alipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Dar es Salaam jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakishuhudia jinsi mashine ya kupiga chapa inavyofanya kazi mara baada ya Balozi kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)  jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakionyesha zawadi ya ramani ya Afrika yenye nembo ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania baada ya Balozi huyo kukabidhiwa zawadi hiyo na Naibu Waziri kuonyesha ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Sweden katika masuala ya utumishi wa umma wakati Balozi aliotembelea chuoni hapo jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakicheza wimbo unaosifu utendaji kazi wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Awamu ya Kwanza mpaka sasa wa kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania  wakati Balozi aliotembelea chuoni hapo jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Kushoto kwa Balozi ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi, Bw. Mick Kiliba.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA LA WILAYA RUANGWA, LINDI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala walipokutana jana Wilayani Ruangwa ziarani.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, akisalimiana na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza Ruangwa, Mkaguzi wa Magereza, Alex Munga’nzo alipowasili kwa ziara ya kikazi Gerezani hapo.
Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine Semwenda(kushoto) akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Magereza Mkoani Lindi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(meza kuu) alipowasili Gereza Ruangwa
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiakagua korosho ambayo tayari imeanza kuvunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza Ruangwa, lililopo Mkoani Lindi.
Ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya mapokezi ya ndugu na jamaa za wafungwa na mahabusu wanaofika Gereza Ruangwa kuwatembelea ndugu zao ukiendelea katika hatua mbalimbali za ujenzi.
(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Waendesha baiskeli kutoka Dodoma hadi kigoma kuhamasisha uchangiaji wa Damu

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Dodoma
Msafara wa waendesha baiskeli 18 kutoka Taasisi ya Kiislamu ya JAMIYATUL AKHLAAQUL ISLAAM (JAI) umeondoka leo mchana jijini Dodoma kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kuhamasisha kampeni ya taasisi hiyo ya kuchangia  damu salama kwa ajili ya wagonjwa.

Kwa mujibu wa Mratibu wa kitaifa kutoka taasisi hiyo bwana Athumani Massanga, msafara huo unatarajia kuwasili mkoani Kigoma kuanzia tarehe 22 hadi 23 mwezi huu, tayari kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha kampeni hiyo ya uchangiaji damu salama inayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika kuanzia  tarehe 24 hadi 27 Oktoba 2019.

Amesema msafara huo wa waendesha baiskeli kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Lindi, Pwani, na Dar es salaam mbali na uhamasishaji  kwa njia ya kuendesha baiskeli pia watafuatana na gari maalum ambalo litakuwa likihamasisha wananchi kuchangia damu, na kugawa vipeperushi kwa wananchi vinavyoelezea  umuhimu zoezi hilo na kutangaza upendo na kutenda matendo mema kwa kusaidia wagonjwa.

Bwana Massanga amesema kuwa kila mwaka taasisi yake imekuwa ikiendesha kampeni ya kuchangia damu ambapo mwaka jana kilele cha kuchangia damu kilifanyika katika viwanja vya Maisara vilivyopo Zanzibar.

Amesema kampeni ya uchangiaji damu unafanyika mkoani kigoma kwani taasisi hiyo imejiwekea malengo ya kufanya kampeni ya uchangiaji damu katika mikoa mbalimbali nchini ambapo mwaka huu mkoa wa kigoma umebahatika kuwa mwenyeji wa kilele cha zoezi la kuchangia damu.

Zoezi kama hilo limewahi kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Tanga na Kilimanjaro.

Mapema kabla ya kuzindua msafara huo wa waendesha baiskeli kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofiasi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo, Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt Ntuli Kapologwe amesema kuwa mahitaji ya damu ni makubwa kulinganisha na upatikanaji wake.

Amesema kwa kutambua juhudi za taasisi ya JAI, Serikali ya awamu ya tano inaunga mkono kampeni ya kuchangia damu ili kuwezesha wagonjwa waliopo katika hospitali na vituo vya afya nchini kupata huduma hiyo.

Amesema katika kuboresha huduma za sekta ya afya  serikali ya awamu ya tano  imejenga vituo 486 vya kutolea huduma za afya vikiwemo vituo vya afya 320 na hospitali za wilaya 67 nchin.

Amesema kuwa vituo hivyo vya kutolea huduma za afya nchini vitahitaji upatikanaji wa damu salama kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa husani akina mama wajawazito pindi wanapohitaji huduma hiyo.

Amesema kuwa serikali inaipongeza na kuishukuru taasisi hiyo kwa namna inavyojihusisha katika kusaidia jamii kwa njia ya kuhamasisha uchangiaji wa damu salama nchini ili kuwasaidia wagonjwa wasio kuwa na uwezo kwani hiyo ni katika utekelezaji wa amri ya upendo.

Aidha Dkt Kapologwe amesema  kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amechangia kiasi cha shilingi laki tano kwa taasisi hiyo na watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi hiyo nao wamechangia shilingi laki tano kwa ajili ya kuwawezesha waendesha baiskeli hao waweze kununua maji na chakula wawapo safarini kuelekea mkoani Kigoma.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mustapha Shabani ambaye aliipongeza taasisi ya JAI kwa kuzingatia misingi ya dini ya Kiislam inayosisitiza upendo.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt Ntuli Kapologwe  akiwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Shaaban na viongozi wengine kutoka jumuiya ya Jamiyatul Akhlaaqul Islaam wakimsikiliza Mratibu Mkuu wa taasisi ya JAI, Athuman Massanga akielezea malengo ya taasisi yake katika kampeni ya kuchangia damu inayotarajiwa kufanyika kigoma kuanzia oktoba 24 hadi 27, 2019 katika viwanja vya  Lake Tanganyika. 
 Baadhi ya waendesha baiskeli 18 kutoka mikoa mbalimbali wakiwa tayari kuanza safari ya kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuchangia damu salama. wanatarajia kufika kigoma tarehe 22 mwezi huu
 Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt Ntuli Kapologwe  akikata utepe kuzindua msafara wa waendesha baiskeli 18 wanaoelekea mkoani Kigoma kuhamasisha uchangiaji damu. 

