Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110172 articles
Browse latest View live

SERIKALI YA AWAMU YA TANO HAITAVUMILIA UZEMBE WA AINA YEYOTE KWA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

$
0
0
Serikali imesema haitavumilia uzembe wa aina yeyote utakaofanywa na Wataalamu wa Ununuzi wa Ugavi katika kipindi hiki cha Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuelekea mapinduzi ya Uchumi wa Viwanda.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael John aliyemuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Filipo Mpango (Mb) wakati wa Mahafali 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam.

Michael John ametoa tahadhari kwa Bodi hiyo isipochukua hatua kwa uzembe wowote, Wizara ya Fedha itachukua hatua dhidi yao, amesema PSPTB inasismia sheria

"Katika hotuba yako umesema Bodi yako inaendelea kutoa miongozi na Maadili ya Kitaaluma, kusimamia mienendo na utendaji kwa Waalamu waliosajiliwa licha ya jitihada hizo bado taarifa mbalimbali za ukaguzi zinaonyesha kuwepo ununuzi holela usiozingatia utaalamu Bodi lazima iweke mikakati mipya  kukabiliana na jambo hilo,'' amesema Michael John

Hata hivyo, PSPTB imepongezwa kwa jitihada za utendaji ikiwa kuwafutia usajili na kuwafikisha mahakamani Wataalamu waliosabisha hasara kwa Taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema Taasisi kumuajiri mtu asiyesajikiwa na Bodi hiyo ni kosa  la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka miwili jela au faini ya milioni mbili au vyote kwa pamoja.

Kwa upande wake, Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Fredrick Mwakibinga amesema taaluma ya Ununuzi na Ugavi ipo kwenye majaribu kutokana na mienendo na tabia ambazo zipo kwenye Jamii kwa Wataalamu wake kutokana na kuhusiana na Fedha za Taasisi. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael John akizungumza kwenye mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo. Mkurugenzi huyo alimuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Filipo Mpango (Mb) kwenye mahafali hayo.
 Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizoma risala pamoja na kutoa neno kwa wahitumu wa Bodi hiyo wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
 Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga akitoa nasaha  kwa wahitimu wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Amani Ngonyani akisoma majina ya wahitimu wa Bodi hiyo waliofika kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Afisa mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Shamim Mdee(wa kwanza kulia) pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael John akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya Bodi wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Mwanasheria wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Suleiman Mnzava(kushoto) akiwalisha viapo vya maadili ya kazi waalamu wa Ununuzi na Ugavi walofika kwenye mahafali ya 10 ya Bodi  hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Wahitimu wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakila viapo vya kazi wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi  hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wahitimu wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael John aliyemuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Filipo Mpango (Mb) kwenye mahafali ya 10 ya Bodi  hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mahafali ya 10 ya Bodi  hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi  akimuongoza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael John kwa ajili ya kuongoza maandamano ya kitaaluma wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael John(katikati) akiongoza maandamano ya kitaaluma  ya mahafali ya 10 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi  na kushoto ni Kamishna wa Idara ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Fredrick Mwakibinga.
Wahitimu wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakifanya maadamano ya kitaaluma wakati wa mahafali ya 10 ya Bodi  hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam leo.
Picha za pamoja

WAZIRI MHAGAMA AHIMIZA VIJANA KUTUMIA MICHEZO KUIMARISHA MSHIKAMANO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana wakati wa bonanza la michezo katika wiki ya vijana lililofanyika Mkoani Lindi Oktoba 12, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mchezo wa Bao walipokuwa wakishindana Mzee Said Masteti na Abdallah Makwela. (Wa nne kulia waliokaa) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. Mchezo huo wa Bao alipenda kuucheza Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Vijana kutoka Shule ya Lindi Sekondari na angaza wakiwa uwanjani wakicheza mpira wa pete wakati wa bonanza hilo.

Mchezaji wa timu ya Sekondari ya Lindi Mwalimu Said (wenye jezi ya bluu) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Angaza wakati wa bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Lindi.


Sehemu ya vijana wakifuatailia mchezo wa mpira wa miguu utambulikao kama soka mara baada ya bonanza hilo kufunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Oktoba 12, 2019.

Baadhi ya Viongozi pamoja na wakazi wa Lindi wakifuatilia michizo ambayo ilikuwa ikiendelea katika viwanja vya Shule ya lindi sekondari.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi kombe kwa Mshindi wa Kwanza wa Mchezo wa Bao Bw. Said Masteti ambao ulikuwa Mchezo unaopendwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. (Wa tatu kutoka kulia ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewamiza vijana nchini kutumia michezo ili kuimarisha amani, upendo na mshikamano.

Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo wakati wa Bonanza la michezo kwa vijana lililofanyika katika shule ya Sekondari Lindi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana nchini kuelekea kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019 na Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo ambalo vijana walikusanyika kwa lengo la kushiriki katika michezo mbalimbali, Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa michezo imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha ushirikiano na kuwajengea vijana ari ya uzalendo.

“Kupitia michezo mnayofursa kama vijana kuendelea kuenzi falsafa za waasisi wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume ambao walikuwa wazalendo kwa taifa lao na waliimarisha muungano kwa maslahi ya watanzania wote,” alisema Mhagama

“Ni matumaini yangu kuwa kupitia michezo hii mtaendela kujikumbusha falsafa za waasisi hao kupitia michezo hii tunayoifungua leo kwa kuwa itatoa hamasa kwa vijana kupenda nchi yao na itajenga ari ya kuendeleza kuimarisha mshikamano kupitia michezo,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa michezo hiyo iliyowakutaisha vijana ikatumike kama sehemu ya kuwa na amani, uvumilivu na mshikamano.

