Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

HESLB kutangaza watakaopata mikopo Alhamisi hii

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema itatangaza orodha ya kwanza ya majina ya wanafunzi walioomba na kupangiwa mikopo Alhamisi, Oktoba 17 mwaka huu.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa kazi ya uchambuzi wa maombi ya mikopo yapatayo 55,444 ya wanafunzi ambao wamepata udahili katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo (Jumatatu, Oktoba 14, 2019), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema wanafunzi watakaopangiwa mikopo wataweza kupata taarifa zao kupitia akaunti zao kwenye mtandao wa taasisi hiyo.

Pamoja na kutangaza orodha hiyo, Badru amesema HESLB pia imeamua kutoa fursa kwa waombaji 4,794 ambao bado hadi sasa hawajakamilisha maombi yao kukamilisha kwa kuambatisha nyaraka muhimu mtandaoni.

“Tulitoa siku sita ambazo zinakamilika kesho, Oktoba 15, lakini bado kuna hao ambao tunawaona katika mfumo kuwa bado hawajakamilisha … inawezekana wapo ambao hawahitaji tena mkopo, lakini inawezekana wapo wahitaji wa kweli … kwa hiyo tumeamua hatutafunga mfumo wetu na wanaweza kuendelea kukamilisha,” amesema Badru.

“Wanaweza kuingia katika akaunti zao na kukamilisha, lakini kwa wale ambao watafika vyuoni wakiwa bado hawajakamilisha, tunakutana na maafisa mikopo Ijumaa wiki hii mjini Morogoro na wawahudumie wanafunzi hawa wakiwa vyuoni kwa kupokea nyaraka zinazokosekana na kuziwasilisha kwetu ili wote wenye uhitaji wapangiwe mkopo,” ameongeza Badru.

Kwa mujibu wa Badru, utoaji wa mikopo pia huzingatia makundi maalum kama yatima waliowasilisha nakala za vyeti vya vifo vya wazazi, wenye ulemavu walioambatisha barua kutoka kwa waganga wakuu wa wilaya au mkoa na waombaji mkopo ambao kutokana na hali duni ya kiuchumi, walifadhiliwa katika masomo yao ya sekondari au stashahada.

Kuhusu malengo ya mwaka huu wa masomo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB amesema Serikali imetenga TZS 450 bilioni ambazo zitawanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, wanafunzi zaidi ya 45,000 watakuwa ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo. Bajeti ya mwaka wa masomo 2018/2019 ilikuwa TZS 427.5 bilioni na iliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,329.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu HESLB Abdul-Razaq Badru akizungumza na waandishi habari kuhusiana na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu jijini Dar es Salaam.

MAZIWA YASIOCHEMSHWA VIZURI CHANZO CHA KIFUA KIKUU, WANAFUNZI LIGOMA SEKONDARI WAOMBA MSAADA

$
0
0
Mratibu wa Kitengo cha Kifua Kikuu na Ukoma kutoka hospitali ya wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Dkt. Mkasange Kihongole amewatahadharisha wananchi katika wilaya hiyo kuacha kunywa maziwa ya Ng’ombe holela kutoka kwa wafugaji wanaoingia katika maeneo yao na kwamba Maziwa hayo yanaweza kuwa na vimelea ambavyo ni chanzo kikubwa cha kuenea kwa Ugonjwa wa Kifua kikuu kwa lugha ya kitaalamu ‘BOVINE TUBERCULOSIS’

Dkt Kihongole ametoa kauli hiyo jana ,wakati akiongea na wakazi wa kijiji cha Semeni kata ya Mtina katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya uhamasishaji na uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa wananchi wa kata hiyo,

Dkt. Kihongole alisema licha ya wilaya ya Tunduru kuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa kifua kikuu, hali hiyo inachangiwa pia na unywaji holela wa maziwa ya Ng’ombe yasiyopimwa ambayo ni hatari zaidi kwani usababisha kwa kiwango kikubwa kuenea kwa ugonjwa huo unaotajwa kuwa ni kati ya magonjwa kumi yanayoongoza kuuwa Watu wengi Duniani.

Kwa mujibu wa Kihongole,siku za hivi karibuni kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa wafugaji katika maeneo mbalimbali wilayani humo wanaoingia kutoka mikoa mingine hapa Nchini, wakiwa na Ng’ombe ambao hawajapimwa jambo linalo changia kuongezeka kwa maradhi ya kifua kikuu pale wananchi wanapokunywa maziwa ya Ng’ombe wasiopatiwa tiba sahihi.

Alisema, ndiyo maana Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Global Fund imeanza kuchukua hatau ya kutokomeza Ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030 na kusisitiza kuwa, ni muhimu jamii kuchukua tahadhari kuhusiana na ugonjwa wa Kifua kikuu.

Kihongole alitaja makundi yaliyo katika hatari ya kupata maradhi hayo ni Wazee kwani kadri Binadamu umri unavyokuwa mkubwa kinga za mwili zinapungua,watoto walio chini ya umri wa miaka mitano,wasafiri,watu walio katika msongamono kama vile wafungwa na wale wanaoishi kwenye nyumba ambazo hazina hewa na mwanga wa kutosha kwani wadudu wa kifua kikuu upendelea kuishi kwenye giza .

Alisema, ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari zaidi kuliko Ukimwi,kwa sababu mgonjwa mmoja anaweza kuambikza watu kumi na tano kwa wakati mmoja na Tb inayoogoza kuambukiza kwa haraka ni Tb ya mapafu ambayo mtu anapata kupitia mfumo wa Hewa.

Kihongole alitaja dalili za mtu aliyeambukizwa Tb ni kukohoa kwa wiki mbili au zaidi,kutokwa na jasho jingi hasa nyakati za usiku,kupungua uzito,kupoteza hamu ya kula, na kwa watoto wadogo kuchelewa kukua,kulia lia na kuwa na homa za mara kwa mara.

Dkt Kihongole,amewakumbusha wazazi na walezi kuwa na utaratibu wa kupeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya uchunguzi wa Afya zao mara kwa mara,badala ya kuamini mambo ya kishirikina ambayo usababisha kupoteza maisha ya watu wengi hasa watoto wadogo.