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA BUNGENI

BENKI YA KCB YASAFIRISHA WAFANYABIASHARA KWENDA CHINA

$
0
0
Benki ya KCB Tanzania kupitia KCB Biashara Club yapeleka wafanyabiashara 10 kwenda nchini China kwa lengo la kukutana na wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza na kutafuta namna bora ya kuweza kuboresha biashara zao. 

Wafanyabiashara hao watakaa nchini China kwa siku 10 na kupata fursa ya kutembelea miji miwili mikubwa. 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Mahusiano na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye alisema wameanza kuwapeleka China wafanyabiashara hao ambao ni wateja wa benki hiyo ili wakakutane na wazalishaji halisi na siwalanguzi au madalali ambao uwauzia bidhaa kwa bei ya juu. 

Amesema kwa muda mrefu wafanyabiashara nchini ambao wanakwenda China wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo za lugha na kuuziwa vitu 

bei za juu hivyo kupitia safari hizo wanazoziandaa mambo hayo hayatajitokeza. 



“Tatizo kubwa ambalo wafanyabiashara walikuwa wanakutana nalo ni kuuziwa vitu kwa bei ya juu na walanguzi au madalali sasa kupitia safari hii tutawakutanisha na wale wazalishaji halisi ambao wanaviwanda ambapo watapata fursa ya kutembelea viwanda vyao kisha kutoa oda za kutengenezewa bidhaa zao,"


"Lakini pia kuna tatizo la lugha kule, kupitia safari hii tuliyoiratibu sisi KCB Benki tutawapatia wakalimani ambao watatembea nao kila mahali ili kurahisisha mawasiliano yao na wazalishaji hao,” amesema. 

Naye Meneja Uhusiano wa Wateja Wadogo na wa Kati wa benki hiyo, Moses Kisaka alisema wanamatumaini kwamba siku hizo 10 wafanyabiashara hao wataweza kuzunguka na kukutana na wazalishaji pamoja na kutumia fursa hizo kufanya manunuzi ya bidhaa zao. 

Amesema wafanyabishara hao watakutana na wazalishaji halisi watakaowauzia vitu kwa bei ya chini kuliko ilivyokuwa awali walipokuwa wakienda wenyewe na kukutana na walanguzi waliokuwa wanawauzia vitu kwa bei ya juu. 

“Tunafanya hivi kwa lengo la kuwasaidia wapunguze gharama za kupata bidhaa, tunaamini safari hizi zitakuwa ni muendelezo na tunatumaini mwakani kuwapeleka wafanyabiashara wengi zaidi,” amesema Kisaka.

Aidha amesema benki hiyo imeanzisha kitengo cha KCB Biashara Club kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara mbalimbali na kuzungumza juu ya changamoto na fursa za kibiashara wanazokutana nazo. 



Kwa upande wake Mwakilishi wa wafanyabiashara wanaoenda China, Saada Sipemba amesema safari hiyo itawasaidia kupata fursa ya kuona maonyesho makubwa yanayofanywa na wenye viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo vyombo vya ndani pamoja na mashine. 

“Pia itatuwezesha kwenda kujifunza na kukutana na wazalishaji wenyewe bila kupitia kwa madalali wowote hivyo itatusaidia kununua bidhaa kwa bei nafuu na kuja kuziuza nchini kwa bei nafuu pia,” amesema Sipemba
 Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja wa wafanya biashara wa vipodozi Irene Moshi, wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye . 
 Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja wa wafanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba, wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa nawalanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye . 
 Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye (kulia) akizungumza wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam Wengine pichani (watatu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago na kati Abdul Juma, Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na Mfanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba. 
 Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago na wakati Masika Mukule (watatu kushoto), akizungumza wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam (kulia) Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye, Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na Mfanyabiashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba. 

Waziri wa Nishati aweka jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi za Tanesco Chato, Geita

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Tanesco katika Wilaya ya Chato na Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita zitakazokuwa na hadhi ya kimkoa ya Kitanesco.

Hafla hiyo iliyofanyika tarehe 15 Oktoba, 2019 katika Kitongoji cha Mlimani, wilayani Chato ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka, Mwakilishi wa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Edson Ngabo na watendaji wengine kutoka Wilaya ya Chato, TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Kabla ya kuweka Jiwe la Msingi, Dkt Kalemani alipongeza juhudi za TANESCO za ujenzi wa ofisi katika maeneo mbalimbali nchini na kueleza kuwa hadi sasa TANESCO ina takribani ofisi 160 kwa nchi nzima.

"Leo tunaanzisha ujenzi huu mwingine wa ofisi mbili mpya, ya Chato na Geita. Hapa Chato Tanesco ilikuwa ikipanga kwenye jengo la mtu binafsi lakini sasa kutakuwa na jengo litakalowezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, lakini nitoe angalizo kuwa, lisiwe kigezo cha kukaa ofisini badala ya kuwafuata wateja kule waliko." alisema Dkt.Kalemani

Dkt Kalemani alitoa maelekezo kuwa, ujenzi wa majengo hayo ulingane na thamani ya pesa iliyotengwa na TANESCO ihakikishe  kunakuwa na wataalam wa kutosha kuhudumia wananchi mara baada ya majengo kukamilika.

Aidha, aliiagiza TBA kuhakikisha kuwa ujenzi wa majengo hayo unakamilika mwezi Aprili 2020 kama ilivyopangwa na wakati wa ujenzi wazingatie kutoa ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya ujenzi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka alieleza kuwa majengo hayo yanajengwa kwa kutumia fedha ya Serikali kupitia TANESCO huku mkandarasi akiwa ni TBA.

