Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

ASILIMI 15 YA MAPATO YA KOROGWE MINI MARATHON KUTUMIKA KUSAIDIA WAHANGA WA MAFUKO WILAYANI KOROGWE

0
0
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kisa Gwakisa katikati kikimbia pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia wakikimbia mbio za kilomita 5 za Korogwe Mini Marathon zilizofanyika leo mjini Korogwe ,ambapo mashindano hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya hiyo yakiwa na lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuchangia maendeleo wilayani humo
Wakimbiaji wa Baiskeli wakiwa wameanza mbio zao kwenye Mashindano ya Korogwe Mini Marathon 


Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia akikimbia kilomita 5 wakati wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon leo mjini Korogwe
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akivalishwa medali na Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 5
Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon kwa upande wa wanaume aliyekimbia kilomita 10 Jumanne Ndege kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon 
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon

 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akimpongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi 
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mbio hizo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akiwa pamoja na washiriki wengine waliojitokeza kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathon kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava

NA MWANDISHI WETU, KOROGWE

ASILIMIA 15 ya mapato yanayotokana na mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kutumika kwenye kuwasaidia waathirika wa mafuriko wilayani Korogwe ambao wamekumbwa na majanga mbalimbali.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wakati wa mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yaliyofanyika mjini Korogwe na kuhudhuriwa na washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema maafa hayo ni makubwa kutokana na wamewaacha baadhi ya wananchi wakikosa makazi huku wengine wakipoteza maisha hivyo wameona watumie nafasi hiyo kuwafariji wananchi hao kwa kuwapatia kiasi hicho. 



“Ndugu zangu Korogwe tumekumbwa na maafa wenzetu wamepoteza maisha maji yamekata barabara kwa kutumia Mashindano hayo ya Korogwe Mini Marathon tutatoa asilimia 15 kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa na mvua hizo kuwapa mkono wa Pole kwa kuwa ni watanzania wenzetu”Alisema DC Kissa. 


Aidha alisema kwamba lengo kuu la mashindano hayo ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa leo ni mwaka 2019 anafikisha miaka 20 wao wana Korogwe tunatumia siku hii kwa kuenzi kwa kufanyika mashindano hayo”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Korogwe wameungana na dunia nzima kumuenzi baba wa Taifa ambayo aliwaachia watanzania demokrasia ya vyama vingi kitu ambacho kinaendeleza kwa vitendo na Rais Dkt John Magufuli.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba lengo la pili ni kuchangia miundombinu ya elimu kupitia kampeni ya Nivushe kuhakikisha wanasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sekta hiyo. 


“Lakini pia tunawashukuru Tanapa wametuchangia milioni 30, tunawashuiru marathon hii isingekamilika kama sio wadau hawa wameweza kudhamini huku mdhamini wa kwanza akiwa Tanapa, wa pili ni Gomba, wa cyclyn ...Lakini Tunawashuku pia NMB na CRDB tunategema kipindi kijacho tutakuwa na ongezeko la wadhamini “Alisema.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume waliokimbia kilomita 10 alikuwa ni Jumanne Ndege kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mkoani Arusha ambaye alikimbia dakika 30 na sekunde 7 ambaye alizawadiwa medali na kitita cha laki mbili.

Nafasi ya mshindi wa pili ilikwenda kwa Jackson Makombe ambaye alikimbia dakika 31 na sekunde 04 ambaye pia akitokea JKT Mkoani Arusha aliyepata kitita cha 140,000 huku mshindi wa tatu ikienda kwa Charles Sule ambaye alikimbia umbali wa dakika 32 na sekunde 07 ambaye pia alitokea JKt mkoani Arusha alizawadiwa kitita cha sh.80,000.

Kwa upande wa wanawake kilomita mshindi wa kwanza ilichukuliwa na Grace Jackson kutoka klabu ya JKT Mkoani Arusha ambaye alikimbia kwa kutumia dakika 35 na sekunde 51 ambaye alipata kitita cha sh.200,000,nafasi ya pili ikichukuliwa na Banuelia Bryson kutoka mkoani Kilimanjaro ambaye alikimbia dakika 41 na sekunde 16 aliyepata kitita cha sh.140,000,huku mshindi wa tatu ikichukuliwa na Pendo Pamba kutoka Klabu ya JKT ya Mkoani Arusha akikimbia kwa dakika 42 na sekunde 18 akizawadiwa kitita cha 80,000.

Hata hivyo kwa upande wa mbio za Baiskeli kilomita 30 wanaume mshindi wa kwanza aliibuka Boniface Saimoni kutoka mkoani Simiyu ambaye alikimbia dakika 49 na sekunde 59 na kupata kitita cha sh.200,000,huku mshindi wa pili ikichukuliwa na Mussa Makala aliyepata kitita cha sh.160,000,na mshindi wa tatu ikichukuliwa na Rashid Ally akizawadiwa kitita cha sh.120,000.

Kwa upande wa mbio baiskeli wanawake kilomita 20 mshindi wa kwanza ilichukuliwa na mshindi wa pili ni Anna Pimax huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo mgeni rasmi wa mashindano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi alimpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kubuni na kuanzisha mashindano hayo ambayo yamekuwa na tija kubwa. 


Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto ya mvua lakini mashindano hayo yamefana na kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi na wana michezo ambao walijotokeza kushuhudia mashindano hayo. 


“Lakini pia nipongeze kamati ya maandalizi kwa kufanikisha dhumuni hili kubwa ikiwa ni kumuenzi baba wa Taifa ambapo kesho ni kumbukizi yake lakini pia kutumia fursa hiyo kuhamamsisha wananchi kuajiandikisha”Alisema

Mwisho.

MDORI FC MABINGWA MICHUANO CHEMCHEM CUP 2019 WAPATA MILIONI 1.7 NA KIKOMBE

0
0
 Nahodha wa Mdori Fc Hassan Sharifu akipokea kombe la ubingwa kutoka kwa Spika wa la hifadhi ya jamii ya wanyamapori burungev Marcelo Yeno baada ya kutwaa ubingwa chemchemnCup 2019
 Mratibu miradi ya jamii ya Chemchem association, Walter Pallangyo  akizungumzia michuano hiyo.
 Mashabiki wakifuatilia mtanange wa fainali kati ya Mdori FC na Majengo FC


Mwandishi wetu, Babati.

Babati. Timu ya soka ya Mdori FC, juzi imetwaa ubingwa wa michuano ya chemchem CUP mwaka 2019, iliyokuwa na lengo la kupiga vita ujangili na kuendeleza utalii, baada ya kushinda kwa penati 4-3 dhidi ya timu ya Majengo FC katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Mdori wilayani Babati.