“Vijana mnatakiwa kujenga taifa kwa vitendo vinavyodumisha amani, upendo na mshikamano kama ambavyo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyotujengea taifa lenye umoja,” alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama aliendelea kuwasihi vijana kutambua wajibu wao katika jamii na kuifanya michezo kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu wanayopaswa kuyaendeleza katika kutekeleza mipango waliyonayo.

Pamoja na hayo alirejea ujumbe wa Mwenge wa uhuru mwaka huu ambao pia umesisitiza ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa. Aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika uchaguzi ili waweze kupata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa.

Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwapongeza wadau mbalimbali na vijana walioshiriki bonanza hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Bonanza hilo la michezo limejumuisha vijana kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaendeleza vijana ili waweze kuimarika kiafya na kiakili.

Mwanariadha Kipchoge aweka historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili

$
0
0
Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili

Raia huyo wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindani la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria siku ya Jumamosi.

Haitatambulika kuwa rekodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwa kuwa halikuwa shindano la kila mtu mbali na kwamba alitumia kundi la wanariadha wa kusukuma kasi waliokuwa wakishirikiana naye na kutoka.

Bingwa huyo wa Olimpiki alikuwa ameikosa rekodi hiyo na sekunde 25 katika jaribio lake la hapo awali 2017.

Alipogundua kwamba alikuwa anakaribia kuweka historia , wanariadha waliokuwa wakidhibiti kasi ya mbio hizo walirudi nyuma na kumwacha bingwa huyo kutimka hadi katika utepe huku akishangiliwa na mashabiki wengi mji mkuu wa Austria.

Bingwa huyo mara nne wa London Marathon alimkumbatia mkewe, akachukua bendera ya Kenya na kukumbatiwa na wanaraidha waliokuwa wakimsaidia kuweka muda huo bora wakiwemo mabingwa katika mbio ndefu duniani.

Katika mitandao ya kijamii walimwengu walimpongeza kila sekunde aliyokimbia hadi kumaliza mbi hizo.



TAMTHILIA YA WILDFLOWER KUREJEA KWA KISHINDO NDANI YA STARTIMES SWAHILI

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi TV
TAMTHIlIA pendwa ya wildflower msimu wa pili inarudi tena kwa kishindo kuanzia Octoba 14 mwaka huu.

Tamthilia hiyo itarushwa moja kwa moja kupitia King'amuzi cha startimes chaneli ya ST swahili saa 4 usiku kila siku ya jumatatu hadi ijumaa.

Maudhui ya tamthilia hiyo inamzungumzia mwanadada lily cruz ambae anarejea poblacion ardiente ili kulipiza kisasi cha wazazi wake ambao ni Dante na calmia ambao waliuawa na familia ya Julia Ardiente.

"Baada ya kunusurika kifo lily akutana na mwanamke tajiri prianka baada ya kufanikiwa na kuachiwa na wauaji, prianka akamchukua lily na kumbadilisha kila kitu kuhusu yeye na kuwa na utambulisho mpya wa ivy Kama vile mtoto wake.

Baada ya miaka kumi na tatu ivy anagundua kuwa mama yake hakuuwawa,baada ya msako mkali ivy alifanikiwa kumuona mama yake, lakini mama yake anagundua kuwa ana matatizo ya kupoteza kumbukumbu ambapo ivy alifanikiwa kumchukua na kumsaidia kurudisha kumbukumbu zake.

Huku ivy alikua kijana machachari na kufanikiwa kumteka kimapenzi kijana arnado,arnado alichanganyikiwa na penzi la ivy lakini lengo la ivy lilikua ni kuanika maovu ya arnado na asiweze kuolewa nae.

TAMASHA LA 38 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

Makampuni ya simu za mkononi yanavyosaidia ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati (SMEs)

$
0
0
Tanzania imeshuhudia ukuaji mkubwa wa kuridhisha wa biashara ndogo na za kati (SMEs). Kwa mujibu wa Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), biashara ndogo na za kati zinajumuisha asilimia 95 ya biashara zote nchini Tanzania, na zinachangia asilimia 35 ya Pato la Taifa (GDP).

Pamoja na kuwa kichocheo kikubwa cha kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi, SMEs inajimuisha mashirika kutoka sekta mbalimbali za uchumi kama vile kilimo, usafirishaji na biashara.

Kwa pamoja mashirika/kampuni hizi zimesaidia kuleta mabadiliko chanya katika uchumi wa Tanzania kwa kuzalisha ajira, kukuza ubunifu, kutoa huduma na bidhaa kwa watu wa kipato cha chini, pamoja na kuchukua nafasi kubwa katika kuwajumuisha wanawake, na vijana katika uchumi. Ni wazi kuwa SMEs itaisaidia Tanzania kwa kiwango kikubwa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, bado SMEs zinakumbana na changamoto mbalimbali katika ukuaji wake. Miongoni mwa changamoto kubwa zinazozikumba biashara hizi ni pamoja na ugumu wa kupata huduma za kifedha, pamoja na kukosekana kwa huduma ya intaneti iliyo imara yay a kuaminiwa.

Lakini, sekta binafsi bado imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa ufumbuzi wa changamoto hizo unapatikana. Kampuni ya Tigo Tanzania ni moja ya mifano ambayo imekuwa ikijishughulisha kuwakikisha inaboresha mazingira ya kibiashara ili kuhakikisha kuwa zinazidi kukua kila iitwapo leo.

Hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kuzinduliwa kwa huduma ya intaneti ya ofisi, huduma ambayo imeletwa madhubuti kuhakikisha inaboresha upatikanaji wa inatenti katika SMEs. Huduma hiyo inatoa uwezo wa vifaa hadi 32 kwa wakati mmoja ambapo vifaa hivyo vitaweza kupata intaneti yenye kasi ya 4G+, na kuweza kutumia programu mbalimbali kupitia Microsoft 365.