Vilevile alisema kuwa ujenzi wa majengo yote mawili unaanza mwezi Oktoba, 2019 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi Sita.

Katika kuimarisha utoaji wa huduma, alisema kuwa, TANESCO imekamilisha ujenzi wa majengo katika maeneo mbalimbali nchini ambayo ni Songea, Kibamba, Mbezi Beach, Ifakara, Bahi, Kaliua, Igunga na Uyui huku majengo ya TANESCO wilayani Kishapu na Kyerwa yakitarajiwa kukamilika mwezi huu.

Aliongeza, ujenzi wa majengo mengine unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini huku ujenzi wa majengo katika Mkoa wa Kilimanjaro, Mtwara na Pwani ukitarajiwa kuanza kabla ya mwezi Disemba mwaka huu.
 Muonekano wa jengo la TANESCO wilayani Geita mara baada kukamilika ujenzi wake mwezi Aprili mwaka 2020.
 Muonekano wa jengo la TANESCO wilayani Chato, Mkoa wa Geita, mara baada kukamilika ujenzi wake mwezi Aprili mwaka 2020.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia, mbele) na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho (kushoto, mbele) wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilayani Chato na Geita, mkoani Geita. Wengine ni watendaji kutoka TANESCO, Wakala wa Majengo (TBA) na Wilaya ya Chato.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia, mbele) na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho (kushoto, mbele) wakipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilayani Chato na Geita, mkoani Geita. Wengine ni watendaji kutoka TANESCO, Wakala wa Majengo (TBA) na Wilaya ya Chato.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akisalimiana na watendaji mbalimbali waliofika katika Kitongoji cha Mlimani wilayani Chato kushuhudia hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilayani Chato na Geita, mkoani Geita.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akisalimiana na watendaji mbalimbali waliofika katika Kitongoji cha Mlimani wilayani Chato kushuhudia hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilayani Chato na Geita, mkoani Geita.
 Baadhi ya wananchi, wilayani Chato wakiwa katika Kitongoji cha Mlimani wilayani Chato kushuhudia hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilayani Chato na Geita, mkoani Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa Ofisi za TANESCO katika Wilaya ya Chato na Geita mkoani Geita wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo iliyofanyika katika Kitongoji cha Mlimani wilayani Chato.  Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho.

SPIKA ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA SINGIDA

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo ya Ntambo Mahinya mtaalamu wa kupika chakula cha asili kutoka Mbeya alipotembelea banda la vyakula hivyo kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida.


Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo alipotembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida.

Dkt. Tulia akipata maelezo jinsi mashine ya kuchakata viazi lishe inavyofanya kazi katika banda la TARI. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Pasacas Muragiri.
Afisa Kilimo Robert Dimoso Idara ya Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo akimuelezea Dkt.Tulia shughuli zinazofanywa na Idara hiyo.
Mratibu wa Mradi wa Tanipac Wizara ya Kilimo, Clepin Josephat akimurleza Dkt.Tulia Ackson shughuli wanazozifanya.
Dkt. Tulia akipata maelezo ya kilimo cha mapapai.


Afisa Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mary Yongolo akimpatia zawadi ya maziwa Dkt.Tulia Ackson baada ya kutembelea banda la wizara hiyo.
Afisa Lishe Mkoa wa Singida, Teda Sinde akimuelekeza Dkt.Tulia Ackson jinsi ya kupika vyakula vya asili ambavyi ni muhimu katika kuboresha lishe. Kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Federick Ndahani.
Dkt.Tulia akipakua chakula cha asili alipotembelea banda la vyakula hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi akila chakula cha asili kilichotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)

MBUNGE AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KWA SIKU MOJA ILIYOBAKI

$
0
0

 Afisa Uandiikishaji  Catherine Alex wa Kijiji cha ilongero katika Halmashauri ya Wilaya Singida Vijijini akimuandikisha Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Aysharose Mattembe kwenye daftari la Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za  mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akisaini katika daftari la Serikali za Mitaa Tamisemi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Singida Vijiji, Naomi David (kulia) akimlaki Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe alipowasili kujiandikisha.

 Wananchi wa Kata ya Ilongero wakimlaki Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe alipowasili kujiandikisha.
 Mbunge Aysharose Mattembe akiwa katika picha ya pamoja na wananchi na viongozi wa Kata ya Ilongero.
 Mbunge Aysharose Mattembe, akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ilongero.
 Wananchi waliohamasishwa na Mbunge Mattembe wakisubiri kujiandikisha.
 Mbunge Mattembe akielezea umuhimu wa kuchagua viongozi wanaofaa.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Singida Vijiji, Naomi David akisaini baada kujiandikisha katika daftari hilo.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM)  Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika daftari la Tamisemi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Mattembe ametoa wito huo leo wakati alipokuwa akiwahamasisha wananchi wa Kata ya Ilongero kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ikiwa imebaki siku moja tu ya kujiandikisha.

Alisema maendeleo  ya nchi yanaanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, wilaya hadi Taifa hivyo tiketi ya kuweza kuchagua kiongozi mwenye sifa nilazima kwenda kujiandikisha ili kumchagua kiongozi anayefaa.

" Bila ya kujiandikisha haitawezekana kumchagua kiongozi mnaye mtaka hivyo wito wangu kwenu kwa hii siku moja iliyobaki kwa ajili ya kujiandikisha jitokezeni kwa wingi  vinginevyo mtapoteza haki yenu ya kumchagua kiongozi mnaye mtaka" alisema Mattembe.

Aliwataka wananchi hao kujitokeza kujiandikisha bila kujali itikadi ya vyama vyao  kwani maendeleo hayana chama yapo kwa ajili ya watu wote.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NACHINGWEA MKOA LINDI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nachingwea mara baada ya kuwasili wakati akitokea Ruangwa.