Kwa upande wake,Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Renatus amewataka watu wanaofanyiwa vipimo na kubainika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Tb ni vema kuhakikisha wanamaliza dozi(Dawa)wanazopewa na kuepuka kukatisha dawa kwani ni hatari sana kwa Afya zao na watu wengine.

Aidha,ameitaka jamii kuwaibua watu wanaohisiwa kupata ugonjwa huo na magonjwa mengine yanayoambukiza na kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma ili kupata tiba itakayowasaidia kuwa na Afya njema na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Amewakumbusha akina mama pindi wanapoona dalili za ujauzito ni vema kwenda kliniki haraka na wenza wao kupata ushauri wa wataalam na kuhakikisha wanatumia zahanati na vituo vya Afya kujifungulia badala ya kubaki nyumbani kwani ni hatari kwa afya zao na watoto wakati wa kujifungua.

Hata hivyo,mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Hamza Malembo ameiomba Serikali kupeleka Dawa na vifaa tiba vya kutosha ili kuwasaidia kwani baadhi ya Zahanati hasa zile za maeneo ya pembezoni zina upungufu mkubwa na wanapofika vituoni wanaelekezwa kwenda kununua kwenye maduka ya watu binafsi,jambo linalowakatisha sana tamaa.

Wajasiriamali Wahimizwa Kuchangamkia Fursa TBS

$
0
0

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa wito kwa wajasiriamali wote nchini kupeleka bidhaa zao ili ziweze kuthibitishwa ubora wake na shirika hilo bure, kwani gharama zote zimeishalipwa na Serikali.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti na leseni 94 kwa wazalishaji wakubwa, wa kati na wadogo ambao bidhaa zao zimethibitishwa na Shirika hilo na kukidhi matakwa ya viwango vya ubora kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba, mwaka huu.

Kati ya vyeti na leseni 94 zilizotolewa, vyeti 25 vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo ambao bidhaa zao zimekidhi matakwa ya viwango.

Dkt.Ngenya, alisema vyeti na leseni zilizotolewa zitawasaidia wazalishaji hao kuongeza imani kwa watumiaji, kwani wanapoona alama ya ubora ya tbs watumiaji wanakuwa na imani kubwa na bidhaa husika, hivyo kupanua soko.

Alisisitiza kwamba bidhaa zinapokuwa zinathibitishwa ubora na shirika hilo, bidhaa hizo zinakubalika moja kwa moja sokoni, zinahimili soko la ushindani na kuingia kifua mbele katika soko la nchi za Afrika Mashariki.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, inaendelea kuwahudumia wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure, hivyo alitoa wito kwa wajasiriamali  kujitokeza kwa wingi kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kwa kuwa gharama zote zinalipwa na Serikali.

Dkt. Ngenya aliishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Dkt.Ngenya aliwahimiza wajasiriamali kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora na Watanzania kuanza kupenda bidhaa za ndani ambazo zimethibitishwa ubora.

"Watanzania tununue bidhaa zenye ubora kuangalia alama ya tbs  hii itatufanya tuingie katika Tanzania ya viwanda kwa kupenda vya kwetu," alisema

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa kutoka Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), Ridhiwani Matange, alisema kazi inayofanywa na Shirika la TBS ni nzuri inajaribu kuweka nchi katika hali ya  usalama kwenye bidhaa mbalimbali.

Naye Mhandisi Cdi Nyakwela kutoka Kampuni ya Plasco wazalishaji wa Makaravati ya Plastiki ,alisema vyeti  hivyo walivyopatia  vitawasaidia kupata soko kubwa ndani na nje ya nchi.

Alisema kutokana na bidhaa hizo kuwa mpya watahakikisha wanajitangaza ili Watanzania waweze kuona kasi ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda inavyokuja na teknolojia mpya.

"TBS wametupatia leseni ya ubora ni jukumu letu sasa kuhakikisha tunazalisha makaravati ya plastiki yenye ubora na viwango kinachotakiwa na sio kufanya ujanja ujanja," alisema Mhandisi Nyakwela

BODI YA UTALII YAGAWA VIPEPERUSHI VYA MAONESHO YA SITE 2019, JIJINI DAR

$
0
0


Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Jaji Maiko Mihayo akiwa anagawa vipeperushi vya matangazo ya Maonesho ya Ya tano ya Swahili International Tourism Expo (SITE) kwa wananchi wanaopita na magari kwenye Barabara ya Kenyata, Maonesho hayo yanatarajia kuanza Oktoba 18-20 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Jaji Maiko Mihayo akiwa anamuangalia muuza magazeti aliyemkabidhi vipeperushi na kuviweka ndani ya magazeti na kuwapatia wateja wake. Zoezi hilo la kugawa vipeperushi limefanyika  leo kwenye barabara ya Kenyata.

 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB), Godfrey Tengeneza akigawa vipeperushi vya matangazo ya maonesho ya tano ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yanayotarajia kuanza Oktoba 18-20 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City.
Mratibu wa Onesho la SITE 2019Joseph Sendwa akigawa vipeperushi vya matangazo ya maonesho ya tano ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yanayotarajia kuanza Oktoba 18-20 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Jaji Mstaafu Frank Mihayo amefanya zoezi la kugawa vipeperushi kwa ajili ya maonesho ya tano ya utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE).

Maonesho hayo yanatarajia kuanza Oktoba 18-20 ya mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumaliza zoezi la kugawa vipeperushi hivyo kwa wananchi, Jaji Mihayo amesema wataendelea na zoezi la kugawa vipeperushi katika maeneo tofauti hadi kufikia siku ya maonesho hayo.

Amesema, watanzania lazima wafahamu umuhimu wa maonesho haya ambapo wageni zaidi ya 400 kutoka mataifa mbalimbali watakaonesha mazao ya utalii wa aina tofauti.

"Watakuja watalii wengi sana, maana kila balozi zetu zimefanikisha kuwaleta wadau wa utalii na wataonesha mazao mbalimbali ili kuhakikisha onesho linafanikiwa,"amesema Mihayo.

Mihayo amesema, matayarisho yamefikia hatua nzuri, kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa ngoma zetu za asili zikiburudisha kusindikiza onesho letu la mazao ya utalii.