Mbali na hilo, wamiliki wa biashara ndogo na za kati wanaweza kupata faida nyingine kwa kuwa mawakala wa huduma ya Tigo-Pesa. Kwa kufanya hivyo zitakuwa zinarahisisha ufanyaji wa biashara kwa kuungana na makampuni zaidi ya 70,000 ambayo yanakubali malipo kwa njia ya simu, pamoja na kulipa ankara mbalimbali kupitia huduma ya Tigo Pesa Wallet.

Kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo zinakumba biashara hizi, Tigo inasaidia kuongeza uzalishaji wan chi, pamoja na kutoa fursa za kiuchumi kwa idadi kubwa sana ya Watanzania.

TUZO YA AMANI YA NOBEL YA DKT. ABIY AHMED KATIKA TASWIRA YA AUNG SAN SUU KYI WA BURMA

$
0
0
Ijumaa tarehe 11/10/2019 ilikuwa ni siku yenye furaha kwa waethiopia na waafrika kwa ujumla kufuatia ushindi wa tuzo ya Amani ya Nobel aliyopata Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed.

Tangu ameingia madarakani mwezi Aprili, 2018, ndani ya miezi sita Dkt. Abiy Ahmed alifanikiwa kuanzisha makubaliano ya amani na Eritrea, alitia saini kuachiwa kwa wafungwa mbalimbali waliofungwa kisiasa na kuomba radhi kwa umma  kwa ukatili uliokuwa ukifanywa na serikali ya Ethiopia hapo awali.

Mbali na hayo aliruhusu kurejea nyumbani kwa makundi mbalimbali ya waasi ambayo yalikuwa yakitambulika kama makundi ya kigaidi likiwemo kundi kubwa la waasi la Ginbot 7 lililokuwa limejificha Kusini mwa nchi hiyo.

Na hatimaye tarehe 9 Julai, 2018 Dkt. Abiy Ahmed na mwenzake Isias Afwerki wa Eritrea walitiliana saini mkataba wa kumaliza vita vya kugombea mpaka wa eneo la Kusini mwa nchi hiyo la Badme vilivyodumu kwa miaka 20 kuanzia miaka ya 1998-2000 mpaka 2018 mkataba ambao ulianza kutekelezwa rasmi mwezi Septemba, 2018.

Dkt. Abiy ameshiriki pia katika usuluhishi wa migogoro nchini Sudani na Sudani Kusini ingawa kushiriki kwake kunaonekana kama kunatokana ushawishi kutoka kwa mataifa ya Magharibi.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Mengitsu Derg mwezi May mwaka 1991 Ethiopia imekuwa ikihangaika sana kurejesha Umoja wa Kitaifa.

Chama kinachotawala nchini Ethiopia cha Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF) ambacho ni muunganiko wa vyama vinne vya makabila ya Oromo, Ahmara, Tigri na wale wa kusini (OPDO, ANDM, TPLF na SEPDM)  kimekuwa na changamoto za kiuongozi kutokana na mgawanyiko wa makabila nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa indexmundi ni kwama kabila la Oromo ndilo lenye idadi kubwa ya watu katika nchi ya Ethiopia likiwa na asilimia 34.4%-36% ya idadi yote ya watu huku kabila la Ahmara likifuatia kwa asilimia 27%.

Makabila kama wasomali lina asilimia 6.2% ya idadi ya watu huku watigray (Tigrinya) wakiwa asilimia 6.1% na Sidama 4%.

Makabila yaliyobaki ambayo yanapatikana zaidi sehemu za Kusini mwa Ethiopia yana idadi ya watu chini wa asilimia mbili; Gurage (2.5%), Welaita (2.3%), Hadiya (1.7%), Afar (1.7%), Gamo (1.5%), Gedeo (1.3), Silte (1.3%), Kefficho (1.2%) na makabila mengine madogo zaidi yakijenga asilimia 8.8% ya watu wote.

Kutokana na mgawanyiko huo wa kimakabila na kisiasa ndani ya chama cha EPRDF ni wazi kuwa tuzo hii inaweza kuwa mwiba kwa baadhi ya wapinzani wake kisiasa na makabila kinzani.

Je ni nini anapaswa kufanya?

Dkt. Abiy Ahmed ana kazi kubwa ya kuitisha mjadala wa maridhiano ya kitaifa yatakayopelekea kuundwa kwa kamisheni ya ukweli ya kudumu na maridhiano ya kitaifa (NTRC)

Pili, ni muhimu kwake kuendelea kufanya mabadiliko katika serikali  yake kujumuisha makundi yote ya jamii yaliyoonekana kutengwa katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini humo.

Kufanya haya ni muhimu kwake ili asije kujikuta anaingia kwenye kivuli cha kiongozi wa Myanmar au Burma bi Aung San Suu Kyi ambaye alishinda tuzo ya  Amani ya Nobel mwaka 1991 kwa harakati za kudai demokrasia na haki za binadamu  zisizoambatana na vurugu nchini Myanmar.

Lakini mara baada ya kufanikiwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo bi Aung San Suu Kyi alijikuta katika shinikizo la jamii ya kimataifa kufuatia mauaji ya watu zaidi ya elfu kumi wa jamii ya Rohingya kutoka jimbo la Rakhine huku wengine zaidi ya laki saba wakikimbilia nchi jirani ya Bangladesh.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) liliunda Tume Huru ya Kuchunguza Mauaji hayo (Fact Finding Mission) iliyoongozwa na Marzuki Darusman wa Indonesia ambayo ilitoa taarifa yake mwezi Septemba, 2018 na kushauri  viongozi watano wa juu wa jeshi (Tatmadaw) la Myanmar akiwemo Amiri Jeshi Mkuu Jenerali Mkuu Min Aung Hlaing na wenzake  walitakiwa kushitakiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari kwa mujibu wa Mkataba wa Rome wa mwaka 1998.