Wananchi wa Nachingwea mkoani Lindi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Ikungu Nachingwea mkoani Lindi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hotuba yake kabla ya kuzungumza na wananchi wa Nachingwea mara baada ya kuwasili wakati akitokea Ruangwa.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Nachingwea mara baada ya kuwasili wakati akitokea Ruangwa. PICHA NA IKULU

SEMINA KWA WANAHABARI KUHUSU KAMPENI SHIRIKISHI YA SURUA RUBELLA SINGIDA

$
0
0

 Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas, akitoa mada katika semina ya waandishi wa habari kuhusu kampeni shirikishi ya Surua  Rubella.
 Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo 
 Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Ernest Mugetta akizungumza kwenye semina hiyo.
 Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas, akisisitiza jambo kwenye semina hiyo. Kulia nMratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida, Jadili Mhanginonya.
 Mratibu wa Magonjwa yanayozuilika na Chanjo kutoka Wizara ya Afya,  Honest Nyaki akizungumza.
 Majadiliano yakifanyika.
Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKOA wa Singida umelenga kutoa chanjo ya Surua- Rubella kwa watoto 225,586 na polio watoto 119,198 na kuhakikisha wanafikisha asilimia 100 ya kutoa chanjo hizo.

Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida, Jadili Mhanginonya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina kuhusu kampeni shirikishi ya Surua-Rubella 2019.

"Tunataka mkoa wetu wa Singida tufikie asilimia 100 ya chanjo hiyo kwani tumejipanga vizuri kwa kazi hiyo" alisema Mhanginonya.

Alisema chanjo ya kitaifa ya mwaka 2014 kwa mkoa huo ilikuwa ni asilimia 98 ambapo waliwafikia watoto 615,000 na walikuwa kuanzia umri wa miezi 9-15 

Alisema maandalizi yote ya kampeni hiyo ya siku tano itakayoanza kesho nchi nzima kwa mkoa wa Singida yamekamilika kwa kupeleka vifaa maeneo yote yaliyotengwa na timu ya watendaji ipo tayari kwa kazi hiyo.

Alisema kwa mkoa huo wanatarajia kuzindua kampeni hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na itazinduliwa na Mkuu wa Mkoa Dkt.Rehema Nchimbi viwanja vya Square Polisi.

Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas alisema waandishi wa habari wanawajibu wa kuhabarisha jamii kuhusu madhara ya ugonjwa wa Surua na Rubella.

"Ninyi wanahabari ndio tegemeo kubwa katika kampeni hii mnatakiwa kuhabarisha umma kuhusu uwepo wa chanjo ya kukinga ugonjwa wa kupooza (polio) na umri sahihi wa kupata chanjo ya Surua, Rubella na Polio" Barnabas.

Barnabas alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wote mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupata chanjo hiyo.

RC MNYETI AUNGURUMA KITETO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kata ya Kijungu Wilayani Kiteto.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kata ya Lengatei Wilayani Kiteto.
Wananchi wa Kata ya Dongo Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti alipotembea eneo hilo.
…………………
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti ameunguruma Wilayani Kiteto kwa kuagiza wakulima waheshimu eneo la malisho la wafugaji wa Amei na wakulima wa Kata ya Dongo walionyang’anywa maeneo yao warudishiwe kwani hawakupewa eneo mbadala. 

Mnyeti alitoa maagizo hayo Wilayani Kiteto alipotembelea maeneo hayo kwenye ziara yake ya siku tano ya wilaya ya Kiteto. 

Alisema wakulima wa Amei wasiingilie eneo la mifugo kwani limewekwa kwa ajili ya wafugaji. 

“Mlishajipangia wenyewe kuwa lile ni eneo la mifugo hivyo wakulima muache kusogelea hapo mtasababisha vurugu ili hali mlijiamulia wenyewe matumizi ya ardhi yenu,” alisema Mnyeti. 

Alisema kwenye eneo la Dongo kuna baadhi ya wakulima walifukuzwa kwenye sehemu yao bila kupewa eneo mbadala hivyo warudi katika eneo lao. 

“Wakulima walifukuzwa bila kupewa eneo lingine hivyo rudini ili muendeshe maisha yenu kama ilivyokuwa awali kwani hamkupewa maeneo mbadala ya kulima,” alisema Mnyeti. 

Pia, aliwataka wafugaji na wakulima kuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi waliyojiwekea ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji. 

“Heshimuni mpango huo mlioamua wenyewe kwani mfugaji akiheshimu sehemu ya wakulima na wakulima wakiheshimu eneo la wafugaji hakutatokea tatizo lolote,” alisema Mnyeti. 

Mkuu huyo wa mkoa alileta faraja kwa mkazi wa kijiji cha Zambia kikongwe aliyenyang’anywa eneo na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho. 

“Kuanzia sasa hivi wewe mama rudi kwenye eneo lake la awali na mtu yeyote asikusumbue mtendaji wa kijiji, kata na ofisa Tarafa mlindeni huyu mama asiguswe na mtu,” alisema Mnyeti. 

Akiwa kwenye kata ya Lengatei aliagiza mkazi wa eneo hilo Hassan Ramadhan kurudishiwa eneo lake lililotaka kujengwa shule shikizi ili hali alishinda shauri lake kwenye baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Kiteto. 

Lengo la ziara hiyo ni kuzungumza na wananchi, kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero na changamoto na kuyapatia majawabu na kuhamasisha wananchi kujiandikisha ili waweze kupiga kura ya kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa.

