Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Free eye camp in Bagamoyo ion honour of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

$
0
0
The Bilal Muslim Mission of Tanzania, Beta Charitable Trust of UK and Hon. Mp for Bagamoyo Dr. Shukuru Kawamba have organised a free eye camp in Bagamoyo district for 3 days starting from 12th to 14th  October, 2019 to mark the 20th Death Anniversary of the Father of the Tanzania nation 
MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Screening will be held at Bagamoyo's Majengo Primary school where Free camp services that include  free eye check up, free spectacles, free eye medicine & cataract operation...

Contact-Dr. Francis
Bagamoyo district eye Coordinator, 
0712 172 873*

Kupona Foundation’s 10th anniversary a hit

$
0
0
By Nathan Chiume
 Last night we celebrated Kupona Foundation’s 10 years in the U.S. They are the fundraising arm of CCBRT Hospital in Tanzania, which works to prevent disability, provide affordable medical and rehabilitative services, and aid the empowerment of people with disabilities and their families. They also seek to prevent disability through early identification by strengthening the maternal and newborn health system throughout Dar es Salaam and beyond

Two years ago my family partnered with Kupona to honour the memory of our dearly departed sister Jessie Wayasa Mgeni Chiume, (who was a maternal and neonatal Head Nurse), by raising funds that help to train maternal nurses and build capacity at the CCBRT Hospital, thus building a legacy of high quality, compassionate maternal healthcare for women and girls. We are grateful for this partnership with Kupona and CCBRT; and for all the generous contributions from family and friends towards keeping our sister’s legacy alive.



MAJALIWA AJIANDIKISHA KWA AJILI YA UCHAGUZI UJAO WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati mkewe Mary alipojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 12, 2019. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na kulia ni Mwandikishaji wa kituo hicho, Shaka Msange. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na Binti Mkumba baada ya kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati mkewe Mary alipojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 12, 2019. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na kulia ni Mwandikishaji wa kituo hicho, Shaka Msange. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



*************************************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amejiandikisha kwenye kituo cha shule ya msingi Nandagala, wilayani Ruangwa, Lindi ili aweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa amejiandikisha kijijini kwao leo asubuhi (Jumamosi, Oktoba 12, 2019) akiwa na mkewe Mama Mary Majaliwa.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Mkuu amesema zoezi la kujiandikisha ni la kitaifa na ni haki ya kila Mtanzania ili aweze kuchagua kiongozi amtakaye au aweze kugombea kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu. 

“Kila mmoja anapaswa kuja kujiandikisha. Zoezi hili ni tofauti na lile la uchaguzi mkuu. Kuna watu wanafanya upotoshaji wa makusudi, wanawadanganya wenzetu kwamba kama una kadi ya uchaguzi huna haja ya kujiandikisha. Hii siyo kweli, hiyo kadi ni ya uchaguzi wa mwakani,” amesema.

“Nawasihi mje kujiandikisha ili muweze kuchagua viongozi mnaowataka. Zoezi hili limebakiza siku mbili tu, mwisho wake ni tarehe 14 Oktoba, 2019 jioni.”

Amesema mtu yeyote aliyefikisha miaka 18, ana haki ya kujiandikisha ili aweze kuwa mgombea au mpiga kura, na pia awe na uhakika kuwa amemchagua kiongozi anayemtaka.

Mara baada ya kujiandikisha, Waziri Mkuu alipita katika vijiji vya Chimbila B, Chimbila A, Michenga (Jerusalem), Michenga (Misri), Nangumbu na Nanganga.

Akiwa njiani, alizumgumza na wanavijiji waliosimama njiani walipoona msafara wake na akatumia fursa hiyo kuwahimiza wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. 

“Wana-Ruangwa tutumie fursa hii ili tuchague viongozi watakaokereketwa na kuleta maendeleo. Tuchague viongozi ambao hata wakipewa fedha za miradi, watazitumia kwa maendeleo na hawatashawishika kirahisi kuzitumia kwa maslahi yao binafsi.”

“Kuna fedha zinaletwa hapa shilingi milioni 60 za elimu, tunaleta fedha za kuchimba visima lazima wazisimamie, tunaleta fedha za afya, lazima wazisimamie. Tunahitaji watu ambao watakuwa waaminifu na wanaoweza kusimamia miradi yetu.”

“Tunatakiwa tuchague viongozi watakaosimamia maendeleo, wanaohamasisha maendeleo. Tunatakiwa tuchague viongozi ambao ni waadilifu, waaminifu, wachapakazi, wasikivu, wapenda watu na wanaoweza kusimamia fedha zinazoletwa hapa. Ninyi mnawafahamu kwa sababu mnaishi nao,” amesema. 

Katika maeneo yote hayo, Waziri Mkuu aliwaeleza kwamba Serikali imetoa fedha za kununua taa za barabarani ambazo zimeanza kusambazwa na zikishafungwa, zitawawezesha wajasiriamali wafanye biashara zao hadi usiku. 