Ingawa ripoti ile haikumtaja bi Aung San Suu Kyi, mtu aliyekuwa akipigiwa chapuo sana na Marekani lakini bado jamii ya kimataifa iliendelea kumuhusisha na mauaji yale akiwemo Askofu Desmond Tutu aliyemshauri kuirejesha tuzo ile kwa kuwa nikono yake ilijaa damu ya warohingya.

Lakini mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya Amani ya Nobel Berit Reiss-Andersen alimtetea bi Kyi kuwa tuzo yake haihusiani na mauaji ya kimbari ya 2017 kwa sababu aliipata mwaka 1991 kwa harakati za kudai demokrasia na haki za binadamu.

Haitapendeza kuona Dkt. Abiy Ahmed akiingia katika kivuli hiki ikiwa anaweza kujenga jamii inayopendana na kuheshimiana kwa misingi ya udugu na umoja wa kitaifa na si kama makabila ya Ethiopia.

Abbas Mwalimu (Facebook, Instagram & YouTube)

+255 719 258 484

Uwanja wa Diplomasia (Facebook & WhatsApp)

OKTOBA 13, SIKU YA KUPUNGUZA MAAFA DUNIANI, BILIONI 30 ZATUMIKA KUREJESHA HALI MKOANI KAGERA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV.
Oktoba 13 kila Mwaka Dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa ambayo husababishwa na majanga mbalimbali na kupelekea athari vikiwemo vifo katika jamii husika.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora, wakati akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ameeleza kuwa kwa kipindi cha takribani miaka mitatu iliyopita Mkoa wa Kagera umekuwa ukipitia katika majanga tofauti likiwemo Tetemeko, Mvua, Radi, moto, yaliyopelekea maafa makubwa, ambapo athari zake ni pamoja Vifo, uharibifu wa miundo mbinu, majengo n.k.

Profesa Kamuzora ameongeza kuwa Kufuatia maafa hayo Serikali imekuwa ikijitahidi kurejesha hali ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 30 zimekwisha tumika Kwa kukarabati majengo ya Taasisi, Ujenzi wa Shule Mpya, miundo mbinu ya Barabara na huku elimu ikizidi kutolewa zaidi namna ya kukabiliana na maafa pindi yanapojitokeza, na tayari ipo kamati ya maafa inayohusisha Serikali, Taasisi binafsi na watu binafsi, ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo ndiyo inasimamia Urejeshaji wa hali kwa kusimamia ujenzi bora wa majengo

Kauli mbiu ya Siku hii Mwaka huu ni, "Chukua hatua endelevu kuounguza uharibifu wa maafa katika miundo mbinu muhimu na huduma za msingi ikiwemo afya na elimu, pamoja na kuimarisha ustahimilivu wake ifikapo 2030" wakati Kitaifa Siku hii inaadhimishwa katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA JENGO LA SHULE YA SEKONDARI YA LINDI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi  wa jengo la Shule ya Sekondari ya Lindi, Oktoba 12, 2019.  Wa nne kulia ni Mkuu wa  Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Wa tatu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge na wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwapungia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi wakati alipowasili shuleni hapo kukagu ujenzi wa jengo la shule hiyo, Oktoba 12, 2019.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhamaga (wa pili kulia), Waziri wa Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Karume  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wa pili kushoto)  wakati alipokagua maandalizi ya Uwanja wa Michezo wa Ilulu wa mjini Lindi kwa ajili ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa  Uhuru, Oktoba 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI KIGWANGALLA AZUNGUMZA AFANYA MIKUTANO YA HADHARA NZEGA VIJIJINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Budushi, Nzega Vijijini mara baada ya kufika shuleni hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kuhamasisha maendeleo, kuzungumza na wananchi na kutatua kero zao katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Nzega Vijijini.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Budushi katika jimbo la Nzega Vijijini alipofanya mkutano wa kuimarisha Chama na kutatua kero za wananchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na viongozi wengine wa CCM kutoka katika Kata mbalimbali za jimbo la Nzega Vijijini wakitazama Kadi za wanachama 100 wa CHADEMA waliohamia CCM kufuatia kuridhishwa na Utendaji Kazi wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Kata ya Ndala, Nzega Vijijini.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimpokea na kumkaribisha katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Lucas Kitambi Maselele, Mwenyekiti Mstaafu na Katibu wa CHADEMA jimbo la Nzega vijijini mara baada ya kujiunga rasmi na CCM.

HAZINA SACCOS KUWEKEZA MRADI WA BILIONI 52 DODOMA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos kimeazimia kujenga kitega uchumi cha kisasa kwa gharamaya  Shilingi bilioni 52 kupitia mradi wa Njedengwa katika Jiji la Dodoma ili kukuza uchumi wa mkoa wa Dodoma na Taifa kwa kupitia kodi.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho cha Ushirika Bw. Aliko Mwaiteleke  wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka  uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hazina,  na kuongeza kuwa mradi huo upo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake.

Mwaiteleke alisema mpaka sasa upembuzi yakinifu wa mradi huo utakaojengwa kwa njia ya ubia kati ya Hazina Saccos na mwekezaji kwenye neo lenye ukubwa wa ekari 22  kupitia utaratibu wa Jenga, Endesha na Hamisha (Build, Operate and Transfer - BOT) ambapo mwekezaji atagharamia ujenzi wote na kuendesha kwa muda ambao utakubaliwa ndani ya mkataba.