PROF NDALICHAKO AKERWA NA USIMAMIZI MBOVU WA MIRADI YA ELIMU, ATOA MAELEKEZO KWA KATIBU MKUU

$
0
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akikagua moja ya nyumba za walimu katika Shule ya Msingi Kasumo iliyoko wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akitoa maelekezo  mara baada ya kukagua ujenzi wa mabweni ya shule sekondari Muyama iliyoko wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari Janda iliyopo Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma mara baada ya kukagua miradi ya elimu inayotekelezwa shuleni hapo


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameonesha kukerwa na usimamizi mbovu wa miradi ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya Buhigwe mkoani Kigoma na kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara anayoisimamia, Dkt. Leonard Akwilapo kuleta wataalamu watakaofanya ukaguzi maalum wa utekelezaji wa miradi ya elimu katika wilaya hiyo.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo  Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma mara baada ya kukagua baadhi ya  miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R)na kubaini uwepo wa kasoro kadhaa ikiwemo matumizi ya vifaa vya ujenzi vilivyo chini ya Kiwango na  majengo ya shule ya Msingi ya mfano Bwega  kutofautiana na ramani iliyopendekezwa na wizara .

"Kwa ujumla usimamizi wa Miradi katika wilaya ya Buhigwe  siyo mzuri, maafisa elimu hawawajibiki katika kuangalia kazi zao, unakuta kazi zimefanyika hovyo, watu hawafuatilii," alisema Waziri Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe hatimizi wajibu wake ipasavyo kwa kuwa ameshindwa kusimamia miradi hiyo kwa viwango vinavyotakiwa na kuruhusu matumizi ya vifaa vya ujenzi visivyo na ubora lakini pia ameshindwa kufuata ramani  katika ujenzi wa majengo ya shule ya msingi ya mfano inayojengwa wilayani humo.

Kiongozi huyo amesema tayari  amewasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Leonard Akwilapo ili ufanyike ukaguzi wa kina katika miradi ya elimu  Wilaya ya Buhigwe lengo likiwa ni kubaini mapungufu na iwapo kuna mtu kafanya uzembe kwa manufaa yake awajibike.

"Inabidi kabla ya kuleta fedha nyingine za miradi ya elimu wilayani Buhigwe ije timu ya watalaamu mainjinia wachunguze walinganishe BoQ na kilichofanyika, haiwezekani turuhusu uzembe kama huu kuendelea kwenye miradi inayotumia fedha ya wananchi wanyonge," aliongeza Waziri Ndalichako.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayanalina amemshukuru Waziri Ndalichako kwa ziara yake wilayani humo na kusema kuwa  mapungufu yote yaliyobainika tayari  Kamati yake imeyatolea maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na kwamba zoezi linaloendelea ni kuwachukulia hatua wahusika.

"Kamati ya Usalama ya wilaya ilibaini mapungufu katika miradi mbalimbali na tulitoa maelekezo kupitia kwa  Mkurugenzi na vyombo vyetu vilishaagizwa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki," amesema Mkuu wa Wilaya hiyo, Ngayalina.


Naye mMkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Anosta Nyamoga amesema ofisi yake tayari imemfukuza kazi fundi aliyekuwa na mkataba wa kufanya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Janda kutokana na kufanya kazi hiyo chini ya viwango na kuahidi kuzifanyia kazi kasoro zote ambazo zimebainishwa na Waziri Ndalichako.

Akiwa wilayani Buhigwe Waziri Ndalichako amekagua miradi ya elimu katika shule ya msingi Bwega, shule ya sekondari Janda,  shule ya sekondari Muyama na shule ya msingi Kasumo ambayo kwa pamoja inatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

Waziri Ndalichako yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Halmashauri ya Mji Kasulu.

DKT. MPANGO AITAKA BENKI YA DUNIA KUSAIDIA SEKTA YA KILIMO NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Ramadhani Kissimba na Eva Valerian, Washington Dc 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ameitaka Benki ya Dunia kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania ili kuweza kuwainua kiuchumi wakulima hasa wale wa kati na wadogo.

Dkt.Mpango aliyasema hayo wakati wa kikao cha majadiliano na timu nzima ya Benki ya Dunia ambayo inafanya kazi nchini Tanzania na wengine kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo nchini Marekani. 

Mhe.Mpango alisema katika mkutano huo  walipitia kwa pamoja utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hivi sasa  inayofadhiliwa na Benki ya Dunia,  lakini pia walipitia na kujadili miradi ambayo inaanza kufikiriwa kwa ajili ya utekelezaji kwa mwaka utakaofuata.

‘’Moja ya vitu vilivyonifurahisha mwaka jana kwenye mjadala niliwaaomba sana kwamba hatuwezi kuendelea kuitaka Benki ya Dunia isaidie kwenye miradi mingine tu ni lazima nguvu kubwa ielekezwe pia kwenye miradi ya kilimo ambayo kwa sasa  msaada wa Benki ya Dunia katika miradi hiyo ni kidogo sana’’ alisema Dkt.Mpango.

Aidha Dkt.Mpango alielezea dhamira ya Tanzania kushirikiana na Benki ya Dunia ili kuanzisha programu itakayohakikisha kuwa tija inapatikana kwenye sekta nzima ya kilimo na mifugo, lakini pia kuweza kuyafikia masoko kwa mazao yanayozalishwa nchini, hasa yale yenye thamani kubwa duniani.

 Dkt. Mpango amefafanua kuwa Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya mabdiliko inayofanyika katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka, lakini vile vile  wakulima wa kati wamezidi kuongezeka. 

Aidha, kuongezeka kwa maeneo ya kilimo imewafurahisha wataalamu wa Benki hiyo, ikiwa ni pamoja na  kuongezeka kwa aina ya mazao yanayolimwa   hasa yale yenye thamani kubwa ambayo yanalimwa  kwa kasi kubwa sana kuliko ilivyokuwa awali.

Pia Dkt. Mpango alisisitiza kuwa, Benki ya Dunia imeshafanya utafiti wao wa kutosha ambao umeonesha kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka.