"Tunahitaji watu wafahamu bodi ya utalii inafanya nini ili kukuza utalii, na lengo pia ni kuwakutanisha wadau wa utalii mbalimbali wakija kuuza na kununua mazo ya utalii na huu ndio mida mzuri wa wadau wa utalii kuja kuonesha bidhaa zao," amesema

Naye Afisa Uhusiano wa TTB, Godfrey Tengeneza amesema maonesho hayo yatakuwa ya siku tatu na yatafunguliwa Oktoba 18 na kufungwa Oktoba 20 mwaka huu, ambapo maandalizi yamekamilika kwa hatua kubwa .

"Tumeandaa matangazo mbalimbali ambapo yamebandikwa kwenye maeneo tofauti,  na tumejiandaa kwa kiasi cha kutosha na nawaomba watanzania waje kutembelea na kujiona mazao ya utalii kutoka dunia nzima,"amesema Tengeneza.

Pia, kutakuwa na semina kutoka kwa wataalamu waliobobea kwenye masuala ya utalii.

Bodi ya Utalii inafanya onesho lake tano la  Utalii la Kimataifa nchini (SITE) linatarajiwa kukutanisha wadau wa utalii wa Kimataifa wa ndani  ya nchi zaidi ya 400.

Washiriki wa maonesho hayo ni mawakala wa utalii wa Kimataifa, waandishi wa habari za utalii wa kimataifa na wafanyabiashsra wa utalii kutoka Tanzania na nchi za jirani.

Washiriki hao wanatarajiwa kutoka nchi zaidi ya 57 Ulimwenguni na  baadhi ya nchi mashuhuri zinazotarajiwa kuleta washiriki ni Marekani, Uingereza, Italia, Ujerumani, Urusi, China, Sweden, Afrika Kusini, Seychelles, Mauritius, Rwanda, Malaysia, Kenya, Thailand, India, Korea ya Kusini na Singapore.

Maonesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwani mwaka 2014 kampuni za uoneshaji utalii zilikuwa 40 na mwaka 2018 zimekuwa 152 na wadau wa safari wakubwa wa kimataifa kwa mwaka 2014 walikuwa 24 na mwaka 2018 walikuwa 335.

MWAKINYO KUPAMBANA NA TINAMPAY KUTOKA UFILIPINO NOVEMBA 29 MKWAKA HUU

$
0
0
 Bondia Hassan Mwakinyo akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye pambano lake dhidi ya Bondia Arnel Tinampay raia wa Ufilipino litakalofanyika Novemba 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa. 
Promota Jay Msangi, anayeratibu pambano hilo akizungumzia maandalizi na kuwataka wadau wa michezo kujitokeza na kuweza kudhamini, na pambano hilo litatanguliwa na mapambano matano ya utangulizi kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.(Kushoto) Bondia Hassan Mwakinyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BONDIA Mtanzania mwenye rekodi ya kushinda mapambano 17 na kupoteza moja Hassan Mwakinyo  atapanda ulingoni Novemba 29 katika pambano la Vitasa Fight Night dhidi ya Arnel Tinampay raia wa Ufilipino kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mwakinyo mwenye rekodi ya kushinda kwa KO mapambano 15, na kupoteza Mmoja dhidi ya Mtanzania Shaban Kaoneka amekuja na kauli mbiu ya do or die  (kufa ua kupona).

Mwakinyo amesema anafahamu kama mchezo huo ni mgumu hususani kulingana na ubora wa mpinzani wake ambaye kwa nchini Ufilipino ana rekodi nzuri na katika mapambano aliyoyapoteza hajawahi kupigwa KO.

" Siwezj kumdharau mpinzani wangu ndio maana naendelea na mazoezi chini ya Kocha wangu, nafahamu ni bondia mzuri, mgumu na mzoefu na hana rekodi ya kupigwa Knock Out (KO), ni mgumu na anahitaji mbinu za ziada na mazoezi ili kumpiga," amesema Mwakinyo.

"Pambano hilo ni la raundi 10, katika uzani wa Super Welter"

Mwakinyo amesema, anajipanga kuweza kushinda pambano hilo, atatumia mbinu zake kuhakikisha anabakiza heshima nchini kwani anapambana kwa ajili ya Taifa na kuliwekea heshima.

"Nitacheza kufa ua kupona kuhakikisha naendeleza rekodi yangu, natambua ugumu wa pambano hili na ubora wa mpinzani wangu ambaye ni bondia huyo ambaye ni namba moja katika viwango vya ubora nchini Ufilipino kwenye uzani wa super welter," amesema.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi amesema Mwakinyo na Tinampay watasindikizwa na mapambano matano ya utangulizi ya mabondia kutoka nchini na nje ya nchi ambao tayari tupo kwenye mazungumzo nao.

Msangi amesema, wapo na mazungumzo na IBF,WBO kuangalia kama pambano hili litakuwa la ubingwa na kama sio basi mshindi acheze pambano la ubingwa.

" Thamani ya Mwakinyo ni zaidi ya milion 100, ila tayari maandalizi yanaenda vizuri na tunazidi kuwaomba wadau wa mchezo wa ngumi kuja kudhamini pambano hili ambapo tayari tumeshapata baadahi ha wadau na pambano hili litarushwa na katika nchi mbalimbali duniani,"amesema Msangi.

Wadau wa michezo hususani wa ngumi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo, na ushindi wa Mwakinyo utawavutia wacheza ngumu wakubwa duniani.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI JIMBO LA MTAMA WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA WILAYANI RUANGWA MKOANI LINDI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Lindi vijijini katika jimbo la Mtama (hawaonekani pichani) mkoani Lindi wakati akielekea katika Jimbo la Ruangwa.
 
Wananchi wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi wakishangilia kwa furaha wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA JIMBO LA MTAMA WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA WILAYANI RUANGWA MKOANI LINDI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Lindi vijijini katika jimbo la Mtama (hawaonekani pichani) mkoani Lindi wakati akielekea katika Jimbo la Ruangwa.
Wananchi wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi wakishangilia kwa furaha wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi. PICHA NA IKULU

Tekinolojia Kuleta Ufanisi Mkubwa Katika Sensa ya Mwaka 2022, Mtakwimu Mkuu wa Serikali.

$
0
0
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa amesema matumizi ya tekinolojia za kisasa zitaleta ufanisi mkubwa katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 hivyo kuipatia nchi Takwimu za uhakika zaidi na kwa wakati kuliko Sensa zilizopita.