Alisema mradi huo unasimamiwa na Kamati ya watu Saba wakiongozwa na Profesa Esta Eshengoma kutoka Chuo Kiuu Cha Dar es Salaam na wajumbe wake kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),  Bodi ya Manunuzi ya Umma (PSPTB), Kituo Cha Uwekezaji (TIC), na Chuo Kikuu cha Ardhi ambao kwa sasa wanafanya kazi ya kusaka mwekezaji ili kufanikisha mradi huo.

Bw. Mwaiteleke alifafanua kuwa Mradi wa Njedengwa upo mbioni kuanza  na unategemewa kuwa chachu ya maendeleo ya chama hicho kwa kukiingizia kipato kutokana na shughuli zitakazokuwa zikifanyika kupitia mradi huo.

Alifafanua kuwa  mradi huo utahusisha ujenzi wa hoteli ya kisasa, kumbi za  mikutano, majengo ya Ofisi,  Viwanja vya Michezo na bwawa maalum la kuogelea.

Aidha alisema Chama hicho cha Hazina Saccos ambacho kina wanachama 5,600 kina mtaji mtaji wenye thamani ya shilingi bilioni 10 ikiwa ni fedha taslimu na mali wanazozimiliki ikiwemo ardhi ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa wanachama..

"Mwaka jana pekee kupitia akiba na mikopo  tulipata faida ya shilingi milioni 64 na kila mwanachama alipewa gawio la asilimia 20 kulingana na hisa zake"alisema Mwaiteleke.

Alisema faida nyingine waliyopata kupitia Hazina Saccoss ni kununua viwanja 150 katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani na kuwakopesha wanachama wao kwa bei nafuu ambapo wanalipa kidogo kidogo kwa miezi 60.

"Pia Dodoma tumenunua viwanja 897 katika maeneo ya Ihumwa Ngaloni, Iyumbu  (maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambavyo tumevigawa kwa wananchi na viwanja vya Nzuguni tutaanza kuvigawa baada ya taratibu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kukamilika ili kuwawezesha wanachama wetu waliohamia Dodoma kupata maeneo ya kujenga makazi yao” alisema Bw. Mwaiteleke

Naye Meneja wa Hazina Saccos Bw. Festo Mwaipaja, alisema Saccoss hiyo sio ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha peke yake bali watumishi wote wa serikali wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho isipokua vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo ni jeshi, Polisi, na Usalama wa  Taifa.

Alisema kwa mtumishi wa umma kujiunga na chama hicho cha ushirika mbali na kuwa muajiriwa pia atapaswa kulipa kingilio cha shilingi 20,000 na kununua hisa kuanzia 20 ambazo kila hisa moja ni shilingi 10,000 na kufanya thamani ya hisa zote kuwa shilingi 200,000.

Aidha alisema kuna mchango wa shilingi 20,000 kila mwezi na kuwataka watumishi wa umma kutoka taasisi na idara zote za serikali kuchangamkia fursa ya kujiunga na ushirika huo ili kujiinua kiuchumi

Kuhusu viwanja, Bw. Mwaipaja alieleza kuwa Chama hicho kimetumia zaidi ya shilingi bilioni 4 kununua viwanja katika Jiji la Dodoma na kuchangia eneo hilo kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha kwa wenyeji na kwamba hayo ni mafanikio yanayoihusu jamii.

Akifungua Mkutano Mkuu huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga, ameipongeza Hazina Saccos kwa kuwapatia viwanja wanachama wake na kuwataka wanachama waliopata fursa ya kupata viwanja hivyo waviendeleze haraka ili kuodokana na changamoto ya malazi kwa kuwa baadhi walipata viwanja hivyo tangu mwaka uliopita, 2018.

Aidha, ameipata kongole Hazina Saccos kwa hatua waliyofikia ya kutafuta mwekezaji katika mradi wa Njedengwa ambao utaongeza mapato ya Ushirika na kuwataka viongozi na wanachama kuhakikisha wanazingatia taratibu Sheria na Kanuni ili kufanikisha mradi huo muhimu.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga, akizungumza jambo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos leo jijini Dar es Salaam,ambapo amekipongeza chama hicho kwa kuwapatia viwanja wanachama wake na kuwataka waliopata viwanja hivyo waviendeleze. 

 Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos,Bw. Aliko Mwaiteleke akifafanua jambo mbele ya Wanachama  waliohudhuria mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hazina, leo jijini Dar es Salaam. 
  Meneja wa Hazina Saccos Bw. Festo Mwaipaja akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya majukumu ya Saccos hiyo kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa Mkutano huo uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga (hayupo pichani). 
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga wa nne kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya bodi ya Hazina Saccos baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Chama hicho cha Ushirika jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Shirika lisilo la kiserikali la CSI latoa elimu kwa wanafunzi kwenye maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI LINDI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU NA KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege aina ya Bombadier ya ATCL alipowasili Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Mji wa Mikindani waliokuwa wakisherehekea Siku ya Mikindani katika tamasha kubwa la utamnaduni la Urithi wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Uwanja wa hedge wa Mtwara Bw. Jackson Elia baada ya kushuka kutoka katika ndege aina ya Bombadier ya ATCL mara tu alipowasili tayari kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakwanwa mara baada ya kushuka kutoka katika ndege aina ya Bombadier ya ATCL alipowasili tayari kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mnazi Mmoja akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria kwenye sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere PICHA NA IKULU

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SMZ PEMBA AKIWA KATIKA ZIARA YAKE