Mhe. Mpango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali tena kuleta timu ya wataalamu nchini Tanzania ambayo itakaa na sekta nzima ya kilimo na ufugaji ili kuona ni namna gani hasa Benki ya Dunia itasaidia kuinua sekta hiyo, na  kuwasaidia wakulima hasa katika matumizi ya nguvu kazi kwa upande mmoja na kuwaongezea kipato kwa upande mwingine.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifuatilia majadiliano katika Mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika uliofanyika Jijini Washington DC. Kulia kwa Mhe.Mpango ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru na anayefuatia ni Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo.
Mtaalam wa Masuala ya Kilimo kutoka Benki ya Dunia Holger Krag akifafanua jambo kwa ujumbe wa Tanzania.

JOPO LA MAJAJI WATATU KUSIKILIZA MAOMBI YA RUFAA

$
0
0
Na Magreth Kinabo-Mahakama

Mahakama ya Rufani Tanzania, imesema kwamba shauri la maombi jinai la mapitio ya nyongeza ya muda, haliwezi kuendelea kusikilizwa kwa sababu linahitaji na jopo la majaji watatu.

Uamuzi huo ulitolewa leo, Oktoba 15, mwaka huu na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rehema Kerefu wakati akisikiliza shauri la maombi ya jinai ya mapitio ya muda linalomkabili Job Mlama na wenzake wawili, dhidi ya Jamhuri,ambayo iliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidambo wote wakiwa mkoani mwanza kwa njia ‘Video conference’.

Shauri hilo liliendeshwa huku wakili huyo na wahusika, wakiwa mkoani Mwanza, na Jaji Kerefu katika Kituo cha Habari na Mafunzo kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Katika shauri hilo, mleta maombi hayo, Mlama aliomba mahakama hiyo isikilize maombi ya mapito ya nyongeza ya muda kwa njia ya ‘Video Conference’.

Jaji Kerefu alitoa uamuzi huo, baada ya kuuliza upande wa Jamhuri kuwa uko tayari kuendelea na maombi hayo ya mapitio ya muda, ambapo ulikubali, ndipo alipotoa uamuzi huo, wa shauri kuwa linapaswa kusikilizwa na jopo la majaji watatu kama sheria inavyosema.

Katika shauri lingine la maombi ya jinai ya mapitio ya nyongeza ya muda linalomkabili, Weisiko Ruchere dhidi ya Jamhuri, ambaye aliwakilishwa na wakili Geofrey Kanje na kusikilizwa na Jaji Kerefu.

Wakili Kanje aliomba mahakama hiyo iongeze muda wa maombi hayo kwa sababu ya mleta maombi kutokuwa na msaada wa kisheria.

Akijibu hoja hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi,Anjelina Nchalla alisema hakuna sababu za msingi alizozitoa mleta maombi zilizosababisha achelewe kuleta maombi hayo kwa kuwa ni mwaka moja na nusu tangu yalipotupiliwa mbali Novemba 29, mwaka 2017.

Akisikiliza maombi hayo Jaji Kerefu alisema atatoa uamuzi na wahusika watataarifiwa baadaye.

Shauri lingine lililosikilizwa na Mhe. Jaji Ignas Kitusi, ambapo mleta maombi ya jinai ya mapitio ya nyongeza ya muda, Reuben Juma dhidi ya Jamhuri iliyowakilishwa na Wakili wa Serikali Maryyasintha Lazaro na Wakili wa serikali Mwanahawa Shangale, ambao walipinga ombi hilo.

Katika shauri hilo, Juma aliomba mahakama hiyo isitilie maanani pingamizi la mawakili hao kwa sababu limekuja nje ya muda na pia alikosa msaada wa kisheria wa kuwasilisha ombi lake, ndani ya wakati. 

Huku Wakili huyo Mwandamizi aliomba mahakama hiyo itupilie mbali maombi hayo kwa kuwa kukosa msaada wa kisheria sio sababu ya msingi na maombi hayo hajazingatia matakwa ya kisheria.

Akijibu hoja ya Wakili huyo Mwandamizi, Jaji Kitusi alisema ni takwa la kisheria la mleta maombi.

Akisikiliza hoja hizo,Jaji Kitusi alisema ataenda kuandaa uamuzi na wahusika watataarifiwa baadaye.

Shauri lingne la madai lililosikilizwa na Jaji huyo, la mleta maombi ya nyongeza ya muda ambaye ni Geita Gold Mine Limited, aliyewakilishwa na Wakili Faustine Mwalongo dhidi ya Truway Muneth na wenzake waliowasilishwa na wakili Mwita Emmanuel, ambaye aliomba mahakama isikubali maombi hayo kwa sababu yalikuwa nje ya muda na yalipaswa kuandaliwa ndani ya siku moja.

Wakati Mwalongo aliomba maombi hayo yakubaliwe na mahakama hiyo kwa kuwa yako ndani ya muda wa siku tatu, yakiwa yanaandaliwa na kuwasilishwa mahakamani, hivyo hakuna nyaraka inayosema maombi yaandaliwe ndani ya siku moja.

Katika hatua nyingine Jaji mwingine wa mahakama hiyo, Mhe. Dkt. Mary Levira alihairisha shauri la maombi ya nyongeza ya muda la Mugeta Manyama dhidi ya Jamhuri kwa sababu mleta maombi haifahamiki yuko gereza gani.

Aidha Dkt. Levira pia alisikiliza shauri la maombi ya mapitio ya nyongeza ya muda la Kafuba Mwangulindi dhidi ya Jamhuri na litatolewa maamuzi baadaye.

Kwa upande wa mkoa wa Bukoba Mahakama hiyo imesikiliza mashauri sita kwa njia hiyo pia, ambapo mashauri matano ni ya maombi ya jinai ya nyongeza ya muda na moja la maombi ya madai ya nyongeza ya muda. Mashauri hayo yalisikilizwa na majaji watatu ambapo kila mmoja alisikiliza mashauri mawili.