Dk. Chuwa alieleza hayo jana wakati alipotembelea wilaya ya Kondoa kukagua maendeleo na ubora wa kazi katika zoezi ya kutenga maeneo katika mtaa wa Mnarani wilayani Kondoa ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

“Lengo letu ni kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Ufanisi mkubwa na nimekuja hapa kukagua na kutathmini ubora wa kazi ya kutenga maeneo katika wilaya yenu” Dk. Chuwa alimueleza Afisa Mtendaji, Kata ya Kondoa Mjini Samson Mtui alipofika Ofisini kwake kujitambulisha.
Wakati wa ukaguzi huo Dk. Chuwa alioneshwa namna maeneo hayo yanavyopimwa na kuwekewa mipaka pamoja na namna taarifa zinavyohifadhiwa katika Kishikwabi (tablet) ambazo zitatumika wakati wa kuhesabu watu tofauti na Sensa zilizopita ambapo Wadadisi walikuwa wakitumia ramani zilizochorwa katika karatasi. 

Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Taarifa za Kijiografia katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Benedict Mugambi alimueleza Mtakwimu Mkuu kuwa kwa kutumia Kishikwambi Mdadisi atafanya kazi yake ya kuhesabu watu katika eneo lake tu na hataweza kuingia eneo la mwenzake.
“Mdadisi akitoka nje ya eneo lake Kishikwambwi kitamuonesha alama kuwa anaingia eneo silo lakini zaidi Dodoso halitaweza kufunguka hivyo hataweza kufanya kazi” alieleza Mugambi. 

Dk. Chuwa alibainisha kuwa matumizi hayo ya tekinolojia yatapunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha watu wanaosahaulika kuhesabiwa wakati wa zoezi la kuhesabu watu.
Katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kiwango cha watu waliosahaulika kuhesabiwa kilikuwa asilimia 5 ambacho hata hivyo ni cha chini ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.

Kwa mfano, katika Sensa iliyopita nchini Afrika Kusini kiwango cha watu waliosahaulika kuhesabuwa kiliwa zaidi ya asilimia kumi. 
 “Tunataka kile kiwango cha asilimia 5 cha waliosahauliwa kuhesabiwa mwaka 2012 kiondoke katika Sensa ijayo ili tupate takwimu halisi na kuongeza ufanisi katika upangaji wa mipango yetu ya maendeleo” Dk. Chuwa alisisitiza.

Awali, akitoa taarifa ya kazi, kiongozi wa timu hiyo Mrasimu Ramani Jerve Gasto wa NBS alieleza kuwa hadi sasa vijiji vyote 84 katika Halmashauri ya Kondoa Vijijni tayari vimetengewa maeneo ya kuhesabia watu na taarifa zote muhimu zimeshachukuliwa na kuweka katika ramani.
Kwa upande wa Halmashauri ya Kondoa Mjini, Gasto alieleza kuwa kazi imeanza na wamekamilisha mtaa mmoja wa Mnarani kati ya mitaa 36 na kuongeza kuwa kazi hiyo inatarajiwa kumalizika baada ya siku kumi.
Kuhusu taarifa zilizokusanywa alieleza kuwa ni za huduma za jamii kama elimu, maji na afya, shughuli za uzalishaji kama viwanda na ofisi za serikali na huduma za kiroho. 

Gasto alieleza kuwa mwitikio wa wananchi ni mzuri na wamekuwa wakiwapa ushirikiano wakati wote wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao na kuwashukuru viongozi wa wilaya kwa kuwa nao bega kwa bega tangu walipoanza kazi hiyo wilayani humo.  
Hata hiyo alieleza kuna changamoto kadhaa wanazopambana nazo wakiwa kazini ikiwemo baadhi ya wananchi kuingia katika mapori ya hifadhi na utata wa mipaka katika baadhi ya vijiji. 

Kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu wilayani Kondoa ilianza tarehe 16 Septemba, 2019 na kushirikisha warasimu ramani kutoka NBS, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) na wataalamu wa mipango miji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Watalamu hao wamegawanyika katika timu tano zenye watu watatu kila moja na kwa mujibu wa Gasto timu ya sita inatarajiwa kujiunga nao sasa kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa.
 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akizungumza na Afisa Mtendaji, Kata ya Kondoa Mjini Samson Mtui alipofika Ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kuanza ziara ya kukagua maendeleo na ubora wa kazi ya kutenga maeneo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022
 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrasimu ramani Emmanuel Mahemba wakati wa ziara ya kukagua kazi ya utengaji maeneo katika Mtaa wa Mnarani, Kata ya Kondoa Mjini mkoani Dodoma.  Kulia ni Mrasimu Ramani Galos Mbedule.
 Mkuu wa Kitengo cha Mfumo wa Taarifa za Kijiografia Ofisi ya Taifa ya Takwimu Benedict Mugambi akitoa maelezo namna maeneo ya kuhesabia watu yanavyotengwa na taarifa za taarifa za kijiografia zinavyokusanywa. Wengine ni warasimu ramani na kwa nyuma ni Meneja wa Takwimu Mkoa wa Dodoama Iddi Mruke.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akitoa maelekezo kwa timu ya warasimu ramani wanafanya kazi ya kutenga maeneo huko wilayani Kondoa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

TANZANIA INATARAJIA KUPATA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 500 KWA AJILI YA MRADI WA ELIMU

$
0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington Dc

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayewakilisha nchi za Afrika Bi. Anne Namara Kabagambe, Mjini Washington DC, Marekani.

Mazungumzo hayo yalilenga katika kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za fedha na namna uchumi wa Dunia unavyoendeshwa.

Katika mazungumzo hayo baadhi ya miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme la mto Rufiji, mradi wa elimu,na miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ilijadiliwa. 

Dr. Mpango alieleza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuinua kiwango cha elimu, kwa kutafuta fedha zaidi na mikopo ya masharti nafuu ambayo itaelekezwa kwenye elimu.