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Watendaji wa SMZ Kisiwani Pemba katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Pemba, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe.Haji Omar Kheri.mkutano huo umefanyika leo wakati wa ziara yake Kisiwani Pemba.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Watendaji wa SMZ Kisiwani Pemba wakati wa ziara yake, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Pemba, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Issa Haji Gavu, Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein na Mshauri wa Rais Pemba.Mhe. Maua Abeid Daftari.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe.Haji Omar Kheri, akizungumza wakati wa Mkutano na Watendaji wa Wizara za SMZ Kisiwani Pemba uliofanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makoyo Wawi Pemba.
 WAZIRI wa Nchi Ofisa ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu, akizungumza na Watendaji wa Wizara za SMZ Kisiwani Pemba kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Pemba.
 MAAFISA wa Vyombo vya Usalama Kisiwani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wake na Watendaji wa SMZ uliofanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makoyo Wawi Pemba.(Picha na Ikulu) 
 MAAFISA Wadhamini na Watendaji wa SMZ wakimsikiliza Rais wa Zanzibar nac Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makoyo Wawi Pemba

WAKAZI KING'AZI HUKO KISARAWE WAKO HATARINI KUKOSA HAKI YA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA ORODHA LA KUPIGIA KURA-NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
WAKAZI wa Kitongoji cha King'azi A wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wako hatarini kukosa haki yao ya msingi ya kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Mitaa ,Vijiji na Vitongoji Novemba 24 mwaka huu ":,ambapo waliojiandikisha hadi sasa ni wanne kati ya 560 wanaotarajiwa kujiandikisha .

Hatihati hiyo inahofiwa kuchukua nafasi baada ya baadhi ya watu kuwadanganya kuwa wanapaswa kujiandikisha kupitia wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam jambo ambalo si la kweli.

Hali hiyo ilibainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye mkoa huo.

Akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo alifika kwenye kituo hicho na kukuta wananchi waliojiandikisha ni wanne tu kati ya 560 wakidai kuwa wao watajiandikisha kitongoji cha King'azi B ambacho kipo upande wa Ubungo.

Alisema baada ya viongozi wa mikoa hiyo na wataalamu mbalimbali waliridhia vitongoji hivyo kugawanywa ambapo walikubaliana King'azi A itabaki mkoa wa Pwani na Kingazi B na sehemu kidogo ni Ubungo Jijini Dar es Salaam.

"Awali kulikuwa na mgogoro lakini Wizara ya  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (TAMISEMI) walipitisha mipaka na kugawanya maeneo hayo lakini baadhi ya wananchi wanasema kuwa mitaa yote iko eneo la wilaya ya Ubungo lakini King'azi A ni Kisarawe na King'azi B ni Wilaya ya Ubungo", alisema Ndikilo.

" Nimesikia kuna mtu anaitwa magodoro ndiyo anayepotosha wananchi wakajiandikishie Ubungo jambo ambalo si kweli na endapo ataendelea kuwapotosha wananchi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwani ni kinyume cha sheria kuvuruga uchaguzi,"alisema Ndikilo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alisema kuwa tayari suala la mipaka ya wilaya ya Kisarawe na Ubungo iliwekwa na wananchi walielezwa.

Akiwa wilayani Mkuranga Ndikilo aliwapongeza viongozi wa wilaya hiyo ambapo hadi juzi walikuwa wameandikisha wananchi 70,000 kati ya wananchi 84,000 wanaotarajiwa kiandikishwa tofauti na wilaya nyingine ambazo zilikuwa bado zina wananchi wachache waliojiandikisha.

WAKANDARASI MIRADI YA MAJI MTWARA WATAKIWA KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI

$
0
0
Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji kwenye Wilaya za Newala, Tandahimba na Masasi, Mkoani Mtwara wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili ikamilike mapema hasa ikizingatiwa mahitaji muhimu ya kukamilisha miradi hiyo yamekamilika.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ametoa agizo hilo Oktoba 12, 2019 Mkoani Mtwara kwa nyakati tofauti alipofanya ziara kwenye miradi ya maji inayotekelezwa kwenye wilaya hizo.

Naibu Katibu Mkuu Sanga alitembelea mradi wa Mkwiti uliyopo Wilaya ya Tandahimba, Chanzo cha Maji cha Mitema, Mradi wa Makonde na aMradi wa Kilidu yote ya Wilaya ya Newala na mradi wa Chipingo Wilayani Masasi.

Mara baada ya kuzungukia miradi, Mhandisi Sanga alisema hajaridhika na kasi ya utekelezaji wake licha ya kwamba vifaa vinavyohitajika kukamilisha miradi hiyo ikiwemo mabomba na mitambo ya kusukuma maji vikiwa vimekamilika.

Alisema haoni sababu kwanini miradi inatekelezwa kwa kusuasua licha ya kuwa vifaa muhimu vipo eneo la mradi. "Nimezungukia maeneo ya miradi nimeona vifaa muhimu vinavyohitajika kukamilisha miradi vipo, hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda," alisisitiza Mhandisi Sanga.

Alisema kinachotakiwa ni wananchi kupata maji mapema iwezekanavyo na kwamba suala la kupoteza muda halitokubalika hasa ikizingatiwa maeneo inapotekelezwa miradi yanasumbuliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Aliagiza wasimamizi wa miradi ambayo ipo katika hatua ya ulazaji bomba kuharakisha kumaliza shughuli hiyo hasa ikizingatiwa msimu wa mvua umefika na kwamba mitaro hiyo ikiendelea kubaki wazi itajifukia na italazimika kuchimbwa upya.

"Nimeona mitaro imechimbwa na imekamilika na mabomba yapo hakikisheni kuanzia sasa mabomba yanalazwa ili kuepusha gharama ya kufanya kazi mara mbili ya kuchimba mitaro ya maji," aliagiza Naibu Katibu Mkuu Sanga.

Mhandisi Sanga aliagiza wasimamizi wa miradi kuhakikisha kwenye kutekeleza miradi wanaanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili wananchi waanze kupata huduma na baadaye waendelee na maeneo mengine wakati ambao tayari wananchi wanakuwa na huduma.