Majaji waliosikiliza mashauri hayo ni Mhe. Winfrida Korosso, Mhe. Barke Sehel na Mhe. Lugano Mwandambo. Mashauri hayo baadhi yamesikilizwa na kumalizika, mengine maamuzi yatatolewa baadaye.

Mahakama hiyo itaendelea na mashauri mengine maombi ya jinai na madai kesho, Oktoba 16 kwa njia ya ‘Video Conference’ yaliyoko masjala ya Mbeya na Mwanza.

Biteko Aomba Maboresho ya Miundombinu “kuvutia Wawekezaji Jimboni”

$
0
0

Mbunge wa Jimbola Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ameomba Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuongeza kasi ya uboreshaji miundombinu ya barabara jimboni humo ili kuvutia wawekezaji zaidi.

Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini ametoa ombi hilo Oktoba 15, 2019 kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Geita ambacho pamoja na mambo mengine kimejadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara.

Amesema wakati Serikali inaendelea kuboresha mapori yaliyopo wilayani Bukombe kuwa na hadhi ya kuvutia watalii, ubora wa miundombinu ya barabara utavutia zaidi wawekezaji hivyo mamlaka hizo ni vyema zikatekeleza miundombinu iliyokwisha ingiza kwenye mpango.

Naye Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel ameshauri mamlaka hizo ikiwemo TARURA kuzingatia vipaumbele vya wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge zinapokuwa zinatekeleza miradi ya barabara. Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko (aliyesimama) ambaye pia ni Waziri wa Madini akizungumza kwenye kikao hicho. Waliokaa kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Alhaji Said Kalidushi, Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Mbunge wa Nyang’hwale Nassor Amar pamoja na Mbunge wa Busanda Lolensia Bukwimba.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Busonzo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukombe, Safari Mayala (CCM) akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko (kulia) amabaye pia ni Waziri wa Madini akikagua taarifa ya utekelezaji miradi mbalimbali ya barabara mkoani Geita. Kushoto ni Mbunge wa Nyang’hwale Nassor.

UJENZI HOSPITALI YA RUFAA YA KWANGWA MUSOMA KUKAMILIKA MWAKANI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kulia) akioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana wakati wa ziara yake mkoani humo. Mradi huo unajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kabla ya kuanza kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana. Katikati ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Carlone Mtapula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kabla ya kuanza kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana. Wa pili kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Carlone Mtapula.

………………….


Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA

Ujenzi wa Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwanga iliyopo Musoma mkoa wa Mara unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 15 unatarajiwa kukamilika Agosti 2020.

Hayo yameelezwa jana mjini Musoma na Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Margret Ezekiel wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya uendelezaji ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo,

Margret alisema, jengo hilo lenye mita za mraba 24482 na majengo mengine ya pembeni yenye mita za mraba 1039 lina sehemu kuu tatu zinazojumisha sehemu zenye ghorofa tano, nne na sehemu ya tatu ghorofa mbili.

Alisema, ujenzi wa mradi wa hospitali ya Kwangwa ulianza septemba 2019 na kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa mradi huo kulitokana na changamoto ya upatikanaji wa michoro ya kujengea pamoja na kutokamilika kwa mchakato wa kumpata Mshauri Mwelekezi wa mradi.

‘’jengo hili ambalo limepitia wakandarasi wawili kabla ya shirika letu kukabidhiwa limefanyiwa maboresho ili kuwa na huduma zote kadri ya hospitali ya Rufaa inavyotakiwa’’. Alisema Margaret

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo Ubunifu wa NHC, kazi za ujenzi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na kupiga lipu katika katika maeneo yote ambayo hayatakuwa na marejkebisho , kuvunja baadhi ya kuta na kuzijenga kwa mujibu wa marekebisho sambamba na kuandaa sehemu ya nyongeza,

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kukamilika kwa jengo la hospitali ya Rufaa la Kangwa itakuwa mkombozi kwa wananchi wa mkoa wa Mara ambao baada ya kukamilika ujenzi watakuwa wakipata huduma za hospitali ya rufaa katika mkoa huo tofauti na awali ambapo waanalazika kwenda hadi Bugando mkoani Mwanza.

‘’ Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kufanikisha kutoa kiasi cha zaidi ya bilioni 15 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambao ulisimama kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2011’’ alisema Dkt Mabula.

Amelitaka shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara kuhakikisha kuchelewa kwa Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo hilo hakucheleweshi ujenzi wa ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka Kampuni ya Kiure Engineering ianyojenga jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa la Mkendo Plaza kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa jengo hilo la ghorofa tano ifikapo Desemba 30 2019 vinginevyo mkataba wa ujenzi wa jengo hilo utavunjwa bila kujali kama kampuni hiyo imefikia asilimia ngapi ya ujenzi na kampuni hiyo itatakiwa kurejesha gharama za ujenzi.

Hatua ya Dkt Mabula inafuatia kampuni hiyo ya Kiure kushindwa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo tangu kuingia kwa mkataba wa ujenzi mwaka 2015. Kwa mujibu wa Mhandsi wa ujenzi wa jengo hilo, kampuni ya Kiure iliingia mkataba wa ujenzi wa jengo hilo mwaka 2015 na ujenzi kuanza rasmi 2017.

SWEDEN YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUFANYA VIZURI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakionyesha zawadi ya ramani ya Afrika yenye nembo ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania baada ya Balozi huyo kukabidhiwa zawadi hiyo na Naibu Waziri kuonyesha ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Sweden katika masuala ya utumishi wa umma wakati Balozi aliotembelea chuoni hapo jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakicheza wimbo unaosifu utendaji kazi wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Awamu ya Kwanza mpaka sasa wa kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakati Balozi aliotembelea chuoni hapo jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Kushoto kwa Balozi ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi, Bw. Mick Kiliba.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg alipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Dar es Salaam jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakishuhudia jinsi mashine ya kupiga chapa inavyofanya kazi mara baada ya Balozi kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika
………………….