Katika mchezo huo wa fainali, ambao ulikuwa umevuta maelfu ya watu, timu hizo zilitoka sale kwa kufungana goli 1-1 kwa dakika 90 na ndipo bingwa akapatikana kwa mikwaju ya penati, Manyara ndio walikuwa wa kwanza kupata gori dakika ya 57 kupitia kwa Andason Agustin na Mdoro walisawazisha dk 87 kupitia Rajabu Said

Baada ya fainali hiyo, Mdori walikabidhiwa kikombe chenye thamani ya zaidi ya sh 1.5 milioni na fedha taslimu sh 1.7 milioni na Spika wa hifadhi ya jamii ya Burunge, Marceli Yeno ambapo washindi wa pili walipewa zawadi ya fedha taslimu 1.1 milioni na kikombe zawadi zote zilizotolewa na mwekezaji wa Chemchem.

Washindi wa tatu wa michuano hiyo, timu ya Kisangaji ilipewa zawadi wa sh 650,000 na washindi wa nne timu ya Sangaiwe ilipata zawadi ya sh 300,000 na upande wa timu za mpira wa pete mabingwa walikuwa Mdori waliopewa zawadi ya sh 250,000 ,wa pili Mbuyuni 150,000 na timu ya tatu walimu 100,000.

Akizungumza baada ya michuano hiyo, Mratibu wa miradi ya jamii ya taasisi ya Chemchem Association ambayo, imewekeza hoteli na utalii wa picha katika eneo hilo,Walter Pallangyo alisema lengo la taasisi yao kudhamini mashindano hayo ni kuhamaisha vijana kupenda uhifadhi, kupiga vita ujangili na kuendeleza utalii.

"tunaamini Chemchem kama wawekezaji katika eneo hilo, michezo hii inasaidia pia kuwakutanisha vijana na kutambua vipaji vyao na baadhi wamekuwa wakipata fursa ya kuchaguliwa timu za nyingine nchini"alisema

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Babati,Ramadhani Mnyoti alipongeza michuano hiyo, kwa kueleza imekuwa ikiibua vijaji lakini pia kusaidia kukuza utalii na kupiga vita ujangili kupitia michezo.

Michuano ya Chemchem CUP ambayo, ilikuwa inashirikisha timu 20 kutoka vijiji vinavyozunguka hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge,lengo lake ni kupiga vita ujangili, kuendeleza uhifadhi na Utalii katika eneo hilo.

Watalii kutoka Israel wawasili nchini kwa ziara ya siku nane.

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi akiwakaribisha watalii kutoka nchini Israel mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ndege ya shirika la El Al Israel, leo tarehe 12 Oktoba 2019.Watalii wapatao 920 wameendelea kuwasili nchini katika makundi tofauti ambapo Watalii wanaowasili kupitia uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro wanatarajiwa kufika 720 na Watalii 200 kwa wale waliokwishawasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar. 
Sehemu ya Watalii kutoka nchini Israel wakipata huduma mara baada ya kuwasili ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.Wakiwa nchini watalii hao watatembelea hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Manyara pamoja na Zanzibar ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali ya mila na utamaduni wa kitanzania. 
Sehemu nyingine ya Watalii kutoka nchini Israel wakipata huduma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. 
Kikundi cha ngoma cha Wamasai kikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kuwalaki wageni hao. 

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WANA WAJIBU WA KUSIMAMIA UTENDAJI SEKTA YA ARDHI-DKT MABULA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya Majalada katika ofisi za Ardhi Jiji la Mawanza jana akiwa katika ziara yake ya kuangalia utendaji kazi sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa ndani ya kivuko kipya cha Kayenze- Baze kinachotarajiwa kuanza majaribio mwezi Novemba 2019 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho jijini Mwanza jana.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha Kayenze- Baze jijini Mwanza kutoka kwa Meneja wa Masuala ya fedha wa Kampuni ya Songoro inayojenga kivuko hicho wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho jijini Mwanza jana.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika kivuko kipya cha Kayenze- Baze jijini Mwanza ambacho kinatarajiwa kuanza majaribio Novemba 2019 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho jijini Mwanza jana.

…………………


Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuelewa kuwa pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi kuhamishiwa Wizara ya Ardhi lakini bado wana jukumu la kusimamia utendaji wa sekta hiyo.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika halmashauri ya jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela akiwa katika ziara ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara na Geita.

Alisema, tangu watumishi wa sekta ya ardhi walivyohamishiwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakurugenzi wengi wa halmashauri wameona kama wamejivua kusimamia utendaji wa watumishi wa sekta hiyo jambo alilolieleza kuwa siyo sahihi kwa kuwa mamlaka ya upangaji Majiji, Miji na Manispaa unabaki kwa halmashauri.

‘’kazi pekee inayosimamiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa watumishi wa sekta ya ardhi ni katika masuala ya nidhamu na ajira ambapo katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi anawajibika’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema katika kuboresha sekta ya ardhi nchini huduma za sekta hiyo sasa zimesogezwa katika mikoa badala ya kutegemea ofisi za Kanda alizozieleza kuwa ziko mbali kwa baadhi ya mikoa jambo linalowafanya wananchi kushindwa kupata huduma kwa urahisi.

Katika kufanikisha hilo Dkt Mabula aliwataka Wakuu wa mikoa kuharakisha uanzishwaji ofisi za mikoa kwa kutenga ofisi ili wananchi waweze kupata huduma za ardhi bila usumbufu ambapo alitolea mfano wa mikoa ya Tanga, Ruvuma, Mtwara na Simiyu kuwa tayari ishatenga ofisi kwa ajili ya mikoa yake.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alisema mkakati wa ofisi yake kwa mwaka huu ni kuhakikisha uanzishaji ofisi za mikoa usaidie kupunguza changamoto za sekta ya ardhi katika mikoa mbalimbali.

Akiwa katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Dkt Mabula lielezwa na Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi katika halmashauri hiyo Shukurani Kyando kuwa, halmashauri hiyo imekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji hati, urasimishaji na upimaji maeneo mbalimbali ingawa imekuwa na changamoto kubwa ya utapeli unaofanywa na madali kwa kuuza kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.

Hata hivyo, alisema katika kukabiliana na utapeli huo tayari wamewakama matapeli saba na baadhi yao tayari wamefikishwa katika vyombo vya sheria huku mmoja akikabidhiwa kwa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (Takukuru) na kuwataka wananchi wanaotaka kununua viwanja kuhakikisha wanajiridhisha katika ofisi za ardhi ama ofisi za ardhi za kanda ili kuepuka kutapelewa.