“Tunaboresha vijiji vyetu kuanzia Nanganga, Nangumbu, Michenga (Misri), Michenga (Jerusalem), Chimbila A na B, Chikunji, Mtope, Likunja, Nkowe, Nandagala, Namichiga na Mandawa.

BALOZI ALI KARUME AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA KITAIFA MKOANI LINDI

$
0
0


Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume akizungumza na Vijana walioshiriki Kongamano la 17 la vijana kitaifa lililofanyika Mkoani Lindi katika Ukumbi wa Kagwe Oktoba 11, 2019 ikiwa ni kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Baadhi ya vijana wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume (hayupo pichani) wakati wa kongamano la vijana walililowakutanisha vijana kujadili mchango wa Baba wa Taifa katika maendeleo ya Bara la Afrika.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika Mkoani Lindi katika Ukumbi wa Kagwe Oktoba 11, 2019.


Bi. Aisha Kombo kutoka Zanzibari akiimba utenzi kuhusu waasisi wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akisikiliza utenzi uliokuwa ukiibwa na Bi. Aisha Kombo. Kulia ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi.


Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akieleza jambo wakati wa Kongamano hilo la Vijana Kitaifa. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama


Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Kenya Bi. Rose Mugu akitoa taarifa fupi kuhusu ushuhuda wa vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika juu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 


Kikundi cha International Youth Fellowship wakitoa burudani wakati wa kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kagwe, Mkoani Lindi.


Bw. Usman Mchinja mwakilishi kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) akielezea mchango wa vijana katika taifa wakati wa Kongamano la vijana lilifanyika Mkoani Lindi.



PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

WAZIRI KIGWANGALLA AZUNGUMZA AFANYA MIKUTANO YA HADHARA NZEGA VIJIJINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Budushi, Nzega Vijijini mara baada ya kufika shuleni hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kuhamasisha maendeleo, kuzungumza na wananchi na kutatua kero zao katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Nzega Vijijini.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Budushi katika jimbo la Nzega Vijijini alipofanya mkutano wa kuimarisha Chama na kutatua kero za wananchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na viongozi wengine wa CCM kutoka katika Kata mbalimbali za jimbo la Nzega Vijijini wakitazama Kadi za wanachama 100 wa CHADEMA waliohamia CCM kufuatia kuridhishwa na Utendaji Kazi wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Kata ya Ndala, Nzega Vijijini.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Nzega vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimpokea na kumkaribisha katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Lucas Kitambi Maselele, Mwenyekiti Mstaafu na Katibu wa CHADEMA jimbo la Nzega vijijini mara baada ya kujiunga rasmi na CCM.

MABULA ALITAKA SHIRIKA LA NYUMBA KUJENGA MAJENGO YENYE UBORA

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa anayeshughulikia Ubunifu Magreth Ezekiel akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati Naibu Waziri alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya Ziwa inayojengwa na NHC jana. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Dkt Phillis Nyimbi wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya Ziwa inayojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa jana. Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Nyamagana Jonas Madulu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya Ziwa alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi na kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa NHC anayeshughulikia Ubunifu Magreth Ezekiel.

……………………..


Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha linajenga majengo yenye ubora katika miradi mbalimbali inayopewa kujenga nchini.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kanda ya Ziwa (TFS) eneo la Mkolani jijini Mwanza akiwa katika ziara yake ya kuangalia utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Kanda ya Ziwa pamoja na kukagua miradi ya ujenzi inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Alisema ni vyema shirika hilo likahakikisha miradi yoyte inayopewa ya ujenzi inakuwa na viwango na kuepuka udanganyifu wowote unaoweza kufanyika kama vile kuweka kiwanga kidogo cha saruji katika ujenzi jambo linaloweza kusababisha majengo yasiyo na ubora.

Aliwataka wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa jengo la TFS mkoani Mwanza kuwa waaminifu wakati wote wa ujenzi ili kuepuka sifa mbaya ya udokozi inayoweza kusababisha shirika la Nyumba kukosa kazi nyingine kwa kujenga majengo yaliyo chini ya kiwango.

‘’Uaminifu lazima uwepo ili ikitokea kazi nyingine mpewe awamu hii NHC mko vizuri’’ alisema Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alilisifu shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kufanya kazi vizuri katika ujenzi wa Ofisi na nyumba za watumishi na kulitaka shirika hilo kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa majengo yake katika kipindi kifupi kwa kuwa linahitaji kufanya kazi usiku na mchana.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza Fadhili Ntahena alisema, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kanda ya Ziwa unaosimamiwa na shirika lake unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 na ulianza Septemba mwaka huu ikiwa ni sehemu ya miradi mbalimbali ambaloShirika hilo limepewa na serikali kuijenga.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Magreth Ezekiel alisema, NHC imejipanga katika miradi yake mbalimbali iliyokabidhiwa na mipango ya Shirika ni kuhakikisha miradi yote inakamilika ndani ya miezi sita na mradi wa ujenzi wa jengo la TFS Mkolani Mwanza walipanga kumaliza April 2020 ingawa jengo hilo linaweza kukamilika kabla ya mwezi huo.