Na Mary Mwakapenda, Dar es Salaam

Serikali ya Sweden imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuongoza nchi ikizingatia utawala bora hususani katika mapambano dhidi ya rushwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjobers alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wa nchi yake katika masuala ya utumishi wa umma kwa wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Dar es Salaam.

Balozi Sjobers amesema, katika nchi yao tatizo la rushwa halipo kabisa kwani Serikali iliongoza vema mapambano dhidi ya rushwa, hivyo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania inavyoendesha vizuri mapambano dhidi ya rushwa kwa ajili ya maslahi ya umma na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Katika mada yake, Mhe. Balozi amefafanua kuwa, nchini Sweden suala la Watumishi wa Umma kuwajibika kwa wananchi limepewa kipaumbele kwani wananchi wote wanahitaji huduma sawa bila ubaguzi wa aina yoyote.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mary Mwanjelwa (Mb) ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kutambua juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwenye eneo la utawala bora.

“Tunaishukuru Serikali ya Sweden kwa kutambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha utawala bora nchini hasa katika mapambano dhidi ya rushwa,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema.

Aidha, katika eneo la uwajibikaji, Mhe. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watumishi wa Umma nchini kuwahudumia wananchi vizuri na kwa wakati kama Serikali inavyosisitiza kila mara.

“Ukiwa Mtumishi wa Umma, tambua wazi kuwa wewe ndio injini kwani wananchi wanahitaji huduma bora kutoka kwako, hivyo unatakiwa muda wote kuwahudumia wananchi kwa uadilifu na bila ubaguzi wa aina yoyote,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Kuhusu uhusiano uliopo kati ya Sweden na Tanzania, Mhe, Mwanjelwa amesema Nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano mzuri tangu utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza na uhusiano huo umeendelea kushamiri hadi sasa kwenye utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

“Uhusiano kati ya Sweden na Tanzania umeanza tangu mwaka 1970 walipojenga Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kwa asilimia 80 na bado tumeendelea kuwa na uhusiano mzuri,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza. 

Mhe. Balozi Sjoberg alitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania na kesho atatembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Tawi la Tabora ili kuona chuo hicho kilichojengwa na Serikali yao na kuangalia jinsi watakavyokienzi.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA LA WILAYA RUANGWA, LINDI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiakagua korosho ambayo tayari imeanza kuvunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza Ruangwa, lililopo Mkoani Lindi.
Ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya mapokezi ya ndugu na jamaa za wafungwa na mahabusu wanaofika Gereza Ruangwa kuwatembelea ndugu zao ukiendelea katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala walipokutana jana Wilayani Ruangwa ziarani(Picha zote na Jeshi la Magereza).





Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, akisalimiana na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza Ruangwa, Mkaguzi wa Magereza, Alex Munga’nzo alipowasili kwa ziara ya kikazi Gerezani hapo.
Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine Semwenda(kushoto) akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Magereza Mkoani Lindi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(meza kuu) alipowasili Gereza Ruangwa

DKT.HINCHA -CHANJO YA SURUA RUBELLA NI SALAMA KWA WATOTO, HAIUI NGUVU ZA KIUME WALA UZAZI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MRATIBU wa huduma za chanjo mkoani Pwani ,Abbas Hincha amesisitiza ni haki ya mtoto kupata chanjo na amewaasa baadhi ya watu kuacha kupotosha kuwa chanjo inayotolewa kwaajili ya surua na surua rubella inaua nguvu za kiume na uzazi ukubwani mwao.

Aidha ameeleza ,mkoa huo unatarajia kufikia watoto 165.875 wenye umri uanzia miezi Tisa hadi chini ya miaka mitano katika kampeni ya chanjo ya magonjwa ya Surua Rubella itakayoanza Octoba 17 -21 mwaka huu.
 Mratibu wa chanjo mkoani Pwani, Abbas Hincha alieleza hayo ,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya afya ya msingi kwa ajili ya kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua Rubella na Polio ya Sindano.

Alisema chanjo hiyo ni muhimu kwa afya ya mtoto na mtoto asiyekamilisha ratiba ya chanjo ni hatari katika maisha yake na jamii inayomzunguka kwani ni rahisi kuambukizwa magonjwa na kuambukiza wengine.

Pamoja na hilo, kampeni hiyo itahusisha utoaji wa chanjo ya polio ya sindano kwa watoto wapatao 93,546 wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.

"Lengo kuu la kitaifa ni kufikia zaidi ya asilimia 99 ya watoto waliolengwa kupata chanjo hizo katika kila eneo na ngazi zote ambapo mkoa umetenga jumla ya timu 156 za uchanjaji ili kufikia vituo 553 vilivyoainishwa na halmashauri zote na maeneo 245 ambayo ni magumu kufikika kutokana na sababu mbalimbali"alifafanua Hincha.
Hincha alisema, hadi sasa mkoa umepokea na kusambaza chanjo katika halmashauri zote na usambazaji ngazi ya vituo unaendelea.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alifafanua, kiwango cha Surua Rubella kimeendelea kuwa juu ,kwa mkoa ni zaidi ya asilimia 100 idadi ya watoto wasiokamilisha chanjo na wasiochanjwa hali ambayo inaweza ikasababisha mlipuko wa ugonjwa wa surua.

Alibainisha ,Rubella ni dada wa surua unatoka vipele vidogo vidogo na mama mjamzito akipata mtoto huathirika zaidi.

Ndikilo alitaja madhara yatokanayo na ugonjwa wa surua kuwa ni ,masikio kutoa usaha,,vidonda vya macho ambao husababisha upofu,Nimonia,utapiamlo ,kuvimba ubongo na kifo.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images