Vodacom Yadhamini Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ZATI, Zanzibar

0
0
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo (kulia) akipokea Router ya Vodacom toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda Vodacom Tanzania, Aileen Meena mjini Zanzibar juzi kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Zanzibar Association of Tourism Investors ZATI. Anayeshuhudia ni Akaunti Meneja wa Vodacom Zanzibar, Faraji Mkumbi.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda Vodacom Tanzania, Aileen Meena akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa ZATI Mjini Zanzibar juzi, Vodacom ndio mdhamini mkuu wa mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda Vodacom Tanzania, Aileen Meena akimkabidhi laini ya Vodacom kwa Waziri wa Habari na mambo ya kale wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa ZATI.
Mfanyakazi wa Vodacom Zanzibar, Fahad (mwenye kofia) akimuelezea jambo Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo.
Wadau wa Utalii

RC MAKONDA AELEKEZA MADUKA YOTE DAR KUFUNGULIWA KESHO SAA TANO ASUBUHI ILI KUTOA NAFASI KWA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA.

0
0
Ikiwa Imesalia siku moja kabla ya kufungwa kwa zoezi la kuandikisha wananchi kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura kwajili ya Kuchagua viongozi wa ngazi ya Mtaa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo amewaelekeza wenye maduka kufungua maduka yao Kesho October 14 kuanzia saa tano ili kutoa nafasi kwa wananchi kwenda kujiandikisha.

RC Makonda amesema kwakuwa kesho ni Siku ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameona ni vyema Wananchi wote wakamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha wanapata Nafasi ya Kutosha ya Kujiandikisha ili waweze kuchagua Viongozi wa mitaa wanaoweza kutatua matatizo yao.

Aidha RC Makonda amewasihi Wamachinga, Bodaboda, Makondakta, madereva, Viongozi wa Taasisi, wafanyakazi wa Bar, Saloon, wamiliki na wafanyakazi wa Sehemu za Starehe kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa, Shule za Msingi,  sekondari na sehemu zilizowekwa mahema maalumu ya kujiandikisha.

EWE MWANANCHI TUMIA HAKI YAKO YA MSINGI YA KUJIANDIKISHA KWAAJILI YA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SIFA.

RC MNYETI AAGIZA WALIONYANG’ANYWA ARDHI KITETO WAPEWE MAENEO MENGINE

0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti ameagiza wakazi wawili wa Wilaya ya Kiteto walionyang’anywa maeneo yao na kujengwa taasisi za Serikali wapewe maeneo mengine. 

Mnyeti alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa kata za Matui na Bwawani, wilayani Kiteto kwenye ziara yake ya siku tano ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero na changamoto za wananchi, kuyapatia majawabu na kuzungumza na wananchi. 

Alisema kutokana na maeneo ya wananchi hao kuchukuliwa na taasisi za serikali na kujengwa shule ingetakiwa wapewe maeneo mengine ili kufidia maeneo yao. “Mkurugenzi nakuagiza utoe maeneo mengine wapewe hawa wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa ajili ya kufidiwa kwani japo ni suala la maendeleo lakini wanapaswa kupata haki zao. 

Alisema baadhi ya kero ambazo hazina sababu ya kuachwa zinapaswa kutatuliwa kwani wananchi wengine wataichukia serikali yao bila sababu ya msingi. 
Awali, mkazi wa kijiji cha Matui Juma Masare alilalamikiwa kuporwa eneo lake ekari 12 na serikali ya kijiji kisha ikajengwa shule ya msingi. 

“Baada ya kupora eneo langu serikali ya kijiji ilijengwa shule lakini hawakunifidia sehemu nyingine japokuwa maeneo mengine yapo,” alisema Masare. 

Kwa upande wake, mkazi wa kijiji cha Wezamtima kata ya Bwawani, Endeni Kilangi alitoa malalamiko kwa mkuu huyo wa mkoa kuwa alinyang’anywa na serikali ya kijiji hicho ekari zake 70 na kujengwa shule ya msingi. 

“Shamba hilo lilichukuliwa na serikali ya kijiji lakini sikufidiwa eneo lingine sehemu nyingine ili hali kuna maeneo mengine wangeweza kunipa haki yangu,” alisema Kiangi. Baada ya uamuzi huo wananchi hao walimpongeza Mnyeti kwa kusimamia haki zao kwani ilikuwa ni haki yao kupatiwa maeneo mengine.

WAZIRI KIGWANGALLA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA JIMBO NZEGA VIJIJINI

0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Itwigu jimbo la Nzega vijijini wakati wa ziara yake ya jimbo ya kuhamasisha shughuli za maendeleo na kutatua kero za wananchi wa jimbo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameambatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mbagwa jimbo la Nzega Vijijini mara baada ya kuwasili katika kata hiyo akiwa katika ziara yake ya jimbo kuhamasisha maendeleo, kuzungumza na wananchi na kutatua kero.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wanachama wa CCM – UWT wa Kata ya Nkiniziwa,jimbo la Nzega Vijijini wakati wa ziara yake ya jimbo ya kuhamasisha shughuli za maendeleo na kutatua kero za wananchi wa jimbo lake.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata ya Nkiniziwa wakati wa ziara yake ya jimbo ya kuhamasisha shughuli za maendeleo na kutatua kero za wananchi wa jimbo hilo.

PICHA – Aron Msigwa – Nzega.

DC IKUNGI ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA SINGIDA

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiangalia papai alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika Uwanja
wa Bombadia mkoani Singida. 

Mratibu wa maonesho hayo, Sadoti Makwaruzi (katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya maonesho hayo na utoaji elimu wa matumizi
ya vyakula vyenye virutubisho. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kasimba (kushoto) akitoa taarifa kuhusu hali ya chakula nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) alipotembelea banda lao. Kutoka kushotoMtafiti Msaidizi wa Zao la Maharage Tari Selian Arusha, Mtafiti wa Kilimo kutoka Tari Makao Makuu Dodoma, Mshaghuley Ishika na Demetria Mugunda, Mtafiti wa Zao la Maharagekutoka Tari Selian Arusha, Edith Kadege.
Afisa Kilimo Wizara Kilimo Idara ya Afya ya Mimea ( PITS) Twaha Balali (kushoto).akimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi matumizi ya dawa za kuua waharibifu wa mazao. 
Mushema Ayubu kutoka Wizara ya Kilimo Dodoma akimuelekeza kuhusu matumizi ya mbegu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alipotembelea banda hilo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

TAFITI zinazofanywa na wataalamu wa kilimo wametakiwa kuzipeleka kwa wananchi badala ya kubaki nazo ofisini ili zikawasaidie wananchi. 

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula kitaifa Mkoani Singida.

Alisema wataalamu hao wanapaswa kutoa semina mbalimbali kwa maafisa ugani huko Wilayani ili na wao wakawasaidie wananchi kupata utaalamu mbalimbali wa masuala ya kilimo. 

Mpogolo ameyapongeza mashirika ya Save the Children Tanzania,WFP, na FAO kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika masuala ya kilimo, huku akiweka bayana hali ya upatikanaji wa chakula katika wilaya yake kuwa inachakula cha kutosha,kinachopaswa ni wananchi wake kupatiwa elimu ya lishe bora. 

Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kassimba alisema maonesho hayo yanatoa hamasa ya ulaji wa vyakula bora na kuwapa elimu wananchi kuhusu vyakula vyenye virutubisho.

WAZIRI LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WANAOWAPOTOSHA WANANCHI UANDIKISHAJI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), ajiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, katika Kituo cha Senta, Kijiji cha Nyamitwebili, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mwandikishaji wa Kituo Kituo hicho, Nicolaus Zakaria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimpongeza Mwandikishaji wa Kituo Kituo cha Senta, Kijiji cha Nyamitwebili, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Nicolaus Zakaria, baada ya kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kibara, JImbo la Mwibara, Wilayani BUnda, Mkoa wa Mara, leo, mara baada ya kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mwandikishaji wa Kituo Kituo hicho, Nicolaus Zakaria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), akiwa katika foleni ya kwenda kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mwandikishaji wa Kituo Kituo hicho, Nicolaus Zakaria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

******************************************

Na Felix Mwagara, MOHA, Mwibara

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Lugola amesema watu hao wanawarubuni wananchi kwa njia za mitandao ya kijamii, kuwafuata majumbani kwao, wakiwapotosha kususia uchaguzi huo, pamoja na kuwadanganya kuwa walishajiandikisha kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo watatumia vitambulisho hivyo hivyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24, 2019.

Akizungumza na wananchi Jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha Sokoni, Kata ya Kibara, alisema taarifa hizo amepewa na viongozi wa Serikali ya Kijiji pamoja na vyanzo mbalimbali, kuwa kuna kundi la wananchi wanapita mitaani kuwapotosha wananchi na pia kuwatisha wasifike vituoni kujiandikisha wakiwa na lengo la kuvuruga uchaguzi.

“Wananchi Kibara, wacha niwaambie, Serikali ya awamu ya tano si ya kuchezewa, watu hao ni wapotoshaji na lengo lao wanataka kuvuruga uchaguzi ambao ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi, sasa naagiza polisi kuwasaka na kuwakamata watu hao, ili wawe mfano,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Wizara yake inalinda amani katika uchaguzi huo, hivyo haiwezi kukaa kimya kuwaacha wapotoshaji hao wakiendelea kuharibu na kutamba mitaa jambo ambalo Serikali haiwezi ikawaacha.

Pia aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo mbalimbali nchini kujiandikisha ili waweze kuwachagua viongozi wao na kuiletea maendeleo nchi.

“Leo mmejitokeza wengi, nawapongeza, nafikiri wengi wenu mmekuja labda baada ya kuniona mimi mbunge wenu nimefika, lakini bado siku hazijaasha, waambieni wananchi wajitokeze kuja kujiandikisha leo, pamoja na Kesho, viongozi msichoke, fanyeni kazi kwa nguvu zote, kwa maendeleo ya jimbo let una nchi kwa ujumla,” alisema Lugola.

Alisema kupitia uchaguzi huo, viongozi wa vijiji na mitaa watasaidia Wizara yake baada ya kuwapata viongozi hao ambao pia wataunda Kamati ya ulinzi na usalama ya Kijiji na usalama wa eneo husika unaimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa viongozi hao.

Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibara B, Laurent Mafwili Mnyaga, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo kijijini kwake, lakini agizo alilolitoa Waziri Lugola litasaidia wananchi kujitokeza kwa wingi na pia litawasaidia viongozi wa Kijiji chake kuwahamasisha wananchi waende kujiandikisha kwa wingi zaidi, kwasababu wapotoshaji hao wanawajua na Serikali ya Kijiji hicho watahakikisha wanawapeleka polisi.

“Nimefurahi sana kumuona Mbunge wetu kufika Mwibara na kutuhamasisha zaidi, lakini alilolisema ni sahihi kabisa, baadhi ya wananchi wamepotoshwa wasije kujiandikisha, wakidanganywa kuwa kadi za zamani zitatumika kapigia kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa jambo ambalo si sahihi,” alisema Mafwili.

Aliongeza kuwa, licha ya kukabiliwa na changamoto ya wananchi kupotoshwa, kutishwa na watu mitaani wenye nia ovu na serikali, lakini Mwenyekiti huyo alisema utoaji wa elimu kuhusu uandikishaji haukua na nguvu kiasi kilichosababisha wananchi kutokujitokeza kwa wingi.

Waziri Lugola tayari amejiandikisha katika Kijiji hicho na kupongezwa na wananchi hao, ambao wengi wao walijitokeza baada ya kumuona Mbunge wao kujitokeza katika kituo hicho.

Waandishi wa habari wahihitimu kozi fupi ya habari za mtandaoni.

0
0
Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo ambaye ndiye mgeni rasmi ,akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Habari Maalum kilichopo Ngaramtoni mkoani Arusha .
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani nArusha Cloud Gwandu akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika chuo cha Habari Maalum.
Wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele pamoja na viongozi wa chuo cha uandishi wa habari na uongozi cha Habari Maalum Media.

Na.Vero Ignatus,Arusha

Waandishi wa habari mkoani Arusha chini ya chama cha waandishi wa habari mkoani hapo( APC)Wamehitimu mafunzo ya muda mfupi ya uandaaji na utayarishaji na video na uzalishaji yaliyoandaliwa na chuo cha Habari Maalum Media lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika kuyatimiza majukumu yao ya kila siku.

Mafunzo hayo yamehusisha utayarishaji wa miradi,upigaji picha,uaandaaji wa picha ,kuhariri na uzalishaji wa vipindi mbalimbali vya mtandaoni sambamba na kurusha vipindi mbalimbali katika mitandao ya kijamii.

Astele Reuben Ndaluka ni Kaimu mkuu wa chuo hicho amesema kuwa waandishi wanaoyo nafasi pana katika kuielimisha jamii,kuihabarisha ,sambamba na kuijkosoa pale inapostahili kufanyiwa hivyo bila kuvunja sheria na taratibu za nchi.

Ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kujitoa kwaajili nya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika nyanja tofauti ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko yaliyopo kwa sasa ya sayansi na teknolojia huku akiwaasa wahitimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kiuandishi.

Willy Chambulo ni Mwenyekiti wa TATO amewasisitiza wahitimu wa mafunzo kuwa na matumizi sahihi ya elimu waliyoipata na kuahidi kuendelea kusaidia waandishi wa habari watakao kuwa na utayari kupata mafunzo zaidi.