‘’Katika Mradi wa Elimu unaotarajiwa kuwasilishwa Benki ya Dunia mwezi Novemba, 2019, tunatarajia kupata dola za Marekani milioni 500, na nimemuomba Bi. Anne Namara Kabagambe azidi kusisitiza ili Taifa liweze kupatafedha hizi kwa wakati, na tunaamini kwamba fedha hizo zitaidhinishwa na Benki ya Dunia kama tunavyotarajia.”Alisisitiza Dkt Mpango.

Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango alisema pamoja na miradi ya Elimu, Sekta ya nishati ya umeme pia ni muhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa sababu ukipatikana umeme wa kutosha utasaidia kwa vitendo agenda ya uchumi wa viwanda kwa kuongeza thamani ya mazao na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii nchini.

Aliiomba Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa zisaidie kwenye miradi ya mikubwa inayotekelezwa na Serikali hasa katika sekta ya umeme na miundombinu.

Aidha Dkt. Mpango alieleza kuwa hivi karibunii Benki ya Dunia iliipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 450 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, awamu ya tatu.

“Hivyo kupitia miradi miwili ya Elimu na TASAF, Tanzania inatarajia kupata dola za Marekani milioni 950”. Aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wa Benki ya Dunia Bi. Anne Namara Kabagambe alielezea kufurahishwa na utekelezaji wa miradi inayofanyika Tanzania kwani alipata fursa ya kuona miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na miradi inayotekelezwa na TASAF, na kuelezea kuwa ni miradi ya mfano na kwa nafasi yake ataendelea kuitangaza miradi hiyo ili Tanzania iweze kupata fedha zaidi ya kutekeleza miradi hiyo.

Dkt. Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Dunia IMF ambapo amesema mikutano hiyo ni muhimu kwa kuwa nchi itapata fursa ya kuweza kujadiliana na Taasisi hizi za IMF na WB kuhusu miradi wanayofadhili.

Aidha, kupitia mikutano hiyo vipaumbele vya nchi vitaelezwa na kupitia changamoto zilizopo kwa sasa, kutetea maslahi mapana ya Tanzania katika utekelezaji wa programu za maendeleo na mabadiliko ya kimfumo katika uendeshaji wa uchumi kutegemeana na mwenendo wa Dunia unavyokwenda,

Alisisitiza kuwa nchi inapata uzoefu wa nchi nyingine wanavyotekeleza na kusimamia program zao na wao pia kuweza kuzieleza nchi nyingine namna ambavyo Tanzania inatekeleza programu mbalimbali za kimaendeleo.
 Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. (Mb)  Philip Isdor Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Mohamed R. Abdiwawa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Khamis M. Omary wakiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (hayupo pichani) kuhusu miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kundi la  Afrika Bi Anne Namara Kabagambe na Mshauri Mwandamizi kundi la Afrika Bw. Zarau Kibwe akielezea mafanikio aliyoyaona alipotembelea miradi ya Maendeleo Tanzania.  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniWizara ya Fedha na Mipango)

WAZIRI KANGI LUGOLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ETHIOPIA NCHINI, JIJINI DODOMA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA, Dodoma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma, leo, ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia. 
Waziri Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. 
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.
Kwa upande wake Balozi Sanbe, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Ethiopia na Tanzania.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dodoma, leo. 
 Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia), akimfafanulia jambo Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (kushoto), wakati walipotembelewa na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, Ofisi za Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimuaga Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya kumaliza mazungumzo yao, Ofisini kwake, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. 
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia) akimuaga Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo pichani), jijini Dodoma, leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya Balozi huyo kuwatembelea viongozi hao, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MIKOA YA KANDA YA ZIWA YAONGOZA MATOKEO DARASA LA SABA

$
0
0
Katibu Mkuu wa baraza la mitihani la Taifa, Dkt. Dkt Charles Msonde.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MIKOA ya kanda ya ziwa yaongoza matokeo ya kumaliza elimu ya Msingi kwa kuongoza kwa shule 10 bora zote zikitokea katika mikoa ya Mara, Kagera na shinyanga. 

Shule kumi zilizofanya vizuri katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi hapa nchini ni, Graiyaki ya Mkoa wa Mara, Twibhoki Mara, Kemebos ya Kagera , Little Treasures Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa Mwanza shule ya Musabe. 

Hata hivyo shule nyingine ni Tulele ya mkoani Mwanza, Kwema Modern ya Mkoa wa shinyanga pia, Peaceland, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill mkoa wa Shinyanga. 

Akitangaza matokeo ya Darasa la Saba leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani la taifa (NECTA) , Dkt Charles Msonde amesema kuwa katika matokeo ya waliofanya mtihani ni  asilimia 81.5 sawa na watahiniwa 933,369 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Dkt. Msonde amesema kuwa kwa mwaka huu 2019 ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78 wakati shule za mikoa ya kanda ya ziwa ikiwa kinara kwa kuongoza.

WATU SABA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUIBA VIFAA KATIKA MIRADI YA MAJI YA BILIONI 520

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi blog,Arusha .

Watu 7 wakiwemo wenyeviti wawili wa vitongoji wametiwa mbarobi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 520 katika eneo ka ujenzi wa moja kati ya visima 53 katika kata ya kikwe kijiji cha mawe wilaya ya Arumeru

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa kukamatwa kwa watu hao kumetokana na mtego alikuwa ameuweka mara baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wananchi wanaoshirikiana na wafanyakazi na walinzi wanaolinda maeneo ya mradi kuiba vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo , mabomba pamoja na mbao na mabati.