“Mnatakiwa kuwa wabunifu wakati wa ujenzi wa miradi, mnapaswa kuanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili kwanza wananchi wapate huduma na huku mkiendelea kutekeleza maeneo mengine,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa Mkoani humo ili kujionea hatua ya utekelezaji wake sambamba na kufahamu changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) alipotembelea mradi wa maji wa Mkwiti, Wilayani Tandahimba. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Mandisi Rejea Ng’ondya.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua mitambo ya kusukuma maji kwenye kituo cha Mtongwele ambacho kitatumiwa kupelekea maji kwenye mradi wa Mkwiti kutokea chanzo cha Mitema (Mitema Well Field). Kulia ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akielekeza jambo wakati wa ziara yake kwenye mradi wa maji wa Kilidu, Halmashauri ya Mji wa Newala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akikagua mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata wa Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara unaotumia maji kutoka Mto Ruvuma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akielekeza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata unaotekelezwa Wilayani Masasi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua mradi wa maji wa Makonde Wilayani Newala ambapo pia ni eneo kilipo chanzo cha maji cha Mitema (Mitema Well Field) ambacho kitatumika kwa ajili ya miradi ya Mkwiti, Makonde na Kilidu.

RC MNYETI AAGIZA WALIONYANG'ANYWA ARDHI KITETO WAPEWE MAENEO MENGINE

$
0
0
 MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti ameagiza wakazi wawili wa Wilaya ya Kiteto walionyang'anywa maeneo yao na kujengwa  taasisi za Serikali wapewe maeneo mengine. 

Mnyeti alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa kata za Matui na Bwawani, wilayani Kiteto kwenye ziara yake ya siku tano ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero na changamoto za wananchi, kuyapatia majawabu na kuzungumza na wananchi. 

Alisema kutokana na maeneo ya wananchi hao kuchukuliwa na taasisi za serikali na kujengwa shule ingetakiwa wapewe maeneo mengine ili kufidia maeneo yao. 

"Mkurugenzi nakuagiza utoe maeneo mengine wapewe hawa wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa ajili ya kufidiwa kwani japo ni suala la maendeleo lakini wanapaswa kupata haki zao. 

Alisema baadhi ya kero ambazo hazina sababu ya kuachwa zinapaswa kutatuliwa kwani wananchi wengine wataichukia serikali yao bila sababu ya msingi. 

Awali, mkazi wa kijiji cha Matui Juma Masare alilalamikiwa kuporwa eneo lake ekari 12 na serikali ya kijiji kisha ikajengwa shule ya msingi. 

"Baada ya kupora eneo langu serikali ya kijiji ilijengwa shule lakini hawakunifidia sehemu nyingine japokuwa maeneo mengine yapo," alisema Masare. 

Kwa upande wake, mkazi wa kijiji cha Wezamtima kata ya Bwawani, Endeni Kilangi alitoa malalamiko kwa mkuu huyo wa mkoa kuwa alinyang'anywa na serikali ya kijiji hicho ekari zake 70 na kujengwa shule ya msingi. 

"Shamba hilo lilichukuliwa na serikali ya kijiji lakini sikufidiwa eneo lingine sehemu nyingine ili hali kuna maeneo mengine wangeweza kunipa haki yangu," alisema Kiangi. 

Baada ya uamuzi huo wananchi hao walimpongeza Mnyeti kwa kusimamia haki zao kwani ilikuwa ni haki yao kupatiwa maeneo mengine. 

TEKNOLOJIA MPYA YA KUZUIA WIZI WA PIKIPIKI NA VYOMBO VYA MOTO YAJA NCHINI

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Benson Security Systems na AfriTrack wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua mfumo wa kimtandao wa kudhibiti vyombo vya usafiri jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Teknolojia ambayo itakayotumia mtandao wa mawasiliano wa internet imezinduliwa na Kampuni ya Benson ya jijini Arusha ikishirikiana AfriTrack ya jijini Dar es Salaam yenye uwezo wa kuthibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto


Miqdaad Kassam ni Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Benson, amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa,kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana kwa kuwa itaonekana eneo iliyopo

“Ni teknolojia rahisi itakayodhibiti wizi wa pikipiki ambao sasa ni moja ya matatizo sugu yanayolalamikiwa na wateja wengi.Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu,”alisisitiza Kassam katika uzinduzi huo.

Salma Rothbletz ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja katika Kampuni hiyo,alisema kifaa hicho maalum hufungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja hupata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika siku yake.

Alifafanua kuwa mfumo huo hudhibiti udanganyifu wa madereva katika matumizi ya mafuta na umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki za kusafirisha abiria kufuatilia biashara yao kwa ukaribu na uhakika kwa kuwa wanaweza kujua kiasi cha mafuta kilichotumika kwa siku na hata umbali ambao pikipiki imetembea,” alifafanua.

Suhail Sheriff ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AfriTrack, amesema katika uzinduzi huo kuwa mtandao huo wa udhibiti wa vyombo vya usafiri unatumika pia katika malori na magari ya abiria na utasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa ajali za barabarani.

Amesema kuwa mfumo huo hudhibiti hali ya dereva kama yuko timamu kuendesha chombo husika na iwapo kuna dosari hutoa ishara ya tahadhari kwa dereva mwenyewe na mwenye gari kabla ya madhara yoyote, ikiwa ni pamoja na ajali, kutokea.

“Kama gari lina hitilafu za kiufundi au dereva ana tatizo lolote, mathalan la kiafya, mfumo hugundua na baada ya muda hutoa ishara ya tahadhari unaosaidia hatua za kuzuia madhara yatokanayo na hitilafu hiyo kuchukuliwa haraka,”alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Sheriff amesema kuwa vyombo vya usafiri vinapokuwa katika maeneo yasiyo na mtandao wa mawasiliano, ikiwa ni pamoja na porini na bahari kuu ambapo mawasiliano ni magumu,wanatumia mfumo wa mawasiliano wa setelaiti kufuatilia mwenendo wa vyombo hivyo katika maeneo hayo yasiyo na mtandao.