Aidha amewataka kuitumia vyema elimu waliyoipata sambamba na kuigeuza kuwa pesa ili ilete manufaa kwa jamii na kuepuka kuwa tegemezi

Cloud Gwandu ni mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha ,ameishukuru TATO kwa kufadhili mafunzo hayo ya kozi fupi kwa waandishi hao, na kuahidi kuwa mafunzo hayo hayataishia darasani ,bali watayaweka kwenye vitendo zaidi ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Gwandu amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu,ambapo kundi lingine la waandishi wa habari litapata mafunzo hayo baadae mwezi huu ,lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuwa na weledi katika kutaarisha kuandaa habari mbalimbali ya matukio katika jamii kwenye mitandao ya kijamii

Amesema waandishi wa habari wanayo nafasi pana ya kwa kutumia mitandao ya kijamii ,kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya utalii ,haswa kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivituo mbalimbali vilivyo nchini.

SERIKALI KUZIPATIA RUZUKU KAYA ZOTE MASKINI NCHINI BAADA YA KURIDHISHWA NA MAENDELEO WANUFAIKA WA TASAF

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.
Baadhi ya wananchi na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Hayupo pichani) katika ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.
Mmoja wa wanufaika wa TASAF wa Kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa, Bi. Mariana Aidani Mkwaila akitoa shuhuda ya namna alivyonufaika na ruzuku anayoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Mnufaika wa TASAF wa Kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa, Bi. Elizabeth Damiani akitoa shuhuda ya namna alivyonufaika na ruzuku anayoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na mmoja wa wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa mbele ya nyumba inayojengwa na mnufaika huyo kupitia ruzuku anayoipata.
Wananchi na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa wakiwa katika mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Hayupo pichani) uliofanyika katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.

………………..


Na James K. Mwanamyoto-Nyasa

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeahidi kuzinufaisha kaya zote maskini nchini baada ya kuridhishwa na namna wananchi katika vijiji vilivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini walivyoboresha maisha yao na kujikwamua katika lindi la umaskini liliokuwa likiwakabili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akizungumza na wanufaika na wananchi wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango huo wilayani humo.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, iwapo wanufaika wasingetumia ruzuku vizuri kuboresha maisha, Serikali isingesita kusimamisha utekelezaji wa Mpango huu wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

“Hongereni wanufaika wa TASAF kijiji cha Nangombo na maeneo mengine kwa kutumia ruzuku kuboresha maisha yenu, kujenga nyumba bora, kununua vifaa vya shule kwa ajili ya watoto na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi,” Mhe. Mkuchika amepongeza.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imeridhika na mafanikio yaliyopatikana, hivyo itaendeleza vita dhidi ya umaskini, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya kaya zote maskini nchini.

Akiwasilisha taarifa ya kijiji cha Nangombo kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Joseph P. Ngogi amesema watoto 66 wa shule wananufaika na ruzuku inayotolewa hivyo imeongeza mahudhurio shuleni na kliniki kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, aidha kaya 65 zimeboresha makazi yao kwa kujenga ama kukarabati na kuezeka kwa bati.

Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa TASAF kijiji cha Nangombo, Bi. Mariana Mkwaila amesema ruzuku anayoipata imemuwezesha kuwanunulia watoto wake sare za shule, viatu na madaftari ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba kubwa ambayo anatarajia kuizeka kwa bati hivi karibuni.

Naye, Bi. Elizabeth Damian amesema, alikuwa akiishi maisha ya kimaskini kwenye nyumba ya nyasi kabla ya kuingizwa kwenye Mpango, lakini baada ya kuanza kupokea ruzuku ameweza kufuga kuku, mbuzi na kufyatua tofali zilizomuwezesha kujenga nyumba iliyoezekwa kwa bati.

Mhe. Mkuchika amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kuitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.

WAKAZI KING’AZI HUKO KISARAWE WAKO HATARINI KUKOSA HAKI YA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA ORODHA LA KUPIGIA KURA-NDIKILO

0
0
mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo

NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE

WAKAZI wa Kitongoji cha King’azi A wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wako hatarini kukosa haki yao ya msingi ya kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Mitaa ,Vijiji na Vitongoji Novemba 24 mwaka huu “:,ambapo waliojiandikisha hadi sasa ni wanne kati ya 560 wanaotarajiwa kujiandikisha .

Hatihati hiyo inahofiwa kuchukua nafasi baada ya baadhi ya watu kuwadanganya kuwa wanapaswa kujiandikisha kupitia wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam jambo ambalo si la kweli.

Hali hiyo ilibainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye mkoa huo.

Akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo alifika kwenye kituo hicho na kukuta wananchi waliojiandikisha ni wanne tu kati ya 560 wakidai kuwa wao watajiandikisha kitongoji cha King’azi B ambacho kipo upande wa Ubungo.

Alisema baada ya viongozi wa mikoa hiyo na wataalamu mbalimbali waliridhia vitongoji hivyo kugawanywa ambapo walikubaliana King’azi A itabaki mkoa wa Pwani na Kingazi B na sehemu kidogo ni Ubungo Jijini Dar es Salaam.
“Awali kulikuwa na mgogoro lakini Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (TAMISEMI) walipitisha mipaka na kugawanya maeneo hayo lakini baadhi ya wananchi wanasema kuwa mitaa yote iko eneo la wilaya ya Ubungo lakini King’azi A ni Kisarawe na King’azi B ni Wilaya ya Ubungo”, alisema Ndikilo.

” Nimesikia kuna mtu anaitwa magodoro ndiyo anayepotosha wananchi wakajiandikishie Ubungo jambo ambalo si kweli na endapo ataendelea kuwapotosha wananchi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwani ni kinyume cha sheria kuvuruga uchaguzi,”alisema Ndikilo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alisema kuwa tayari suala la mipaka ya wilaya ya Kisarawe na Ubungo iliwekwa na wananchi walielezwa.

Akiwa wilayani Mkuranga Ndikilo aliwapongeza viongozi wa wilaya hiyo ambapo hadi juzi walikuwa wameandikisha wananchi 70,000 kati ya wananchi 84,000 wanaotarajiwa kiandikishwa tofauti na wilaya nyingine ambazo zilikuwa bado zina wananchi wachache waliojiandikisha.

WASANII WANAWAKE TANZANIA WATEMBELEA HOSPITALI YA MLOGANZILA

0
0
Muuguzi Odax Myinga wa Muhimbili- Mgonzila (wa pili kushoto) akitoa ufafanuazi kwa wasanii juu ya huduma mbalimbali zinazopatikana katika wodi ya wagonjwa binafsi (private ward).
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akielezea huduma zinazotolewa hospitalini hapo mara baada ya kundi la wasanii wanawake Tanzania kutembelea Hospitali ya Mloganzila hii leo.
Baadhi ya wasanii wanawake wakiwa katika ziara ya kuangalia mafanikio ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Mloganzila.

Naibu Mkurugenzi Dkt. Julieth Magandi, baadhi ya watumishi wa Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja na kundi la wasanii wanawake Tanzania mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.