Alisema kuwa Kutokana na taarifa hizo ilimlazimu kufanya msako wa ghalfa na kustukiza katika nyumba za baadhi ya wananchina wafanyakazi wa mradi huo wanaodaiwa kuiba vifaa hivyo ambapo walifanikiwa kukuta nondo zaidi ya 40 zikiwa zimetelekezwa nje ya nyumba ya mwananchi mmoja ambae awali alikuwa akifanya kazi katika mradi huo baada ya wezi wa nondo hizo kustuka kuwa wanafuatiliwa na kuamua kukimbia 

"msako huu ulianza alfajiri mpaka mchana na tumeamua kufanya zoezi hilo nanatoa onyo kwa watu wote wanaotaka kuhujumu miradi hii ya maji kuacha tabia hiyo mara moja nana sisitiza kuwa nitawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuiba na kuficha vifaa vya ujenzi katika miradi"alisema Muro 

Kwa upande wao baadhi ya watuhumiwa mbali na kukiri kuiba vitu katika miradi wamesema mtandao wa wizi huo ni mkubwa uku ukihusisha baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji ambavyo mradi huo unatekelezwa 

Kwa upande wake Diwani wa kata ya kikwe Paul Shango ambae alikuwa kwenye kikosi cha mkuu wa wilaya cha kusaka wezi , mbali na alipongeza jitihada zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ya kusimamia miradi hiyo kikamilifu amewataka wananchi kutothubutu kuhujumu miradi hiyo kwa kuwa ina manufaa kwa wananchi haswa katika kuwapatia maji safi na salama 

Katika hatua nyingi Mkuu wa wilaya ya Arumeru ametoa mwezi mmoja kwa kamanda wa polisi wa wilaya ya Arumeru mlowola kuwahamisha askari polisi ambao sio waaminifu wanaofanya kazi katika kituo cha polisi mbuguni kutokana na baadhi yao kutuhumiwa kuwalea wezi wanaoiba vifaa katika miradi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwahoji baadhi ya watuhumiwa wanaoabiliwa na tuhuma za wizi wa vifaa vya mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 520.

SERIKALI YAENDELEA KUWAWEZESHA WAWEKEZAJI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha.

SERIKALI imesema kuwa itahakikisha inaendelea kushirikiana na wawekezaji hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira mazuri ili waweze kufanya shughuli zao pasipo kuwa na bughudha zozote kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la Taifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo,Elisante ole Gabriel
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara yake ya
kutembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Happy Sausage kilichopo
Sakina jijini hapa.

“Wawekezaji wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuinua pato la
taifa pamoja na uchumi wa n chi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na
kuchangia kupatikana kwa ajira nyingi kwa wananchi hivyo hawana budi
kuthaminiwa kwa mchango wao huo’’alisema Katibu Mkuu huyo.

Ole Gabriel alisema kuwa anatambua changamoto mbalimbali
zinazokikabili kiwanda hicho cha Happy Sausage ikiwemo mgogoro wa muda mrefu kati yake na halimashauri ya jiji la Arusha hali ambyo imekuwa
ikichangia kusuasua kwa uzalishaji na kuhahidi kulipatia ufumbuzi
ndani ya muda mchache.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu huyo,Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kiwanda hicho,Andrew Mollel alimweleza katibu mkuu huyo kuwa kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 1990 na kwamba kimekuwa kikizalisha bidhaa zenye ubora ambapo kwa sasa kimejipanga kutanua soko lao kufikia nchi zote za Afrika Mashariki.

“Kiwanda kimeshindwa kufikia malengo ya kuongeza uzalishaji kutokana
na kujikuta ikikwamishwa kufanya ukarabati wa kiwanda hicho ilihali
serikali kupitia vizara ya mifugo na uvuvi kwa nyakati tofauti imekuwa
ikikitaka kiwanda hicho kufanya ukarabati imekuwa ndio changamoto yetu
kufikia malengo ya uzalishaji”.alisema Mollel

Mwenyekiti huyo wa bodi aliongeza kuwa pia halimashauri ya jiji la
Arusha imekuwa ikikwamisha ukuaji wa kiwanda hicho kwani imekataa
kutoa kibali cha ukarabati na upanuzi wa majengo ya kiwanda
hicho(building permit) jambo linalokwamisha uongezaji wa thamani na
uzalishaji hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa sana kwao na
kuiomba serikali kuu kuu kuingilia kati.

Mollel aliiomba Serikali kumpatia eneo lenye ukubwa wa ekari 300
katika eneo la Muriet jijini hapa ili aweze kuanzisha shamba kubwa la
mifugo litakalokiwezesha kiwanda hicho kufuga mifugo mingi ikiwemo
nguruwe kwani tayari wamekwishafanya mazungumzo na serikali ya
Ujerumani ambapo imewaahidi kuwapatia mbegu za nguruwe wanaokua kwa muda mfupi ukilinganisha na wa hapa Tanzania ambao huchukua muda
mrefu kukua.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI RUANGWA MKOANI LINDI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasili Ruangwa mkoani Lindi leo tarehe 15/11/2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Nanganga- Ruangwa sehemu ya Kitandi-Ruangwa km 5 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha Lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ruangwa mara baada ya ufunguzi wa barabara ya Nanganga- Ruangwa sehemu ya Kitandi-Ruangwa km 5 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha Lami. Kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakiweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Ghala la Mazao Ruangwa mkoani Lindi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Ghala la Mazao Ruangwa mkoani Lindi. PICHA NA IKULU

WANAUME WATAKIWA KUEPUKANA NA MFUMO DUME

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

WANAUME hapa nchini wameshauriwa kuepukana na mfumo dume ambao kwa muda mrefu umekuwa ukiwakandamiza wanawake ikiwa ni pamoja na kuepukana na kuwadhania au kuwatumia wanawake kama kifaa cha kazi.

Hayo yalisemwa jana na Mwalimu Daniel Mgogo kutoka katika kanisa la Baptist la Tukuyu Mbeya,alipokuwa akizungumza katika kongamano la siku ya Mke Mwema,kongamano lililofanyika jijini hapa.

Alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wanaume kubadilika na kuachana na dhana,desturi na mila potofu ambazo zimepitwa na wakati ambapo aliwasihi wadumishe upendo katika ndoa zao ikiwa ni pamoja na
kuwaheshimu wake zao.

“Mfumo dume unatakiwa upigwe vita na ukomeshwe,angalia mwanamke anabeba mimba kwa miezi tisa na mwanaume yupo tu,ila baada ya kujifungua motto ni wa baba,ni lini ulisikia mtoto kapewa jina la mama”alihoji .

Mwalimu Mgogo alisema kuwa wanawake hapa nchini wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo masuala ya mirathi kutokana na mfumo dume,ikiwa ni pamoja na kuachiwa peke yao jukumu la matunzo ya mtoto.