RAIS DKT. MAGUFULI AJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KATIKA KITONGOJI CHA SOKOINE CHAMWINO MJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandikisha katika daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. Kulia aliyekaa ni Afisa wa NEC Mary Joseph Mwambongo 



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuangalia Afisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Mary Joseph Mwambongo akimalizia taratibu za uandikishaji katika katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019.

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijiandikisha katika daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. Kulia aliyekaa ni Afisa wa NEC Mary Joseph Mwambongo 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama kwenye msari na mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na wananchi wengine wakati wakielekea kujiandikisha katika daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kitongoji  cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo mara baada ya kujiandikisha katika katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kuchukua chakula pamoja na Waandishi wa Habari mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ana kula chakula pamoja na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya habari wa mkoani Dodoma leo. PICHA NA IKULU



UDP yataka Wananchi wajiendikishe katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama cha (UDP), John Cheyo ametoa rai ya kuwataka  wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ndiyo chanzo cha maendeleo nchini.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam, Cheyo amesema uchaguzi huo ndiyo kichocheo cha kupata viongozi ambao watakaoleta maendeleo katika mitaa kwani na mipango ya taifa yanaanzia katika serikali za mitaa.

Amesema  uchaguzi wa serikali za mitaa una umuhimu kwani  chama cha UDP kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo wanachama kugombea uenyekiti wa serikali za Mtaa.

Cheyo amesema UDP maendeleo na watashirikiana na serikali katika masuala yote yanayohusu maendeleo.

Cheyo amesema kuwepo kwa vyama vingi si sababu ya kurudisha maendeleo nyuma bali inatakiwa kushirikiana ili kupigania maendeleo.

“Uchaguzi maana yake ni kumchagua yule kiongozi ambaye unamuona ataweza kukuongoza na kukuletea maendeleo ndiyo maana na sisi tutashiriki kikamilifu ili kusaidia wananchi wetu katika matatizo yao mbalimbali”amesema.

Cheyo amemuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwajali wanyonge hasa wakulima ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao kupitia kilimo.

Amesema baada ya kusikia lile agizo la Rais Magufuli la wakulima hao wa pamba kulipwa pesa zao, alithibitisha kweli Magufuli ni Rais anayejali wanyonge.“Mimi ni mmoja kati ya watu ambao wanaunga mkono wakulima, na baada ya kusikia lile agizo nimefurahi sana  kwani ile ni haki yao ambayo inasaidia kuendesha maisha  siku amesema

Aidha ameiomba serikali kuandaa mipango ya kuuza mazao ya wakulima mapema ili inapofika msimu kusipo kukwama kwa kilimo hicho kutokana na kukosa fedha.

Cheyo pia alimpongeza Rais Magufuli kwa kuwa mkali kuhusu suala la watu kubambikiwa kesi kwani jambo hilo lkimekuwa likimchafua Rais kwa wananchi wake.“Watu wanatakiwa kushitakiwa kwa makosa yaliyona haki na si kumpa mtu tu kesi kisa unamaslahi yako binafsi kwani kufanya hivyo kunamchafuya Rais Magufuli”amesema

USAJILI WA LAINI YA SIMU KWA ALAMA ZA VIDOLE

$
0
0
Ndugu Mwananchi mwenzangu ambaye tayari una kitambulisho cha Mamlaka ya Kiambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya Kitambulisho. Wahi ukajiandikishe kwenye maduka au mawakala wa makampuni ya huduma za simu haraka na mapema. Usisubiri dakika za mwisho kuepuka msongamano na usumbufu. Nenda sasa. Sajili laini yako ya simu kwa alama za vidole sasa. Usalama wako ndiyo kipaumbele chetu.

Kama hujapata Namba ya NIDA hakikisha unawasiliana na NIDA. Usajili laini ya simu kwa alama za vidole unafanyika bure yaani bila malipo na upatikanaji wa Namba ya NIDA ni bure. 

Imetolewa na:
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
12/10/2019.

VIJANA WILAYANI RUAGWA WAPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA STADI ZA KILIMO CHA KISASA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo alipokuwa akigagua Kitalu nyumba kilichojegwa katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilayini Ruangwa. Kulia ni Bw. Lucas Mwindima ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika na mafunzo ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) katika kijiji cha Chimbila “A” alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya mafunzo hayo Wilayani Ruangwa.
Sehemu ya Vijana walionufaika na Mafunzo hayo ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipowatembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mafunzo yao.
Bw. Lucas Mwindima ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio waliyopata kupitia teknolojia ya kilimo cha Kitalu Nyumba.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na vijana wa Kikundi cha Ruwangwa Materials wanaojihusisha na utengenezaji wa matofali walipotembelea kikundi hiko kukagua maendeleo ya mradi wao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa.