………………

Wasanii wanawake Tanzania leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila kwa lengo la kuona mafanikio katika utoaji wa huduma za afya chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema hospitali imekua na mafanikio katika utoaji wa huduma za afya, ikiwemo za kibingwa ambapo hivi karibuni imefanikiwa kupandikiza watoto watatu vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear implants) na kwamba hatua hii inaifanya Hospitali ya Mloganzila kuimarika katika utoaji huduma za kibingwa nchini.

‘’Pia Juni mwaka huu kwa mara ya kwanza Mloganzila ilifanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe katika mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebral aneurysms) kwa mgonjwa aliyekuwa na tatizo hilo na kuifanya Hospitali hii kuwa ya pili baada ya MOI katika kutoa huduma hiyo’’ amesema Dkt. Magandi.

Kwa mujibu wa Dkt. Magandi Hospitali ya Mloganzila ina jumla ya vitanda 608 na hivyo kuwa hospitali ya tatu kwa ukubwa nchini.

Awali mkuu wa msafara Bi. Mwantumu Mgonja amesema pamoja na mambo mengine ziara hiyo inaangazia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ili kuwaeleza wananchi ambacho serikali imefanya.

“Lengo ni kutembelea miradi ambayo imetekelezwa na serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. John Magufuli, tumepita katika miradi mbalimbali na hii leo tumekuja hapa Hospitali ya Mloganzila ili kujionea wenyewe mafanikio katika utoaji wa huduma za afya na tuwaeleze wananchi juu ya mafanikio haya makubwa’’ amesema Bi.Mgonja .

JAFO AONGEZA SIKU TATU UANDIKISHAJI DAFTARI LA ORODHA WAPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akijiandikisha kwenye Orodha ya Daftari la Mpiga kura kwenye Kitongoji cha Kimani Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani leo Tarehe 13.10.2019
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akitoa Tangazo la Ratiba ya Uandikishaji wa Orodha ya Mpiga Kuta katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019


Na Oscar Job, Kisarawe

WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameongeza siku tatu kwa wananchi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.

Akizungumza kabla ya kujiandikisha Kijijini kwake Kimani,Kisarawe mkoani Pwani jana, Waziri Jafo alisema kuongezwa kwa siku tatu hizo kumetokana na sababu mbalimbali ambazo kimsingi zimesababisha wananchi kuikosa fursa hiyo.

Alisema kimsingi siku za uandikishaji huo zilizoongezwa kutoka leo hadi Oktoba 17, kumesabishwa na tatizo la mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na hivyo kuleta shida kwa wananchi wengi kujiandikisha.

Aliitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na uwepo wa zoezi la wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyoleta dhana kwa baadhi ya wananchi kuwa kitambulisho cha mpiga kura kitawawezesha kupiga kura katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa.

“Kutokana na sababu hizo na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 na matangazo ya Serikali Na 371,372,373 na 374 ya Mwaka 2019 Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa” alisema Jafo

Alisema kutokana na kanuni hizo na changamoto zilizojitokeza Wizara yake imeona vyema kuongeza siku hizo tatu ili kuwapa nafasi wananchi kujiandikisha na hivyo kutumia fursa yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka.

Aidha alisema tangu kuanza kwa Oktoba 8 hadi Octoba 12 Mwaka huu wananchi zaidi ya Milioni 11 walikuwa tayari wamejiandikisha nchi nzima kushiriki uchaguzi huo huku akilitaja zoezi hilo kuwa lenye mafanikio makubwa ikilinganishwa na kipindi kingine chote.

Alisema kufuatia mabadiliko, ratiba ya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na matukio yanayohusu uandikishanji yatakuwa na mabadiliko fulani fulani ikiwemo kubandikwa kwa orodha ya wapiga kura litakalofanyika kuanzia Oktoba 18, utoaji wa pingamizi kuhusu uandikishaji wapiga kura litakalofanyika Oktoba 14 hadi 24.

Mabadiliko mengine ni pamoja na uamuzi kuhusu pingamizi litalofanyika kuanzia Oktoba 24 hadi 25,marekebisho ya orodha ya wapiga kura kuanziaa Oktoba 25 hadi 25 pamoja na ukataji wa rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi utakaofanyika Oktoba 24 hadi 26 sambamba na ukataji wa rufaa utakaofanyika Oktoba 24 hadi 29 Mwaka huu.

Aidha alisema matukio mengine yote zikiwemo kampeni za wagombea zitaendelea kubaki kama kawaida huku akiwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi huo.


WAKANDARASI MIRADI YA MAJI MTWARA WATAKIWA KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) alipotembelea mradi wa maji wa Mkwiti, Wilayani Tandahimba. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Mandisi Rejea Ng’ondya.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua mitambo ya kusukuma maji kwenye kituo cha Mtongwele ambacho kitatumiwa kupelekea maji kwenye mradi wa Mkwiti kutokea chanzo cha Mitema (Mitema Well Field). Kulia ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akielekeza jambo wakati wa ziara yake kwenye mradi wa maji wa Kilidu, Halmashauri ya Mji wa Newala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akikagua mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata wa Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara unaotumia maji kutoka Mto Ruvuma. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akielekeza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata unaotekelezwa Wilayani Masasi. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua mradi wa maji wa Makonde Wilayani Newala ambapo pia ni eneo kilipo chanzo cha maji cha Mitema (Mitema Well Field) ambacho kitatumika kwa ajili ya miradi ya Mkwiti, Makonde na Kilidu.

…………….

Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji kwenye Wilaya za Newala, Tandahimba na Masasi, Mkoani Mtwara wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili ikamilike mapema hasa ikizingatiwa mahitaji muhimu ya kukamilisha miradi hiyo yamekamilika.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ametoa agizo hilo Oktoba 12, 2019 Mkoani Mtwara kwa nyakati tofauti alipofanya ziara kwenye miradi ya maji inayotekelezwa kwenye wilaya hizo.

Naibu Katibu Mkuu Sanga alitembelea mradi wa Mkwiti uliyopo Wilaya ya Tandahimba, Chanzo cha Maji cha Mitema, Mradi wa Makonde na aMradi wa Kilidu yote ya Wilaya ya Newala na mradi wa Chipingo Wilayani Masasi.

Mara baada ya kuzungukia miradi, Mhandisi Sanga alisema hajaridhika na kasi ya utekelezaji wake licha ya kwamba vifaa vinavyohitajika kukamilisha miradi hiyo ikiwemo mabomba na mitambo ya kusukuma maji vikiwa vimekamilika.