“Mwanamke anapoolewa anaamini kaolewa na mtu mmoja ila baada ya mudaanajikuta kaolewa na ukoo, wifi,shemeji,mama na baba mkwe kila mtu atakuwa anamtaka kufanya au kutofanya jambo Fulani na kila mmoja kwa wakati wake hali ambayo humfanya mwanamke asijue amsikilize nani na asimsikilize nani kwani muda mwingi huwa na hao,alisema

Naye Mhubiri kutoka huduma ya New Life in Christ ya Mkoani hapa,Mhandisi Tunzo Mnzava,ametoa wito kwa wanawake kuzingatia mafundisho kwani ndio msingi wa maisha ikiwamo kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na kuhakikisha wanawaheshimu na kuwathamini waume zao.

Mhandisi Mnzava amewataka wawe waaminifu ikiwa ni pamoja na kuwa na utoshelezi kwa waume zao pamoja na kujiamini na watamani ndoa zao ziwe za milele,Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Mke Mwema,Aimbora Kwayu alisema kuwa kikindi hicho kilianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa kina wanachama zaidi ya 200 kutoka maeneo mbalimbali.

“Siku ya Mke Mwema huazimishwa tarehe kumi na nne oktoba kila mwaka ambapo huwakutanisha wanachama ambao wamegawanyika katika timu pamoja na wageni waalikwa mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano baina yao.

Alisema kuwa kikundi cha mke mwema kimegawanyika katika timu mbalimbali ambapo mpaka sasa wana timu tano ambazo ni Njiro,Moshono,Uswahilini,Wilayani na Sakina ambao ndio walioandaa
tukio hilo.

UHAMIAJI ARUSHA:TUJENGE TABIA YA KUTEMBELEA HIFADHI ZETU.

$
0
0

Baadhi ya watumishi wa Idara ya uhamiaji ,Wahifadhi pamoja na watumishi wa Mega Group wakiwa kwenye eneo la hifadhi ya Tarangire wakati walipotembelea hifadhi hiyo kuhamasisha utalii wa ndani


Na Vero Ignatus,Arusha.

Katika kuhamasisha utalii wa ndani nchini Idara ya Uhamiaji mkoa wa Arusha imeshiriki kutembelea hifadhi hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambapo wamejionea vivutio mbalimbali ikiwemo makundi makubwa ya tembo,twiga,pundamilia na vivutio vingine.

Naibu Kamishna Abdallah Towo ni Afisa wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, amesema kuwa wameamua kutembelea hifadhi ikiwa ni moja kati ya njia za kuhamasisha Taasisi nyingine za serikali kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi wakiwa na wafanyakazi wao lengo ikiwa ni kuhimiza ufanisi kazini na kujenga mahusiano bora kazini.

Issa Mlweta ni Mrakibu wa Uhamiaji amesema kuwa Uhamiaji ni wadau wakubwa wa utalii kwani wanawakaribisha watalii wanapoingia na kutoka katika mipaka ikiwa ni pamoja na kuhamasisha utalii na kutangaza vivutio muhimu tulivyonavyo.

Harieli Msaki ni Mhifadhi Mwandamizi Ujirani Mwema hifadhi ya Tarangire ,amesema kuwa hifadhi hiyo inatembelewa na watalii laki moja kila mwaka kutoka nchi za nje huku utalii wa ndani ukiwa chini hivyo ameipongeza uhamiaji na kuzitaka Taasisi nyingine ziige mfano wake.

Hikloch Ogola ni Mkurugenzi wa tafiti na Maendeleo kutoka Mega Media Group ,ambao ni waandaaji wa ziara hiyo amesema kuwa wameanzisha program maalumu ya kuhamasisha taasisi za umma na binafsi kutembelea vivutio vya utalii ili kuinua mapato ya utalii wa ndani na vile vile kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii..

Utalii ni moja kati ya sekta ambazo zinaongoza kwa kuliingizia taifa fedha za geni na kuchangia kiasi cha asilimia 17% katika pato la taifa hivyo juhudi endelevu zinahitajika katika kuhamasisha utalii wa ndani.

AFISA TARAFA ITISO AKATAA TAARIFA YA KAMATI YA MAJI, AAGIZA IANDIKWE UPYA

$
0
0
AFISA Tarafa wa Itiso, wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Remidius Emmanuel amewahamasisha wananchi  wa tarafa hiyo kuendelea kujiandikisha katika orodha ya Daftari la Wapiga kura kwa  kutambua thamani yaa kuchagua viongozi wa Kijiji na Kitongoji chao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novenba  24 mwaka .

Afisa Tarafa huyo ameyasema hayo wakati akiwa katika ziarani katika  Kitongoji cha Wali (Kijiji cha Izava) kwa lengo la kuhamasisha wananchi hao kuendelea kujiandikisha katika orodha ya Daftari la Wapiga kura, ameesema kuwa  serikali inapanga maendeleo yake kuanzi ngazi ya mtaa, Kijtongoji  pamoja na Kijiji.

"Nyinyi ni mashahidi, wengi tumeshuhudia na kusikia Oktoba 12 mwaka huu  katika ardhi hii ya Wilaya ya Chamwino Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli alijiandikisha katika Kituo cha Sokoine (Chamwino Ikulu), Mheshimiwa Mkuu Wa wilaya yetu nae ameisha jiandikisha,mimi Afisa Tarafa wenu tayari nimejiandikisha, Sasa ni zamu yenu kujiandikisha kwa wingi wale ambao hawajashiriki zoezi hili.amesema Afisa Tarafa huyo.

 Katika hatua nyingine Afisa Tarafa  huyo ameikataa taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kijiji cha Izava  iliyosomwa mbele yake baada ya wananchi kulalamika kwa  kipindi kirefu pasipo kusomewa mapato na Matumizi ya mradi wa Maji Kitongojini  hapo baada ya Afisa huyo kuwataka wananchi  waseme kero  zote zinazowakabili. 

Emmanuel amesema kuwa viongozi tunapaswa kuwajibika na kutendea haki nafasi na nyadhifa tulizo nazo, mambo haya ya kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi ni tafsiri ya baadhi yetu kushindwa kutimiza wajibu wetu na kuwafanya wananchi kupunguza imani na viongozi wao.

Amesema wananchi wachague viongozi ambao watakuwa wanasoma mapato na matumizi kwa wakati  na kuweza kufanyika maendeleo kutokana na miradi  inayoendelea.
Hata hivyo Afisa tarafa huyo alikataa kuipokea taarifa iliyosomwa mbele yake na kamati hiyo  na kuagiza iandaliwe taarifa nyingine  itakayotoa mchanganuo sahihi pamoja na nyaraka muhimu ili wananchi hao waweze kusomewa taarifa sahihi ya mradi huo.