Kiongozi wa Kikundi cha Ruagwa Materials Bw. Mohammed Moshi akisoma taarifa fupi kuhusu utekelezaji wa mradi wao walipotembelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. (Wa tatu kutoka kulia) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe.


Baadhi ya Vijana wa Kikundi cha Ruangwa Materials wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), alipowatembea kwa lengo la kukagua maendeleo ya kikundi hicho.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

……………………………..

Na; Mwandishi Wetu

Vijana Wilayani Ruagwa wameipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) ambayo yamekuwa ni chachu kwao kujikwamua kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2019 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilaya ya Ruagwa kukagua maendeleo ya mafunzo waliyopata vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.

Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeonesha kuwajali, kuwatambua na kuwathamini vijana kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiwasaidia sana katika kuwaendeleza vijana kulima kwa mkakati.

“Mafunzo hayo yamewajengea uwezo vijana wa kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hii kwa kuwa kinatija na ufanisi, hivyo vijana watakuwa kupata mavuno zaidi katika eneo dogo kuliko eneo la wazi, uwezo wa kupata soko la mazao utakuwa wa uhakika, matumizi ya maji ni madogo katika kilimo hiko na hudhibiti viwatilifu,” alisema Mhagama

Alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilianzisha Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo mafunzo hayo ya kilimo cha Kisasa ikiwa ni mkakati wa serikali baada ya kubaini asilimia 56 ya nguvukazi nchini ambao ni vijana wamekuwa na changamoto ya ajira, katika kutatua changamoto hiyo kundi hilo limewezeshwa kwa kujengewa uwezo wa kupatiwa ujuzi katika fani mbalimbali.

Waziri Mhagama aliongeza kuwa Mafunzo hayo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba yatawasaidia kuboresha stadi bora za kilimo kwa vijana hususan waliopo vijijini ili waweze kujiajiri, kuajiri wenzao na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha aliwasihi vijana kuendelea kutunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika kiuchumi na sambamba na kuwaleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya vijana walionufaika na mradi huo akiwemo Bw. Lucas Mwindima alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeonesha dhamira ya dhati katika kuwawezesha vijana wanapata ujuzi utakaowawezesha kukuza ujuzi wao na kuwaondoa katika hali ya umaskini.

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kutuwezesha vijana kupata mafunzo haya ya kilimo cha kitaalamu yaliyoleta tija tunaona uzalishaji wa mazao ulivyokua tofauti na zamani na mazao tunayozalisha yanafursa ya kupata masoko ndani au nje ya nchi,” alisema Mwindima

Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata ujuzi wa kilimo cha mazao biashara pamoja na ongezeko la ajira kwa vijana waliowezeshwa elimu hiyo.

Pia Waziri Mhagama alitembelea kikundi cha Ruangwa Materials ambacho kimenufaika na Mkopo wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi yake kupitia Idara ya Manedleo ya Vijana.

KOROGWE MINI MARATHON KUFANYIKA KESHO JUMAPILI MJINI KOROGWE

$
0
0

MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusiana namna watakavyotumia mashindano ya Korogwe Mini Marathon kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 
MKUU wa wilaya ya Korogwe kulia Kissa Gwakisa akimkabidhi namba ya ushiriki mmoja wa wananchi wa wilaya ya Korogwe Noah Gondwe ambao wamejitokeza kuajiandikisha kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathoni yatakayofanyika leo Jumapili ambayo yameandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya
MKUU wa wilaya ya Korogwe kulia Kissa Gwakisa akimkabidhi namba ya ushiriki mmoja wa wananchi wa wilaya ya Korogwe Magesa Kuboja ambao wamejitokeza kuajiandikisha kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathoni yatakayofanyika leo Jumapili ambayo yameandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha kushiriki kwenye mashindano ya Korogwe Mini Marathon yatakayofanyika kesho Jumapili wilayani Korogwe
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa na baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha kushiriki kwenye mbio za Korogwe Mini Marathon ambazo zitafanyika kesho Jumapili wilayani Korogwe
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akiwasikiliza wanariadhaa ambao wamefika wilayani humo kutoka mkoani Arusha kujiandikisha kushiriki kwenye mashindano ya Korogwe Mini Marathon yatakayofanyika kesho Jumapili mjini humo 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa aliyesimama katikati akiwa kwenye picha ya pamoja nao


MASHINDANO ya Riadha ya Korogwe Mini yanatarajiwa kufanyika kesho Jumapili mjini hapa huku yakitumika kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.