Alisema haoni sababu kwanini miradi inatekelezwa kwa kusuasua licha ya kuwa vifaa muhimu vipo eneo la mradi. “Nimezungukia maeneo ya miradi nimeona vifaa muhimu vinavyohitajika kukamilisha miradi vipo, hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Alisema kinachotakiwa ni wananchi kupata maji mapema iwezekanavyo na kwamba suala la kupoteza muda halitokubalika hasa ikizingatiwa maeneo inapotekelezwa miradi yanasumbuliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Aliagiza wasimamizi wa miradi ambayo ipo katika hatua ya ulazaji bomba kuharakisha kumaliza shughuli hiyo hasa ikizingatiwa msimu wa mvua umefika na kwamba mitaro hiyo ikiendelea kubaki wazi itajifukia na italazimika kuchimbwa upya.

“Nimeona mitaro imechimbwa na imekamilika na mabomba yapo hakikisheni kuanzia sasa mabomba yanalazwa ili kuepusha gharama ya kufanya kazi mara mbili ya kuchimba mitaro ya maji,” aliagiza Naibu Katibu Mkuu Sanga.

Mhandisi Sanga aliagiza wasimamizi wa miradi kuhakikisha kwenye kutekeleza miradi wanaanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili wananchi waanze kupata huduma na baadaye waendelee na maeneo mengine wakati ambao tayari wananchi wanakuwa na huduma.

“Mnatakiwa kuwa wabunifu wakati wa ujenzi wa miradi, mnapaswa kuanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili kwanza wananchi wapate huduma na huku mkiendelea kutekeleza maeneo mengine,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa Mkoani humo ili kujionea hatua ya utekelezaji wake sambamba na kufahamu changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.

DC RUFIJI AWAHIMIZA WANANCHI KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOLETA MAENDELEO

0
0

Na Aalliyah Habib Rufiji Pwani

MKUU wa WIlaya ya Rufiji mkoani Pwani Juma Njwayo amewataka wananchi wilayani humo kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia kuleta maendeleo badala ya kuchagua viongozi wanaochangia kuchochea migogoro ikiwemo ya wafugaji na wakulima huku viongozi hao wakijinufaisha kwa maslahi yao binafsi.

Ameyasema hayo wakati akihamasisha  uandikishaji wa daftari la wakazi kwa ajili ya kupiga kura kwa ajili ya  uchaguzi wa viongozi wa mitaa vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu nchi nzima.

"Msichague viongozi wanaoingiza ng'ombe usiku kwenye maeneo yenu huku nyie mnagombana wenzenu wanakusanya fedha wakati umefika wa kutowachagua viongozi hao chagueni wanoaweza kuwasaidia kuwaletea maendeleo yenu hiyo ndiyo dawa," alisema Njwayo.

Aliwakumbusha wananchi hao kuwa vitambulisho vya kupiga kura na vya utaifa havitatumika katika zoezi la kupiga kura na kuwataka kujitokeza kwasiku zilizobakia kujiandikisha kwakuwa hiyo nafasi pekee itakayomuwezesha kila mwananchi kupiga kura.

"Nawaambieni ndugu zangu msijidanganye vitambulisho hivyo havitatumika haviruhusiwi kisheria kajiandikisheni na nyie watendaji piteni nyumba hadi nyumba mashambani wafateni wananchi wajiandikishe ni haki yao kupiga kura," alisema Njwayo.

Awali Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Rufiji Gwakisa Mwaikela aliwataka wagombea kuepuka vitendo vya rushwa katika uchaguzi na wananchi nao kukataa kupokea rushwa kwa kuwa sheria itachukua mkomdo wake.

"Chagueni viongozi watakaoweza kuwasaidia kuwaletea maendeleo msikubali kupewa zawadi wala kitu Chochote chenye kiashiria cha rushwa sheria itawabana haitaangalia nani ni nani,"alisema Gwakisa.

Baadhi ya Wananchi walisema mwitikio mdogo wa kijiandiksiha unatokana na baadhi ya wananchi kushinda mashambani na wengine kuishi maeneo ya mbali na kilipo vituo vya kujiandikisha hivyo kuona shida kama wanapoteza muda kwenda kujiandikishwa kwenyw daftari ka wakazi.
 Wananchi kijiji cha Muhoro wakimsikiliza Mkuu wao a Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo pichani haonekani wakati akiwahamasisha kujitokeza kujiandikisha katika daftari.la orodha ya wakazi ili waweze kuliga kura kychagua vi0ngozi wa serikali za vijiji vyao na vitongoji Rufiji Mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Juma Njwayo akitoa elimu kwa wananchi umuhimu wa kujiandikish katika daftari la orodha ya wakazi ili waweze kushiriki kupiga kura Nov 24 mwaka huu katika kijiji cha Mbwara Rufiji Mkoani Pwani akiwasisitizia kitambulisjo cha kupiga kura na uraia hakitaruhusiwa katika zoezi la upigaji kura.

WAZIRI MHAGAMA AWATAKA VIJANA KUENZI MCHANGO WA BABA WA TAIFA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia vijana wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi.
Baadhi ya Vijana wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Mkoani Lindi.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Sehemu ya viongozi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi. Katikati ni Katibu Mkuu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally.
Mama Gertrude Mongela akiwasilisha mada kuhusu Miaka 20 bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo uliofanyika Mkoani Lindi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mama Gertrude Mongela kuhusu Miaka 20 bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo. (Wa pili kutoka kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Abeid Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. Kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo huo wakifuatailia mada zilizokuwa zinawasilishwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba. (Wa pili kutoka Kushoto ni Mjukuu wa Mwalimu Julius Kambarage NyerereMjukuu wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bi. Ngusekera Nyerere akitoa salamu wakati wa mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Mkoani Lindi.
Wawasilishaji Mada wakisikiliza hoja zilizokuwa zikichangiwa na baadhi ya washiriki wakati wa mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi.
Kijana mmoja wapo aliyeshiriki mdahalo huo akichangia mada kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuenzi na kuziishi fikra na mitazamo za Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuendeleza umoja uliopo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Mkoani Lindi Oktoba 13, 2019, Waziri Mhagama alisema kuwa vijana wanapaswa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake ili waendelee kujivunia juu ya misingi ya amani na umoja iliyopo nchini.

“Vijana mna kila sababu ya kujivunia amani na umoja ulipo katika taifa letu kwa kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi aliyewapenda watu wote bila kujali imani zao wala itikadi zao, alikuwa mzalendo na alitaka watanzania wote waishi kwa umoja,” alisema Mhagama.

Aidha alifafanua kuwa, Amani na umoja zilikuwa ni miongoni mwa tunu na falsafa kuu za Baba wa Taifa ambayo ndiyo matokeo ya umoja na mshikamano wa taifa uliopo sasa.

Aliongeza kuwa miongoni mwa mambo muhimu ambayo Baba wa Taifa alikuwa akisisitiza katika kuwaunganisha watanzania ni pamoja na kulijengea uhuru taifa na watu watu wake, kudumisha amani, upendo, umoja, uzalendo, mshikamano na kuandaa sera za kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi.