Aidha amesema kuwa mfumo huo tayari umeshaanza kwa mafanikio makubwa katika nchi za Ivory Coast, Malawi,Zambia na sasa umeingia nchini katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya

Kiure, Omar Kiure ni Mwakilishi wa Kampuni ya Uhandisi ya amesema katika uzinduzi huo kuwa mfumo huo wa udhibiri magari na madereva katika sekta ya usafirishaji ni ukombozi kutokana na kukithiri kwa wizi hasa wa mafuta unaosababisha hasara kubwa.

“Wizi wa mafuta katika katika sekta ya usafirishaji na ujenzi ni sehemu ya tatizo sugu na linalokera mno katika sekta ya ujenzi na kwa kweli mfumo huu utatusaidia kudhibiti wizi huu unaotutia hasara mno na kusababisha gharama kuwa juu,” alisema Kiure.

Athilyo Choga ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha amesema katika uzunduzi huo kuwa mfumo huo wa udhibiti utasaidia jeshi hilo kudhibiti na kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la ajali za barabarani

NAIBU WAZIRI WA MADINI ATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO WA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisikiliza kero za wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu katika eneo la Misigiri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida


Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kushoto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula wakijadiri jambo baada ya kuwasili kwenye eneo lenye mgogoro katika Kata ya Misigiri Wilayani Ilamba Mkoa wa Singida


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula kulia akimuelekeza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo eneo lenye mgogoro

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikakati, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula, Kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo wakijadiri jambo wakati wanaelekea eneo lenye mgogoro
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula, Kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo wakielekea eneo lenye mgogoro

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula, Kulia ni Nabii Elia ambaye ndiye anae chimba eneo hilo lenye mgogoro 

……………………

Serikali imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la wachimbaji wadogo lililopo katika Mlima wa Sakenke kata ya Misigiri Wilaya ya Iranga Mkoani Singida.

Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka 3 ni kati ya mchimbaji mdogo aliyekuwa afisa usalama wa taifa mstaafu John Lutebeka, na Nabii Elia wote wanagombea eneo hilo ambalo Lutebeka anamiliki ardhi ya juu na Elia ameliombea Leseni ya Uchimbaji Madini.

Akizungumza kwenye eneo linalogombewa, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amewataka Lutebeka, Nabii Elia na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo wafike ofisini kwake Jijini Dodoma siku ya Jumatano Oktoba 16 mwaka huu kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kila mmoja aje na vielelezo vinavyomruhusu kuchimba madini katika eneo hilo.

Aidha, Nyongo amewataka Maafisa Madini kote Nchini kutoa elimu kwa wachimbaji juu ya sheria za madini ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima maana kuna haki ya umiliki wa ardhi ya juu na kuna haki ya umiliki wa ardhi ya chini kwa maana ya leseni ya uchimbaji hawa wote wana haki sawa wanaweza wakakaa wakazungumza wakachimba pamoja.

Wakati huo huo Naibu Waziri Nyongo, amemtaka Nabii Elia aachane na uchimbaji wa madini karibu na nguzo za umeme anatakiwa awe mita 100 kutoka kwenye nguzo za umeme, vinginevyo atachukuliwa hatua.

Pia nyongo amewapongeza wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Singida kwa ulipaji mzuri wa kodi na amesema rasilimali ya madini ni ya Watanzania wote, hatuko tayari kumuoneo mtu wala hatakubari mtu achimbe amdhulumu mwingine.

“Kwenye uchimbaji kuna kelele nyingi, kuna wengine wanamiliki leseni nyingi hata kuzihudumia hawawezi, mpaka sasa tumefuta leseni elfu 13 hivyo wale wanaojua wasitumie ujuaji wao kuwadhuru wengine tutampa haki mwenye haki yake,” alisema Nyongo.

Awali Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Malembo, alisema kwa nyakati tofauti, ofisi yake imesuluhisha mgogoro huo, lakini Lutebeka huwa haridhiki na maamuzi tunayofikia ikabidi tuligawe eneo hilo leye hekari 7.2 na kumpa Lutebeka hekari 4 lakini bado hakuridhika.

Akizungumza kwa masikitiko, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Huhahuka amesema anasikitika kuingizwa kwenye mgogoro huo ambapo Afisa Usalama wa Taifa Mstaafu Lutebeka amekuwa akimtuhumu kuwa anawadhamini hao wanaotaka kuchimba eneo hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Madini Mkazi wa Singida, Malembo amesema, kati ya Julai na Oktoba 11 mwaka huu, wamekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 1.3 bilioni, Mapato hayo ni sawa na asilimia 271.94 ya lengo kwa awamu ya kwanza la kukusanya shilingi 500,000,000, na asilimia 90.65 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi 1,500, 000,000/=.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AKAGUA UJENZI WA BARABARA ZA USANGI NA UGWENO

$
0
0
Muonekano wa barabara ya Kikweni- Usangi Km 12.5 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua barabara ya Kikweni- Usangi Km 12.5 na Kikweni-Ugweno km 17 ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea wilayani Mwanga (kulia), ni meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro Eng. Nkolante Ntije.
Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua barabara ya Kikweni- Usangi Km 12.5 na Kikweni-Ugweno km 17 ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akisisitiza uendeshaji makini na mahiri wa pikipiki za bodaboda kwa vijana wa Kata ya Kifula-Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kufuatia kuanza kukamilika kwa barabara za lami katika baadhi ya maeneo yenye milima na kona kali ili kuepuka ajali.
Muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini TBA.
Viewing all 110172 articles
Browse latest View live




Latest Images