Mashindano hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa Alisema lengo kubwa ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutimiza miaka 20 ya kumuenzi lakini pia kuchangia maendeleo wilaya ya Korogwe huku akitoa wito kwa wananchi wajitokeza waungane pamoja kushiriki kwenye mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa alisema kwamba mashindano hayo watatumia muda mchache ambapo wataanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa mbili nusu asubuhi yatakuwa yamemalizika.

Alisema pamoja na kumuenzi baba wa Taifa ambaye alipenda demokrasi ya nchi yetu na ndio maana alipigania sana vyama vingi kwenye nchi yetu na hadi kufikia kusema wachache wapewe mpaka hivi leo kuna vyama vingi.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mambo makubwa aliyoyafanya Mwalimu Nyerere mpaka leo yanaendelea kufanywa na Rais aliyepo madarakani Dkt John Magufuli kwa kuendelea kuenzi demokrasia ndio maana alihamasisha nchi nzima watanzania waendelee kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwenye uchgaguizi wa serikali za mitaa.

Alisema kwamba Rais Dkt John Magufuli alisema watu wajitokeza kwa wingi kuiandikisha kwenye daftari la kupiga kura huku akieleza kwamba watakaofika kwenye mashindano hayo watapewa hamasa ya kwenda kujiandikisha na watatoa usafiri kwa wale ambao hawajiwezi.

“Sisi kama ofisi ya DC kwa wale ambao watakuwa hawajiwezi ili tutawapeleka waende kujiandikisha Korogwe lakini pia Korogwe Mini Marathon italeta hamasa kwa wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kwenye kujiandikisha “Alisema

“Lakini pia niwaambie kwamba ile mvua au jua tutaendelea kuhamasisha wananchi kujiandikisha tokea tuanze tumeona mafanikio Halmashauri ya wilaya tayari juzi wamejiandikisha asilimia 42 hivyo ninaamini kwamba siku zilizobakia tutavuka lengo ambalo tumewekewa “Alisema DC Kissa.

Naye kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Mbeza wilayani Korogwe Magesa Luhoga alisema kwamba wao wamejiandaa vema kushiriki kwenye mashindano hayo na kwamba atashiriki kwenye kilimota 10.

Alisema mashindano hayo ni jambo jema kwa wananchi wa wilaya ya Korogwe huku akimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuandaa mashindano hayo kwani yataimarisha maendeleo huku wananchi wakiimarisha miili yao.

Hata hivyo kwa upande wake Bakari Nchimbi ambaye ni meneja mauzo kampuni ya TBL alisema kwamba watashiriki kwenye mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi za mkuu huyo wa wilaya za kuhamasisha maendeleo

Hata hivyo naye kwa upande wake Noah Gondwe ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyuzi alisema kwamba watashiriki mashindano hayo kwa kuhakikisha wanamuunga mkono Mkuu huyo wa wilaya.

MBUNGE WA GEITA MJINI AAHIDI KUTOA MIL.20 YA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA SHULE YA SEKONDARI SHANTAMINE.

$
0
0
Na Ripota Wetu- GEITA
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya  kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa chakula katika shule ya Sekondari ya Shantamine.
Amesema ataitoa fedha hiyo kwa ajili ya kupunguza adha kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaolazimika kukaa nje wakati wa kula  chakula hasa katika kipindi cha mvua.
Ahadi hiyo ameitoa leo mkoani Geita wakati alipokuwa akizungumza na jumla ya  Wahitimu 263   wa kidato cha nne  kwenye  mahafali  yaliyofanyika  katika Shule ya Sekondari ya Shantamine.
Ombi hilo linakuja kufuatia risala iliyosomwa kwake na Wahitimu wa kidato cha nne wakiomba kukamilishiwa ujenzi wa ukumbi huo utakaoweza kuwahudumia wanafunzi wengi kutokana na idadi yao kuongezeka  hali inayowalazimu kupata shida wakati mvua ikiwa inanyesha
Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameahidi kuchimba kisima kirefu zaidi katika shule hiyo kwa ajili ya  kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaolazimika kutoka nje ya shule  kutafuta maji
Ameeleza kuwa  maombi kwa ajili ya   uchimbaji wa  kisima hicho yamewashawasilishwa katika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na wanachosubili ni utaratibu wa namna ya kukichimba kisima hicho.
Hata hivyo  Mhe. Kanyasu ameeleza kuwa  jumla ya visima viwili vilishachimbwa katika shule hiyo lakini ilibainika kuwa havina maji na eneo hilo lilionekana kuwa maji yake yana chumvi sana.
Akizungumzia kuhusu ombi la kupatiwa umeme katika shule hiyo, Mhe. Kanyasu amesema ifikapo mwezi mei mwakani shule hiyo itakuwa tayari ina umeme.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewaahidi wanafunzi wa shule hiyo kuwa atashirikiana na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita  kujenga mabweni kadiri pesa inavyojitokeza ili kuwanusuru wanafunzi wanaolazimika kupanga nyumba nje ya shule hali inayopelekea wanafunzi wengi wa kike kuacha masomo baada ya kupata mimba.
Mbali na hilo, Mhe. Kanyasu amewatakia heri wahitimu hao katika mitihani yao na kuwataka wasiridhikena elimu hiyo na badala yake wajiendeleze zaidi
Naye. Diwani wa Kata ya Mtakuja. Constantine Morandi amewataka wananfunzi hao wajiandae kikamilifu katika mitihani ya kuhitimukidato cha nne ili kuweza kuileta sifa shule hiyo.
‘’Nina washukuru wazazi pamoja na waalimu kwa ushirikiano wenu katika kuhakikisha wanafunzi 263 wanahitimu masomo yao’
Akizungumza mhitimu wa kidato cha nne kwa niaba ya wenzake , Anna Masumbuko amesema wapo tayari kwa ajili ya mtihani wa mwisho na wanategemea  kufaulu vizuri katika mitihani yao.
 Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine akizungmza na wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263 yaliyofanyika leo  katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita
 Baadhi ya Wahitimu wa kidato cha nne wakituimbiza wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzoa  katika mahafali yao yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Shantamine
  Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi bora, Editha Karlo  aliyekuwa akiongoza masomo  kwa jumla ya Wahitimu 263 wa kidato cha nne wakati wa mahafali yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita


 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Shantamine wakionesha ubunifu wa mavazi mbela ya Mbunge wa Geita mjini, Mhe Constantine Kanyasu wakati wa mahafali kaidato cha nne
 Diwani wa kata ya Mtakuja, Constantine Morandi akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne kabla ya Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263
 Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi bora kwa masomo ya Sayansi, Elinami Habakuki wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa jumla  Wahitimu 263 yaliyofanyika leo   katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Shantamine wakiwa wameshika jezi za michezo kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kiume ambayo ni zawadi  walizokabidhiwa na Mbunge huyo.

  

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA ATCL KUTOKA DAR KWENDA MPANDA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka kuelekea mkoani Dodoma kwa
kutumia usafiri wa shirika la ndege la ATCL mara baada ya kumaliza ziara yake Mpanda mkoani Katavi.
Ndege ya ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi huku ikimwagiwa maji (water salute)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono vikundi vya ngoma na kwaya vya Mpanda mkoani Katavi kabla ya
kuzindua safari za Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 12/10/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, viongozi wa mkoa wa Katavi,
Wabunge, Mawaziri na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa safari za Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi leo  tarehe 12/10/2019.


DC IKUNGI AWAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo amewata wananchi wa Wilaya hiyo kutumia muda uliobaki kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kutumia haki yao kuchagua viongozi.

Mpogolo alisema hayo  leo alipozungumza na waandishi wa habari katika Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Ikungi katika Wilaya hiyo alipokwenda kujiandikisha, aliwataka wananchi wa Ikungi kutumia haki yao ya Kidemokrasia ya kuchagua na kuchakuliwa. 

Aidha amesema uchaguzi ngazi wa serikali ngazi ya Vitongoji na Vijiji ni muhimu wananchi hushiriki moja kwa moja kupanga na kuamua kutekeleza maendeleo yao. 

"Hivyo ni muhimu kwa kila mwana Ikungi kushiriki kwakuwa inaamua hatima yake ya kujiletea maendeleo ambayo Rais John Magufuli amekuwa akipambana kwa watanzania. 

Alisema hadi jana wameandikikura.zaidi ya asilimia 41  ambapo wameweka mikakati kuhakikisha wanafikia lengo la kuandikisha watu 154137.

Mpogolo aliwahimiza wananchi aliowakuta katika kituo hicho  pamoja na vituo vingine alivyotembelea kuwahimiza vijana wao ambao umri wao ni juu ya miaka 18 kuhakikisha nao wanajiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi ambao watawaletea maendeleo.

"Wazee wangu, tuwahimize na vijana wetu nyumbani nao wajiandikishe tusikubali wakabaki bila kujiandikisha nafasi hii ni muhimu kuitumia ili nao wawe sehemu ya kuchagua viongozi wanaowataka," alisema Mpogolo.

Aidha, alisema maendeleo katika nchi hayawezi kushuka kutoka Mbinguni bali kwa kuchagua viongozi imara, wenye mapenzi na maendeleo ya wananchi na pia maendeleo ya nchi yao.

Mpogolo alitembelea vituo vingine katika Wilaya hiyo ambapo alizungumza na wananchi kujua changamoto zao katika uandikishaji huo na pia kuwahamasisha kuwashauri na watu wengine kujitokeza.

"Msiwaache watu nyumbani tuhakikishe wote wanajiandikisha, kina mama nyumbani, majirani," alisema. 