Pamoja na hayo alisisitiza pia vijana na wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuendeleza maono ya Baba wa Taifa ikiwemo mageuzi ya kiuchumi yenye manufaa kwa taifa.

Akitolea mfano sekta ya elimu ambayo serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa elimu bure ilikuwa ni falsafa ya Mwalimu katika kuwajenga watanzania fikra ya kujitegemea ili waweze kuukabili umasikini.

Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wananchi kuendeleza maudhui ya Mwenge wa uhuru ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha watanzania na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Mwalimu Julius Nyerere ataendelea kukumbukwa na Watanzania kwa mchango wake aliojitolea katika kulijenga taifa.

TAARIFA YA HALI YA USALAMA KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA UCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA.

0
0
Ndugu wanahabari, Hali ya usalama Mkoa wa Arusha katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa ni shwari mpaka hivi sasa na hakuna tukio lolote la kihalifu limeripotiwa wala mtu kukamatwa kuhusiana na zoezi hilo. Kwa mujibu wa ratiba zoezi hili lilikuwa likamilike kesho tarehe 14.10.2019 lakini limeongezewa muda hadi tarehe 17.10.2019 saa 12 jioni. Jeshi la Polisi mkoani hapa litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Mkoa wa Arusha na litafanya kazi bila kumuonea mtu na halitakuwa na upendeleo kwa chama chochote cha siasa. Askari wote wameelekezwa kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo katika zoezi hili. 
Hivyo nitumie fursa hii kuwahakikishia Wananchi wote wa Mkoa wa Arusha wenye sifa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwani tumejipanga katika kuhakikisha usalama wao na mali zao. 
Aidha kwa mujibu wa ratiba tunategemea msimamizi wa uchaguzi kuwasilisha kwa OCD ratiba za mikutano ya kampeni tarehe 14.11.2019. Kampeni zitaanza rasmi tarehe 17.11.2019 hadi tarehe 23.11.2019. Uchaguzi utakua tarehe 24.11.2019 narudia tena tarehe za uchaguzi ni zile zile kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na hazijabadilika. 
Imetolewa naJonathan Shanna – ACP Kamanda wa Polisi – Arusha

Wanachama 10 Klabu za Biashara NMB kushiriki Canton Fair China

0
0


Mkuu wa Kitengo cha biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akikabidhi mfano wa tiketi ya kwenda china Mfanyabiashara kutoka Musoma mkoani Mara, Oliver Kisamba (wa pili kutoka kushoto) wakati wa hafla ya kuwakabidhi tiketi wafanyabiashara kumi kwa ajili ya kwenda nchini China kwa ajili ya kushiriki maonyesho ya 125 ya biashara yakayofanyika chini humo. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa benki ya NMB Idara ya biashara, Theresia Mayanie na wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha wafanyabiashara wadogo,
Beatrice Mwambije
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard(wa tatu kutoka kulia) akiwakabidhi mfano wa tiketi wafanyabiashara kumi waliodhaminiwa na benki ya NMB kwenda nchini China kwa ajili ya kushiriki maonyesho ya biashara nchini humo kyanayotarajia kuanza wiki ijayo
Mkuu wa Kitengo cha biashara wa NMB, Donatus Richard akizungumza na wafanyabiashara kati ya kumi waliofadhiliwa na benki ya NMB kwenda nchini China kwa ajili ya kwenda kushiriki maonyesho ya biashara yanayaotarajia kuanza wiki hii nchini humo wakati wa hafla ya kuwakabidhi tiketi jijini Dar es Salaam


WAFANYABIASHARA 10 wanachama wa Klabu za Biashara za Benki ya NMB (NMB Business Club), wameondoka nchini jana kwenda China, kushiriki Maonesho ya 125 ya Canton Fair 2019, yanayofanyika wiki hii mjini Guangzhou, ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kibiashara ya siku 10.

Tiketi za safari ya wafanyabiashara hao (kwenda na kurudi), malazi, chakula na kila kitu, vimegharamiwa Benki ya NMB, ambayo iliwataka kuitumia fursa hiyo vema kwa kwenda kujifunza namna ya kuboresha biashara, kukuza mitaji na kuchangia uchumi wa taifa.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyabiashara hao kutoka Kanda mbalimbali za klabu zao nchini, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Donatus Richard, (Head of Business Banking) aliwataka kuwa mabalozi wema NMB wakiwa China na kutumia vema elimu watakayopata kupitia maonesho watakayoshiriki.

“Ni matumaini yetu kwamba mtaitumia vizuri safari hii kujifunza fursa mbalimbali za kibiashara zikiwemo za uwekezaji wa viwanda ili kuendana na kasi ya Tanzania ya Viwanda inayochakatwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

“Kufanya hivyo kutawasaidia kuongeza mbinu katika nyanja mbalimbali, ikiwemo kujua kwa namna gani mnaweza ushirikiana kufanya biashara kimataifa, hatua ambayo itawanyanyua kiuchumi,” alisema Richard huku akiwataka kurejea wakiwa bora zaidi kimbinu katika kukuza mitaji yao.

Kwa niaba ya NMB, Donatus akawasistiza wafanyabiashara hao kuwa, furaha yao kama taasisi kinara ya fedha nchini itakuwa ni kushuhudia mapinduzi chanya ya kimaendeleo kupitia elimu watakayopata kupitia ziara na maonesho watakayoshiriki China.

Akitaja vigezo vilivyotumika kupata wafanyabiashara hao 10 kutoka miongoni mwa wanachama zaidi ya 200,000 kote nchini, Richard alisema ni pamoja na rekodi nzuri za marejesho ya mikopo na nguvu ya ushawishi ya mwanachama kuongeza wanachama/wateja wapya katika NMB.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NMB Business Club wilaya ya Ilala, Award Mpandilah, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamuni ya Mpandilah General Supplies Ltd, aliishukuru NMB kwa fursa waliyowapa, ambayo ana uhakika inaenda kubadili mifumo yao kibiashara.

Alibainisha ya kwamba, ziara ya siku 10, inayoambatana na ushiriki wa Maonesho ya Canton Fair 2019, vitawaongezea elimu na kuwatia chachu ya mafanikio kibiashara na kwamba watarejea wakiwa wamejenga chaneli za ushirikiano na wafanyabishara wa nchi hiyo.

“Ni fursa ambayo inatamaniwa na kila mtu aliye na kiu ya maendeleo. Tunaishukuru NMB kwa nafasi waliyotupatia na tunaahidi kuitumia vema kuhakikisha tunapiga hatua za haraka kimaendeleo ya mfanyabiashara mmoja mmoja, benki inayotuhudumia na taifa kwa ujumla,” alisema Mpandilah.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images