" Mfano,nimesikia kuna mahala hapa taarifa inaonyesha kwamba wajumbe walienda  kufungua akauti ya Maji  Dodoma na walitumia Tsh.400,000/=, Yaani kwenda Dodoma  na kufungua akauti mnatumia kiasi hiki cha fedha ?..Sasa nataka iandaliwe taarifa nyingine na iwe na mchanganuo wa mapato na matumizi ya fedha hizi ili wananchi wafahamu na lazima muweke na nyaraka zitakazoonyesha uhalisia wa matumizi hayo"  Amesema Afisa Tarafa.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa kamati ya Maji  Amosi Mainaa Lugumbau aliwaomba radhi wananchi hao baada ya  kukiuka  makubaliano ya awali na kushindwa kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wa kitongoji hicho pamoja na kutohusisha uongozi wa kijiji katika shughuli zote za mradi huo.

Katika ziara yake, Afisa Tarafa aliambatana na Mtendaji wa kata ya Segala Bi.Twahia komba pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Izava.

 Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akionyesha Stakabadhi ya Shilingi Milioni Moja iliyorejeshwa katika akaunti ya maji baada ya kamati ya maji kushikilia fedha hiyo kinyume na taratibu.

 Juma Mohamedi Moja ya wananchi wa Kitongoji cha Wali akiwasilisha kero yake kwa Afisa Tarafa -Itiso  Remidius Emmanuel katika mkutano huo.
 Mwananchi wa Kitongoji cha Wali Emmanuel Panga akisoma taarifa ya Mapato na Matumizi kwa niaba ya kamati ya Maji.Taarifa ambayo hata hivyo haikupokelewa na Afisa Tarafa. 

 Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Wali walioshiriki Mkutano huo.
 Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel  akiwa na viongozi wa ngazi ya Kata, Kijiji na  Kitongoji husika

Watoa huduma kwa wateja wa TIGO wapewa zawadi katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja

$
0
0


Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Bw.Tarik Boudiaf akizungumza na watoa huduma katika hafla ya kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja iliyofanyika mapema ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Hafla hii ilifanyika jana mapema jijini Dar Es Salaam.

Mkurungezi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akizungumza na watoa huduma katika hafla ya kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja iliyofanyika mapema ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Hafla hii ilifanyika jana mapema jijini Dar Es Salaam.

Baadhi ya watoa huduma wa Tigo wakiwa makini kufuatilia hotuba ya Mkurungezi mtendaji wa Tigo Simon Karikari a hafla ya kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja iliyofanyika mapema ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Hafla hii ilifanyika jana mapema jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Tigo , Mwangaza Matotola akizungumza na a watoa huduma katika hafla ya kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja iliyofanyika mapema ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Hafla hii ilifanyika jana mapema jijini Dar Es Salaam.

Baadhi ya watoa huduma wa Tigo wakiserebuka na burudani ya muziki katika hafla ya kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja iliyofanyika mapemaikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Hafla hii ilifanyika jana mapema jijini Dar Es Salaam.
vicheko na furaha vilitawala hafla hiyooo
Mkurungezi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma katika hafla ya kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja iliyofanyika mapema ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Hafla hii ilifanyika jana mapema jijini Dar Es Salaam.

MAGUFULI: NATAMANI HAMONIZE AGOMBEE UBUNGE

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli atamani msanii mziki wa Kizazi kipya maarufu kama Bongo freva, Rajabu abdul a.k.a Hamonise  anatamani agombee katika jimbo la Tandahimba lililopo mkoani Mtwara.

Ameyasema hayo leo Oktoba 15,2019 wakati wa ziara yake mkoani wa Lindi wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi baada ya kumaliza kuhutubia.

"Na kumalizia nawapongeza sana waimbaji hawa wakinababa na mmoja alikuwa akisema sisi vijana na nilipo muona ni mzee kuliko mimi nikasema kumbe vijana wa hapa wanaumri mzuri,  lakini nampongeza sana Hamoniza (Hamonise) sijui anatoka jimbo gani? anatoka jimbo gani huyu? Tandahimba!, Mbunge wa kule ni nani? Akhaaa nilitamani kweli Hamoniza aende akagombee kule akawe Mbunge wa Tandahimba ndugu zangu Asanteni Sana Mungu awabariki Sana". Amesema Rais Magufuli

Msanii Hamonise hivi karibuni aliondoka katika Kundi la WCB lilikuwa likisimamiwa na Msanii Nasibu Abdul maarufu kama Diamond na kuanza kujitegemea mwenyewe katika kazi zake za kimziki.

YANGA KUFUANA NA PAN AFRICAN JIJINI DAR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha   Yanga kesho kinatarajia kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili kirafiki dhidi ya Pan African utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Yanga walicheza mchezo wa kwanza dhidi ya Friends Rangers kwenyw Uwanja wa Polisi Kurasini na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli amesema mchezo huo utakuwa ni muendelezo wa kujiweka sawa kwa ajili ya michezo ya Ligi kuu pamoja Mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids.

Bumbuli amesema, timu itakuwa chini ya Kocha Noel Mwandila ambaye atasimamia timu mpaka hapo Kocha Mkuu Mwinyi Zahera atakaporejea kutoka kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa.

Amesema, wachezaji waliokuwa majeruhi wameanza mazoezi isipokuwa Mohamed Issa 'Banka' ambaye bado anauguza majeruhi yake.

" Wachezaji wote waliokuwa majeruhi wameanza mazoezi isipokuwa Banka, Pauk Godfrey tayari amejumuika na wenzake na hata  Yondani  aliyeshindwa kwenda kwenye majukumu ya timu ya Taifa ameanza mazoezi jana,"amesema Bumbuli.

Yanga baada ya kumaliza mchezo wake wa Kesho, watajiandaa na safari ya kwenda Mwanza kuiwinda na michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao na Alliance na kisha kumalizia na mchezo wao dhidi ya Pyramids.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Pan Africa utachezwa majira ya saa 10 alasiri.
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live




Latest Images