Mpogolo alisema katika Wilaya hiyo uandikishaji unaenda vizuri, watu wanajitahidi kujitokeza na pia viongozi wanajitahidi kuhamasisha wananchi kujitokeza ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki kupiga kura.
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo akijiandikisha  katika daftari la uchaguzi wa serikali za mitaa,katika Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Ikungi Wilayani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Awazawadia Watoa Huduma wa Kituo cha Huduma kwa Wateja

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (kushoto) akiwapongeza wafanyakazi wa kituo cha huduma kwa Wateja (Call Centre) kwa namna wanavyotoa huduma bora kwa wateja wao, wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Wateja . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Stella Mboyelwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Restituta Masondore kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Kelvin Mrema kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Godfrey Shayo kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma kwa wateja Vodacom (call centre) wakimsikiliza mkurugenzi wao , Hisham Hendi.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE WA WILAYA YA WETE PEMBA LEO

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jamuhuri Wete Pemba leo 12-10-2019.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Jamuhuri Wete Pemba, wakati wa mkutano wake na Wazee wa CCM Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba leo 12-10-2019.(Picha na Ikulu)

WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Pemba wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mh.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wake na Wazee hao uliofanyika katika ukumbi wa Jamuhuri Wete leo,12-10-2019.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kukabidhiwa risala ya Wazee wa CCM Wilaya ya Wete Pemba na Katibu wa CCM Wilaya ya Wete Pemba.Ndg,Salum Khamis Haji, wakati wa mkutano wa Wazee wa CCM Wilaya ya Wete Pemba uliofanyika katika ukumbi wa Jamuhuri Wete,kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr.Abdalla Juma Mabodi na kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba.Ndg.Mberwa Hamaad Mberwa.(Picha na Ikulu)

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa akizungumza wakati wa mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Wazee wa CCM wa Wilaya Wete Pemba, uliofanyika katika ukumbi wa Jamuhuri Wete.(Picha na Ikulu)NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi akizungumza na Wazee wa CCM Wilaya ya Wete Pemba kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,kuzungumza na Wazee hao katika ukumbi wa Jamuhuri Wete Pemba.(Picha na Ikulu)

UJIO WA TAMASHA LA 38 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YAMUENZI BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KWAKUTOA MISAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii  
Katika kumuenzi baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Shule ya Sekondari ya Makongo imefanya  shughuli mbalimbali  katika Hospital ya Mwananyamala ikiwa ni pamoja na kufanya usafi Kuchangia Damu na kutoa kutoa msaada wa Maji .

Shughuli hiyo  imeanza kwa maandamano na imeongozwa na mbunge wa Kinondoni Abdallah Mtulia kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza kutembelea Hospitali hiyo na kukabidhi misaada mbali mbali Mkuu wa Shule ya Makongo, KanaliBYuda Kitinya amesema kuwa lengo kubwa la kufanya zoezi hilo ni kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo uzalendo  kama baba wa Taifa alivyokuwa akifundisha ambae alikuwa  anasisitiza uzalendo  katika nchi.

"Tunawafundisha vijana wetu uzalendo ili wafahamu kwamba ukiwa kijana unajukumu la kujitoa kwa ajili ya jamii inayokuzunguka kwani ninaimani kama tukiwafundisha na wakaelewa basi wataendelea kuelimisha wenzao na kujitoa siku hadi siku katika maisha yao yote".amesema Kanali Kitinya.

 Amesema, wanafanya yote hayo kwa ajili ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa tangu alipofarikiwa miaka 20 iliyopita.

Kwa upande wake, Mbunge wa  Kinondoni, Mtulia  ameupongeza uongozi mzima wa Shule ya Makongo kwa kufanya kitendo cha uzalendo kama hicho ambacho kinagusa jamii nzima, na pia kuwafundisha vijana uzalendo na moyo wa kusaidiana na kuwa na uzalendo.

"Kitendo hiki ni cha kuigwa na watanzania wote katika kumuenzi Baba wa Taifa kwa kufanya mambo yale mazuri aliyotuagiza na aliyotuachia ukizingatia amefanya mambo mengi sana ambayo hayatasahaulika kamwe" amesema Mtulia.

Amesema Baba wa Taifa kabla hajafariki alikuwa akihimiza sana upendo na kusaidiana na pia alileta sera ya ujamaa na kujitegemea. "Tunamuenzi Mwalimu Nyerere katika  kazi zake hasa katika mambo ya viwanda  na  afya kwani Mwalimu alijenga viwanda vingi sana vidogo na vya kati bila ya kusahau Kiwanda cha silaha cha nyumbu" amesema.

Aidha ameongeza kuwa katika kumuenzi baba wa Taifa tukumbuke pia siasa zake safi na uongozi bora. Pia amewaasa 

Naye Kaimu mganga mfawidhi wa hospital ya  Mwananyamala, Dkt. Isidory Kiwale amesema msaada huo utawasadia  kwa kiasi kikubwa hususani damu kwa kwani  upungufu wa damu imekuwa changamoto kubwa katika   sekta ya afya.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ) Kanali, Yuda Kitinya na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (katikati) wakikabidhi Maji kwa ajili ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam, anayepokea kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt.  Isdory Kiwale.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ) Kanali, Yuda Kitinya na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (katikati) wakikabidhi Maji kwa ajili ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni Kumbukizi ya Miaka 20 tangu kutokea Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, anayepokea kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt.  Isdory Kiwale.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ) Kanali, Yuda Kitinya (kushoto) akielezea Nembo ya Shule hiyo ilichorwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya Shule hiyo kutoa misaada mbalimbali katika moja ya Wodi ikiwa ni sehemu ya Kumbukizi ya miaka 20 tangu Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kulia ni Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia
 Maandamano ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo kutoka Bamaga jijini Dar es Salaam hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala katika kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tangu kutokea Kifo chake miaka 20 iliyopita.
Maandamano ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ) na baadhi ya Askari Jeshi hilo.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WADAU WA MAENDELEO WA MANISPAA YA LINDI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha Wadau wa Maendeleo wa Manispaa ya Lindi kwenye ukumbi wa Hoteli ya Sea View mjini Lindi, Oktoba 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha Wadau wa Maendeleo wa Manispaa ya Lindi kwenye ukumbi wa Hoteli ya Sea View mjini Lindi, Oktoba 12, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI HASUNGA AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA KANDA YA SUMBAWANGA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati  akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa na Meneja wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya KIlimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi huo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati  akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa (Kushoto) na Meneja wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa  (Kulia) mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi huo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa na Meneja wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa NFRA mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Katavi


Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maghala na vihenge vya kisasa kanda ya Sumbawanga kuongeza kasi ili kukamilisha haraka mradi huo kwa mujibu wa makubaliano.


Alisema kuwa kampuni iliyoteuliwa baada ya kushinda zabuni kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo ni UNIA ARAJ REALICZJE ya nchini Poland ambayo ilimteua mkandarasi msaidizi mzawa anayejulikana kwa jina la ELERAI CONSTRUTION CO. LTD wa Arusha, hivyo napaswa kuongeza kasi ya ujenzi kutokana na kasi iliyopo kwa sasa kutoridhisha.


Waziri Hasunga ameyasema hayo juzi tarehe 10 Octoba 2019 mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo kwenye Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi utakaowanufaisha wakulima wa mazao ya nafaka kwani serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) itakuwa na uwezo wa kununua mazao mengi kwa wakulima na kuyahifadhi kwa muda mrefu.


Alisema kuwa kampuni hiyo inayojenga vihenge vya kisasa na miundombinu mingine ikiwemo maghala katika eneo la Kanondo Manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa na Mpanda Mkoani Katavi bado haijamfurahisha kutokana na kasi ndogo ya ujenzi wa mradi.


Mhe Hasunga amesema kuwa serikali imekusudia kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka nchini ili kuwanufaisha wakulima punde wanapovuna mazao yao hususani nafaka kwani kufanya hivyo wakulima wataongeza uzalishaji na tija kwenye mazao na kuliongezea Taifa pato kubwa.


Alisema kuwa vihenge hivyo vitakuwa na uwezo wa kuhifadhi jumla ya Tani 20,000 za nafaka huku ujenzi wa miundombinu mingine ukiendelea kama jingo la Ofisi ya utawala, Ghala la kawaida la ujazo wa Tani 5000 za nafaka, na Mzani mkubwa wa daraja (Electronic weighbridge).


Mradi huo utakuwa na gharama ya Dola za kimarekani 6,019,399 ambazo ni takribani shilingi za Kitanzania Bilioni 14 kwa mradi wa eneo la Kanondo Sumbawanga na vilevile Dola za Kimarekani 6,180,857 sawa na fedha za kitanzania Shilingi Bilioni 14.2


Mhe Hasunga ametilia nyundo kuwa serikali haitaongeza muda kwa mkandarasi endapo atashindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa.


Muda wa mradi kuanza hadi kukamilika ni jumla ya miezi 18 (Mwaka mmoja na nusu), Kwa upande wa Mpanda mkoani Rukwa mradi umeanza tarehe 14 Januari 2019 na umepangwa kukamilika tarehe 14 Julai 2020 wakati upande wa Kanondo mkoani Katavi mradi huo umeanza tarehe 8 Septemba 2019 na unatarajiwa kukamilika tarehe 8 Machi 2021.


Punde mradi huu utakapokamilika mkoa wa Rukwa utakuwa na Maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka za Tani 58,500 wakati mkoa wa Katavi utakuwa na uwezo wa kuhifadhi Tani 28,000 ikihusisha pia maghala ya zamani.


MWISHO
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images